Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Jioni tunaweza kuendelea season 3 kama nitapata mb maana nipo site sina access ya vocha huku
Mkuu mbona kimya sana. Tusubiri mavitu. Hii novel nashauri iingie moja kwa moja kwenye syllabus ya kufudishia. Itumiwe na kidato Cha tano na sita.
 
I DIED TO SAVE PRESDENT

Sehemu 32

Season 3

ILIPOISHIA SEASON 2
Elvis ndiye aliyekuwa wa
kwanza kuamka.Pembeni yake
alikuwa amelala Doreen.Elvis
akahisi uchungu sana kwa
kitendo kile cha kumsaliti mke
wake Patricia.
“Sijui shetani gani
amenishawishi hadi nikakubali
kuingia katika mtego wa Doreen
na kumsaliti mke wangu ambaye
niliapa mbele ya madhabahu
kwamba nitampenda kwa moyo
wangu wote” Akawaza Elvis na
kuinama
“I’m so stupid.Very stupid !!
akasema Elvis kwa sauti
akjilaumu kwa kitendo kile.Doreen
aliyekuwa amelala akafumbua
macho na kumtazama Elvis huku akirembua macho yake.Asubuhi
hii alizidi kuonekana mrembo
“You are not stupid Elvis”
akasema Doreen huku akiupeleka
mkono wake kifuani kwa Elvis.
“Tafadhali Elvis usijilaumu
kwa hiki tulichokifanya.You
needed it and Patricia wasn’t
here.Hata hivyo you are
amazing.Mambo unayaweza.Thank
you so much Elvis” akasema
Doreen
“You are crazy.Hiki
tulichokifanya ni kosa kubwa
sana” akasema Elvis
“Usiseme hivyo Elvis.Huna
cha kujutia kwa sababu hata
Patricia naye amefanya kama
wewe.Unajua ni mara ngapi
amekuwa akichepuka?Tafadhali
usiwe na mawazo hayo.Just relax.You are with me
now.Ulichokikosa kwa Patricia
utakipata kwangu na kwa muda
huu tutakaokuwa tunaishi hapa
just forget about Patricia.Niko
hapa na nitakupa kila aina ya
raha ya hii dunia.I need you Elvis,I
need you so badly in my life”
akasema Doreen.Elvis akakunja
uso na kutaka kusema kitu lakini
simu yake ikaita akaichukua na
kutazama mpigaji alikuwa ni
MeshackJumbo akasita kupokea
“Mbona hutaki kupokea hiyo
simu,inatoka kwa Patricia?
Akauliza Doreen baada ya kuona
Elvis akisita kuipokea ile simu
“Inatoka kwa mkurugenzi.Si
kawaida yake kunipigia asubuhi
namna hii,nahisi lazima kuna
jambo” Akasema Elvis Pokea usikie
anachokuambia”akasema Doreen
na Elvis akaipkea ile simu
“Shikamoo mzee”
“Marahaba Elvis.Nahitaji
kukuona haraka sana”
Elvis akastuka kidogo na
kuuliza
“Kuna nini mkurugenzi?
“Kuna suala linahitaji
ufumbuzi wa haraka sana”
“Tukutane wapi mzee?
Akauliza Elvis
“Tukutane pale kwa Salhat”
akasema Mkurugenzi
“Sawa mzee ninaelekea huko
sasa hivi”akasema Elvis
“What hapened? Akauliza
Doreen baada ya kuona Elvis
amebadilika Mkurugenzi anahitaji
kuniona sasa hivi”
“Kuna nini?
“Hajanieleza kuna nini lakini
kwa namna alivyosisitiza
inaonekana kuna jambo.I have to
go” akasema Elvis na kuinuka
akaingia bafuni akaoga haraka
haraka na kutoka akavaa na
kuchukua funguo za gari
akamuaga Doreen na kutoka mbio
kuelekea gereji akafungua geti na
kuondoka
“Jamani Elvis katika kazi zote
za hii dunia kwa nini ukaichagua
hii? Hufanani kabisa na hii kazi”
akasema kwa masikitiko Doreen
akimchungulia Elvis dirishani
akiondoka.
“Lazima kuna jambo kubwa
limetokea.Si kawaida ya mkurugenzi kunitaka tuonane
haraka tena si ofisini bali kwa
Salhat kimada wake.Nini
kimetokea? Akajiuliza

ENDELEA SEASON 3

Salhat beauty salon ni saluni
yenye jina kubwa jijini Dar
inayomilikiwa na Bi Salhat
mwanamke mwenye asili ya
kiarabu ambaye uzuri wake ni wa
kipekee kabisa.Mama huyu
alikuwa na mahusiano ya siri ya
kimapenzi na Mr
MeshackJumbo.Inasemekena
kwamba ni MeshackJumbo ndiye
aliyesaidia kumtorosha mama
huyu toka katikati ya mapigano nchini Syria na kumtafutia kibali
cha kuishi nchini Tanzania na
kumsaidia kupata uraia wa
Tanzania .Jumbo na Salhat wana
mtoto mmoja wa kike anaitwa
Faizat.Mahusiano haya ni ya siri
na anayefahamu siri hii ni Elvis
ambaye ndiye aliyetumiwa na
MeshackJumbo kuhakikisha
kwamba Salhat anafika salama
nchini Tanzania na hivyo
kumfanya mtu peke
anayeyafahamu kwa undani
mahusiano ya siri ya Salhat na
MeshackJumbo
Nje ya jengo ilipo saluni hii
kubwa na nzuri kulikuwa na
magari kadhaa yameegeshwa ya
wateja wakihudumiwa asubuhi
kabla ya kwenda makazini.Elvis
akashuka garini akaangaza angaza kuhakiki usalama halafu
akafungua mlango na kuingia
ndani.Wateja hawakuwa wengi
asubuhi hii na mara
akagonganisha macho na bi
Salhat ambaye alitabasamu na
kumfuata
“Karibu Elvis.Umeadimika
sana.Siku hizi unaonekana kwa
nadra”
“Nimebanwa na kazi Salhat
na ndiyo maana sifiki mara kwa
mara kuwajulieni hali lakini
nitajitahidi kukutembela kila pale
nipatapo muda.Vipi maendeleo ya
Faizat?
“Faizat anaendelea vyema”
akasema Salhat halafu
akamuuliza Elvis kwa sauti ndogo
“Elvis kuna nini
kimetokea?Mbona Meshackamekuja hapa jasho
linamvuja asubuhi asubuhi?
“Mzee Meshacktayari
amefika?
“Ndiyo amefika kitambo
kidogo anakusubiri”
“Katumia usafiri
gani?Sijaliona gari lake hapo nje”
“Hakutumia gari lake
amekuja na piki piki.Hata mimi
nimeshangaa sana kwani sijawahi
kumuona Meshack amepanda piki
piki .Kitu gani kinaendelea Elvis?
Akauliza Salhat kwa wasi wasi
“Hata mimi sifahamu nini
kimetokea hadi nitakapoonana
naye.Yuko wapi?
Bila kupoteza muda Salhat
akampeleka Elvis katika chumba
alimokuwamo MeshackJumbo Shikamoo mzee” akasema
Elvis
“Marahaba Elvis.Ahsante
sana kwa kufika kwa wakati”
akasema Meshackhuku akivua
miwani yake na kujifuta machoni
halafu akamgeukia Salhat
aliyekuwa amesimama
akimtazama
“Salhat lile gari liko tayari?
“Ndiyo liko tayari” Akajibu
Salhat.
“Elvis twende tuondoke”
akasema Meshackna
kuinuka.Salhat akawaongoza
wakapita mlango wa nyuma
wakazikuta gari tatu zimeegeshwa
“Tumieni gari hili hapa”
akasema Salhat akiwaonyesha gari
la kutumia.Elvis akachukua
funguo kwa Salhat wakaingia garini na kwa kupitia geti la
nyuma wakaondoka
“Tunaelekea wapi mzee?
Akauliza Elvis
“Samawati beach hotel”
akajibu MeshackJumbo.Elvis
akaendelea kukanyaga mafuta bila
kumsemesha chochote.Mara kwa
mara MeshackJumbo alikuwa
anageuka kutazama nyuma
akihakiki kama kuna gari lolote
linawafuata
“Relax Mr jumbo.No body is
following us” akasema Elvis.
“Are you sure?
“Yes” akajibu Elvis
Iliwachukua takribani dakika
arobaini kufika Samawati beach
hotel, moja ya hoteli tulivu iliyo
pembezoni mwa bahari ya Hindi.Walishuka garini na
kutafuta sehemu tulivu wakakaa
“Pole sana mzee” Elvis
akaanzisha maongezi.Ilimlazimu
kumpa pole MeshackJumbo
kutokana n na hali aliyokuwa
nayo.
“Ahsante sana Elvis.leo
kijasho kimenitoka.Tangu
nimeanza kuifanya kazi hii
nadhani leo ndiyo siku yangu
ngumu zaidi” akasema Meshack
“Kuna nini kimetokea
mzee?akauliza Elvis.Kabla
MeshackJumbo hajajibu ikaletwa
supu waliyoagiza,akanywa halafu
akasema
“Nilipigiwa simu jana usiku
na makamu wa rais Dr Shafi
akinitaka nifike nyumbani kwake
leo alfajiri na mapema.Sikujua ananiitia nini lakini kwa namna
alivyonipa msisitizo nilihisi kuna
suala zito analonitia” akatulia na
kunywa supu kisha akaendelea
“Nilifika nyumbani kwake
alfajiri kama alivyonitaka
tukaingia katika chumba cha
maongezi ya siri na tukaanza
maongezi.Alianza kunieleza
mambo mengi tofauti tofauti na
mwisho akanieleza kile
alichoniitia.Alisema kwamba kuna
mmoja wa vijana wangu ambaye
amenusa harufu ya jambo Fulani
na ameanza kulifuatilia.Aliweka
wazi kwamba mtu huyo ni
wewe.Ingawa alikataa kata kata
kunieleza ni jambo gani umelinusa
na unalifuatilia lakini nilijua
lazima litakuwa ni suala la ile biashara ya silaha” akanyamaza
akanywa supu na kuendelea
“Kama ulivyoniambia awali
kwamba yawezekana mtandao wa
vigogo wanaojihusisha na biashara
hii ya silaha ni mkubwa na siwezi
kushangaa kama Dr Shafi naye ni
mmoja wao.Katika maelezo yake
alisema kwamba jambo
unalolifuatilia ni zito na athari
zake ni kubwa kitaifa na kimataifa
endapo watanzania
watalifahamu.Ili kuendelea
kulinda maslahi ya vigogo
waserikali wanaojishughulisha na
biashara hizi haramu Dr Shafi na
wenzake wamefanya maamuzi”
Meshackakasita na kumtazama
Elvis usoni
“Wameamua nini mzee? Elvis
akaulizaWameamua…” akataka
kusema na kusita tena
“Nieleze mzee wameamua
nini?
“wanataja uuawe”
Elvis akatoa kicheko kidogo
na hakuonyesha kustushwa hata
kidogo na taarifa
ile.MeshackJumbo akamshangaa
“Elvis kulikoni unafurahi kwa
taarifa hizi mbaya?Hili si jambo
dogo kama unavyolichukulia
kimzaha.Ni jambo zito sana.Watu
hawa wamekwisha kuona wewe ni
hatari na kikwazo kikubwa kwa
biashara zao hivyo suluhu pekee
hapa ni kukuua.Wamekwisha
dhamiria hivyo na watafanya kila
wawezavyo kuhakikisha kwamba
wanatimiza lengo lao.Hupaswi
kuweka mzaha katika jambo nyeti kama hili.Nafahamu unaweza
kuliona ni jambo dogo kwa kuwa
unao uwezo wa kujilinda lakini
hawa jaama ni wanyama sana na
wana nguvu.Wanatumia
madaraka waliyonayo kufanikisha
mipango yao.Huwezi pambana nao
ukiwa mwenyewe lazima
watakumaliza tu” akasema
MeshackJumbo akionekana
kukerwa sana na namna Elvis
alivyolipokea suala lile
“Nimekuelewa mzee na
nimecheka kidogo kwa sababu
tayari nilikwisha fahamu jambo
kama hili lipo na linaweza kutokea
muda wowote.Nilikuwa na imani
kubwa kwamba katika biashara
hii ni kubwa na inahusisha watu
wazito na kitendo cha kuingiliwa
maslahi yao ni kujichimbiakaburi.Ninafahamu vizuri mambo
haya yanavyokwenda mzee na kile
nilichokuwa nimekifikiria tayari
kimetokea.Tayari tumefahamu
kwamba vigogo wakubwa wa
serikali nao ni wanufaika au
wanashiriki katika biashara hii na
ndiyo maana wako tayari kuondoa
kizingizi chochote kinachojitokeza
mbele yao ili biashara yao
isikwame.Hii ni vita kali mzee”
akasema Elvis
“Elvis nashukuru kama
ulilitambua hilo mapema na
ukajiandaa.Sasa tuna uhakika
mkubwa kwamba mtandao huu
unawahusisha watu wakubwa wa
serikali na makamu wa rais
akiwemo.Hatuna ushahidi wa
moja kwa moja kwamba
anahusika lakini kwa hili alilolitamka leo nina uhakika
mkubwa kwamba na yeye ni
mmoja wao.Elvis naomba
ufahamu kwamba ofisi yangu
imekuwa ikitumiwa vibaya kwa
muda mrefu makamu wa rais
ambaye idara ninayoiongoza iko
chini yake.Amekuwa akitumia
idara yangu mara kadhaa kuficha
baadhi ya maovu yanayofanywa na
viongozi wetu na kwa kwa
kutumia kigezo cha usalama wa
nchi tumewatoa kafara baadhi ya
vijana mahiri na wazalendo
walionusa harufu ya mambo
yanayofanywa na wakubwa na
kuanza kuyafuatilia.Kila maslahi
ya wakubwa yalipoguswa basi
hutolewa amri ya kumnyamazisha
mtu huyo hata kama ni tegemeo
kwa taifa na amri zote hizo hutolewa na makamu wa
rais.Ndani ya mwaka huu pekee
tayari tumekwisha wapoteza vijana
watatu mahiri na sasa wanataka
wakuondoe na wewe baada ya
kuzinasa siri za mtandao wao.Siko
tayari jambo hili liendelee”
akasema Meshackna kumalizia
supu yake
“Elvis wewe ni kijana
wangu.Nimekupokea na kukulea
katika kazi hii na ninakuchukulia
kama mwanangu kwa maana hiyo
katu sintakubali jambo kama hili
litokee kwako.Nitakulinda kwa kila
nguvu niliyonayo” akasema
Meshackhuku akigonga meza kwa
hasira.Kimya kifupi kikatanda
“Makamu wa rais aliponieleza
kuhusu suala hili nilikataa na hii siko tayari kufanya hivyo
wanavyotaka nifanye.Alijaribu
kunishawishi nikakataa
ikamlazimu kuanza kutumia
vitisho.Aliniambia kama ninakataa
itamlazimu kutafuta watu wengine
wenye uwezo wanaoweza kufanya
kazi hiyo ya kukutoa uhai.Kauli ile
ilionyesha wazi kwamba
wamedhamiria kukuua hivyo
ikanilazimu nikubaliane naye
kwamba nitatekeleza ombi lake”
akasema MeshackJumbo halafu
Elvis akauliza
“How am I going to die?
“Kwa mujibu wa mipango
waliyoipanga ni kwamba itapigwa
simu ofisini kwangu na mtu
ambaye hafahamiki na atasema
kwamba amemuona Yule mtu
ambaye tumekuwa tukimsaka kwa muda mrefu akihusishwa na
milipuko ya mabomu Arusha
ajulikanaye kama Abdullah.Mtu
huyo atasema kwamba Abdullah
anajificha katika msitu wa
Ngezi.Baada ya kupokea taarifa
hiyo nitakutuma uende huko na
tayari wao watakuwa
wamewaandaa vijana wao eneo
hilo na utakapofika
watakushambulia kwa kustukiza
na kukuua” Meshackakanyamaza
akamtazama Elvis na kusema
“I”m so scared Elvis.Sijawahi
kuogopa katika maisha yangu
kama sasa.Nimechanganyikiwa na
sijui nini cha kufanya” akasema
MeshackJumbo
“Tafadhali usiogope mzee
wangu.Najua hili ni jambo zito
lakini nashukuru kwa kuwa muwazi kwangu kuhusiana na
mpango wao wa kuniua.Mpango
huu wa kuniua unaonyesha ni
jinsi gani jambo hili tunalolifuatilia
lilivyo kubwa .Hakuna ubishi
kwamba hata makamu wa rais
naye anahusika katika mtandao
huu na ndiyo maana ametoa amri
niuawe.Tayari wamekwisha anza
kuingiwa na hofu na ndiyo maana
zinafanyika kila juhudi ili
waniondoe nisiwe kikwazo kwa
biashara yao kuendelea.Kama
makamu wa rais naye
anajihusisha na mtandao huu ni
wazi kuna mambo mengi
makubwa yanayofanywa na huu
mtandao zaidi ya biashara ya
silaha na ambayo tunapaswa
kuyafahamu.Nina uhakika
mkubwa kwamba kuna mambo mengi mazito yanayofichwa kwa
hiyo tunatakiwa kwanza
kuwafahamu wote waliomo katika
mtandao huu na pili kufahamu
mambo wanayoyafanya na mwisho
kuwafichua uovu wao”
“Elvis vita hii haitakuwa
nyepesi” akasema Meshackkwa
wasi wasi
“Nalifahamu hilo mzee
kwamba vita hii si ndogo kwani
tunapigana na watu wenye nguvu
na uwezo mkubwa ila hakuna
namna nyingine ya kufanya zaidi
ya kupambana.Mtandao huu ni
hatari mno lakini kwa namna
yoyote itakavyokuwa lazima
tupambane nao.Damu nyingi za
watu wasio na hatia inamwagika
huko Congo kwa sababu ya silaha zinazouzwa na mtandao huu.We
have to stop them!!
“Elvis narudia tena huu si
mtandao wa kufanyia
masihara.Ndani yake kuna watu
wazito.Kuna makamanda wa jeshi
na sasa tumeona hata makamu
wa rais naye anashirikiana nao na
bado hatujui nani na nani
wanahusika .Tayari wamedhamiria
kukuua and they’ll do anything to
make sure you die.Suluhisho
pekee ambalo tunaweza kulifanya
kwa sasa ni wewe kupotea.Go far
away from here.Nitashughulikia
kila kitu ili uweze
kutoweka.Usipofanya hivyo hawa
jamaa watakuua na mimi sitaki
hilo litokee” Akasema Meshack
“Mzee Jumbo nakushukuru
sana kwa kunijali na kujitolea kunisaidia kwa kiwango kikubwa
namna hii.Umekuwa nami toka
siku ya kwanza nilipoianza kazi hii
lakini naomba kwa mara ya
kwanza nitofautiane
nawe.Sintakimbia wala
kujificha.Wakati umefika wa
kupambana na mtandao huu na
kuyaanika maovu yao kwa dunia
nzima.Sijali nini kitatokea lakini
lengo langu ni kufikikisha mwisho
biashara hii haramu na uovu huu
ukome.Marais wetu wanahangaika
kila uchao kutafuta amani ya
Congo lakini amani haitapatikana
kama hawa watu wanaoendelea
kuchochea mapigano ya Congo
hawatadhibitiwa.Mzee mtandao
huu ni mkubwa na inaonekana
una wafadhili wake kutoka nje ya
nchi kwa hiyo lazima tupambane nao kwa gharama zozote.Kukimbia
si suluhu ya kulimalizia suala hili
na wala hakutaweza kuuzuia
mtandao huu na mamia ya watu
wataendelea kuteketea huko
Congo kwa silaha zinazouzwa na
akina Frank na genge lake.Mzee
lazima tupambane nao” akasema
Elvis.Mzee MeshackJumbo
akakuna kichwa chake na kusema
“Namna gani tutapambana na
watu hawa?Ni wazi nguvu yao ni
kubwa kuliko sisi.Mtandao huu
kama ulivyosema unaonekana
umeanzia huko nchi za
nje.Tutawezaje kuukata mzizi
wake?
“Tunaweza mzee.Tunaweza
kupambana nao” akasema Elvis
“Kivipi? Akauliza mzee
Meshack Kwa mimi kufa”
Mzee MeshackJumbo
akastuka na kumtazama Elvis
kana kwamba anatazama kitu cha
kutisha
“Mbona umestuka hivyo
mzee? akauliza Elvis
“I don’t understand you
Elvis.Suala hili ni zito mno lakini
wewe unaingiza mzaha”
“Hakuna mzaha mzee.Kama
ulivyosema nguvu yetu sisi ni
ndogo na hatuwezi kupambana na
mtandao huu mkubwa na hata
nikisema nikimbie watanitafuta
mahala kokote nitakakokimbilia
kwani mtandao wao ni mrefu
sana.Njia pekee ya kupambana
nao ni mimi kufa.They want to kill
so I have to die” akasema Elvis MeshackJumbo bado
aliendelea kumuangalia Elvis
usoni kwa macho ya mshangao
“Nashindwa kukuelewa
Elvis.Una maana gani
unapotamka hayo maneno?Please
Elvis these people are very
dangerous and they’ll kill you !!
akasema Meshack
“Mzee nina maana kwamba
watu hawa tayari wamekwisha
tambua kwamba nimewagundua
na jambo hili linawapa joto sana
na ndiyo maana suluhisho pekee
walilonalo kwa sasa ni
kuhakikisha kwamba wananiua ili
biashara zao ziendelee kama
kawaida bila matatizo.Baada ya
mimi kufa hawatakuwa na
wasiwasi tena kuhusu mambo yao
kuingiliwa na wataendelea na biashara zao wakiamini kikwazo
kikubwa kwao kimeondoka.Kwa
hiyo mzee lazima mimi nife.Hii
ndiyo njia pekee ya kuweza
kuufuatilia na kuufutilia mbali
mtandao huu.Najua unastuka
ninaposema kwamba lazima
nife.Hapa ninamaanisha kwamba
nitatengeneza kifo changu ili hata
hao jamaa waamini kwamba ni
kweli nimekufa.Baada ya
kushuhudia jeneza langu
limefukiwa kaburini basi lengo lao
litakuwa limetimia na wataendelea
na shughuli zao huku mimi
nikipata nafasi nzuri zaidi ya
kupambana nao” akasema Elvis
MeshackJumbo akavuta
pumzi ndefu na kusema
“Hapo sasa nimekuelewa
unachokimaanisha.Lakini suala la kutengeneza kifo lina changamoto
nyingi na linatakiwa lifanywe
kitaalamu mno vinginevyo endapo
kutafanyika hata kosa dogo basi
unaweza ukapoteza maisha
kabisa.Tunapaswa kujipanga sana
katika jambo hilo” akasema
MeshackJumbo
“Ni kweli mzee.Suala hili ni
gumu na linachangamoto zake
lakini pamoja na ugumu na
changamoto zake lakini lazima
tulifanye.Hii ndiyo njia pekee ya
kutuwezesha kupambana na hawa
jamaa.Hili suala linawezekana
kufanyika lakini tunahitaji
kuwashirkisha pia watu
kadhaa.Wa kwanza ni daktari
wetu wa idara Dr Philip
maguswa.Yeye ni mtaalamu na
mzoefu katika mambo haya.Atatupa mawazo mazuri zaidi
ya kufanikisha mpango
huu.Amepata mafunzo makubwa
nchini Ujerumani kwa hiyo ni
msaada mkubwa
kwetu.Tutawashirikisha pia watu
wa chumba cha maiti hospitali
kuu ya St Clara.Wale haitakuwa
shida kubwa kuwashawishi kwani
ni pesa tu itatumika na kila kitu
kitakwenda sawa” Akasema Elvis
na kuendelea
“Mpango wenyewe utakuwa
hivi.Utapokea simu toka kwa hao
jamaa kama alivyokuelekeza
makamu wa rais na utamwagiza
katibu wako anitaarifu nifike
ofisini haraka sana.Lengo ni
kuweka ushirikishwaji kwa watu
wengine pia wa pale ofisini.Nikifika
ofisini utanielekeza nikafanye uchunguzi kuhusiana na mtu
tunayemtafuta anayedaiwa
kujificha katika msitu wa Ngezi na
wakati unanipa maelekezo hayo
wanatakiwa wawepo vijana
wengine wawili wa idara
yetu.Lengo hapa ni kulifanya
jambo hili lisionekane kuwa
siri.Katika maelekezo yako utataka
niongozane na vijana hao lakini
mimi nitapinga na kutaka niachwe
niende mwenyewe nikafanye
uchunguzi na wewe utakubali kwa
sharti kwamba mimi nitangulie
halafu wewe na hao vijana
mtakuwa nyuma yangu ili kunipa
msaada pindi ukihitajika.Mimi
nitakwenda huko eneo la tukio na
nitafanya kile ninachotakiwa
kufanya na baada ya hapo
nitawasiliana nawe kukutaarifukwamba kila kitu tayari kisha
mtasogea eneo la tukio halafu Dr
Philip mtakayekuwa
mmeongozana naye atanichukua
na kuniingiza katika gari lake
kunikimbiza hospitali ya St.Clara
ambako kila kitu kitakuwa
kimewekwa sawa nao
watathibitisha kwamba
nimefariki.Baada ya hapo
maandalizi ya mazishi
yatafanyika.Siku ya mazishi ni
watu wachache tu
watakaoruhusiwa kuniona katika
jeneza wakiwamo viongozi
wachache wa juu na makamu wa
rais akiwemo ili athibitishe
kwamba ni kweli nimekufa.Baada
ya mazishi ndipo picha
likapoanza.unaonaje kuhusu
mpango huu? akasema Elvis MeshackJumbo akakuna
kichwa kutokana na maelezo yale
ya Elvis.Akafikiri kidogo na
kusema
“Huu ni mpango mzuri sana
na utekelezaji wake unahitaji pia
kutumia fedha nyingi.lakini suala
la fedha halitakuwa na tatizo
kwetu kwani Dr Shafi alisema
kuna kiasi kikubwa cha fedha
nitapatiwa kwa ajili ya kufanikisha
mpango huu wa kukuua.Pesa hizo
ndizo tutakazozitumia katika
kupamba nao” Akasema Meshack
“Pamoja na hayo mzee kuna
vitu vya muhimu nitavihitaji”
akasema Elvis
“Sema unavyohitaji Elvis ili
vifanyiwe kazi mara moja”
“Kuna mtu namuhitaji katika
mpango huu” Unamuhitaji nani?
“Namtaka Steven mugo.
“Unamtaka Steven Mugo?!!
MeshackJumbo akastuka sana
“Ndiyo mzee.Namuhitaji
Steven Mugo.Yule ni mzoefu
katika mambo makubwa kama
haya na zaidi ya yote ninamuamini
kuliko wote katika idara
yetu.Nahitaji mtu wa kushirikiana
naye katika jambo hili lakini
lazima awe ni mtu jasiri,mwepesi
kutekeleza mambo na kufanya
maamuzi ya haraka na Steven
Mugo ndiye hasa anayefaa
MeshackJumbo akavua
miwani yake na kuiweka mezani
akakuna kichwa
“Elvis tafadhali naomba
uchague mtu mwingine ambaye
unaona anaweza akakufaa kushirikiana naye katika mpango
huu na si Steven Mugo.Kuna
vijana wengi katika idara yetu
wanafanyakazi nzuri sana na
mahiri katika kazi.Chagua yeyote
na mimi nitakupa ila si Steven
Mugo.Yule hatuwezi kumpata
kwani unafahamu fika yuko
kizuizini kwa usalama wa
nchi.Alitoa siri za usalama wa nchi
na hili ni kosa kubwa .Tafadhali
naomba usahau kuhusu Steven
.Tafuta mtu mwingine.Huyu
hatutaweza kumpata kabisa”
akasema MeshackJumbo.Elvis
akakohoa kidogo na kusema
“Mzee namuhitaji Steven
Mugo pekee.Kuna nguvu kubwa
inatumika kushinikiza kwamba
Steve alifanya h ivyo
anavyotuhumiwa kufanya yaani kuvujisha siri za usalama wan chi
lakini ukweli ni kwamba Steven
hakufanya hivyo na hahusiki
kabisa na uvujishaji wa taarifa zile
za siri za kuwakamata na
kuwatesa majasusi wa nchi
jirani.Nimelifanyia uchunguzi
suala hili na nimebaini kwamba
Steven hahusiki hata kidogo bali
ni mpango uliosukwa na wakubwa
Fulani ili kummaliza
nguvu.Sababu kuu iliyomfanya
aangukie katika tuhuma hizi ni
sababu za kipuuzi kabisa na za
kibinafsi zaidi lakini kwa kuwa
aliingia katika anga za watu wenye
nguvu basi wameamua
kumuonyesha nguvu zao ila
ukweli ni kwamba Steve hana
hatia.Tafadhali mzee naomba
ufanye kila linalowezekana ili nimpate Steven.Nakuahidi baada
ya suala hili kumalizika mimi na
yeye tutawasilisha mezani kwako
ushahidi usio na shaka wa
kuonyesha kwamba Steven
hakuhusika na kuvujishwa kwa
taarifa za siri”
MeshackJumbo akainama na
kufikiri kwa muda akashusha
pumzi na kusema
“Elvis umeniweka katika
wakati mgumu sana lakini hata
hivyo nitaangalia namna ya
kufanya ili aweze kupatikana
lakini hakikisha kwamba hatoroki
na wala hafanyi jambo lolote
litakalomuingiza katika matatizo
makubwa.Nimeamua kujitoa
mhanga kuubeba mzigo huu kwa
kuwa ninakuamini Elvis hivyo
usiniangushe tafadhali.Mchunge sana Steven asituingize katika
matatizo mengine.Kitendo cha
mimi kumtoa tayari kitakuwa
kimeniweka matatizoni na sitaki
kuongeza matatizo zaidi kwa
wakati huu ambao tuko katika
matatizo makubwa” akasema
Meshack.
“Usihofu mzee.Steven ni
kijana mzuri na atakuwa na
msaada mkubwa kwetu .Naomba
sasa umuite DrPhilip ili afike hapa
mara moja tumueleze mpango huu
na yeye atupe mawazo yake”
akasema Elvis na MeshackJumbo
akatoa simu akampigia DrPhilip
akamtaka afike mara moja pale
hotelini
*******************
 
Back
Top Bottom