RIWAYA: Black star

Black Star 2: Astra 27



Hali ya joto lilichanganyika na ubaridi kwa mbali ukamfanya Fahad asisimke japo alikuwa usingizini. Miale ya jua iliyopenya dirishani ikampiga machoni na kumafanya aweweseke kabla ya kufunguwa macho. Mkononi kwake alihisi ameshika kiti laini chenye kubonyea bonyea.



Mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, kichwani akajaribu kujiambia kuwa kitu hicho kilaini sicho anachofikiria. Lakini hata kabla hajamaliza shuka yake ikacheza.



"Sijagusa kitu" Akajisemea huku akijaribu kuutoa mkono wake sehemu uliokuwa umegusa. "Anh!" Sauti laini ya kike ikasikika kutoka ndani ya shuka.



Shuka hilo likasukumwa nyuma, kichwa kilichojaa nywele za kijani zenye kutoa aroma nzuri na kusuuza nafsi ndicho kilichomkaribisha. Mschana huyo akainuwa kichwa na kumuangalia Fahad machoni.



"Umeamka bwana wangu" Akaongea. Fahad hakujibu kitu badala yake akameza funda kubwa la mate.



Akainuwa shuka ili kuthibitisha alichokuwa anahisi, hakuwa na nguo hata moja!.



"Umelalaje bwana wangu" alirudia mschana huyo na kujikandamiza zaidi mkononi mwa Fahad.



"Unafanya nini, Nephira" aliongea akijaribu kumtoa mikononi mwake.



"Ah bwana wee, mi bado nina usingizi" alijibu na kujigeuza upande jambo ambalo lilisababisha shuka lote kutoka mwilini mwake. Fahad akashuhudia umbile maridadi la kike, kwa sekunde chache mwili wake uligoma kabisa kutii akili yake. Umbile la mschana lilithibitisha uwanawake wa Nephira. Pasi na matarajio yake, akajisogeza karibu na kukagua kiuno cha binti huyo kwa mkono wake wa kushoto.



"Bwana, niache nipumzike. Siku tatu zotw hukunipa hata nafasi ya kupumuwa" aliongea Nephira kwa sauti ya nataka sitaki. Kama ilivyo kwa rijali yeyote kuushinda mtihani wa matanio na kwa Fahad haikuwa vinginevyo. Hakuna kiungo hata kimoja kilichotii akili yake, vilifuata hisia za asili za kiume na kumfakamia bibie huyo.



Fahad anakuja kuzinduka baada ya kuguswa kifuani na mkono wenye joto. "Umepumzika vizuri bwana wangu" aliuliza Nephira akiwa anajilaza kifuani kwa Fahad.



"Nini kimetokea" akauliza.



"Umenichukuwa na kunifanya wako" aliongea Nephira na kukaa kitako, kisha akatoa shuka mwilini mwake. Chini ya kitovu alikuwa na mchoro wa ajabu ambao Fajad hakuwahii kuuona katika maisha yake.



"Jifunike na uwe na heshima" alitaka kuongea kwa kufoka lakini akili ikamsaliti.



"Hii unayoiyona chini ya kitovu changu inaitwa Sigil" aliongea Nephira.



"Sigil ndio nini?".



" Sigil ni alama ya muuganiko wa mwanaume na mwanamke, muunganiko wa akili, mwili na kiwiliwili".



"Mbona mi sijawahi kuona kitu kama hicho"



"Ni kwasababu hukuwa na muda kuukagua mwili wako, mi najua kama una mke na unampenda sana. Hiyo inathibitishwa na sigil kubwa kifuani kwako" aliongea Nephira na Fahad akajiangalia kifuani. Akakutana mchoro mkubwa ambao hakuuelewa kabisa.



"Hiyo ni sigil ya malikia wa kwanza wa moyo wako, na ni ushahidi kiasi gani unampenda. Unaweza ukahisi kama umemsaliti lakini nina uhakika hata yeye alifahamu kuwa itafika siku ambayo hutakuwa wake peke yake. Katika mkono wako wa kulia kuna alama ya jani lenye kung'ara, hiyo ni sigili yangu. Kwa maneno mengine mwili wako umenichagua mimi kuwa malkia wa pili wa moyo wako" alifafanua Nephira.



Akaendelea, "Fahad wewe huna haki ya kuchagua nani umpende na nani usimpende. Na najua unalijua hilo vyema kwasababu kuna dalili za sigili nyingine ambayo haikufanikiwa kujichora. Mwili na akili yako vinachagua ni mwanamke gani awe mwandani wako, na vinafanya hivyo kuchagua warithi wenye uwezo wa kupokea uwezo wako".



Kwa Fahad maelezo yote yalikuwa yakimchanganya akili tu, alihisi kama hadithi ya abunuasi tu.



"Huko mbeleni unaweza kuwa na wake wengi zaidi, una maisha marefu sana mbele" alimalizia Nephira kusimama, akamuinamia Fahad na kumzawadia busu jepesi la mdomoni.



********



"Fahad tulikuwa tunakusubiri" aliongea Fang Shi punde tu baada Fahad ndani. Hakuwa peke yake, walikuwepo wengine wengi ambao hata Fahad mwenyewe hakuwa akiwafahamu.



"Kuna nini, mbona mumekusanyika hivi" ilibidi aulize maana kwa yeye hakuona haja ya wote kuwa hapo.



"Ulikuwa umelala kwa siku tatu mfululizo, watu wengi walikuwa na wasiwasi sana" alijibu Fang Shi.



"Vipi? mumeshafanya harakati za msiba"



"Ndio tumemaliza jana ila tulikuwa tunakusubiri wewe ukaage kabla ya kutangaza rasmi".



"Sawa, nipelekeni" aliongea.



Fang Shu akaongoza njia mpaka lilipo jiwe kubwa, lilikuwa na majina ya watu wengi sana ambao walipoteza maisha katika vita iliyoisha. Kwa tamaduni za kule, heshima ni kuwasha kijiti maalum chenye kutoa moshi kisha unakichomeka chini. Unakiacha kinawaka mpaka kinaisha.



Fang Shi akamkabidhi kijiti na kukiwasha, Fahad akakipokea na kukichomeka chini kisha akapiga magoti.



"Mumefanya vyema, haikuwa kazi rahisi sana kuacha familia zenu na kwenda katika uwanja ambao mulijuwa wazi kuna uwezakano wa kutorudi nyumbani. Lakini mlikaza meno na kupiga moyo konde, kwa hilo mna heshimza yangu".



"Nina uhakika katika dakika zenu za mwisho, mulikiangulio kifo usoni maana hivyo ndivyo shujaa wa kweli anavyotakiwa kuondoka. Pumzikeni kwa amani, sisi tuliobaki tutailinda amani mlioipigania" alimaliza kuongea na kusimama kisha akainamisha kichwa kama ishara ya heshima.



Hali ya hewa ikabadilika ghafla na mawingu yakajikusanya, mvua nyepesi ikaanza kunyesha. Hakuna alieondoka, mvua hiyo iliwapa nafasi wale walozuia machozi wayaachie. "Pumzikeni, sitamwaga chozi" aliongea Fahad na kugeuka akaanza kuondoka.



Pasi na matarajio yao yake, ilishuka radi kali sana na kumtandika. Radi hiyo haikuwa ya kawaida, kwasababu ilipiga bila kuacha kwa karibu dakika nzima.



Ilipokata, Fahad alibakia amesimama huku mwili wake ukifoka moshi. Nywele zake ziliongezeka urefu na mwili wake ulizidi kutanuka na kuwa mkubwa.



"Hongera Fahad, umevuka daraja" aliongea Fang Shi na kutoa heshima. Akaendelea "umeingia daraja gani".



"Nimeingia daraja la Qin" alijibu Fahad, mwili wake ulikuwa ukizungukwa na Qi ya ajabu. Fang Shi alibaki akiangalia tu. Alijaribu kutafsiri hali hiyo lakini ubongo wake ukakataa kutoa uwezo kabisa.



"Fang Shi unaweza kunikusanyia mtu mmoja kutoka katika kila familia kwa wale ambao wameshoriki" aliongea na sauti haikumaanisha kama ni ombi. Fang Shi akajikuta akiitika na kukubali hilo bila akili yake kutoa.



"Nitafanya hivyo, nipe muda mchache tu" aliongea na kuondoka, Fahad akabakia eneo hilo na kutafakari sana wakati wengine wakiondoka. Pasi na umakini wake, saa mbili zilikatika kama mchezo.



"Fahad wamefika tayari" alifika Famg Shi na kuongea, Fahad akampa ishara aongoze njia. Wakaelekea katika uwanja mkubwa, walikuwepo watu wengi sana. Vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume.



"Ahsanteni kwa kuja japo nimewaita kwa kuwashtukiza" alianza kuongea, kisha akaendelea. "Kilichotokea wakati huu kiwe fundisho kwenu kwamba katika ulimwengu wetu kila mtu anajali kilicho chake. Hata wakati huku wapendwa wetu wanapambana, walioahidi kutoa msaada hawakuja. Sina cha kuwapa ili kutoa majonzi yenu lakini nina njia ya kuwafanya muwe itakayoogopeka sana" alinyamaza na kuangalia.
 
Black Star 2: Astra 29





*********



Ngome ya Lorei.



Mlango mkubwa unafunguliwa, anaingia mtu alievalia gaguro zito kutoka kichwani mpaka chini. Mtu alitembea haraka haraka mpaka karibu kilipo kiti cha mfalme. Akapiga magoti na kusujudi kisha akainua kichwa chake.



"Mfalme wangu nina taarifa muhimu sana nataka nikufikishie" aliongea mtu huyu pasi na kumuangalia mfalme usoni.



"Endelea" aliongea mfalme Lorei wa ishirini na moja.



"Hatimae ngome ya Zinga wameamua kukusaliti" aliongea kama vile mtu aliekuwa akitarajia hilonkwa muda mrefu sana.



"Hahaha! Hatimae ndoto yangu itatimia" aliongea Mfalme Lorei.



"Ila anaeongoza usaliti huwo si mtu asili wa Zinga bali ni mgeni aliefila hivi karibuni. Na amediriki kusema ikiwa utaamua kuvamia na wewe ujiandae kupoteza kila kitu" aliendelea yule mtu.



"Pffff hahahah, nani huyo ana diriki kunitishis mimi mfalme mtukufu mwenye nguvu sana kuliko mtu yeyote katika ulimwengu huu. Hata wafalme wa ngome nyingine wananiogopa, huyo sisimizi amechoka kuishi" aliongea kwa majigambo mfalme Lorei.



"Mfalme wangu naomba nikujuze kuwa mtu mmoja ndie alieweza kugeuza wimbi la vita ile ya majini ambayo mtukufu uliipanga kwa muda mrefu sana". Kauli hiyo ikamshtua kidogo mfalme, "huyo mtu ndie aliemshinda Starodastu".



"Ndio bwana wangu nina uhakika si mtu wa kawaida kwa maana amengia katika vita na kupambana kwa siku mia moja bila kupumzika wala kuishiwa na Qi" aliongea yule mtu.



Mfalme akahisi hali fulani ya ubaridi ukitambaa mwilini mwake, "kisima cha Qi cha huyu mtu ni kikubwa kiasi gani" alijisemea kichwani mwake.



"Sawa unaweza ukaenda, endelea kufatilia kwa siri na kunipa taarifa" aliongea Mfalme Lorei na kumruhusu mleta taarifa aondoke.



"Niitieni waziri wa vita" alitoa amri na mmoja kati ya watumishi waliokuwepo akaondoka na kuelekea alipo waziri husika. Baada ya muda mfupi akarudi akiwa amefuatana na kipande cha mtu kilichopanda na kujaa kisawasawa. Mavazi yale yalikuwa ni kama chuma chenye kung'aa na mkononi alikuwa na kofia kubwa ya chuma yenye usinga wa nywele nyekundu kwa juu.



"Nimeitika mfalme wangu" aliongea nankupiga goti moja.



"Andaa kikao na makamanda wa vikosi vyote, kuna jambo nataka tujadili" alitoa amri.



"Sawa mtukufu Mfalme" akaitika na kuinuka kisha akaondoka na kwenda kufanya alichoambiwa.



Saa mbili baadae katika ukumbu mkubwa.



"Najua nyote mnafahamu kama ngome ya Zinga imeamua kusaliti, na kwa mujibu wa taarifa nilizozipokea kiongozi wa usaliti huwo si mtu wa kawaida. Ni mtu aliepambana na viumbe wa kijini kwa siku mia moja bila kuchoka wala kuishiwa Qi. Lengo la kuwaita hapa ni kupata maoni yenu juu ya suala hili" aliongea mfalme.



"Mimi nahisi kwanza tuendelee kukusanya taarifa zake, tujue wapi ana kasoro kisha tuzitumie kasoro hizo kumuangusha kutoka mioyo ya wale wanaomkubali" aliongea kamanda mmoja.



"Japp hilo ni wazo zuri nij lakini hivi tunavyoongea anawapa watu mafunzo. Tukisubiri mpaka awaivishe mwisho itakuwa kazi kwetu. Hatuwezi kumadharau hata kidogo, kama taarifa ziko sahihi maana yake hapa tunacheza grandmaster" aliongea waziri wa vita.



"Kama ni hivyo kwanini tusitume mtu mwenye uwezo zaidi kwenda kumuona" alitoa maoni kamanda mwengine.



"Mimi naunga hoja mfalme wangu" aliongea mwengine na baada ya hapo wachache wengine wakaunga mkono.



"Nilijua tu haya majinga yanatafuta mafasi ya kunitoa kwenye kiti cha uwaziri" alijisemea waziri wa vita.



"Kuliko kwenda vitani na mtu tusiejua kitu juu yake ni vyema tukatuma mtu kwenda kufanya mahojiano nae. Na katika hilo atapima uwezo wake na baada ya hapo tutapanga mipango mingine" aliongea mfalme na kumuangalia waziri wa vita.



"Nitafanya kama unavyotaka mfalme wangu, nitaundoka punde tu baada ya kikao hichi" aliongea waziri huyo na kuwaangalia wengine kwa jicho kali sana. Baada ya hapo kikao kikaghairishwa na wote wakatawanyika.



Waziri wa vita alipotoka akaita kipandoa chake, lilikuwa joka kubwa lenye rangi ya dhambarau na mapembe latika kichwa chake. Yalikuwa matatu na yalikuwa kama yanawaka moto, akaruka juu na kutuwa kwenye kichwa joka hilo na kuondoka. Njia nzima alikuwa amekunja sura, "sijui wewe ni nani lakini umekaa katika upande mbaya na mimi" alijisemea.



*********



"Unaweza kumsaidi mamaangu" aliuliza Nephira na kumuangalia Fahad kwa macho yanayomwambia tafadhali usije ukakataa. Fahad akameza funda kubwa la mate maana kumkatalia mwanamke huyo halikuwa jambo lenye kuwezekana.



"Kwanini nisimsaidie mama mkwe wangu" aliongea Fahad na kutabasamu. Nephira akaruka kwa furaha na kumkumbatia kisha akamzawadia busu la shavu.



"Kawaida ya wachawi hamtumii Qi badala yake nnatumia Mana au Runi. Kawaida binadamu huzaliwa na kiwango kidogo cha mana hivyo kiwango kikubwa mnakikusanya kutoka katika mazingira. Na mazingira mazuri ya kukusanya mana na runi ni kupitia misitu. Lakini mama mkwe wewe inaonekana ulijaribu kunyonya runi nyingi kwa wakati mmoja na kupelekea kisima chako cha kukusanya runi kuharibika" aliongea Fahad na kuwaacha wote wawili wakimshangaa.



"Kukutibu si kazi kubwa sana" aliongea Fahad na kwa kasi ya ajabu kusimama nyuma ya mama mkwe wake. Viini vya macho yake vikabadilioa rangi na kuwa kama anga ya usiku iliopambwa na nyota. Kwa kutumia kidole chake cha shahada na cha kati akamgonga mara kadhaa mgongoni.



Ikasikika kengele kali sana kisha, chini mamaake nephira ikajichora nyota kubwa na kuzungukwa na duara kubwa. Runi ikaanza kukusanyika ndani chumba hicho, mama ake Nephira akaanza kuelea. Mwili wake wa kizee ukaanza kunyooka, ni kama alikuwa anarudi katika ujana wake.



Mwanga mkali sana ukawa na baada ya kutoweka ndani ya chumba na waschana wawili. Mmoja alikuwa Nephira na mwengine alikuwa mama yake lakini ni kama walikuwa mtu na dada yake. Walifanan kila kitu chenye nywele maana yake ni Nephira za rangi ya dhahabu kumeremeta.



"Ahsante sana mtukufu mfalme" aliongea mama huyo na kupiga goti. Akaendelea kuongea "jina langu Magdalena".



"Unaweza kusimama Magdalena" aliongea Fahad jicho lake la kulia lilibaki likiwaka rangi ya kijani yenye kung'ara na kiini cha jicho hilo swali na mchoro kama V.



"Nimeishi miaka mingi lakini zaidi ya kwenye vitabu sijawahi kumshuhudia mfalme wa wachawi. Mara zote huwa ni malkia tu. Zaidi yako wewe katika historia kuna mtu mwengine mmoja tu ambae ameweza kupata crest ya wachawi katika jicho lake" aliongea Magdalena.



"Ni nani huyo" aliuliza Fahad.



"Ni marufuku kutajwa jina lake mtu huyo, kwani ndio binadamu peke alieweza kusimama jicho kwa jicho miungu. Alikuwa ni binadamu mwenye kutokea kutokea, aliweza kutumia aina ya nguvu inayopatikana katika asili na nguvu ya nguvu iliyomuwezesha kutuma woga kwa miungu" aliongea Magdalena .



"Basi huna haja ya kuniambia jina lake, huyo mtu ni mwalimu wangu na mimi ndio mrithi wake" aliongea Fahad na mwili wake ukaanza kubadilika. Joho kubwa jekundu likatokea nyuma yake, na suti ya chuma ikauvaa mwili wake. "Jina langu ni Asura Fey" aliongea na kuachia wimbi kubwa la upepo.
 
WASOMAJI NILIKUWA NA MAJUKUM YA KUPAKA RANGI TAIFA. KWA SASA NAENDELEA KUSAFISHA.
 
NA TARIQ HAJJ 30--------31
Black Star 2: Astra 30





Magdalen akadondokea magoti yake na kusujudu, "wow" kwa Nephira hali hiyo ilikuwa ni kama muujiza. Alikodoa macho, damu ilimuenda mbio sambamba na mapigo ya moyo.



"Wewe mtoto sujudu haraka" aliongea Magdalena lakini Nephira ni kama alipatwa ukiziwi wa ghafla. Mara chini ya kitovu cha Nephira kukaanza kuonekana mwanga na kadri muda ulivyokwenda ndivyo mwanga huwo ulivyoongezeka. Sigil yake ikaanza kuenea mwili mzima.



Fahad akamsogelea na kumishika kisha akamkumbatia, ghafla vitu kama mabawa ya kijani yakachana nguo ta nephira kwa nyuma na kusambaa ndani ya chumba kizima. Baada kama dakika tano hivi zile mbawa zikapotea, akalegea na kupoteza fahamu. Akambeba na kumlaza kitandani, na kumuangalia usoni. Alizidi kuwa mrembo kuliko alivyokuwa mwanzo.



"Magdalena unaweza kunieleza kilichotokea" aliongea.



"Ndio, sisi wachawi wa msitu huu ni tofauti kidogo. Kawaida mchawi kadri anavyokuwa na chuki na hasira ndivyo uwezo wake unavyoongezeka lakini si kwetu sisi. Kadiri tunavyopenda ndivyo uwezo wetu unavyoongezeka. Na ulichoshuhudia sasa ni kiwango cha juu kabisa mtu anachoweza kupenda baina yetu. Ni kama nyinyi mnavyopara utakaso wa radi, na kutokana na hilo katika ulimwengu huu Nephira akiamka atakuona kama mungu ambae ni lazima akuabudu".



"Hatoweza tena kuishi mbali na wewe, atakufuata utakapokwenda na hata siku ukifa na yeye hatokuwa na maisha tena. Maisha yako na yake yameunganika kwa mnyororo wa kiroho, mnyororo ambao una faida kwako na hasara kwake. Kwasababu ukifa wewe na yeye atakufa lakini akifa yeye kwanza mnyororo huwo utakatika na kukuacha hai. Na kutokana na hilo Nephira amepoteza sifa ya kuwa malikia wa msitu huu" alifafanua.



Nephira anafungua macho na moja kwa moja anainuka kitandani na kumikimbilia Fahad na kujirusha mikononi mwake. "Ni vizuri kuona umeamka na nguvu za kutosha" aliongea Fahad na kumbusu kwenye paji la uso.



"Magdalena madhali kashaanka ni wakati sasa wa miminkurudi nyumbani kuna mtu anahitaji kuonana na mimi" aliongea.



"Mimi sina la kusema zaidi ya kushukuru, lakini kabla hujaondoka nikuombe kitu kimoja" aliongea Magdalena.



"Enhe"



"Kuwa mlezi wa msitu huu" aliongea.



"Hilo si tatizo lakini hapa sina kitu cha kuacha" aliongea Fahad.



"Usijali kuhusu hilo, kuna kandili yenye kuwaka kwa kutumia Qi lakini hakuna miongoni mwenye uwezo wa kuiwasha kwasababu inatumia kiwango kikubwa sana cha Qi. Ila ikishawaka, itaendelea kuwaka hata utakapokufa. Itazima pale tu kila kitu kuhusu wewe kitakapopotea" aliongea.



Akafungua sehemu na kutoa kandili iliyojaa mavumbi, akaifuta na kuiweka mezani. Akamuelekeza Fahad aweke mkono katika sehemu fulani. Alipoweka tu Qi yake ikaanza ksafiri kuelekea ndani ya kandili hiyo. Baada ya sekunde chache kandili ikawaka na kutoa muangaza mkali sana.



"Inatosha" aliongea Magdalena na Fahad akatoa mkono wake.



"Mpaka tutakapoonana tena mi nikutakie afya njema" aliongea na kuinamisha kichwa. "Nephira tuondoke" aliongea, "mama mi nakwenda" aliongea na kuinamisha kichwa, wakapotea na kutokea Zingi katika chumba alichokuwa amelala Fahad wakati amepoteza fahamu.



"Wewe pumzika mimi naenda kuonana na mtu, atafika muda si mrefu" aliongea Fahad na kutoka. Nephira akapanda kitandani na kujilaza, alikuwa amelewa penzi.



Alipotoka moja kwa moja akaenda mpaka kwenye katika ukumbi wa mikutano na kukaa kwenye kiti. Akamuita mlinzi "kuna mtu atafika muda si mrefu, msipambane nae na mumlete kwangu" aliongea. "Sawa meya" aliitika na kuondoka.



Saa mbili baadae getini.



"Nimetoka Lorei, niko hapa kuonana na Meya" aliongea yule waziri wa vita. "Karibu Zinga Meya alikuwa anakungoja" aliongea mlinzi mmoja na kufungua mlango kisha akamuomba amfuate. Hakuna mtu alieonesha iadui mbele ya mtu. Wote walifuata maelekezo ya Fahad kwa utiifu wa hali ya juu.



Akapelekwa mpaka kwenye ukumbi ambao Fahad alikuwa anasubiri. "Meya yupo ndani" aliongea mlinzi alomleta na kumkabidhi kwa walinzi waliokuwepo hapo. Wakafungua mlango na kumfanya ishara ya kuingia.



Kijasho chembamba kilimchuruzika, "nilikuwa nakusubiri" aliongea Fahad kwa sauti ya juu kidogo.



"Nashukuru kwa ukarimu wako, mimi naitwa Garaaji waziri wa vita katika ngome ya Lorei" alijitambulisha.



"Karibu Garaaji, mimi naitwa Fahad" aliongea na kutabasamu, hali ya hewa ndani humo ikabadilika na kuwa ya kawaida. Akamuonesha ishara ya kuketi, Garaaji akaelekea mkono ulipoelekea na kukaa.



"Kwasababu si rafiki sana ningeomba uende moja kwa moja kwenye jambo lililokuleta" aliongea Fahad.



"Sawa, niko hapa kwa niaba ya mfalme Lorei wa ishirni na moja" alianza kuongea. "Mfalme anakutaka usalimu amri na ufike mbele yake kuomba msamaha kwa kuongoza usaliti wa ngome hii".



"Je kama sitafanya hivyo" aliuliza Fahad.



"Ikifika mbala mwezi tutaongoza vikosi vya ngome kuu kwa ajili ya kukulazimisha. Na kama hutaki kuona watu wako wakifa ni vyema ukasalimu amri" aliongea Garaaji.



"Una diriki kunitisha katika himaya yangu, kamwambia huyo mfalme wako kama atakuwa na mgongo mgumu wa kubeba madhila yatakayomkuta nitakutana nae uwanjani. Itakuwa jeshi la ngome nzima na mimi, nitakuwa peke yangu lakini nawahakikishia hakuna atakaerudi nyumbani akiwa na uhai" aliongea na ghafla jengo hilo likaanza kutikisika.



"Nimefikisha ujumbe, sitachukuwa muda wako zaidi. Nitafikisha salamu zako kwa mtukufu mfalme. Natumai hatutakutana vitani" akainuka na kuaga kisha akatoka nje.



Akasindikizwa mpaka getini, akaliita joka lake na kupanda akaondoka. Kilometa kadhaa kutoka getini aliamuru joka hilo lisimame, akashuka chini. Ghafla akanguka na kukohoda damu. Jasho jingi lilikuwa likimtoka, alijaribu kusimama lakini miguu ikagoma kutoa ushirikiano.



"Yule hawezi kuwa mtu, binadamu hawezi kuwa neigong nyingi kiasi kile" alijisemea na kudondoka chini, akapoteza fahamu. Alikuja kushtuka baada ya kuhisi kitu kikisimama, alikuwa amefika Lorei. "Ahsante Jeiku" aliongea akigusa kichwa cha nyoka hilo na hapo ndio akagundua kuwa hata mdudu huyo alikuwa ameathirika.



"Ila haiwezekani neigong kumuathiri mnyama, lazima Fahad atakuwa na mnyama wa kiroho ambae yuko juu zaidi kiuwezo kuliko Jeikuu" alijisemea akimuonea huruma.



"Rudi ndani ukapumzike" aliongea na joka lile likabadilika na kuwa moshi. Mchoro msogo ukatokea katika paji lake la uso. Akapiga mruzi mkali na baada ya sekunde chache akafika farasi mweusi. Akapanda na kuelekea ndani ya ngome hiyo. Alijitahidi japo bado mwili wake ulikuwa umechoka kutokana na kutumia neigong nyingi ili asipoteze fahamu kipindi anaongea na Fahad.



Safari uake ilikomea nje ya mlango mkubwa, akashuka na kumkabidhi farasi wake kwa mlinzi aliemkuta. Yeye akajitahidi na kupanda ngazi huku akiyumba yumba. Mlango ukafunguliwa, akatembea chap chap mpaka karibu na mfalme na kupiga goti. Ila kabla hajaongea akakohoa na kutokwa na damu nyingi mdomoni.



"Garaaji umepata madhila gani" aliongea waziri mkuu na kumuwahi asianguke.



"Nimerudi mfalme kutoka katika kazi ulionipa, nimefikisha ujumbe kama ulivyosema" aliongea kwa tabu.



"Tutaongea vizuri afya yako ikitengemaa, mpelekeni kwa mtoa tiba na mpeni kidonge cha kuituliza bahari ya taaluma. Inaonekana imechafuka" aliongea mfalme.







Black Star 2: Astra 31



Zinga.



Nje ya nyumba ya Fahad, ulionekana msururu mkubwa wa watu. Walikuwa wakiagana na wapendwa kabla ya kuongia ndani humo kwa ajili ya mafunzo.



"Ndugu na familia msijali, mimi Fahad nawaahidi kuwa nitawafunza ndugu zenu na kuwalinda pamoja na nyie. Ni muda sasa wa kuingia mafunzoni" aliongea Fahad na kusukuma geti kubwa.



"Karibu nyumbani Mwalimu" aliongea Rahee na kuonamisha kichwa. Mwili wake ulikuwa mkubwa na kututumka mithili ya jabala kubwa lililozungukwa na mawe. Kwa makadirio tu alikuwa na urefu wa zaidi ya futi nane. Mwili wake ulikuwa ukitoa hali fulani ya hatari, kila aliemuona alihisi baridi ikitambaa mwili mzima.



"Sogea pembeni usitishe watu" aliongea Fahad, Rahee akiwa anatabasamu huku akikuna kichwa akasogea. "Karibuni" aliongea na kuendelea kutabasamu. Wengi walidhani tabasamu hilo ni la upendo lakini kwa Rahee ilikuwa ni furaha kwasababu alikuwa anapata wenzake wa kuteseka pamoja. Aliyajua mafunzo ya Fahad vizuri, hata vitabu vyake havina tofauti.



Baada ya wote kuingia, akafunga mlango na kuwaongoza mpaka katika uwanja mkubwa. Akawaelekeza jinsi ya kukaa, aliwapanga kutokana na uwezo wao wa kunyonya nguvu za asili. Wale wenye uwezo mkubwa walikaa mbali na chanzo na wale wenye uwezo mdogo walikaa karibu.



Kwa kutumia mguvu akaikita ile fimbo yale ya chuma chini, "refuka nyoika" akatoa amri. Ile fimbo ikawa ndefu mpaka kupotelea mawinguni. "Hii fimbo itakuwa sehemu ya mkusanyiko wa Qi, kila mtu anatakiwa kuanza mafunzo" aliongea na kila akakaa vizuri na kufumba macho. Wakaanza kunyonya Qi iliokuwa inakuja eneo hilo kwa wingi.



Fahad yeye akakutanisha viganja vyake na kutuhusu Qi iliokuwa ndani yake, na kwa sababi kila mmoja alikuwa kazama katika mazoezi bila kujua akanyonya Qi ya Fahad. Na baada ya muda Fahad akatumia nguvu nyingi kurudisha Qi yake iliokuwa ndani ya miili ya wengine. Kitendo hicho kikawafanya wote wapoteze uwezo wa kunyonya Qi.



"Nini kimetokea", minong'ono ikaanza kusikika. Wote walonekana kuwa na wasiwasi.



"Najua wote mtakuwa na wasiwasi, maswali kama 'kwanini mumepoteza uwezo wa kunyonya Qi, uwezo wenu wa awali umetoweka'. Musiwe na shaka, nilichokifanya ni kusafisha miili kutokana na sumu mliokuwa nayo kwa muda mrefu. Ila malipo ya hilo ni kwamba mumepoteza kila kitu mlichokifanyia kazi kwa miaka yote ya nyuma. Kwa maneno mengine leo munaanza moja, mnaanza kujenga msingi upya. Kiti ambacho hakijabadilika ni uwezo wa binafsi kunyonya nguvu za asili" alifafanua.



Baada ya maelezi kila mtu akatulia na kuanza kufanya mazoezi. Fahad akawaacha na kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika. Alikuea ametumia Qi nyingi mno.



*******



Lorei.



"Mtukufu mfalme, Garaaji ameamka" alifika mtu mmoja na kutoa taarifa na baada ya dakika moja akafika Garaaji akiwa katika mavazi yake ya kiwaziri.



"Samahani mtukufu mfalme kwa kushindwa kukupa majibu ndani muda ulotakiwa" aliongea na kusujudu.



"Bila samahani, uliporudi maisha yako yalikuwa hatarini na isingekuwa na faida kama ungetoa taarifa na ukafa" alijibu mfalme Loreio wa ishirini na moja. Akampa ruhusa ya kuendelea. Garaaji akainuka na kuelekea kwenye kiti chake.



"Nimefanya kama ulivyonambia, kwenda kutembea Zinga na kumjaribu kiongozi wa sasa. Yafuatayo ndio majibu yangu, kwanza kiongozi wa Zinga wa sasa anaitwa Fahad na sio mkazi asili wa ulimwengu huu. Uwezo wake haupimiki, ni sawa na kujaribu kupima upana kati ya mbingu na ardhi ardhi. Na alichosema ni kwamba ikiwa tutaamua kwenda vitani basi na sisi tujipange na maumivu na hakukuwa na shaka ndani ya maneno yake".



"Unataka kusema kuwa huyo mpuuzi ana nguvu kuliko mfalme wetu" aliuliza waziri mwengine.



"Kwa heshima na taadhima sikusudii kusema kama mfalme wetu hana nguvu ama uwezo wake ni mdogo lakini kuna baadhi ya vita ushindi wake ni kutokupigana kabisa. Nasikitika kusema kuwa, hakuna mtu mtu katika ulimwengu huu mwenye nguvu kumshinda kiongozi wa Zinga wa sasa" akanyamaza na kumuangalaia mfalme. Alikuwa amekunja ndita kabisa kuashiriq hakupendezwa na maneno hayo.



"Nilipofika tu Zinga, niliambiwa kuwa Fahad alikuwa akinitarajia. Nadhani mnafahamu mimi nikiziba njia zangu za Qi hakuna mtu zaidi ya mfalme katika chumba hichi mwenye uwezo wa kujua. La pili ngome kama Zinga inayotambulika kwa ukorofi lakini nilipofika hakuna aliethubutu kunigusa kwa ubaya, neno lake ni sheria. Tatu nadhani mumeona hali niliorudi nayo, msinikariri vibaya. Sikupigana nae kabisa, madhila yote yalionikuta ilikuwa ni mimi kutumia kila tone Qi katika mwili wangu kujilinda wakati yeye alionekana yupo kawaida na wala hakuwa akiachia aura ya kukusudia kuniua".



"Nini maamuzi yako baada ya kukutana nae" aliuliza mfalme.



"Nimefikia hitimisho kuwa kwasasa tusiende vitani nae, tusubiri mpaka wazee wa kale waliokwenda katika utengo kwa ajili ya mafunzo warudi. Labda huenda tukawa na nafasi ya kushinda, na vita na Fahad haitakuwa ni vita ya nani ana nguvu bali itakuwa ni nani atakaeweza kusimama mpaka mwisho. Ameahidi kuwa yeye ni jeshi la mtu mmoja, hata tukienda ngome nzima yeye atasimama peke yake. Anaonekana ni mtu mwenye kujiamini sana, hatirudi nyuma kutoka katika neno lake".



"Huo ni upuuzi, nasemaje waziri wa vita Garaaji ameshindwa kuitumikia nafasi yake. Haiwezekani kumfananisha meya wa ngome ndogo na mtukufu mfalme wetu"



"Mi nakubaliana na waziri wa ndani, tumekosa imani na waziri wa vita. Tunatka mfalme utoe tamka kuwa Garaaji aachie nafasi yake na aadhibiwe kwa kosa la kukudhalilisha" alidakia waziri muweka hazina.



"Mtukufu mfalme kama katika maneno yangu kuna sehemu yeyote nimekudhalisha basi tambua hilo halikuwa kusudio langu. Na kama utaamua kwenda vitani na Fahad, mimi Garaaji waziri wa vita nitawasilisha rasmi tokeni yangu ya uwaziri na kujivua pasi na shuruti" aliongea Garaaji na kusimama kutoka kwenye kiti chake. Akapiga magoti na kusujudu aliposimama akatoa tokenu yake na kuiweka mbele ya mfalme.



Mfalme akasimama na kumuangalia Garaaji kwa macho makali sana."Kuanzia sasa natangaza rasmi kumvua uwaziri waziri wa vita Garaaji kwa kosa la usaliti. Lakini kutokana na mchango wake mkubwa, hatoadhibiwa kuvunjiwa dantian yake bali atafukuzwa bila kurudi katika ngome hii katika maisha yake yote. Mali yake yote itakuwa ni mali ya familia ya kifalme ikiwa ni pamoja na mke na watoto wote, una la kuongea Garaaji".



"Hapana mfalme na nashukuru kwa ukarimu wako, sitafanya chochote na nikitoka tu hapa nitaondoka. Natumai kuondoka kwangu kutakupa furaha katika moyo wako. Najivunia kuitumikia familia ya kifalme kwa muda wote nilioitumikia. Naomba nitoe heshima yangu ya mwisho kabla ya kuondoka" aliongea na kusujudu mara tatu kisha akainukea na kuondoka. Mawaziri waliobaki waliangaliana na kutabasamu huku wakitikisha vichwa. Kisha wakamwangalia mfalme nae pia akatabasamu, mpango wao ulikuwa umefanikiwa.
 
BADO KIDOGO KITABU CHA PILI KIFIKIE MWISHO.......................................... ................................MNAKARIBISHWA KUNANUA VITABU VIWILI VINAVYO ENDELEA BAADA YA KUMALIZA HICHI CHA PILI...... .................................................. ............
.
.
.
.
.
.

Black Star 2: Astra 32







Siku tatu baadae, nje ya geti kubwa Zinga.



Mtu alieonekana kuchakaa alikuwa akilikaribia geti hilo, tembea yake ilionekana ni ya tabu. Mwili wake mzima ulikuwa umerowa damu.



"Simama hapo hapo" aliongea mmoja kati ya walinzi waliokuwepo getini hapo.



"Naomba kuonana na meya" aliongea mtu huyo akionekana kujitahidi asianguke. Macho yake legevu yalionekana kupoteza nuru kabisa.



"Nini kimekutokea Garaaji" aliongea Fahad akitua mbele ya mti huyo ambae wengi walishindwa kumtambua mwanzo. "Mengi yamenitokea lakini siko hapa kuyazungumzia hayo" alijibu na kuyumba kidogo.



Fahad akamuwahi na kuzuia, ghafla jicho lakw la kulia likang'aa rangi ya kijani na ile crest ya wachawi ikawaka. Vidonda vyote vya Garaaji vikapona papo hapo na mwili wake ukapata nguvu.



Garaaji akarudi nyuma na kupiga magoti na kuongea, "nina macho lakini nimeshindwa kuona, kama kwa namna yeyote ile nilikukwaza nitapokea adhabu yeyote ile mtukufu Asura". Kauli hiyo ikamshtua mpaka Fahad mwenyewe kwasababu hakuwahi kumwambia mtu mwengine siri hiyo isipokuwa Nephira na mama ake katika ulimwengu huwo.



"Twende tukaongee ndani" aliongea na kupiga mruzi, Gorigo akatua na kusababisha upepo mkali sana. Mwili wake ulikuwa umeongezeka ukubwa mara mbili ya mwanzo. Jeiko akatoka kwenye mwili wa Garaaji na kujizungusha kabla ya kulaza kichwa chake chini. Hapo ndio Garaaji alielewa kwanini mwanzo mpaka mnyama huyo alipata majeraha.



"Gorigo acha ujinga wako, huoni kama unamzuru Jeiku" aliongea Fahad na kumkata jicho kali sana ndege huyo mweusi ti kama kiza cha anga lisilo na nyota.



"Nilikiwa namjaribu tu" alijitetea Gorigo, akainamisha kichwa, Fahad na Garaaji wakapanda katika mgongo ndege huyo, Jeiku akapotea na kurudi kwa muhusika wake.



Safari yao ikaishia katika ukumbi mkubwa, Fahad akamkaribisha Garaaji ndani.



"Nini kimekusibu Garaaji' aliuliza Fahad.



"Mfalme pamoja na mawaziri wenzangu walikuwa wakipanga muda mrefu kuniondoa katika uwaziri. Safari ya kuja kwako mara ya kwanza ilikuwa ni kunitafutia sababu ya kuniondoa. Na kwasababu nilikuwa na ushawishi mkubwa, wameniondoa kimya kimya na kupanga kunimaliza nikiwa nje ya ngome. Kwa siku mbili mfululizo nimekuwa nikifukuzwa na kupambana na wauwaji kutoka katika kikosi maalum cha mfalme. Japo nilifahamu kuwa sistahiki kuja huku lakini sikuwa na budi" alifafanua.



"Usiniaminishe kuja kwako huku ni bahati, kuna jambo ndio limekuleta" aliongea Fahad.



"Ndio" alijibu na kusimama kutoka kwenye kiti, akapiga magoti.



"Katika ulimwengu kuna mtu mmoja mwenye thaman zaidi kuliko hata maisha yangu nae ni binti yangu. Na hivi tunavyoongea atakuwa njiani akirudi kutoka katika safari yake ya mafunzo. Huyo ndio mtoto wangu wa pekee na waliobaki japo wametokana na mke wangu lakini si watoto wangu"



"Unamaanisha nini?"



"Mke wangu ni miongoni mwa wabaya wangu, miaka kama miwili nyuma nimegungua kuwa hakuwa mwanamke niliemfahamu. Alikuwa kimada wa mfalme, alikuja kwangu kama sehemu ya kazi maalum aliopewa na mfalme" alionekana kusita kidogo kuendelea.



"Nasubiri uniambie mwenyewe" aliongea Fahad.



"Katika ukoo wetu kuna siri kubwa sana, wanaume tunazaliwa na miili yenye uwezo mkubwa sana wa kunyonya Qi kutoka katika mazingira. Unaitwa mwili wa dragon, na aina ya martial art tunayojifunza haijaandikwa popote kwenye kitabu. Inarithishwa moja kwa moja kutoka siku ambayo mimba inaanza kutunga. Tukifika umri wa kujielewa tunajikuta tu tunaanza kicheza martial art ya aina hiyo".



"Kwa wanawake huzaliwa na mwili unaoitwa mwili wa maua, wao wanakuwa ni kama kisima cha kuhifandhia maji. Mwanaume yeyote atakaekutana nae kimwili kwa mara ya kwanza atanyonya uwezo wote na kumuacha akiwa anaelekea katika kifo chake. Sasa lengo la mwanamke niliemtambua kuwa kama mke wangu ilikuwa ni kunipa mtoto wa kike ambae baadae angekuwa kama shamba la mavuno kwa mfalme. Ikiwa atafanikiwa hilo, uwezo wake utazidi na kufikia daraja la KyoDan ambalo ni daraja moja chini ya daraja la kuzaliwa tena".



"Na kutokana na aina ya martial art ya familia ya kifalme, ndani ya muda mfupi atafika daraja la uzima na kifo. Akifanikiwa kupita katika utakaso wa radi basi kuna uwezekano akafika daraja la selesti ambalo ni njia ya mtu kupata uzima wa milele" alifafanua kwa kina Garaaji.



"Hivyo unataka mimi nikusaidie kumuokoa mwanao" aliuliza Fahad.



"Ndio"



"Na utanipa nini kama sehemu ya malipo yangu"



"Kwa hapa sina kitu chochote cha thamani lakini niko tayari hata kukupa maisha yangu" aliongea.



"Ikiwa nitachukuwa uhai wako basi safari yako yote ya kuja hapa itakuwa haina faida. Nitumikie mimi kuanzia leo, ndio itakuwa malipo yangu" aliongea Fahad na kutabasamu.



"Niko tayari kufanya hivyo, naahidi kukufuata na kutumika kama ngao yako katika maisha yangu yote" aliongea na kutaka kusujudu.



"Mimi sina haja ya kusujudiwa, imani yangu hainiruhus. Madhali umekubali hilo, wewe bakia hapa upumzike. Kesho mimi na wewe tutatoka kwenda kumfata mwanao, utamuokoa wewe mwenyewe" aliongea Fahad.



"Nashukuru Asura" aliongea.



"Kuhusu hilo tutaongea vizuri baada ya kukamilisha jambo lako, nataka nifahamu kwa kina umejuaje cheo changu".



"Sawa"



"Na pia unaweza kumwambia Jeiku atoke, nataka nimuone".



Sekunde chache tu, nyoka kubwa la rangi likatokea na kujikunja ili lienee katika sehemu hiyo.



"Marvellous! Ulipoingia mkataba nae alikuwa na umri gani" alihoji Fahad.



"Alikuwa mdogo sana, alikuwa amefikisha miaka mia sita" alijibu.



"Unajua kwanini mpaka leo hajavunja sheria na kuingia katika asili yake kabisa" aliuliza Fahad.



"Mbona mi namuona amekuwa sana tokea tulivyokutana"



"Hapana, Jeiki amekuwa akikutakasa kutokana na sumu uliingia ukiwekewa kila siku. Jambo limemfanya ashindwe kuvunja sheria na kuvuka daraja katika asili yake, unadhani Jeiku ni nyoka?".



"Ndio tafsiri pekee ninayoijua"



"Niruhusu nikuoneshe asili yake" aliongea Fahad na kusimama, akalisogelea joka hilo na kuligusa katika kichwa.



"Umefanya vyema kumlinda rafiki yako japo ulifahamu ilikua inakugharimu maisha yako. Kwa mamlaka mbingu na ardhi, mimi Asura Fey nitakuvusha na kukurudisha katika mwili wako Divai uchukue nafasi yako katika viti kumi na mbili vya wanyama wenye taji la kifalme. Nakuita kwa jina lako Veremin. amka".



Ghafla ngozi ya Jeiku ikaanza kutanuka na kutoa nyufa nyingi, katika nyufa hizo ukaanza kutoka mwanga mkali sana. Katika kichwa cha hola hilo likajichora taji, hali ya hewa nje ikaanza kubadilika.



Fahad akanguruma kwa nguvu na jengo zima likaanza kusambaratika na kuwa kama vumbi. Radi zikaanza kupiga, mvua kali iliyoambatana na pepo zilizokasirika ikaanza kunyesha. Mwili wa Jeiki uliendelea kuatanuka mpaka ukasambaratika.



"Kabla ya uhai ni kifo, na kifo ndio kimetoa maana ya uhai" alinena Fahad. Damu iliyosambaa kila pahali ikaanza kujikusanya sehemu moja na kutengeneza yai kubwa sana.



"Garaaji ingiza Qi yako katika hilo yai, unaingua mkataba mpya na Jeiku ambae jina lake halisi ni Veremin mfalme wa madragon ya kuzimu" aliongea Fahad na Garaaji akalisogelea yai hilo na kuweka mkono wake kisha akaanza kusafirisha Qi kuelekea ndani ya yai hilo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…