Riwaya: I died to save my President

Mkuu Kulubule shusha vi2 tuone usaliti wa Patricia....Ila mtunzi Patrick CK katenda haki maana mwanamke akiwa kwenye stress haichukui sekunde kukusaliti...Ndivyo walivyo hakuna namna.
 
Mkuu Kulubule shusha vi2 tuone usaliti wa Patricia....Ila mtunzi Patrick CK katenda haki maana mwanamke akiwa kwenye stress haichukui sekunde kukusaliti...Ndivyo walivyo hakuna namna.
Mkuu Wala husiumize kichwa kuhusu usaliti wa Patricia. Toka zamani mwanamke anahesabiwa Kama kiumbe dhaifu duniani. Cc. Madame B, Miss chagga, miss natafuta n.k
 
Bila Shaka Elvis watakutana na Patricia kwa hotel
 
Safi sana...

Nimesikitika sana... Patricia mke wa Elvis analiwa uroda kizembe hivyo na Dr. Steven kisingizio stress za mama mkwe...

Elvis anajaribu kwa kila hali kukwepa vishawishi vya Doreen rafiki yake Patricia yote sababu ya kumpenda mke wake... ila mke ameenda kuliwa uroda...

Haya sasa Elvis ameelekea hoteli ambayo nae Patricia yumo humo humo akigawa utamu...

Ngoja tuone...


Cc: mahondaw
 
I DIED TO SAVE MY PRESDENT

Sehemu 29

na kumfahamu vyema lakini
kwanza ngoja nitafute taarifa za
kuhusiana na mtandao wa akina
Frank” Akawaza Elvis.Akaegesha
gari na kushuka akaelekea moja
kwa moja mapokezi ambako
alijitambulisha kama Robin na
ana miadi ya kuonana na
Vicky.Mmoja wa wasichana
aliyekuwa mapokezi akainua simu
na kupiga sehemu Fulani na
baada ya dakika mbili akaja
mwanadada mmoja aliyependeza
kwa mavazi aliyovaa akamchukua
Elvis na kumpeleka katika
chumba kimoja kikubwa
“Madam amesema umsubiri
hapa anakuja sasa hivi” akasema
Yule muhudumu na kutoka
“Haiwezekani kabisa mtu
anayefanya biashara ya ukahaba akamiliki hoteli kama
hii.Uchunguzi wa kina unahitajika
hapa.Lazima kuna mambo mazito
yanayoendelea kuhusu huyo
kahaba yanayotakiwa
kuchunguz………………”
akaondolewa mawazoni baada ya
mlango kufunguliwa na
mwanamke mmoja mrefu
mwembamba mwenye weupe wa
kung’aa kuingia.Alivaa suti fupi
nyeusi kiasi kwamba sehemu
kubwa ya mapaja yake ilikuwa
wazi.Alikuwa na nywele ndefu
alizozibana kwa nyuma.Uzuri
wake ulimstua kidogo
Elvis.Hakutegemea kabisa kama
Vicky angekuwa mzuri vile.
“Hallo Robin.Karibu sana”
akasema Vicky kwa sauti laini
sana huku uso wake ukipambwa na tabasamu pana.Kati kati ya
meno yake meupe kulikuwa na
mwanya uliozidi kumpendezesha
kimwana huyu hasa
anapotabasamu.
“Hivi ni kweli huyu ndiye
kahaba Victoria? Akawaza Elvis
wakati akimpa mkono Vicky
ambaye vidole vyake vyote
vilichafuka kwa pete za dhahabu.
“hallo Vicky” akasema Elvis
“karibu sana”akasema Vicky
na kuketi katika sofa akitazamana
na Elvis
“Ahsante sana” akajibu Elvis
“You are so handsome.Sina
hakika kama tumewahi
kuonana.Ulipataje namba zangu?
Namba ile huwa naitoa kwa watu
wachache sana na wa muhimu tu”
akasema Vicky Usijali Vicky nimeipata wapi
namna yako lakini fahamu tu
wewe ni mtu maarufu sana hapa
mjini na kwa kuwa nilikuwa na
shida na wewe nilihangaikahadi
nikaipata namba yako” akasema
Elvis na Vicky akatabasamu
“Nikusaidie nini Robin?
Akauliza Vicky
“Kama nilivyokueleza jana
usiku simuni kwamba shida
yangu mimi ni tofauti kidogo na
huduma unayotoa lakini
nitakulipa vizuri sana na wewe
utafurahi” akasema Elvis
“Nieleze ni shida gani hiyo ili
nione namna ninavyoweza
kukusaidia.Kitu kingine uko tayari
kwa gharama zangu?
“Usihofu kuhusu
gharama.Ninafahamu unatoza kiwango cha juu cha pesa kwa
watu unaowahudumia kwa hiyo
nimekwisha jiandaa kwa hilo”
akasema Elvis.
“Gharama zangu ni kubwa na
ndiyo manaa huwa ninahudumia
watu maalum tu.Nitakapoisikia
shida yako nitajua nikutoze kiasi
gani” akasema Vicky huku uso
wake ukiendelea kuwa na
tabasamu lisilokauka.Elvis
akasema
“Shida yangu mimi si
kubwa.Kuna taarifa naihitaji toka
kwako”
“taarifa gani Robin?
“Unamfahamu mtu mmoja
anaitwa Norman?
“Norman?!! Vicky akastuka
sana na lile tabasamu lake
likatoweka “Ndiyo.Alikuwa kanali wa
jeshi”
Vicky bado alionyesha mstuko
mkubwa.Akafikiri kidogo halafu
akasema
“Sina kumbu kumbu ya
kumfahamu mtu yeyote anayeitwa
Norman.Mimi huwa nahudumia
watu wengi na wengi wao ni watu
wenye nyadhifa na wafanya
biashara wenye pesa.Sina kumbu
kumbu za wateja wangu kwani
huwa ninapata wateja wapya
karibu kila siku.Nani kakueleza
kwamba ninamfahamu mtu huyo?
Akauliza Vicky
Elvis akamtazama kwa makini
na kuuliza
“kanali Norman amekwisha
fariki dunia na siku aliyofariki dunia ulionekana naye.Unaweza
kukumbuka chochote?
Sura ya Vicky ikaonyesha
kukashirishwa kwa swali lile
“Robin mambo gani hayo
unayaongea.Tafadhali naomba
usinipotezee wakati wangu kwa
upuuzi huo unaonieleza.Nina
mambo mengi sana ya kufanya na
sina muda mchafu.Kama hauna
jambo la maana la kunieleza
tafadhali inuka uende zako”
akasema Vicky kwa ukali
“Tafadhali usikasirike
Vicky.Sina lengo baya kwa
maswali yangu.Ninahitaji tu
kumfahamu mtu huyo” akasema
Elvis
“Unataka kumfahamu ili
iweje? Wewe ni polisi? Umetumwa
kunipeleleza? Akafoka Vicky Hapana Vicky mimi si polisi
wala sina nia yoyote
mbaya.Naomba tu unieleze kama
unamfahamu mtu huyo na
nikulipe pesa zako tumalize
biashara yetu.Niambie nikulipe
shlingi ngapi kwa ajili ya taarifa
hiyo? Akauliza Elvis.
“Robin nadhani mimi na wewe
hatuna cha kuzungumza
tena.Nakuomba utoke uende
zako.Mambo unayoyaongea mimi
siyaelewi kabisa.Taarifa za namna
hiyo ulipaswa kuwauliza polisi na
si mimi.Tafadhali naomba
uondoke.Sina muda wa kupoteza
na wewe!! Akasema kwa ukali
huku akimuelekezea Elvis mlango
“Unamfahamu Deusdedith?
Elvis akauliza Swali lile likazidi
kumpandisha hasira Vicky
akamtazama Elvis kwa jicho la
chuki kana kwamba anataka
kumvamia na kumrarua
“Naomba uondoke haraka
sana kabla sijaita walinzi wangu
wakutoe kwa nguvu humu ndani.!!
Akasema Vicky na Elvis akainuka
“sawa ninaondoka Vicky
.Naomba ufikirie nilichokuomba
.Nitakupigia simu kujua umefanya
maamuzi gani.Kumbuka
nitakulipa fedha nyingi kwa taarifa
hiyo.More than ten million”
akasema Elvis na kutoka nje
akimuacha Vicky akiwa amefura
kwa hasira
“Huyu mtu ni nani?
Amezipataje taarifa hizi? Tayari
nilikwisha sahau kuhusu Norman lakini yeye amenikumbusha kila
kitu.Amejuaje kama nilionekana
na Norman siku ile?Inaonekana
suala lile tayari
limevuja.Inaonekana kuna watu
wanaanza kulichunguza suala hili
na huyu Robin ni mpelelezi.Ngoja
nimpigie simu Frank
nimtaarifu.Niliwaonya toka
mwanzo wahakikishe siingii katika
matatizo na wakaahidi kufanya
hiyo lakini mamabo yamebadilika
tofauti na tulivyokubaliana.They
must do something.Sitaki kuingia
katika matatizo kwa sasa”
akawaza Vicky huku macho yake
yakionyesha woga wa
wazi.Akainua simu na kwa haraka
akampigia Frank
“hallow Frank” akasema Vicky
baada ya Frank kupokea simu hallow Vicky.habari za siku?
Akauliza Frank
“Mi mzima sijui wewe”
“Niko salama.Nimeshangaa
leo umenipigia simu asubuhi
asubuhi namna hii.Kwema huko?
Akauliza Frank
‘Frank kuna tatizo limetokea
asubuhi hii”
“Tatizo gani Vicky?
“Ni kuhusiana na lile suala la
Norman”
“Norman ?!! Frank
akashangaa
“Ndiyo.Kuna mtu alinipigia
simu jana usiku anaitwa Robin
akaniomba tuonane leo .Nilidhani
ni mteja mpya na alipofika alianza
kuniuliza Kama ninamfahamu
Norman.Nilistuka sana kwani
suala lile tayari nilikwisha lisahau.Nilimkatalia kwamba
simfahamu Norman,akaendelea
kusisitiza kwamba nilionekana
nikiwa na Norman siku ile
alipofariki.Nilichanganyikiwa
nikapandwa na hasira ikanilazimu
kumtimua.Wakati akiondoka
akaniuliza tena kama
ninamfahamu Deusdedith
nikachanganyikiwa zaidi.Frank
mliponika kazi mlinihakikishia
kwamba katu suala hili haliwezi
kujulikana lakini tayari kuna watu
wamekwisha hisi kwamba
ninahusika na kifo kile cha kanali
Norman.Nimechanganyikiwa na
sijui nifanye nini.Mtu Yule
anaonekana ni mpelelezi na
anafahamu mambo mengi
kuhusiana na kifo cha Norman
.Tafadhali Frank naomba ufanye kila linalowezekana kuhakikisha
siingii matatizoni” akasema Vicky
akiwa katika hali ya wasi wasi
mwingi.Suala lile likaonekana
kumstua sana Frank,akavuta
pumzi ndefu na kusema
“Kijana mwenyewe yukoje?
Umewahi kumuona?
“Ni mara yangu ya kwanza
kumuona .Namna alivyo kwa
kweli ninashindwa
kumuelezea.Please do something
Frank.I don’t want trouble
.Ulinihakikishia kwamba
hakutakuwa na tatizo loloye sasa
matatizo yameanza.Please help
me!!! Akasema Vicky
Kimya cha sekudne kadhaa
kikapita kisha Frank akasema “Ok usiogope Vicky.Ninakuja
hapo sasa hivi naomba unisubiri”
akasema Frank na kukata simu
*****************
Dr Steven ndiye aliyekuwa wa
kwanza kustuka toka
usingizini.Akatazama saa
iliyoonyesha ni saa mbili kasoro
dakika kumi za asubuhi.Pembeni
yake alilala Patricia ambaye
alionekana bado kuwa katika
usingizi mzito.Dr Steven
akamtazama kwa makini na
kutabasamu
“Patricia ni mwanamke
mrembo sana.Hata akiwa
usingizini bado uzuri wake wa asili
unaonekana.Analala kama
malaika.Anatabasamu hata akiwa usingizini” akawaza Dr Stenven
huku akizichezea nywele za
Patricia.
“Kwa nini mwanamke kama
huyu anateseka kiasi hiki?Patricia
ana kila sifa nzuri kiasi kwamba
namuonea wivu mwanaume
aliyemuoa.Inaoenakana
mwanaume huyo bado hajaiona
thamani ya Patricia na ndiyo
maana anadiriki hata kumuacha
peke yake kwa wakati huu ambao
anamuhitaji sana awe karibu
yake.Kama angekuwa ni mke
wangu kamwe nisingekubali
kumuacha peke yake hasa kwa
wakati huu” akawaza Dr Steven
huku akitabasamu
Wakati Dr Steven akiendelea
kumtazama,Patricia akaamka akafikicha macho na kutazama
pembeni.
Alikuwa mtupu na pembeni
yake alikuwepo Dr Steven naye
akiwa mtupu.Patricia akahisi aibu
kubwa
“What have I done?!! akawaza
“Unajisiaje Patricia? Akauliza
Dr Steven.Patricia hakujibu kitu
akazama mawazoni na macho
yake yakaonekana kujaa machozi
“Nyamaza kulia
Patricia.Usiianze siku yako kwa
machozi” akasema Dr Steven
“Steven ,moyo wangu unauma
sana kwa kitendo
nilichokifanya.Sikuwahi kufikiria
kabisa kwamba siku moja
nitaisaliti ndoa yangu.Nimemkosea
sana mume wangu kwa kitendo
hiki” akasema Patricia Usiumie moyo Patricia na
wala usijilaumu.Anayepaswa
kulaumiwa ni mumeo ambaye
naweza kusema kwa kiasi
kikubwa ndiye aliyesababisha
ukawa katika hali hii.Amekuacha
katika wakati ambao unamuhitaji
sana.Yeye ndiye aliyetakiwa kuwa
karibu yako katika wakati huu
mgumu.Alitakiwa asimame nawe
akufariji na akupe moyo wa
kupambana na majaribu yote
unayokumbana nayo katika
maisha yako hivi sasa.Hukuwa na
namna nyingine ya kufanya zaidi
ya kutafuta liwazo la
moyo.Ingekuaje endapo ungekuwa
peke yako kwa usiku wa jana?
Lolote baya lingeweza kutokea
kutokana na hali uliyokuwa nayo”
akasema Dr Steven Nakubali jana nilikuwa na
hali mbaya sana na nisingeweza
kuwa mwenyewe lakinikwa hili
nililolifanya nilivuka mipaka.Moyo
wangu unaumia sana kwa kitendo
hiki nilichokifanya na nitateseka
hadi siku naingia kaburini”
akasema Patricia
“Patricia jambo hili
limekwisha tokea na
kinachotakiwa hapa ni
kuyaruhusu maisha
yaendelee.Amka na ujiandae
nikupeleka nyumbani ukajiandae
kwa ajili ya kuelekea kazini”
“Hapana Dr Steven.Leo
sintaingia kazini.Siwezi kufanya
kazi nikiwa katika hali ya mawazo
namna hi.Nahitaji kupumzisha
akili yangu.Halafu kuna jambo
nataka nikuombe Omba chochote Patricia”
“Naomba mtu yeyote
asifahamu chochote kuhusiana na
hiki tulichokifanya.Hii ibaki siri
yetu peke yetu na jambo kama hili
lisijirudie tena”
“Usihofu Patricia.Hakuna mtu
atakayefahamu na wala
halitajirudia tena lakini muda
wowote ukihitaji mtu wa
kukuliwaza au kumweleza kile
kinachokusibu mimi nipo nieleze
na nitakusaidia” akasema Dr
Steven.Patricia akainuka akaenda
bafuni kuoga
*****************
“Sasa nina uhakika mkubwa
kwamba Vicky ana mahusiano na
mtandao wa akina Frank na ni wazi anamfahamu mtu huyo
anayeitwa Deusdedith kwani ndiye
aliyemtumia katika kumuua
Kanali Norman.Nimepata sehemu
nzuri ya kuanzia.Huyu Vicky
atanisaidia kumfahamu Deus.Kwa
sasa ngoja niende kwa
mkurugenzi ana hamu ya kutaka
kujua kile ninachokichunguza”
akawaza Elvis huku akielekea
eneo la maegesho baada ya kutoka
kuonana na Vicky.Wakati
akiligeuza gari lake kwa ajili ya
kuondoka eneo lile mara
akastushwa na kitu alichokiona
akabaki ameduwaa kwa sekunde
kadhaa.Katika mlango wa
kuingilia pale hotelini watu wawili
mwanaume na mwanamke
walikuwa wanatoka “Am I dreaming? Thats
Patricia my wife !! akasema Elvis
kwa sauti ndogo
“Hii si ndoto na wala
sijafananisha .Kweli yule ni
Patricia.Amefuata nni hapa
hotelini? halafu mbona hayuko
kikazi,mavazi yale aliyoyavaa
hupenda kuvaa tunapotoka usiku
au kwenda katika sherehe
.Alipaswa kuwa kazini muda
huu,hapa amefuata nini?
Akajiuliza Elvis.Akabaki
ameduwaa
Patricia na Dr Steven
walielekea mahala walikoegesha
gari,wakaingia katika gari la
Patricia wakaondoka.Dr Steben
ndiye aliyekuwa akiendesha gari
lile Yule ni Patricia mke wangu
nimemshuhudia kwa macho
yangu akitoka hotelini akiwa na
mwanaume.Ametoka kufanya nini
hapa?halafu toka jana simu yake
haipatikani.Whats going on? Si
kawaida yake kabisa kuzima
simu”Akawaza Elvis huku gari la
Patricia likivuka geti na kuingia
barabara kuu.Bado Elvis alikuwa
katika mshangao.Alilitazama gari
la Patricia likitokomea akachukua
simu na kuzitafuta namba za
Patricia akampigia lakini bado
simu haikuwa
ikipatikana.Akaamua kumpigia
simu mtumishi wao wa ndani
Stella
“kaka shikamoo” akasema
Stella Marahaba Stella,habari za
hapo nyumbani?
“habari nzuri.Pole na kazi”
“Ahsante sana Stella.Dada
yako yupo hapo nyumbani?
‘Hapana hayupo”
“Amekwenda kazini?
Stella akababaika kidogo na
kushindwa ajibu nini kwani
hakujua Patricia alikwenda wapi
“Mbona hunijbu
Stella?Nimekuuliza dada yako
amekwenda kazini?
“Hapana sifahamu kaka”
“Hufahamu?Hukuwepo
wakati anaondoka? Akauliza Elvis
kwa ukali kidogo na kumfanya
Stella aogope
“Kaka naomba niseme
ukweli.Dada Patricia aliondoka
jana jioni lakini hakuniaga anakwenda wapi na mpaka sasa
bado hajarejea” akasema Stella
“Ulivyomuona wakati
anaondoka alikuwa anaenda
kazini?
“Hapana kaka,sina hakika
kama alikuwa anakwena kazini
kwani alivaa gauni la kutokea
usiku”
Elvis akavuta pumzi ndefu na
kuegemea kiti halafu akasema
“Ahsnte Stella.Naomba
usimweleze kama nimekupigia
simu” akasema Elvis na kukata
simu.Akazama katika mawazo
mengi halafu akampigia simu
Doreen
“hallow Elvis” akasema
Doreen baada ya kupokea simu
“ Doreen ,tayari umeondoka
hapo nyumbani? Ndiyo Elvis.Nimekwisha
ondoka nimemuacha Graca
anapumzika.Ninataka nielekee
kazini nikaombe likizo ya dharura
ya mwezi mmoja.Vipi kuna mahala
unataka unitume?
“Nakukumbusha tafadhali
usisahau kwenda kumuona
Patricia”
“Hapana Elvis siwezi
kusahau.Nikimaliza mizunguko
yangu nitakwenda kuonana naye”
akasema Doreen
“Ahsante Doreen” akasema
Elvis na kukata simu akaizima
kabisa
“Siku yangu imeanza
vibaya.Ngoja kwanza nikaonane na
mkurugenzi halafu nitajua nini
cha kufanya.I’m so confused right
now.Patricia hakulala nyumbani jana na leo hii ninamshuhudia
akitoka hotelini akiwa
ameongozana na mwanaume.Je
alilala pale hotelini? Yule
mwanaume aliyekuwa naye ni
nani? Akajiuliza maswali na
kukosa majibu akaondoka
******************
Baada ya kutoka hotelini kwa
Vicky,Elvis akaelekea moja kwa
moja ofisini kwa mkurugenzi wake
Mr Meshack Jumbo.Mara tu
baada ya kushuka garini
hakutaka maongezi na mtu
akaelekea moja kwa moja ofisini
kwa mkuu wake
“Karibu Elvis” akasema Mr
Meshack “Ahsane sana mzee” akajibu
Elvis na kuketi.Mkurugenzi
akafunika faili alilokuwa analipitia
na kumtazama Elvis
“Nadhani umekuja
kunifahamisha kile ambacho
umekuwa unakichunguza”
akasema mkurugenzi,Elvis
akamueleza kila kitu hadi
alipofikia.Kimya kikatawala mle
ofisini alipomaliza kutoa
maelekezo yake kwa mkurugenzi.
“Kuna nyakati niliwahi pata
fununu toka kwa mtu mmoja
aliyeko ndani ya serikali ya Congo
kwamba waasi wanaopambana na
serikali yao wana silaha kali
ambazo zinapitia Tanzania.Taarifa
hiyo ilidai kwamba kuna mtandao
wa watu wanaofanya biashara
hiyo walioko Tanzania na ndani ya serikali ya Congo DRC.Sikuzipa
uzito mkubwa sana taarifa hizo
kwa kuwa sikuwa nakiamini sana
chanzo hicho cha taarifa lakini
kwa hili ulilonieleza leo ninaamini
kwamba jambo hili kweli lipo.Hii
ni aibu kwetu,aibu kwa nchi yetu
ambayo jeshi lake limekuwa
mstari wa mbele katika
kuhakikisha amani inapatikana
Congo lakni kuna watu ndani ya
serikali wanawauzia silaha
waasi.Hili ni suala zito Elvis”
akaseam Meshack na kukuna
kichwa .Taarifa ile ilimstua sana
“Elvis suala hili ni suala zito
na lazima tumtaarifu rais haraka
ili kwa pamoja tujue nini cha
kufanya na tuudhibiti mtandao
huu haraka iwezekanavyo”
akasema Meshack Jumbo huku akiinua mkono wa simu na kutaka
kubonyeza namba,Elvis akamzuia
“Mzee usimtaarifu kwanza
rais.Hatuwezi kufanya hivyo kwa
sasa.Tunachtakiwa kufanya ni
kuanza kwa uchunguzi ili
tuufahamu kwa kina mtandao huo
ndipo tumtaarifu rais.Kuna
uwezekano mtandao huu
ukawahusisha watu wazito
serikalini kwa hiyo tukimtaarifu
rais mapema kabla
hatujawafahamu inaweza
ikavuruga uchunguzi wetu”
akasema Elvis.Meshack Jumbo
akamtazama Elvis na kusema
“Elvis hili ni jambo zito la
kitaifa na hatuwezi kuendelea nalo
bila kiongozi wa nchi na amiri
jeshi mkuu kulifahamu” akasema
Meshcak Nakubaliana nawe mzee
kwamba jambo hili ni zito sana na
kuna ulazima wa kumtaarifu rais
lakini kwa sasa sidhani kama ni
muda muafaka kwa yeye
kulifahamu.Nipe muda zaidi
niendelee kufanya uchunguzi
wangu na baada ya kupata taarifa
zenye uhakika zaidi tutamtaarifu
rais” akasema Elvis
Meshack Jumbo akafikiri kwa
muda halafu akasema
“Sawa ninakubaliana na wazo
lako lakini hata hivyo inabidi
tuunde timu Ambayo utaiongoza
kwa ajili ya kulichunguza jambo
hili kwa haraka.”
“Hapana mzee.Hakuna haja
ya kuunda timu.Niache niendelee
na uchunguzi wangu na pindi
nikiona kuna ulazima wa kuomba nguvu zaidi nitakueleza lakini kwa
sasa nataka niendelee na
uchunguzi mimi mwenyewe”
akasema Elvis.
“Are you ssure?
“Ndiyo mkurugenzi.Nina
hakika ninaweza kulishughulikia
suala hili mwenyewe.Uwezo wangu
unaufahamu vyema na endapo
nitahitaji msaada nitakueleza”
akasema Elvis
Meshack Jumbo akamtazama
Elvis kwa makini na kusema
“I trust you Elvis .Sina shaka
kabisa kwamba unaweza
ukalichunguza suala hili lakini
bado nina mashaka makubwa kwa
mtu mmoja kuweza kupambana
na mtandao mkubwa kama huu
ambao wahusika wake bado hawajulikani” akasema Meshack
Jumbo kwa wasi wasi
“Usiwe na wasi wasi mzee
ninaiweza kazi hii” akasema Elvis
Baada ya tafakari ya dakika
mbili Meshack Jumbo akasema
“Sawa Elvis.kwa kuwa
ninakuamini nitafanya unavyotaka
lakini inabidi tufanye kazi hii bega
kwa bega sisi wawili.Siwezi
kukuachia kazi hii peke
yako,lazima na mimi nishiriki”
“Ahsante mkurugenzi kwa
kukubali ombi langu.Hata hivyo
kuna mambo mawili nataka
nikuombe msaada wako.kwanza ni
kuchunguza akaunti za benki za
Frank ili tujue mwenendo wake wa
kifedha .Tufahamu anapokea
fedha toka wapi na anatuma
kwenda wapi.Hii inaweza kuwa njia moja ya kuufuatilia mtandao
huu.Pili ni kufuatilia mawasiliano
ya Frank na kujua anawasiliana
na akina nani na wanaongea
kuhusu nini.Yule mwanamke
Victoria ambaye alitumika
kumuua kanali Norman naye
anatakiwa achunguzwe
anakoishi.Kuna kitu
anakifahamu.Nataka kufahamu
mahala anapoishi ili nimfuate
nyumbani kwake.Naomba tuma
kijana mmoja amfuatilie na
afahamu mahala anapoishi na
nipate majibu kabla ya jioni leo”
Akasema
“Sawa Elvis.Huyu mwanamke
anaweza akasaidia sana.Endapo
tutampata huyo Deusdedith
tunaweza kupata taarifa za
muhimu za kutusaidia kuubaini mtandao huu kwani inaonekana
ni mtu mwenye sauti ndani ya
mtandao”
“Kweli kabisa mzee.Halafu
kuna jambo lingine ambalo
nahitaji msaada wako”
“Jambo gani Elvis?
“Ni kuhusiana na usalama wa
Graca.Kama nlivyokueleza
kwamba baba yake Frank
anamtafuta kwa udi na uvumba
na kwa sasa tayari amekwisha
fahamu kwamba nimemtorosha na
tayari wanajua nini nitakipata
toka kwake kwa hiyo watamtafuta
kwa kila uwezo walio nao na
wakifanikiwa naamini
watamuua.Kutokana na uzito wa
suala hili sina hakika kama
nitaweza kumlinda Graca muda
wote kwa hiyo nataka umsaidie huyu binti ambaye amepitia
maisha magumu sana na ya
mateso mengi” akasema Elvis
“Nakubaliana nawe
Elvis.Niachie suala hilo
nitalishughulikia.Ametupa taarifa
za muhimu sana na lazima
tumlinde” akasema meshack.
“Ahsante sana
Mkurugenzi.Huo utakuwa ni
msaada mkubwa sana kwa binti
huyu” akasema Elvis
Walijadiliana mambo kadhaa
kwa saa zaidi ya moja na kisha
Elvis akarejea katika makazi
yakeya muda.Bado kichwa chake
kiliendelea kuwa na mawazo
mengi sana kuhusiana na mkewe
Patricia
“Is she cheating on me?
Akajiuliza swali hili marakwa mara Nimemfahamu Patricia kwa
miaka mingi na sina kumbu
kumbu kama amewahi
kunidanganya au kunificha na
ndiyo maana nimepata shida sana
kufahamu pale hotelini alikuwa
anatafuta nini.I do trust her very
much lakini jana haja rejea
nyumbani alikuwa wapi? Kwa nini
simu yake kaizima?akaendelea
kujiuliza
“Suala hili limetokea kwa
wakati huu ambao
ninashughulkia suala lingine
zito.Patricia ni zaidi ya maisha
yangu.Ninampenda kwa namna
ambayo siwezi kuielezea.Patricia ni
maisha yangu.Kwa mara ya
kwanza ninaanza kuyaonja
machungu ya kazi hii.Siku zote
nimekuwa mvumilivu sana lakini naona uvumilivu huu unaelekea
kunishinda.Nimekuwa nikitumia
muda mwingi kwa kazi kuliko ule
ninaotumia nikiwa na mke
wangu.Endapo nitagundua
kwamba Patricia anatoka nje ya
ndoa sifahamu nitafanya nini ”
akawaza Elvis
*********************
Mara tu alipomaliza
kuzungumza na Vicky
simuni,Frank akampigia simu
Pascal na kumpatia taarifa zile
zilizomstua sana
“Nilijua tu,mambo haya
lazima yatatokea kama Elvis
amempata Graca.Tayari
amefahamu kila kitu na sasa
anaanza kutusaka.Frank kazi imeanza” akasema Pascal na
kimya kifupi kikapita
“Uko wapi Pascal?
“Niko hapa Ramona
restaurant napata supu”
“Nisubiri hapo ninakuja sasa
hivi.Nataka tukaonane na Victoria”
akasema Frank na kwa haraka
akaelekea katika gari akaondoka
kumfuata Pascal.
Nusu saa baadae tayari
alikwisha mpitia Pascal na
walikuwa njiani kuelekea hotelini
kwa Vicky
“Kwa nini huyu Elvis atokee
wakati huu wa neema kubwa
kwetu na kutaka kuvuruga
mipango yetu yote? Anaonekana
ni kijana mwenye kihere here sana
cha kuchunguza maisha ya watu”
akasema kwa hasira Frank “Frank lazima tukubali tuna
kazi ya ziada ya kufanya ili
kumzuia Elvis asiendelee
kutuchimba.Kwa hatua aliyofikia
ni wazi tayari atakuwa na taarifa
zetu na anachokifanya hivi sasa ni
kutuchimba.Tayari Graca atakuwa
amemuelekeza kila kitu kuhusiana
na biashara
tunayoifanya.Ninamfahamu vyema
Elvis.Huyu ni nyoka mwenye
sumu kali sana na ambaye
anatakiwa kupondwa kichwa
haraka sana.He’s very dangerous”
akasema Pascal na Frank
akaupiga usukani kwa hasira.
Najilaumu sana kwa uzembe
wangu wa kutunza kumbu kumbu
hadi Yule mwanamke akazipata na
kumpa mwanae Graca.Najlaumu
sana kwa nini nilimuoa mwaname mjinga kama Yule ambaye naye
kanizalia mtoto mjinga mwenye
akili kama zake.Wao ndio chanzo
cha haya yote.Nilifanya kosa
lingine kubwa kumuacha Graca
hai hadi leo.Aombe sana nisimtie
mikononi mwangi kwani sintampa
tena nafasi hata ya kutamka neno
lolote.Nitampata tu hawezi
kujificha kamwe” akasema Frank
kwa hasira
“Vipi kuhusu Vicky? Tayari
Elvis amekwisha gundua kwamba
ana mahusiano na sisi kwa hiyo
tayari amekuwa ni hatari
kwetu.Tutamfanyaje? akauliza
Pascal
“Wewe unafikiria tumfanye
nini? Frank naye akauliza
“Kwa sasa Vicky ndiye njia
pekee ya Elvis kuweza kupata taarifa zetu.Vicky atakuwa katika
hatari kubwa.Yawezekana akawa
anamfuatilia kwa siri bila yeye
kujua.Frank hatupaswi kumpa
Elvis nafasi ya kumpata Vicky”
akasema Pascal
“Unataka tufanye nini Pascal?
Unataka tumuue Vicky? Frank
akauliza
“Hivyo ndivyo tufanyavyo kwa
wale wote ambao wanaonekana
hatari kwetu” akasema Pascal
“No ! we cant do that.We cant
kill her.Yeye ndiye atakaye
tusaidia kummaliza huyu mdudu
anayetufuata kwa nyuma kama
fisi,Elvis !!
“What are your plans Frank?
Pascal akauliza
“Just wait and see” akasema
Frank Walifika katika hoteli ya Vicky
wakaelekea moja kwa moja ilipo
ofisi yake .Vicky alikuwa
amesimama dirishani huku
mkononi akiwa na glasi ya
pombe.Alionekana wazi kwamba
alikuwa katika mawazo mengi.
“Hallo Vicky” akasema Frank
“You have to tell me right now
what is going on? You promised
me that there will be no
trouble.who was that man?
Akauliza kwa ukali Vicky bila hata
salamu
“Please calm down Vicky”
akasema Frank akijaribu
kumtuliza Vicky aliyeonekana
kuwa na hasira nyingi.Frank na
Pascal wakaketi vitini halafu
Frank akasema Hebu tueleze Vicky,tukio
zima namna lilivyokuwa”
“Jana usiku” akaanza kueleza
Vicky
“Nilipigiwa simu na mtu
nisiyemfahamu akajitambulisha
kwangu anaitwa Robin.Alisema
kwamba ana shida na
mimi.Nilipanga kuonana naye leo
na asubuhi ya leo akafika kama
nilivyomtaka afanye.Shida yake
kubwa ambayo alikuwa tayari
kunipa fedha nyingi ni kutaka
kujua kama ninamfahamu mtu
aitwaye Norman.Niliposikia jina
hilo niliogopa na kustuka
mno.Nilikana kumfahamu mtu
huyo halafu akaniambia kwamba
kama simfahamu mbona
nilionekana naye siku ile kabla
hajafariki? Niliogopa zaidi aliponikumbusha kuhusu jambo
hilo ambalo tayari lilikwisha
nitoka akilini.Naamini Yule jamaa
atakuwa mpelelezi.Nilikasirikka na
kumtaka atoke haraka ofisini
kwangu na wakati akitoka
akaniuliza kama ninamfahamu
Deusdedith.Nilizidi kuogopa
nusura nitokwe na haja
ndogo.Baada ya kumtishia
kumuitia walinzi akaondoa
zake.Jambo hili limenichanganya
sana kwa sababu Yule jamaa
anaonekana kunifahamu sana na
kulifahamu suala zima la mauaji
ya Norman.Tafadhali naombeni
mnisaidie sitaki kuingia katika
matatizo” akasema Vicky
“Pole sana Vicky kwa mstuko
ulioupata .Tunakuahidi mambo
yote yatakaa sawa” How can I trust you again
Frank?Mara ya kwanza uliniambia
hivyo hivyo lakini leo hii tayari
nimejulikana” akasema Vicky.
Frank akamtazama Vicky
usoni halafu akasema
“Tayari tumekwisha mfahamu
mtu huyo.Jina lake si Robin kama
alivyokwambia bali anaitwa Elvis
na ni mfanyakazi wa idara ya
ujasusi’
“I’m finished !! akanong’ona
Vicky
“Vicky nadhani niliwahi
kukutaarifu kwamba ninaye mtoto
mwenye matatizo ya akili
anatibiwa afrika kusini.Hivi majuzi huyu Elvis amemfuata mwanangu
Afrika kusini na kumtorosha
amempeleka mahala
kusikojulikana.Kupitia mwanangu
huyo ameweza kuyafahamu
mambo yangu mengi ambayo
niliyahifadhi katika kompyuta
ambayo huyo mwannagu
aliiba.Pamoja na hayo nakuomba
usiogope Vicky kwani
nitahakikisha mwanaharamu
huyu hafiki kokote.Safari hii
amejiingiza yeye mwenyewe katika
tanuru la moto na hatatoka
salama.Kitu ambacho nataka
kifanyike sasa hivi ni kukupeleka
mafichoni shambani kwangu
wakati tukiendelea
kulishughulikia suala hili.Ndani
ya kipindi kifupi sana lazima Elvis awe ametoweka katika ardhi ya
Tanzania”
“Frank niko tayari kwenda
mafichoni lakini tafadhali naomba
safari hii maneno yako yawe ya
kweli na uhakikishe kwamba
suala hili linakwisha.Timiza ahadi
yako na unitoe katika matatizo”
akasema Vicky
“Vicky naomba usiwe na hata
chembe ya woga kuhusu suala
hili.Wewe mwenyewe utashuhudia
Elvis akiuawa na amani itatamalki
tena” akasema Frank
‘Nitashukuru kuona hilo
likitekekelzwa.Yule jamaa
ameninyima amani kabisa.Lini
utanipeleka mafichoni?
“Right now !! akasema Frank
na Vicky akastuka
‘Right now?
 
Tokea Jana nasikitika Kama mimi ndio Elvis[emoji22]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…