Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Dr kaokota dodo kwenye mnazi
Kala kilaini hata hajaangaika kupiga sauti like ....I love you Patricia bla bla.....yeye kazi yake ilikuwa ni kutafuta sehemu salama akajipigie mzigo taratibu
 
Nmeshindwa kutuma sehemu mbili leo nimekosa Mb maybe kesho
 
Kweli Mkuu Patricia atajiona Hana dhamani tena na iyo itachagizwa baada ya Elvis kuzaa na Doreen

Kheri Particia angebaki na msimamo wake ule ule wa kutokugongwa nje... hivi kaanza kugongwa nje... atazea mwishowe kuharibu ndoa yake...

Cc: mahondaw
 
Kheri Particia angebaki na msimamo wake ule ule wa kutokugongwa nje... hivi kaanza kugongwa nje... atazea mwishowe kuharibu ndoa yake...

Cc: mahondaw
Acha watu wagongane siku zisogee. Mwanamke ni chombo Cha starehe...kiumbe dhaifu

Themes Mpaka Sasa.

1. Usaliti wa kimapenzi. Hapa tunamuona Patricia akimsaliti mumewe Elvis na kugawa uroda kwa Dr. Steven
2. Usaliti wa kazi. Hapa tunamwona Frank na Pascal wakisaliti serikali yao kwasababu ya tamaa ya fedha na madaraka.
3. Tamaa. Hapa tunaona tamaa ya aina mbili ya fedha na madaraka. Frank na Pascal wakishirikiana na aliyekuwa waziri mkuu kutaka kupindua serikali iliyopo madarakani ili waweze kugawana madaraka.
4. Rushwa. Hapa tunamwona ndugu waziri wa zamani akiwapa rushwa wapizani ili kutekeleza dhima yao ya kuangusha serikali iliyopo madarakani.
5. Uzalendo. Hapa tunamwona ndugu Elvis alivyojitoa mwanga kuukomboa taifa kutokana na biashara haramu inafanywa na mkuu wa majeshi ndugu Frank wakisaidiana na Pascal
6. Ujasiri. Hapa tunawaona Granca, Eliza mfanya kazi wa Pascal na mama yake Granca. Pamoja na kuteswa lakini bado hawakuwa tayari kuongea ukweli kuhusu begi aliyoiba mke wa Frank na mkoba aliyookata Eliza mfanya kazi wa Pascal.
7. Mapenzi ya Dhati. Hapa tunamuona kijana mahiri Elvis kwa mpenzi wake Patricia. Pamoja na matizo makubwa ya mkewe bado anampenda kwa moyo wa pekee.
8. Biashara haramu ya kuuza silaa za kivita. Hapa yupo Mr Pascal, Frank, Deusdedith
9.Mwanamke ametumika Kama chombo Cha starehe. Hapa tunamwona kahaba Vick anavyotumia mwili wake kustarehesha wanaume ili kujipatia fedha nyingi. Na mke wa Elvis - Patricia alivyogawa uroda kwa Dr. Steven

Hongezea nyingine.
 
I DIED TO SAVE PRESDENT

Sehemu 30

Ndiyo.Hakuna muda wa
kupoteza kwani tayari umekwisha
anza kumulikwa na Elvis na
hatujui ana mipango gani kwa
hiyo lazima tuchukue tahadhari
mapema ya kukupeleka sehemu
salama kwa sasa” Akasema Frank
“Sikutegema kabisa kama
siku moja mambo yangeweza
kugeuka namna hii” akalalamika
Vicky
‘Usiogope Vicky.Suala hili
litakwisha lakini kabla ya kwenda
huko mafichoni kuna jambo
ambalo tunatakiwa
kulifanya.Tutakwenda nyumbani
kwako na kuondoa kila kitu
ambacho kinaweza kumsaidia
Elvis au mtu yeyote Yule ambaye
anakufuatilia” Akasema Frank bila kupoteza wakati wakaondoka
kuelekea nyumbani kwa Vicky
********************
Alipomaliza mizunguko yake
aliyoipanga Doreen akawasili
nyumbani kwa akina Elvis
kuonana na
Patricia.Alikaribishwa sebuleni na
Stella mtumishi wa ndani kisha
akaenda kumtaarifu Patricia
ambaye alielekeza Doreen amfuate
chumbani.Doreen alipoingia
chumbani akastuka sana kwa hali
aliyomkuta nayo Patricia.Macho
yalikuwa mekundu na yamevimba
“Patricia !! Doreen akastuka
sanaDoreen ! Karibu” akasema
Patricia kwa sauti ya uchovu huku
akiinuka na kukaa kitandani
“Patricia what happened? Are
you sick? Akauliza Doreen.Patricia
akavuta pumzi ndefu na kusema
“Doreen siumwi ndugu yangu”
‘Kama huumwi kitu gani
kimetokea? Toka jana nimejaribu
kukutafuta lakini simu yako
haipatikani.Hali yako
imeniogopesha sana”
Patricia akanyoosha mkono
wake na kuchukua simu iliyokuwa
pembeni akaiwasha na kuitupa
pembeni huku jumbe nyingi
zikiingia mfululizo lakini hakutaka
kujishughulisha nazo
“Patricia hebu nieleze una
tatizo gani? Akauliza Doreen “Doreen unanifahamu vizuri
mimi ni mwanamke mvumilivu na
mwenye ujasiri mkubwa lakini
kwa sasa naona ninaelekea
kushindwa kuvumilia tena”
“Kuna nini kimetokea?
Akauliza Doreen.Patricia
akainama akafuta machozi na
kusema
“Doreen nashindwa nianzie
wapi kukueleza”
“tafadhali nieleze
Patricia.Mimi ni rafiki yako
nitakusikiliza na nitakusaidia kwa
lolote” akasema Doreen huku
akimsaidia Patricia kufuta
machozi
“Doreen nimefanya jambo
baya sana ambalo sikutegemea
kulifanya katika maisha yangu”
akasema Patricia Umefanya nini Patricia?
Patricia akamtazama Doreen
kwa muda halafu akasema
“Nimetembea nje ya ndoa
yangu Doreen.Nimemsaliti Elvis”
akasema Patricia na kushindwa
kujiuzia akaanza kulia
tena.Doreen akabaki katika
mshangao
“Doreen I’m so stupid !!
akasema Patricia
“Nyamaza kulia
Patricia.Tafadhali nieleze ilikuaje
hadi ukafanya hivyo?Shetani gani
alikuingia hadi ukaamua kufanya
hivyo Patricia?
Patricia akafuta machozi na
kusema
“Jana tulikuwa na sherehe ya
kumkaribisha Dr Steven
Washington anayetokea Marekani.Nilirudi nyumbani
kujiandaa kwa sherehe hiyo
nikapata taarifa toka kwa Stella
kwamba Elvis amerejea na
kuondoka tena kwenda katika kazi
nyingine.Aliyenitibua zaidi ni
Stella ambaye alinieleza kwamba
Elvis alikuwa na mwanamke ndani
ya gari.Sikufichi Doreen nilijikuta
nikiwa na wivu mkali.Nilijiuliza
maswali mengi kuhusu
mwanamke huyo aliyekuwa na
Elvis katika gari ni nani na
wanakwenda
wapi?Kilichonishangaza zaidi ni
Elvis kutonitaarifu moja kwa moja
kwamba amerejea.Nilihisi mambo
mengi na kudhani yawezekana
hakuwa amekwenda Afrika kusini
kama alivyoniambia,yawezekana
amepata mwanamke mwingine.Baadae niliamua
kuyapuuza mawazo haya na
kuendelea na safari kwenda katika
sherehe.Nikiwa njiani mama mkwe
akanipigia simu lakini sikupokea
akaamua kuniandikia ujumbe”
Patricia akaufungua ujumbe
ule aliotumiwa na mama mkwe
wake akamuonyesha Doreen
ambaye alipousoma sura yake
ikabadlika akashikwa na hasira
“Huyu mama mkwe wako ni
mzima kweli?Anawezaje
kukuandikia ujumbe mchafu
kama huu? Akasema Doreen kwa
hasira
“Patricia wewe ni mvumilivu
sana.Ningekuwa mimi nisingejali
ni mama mkwe ningekwenda
kucharuana naye.Huu ni
udhalilishaji mkubwa sana.Hii imevuka mipaka!! Akasema
Doreen
“Doreen hiyo ndiyo hali halisi
ilivyo hivi sasa.Ninapitia kipindi
kigumu sana na ndiyo maana
nilipousoma ujumbe huo
nlichanganyikiwa na kushindwa
nifanye nini.Nililia sana na
kujiuliza aliko Elvis.Yeye ndiye
mtu pekee ambaye huwa
ananifariji katika nyakati kama
zile.I needed him so badly.I needed
someone to comfort me.kwa hali
niliyokuwa nayo ningeweza hata
kufanya kitu kibaya.Sikutaka
kurejea nyumbani.Nyumba hii ni
nzuri lakini kwa sasa naiona kama
gereza la mateso.Ni katika hali
hiyo nikajikuta nikilala na Dr
Steven ” akasema Patrica na kuinama akaufunika uso kwa
viganja vya mikono
“I made the biggest mistake in
my life” akasema Patricia
“Usilie Patricia na wala
usijilaumu .Ninakufahamu vizuri
sana na ninaamini hukufanya kwa
kukusudia.Ulihitaji faraja na mtu
pekee ambaye alitakiwa kukufariji
ni Elvis lakini hakuwepo.Wa
kulaumiwa hapa ni Elvis na si
wewe.Kwa wakati kama huu Elvis
alipaswa aachane kwanza na kazi
zake na kukaa nawe.Wewe ni wa
thamani kubwa sana kwake kuliko
hata kazi hiyo anayoifanya”
akasema Doreen
“Doreen nimekwisha ongea
kuhusu kazi hiyo hadi
nimechoka.Elvis hataki
kumsikiliza mtu yeyote kuhusiana na kazi hiyo.Doreen nina matatizo
makubwa katika ndoa yangu na
mengine siwezi kuyaweka wazi
inabaki siri yangu” akasema
Patricia
“Naelewa unachokisema
Patricia lakini haya yote
yasingetokea kama isingekuwa
kazi hii ya Elvis.kwa nini asiache
na kufanya kazi nyingine?Halafu
kuhusu mama yake umewahi
kumueleza namna anavyokutenda
na kukutumia jumbe za kejeli
namna hii? Akauliza
Doreen.Wakati patricia akijiandaa
kujibu mara simu yake
ikaita.Akatazama mpigaji na
kustuka
“mbona umestika ? akauliza
Doreen
“rais ananipigia” rais ?!! akauliza Doreen
“Ndiyo.Nimeshangaa kwani si
kawaida yake kunipigia simu na
hasa mida hii” akasema Patricia
na kuipokea simu ile
“baba shikamoo” akasema
Patricia kwa adabu
“Marahaba Dr
Patricia.Hujambo?
“Sijambo baba.hajambo
mama?
“Mama yako hali yake si nzuri
na ndiyo maana nimekupigia
simu.Nimeambiwa kwamba leo
hujafika kumuona.Una tatizo
lolote? akauliza rais
“Nilipatwa na dharura
asubuhi ya leo na kushindwa
kuja.Mama amepatwa na tatizo
gani? Hali yake imebadilika sana
,nadhani ungekuja kumuangalia
wewe mwenyewe kama utakuwa
na nafasi muda huu”
“Ok nakuja sasa hivi”
akasema Patricia
“Ahsante sana Dr Patricia na
samahani sana kwa usumbufu”
akasema rais na kukatasimu.
“Mke wa rais hali yake si
nzuyri hivyo natakiwa niende
ikulu mara moja
kumtazma.Doreen tutaongea zaidi
kesho.Nitaktafuta” Akasema
Patricia wakaagana Doreen
akaondoka akimuacha Patricia
akijiandaa kwenda ikulu
******************* Saa tisa na dakika kumi
alasiri,Doreen akawasili katika
makazi ya muda ya Elvis.Graca
alikuwa sebuleni akitazama
filamu.Wakasalimiana na Doreen
akauliza kama tayari Elvis
amerejea akaambiwa tayari
amerejea na yuko chumbani
kwake anapumzika.Doreen
akaelekea chumbani kwa Elvis
akagonga mlango
Toka amerudi Elvis alikuwa
amejifungia chumbani kwake
akijaribu kuwaza mambo
mbalimbali .Kikubwa kilichotawala
kichwa chake ni kitendo cha
kumuona mke wake paticia
akitoka hotelini akiwa na
mwanaume mwingine .Akiwa
katika tafakari mlango wake ukagongwa akavaa shati na
kwenda kuufungua.
“Doreen.karibu sana”
Akasema Elvis kwa sauti ya
uchovu
“Umeshindaje Elvis? Akauliza
Doreen
‘Nimeshida salama” akasema
Elvis na kumkaribisha ndani
Doreen
‘habari za huko utokako?
Mambo yote yamekwenda vizuri?
Elvis akauliza
“Ndiyo.Kila kitu kimekwenda
vizuri kabisa.Vipi kuhusu wewe
mambo yako yamekwenda sawa?
“mambo yamekwenda vizuri”
akasema Elvis na kimya kifupi
kikapita
“Umefanikiwa kuonana na
patricia? Elvis akauliza Ndiyo nimeonana naye”
“Ulimfuata kazini?
“Nimemfuata
nyumbani.Kazini hakuingia leo”
“Is she fine? Elvis akauliza
“Some how” akajibu Doreen
.Elvis akavuta pumzi ndefu na
kuuliza
“Where was she last night?
Doreen akastuka kwa swali
lile
“Umeuliza nini Elvis?
Akasema Doreen
“Nimeuliza Patria
amekwambia jana usiku alikuwa
wapi? Swali lile likamfanya Doreen
atetereke katika kujibu.Alistuka
Elvis amefahamuje kuhusiana na
suala lile la Patricia kutokulala
nyumbani kwake Sielewi kwa nini umeuliza
swali kama hilo? Unahisi Patricia
halali nyumbani wakati haupo?
Don’t you trust her? Akauliza
Doreen.Elvis akamtazama kwa
makini machoni na kusema
“Tell me the truth
Doreen.Patricia alikuwa wapi jana
usiku? Ninafahamu wewe ni rafiki
yake mkubwa na hakuna kitu
anachoweza kukuficha” Akasisitiza
Elvis
“Elvis kwa nini unakuwa na
mashaka na mke wako? Mbona
Patricia hajanieleza kuhusiana na
jambo lolote la yeye kutokuwepo
nyumbani jana usiku? Tafadhali
muamini mkeo.Anakupenda mno”
akasema Doreen.Elvis akainuka
akaenda dfirishani akachungulia nje.Doreen akainuka na kumfuata
akamshika bega
“Elvis kuna nini? Mbona
umebadilika hivyo? Elvis akageuka
akamtazama Doreen na kusema
“Siku ya kwanza kukutana na
Patricia nilijua yeye ndiye
mwanamke wa maisha yangu.Toka
dakika hiyo upendo wangu kwake
haujawahi kupungua na
unaongezeka siku hadi
siku.Kwanguyeye ni kila
kitu.Ninampenda zaidi ya
ninavyoweza kueleza” akanyamaza
kwa muda halafu akasema
“Asubuhi ya leo nimemuona
mke wangu Patricia akitoka
hotelini akiwa ameongozana na
mwanaume mmoja ambaye
simfahamu.Kwa muonekano
aliokuwa nao ilionyesha wazi kwamba hakuwa kazini kwani
mavazi aliyoyavaa ni ya kutokea
usiku.Nilimpigia simu mfanyakazi
wetu pale nyumbani akasema
kwamba Patricia aliondoka jana
jioni na hakurejea
nyumbani.Najiuliza kama hakulala
nyumbani alilala wapi? Alilala
hotelini? Yule mwanaume
aliyekuwa naye ni nani? Je alilala
naye? Kama hakulala naye pale
hotelini alitoka kufanya
nini?Doreen nina wasi wasi
kwamba Patricia ananisaliti.Kuna
uwezekano mkubwa akawa
anatoka nje ya ndoa yetu”
akasema Elvis na kuonekana
kuumizwa sana na jambo
lile.Doreen alikuwa katika wakati
mgumu .Alitamani amueleze
ukweli Elvis lakini akaogopa Namuonea huruma
Elvis.Ameumizwa mno na kitendo
cha kumuona Patricia akitokea
hotelini akiwa na mwanaume
mwingine.Itakuaje nikimweleza ni
kweli patricia amemsaliti? Hata
hivyo kama tayari amekwisha
waona wakitoka hotelini na papo
hapo ana u hakika kwamba
Patricia hakulala nyumbani ni
vigumu kuamini kwamba Patricia
hakulala na Yule mwanaume
aliyekuwa naye.Ni bora nimweleze
ukweli ili kulimaliza suala
hili.Endapo atagundua kwamba
ninalifahamu jambo hili na
nikamficha hataniamini tena.Hii ni
nafasi yangu pia ya kujisogeza
karibu zaidi na Elvis” akawaza
DoreenElvis naomba nikueleze
ukweli” Akasema Doreen.Elvis
akainua kichwa na kumtazama
“Ni kweli Patricia hakulala
nyumbani jana na nitakueleza
kisa chote kilichotokea kwani
amenieleza kila kitu” akasema
Doreen na kumueleza Elvis kila
kitu kama alivyoambiwa na
Patricia bila kuacha hata neno
moja.Elvis alipandwa na hasira
kali
“Kumbe ni ndugu zanu ndio
wanaochangia kuivurga ndoa
yangu!! Akasema Elvis kwa hasira
akachukua simu ya Doreen
akaandika namba za mama yake
na kupiga.
“Hallow” ikasema sauti ya
mama yake baada ya kupokea
simu Mama shikamoo.Ni mimi
Elvis hapa ninaongea” akasema
Elvis
“Oh ! Elvis kumbe
umesharejea toka safari.mambo
yako yanakwendaje? Akauliza
mama yake
“Mama sina muda mrefu wa
maongezi.Ninataka kuweka sawa
baadhi ya mambo.Tafadhali mama
usiingilie ndoa yangu.Kaa mbali
na mke wangu na sitaki mtu
yeyote awe wewe au ndugu yeyote
mwingine kumkoseshaamani mke
wangu.Sitaki kusikia mtu yeyote
akimuuliza habari za
mtoto.Yeyote atakayethubutu
kwenda na kumuuliza eti mbona
hutuzalii mtoto atakutana na
mimi.Leave us alone!!! Akasema
Elvis na kukata simu. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza
kuzungumza na mama yake kwa
ukali namna ile.
“Umefanya vizuri Elvis
kuwaeleza ukweli.” Akasema
Doreen
“Doreen uliwahi kunieleza
kwamba kazi yangu imenifanya
nijiweke mbali na Patricia.Ulikuwa
sahihi.Patricia ananipenda sana
na hawezi kufanya kitendo kama
kile bila sababu.Yote haya
yamesababishwa na
mimi.Nimekuwa nikitumia muda
mwingi sana katika kazi kuliko
muda ninaoutumia na mke
wangu.Japokuwa imeniumiza
kusikia mke wangu ametembea
nje ya ndoa lakini lazima nikubali
ukweli kwamba chanzo ni
mimi.Patricia anahitaji faraja na mtu pekee ambaye nilipaswa kuwa
karibu naye kumfariji ni mimi”
akasema Elvis na kuzama
mawazoni
“Doreen I need to be alone for
now” akasema na taratibu Doreen
akatoka mle chumbani
akamuacha Elvis peke yake
“Kwa nini maisha yangu
yanakuwa hivi? Kwa nini
nashindwa kuwa na maisha ya
kawaida nifurahi na mke wangu
Patricia?kwa nini ndugu zangu
wanaingilia ndoa yangu na kutaka
kuivuruga? Akajiuliza.Aliwaza
mambo mengi sana
“Mimi nadhani suluhisho
pekee ni kuachana na hii kazi ili
niokoe ndoa yangu inayotaka
kuzama.Patricia amelazimika
kutembea nje ya ndoa na chanzo cha haya yote ni mimi.Sitaki
kumuona Patricia akiendelea
kuteseka.Amani furaha na upendo
lazima virejee tena katika ndoa
yangu.Ili haya yote yafanikiwe
lazima niachane na hii kazi
haraka” akawaza
“Nafahamu nina jukumu
kubwa mbele yangu la kufumua
mtandao mkubwa na hatari wa
watu wanaofanya biashara ya
kuuza silaha kwa waasi wa Congo
lakini kutokana na suala zito
linalomkabili Patricia kwa sasa
sina budi kuwapa nafasi wengine
waendelee na kazi hii
niliyoianza.Natakiwa kuwahi
kujenga nyumba yangu inayoanza
kuweka ufa” Akawaza Elvis na
sura ya Graca ikamjia“Lakini kabla ya kuacha kazi
hii lazima nihakikishe kwamba
huyu binti anakuwa katika
sehemu salama.Nilimuahidi hivyo
na lazima nitekeleze
nilichomuahidi.Siwezi kumuacha
hivi hivi.Nitamsisitiza mkurugenzi
alishughulikie kwa haraka suala
lake ili limalizike mapema na mimi
niweze kurejea nyumbani kwangu”
akawaza Elvis
*****************
Saa kumi na mbili za jioni
hali ilikuwa ya utulivu mkubwa
ndani ya jumba kubwa la brigedia
Frank kwaju lililopo katikati ya
shamba lake.Ndani ya jumba hili
watu watatu walikuwa wamekaa
sebuleni wakiongea.Brigedia Frank alikuwa pamoja na mshirika wake
wa karibu pascal pamoja na
Victoria ambaye wamempeleka
kule shambani kwa ajili ya
kumficha
“Vicky sisi inabidi tukuache
hapa kwa muda.Kuna sehemu
tunahitajika usiku huu.Usiwe na
hofu yoyote kuhusu usalama
wako.Mahali hapa ni salama
sana.Hata hivyo nitarejea mimi
baadae.Siwezi kukuacha hapa
peke yako” akasema Frank huku
akitazama saa yake
‘I’m so scared Frank.Sijazoea
kukaa sehemu yenye ukimya
mkubwa kama hii.No one is
moving around. Gosh ! its’s like
hell !.tafadhali Frank ukimaliza
shughuli zako njoo mara moja
sina hakika kama nitaweza kupata usingizi usiku wa leo nikiwa peke
yangu ndani ya jumba hili”
akasema Vicky
“ Usihofu Vicky,mara tu
nitakapomaliza mambo yangu
nitarejea mara moja.Kila
unachokihitaji ndani ya jumba hili
utakipata.Jisikie huru” akasema
Frank halafu akamfanyia ishara
Pascal wakaondoka.
“Una hakika utarudi kama
ulivyomuahidi Vicky au ulikuwa
unamdanganya kumuondoa woga?
Akauliza Pascal
“Ndiyo nitarejea.Ni dhambi
kumuacha malaika kama Yule
alale peke yake.Lazima na mimi
niufaidi uumbaji wa Mungu usiku
wa leo.Japokuwa Vicky ni kahaba
lakini si rahisi kumpata.Ana pesa
nyingi na mapenzi anafanya kwa starehe ndiyo maana kwa usiku
mmoja anatoza hadi milioni
tano.Hii ndiyo sababu nimeitisha
kikao cha leo kianze mapema ili
niwahi kujipumzisha na Vicky
mwanamke kahaba mwenye uzuri
wa kipekee” akasema Frank huku
akitabasamu
‘Vipi kuhusu Elvis? Namna
gani tutaweza kumuondoa?
Frank akatabasamu na
ksuema
“Usijali Pascal.Elvis ni mtu
mdogo mno.Masaa yake ya kuishi
yanahesabika.Sisi ni watu wenye
nguvu sana na hatuwezi kukubali
kutiwa tumbo joto na mdudu
mdogo kama Elvis.Mambo yetu
yote yatakwenda kama
tunavyotaka na hakuna wa kutuzuia” akasema Frank huku
safari ikiendelea
Saa moja na nusu za usiku
wajumbe wote wanaotakiwa
kuhudhuria kikao cha usiku huu
tayari wamekwisha wasili na
Frank akafungua kikao
“Ndugu zangu kwanza kabisa
napenda kuwashukuru kwa
kufika kwenu katika kikao cha
leo.Kama mtakumbuka katika
kikao kilichopita tulipeana
majukumu kadhaa kwa baadhi
yetu ambayo yatatupa uelekeo
mzima kuhusiana na mpango
wetu.Kikao cha leo ni maalum
kabisa kwa ajili ya kupeana taarifa
ni wapi tumefikia.Namkaribisha
kwanza rais wetu mtarajiwa David
ili aweze kutueleza amefikia wapi
katika jukumu alilopewa” David akatabasamu baada
wajumbe kumpigia makofi
“Ahsanteni sana.Nashukuru
sana ndugu zangu kwa heshima
hii kubwa.Tuzidi kuomba ili
mambo yaende kama
tunavyotaka” Akasema
“Katika kikao kilichopita
nilikabidhiwa majukumu
mawili.Moja ni kuonana na
makamu wa rais na kumshawishi
aungane nasi na pili ni kuongea
na wanasiasa na kuwashawishi
waanzishe maandamano
yatakayokuwa na lengo la kupinga
kitendo cha makampuni ya
Marekani kupewa fursa ya
kuwekeza katika sekta ya mafuta
na gesi hapa nchini.Mambo haya
yote mawili nimeyafanikisha vizuri
kama mlivyoniagiza.Kwanza kabisa nilionana na wakuu wa
vyama vya upinzani.Kwa bahati
nzuri wakuu wote niliowaalika
kuonana nao walifika.Niliongea
nao kwa kirefu na ninapenda
kuwataarifu kwamba wamekubali
kufanya
niliyowaomba.Wamekubali
kuungana na kuanzisha
maandamano makubwa yasiyo na
ukomo yatakayoambatana na
vurugu.Kwa sasa tayari wameanza
maandalizi ya kampeni hiyo
kubwa ya kitaifa na nimewataka
ndani ya siku mbili waniletee
mchanganuo wa gharama zote za
kampeni hiyo.Ni pesa nyingi
itahitajika lakini hatuna namna
lazima tutumie pesa.Wanasiasa
hawa hawaelewi ni kitu gani
kilicho nyuma ya kampeni hiyo.Hawaelewi kama nyuma ya
kampeni hiyo kuna mipango ya
kuiangusha serikali.Siku yoyote
ndani ya wiki hii mtasikia tamko
la pamoja la wenyeviti hawa wa
vyama vya upinzani nchini la
kuzindua rasmi kampeni hiyo”
David akanyamaza na wajumbe
wakampigia makofi.Akaendelea
“Kwa upande wa makamu wa
rais nilifanikiwa kuongea
naye.Haikuwa kazi nyepesi
kumshawishi lakini nilitumia kila
aina ya ushawishi na hatimaye
nikafanikiwa kumshawishi
akakubali.Kwa hiyo napenda
kuwatamkia rasmi kwamba
makamu wa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania ni
mwenzetu katika harakati
hizi.Japokuwa kuna masharti aliyatoa lakini yanatekelezeka
hivyo msiwe na hofu.Makamu wa
rais ni mtu muhimu sana katika
mchakato huu.Yeye ndiye
atakayetusaidia kutupa taarifa
mbali mbali za ndani ya
serikali”akasema David na
wajumbe wakampigia tena makofi
“Jukumu lingine ambalo bado
natakiwa kulifanya ni
kuwashawishi baadhi ya viongozi
wa serikalini na wote ambao
wataonekana kuwa na umuhimu
katika mchakato huu.Kuna baadhi
ya mawaziri ambao nadhani
watafaa kuhusishwa.Si mawaziri
tu bali kuna watu wengine ambao
ni muhimu nao wakashirikishwa
pia.Nadhani katika kikao kijacho
tayari nitakuwa nimekwisha fanya hiyo kazi na nitakuja na majibu”
akasema David na kukaa
“Ahsante sana mheshimiwa
rais mtarajiwa” akasema Frank
“Tunashukuru kwa kazi hiyo
kubwa uliyoifanya.Kwa upande
wangu mimi nilikabidhiwa jukumu
la kuwashawishi makamanda wa
vikosi vitakavyoasi.Kazi
imekwenda vizuri na tayari
nimefanikiwa kuwashawishi
makamanda wawili na
wamekubali.Makamanda watatu
bado kuna mambo
hatujakubaliana lakini
tunaendelea na maongezi na nina
uhakika muda si mrefu tutafikia
makubaliano.Kikao kijacho
nitakuwa na jibu zuri la
kuwapeni” akasema Frank Majadiliano yakaendelea hadi
ilipotimu saa tano za usiku
wajumbe wakaagana na kuondoka
isipokuwa Frank na Pascal
waliokuwa na maongezi na David
“Frank uliniambia una
tatizo.Ni tatizo gani? Akasema
David
“David kuna tatizo
limejitokeza .Kuna mdudu
amejitokeza ambaye
asipodhibitiwa haraka anaweza
kuleta madhara makubwa kwetu”
akasema Frank
“Mdudu gani huyo? Akauliza
David kwa wasi wasi.Frank
akamueleza kila kitu kuhusiana
na Elvis.
“Huyo kijana tutamdhibiti
vipi? Ni wazi anaonekana ni hatari
sana kwetu”Akauliza David. ‘Ndiyo maana tumekuja
kwako kuomba msaada wa
kumdhibiti huyu kjana haraka
iwezekanavyo” Akasema Frank
“Hebu nielezeni ninaweza
kusaidia vipi kumuondoa huyo
kijana?
“Nataka umweleze makamu
wa rais.Kitengo anachofanyia kazi
Elvis kimehamishiwa katika ofisi
yake kwa hiyo yeye ana sauti
kubwa na atatoa amri huyo kijana
auawe” akasema Frank
‘Endapo makamu wa rais
akatoa amri Elvis auawe nyie
mmejipangaje? Atauawa vipi?
“Ataelekezwa aende mahala
akaonane na mtu mwenye taarifa
za muhimu sana na huko
tutawapanga watu wetu
watamshambulia na kuuawa.Kifo chake hakitahojiwa kwa sababu
mkurugenzi wake atakuwa
anafahamu kila kinachoendelea
hivyo atahakikisha hakuna aina
yoyote ya uchunguzi
utakaofanyika.Mwenye uwezo wa
kufanikisha haya ni makamu wa
rais pekee” akasema Frank.David
akainama na kukuna kichwa
chake akafikiri kwa muda na
kusema
“Sawa Frank.Niachie suala
hilo nilishughulikie Nitazungumza
na makamu wa rais na
nitamueleza kila kitu.Nitakupa
jibu asubuhi”akasema David
“Ahsante sana David.Suala
hili ni la muhimu mno endapo
tusipowahi kumdhibti mtu huyu
kuna hatari akatuvurugia kila
kitu” Usihofu Frank.Nitajitahidi
kufanya kila linalowezekana ili
tulimalize jambo hili na kusiwe na
kizingiti chochote katika mpango
wetu” akasema David kisha
akaagana na Frank kwa ahadi ya
kumpigia simu asubuhi na
mapema.Frank na Pascal
wakaondoka
****************
Mara tu baada ya akina Frank
kuondoka David akampigia simu
makamu wa rais kupitia namba
yake maalum
“Halow David” akasema
makamu wa rais baada ya
kupokea simu
“Hallo Mr Shafi.Samahani
kwa kukusumbua usiku huu” “Bila samahani
David.Nadhani kuna jambo la
muhimu unataka kunieleza”
“Ndio Mr Shafi.Kuna jambo
ambalo limejitokeza na linahitaji
utekelezaji wa haraka na ambaye
anaweza kulifanya jambo hili
likamalizika ni wewe”
“Jambo gani hilo David”
David akamweleza makamu
wa rais kila kitu kuhusiana na
Elvis. Makamu wa rais
akanyamaza na kufikiri kwa muda
kisha akasema
“Ok David.Niachie suala hili
nilishughulikie kesho asubuhi
halafu nitakupigia simu
kukufahamisha” akasema
makamu wa rais wakagaana na
bila kupoteza muda Dr Shafi mkurugenzi wa idara ya ujasusi
akamuomba afike nyumbani
kwake asubuhi na mapema
“Kazi imeanza.Haya ndiyo
mambo ambayo sikuwa nayataka”
akasema Dr Shafi kwa sauti ndogo
na kuelekea chumbani kwake
kulala
********************
Kwa muda sasa Elvis alikuwa
akiitazama mishale ya saa kubwa
iliyokuwa inapishana na
kubadilisha majira.Muda ulizidi
kuyoyoma na hadi mida hiyo ya
saa saba za usiku hakuwa
amepata usingizi.Kichwa chake
kilijaa mawazo mengi
“Endapo ningechagua
kufanya kazi nyingine maisha yangu yangekuwa mazuri sana
hivi sasa.Hata hivyo bado
sijachelewa,baada tu ya Graca
kuondoka utakuwa ni mwisho
wangu kuifanya kazi hii.Najua si
jambo jepesi lakini kwa ajili ya
Patricia nitafanya kila
linalowezekana” akawaza Elvis
Wakati akiendelea kuwaza
mara mlango wake ukagongwa
akainuka na kwenda
kuufungua.Alikua ni Doreen
“Doreen hujalala mpaka mida
hii? Akauliza Elvis huku macho
yake akiwa ameyaelekeza katika
kifua cha Doreen ambacho
kilibeba matiti yaliyojaa ambayo
yalionekaa kwa urahisi kutokana
na nguo nyepesi ya kulalia
aliyoivaa. Elvis samahani kama
nimekusumbua” akasema Doreen
“Hujanisumbua Doreen. Una
tatizo lolote? Akauliza Elvis
“Nimeshindwa kabisa kupata
usingizi Elvis.nNaweza kuingia
ndani? Akauliza Doreen
“Bila wasi wasi.karibu ndani”
akasema Elvis na Doreen akaingia
ndani.Mwili wote wa Doreen
uliweza kuonekana vyema kupitia
nguo ile nyepesi aliyoivaa.Elvis
akajikuta akisismka mwili mzima
akafunga mlango na kwenda
kuketi sofani.Doreen naye
akainuka mahala alipokuwa
amekaa akamfuata Elvis
“Elvis najua una mawazo
mengi sana yanayokusumbua
kichwa chako na kubwa ni hili
suala la Patricia ambalo naamini limekuumiza mno.Hata mimi
nimeumia vile vile kwaniPatricia ni
rafiki yangu kipenzi.Pamoja na
hayo naomba usihuzunike sana
Elvis.Hayo ni majaribu katika
ndoa yenu na yatakwisha”
akasema Doreen na kuupeleka
mkono wake kifuani kwa Elvis na
kuanza kumpapasa.Elvis
akamzuia
“Unafanya nini Doreen?
Kwa sauti laini ya kimahaba
Doreen akasema
“Please don’t say no Elvis.I
want to make you happy.Just for
tonight I want you to forget the
world.Please Elvis” akasema
Doreen
“Doreen tafadhali nakuomba
inuka uende chumbani kwako
ukalale.Siwezi kumsaliti Paticia.Nampenda mno mke
wangu na hata wewe unalifahamu
hilo” akasema Elvis.Doreen
akinuka na kupiga magoti huku
akiendelea kumpapasa Elvis
mabegani
“Nafahamu unampenda na
kumheshimu mkeo lakini je yeye
anakuheshimu? Amevunja kiapo
cha ndoa kwa kutembea na
mwanaume mwingine.Japo
anasema ni mara moja lakini
utamuaminije? Unafahamu ni
mara ngapi anafanya hivyo?
Akauliza Doreen
“Please stop that
Doreen.Tafadhali usiendelee
kuniumiza kwa suala hili’
“That’s the reason I’m here
Elvis.To make you happy and
forget what happened.Forget about Patricia just for tonight” akasema
Doreen kwa sauti laini huku
akiendelea kumpapasa
Elvis.Taratibu Elvis akaanza
kupandwa na hisia na mwili
ukamsisimka.Doreen akaendelea
na utundu wake na taratibu
akaivua fulana ya Elvis na
kukishuhudia kifua kilichojengeka
akazidi kupagawa.Elvis alishindwa
kujizuia akajikuta ameanza kutoa
ushirikiano na kuzidi
kumpagawisha Doreen.Baada ya
dakika zipatazo kumi wakajikuta
wakiogelea katika mahaba
mazito.Kwa mara ya kwanza Elvis
akavunja kiapo cha ndoa na
kumsaliti mkewe
******************
akampiga simu Meshack Jumbo
 
Back
Top Bottom