RIWAYA: Black star

RIWAYA: Black star

MSIMU WA PILI WA BLACK STAR UNAANZA SASA......
BLACK STAR SEASON 2

Black star 2: Astra 01

Mdani ya msitu mnene kinasikika kishindo kikubwa, "wapi huku" alijisemea akiinuka baada ya kujabamiza na miti kadhaa alipotuwa katika eneo hilo. Alijikumuta mchanga pamoja na kutoa majani kadhaa pamoja na vipande vya miti vilivyochoma katika nguo zake.

"Hii ndio shida ya kuvamia nyumbani kwa mtu pasi na mualiko" mpaka wakati huwo Fahad hakujua yuko wapi. Imepita karibia saa nzima kabla hajafanya maamuzi ya kuondoka eneo hilo. Alitembea kwa nusu nzima kabla ya kuanza kuona mwisho wa pori hilo.

Tabasamu laini likajichora usoni mwake, akaongeza mwendo ili afike alipopaona. Akiwa ana karibia kumaliza pori akaanza kusikia sauti za watu wakiongea ila hakuelewa kilichokuwa kikiongelewa kitokana na lugha hiyo kuwa ngeni katika masikio yake.

Akatahamaki alipokutana na watu wengi na wote walionekana wakielekea upande mmoja. Akawaangalia wote kwa makini na kugundua kuwa kila mmoja alikuwa na silaha. Alipojiangalia yeye alikuwa amevaa kofia tu. "Oh wewe pia ni mgeni" alisikia sauti ikitokea nyuma yake.

Akageuka, kama hisia za kujilinda tu. Akarudi nyuma, mbele kulikuwa na jitu kubwa. "Rahee nmekwambia usitishe watu" sauti nyingine ikatokea nyuma ya lile jitu kubwa.

"Lakini Masta mi sijamtisha eti" aliongea, Fahad akashusha pumzi. "Nmeshtuka wala usijali" aliongea na kustaajabu amewezaje kuelewa lugha ya wati hao. "Unashangaa umewezaje kuelewa lugha, hilo ni moja kati ya maajabu ya huku. Kila mtu anaongea lugha yake lakini tunaelewana hivyo hivyo. Kama hapa mimi naongea ulimi wa kwetu lakini wewe unaelewa" aliongea yule mtu mwengine.

"Anha sawa, mimi naitwa Fahad naweza kuungana na nyinyi" alijutambulisha.

"Hakuna shida, mimi naitwa Gahena na huyu Rahel mdogo wangu" yule mtu mwengine nae akajitambulisha.

Kiumbo Gahena alikuwa mdogo kuliko Rahee lakini alionekana kuchuchuka zaidi kiakili. Walitembea kwa muda huku Gahena akimueleza Fahad mawili matatu ya eneo hilo. Baada ya muda mrefu wakafika mbele ya mlango mkubwa. Ulikuwa mkubwa kiasi cha juu kutoonekana.

Wote wakakusanywa sehemu moja, "karibuni Astra sehemu ambayo kila kiti kinawezakana. Baada ya muda kidogo mtaonwa na wakufunzi wa hapa kwa ajili ya maswali kadhaa. Baada ya hapo mtangazaji akaondoka wakabakia wakiangaliana.

Macho mengi yalikuwa kwa Fahad ambae aliyapuuzia, hilo lilitokana na kuwa yeye alikuwa ni tofauti na wengi katika eneo hilo.

Wakiwa eneo hilo wakaanza kusikia watu wakiguna na wengine kupiga mayoe. "Pisheni bosi apite" walisikia sauti ikitokea nyuma. Waliomfahamu wakaanza kusogea isipokuwa Fahad.

"Fahad sogea, huyo anae kuja ni mtoto wa familia kubwa katika eneo hili" aliongea Gahena. Fahad akafanya kama hakumsikia, akaendelea kusimama pasi na kushughulika.

"Masiki atakufa yule" mtu mmoja akaongea akimnyooshea kidole. "Mwache afe tu, mtu gani asiejuwa nafasi yake" mwengine akajibu na kucheka.

"Wewe ni naji usietaka kumpisha bosi wangu, unamjuwa mtoto wa nani huyu" aliongea mtu mmoja aliekuwa mbele. Fahad hakujibu kitu, alimpotezea kabisa na kuendelea kuangalia mbele.

Mtu yule akatoa upanga na kumuwekea shingoni, "unajua jinsi ya kuutumia lakini" aliuliza Fahad.

"Hahaha, ina maana nibebe upanga na nisijue kazi yake" aliongea na kuendelea, "nahesabu mpaka tatu, kama hujasogea nakukata kichwa".

"Unapojiandaa kuuwa na wewe ujiandae kuweka maisha yako rehani" aliongea na kukunja ngumi, aliikaza ksawasawa. Alidhamiria kugeuka na kumtwanga ngumi hiyo ambayo aliamini kabida ingechukuwa uhai wa mtu huyo.

"Muda wa kuonana na walimu umefika, kila mtu atapita sehemu mtakayoelekezwa na kichukuwa kibao. Kibao hicho kitakuwa na namba ambayo ndio itakuwa tiketi yako ya kuonana na mwalimi" kabla hajafanya hivyo yule mtoa matangazo alirudi na kutoa tangazo.

"Una bahati sana mpuuzi wewe" aliongea yule mtu mwenye upange akiurudisha kwenye ala yake. Fahad akashusha pumzi na kuondoka. Akaelekea sehemu waliolekezwa na kuchukuwa namba yake. "Mia mbili na sabini" alijisemea na kutabasamu.

Akasogea pembeni na kukaa chini ya mti wenye kivuli. Gahena na Rahee wakafika nao na kuketi pembeni yake. "Umepata namba ngapi" aliuliza Gahena.

"Mia mbili na sabini"

"Mimi nimepata mia na hamsini na saba na Rahee kapata tisini na tisa".

"Hatuna budi kusubiri, kila mtu atakwenda ikifika zamu yake" aliongea Fahad na kulalia mgongo. Akavua kofia yake ya duara (alambara) na kujifunika usoni.

"Yaani huyu jamaa ni ndege huru, haoneshi kuwa na wasiwasi wowote ule wakati akijuwa kabisa kazungukwa na watu wenye nguvu sana" alijisemea Gahena.

Watu walikwenda kwa mujibu wa namba zao, Rahee alikwenda ilipofika ya kwake. Vile vile Gahena nae akaenda ilipofika namba yake.

Fahad hakuonesha kuwa na pupa yeyote ile, alitulia mpaka ilipotangazwa namba yake. Akainuka na kuwaaga wenzake, akaelekea alipoitwa na kupeleka chumba cha mwalimu ambae alitakiwa kumuuliza maswali.

Alipoingia ndani humo, akakaa kwenye kiti bila kuonesha wasiwasi wowote ule.

"Kwanini umekuja Astra" aliuliza mwalimu.

"Natafuta ukweli"

"Ukweli wa aina gani"

"Ukweli wa kila kitu"

"Kijana wewe ni mtu wa ajabu sana, katika maisha yangu nimewafanyia majaribio wengi lakini wote kama walikuwa hawatafuti utajiri basi ni umaarufu na nguvu. Unaweza kuenda".

Fahad akainuka na kushukuru, akaaga na kuondoka. Yule mwalimu akabaki akiuwangalia mgongo mkubwa wa Fahad uliokuwa umejaa na kujitandaza ndani ya nguo aliovaa.

Akarudi walipo Gahena na mdogo wake na kukaa, walikaa eneo hilo mpaka jioni ambako walipata ratiba kuwa, sehemu ya pili ya itaendelea siku inayofata.

Wakatawanyika na kuelekea katika majumba ya kufikia wageni. "Sisi tutalala hapa, wewe je?" Aliuliza Gahena.

"Mi sina pesa kabisa, nitatafuta mti nitalala. Nishazoea" alijibu. "Oh! Natamani ningekusaidia, lakini pesa haitoshi".

"Nashukuru kwa ukarimu wako, ila usijali" alijibu na kuwaaga. Akatafuta sehemu na kukaa kitako, akakunja miguu na kujiinamia.

Siku ya pili mapema akawahi sehemu ya majaribio na kukuta baadhi ya watu wakiwa tayari wamewasili. Maua yalivyomaliza kuchanua akafika yule mtoa matangazo.

"Kila mmoja atapita kwenye hilo jiwe, ataingiza QI yake. Hapa kutakuwa na walimu kutoka shule mbalimbali za Martial Art, watachagua wanafunzi watakaovutiwa nao. Ikiwa hutapata bahati ya kuchaguliwa na shule jua tu huna kipaji na ni vyema ikiwa utaondoka bila kufanya vurugu" aliongea.

Akaendelea, "baada ya kuongiza Qi yako kwenye hilo jiwe, litabadilika rangi. Ikiwa ni nyeupe wewe utakuwa na kipaji cha kawaida sana, manjano utakuwa na kipaji cha kawaida, buluu utakuwa na kipaji cha kiasi kuliko kawaida, kijani utakuwa na kipaji cha hali ya kati, zambarau utakuwa na hali juu kiasi, nyekundu cha juu na nyeusi cha juu zaidi (genius)".

Vijana wengie wakaanza zoezi hilo, wengie wakaangukia kwenye rangi ya buluu. Wachache wakaangukia kwenye manjano, wachache zaidi wakaangukia kwenye kijani. Asilimia moja ya wote wakaangukia kwenye zambarau na wawili tu wakaangukia kwenye nyekundu. Hakukuwa na rangi nyeusi.
_cbea0a0f-39f8-4d58-bb62-0bfb9f9573eb.jpeg
 
Black star 2: Astra 02
Na Tariq Haji
0624065911


Fahad alikuwa miongoni mwa kundi la mwisho, alipofika akaweka mkono na kusubiri. Hakuna rangi iliyotokea, akajaribu kuongeza Qi lakini majibu yalikuwa yale yale.

Vijana wengi wakaanza kumcheka, hakushughulika nao. Akashuka kwenye jukwaa hilo na kutoka nje ya geti. Wengi walimwita takataka, katika uliwmengu huwo ukiwa huna Qi wewe ni sawa na takataka.

Alipofika mlangoni akakutana na Gahena pamoja Rahee, wote wao walipata rangi ya kijani. "Usijali nina uhakika kuna jambo unaweza kufanya" aliongea Gahena. Sauti ilionekana kama kuwa dharau fulani hivi, "hakuna binadamu anaekosa kila kitu" akajibu Fahad.

"Anaesema hivyo hana tofauti na taka taka" alijisemea Gahena kwa sauti ya chini. "Gahena usiwe hivyo, mbona hajafanya kitu cha kukukera" Rahee alionekana kukereka na jambo alilofanya kaka ake.

"Usijali Rahee, katika ulimwengu wa Martial art, mtu bila Qi ni sawa na mfu. Ila nashukuru kwa kujali kwako, ikiwa Mungu ataruhusu tutaonana tena" aliongea a kupunga mkono, akaondoka.

"Nasali tusije tukakutana tena" aliongea Gahena na kutema mate. Kitendo cha kuwa karibu na takataka kilimuudhi sana, alionekana kudhalilika. Hasa alipofikiria kama alitaka kumsaidia sehemu ya kulala.

"Takataka" kila alipopita maneno yalikuwa hayo, kuanzia wazee, vijana mpaka watoto walimkejeli. Ila yeye wala hakujali.

"Unataka uondoke ndani ya mji huu" alifika mtu mmoja alieonekana kama askari.

"Huna haja ya kunambia, si unaniona hapa naelekea nje au vipi" aliongea Fahad. Yule askari akajifanya hajasikia, akamshika shati na kumkuta. "Usinishike tafadhali, nimesema natoka bila kushurutishwa na mtu" aliongea na kumshika mkono na kuutoa.

"Unajifanya mkaidi sio, unataka kushidana na sheria takataka wee" aliongea akijaribu kujitoa mkononi mwa Fahad bila mafanikio.

"Nitakuuwa nakwambia, huna faida takataka wewee" aliongea na kuendelea kuminyana ili atoke katika mikono ya mtu lakini juhudi zake hazikuzaa matunda.

"Naona, neno kuuwa limewakaa mdomoni. Unafahamu kuwa ukitaka kuuwa na wewe ujiandae kufa" aliongea na kumuangalia kwa macho makavu.

Yule askari akajikuta akishwindwa kuhema, alihisi kama anakabwa. Macho yalimtoka kama mwanaume aliejibana uume kwa zipu.

Akazunguka kwa kasi na kumbamiza katika mti uliokuwa karibu. Yule askari akapoteza fahamu hapo hapo, "pumbafu mkubwa" alijisemea na kuondoka.

Miongoni mwa watu walioshuhudia tukio lile, alikuwepo mzee mmoja wa makamo hivi. Na yeye pia alikuwa anakwenda nje ya mji huwo. Akamuwahi Fahad baada ya kutoka tu, "kijana tunaweza kuongea".

"Hakuna shida mzee wangu" Fahad alijibu na kutabasamu.

"Mimi naitwa mzee Mash, ni mfua vyuma" alijitambulisha.

"Mimi naitwa Fahad"

"Fahad, mi natafuta mtu wa kunisaidia katika kazi yangu. Unaonaje nikakuajiri, nitakupa sehemu ya kukaa na kukulipa vizuri. Pia sitakuzuia kama utakuwa na mambo yako ya kufanya".

"Sawa hata hivyo kwasasa sina kazi ya kufanya" alijibu na kutabasamu. Kwa wakati huwo alihitaji hasa apate sehemu ya kuweka kichwa na kazi ambayo itakuwa inamlisha.

************
Siku zilikatika huku Fahad akiwa anajishughulisha na kazi ya ufuaji vyuma. Mara kadhaa aliingia porini na kusaka mnyama kwa ajili ya kitoweo. Chakula cha nyumbani hakikumtosha kabisa. Mwili ulihitaji chanzo kikubwa sana cha nguvu kutika na muda wote kuizungusha Qi yake.

Miezi miwili baadae

"Fahad kuna mzigo unatakiwa uende mjini" aliongea mzee Mash.

"Lini"

"Kesho jioni utakuwa umekamilika, kesho kutwa mchana unahitajika uwe ushafika" aliongea mzee Mash.

"Sawa, hakuna shida kwa hilo. Ila nina ombi na mimi"

"Ombi gani"

"Nahitaji unitengezee bangili nne ambazo ukizichanganya pamoja uzito wake unakuwa nusu ya uzito wangu".

"Kwani wewe uzito wako ni tael ngapi" (tael ni pesa inayotumiaka katika ulimwengu huwo, imegawanyika katika sehemu tatu. Tael za chuma ambazo zina thamani ndogo sana, zinazofata ni za shaba ambazo zina thamani ya kati na zenye thamani ya juu kabisa ni tael za dhahabu).

"Mimi sijui lakini kwa huko nilipotoka, uzito unapimwa kwa kilogram" aliongea Fahad. Mzee Mash akakuna ndefu na kuwaza jambo.

Alimuangalia Fahad kwa muda, kisha akasuuza koo na kutikisa kichwa. Ni kama vile mtu aliekuwa anajiongelesha jambo kichwani.

"Sawa, nitakutengenezea lakini si unajua kama sifanyi kazi bure".

"Ndio najuwa, utaniambia kiasi ninachohutajika kulipa kisha utakata kwenye mshahara wangu"

"Wala sihitaji kukata mshahara wako, nachohitaji ni wewe ukae hapa kwa mwaka mmoja tu kisha ukiamua utaondoka".

"Mwaka mmoja ni mkubwa sana, nilipotoka nimeahidi nitarudi baada ya miaka kumi na tano. Na nimekuja kwa ajili ya kutafuta ukweli wa mwanzo na mwisho".

"Kwani umetokea ulikwengu gani"

"Nimetoka Dao"

"Una uhakika unataka kukaa huku kwa muda wa miaka kumi na tano ya Dao?" Aliuliza huku uso wake ukionekana kuwa na mashangao.

"Ndio kwani vipi"

"Fahad inaonekana kuna mambo mengi sana huyajui, kadiri unavyozidi kwenda limwengu za juu ndivyo pengo la wakati linavyoongezeka. Na nina imani hutaki tu kuishia hapa, kwasababu hapa ni mwanzo tu. Kuna limwengu nyingine za juu zaidi kumi".

"Kutokea chini kwenda juu ni Sekai, Vagra, Kengan, Kempoera, Feliora, Danjin, Danuwa, Nirvana, Mythril na Yuggdrasil. Miaka kumi na tano ni mingi mno ukiwa huku, inawezekana usiishi kabisa kuimaliza miaka hiyo. Na mpaka ukifika Yuggdrasil unaweza ukawa umeishi zaidi ya miaka elfu kwa miaka kumi na tano Dao japo hakuna aliefika Yuggdrasil, wengine wameishia Nirvana, na asilimia moja tu ya hao ndio wamefika Mythril".

"Hivyo basi usiwe na shaka, fanya mambo yako taratibu. Ukirudi kupeleka hizo bidhaa. Nitakuambia jinsi ya kuweza kufika hizo limwengu nyingine" baada ya maelezo hayo mzee Mash akaelekea katika sehemu yake ya kazi na kuendelea majukumu yake.

Siku ya pili mapema mzigo ukapakiwa kwenye gari maalum ya farasi. Fahad akaagana na kuondoka, alitembea kwa makini ili asiharibu bidhaa hizo baada ya masaa kadhaa akawasili katika geti la kuingia ndani ya mji huwo.

"Onesha kibali chako" aliongea mlinzi, Fahad akatoa kibao kilichokuwa na mchoro unao wakilisha biashara ya mzee Mash. Yule mlinzi akakipokea na kukiangalia kisha akamrudishia na kuwapa ishara wengine wamruhusu apite.

Akakipokea kibao chake na kumuamuru farasi atembee, akaelekea mpaka alipoelezwa afikishe mzigo na kusimama. Akashuka na kwenda kugonga mlango. Kipande cha mtu kikafunguwa mlango, Fahad akamuonesha kile kibao.

"Fuata hiyo njia, nyuma kuna sehemu ya kuwekea mizigo" kiliongea kile kipande cha mtu. Fahad akamvuta farasi wake na kuelekea upande alioelekezwa na kuanza kupakuwa mzigo. Alijitahidi asiharibu kifaa chochote kati ya hivyo.

Alivyomaliza akamuita muhusika kwa ajili ya ukaguzi. Alipojiridhisha kuwa bidhaa zote zilikuwa salama na hakuna iliyopunguwa. Akatoa mfuko wa ngozi ma kumrushia Fahad, akaudaka na kuutikisa kisha akatoa karatasi na kumkabidhi. Bwana yule akatoa muhuri mdogo na kuweka katika ile karatasi na kumrudishia Fahad. Hakutaka kuendelea kubakia eneo hilo, akaaga na kuondoka.
 
Black star 2: Astra 03
Na Tariq Haji
0624065911

Alitoka nje ya mji huwo na kuanza safari ya kurudi nyumbani akiwa umbali wa kilomita kadhaa alahisi watu wanamfata. Akamsimisha farasi na kusuka kama vile aliekuwa anakwenda kunisaidia.

"Oi ukitaka uondoke salama, acha farasi wako pamoja gari lake na vitu vyote ulivyokuwa navyo mwilini" aliongea alieonekana kuwa kiongozi wa kikundi hicho cha vibaka.

Fahad akajifanya kama hajasikia, "hujasikia au, shabbash noshabadilisha maamuzi. Nitakuuwa hapa kisha nitaondoka na kila kitu chako".

"Hakuna tatizo ikiwa utaweza kufanya hivyo, lakini ukishindwa tambua kwamba wewe ndie utakaekufa" aliongea Fahad kwa mara ya kwanza.

"Hahahah, wewe uniue mimi. Unatoa wapi hicho kiburi kwa mtu ambae huna tofauti na mfu. Mwili hauna hata Qi na bado unadiriki kunitishia maisha".

"Ndio umefundishwa kuchamba ama vipi, kama unataka kujitutumua tumia misuli bwana mdogo" aliongea Fahad akirudi kwenye gari lake pa farasi.

Yule kibaka akageuka kwa kasi na kutoa upanga, kwa kasi akamfata Fahad kwa lengo la kumkata kichwa. Fahad akabonyea kidogo na kugeuka kwa kasi akiwa amekunja ngumi.

Kwa vile yule kibaka alikuwa ameruka juu, Fahad akaivurumisha kwa kasi na kumtandika ngumi ya tumbo. Kibaka akacheuka damu, macho yakamtoka. Akajikuta yuko hewani kabla ya kutua na kujibamiza kwenye mti.

Mmoja kati ya vibaraka wake wakamuwahi na kumgusa shingoni. "Amekufa" akapiga kelele, wale walobaki wakapatwa na hasira na kumvamia Fahad kwa pamoja. Baada ya dakika tano wote wakawa chini. Miili yao ilikuwa ya baridi, haikuwa na maisha tena.

Fahad akapanda gari la farasi na kuondoka eneo hilo. Siku ya pili taarifa za vifo za vibaka hao zikasambaa kama moto wa porini.

"Fahad, niambie kuwa wewe huhusiki na vifo vyao" aliongea mzee Mash.

"Hapana, mimi nilipopita hakukuwa na mtu hata mmoja" alijibu.

"Kama ni kweli basi sawa, ila kama umehusika jiandae maana lile genge lina tabia ya kulipa kisasi. Na hasa ukizingatia mara hii aliekufa ni mtoto wa kiongozi wa genge hilo".

"Sihusiki na chochote ila kama kuna mtu anadhani mimefanya anakaeibishwa kujaribu bahati yake"

"Sawa, bangili zako zipo tayari. Kila mmoja ina uzito wa tael kumi ambazo kwa makadirio ni kama kilo kumi na tano" aliongea akimuoneshea meza.

Fahad akaziendea na kuibeba moja, "sio mbaya kwasasa ila baada ya kama miezi miwili nitahitaji zenye uzito wa kilo thalathini kila moja" aliongea na kuzifaa. Alivaa mbili mkononi na mbili miguuni, kisha akaruka ruka kidogo kwa ajili ya kupima uzito.

"Ulinambia utanieleza jinsi jinsi ya kufika hizo limwengu (sayari) nyingine".

"Kwanza unatakiwa ujiunge na cha cha wawindaji, chama hicho hakichagui mtu. Ili uweze kujiunga, watakupa kazi ya kwenda kuwinda. Ukirudi na huyo mnyama watakae kwambia. Utakabidhia kibao cha utambulisho. Na kupotia chama hicho utafanya kazi mbalimbali ambazo si tu zitakupa hela bali zitakupa uzoefu pia. Maelezo mengine watakupa wao wenyewe, na kuelekea limwengu inayofata pia wao watakueleza taratibu".

"Sawa, acha mimi niende kwanza" aliongea na kuondoka. Bangili alizovaa zilifunikwa na nguo yake hivyo haikuwa rahisi kuonekana. Safari hii hakutumia farasi. Alikimbia kama sehemu ya kuuzoea uzito ulioongezeka mwilini mwake.

Baada muda kidogo akawasili nje ya geti na kuonesha kibao cha utambulisho. Akaingia ndani na kuomba maelekezo ya kilipo chama cha wawindaji. Baada kupata maelezo haya akashukuru na kuendelea na safari.

Baada ya mwendo kama wa dakika kumi hivi akawasili nje ya jengo kubwa. Juu lilikuwa na maandishi makubwa yaliosomeka "CHAMA CHA WAWINDAJI". Akasukuma mlango na kuingia, ndani humo kulikuwa na watu wengi lakini hakuna alieshughulika nae.

Akaelekea mpaka dawati la mapokezi, "karibu" aliongea mwanaume aliekuwa mapokezi.

"Ahsante nimekuja kujisajili kwa ajili ya kuwa muwinsaji" aliongea, hakutaka kupindisha maneno.

"Shika hichi kibao kaungane na wale pale", akakipokea na kwenda kukaa kwenye foleni. Hapo walikuwa wanaingia katika chumba cha mahojiana kwa kikundi cha watu sita sita.

Ilipofika zamu ya Fahad alikuwa kabakia peke yake, hakukuwa na mtu mwengine. Akainuka na kuingia ndani, "mbona uko peke yako" akaliza mtu aliekuwa nyuma ya dawati.

"Hakuna mwengine, mimi nilikuwa wa mwisho"

"Kama hakuna watu wengine inabidi usubiri mpaka kesho"

"Kwani siwezi kujisajili peke yangu"

"Hapana haiwezekani, kwasababu kabla ya kusajiliwa inatakiwa ufanye kazi ndogo ili kututhibitishia kama unaweza kuwa muwindaji".

"Sasa itakuwaje, maana nimetoka mbali mno"

"Ila kama unahisi unaweza kumudu kazi peke yako, ipo sheria inayokuruhusu lakini inabidi uingie makubaliano kuwa jambo lolote baya likikukuta, chama hichi hakitahusika"

"Ungesema mapema kama kuna sheria hiyo, wapi nafanya makubaliano hayo"

Yule mtu akatoa karatasi na kuiweka juu ya meza, Fahad wala hakuisoma. Akaweka alama ya dole gumba.

"Nenda pale kwenye ubao, kuna kazi mbali mbali. Chagua moja, chukuwa kisha pachika hichi kibao. Nikutakie kazi njema"

Fahad akachukuwa kile kibao na kwenda katika ubao alioelekezwa. Akaangalia karatasi zilizokuwa na maombi ya kazi, moja ikakamata jicho lake. Akaichukuwa na kuweka kile kibao. Akaaga na kutoka, hakuongea chochote hata alipopita mapokezi.

Akatoka nje ya jengo hilo na kupotea maeneo hayo. Dakika kama kumi baadae yule kijana wa mapokezi akakimbilia katika ofisi ya kiongozi wake.

"Mkuu ile kazi ya kuwinda ngiri mwenye pembe tatu, imeongezeka nyota mbili" aliongea.

"Nenda kwenye ubao pale uitoe"

Akaenda ulipo ubao, macho yakamtoka. "Mkuu, haipo. Imechukuliwa"

"Kibao namba ngapi"

"Mia moja na moja"

Yule kiongozi akainuka mapigo ya moyo yakienda kasi. Akili yake ilishajua hatari gani anakwenda kukutana nayo alochukuwa kazi hiyo.

"Kusanya kikosi cha watu watatu haraka sana, wazunguke mji mzima kumtafuta kijana alietoka muda si mrefu hapa. Ni yule wa mwisho kuingia na bahati mbaya yuko peke yake. Hivyo kuifanya kazi hii iwe haiwezakani hasa kukamilika" aliongea kwa tafrani.

"Sasa hivi" akaijibu yule kijana na kutoka na kwenda kufanya alichoambiwa.

Fahad alifika nyumbani na kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya maandalizi. Alipouakikisha yamekamilika akatoka na kuelekea eneo la kazi la mzee Mash.

"Mzee hivi kuna silaha yeyote naweza pata, isiwe yenye makali tu" aliongea.

"Chumba cha pili hapo kuna chuma chembamba kirefu, nilikitengeza kwa ajili ya kukifanya mkuki lakini ni kizito hivyo haikuwezekana"

"Kiasi gani"

"Ah! Hicho ni bure tu, kwasababu hata kwangu hakina faida" aliongea mzee Masha na kutabasamu.

Fahad akaelekea chumba cha pili na kukitafuta, kilikuwa kwenye kona ya chumba hicho. Kilikuwa kimejaa mavumbi. Akakishika na kukinyanyua, bila matarajio akakunja sura. Kilikuwa kizito kuliko alivyotegemea.

Akatabasamu na kukaza mkono, akakiinuwa na kukiweka begani kisha akatoka chumbani humo. Akaelekea alipo mzee Masha na kumuaga, akaondoka​
 
Black star 2: Astra 05
Na Tariq Haji
0624065911

Akagonga mlango na kusubiri kuotikiwa, "ingia" sauti nzito ikasikika. Akafunguwa mlango na kuingia kisha akaufunga. Macho yake yakakutana na watu watatu wakimuangalia kwa udadisi zaidi. "Nimerudi" aliongea, "umemaliza kazi bila shida yeyote" aliuliza yule kiongozi.

"Haikuwa ngumu sana" alijibu na kuwafanya wale wengine wawili washangae. "Fahad hebu kaa hapo kwanza kuna jambo tunataka kujadili na wewe" aliongea yule kiongozi.

"Samahani sikujitambulisha mwanzo, jina langu ni Jerome. Hapa watu wote wananiita Master Jerome, na ndio mwenyekiti wa tawi hili" alijitambulsiha. Fahad alitulia, hakujibu kitu.

"Tusipoteze muda acha nielekee moja kwa moja kwenye nilichokuitia hapa" alisafisha koo kidogo na kuendelea. "Unao waona hapa wazee washauri wa tawi hilo, huyo mwenye kipara ni Master Lu na huyo mwengine ni Master Chen. Wote wawili ni wawindaji wakongwe sana kuliko mimi".

Fahad akawaangalia wazee hao na kutabasamu kisha akainuka na kuinamisha kichwa kidogo, akaongea "nawasilimu wazee wangu".

"Kaa tu" aliongea Master Lu akigusa kipara chake, alionekana kufurahishwa na tabia ya Fahad. Fahad akashukuru na kukaa.

"Lengo la kukuita hapa hasa ni kutaka mawazo yako juu ya daraja gani tukuweke. Kazi ulioifanya, awali ilikuwa ni kazi ya nyota moja lakini dakika chache baada ya wewe kuondoka tulipokea taarifa zilizoifanya kazi hiyo ipande kutoka nyota moja hadi tatu na kuwa hatari hata kwa wawindajiwa nyota nne".

"Lakini wewe umeifanya kama kwamba si chochote si lolote, mimi binafisi nimeshuhudia. Ila sitaki kujuwa siri yako, nini maoni yako kuhusu hili".

"Kwanza nafurahi kwa kuheshimu nafasi yangu, mimi sitaki kujulikana sana. Kwa hiyo kunipa daraja kubwa mapema ni kinyume na matakwa yangu. Niweke katika daraja ambalo sitasumbuliwa sana na wengine" aliongea Fahad na kuwashangaza wote.

"Unajua Fahad, kadri unavyozidi kuwa na daraja kubwa ndivyo malipo yako yanavyozidi kuwa mazuri. Pia ndivyo unavyo wasaa wa kuchagua miongoni mwa silaha bora zaidi. Hivyo watu wote wanatamani sana kuwa angalau nyota nne kama kianzio japo wengie huwa hawafikii mahitaji ya daraja hilo. Katika kesi yako, daraja la chini kukuweka basi angalu liwe la nne. Ila haki yako ni la tano au la sita" aliongea Master Jerome.

"Master Jerome nahisi unampa upendeleo mkubwa sana, kwa maoni yangu anatakiwa awe daraja la pili au la tatu kwa upendeleo" kwa mara ya kwanza aliongea Master Chen.

"Master Chen, kwasababu hujaona mpambano wake na ngiri wa pembe tatu. Kwa lolote lile naweza sema, huyu kijana si wa kawaida" aliongea Master Jerome akionekana kukasirishwa na kauli ya mzee mwenzake.

"Fahad, wewe ungependa ukae daraja ngapi kati ya la pili, tatu na nne" aliongea Master Lu.

"La tatu inaonekana si mbaya, hata mkiniweka hapo haitakuwa shida" alijibu.

"Una uhakika Fahad" aliongea Master Jerome na kuendelea "utakosa faida nyingi sana za daraja la nne, utakosa nguo nzuri na silaha kali zaidi za kuwindia".

"Hapana Master, silaha nilokuwa nayo inanitosha kwa sasa. Kuhusu nguo si tatizo sana, nitazipata nikipanda daraja. Ila nina ombi moja tu" aliongea Fahad.

"Enhe, ombi gani"

"Nahitaji jiwe lenye madini ya chuma ambacho kinaweza kupokea Qi" aliongea.

Master Jerome na wenzake wakaangaliana kisha wakamuangalia Fahad kwa mshangao. "Hilo jiwe hapa hatuna" aliongea Master Jerome.

"Fahad ukipata muda njoo unitembelee nyumbani kwangu, nina imani utapata ufumbuzi wa jambo lako" aliongea Master Lu.

"Nashukuru sana".

"Baada ya mazungumzo haya natumai wote tumekubaliana kuwa tutampa nyota tatu" aliongea Master Jerome na kumkabidhi Fahad kipande cha silver.

"Hicho ni kibali kinachowakilisha nyota tatu, karibu katika chama cha wawindaji" aliongea na kutabasamu.

"Ahsante natumai mtanilea na kuniongoza vizuri" alijibu. Baada ya mazungumzo hayo kikao kikafikia tamati, Master Chen akatangulia kutoka.

"Fahad tembea na mimi" aliongea Master Lu, akainuka na kuanza kuondoka. Fahad nae akainuka na kuaga kisha akamfuata.

Wakatoka nje ya jengo hilo na kuingia kwenye gari la farasi, wakaondoka. "Tunaelekea nyumbani kwangu, kuna jambo nataka tujadili" aliongea Master Lu. Fahad akatikisa kichwa kuashiria kumuelewa, farasi alitembea kwa dakika takriban ishirini. Wakawasili mbele ya ukuta mkubwa.

Wakashuka na kuelekea mlangoni, walipofika Fahad akasita kidogo. "Mbona hali ya hewa ni ya tofauti ndani ya nyumba yako" ilibidi aulize.

"Umegundua, ni binti yangu. Amekuwa mgonjwa kwa muda mrefu na maradhi yake hayajulikani. Nimehangaika kwa kila njia niijuayo lakini hatujafanikiwa. Harufu unayoisikia ni inatoka katika mwili wake ambao ni kama vile unaharibika ndani kwa ndani" aliongea kwa sonono.

"Naweza kumuona" aliongea Fahad.

"Hata ukimuona hutaweza kufanya kitu, wameshindwa matabibu bingwa katika tiba asilia".

"Acha tu nimuone" alisisitiza, Master Lu hakutaka kupingana nae tena. Akaongoza njia kuelekea katika nyumba iliyojitenga ndani ya ukuta huwo. Nje ya nyumba hiyo kulikuwa na walinzi waliokuwa wamejifunga vitambaa puani.

"Waambie waondoke" aliongea Fahad na safari hii sauti yake ilikuwa kali. Master Lu akajikuta akipata baridi katika uti wake wa mgongo. "Ondokeni" aliongea pasi na kutaka, ni kama vile alipokea amri aliyoshindwa kuipinga.

"Baba umekuja kufanya nini huku" ilisikika sauti ya binti ikitokea ndani ya nyumba hiyo.

"Kuna mtu anahitaji kukuona, huenda akawa na msaada" alijibu kisha akasukuma mlango. Walikaribishwa na harufu kali sana ya kitu kilichooza.

Fahad akamuangalia binti huyo kwa makini, "huu ni ugonjwa wa Qi" aliongea na kumuangalia Master Lu.

"Unamaanisha nini" aliuliza mzee huyo.

"Qi ya binti yako inazunguka isivyotakiwa hivyo kuharibu viungo vya ndani. Ikishavimaliza itaanza kula na vya nje. Na meridian zake nane kati ya kumi na mbili zimeziba. Inaonekana pia huu ugonjwa haukuja kwa asili bali alipewa sumu" alifafanua.

"Nani anaediriki kumpa sumu mtoto wangu" aliongea Master Lu kwa hasira.

"Tumtibu kwanza, mhusika utamatafuta baadae"

"Una mtibuje"

"Ni rahisi sana ila nahitaji nitakachokifanya hapa kiwe siri kati yetu sisi tu"

"Usijali kwa hilo, niko tayari kufanya chochote kwa ajili ya mtoto wangu"

"Una mawe ya cristali yenye ubora wa juu zaidi" aliuliza Fahad.

"Ndio, unahitaji mangapi"

"Nahitaji tisa, yapange katika kila kona ya chumba hichi"

Master Lu alikuwa na pete ya ajabu, pete amabyo ilitumika kama kitu cha kuhifadhia vitu. Akatikisa mkono mawe makubwa meupe yenye kung'aa yakadondoka chini. Akayachukuwa na kuyapanga katika pemben za chumba hicho.

"Moja liweke kati" alitoa maelekezo na mzee huyo akafanya hivyo.

"Tayari".

"Wewe nenda nje, hakikisha hakuna anaeingia humu. Nipe masaa mawili nitakuwa nimemaliza", Mster Lu akatoka nje na kusimama mlangoni. Alitamani sana ashuhudie nini kinaenda kutokea lakini haikuwezekana. Kwa wakati huwo Fahad alikuwa ni mtu tofauti kabisa na yule aliemuona mwanzo.​
 
.
Black star 2: Astra 06

Na Tariq Haji

0624065911

"Mimi naitwa Fahad, wewe je" alijitambulisha. "Yuna" alijibu kwa mkato, bado alikuwa hamuani vizuri. "Sawa Yuna, najua hujakata tamaa kutokana na ugonjwa huwo. Umefanya kazi nzuri sana kulinda viungo muhimu vywa mwili wako" aliongea ili kumtoa hofu.

"Sikwambii uniamini lakini nipe nafasi ya kukupatia tiba, nikishindwa haitaleta tofauti sana kwasababu unakaribia mwisho wa vita yako" aliongea kwa taratibu sana.

Yuna alimuangalia Fahad kwa makini, ni kama vile alikuwa akimtathmini. "Sawa hata hivyo mi pia nimechoka na haya mateso" alijibu Yuna.

"Unaweza kukaa?" aliuliza Fahad

"Ndio" alijibu na kuanza kujiinua, alipata shida lakini Fahad hakupiga hata hatuwa moja kumsaidia. Alifahamu wazi hilo lilikuwa ni pambano lake binafsi.

"Vua nguo yako ya juu, usijali mi sitaangalia"

"Umekuja kunichungulia au kunipa matibabu, hakuna mwanaume aliyewahi kuona mwili wangu" alifoka.

"Nahitahi kusafirisha Qi yangu kuelekea katika dantian yako ya tumboni. Unajua kama Qi inasafiri ikiwa kuna mgusano kati ya mtu na mtu mwengine" Fahad aliongea kwa upole.

Baada ya kujishauri, akaamua kuvua. Alikuwa akiona aibu japo Fahad hakuwa akiangalia. Alikuwa nyuma yake, alikuwa amefunga macho kabisa.

"Tayari" aliongea Yuna.

"Sawa tulia hivyo hivyo" aliongea Fahad na kufungua macho. Viini vya macho yake havikuwa vya kawaida, kila kiini kimoja kilikuwa na rangi mbili ndani yake. Nyeusi na nyeupe (yin na yang). Rangi hizo zilikuwa zikizungukana bila kuchanganyika.

Akajibonyeza sehemu katika chini ya kifua, kufanya hivyo kulifungua meridian moja kati ya kumi na mbili ambazo alikuwa amezifunga na kufanya ziachie Qi kwa matone madogo madogo.

Qi yake iliokuwa imejikusanya kwa muda mrefu katika dantian ya tumbo ilitoka na kuanza kuzunguka kwa kasi sana mwilini. Akaegemeza viganja vyake juu kidogo ya kiuno cha Yuna na kuanza kusafirisha Qi kuelekea mwilini mwa binti huyo.

"Kwanza kabla ya kuitoa sumu inabidi nirekebishe mzunguko wako wa Qi kwasababu unazunguka kinyume na unavyotakiwa" aliongea.

Akalazimisha Qi nyingi sana kuingia kwa kasi, Yuna akapiga ukwenzi kutokana na maumivu makali sana aliyohisi. "Ni lazima uvumilie maumivu, itauma zaidii huko mbele" aliongea Fahad akiendelea kumimina Qi.

Nusu saa ilikatika kwa kasi, Fahad akaacha kumimina Qi katika mwili wa Yuna na kutoa pumzi nyingi. "Tayari mzinguko wa Qi umerudi kawaida, sasa nahitaji kuanzia hapa tuende pamoja. Mwili wako umejaa Qi yangu ila nahitaji uizungushe katika mwili wako wakati huwo huwo nitakuwa nakusaidia kuisafirisha sumu katika ncha za vidole" aliongea Fahad.

Yuna akatikisa kichwa na kuanza kufanya alichoambiwa, jasho nyingi likaanza kimtoka. Lilikuwa na harufu kali sana, ila halikumkera Fahad. Viini vya macho yake vilizungukwa na pete tatu pamona na vidoti kadhaa. Hapo alikiwa akiona meridian zote za Yuna kama vile x-ray.

Taratibu akaanza kuiongoza sumu kuelekea katika vidole, zoezo lote lilikuwa ni la maumivu makali sana kwa Yuna. Alijitahidi sana kuvumilia maumivu, ilifika wakati alikaribia kukata tamaa. Lakini alipokumbuka kuwa hiyo ilikuwa ni njia pekee ya yeye kurudi katika afya yake aliendelea.

Masaa mawili yakakatika na mawe yote ya cristal ndani humo yalikuwa mekundu. Lile la kati ndio lilikuwa limekoza kuliko yote.

"Sumu imeisha lakini endelea kuzungusha Qi ili kiponya viungo vyako vya ndani" aliongea Fahad na kutoa viganya vyakw katika mgongo wa binti huyo. Akayakusanya yale mawe na kutoka nje.

"Vipi?" Aliuliza Master Lu.

"Zoezi limeenda vizuri, ila atahitaji wiki moja hivyo asisumbuliwe" alijibu.

"Sawa hakuna shida"

"Haya mawe yahifadhi vizuri isipokuwa hili, liweke mlangoni. Miongoni wa watakao kuja leo mmoja wao ndio atakuwa muhusika"

"Nashukuru sana sijui niseme au nikupe nini"

"Tutaongea siku nyingine nahitaji kipumzika"

"Kama hutojali naomba nikuandalie eneo la kupumzika hapa hapa kwangu"

"Nataka sehemu tulivu isiyokuwa na harakati za watu. Nahitaji kutulia ili nirudi katika hali yangu ya kawaida"

"Ipo sehemi ya hivyo, twende nikupeleke" aliongea Master Lu na kuongoza njia. Akaacha maagizo kiwa Yuna asisumbuliwe na mtu yeyote yule. Nyumba ya mzee huyo ilikuwa katika eneo kubwa sana ni kama vile ngome ya kifalme.

Wakaelekea mpaka katika mlango mkubwa, wakaingia na kutokea katika bustani. Katikati ya bustani hiyo kulikuwa na nyumba kubwa kiasi. Wakaelekea ilipo nyumba hiyo, "kaa hapa mpaka utakapomaliza mapumziko yako" aliongea Master Lu.

"Nashukuru, nahitaji pia unipelekee barua kwa mzee Mash. Mwambie asiwe na shaka nitarudi baada ya kupumzika" aliongea Fahad na kuingia ndani ya nyumba hiyo.

**********
Wiki moja baadae.

Miale ya jua ilianza kung'ara, rangi ya dhahabu katika mawingu iliwafanya ndege waanze kuimba kuimba katika viota vyao. Wakazi wa nyumba ya mzee ya Lu wakaanza kutoka katika maeneo ya malazi yao.

"Master" alifika nyumbani kwa mzee Lu mfanyakazi mmoja akionekana kuishiwa na pumzi. "Nini asubuhi hii tena" alifungua mlango.

"Ni bora uje kujionea mwenye" aliongea na kuongoza njia. Walipofika wakakuta wengine wakiwa wanashangaa.

Hata yeye mwenyewe akajikuta akishangaa, maji maji yakajaa kwenye macho yake. "Yuna mwanangu ni wewe" aliongea akipita mbele.

Mbele yake alikuwa mschana mrembo kupita maelezo. Nywele zake ndefu mithili ya silky zilikuwa zikining'inia karibi na kiuno chake. Alikuwa aking'ara kupita maelezo.

"Baba, ni muda mrefu sana sijakanyaga nje" aliongea kwa sauti ya chini na laini.

"Mungu wangu wa Nirvana, hata nikifa leo sitakuwa majuto yeyote. Hatimae nimeona tabasamu lako lilitoweka kwa muda mrefu" Master Lu aliangukia magoti. Machozi yakatengeza michirizi katika mashavu yake.

"Baba inuka" aliongea binti huyo akimshika mkono babaake. Mwalimu Lu akainuka ila bado machozi yalikuwa yakimtoka. Alikuwa na furaha maelezo. "Twende ndani tukaongee vizuri" hatimae akakusanya nguvu na kuongea.

Wakaelekea katika nyumba kubwa, Master Lu akaagiza chai. Wakakaa mezani, akamuangalia vizuri binti yake na kutabasamu.

"Wazee wanasema msaada unakuja pale usipotarajia" aliongea.

"Yuko wapi bwana alienisaidia" aliuliza Yuna.

"Amesema anahitaji kuwa peke yake kwa ajili ya biashara"

"Naweza kwenda kumuona"

"Haitawezekana mpaka pale atakapotoka mwenyewe"

"Unamaanisha, amejitenga kwa muda"

"Ndio, zawadi ametumiq nguvu sana kukutibu"

"Sidhani, yule si mtu wa kawaida. Nilichokuwa nahisi katika moyo wangu ilikuwa ni kama nimesimamiwa na kiumbe mtakatifu. Qi yake haikuwa na hata chembe za uchafu" aliongea Yuna na kumshangaza babaake.

"Qi kutokuwa na chembe chembe za uchafu, unataka kunambia yupo katika daraja la Nirvana" aliuliza kwa mshangao.

"Sijui ila ni wazi kwamba, si mtu miongoni mwetu. hata akawa mungu ambae ametusbukia katika umbile la binadamu" aliongea Yuna.

"Kama ni hivo hata mimi nataka kwenda kumuona, ikiwezekana tumshawishi ajiunge na familia yetu" baada ya muda mrefu wakakubaliana waelekee ilipo bustani ndipo Fahad alikuwepo.
 
Black star 2: Astra 07
Na Tariq Haji
0624065911

Ndani ya bustani.

Fahad alikuwa kasimama akiangalia angani, mikono yake ikiwa imekutana kwa nyuma. "Eunice, Minhe, Zayan ni matumaini yangu mko vyema" alijisemea. Alihisi upweke ndani ya moyo wake lakini hakuwa na namna zaidi ya kuukubali kutokana uhalisia wa mambo ulivyo.

"Karibuni" aliongea na kugeuka, nyuma yake walikuwa wamesimama Master Lu na Yuna. "Umejuaje kama tumefika wakati tumejitahidi kuficha uwepo wetu" aliuliza Yuna.

"Kuna mengi ambayo huyajui binti" alijibu na kutabasamu.

"Naomba utusamehe lakini udadisi umeshinda uvumilivu" aliongea Master Lu na kuinamisha kichwa. "Master Lu, mzazi hatakiwi kuinamisha mbele ya mtoto wake. Ni alama ya udhaifu" aliongea Fahad akinpa ishara ya kuinua kichwa chake.

"Nikuiteje, mpaka sasa sielewi" aliongea Master Lu.

"Fahad linatosha"

"Sitakuwa nakuvunjia heshima kukuita hivyo" aliongea kwa wasiwasi kidogo.

"Hapana, mimi sifati mila zenu kwa sababu si miongoni mwenu. Nitokapo watu wote wananiita kwa jina langu tu. Na hivyo ndivyo nitakavyo hata kutoka kwako" alijibu Fahad na kumtoa wasiwasi.

"Sawa Fahad, kuna jambo Yuna anataka kuongea ma wewe" aliongea na kumuangalia Yuna.

Yuna akasogea mbele kidogo na kupiga magoti, "kama sehemu ya shukrani naomba nikusujudie mara tatu" aliongea binti huyo na kutaka kufanya hivyo.

"Yuma, mwanamke yeyote anatakiwa kushuka chini mbele ya mumewe tu. Hata hivyo imani yangu hairuhusu mtu kunisujudia wala kusujudia mtu mwengine. Badala ya kusujudu kwanini usiwe mdogo wangu tu".

"Hivyo unaniruhusu nikuite kaka mkubwa" aliongea mwanamke huyo.

"Ndio, na ndugu hawasujudiani" aljibu Fahad na kumuinuwa.

Machozi yakatengeza njia mashavuni mwa Yuna, akaangua kilio kizito. "Nilijuwa sitaweza tena kutoka ndani ile nyumba. Laiti ungechelewa kidogo tu basi ningechukuwa uhai wangu mwenyewe" alionga kwa kwikwi.

"Yuna, wewe mschana mwenye nguvu sana. Angekuwa mwengine wala asingeweza kupambana kwa muda mrefu kiasi hichi" aliongea Fahad na kumgusa kichwani.

"Master Lu, umemjua aliempa sumu Yuna" aliongea na kumuangalia mzee huyo.

"Ndio, ila kwasasa siwezi kufanya chochote kile. Ni jambo lililo nje ya uwezo wangu" alijibu na kujiinamia.

"Una maanisha nini kusema kuna mtu amenipa sumu" aliuliza Yuna kwa macho yaliyojaa udadisi.

"Ugonjwa wako haukuwa wa asili, kuna mtu amekupa sumu iliyosababisha mzunguko wako wa Qi kizunguka kinyume na kawaida. Na hilo ndilo lililokuwa linakuuwa kwasababu lilikuwa linaathiri viungo vyako vya ndani" alifafanua Fahad.

"Nani anadiriki kunipa sumu, kwa kosa gani nilomfanyia. Baba umesema unamjua aliefanya hivyo, naomba uniambie ni nani sasa hivi?" Alivimba kwa hasira.

"Siwezi kukwambia" aliongea Master Lu bila kusita.

"Kwanini?" Alifoka.

"Tupunguze hasira Yuna, ana sababu zake za kutokukwambia usishindane nae" aliongea Fahad.

"Ahsante Fahad, muda ukifika nitamwambia lakini kwasasa naomba anisamehe" aliongea.

"Ndani ya mwaka mmoja, niachie Yuna niondoke nae. Akirudi utamwambia kila kitu kwasababu atakuwa na uwezo wa kujibu alichofanyiwa" aliongea Fahad na kuwafanya wote wawili wamuangalie kwa macho ya sintofahamu.

"Sidhani kama mwaka mmoja utatosha kumfikisha katika daraja ambalo ataweza kupambana nao" aliongea Master Lu.

"Yuna kwasasa yupo daraja la transidens ila ndani ya mwaka mmoja nitamfikisha si chini ya daraja la Jin dan. Ikiwa ataweka juhudi zaidi huenda akavuka na kuwa juu zaidi" aliongea Fahad kwa kujiamini.

"Kwani wewe ukobdaraja gani" aliuliza Yuna.

"Hilo utajua siku nyingine lakini niamini naweza kupigana watu wote katika ulimwengu huu kwa wakati mmoja bila kutoka hata jasho" alijibu.

"Mtu mwenye nguvu zaidi katika mji huu ni mfalme, na yeye yupo daraja la Tong san" aliongea Master Lu.

"Ndio maana nikakakwambia hakuna mtu katika ulimwengu huu anaeweza kunitoa jasho. Jin dan ni daraja moja la chini kabla ya kufika Tong san" alikuwa akijiamini kupita maelezo.

Baada ya mdahalo wa muda mrefu, hatimae Yuna akakubali kuenda safari ya mafunzo pamoja na Fahad. "Kesho tutaondoka, lakini itabidi ukajisali katika chama cha wawindaji kwanza" aliongea.

"Kuhusu hilo usijali, sisi wazee huwa tumepewa nafasi mbili kwa ajili ya watu wetu" aliongea Master Lu.

"Sawa basi kesho tutatoka, hatutarudi humu ndani kwa mwaka mzima. Na ndani ya kipindi hicho, shitaji miwe mnawasiliana kwa njia yeyote ile. Tukirudi ndani ya mji ni kwa ajili ya kuchukuwa kazi tu au kuleta majibu ya kazi" alifafanua Fahad.

********

Miezi sita baadae

Katika msitu mnene, mingurumo ya kiumbe ilisikika maeneo yote ya pori hilo. Watu wawili wakapita kwa kasi wakikimbiza kiumbe hicho, "Yuna zamu yako" aliongea Fahad na kuounguza mwendo. Yuna aliekuwa na upanga mkononi akaruka juu kwa nguvu na kutua mbele ya kiumbe hicho.

"Huendi pahali leo" aliongea na kuweka upanga wake sawa. "Grrrr" kiumbe huyo alinguruna na kitoa makucha yake. Kwa kasi akamfata Yuna, akamkwepa na kumkata mguu mmoja, hakumuachia hata nafasi ya kuugulia. Akatenganisha kichwa na kiwili wili.

"Umeiva sasa" Fahad alitua kutoka mtini na kuongea, "yote ni kwasababu ya maelezo yako" alijibu akiuzungusha upanga wake kwa ajili ya kuutoa damu kisha akauridisha kwenye ala yake.

"Tutapumzika karibu na mto, kesho tutaelekea Astra kwa ajili ya kukabidhi kichwa" aliongea.

"Hamtaweza kuondoka na kichwa cha mnyama huyo" ghafla wakasikia sauti ikitokea juu ya mti akatua mtu aliekuwa amevaa kinyago.

"Na kwanini tusiweze kuondoka nacho" aliuliza Yuna

"Kwasababu sisi ndio tumeanza kumuwinda, baada ya kujeruhi nyinyi mmekuja kumalizia tu" alijibu mtu huyo na baada ya sekunde kadhaa wakadika wengine zaidi ya kumi.

"Samahani, huyu mnyama tumekuwa tukimuwinda kwa wiki sasa. Na hatujawahi kuwaona hata siku moja, inakuaje mseme leo kuwa nyinyi ndio mlomjeruhi" aliongea Fahad kwa sauti ndogo.

"Ndio hivyo haijalishi kama ni kweli au si kweli, huyo mnyama ni wa kwetu" aliongea kwa kebehi.

"Kwa hiyo unakiri kuwa unataka kutudhulumu".

"Shaini, nani anadiriki kusema wanafunzi wangu wanataka kudhulumu" sauti nzito na kali sana ikasikika kutoka nyuma ya kikundi hicho.

"Mwalimu huyu mpuuzi anataka kuchukuwa lindo letu" aliongea yule aliekuwa mbele na kusogea pembeni.

"Ili nikusamehe sujudu mara tati kisha ukate mkono wako mmoja" aliongea mzee mmoja mtu mzima sana.

"Kwani kosa langu ni lipi mpaka niombe msamaha" aliongea Fahad na kupita mbele. Yuna alikuwa nyuma yake, "hahahhah, vizuri sasa madhali umekataa kufanya nilivyokuambia nitakuuwa kisha nitamchukuwa huyo mwanamke akawe kahaba katika shule yangu. Nina imani wanafunzi wangu watajifunza kuwa wazima kupitia mwili wake".

Kauli hiyo ikamkera sana Yuna, akataka kuchomoa upanga wake lakini Fahad akamzuia ns kutikisa kichwa akimpa ishara ya kutofanya hivyo.

"Mzee umefanya kosa kubwa sana, kunitukana mimi si tatizo lakini linapokuja suala linalohusu mdogo wangu. Usinilaumu kwa kitakachokukuta" aliongea Fahad.

"Mshenzi mkubwa wee" kijana mmoja akaongea na kumfata Fahad kwa kasi. Fahad akakunja ngumi na kukaza misuli ya mguu. Yule kijana alipokaribia akakutana na mimi kali sana iliyotua kifuani. Kwa sekunde kadhaa ni kama vile mida ulisimama kisha akafyetuka kutoka mkononi kwa Fahad na kujibamiza katika mti.

Mwenzake mmoja alikwenda kumgusa na kumeza funda kubwa la mate. Akamgeukia mwalimu wake na macho yaliyojaa huzuni "amemuua".
 
Kiongozi,shukrani sana kwa somo lako,hii ni zaidi ya kuwa spiritual,haya mambo unayoandika hapa ni kama muunganiko wa vingi sana,kuchumbua mmoja mmoja itakuwa ndefu sana, nasubiri muendelezo nipate jibu la maswali niliyo nayo. Asante

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Black star 2: Astra 08
Na Tariq Haji
0624065911


"Unapoongelea suala la kuchukuwa uhai wa mtu basi huna budi kujipanga kuutoa wako" aliongea Fahad na kutoa ile fimbo yake ya chuma. Akaizungusha mara kadhaa na kuikita chini, "kama kuna mwingine anataka kuchukuwa maisha yangu, anakaribishwa kujaribu".

"Hahaha, takataka kama wewe unajiamini kupita maelezo" aliongea yule mwalimu wa wale vijana. "Ni takataka tu ndio inaijuwa takataka mwenzake" alijibu.

Yuna aliekuwa nyuma akajikuta anacheka kwa nguvu, yule mwalimu akapandwa na hasira. "Sina haja ya kupigana na wewe nisije nikaambiwa nilikuwa naonea mtu" aliongea na kuinuwa mkono juu.

Vijana wake wote wakamzunguka Fahad na kutoa silaha zao. "Ni matumaini yangu mtanipa pambano zuri" aliongea na kuchomoa fimbo yake. Akaishika vilivyo mkononi. Wale vijana wakaanza kumsogelea, Fahad akawaangalia kwa makini kisha akatabasamu.

Wale vijana wakamvaa, Fahad akawa anawakwepa pasi na kushambulia. "Hii shule yenu inatoa mafunzo ya ulemavu ama vipi" akazidi kumchokonoa. Kijana mmoja akasogea kwa kasi na kukita ncha ya upanga wake katika mgongo wa Fahad.

"Nimekupata" akaongea kama sehemu ya kujipongeza, "Yuna nimehisi kama kuguswa mgongoni" aliongea na kukaza misuli ya mgongo. Yule kijana kila alivyojaribu kuuvuta upanga wake, haukutoka.

"Master huyu si binadamu" alipiga kelele, Fahad akalegeza misuli na ule upanga ukatoka. Akageuka kwa kasi na kwa kutumia ile fimbo. Akamchapa ya mbavu, yule kijana akagugumia. Fahad akazungusha silaha yake kwa kasi na kumchapa mgongoni.

"Aghhhh!" Alilia, hakuishia hapo. Akazunguka kwa kasi na kumchapa teke la tumbo na kumbamiza katika jiwe. "Master amenitia ulemavu" alilia akitokwa damu za mdomo.

Sasa Fahad alikuwa ameshika kasi, alinepa kulia akanepa kushoto. Akadunda na kuruka, alipotuwa silaha yake ilituwa kichwani kwa mtu. Na baada ya dakika moja tu, wote wakawa chini wakiugulia.

"Unaweza kuja mwenyewe sasa" aliongea akimnyooshea yule mwalimu ile fimbo.

"Ngoja nikuonyeshe ufundi wangu sasa" aliongea yule mwalimu na kukutanisha viganja vyake. Mvuke mwekundu ukaanza kutoka mwilini mwake. Mvuke huwo ukajiunda na kuwa upanga mkubwa, karibu mita nne. Akamshushia Fahad na kumtandika kwa nguvu, "Fahad" Yuna aliita huku moyo ukimuenda mbio.

"Hahaha, bahati yako ilikuwa mbaya ulivokatoza njia yangu" ali0ngea kwa majivuno.

"Mi nikajua kitu kikubwa kumbe mchezo wa kitoto" aliongea Fahad baada vumbi kutawanyika. Iliokuwa imechanika ni nguo yake ya juu tu.

Yuna akashangaa, "hivi huu ni mgongo wa mtu au jabali" akataka kuugusa. "Binti, tambuwa mipaka yako" aliongea Fahad na kuzinduwa. "Samahani halikuwa kusudio langu" alijibu Yuna mashavu yake yakiwa mekundu. Akaangalia chini kwa aibu.

"Haiwezekani, nimeweka uwezo wangu wote latika pigo lile" aliongea yule mwalimu macho yakikaribia lutoka kwenye matundu yake. "Ila tutakutana tena na niamini utalipa kwa udhalilishaji wa leo" aliongea na kutoa kitu kama karatasi. Akaichana, ukatokea mwanga mkubwa ulipotoweka alikuwa kashapotea.

"Sikujua kama mwalimu wenu ana mbio kiasi kile" aliongea akiwaangalia wale wanafunzi waliokuwa wamelala chini wakigugumia. "Tafadhali usituue" aliongea mmoja akijaribu kupiga magoti.

"Sina haja ya kuua sisimizi" alijibu na kumuangalia mmoja aliekuwa na mwili mkubwa. "Wewe vua hiyo nguo ya juu" alitoa amri. Yule kijana hakutaka hata kuchelewa akaivua na kumkabidhi. Akaivaa na kumgeukia Yuna, "tuondoke" aliongea.

*******
Astra.

"Master Jin nini kimetokea" alifika mmoja kati ya wanafunzi na kumsaidia. "Nenda kamwite Master Li na Master An, waambie kuna kikao cha.muhimu sana" aliongea akihema. "Pia na wazee wote" aliongea kwa nguvu.

Gahena ambae ndie mwanafunzi aliempokea mwalimu huyo, akakimbilia katika ukumbi wa mapumzio ambako walimu wengine ndipo walipokuwepo.

"Samahani walimu, nimeambiwa nije kuwaita kwa ajili ya kikao cha dharura" aliongea baada ya kuingia katika ukumbi huwo.

"Nani aliekuagiza" aliuliza mzee mmoja

"Master Jin amerudi kutoka mawindo lakini anaonekana amejeruhiwa. Pia hakuna hata mwanafunzi mmoja alierudi" aliongea.

"Eti nini" alifoka Master Chen ambae pia ni miongoni mwa wazee wa shule hiyo ya martial arts.

"Hebu tusikurupuke, twendeni tukamuone kwanza tutajuwa kila" aliongea mtu mwengine ambae alionekana kuwa mzee zaidi ya wote waliokuwa hapo.

Gahena akageuza na kuongoza njia, wote wakaelekea katika ukumbi wa Master Jin. Wakamkuta akiwa kakaa kwenye kiti chake. Alionekana kuchoka sana, "haraka mpeni kidonge cha Qi, inaonekana ameitumia karibia yote" aliongea Master Chen.

Mmoja kati ya walimu akamfata na kumpa kidonge cheusi, Master Jin akakitafuna kukimeza. Miale ya rangi mbali mbali ikamzunguka. Ilipotoweka akashusha pumzi ndefu na nzito. Ilikuwa alama ya unafuu kwake.

"Master Jin, nini kimetokea na wanafunzi uliotoka nao wako wapi?" Aliuliza Master Chen.

Master Jin akawaeleza kila kilichotokea isipokuwa aliongezea uongo mwingi na kuwafanya wapate hasira.

"Fahad nilijua tu tokea nilivyomuona alikuwa amezungukwa na upepo mchafu" aliongea Master Chen.

"Master Chem unamjuwa huyo mtu" aliuliza Master An.

"Ndio, ni miongoni mwa watu waliokuja kwa ajili ya kuongeza taaluma" alijibu.

"Kama ni hatari hivyo, kwanini hujamshawishi akajiunga na shule yetu" aliongea Master Dan ambae ndie yule mzee kuliko wote.

"Hapana, hana uwezo kiasi hicho. Kwanza ni takataka tu, mwili wake hauna hata Qi. Alishindwa katika majaribio ya kujiunga na shule za martial art" alifafanua.

"Sasa inakuwaje mtu ambae hata Qi anaweza kusimama bega kwa bega na Master aliefika daraja la Jin dan" aliuliza Master Dan.

"Ndio hilo ninalo shindwa kuelewa, anaweza akawa anajifunza martial art ya majini. Kawaida huwa hatuna njia ya kupima Qi ya majini" aliongea.

"Hivi sasa yuko wapi?"

"Amejiunga na chama cha wawindaji"

"Andikeni barua ya kumtaka aje kwa ajili ya kupata adhabu yake" aliongea Master Dan na kuondoka. Alionekana kama yeye ndie kiongozi wa shule hiyo ya Hai Yu martial art. Shule ambayo upanga kama silaha pekee.

"Fahad umekwisha" alijisemea Master Chen na kuinuka, akaaga na kuondoka. Mtu huyo alitokea kumchukia sana Fahad, chuki yake ilianza punde tu baada ya kumuona mara ya kwanza.

"Master Jin tuone kama utaweza kumsaidia" alijisemea kuelekea katika nyumba anayoishi.

"Nitamtumia shelisisa, unajuta kuninyima binti yako. Urafiki wetu wa miaka mingi ulikwisha siku uliyokataa kunikabidhi mkono wa Yuna. Sijui nani kamponya lakini nakuahidi safari hii, nakuangusha na Yuna anakuwa chombo changu cha starehe" akacheka kwa nguvu na kukaa kwenye kito chake.

Akatoa karatasi ndefu, akachukuwa brashi dhana na kuichovya kwenye wino mweusi. Akaandika barua kama Master Dan alivyoagiza, alipomaliza akaikunja vizuri na kufanya kwenye bahasha. Akamuita Gahena ambae ndio mwanafunzi wake pendwa.

"Ipeleke chama cha wawindaji" alimpa maagizo. Gahena akatoka na mnyama wake. Mnyama huyo alifanana na simba lakini alikuwa na mbawa pamoja na kichwa cha mwewe. Akaelekea chama cha wawindaji na kuikabidhi barua hiyo. Akaaga na kuondoka.
 
Black star 2: Astra 09
Na Tariq Haji
0624065911


Siku ya pili mchana, Fahad na Yuna wakarudi Astra katika chama cha wawindaji kwa ajili ya kukabidhi kichwa cha mnyama waliemuua.

"Fahad afadhali umefika" aliongea Raul ambae ni kijana wa mapokezi.

"Kuna nini kwani?"

"Master Jerome anahitaji kukuona, ni muhimu sana" alijibu. Fahad akakikabidhi kichwa kwa Raul, akampa ishara Yuna amfate. "Hapana unahitajika peke yako" aliongea Raul.

"Yuna ni mdogo wangu, ninapokwenda anakwenda anasikia ninachosikia" aliongea pasi na kugeuka. Akaelekea mpaka katika mlango wa kuongia katika ofisi ya Master Jerome.

"Ingia" kabla hajagonga, akasikia sauti ikitokea ndani. Akafunguwa mlango na kuingia. Ndani alikuwa Master Jerome pamoja na Master Lu. "Ba...", "Yuna". Yuna alitaka kuita lakini Fahad akamkatisha.

"Samahani, Master Lu ni muda mrefu hatujaonana" aliomba msamaha na kuongea. "Ndio Yuna" alijibu kwa mkato bila kuongea kitu kingine. Hayo ndiyo yalikuwa makubaliano yao.

"Master Jerome nimesikia unahitaji kuniona" aliongea Fahad akimuangalia mtu alieonekana kuwa mashaka kidogo akilini mwake.

"Ndio tumepokea malalamiko kutoka shule ya Hai Yu kuwa umetumia nguvu zao kumaliza kazi yako" aliongea.

"Nilitegemea watarudi ila sikudhani kama itakuwa haraka kiasi hiki" alijibu na kuvuta kiti. Akakaa na kutabasamu, tabia hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa watatu hao kuishuhudia kutoka kwa Fahad.

"Kwa hiyo unakiri kuwa umefanya hivyo au"

"Hapana sijakiri kwa chochote kile, hata hivyo mimi sie niliemaliza hiyo kazi. Ni kazi ya mdogo wangu Yuna, na ngoja nikwambie kitu Master Jin. Mtu yeyote anaediriki kuongea upuuzi kwa mmoja kati ya watu wangu basi ajipange kulipa kwa damu" aliongea na kuachia tabasamu zito.

Ghafla hali ya hewa ndani ya chumba hicho ikabadilika. Master Lu, Jerome pamoja na Yuna wakajikuta katika wakati mgumu sana. Mapafu yao yakawa yanapata shida kupata pumzi.

"Mume wangu" sauti hiyo ikamzindua kutoka kwenye dimbwi la hasira zake. Ilikuwa ni sauti pekee iliompoza hasira. "Eunice" akajisemea na kushusha pumzi, hatimae wote humo ndani wakakohoa na kupata pumzi nzuri.

"Nini kilichotokea" aliuliza Yuna, Master Lu pamoja na Master Jerome wakatoka kwenye viti vyao na kupiga magoti. "Tusamehe sisi tumeshindwa kuona uwezo wako" waliongea kwa pamoja wakitetemeka.

Kwa Yuna muonekano wa Fahad ulikuwa wa kawaida, lakini kwa master Lu na Jerome walikuwa wakiona kitu kingine kabisa.

Nyuma ya Fahad kulikuwa na kivuli kikubwa. Kilikuwa na mikono zaidi ya sita na Qi iliokuwa inatoka kwenye kivuli hicho ilikuwa ni Qi ambayo hawajawahi kuiona zaidi ya kuisoma kwenye vitabu vya kale.

"Simameni" aliongea Fahad, "tunawezaje kusimama wakati tumekuwa vipofu" alijibu Master Lu.

"Nitawaadhibu siku nyingine, kwanza tumalizane na hawa" kauli hiyo ikawainuwa wakiwa na tabasamu. Walijuwa fika watasamehewa baada ya adhabu.

"Sasa niambieni, nani alieandika hiyo barua na inasemaje?" Aliuliza.

"Alieandika ni Master Chen kwa niaba ya Master Dan ambae ni mlezi wa shule ya Upanga ya Hai Yu" aliongea Master Jerome.

"Wamesema nifike baada ya muda gani na kwanini?"

"Wamekupa mwezi mmoja ufike kwa ajili ya kupokea adhabu yako"

"Kwa hiyo wameshafanya maamuzi kabla ya kusikiliza upande wangu, wazee wa huku inaonekana hawajafunzwa vizuri udogoni. Sasa wajibu, waambie nitakwenda baada ya miezi sita, na waambie pia ndani ya miezi hiyo wajipike kisawasawa kwasababu itakuwa ndio mwisho wa shule yao. Na sitojali ikiwa wataomba msaada kutoka shule nyingine yeyote ama kutoka tawi kuu kwasababu vyovyote itakavyokuwa kiama kitawashukia"

"Nimesahau, waambie pia ndani ya kipindi hicho yeyote atakaenitafuta atakufa kwa mikono yangu" alimaliza kuongea, akasimama na kumuamuru Yuna waondoke.

Master Lu na Master Jerome wakabaki wakiangaliana, "sikuwahi kutegemea katika maisha yangu kama nitakutana na Master mwenye uwezo kama ule" aliongea Master Jerome akikaa kitini. Muda wote huwo alikuwa amesimama, akatoa kitambaa na kujifuta jasho.

"Andika hiyo barua haraka wewe, au hujasoma historia yake vizuri" aliongea kwa kihoro Master Lu.

Master Jerome akatoa karatasi na kuandika kama Fahad alivyotaka, hakuongeza wala kupunguza jambo. Master Jerome alikuwa na mtaalamu wa aina yake, alikuwa na uwezo wa kuongea na mtu ndani ya jengo hilo kwa mawazo tu bila hata kufunguwa mdoma.

"Raul njoo ofisini" aliongea na baada ya sekunde chache Raul akafika.

"Shuka hii barua, ifikishe shule ya Upanga ya Hai Yu. Usiifungue, wakabaidhi na uondoke haraka iwezekanavyo na jambo jingine. Usiongelee habari yeyote inayohusiana na Fahad. Futa taarifa zake zake zote, na andaa kitambulisho cha dhahabu kwa jina lake" alitoa maelekezo.

"Lakini hajafikisha hata mwaka, kumpa kitambulisho cha dhahabu ni kukiuka sheria za chama. Nahofia makao makuu watatuandama bila huruma" aliongea Raul.

"Raul kijana wangu kuna sheria hazifanyi kazi kwa baadhi ya watu. Si za chama tu bali hata za ulimwengu, nina uhakika makao makuu wataelewa"

Maneno yakamfanya Raul asiendelee na kuuliza chochote, akaaga na kutoka. Akaelekea sehemu lilipo banda kubwa. Akapiga mruzi, mwewe mkubwa mweupe akatua kwa kasi akaitokea angani.

Akapanda katika mgongo wa ndege huyo na kupotelea angani kwa kasi kama aloshuka nayo. Ndege huyo alisafiri kwa kasi na baada kama dakika tatu hivi akawasili katika uwanja wa shule hiyo.

"Umekuja kufanya nini?" Aliongea mmoja kati ya walinzi waliyokuwepo eneo hilo.

"Nimepewa ujumbe niufikishe kwa Master Dan" alijibu bila kuonesha alama yeyote ya wasiwasi.

"Tayari imefika, nipe mimi nimpelekee"

"Kuwa na adabu bwana mdogo, nimepewa maelekezo niikabidhi kwa Master Dan yeye kama yeye"

"Unadiriki kunitusi katika viwanja vya eneo ninalosoma, jipige vibao kumi labda nitakusamehe" aliongea na kutoka upanga wake.

"We lofa sikia, ukiwa tayari kufa ndio utoe silaha yako, natala nimkabidhi mwenye mbwa na sio mbwa" alifoka Raul na kuinuwa mkono juu.

Mwewe wake akatanua mabawa na kutoa ukwenzi mkali sana. "Kuna nini mbona vurugu mchana wote huu" alitoka Master Chen na kuongea.

"Inaonekana hamuwapi malezi mazuri watoto wenu, kijana mchanga kama anadiriki kunikosea heshima. Hata babaake na babu yake wangeniona leo wangepiga magoti" aliongea Raul.

"Samahani kwa kutokuwa na maelewano mazuri, kijana ondoka nitachukuwa kutoka hapa" aliongea Master Chen. "Nikusaidie nini" aliendelea.

"Nimepewa barua na Master Jerome kwa niaba ya Fahad niifikishe mkononi mwa Master Dan" aliongea.

"Anha, kama ni hivyo hakuna shida. Wewe nikabidhi tu mimi nitamfikishia" aliongea akitoa mkono.

"Kwa heshima na taadhima, tafadhali usisukume uvumilivu wangu kwenye kingo. Nataka hii barua ipokelewe na Master Dan bila hivyo nitaondoka nayo" alifoka.

"Mwanaharamu mkubwa wewe, unadhani hapa ni chama cha wawindaji kwamba unaweza kufanya unalojisikia" alifoka Master Chen.

"Unataka kupigana sio" aliuliza Raul.

"Wewe ni bwana mdogo tu, huna hadhi ya kupigana na mimi"

Raul akavuta pumzi nyingi na kupiga mruzi mkali sana, mruzi huwo ulisikika kwa umbali mkubwa sana. Baada ya sekunde chache upepo mkali sana ukavuma kupita eneo hilo.

************
Black star 2: Astra 10
Na Tariq Haji
0624065911


Kivuli kikubwa cha mwewe aliekuwa anazunguka angani kilionekana ardhini. Kivuli hicho kilimfanya mpaka yule mwewe mweupe alaze kichwa chini kama ishara ya woga na kutoa heshima kwa ndege aliekuwa akizunguka angani.

"Bado unataka kupigana" aliuliza.

"Inatosha" sauti nzito ikatokea mlangoni. Master Dan akatoka akionekana kukerwa na jambo hilo.

"Master Chen unataka kuleta maafa katika shule kisa ni kujisikia kwako, unaweza wapi kupigana mwewe wa vita" alifoka kwa nguvu.

Mwewe mkubwa rangi ya dhahavu akatuwa nyuma ya Raul na kufunguwa mbawa zake kama ishara ya kuwa tayari kwa vita. "Daraja la Tong san" alijisemea Master Chen na kumeza funda kubwa la mate. "Raul acha yaliyopita yapite, mimi na wewe hatuna kinyongo" aliongea akirudi nyuma.

"Master Dan, hii barua nimeambiwa nikufikishie" alimpuuza Master Chen na kumpa heshima Master Dan. Akatoa ile bahasha yenye barua na kumkabidhi.

"Kukukabidhi huku kunanifanya niwe nimekamilisha kazi yangu" akaaga na kugeuka. Akampa ishara yule mwewe mkubwa, akapaa na kupotelea angani. Akapanda mgongoni kwa yule mwewe mweupe nae akapotelea huko huko.

Master Dan akarudi ndani kwake akiwa na ile barua mkononi. Alipofika tu akaifunguwa na kuisoma, akajikuta akivimba kwa kwa hasira. "Bwana mdogo anadiriki kutufanya tumngojee" alisema kwa hasira mpaka vitu baadhi vikaanguka ndani ya chukba hicho.

Akatoka ndani ya chumba hicho na kuwakuta walimu wengine wakimsubiri. "Wamesema nini?" akauliza Master Chen, alionekana kuwa na pupa kuliko wengine.

"Tunahitaji, kukutana tena tujadili hili. Huyu bwana mdogo anaonekana si mtu wa kawaida. Mpaka kumfanya mtu mkorofi kama Jerome aandike barua ya hivi" aliongea akielekea katika ukumbi wa makutano.

Ndani ya ukumbi huwo.

"Fahad anaonekana kuwa na kiburi sana, mtu hawezi kuwa na kiburi kama hakuna mkono mwingine nyuma yake. Kwanza inabidi tufanye uchunguzi wa kina kuhusu maisha yake kabla hajaja Astra. Wakati tunafanya hilo, Master Chen andika barua kuelekea makao makuu. Omba vijana wote walio kuanzia daraja la tramsidient waje huku wiki kabla ya muda aliosema huyu mpuuzi".

"Andika barua nyingine kadhaa kwenda shule kadhaa ambao zimeingia makubaliano ya kimsaada na shule yetu. Waambie tunahitaji wanafunzi wao gwiji zaidi , hivyo wote wawalete huku wiki moja kabla".

"Andika barua nyingine kuelelekea katika familia ya mfalme, tumuombe awe mgeni rasmi kushuhudia pambano hilo. Na pia hakikisha una pandikiza chuki ya kutosha. Itakuwa jambo jema ikiwa mfalme ataingilia binafsi pale mambo yatakapokuwa si mazuri upande wetu".

"Mwisho andika barua kuelekea katika kikomundi cha Fenshi, wape kazi ya kumuwinda. Wasimuue lakini wamjeruhi kiasi cha kushindwa kushiriki au kuonekana siku ya pambano"

"Baada ya hapa nataka wanafunzi wote kuanzia daraja la transidient, wapelekwe katika chumba cha enzi. Ni wakati wa kuwapa martial art halisi ya shule yetu" alimaliza kuongea Master Dan. Akawaruhusu wote waondoke.

Master Chen baada ya kutoka hapo, akaelekea katika ofisi yake. Huko alitoa karatasi kadhaa na kuandika maagizo aliyopewa. Baada kama saa nzima akawa amemalizi, akatoka nje na kuita kipando chake. Alikuwa ni kunguru mkubwa mwenye macho mekundu. Alitisha haswa, akapanda mgongoni kwa ndege huyo na kuondoka.

Alizifikisha barua zote sehemu husika kama alivyoelekezwa. Haswa ile barua iliyokwenda kwa mfalame, ilikuwa imesukwa kuhakikisha sumu ya chuki inamvaa kisawasawa mfalme huyo.

Katika umbali mkubwa mrefu sana, karibua kilometa mia tano kutoka mji wa Astra. Katika milima mikubwa iliopambwa theluji katika vilele vyake. Fahad na Yuna walikuwa katika njia kuelekea katika kilele cha mlima mmoja wapo.

"Kaka mkubwa, kwanini tumekuja huku" aliuliza Yuna.

"Kwa miezi sita tutakuwa huku, na ndani ya kipindi hicho utajifunza na kuvuka madaraja mpaka kufika daraja la Jin dan" aliongea Fahad.

"Kwanini huku huku"

"Milima hii ina Qi ya kutosha itokanayo na mazingira, nitakufunza jinsi ya kunyonya nguvu hiyo na kuifanya ya kwako kabisa. Nitakufunza pia kuzalisha Do Qi kutoka katika mazingira yaliokuzunguka"

"Do Qi ni nini?"

"Kama ilivyo Qi, wengi wenu mnazungusha na kuishughulikia zaidi Qi ya ndani ya miili yenu. Ndio maana mnapokutana na mtu ambae ameipika misuli yake kisawasawa mnashindwa hata kama mumemzidi sana ki uwezo"

"Mmh!"

"Do Qi ni Qi ambayo unaizungusha kuzunguka mwili wako lakini kwa nje. Kazi yake kubwa kuipa misuli uimara zaidi na kuweza kustahamili vishindo".

"Lakini kutoka katika vitabu, binadamu ana meridian kumi na mbili na dantian tatu na vyote hivyo kazi yake ni kusafirisha Qi iliyokuwa ndani ya mwili tu".

"Na hapo ndipo wengi mnapokosea, ni kweli binadamu ana meridian kumi na mbili na dantian tatu. Lakini jambo ambali hamulijui binadamu wote wana meridian ishirini. Nane zinakuwa zimelala, zitaamka pale tu mtu atakapoanza kuzungusha Do Qi"

"Sijawahi sikia hilo"

"Hivi unajua maana halisi ya meridian na dantian"

"Hakuna asiejuwa hilo, mpaka mtoto ambae ameanza kuhisi jua usoni mwake basi anajuwa".

"Sidhani kama unajuwa maana halisi, wengi wenu mnafahamu kuwa meridian ni kama mito ushuruzikiyo kutoka katika mabonde, mito ambayo husafirisha Qi na kuikusanya katika sehemu moja kati ya dantian tatu zilizokuwepo katika mwili wa binadamu, si ndio?"

"Haswaa" Yuna alijiona ameshashinda.

"Kwa lugha rahisi ni hivyo ila kwa tafsiri yake halisi, ni zaidi ya hivyo"

"Ah!" Yuna akamaka.

"Meridian katika mwili wa binadamu ni njia maalum zinazosafirisha asili ya uhai wenyewe. Njia hizo zinataka kufanana na mito lakini sio ichurizikayo kutoka mabondeni kama mnavyodhani. Wengi mnajuwa kuwa Qi inatiririka kuelekea upande mmoja tu lakini kiuhalisia inatiririka kuelekea pande zote za mwili".

Yuna akaonekana kuchanganyikiwa kidogo, taarifa yote hiyo ilikuwa ni kama inaijaza kichwa chake. Alijaribu kutaka kuielewa yote kama ilivyo lakini ikashindikana.

"Huna haja ya kukariri kila ninachoongea, nitakufundisha kwa vitendo na hapo ndiyo utaelewa vizuri" aliongea Fahad na kuendelea.

"Dantian ni kama bwawa la maji, ili bwawa hilo liendelee kuwa vizuri basi ni lazima maji yawe yanaingia na kutoka pasi na kulazimishwa kujaa tu na kutoka mpaka yavutwe"

"Kama ulivyosema dantian ziko tatu, katikati ya macho mawili, katikati ya kifua na kwenye kitovu tumboni. Na kati ya hizo, kubwa yao ni hii ya tumboni na ndio ambayo wengo mnaijali sana. Mnasahau kuwa iliopp katikati ya macho imeungana na meridian zinazotoka katika ubongo na pia imeunganisha na ya kifua".

"Umewahi kusikia msemo usemao pale akili na moyo vinapoungana pamoja basi mmoja atafaidi matunda ya ukweli wa ulimwengu" alinyamaza kidogo kumuangalia Yuna ambae alikuwa haelewi tena kinachoongelewa. Ni kama kila alichokuwa ana kiamini kimefutwa kwa lazima katika akili yake na kumfanya kama mtoto ambae ndio anaanza kujifunza martial arts.
 
Back
Top Bottom