MSIMU WA PILI WA BLACK STAR UNAANZA SASA......
BLACK STAR SEASON 2
Black star 2: Astra 01
Mdani ya msitu mnene kinasikika kishindo kikubwa, "wapi huku" alijisemea akiinuka baada ya kujabamiza na miti kadhaa alipotuwa katika eneo hilo. Alijikumuta mchanga pamoja na kutoa majani kadhaa pamoja na vipande vya miti vilivyochoma katika nguo zake.
"Hii ndio shida ya kuvamia nyumbani kwa mtu pasi na mualiko" mpaka wakati huwo Fahad hakujua yuko wapi. Imepita karibia saa nzima kabla hajafanya maamuzi ya kuondoka eneo hilo. Alitembea kwa nusu nzima kabla ya kuanza kuona mwisho wa pori hilo.
Tabasamu laini likajichora usoni mwake, akaongeza mwendo ili afike alipopaona. Akiwa ana karibia kumaliza pori akaanza kusikia sauti za watu wakiongea ila hakuelewa kilichokuwa kikiongelewa kitokana na lugha hiyo kuwa ngeni katika masikio yake.
Akatahamaki alipokutana na watu wengi na wote walionekana wakielekea upande mmoja. Akawaangalia wote kwa makini na kugundua kuwa kila mmoja alikuwa na silaha. Alipojiangalia yeye alikuwa amevaa kofia tu. "Oh wewe pia ni mgeni" alisikia sauti ikitokea nyuma yake.
Akageuka, kama hisia za kujilinda tu. Akarudi nyuma, mbele kulikuwa na jitu kubwa. "Rahee nmekwambia usitishe watu" sauti nyingine ikatokea nyuma ya lile jitu kubwa.
"Lakini Masta mi sijamtisha eti" aliongea, Fahad akashusha pumzi. "Nmeshtuka wala usijali" aliongea na kustaajabu amewezaje kuelewa lugha ya wati hao. "Unashangaa umewezaje kuelewa lugha, hilo ni moja kati ya maajabu ya huku. Kila mtu anaongea lugha yake lakini tunaelewana hivyo hivyo. Kama hapa mimi naongea ulimi wa kwetu lakini wewe unaelewa" aliongea yule mtu mwengine.
"Anha sawa, mimi naitwa Fahad naweza kuungana na nyinyi" alijutambulisha.
"Hakuna shida, mimi naitwa Gahena na huyu Rahel mdogo wangu" yule mtu mwengine nae akajitambulisha.
Kiumbo Gahena alikuwa mdogo kuliko Rahee lakini alionekana kuchuchuka zaidi kiakili. Walitembea kwa muda huku Gahena akimueleza Fahad mawili matatu ya eneo hilo. Baada ya muda mrefu wakafika mbele ya mlango mkubwa. Ulikuwa mkubwa kiasi cha juu kutoonekana.
Wote wakakusanywa sehemu moja, "karibuni Astra sehemu ambayo kila kiti kinawezakana. Baada ya muda kidogo mtaonwa na wakufunzi wa hapa kwa ajili ya maswali kadhaa. Baada ya hapo mtangazaji akaondoka wakabakia wakiangaliana.
Macho mengi yalikuwa kwa Fahad ambae aliyapuuzia, hilo lilitokana na kuwa yeye alikuwa ni tofauti na wengi katika eneo hilo.
Wakiwa eneo hilo wakaanza kusikia watu wakiguna na wengine kupiga mayoe. "Pisheni bosi apite" walisikia sauti ikitokea nyuma. Waliomfahamu wakaanza kusogea isipokuwa Fahad.
"Fahad sogea, huyo anae kuja ni mtoto wa familia kubwa katika eneo hili" aliongea Gahena. Fahad akafanya kama hakumsikia, akaendelea kusimama pasi na kushughulika.
"Masiki atakufa yule" mtu mmoja akaongea akimnyooshea kidole. "Mwache afe tu, mtu gani asiejuwa nafasi yake" mwengine akajibu na kucheka.
"Wewe ni naji usietaka kumpisha bosi wangu, unamjuwa mtoto wa nani huyu" aliongea mtu mmoja aliekuwa mbele. Fahad hakujibu kitu, alimpotezea kabisa na kuendelea kuangalia mbele.
Mtu yule akatoa upanga na kumuwekea shingoni, "unajua jinsi ya kuutumia lakini" aliuliza Fahad.
"Hahaha, ina maana nibebe upanga na nisijue kazi yake" aliongea na kuendelea, "nahesabu mpaka tatu, kama hujasogea nakukata kichwa".
"Unapojiandaa kuuwa na wewe ujiandae kuweka maisha yako rehani" aliongea na kukunja ngumi, aliikaza ksawasawa. Alidhamiria kugeuka na kumtwanga ngumi hiyo ambayo aliamini kabida ingechukuwa uhai wa mtu huyo.
"Muda wa kuonana na walimu umefika, kila mtu atapita sehemu mtakayoelekezwa na kichukuwa kibao. Kibao hicho kitakuwa na namba ambayo ndio itakuwa tiketi yako ya kuonana na mwalimi" kabla hajafanya hivyo yule mtoa matangazo alirudi na kutoa tangazo.
"Una bahati sana mpuuzi wewe" aliongea yule mtu mwenye upange akiurudisha kwenye ala yake. Fahad akashusha pumzi na kuondoka. Akaelekea sehemu waliolekezwa na kuchukuwa namba yake. "Mia mbili na sabini" alijisemea na kutabasamu.
Akasogea pembeni na kukaa chini ya mti wenye kivuli. Gahena na Rahee wakafika nao na kuketi pembeni yake. "Umepata namba ngapi" aliuliza Gahena.
"Mia mbili na sabini"
"Mimi nimepata mia na hamsini na saba na Rahee kapata tisini na tisa".
"Hatuna budi kusubiri, kila mtu atakwenda ikifika zamu yake" aliongea Fahad na kulalia mgongo. Akavua kofia yake ya duara (alambara) na kujifunika usoni.
"Yaani huyu jamaa ni ndege huru, haoneshi kuwa na wasiwasi wowote ule wakati akijuwa kabisa kazungukwa na watu wenye nguvu sana" alijisemea Gahena.
Watu walikwenda kwa mujibu wa namba zao, Rahee alikwenda ilipofika ya kwake. Vile vile Gahena nae akaenda ilipofika namba yake.
Fahad hakuonesha kuwa na pupa yeyote ile, alitulia mpaka ilipotangazwa namba yake. Akainuka na kuwaaga wenzake, akaelekea alipoitwa na kupeleka chumba cha mwalimu ambae alitakiwa kumuuliza maswali.
Alipoingia ndani humo, akakaa kwenye kiti bila kuonesha wasiwasi wowote ule.
"Kwanini umekuja Astra" aliuliza mwalimu.
"Natafuta ukweli"
"Ukweli wa aina gani"
"Ukweli wa kila kitu"
"Kijana wewe ni mtu wa ajabu sana, katika maisha yangu nimewafanyia majaribio wengi lakini wote kama walikuwa hawatafuti utajiri basi ni umaarufu na nguvu. Unaweza kuenda".
Fahad akainuka na kushukuru, akaaga na kuondoka. Yule mwalimu akabaki akiuwangalia mgongo mkubwa wa Fahad uliokuwa umejaa na kujitandaza ndani ya nguo aliovaa.
Akarudi walipo Gahena na mdogo wake na kukaa, walikaa eneo hilo mpaka jioni ambako walipata ratiba kuwa, sehemu ya pili ya itaendelea siku inayofata.
Wakatawanyika na kuelekea katika majumba ya kufikia wageni. "Sisi tutalala hapa, wewe je?" Aliuliza Gahena.
"Mi sina pesa kabisa, nitatafuta mti nitalala. Nishazoea" alijibu. "Oh! Natamani ningekusaidia, lakini pesa haitoshi".
"Nashukuru kwa ukarimu wako, ila usijali" alijibu na kuwaaga. Akatafuta sehemu na kukaa kitako, akakunja miguu na kujiinamia.
Siku ya pili mapema akawahi sehemu ya majaribio na kukuta baadhi ya watu wakiwa tayari wamewasili. Maua yalivyomaliza kuchanua akafika yule mtoa matangazo.
"Kila mmoja atapita kwenye hilo jiwe, ataingiza QI yake. Hapa kutakuwa na walimu kutoka shule mbalimbali za Martial Art, watachagua wanafunzi watakaovutiwa nao. Ikiwa hutapata bahati ya kuchaguliwa na shule jua tu huna kipaji na ni vyema ikiwa utaondoka bila kufanya vurugu" aliongea.
Akaendelea, "baada ya kuongiza Qi yako kwenye hilo jiwe, litabadilika rangi. Ikiwa ni nyeupe wewe utakuwa na kipaji cha kawaida sana, manjano utakuwa na kipaji cha kawaida, buluu utakuwa na kipaji cha kiasi kuliko kawaida, kijani utakuwa na kipaji cha hali ya kati, zambarau utakuwa na hali juu kiasi, nyekundu cha juu na nyeusi cha juu zaidi (genius)".
Vijana wengie wakaanza zoezi hilo, wengie wakaangukia kwenye rangi ya buluu. Wachache wakaangukia kwenye manjano, wachache zaidi wakaangukia kwenye kijani. Asilimia moja ya wote wakaangukia kwenye zambarau na wawili tu wakaangukia kwenye nyekundu. Hakukuwa na rangi nyeusi.