RIWAYA: Am not a Doctor

RIWAYA: Am not a Doctor

ILIPOISHIA
Baba akaka kimya huku akishusha pumzi. Taratibu baba akanyanyuka na mimi nikanyanyuka taratibu akanikumbatia huku akinipiga piga mgongoni mwangu.
“Hakikisha una ua mtu mmoja baada ya mwingine, nitakulinda kwa kila jambo baya au zuri utakalo lifanya mwanangu” Baba alizungumza kwa sauti ya chini iliyo jaa uzito mwingi huku akiendelea kunikumbatia kwa nguvu.
“Nimekuahidi baba ninatakwenda kuwa vunja mikund** yao mmoja baada ya mwengine aliye ingia kwenye kumi na nane zangu” Nilizungumza kwa hasira huku nikiyang’ata meno yangu nikionyesha ni jinsi gani nimedhamiria kuwashuhulikia maadui wote walio ingia kwenye maisha yangu, sinto jali ni nani hata kama ni Rose ni lazima nitamuua tu.

ENDELEA
Taratibu tukaachiana na baba, akaninisha mkono wangu wa kulia kwa mikono yake yote miwili huku akiitingisha.
“Ninakutegemea katika hili Erick mwanangu” “Shukrani sana baba, ila ninaomba nipatie gari moja” “Hakuna tabu twende nje” Tukatoka nje na baba, akamuita mlinzi wake mmoja akamuagiza kuniletea gari lenye uwezo wa kwenda masafa marefu pasipo taba ya aina yoyote.
“Dakika tano nitakuwa nimesha lileta hapa” “Sawa” Mlinzi huyu akaondoka na kutuacha tukiwa tumesimama nje mimi na baba.
“Uongozi nilio pewa kwa sasa ni mgumu sana nitahitajika niwe makini sana kwa kila jambo ambalo ninalifanya” “Ni kweli baba, ila pia kuna jambo ninaomba unisaidie” “Jambo gani?” “Yule dokta Benjamini mkuu wa hospitali ya Muhumbili, ningeomba uweze kumpa nafasi nzuri kwenye serikali yako” “Kwa nini yeye?” “Yule ndio mtu aliye weza kunihudumia mimi kwa vitu vingi sana, alinichukualia kama kijana wake alinipa upendo wa kama baba nilio weza kuukosa kwa muda mrefu kwako” Baba akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akionekana kufikiria jambo nililo mueleza.
“Nimekuelewa, nitampatia nafasi nyingine nzuri” “Nitashukuru baba kwa hilo” Mlinzi wa baba ndani ya muda mchache akarudi akiwa na gari aina ya Ford Ranger la rangi nyeusi, akatembea kwa mwendo wa haraka hadi tulipo simama na baba, akanikabidhi fungio.
“Gari imejaa mafuta na ni halina shinda la aina yoyote” “Shukrani John” “Sawa mkuu”
Mlinzi wa baba akaondoka, baba akanitazama usoni mwangu kwa umakini. “Niahidi ukiridi hapa utakuwa na ripoti ya kunifurahisha juu ya hawa washenzi” “Ninakuahidi baba nitafanya kila niwezalo” “Wewe ndio mwanangu niliye kuwa ninamtazamia kwenye maisha yangu yote. Hakikisha unafanya kile ulicho niahidi” “Shukrani baba” Nikaondoka eneo hili na kielekea kwenye gari, nikafungua na kuingia ndani ya hili gari ambalo bado ni jipya. Safari ya kuelekea mkoa wa Tanga aikaanza, nikatoa simu yangu na kumpigia Hussein.
“Za asubuhi” “Salama tu bosi za kwako” “Safi, mumefikia wapi kufahamu ni nani muhusika wa mauji ya bibi na pamoja na uchomaji wa kiwanda changu?” “Hadi sasa hivi bosi polisi hawajapata ripoti yoyote ya kuhusiana na mauji ya bibi” “Maiti yake ipo wapi?” “Ipo katika hospitali ya wilaya Lushoto.” “Hakikisha ninakukuta hapo” “Sawa bosi” Nikakata simu na kuendelea na safari yangu. Ndani ya masaa matano nikawa nimefanikiwa kufika Lushoto na nikaelekea katika hospitali ya wilaya. Nikawakuta baadhi ya wafanyakazi wangu pamoja na marafiki zangu, kila aliye niona hakusita kuonyesha furaha yake ya kuweza kuniona kwani hatujaonana kwa muda fulani. “Jamani ninatambua kwamba kwa sasa tupo katika wakati mgumu, ila nina waahidi kwa kuwa sote tupo hapa kila jambo litakwenda kama tulivyo panga” Nilizungumza huku nikiwa nimesimama katikati ya wafanyakazi wangu hawa walio nizunguka.
“Nikatacho waomba mpango wa mazishi ninaamini haoa Hussein atakuwa amesha upanga, na baada ya mazishi nitawaomba tuweze kufanya kikao cha dharura ofisini kwangu, sasa tunaweza kutawanyika” Nikamaliza kuzungumza na wafanyakazi wangu, nikaongozana na Hussein pamoja na marafiki zangu wengine hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti na tukawakuta askari wawili wakiwa wamesimama nje ya eneo hili.
“Habari zenu” “Salama” “Mumefikia wapi katika uchunguzi wa maiti ya bibi yangu?” “Hadi sasa hivi hatujapata alama yoyote ya vidole kwenye mwili wake na inavyo onyesha muuaji aliye fanya haya mauaji ni mtaalamu mkubwa sana” “Na ameuwawa na nini?”
Askari niliye muuliza kakaa kimya kidogo kwa sekunde kadhaa kisha akatoa camera ndogo ya aina ya digital mfukoni mwake.
“Amechinjwa na hizi ndio picha zake” Nikaichukua kamera hii na kuanza kutazama picha moja baada ya nyingine. Nikajikuta machozi yakinitiririka usoni mwangu, kwani bibi huyu amechinjwa vibaya sana na koromeo lake limetolewa nje, sikuweza kumaliza kutazama picha hizi, nikamrudishia polisi kamera yake, taartibu nikajikuta nikikaa kwenye kiti kilichopo pembeni, nikainama chini na kufunika uso wangu kwa viganja vyangu viwili. Nikaanza kulia kwa uchungu sana huku nikiendelea kujiapiza kwamba ni lazima nitawaua wale wote ambao wamehusika na mauaji ya bibi huyu asiye na hatia.
“Bosi” Hussein aliniita kwa sauti ya upole huku akiwa amechuchumaa mbele yangu.
“Bosi natambua kwamba hili jambo linaumiza sana, ila inabidi ujikaze wewe ni mwanaume mkuu” Taratibu nikayapangusa machozi yangu, kisha nikamtazama Hussein usoni mwakekwa macho makali sama. “Itoeni maiti tukaizike” “Sawa bosi” Husseina akanyanyuka, askari niliye kuwa ninazungumza naye akanifwata na kusimama pembeni yangu.
“Samahani, kwa sasa tumeizuia maiti kutoka hadi uchunguzi uweze kukamilika” Nikanyanyuka taratibu na kumsogelea karibu askari huyu nikiendelea kukazia macho.
“Uchunguzi gani munao ufanya wakati hadi sasa hivi hamjafanikiwa kupata chochote” “Kuna wataalamu tunawasubiria kutoka makao makuu ya mkoa Tanga watakuja kufanya uchunguzi na kwa sasa wapo njiani kufika” “Hakuna haja ya uchunguzi tena na hili swala kuanzia sasa polisi haliwahusu” Nilizungumza kwa hasira na kumfanya askari huyu kukaa kimya. Hussein na wafanyakazi wengine wakabaki kimya wakiwa wamaeismama nje ya mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti huku wakiwa wamezuwa na askari mwengine. Nikatembea hadi mlangoni, aksari huyu ambaye anaonekana anapoke amari kutoka kwa huyu mkuu wake, aliendelea kusimama pasipo kunipisha.
“Sogea njiani?” Nilizungumza kwa sauti nzito iliyo jaa mikwaruzo ya hasira, askari huyu akaonekana kukaidi ninacho muuambia. Kwa nguvu za ajabu nikamvuta shati lake na kumsogeza pembeni hadi wafanyakazi wangu wakabaki wakiwa wameduwaa, nikaingia katika chumba hichi cha maiti pasipo woga wa aina yoyote.
Nikatazama mafriji makubwa yaliyomo humu ndani, nikaanza kutembea kwenye mlango wa friji moja ambalo ndio la kwanza, nikaanza kuvuta mlango wake, nikakuta maiti ya mtu aliye pasuka kichwa chake. Nikasunya na kufunga mlango huu.
Hussein na wafanyakazi wengine wakiangia ndani na kuanza kunisihi kwamba nitoke katika hili eneo kwani lina vitu vya kutisha sana. Sikuhitaji kumsikiliza hata mmoja kwa maana hakuna hata mmoja hapa anaye tambua roho yangu kwa sasa sio ya yule Erick niliye kuwa mcheshi kwao.
Nikeendelea kufungua milango ya mafriji haya, hadi ninafika friji la nne nikafanikiwa kuiona maiti ya bibi yangu. Machozi ya hasira yakaanza kunibubujika tena, nikataka kumtoa ila madaktari wakawahi kufika na kuzidi kunisihi kwamba nisimtoe hadi wamchome dawa ya kumkausha.
Ikawalazimu wafanyakazi wangu kunitoa kwa nguvu ndani ya chumba hichi cha maiti. Nikatolewa nje kwa nguvu hadi wafanyakazi wengine wa kike pamoja na watu walipo hapa hospitali wakabaki wakiwa wananishangaa. Hussein na wezake wakaniingiza kwenye gari la kampuni na kuniacha ndani humu na kulifunga gari kwa nje. Nikabaki ndani ya gari kwa lisaa zima hadi machozi yakanikauka kabisa usoni mwangu. Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia Hussein ambaye yupo ndani ya hospitali.
“Nifungulieni” “Bosi haupo sawa” “Hussein hili sio ombi ni amri nifungulie gari” “Sawa mkuu” Baada ya dakika kadhaa Hussein akafika katika gari hili, akanifungulia mlango, sikumsemesha kitu chochote zaidi ya kuanza kutembea kueleka ndani ya hospitali.
“Bosi hadi kwa sasa askari hawajafanikiwa kupata chochote” Hussein alizungumza huku akijitahidi kutembea kwa haraka kadri awezavyo. Sikujibu kitu chochote hadi nikafika nje ya chumba cha kuhifadhia maiti.
“Muandaeni bibi kwa ajili ya mazishi” “Sawa bosi” “Ila tupo katika hatua za mwisho za uchunguzi” “Hili swala kwa sasa haliwahusu polisi nitadili nalo mimi mwenyewe” “Tupe muda ndugu” “Kwani ndani ya mwiliwa bibi yangu kuna dhahabu eheee?” Niliulia kwa ukali huku nikiwatazama wataalamu hawa wa jeshi la Polisi wanao dili na mambo ya upelelezi.
“Hapana, tunatambua kwa sasa akili yako haipo sawa…..” “Niombe radhi kwa hiyo kauli sawa afisa wa Polisi. Sihitaji siasa kwenye mwiliwa bibi yangu. Kama ni sehemu ya kufanya uchunguzi nendeni nyumbani kulipo tokea mauaji sawa” “Tumekuelewa” “Hussein simamia swala zima la uoshwaji wa maiti” “Sawa mkuu” “Itachukua muda gani?” “Kama nusu saa” “Fanyeni hivyo, je sanda ipo?” “Ndio mkuu” “Ipi wapi?” “Hii hapa” Mafanyakazi mmoja alizungumza huku akifungua begi la mgongoni alilo livaa, nikaitazama na kuikuta ina ridhisha kwa weupe wake. Zozei la kuuosha mwili wa bibi yangu ukaanza kufanywa haraka kama nilivyo hitaji. Sote tukaka nje ya chumba cha maiti huku tukiwasubiria waoshaji waweze kumaliza zoezi lao la kuosha maiti.
“Mulipanga ni wapi maiti ikazikwe?” “Bado mkuu tulikuwa tunasubiria kauli yako”
“Agiza vijana wakamzike katika makaburi tuliyo mzika mzee” “Sawa mkuu” Hussein akajitenga nasi huku akiwa ameshika simu yake akawapigia wahusika wanao takiwa kwenda kuchimba kaburi. Jeneza maalumu linalo tumiwa na wamini wa dini ya kiislamu katika kubebea maiti likaletwa eneo la chumba cha kuhifadhia maiti. Nikanyanyuka na kuomba uingia ndani ya chumba cha maiti.
“Tumesha muandaa mkuu hakuna haja ya kuingia humu ndani” “Nimekuambia nahitaji kuingia ndani” Nilimuambia muosha maiti, hakuwa na budi zaidi ya kuingia naye ndani, nikamkuta wakiwa wamemlaza kwenuye moja ya kitanda cha bati.
“Mfungue usoni” “Umesemaje?” “Umenisikia, nimekuambia mfungue usoni mwake” Muosha maiti huyu akatii, nikaiona ni sura ya bibi yangu, taratibu nikashusha pumzi yangu, nikamgusa usoni mwangu kwa kiganja cha mkono wangu wa kilia, kisha nikamuomba muosha maiti huyu amfunge. Maiti ikaingizwa kwenye jeneza, likafunikwa vizuri mimi na wafanyakazi wangu tukalibeba na kutoka nalo nje ya hospitali. Tukamuingiza kwneye gari maalumu la kubebea maiti, kisha nikaingia kwenye gari langu nililo kuja nalo huku nikiwa nimempakiza mfanyakazi wangu mmoja wa kike.
“Bosi una uhakika wa kuendesha gari?” Mfanyakazi wangu huyu aliniuliza, jicho nililo mtazama nalo, likawa jibu tosha kwake kwamba ninauhakika na hichi ninacho kifanya. Msafara wa magari zaidi ya kumi ukaanza kuondoka eneo la hapa hospitali huku gari langu likiwa nyuma ya gari la maiti. Sikutaka kuzungumza chochote zaidi ya kufikiria mpango wa kuwasaka wale wote ambao kwa sasa tayari wamesha ingia uadui na mimi kwenye maidha yangu. Simu yangu ikaita, nikaitoa mfukoni na kukuta ni Zari ndio anye piga nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Baby unandeleaje huko?” “Sipo poa” “Pole sana mume wangu, umeweza kujua ni kitu gani ambacho kimesababisha mauaji ya bibi?” “Hapana” “Ok Brian anahitaji kuzungumza na wewe” Nikaka kwa sekunde kadhaa huku nikifikiria kitu cha kumjibu Zari.
“Mpe simu” “Dady shikamoo” Sauti ya Brian na kuniita kwake baba kukanifanya mwili mzima kunisisimka.
“Marahaba mwanangu vipi?”
“Safi, babu amekuwa raisi” “Yaaa mpe hongera” “Asante dady. Upo wapi?” “Ahaa nipo barabarani ninakuja nyumbani” “Sawa dany I love you” “I love you my son”
Nikajikuta nikitabasamu kwa furaha kwani sikuwahi kuzungumza kwa furaha na Brian tangu kuzaliwa kwake.
“Leo mwanao ameamka na nguvu mpya kwa maana amekuita baba, kazi kweli kweli” “Yaa nimeona, hakikisha kwamba anakuwa katika usalama mzuri kwa maana watu ambao wamesababisha mauaji ya bibi nina imani wanaweza kukutafuta wewe na mwanangu” “Sawa mume wangu” “Poa badae” “Sawa” Nikakata simu na kuirudisha mfukoni, mfanyakazi wangu huyu akanitazama usoni mwangu, akaonekana kama ana jambo anahitaji kuuliza ila anashindwa kutokana na ukali wangu nilio muonyesha kwa mara ya kwanza.
Tukafika soni, na moja kwa moja tukaelekea makaburini, ambapo nikakuta wanakijiji wanaume wengine wakiwa wamekusayika tayari eneo la makaburi. Ustazi akaanza kusoma sala ya kumuombea maiti, baada ya kumaliza sala hii, nikawa mtu wa kwanza kuweka mchanga kwenye kaburi kisha wakafwatia watu wengine. Nikachukua chepe moja na kuanza kusaidiana na watu wengine katika kufukia kaburi hili. Nilipo jihisi kuchoka nikakabidhi mtu mwengine chepe na taratibu nikasogea pembeni, ila katika kutazama kwa mbali kwenye moja ya kaburi lililopo eneo hili na nililo jengewe nikamuona Rose akiwa amekaa huku amejifunika nywele zake kwa ushungi mweusi na usoni mwake amavaa miwani yeusi jambo lililo nifanya nianze kumfwata taaratibu pasipo kumuaga mtu wa aina yoyote.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
Nikachukua chepe moja na kuanza kusaidiana na watu wengine katika kufukia kaburi hili. Nilipo jihisi kuchoka nikakabidhi mtu mwengine chepe na taratibu nikasogea pembeni, ila katika kutazama kwa mbali kwenye moja ya kaburi lililopo eneo hili na nililo jengewe nikamuona Rose akiwa amekaa huku amejifunika nywele zake kwa ushungi mweusi na usoni mwake amavaa miwani yeusi jambo lililo nifanya nianze kumfwata taaratibu pasipo kumuaga mtu wa aina yoyote.
ENDELEA
Nikazidi kwenda mbele huku nikimkazia macho Rose aliye simama, nikawaona wanaume wawili wakitoka nyuma ya mti mkubwa na wakasimama nyuma ya Rose. Nikajikuta nikipunguza mwendo wa kuwasogelea. "Erick" Nikiisikia sauti ya Hussein ikiniita nyuma yangu. Ikanibidi nisimame na kugeuka nyuma. "Bosi unakwenda wapi wakati mazishi hayajaisha?" "Erick! " Niliuliza huku macho yakiwa yamenitoka. Hussein akanishika mkono nataratibu tukaanza kurudi sehemu ya kaburi huku baadhi ya watu wakiwa wananishangaa. "Erick tulia mwanangu kumbuka huu msiba ni wako Hussein aliendelea kuzungumza huku akininong'oneza sikioni mwangu. Nikatazama eneo alipokuwa amesimama Rose na watu wake ila sikumuona. Nikasikiliza mawaidha ya mwisho mwisho ya shehe huyu aliyo ongoza mazishi haya. Tukaruhusiwi kuondoka makaburini, nikaanza kutembea kwa haraka kuelekea katika eneo nililo muona Rose na watu wake ila sikuweza kumuona. "Erick unamtafuta nan?" "Nilimuona Rose hapa" "Rose afwate nini huku makaburini?" "Nimemuona Rose akiwa na walinzi wake wawili katika hili eneo" "Erick haupo sawa rafiki yangu, ninakuomba twende nyumbani ukapumzike" "Hussein kuwa karibu yangu na mshauri wangu wa karibu kusikufanye uzungumze chochote uncho kisikia. Heshimu kile ninacho kizungumza sawa" Nilizungumza kwa kufoka sana na kumfanya Hussein kuwa mpole sana. "Hakikisha kwamba unamtafuta Rose katika hili eneo sawa?" "Sawa bosi" Nikaondoka eneo hili la makaburini. Nikaingia kwenye gari na kumkuta mfanyakazi wangu wa kike akiwa ananisubiria. "Ninaelekea nyumbani wewe je" "Bosi ulisema kwamba tutakuwa na kikao baada ya msiba" "Poa" Nikawasha gari na kuondoka katika eneo hili. Moja kwa moja tukafika ofisini kwangu, nikakuta baadhi ya wafanyakazi wakiwa wamesha ingia katika ukumbi wa mikutano kama nilivyo waagiza. Nikapitiliza moja kwa moja hadi kwenye kiti ambacho huwa ninakaa. Nikawatazama wafanyakazi wangu, kila mmoja akaonekana kusubiri kusikiliza kile nitakacho kizungumza. "Kampuni yetu kwa sasa ipo katika wakati mgumu, ila kama tukianza pamoja naamini kwamba hii ni changamoto ambayo tunaweza kuipita kwa pamoja. Naamini kwamba sinto sikia mtu akizungumzia swala la kuacha kazi wala kuhamia kampuni nyingine. Mtu akifanya hivyo basi kwangu ninaweza kumuita msaliti" Nilizungumza kwa kujiamini sana na kuwafanya wafanyakazi wangu kunipigia makofi. "Natambua kwamba mulikosa ongozi wangu kwa kipindi cha mwezi sasa, hayo yote yalitokea kutokana na sababu zilizopo nje ya unaweza wangu." "Kwa leo ninawaomba tuishie hapa, ninawakaribisha nyumbani kwangu tukashiriki msiba pamoja" Nikafunga kikao, nikaongozana na wafanyakazi wangu hadi nyumbani kwangu. Nikakuta ulinzi wa askari ukiwa umeimarishwa. "Pole sana Erick" Mkuu wa polisi kwa wilaya ya Lushoto alizungumza huku akinipa mkono "Asante muheshimiwa" "Ninakuahidi nitahakikisha wale wote walio sababisha mauaji ya bibi tunawakamata na sheria inachukua mkondo wake" "Nitashukuru sana. Mauaji yalitoke eneo gain?" "Njoo nikuonyeshe" Tukaingia ndani na mkuu wa polisi, tukafika sebleni na akaanza kunielekeza eneo ambalo bib alianza kupata hekaheke za kaundamwa na muuaji. "Bibi alichinjiwa katika mlango wa kuingilia chumbani kwake nina imani alikuwa anakimbilia ndani ili ayaokoe maisha yake" "Kuna alama yoyote ya muuaji?" "Kusema kweli muuaji huyo alikuwa ni professional hakuacha alama ya aina yoyote." "Ngoja kwanza" Nilizungumza huku nikirudi sebleni kwenye moja ya ua la urembo kuna kamera ndogo sana niliitega kipindi cha nyuma pasipo mtu yoyote kuweza kugundua. Nikaitazama na kuikuta ikiwa bado inafanya kazi. Sikumuambi kitu chochote mkuu wa polisi, nikaingi chumbani kwangu, nikaafungua kabati langu ambalo nimehifadhi laptop yangu. Nikaichukua laptop yangu na kuiwasha. Nikaingia katika faili ambalo matukio yote ya kamera huwa yanarekodiwa hapa. Nikaanza kutazama matukio ya siku iliyopita. Asubuhi alionekana Hussein akifika katika nyumba hii, akazungumza na bibi wakiwa wamekaa katika sebleni. Sikusikia wamezungumza kitu gani kwani kamera hiyo inarekodi video tu pasipo sauti. Hussein aliondoka nyumbani hapa majira ya saa tano asubuhi, na wafanyakizi wa ndani wakaondoka majira ya saa kumi na mbili jioni. Baada ya ya hapo hapaakuwa na mfanayakazi yoyote zaidi ya bibi. Majira ya saa nne usiku mlango ukagongwa, bibi aliyekuwa amekaa sebleni akanayanyuka na kuufungua mlango. Akaingia jamaa aliye valia kinyago usoni mwake huyu ndio aliye anza kumsumbua bibi aliyekimbilia katika chumba chake na kabla hajafika ndio akachinjwa kikatili. Nikaizima laptop yangu kwani hata muuaji sijaweza kumfahamu kabisa. Nikatoka chumbani kwangu, nikafika sebleni na kumkuta Hussein kizungumza na mkuu wa polisi. Nikamuita Hussein na kusimama naye pembeni. "Vipi umeweza kumuona Rose" "Hapana vijana wanaendelea kumtafuta" "Sawa sawa hakikisha kwamba tunampata" "Sawa bosi" "Jana ulikuja nyumbani kumuona bibi?" Nilimuuliza Hussein huku nimekazia macho. Hussein akanitazama kwa macho yaliyo jaa unyenyekevu mkubwa. "Hapana jana sikuja kabisa nyumbani hapa kwani vipi kaka?" Nikajikuta nikistuka sana ila sikutaka kumuonyesha Hussein kwamba nimestuka kwani hichi alicho kizungumza ni uongo mtupu na inavyo onekana anafahamu kilichokuwa kimetokea. ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
"Vipi umeweza kumuona Rose?" "Hapana vijana wanaendelea kumtafuta" "Sawa sawa hakikisha kwamba tunampata" "Sawa bosi" "Jana ulikuja nyumbani kumuona bibi?" Nilimuuliza Hussein huku nimemkazia macho. Hussein akanitazama kwa macho yaliyo jaa unyenyekevu mkubwa. "Hapana jana sikuja kabisa nyumbani hapa kwani vipi kaka?" Nikajikuta nikistuka sana ila sikutaka kumuonyesha Hussein kwamba nimestuka kwani hichi alicho kizungumza ni uongo mtupu na inavyo onekana anafahamu kilichokuwa kimetokea.
ENDELEA
“Ahaa hapana nimekuuliza tu” Nilizungumza huku nikitabasamu ili kumficha Hussein ukweli ninao ufahamu, ila kichwani mwangu kwa sasa nimesha weke alama ya kujiuliza.
“Vipi askari wamesemaje?” “Hawajaweza kugundua chochote” Akaingia askari mmoja mwembana sana, akamnong’oneza mkuu wa polisi wa wilaya ya Lushoto bwana Isaya, kisha akamkabidhi na bahasha ya kaki. Bwana Isaya akaifungua bahasha hiyo na kuifungua, akatoa picha kadhaa kisha akazirudisha ndani ya bahasha hiyo. Akanifwata sehemu nilipo simama na Hussein, akatutazama kwa sekunde kadhaa huku akionekana kama anahitaji kuzungumza jambo fulani kwangu mimi.
“Samahani bwana Erick tunaweza kuzungumza kidogo” “Ndio tunaweza. Hussein naomba utupishe” “Sawa bosi” “Hakikisha watu wanakula, wanakunywa sawa” “Hakuna tabu mkuu” Hussein akaondoka na nikabaki nikisindikiza kwa macho hadi akatoka nje. Mkuu wa polisi akatoa picha nilizo kuwa ninamuona akizitazama.
“Kuna picha hapa za wafanyazi wa ndani, wamekutwa milimani huko wakiwa wametupwa huku wameuwawa” Mikono ikaanza kunitetemeka huku nikipokea picha hizi. Nikatazama picha ya kwanza, sikuamini macho yangu kumuona msichana ambaye alikuwa anamuhudumia bibi na nilimpa jukumu hilo hadi pale bibi atakapo fariki, nikchukua picha nyingine ya mfanyakazi mwengine wa ndani. Nikajikuta nikifumba macho yangu.
“Muuaji aliye waua hawa ni huyu huyu aliye muua bibi” “Wanataka nini kutoka kwangu” Nilizungumza huku nikiendelea kuyafumba macho yangu.
“Je kuna mtu yoyote ambaye uliweza kumkosea au kugombana naye?” “Sina mkuu, ninaishi na watu vizuri sana na siku zote ninaepuka kugombana na watu. Ila ninaona walianza kunitafuta tangu muda” “Kivipi bwana Erick” “Watu hawa ndio walio fanya mlipuko katika mkutano wa kisiasa wa baba yangu pale Jangwani” “Unataka kuniambia kwamba mkutano ule uliweza kufahamu ni kitu gani kinakwenda kutokea?” “Ndio niliweza kujitahidi kardi ya uwezo wangu katika kuzuia tukio lile lisijitokeze ila nikashindwa kabisa kufanya hivyo” “Na umesema kwamba ni mkutano wa baba yako, kivipi?” “Raisi Almeida ni baba yangu. Jina langu ninaitwa Erick Almeida” “Weee, mimi siku zote nilikuwa ninajua wewe ni mtoto wa marehemu Omary” “Hapana huwa sihitaji watu wanifahamu na wewe sinto taka umueleze yoyote juu ya mahusiano yangu na raisi huyu mpya” “Sawa mkuu” Mkuu wa polisi alizungumza huku akitabasamu na muda wote hakuwa na furaha kama hii niliyo mueleza kwamba raisi Almeida ni baba yangu.
“Je muuaji mumempata?” “Ndio tunaendelea kushuhulika na hilo swala” “Na aliye husika katika kuchoma kiwanda changu, mumeweza kumfahamu?” “Bado pia” “Hivi kitengo chenu cha upelelezi kina kazi gani?” “Tunazidi kujitahidi mkuu, nakuhakikisha kwamba tunawapata” “Fanyeni hivyo basi, au ndio hadi muhongwe pesa?” “Ahaa..hapanaa mkuu” Bwana Isanya alinijibu kwa upole na unyenyekevu mkubwa. Nikamrudishia picha zake na kutoka zangu nje, nikajumuika na wafanyakazi wengine pamoja na wananchi kukaa kwenye jamvi lililo tandikwa chini, tukisubiri kula chakula.
“Samahani bosi” Msichana niliye kuwa naye kwenye gari alininong’oneza kwenye sikio langu la upande wa kushoto huku akiwa ameinama nyuma yangu.
“Ndio” “Nakuomba kidogo” Nikajifikiria kwa sekunde kadhaa huku nikiwatazama watu nilio kaa nao. Nikanyanyuka kwenye mkeka na kuanza kuongozana naye. Tukasimama eneo ambalo halina watu kabisa.
“Bosi nina taarifa ambayo sidhani kama kwako inaweza kuwa ni nzuri” “Vipi unahitaji kuacha kazi?” “Hapana ni bora ningeacha kazi mimi?” “Je kuna msiba?” “Hapana bosi Erick, ninakuomba unipe nafasi basi niweze kuzungumza hichi ninacho hitaji kukizungumza kwako” “Eheee” “Dakika kama sita au kumi zilizo pita, nilimsikia bosi Hussein alizungumza na simu, mazungumzo ambayo kidogo yalinipa mashaka kidogo, hadi ikafikia nimrekodi” “Alikuwa anazungumza na nani?” “Na mmoja wa wapishi hapa, ila walikuwa wamejificha nyuma ya nyumba” “Wewe huko ulikuwa unafanyaje?” “Bosi ni vyema ukayasikiliza haya mazungumzo” Binti huyu akatoa simu yake akaweka upande wa sauti na tukaanza kuyasikiliza mazungumzo yao.
“Hakikisha kwamba chakula unakipika kama nilivyo kuambia” “Ila huoni inaweza kuwa hatari mkuu” “Wewe fanya hivyo kwa maana nahitaji na yeye aangamie” “Chakula atampelekea nani?” “Mimi mwenyewe, natambua hawezi kuchomoa nikimpelekea chakula” “Sawa bosi na niweke pilipili kwa mbali?” “Ndio kwa maana anapendelea sana pilipili” Mazungumzo yakaishia hapa, nikabaki nikimtazama binti huyu usoni na yeye akabaki akinitazama usoni mwangu.
“Bosi hapa kuna mpango wa kukuua wewe kupitia chakula, hicho ndio kitu kikubwa ambacho nimekifikiria kwa haraka haraka” Nikashusha pumzi nyingi sana, kwa maana uovu wa Hussein kwa sasa umeanza kudhihirika, na ninaimani kwa asilimia mia moja yeye ndio mtu wa pekee anaye nifahamu mimi vizuri sana kuanzia nilipokuwa masikini hadi sasa ni tajiri na pia ndio mshauri wangu mkubwa sana.
“Bosi ninakuomba chochote atakacho kueletea bosi Hussein usile watakuua bosi wangu” Binti huyu alizungumza kwa masikitiko makubwa sana, huku kwa mbali machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Unaitwa nani?” “Mariana” “Nashukuru Mariana, nitaandaa zawadi yako” “Nashukuru bosi, ila ninakuomba bosi wangu usile hicho chakula kwa maana bado ninakupenda” Safari hii Mariana machozi yalizidi kumtiririka usoni mwake.
“Usijali” Nilizungumza huku nikimfuta Mariana machozi kwa kiganja cha mkono wangu wa kulia, nikaondoka eneo hili huku nikurudi kwenye jamvi nilio kuwa nimekaa.
“Erick” Hussein aliniita hata kabla sijakaa kwenye jamvi hili.
“Ndio” “Chakula chako kipo tayari” Mapigo ya moyo yakanidunda kwa kasi sana huku nikimtazama Hussein usoni mwake, nikajikaza kutabasamu usoni mwangu. “Kilete hapa nile na rafiki zangu” Nilizungumza kwa sauti ya chini pasipo hata watu walio kaa kwenye jamvi kuweza kunisikia.
“Hapana Erick, kumbuka wewe ni mfiwa unatakiwa kula peke yako, hichi ni chakula cha wengi unaweza kujikuta haujashiba na sidhani kama siku ya leo umeweza kula tangu utoke Dar es Salaam” “Kweli sijakula, ila poa kipo wapi chakula?” “Tayari nimesha kiandaa mezani” “Twende” Nikamtazama Mariana kwa jicho la kuiba, nikamuona ni jinsi gani anavyo sikitika. Kabla ya kufika katika mlango wa kuingilia sebleni nikakutana na mkuu wa polisi.
“Hussein tangulia ninakuja” “Sawa muu” “Bwana Isaya ninakuomba” “Hakuna tabu mkuu” Nikazunguka na mkuu wa polisi nyuma ya nyumba, nikatazama eneo nililo simama naye kama lina usalama.Hapakuwa na dirisha wala mtu yoyote ambaye anaweza kutusikia.
“Ndio” “Ninaomba unipatie bastola yako” “Mkuu!!” “Fanya hivyo, natambua hili jambo ni la hatari ila tambua kwamba ninahitaji silaha yako kwa sasa” “Siwezi kukupatia kabla hujanieleza ni kitu gani ambacho unakwenda kufanya” “Unataka kupandishwa cheo hau hutaki?” Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama bwana Isaya usoni mwake. Akajifikiria kwa sakika mzima, taratibua kaichoma bastola yake kwenye sehemu alipo ichomeka. Nikaichomo magazine ya hii bastola nikakuta ina risasi za kutosha, nikairudisha kwa nguvu na kuikoki.
“Ila Erick hujaniambia unakwenda kufanya nini?” “Una hitaji kupandishwa cheo ndio maana ukanipatia hii bastola yako, ninakuahidi utapandishwa na kupewa hata ukuu wa mkoa, ila mambo mengine ninaomba uniachie mimi mwenyewe sawa” “Sawa mkuu” Nikaichome bastola kiunoni mwangu, nikaifunika vizuri pasipo mtu yoyote kuona. Nikaanza kutembea kuelekea ndani, nikamkuta Mariana akiwa amesimama mlango akinisubiria.
“Bosi ina maana unakwenda kula hicho chakula?” Mariana alizungumza kwa sauti ya chini sana huku akiwa amenisogelea karibu sana kwa watu ambao wana hisia mbaya wanaweza kuhisi kwamba mimi na Mariana tuna mahusiano ya kimapenzi.
“Naomba simu yako” “Sawa” Mariana akanipatia simu yake. Nikaiingiza mfukoni na kuingia ndani, nikamkuta Hussein akiwa anapakua chakula chake kutoka kwenye poti. Sikuhitaji kumuonyeshea Hussein kwamba ninagundua jambo lilote katika mipango yake aliyo ipanga, nikaka kwenye kiti.
“Mkuu wa poolisi ameniambia kwamba hata wale wafanyakazi wa ndani nao wamekutwa huku milimani wakuwa wameuwawa” “Nini!!?” “Yaa wameuwawa, nao wameuwawa kabla ya bibi kuuwawa. Na muuaji ni mmoja sasa hapa tuna kibarua kikubwa sana cha kujua ni nani ambaye yupo nyuma ya mauaji haya yote” “Kweli kaka” “Je umeweza kupata taarifa kwa vijana wako hususiana na msako wa kumtafuta Rose?” “Hapana bado hawajanipa ripoti yoyote. Vipi nikupakulie chakula au unapakua?” “Ahaa nipakulie tu” Hussein akafungua hotpot jengine na kutoa viazi vilivyo ungwa vizuri na kunukia. Akaanza kunipakulia kwenye sahani, nikajikuta kimoyo moyo nikitamani kumuua Hussein kwani anahitaji kuniua mimi kwa chakula ninacho kipenda sana.
“Karibu bosi” “Asante ndugu, hivi unajua kwamba siamini kama bibi amekufa” “Ndio hivyo bwana kikubwa ni kumshukuru Mungu kwamba upo hai” “Ubwabwa wako umenona maharage” “Hahaa kama kawaida yangu, unajua ninapenda ubwabwa maharage” “Tubadilishane bwana, najisikia kula maharage” “TUBADILISHANEEE!!?” Hussein alizungumza huku macho yakimtoka, nikazidi kumkazia macho huku nikimtazama usoni mwake.
“Ndio tubadilishane” Nilizungumza huku nikimsogezea sahani ya viazi na nikaichukua shahani yake ya wali maharage huku usoni mwangu nikiweka tabasamu la kinafki.
“Vipi ndugu mbona umenitolea macho. Tule baba tuleee tuu” Nilizungumza huku nikiwa na tabasamu pana, nikamuona Hussein jinsi anavyo meza fumba kubwa la mate kooni mwake. Akachukua kijiko chake akachota kiazi kimoja na kukifikisha hadi karibu na mdomoni mwake, simu yak ikaita na kumfanya ashushe kijiko, akatoa simu mfukoni mwake, akaitazama vizuri kisha akasimama.
“Samahani basi naomba nipokee simu hii” “Sawa” Nilizungumza huku nikimtazama, nikamuona akielekea nje kwa mwnedo wa haraka. Alipo toka tu sebleni, nikanyanyuka na kutembea kwa mwendo wa kunyata hadi kwenye mlango, nikamchungulia, nikamuona akielekea kwenye maegesho ya magari. Hussein akaingia kwenye gari lake na taratibu akaanza kuondoka eneo hili. Nikatoka nje kwa haraka, nikamuoma Mariana akiwa amesimama akitazama gari la Hussen jinsi linavyo ondoka eneo hili.
“Umekula?” Mariana aliniuliza huku akiwa amenitolea mimacho.
“Hapana, twende kwenye gari” Nilizungumza huku nikimrudishia Mariana simu yake, tukaingia kwenye gari na kuondoka eneo hili kwa kasi na kuwaacha watu wakishangaa. Mlinzi kwa haraka akafungua geti na nikatoka nje na kufunga breki za gafla huku nikitazama ni wapi alipo elekea Hussein. Nikashusha kioo changu na kumuuliza mlizi kwa sauti ni wapi alipo elekea Hussein. Mlinzi akanionyesha kwa ishara tu kwamba jamaa amelekea upande wa kushoto. Nikachia breki na kuendelea kuendesha gari kwa kasi.
“Funga mkanda” Nilimuambia Mariana, akaanza kunifunga mimi mkanda wa gari kisha na yeye akaufunga. Nikaiona gari ya Hussein kwa mbali akikata kona ya kuelekea kwenye moja ya msitu mkubwa. Nikazidisha kasi ya gari langu, kwani ni lazima Hussein alipe kwa mauaji ya familia bibi yangu pamoja na wafanyakazi wa ndani ambao hawana hatia yoyote kwenye haya maisha na mbaya zaidi alimehitaji kuniangamiza na mimi.
“Bosi huku tunapo kwenda ni porini” “Unaogopa?” “Mmmmmm…….” Mariana alijibu kwa woga woga, nikaendelea kuendesha gari na kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo nilivyo zidi kumkaribia Hussein kwani gari langu lina uwezo mkubwa sana kuliko gari lake.
Nikaichomoa bastola niliyo ichomeka kiunoni mwangu na kumfanya Mariana kunitumbulia macho kwani hakutegemea kuona silaha hii ambayo ni adimu sana kwenye macho ya Watanzania wengi. Hussein akakunja kulia kwake kwa kasi ya ajabu sana na kunifanya na mimi nikunje huko huko, laiti kama gari langu ni bovu basi kwa kukunja huku kungetufanya tuanguke. Hussein akazidi kusonga mbele hadi kwenye moja ya nyumba iliyo jengwa kwa mbao. Gafla risasi zikaanza kurindima kwenye gari letu na kutufanya sote tuiname chini huku nikiwa nimefunga breki kali. Mariana akaanza kupiga kelele kwa woga mwingi kwani shambulizi hili hakuna aliye litarajia. Kitu nilicho kigundua ni uimara wa hili gari kwani kioo chake cha mbele wala sehemu yoyote haiingizi risasi.
“Mariana Mariana Marana” Nilzungumza huku nikimumshika Mariana kwa nguvu mikono yake.
“Tulia na endelea kuinama sawa” Nilizungumza kwa ukali, Mariana akabaki akitoa macho. Nikaka sawa kwenye kwenye siti yangu. Nikawaona watu wanao tuvamia ni wawili na wanabunduki aina ya SMG. Nikaufungua mkanda wa gari langu kisha nikafungua mlango kidogo pasipo kushuka. Nikafyatua risasi mbili kwa kasi ya haraka sana na zikatua vichwani mwa watu hawa wanao tushambulia. Nikaufunga mkango wa gari kisha nikaanza kuingia eneo la hii nyumba huku nikiikanyaga miili ya watu nilio wapiga risasi, kisha nikalisimamisha nyuma ya gari la Hussein.
“Kaa ndani ya gari sawa” “Naogopa Bosi” “Mariana hii sehemu hakuna ambaye anaifuhamu, si wewe wala mimi sasa ninakuomba usishushe miguu yako kwenye gari umenielewa” Ilinibidi kuzungumza kwa ukali sana huku nikimtazama Mariana usoni mwake.
“Sawa bosi” “Wapigie simu polisi sawa” “Sawa” Nikashuka kwenye gari kwa umakini, nikaanza kulisogelea gari la Hussein, nikatazama kwa ndani sikuona mtu yoyote. Kwa umakini mkubwa nikarudi hadi kwenye maiti za watu nilio waua, nikachukua bunduki zote mbili. Nikarudi kwenye gari langu na kufungua, nikagonga kioo cha upande alipo Mariana, akashusha kioo.
“Chukua hii bastola atakaye kusogelea kama humjui wewe piga sawa” “Napijaje” “Unavuta hapa sawa” “Sawa bosi” Nikavaa mkanda wa bunduki moja na kuifanya ining’inie mgongoni mwangu. Kwa taratibu nikaanza kutembea kwa umakini huku nikiusogelea mlango wa hii nyumba. Nikakumbua tukio nililo tekwa na watu wa Jihad John katika kuivamia nyuma hivi hivi. Nikausukuma mlango wa hii nyumba kwa kuupiga teke zito na ukafunguka, nikajibaza pembeni kidogo huku nikiwa nimeishika bunduki hii.
Nikaingia ndani kwa umakini sana, nikatazama kila eneo la hii seble ndogo sikuona mtu yoyote, nikaanza kuchunguza chumba kimoja baada ya kingine huku nikiendelea kuwa makini sana. Nikasikia kurupushani kwenye mlango wa kutoke upande wa pili kwa haraka nikakimbilia katika mlango huo na kukuta mlango ukiwa wazi na watu wakikimbilia porini kwenye miti. Nikaanza kukimbia huku nikiwa makini sana na sikusita kutazama kuanzia juu ya miti hadi chini. Gafla nikasikia mlio wa bunduki, nikajikuta nikijibanza kwenye moja ya mti huku nikiheha sana na kuuchunguza mwili wangu kuanzia chini hadi juu.
“Erick my baby, muda wako umekwisha sasa, haku ulipo kuja huwezi kurudi au kutoka ukiwa hai. Ninakuomba tu utoke kwneye huo mti ulio jificha kwa maana nikiamua kukua ninaweza kukua muda wowote kianzia hivi sasa mpenzi wangu wa zamani”
Sauti ya Rose niliisikia vizuri masikioni mwangu akizungumza kwa kejeli sana jambo lililo nifanya niyang’ate meno yangu kwa hasira kumbe kwa kipindi chote nilicho kuwa ninaishi na Hussein kumbe alikuwa yupo chini ya Rose jambo ambalo ni baya sana kwenye maisha yangu hadi kwenye biashara zangu kwani Hussein ana siri nyingi sana za maisha yangu pamoja na kampuni yangu.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA “Erick my baby, muda wako umekwisha sasa, haku ulipo kuja huwezi kurudi au kutoka ukiwa hai. Ninakuomba tu utoke kwneye huo mti ulio jificha kwa maana nikiamua kukua ninaweza kukua muda wowote kuanzia hivi sasa mpenzi wangu wa zamani”
Sauti ya Rose niliisikia vizuri masikioni mwangu akizungumza kwa kejeli sana jambo lililo nifanya niyang’ate meno yangu kwa hasira kumbe kwa kipindi chote nilicho kuwa ninaishi na Hussein kumbe alikuwa yupo chini ya Rose jambo ambalo ni baya sana kwenye maisha yangu hadi kwenye biashara zangu kwani Hussein ana siri nyingi sana za maisha yangu pamoja na kampuni yangu.

ENDELEA
“Erick toka basi mume wangu tuyajadili, ninaimani unashangaa ni kwa nini ninafanya haya yote kwako si ndio?” Rose aliendelea kuzungumza na kunifanya, nitoe magazine ya bunduki hii niliyo ishika, nikakuta inarisasi tano tu. Nikairudisha magazine hii huku jasho likinimwagika japo ndani ya huu msitu huu kuna baridi kali.
“Rose” Niliita kwa sauti ya juu huku nikiendelea kujibanza kwenye huu mti.
“Nakusikiliza Erick” “Kwa nini umeyachagua maisha haya?” “Wewe ndio umenifanya niyachague maisha haya” “Mimi!!?” “Ndio Erick, wewe uliniacha nikifa pale hospitali ukaendelea na maisha yako. Ulitambua ni jinsi gani ninavyo kupenda na kukuheshimu. Ila haukulijahi hilo tena isitoshe wewe ndio ulinisababisha kuwa hapo hospitalini” Rose alizungumza kwa sauti ya juu ila iliyo jaa simanzi kubwa sana.
“Mama yako alinikataa kabisa kisa yule malaya wako uliye zaa naye, kweli? Tena alinifukuza kama mbwa nyumbani kwenu akidai kwamba nikuridia kufika nyumbani kwenu atanifunga so ni bora nifanye hichi ninacho kifanya ili hata kama atanifunga atanifunga kwa haki” “Rose hivi tunaweza kuyazungumza haya, hutambui ni jinsi gani ninavyo kupenda” “Acha uongo Erick” Nikasikia vishindo vya risasi vikipiga nyuma ya mti huu vikitokea upande walipo Rose na watu wake akiwemo Hussein.
“Ukirudia uongo wako nitawaruhusu watu wangu kukupiga risasi kwa maana hapo ulipo jificha hata ukitokea kidole basi watakipiga” Rose aliendelea kuzungumza maneno ya vitisho.
“Rose najua huwezi kuniua, na kama bado ninaishi moyoni mwako niue sasa hivi” Baada ya kumaliza kuzungumza maneno haya nikairusha bunduki yangu pembeni, nikaivua nyingine niliyoivaa kisha nikajitoa taratibu nyuma ya huu mti huku nikiwa nimeinyoosha mikono yangu juu. Kwa mara nyingine nikaonana na Rose uso kwa uso. Watu si chini ya ishirini wamemzunguka Rose pamoja na Hussein huku wote wakiwa na bunduki mikoni mwao. Japo ni jambo la hatari ninalo lifanya ila ninatambua kwamba siwezi kupambana na Rose akiwa na watu wote hawa ni bora kujisalimisha mapema kuliko kufa kwenye mapambano ambayo yananifupishia maisha yangu. Rose kwa ishara akawaamrisha watu wake wasilinipige risasi.
“Unatambua kwamba unashangaa kwa nini nimejishalimisha mikononi mwako, sijajisalimisha kwamba nimeshindwa kupambana na watu wako au na wewe. La hasa, nimefanya hivi kwasababu ya upendo wangu juu yangu. Ninakupenda sana Rose, japo umevuka mstari wa kuwamiza watu ninao wapenda ila ninaweza kukusamehe kwa hilo. Kumbuka tumetoka mbali, kumbuka ni mambo mangapi tumeyafanya tukiwa pamoja Rose. Leo hii utakubali kuona damu yangu inamwagika mbele yako tena mikono ya watu wako ambao hawakujuia ni wapi ulipo tokea” Nilizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa hisia kali za mapenzi. Nikamuona Rose akinitazama kwa macho yake ya upole ambayo siku zote nilisha zoeza kuyaona.
“Rose nilifanya juhudu za kukutafu, hata Hussein huyo hapo pembeni yako analitambua hilo. Nilivipa vinywaji vya kampuni yangu jina lako. Yote ni kwasababu ninakupenda Rose, ninakuhitaji, yaliyo wahi kutokea hapo nyuma mpenzi wangu ninakuomba tuyaache yapite” Nilizidi kuzungumza mameno ya ushawishi huku machozi yakianza kunimwagika usoni mwangu.
“Bosi huyu ni muongo tumuue tuondoke naye” Kijana mmoja alizunguma huku akimtazama Rose usoni mwake, Rose akamtazama jamaa huyo huku akiwa amekazia macho, akaachia msunyo mkali sana na kumfanya jamaa huyu kutulia tuli.
“Rose natambua kwamba unanipenda ila……” Sikuimalizia sentensi yangu, nikasikia milio ya risasi nyuma yangu na kumfanya mtu mmoja wa Rose kuanguka chini, kwa haraka nikageuka nyuma na kukuta kundi kubwa la polisi wenye risasi wakijipanga katika kufyatua risasi, nikalala chini nikamshuhudi Rose, Hussein na baadhi ya watu wakianza kukimbillia porini huku wengine wakiendelea kupambana na askari hao walio kuja kuniokoa. Sikuweza kunyanyuka kabisa chini kwani sijui ni nani ambaye anaweza kunipiga risasi. Watu wachache walio salioa nao pia wakakimbilia posini na kuwafanya askri kuzidi kusonga mbele.
“Mkuu mkuu” Nilisiisikia sauti ya bwana Isaya akiniita, nikanyanyuka huku nikimtazama usoni mwake.
“Vipi upo salama?” “Ndio nipo salama” “Hakikisheni munawakamata wote hap” “Sawa mkuu” Polisi wakazidi kusonga mbele na nikazidi kusikia milio ya risasi ikiendelea kurindima kwenye msitu huu. Nikamuona Mariana akija kwa kasi, akanikumbatia kwa nguvu huku machozi yakimwagika. “Nilikuwa nina hofu na wewe” Mariana alizungumza huku kichwa chake akiwa amekilaza kwenye bega langu.
“Nipo salama” “Inabidi murudi kwenye gari sasa” Mkuu wa polisi alizungumza, nikamshika mkono Mariana na kuanza kutemeba naye kuelekea lilipo gari, nikakuta polisi wengine wakiendelea kuimarisha ulinzi katika eneo hili.
“Mkuu unatakiwa tukurudishe sehemu salama kama jinsi muheshimiwa raisi alivyo seme” “Ina maana mulimuambia baba yangu?” Nilimuuliza mlinzi huyu nikiwa nimeshangaa sana kwa manaa endapo Rose atakamata na baba yangu nilazima atauwawa tu kwani tayari baba yangu alisha nipa jukumu la kumshuhulikia Rose.
“Ndio mkuu na amri hii imetoka kwa raisi anaye achia madaraka kesho kutwa tu” “Nani amemueleza?” “Mkuu” “Shitiii” Nilizungumza huku nikimuachia mkono Mariana
“Erick unakwenda wapi jamaani” “Tulia nina kuja” “Erick” “Muingizeni kwenye gari huyo” Nilizungumza huku nikielekea eneo niliuwepo, sikumkuta mkuu wa polisi, nikatambua kwamba ni lazima atakuwa amesonga mbele na vijana wake. Na mimi nikazidi kusonga mbele ili hata kama kuna jambo baya litampata Rose niwe tu wa kwanza kuweza kugundua hilo.
Nikisikia milio ya risasi ikitokea upande wa kaskazidi kwangu, na ikanifanya nizidi kusonga mbele huku nikiifwata milio hiyo ya risasi, japo ni msitu wa kutisha ila sikuhitaji kukata tamaa. Kadri nilivyozidi kusonga mbele ndivyo jinsi nilivyo zidi kuisogelea milio hii ya risasi.
Nikawaona askari wakiwa wamejibaza kwenye miti wakiendelea kujibizana risasi na watu wa Rose. Kusema kweli baba ana changamoto kubwa sana ya kupambana na ujambazi pamoja na ugaidi kwani watu hawa wa Rose unaweza kusema kwamba ni askari au wanajeshi wa kikosi fulani, kwani wanambinu zote za kijeshi na hata askari wenyewe wanaonekana kuelemewa na watu hawa.
“Mkuu unafanya nini huku” Mkuu wa polisi alizungumza huku akinitazama.
“Naomba bastola yako” “Ila hukupaswa kuwa hapa” “Tazama vijana wako wanavyo jeruhiwa unadhani kwamba unaweza kuwapata hawa majambazi hawa kirahisi, munamaliza tu risasi” “Baba yako alitoa agizo la wewe kurudishwa nyumbani kwako” “Yeye ndio aliye nituma kuwatafuta watu hawa, sasa naomba bastola yako na mimi nipambane” “Sawa ila kuwa makini sana kwa maana jukumu la kukulinda wewe ninalo mikononi mwangu” “Usiogope”
Mkuu wa polisi akanipatia bastola yake nyingine pamoja na magazine moja iliyo jaa risasi. Nikawatazama watu hawa wa Rose ni sehemu gani walipo jificha, nikalitazama eneo hili, nikatambua kwamba hapa kuna njia nyingine ambayo ninaweza kuwazunguka na kutokea nyuma ya hawa watu. Nikaanza kukimbia kwa kasi sana kwenye njia hii yenye vichaka.
Nikafanikiwa kutokea eneo ambalo ninawaona majambazi hawa kwa nyuma, ila katika kuwachunguza sikumuona Rose wala Hussein, kidogo nikajikuta nikipata amani moyoni mwangu, kwani bado ninahitaji kusawazisha matatizo yaliyopo kati yangu mimi na Rose kwa mazungumzo ya amani kabisa.
Nikaikoki bastola hii vizuri huku magazine ya ziada niliyo pewa nikiiweka mfukoni mwangu, nikaanza kumpiga jambazi mmoja baada ya mwingine na kuwafanya waanze kuchangayikiwa, walio kuwa wamejificha kwenye miti walijikuta wakijitokeza na wakawa chakula cha polisi hawa ambao wana hasira kweli kwani kuna baadhi yao wamejeruhiwa.
Ndani ya muda machache tukajikuta tukiwa tumewamaliza majambazi hawa. Taratibu nikaanza kulisogele eneo la majambazi huku nikiwa makini sana,
“Kazi nzuri bwana Erick” “Nanyi pia siku nyinyine uwafundishe vijana wako mbinu za kupambana na majambazi la sivyo watakufa” “Ninaweza kukuuliza swali?” “Uliza tu” “Umejifunza wapi mbinu hizi za mapambano?” “Nilikuwa katika kitengo cha NSS, ila kwa sasa nimeachana na hii kazi kwani ni hatari sana kwangu na familia yangu” “Ahaa kweli kweli, je **** majambazi wengine ambao wamekimbia kwa maana tulimuona mwanamke kati yao na katika hizi maiti hakuna maiti ya kike” Nikamtazama mkuu wa polisi usoni mwake kwa sekunde kadhaa, kisha nikatazama maiti hizi jinsi zilivyo lala ardhini.
“Musimtafute huyo msichana” “Kwa nini mkuu wakati ni jambazi ambaye angekuua” “Hajaniua na sihitaji askari wako wasonge mbele katika hili” “Hapana mkuu, mimi nimapokea amri kutoka ikulu kwanbta tumpate msichana huyo” “Kwanza ni nani aliye kuambia kwamba upige simu ikulu?” “Kwa sababu niliona upo katika hatari” “Ndio ukaamu upige simu” “Ndio” “Sasa ninakuambia sihitaji mwanamke huyo aweze kufwatiliwa sawa” “Siwezi kupokea amri yako kwa sasa, ninafwata kila alicho niagiza raisi wangu. Tusongeni mbele” Mkuu wa polisi alizungumza kwa kujiamini sana, vijana wake wakaanza kusonga mbele, ila kwa haraka nikamnyooshea bastola ya uso mkuu huyu wa polisi na kuwafanya vijana wake wote kuninyooshea bunduki zao.
“Nitakuua kabla ya baba yangu hajamuua msichana ninaye mpenda kwenye maisha yangu sasa kuwa makini katika hili kwa maana kumkamata kwake kupo mikononi mwangu na si kwako umenielewa” Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimemakazia macho mkuu huyo wa polisi na akabaki akitingisha kichwa huku mwili mzima ukimtetemeka kwani maneno yangu hakuna hata moja lenye mzaha katika hili swala.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
“Sasa ninakuambia sihitaji mwanamke huyo aweze kufwatiliwa sawa” “Siwezi kupokea amri yako kwa sasa, ninafwata kila alicho niagiza raisi wangu. Tusongeni mbele” Mkuu wa polisi alizungumza kwa kujiamini sana, vijana wake wakaanza kusonga mbele, ila kwa haraka nikamnyooshea bastola ya uso mkuu huyu wa polisi na kuwafanya vijana wake wote kuninyooshea bunduki zao.
“Nitakuua kabla ya baba yangu hajamuua msichana ninaye mpenda kwenye maisha yangu sasa kuwa makini katika hili kwa maana kumkamata kwake kupo mikononi mwangu na si kwako umenielewa” Nilizungumza kwa hasira huku nikiwa nimemakazia macho mkuu huyo wa polisi na akabaki akitingisha kichwa huku mwili mzima ukimtetemeka kwani maneno yangu hakuna hata moja lenye mzaha katika hili swala.

ENDELEA
“Wakusanye vijana wako na turudi tulipo toka”
Nilizungumza huku nikiishusha bastola yangu chini. Sikutaka kuendelea kusimama mbele ya mkuu huyu wa polisi, nikaanza kutembea kurudi kwenye nyumba ambayo Hussein alikimbilia. Sikuchukau muda mwingi nikafanikiwa kufika katika nyumba hii, nikawakuta Mariana na baadhi ya askari wakiimarisha ulinzi.
“Vipi umefanikiwa kumkamata Hussein?” “Hapana ametoroka, ila kuna baadhi ya majambazi ndio tume waua” “Haujaumia?” “Hapana sijauimia, ingia kwenye gari tuondoke”
Nilizungumza huku nikizunguka upande wa pili wa gari hili tulilo kuja nalo japo limejaa alama nyingi za risasi, ila sikuhitaji kuliacha kabisa. Ndani ya gari sikuzungumza kitu chochote zaidi ya kumfikiria Rose, kwa jinsi nilivyo muona kwa siku ya leo, upendo wake kwangu bado unaishi, japo usoni anazungumza na kujidhihirisha kwamba hanipendi ila macho yake yana dhihirisha kabisa ana nipenda.
“Bosi” “Ndio Mariana” “Pole kwa yale niliyo kueleza leo hukusiana na bosi Hussein” “Kuanzia leo sio bosi tena na wewe utakuwa msimamizi mkuu hadi pale nitakapo pata mtu sahihi wa kusimamia” “Aha…..bosi mimi sina elimu ya kusema ninaweza kuongoza kampuni?” “Sikiliiza Mariana, umefanya kitu kikubwa sana kwenye maisha yangu, japo hapo mwanzoni nilisha muhisi Hussein vibaya ila sikufikia katika hatua ya kumfikiria kwamba anaweza siku akapanga kuniua” “Pia kitu kingine ambacho ninataka kukueleza ni kwamba, hakuna shule wala chuo kinacho fundisha watu kuwa matajiri, shule sahihi kutaka kuwa tajiri ni moyo wako. Ukiamua, ukipenda kuwa tajiri basi unaweza kuwa. Kuna watu wanapenda kwa kusema kwamba wanahitaji kuwa matajri, ila ukitazama hawaonyeshi juuhudi yoyote ya kuutafuta huo utajiri baada ya hapo wanakazi ya kulalamikia kwamba serikali ni ngumu au wanalalamika kwamba maisha ni magumu.” “Kwa nini unaniambia hivyo bosi?” “Nimeona kitu kikubwa sana kwenye ubongo wako. Kitendo cha kuweza kurekodi japo mazungumzo ya Hussein na mpishi, ni akili ya kiwango cha juu. Kuna wengine wala wasinge weza kufanya hivyo na angekuja moja kwa moja kuniambia kwa maneno na kama ningekuwa sina hisia yoyote mbaya juu ya Hussein basi kwa sasa ungenikuta nikiwa katika wakati mgumu au nimesha kufa”
“Una uwezo wa kufanya kitu kikubwa kwenye maisha yako Mariana, nimekuamini katika hili” “Nashukuru bosi. Ila ninaweza kukuuliza swali?” “Uliza tu” “Una mke na mtoto?” Nikamtazama Mariana usoni mwake kisha nikamjibu kwa kutingisha kichwa kwamba ni kweli nina mke na mtoto.
“Hongera sana bosi” “Asante, vipi wewe?” “Mimi bado sijapata wa kuazaa naye” “Nakuombe kwa Mungu upate” “Nitashukuru” Tukafika nyumbani tukakuta ulinzi wa askari ukiwa umeimarisha. Sikuweza kulishangaa hili sana kwanini ninatambua kwa nafasi ambayo sasa hivi ninaishi, siishi tena kama Erick, ila ninaishi kama mtoto wa raisi.
Usiku mimi na wanakijiji waliofika katika msiba wa bibi yangu tukakesha, kuendelea kuomboleza huu msiba.
“Mkuu ninaweza kuzungumza na wewe japo kwa dakika” Mkuu wa polisi aliniambia, taratibu nikanyanyuka kutoka sehemu nilipo kaa na wafanyakazi wangu ambao wamesikitika sana kuweza kusikia kwamba Hussein ndio msaliti katika kampuni yetu.
“Ndio muheshimiwa” “Baba yako alituuliza kama tumempata binti huyo aliye nitajia kwa jila la Rose” “Ukamuambiaje?”“Akaniambia kwamba hilo swala atawaachia NSS, na hadi sasa hivi ninapo zungumza msako unazidi kuendesha Mkoa huu wote na hata mikoa ya karibu” Nikajikuta nikishusha pumzi nyingu huku nikijishika kiuono, kwani sina uwezo wa kumzuia baba yangu katika kuamua maamuzi yake kwania lisha nipa hata mimi kazi ya kuhakikisha kwamba ninampata Rose na kumuua tena akiwa na mume wake.
“Sasa sijajua hata cha kukusaidia katika hilo” “Usijali nitalichukulia uangalizi” “Sawa” “Ila mzee wangu samahani kwa kile nilicho kifanya muda ule, sikuwa mimi ila ni hasira tu ndio ilipelekea kufanya vile” “Nalitambua hili na wala hukupaswa kuniomba msamaha” “Hapana wewe ni mtu mzima kwangu, na ikitokea nimefanya kosa sinto jali kama mimi ni mtoto wa raisi, ila ni lazima niweze kuomba msamaha” “Tupo pamoja kijana, nitakufahamisha kwa kila hatua ambayo NSS, wamefikia kwa maana hata vijana wangu nao wapo porini wanaendelea kumtafuta binti huyo” “Sawa mkuu” Mkuuw a polisi akaondoka na kuniacha nikianza kumfikiria Rose tena.
“Bosi” Nilisikia sauti ya Mariana ikanifanya nigeuka, nikamkuta akiwa amesimama nyuma yangu huku ameshika koti kubwa.
“Nimekueletea koti naona baridi imezidi kuwa kali” “Nashukuru kwa kunijali Mariana” “Ni jukumu langu, nikutakie usiku mwema” “Nawe pia”
Mariana akaanza kutembea kuelekea walipo wasichan wezake, nikamtazama makalio yake makubwa kiasi jinsi yanavyo tingishika nikajikuta nikijikoholesha kidogo na Mariana akasimama. “Bosi vipi?” “Ahaa kidogo kifu kimenibana ila hakuna shida” “Sawa bosi” Nikarudi sehemu nilipo kuwa huku nikilivaa koti hili, nikaendelea kuzungumza mazungumzo ya hapa na pale na wafanyakazi wangu hawa. Asubuhi ikawadia na watu wakapata huduma ya kifungua kinywa kama kawaida. Nikaelekea kwa mkuu wa polisi kumuuliza kama kuna habari yoyote ambayo wameweza kuipata. “Hakuna jipya” “Basi kuna mtu ndani ya NSS, anaweza kunipatia taarifa ya kila kinacho endelea” “Sawa” Siku hii nayo ikapita huku watu walio toka mbali na hapa nyumbani wakianza kurudi makwao. Ila Mariana upendo wake wa kunifariji na kunishauri hakuupunguza kabisa, japo kwa wazi wazi alianza kudhihirisha kwamba ana hisia za kimapenzi dhidi yangu.
Siku ya kuapishwa kwa baba ikawadia, maelfu ya Watanzania wamekusanyika katika kiwacha cha mpira cha Mapinduzi. Seble mzima imejaa wafanyakazi wangu ambao bado nao wanaendelea kunifariji bosi wao huku wengine wakiahidi kunilinda. Tukashuhudia jinsi baba akiapishwa na jaji mkuu na kuchukua kiti cha uraisi kutoka kwa raisi ambaye muda wake kwa sasa umeshakwisha.
“Bosi ninaweza kuzungumza na wewe” Mariana alizungumza na kunifanya ninyanyuke kwenye sofa na kuanza kuongozane naye kuelekea katika chumba ambacho ninakitumia kama ofisi ya hapa nyumbani.
“Ndio Mariana” “Erick natambua kwamba upoa katika wakati mgumu wa kumkumbuka bibi yako, ila nina jambo ninahitaki kukuomba” “Niombe tu” “Ninakuomba ila basi….” Mariana alikatisha sentensi yake huku akianza kuelekea kwenye mlango, nikamuwahi kushika mkono wake, kwa haraka nikamvuta na kumsogeza karibu na kifua changu.
“Omba unacho hitaji kukiomba” “Bos…….” Sikutaka Mariana amalizie sentensi yake, nikaanza kumnyonya lispi zake, jambo lililo mfanya Mariana kulianika viongo vyake. Taratibu akaanza kuipitisha mikono yake kwenye shingo yake huku akizidi kuninyonya mdomo wangu kwa kasi. Nikaanza kumvua Mariana nguo zake
“Erick hii sio sehemu sahihi” “Unamuogopa nani, nyumba hii yote ni yangu” “Watu wanaweza kuingia humu ndani” “Hakuna mtu anaye weza kuingia” “Sawa” Mariana akazidi kuajiachia mwili wake, kila nilipo hitaji kumshika hakuwa na kipingamizi cha aina yoyote. Nikaendele kucheza na maziwa yake huku kwa mara kadhaa mikono yangu inashuka hadi kwenye makalio yake na kuyashika kwa nguvu huku nikiyaminya.
Simu yangu ikaanza kuita, jambo lililo tukurupusha katika zoezi la kuvuana nguvo zetu kwani tayari nilisha mvua Mariana shati alilo vaa na amebakiwa na suruali pamoja na sidiria.
“Samahani naomba kupokea samu” “Sawa bosi” Nikaipokea simu yangu na kuiweka sikioni mwangu.
“Halooo”
Niliita ila mpiga simu akaka kimya pasipo kuzungumza chochote.
“Halooo, ni nani mwenzangu ninazungumza naye?” Mtu huyu akaendelea kukaa kimya nikataka kukaa simu nikiamini kwamba mpigaji atakuwa amekosa namba kwani hii ni namba mpya kwenye simu yangu.
“Erick ni mimi” Nilisikia sauti ya Rose, nikamtazama Mariana kwa jicho la kuiba, nikamuona akiwa ananitazama mimi.
“Yap” “Erick natambu hii simu inaweza kuniletea matatizo kwenye maisha yangu, ila imenibidi kufanya hivi kwa sababu ya upendo wangu kwako” “Erick nina kupenda sana, sijawa hivi kwa ajili yako tu peke yako, ila umasikini katika familia yangu umechangia kwa mimi kuwa hivi, nimeishi kimasikini na mama yangu, sikuwa na jinsi zaidi ya kujitoa mimi sadaka kuifanya hii kazi” Rose alizungumza huku nikimsikia akilia kwa uchungu sana, jambo lililo nifanya nianze kulengwa lengwa na machozi.
“Erick, dhumuni la kukupigia hii simu, ni kukuomba msamaha kwa kile ambacho nimekifanya kwenye maisha yako, hata mimi pia nimekusamehe katika hili” “Kwa sasa najiandaa kuelekea karibu na eneo la uwanja wa Mapinduzi kwenye kuapishwa kwa baba yako. Kazi inayo nipeleka hapo naamini huto kuja kunisikia tena wala kuniona kwenye maisha yako na ninakuomba usihangaie kunitafuta kwani hii ndio simu yangu ya mwisho kwako” “Rose” Niliita huku machozi yakinimwagika usoni mwangu kwani nimeshindwa kuvumilia sauti ya unyonge aliyo nayo Rose.
“Erick usizungumze chochote, imekwisha sasa” “Rose niambie unakwenda kufanya nini?” “Natambua upo Lushoto na kama upo karibu na Tv ninakuomba usibanduke kwenye Tv, ndani ya dakika tano utaweza kuona kitakacho tokea” “Roseeeeee” Simu ikakatwa, kwa haraka nikaipiga namba ya simu Rose aliyo nipigia ila cha kushangaza nikaambiwa kwamba namba ninayo ipiga haipo. Nikajaribu kuipiga tena na tena ila jibu ni kwamba namba hiyo haipo. Kwa haraka nikatoka ofisi humu huku nikimuacha Mariana akivaa shati lake kwa haraka, hata anavyo niita wala sikuweza kuelewa. Wafanyakazi wangu wote wakanitazama kwani walisha anza kusikia sauti ya Mariana anavyo niita tangu nilipokuwa ninatoka chumbani. Macho yangu yote mawili nimeyaelekezea kwenye Tv kubwa iliyopo hapa sebleni kwangu.
“Bosi kuna nini kinacho endelea” Mlipuko wa bomu katika kiwanja hichi ukawafanya wafanyakazi wote ndani ya hii seble kushangaa, nikajikuta nikikaa chini na kuanza kuanguua kilio kikali kwani Rose amekwenda kujitoa muhanga wa kujilipuka katika siku ya kuapishwa kwa baba yangu.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
Nikajaribu kuipiga tena na tena ila jibu ni kwamba namba hiyo haipo. Kwa haraka nikatoka ofisi humu huku nikimuacha Mariana akivaa shati lake kwa haraka, hata anavyo niita wala sikuweza kuelewa. Wafanyakazi wangu wote wakanitazama kwani walisha anza kusikia sauti ya Mariana anavyo niita tangu nilipokuwa ninatoka chumbani. Macho yangu yote mawili nimeyaelekezea kwenye Tv kubwa iliyopo hapa sebleni kwangu.
“Bosi kuna nini kinacho endelea” Mlipuko wa bomu katika kiwanja hichi ukawafanya wafanyakazi wote ndani ya hii seble kushangaa, nikajikuta nikikaa chini na kuanza kuanguua kilio kikali kwani Rose amekwenda kujitoa muhanga wa kujilipuka katika siku ya kuapishwa kwa baba yangu.

ENDELEA
Mariana akawa na kazi ya kunibembeleza. Kwa haraka nikanyanyuka, nikaelekea chumbani kwangu na kumfanya Mariana kunifwata kwa nyuma.
“Erick Erick” Mariana aliniita huku akiendelea kunifwata kwa nyuma. Nikafungua kabati langu la nguo, nikachukua funguoa ya gari langu moja aina ya Aud A7.
“Unatakwa kwenda wapi na funguo ya gari?” “Naelekea Dar es Salaam” “Ukiwa katika hali hiyo ya majonzi utaweza kuendesha gari kweli” “Ninaweza” “Hapana Erick unanitania, haupo sawa na siwezi kukuacha uondoke ukapate matatizo” “Unanizuia wewe kama nani?” Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazam Mariana usoni mwake, cha kushangaza Mariana hakuogopa kabisa hasira yangu zaidi alicho kifanya ni kunisogelea kwa na kusimama mbele yangu.
“Ninazungumza kama mwanamke ninaye kupenda na kuyajali maisha yako kuliko kitu cha aina yoyote” “Mariana hunijui mimi, tafadhali ninakuomba unipishe” “Siwezi kukupisha” Nikamsukuma Mariana kwa nguvu kitandani, nikaanza kutembea kuelekea nje, watu wote sebleni wakanitazama, nikasimama kwa sekunde kadhaa huku nikiwatazama,
“Mariana atachukua nafasi ya Hussein hadi pale nitakapo rudi sawa” “Bosi unakwenda wapi?” “Hilo haliwahusu, nilicho zungumza ninaomba mukifwatake sawa” “Sawa bosi” “Jamani naombeni mumkamate Erick hayupo sawa jamani” Mariana alizungumza na kuwafanya wafanyakazi wangu wote wabaki wakimshangaa kwani hapakuwa na mtu aliye weza kufwata amri yake. Nikatoka nje na kuzuguka uwani kwenye banda kubwa la kuhifadhia magari, nikaingia kwenye gari langu na kuliwasha.
“Erick ninaomba twende wota kama huto jali siwezi kukaa hapa peke yangu na kukuona unaondoka ukiwa katika hali kama hiyo” Mariana alizungumza huku akiwa amesimama mbele ya gari hili, nikamtazama kwa nguvu huku nikiwa nimekanyaga breki, nikazima gari na kushuka.
“Niambie unataka nini kwangu?” “Nicho kihitaji kwako ni usalama wako tu, amani ya moyo wangu ninaweza kuitafuta hata kwa mtu mwengine” “Natambua kwamba unanijali, ila bado hujanijua” “Kwani wewe ni nani hadi useme sijakujua” Nikamshika Mariana mkono hadi kwenye chumba cha gareji kilichopo humu ndani, nikaufunga mlango kwa ndani na kuwasha taa, nikamsukuma Mariana hadi ukutani huku mkono wangu mmoja ukiwa umemkaba koo lake. “Nione nikiwa nimecheka, tabasamu na kufurahi, sijui ni watu wangapi wamefariki pale, unajua ni nani aliye weza kusababisha lile tukio kutoke eheee” Nilizungumza kwa hasira na kumfanya Mariana kutingisha kichwa huku sura yake akiwa amikunja kwa maumivu ya koo lake ninalo libana. “Aliye kufa pale ni mwanamke ninaye mpanda kwenye maisha yangu, mwanake niliye msababishia aweze kuonja harufu ya kifo kwa ajili yangu, mwanamke niliye aliye jiunga kwenye ugaidi kwa ajili yangu so wewe ni nani ambaye unajaribu kuzuia maamuzi yangu?” Nikamuachia Mariana koo lake na kumfanya aanze kukohoa kwani ni kwadakika kadhaa aliweza kukosa pumzi.
“Nimekuachia kampuni yangu iongoze katika njia inayo eleweka ukishindwa atachukua mtu mwengine umenielewa” “Sawa mkuu” Mariana alinijubu kwa sauti ya woga huku mwili mzima ukimtemeka. Nikatembea kwa haraka hadi mlangoni, nikataka kuufungua mlango, ila nikageuka na kumtazama Mariana aliye inama huku mikono yake akiwa ameshika magotini mwake. Nikarudi katika sehemua aliyopo, kwa haraka akanyanyuka na kunitazama huku akizidi kutetemeka.
“Ninakuomba unisamehe kwa hili lililo jitokeza” Mariana alishindwa kunijibu kwa woga, nikaupitisha mkono wangu wa kushoto kiuononi mwake, taratibu nikausogeza mdomo wangu karibu na lipsi zake jambo lililo mfanya Mariana kufumba macho yake. Nikaanza kumnyonya midomo yake, huku ulimi wangu ukiwa na kazi ya kupita kila sehemu katika kinywa chake. Nikafungua kifungo cha suruali yake aliyo ivaaa, nikaishusha chini kidogo, mkono wa kulia ukaanza kuchezea ikulu yake, jambo lililo mfanya Mariana kuanza kutoa miguno ya mahaba, nikaishusha chupi yake. Mariana naye akanza kufungua jinsi niliyo ivaa, akamalizia na boksa kabisa.
Hatukuwa na muda wa kuandaa, kazi ikawa ni moja tu, kuhakikisha kwamba jogoo wangu anakula kitumbua chake kisawa sawa. Mariana akazidi kutoa vilio vya mapenzi ambavyo nilianza kuhisia vinaweza kusikia nje, ikanibidi kumzima mdomo wake, ndani ya dakika kumi na tano tukawa tumemaliza mtanange huu wa kaukata kwa shoka.
“Asante mpenzi wangu Erick” “Asante nawe pia” Nikapandisha boksa yangu pamoja na suruali yangu. Mariana akanifuta jasho linalo nitiririka usoni mwangu kwa viganja vyake.
“Nakuahidi nitaongoza kampuni yako, na hakuna atakaye weza fanya ujinga kama alio ufanya Hussein” “Shukrani” Mariana alipo maliza kuvaa nguo na kujiweka sawa tukatoka kwenye chumba hichi.
“Kuwa makini huko barabarani” “Usijali” “Ila si ungeoga kwanza” “Muda ni mdogo” “Haya” Nikaingia ndani ya gari langu na kuondoka zangu katika eneo hili la nyumba, nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia mama, simu yake ikaita na haikupokelewa, jambo lililo anza kunipa mashaka makubwa, nikampigia tena, na ikapokelewa.
“Mama upo salama?” “Ndio mwanangu, familia nzima ipo salama. Tuliweza kuondolewa uwanjani na wana usalama wa taifa” “Asante Mungu” “Upo wapi kwa maana baba yako aliniambia kwamba upo kwenye kazi sasa umeimaliza?” “Sijaimaliza ila kwa sasa nipo njiani ninarudi Dar es Salaam” “Sawa ukifika utatupigia na nitakuambia kwamba ni wapi tulipo” “Sawa mama”
Nikakata simu na kuiweka siti ya pembeni. Safari ikazidi kusonga mbele na ikanichukua masaa matano kufika Dar es Salaam. Nikampigia simu mama na akanieleza ni sehemu gani walipo. Moja kwa moja nikaelekea hadi katika eneo hilo ambalo nikakuta ulinzi mkali wa askari pamoja na wanajeshi.
“Mimi ni mtoto wa muheshimiwa raisi”
“Onyesha kitambulisho chako” Mwanajeshi aliyopo getini aliniambia, nikatoa simu yangu na kumpigia baba.
“Baba nipo getini nimezuiliwa kuingia” “Mpatie simu huyo askari” Nikampatia simu mwanajeshi huyu, akaiweka sikioni mwake.
“Ndio” “Sawa mkuu” Akakata simu na kunirudishia simu yangu, wakanifungulia geti la kwanza, taratibu nikaingiza gari langu ndani, niaruhusiwa kupita katika geti la pili na la tatu la mwisho ambalo linalindwa na walinzi wa raisi mwenyewe. Nikasimamsiha gari kwenye magesho, nikashuka, mlinzi mmoja akanipeleka moja kwa moja hadi ndani.
Mama alipo niona kwa haraka akanyanyuka kwenye sofa alilo kaa na kunikumbatia kwa nguvu, huku machozi yakimwagika, Zari na Brian nao pia wakanifwata na kunikumbatia.
“Mupo salama” “Tupo salama mwanangu” “Mungu ni mwema” Nilizungumza huku nikiwaachia, nikamfwata baba sehemu alipo simama, nikampa mkono huku nikimtazama usoni mwake.
“Kazi imeanza” Baba alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Ndio baba wamevuka mpaka sasa, sio wakati wa kuweza kuwaangalia” “Ni kina nani hao?” Mama alituuliza huku akituzama, baba akaka kimya kwa dakika kadhaa na kunifanya nishindwe kulijibu swali la mama.
“Ninawauliza ni kina nani hao?” “Rose na kundi lake” “Rose! Rose yupi?” Nikamtazama Zari usoni mwake kisha nikamtazama na mama.
“Yule aliye kuwa mpenzi wangu.” “Weeee unataka kuniambia kwamba Rose yeye ndio anahusika na mpango mzima wa kulipuka kwa hili bomu?”
“Si bomu tu hili la kwanza yeye na mume wake ndio wamehusika katika matukio yote tangu kupindi kile chauchaguzi” Taratibu mama akaka kwenye sofa alilo kuwa amekalia huku akiwa ameshikwa na bumbuazi kubwa sana.
“Niliongea na mkuu wa polisi wa Lushoto akaniambia kwamba wameweza kuwaa majambazi wanao fanya kazi chini ya Rose” “Ndio, mimi ndio niliye fanikisha kuweza kuwaua. Baba nchi kwa sasa ipo kwenye hatari kubwa sana, Hakikisha kwamba unachagua watu walio sahihi, hakikisha kwamba jeshi la polisi linaongezewa mafunzo ya kupambana na hawa magaidi, pia vifaa na mishahara inakuwa ni pendekezo la kwanza.” Nilizungumza kwa kujiamini huku nikimtazama baba yangu usoni mwake.
“Sawa hilo nimekuelewa, ninaimani kwa sasa utakuwa mshauri wangu mkuu na wa mwisho katika kuiongoza hii nchi” “Baba, sidhani kama nitaweza kufanya hivyo, ila kuna mtu ambaye ninaimani anaweza kufanya hivyo” “Mtu, mtu gani?” “Dokta Benjamini, ningependa kwamba uweze kumuweka awe ni sekretari wako mkuu, yeye anaijua hii nchi na matatizo yanayo wakumba wananchi hususani kwenye swala la afya” “Unaweza kumpigia simu?” “Ndio”
“Fanya hivyo” Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia dota Benjamini, simu yake ikata kwa muda kidogo kisha ikapokelewa.
“Shikamoo dokta” “Marahaba Erick, habari yako” “Salama tu, dokta ninaomba moja kwa moja niende kwenye pointi yangu” “Ndio” “Kuanzi hivi sasa raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Bwana Almeida amekuteua kuwa sekretari mkuu wa ofisi yake, na kama una upo kazini hakikisha kwamba unaachana na hicho unacho kifanya na uniambie kwamba upo wapi mimi mwenyewe nitakuja kukuchukua hapo”
Ukimya wa sekunde kama ishirini ukatawala kwenye simu, nina imani kwamba daktari atakuwa yupo katika hali kubwa ya mshangao, kwani hii ni bahari njema kwake.
“Erick hembu acha utani wa usiku huu” “Wewe ni baba yangu mlenzi na wala sikuwahi kufanya utani na wewe, ninakuomba uweze kuniambia kwamba upo wapi nije kukufwata sasa hivi nyumbani?” “Nipo hospitali kwa sasa tunashuhulika na majeruhi walio lipuka katika mlupuko” “Basi sawa nipe nusu saa” Nikakata simu na kuirudisha mfukoni mwangu.
“Ila kwa nini umeamua kuniletea dokta Benjamini?” “Kama nilivyo kuwambia baba, mzee huyo anaweza kukusaidia sana katika kuiongoza hii nchi, wewe utakuw andio raisi umeingia madarakani kwa matatizo makubwa kama hili la leo. Na wamekufa watu wangapi?” “Hadi ripoti ya mwisho ninaletewa, wamefariki watu elfu moja na mbili” “Hiyo ni nje ya majeruhi?” “Ndio” “Umeona sasa baba, ila kuna kitu ninaomba nikuombe” “Zungumza tu” “Nahitaji kurudi NSS, nahitaji kukusaidia wewe nikiwa ndani ya hicho kitengo kwa maana kwa sasa hakuna mtu wa kumuamini, mtu wa pekee ni hii familia yako labda na daktari ninaye mleta. Watu hawa wanaiandamisha familia yetu na kuangamiza hii familia kwao ndio itakuwa ni ushindi sawa baba yangu” “Yote ni makosa yangu” Sauti ya mama ikatufanya sisi sote kumgeukia na kumtazama, mama akakaa kimya huku akiinamisha kichea chake chini.
“Kwa nini unazungumza hivyo mama?” “Laiti nisinge mkataa Rose na kumuambia maneno mabaya ya kejeli, nina imani haya yote yasinge tokea na wala asinge yafaya” “Hapana mke wangu, umefanya kile ulicho kifanya hakuna muda wa kujilaumu, ni wakati wa kupambana kuhakikisha kwamba tunalitatua hili tatizo” “Samahani kwa kuingilia mazungumzo yenu” Zari alizungumza kwa sauti ya upole sana.
“Zungumza” “Haya matatizo yanatokea kwa ajili ya mapenzi?” Sote tukaka kimya tukimtazama Zari kwani swali lake ni gumu kulijibu.
“Eti Erick, ni kwaajili ya mwanamke aliye kupenda?” Zari aliuliza huku machozi yakimlenga langa, mama taratibu akahamia kwenye sofa alilo kaa Rose, akamshika mikoni yake yote miwili.
“Hapana mwanangu, si kwa ajili yako wala kwa ajili ya mapenzi” “Baby ninawaomba mukazungumzie chumbani”
Nilimuambia Zari, taratibu wakanyanyuka na mama na kuelekea chumbani.
“Baba nitahitaji bastola ngoja niende kumchukua huyu dokta kwanza, mambo mengine tutayajadili. Ila hakikisha hutoi ujumbe wowote kwenye vyombo vya habari hadi nitakapo rudi” “Sawa” “Naomba nipatiwe bastola moja” “Umepata” Baba alizungumza, tukatoka nje pamoja, akamuita mlinzi wake ambaye anamuamini, akanipatia bastola iliyo jaa risasi.
“Kuwa makini huko uendapo” “Sawa baba” Nikaingia kwenye gari, nikageuza kwa haraka na kuondoka eneo la nyumba hii ya kifahari, safari ya kuelekea hospitali ya Muhimbili ikanichukua lisaa zima hii ni kutokana na foleni niliyo kutana nayo barabarni, moja kwa moja nikaelekea ofisini kwa dokta Benjamini. Nikamkuta akiwa anakusanya kusanya vitu vyake muhimu na kuviweka kwenye boksi.
“Erick ni surprise ya aina gani ambayo umenifanyia?” “Ndio hivyo naamini baba zangu wawili mukikaa sehemu moja basi munaweza kuhakikisha kwamba nchi inakwenda katika hali ambayo itakuwa ni sahihi” “Nashukuru sana kwa kuweza kunikumbuka katika ufalme wa baba yako” “Usinishukuru sana mimi, kikubwa ni kumshukuru Mungu kwani yeye ndio aliye nifanya mimi kuweza kukukumbuka” “Amen, ila ningeomba tuelekee nyumbani kwangu nikabadilishe nguo” “Sawa hilo halina shaka” Nikamsaidia kubeba boksi lake moja na kutoka nje, akaingia kwenye gari lake na mimi nikakingia kwenye gari langu. Tukafika nyumbani kwake majira ya saa tao kasoro usiku, tukapokelewa na Cesilia ambaye akaonekana kushangaa ugeni wangu usiku wote huu.
“Erick mbona hapa saizi” “Hapa ni kwetu mama yangu” “Mke wangu tumshukuru sana Erick, yaani hapa udaktari ndio kwa heri”
“Kwa heri kivipi?” “Yaani kuanzia hivi sasa mimi ndio nitakuwa mshauri mkuu wa raisi” “Waooooo” Cesilia kwa haraka akamkumbatia ume wake na kuanza kumpiga mabusu mengi mashavuni mwake.
“Baby niandalie suti kali niondoke na mwanangu” “Sawa baby” Cesilia akakibilia gorofani huku akishangilia kwa furaha sana. Doka Benjamini kwa mara nyingine akanipatia mkono wa shukrani.
“Utauyafanya maisha yangu kubadilika sasa” “Mungu ni mwema, kajiandae haraka baba yangu, muda hautusubiri, hapa raisi anakusubiria wewe” “Sawa mwanangu” Dokta Benjamini akaondoka, nikabaki nikiwa hapa sebeni nikitembea huku na kuele nikiwasubiria watoke, hawakuchukua muda mwingi wakashuka huku dokta Benjamini akiwa amevalia suti nyeusi na shati jeupe.
“Hapo baba yangu umependeza” “Etiee eheee” “Ndio”
“Yaaaa” Cesilia akanikonyeza na kuioyeshea ishara ya kunipigia simu pasipo dokta Benjamini kuona mwenyewe. Tukamuaga Cesilia na kutoka nje, tukaingia kwenye gari na kuondoka nyumbani kwake hapa.
“Naamini kwamba kuanzia kesho nyumba yako italindwa” “Nitashukuru sana” Tukiwa njiani kwa kioo cha pembeni nikaoga gari mbili aina ya Range Rover sport zikitugwata kwa kasi huku zikiwasha taa.
“Vipi?” “Kuna gari mbili zinatufwata kwa nyuma” Dokta Benjamini akageuka na kutazama nyuma.
“Ulimuambia mtu yoyote kwamba umeteuliwa kuwa mshauri wa raisi?”
“Ndio, ni madaktari wangu wawili ambao ni wasiaidizi ndio niliwaambia” “Sawa”
“Vipi kwani kuna ubaya?” “Nchi kwa sasa, hakuna mtu ambaye tunatakiwa kumuamini kwa maana kuna watu wanahitaji kuiteketeza familia yam zee kama unavyo jua” “Kweli sasa tunafanyaje kwa maana hizi gari zitatufwata kwa kasi” “Subiri uone” Nikafunga breki za gafla na kufanya gari moja kunipita na nyingine kusimama kwa nyuma ya gari letu, vioo vya gari la mbele vikafunguliwa watu waliomo kwenye gari hii wakatoa mitutu ya bunduki na kuanza kutushambulia gari letu kwa risasi.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
“Ulimuambia mtu yoyote kwamba umeteuliwa kuwa mshauri wa raisi?”
“Ndio, ni madaktari wangu wawili ambao ni wasiaidizi ndio niliwaambia” “Sawa”
“Vipi kwani kuna ubaya?” “Nchi kwa sasa, hakuna mtu ambaye tunatakiwa kumuamini kwa maana kuna watu wanahitaji kuiteketeza familia yam zee kama unavyo jua” “Kweli sasa tunafanyaje kwa maana hizi gari zitatufwata kwa kasi” “Subiri uone” Nikafunga breki za gafla na kufanya gari moja kunipita na nyingine kusimama kwa nyuma ya gari letu, vioo vya gari la mbele vikafunguliwa watu waliomo kwenye gari hii wakatoa mitutu ya bunduki na kuanza kutushambulia gari letu kwa risasi.

ENDELEA
Nikairudisha gari yetu nyuma kwa kasi huku nikiichomoa bastola yangu, nikaligonga gari lililo simama nyuma yetu. Ila gari likashindwa kurudi sana kutokana na gari lililopo nyuma yetu limetuzuia.
“Erick lete bastola yako” “Unaweza kutumia” “Ndi wewe lete tu” “Kazi yangu ni kukufikisha sehemu husika salama, chukua simu yangu umpigie baba ninahitaji msaada” “Kumbuka wewe ni mtoto wa raisi” “Hilo halijalishi ninacho kiangalia hivi sasa ni wewe kuwa salama sawa” “Sawa”
Nikashusha kioo cha gari na kuanza kujibu mashambulizi ya wat wa gari lililopo mbele yetu.
“Muheshimiwa tumevamiwa” Dokta Benjamini alizungumza huku akiwa ameinama kwenye siti yake.
“Tupo nyerere road gari mbili zimetuzuia tunaomba masaada wenu” “Shukrani muheshimiwa” “Wamesemaje?”
Nilimuuliza dokta Benjamini huku nikijitahidi kurudisha gari nyuma kwa kadri ninavyo weza, cha kumshukuru Mungu kioo cha mbele cha hili gari ni imara kwa kiasi fulani kwani hadi sasa hivi hakuna risasi iliyo ingia japo kimetengeneza nyufa nyingi sana.
Ving’ora vya gari za polisi vikaanza kusikika karibu na eneo hili jambo lililo wafanya watu hawa walio tuvamia kuwasha gari zao na kundoka, ili kuepuka kuingia mikononi mwa askari.
“Asante Mungu” Dokta Benjamini alizungumza baada ya kuona gari mbili za polisi zikisimama mbele yetu, askari wakashuka wakiwa na bunduki.
“Tokeni nje mikono ikiwa juu” Asakari mmoja alizungumza huku akiwa ametunyooshea bunduki yake.
“Tutoke” Nilizungumza huku nikifungua mlango wa gari, nikashuka huku mikoni ikiwa juu na bastola nimeiacha ndani ya gari. Dokta Benjamini naye akatoka ndani ya gari, askari wakatusogelea na kuanza kutukagua ili kuona kama tuna silaha au laa.
“Mimi ni Erick Alemeida mtoto wa raisi Almeida” “Una kitambulisho?” “Sina ila unaweza kuzungumza na raisi moja kwa moja kupitia simu yangu”
“Lete simu tuzungumze naye” “Ipo kwenye gari humo” “Ninayo”
Dokta Benjamini alizungumza huku akiwa amenyoosha mikono juu, askari mmoja akaichukua simu yangu na kunipatia. Nikampigia baba huku nikiwa nimeweka loudspeker ili kila mtu aweze kusikia.
“Erick vipi upo salama” “Ndio baba polisi wameweza kufika katika muda husika wamefanikiwa kutukomboa” “Ohoo asante Mungu, je walio wavamia wamekamatwa?” “Waliwahi kuondoka kabla ya polisi kuweza kufika japo wametushikilia”“Mkuu wao ni nani?” Tukatazamana na askari hawa, akasogea askari mmoja.
“Yupo hapa” “Muheshimiwa raisi” “Ndio, hakikisha munawafikisha hapa nilipo salama salimini” “Sawa muheshimiwa” “Maelekezo yote atawapatia kijana wangu” “Sawa muheshimiwa” Nikakata simu na kuiingiza mfukoni, hapakuwa na sakari mwenye maswali tena.
“Hii gari hatuwezi kwenda nayo”
Nilizungumza huku nikitoa bastoka yangu ndani ya hii gari, tukaingia kwenye gari za polisi na kunza kuridi katika jumba alilopo baba. Nikawa na kazi ya kuwaeleza askari hadi tukafika kwenye nyumba ilipo familia yangu. Moja kwa moja tukaingia ndani.
“Poleni sana”
Baba alizungumza huku akimpa mkono dokta Benjamini.
“Shukrani muheshimiwa” “Erick alinieleza uwezo wako katika hii kazi hii ambayo nimekuitia nina amini kwamba inaweza kwenda vizuri” “Muheshimiwa raisi kwa hilo wala usijali nitahakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa ndani ya serikali yako” “Nitashukuru sana. Dany umeweza kufahamu ni kina nani walio weza kukuvamia?” “Bado ila itakuwa ni watu ambao wnaafwatilia nyendo zetu kwa umakini sana” “Ukirudi NSS, hakikisha kwamba unaweza kufahamu ni nani wanao husika katika haya matukio mawili” “Sawa baba” “Erick samahani ninakuomba” Mama alizungumza huku akiwa amesimama kwenye mlango wa kuingilia katika seble hii, nikamsogelea mama hadi sehemu alipo simama, hakuzungumza chochote zaidi ya kutangulia na tukaingia kwenye chumba kimoja, ambapo tukamkuta Zari akiwa amekaa kwenye sofa.
“Brian yupo wapi?” “Amelala chumbani kwetu” Mama alinijibu huku akikaa pembeni ya Zari, nikaka kwenye sofa jingine linalo tazamana na sofa walilo kalia.
“Kuna maswali ambayo ninahitaji kukuhoji Erick” “Maswali ya aina gani mama?” “Utayasikia tu” Nikamuangalia Zari sura yake inaonekana hana furaha yoyote.
“Nataka kufahamu kwamba ndani ya moyo wako unampenda Zari mama Brian au kuna mwanamke mwengine unaye mpenda?”
Swali la mama likanifanya nishushe pumzi nyingi huku nikimtazama usoni mwake.
“Mam……” “Jibu ni ndio au hapana” “Mama naomba unisikilize kwanza. Mbona hilo jambo linaeleweka, ninampenda Zari sana kwa maana ni mke wangu mama wa mwanagu” “Kama unampenda nitahitaji ndoa yenu mufunge haraka iwezekanavyo” “Kwa nini mama unataka kuharakisha mambo ikiwa serikali ya baba bado haijatulia, tulikuwa njiani tu leo tukavaniwa na watu, nusu kufa. Hivi unahisi hiyo harusi itakamilika kweli” “Hilo mimi sihitaji kulisikia, na nimepanga arusi yenu itakuwa ni mwe ujao, na kwanza wala sinto hitaji watu wengini kuweza kufika katika harusi yenu sawa?” Nikajikuta nikishusha pumzi taratibu huku nikimtazama mama usoni mwake.
“Umezungumza na baba hili swala?” “Nitazungumza naye” “Sawa, kuna vitu ambavyo ninahitaji kuvishuhulikia” “Sawa” Nikanyanyuka na kutoka chumbani humu, swala la mama sikuhitaji kulifikiria sana kwani sihitaji kuumiza kichwa changu katika hili. Nikafika sebleni na kuwakuta baba na doka Benjamini wakiwa katika mazungumzo.
“Baba ninaweza kuzungumza na wewe kidogo?” “Sawa” Baba akanyanyuka na tukasogea pembeni kidogo.
“Baba mama amelete pendekezo la ndoa yangu na Zari kuweza kufungwa wiki ijayo…” “Wiki ijayo…..! Anafikiria nini?” “Sijajua anacho kifikiria ni nini, ila naomba akikuletea hili pendekezo kwa sasa uweze kulizuia wewe kama baba, kwa maana bado famili yetu haijawa katika usalama wa kueleweka” “Sawa nitafanya hivyo” “Kuna lipi jipya?” “Nimezungumza na mkuu wa NSS, nimemueleza kwamba unakwenda huko, pia wameniambia kwamba wameweza kumkamata gaidi mmoja ambaye wanaendelea kumuhoji” “Hoyo gaidi wamemlamata wapi?” “Ni kati ya hawa walio wavamia usiku huu” “Sawa, nitaekea huko” “Dokta Benjamini, nina imani kwamba utamsaidia baba” “Sinto kuangusha katika hilo” “Baba tutawasiliana” “Ila unatakiwa kupumzoka japo kidogo?” “Baba nitapumzika baada ya hili swala kuisha” “Sawa kuwa makini” “Nashukuru, ila sijakuja na gari nililo ondoka nalo” “Usijali NSS, wamekutumia gari kuja kukuchukua baada ya muda mchache watakuwa hapa” “Sawa baba” Nikarudi chumbani walipo mama na Zari,nikawakuta wakicheka kwa furaha, walipo niona wote wakaka kimya.
“Mama chumba chenu ni kipi, nahitaji kumuona Brian” Mama akanyanyuka kwenye sofa, nikaongozana naye hadi kwenye chumba chao, nikamkuta Brian akiwa amelala, taratibu nikaka pembeni yake huku nikimtazama vizuri Briana usoni mwake, taratibu nikaanza kuchezea nywele zake kwa kiganja cha mkono wangu wa kulia.
“Mwanake amakuazalia mtoto mzuri kiasi hicho, unatakiwa kumshukuru kwa kumuoa” “Hilo natambua mama ila kwa sasa kuna mambo tunatakiwa kuweza kuyawekea uangalizi” “Hayo ni mambo ya nchi na si mambo ya familia yangu, nikiwa kama first Lady natakiw akuhakikisha kwamba mkwe wangu hata nikitembea naye mbele za watu basi anajisikia vizuri akiwa na pete ya ndoa, sio ninamtambulisha ni mkwe wangu wa ndoa na hana pete kidoleni, utakuwa unaniangusha mwanagu” “Usijali hilo mama” “Yaani nina ndoto harusi yako ije kuwa ni harusi kabambe ambayo Tanzania haijawahi kutokea siu hata moja” “Sawa mama nimekuelewa” Mlango ukagongwa, akakingia Zari akiwa amejawa na furaha.
“Erick baba anakuhitaji” “Sawa” Nikatoka chumbani humu, nikiwa kwenye kordo Zari akaniita ikanibidi kusimama na kutazama nyuma.
“Erick natambua kwamab upo bize, ila samahani kama nitakuwa ninakusumbua” “Hunisumbui zungumza tu mke wangu” “Ninakupenda sana mume wangu, ninakuhitaji kwenye maisha yangu. Ninakuomba uwe makini sana katika hii kazi ya kumsaidia baba” “Usijali mke wangu” Nikamsogelea Zari na kumbusu mdomoni mwake kisha nikelekea sebeleni kumsikiliza baba.
“Ndio baba” “Gari limefika” “Sawa tutawasiliana, ila baba ninaomba mwanangu aweze kuwekewa ulinzi wa kueleweka” “Yule ni mjukuu wangu sinto weza kumfanya aingie kwneye mikono ambayo sio salama” “Nashukuru baba yangu”
Nikaagana na dokta Wiliam kisha nikatoka ndani hapa, nikakuta agent wawili wa NSS wakiwa wananisubiria kwenye gari, dafari ya kueleka makao makuu ya NSS, yakaanza.
“Gaidi muliye mkamata hadi sasa hivi amezungumza chochote?” “Hapana hajazungumza chochote”
“Anaye muhoji ni nani?” “Mkuu Jackline”
“Sawa” Hatukuchukua muda mwingi tukafika katika makao makuu ya NSS. Watu wote ndani ya hii hoteli wanafanya kazi kwa kuchacharika, kila mmoja anashuhulika katika kitengo chake.
“Erick” Nilisikia sauti ya Jackline akiniita kwa nyuma, nikageuka tukasalimiana kwa kupeana mikono.
“Za masiku?” “Salama tu” “Pole nasikia kwamba ulivaniwa njiani?” “Yaaa” “Ila tumefanikiwa kuwaua majambazi wengine na tumemkamata mmoja” “Yupo wapi?” “Katika chumba cha mahojiano” “Twende” Tukangozana na Jackline hadi kwneye moja ya chuma cha mahijiano, nikamkuta jamaa mmoja akiwa amefungwa pingu za mikononi na miguuni.
“Hadi sasa hivi amezungumza chochote?” “Hapana tumemuuliza kwa mahojiano ya kawaida, ila hajazungumza chochote” “Sijakuelewa yaani umemuahoji kawaida kivipi?” “Kama tunavyo hoji waalifu” “Hembu nifungulieni nikamuhoji” Niliuzumza huku nikimtazama mtuhimiwa huyu kutokea upande wa pili wa chumba hichi cha kusikilizia mahojiano ambacho tumetenganishwa na kioo kigumu ambacho mtuhumiwa hawezi kutuona sisi tulimo ndani ya hichi chumba.
“Erick huruhusiwi kuingia na silaha ndani ya chumba cha mahujiano” “Jackline ukifwata taratibu za kikazi huyu jamaa hawezi kuzungumza chochote sasa ninakuomba nifanye kazi yangu iliyo nileta hapa”
“Erick” “Jack hii ni amri ya raisi sawa” Jackline akatingisha kichwa kukubalina na mimi kishongo upande, nikaingia ndani ya chumba hichi ya mahojiano nikiwa na bastola yangu mkononi.
“Naamini aliye watuma aliweza kuwaonyesha hii sura yangu, ndio maana mulinivamia si ndio?” Mtu huyu akuzungumza chochote zaidi ya kuniangalia kwa macho yake yaliyo jaa wekundu wa bangi.
“Tukizungumza kirafiki, nakukikishia kwamba utaweza kuachiliwa na kuwa huru, ila ukileta ubishi nitahakikisha kwamba huondoki humu ukiwa hai” “Rafiki zangu wamekufa na mimi siogopi kufa” “Aahaa huogopi kufa ehee” Kwa haraka nikashika mkono wa kulia wa jamaa huyu na kukilaza kihanja chake kwenye meza hii ya chuma, nikaigandamiza bastola yangu juu ya kiganja na kufyatua risasi moja, jambo lililo mfanya jamaa huyu kulia kwa uchungu sana.
“Ni nani aliye waagiza muje kunivamia” Nilimuuliza kwa hasira huku nikiendelea kukandamiza jeraha la risasi niliyo mpiga.
“Rose Rose ndio mkuu wetu” Jamaa huyu alizungumza kwa sauti kubwa, ila kulitaja jina la Rose kukanifanya niweze kustuka kidogo kwa maana mtu anaye mzungumzia hapa tayari ni marehemu alijilipua na bomu masaa kadhaa yaliyo pita.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
“Aahaa huogopi kufa ehee” Kwa haraka nikashika mkono wa kulia wa jamaa huyu na kukilaza kihanja chake kwenye meza hii ya chuma, nikaigandamiza bastola yangu juu ya kiganja na kufyatua risasi moja, jambo lililo mfanya jamaa huyu kulia kwa uchungu sana.
“Ni nani aliye waagiza muje kunivamia” Nilimuuliza kwa hasira huku nikiendelea kukandamiza jeraha la risasi niliyo mpiga.
“Rose Rose ndio mkuu wetu” Jamaa huyu alizungumza kwa sauti kubwa, ila kulitaja jina la Rose kukanifanya niweze kustuka kidogo kwa maana mtu anaye mzungumzia hapa tayari ni marehemu alijilipua na bomu masaa kadhaa yaliyo pita.

ENDELEA
Taratibu nikajikuta nikiinyanyua bastola yangu kutoka kwenye jeraha la huyu jamaa.
“Rose amekufa, unanidanganya?” “Rose hajafa yupo hai na sasa anajiandaa kulipua bomu la nyuklia, katika eneo lenye watu wengi” “Bomu la nyuklia, wapi na saa ngapi?” “Sijui ila mpango wa kulipua bomu la nyuklia upo” Nikamtazama jamaa huyu kwa macho makali, sikuwa na haja ya kukataa kwa maana roho ya Rose tayari imesha chafukwa. Nikatoka katika chumba hichi na kukutana na Jackline pamoja na mkuu wa kitengo hichi cha usalama wa nchi wakiwa wananitaza. “Nahitaji muwasiliane na raisi haraka iwezekanavyo” Nilizungumza huku nikiwatazama kwenye nyuso zao.
“Sawa” “Mkuu ninaimani kwamba umeweza kusikia kwa masikio yako kwa sasa nchi ipo katika hali ya hatari, bomu ambalo Rose na watu wake wanakwenda kulilipua, litaipelekea nchi katika mtikisiko mkubwa wa kiuchumi na amani, tunacho takiwa kuweza kukifanya kwa sasa ni kuhakiksha kwamba tunaweza kupata bomu hilo” “Nimekuelewa bwana Erick” Tukatoka katika chumba hichi na kuingia katika chumba cha majadiliano.
“Mkuu raisi anawasubiria nyinyi” Jackline alizungumza huku akiwa amesimama pembeni ya simu iliyopo mezani. Tukaka kwenye viti vilivyo izunguka meza hii kubwa, huku kukiwa na askari wawili wa NSS.
“Ndio mumeweza kufanikiwa kupata kitu gani kutoka kwa huyo gaidi muliye mkamata?” “Muheshimiwa raisi, kwa hivi sasa tunavyo zungumza ni kwamba, gaidi ameweza kutueleza kuwa kuna bomu la nyuklia, litakwenda kulipuliwa na Rose katika sehemu yenye watu wengi ambayo hadi sasa hivi hatujaweza kuelewa ni sehemu gani” Mkuu wa NSS alizungumza kwa sauti ya kujiamini huku sote tukimtazama usoni mwake.
“Hamjaweza kujua ni lini na saa ngapi bomu hilo litakwenda kulipuliwa?” “Ndio muheshimiwa raisi, ila tunahakikisha kwamba tunashuhulika katika kutafuta ni wapi bomu hilo lilipo” “Hakikisheni munanipatia ripoti kila baada ya dakika kumi na tano” “Sawa muheshimiwa” “Muheshimiwa raisi” Nilimuita baba na kuwafanya watu wote kunitazama.
“Ndio Dany” “Ninaomba tuweze kupata msaada kutoka mataifa makubwa yenye uwezo wa upelelezi, kwa maana pasipo kufanya hivyo baba tutazidi kuiweka hali ya nchi katika wakati mgumu na tumekuwa tukisifiwa na mataifa makubwa duniani kwamba nchi yetu kwa sasa ni nchi ya amani, ila kwa sasa muheshimiwa raisi, nchi inawakati mgumu” Nilizungumza kwa msisitizo.
“Unashuri ni nchi gani ambayo tunaweza kupata msaada wa kiupelelezi na itawachukua muda gari hadi wao kuweza kuja Tanzania ikiwa gaidi yupo ndani ya hii nchi?” “Muheshenimiwa raisi msaada wa haraka ambao ninapendekeza kuweza kuupata ni kutoka nchini Marekani, tuombe waweze kutusaidia kutumia satelaiti zao katika kuhakisha kwamba tunapata sehemu husika lilipo bomu hili kwa maana kwa mtazamo wangu wa kawaida, satelaiti za Tanzania, magaidi hawa watakuwa wamesha zichezea na kila tunacho kiona sisi na wao watakiona na itakuwa ni nafasi yao nzuri katika kutuvamia na kutuangusha chini kabla ya sisi kuwaangusha” Watu wote ndani ya hii ofisi wakabaki wakinikodolea macho kwa manaa kitu ninacho kizungumza kinaendana na ukweli kabisa, kwani kama satelaiti zetu zingekuwa sahihi, basi tusinge vamiwa njini nilipo kuwa na dokta Benjamini.
“Nitajitahidi kufanya hivyo Dany” “Nitashukuru muheshimiwa raisi” Nikakata simu na kusimama kwenye kiti nilicho kalia. “Jackline Satelaiti zenu humu ndani zinafanya vipi kazi?” Nikamuona Jackline akimtazama bosi wake na wote wakabakiw akiwa na kigugumizi.
“Nini?” Niliwauliza huku nikiwa nimewatolea macho.
“Ahha satelaiti zenu ni ndani ya msaa manne sasa hazifanyi kazi, ila tunajitahidi kuzifanyia marekebisho ya kimtandao” “Mungu wangu, ndani ya masaa manne satelaiti hazifanyi kazi, na mumekaa kimya, au mumeripoti sehemu gani?” “Hakuna sehemu tuliyo ripoti ila tutahakikisha ndani ya muda mchache zinakwenda hewani?” “Jamani mimi sio mkuu hapa, na ni mgeni katika hii ofisi, ila ninacho waambia, tuache kuishi kimazoea, tuache kufanya kazi kimazoea. Nyinyi ndio watu pekee ambao munatakiwa kuhakiksha kwamba nchi inakwenda katika hali ya usalama, matukio yote ya kigaidi nyinyi munatakiwa kuwa wa kwanza kuweza kuyagundua. Ila kwa mfumo huu munao kwenda nao, nchi kila siku itaendelea kuingia katika majanga kwa ajili ya uzembe wenu” Nilizunumza kwa ukali kidogo, huku nikimtazama Jackline na bosi wake.
“Ila Erick pasipo kukuvunjia heshima, tazama kinywa chako unapo zungumza kumbuka kwamba mimi hapa ndio mkuu wa hichi kitengo, hata kama baba yako ni raisi, ila hatufanyi kazi kutokana na kuharakishwa, utafwata taratibu na kanuni zilizopo ndani ya hichi kitengo” Taratibu nikaanza kumsogelea mkuu huyu wa NSS, huku nikiwa nimemkazia macho yangu, nikasimama sentimita chache mbele yake.
“Kwa ujinga wenu, uzembe wanu, upumbavu wenu maelfu ya watanzania leo wamepoteza maisha katika mlipuko wa bomu, na nyinyi hadi sasa hivi hamuelewi cha kufanya, na unahisi hapa kuna utaratibu gani wa kufwata ikiwa gaidi kama yule munamuhoji kama bwana harusi aliye mpa talake mkewe?” Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimeyang’ata meno yangu, mkuu huyu wa NSS, akabaki akiwa amenikazia macho.
“Siringii kuwa mtoto wa raisi, ila ninafanya kazi kuhakikisha kwamba nchi yangu inakuwa katika hali ya usalama, na yoyote atakaye kwenda kinyume na usalama wa nchi yangu, nitahakikisha kwamba ninamuangamiza. Umenielewa” Mkuu huyu wa NSS, hakuzungumza chochote zaidi ya kuendelea kunitazama kwa macho ya dharau. Nikatoka katika chumba hichi huku Jackline akinifwata kwa nyuma.
“Erick” “Ndio” “Pasipo kumkazia huyu jamaa, hili bomu linaweza kwenda kulipuka na lawama zote zitakuja kwetu” “Kwani kwa kipindi chote munafanya fanya kazi?” “Yaani kazi inafanywa kizembe, wasichana karibia wote hapa ametembea nao. Yaani humu kuna danguro dogo na ninaimani katika swala la satelaiti kuna kitu kitakuwa kimefanyika hapo” “Una uhakika?” “Ndio kwa maana kabla ya mlipuko wa eneo la uwanjani satelaiti zilizima, baada ya mlipuko zikarudi, basi tukajua labda magaidi watakuwa wame zihark lakini hapakuwa na mtu wa kuulizwa” Jackline alizungumza kwa sauti ya chini huku kwa macho ya kuiba tukimtazama jamaa huyu akiwa amesimama kwenye moja ya meza akimuelekeza jamaa mmoja kitu cha kufanya kwenye computure yake.
“Kwani anaitwa nani?” “Anaitwa Kasimu Danga” “Kasimu Danga?” “Ndio” “Naomba unipatie maelezo yake kuanzia elimu yake na baadhi ya ofisi alizo weza kuzipitia” “Sawa twende kwenye meza ile pale” Jackline alizungumza huku akinionyesha meza iliyo na computer kubwa, tukatembea kwa mwendo wa haraka hadi tukaifika, Jackline akaka kwenye meza hii na kuanza kumimnya minya batani za computer hii. Haikuchukua hata dakika moja tukaanza kuyasoma maelezo ya Kasimu Danga. Amepitia hatua karibia zote za elimu, pia amepata mafunzo kwenye chuo ambacho mimi na Jackline tumepitia, amefanya akazi katika vitengo tofauti tofati vya usalama ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
“Mbona CV yake ipo vizuri?” Nilimuuliza Jackline huku nikimtazama usoni mwake.
“Sijajua kwa kweli?” “Hakikisha kwamba tunamfwatilia nyendo zake” “Sawa” “Simu zake unaweza kuzi hark, tukawa tunazifwatilia?” “Hilo ni kosa lakini Erick?” “Tunaishi kwa mazoe, acha mazoea, baba yangu hana hata siku katika kuapishwa ila nchi kwa mwendo huu, unahisi ataweza kuiongoza?” Jackline akaka kimya kwa sekunde kadhaa huku akinitazama.
“Fanya hivyo sawa, kila kitu kibaya kikitokea mimi nitahusika katika kukijibu” “Sawa” Jackline akaanza kiminya minya batani za hii computure, kitu ninacho kipenda katika utendaji wa kazi wa Jackline ni umakini mkubwa sana na ana uelewa mkubwa sana kwenye maswala ya kimtandao kwa manaa yeye ndio aliye weza kunisaidia katika kugundua ni nani mhusika aliyekuwa amemteka mwanangu Brian.
“Niunganishe kwenye simu yako?” “Ndio” “Nitajie namba” Nikamtjia namba Jackline kwa haraka akaiingiza, kisha akaninyooshea kidole gumba cha mkono wa kuliaa akiniashiria kwamba kazi tayari imesha kamilika. “Simu, meseji zote zitakazo ingia kwake basi hata kwako zitaingia” “Sawa nashukuru, ila hato gundua?” “Hawezi ujuzi nilio utumia hapa hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kuugundua” “Safi”
Nikaanza kumtafuta Kasimu Danga katika hili eneo, ila sikumuona. Mtetemesho wa simu yangu niliyo iweka mfukoni, ukanifanya niingize mkuno wangu mfukoni na kuitoa.
“Kuna mtu anampigia” “Ngoja apokee” Kasimu Danga alipo pokea tu simu yake na mimi nikaipokea yangu na kuweka sikioni.
“Nimekuta missed call yako Kasimu” Niliisikia sauti ya Rose, jambo lililo nifanya nishushe pumzi taratibu huku nikimtazama Jackline usoni mwake.
“Mambo sio mazuri, uliniambia utahakikisha kwamba munamuua Erick, ila mumeacha hadi kwa sasa amenikaribia” “Danga, Danga, nyoosha maelezo kidogo. Amekukaribia kivipi?” “Ninavyo zungumza hivi sasa Erick yupo ofisini kwangu, na amelete sera yake ya satelaiti kushuhulikiwa haraka iwezekanavyo na pia amemuomba baba yake waombe msaada Marekani, sasa Rose hili swala kwa sasa linakwenda kuniwia ugumu” “Danga hakikisha Erick wala mtu yoyote anagundua kwamba wewe ndio unahusika katkka kutoa taarifa ndani ya kitengo cha NSS” “Sawa bosi, na bomu munakwenda kulilipua saa ngapi kwa maana nahitaji muda huo niwe nje kabisa ya Dar es Salaam” “Nitakuambia muda husika mume wangu akirudi, ila hakikisha kwamba Erick unadhibiti kwa kila hali” “Sawa nitafanya hivyo na akizidi mpaka, nitampiga risasi afe” “Usimuue kwanza” “Kwa nini usimuue” “Elewa kwamba usimuue, katika hilo sihitaji unihoji maswali” “Sawa bosi badae” “Poa” Simu ikakatwa, nikaishusha simu yangu na kurudia tena kumtafuta Danga ndani ya hilu eneo, ila sikumuona.
“Amesemaje” “Danga ndio msaliti amewasiliana na Rose, hembu jaribu kuitafuta hii namba kwa setelaiti” “Umesahau muda huu, hazifanyi kazi” “Shitiiii, nyayuka tunatakiwa kumkamata Danga, yeye ndio atatoa eneo la wapi alipo Rose” “Erick ni mapema sana” “Mapema wapi wakati hapa anampango wa kuniua” “Unasema!!?” “Umenisikia Jackline, yeye ndio ameweza kuhisika pia katika swala la kunivamia njiani sasa nahitaji tumtafute sawa” “Sawa”
Jackline akasimama kwa haraka, kabla hatujapiga hata hatua, tukamuona Danga akitoka ndani ya lifti huku akiwa na tabasamu pana usoni mwake. Nikataka kumfwata ila Jackiline akanishika mkono.
“Niachie” “Huu sio muda sahihi?” “Kwa nini?” “Najua cha kufanya” “Jackline nimekuambia kwamba sihitaji kufanya kazi kimazoea, so ninahitaji kumshika sasa hivi” Jackline akakaa kimya baada ya kumuona Danga akitufwata katika sehemu tuliyo simama.
“Satelaiti zinakwenda kuwa hewani baada ya dakika moja, tumejitahidi kadri tuwezavyo” “Sawa mkuu” Jackline aliwahi kujibu kabla hata sijafungua kinywa changu.
“Sawa Erick kazi kwako” Danga alizungumza huku akigeuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kudunda na ulio jaa nyodo nyingi.
‘Hanijui’
Nilizungumza kimoyo moyo, kwa haraka nikachomoa bastola yangu na kumtandika Danga risasi ya paja, na kumfanya aanguke chini na watu wote ndani ya hichi chumba wakabaki wakishangaa huku wengine wakiwa wamejawa na na hofu kubwa kwenye nyuso zao.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
Jackline aliwahi kujibu kabla hata sijafungua kinywa changu.
“Sawa Erick kazi kwako” Danga alizungumza huku akigeuka na kuanza kutembea kwa mwendo wa kudunda na ulio jaa nyodo nyingi.
‘Hanijui’
Nilizungumza kimoyo moyo, kwa haraka nikachomoa bastola yangu na kumtandika Danga risasi ya paja, na kumfanya aanguke chini na watu wote ndani ya hichi chumba wakabaki wakishangaa huku wengine wakiwa wamejawa na na hofu kubwa kwenye nyuso zao.

ENDELEA
Nikaanza kumsogelea Danga huku nikiwa nimeishika bastola yangu kwa umakini mkubwa. Kwa haraka nikaic homoa bastola ya Danga kiunoni mwake, kisha nikamsimamisha kwa nguvu.
“Jackline tunahitaji kumpeleka Danga chumba cha mahojiano” “Ila……” “Hakuna haja ya ila tangulia ukanifungulie katika chumba cha mahojiano.
“Sawa”
Tukaanza kuongozana na Jackline hadi kwenye chumba cha mahojiano. Nikamsukuma Danga chini, na kumfanya gaidi aliyomo ndani ya hichi chumba kupatwa na mshangao japo aneendelea kuugulia mamumivu yake.
“Ni wapi alipo Rose?” “Nilimuuliza Danga huku nikiwa nimemnyooshea bastola.
“Mimi sijui chochote jamani” “Acha unafki Danga ni muda mchache umetoka kuzungumza na Rose, na wewe ndio mtu wa pekee utakaye tuwezesha kufahamu ni wapi alipo Rose na kundi lake” “Una ushahidi gani kwamba nilizungumza na Rose” “Samahani mkuu nili hack simu zako” Rose alizungumza huku kimtazama Danga usoni mwake.
“Malaya mkubwa wewe, unahisi kunikamata mimi ndio mutazuia mipango ambayo imepangwa. Ni lazima baba yako ni lazima aweze kulipa kwa kila kitu alicho kifanya kwenye familia za mamia ambao wanamuwinda hadi kufa kwake” Nikabaki nikiwa ninamshangaaa Danga, nikatamani kumuuliza ni mambo gani ambayo baba yangu ameyafanya kwenye familia za mamia ya watu hao, ila nikashindwa kuzungumza chochote.
“Zungumza ni wapi bomu la nyuklia lilipo?” “Niuee tuu kwa maana wewe upo kama baba yako, hakuna tofauti yoyote kati yetu” Danga aliendelea kuzungumza kwa uchungu huku machozi yakimwagika usoni mwake. Nikashusha pumzi nyingi sana, nikaichomeka bastola yangu kiunoni.
“Niletee pingu” “Sawa”
Jacline akatoka chumbani humu.
“Baba yako ni gaidi, baba yako hata huo uraisi alio upata ameupata kwa kudhulumu roho za watu wasio na hatia na kuwaacha watu wengi wakiwa na machungu makubwa kwneye familia zao.” Danga aliendelea kuzungumza kwa uchungu huku akiendelea kumwagikwa na machozi usoni mwake. Sikuzungumza chochote zaidi ya kumkodolea macho huku nikikumbuka baadhi ya maagizo ambayo tayari baba alisha wahi kunipatia kuhusiana na kumuua Rose na mume wake.
“Unahisi baba yako ataweza kuishikilia hii nchi kwa miaka mitano, si wewe ambaye utaweza kuizuia harakati hizi kwa maana hata mtu wako wa karibu ni adui na baba yako” Maneno ya Danga yakazidi kunichanganya kichwa changu, Jackline akaingia chumbani humu akiwa na pingu, kwa ishara nikamuagiza amfunge Danga, ambaye hakuwa na ubishi wowote zaidi ya kukubali kufungwa mikono yake.
“Erick inabidi kumuita daktari kuja kumuhudumia, kwa maana damu nyingi itazidi kumtoka” “Like a father, like a son”(Baba kama mtoto)
Danga alizungumza maneno hayo huku akitabsamu na kunitazama usoni mwake.
“Nenda kamuite dokta” Jackline akatoa simu yake mfukoni, akapiga simu kwa daktari.
“Njooni chumba cha mahojiano” “Fanyeni haraka, na muje na akiba ya damu” Nikatoka chumbani humu nikiwa nimechoka sana, si mwili pekee bali hata akili yangu imechoka. Nikatoa simu yangu mfukoni na kumpigia baba. Simu ya baba ikaita baada ya muda ikapolekwa.
“Mumefanikiwa kupata taarifa yoyote ya wapi walipo maaduia” “Baba” Niliita kwa sauti ya unyonge sana.
“Ndio Erick vipi kuna chochote kibaya kinacho endelea” Nikanyamaza kimya baada ya kuwaona madaktari wakija kwa kasi, wakaingia katika chumba cha mahojiano, walipo ufunga mlango kwa ndani ndipo nikapata nafasi ya kuzungumza.
“Baba ni kweli kwa hichi nilicho kisikia?” “Umesikia kitu gani?” “Kuna mamia ya familia uliweza kuyaumiza katika harakati za kuupata uongozi wako” “Ni nani amezungumza ujinga kama huo” “Tafadhali baba, mimi ni mwanao ninakuomba unieleze ukweli” Nikasikia jinsi baba anavyoshusha pumzi zake nyingi.
“Baba niambie ukweli, la sivyo hii kazi sinto weza kuifanya kabisa baba yangu, nipo radhi niondoke na mwanagu tukaishi mbali na Tanzania, kwa maana kila mtu ni adui yako. Niambie ni nini ulikifanya baba yangu?” Nilizungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Ukimya ukatawala kwa dakika kadhaa kwenye simu, si mimi wala baba aliye zungumza.
“Erick ninaomba mwangu ufanye hiyo kazi kwa ajili yangu. Ninakuomba tafadhali, baada ya hili tatizo nitakueleza kila kitu kinacho endelea” “Baba nitaweza kufanya hii kazi ikiwa kila mtu ninaye mshika anadai wewe ni mkosefu. Tazama hata huyu mkuu wa NSS, ni adui yako anashirikiana na Rose bega kwa bega. Ikiwa watu ndani ya serikali yako ni maadui kwako, unadhani kweli nitaweza kuifanya hii kazi kwa amani?” Niliendelea kuzungumza huku machozi yakinimwagika. Mlango ukafunguliwa kwa haraka, akatoka Jackline na kusimama mbele yangu huku akionekana kuwa na wasiwasi mwingi, nikajifuta machozi yangu, na kumruhusu kwa ishara azungumze kitu kilicho mfanya kuja kusimama mbele yangu.
“Mkuu Danga amejiua?” “Nini?” “Ndio” “Baba nitakupigia” Nikakata simu yangu na kuingia ndani ya chumba cha mawasiliano, nikamkuta Danga akiwa amelala chini, na mdaktari wakiwa wamesimama pembebi yake.
“Kuna nini kilicho tokea?” “Amekata kipande cha ulimi kwa meno yake na kukimeza, jambo lililo mpelekea kufariki” “Ameung’ata ulimi wake?” “Si kuung’ata tu bali aliukata na kuumeza kabisa” “Ohoo Mungu wangu!!”
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, daktari mmoja akamfungua Danga mdomo wake, kitu nilicho kiona kinaogopesa sana.
“Erick tumepoteza kila kitu”
Jackline alizungumza huku akinitazama usoni mwnagu, nikamatazama gaidi aliye kaa pembeni naye akiwa katika woga mkubwa sana. Nikamsogelea huku nikichomoa bastola yangu kiunoni.
“Ni wapi alipo Rose” “Erick” “Tulia Jackline?” Nilizungumza kwa ukali huku huku nikumzuia Jackline kwa ishara ya mkono kuto kusogea karibu na eneo nililo simma. “Si…s….fahamu jamani?” Gaidi huyu alizungumza huku akilia kwa uchungu sana.
“Utafahamu ni wapi alipo Rose” Nilizungumza huku nikimnyanyua kwenye kiti chake, nikaanza kumpiga na kitako cha bastola hii kwenye uso wake, huku hasira kali ikiwa imenitawala usoni mwangu.
“YUPOOOOO WAPIIIIII ROSEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE”
Nilizungumza kwa hasira na kumfanya Jakcline na madaktari hawa kunikamata kwa nguvu, Jackline akanipokonya bastola yangu, wakaitwa askari wengine wa NSS, wakanitoa katika chumba hichi kwa nguvu bila ya kupenda huku gaidi huyu nikimuacha akivuja damu nyingi sana.
“Niachieni”
Nilizungumza huku nikijaribu kujitoa kwenye mikono ya askri hawa, ila sikuweza kufanya hivyo kwa maana wamenishika kwa nguvu sana. Wakaniingiza kwenye moja ya ofisi iliyo tulia na wakanifungia humu peke yangu. Taratibu nikakaa kwenye kiti, huku mawazo yakidizi kunitawala kichwani mwangu. Nikatoa simua yangu mfukoni na kumpigia Zari.
“Upo wapi?” “Nipo nyumbani, mbona alfajiri hii” “Kwani kumepambazuka?” “Ndio vipi?” “Muandae Brian” “Nimuandae Brian” “Nimekuambia fanya ninacho kuambia muandae Brian na nitakuambia ni wapi uweze kumleta” “Ngoja basi nimuambie mama” “Nimekuambia wewe mwenyewe, kwa sasabu ni mama wa mwanangu sinto hitaji umuambie baba wala mama sawa” “Erick” Zari aliniita kwa sauti ya upole.
“Nini?” “Naomba uniambie ni kitu gani kinacho endelea” “Hili swala halikuhusu, wewe muammshe mwanangu, muandae na umlete nitakapo kuambia sawa” “Kusema kweli Erick sinto weza kufanya hivyo kabla hujaniambia ni kitu gani kinacho endelea” “Nitakuja kumchukua mwenyewe” Nikakata simu na kurudisha umfukoni, kwa hasira nikajikuta nikikinyanyua kiti kilichopo mbele yangu na kukipigiza mlangoni. Mlango ukafunguliwa na wakaingia askari wawili walio shika bunduki mikonini mwao.
“Nini?” Akaingia Jakcline akiwa kasi, akanikabidhi bunduki yangu pasipo kuangalia hali yangu kama nipo kwenye hasira au laa.
“Jengo letu limevamiwa, tunahitaji msaada wako” “Limevamiwa na kina nani?” “Hadi sasa hatujafahamu ila askari wanaendelea kupambana chini huko kuhakikisha kwamba maadui hawapandi juu” “Nipatie jakati la kuzuia risasi” Nilizungumza huku nikianza kutoka katika chumba hichi, masiko yangu yakatawaliwa na ving’ora vya vya tahadhari, wafanyakazi wa kawaida wote wamehifadhiwa katika chumba maalumu ambacho milango na kuta zake haziingii risasi. Askari mmoja akanikabidhi jaketi la kuzuia risasi, nilalivaa na kuifunga mikanda yake vizuri.
“Gorofa namba moja wamesha ichukua, tupo wapo gorofa ya pili na hapa lifti zote tumezifunga katika huduma ya kupanda, sisi ndio tunaweza kushuka” Jackline alizungumza huku akiwa ameshika tablet kubwa inayo onyesha video za kamera zinavyo chukua matukio katika gorofa namba mbili.
“Je juu hawajavamia?” “Kwa juu hawajavamia na timu ya askari zaidi ya ishiri wapo juu ya gorofa, hakuna helicopter ya maadui ambayo inaweza kutua” “Mumeweza kutambua wapo wangapi?” “Magaidi hawa walio tuvamia wote ni professional killers kwa manaa hata upambanaji wao ni tofauti kabisa na upambanaji wa mafunzo ya askari wetu, sasa sijajua uwezo wao ni upi?” “Tuangalie tutakacho fanya, tushuke chini?” “Ndio, hapa hakuna cha kufanya au unaogopa kufa?” Jackline akanitazama kwa sekunde kadhaa, akatingisha kichwa huku akinitazama usoni mwangu akimaanisha kwamba haogopi kufa.
“Inabidi tushuke chini, je kuna msaada wowote ambao muliomba kutoka katika jeshi lolote?” “Mawasiliano ya humu ndani yote yamekata” “Hadi simu za mkononi?” “Sijapata akili ya kuangalia simu za mkononi” “Ahaaaa…..” Nikatoa simu yangu nikakuta mtandao upo, nikampigia simu baba ikaita baada ya muda kidogo ikapokelewa.
“Baba jengo la NSS, limevamiwa, tunaomba msaada wa jeshi” “Tumeliona hilo Dany, kikosi cha wanajeshi kinafika hapo ndani ya dakika mbili au tatu” “Shukrani baba, ila waambie kwamba watu walio kuja kutuvamia ni wauji wenye uwezo kwa maana wana ujuzi mkubwa katika kunyofoa roho za watu” “Sawa nimetuma kikosi cha makomandoo” “Sawa baba” Nikakata simu, na kumgeukia Jackline.
“Hakuna haja ya kwenda chini kuna msaada wa makomandoo unakuja” “Sawa” “Ila kila mtu akae kwenye nafasi kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaye ingia katika jengo hili”
“Sawa, wote tawanyikeni kila mtu akae kwenye nafasi yake” Jackline alizungumza na kuwafanya askari wake wanao sikiliza amri yake kutawanyika. Mimi na yeye tukatafuta moja ya meza na kujificha huku sote macho yetu yakiwa kwenye mlango wa kuingilia katika gorofa yetu.
“Umesha wahi kukutana na ambushi kama hizi?” Nilimuuliza Jackline huku nikimtazama kwa jicho la kuiba.
“Hii kazi nitaacha kusema kweli” “Hahahaaa huwezi kuacha, hizi ndio changamoto zenyewe” “Yaani kusema kweli roho yangu ninaiona kabisa haina gerentii kwneye haya maisha ukitegemea kwamba sina mtoto hata mmoja ni jambo la kusikitisha kwa kweli” “Hahahaaa usijali huto kufa ila utaishi” “Mmmm kwa mfumo huu?” “Ndio kwa mfumo huu utaishi” “Mmmm kusema kweli ninaogopa Erick” Simu yangu ikaita, kwa haraka nikaichomoa mfukoni, nikaipokea kwa haraka na kuiweka sikuoni mwangu, pasipo hata kuangalia aliye nipigia ni nani.
“Tumekuja kuwasaidia sisi tupo gorofa ya kwanza tumesha safisha vizusi wote” Sauti ya mwanaume ilizungumza na kunifanya nimtazame Jackline usoni mwake.
“Ninazungumza na nani?” “Unazungumza na Lutenat Michael” “Umeagizwa na nani?” “Ni amri ya raisi” “Una uhakika na kitu unacho kizungumza?” “Ndio nina uhakika na kitu ninacho kizungumza” “Unacho hitaji sisi ni kufanya nini?” “Ni kufungua milango tuje ndani kuwasaidia” “Sawa” Nikakata simu na kunyanyuka nilipo jificha.
“Vipi?” Wanajeshi wamesha safisha gorofa ya kwanza wanacho kiomba ni sisi kufungua milango” “Utawaamini vipi?” “Nimewaamini kwa sababu hakuna mtu mwenye namba yangu?” “Rose hana namba yako. Huoni kama huu unaweza ukawa ni mtego?” “Unataka mimi nifanyaje sasa?” “Mpigie tena na nitaomba nizungumze naye” “Sawa” Nikaitoa simu yangu mfukoni na kumpigia Letenati Michael.
“Ndio Lutenati Michael mkuu wa NSS, mkuu msaidizi wa NSS, nahitaji kuzungumza na wewe” “Haloooo Erick, unahisi baba yako anaweza kutuzuia sisi, watu wote hawa wanakufa kwa ajili yako na tumekuja hapa kwa ajili yako tu, jisalimieshe la sivyo jengo zima tutakwenda kulilupua na bomu la nyuklia” Sauti ya Rose, ikanifanya nianze kutetemeka mwili mzima, huku nikimeza mate mfululizo na ninashindwa nizungumze kitu gani cha kumjibu Rose ambaye ndio anaye ongoza uvamizi wote huu katika makao makuu ya jengo la NSS.
ITAENDELEA
 
ILIPOISHIA
Nikaitoa simu yangu mfukoni na kumpigia Letenati Michael.
“Ndio Lutenati Michael mkuu wa NSS, mkuu msaidizi wa NSS, nahitaji kuzungumza na wewe” “Haloooo Erick, unahisi baba yako anaweza kutuzuia sisi, watu wote hawa wanakufa kwa ajili yako na tumekuja hapa kwa ajili yako tu, jisalimieshe la sivyo jengo zima tutakwenda kulilupua na bomu la nyuklia” Sauti ya Rose, ikanifanya nianze kutetemeka mwili mzima, huku nikimeza mate mfululizo na ninashindwa nizungumze kitu gani cha kumjibu Rose ambaye ndio anaye ongoza uvamizi wote huu katika makao makuu ya jengo la NSS.

ENDELEA
“Unahitaji nini Rose” Kauli yangu ikamfanya Jackline kustuka sana na kubaki akinitazama usoni mwangu.
“Ninakuhitaji wewe tu, wengine mimi siwahitaji, je upo tayari kuendelea kuona watu wako wakizidi kuangamia?” “Unaniahidi nikijikabidhi mikononi mwako utaacha watu wangu salama?” “Ndio itakavyo kuwa, ninakuahidi sinto mgusa mtu wako yoyote kama naye hato jaribu kunigusa” “Ok ninatoka sasa hivi” “Erick……!!” Jackline aliniita huku akinishangaa sana, sikutaka kusikiliza chochote zaidi ya kuanza kutembea kualekea kwenye lifti.
“Erick huwezi kujisalimisha mikononi mwa magaidi, kumbuka kwamba kupitia wewe wanaweza kumshinikiza baba yako kuachia madaraka ikiwa ndio kwanza amekabidhiwa ofisi” “Jackline hili swala ninakuomba usiingilie” “Hapana Erick ni lazima ulifikirie hili” Jackline aliendelea kuzungumza kwa msisitizo huku akijaribu kusimama mbele yangu. Nikaishusha simu chini pasipo kuikata.
“Jackline hivi unajua kwenye hili gorofa kuna watu wangapi. Hivi unafahamu ni askari wako wangapi ulio wapoteza hadi sasa eheeee?” “Hata kama Erick, jukumu langu ni kulinda taifa na wewe” “Unanilinda mimi kama nani, ikiwa bomu la nyuklia lipo kwenye hili gorofa” Nilizungumza kwa kufoka na kumfanya Jackline kubaki akinitumbulia macho.
“Ninatakiwa kuokoa maisha ya hawa watu humu ndani, na kuonkoa maisha karibia ya watu wa Dar es Salaam, unataka niwe mbinasi wa uhai niendelea kuona damu za watu zikizidi kumwahika eheee.?” Niliendelea kuzungumza kwa kufoka, Jackline akabaki kimya na kukosa cha kuzungumza. Nikaiweka simu yangu sikioni.
“Rose nahitaji kuingia makubaliano na wewe” “Makubaliano gani Erick?” “Ninahitaji bomu la nyuklia mulilo hitaji kulilipua, muweze kulikabidhi katika serikali” Ukimya ukatawala, na inavyo onekana Rose anafikiria juu ya jambo hili ambalo tunahitaji kulifanya.
“Sawa nimekuelewa bomu nitawapo maelekezo ni sehemu gani watakapo lipata” “Wapi na saa ngapi?” “Erick maelezo yote watayapata baada ya wewe kuwa mikononi mwangu hilo ndio chaguo la pekee ulilo bakiwa nalo” “Sawa” Nikaminya kitufe pembeni ya hii lifti, kikafunguka na nikaingia ndani, taratibu mlango ukaanza kujifunga na kumfanya Jackline abaki akiwa analengwa lengwa na machozi usoni mwake.
“Upo gorofa namba ngapi?” “Nipo chini kabisa sehemu ya maegesho hakikisha kwamba unashuka chini” “Sawa” Lifti taratibu ikaanza kushuka chini, sikumaliza hata dakika moja nikawa nimesha fika chini sehemu ya maegesho ya magari. Lifti ikafunguka, nikakutana na watu watano walio funika nyuso zao huku Rose akiwa amesimama katikati yao. Nikakata simu na kuitaka kuiingiza mfukoni, ila Rose akaniomba kwa ishara ya kuninyoshea mkono, taratibu nikaanza kutembea hadi alipo, watu wake wakanikagua na kuchomoa bastola yangu niliyo ichomeka kiunoni kisha nikamkabidhi simu Rose.
Rose akaipiga simu chini, ikachanguka changuka. Watu wake wakanishika mikono yangu na kunifunga pingu kwa nyuma na kuanza kutembea na mimi hadi kwenye gari mbili aina ya GVC, zenye rangi nyeusi hadi kwenye vioo vya pembeni. Nikaingia gari moja na Rose na safari ikaanza, ukimya ukatawala ndani ya hili gari huku kazi yangu ikiwa ni kumtazama Rose kwa macho ya kuiba.
“Kwa nini unafanya hivi Rose?” “Sababu ni baba yako, laiti ingekuwa sio baba yako wala haya yote yasinge tokea” “Hembu niweni wazi basi, mkuu wa NSS, naye anasema tatizo ni baba yangu, na wewe naye ndio vile vile. Hembu niambie kuna nini hap kakati?” “Usijali utajua” “Tafadhali Rose kama unahitaji kuniua, wewe niue mimi” “Erick tulia sihitaji kuzungumza na wewe” “Najua unahitaji kuzungumza na mimi na bado unanipend……” Nikastukia kitu kizito kikitua kichwani mwangu na kuyafanya macho yangu kutawaliwa na ukungu kiasia kisha giza zito likanitawala na sikujua ni kitu gani kinacho endelea katika eneo hili.
***
Mwanga mkali wa jua wa taa una nimulika machoni mwangu, ukaanza kunifanya nikitingishe kichwa changu taratibu ili kuhakikisha kwamba ninaona vizuri watu au sehemu niliyopo. Ila kusema kweli mwangu huu ni mkali sana, kwani hata mtu wa mbele yangu sikuweza kumuona.
“Nipo wapi?” Niliuliza huku nikijaribu kunyanyuka, ila nikashindwa kwani mwili wangu wote umefungwa kwenye kiti chini nilicho kalia. Huku pia mikono yangu imefungwa na kukazwa vizuri tu. Cha kumshukuru Mungu taa hii ikazimwa, taratibu sasa nikaanza kuona watu walio simama katika hili eneo. Watu wote nyuso zao zimezibwa na vitambaa vyeusi kasoro watu wawili ambao ninawafahamu vizuri sana. Nikamkazia macho mume wake Rose, aliye shika kisu kikubwa mkonini mwake, huku akijipiga piga kwa kutumia ubapa wa kisu hichi katika kiganja cha mkono wake wa kushoto. Kamera zaidi ya nne zimenielekea kwangu, na zote zinanirekodi mimi, nikajichunguza na kujikuta nikiwa na bukta tu ya ndani na nguo zote wamenivua.
“Ni kitu gani munacho kihitaji?” “Hukumu”
Mume wa Rose alizungumza kwa sauti nzito sana.
“Siogopi kufana, kama munahitaji kuniiua niueni tu, wala hakuna haja ya kunirekodi ili dunia nzima ione kwamba nyinyi ni magaidi wakubwa na mutakwenda kutangazwa kama walivyo kuwa wanatangazwa kina Osama Bin Laden” Nilizungumza kwa kujiamini sana huku nikimkazia macho mume wa Rose.
“Hahahahaaaa. Baba yako yako ndio anatakiwa kukumbana nah ii hukumu” “Hivi unahisi baba yangu ni mjinga sana wa kukubali kujisalimisha mikononi mwenu kirahisi hivi. Baba yangu ni raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, hawezi kufanya upumbavu” “Eti eheee” Mume wa Rose akavaa kitambaa cheusi na kuficha sura yake, taa kubwa ikawashwa na ikaanza kunimulika tena usoni mwangu. Mume wa Rose akaanza kunipiga ngumu mfulizo za sehemu mbalia mbali ya mwili wangu. Maumivu makali yakazidi kutawala kila kona ya mwili wangu, sikuwa na jinsi ya kufanya zaidi ya kutoa miguno ya kuugulia kwa maumuvu. Jamaa akanishika nywela zangu na kuzivuta kwa nyuma.
“Raisi Almeida, hivi ndivyo mwanao atakavyo zidi kuteseka teseka siku hadi siku. Tunacho hitaji ndani ya masaa ishirini ni wewe kujisalimisha mikononi mwetu” Nikaanza kucheka kwa dharau sana, jambo lililo mfanya mume wa Rose kunitandika kofi zito la uso.
“Baba, achana na hawa waseng** ogoza nchi, hata nikifa nitakufa kwa jili ya hii nchi” Mume wa Rose akachomoa kisu chake na kutaka kukipitisha shingoni mwangu, ukelele wa Rose ukamfanya sitishe.
“Nini au kwa sababu alikuwa ni mpenzi wako?” Mume wa Rose alizungumza kwa ukali huku akimtazama Rose
“Muda wake bado” “Bado bado hadi saa ngapi, kejeli kama hizi sikuwahi kufanyiwa na mjinga mjinga yoyote tangu kuzaliwa kwangu” “Natambua hilo ila tumpe muda baba yake atakuja” Mume wa Rose akanitazama kwa nguvu akakisukumia kichwa changu pembeni, mume wa Rose akaondoka eneo hili na taa ikazimwa.
“Upumbavu wa kumuonea huruma huyu mjinga mimi siuhitaji” “Kama ningekuwa ninamueonea huruma nisinge mleta mikonino mwako” Rose alizungumza kwa ukali huku akimtazama mume wake usoni mwake. Mume wake akanigeukia kwa jicho kali kisha akatoka katika chumba hichi.
“Mpelekeni sero” “Sawa mkuu” Rose akaondoka hili eneo na kuwaacha watu wake wakianza kunifungua katika kiti nilicho kalia, wakaanza kunikokota hadi kwneye moja ya chumba kisicho na kitu chochote na kunisukumia ndani kisha wakaufunga mlango. Taratibu nikajaribu kusimama ila kwa kizunguzungu na maumivu ya kifua na tumbo nikajikuta nikianguka chini. Nikakaa kitako na kuegemea ukuta huku nikishusha pumzi mfululizo.
‘Siwezi kuwaacha Rose na mume wake hai’
Nilizungumza huku nikiutazama mlango huu wa kuingilia humu ndani. Muda ukazidi kwenda pasipoo mlango huu kufunguliwa, kijiusingizi kikaanza kunichukua. Mlango ukafunguliwa na kujikuta nikistuka kutoka usingizini, akaingia jamaa akiwa ameshika bakuli la kunawia mikono, huku mkononi mwake akiwa amehsika bunduki aina ya SMG. Taratibu akaanza kuliweka bakuli hilo chini huku akiwa amenitazama kwa umakini sana, nikautazama mkono wake ulio shika bunduki yake, nilicho gundua, ni kwamba mkono wake upo mbali na kifyatulio cha risasi, jambo lililo nifanya nimrukie kwa kasi huku nikiwa nimejitoa muhanga kufa na kupona.
Jaribio langu likafanikiwa kwa asilimia kubwa, kwani nimefanikiwa kumuangusha mtu huyu chini, akajaribu kujikurupusha, ili kujitoa mikononi mwangu, ila nikamzidi ujanja kwa maana hapa mimi ninapigania maisha yangu na kosa langu moja ndio kifo changu. Nikamtandika kisukusuku cha shavu na kumfanya agugumie kwa maumivu makali sana kwani nina uhakika kuna baadhi ya meno yatakuwa yamechomoka kwenye fidhi na kama si kuchomoka kwneye fidhi basi yatakuwa yananing’inia. Nikamshusha kisuku suku kingine kwenye shavu hilo hilo na hapo ndipo nikayashuhudia meno ya jamaa huyu ambaye sijuia analipwa shilingi ngapi hadi anajaribu kufanya hii kazi, yakitoka nje na kutua kwenye hii sakafu huku yakiambatana na damu damu. Kwa ajili ya kumkomesa zaidi nikachukua bakulia la uji huu unao fuka moshi mwingi na unaonekana ni muda mchache umetoka jikoni. Jamaa huyu akaendelea kuugulia muamivu haya, kwa guvu zangu zote nikakishika kichwa chekena kukizungusha kwa nguvu na kuifanya shingo yake kuvunjika jambo lililo pelekea mauti kwa jamaa huyu.
Nikaiokota bunduki yake, nikachomoa magazine yake na kukuta ikiwa imejaa risasi. Kwa haraka haraka nikaanza kumvua suruali yake, nilipo maliza, nikaivaa. Nikachukua viatu vyake ambavyo ni buti za kijeshi kabisa, nikavivaa. Nikachukua na shati lake ambalo ni zito kidogo, nikalivaa, nilipo hakikisha kwamba nimejiweka sawa, japo nina maumivu ya kifua na tumbo, nikajibanza kwenye mlango na kuchungulia nje. Kwenye kordo hii iliyo tulia sikuona mtu yoyote, nikaanza kutembea kwa kujiamini huku bunduki yangu ikiwa mkononi mwangu.
Kelele ya maji ya mvua yanayo tua kwenye bati ya jengo hili walilo nifungia, kidogo ikanipa wepenzi wa kutembea kwa haraka kwneye baadhi ya meeno ya humu ndani nikihakikisha kwamba ninatafuta sehemua ambayo ninaweza kutoka na kutoroka katika hili eneo.
“Baby nitakuja tu siku mbili hizi, nipo bize si unajua kazi zetu” Nilisikia sauti ya kiume kwenye moja ya kona, ikanibidi kupunguza mwendo wa kutembea. Nikaanza kumnyatia huku nikisikiliza anavyo zungumza.
“Ahaa huku mvua ndio kali sana mpenzi wangu. Vipi Dar es Salaam haijanyesha?” “Huku inayesha kishenzi hapa baridi, natamani niwe karibu yako unipe nipe joto mpenzi wangu” Nikamchungulia huyu jamaa na kumkuta akiwa amenipa mgongo, kwa mwendo wa kunyata huku nimeishika bunduki yangu vizuri, nikamkandamiza na mdomo wa bunduki mgongoni mwake. Taratibu nikaichukua simu yake kwani mwili mzima unanamtetemeka, nikaikata simu yake na kuiweka mgongoni.
“Ukigeuka tu ninakuchangua mgongo” Nilizungumza kwa sauti nzito jambo lililo mfanya jamaa huyu kujikausha kimya.
“Nimesikia una mpenzi wako, je unahitaji joto lake ukalipate kuzimu si ndio?” “Ha….a…..pa…ana” “Safi sasa ninahitaji kuweza kutoka hili eneo” “N….ni…..ngumu” Jamaa alinijibu huku mwili ukimtetemeka.
“Niambie ni wapi ninaweza kutoka” “Ukinyoosha hivi utakunja kushoto utakuta chumba cha magari na kuna geti la kutoka hamo limefungwa” “Twende ukanifungilie” “Mimi sina uwezo wa kukufulikia kwani linafungwa kwa umeme na mfunguaji yupo sehemu nyingine” Nikampiga jamaa kwa kitako cha bunduki kichwani mwake na kumfanya anguke chini na kupoteza fahamu. Nikaanza kukimbi kuelekea katika eneo ambalo jamaa huyu amenielekeza, nikafanikiwa kufika katika eneo lenye magesho ya magari ambayo karibi yote ni magari ya kijeshi.
Sikuwa na muda wa kujihoji kwamba nipo sehemu gani, kwa haraka nikaanza kujaribu kufungua gari moja baaya jingine, mengi yamefungwa ila nikafanikiwa kupata gari moja aina ya Hammer likiwa wazi, nikaanza kuitafuta funguo yake kwa bahati nzuri nikakuta ikiwa imefichwa pembeni ya siti ya dereva.
Nikaliwasha kwa haraka, likafanikiwa kuwaka, nikakanyaga mafuta kwa nguvu, na gari likaanza kuondoka eneo hili, nikalilenga geti hili. Ugumu wa gari hili ukafanikisha kulivinja geti hili na kutoka nje, sifahamu ni wapi ninapo elekea ila nikajitahidi kuendesha gari hili hivyo hivyo. Kwa uelewa wangu wa haraka haraka hili eneo ni shamba moja kubwa ambao lina majengo machache sana na lipo nje ya mji na wala sifahamu ni mji gani. Nikatoa simu yangu mfukoni mwangu kwa haraka na kuanza kumpigia simu baba, simu yake haipatikani hewani. Mvua inayo nyesha usiku huu haikunizuia kuhakiksha kwamba ninajitahidi ninatoroka katika hili eneo. Nikampigia mama simu, simu yake ikaita baada ya muda kidogo ikapokelewa.
“Mama” Nilita huku nikizidisha mwendo wa gari hili.
“Erick” “Ndio mama, hivi sasa ninatoroka kwenye hii ngome niliyokuwa nimeshikiliwa, baba yupo wapi?” “Baba yako amekwenda kujisalimisha mikononi mwa magaidi hao” “NINI……!!?” “Ndio mwanangu baba yako ameamua kufanya maamuzi hayo kwa ajili ya familia yake nzima” “Huo ni ujinga mama, amekwenda na nani?” “Erick” Nikasikia sauti ya dokta Benjamini
“Ndio dokta?” “Muheshimiwa raisi hivi sasa amekwenda kuwatega magaidi hao, na si kujisalimisha kama alivyo sema mama yako, niambie upo wapi ili askari waje kukushukua?” “Sifahamu, nipo kwenye shamba moja kubwa sifahamu lipo wapi, ila unaweza kutuma namba hii katika kitengo cha NSS, na wakaweza kunitafuta kwa kutumia Satelaiti” “Sawa usikate simu ninakuunganisha na mkuu wa NSS?” “Ni nani?” “Jackline” “Ok huyo nina muamini” Nikaiweka simu yangu loud speker, na kuiweka pembeni kwenye sehemu naalumu ya kuwekea simu.
“Erick?” Nikasikia sauti ya Jackline.
“Jackline vipi baba amefanikiwa kufika katika eneo husika la magaidi hao?” “Amefika kama dakika moja iliyo pita” “Ni wa……..” Kabla sijamalizia sentensi yangu nikajikuta nikifunga breki kali baada mbele yangu kuona vifaru sita vya kijeshi vikiwa vimesimama, hewani kukiwa na helicopter mbili za kijeshi na zote zimeelekeza mitutu yao kwangu. Kupitia kioo cha pembeni yangu nikaona vifaru vingine vya jeshi vikisimama nyuma ya gari langu na kuniweka katikati na kunifanya nibaki nikiwa nimeshikwa na bumbuazi kwani nikifanya ujinga wowote wanakwenda kunilipua mimi na gari langu.
ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom