Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Mimi nahisi ndoa ya Elvis na Patricia itavunjika na Dr atajibebea Patricia na kwenda naye marekani. Huko wataasili mtoto.

Elvis ni Kama ataishia kumwoa Doreen.

Steve atamwoa Graca.

(Nawaza tu kwa sauti kuu)
Sema ukiangalia kwa umakini Patricia from the first time sio kwamba alikua anampenda Elvis kiviile so mi sikushangaa alivyogawa papuchi
 
Sema ukiangalia kwa umakini Patricia from the first time sio kwamba alikua anampenda Elvis kiviile so mi sikushangaa alivyogawa papuchi
Huyo anashawishika na vitu vidogo sana.

Kwa Godson alishawishika na ukwasi wa familia ya godson, Elvis alivutiwa nae kwa sababu alikuwa naye kwenye top ten ya wanafunzi bora, Huyu Dr wa marekani kavutiwa na uraia wake tuseme hivyo, Of all people kwenye ile part kwa nini amwambie huyo ndo amsindikize?

She is so weak when it comes to her papuchi.
 
Huyo anashawishika na vitu vidogo sana.

Kwa Godson alishawishika na ukwasi wa familia ya godson, Elvis alivutiwa nae kwa sababu alikuwa naye kwenye top ten ya wanafunzi bora, Huyu Dr wa marekani kavutiwa na uraia wake tuseme hivyo, Of all people kwenye ile part kwa nini amwambie huyo ndo amsindikize?

She is so weak when it comes to her papuchi.
Yeah exactly pale hamna mke pale
 
I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 35

Elvis aliwasili ofisini kwao na
moja kwa moja akaelekea ofisini
kwa mkurugenzi wake Mr
MeshackJumbo.Silvia katibu
muhtasi wa mzee Jumbo
alimuelekeza aingie moja kwa
moja katika chumba cha mikutano
cha mkurugenzi ambako alikuwa
anasubiriwa.
Ndani ya chumba kile kidogo
cha mikutano walikuwamo watu
wawili ambao wote ni wafanyakazi
wa idara hii.Albert Chukwe na
Rosa Mkude.Nao pia waliitwa
katika kikao hiki bila kuelewa
wanaitiwa nini.Mara tu Elvis alipoingia mle chumbani
wakastuka na kujua kulikuwa na
shughuli kubwa kwanimara nyingi
kikao kinachomuhusisha pia Elvis
huwa ni kunakuwa na kazi.Elvis
akawasalimu na kupitisha utani
kidogo halafu mlango
ukafunguliwa akaingia
mkurugenzi.Buila kupoteza wakati
mkurugenzi akafungua kikao.
“Vijana wangu nimewaiteni
hapa kuna jambo la dharura
limetokea.Nadhani nyote
mnafahamu kwa kipindi Fulani
kulitopkea mashambulizi ya
mabomu jijini Arusha yaliyoua na
kujeruhi watu kadhaa.Uchunguzi
ulionyesha kwamba aliyefanya
mashambulio yale ni mtu
anayejulikana kama Abdullah
Abdullah.Huyu mtu anasakwa sana lakini mpaka sasa bado
hajapatikana .Ni mtu mwenye
mbinu za hali ya juu za kujificha”
MeshackJumbo akanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Leo asubuhi nimepokea
taarifa toka kwa chanzo chenye
uhakika kwamba Abdullah
anajificha katika msitu wa
Ngezi.Inasemekana kwamba
amekuwa akijificha hapo nyakati
za mchana na hutoka usiku
kwenda kujitafutia mahitaji mbali
mbali.Ndani ya msitu huo kuna
pango kubwa ambalo wenyeji
hulitumia kwa ibada za kimila na
Abdullah analitumia pango hilo
kama maficho yake.Taarifa hizo
zimetoka kwa chanzo cha uhakika
hivyo lazima tuzifanyie
kazi.Nimewaiteni hapa kuwafahamisha kwamba tunataka
tufanye uchunguzi wa suala hili
na tubaini kama ni kweli Abdullah
anaishi katika msitu huo wa Ngezi
kabla ya kuchukua hatua
nyingine” akasema mzee Jumbo
Elvis alionyesha sura ya
mstuko.Hakutaka wale vijana
wawili wang’amue kama tayari
alikuwa na taarifa zile.Akakohoa
kidogo na kusema
“Mkurugenzi sina lengo la
kuhoji wapi umepata taarifa hizi
lakini ninachotaka ni uthibitisho
toka kwako kama una uhakika na
taarifa hizi kwa sababu tumekua
tunapokea taarifa nyingi kama hizi
na baada ya kuzifanyia kazi
tunagundua hakukuwa na ukweli
wowote.Ninachohitaji ni wewe
kutuhakikishia kwamba una uhakika kwamba taarifa hizi
umezipata toka katika chanzo cha
kuaminika”
MeshackJumbo akamtazama
Elvis kwa macho makali na
kusema
“Elvis mimi ndiye mkurugenzi
wenu hapa na ndiye mwenye kauli
ya mwisho kuamua ni taarifa ipi
ya kweli na ipi si ya kweli.Hivyo
basi hadi kuwaiteni hapa na
kuwapa taarifa hizi nina uhakika
nazo”
“Ahsante sana mzee.Nilihitaji
tu uthibitisho wako.Hata hivyo
nina ombo moja.Umetueleza
kwamba tunatakiwa tufanye
kwanza uchunguzi kabla ya
kuchukua hatua nyingine.Mimi
naomba nijitolee nikafanye kwanza
uchunguzi mahala hapo na kisha nitawapa majibu nini hasa
kilichopo hapo Ngezi.Nataka
kwanza tupate picha kamili na
ndipo tutafaya maamuzi mazuri
zaidi ni hatu aipi tuichukue”
akasema Elvis.MeshackJumbo
akakuna kichwa na kusema
“Mawazo yako ni mazuri sana
Elvis na kwa kiasi Fulani naweza
kukubaliana nayo lakini Abdullah
ni mtu hatari sana na kama ni
kweli amejificha huko hatujui
amejihami vipi .Kwenda huko
Ngezi peke yako inaweza kuwa
hatari kubwa kwako.Hatuwezi
kuhatarisha maisha yako kiasi
hicho.Abdullah anajua kwamba
anatafutwa anajihami muda
wote.Mimi nadhani iundwe timu
ya watu muende huko msituni
mkafanye uchunguzi na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya”
akasema MeshackJumbo
“Wazo lako ni zuri mzee lakini
katika hili napendekeza niende
kwanza peke yangu.Kupeleka timu
ya uchunguzi inaweza ikawa ni
hatari zaidi na kumfanya Abdullah
kama amejificha agundue na
atoroke.Nina hakika endapo
nikienda mwenyewe ninaweza
kupata kitu kizuri zaidi cha
kutusaidia.Endapo nitahitaji
msaada wa haraka basi
nitawataarifu” akashauri Elvis
“Mkurugenzi nadhani wazo la
Elvis ni la msingi” akasema Albert
“Lakini hata hivyo endapo
Elvis atakwenda peke yake katika
msitu huo basi kuwe na timu
ambayo itakuwa karibu ili kutoa
msaada wowote pindi ukihitajika.Abdullah hawezi kuwa
mwenyewe lazima atakuwa na
watu wanaomlinda na ni lazima
atakuwa amejihami hivyo lazima
tuwe karibu kumsaidia Elvis pindi
akihitaji msaada” akasema
MeshackJumbo
“Elvis utaingia msitunio
kufanya uchunguzi na sisi
tutakuwa maeneo ya karibu ili
kutoa msaada pale
utakapohitajika .Unaonaje kuhusu
wazo hili Elvis?akauliza mzee
Jumbo
“Ni wazo zuri pia lakini timu
hiyo ya msaada inabidi iwe mbali
kidogo ya msitu ili kutoweza
kuleta shaka yoyote hata kwa
wenyeji wanaouzunguka msitu
huo.Mimi nitakuwa nikiwasiliana
nanyi na kuwafahamisha kila kitu nitakachokiona na pindi nikiona
hatari yoyote nitawataarifu mara
moja” akasema Elvis
“Vizuri.Albert na Rosa
jiandaeni tutaondoka kwenda
kumsaidia Elvis .Ninyi
mtatangulia na mimi nitafuata
nyuma nikiwa na daktari wetu Dr
Philip.Elvis hakikisha mawasiliano
kati yako na sisi tulio nyuma yako
hayakatiki ili tujue nini
kinachoendelea ndani ya msitu”
akasema MeshackJumbo
“Usihofu
mzee.Nakuhakikishia kazi nzuri
na tutaufahamu ukweli” akasema
Elvis halafu wakainuka wote
wakaelekea kujiandaa
“Elvis suala hili naomba katu
usilifanyie mzaha hata
kidogo.Abdullaj ni mtu hatari.kama kweli amejificha
katika msitu huo basi hiyo si
sehemu salama hata kidogo”
akasema Albert wakati
wakijiandaa
“Usihofu Albert.Ninaenda
kufanya uchunguzi na si
kupambana.Hata hivyo nitakuwa
makini sana” akasema Elvis
Dakika kumi na tano tayari
Elvis alikwisha jandaa.Gari tatu
zilikuwa tayari na Elvis akamfuaa
mkurugenzi wake ofisini
“Mzee mimi natangulia”
“Elvis be carefully”
“I will” akasema Elvis na
kuingia katika gari akaondoka
kuelekea katika msitu wa Ngezi
****************** Dakika takribani kumi na
tano zilikatika bado Steven akiwa
ndani ya pango.Wale jamaa wanne
waliendelea kujadiliana jambo
huku wakigeukia mlango wa
pango mara kwa mara na
hatimaye mmoja wao akapiga
hatua kuelekea mlango wa pango
“hallow Mganga !! akapaaza
sauti .Steven aliyekuwa amejificha
nyumba ya jiwe alimuona na
kumsikia vizuri
“Mganga nakuomba umalize
shughuli zako na uondoke hapa
mara moja” akasema Yule jamaa
kwa sauti ya ukali.Zikapita
sekunde kadhaa bila ya Steven
kutokea au hata kuitika.Yule
jamaa akasema tena kwa ukali
“Mganga nakuomba kwa mara
ya mwisho toka huo ndani yapango haraka sana kabla sijaingia
na kukutoa kwa nguvu .Nakupa
dakika moja uwe umetoka humo
ndani!!
Steven aliyasikia maneo yale
na kuitabasamu
“Its show time” akawaza na
kuinuka akaanza kupiga hatua
kutoka mle ndani ya pango.Mara
tu alipotokeza wale jamaa
wakamtazama kwa hasira
“Samahani ndugu zangu kwa
kuwachelewesha kuanza shughuli
.Hata hivyo sikuwa nimemaliza
dawa nimeamua niwaache kwanza
mmalize kazi zenu na mimi
nitakuja baadae kumaliza dawa
zangu” akasema Steven huku
akipita pembeni yao.Wale jamaa
wakamtazama bila kumsemesha
kitu.Alipiga hatua kama tano hivi na ndipo kilipotokea kitu ambacho
wale jamaa hawakuwa
wamekitarajia.
Kwa kasi ya ajabu Steven
aliipandisha juu kanzu aliyoivaa
na kuzichomoa bastora mbili
alizozifutika kiunoni.Kwa wepesi
wa aina yake aliweza kuwaona
wale jamaa walivyokaa na bila
kupoteza hata sekunde moja
akaanza kuwamiminia risasi.Kwa
kuwa hawakuwa wametarajia kitu
kama kile kutokea wale jamaa
hawakuweza kujibu mashambulizi
na hivyo kujikuta wakichakazwa
na risasi toka katika bastora za
Steven.Wote wanane walianguka
chini.Bado Steven aliendelea
kuzishikilia bastora zake mbili
zilizofuka moshi alizozifunga
kiwambo cha sauti huku akiwaangalia wale jamaa waliolala
chini wakivuja damu.Hakuna
aliyeonekana kuwa na uhai kati
yao.Hakuridhika akaendelea
kuwachakaza kwa risasi.
“Nina hasira na ninyi
mabazazi.Hizi ni salamu kwa hao
wakuu wenu.Nitahakikisha
ninawashughulikia mmoja baada
ya mwingine.Kitendo cha
kufungwa mwaka mzima bila hatia
kimeniumiza sana,mashetani
wakubwa nyie” akasema kwa
hasira Steven huku akiwageuza
kwa mguu wake kuhakiki kama
wote wamekufa.Sura zao hazikuwa
zikitazamika kwa namna
zilivyoharibiwa kwa risasi.Steve
alipohakikisha wote wamekufa
akawapekua na kuwakuta na
picha mbili za Elvis na ramani ya msitu ule,fedha pamoja na
misokoto ya bangi.Katika sanduku
kubwa walilokuwa nalo kulikuwa
na bastora sita ,risasi,bunduki
tatu aina ya SMG,mabomu mawili
ya kutupa kwa mkono,fulana za
kujikinga na risasi pamoja na
bunduki ya kivita yenye uwezo wa
kupiga masafa marefu
“Mabazazi hawa walikuwa
wamejiadaa mno.Elvis alifanya
vizuri sana kunishirikisha kwani
asingeweza kupambana nao peke
yake.Wangeweza kumuondoa
haraka sana” Akawaza Steven
akawavuta wale jamaa na
kuwaingiza ndani ya pango.Baada
ya kuwaficha pangoni akafukia
damu kwa udongo halafu
akachukua simu aliyopewa na Elvis kwa ajili ya mawasiliano
akampigia
“halow Steve” akasema Elvis
baada ya kupokea simu
“Elvis huku kazi imekwisha”
“What !! Elvis akashangaa
“Ninasema huku kazi
imekwisha.Njoo kwa amani .Huku
sinema imemalizika”
“Wow ! The ghost is back !!
Niko njiani ninakuja” akasema
Elvis
********************
“Sikukosea kumchukua
Steven anisaidie katika operesheni
hii.Ni kijana hodari mno na
mwenye uwezo wa
ajabu.Sikutegemea kabisa kama
angeweza kuimaliza kazi hii mapema namna hii.Lakini hata
hivyo lazima nichukue tahadhari
kubwa,inawezekana kabisa Steven
akawa amekamatwa na
anatumiwa na hawa jamaa ili
kunipa taarifa za uongo nisiende
nikiwa nimejihami ili iwe rahisi
kwao kunikabili” akawaza Elvis
Alitumia takribani saa moja
na dakika kumi na mbili kuwasili
kijiji cha Mpendae ulipo msitu wa
Ngezi.Akaegesha gari katika ofisi
ya chama akashuka na kuanza
kutembea kwa miguu kuelekea
msituni.Alitamani sana
kuwasiliana na Steven ili
kumfahamisha kwamba
amekaribia kufika msituni lakini
akaogopa
Hatimaye aliwasili msituni
akaiweka tayari bastora yake na kuanza kuingia ndani ya msitu
huu mkubwa wenye miti mikubwa
na kiza.Alitembea kwa tahadhari
kubwa sana akifuata maelekezo
aliyopewa na mkurugenzi wake
“Elvis ! Elvis ..unanipata
vizuri? Ilikuwa ni sauti ya Albert
Chukwe iliyosikika toka katika
kifaa kidogo cha mawasiliano
alichokiweka sikioni kwa ajili ya
kuwasiliana na akina Albert
“Nakupata vizuri sana
Albert.Tayari nimeingia msituni na
sasa ninaitafuta njia ya kuelekea
katika pango la Ngezi” akasema
Elvis kwa sauti ndogo
“Sawa,kuwa makini .Sisi
tayari tumekwisha wasili hapa
kijijini na tunasogea karibu na
msitu.Ukihitaji msaada tujulishe
mara moja.Mkurugenzi na Dr Philip nao wamekwisha wasili pia”
akasema Albert
“Sawa Albert” akasema Elvis
halafu akakivua kifaa kile sikioni
na kukitupa
“Sihitaji mawasiliano yoyote
tena na hawa vijana” akasema na
kuendelea kutembea kwa
tahadhari kuelekea katika
pango.Kwa kufuata maelekezo
aliyopewa na mkurugenzi
wake,Elvis alifanikiwa kufika
mahala lilipo pango la Ngezi
sehemu ambapo mpango wote wa
mauaji yake ulikuwa
ufanyike.Alijibanza nyuma ya mti
mkubwa akachunguza kwa makini
.Hakukuwa na mtu wala maiti
yoyopte maeneo yale.Takribani
dakika nne alikuwa amejificha
nyuma ya ule mti.Alitamani kuwasiliana na Steven kumjulisha
kuwa tayari amefika lakini
akasita.Baada ya tafakari ya muda
akaamua kujitokeza na kulikabili
pango huku akiwa na bastora
yake mkononi
Akiwa amejificha ndani ya
pango,Steven aliweza kuona kila
kilichokuwa kinaendela nje,hivyo
aliweza kumuona Elvis akitembea
kulielekea pango.Akasimama na
kuelekea nje ya pango.
Elvis alikuwa anatemba kwa
tahadhari kubwa na mara ghafla
akamuona mtu akitokea ndani ya
pango akiwa na bastora mkononi
kwa kasi ya ajabu akamuelekezea
bastora na kumtaka asimame pale
alipo.Mtu Yule akatupa chini
bastora yake na kunyoosha
mikono juu.Hakuweza kuonekanavizuri kutokana na kiza
kilichokuwamo ndani ya
pango.Elvis akamuamuru mtu
Yule atoke ndani ya pango na
mara akajikuta akitabasamu
baada ya kugundua mtu Yule ni
Steven
“Siku nyingine uwe unawahi
kujitambulisha vinginevyo
yanaweza kutokea maafa”
akasema Elvis
“Nilikuona nikiwa ndani ya
pango ndiyo maana nikatoka”
akasema Steven na kumuelezea
Elvis kila kitu kilichotokea halafu
wakaingia ndani ya pango
akamuonyesha maiti za wale
jamaa pamoja na silaha walizokuja
nazo
“Ahsante sana Steven.Bila
wewe ningepata wakati mgumu sana kukabiliana na hawa jamaa
waliokuwa wamejiandaa
vyema.Nadhani umeamini kuwa
mtandao huu tunaopambana nao
nao ni mtandao hatari .Tazama
aina ya silaha wanazozitumia,hizi
ni silaha za hali ya juu na za
kijeshi na inaonekana hawa jamaa
ni watu wenye mafunzo ya hali ya
juu.Endapo usingewawahi kabla
hawajajiandaa tungepata wakati
mgumu sana kukabiliana nao.Vipi
umewapekua tayari? Kuna
chochote umewakuta nacho?
Akauliza Elvis
“Nimewapekua lakini hakuna
kitu chochote cha
maana.walikuwa na ramani ya
msitu huu pamoja na picha zako
mbili .Vingine ni pesa taslimu
pamoja na misokoto ya bangi” “Ok hakuna cha kuweza
kutusaidia hapo.Una hakika
hakuna mtu yeyote aliyebakia?
“Nadhani hakuna kwani
endapo kungekuwa na mwingine
aliyebaki tayari angekwisha
jitokeza lakini hadi sasa hakuna
yeyote aliyejitokeza.Kingine cha
kushangaza kati ya hawa jamaa
wote hakuna hata mmoja
niliyemkuta na simu au kifaa
chochote cha
mawasiliano.Inawezekana
walifahamu kwamba katika
mapambano haya chochote
knaweza kutokea na hivyo
wakachukua tahadhari mapema
ya kudhibiti mawasiliano ili
isijulikane wametumwa na nani”
“Uko sahihi Steve lakini sisi
tayari tunafahamu wametumwa na nani hivyo tusipoteze wakati
kwa jambo hilo,twende mara moja
katika kazi yetu.Kitu cha kwanza
inabidi tuzitoe nje ya pango hizi
maiti ili zionekane” akasema Elvis
wakaanza kuziondoa maiti za wale
jamaa na kuziweka nje ya
pango.Baada ya zoezi hilo
kukamilika Elvis akachukua
fulana isiyopenya risasi akaiweka
chini halafu akachukau bastora
yake yenye kiwambo cha sauti na
kuimiminia risasi fulana ile kwa
karibu na kuitoboa toboa
“Kitakachofuata utachukua
bunduki moja ya hao jamaa na
kupiga risasi nyingi hewani ili
ionekane kana kwamba kuna
mapambano halafu nitampigia
simu mkurugenzi na kumtaarifu
kwamba kazi imekamilika.Nitaivaa fulana hii iliyotobolewa kwa risasi
na kujimwagia damu mwilini
nitaonekana kama nimechakazwa
kwa risasi na hapo itakuwa rahisi
watu kuamini kwamba haikua
rahisi kwa mimi kupona.Kila mtu
ataamini kweli nimekufa katika
mapambano” akasema Elvis
********************
 
I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 35

Elvis aliwasili ofisini kwao na
moja kwa moja akaelekea ofisini
kwa mkurugenzi wake Mr
MeshackJumbo.Silvia katibu
muhtasi wa mzee Jumbo
alimuelekeza aingie moja kwa
moja katika chumba cha mikutano
cha mkurugenzi ambako alikuwa
anasubiriwa.
Ndani ya chumba kile kidogo
cha mikutano walikuwamo watu
wawili ambao wote ni wafanyakazi
wa idara hii.Albert Chukwe na
Rosa Mkude.Nao pia waliitwa
katika kikao hiki bila kuelewa
wanaitiwa nini.Mara tu Elvis alipoingia mle chumbani
wakastuka na kujua kulikuwa na
shughuli kubwa kwanimara nyingi
kikao kinachomuhusisha pia Elvis
huwa ni kunakuwa na kazi.Elvis
akawasalimu na kupitisha utani
kidogo halafu mlango
ukafunguliwa akaingia
mkurugenzi.Buila kupoteza wakati
mkurugenzi akafungua kikao.
“Vijana wangu nimewaiteni
hapa kuna jambo la dharura
limetokea.Nadhani nyote
mnafahamu kwa kipindi Fulani
kulitopkea mashambulizi ya
mabomu jijini Arusha yaliyoua na
kujeruhi watu kadhaa.Uchunguzi
ulionyesha kwamba aliyefanya
mashambulio yale ni mtu
anayejulikana kama Abdullah
Abdullah.Huyu mtu anasakwa sana lakini mpaka sasa bado
hajapatikana .Ni mtu mwenye
mbinu za hali ya juu za kujificha”
MeshackJumbo akanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Leo asubuhi nimepokea
taarifa toka kwa chanzo chenye
uhakika kwamba Abdullah
anajificha katika msitu wa
Ngezi.Inasemekana kwamba
amekuwa akijificha hapo nyakati
za mchana na hutoka usiku
kwenda kujitafutia mahitaji mbali
mbali.Ndani ya msitu huo kuna
pango kubwa ambalo wenyeji
hulitumia kwa ibada za kimila na
Abdullah analitumia pango hilo
kama maficho yake.Taarifa hizo
zimetoka kwa chanzo cha uhakika
hivyo lazima tuzifanyie
kazi.Nimewaiteni hapa kuwafahamisha kwamba tunataka
tufanye uchunguzi wa suala hili
na tubaini kama ni kweli Abdullah
anaishi katika msitu huo wa Ngezi
kabla ya kuchukua hatua
nyingine” akasema mzee Jumbo
Elvis alionyesha sura ya
mstuko.Hakutaka wale vijana
wawili wang’amue kama tayari
alikuwa na taarifa zile.Akakohoa
kidogo na kusema
“Mkurugenzi sina lengo la
kuhoji wapi umepata taarifa hizi
lakini ninachotaka ni uthibitisho
toka kwako kama una uhakika na
taarifa hizi kwa sababu tumekua
tunapokea taarifa nyingi kama hizi
na baada ya kuzifanyia kazi
tunagundua hakukuwa na ukweli
wowote.Ninachohitaji ni wewe
kutuhakikishia kwamba una uhakika kwamba taarifa hizi
umezipata toka katika chanzo cha
kuaminika”
MeshackJumbo akamtazama
Elvis kwa macho makali na
kusema
“Elvis mimi ndiye mkurugenzi
wenu hapa na ndiye mwenye kauli
ya mwisho kuamua ni taarifa ipi
ya kweli na ipi si ya kweli.Hivyo
basi hadi kuwaiteni hapa na
kuwapa taarifa hizi nina uhakika
nazo”
“Ahsante sana mzee.Nilihitaji
tu uthibitisho wako.Hata hivyo
nina ombo moja.Umetueleza
kwamba tunatakiwa tufanye
kwanza uchunguzi kabla ya
kuchukua hatua nyingine.Mimi
naomba nijitolee nikafanye kwanza
uchunguzi mahala hapo na kisha nitawapa majibu nini hasa
kilichopo hapo Ngezi.Nataka
kwanza tupate picha kamili na
ndipo tutafaya maamuzi mazuri
zaidi ni hatu aipi tuichukue”
akasema Elvis.MeshackJumbo
akakuna kichwa na kusema
“Mawazo yako ni mazuri sana
Elvis na kwa kiasi Fulani naweza
kukubaliana nayo lakini Abdullah
ni mtu hatari sana na kama ni
kweli amejificha huko hatujui
amejihami vipi .Kwenda huko
Ngezi peke yako inaweza kuwa
hatari kubwa kwako.Hatuwezi
kuhatarisha maisha yako kiasi
hicho.Abdullah anajua kwamba
anatafutwa anajihami muda
wote.Mimi nadhani iundwe timu
ya watu muende huko msituni
mkafanye uchunguzi na baada ya hapo tutajua nini cha kufanya”
akasema MeshackJumbo
“Wazo lako ni zuri mzee lakini
katika hili napendekeza niende
kwanza peke yangu.Kupeleka timu
ya uchunguzi inaweza ikawa ni
hatari zaidi na kumfanya Abdullah
kama amejificha agundue na
atoroke.Nina hakika endapo
nikienda mwenyewe ninaweza
kupata kitu kizuri zaidi cha
kutusaidia.Endapo nitahitaji
msaada wa haraka basi
nitawataarifu” akashauri Elvis
“Mkurugenzi nadhani wazo la
Elvis ni la msingi” akasema Albert
“Lakini hata hivyo endapo
Elvis atakwenda peke yake katika
msitu huo basi kuwe na timu
ambayo itakuwa karibu ili kutoa
msaada wowote pindi ukihitajika.Abdullah hawezi kuwa
mwenyewe lazima atakuwa na
watu wanaomlinda na ni lazima
atakuwa amejihami hivyo lazima
tuwe karibu kumsaidia Elvis pindi
akihitaji msaada” akasema
MeshackJumbo
“Elvis utaingia msitunio
kufanya uchunguzi na sisi
tutakuwa maeneo ya karibu ili
kutoa msaada pale
utakapohitajika .Unaonaje kuhusu
wazo hili Elvis?akauliza mzee
Jumbo
“Ni wazo zuri pia lakini timu
hiyo ya msaada inabidi iwe mbali
kidogo ya msitu ili kutoweza
kuleta shaka yoyote hata kwa
wenyeji wanaouzunguka msitu
huo.Mimi nitakuwa nikiwasiliana
nanyi na kuwafahamisha kila kitu nitakachokiona na pindi nikiona
hatari yoyote nitawataarifu mara
moja” akasema Elvis
“Vizuri.Albert na Rosa
jiandaeni tutaondoka kwenda
kumsaidia Elvis .Ninyi
mtatangulia na mimi nitafuata
nyuma nikiwa na daktari wetu Dr
Philip.Elvis hakikisha mawasiliano
kati yako na sisi tulio nyuma yako
hayakatiki ili tujue nini
kinachoendelea ndani ya msitu”
akasema MeshackJumbo
“Usihofu
mzee.Nakuhakikishia kazi nzuri
na tutaufahamu ukweli” akasema
Elvis halafu wakainuka wote
wakaelekea kujiandaa
“Elvis suala hili naomba katu
usilifanyie mzaha hata
kidogo.Abdullaj ni mtu hatari.kama kweli amejificha
katika msitu huo basi hiyo si
sehemu salama hata kidogo”
akasema Albert wakati
wakijiandaa
“Usihofu Albert.Ninaenda
kufanya uchunguzi na si
kupambana.Hata hivyo nitakuwa
makini sana” akasema Elvis
Dakika kumi na tano tayari
Elvis alikwisha jandaa.Gari tatu
zilikuwa tayari na Elvis akamfuaa
mkurugenzi wake ofisini
“Mzee mimi natangulia”
“Elvis be carefully”
“I will” akasema Elvis na
kuingia katika gari akaondoka
kuelekea katika msitu wa Ngezi
****************** Dakika takribani kumi na
tano zilikatika bado Steven akiwa
ndani ya pango.Wale jamaa wanne
waliendelea kujadiliana jambo
huku wakigeukia mlango wa
pango mara kwa mara na
hatimaye mmoja wao akapiga
hatua kuelekea mlango wa pango
“hallow Mganga !! akapaaza
sauti .Steven aliyekuwa amejificha
nyumba ya jiwe alimuona na
kumsikia vizuri
“Mganga nakuomba umalize
shughuli zako na uondoke hapa
mara moja” akasema Yule jamaa
kwa sauti ya ukali.Zikapita
sekunde kadhaa bila ya Steven
kutokea au hata kuitika.Yule
jamaa akasema tena kwa ukali
“Mganga nakuomba kwa mara
ya mwisho toka huo ndani yapango haraka sana kabla sijaingia
na kukutoa kwa nguvu .Nakupa
dakika moja uwe umetoka humo
ndani!!
Steven aliyasikia maneo yale
na kuitabasamu
“Its show time” akawaza na
kuinuka akaanza kupiga hatua
kutoka mle ndani ya pango.Mara
tu alipotokeza wale jamaa
wakamtazama kwa hasira
“Samahani ndugu zangu kwa
kuwachelewesha kuanza shughuli
.Hata hivyo sikuwa nimemaliza
dawa nimeamua niwaache kwanza
mmalize kazi zenu na mimi
nitakuja baadae kumaliza dawa
zangu” akasema Steven huku
akipita pembeni yao.Wale jamaa
wakamtazama bila kumsemesha
kitu.Alipiga hatua kama tano hivi na ndipo kilipotokea kitu ambacho
wale jamaa hawakuwa
wamekitarajia.
Kwa kasi ya ajabu Steven
aliipandisha juu kanzu aliyoivaa
na kuzichomoa bastora mbili
alizozifutika kiunoni.Kwa wepesi
wa aina yake aliweza kuwaona
wale jamaa walivyokaa na bila
kupoteza hata sekunde moja
akaanza kuwamiminia risasi.Kwa
kuwa hawakuwa wametarajia kitu
kama kile kutokea wale jamaa
hawakuweza kujibu mashambulizi
na hivyo kujikuta wakichakazwa
na risasi toka katika bastora za
Steven.Wote wanane walianguka
chini.Bado Steven aliendelea
kuzishikilia bastora zake mbili
zilizofuka moshi alizozifunga
kiwambo cha sauti huku akiwaangalia wale jamaa waliolala
chini wakivuja damu.Hakuna
aliyeonekana kuwa na uhai kati
yao.Hakuridhika akaendelea
kuwachakaza kwa risasi.
“Nina hasira na ninyi
mabazazi.Hizi ni salamu kwa hao
wakuu wenu.Nitahakikisha
ninawashughulikia mmoja baada
ya mwingine.Kitendo cha
kufungwa mwaka mzima bila hatia
kimeniumiza sana,mashetani
wakubwa nyie” akasema kwa
hasira Steven huku akiwageuza
kwa mguu wake kuhakiki kama
wote wamekufa.Sura zao hazikuwa
zikitazamika kwa namna
zilivyoharibiwa kwa risasi.Steve
alipohakikisha wote wamekufa
akawapekua na kuwakuta na
picha mbili za Elvis na ramani ya msitu ule,fedha pamoja na
misokoto ya bangi.Katika sanduku
kubwa walilokuwa nalo kulikuwa
na bastora sita ,risasi,bunduki
tatu aina ya SMG,mabomu mawili
ya kutupa kwa mkono,fulana za
kujikinga na risasi pamoja na
bunduki ya kivita yenye uwezo wa
kupiga masafa marefu
“Mabazazi hawa walikuwa
wamejiadaa mno.Elvis alifanya
vizuri sana kunishirikisha kwani
asingeweza kupambana nao peke
yake.Wangeweza kumuondoa
haraka sana” Akawaza Steven
akawavuta wale jamaa na
kuwaingiza ndani ya pango.Baada
ya kuwaficha pangoni akafukia
damu kwa udongo halafu
akachukua simu aliyopewa na Elvis kwa ajili ya mawasiliano
akampigia
“halow Steve” akasema Elvis
baada ya kupokea simu
“Elvis huku kazi imekwisha”
“What !! Elvis akashangaa
“Ninasema huku kazi
imekwisha.Njoo kwa amani .Huku
sinema imemalizika”
“Wow ! The ghost is back !!
Niko njiani ninakuja” akasema
Elvis
********************
“Sikukosea kumchukua
Steven anisaidie katika operesheni
hii.Ni kijana hodari mno na
mwenye uwezo wa
ajabu.Sikutegemea kabisa kama
angeweza kuimaliza kazi hii mapema namna hii.Lakini hata
hivyo lazima nichukue tahadhari
kubwa,inawezekana kabisa Steven
akawa amekamatwa na
anatumiwa na hawa jamaa ili
kunipa taarifa za uongo nisiende
nikiwa nimejihami ili iwe rahisi
kwao kunikabili” akawaza Elvis
Alitumia takribani saa moja
na dakika kumi na mbili kuwasili
kijiji cha Mpendae ulipo msitu wa
Ngezi.Akaegesha gari katika ofisi
ya chama akashuka na kuanza
kutembea kwa miguu kuelekea
msituni.Alitamani sana
kuwasiliana na Steven ili
kumfahamisha kwamba
amekaribia kufika msituni lakini
akaogopa
Hatimaye aliwasili msituni
akaiweka tayari bastora yake na kuanza kuingia ndani ya msitu
huu mkubwa wenye miti mikubwa
na kiza.Alitembea kwa tahadhari
kubwa sana akifuata maelekezo
aliyopewa na mkurugenzi wake
“Elvis ! Elvis ..unanipata
vizuri? Ilikuwa ni sauti ya Albert
Chukwe iliyosikika toka katika
kifaa kidogo cha mawasiliano
alichokiweka sikioni kwa ajili ya
kuwasiliana na akina Albert
“Nakupata vizuri sana
Albert.Tayari nimeingia msituni na
sasa ninaitafuta njia ya kuelekea
katika pango la Ngezi” akasema
Elvis kwa sauti ndogo
“Sawa,kuwa makini .Sisi
tayari tumekwisha wasili hapa
kijijini na tunasogea karibu na
msitu.Ukihitaji msaada tujulishe
mara moja.Mkurugenzi na Dr Philip nao wamekwisha wasili pia”
akasema Albert
“Sawa Albert” akasema Elvis
halafu akakivua kifaa kile sikioni
na kukitupa
“Sihitaji mawasiliano yoyote
tena na hawa vijana” akasema na
kuendelea kutembea kwa
tahadhari kuelekea katika
pango.Kwa kufuata maelekezo
aliyopewa na mkurugenzi
wake,Elvis alifanikiwa kufika
mahala lilipo pango la Ngezi
sehemu ambapo mpango wote wa
mauaji yake ulikuwa
ufanyike.Alijibanza nyuma ya mti
mkubwa akachunguza kwa makini
.Hakukuwa na mtu wala maiti
yoyopte maeneo yale.Takribani
dakika nne alikuwa amejificha
nyuma ya ule mti.Alitamani kuwasiliana na Steven kumjulisha
kuwa tayari amefika lakini
akasita.Baada ya tafakari ya muda
akaamua kujitokeza na kulikabili
pango huku akiwa na bastora
yake mkononi
Akiwa amejificha ndani ya
pango,Steven aliweza kuona kila
kilichokuwa kinaendela nje,hivyo
aliweza kumuona Elvis akitembea
kulielekea pango.Akasimama na
kuelekea nje ya pango.
Elvis alikuwa anatemba kwa
tahadhari kubwa na mara ghafla
akamuona mtu akitokea ndani ya
pango akiwa na bastora mkononi
kwa kasi ya ajabu akamuelekezea
bastora na kumtaka asimame pale
alipo.Mtu Yule akatupa chini
bastora yake na kunyoosha
mikono juu.Hakuweza kuonekanavizuri kutokana na kiza
kilichokuwamo ndani ya
pango.Elvis akamuamuru mtu
Yule atoke ndani ya pango na
mara akajikuta akitabasamu
baada ya kugundua mtu Yule ni
Steven
“Siku nyingine uwe unawahi
kujitambulisha vinginevyo
yanaweza kutokea maafa”
akasema Elvis
“Nilikuona nikiwa ndani ya
pango ndiyo maana nikatoka”
akasema Steven na kumuelezea
Elvis kila kitu kilichotokea halafu
wakaingia ndani ya pango
akamuonyesha maiti za wale
jamaa pamoja na silaha walizokuja
nazo
“Ahsante sana Steven.Bila
wewe ningepata wakati mgumu sana kukabiliana na hawa jamaa
waliokuwa wamejiandaa
vyema.Nadhani umeamini kuwa
mtandao huu tunaopambana nao
nao ni mtandao hatari .Tazama
aina ya silaha wanazozitumia,hizi
ni silaha za hali ya juu na za
kijeshi na inaonekana hawa jamaa
ni watu wenye mafunzo ya hali ya
juu.Endapo usingewawahi kabla
hawajajiandaa tungepata wakati
mgumu sana kukabiliana nao.Vipi
umewapekua tayari? Kuna
chochote umewakuta nacho?
Akauliza Elvis
“Nimewapekua lakini hakuna
kitu chochote cha
maana.walikuwa na ramani ya
msitu huu pamoja na picha zako
mbili .Vingine ni pesa taslimu
pamoja na misokoto ya bangi” “Ok hakuna cha kuweza
kutusaidia hapo.Una hakika
hakuna mtu yeyote aliyebakia?
“Nadhani hakuna kwani
endapo kungekuwa na mwingine
aliyebaki tayari angekwisha
jitokeza lakini hadi sasa hakuna
yeyote aliyejitokeza.Kingine cha
kushangaza kati ya hawa jamaa
wote hakuna hata mmoja
niliyemkuta na simu au kifaa
chochote cha
mawasiliano.Inawezekana
walifahamu kwamba katika
mapambano haya chochote
knaweza kutokea na hivyo
wakachukua tahadhari mapema
ya kudhibiti mawasiliano ili
isijulikane wametumwa na nani”
“Uko sahihi Steve lakini sisi
tayari tunafahamu wametumwa na nani hivyo tusipoteze wakati
kwa jambo hilo,twende mara moja
katika kazi yetu.Kitu cha kwanza
inabidi tuzitoe nje ya pango hizi
maiti ili zionekane” akasema Elvis
wakaanza kuziondoa maiti za wale
jamaa na kuziweka nje ya
pango.Baada ya zoezi hilo
kukamilika Elvis akachukua
fulana isiyopenya risasi akaiweka
chini halafu akachukau bastora
yake yenye kiwambo cha sauti na
kuimiminia risasi fulana ile kwa
karibu na kuitoboa toboa
“Kitakachofuata utachukua
bunduki moja ya hao jamaa na
kupiga risasi nyingi hewani ili
ionekane kana kwamba kuna
mapambano halafu nitampigia
simu mkurugenzi na kumtaarifu
kwamba kazi imekamilika.Nitaivaa fulana hii iliyotobolewa kwa risasi
na kujimwagia damu mwilini
nitaonekana kama nimechakazwa
kwa risasi na hapo itakuwa rahisi
watu kuamini kwamba haikua
rahisi kwa mimi kupona.Kila mtu
ataamini kweli nimekufa katika
mapambano” akasema Elvis
********************
Kazi nzuri sana
 
Back
Top Bottom