I DIED TO SAVE PRESDENT
Sehemu 31
Mishale ya saa ilionyesha ni
saa tisa za usiku.Bado Patricia
hakuwa amepata usingizi.Pembeni
ya kitanda chake kulikuwa na
chupa ya pombe ambayo
amekuwa akinywa tangu
aliporejea toka ikulu alikoenda
kumtazama mke wa rais.Macho
yake mazuri yenye kurembua
muda wote leo hii yalikuwa
yamemvimba kutokana na kulia
sana.Alikuwa katika wakati
mgumu mno katika maisha yake
Taratibu akainuka na kwenda
sofani akafuta machozi na kuinua
macho juu
“Ee Mungu wangu kwa nini
umeniacha peke yangu nateseka
namna hii? Kam unayaona mateso
ninayopata naomba
usiniache.Simama nami ee bwana ili niweze kuyashinda majaribu
yote yanayokuja mbele zangu”
akaomba halafu akaufunika uso
wake kwa viganja vya mikono
“Elvis uko wapi ? Nakuhitaji
sana katika wakati huu mgumu
ninaoupitia.Neno lako moja tu
linaweza kuniondolea haya
maumivu yote niliyonayo na
nikawa na furaha kuliko
wanawake wote duniani.I love you
Elvis,I love you so much.Please
come back !!
Akatolewa mawazoni baada ya
picha ya Dr Steven kumjia
“I cheated on my
husband.Kwa namna
ninavyompenda mume wangu
Elvis sikutegemea kama siku moja
ningeweza kumsaliti.Nilikuwa
nawaza nini hadi nikavunja kiapo cha uaminifu katika ndoa?Jambo
hili litanitesa hadi siku ninaingia
kaburini” akawaza Patricia
“Upendo wa Elvis kwangu
siwezi kuuelezea.Ananipenda
kupita kitu choche na siku zote
amekuwa akisimama pamoja nami
na amekuwa niwe mwanamke
mwenye furaha zaidi.Anaifahamu
hali yangu na ameikubali.Kwa nini
nimekosea mtu kama
huyu?Sifahamu nini kitatokea
siku akigundua kwamba
nimetembea nje ye ndoa” Patricia
akazidi kulia
“ lakini kwa upande wa pili
haya yote yamesabishwa na yeye
mwenyewe kuwa mbali nami hasa
wakati huu wa matatizo makubwa
niliyo nayo ambayo
yanasababishwa na ndugu zake” Patricia akainuka na kwenda
katika picha kubwa ya Elvis
iliyotundikwa ukutani akaitazama.
“I’m sorry Elvis.I’m real
sorry.Nimekukosea sana na sijui
nitafanya nini ili uweze
kunisamehe kosa hili” akasema
Patricia ambaye alionekana ni
kama mtu aliyechanganyikiwa.
“Sikutegemea kama siku moja
nitapata wakati mgumu katika
maisha yangu kama hivi
sasa.Naona kama dunia
inaniadhibu kwa makosa
niliyoyafanya ya kuitoa ile mimba
wakati ule ninasoma” akalia
Patricia na kwenda kujitupa
kitandani
***************** Saa kumi mbili za Alfajiri
ilimkuta mkurugenzi wa idara ya
ujasusi Meshack Jumbo
nyumbani kwa makamu wa rais
Dr Shafi Abdulkareem
Omar.Aliwahi sana kufika
kutokana na agizo la makamu wa
rais aliyemtaka afike nyumbani
kwake asubuhi na mapema.
Baada ya dakika tano toka
mzee Jumbo alipowasili makamu
wa rais akatokea wakasalimiana
halafu wakaeleka katika chumba
Fulani kwa maongezi
“Mr Jumbo kwanza
nakuomba samahani sana kwa
kukusumbua.Sikupaswa kuonana
nawe asubuhi kama hii lakini
kutokana na unyeti wa suala
nililokuitia imenilazimu kufanya hivyo” akaanzisha mazungumzo
Dr Shafi.
“Usijali mkuu.Hizi ni kazi zetu
na muda wote tuko kazini kwa ajili
ya kuhakikisha kwamba nchi yetu
na watu wake wanakuwa salama”
akasema Meshack Jumbo
“Nafurahi kusikia hivyo Mr
jumbo”Akasema Dr Shafi
“Mr Jumbo mimi na wewe
tuna historia ndefu.Tumekuwa na
ushirikiano mkubwa sana na
kutokana na uongozi wako thabiti
idara yako imekuwa ikifanya kazi
zako kwa mafanikio
makubwa.”akasema
DrShafi.Meshack Jumbo hakujibu
kitu zaidi ya kutabasamu kwa
mbali Mr Jumbo” akasema Dr Shafi
halafu akatulia kidogo kisha
akasema
“Nimekuita hapa kwa jambo
moja muhimu sana.Nadhani
unaelewa fika kwamba pamoja na
idara yako kushughulikia mambo
makubwa ya ulinzi na usalama wa
nchi yetu kuna baadhi ya mambo
ambayo hatutakiwi kuyagusa na
hata kama tukiyafahamu
inatulazimu tuyaache kwani
kuyaingilia kunaweza kuipasua
nchi”Akasema Dr Shafi na
kunyamaza kidogo halafu
akasema
“Kuna kijana wako mmoja
ameingia mahala kusikomuhusu
na endapo hatutachukua hatua za
haraka kumdhibiti nchi yeu
itatikisika” Ni kijana gani huyo na
ameingia mahala gani?
“Anaitwa Elvis” Akajibu Dr
Shafi
“Elvis !! Mzee Jumbo
akastuka sana
“Ndiyo.Anaiwa Elvis.Mbona
umestuka sana Mr Jumbo?
“Dr Shafi,imenilazmu kustuka
kwa sababu unapomzunguzia
Elvis unazungumzia kuhusu
vijana wachache sana wazalendo
ambao wako tayari hata kuimwaga
damu yao kwa ajili ya nchi hii”
“Sina shaka na uadilifu na
uzalendo wake na tunajivunia
kuwa na kijana kama huyu lakini
pamoja na yote hayo mazuri
aliyoyafanya kwa hivi sasa ni mtu
hatari mno kwa taifa letu” Mzee Jumbo akainuka na
kumtazama Dr Shafi kwa
mshangao
“Dr Shafi naomba nikuweke
wazi kwamba Elvis ni kijana
ninayemuamini pengine kuliko
wote katika idara
yangu.Unaposema eti ni hatari
kwa taifa nashindwa kukuelewa”
Dr Shafi akatabasamu kidogo
na kusema
“Usiwe na jazba Mr
Jumbo,naomba ukae tuongee
kuhusiana na masuala haya
mazito”
Mzee Jumbo akakaa halafu
Dr Shafi akaendelea
‘Mr Jumbo nadhani
unafahamu fika kwamba kuna
mambo ya ndani kabisa ya
kiserikali ambayo yanafahamika kwa watu wachache tu na hata
hao wachache hata kwa kuutoa
uhai wao hawawezi wakatoa
siri.Sifahamu kwa namna gani
lakini huyu kijana Elvis ameweza
kufahamu jambo moja kubwa na
zito la siri na lengo lake ni
kulianika jambo hilo kwa
umma.Mara tu jambo hili likifika
kwa umma wa watanzania taifa
litatikisika.Hakuna anayetaka hilo
litokee hasa kwa wakati huu
ambao tumeanza kufanya vizuri
kiuchumi” akasema Dr Shafi
Meshack Jumbo akavua
miwani yake na kuiweka
mezani,akakumbuka mambo yote
aliyoambiwa na Elvis jana
kuhusiana na biashara ya silaha
“Mheshimiwa makamu wa
rais unaweza kuniambia ni jambo gani hilo la hatari aliloligundua
Elvis? Nahitaji kulifahamu”
akasema Mzee Jumbo
“Kwa sasa sintaweza
kukueleza ni jambo gani kwani
bado uchunguzi unaendelea
kuhusiana na amefahamuje jambo
hilo lakini naomba uniamini
kwamba kwa sasa Elvis ni hatari
sana kwa taifa”
“Mheshimiwa makamu wa
rais ninapata kigugumizi
unaponieleza kwamba Elvis ni
hatari na kwamba ana jambo
analifahamu ambalo ni hatari kwa
taifa.wakati mimi kama mkuu
wake wa kazi sifahamu chochote
kuhusiana na suala hilo naomba
unifafanulie tafadhali” akasema
Meshack Mr Jumbo utafahamishwa
kila kitu mara uchunguzi
ukikamilika.Wakati uchunguzi
ukiendelea kuna jambo nataka
lifanyike haraka sana”
Kimya kifupi kikatanda mle
chumbani baada ya muda Dr
Shafi akasema
“I want Elvis dead by today
evening”
“What ?!! mzee Jumbo
akastuka na kusimama
“That’s impossible.We cant do
that!! Akasema
“Mr Jumbo hilo ni agizo
umepewa na lazima ulitekeleze
kama ulivyoagizwa!!
“Mheshimiwa makamu wa
rais nafahamu idara
ninayoiongoza iko chini yako na
wewe unaweza kutoa amri ya kitu chchote kifanyike ndani ya idara
yangu na mimikazi yangu ni
kutekeleza lakini kwa hili
unaloliagiza nataka kupata
sababu itakayoniridhisha kwa nini
Elvis auae?
“Mr Jumbo nimekwisha
kueleza kwamba Elvis ni mtu
hatari kwa maslahi ya taifa na kwa
maana hiyo lazima tumuondoe
haraka sana kabla hajasababisha
madhara makubwa”
Uso wa mr Jumbo uliloa
jasho.Hakuamini kama maneno
yale yanatoka katika kinywa cha
makamu wa rais
“Dr Shafi wewe ni mkuu
wangu na siku zote nimemkuwa
nikitii maagizo yako lakini katika
hili utanisamehe.Siko tayari
kufanya hivyo unavyonitaka nifanye.Elvis ni kijana ambaye
taifa linatakiwa kujivunia kuwa
naye na si kufikiria kumuua”
Dr Shafi akaonekana kuanza
kukasirika,akasema
“Mr Jumbo si mara ya kwanza
tumewakata kauli baadhi ya vijana
wetu ambao wamekuwa na
mwelekeo hasi na hatari kwa
taifa.Umesahau kuhusu Alfred
Chiteka? Vipi kuhusu David
Agomwile?Diana katope je?hawa
walikuwa ni vijana mahiri na
wenye mchango mkubwa kwa taifa
lakini kwa sababu waligusa
mahala wasipotakiwa ilitulazimu
tuwaondoe na hivyo ndivyo
tutakavyofanya kwa Elvis.Lazima
naye tumuondoe hata kama ana
umuhimu mkubwa kwa taifa”
akasema Dr ShafiMeshack Jumbo alionyesha
kuchanganyikiwa .Akasema
“Dr Shafi usinidanganye eti
Elvis anatakiwa kuuawa kwa ajili
ya maslahi ya nchi.Huo ni uongo
wa mchana.Ninakufahamu vyema
umekuwa ukitumia idara yangu
kulinda maslahi ya vigogo na
wakati mwingine kupelekea hata
kupoteza maisha ya vijana
wazalendo wenye uchungu na nchi
yao.Elvis siko tayari
kumuangamiza kwa sababu ya
maslahi ya wakubwa!! akasema
kwa hasira Meshack Jumbo huku
akigonga meza.Kitendo kile
kikamkasirisha sana Dr Shafi
“MrJumbo tafadhali naomba
tusilifanye jambo hili kuwa
gumu.Mimi ni mkubwa wako kiazi
na idara yako iko chini yangu kwa maana hiyo nikisema kitu hakuna
wa kukipinga.Kama hutakuwa
tayari kutekeleza maagizo yangu
basi nitatafuta watu wengine
ambao wako tayari
kuyatekeleza.Nadhani unaelewa
ninamaanisha nini” akasema Dr
Shafi
“Huu ni mtihani mkubwa
kwangu.Elvis amegusa maslahi ya
vigogo na sasa maisha yake yako
hatarini.Hapana siwezi kuwapa
nafasi ya kumuua Elvis.Lazima
nimsaidie.I have to do something”
akawaza Mr Jumbo kisha
akasema
“Dr Shafi wewe ni kiongozi
wangu na siwezi kupingana na
maamuzi yako.Utanisamehe kwa
matamshi yangu ni kutokana na
namna nilivyostuka kwani Elvis ni mmoja wa vijana ninaowaamini
sana.Lakini hata hivyo hainizuii
kumuondoa kwa maslahi mapana
ya taifa.Niko tayari kufanya hivyo
lakini nina ombi moja.Hakikisha
damu ya Elvis haipotei bure bali
iwe ni kweli kwa maslahi mapana
ya nchi vinginevyo damu ya kijana
huyu itaendelea kutulilia hadi
siku ya mwisho” akasema
Meshack Jumbo.Kauli ile
ikaonekana kumfurahisha Dr
Shafi akatabasamu na kusema
“Sasa tunaweza
kuzungumza.” Akacheka kidogo
kisha akaendelea
“Mr Jumbo uongozi ni kitu
kigumu sana na wakati mwingine
tunalazimika kufanya maamuzi
magumu na mojawapo ni hili la
kumuondoa Elvis.Ninakuhakikishia kukupa
taarifa kuhusu uhatari wa Elvis
mara uchunguzi ukikamilika
ndani ya kipindi kifupi toka
sasa.Pili kuna kijana atakuletea
kamzigo Fulani naona
ukapokee.Kuna kijihela cha
kunywea maji kama milioni mia
moja”
Mzee Jumbo akatabasmu na
kusema
“Nimekuelwa vizuri Dr
Shafi.Niambie unataka kazi hii
tuifanye lini?
“Soon as possible.Nataka hadi
saa sita za usiku leo Elvis asiwepo
katika dunia hii.Mpango wote uko
hivi.Utapigiwa simu na mtu
asiyejulikana akikueleza kwamba
mtu anayetafutwa sana na serikali
ya Tanzania akihusishwa na vitendo vya kigaidi Abdullah
Abdullah ameonekana katika
msitu wa Ngezi .Utamtuma Elvis
aende akafanye uchunguzi na
huko atakutana na vijana
walioandaliwa na
watamzimisha.Kila kitu tayari
kimeandaliwa na tukio linatakiwa
litokee saa nne hadi tano leo
asubuhi.Hakuna uchunguzi
utakaofanyika kwani itaonekana
ni kifo kilichotokana na ajali
kazini” akasema Dr Shafi
“Dr Shafi nimekuelewa vizuri
sana lakini naomba ufahamu
kwamba moyo wangu unaumia
mno kwa jambo hili lakini sina
namna nyingine ya
kufanya.Maslahi ya taifa lazima
yalindwe” akasema Jumbo Maongezi yaliendelea saa
moja na dakika ishirini Mesachk
Jumbo akaondoka
“Toka nimekuwa kiongozi
katika idara hii ya ujasusi hili ni
jaribu langu la kwanza kubwa na
zito.Elvis kuuawa?? Tena kwa ajili
ya kulinda maslahi ya vigogo
!!akawaza
“Nilijua lazima jambo hili
aliloligundua Elvis limletee
matatizo makubwa.Biashara ile ya
silaha inafanywa na vigogo
wakubwa na wamekwisha fahamu
kwamba wamegundulika hivyo
wanataka kummaliza Elvis ili siri
zao zisigundulike” Akawaza
Meshack jumbo
“Makamu wa rais naye
anahusika na mtandao huu ndiyo
maana hataki kabisa Elvis aendelee kuuchimba mtandao huu
kwani atagundua vitu vingi na
wanataka afe na biashara zao
ziendelee kama kawaida.Siwezi
katu kuruhusu Elvis auliwe.Katika
suala hili na mimi lazima niingie
katika mapambano.Kwanza
kupambana kumlinda Elvis na pili
kupambana kuuficha mtandao
huu na vile vile kuitokomeza
kabisa biashara haramu ya silaha
inayofanywa na hawa vigogo wa
jeshi wakishirikiana na watu
waliomo serikalini” Akawaza Mzee
Jumbo
*****************
Baada ya dakika tano toka
alipoondoka Meshack Jumbo,makamu wa rais Dr Shafi
bado alikuwa na mawazo mengi
“Elvis Tarimo !! akawaza Dr
Shafi
“Inaonekana ni kijana mahiri
sana katika kazi yake na ndiyo
maana hata Meshack alistuka
nilipomtajia mpango wa
kumuua.Kwa upande Fulani nafsi
yangu inanisuta kuidhinisha
kijana mahiri kama huyu auliwe
lakini kwa upande mwingine
ninalazimika kufanya hivyo.Kama
tayari amekwisha anza
kumchunguza Frank basi kuna
uwezekano mkubwa akaweza
kuchunguza na kuugundua ule
mpango wetu wa kuiangusha
serikali.Sitaki hilo litokee kwani
ikitoea mpango huu ukajulikana
basi tumekwisha.Nitakosa kila kitu na kuozea gerezani.
Tunatakiwa kuchukua tahadhari
angali bado mapema.Kitu
chochote au mtu yeyote ambaye
ataonekana kuwa ni kikwazo
kwetu lazima tumuondoe haraka
sana.Katika suala hili sintakuwa
na huruma hata chembe” akawaza
Dr Shafi na kumpigia simu David
“hallo mheshimiwa Shafi”
akasema David baada ya kupokea
simu
“Habari za asubuhi David?
“Habari nzuri Dr
Shafi.Nimestuka kidogo na simu
hii ya asubuhi asubuhi”
“Usistuke David,nimekupigia
kukupa taarifa kwamba nimetoka
kuongea na Meshack Jumbo
mkurugenzi wa iadara ya ujasusiasubuhi hii na kila kitu
kimekamilika”
“That’s good news”
“It’s real good news but it
wasn’t easy.Jumbo anamuamini
sana Elvis na ilikuwa kazi ngumu
kumshawishi akubaliane na
mpango wa kumuua.Lakini
nashukuru alinielewa na
akakubali.Kinachofuata sasa ni
kujiandaa kuutekeleza mpango
huu” akasema Dr Shafi na
maongezi yao hayakuchukua
muda mrefu wakaagana
******************
Elvis ndiye aliyekuwa wa
kwanza kuamka.Pembeni yake
alikuwa amelala Doreen.Elvis
akahisi uchungu sana kwa kitendo kile cha kumsaliti mke
wake Patricia.
“Sijui shetani gani
amenishawishi hadi nikakubali
kuingia katika mtego wa Doreen
na kumsaliti mke wangu ambaye
niliapa mbele ya madhabahu
kwamba nitampenda kwa moyo
wangu wote” Akawaza Elvis na
kuinama
“I’m so stupid.Very stupid !!
akasema Elvis kwa sauti
akjilaumu kwa kitendo kile.Doreen
aliyekuwa amelala akafumbua
macho na kumtazama Elvis huku
akirembua macho yake.Asubuhi
hii alizidi kuonekana mrembo
“You are not stupid Elvis”
akasema Doreen huku akiupeleka
mkono wake kifuani kwa Elvis. Tafadhali Elvis usijilaumu
kwa hiki tulichokifanya.You
needed it and Patricia wasn’t
here.Hata hivyo you are
amazing.Mambo unayaweza.Thank
you so much Elvis” akasema
Doreen
“You are crazy.Hiki
tulichokifanya ni kosa kubwa
sana” akasema Elvis
“Usiseme hivyo Elvis.Huna
cha kujutia kwa sababu hata
Patricia naye amefanya kama
wewe.Unajua ni mara ngapi
amekuwa akichepuka?Tafadhali
usiwe na mawazo hayo.Just
relax.You are with me
now.Ulichokikosa kwa Patricia
utakipata kwangu na kwa muda
huu tutakaokuwa tunaishi hapa
just forget about Patricia.Niko hapa na nitakupa kila aina ya
raha ya hii dunia.I need you Elvis,I
need you so badly in my life”
akasema Doreen.Elvis akakunja
uso na kutaka kusema kitu lakini
simu yake ikaita akaichukua na
kutazama mpigaji alikuwa ni
Meshack Jumbo akasita kupokea
“Mbona hutaki kupokea hiyo
simu,inatoka kwa Patricia?
Akauliza Doreen baada ya kuona
Elvis akisita kuipokea ile simu
“Inatoka kwa mkurugenzi.Si
kawaida yake kunipigia asubuhi
namna hii,nahisi lazima kuna
jambo” Akasema Elvis
“Pokea usikie
anachokuambia”akasema Doreen
na Elvis akaipkea ile simu
“Shikamoo mzee” Marahaba Elvis.Nahitaji
kukuona haraka sana”
Elvis akastuka kidogo na
kuuliza
“Kuna nini mkurugenzi?
“Kuna suala linahitaji
ufumbuzi wa haraka sana”
“Tukutane wapi mzee?
Akauliza Elvis
“Tukutane pale kwa Salhat”
akasema Mkurugenzi
“Sawa mzee ninaelekea huko
sasa hivi”akasema Elvis
“What hapened? Akauliza
Doreen baada ya kuona Elvis
amebadilika
“Mkurugenzi anahitaji
kuniona sasa hivi”
“Kuna nini?
“Hajanieleza kuna nini lakini
kwa namna alivyosisitiza inaonekana kuna jambo.I have to
go” akasema Elvis na kuinuka
akaingia bafuni akaoga haraka
haraka na kutoka akavaa na
kuchukua funguo za gari
akamuaga Doreen na kutoka mbio
kuelekea gereji akafungua geti na
kuondoka
“Jamani Elvis katika kazi zote
za hii dunia kwa nini ukaichagua
hii? Hufanani kabisa na hii kazi”
akasema kwa masikitiko Doreen
akimchungulia Elvis dirishani
akiondoka.
“Lazima kuna jambo kubwa
limetokea.Si kawaida ya
mkurugenzi kunitaka tuonane
haraka tena si ofisini bali kwa
Salhat kimada wake.Nini
kimetokea? Akajiuliza
MWISHO WA I DIED TO SAVE
PRESIDENT PART 2.
USIKOSE PART 3.