Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESDENT

Sehemu 33

Ilimlazimu Dr Philip kutumia
usafiri wa pikipiki ya kukodi
kumfikisha Samawati beach hotel
kwani mkurugenzi wake
MeshackJumbo alimtaka asitumie
gari.Alimlipa kijana wa piki piki
akaangaza pande zote kuhakiki
usalama wake halafu akaingia
hotelini akaelekea moja kwa moja
mahala alikokuwa MeshackJumbo
“Karibu sana Dr
Philip.Nashukuru umefika kwa
wakati”
“Imenilazimu kutumia
bodaboda” akajibu Philip
“good.Umefanya jambo
zuri.Una hakika hakuna
aliyekuwa anakufuatilia huko
utokako?
“Hakuna mzee.Ni salama
kabisa” akasema Dr Philip “Mzee uliniambia uko na
Elvis,mbona simuoni hapa?
Akauliza DrPhilip
Kabla MeshackJumbo
hajajibu kitu Elvis
akatokea,akasalimiana na Dr
Philip na maongezi yakaanza
“Dr Philip hatuna muda
mwingi mahala hapa kutokana na
jukumu kubwa lililoko mbele yetu”
akasema Meshackakanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Sina shaka nawe hata kidogo
Dr Philip na ndiyo maana
nimekuita hapa kukushirikisha
jambo kubwa .Nina imani
utakuwa ni msaada mkubwa
kwetu kwani jambo
ninalotakakukushirikisha ni la siri
kati yetu sisi tuliopo hapa”
akanyamaza tena na kumtazama Philip ambaye alitikisa kichwa
kukubaliana na kile alichokisema
Mechack Jumbo.
“Alfajiri ya leo nimeitwa na
makamu wa rais nyumbani
kwake.Jambo aliloniitia ni zito na
la kustusha.Kuna mtandao wa
watu unaofanya biashara haramu
na ndani ya mtandao huo wamo
vigogo wa serikali na baadhi ya
wafanya biashara wakubwa.Elvis
amegundua biashara
wanazozifanya na baada ya
kugundua kwamba wamekwisha
fahamika wanataka wamuue Elvis
kwani tayari amekuwa kikwazo
kwao”
Dr Philip akapatwa na
mstuko mkubwa.Kimya cha
sekunde kadhaa kikapita. Mzee umenistua sana kwa
hiki ulichokisema .Ninaomba
unifafanulie kidogo nilifahamu
jambo hilikwa kina” akasema
DrPhilip
“Ni hivi” akasema Elvis
“Katika siku za karibuni
nimefanikiwa kugundua
kuhusiana na mtandao unaofanya
biashara ya kuwauzia silaha wasi
wanaopambana na serikali ya
Congo.Mtandao huo
unawahusisha watu waliomo
ndani ya serikali hapa Tanzania
na ndaniya serikali ya
Congo.Silaha hizo huagizwa nje ya
nchi na kupita katika bandari yetu
halafu huishia mikononi mwa
waasi wanaopigana na serikali ya
Congo ambao huzinunua kwa pesa
nyingi na wakati mwingine kubadilishana na
madini.Uchunguzi wa mtandao
huu na hii biashara bado
unaendelea lakini wakati
uchunguzi ukiendelea hawa jamaa
wamegundua kwamba
wamefahamika na suluhisho
pekee walilonalo ni kuniua ili
wawe salama.Leo alfajiri
mkurugenzi ameitwa na makamu
wa rais nyumbani kwake na
akapewa maagizo ya kuhakikisha
ninauawa siku ya leo” akasema
Elvis.
“Sijawahi kupata taarifa
mbaya na ya kustusha kama hii
toka nimeanza kazi.Wanataka
kumuua Elvis?!! Akasema kwa
mshangao Dr Philip.
“Najua umestuka sana Dr
Philip lakini naomba nikutoe wasiwasi kamba lengo lao haliwezi
katu kufanikiwa.Nilipoanza
kulichunguza jambo hili
nilitegemea kitu kama hiki
kingeweza kutokea kwa hiyo
nilikwisha jiandaa kisaikolojia.Hizi
ni changamoto tunazokumbana
nazo katika hizi kazi zetu”
akasema Elvis.
“Elvis mimi kwa mara ya
kwanza nimekasirishwa mno na
hiki kitendo kinachotaka
kufanywa na hawa
vigogo.Sikutegemea kama watu
hawa wanaweza kufikia maamuzi
makubwa namna hii ya kutaka
kukuua mtu kama wewe.Elvis
hawa watu kama dhamira yao ni
kutaka kukuua basi hawatalala
usingizi hadi wahakikishe mpango
wao umetimia.Elvis you have to run.Go far away from here”
akasema Dr Philip
Elvis akatabasamu kidogo na
kusema
“Ahsante kwa ushauri
DrPhilip na hata mkurugenzi
alinieleza hivyo kwamba nikimbie
lakini mimi siwezi
kukimbia.Lazima nipambane
nao.Nimekwisha gundua biashara
yao haramu lazima niifikishe
mwisho.Nitapambana nao hadi
dakika ya mwisho.Kukimbia si
suluhu kwani hata huko
nitakakokimbilia wanaweza
wakanisaka na kunipata
wakaniua”
“Elvis mtandao huu ni
mkubwa na una watu wenye
nguvu kubwa.Kama maelekezo ya
kukuua yametoka kwa makamu wa rais ni wazi mtandao huu ni
mkubwa na unaweza kufanya
jambo lolote walitakalo kwa wakati
wowote.You have to run brother”
akasema Dr Philip
“Dr Philip nataka lengo lao
litimie”
“Lengo gani? Akauliza
DrPhilip
“Wanataka kuniua basi
lazima nife ili wawe na amani na
waendelee na biashara zao kama
kawaida” akasema Elvis na kuzidi
kumchanganya Dr Philip
“Nashindwa kukuelewa
Elvis.Watu hawa wanataka
kukuua na wewe bila wasi wasi
unakubali wakuue?Kifo chako
kitakuwa na msaada gani kwa
watu wasio na hati wanaoendelea
kuteseka huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo? Tafadhali
lifikirie upya hili suala na
usilifanyie mzaha!!akasema Dr
Philip
“Hakuna mzaha katika hili
DrPhilip .Kutokana na umuhimu
wake ndiyo maana nimekuita hapa
ili kwa pamoja tujadiliane namna
nitakavyokufa .Ninataka
nitengeneze kifo changu ili watu
hawa wanaoniwinda wawe na
amani na wendelee na shughuli
zao.Nataka wawe na uhakika
kwamba sipo tena duniani na hiyo
itakuwa ni fursa kwangu ya
kuwachuguza vizuri na
kuufahamu mtandao wao wote”
Dr Philip akatikisa kichwa na
kusema
“Kidogo sasa ninaanza
kukuelewa Elvis unachomaanisha.Tayari nilikwisha
taharuki kusikia kwamba unataka
kufa” akasema Dr Philip
“Ahsante kwa kunielewa Dr
Philip.Ni kweli kifo changu
kitakuwa cha kutengeneza lakini
chenye uhalisia mkubwa.Mpango
wenyewe umekaa hivi.Mkurugenzi
atapigiwa simu na mtu ambaye
atajitambulisha kwamba anatoka
katika chombo cha usalama na
atampa habari kwamba mtu
anayetafutwa sana na serikali kwa
kuratibu mashambulio mawili ya
mabomu jijini Arusha Abdullah
Abdullah ameonekana katika
msitu wa Ngezi.Baada ya kuipokea
taarifa hiyo mkurugenzi atanituma
mimi niende huko Ngezi kufanya
uchunguzi wa taarifa hizo ambako
tayari kuna watu watakuwa wamewekwa ili wanimalize pindi
tu nikitokea” akasema Elvis.
“Huo ni mpango walioupanga
wao ili wanimalize.Sisi mpango
wetu ni huu.Akishapokea simu
hiyo toka kwa hao jamaa
,mkurugenzi atanituma katika
msitu wa Ngezi.Mkurugenzi
akiambatana nawe mtanifuata
kwa nyuma.Katika eneo
nitakaloelekezwa atakuwepo
Steven Mugo yeye ndiye
nitakayeshirikiana naye katika
operesheni hii.Mimi na Steve
tutapambana na hao jamaa
watakaokuwa wamewekwa hapo
kunimaliza na kisha nitawataarifu
wewe na mkurugenzi mtafika pale
mara moja na wewe kama daktari
wa idara utathibitisha kwamba
nimekufa na kisha nitapelekwakatika hospitali ya St Clara
ambako watathibitisha pia
kwamba nimekufa.Katika hatua
hiyo wewe ndiye utakayechukua
nafasi kubwa kwani itahusisha
sana utaalamu wa hali ya juu na
ndiyo maana tumekuita hapa ili
kwa pamoja tujadili namna ya
kufanya kuufanikisha mpango
huu” akasema Elvis.
Dr Philip akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Nimeusikia mpango Elvis ni
mzuri lakini unahitajika utaalamu
mkubwa sana na endapo kutaokea
kosa hata dogo tu basi tunaweza
tukakupoteza moja kwa
moja.Naomba niwatoe wasiwasi
kwamba jambo hili linawezekana
kabisa kukafanyika na kwa
upande wangu ninaweza kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu
kuufanikisha.Kuna dawa inaitwa
Mephotexis II ambayo hutumiwa
na majasusi.Hii ni dawa ambayo
inampoteza mtu fahamu kwa
muda mrefu na mtu yeyote
akimuona mtu aliyepotezwa
fahamu kwa dawa hii atahisi
amekufa.Dawa hii ni hatari na
endapo ikikosewa hata kidogo
ikazidishwa basi hautaamka
tena.Baada ya tukio la msituni
kumalizika nitakuchoma dawa
hiyo na utaonekana kama
mfu.Mimi ndiye daktari wa idara
nikishathibitisha kwamba
umekufa hakuna atakayehoji
tena.Mkurugenzi atatoa taarifa
rasmikwamba umekufa.Baada ya
hapo umechagua hosptali ya St
Clara lakini napendekezatusiitumie hospitali ile kwani kuna
watu wa dini pale na inaweza
kuwa vigumu kuwashawishi
wakubali kujiunga nasi katika
mpango wetu.Nashauri tutumie
hospitali ya Rajesh Memorial
hospital.Mmiliki sa hospitali ile Dr
Rajesh ni rafiki yangu na nina
uhakika lazima watakubaliana
nami kirahisi.Tutakupeleka pale
nao pia watatoa ripoti yao
kuthibitisha kwamba ni kweli
umekufa.Baada ya hapo
nitakuzindua na kukutibu jeraha
utakalokuwa umelipata la risasi
kisha utaenda mapumzikoni
ukisubiri siku ya mazishi”
Dr Philip akanyamaza
akamtazama Elvis na mzee
Meshackkisha akasemaHakuna yeyote
atakayeruhusiwa kukuona katika
chumba cha maiti hadi siku ya
mazishi ambayo napendekeza
yafanyike haraka kesho
kutwa.Kitakachofanyika siku ya
mazishi ni kwamba katika jeneza
utakamowekwa kutafungwa kifaa
maalum cha kukusaidia
kupumia.Mirija miwili midogo
itatoka katika kifaa hicho na
kuingia mdomoni mwako.Hii ni
kwa ajili ya kuingiza hewa safi
mwilini.Hakuna atakayeweza
kuiona mirija hii kwani itakuwa
imefunikwa na bendeji
itakayofungwa kuanzia puani hadi
shingoni kwa kisingizio kwamba
sehemu hiyo imeharibiwa kwa
risasi.Kaburi utakamozikwa
litajengwa kitaalamu sana ili kuruhusu hewa kuingia
ndani.Kwa kigezo kwamba
umeumia vibaya sana kwa risasi
mwili wakohautaonyeshwa
hadharani isipokuwa kwa watu
wachache sana wa karibu
wakiwemo viongozi ili upatikane
ushahidi kwamba ni kweli
umekufa.Shughuli za mazishi
itabidi zichelewe kidogo ili hadi
tutakapofika makaburini kijua
kiwe kinazama.Kwa kuwa muda
utakuwa umekwenda shughuli
zitafanyika haraka haraka hapo
makaburini na watu wataombwa
kurejea majumbani na kuwaacha
mafundi wakilifunika
kaburi.Baada ya watu kuondoka
mafundi hao nao wataondolewa
kwa kigezo cha kufanya mambo ya
kiusalama na hapo ndipo Stevenatakapoingia na gari lenye jeneza
lingine na tutalibadilisha jeneza
kisha kaburi litafunikwa na picha
itaishia hapo”
Kimya kikatawala.Baada ya
muda Elvis akasema
“Una mpango mzuri sana Dr
Philip.Ahsante kwa mchanganuo
huo mzuri.Binafsi ninakubaliana
na mpango huo japo kuna baadhi
ya vitu tutaviongeza ili kuuweka
mpango huu vizuri zaidi”
“hata mimi sikutegemea kama
Dr Philip unaweza kuwa mwepesi
wa kufikiri namna hii.Nimeupenda
mpango huu.Natumai kama
ukienda vizuri basi lengo letu
litafanikiwa” akasema mzee
MeshackJumbo
Majadiliano marefu
kuhusiana na mpango ule yaliendelea na hatimaye
wakatawanyika ili kwenda kuanza
maandalizi.Dr Philip akaelekea
Rajesh memorial hospital kuonana
na Dr Rajesh ,mzee
MeshackJumbo na Elvis
wakaelekea katika nyumba
alikofungwa Steven Mugo.
******************
“Sasa nayakumbuka maneno
ya Patricia ambayo amekuwa
akiniambia mara kwa mara
kwamba katika kazi zote za dunia
hii kwa nini niliamua kufanya kazi
hii?Ninaipenda sana kazi hii lakini
kwa sasa ninaanza kuyaonja
machungu yake.Ni kazi iliyojaa
hatari kila kukicha.Wanataka
kuniua.Nitakufa kama wanavyotaka lakini hawajui kama
nitarejea kama mzimu na
kuwawinda usiku na
mchana.Hawatapata usingizi na
mwisho wa yote nitahakikisha
mtandao wao wote
unasambaratishwa.Sintafumba
jicho hadi pale nitakapohakikisha
mtu wa mwisho katika mtandao
huu ametiwa nguvuni.Siwezi
kukimbia na kwenda kujificha
mbali wakati ndugu zetu wa
Congo wakiangamia kwa silaha
zinazouzwa na genge hili la
maharamia.Lazima nipambane
nao hadi mwisho” akawaza Elvis
na kumkumbuka Patricia akahisi
kuumia moyoni
“Masikini Patricia mke wangu
sipati picha atakuwa katika hali
gani pindi akipata taarifa za kifo changu.Pamoja na yote yaliyotokea
katika ndoa yetu lakini kuna kitu
kimoja tu ninachokiamini,Patricia
ananipenda mno na atakapopata
taarifa za mimi kufariki maisha
yake hayatakuwa sawa tena.She”ll
never be the same ! nifanye nini
sasa? Akajiuliza Elvis wakiwa
garini
“Jambo hili la kifo changu
litawaumiza watu wengi sana hasa
mke wangu kipenzi na mama
yangu,pia ndugu zangu,lakini sina
namna nyingine ya kufanya zaidi
ya kutengeneza kifo changu ili
niweze kuumaliza mtandao huu
hatari.Hata nikiamua nikimbie
bado maisha yangu hayatakuwa
na amani na nitakimbia hadi
lini?Kitu pekee hapa ni kutulia na
kupambana.Nisipofanya hivi maisha ya watu wengi yataendelea
kupotea .Hawana mwingine wa
kuwaokoa zaidi yangu” akawaza
Elvis
“Nina imani Patricia
atanielewa nitakapokuja
kumueleza dhumuni la kufanya
hivi.Japokuwa itakuwa na ugumu
kuelewa lakini nitajitahidi hadi
aelewe kwamba nilifanya hivi kwa
ajili ya kuwaokoa mamia ya watu
wasio na hatia wanaopoteza
maisha katika nchi jirani ya
Congo” Akaendelea kuwaza Elvis
“Najaribu kutengeneza picha
namna Patricia
atakavyoumia.Sikutegemea kama
itatokea siku nitamuumiza
Patricia kiasi hiki.Naomba Mungu
aniwezeshe nimalize kazi hii
salama na baada ya kazi hii sitaki tena kuendelea nayo.Nataka
nitulie na mke wangu nimfute
machozi na kumrejesha katika
hali yake ya kawaida.Nataka kuwa
huru niishi maisha yenye furaha
na mke wangu Patricia” Elvis
akaendelea kuumiza kichwa kwa
mawazo.Muda wote toka
wametoka Samawati hoteli mzee
MeshackJumbo amekuwa kimya
na hakuongea lolote.Alionekana
kusongwa na mawazo mengi.Elvis
aliligundua hilo akageuza shingo
na kumtazama mzee
Meshackaliyekuwa ameinamisha
kichwa
“Mzee !! akaita Elvis na
kumstua MeshackJumbo toka
mawazoni Usiwaze sana mzee haya mni
mambo ya kawaida katika kazi
zetu” akasema Elvis
“Ndiyo Elvis ni mambo ya
kawaida lakini nashindwa kujizuia
kuwaza kwa sababu jambo
tunalokwenda kulifanya ni kubwa
na la hatari sana.Endapo
tutakosea kidogo tu basi
tutapelekea mauti yako jambo
ambalo sitaki litokee”
Elvis akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Ni kweli mzee.Jambo hili ni
la hatari sana na kosa dogo tu
basi nitakwenda moja kwa moja
lakini kitu kimoja kinachonipa
matumaini ni kwamba namuamini
sana Dr Philip.Nina imani
atasimamia zoezi hili na litakuwa
na mfanikio” Hata mimi namuamini sana
Dr Philip lakini kuna makosa ya
kibinadamu yanaweza yakatokea
na kusababisha maafa.Sitaki
jambo lolote likutokee Elvis na
ndiyo maana nathubutu kusema
kwamba mpango huu ni mzuri
lakini moyo wangu hauna amani
kabisa .Vipi kuhusu
mkeo?Utamuacha katika hali
gani?Ni vipi endapo atagundua
kwamba ulimdanganya kuhusu
kifo chako?Ndugu zako je
watakuchukuliaje pindi
wakikuona ukiwa hai hali
walihakikisha kwamba umefariki
dunia na wakakuzika kaburini?
Elvis haya ni maswali ambayo
nimekuwa najiuliza kuhusiana na
mpango huu tunaotaka
kuufanya.Mimi bado nakushauri Elvis kama inawezekana
ukubaliane na mpango wangu wa
kuondoka kwenda mbali wewe na
mkeo na nitawasaidia kwa kila
kitu ili muweze kuyaanza upya
maisha yenu huko mbali na
uachane kabisa na kazi
hizi.Ninakupenda sana kijana
wangu na ndiyo maana
ninakuomba ufanye hivi” akasema
mzee MeshackJumbo
“Mzee ondoa hofu.Nilikwisha
sema kwamba siwezi kukimbia
kabisa na wala kukimbia si
suluhu ya matatizo haya.Nitabaki
hapa na tutaendelea na mipango
yetu kama
tulivyoipanga.Nitapambana na
hawa watu na kama ikitokea
nikafariki basi nitakuwa nimekufa
kishujaa kwa kutetea damu zawananchi wanyonge wa Congo
wasiendele kuuawa.Kuhusu mke
na ndugu zangu ni kweli
wataumia na hata mimi ninaumia
sana moyoni kila nikivuta picha
namna mke wangu Patricia
atakavyoumia lakini hakuna
namna nyingine ya kufanya
kuwasaidia ndugu zetu wa Congo
zaidi ya kufa.Ninaamini zoezi hili
likikamilika basi nitamuelewesha
na atanielewa tu lakini kuna
jambo moja nataka nikufahamishe
mzee wangu” akasema Elvis
“Jambo gani?
“Baada ya operesheni hii
kumalizika na wote tukawa
salama hii itakuwa ndiyo kazi
yangu ya mwisho.Nataka
kuachana na kazi hii na kuanza
maisha mapya” Elvis kazi hii huwezi
kuiacha.Ni kama vile ukipakwa
mafuta ya kichungaji huwezi
kuacha uchungaji utaendelea hadi
kifo chako.Kwa hiyo sahau kabisa
kuhusu kuacha kazi
hii.Tunakutegemea sana na hata
taifa bado linakuhitaji hivyo ni
mapema sana kuanza kufikiria
kuacha kazi hii” akasema mzee
Jumbo
“Mzee msimamo wangu ndio
huo kwamba hii ni kazi yangu ya
mwisho .Nimefanya maamuzi haya
kwa ajili ya mke wangu Patricia
ambaye ameteseka kwa muda
mrefu kutokana na kazi
hii.Nimekosa muda wa kutosha wa
kuwa naye.Naomba unielewe mzee
wangu” akasema Elvis.mzee Jumbo akafikiri kwa muda na
kusema
“Sawa tutaangalia lakini sijui
kama itawezekana” akasema
Jumbo na kumuelekeza Elvis njia
ya kupita kuelekea mahala
alikofungwa Steven Mugo.Ni watu
wachache tu aliokuwa
wakifahamu mahala aliko
Steven,hata Elvis mwenyewe
hakuwa akipafahamu
Waliwasili katika nyumba
iliyozungushwa ukuta mrefu
wenye rangi nyeupe.Kuuzunguka
ukuta ule kulipandwa nyasi nzuri
za kupendeza .Elvis akasimamisha
gari katika geti kubwa
jeusi.MeshackJumbo akashuka
garini na kwenda katika nguzo
moja ya geti ambako kulikuwa na
kifaa Fulani mithili ya mita ya umeme wa luku akabonyeza
namba kadhaa halafu ukatoka
mwanga na kummulika
usoni.Baada ya muda geti likaanza
kujifungua na toka ndani
akaonekana mtu mmoja aliyekuwa
amevaa suti
nyeusi.Meshackakamfanyia ishara
Elvis aingize gari ndani.Mzee
Jumbo akasalimiana na yule
jamaa aliyekuwa ndani Elvis
akashuka garini na kuwafuata
“Elvis kutana na Meja Adolf
kutoka jeshi la polisi .Yeye ndiye
anayesimamia ulinzi wa nyumba
hii” Akatambulisha Mzee Jumbo
kisha akamgeukia Adolf
“Meja Adolf kutana na
Elvis,yuko katika ofisi yangu”
Meja Adolf akatabasamu Oh,kumbe wewe ndiye
Elvis.Nimekusikia mara kwa mara
lakini sikuwahi kupata bahati ya
kukutana nawe ana kwa
ana.Karibu sana Elvis” akasema
Meja Adolf.Mzee Jumbo
akamuomba Elvis waongozane
kuelekea ndani
“Nadhani ni mara yako ya
kwanza kufika hapa Elvis”
akasema mzee Meshackwakipiga
hatua kuelekea ndani zaidi
“Ndiyo mzee ni mara yangu ya
kwanza.Sijawahi kufika mahala
hapa”
“Hapa ni mahala pa siri
ambako huwa tunawahifadhi watu
mbali mbali kwa mfano rais wa
Burundi aliyepinduliwa na
kukimbilia Tanzania aliishi hapa
,baadhi ya viongozi wengine wandani na nje pia wamewahi kuishi
hapa.Kwa sasa Steven Mugo pekee
ndiye anayeishi humu ndani akiwa
chini ya uangalizi maalum wakati
uchunguzi wa suala lake
unaendelea” akasema mzee Jumbo
huku akiufungua mlango wa
chumba kimojawapo na kuingia
katika sebule nzuri.Jumbo
akamuomba Elvis amsubiri pale
sebuleni halafu akaelekea katika
chumba anakolala Steven Mugo
akabisha hodi mara tatu na sauti
toka ndani ya chumba kile
ikamruhusu aingie ndani.Taratibu
akakinyonga kitasa na kuingia
ndani.Steven Mugo alikuwa
amejilaza kitandani huku akivuta
sigara.Alipomuona MeshackJumbo
akachukua gazeti na kuanza
kusoma.Hakutaka kumtazama usoni.Mzee Jumbo akaketi katika
sofa lilokuwamo mle chumbani
akavuta pumzi ndefu na kusema
“Habari yako Steven”
Steven hakujibu kitu
akaendelea kusoma gazeti lake
“ Najua hukutegemea kama
ningekuja kukuona muda huu na
ninafahamu kwamba hautaki
kabisa kuiona sura yangu
hapa.Ninafahamu mimi nawe
hatutazamani usoni hasa
kutokana na jambo lililotokea
lakini kilichonileta hapa si
kulionelea suala hilo ila kuna mtu
nimemleta anahitaji kukuona”
Steven Mugo akaliweka chini
gazeti lake na kumtazama mzee
Jumbo
“Mgeni gani? Kwa mara ya kwanza baada
ya karibu mwaka mmoja na nusu
toka amefungwa katika nyumba
hii Steven akamsemesha Jumbo
“Ni mtu ambaye hukutegemea
kabisa kumuona.Uko tayari
kuonana naye?
Steven Mugo akafikiri kwa
muda na kusema
“sawa,mlete nionane naye”
MeshackJumbo akatoka kwa
haraka na kumfuata Elvis
“Steven amekubali kuonana
nawe.Nafasi ni yako Elvis ongea
naye na tafadhali mshawishi
akubali kujiunga nawe” akasema
MeshackJumbo.Elvis akainuka na
kuingia katika chumba alimo
Steven.
Kwa sekunde kadhaa Elvis na
Steve walikuwa wanatazamana.Kila mmoja
alikuwa anamshangaa
mwenzake.Steven akainuka pale
kitandani alipokuwa amekaa na
kumfuata Elvis wakakumbatiana
kwa furaha
“Elvis ! akasema Steven kwa
mshangao
“Siamini kama hisia zngu
zilikuwa za kweli.Nilijua tu lazima
siku moja utakuja.Niliwahi kuota
kwamba wewe ndiye utakayekuwa
mkombozi wangu na leo ndoto ile
niliyoota imetimia na Elvis umetia
mguu wako hapa .karibu sana”
akasema Steven na kumkaribisha
Elvis katika sofa lililokuwamo mle
chumbani kisha akaenda sebuleni
na kurejea na chupa kubwa ya
mvinyo na glasi mbili akamimina mvinyo katika glasi zile na
kumpatia moja Elvis
“Pole sana Steven” akasema
Elvis
“Ahsante Elvis.Nashukuru
umekuja kuniona na ujio wako
huu ninaamini utakuwa na neema
kubwa kwangu.Elvis nimekuwa
nikiishi katika jumba hili kwa
miaka kadhaa sasa na hakuna
mtu aliyewahi kuja kunitazama
zaidi ya huyu mzee wenu na
walinzi wa hapa
wanaonilinda.Japo ninapata kila
ninachokihitaji lakini ni mateso
makubwa kuwamo ndani ya
jumba hili” akasema Steven.
“Pole Steven.Mambo haya
yatakwisha tu usihofu” akasema
Elvis Elvis ninateseka bila
kosa.Nina hakika unazifahamu
tuhuma ninazokabiliana nazo
lakini naomba nikuweke wazi
kwamba sikufanya hicho
ninachotuhumiwa kukifanya.Sina
kosa lolote nimefungwa hapa
bure.Please Elvis help me
brother.Bila wewe kunisaidia
nitafia ndani ya jumba hili
.Nadhani kuna watu wanataka
kuniangamiza bila kosa lolote.Do
you believe me Elvis?” akauliza
Steven.Uso wake ulionyesha
huruma.
“I do believe you Steven and
I”m here to help you .I”m here to
take you out of here” akasema
Elvis. Steven akashindwa kujizuia
kwa furaha aliyoipata akainuka na
kumpa mkono Elvis
“Ahsante Elvis kwa kuja
kunitoa kifungoni.Nimeteseka
mno.Tafadhali naomba usiniache
humu ndani leo” akasema Steven
kwa furaha
Elvis akamueleza Steven kila
kitu kuhusiana na kinachoendelea
baina yake na mtandao wa akina
Frank.Steven akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Dah,hawa watu nina hasira
nao sana.Usijali Elvis mimi niko
pamoja nawe na nitafanya kila
niwezalo ili mpango huu
ufanikiwe.Nina hasira sana na
hawa viongozi wenye kutumia
madaraka yao kukandamiza
wanyonge.I swear this time I’m going to show them who I real am”
akasema Steven kwa hasira
“Ahsante Steven kwa
kukubali kujiunga nami.Nina
imani kubwa nawe na nina
uhakika vita hii
tutashinda.Naomba unipe dakika
mbili nizungumze na mkurugenzi”
akasema Elvis na kutoka
akaelekea sebuleni alikokuwapo
MeshackJumbo
“Vipi mambo yamekwendaje?
Akauliza Mzee Jumbo
“mambo mazuri mzee.Steven
amekubali kushirikiana nami”
“Good” akasema mzee Jumbo
halafu akamtazama Elvis kwa
makini na kusema
“Elvis kabla hatujatoka hapa
una uhakika na hiki unachotaka
kukifanya kuhusu kumtumia Steven katika operesheni hii?
Akauliza.Elvis akatabasamu
kidogo na kusema
“Ndiyo mzee nina uhakika na
ninachotaka
kukifanya.Ninamfahamu vyema
Steven Mugo na ndiyo maana
nikamchagua yeye ashirikiane
nami.Ondoa hofu mzee kila kitu
kitakwenda vizuri”
“Nashukuru kusikia hivyo
kwani siku zote ninayaamini
maneno yako lakini mambo
yakienda vinginevyo tutakuwa
tumejiingiza katika hatari kubwa
sana.Tafadhali naomba usimuache
Steven afanye jambo lolote la
kijinga na kutuletea matatizo sisi
tuliomtoa humu hasa mimi”
akasema Mzee Jumbo. “mzee naomba usihofu
chochote.Tafadhali niamini”
akasema Elvis
“Nakuamini Elvis” akasema
mzee Jumbo kisha akaongozana
na Elvis wakaingia chumbani kwa
Steven
“Steven mkurugenzi ana
jambo anataka kukueleza”
akasema Elvis na Steven
akamtazama mzee Jumbo kwa
jicho la chuki .Mzee Jumbo
akakohoa kidogo na kusema
“Steve nadhani Elvis
amekwisha kuelekeza kila kitu
kinachoendelea na kwa nini
tumekuja hapa hapa kwa hiyo
sitaki kupoteza muda kwa
kuyarudia yale uliyokwisha
elezwa.Ni kutokana na suala hilo
alilokueleza Elvis nimeamuakufanya maamuzi magumu sana
ya kukutoa humu ndani.Naomba
ufahamu kwamba maamuzi haya
niliyoyafanya yataniletea matatizo
makubwa lakini kutokana na uzito
wa jambo tunalokwenda kulifanya
na baada ya kuhakikishiwa na
Elvis kwamba wewe ndiye pekee
anayekuhitaji katika operesheni
hii nimelamika kukutoa humu
ndani.Ninachokuomba ni kwamba
tafadhali usifanye jambo lingine
lolote tofauti na kile
atakachokuelekeza Elvis.Vile vile
naomba usijaribu wala kufikiria
kutoroka kwani kwa………………”
“Usihofu mzee” Steven
akamkatisha mzee Jumbo
“Siwezi kutoroka .Kama
ningetaka kutoroka ningekwisha
ondoka kitambo sana lakini ninaziheshimu mamlaka
zilizoniweka humu ndani na ndiyo
maana mpaka leo hii niko humu
ndani.Siwezi kutoroka kwa sababu
sikuwahi kufanya kosa lolote la
kunifanya nikimbie.Nitaendelea
kuipigania haki yangu hadi pale
nitakapoipata .Kama hakuna
kingine cha kuniambia tunaweza
kuondoka? Akauliza Steven.Elvis
na MeshackJumbo wakatazama
“Elvis mnaweza kwenda mimi
nitabaki hapa kuna mambo
nataka kuyaweka sawa.Usijali
kuhusu usafiri nitatumia gari la
Meja Adolf.Nenda kajiandae kwani
muda wowote toka sasa shughuli
itaanza” akasema kwa sauti ya
chini mzee Jumbo.Elvis na Steven
wakatoka na kuingia katika gari wakaondoka kurejea kwa Salhat
alikoliacha gari lake.
“Namchukia sana Yule
mzee.Kwa zaidi ya mwaka sasa leo
hii ameweza kusikia sauti
yangu.laiti angekuja peke yake
ningeweza hata kumfumua
magumi.yeye ni sababu ya mimi
kuteseka namna hii.Anafahamu
kabisa kwamba sina kosa lolote
lakini ameshindwa kunitetea”
akasema Steven
“Usijali Steven mambo haya
yatakwisha tu.Ninakuahidi baada
ya mambo haya kumalizika basi
tutaanza kulishughulikia suala
lako na utasafishwa dhidi ya
tuhuma zinazokukabili.Mpaka
hapa hesabu tayari suala lako
limekwisha” Sijui nikushukuruje Elvis
kwa kuja kunisaidia .Bila wewe
ningefia katika ile nyumba.Hata
hivyo sitaki tena kuendelea na hii
kazi.Nafikiria kuanza shughuli
nyingine .Nitafungua biashara na
nitaishi maisha mazuri tu”
akasema Steven
“Wazo lako ni sawa na
langu.Mimi ninaipenda kazi hii
lakini nitaachana nayo kwa ajili ya
kuwa karibu na Patricia”
“Oh ,anaendeleaje mkeo?
Tayari mmekwisha pata mtoto?
Akauliza Steven na Elvis akahisi
kama kuna kitu kimemgonga
kichwani.
“ Bado hatujapata mtoto”
akajibu
“mnasubiri nini Elvis?
Unataka ufe bila kuacha ukumbusho duniani? Nyie
mliobahatika kuoa mnatakiwa
kuwa na watoto kwa sababu hizi
kazi zetu hazitabiriki muda
wowote unaweza poteza maisha”
akasema Steven
“Ni kweli hayo uyasemayo na
ndiyo maana nimefanya maamuzi
kwamba hii ni kazi yangu ya
mwisho ili nipate muda mzuri wa
kuwa na mke wangu.Yeye ndiye
kila kitu kwangu.Nitaacha kila
kitu nikipendacho kwa sababu
yake” akasema Elvis
“Patricia anafaa kujivunia
sana kuwa na mwanaume
anayempenda kama wewe.Toka
nimekufahamu ukiwa na Patricia
sijawahi kukuona ukiwa na
mwanamke mwingine wa pembeni
au hata kusikia sifa zako mbaya.Hata mkeo ni mwanamke
mtulivu sana.Mna bahati ninyi
kukutana.Uamuzi unaotaka
kuuchukua Elvis ni uamuzi sahihi
na mimi nitakusaidia
tutapambana hadi tuhakikishe
kwamba tunawafyeka hawa wote
wanaosababisha maisha ya ndugu
zetu huko Cogo yanapotea kila
uchao huku wao matumbo yao
yakishiba kwa mauzo ya silaha
wanazowauzia waasi”
“Mimi na Patricia tuna
historia ndefu na ndiyo maana
ninasema niko tayari kuacha kila
kitu nikipendacho kwa ajili yake”
akasema Elvis na mara
akakumbuka mambo
alioyoyafanya na Doreen na
akakumbuka namna alivyomkuta
Patricia akitoka hotelini akiwambaya.Hata mkeo ni mwanamke
mtulivu sana.Mna bahati ninyi
kukutana.Uamuzi unaotaka
kuuchukua Elvis ni uamuzi sahihi
na mimi nitakusaidia
tutapambana hadi tuhakikishe
kwamba tunawafyeka hawa wote
wanaosababisha maisha ya ndugu
zetu huko Cogo yanapotea kila
uchao huku wao matumbo yao
yakishiba kwa mauzo ya silaha
wanazowauzia waasi”
“Mimi na Patricia tuna
historia ndefu na ndiyo maana
ninasema niko tayari kuacha kila
kitu nikipendacho kwa ajili yake”
akasema Elvis na mara
akakumbuka mambo
alioyoyafanya na Doreen na
akakumbuka namna alivyomkuta
Patricia akitoka hotelini akiwatu na ilikuwa ni bahati
mbaya.Sikuwa nimedhamiria
kufanya kitu kama kile japokuwa
Doreen amekuwa akihitaji sana
kufanya mapenzi nami toka
alipopewa ruhusa hiyo na Patricia
kwa kusudi la kuzaa mtoto na
mimi.Sijui nilikuwa nawaza wapi
hadi nikajikuta nikinasa katika
mtego wa Doreen.Ni vipi kama
akija leo na kunieleza kwamba ana
mimba yangu?Nitakataaje wakati
nimefanya naye mapenzi? ”
akawaza Elvis
 
Kiukweli na kwa dhati binafsi nasema hii kazi ni nzuri yenye msisimko wa kipekee Hongera sana kulubule
 
I DIEDTO SAVE PRESDANT

Sehemu 34

Mlio wa gari ulimfanya
Doreen ainuke kitandani na
kuchugulia nje kupitia
dirishani.Uso wake ukapambwa
na tabasamu baada ya kuliona
gari alilokuwa akiendesha Elvis
likiingia mle ndani.Haraka haraka
akajifunga taulo na kutoka
kwenda kumlaki Elvis.Mambo
aliyoyafanya na Elvis usiku
uliopita yalikwisha mchanganya
na alikuwa anamuwaza kila
dakika.
Mara tu alipofungua mlango
alistuka baada ya kumkuta Elvis
akiwa na mtu mwingine.Elvis
akautambua mstuko ule wa Doreen akatabasamu na kufanya
utambulisho.
“Doreen huyu ni rafiki yangu
anaitwa Steven Mugo.Tutakuwa
naye hapa nyumbani kwa siku
kadhaa”
“Steven huyu ni Doreen.Ni
rafiki yangu mkubwa na amekuwa
ni msaada mkubwa kwangu.Yeye
niko naye hapa pamoja na Yule
msichana niliyekueleza anaitwa
Graca” Elvis akamaliza
utambulisho
“Karibu sana Steven”
akasema Doreen
“Ahsante sana Doreen
nafurahi kukufahamu” akasema
Steven halafu wakaingia
ndani.Elvis na Doreen wakaelekea
chumbani kwa Elvis Doreen kuna jambo kubwa
limetokea” akasema Elvis wakiwa
wamekaa kitandani
“Jambo gani Elvis? Akauliza
Doreen kwa wasiwasi.Elvis
akamsimulia Doreen kila
kitu.Doreen hakutaka kumuacha
Elivs aendelee
“Stop Elvis !! Please stop !! Oh
jamani balaa gani hili tena?
Akasema Doreen huku michirizi ya
machozi ikionekana mashavuni
pake.Elvis akatoa kitambaa na
kumfuta machozi
“Usiogope Doreen.Pamoja na
nia yao hiyo ya kutaka kuniua
lakini nakuhakikishia kwamba
hawatafanikiwa.
“No Elvis ! Watu hawa ni
hatari na wana mtandao mrefu.Si rahisi kupambana nao.Si watu wa
kufanyia mchezo hata kidogo
Elvis akampiga piga Doreen
mgongoni na kusema
“Doreen si wewe tu mwenye
hofu kuhusiana na jambo hili
lakini naomba nikuhakikishie
kwamba hawataweza kufanikisha
lengo lao.Mimi na timu yangu
ndogo tumejipanga vizuri ili
kukabiliana nao”
Doreen akamshika mikono
Elvis akamuangalia kwa huzuni
na kusema
“Elvis naomba unisikilize kwa
makini sana”
“Nakusikiliza Doreen”
“Nakuomba tafadhali usifanye
mchezo na hawa watu ni hatari
sana na wanaweza kukuua dakika
yoyote wanayotaka.Tafadhali naomba usijihusishe tena na kazi
hizi zisizokuwa na
manufaa.Umekwisha fanya
mambo mengi kwa nchi hii na hizi
ndizo fadhila zake?Ni wakati
muafaka wa kuachana na kazi hii
na kuishi maisha ya amani na
furaha.Let’s get out of here.Let’s go
far away from here ambako
tutaishi maisha mzuri yenye
furaha na amani.Ninazo fedha
nyingi benki tutaweza
kuyamudumaisha.Tafadhali Elvis
nakwambia maneno haya toka
ndani kabisa mwa moyo wangu na
ninakwambia kwa sababu
ninakupenda Elvis” akasema
Doreen kwa hisia kali maneno yale
yalionekana kumuingia Elvis na
kumfanya akae kimya kwa muda
akatafakari na kusema Doreen ninakuelewa
unachokisema na ninatamani
sana kufanya hivyo lakini
nasikitika kukwambia kwamba
siwezi kukimbia.Kukimbia na
kwenda kuishi mbali halitakuwa
suluhisho la jambo hili
zito.Ninajua wapo watu wengi
wanaonipenda na wasingependa
kuniona nikihatarisha maisha
yangu kiasi hiki.Mke wangu
Patricia najua ananipenda sana
hali kadhalika mama yangu ndugu
na marafiki zangu.Wote hawa
wataumia sana pindi wakipata
taarifa za kifo changu lakini sina
njia nyingine ya kufanya
kukabiliana na hawa jamaa.Nina
hakika ipo siku watanielewa na
kunisamehe.Hakuna atakayeweza
kupamba na mtandao huu zaidi yangu.Nimedhamiria kupambana
nao na Mungu atakuwa upamnde
wangu kwani ninalolifanya ni
jambo lenye manufaa makubwa
kwa taifa na wale wanaouawa bila
kuwa na hatia yoyote,kwa
wakimbizi wanaokimbia nchi yao
kutokana na mapigano kati ya
serikali ya Congo na waasi
wanaouziwa silaha na watu ambao
nina uhakika ni kutoka mataifa ya
nje ambao wanawatumia akina
Brigedia Frank kama mawakala
wao” akasema Elvis
Huku uso wake ukiwa umeloa
machozi Doreen akasema
“Sijui kwa nini Elvis unakuwa
mgumu kuelewa,watu hawa
watakuua.Hawatalala hadi
wahakikishe wamekuondoa
duniani.Wewe ni kikwazo kikubwa kwao na watatumia kila nguvu
waliyonayo kukuanagmiza.I swear
in heaven and earth,if you let them
kill yopu,I’ll kill myself
too.Sintaweza kuvumilia mateso
makali nitakayoyapata.Elvis bado
nahitaji kuishi na sitaki kufa
katika umri huu mdogo kwa hiyo
naomba unisaidie nisife kwani
endapo watakuua lazima na mimi
nijimalize.Sikutanii Elvis” akasema
Doreen.
Elvis akamtazama usoni kwa
makini akagundua alikuwa
anamaanisha anachokisema
.Akamvuta kwake na
kumkumbatia huku akimpiga piga
mgongoni.
“Doreen ninafahamu kwamba
unamaanisha unachokisema na si
lengo langu kukusababishia maumivu wewe au mtu mwingine
yeyote.Ninachotaka kukifanya
kina manufaa makubwa kwa taifa
na ndugu zetu wa Congo kwa hiyo
napenda kukuhakikishia kwamba
hakuna jambo lolote
litakalonitokea.Naomba uniamini
ninachokwambia.I’ll be fine”
akasema Elvis kwa msisitizo
“Elvis sina namna nyingine ya
kubadili maamuzi yako.
Ninalazimika kuyaamini maneno
yako kwamba utakuwa salama
lakini endapo litatyokea jambo
lolote baya na kupelekea upoteze
maisha basi fahamu kwamba
tutakutana huko huko peponi kwa
sababu maisha yangu hayatakuwa
na maana tena bila wewe.Elvis
naomba nikueleze ukweli kwamba
japokuwa nafahamu umeoa na mkeo ni rafiki yangu kipenzi lakini
naomba uje kwamba ninakupenda
sana na ninamuonea hata wivu
Patricia kwa kuwa na mwanaume
kama wewe.Sijawahi kukueleza
chochote kuhusiana na jambo hili
lakini ukweli ni kwamba wewe
ndiye mwanaume wa ndoto zangu
,ambaye kwa miaka mingi
nimekuwa ninaota kuwa
naye.Tafadhali usinielewe vibaya
lakini kwa namna ninavyopenda
nataka niwe wazi kwako.Niko
tayari hata kuwa na mapenzi ya
siri nawe kwa sabbu sitaki kuleta
mgogoro wowote kati yako na
Patricia.Najua wakati huu si
muafaka wa kuyaongelea mambo
haya lakini nataka tu ufahamu
kwamba moyo wangu haujiwezi
kwako.Nakupenda kiasi ambacho siwezi kukueleza.Naomba
utakapokuwa katika shughuli
zako uyakumbuke haya
niliyokueleza”
Elvis hakujibu kitu akainama
akafikiri kwa muda halafu
akainua kichwa na kusema
“Nimekuelewa
Doreen.Tutaongea zaidi baadae
kwani tutakuwa na muda wa
kutosha.Kwa sasa naomba
niendelee na maandalizi kwani
muda uliobaki ni mfupi” akasema
Elvis.
Doreen akamkumbatia Elvis
kwa nguvu na kumbusu kisha
Elvis akaanza kupiga hatua
kuelekea mlangoni kabla
hajafungua mlango Doreen
akamuita akageuka “Elvis nakupenda sana”
akasema Doreen
Elvis akatabasamu na
kuufunga mlango akatoka
“Wanawake !! akawaza huku
akitabasamu
Bila kupoteza muda
akamchukua Steven wakaelekea
katika chumba cha kusomea .
“Elvis vipi kuhusu Yule mtoto
Doreen unammiliki? Akauliza
Steven na kumfanya Elvis
atabasamu
“Achana na hayo mambo
Steven na tujielekeze katika kazi
kubwa inayotukabili”
“C’mon Elvis,unajua
nimekuwa kifungoni kwa muda
sasa na sijabahatika kukutana na
watoto wazuri kama
hawa.Nilipokutana tu na Doreen moyo wangu ulistuka mno
nikadhani ninatazama na na
malaika .Sijawahi kukutana na
mrembo kama huyu.kama si mali
yako tafadhali nifanyie mpango”
akasema Steven na Elvis akacheka
“Steven achana na hayo
mambo” akasema Elvis
Dakika zaidi ya arobaini
walizitumia humo chumbani
wakijiandaa.Baada ya kumaliza
maandalizi yao Elvis akampeleka
Steven katika chumba ambacho
angekitumia muda wote ambao
angekuwepo pale halafu akaelekea
chumbani aliko Doreen.Bado
alikuwa amelala kitandani macho
yamemvimba na aliendelea
kulia.Elvis akamuonea huruma
sana akamfuata pale kitandani Tafadhali usilie
Doreen.Niamini nikwambiavyo
kwamba nitakuwa salama.Mimi na
wenzangu tutafanya kila
litakalowezekana kuhakikisha
kwamba ninakuwa salama.Bila
kufanya hivi sintaweza
kupambana na mtandao huu
mkubwa na maisha ya ndugu zetu
kule Congo yataendelea kuwa
magumu kila uchao”
“Elvis ninakuamini sana kwa
kila unachoniambia lakini katika
hili moyo wangu unakuwa mgumu
sana kukubaliana nawe.Ni jambo
la hatari sana.Kama mimi
nimeumizwa namna hii ni vipi
Patricia atakapopata taarifa
kwamba umekufa? Nadhani
anaweza akarukwa na akili kwa namna anavyokupenda.Moyo
wangu unaumia sana na”
“Usiseme chochote Doreen”
Elvis akamzuia Doreen kusema
chochote
“Nakuomba uniamini
nilivyokwambia kwamba nitakuwa
salama na hakuna chochote
kibaya kitakachonitokea” akasema
Elvis na Doreen akafuta machozi
“Vipi kuhusu Patricia?
Unafikiria kumwambia chochote
kuhusiana na jambo hili
unalokwenda kulifanya?
“Patricia hafahamu chochote
na wala sitaki afahamu kwani
hatakubali nifanye
hivi.Atapelekewa taarifa za kifo
changu na sipati picha atakuwa
katika hali gani lakini ninachojua
ni kwamba ataumia sana.Sikutegemea kama siku moja
nitamuumiza mke wangu namna
hii.Picha ya namna anavyoteseka
kwa uchugu baada ya kupata
taarifa za kifo changu zinanijia
kila dakika kichwani na
kuniumiza mno lakini sina namna
nyinghine ya kufanya I have to
die” akasema Elvis
“kwa nini usimueleze ukweli
kwamba tukio lile si la kweli ili
asiumie? Akauliza Doreen
“Natamani sana kufanya
hivyo kwani sipendi kumuona mke
wangu mpenzi akiumia lakini
mazingira hayaniruhusu kufanya
hivyo.Endapo akifahamu chochote
kuhusiana na mpango huu basi
maisha yake yatakuwa hatarini.Ni
bora aumie kwa siku chache kwa
kutofahamu chochote kuliko kumuweka katika hatari kwa
kuufahamu mpango huu.Ninaapa
hii itakuwa ni kazi yangu ya
mwisho na baada ya hapa
ninataka nipate nafasi ya kukaa
na mke wangu na kuyatengeneza
maisha yetu”
“What about me? Akauliza
Doreen
“Doreen naomba nikuweke
wazi kwamba japokuwa umekiri
kwamba unanipenda lakini mimi
ni mume wa mtu na ninapendana
mno na mke wangu.Kilichotokea
jana kati yetu ni bahati mbaya na
sitaki jambo lile lijirudie tena.Kwa
hiyo naomba usiwe na matumaini
makubwa kwamba kuna kitu
kinaweza kutokea kati yetu.Baada
tu ya operesheni hii kumalizika
nitarejea kwa mke wangu na yote yaliyotokea hapa yataishia
hapa.Mimi na wewe tutaendelea
kuwa marafiki” akasema Elvis
“Elvis lazima utakuwa wangu
tu” akawaza Doreen.
Kimya kifupi kikapita Elvis
alikuwa ameinama
akitafakari.Doreen akamstua
“Are you nervous Elvis?
“Doreen siwezi kukataa
kwamba sina wasi wasi.Ninao
mkubwa kwani jambo
ninalokwenda kulifanya ni kubwa
na hatari na sijawahi kulifanya
hata mara moja hivyo lazima niwe
na wasi wasi”
Doreen akamvuta Elvis
akamkumbatia na kusema
“Elvis usiogope
tafadhali.Mungu anaiona dhamira
yako njema na ya dhati kabisa ya kutaka kupambana na watu hawa
wenye roho za kinyama na
atakutangulia na kukupa
ushindi.Wewe ni mmoja na huna
nguvu za kutosha kupamba na
wakubwa hawa wenye nguvu
kubwa lakini nakuhakikihsia
kwamba Mungu hatakuacha
kamwe.Atakuwa nawe na
atakushindia.Liite jina lake naye
atapigana na wabaya wako .You
can do it Elvis.I trust you”
akasema Doreen na maneno yale
yakampa faraja sana Elvis na
kumfanya atabasamu
“Nashukuru Doreen kwa
maneno hayo mazito ya
faraja.Najihisi nimepata nguvu
zaidi ya kuendelea na mpango
wangu huu na nia uhakika
nitashinda” Akasema Elvis. Ahsante pia nawe kwa
kuniamini na kunishirikisha
katika mambo yako muhimu na ya
siri kama hili.Nakuahidi
kusimama nawe katika nyakati
zote hata zile ngumu kabisa.Kama
kuna chochote ninachoweza
kusaidia tafadhali naomba
uniambie.Niko tayari kufanya
chochote kile utakachoniomba
nifanye”
“Nashukuru sana Doreen.Kitu
cha pekee unachoweza kukifanya
ni kuniombea ili kila kitu kiende
kama ninavyopanga.Huo utakuwa
ni msaada mkubwa sana
kwangu.Kitu kingine ninachotaka
kukuomba ni ku…………”
hakumaliza sentensi yake simu
yake ikaita.Alikuwa ni
mkurugenzi mzee MeshackJumbo.Akavuta pumzi
ndefu na kusema kwa sauti ndogo
ya wasi wasi
“mambo yameiva”
Akaipokea simu
“hallow mzee”
“Elvis tayari nimekwisha
pokea maelekezo toka kwa hawa
jamaa na wamenieleza namna kila
kitu kitakavyokwenda.Kila kitu
kitafanyika katika msitu wa Ngezi
kama nilivyokwambia
awali.Upande wa kusini mwa
msitu huo kuna shamba la
minazi.Ukilifuata shamba hilo
utakutana na kijito kidogo
utakivuka hicho kijito na
kukifuata kiujia kidogo
kinachokupeleka hadi ndani ya
msitu.Kwa mujibu wa maelekezo
ni kwamba utakutana na njianyingine mbili na utafuata njia
inayoelekea kulia ambayo
itakupeleka hadi katika pango
moja lililo kati kati ya msitu
ambalo hutumika na wakaazi wa
maeneo hayo kwa
matambiko.Hapo ndipo
palipoandaliwa kwa ajili ya kuitoa
roho yako.Kuna vijana tayari
wamewekwa hapo kwa kazi hiyo
ya kukuondoa uhai na
wamajipanga vilivyo” akasema
MeshackJumbo na baada ya muda
akasema
“Kwa hiyo Elvis nitamtuma
Silvia atakupigia simu na
kukwambia kwamba unahitajika
hapa ofisini haraka na
utakapofika nitawaita wale vijana
wengine kama tulivyokuwa
tumepanga na nitakupa taarifa hizi mbele yao.Mambo haya
yatakuwa ya wazi ili isionekane
kama vile kuna jambo la siri kati
yetu.Katika kikao hicho utashauri
kwamba nikuache ukafanye
kwanza uchunguzi peke yako
halafu baadae ukishapata uhakika
ndipo ipangwe timu ya kwenda
kuvamia eneo hilo.Mimi
nitakubaliana nawe na utaenda
huko peke yako.Natumai utakuwa
tayari umejipanga vizuri na Steven
kukabiliana na hao vijana
waliowekwa huko msitu wa
Ngezi.Kwa mujibu wa maelezo
niliyopewa watakuwa wanne.Mimi
na Dr Philip hatutakuwa mbali
sana na baada ya kazi ya
kumalizika utanitaarifu na
tutakuja kumaliza shughuli ya
kuandaa kifo chako” Akanyamaza kidogo na
kuvuta pumzi ndefu halafu
akasema
“Elvis are you sure you want
to do this?
Kimya cha sekunde kadhaa
kikapita kisha Elvis akasema
“Ndiyo mzee.Nahitaji kufanya
hivyo.Hakuna namna nyingine
zaidi ya njia hiyo”
“Vizuri.Jiweke tayari”
akasema mzee na kukata simu
“Elvis kuna nini mbona
umebadilika hivyo? Akauliza
Doreen
“Mkurugenzi alikuwa
ananitaarifu kwamba ile kazi
imeanza”
Doreen akamtazama Elvis
usoni na kusemaElvis tafadhali usiogope.You
can do it”
Uso wa Elvis ukatabasamu
tena baada ya maneno yale ya
Doreen
“Ahsante Doreen” akasema
Elvis na kutoka mle chumbani
akamfuata Steven
“Tayari mkurugenzi
amenipigia simu na kunielekeza
namna kila kitu
kitakavyofanyika.Mambo yote
yatafanyika katika msitu wa Ngezi”
akasema Elvis.Steven aliyekuwa
amejilaza kitandani akainuka na
kukaa.Elvis akamueleza kila kitu
alichoelezwa na MeshackJumbo
.Wakatumia dakika chache
zilizopo kujadiliana namna ya
kufanya na wakati wakiendelea
kujadiliana simu ya Elvis ikaita.Alikuwa ni Silvia katibu
muhtasi wa MeshackJumbo
ambaye alimtaarifu Elvis kwamba
anahitajika ofisini kwa
mkurugenzi haraka iwezekanavyo
“Steven nadhani hatuna tena
muda wa kupoteza twende
tukaianze kazi mara moja”
akasema Elvis .Steven akaitazama
bastora nne alizopewa na Elvis
akatabasamu
“I missed this very much.I’m
back to the show again.Thank you
Elvis” akasema Steven.
Kabla hajaondoka Elvis
akamfuata Doreen chumbani
“Doreen this is it.We have to
go now”
Doreen akamtazama na
kushindwa kujizuia kuangusha
machozi akamkumbatia akambusu na kumtaka arejee
salama
“Doreen ahsante kwa kila
kitu.Nakuahidi nitarejea salama”
akasema Elvis na kuanza kupiga
hatua kuelekea mlangoni
akakinyonga kitasa lakini kabla
hajatoka akageuka na kusema
“Doreen naomba usimweleze
chochote Graca kwa
sasa.Nitakaporejea nitamueleza
kwa kirefu kuhusiana na jambo
hili.Endapo sintarejea …” Elvis
akasita kidogo kisha akamfuata
Doreen akaketi pembeni yake
“Endapo itatokea bahati
mbaya na nikashindwa kurejea
tena naomba unisaidie kitu
kimoja”
“Please Elvis don’t say
that.Hujui ni jinsi gani unaniumiza kwa hayo maneno
yako” akasema Doreen
“I’m sorry Doreen lakini
lazima tukubaliane na ukweli
kwamba lolote linaweza
kutokea.Ninaweza kurudi au
nisirudi tena lakini nina uhakika
mkubwa kwamba nitarejea salama
ila ninakwenda katika
mapambano na katika
kupambana chochote kinaweza
kutokea kwa hiyo endapo
sintafanikiwa kurejea salama
ninaomba msaada wako katika
jambo moja muhimu sana”
akasema Elvis
“Jambo gani hilo Elvis?
Akauliza Doreen huku akifuta
machozi
“Nilipomtoa Graca afrika
kusini nilimuahidi nitahakikisha anakuwa salama.Kwa hiyo endapo
sintarejea naomba tafadhali
uhakikishe kwamba anaendelea
kuwa salama na usalama pekee ni
kumpeleka sehemu ya mbali
kabisa na hapa.Can you do that
for me?
Doreen akafuta tena machozi
na kusema
“Yes I can”
“Thank you” akasema Elvis na
kuinuka akatoka mle chumbani
moja kwa moja akaelekea
alikoegesha gari akaingia Steve
akamfuata na kabla hajaingia
garini Doreen akamuita na
kumuomba amsubiri
“Unasemaje Doreen? akauliza
“Steven tafadhali hakikisha
Elvis anarudi hapa akiwa
mzima.Can you promise me that? Akasema Doreen.Steven
akatabasamu na kusema
“Elvis will be fine.I give you
my word” akasema Steven huku
akitabasamu
“Thank you Steven” akasema
Doreen
“You are welcome” akajibu
Steven huku akiufungua mlango
wa gari akaingia.Elvis ndiye
aliyekuwa dereva akawasha gari
wakaondoka wakimuacha Doreen
amesimama akilikodolea macho
gari
“Doreen alikuwa anakueleza
nini? Akauliza Elvis
“Alitaka nihakikishe kwamba
unarejea salama”
“Ulimjibu nini? Nilimuhakikishia kwamba
utarejea salama” akasema Steven
na safari ikaendelea
“Let’s go far away from here
ambako tutaishi maisha mazuri
yenye furaha na amani.Tafahali
Elvis nakwambia maneno haya
kwa sabau ninakupenda” maneno
haya ya Doreen yakajirudia
kichwani kwa Elvis
“Sikutegemea kama siku moja
ningefikia hatua ya kumsaliti mke
wangu na kutembea na rafiki yake
kipenzi.Lakini hata hivyo Doreen
ana vitu adimu sana .Mwanaume
atakayemuoa atafaidi mno.Anajua
sana kujali na hata kitandani ni
mjuzi wa mambo.Kuna wakati
ananiweka katika majaribu
makubwa lakini sitaki tena kuendelea kumsaliti mke wangu
Patricia” Akawaza Elvis
“Patricia ndiye aliyeanza
kutembea nje ya ndoa yetu na
nilimshuhudia kwa macho yangu
akitoka hotelini na
mwanaume.Kitendo kile
kiliniumiza sana na ndiyo maana
hata Doreen aliponishawishi
kulala naye nilijikuta namkubalia
kutokana na hasira nilizokuwa
nazo”
“Elvis ! akaita Steven
“Wewe ni mwanaume
mwenzangu na siku zote wanaume
huwa hawafichani bali
wanaambiana ukweli.Doreen
anakupenda mno .Nimemtazama
machoni na kugundua hilo.Doreen
ni mwanamke aliyeumbwa
akaumbika .Hata mimi nilipomuona mwili wote
ukanisisimka.Ana uzuri na umbo
la kumsisimua mwanaume yeyote
.Najua una mke mzuri na
anakupenda sana lakini tafadhali
naomba usiuvunje moyo wa huyu
binti malaika anayeonekana kuwa
tayari kufanya chochote kwa ajili
yako.Itakuwa ni dhambi
kumuumiza moyo mtoto kama
Yule” akasema Steven.Elvis
akatabasamu na kusema
“Steve bado hujaacha mambo
yako tu” akasema Elvis huku
akitabasamu
“Huu ndio udhaifu wangu
Elvis na wewe unafahamu.Watoto
wazuri mimi ndio ugonjwa
wangu.Nikiona mtoto mzuri
ninachanganyikiwa kabisa .Hii
ndiyo iliyoniponza hadi nikaingia katika matatizo haya ya
kufungwa.Ngoja nikupe siri
Elvis.Kilichosababisha nikafungwa
ndani ya ile nyumba ni baada ya
kutembea na kimada wa kigogo
mmoja hivi wa serikali.Mwanamke
huyo ni mzuri ajabu na
nilishindwa kuvumilia ikanilazimu
kurusha nyavu akanielewa na
ndipo nikaanza kujilia vyangu
.Mtoto akakolea na mziki wangu
akaanza kupunguza mahaba kwa
yule kigogo aliyekuwa
anamgharamia mno.Alipofanya
uchunguzi kwa nini mapenzi
yamepungua ghafla akagundua
kwamba kimada wake ana mpenzi
mwingine ambaye ni
mimi.Akanitafuta na akanikanya
niachane na kimada wake lakini
nikaendelea kwa kuwa nilikuwa nimenogewa mno.Baadae
yakanikuta haya
yaliyonikuta.Naamini kufungwa
kwangu ni mipango ya Yule kigogo
na hakuna sababu nyingine.Hizo
tuhuma walizonirundikia eti sijui
nimeuza siri za serikali ni uongo
mtupu hazina ukweli wowote”
akasema Steven
“Ninalifahamu hilo Steve
lakini kama rafiki yangu nataka
nikushauri kitu kimoja.Steve
umekwisha kuwa mtu mzima hivi
sasa.Achana na hayo maisha ya
namna hiyo.Badilika na fikiria
kuanza maisha mapya.Tafuta
mwanamke mzuri atakayekufaa oa
na utengeneze familia.Mambo
haya ya kurukia rukia wanawake
za watu si mambo mazuri.Ni vipi
endapo utagundua mwanamke wako anatembea na mtu
mwingine? Unafahamu uchungu
wake? Nakushauri rafiki yangu
achana na hiyo tabia mara moja”
akasema Elvis na safari ikaendelea
kimya kimya hadi walipofika hoteli
79
“Mimi nitashuka hapa na
kuchukua taksi wewe tangulia
eneo la tukio” akasema Elvis na
kuegesha gari akashuka
“Good lucky brother” akasema
Elvis na kumpa mkono Steve
halafu akaelekea eneo
zinakoegesha taksi.Steven
akageuza gari na kuondoka
kuelekea msitu wa Ngezi
*****************
Msitu wa Ngezi ni msitu
mkubwa wa asili uliopo nje kidogo
ya jiji la Dar es salaam.Ni msitu
uliopo mpakani mwa mkoa wa Dar
es salaam na Pwani.Kwa miaka
mingi wenyeji wanaozunguka
msitu huu wamekuwa wakiutumia
kwa kufanya matambiko mbali
mbali ya kimila.Inaaminka
kwamba ndani ya msitu huu
aliishi mzimu ajulikanaye kama
Ngezi na hadithi zinasema
kwamba baadhi ya watu wa kale
waliwahi kufanikiwa kumuona.
Simulizi hizo zinasema kwamba
kuna wakati Ngezi aliwahi
kuwatokea watu mbali mbali
walioingia humo msituni na kuna
waliobahatika na kupewa utajiri
mkubwa mara walipokutana
naye.Ndani ya msitu huo kuna pango ambalo ndimo inaamika
Ngezi alikuwa akiishi.Ni katika
pango hilo wenyeji wanaozunguka
msitu huu wamekuwa wakifanya
ibada zao za matambiko
kumuomba Ngezi awasaidie katika
mambo yao mbalimbali.Wenyeji
hawa wamekuwa wakiulinda sana
msitu huu ili asili yake isipotee
Steven Mugo alisimamisha
gari katika kijiji cha Mapindo
akakodisha piki piki iliyompeleka
hadi katika kijji cha Mpendae
ulipo mzitu wa Ngezi.Hakuwa
mgeni wa maeneo haya kwani
aliyafahamu vyema hivyo
aliposhuka katika piki piki
akashika moja kwa moja njia
inayoelekea msitu wa
Ngezi.Umbali wa kama mita mia
tano hivi akachepuka kulia na kukifuata kiujia kidogo
kinachoelekea katika shamba la
minazi lililopakana na
msitu.Alitembea kwa tahadhari
kubwa na kila mara alihakiki
usalama wake kama kuna mtu
anamfuatilia.Alitembea haraka
haraka na kuufika msitu.Kabla ya
kuingia msituni alihakiki usalama
na aliporidhika hakuna mtu
yeyote aliyekuwa akimfuatilia
akajitoma msituni na kuingia
kichakani akafungua begi lake na
kutoa kanzu nyeupe akavaa
pamoja na kofia ya baraghashia
akajitazama na kuridhika na
mwonekano wake halafu akatoa
bastora tatu na kuzifutika katika
suruali yake.Katika mfuko mweuzi
aliokuwa nao kulikuwa na kuku
mweusi akamtoa na kumshika mkononi halafu akalificha begi
lake katika kile kichaka akatoka
na kuangaza pande zote.
Msitu ulikuwa kimya kabisa
ni sauti tu za ndege ndizo
zilizosikika.Taratibu akaanza
kutembea kulitafuta
pango.Mwendo wa kama dakika
tano akakutana na akina mama
wawili waliokuwa wanaokota
kuni.Hawakustuka walipomwona
kutokana na mwonekano wake
.Alionekana kama mhanga wa
kienyeji.Steven akawasalimia na
kuwaomba wamuelekeze njia ya
kuelekea katika pango la
Ngezi.Bila wasiwasi
wakamuelekeza akashukuru
akaendelea na safari yake.Baada
ya mwendo wa dakika kumi na
tano ndani ya msitu huu mnene wenye miti mikubwa akawasili
katika pango la Ngezi.Ni sehemu
inayotisha .Ukimya mkubwa
ulitawala mahala pale.Pamoja na
ujasiri wake lakini alihisi kuingiwa
na woga kutokana na mazingira
yaliyolizunguka pango
lile.Takribani dakika tano Steven
alikuwa amesimama akitafakari
kitu cha kufanya na namna
atakavyoweza kujificha.Alikuwa na
woga mwingi kuingia ndani ya
pango lile linalotisha.Baada ya
tafakari akakata shauri aingie
ndani ya pango.Wakati akijiandaa
kuitoa bastora yake mara akasikia
vishindo vya hatua za
mtu.Akastuka na kugeuka.Ni
kweli kulikuwa na mtu nyuma
yake.Mwili ukamsisimka.Mtu Yule
mwenye mwili uliojengeka vyema alivaa kofia na miwani myeusi na
sura yake haikuonyesha kama ni
mtu wa masihara.Kwa sekunde
kadhaa Steve na mtu Yule
walitazamana.Ghafla toka upande
wa juu wa kushoto akatokea mtu
mwingine ambaye mwonekano
wake haukutofautiana na Yule wa
kwanza.wakati aiendelea
kuwasoma wale watu ambao mara
moja aliwatambua kuwa ndio wale
ambao walikuwa wamekwenda
kupambana nao na mmoja wao
alikuwa na kitu mfano wa
sanduku
“Habari yao ndugu” Yule
jamaa aliyetangulia akamsalimu
Steven.Sauti yake ilikuwa nzito na
ya kukwaruza
“Nzuri .habari zenu? Unafanya nini hapa?
Akauliza yule jamaa
“Naitwa mganga
Nyandwile.Nimekuja kufanya dawa
kwa mgonjwa wangu”
“Yuko wapi mgonjwa wako?
“Tayari amekwisha ondoka na
hapa ninamalizia uganga wa
mwisho mwisho ili tiba
ikamilike.Ninyi mmekuja kufanya
dawa pia?
“Tafadhali mganga tunaomba
umalize haraka shughuli zako
uondoke mahala hapa kuna kazi
tunahitaji kuifanya hapa muda si
mrefu sana” akaamuru Yule
jamaa.
“sawa ndugu ninamalizia
shughuli za wisho na nitaondoka
hapa muda si mrefu.Kuna dawa
nahitaji kufanya ndani ya pango la mzimu” akasema Steven huku
akimshika vizuri kuku wake na
kuanza kupiga hatua kuingia
pangoni
“Mganga subiri kidogo”
akasema jamaa mwingine aliyevaa
fulana ya kumbana na
kuuonyesha mwili wake
uliojengeka.Steven akageuka na
mtu yule akamsogelea
karibu.Akajiweka tayari endapo
kungetokea mapambano yoyote
“Umesema kuna dawa
unakwenda kuifanya ndani ya
pango hili? Akauliza
“Ndiyo”
“Watu wanaruhusiwa kuingia
ndani ya pango hili?
“Ndiyo wanaruhusiwa lakini
hadi uwe umeongozana na mtu
mwenye kulifahamu vyema pango hili na ambaye anafahamika na
mzimu Ngezi kwani ukiingia bila
kuongozana na mtu huyo
anayelifahamu vyema pango hili
hautarejea tena” akasema Steven
na mtu yule akaonekana kuogopa
kidogo
“Umefika hapa muda gani?
akauliza yule jamaa
“Nina zaidi ya saa mbili hapa”
“Toka umefika kuna mtu
yeyote umemuona amefika hapa?
“Hapana sijamuona mtu
yeyote katika kipindi hiki chote
nilichokuwa namtibu mgonjwa
wangu”
“Sawa,maliza shughuli zako
uondoke” akasema Yule jamaa
“Kuna yeyote kati yenu
angependa kuingia ndani ya pango
na kutazama lilivyo ndani? Akauliza Steven.Yule jamaa
akafikiri kidogo na kusema
“maliza shughuli zako na
uondoke mganga” akasema na
kutejea kujiunga na
wezake.Steven akavuta pumzi
ndefu
“Hawa ndio wenyewe.kwa
namna nilivyowasoma si watu wa
masihara lakini nitakabiliana
nao.Hawatanishinda” akawaza
Steven na kuanza kuingia ndani
ya pango lililokuwa na kiza.Hali ya
mle pangoni ilikuwa ni ya ubaridi
na ukimya mkubwa.Hakulifahamu
pango lile na wala hakujua aelekee
wapi akaanza kuingiwa na woga
“Bwana ndiye mchungaji
wangu na sintoogopa chochote
nikiwa naye.Ninaamini katika
Mungu na si katika mizimu na mapepo wachafu” akasema Steven
kwa sauti ndogo na kupiga hatua
nne akakutana na jiwe kubwa
.Akapiga magoti nyuma ya jiwe lile
halafu akageuka na kutazama nje
.Akawaona wale jamaa wakiwa
wamesimama wakielekezana
jambo na mmoja wao alikuwa
ameshika kitu kama karatasi
kubwa ya ramani
“Watakuwa wanaelekezana
namna watakavyojipanga
kumuondoa Elvis” akawaza Steven
kwani kwa pale alipokuwa
hakuweza kuyasikia maongezi yao
“Lile sanduku nahisi litakuwa
na silaha .Ngoja niendelee
kuwasoma nyendo zao kwanza
kabla ya kufanya chochote”
akawaza Steve Akiwa ndani ya Pango Steven
aliendelea kumminya kuku Yule
ambaye alitoa ukelele ili watu wale
wajue kuna kitu kinaendelea mle
ndani ya pango.Aliendelea
kuwasoma watu wale waliokuwa
wamesimama wakijadiliana
“Pango linatisha mno hili na
nimewahi kusikia sifa zake si
nzuri sana.Kuna watu wengi tu
wamewahi kupotelea humu ndani
walipotaka kuja kuchunguza kuna
nini.Wengine wanasema
wamewahi kuliona joka kubwa
sana ndani ya hili pango wengine
wanasema vile ilimradi kila mmoja
anatoa ushuhuda wake kuonyesha
kuwa hapa kuna mzimu”
Akaendelea kuwaza Steve akiwa
makini sana ndani ya pango akiwasoma wale jaama nyendo
zao.
*****************
 
Back
Top Bottom