I DIED TO SAVE PRESDANT
Sehemu 36
Milio ya risasi iliyovuma
mfululizo iliwastua
MeshackJumbo na Dr Philip
waliokuwa kandoni mwa msitu wa
Ngezi wakisubiri kupewa taarifa na
Elvis
“Ee Mungu msaidie Elvis”
akasema MeshackJumbo kwa
sauti ndogo “Inaonekana mapambano ni
makali kwa namna risasi
zinavyorindika” akasema Dr Philip
kwa wasiwasi
Baada ya dakika kama kumi
hivi za kusikika milio ya risasi
mfululizo kukawa kimya na simu
ya MeshackJumbo ikaita.Alikuwa
ni Elvis.MeshackJumbo akaipokea
simu ile
“hallow” akasema
“mzee mnaweza kuja ,kazi
imemalizika” akasema Elvis
MeshackJumbo akashusha
pumzi na kusema
“wote mko salama?
“tuko salama mzee” akasema
Elvis na kukata simu
Baada ya kuwasiliana na
Elvis MeshackJumbo akampigia simu Albert aliyekuwa katika
upande mwingine wa msitu
“Albert najaribu kuwasiliana
na Elvis lakini mawasiliano
yamekuwa magumu hapatikani,ni
wakati wa kuingia msituni kumpa
msaada.Yawezekana amezidiwa
nguvu.Mimi na Dr Philip
tunaelekea pangoni wewe na
mwenzako elekeeni upande wa
mashariki ambako kuna njia ya
kutokea ili kuwadhibiti wale
watakaojaribu kutoroka” akasema
mzee Jumbo na kukata
simu.Wakiwa na bastora mikononi
wakaanza kutembea kuelekea
ndani ya msitu kuliendea pango la
Ngezi
Elvis alikuwa amelala chini
pembeni ya jiwe akiwa amevaa
fulana yenye matundu mengi yarisasi.Alikuwa ametapakaa damu
mwili mzima.MeshackJumbo
aliogopa mno alipomuona Elvis
katika hali ile,akaitupa chini
bastora yake na kumuendea
“Elvis..Elvis !! akaita
“Elvis akafumbua macho na
kutazama pande zote akamuona
mkurugenzi wake pamoja na Dr
Philip akainuka na
kukaa.MeshackJumbo akashusha
pumzi.
“Dah ! tayari nilikwisha anza
kuogopa.Pole sana Elvis kwa
mapambano.Haikuwa kazi rahisi
kukabiliana na hii mijitu”
akasema mzee Jumbo huku
akiikodolea macho miili ya wale
watu waliouliwa na Steven
“Steven yuko wapi? Akauliza
Meshack Amekwisha maliza kazi yake
na kuondoka.Hata sisi hatutakiwi
kuchukua muda mrefu
hapa.Tumalize kazi yetu
tuondoke.Milio ya risasi iliyosikika
itawavuta wanakijiji waje haraka
eneo hili” akasema Elvis
Haraka haraka Elvis akajilaza
chini na kwa kutumia simu ya
mkononi MeshackJumbo
akampiga picha pamoja na miili ile
ya watu aliowaua Steven halafu
akampa nafasi Dr Philip afanye
kazi yake.Haraka haraka
akafungua mkoba wake na kutoa
chupa ya dawa akaivuta katika
bomba la sindano akamfuata Elvis
na kumchoma
“Sasa anza kuhesabu kuanzia
kumi kushuka chini” akasema Dr
Philip ten..nine…..eigh..t….sev…ee.
.e……” akashindwa kuendelea na
kupoteza fahamu
“Good.Kazi tayari” akasema
Dr Philip
Mzee Jumbo akachukua simu
na kumpigia Albert
“Albert naomba mje haraka
sana hapa pangoni,tunahitaji
msaada wa haraka .Elvis kapigwa
risasi na hali yake ni mbaya”
akasema mkurugenzi na kumstua
Albert
“Sawa mzee tunakuja sasa
hivi” akasema Albert
Kwa mtu yeyote ambaye
angemuona Elvis namna alivyolala
pale chini ni wazi angeamini
hakuwa na uhai tena.Alikuwa
ametapakaa damu mwili mzima Akina albert walifika haraka
sana na kustushwa na hali
waliyoikuta pale.Rosa akashindwa
kujizuia kutoa machozi.
“Vijana hatuna muda wa
kupoteza,tunatakiwa kumkimbiza
Elvis hospitali ili kuyaokoa maisha
yake” akasema
MeshackJumbo.Wakasaidiana
kumuinua Elvis na kuelekea liliko
gari la MeshackJumbo
“Nilimtahadharisha Elvis
kuhusu kuja peke yake mahala
hapa.Nilijua lazima kuna hatari
kubwa eneo hili” akasema Albert
kwa hasira
Njiani walikutana na kundi la
raia wakiwa na silaha za jadi
wakielekea katika msitu baada ya
kusikia milio ya risasi.Mkurugenzi
akajitambulisha kwao na kuwaleza kilichotokea na kisha raia wale
wakasaidia kumbeba Elvis hadi
katika gari la Meshack.
“Albert utabaki hapa na Rosa
mkiendelea na uchunguzi wa eneo
hili kubaini kama kweli Abdullah
anaishi hapa.Mimi na Dr Philip
ngoja tumkimbize Elvis hospitali
tujaribu kuokoa maisha
yake.Nitawataarifu polisi na
watafika hapa mara moja”
akasema MeshackJumbo na
kuingia garini wakaondoka kwa
kasi kubwa
********************
Makamu wa rais wa jamhuri
ya muungano wa Tanzania Dr
Shafi Abdulkhareem Omar
alikuwa ofisini kwake akiendelea na kazi mara simu yake ya
mkononi ikaita.Alikuwa ni
Meshack
“Hallo Meshack” akasema Dr
Shafi
“Mkuu ile kazi tayari
imekamilika.Elvis amekwisha
uawa.Nitakurushia picha zake
sasa hivi”
“Good ! hakukuwa na
mapambano makubwa au jambo
lolote linaloweza kutia shaka
katika kifo chake?
“Yalitokea mapambano ya
kurushiana risasi kwa takribani
dakika ishirini hivi kati ya Elvis na
wale vijana na wote wanne
wameuawa.Elvis mwenyewe
amefia njiani wakati akipelekwa
hospitali alikuwa amejeruhiwa
sana” Mhh …..!! Dr Shafi akaguna
“Kumbe huyu kijana alikuwa
hatari mno.Kwa sasa uko wapi
Meshack?
“Niko hapa Rajesh hospitali
nikifanya taratibu za kuuhifadhi
mwili wa Elvis kabla ya taratibu
nyingine kufuata”
Dr Shafi akainama akafikiri
kwa muda kidogo halafu akasema
“Meshackahsante sana.Mzigo
wako niliokuahidi utapelekwa
nyumbani kwako.Kuwa karibu na
familia ya marehemu na kama
kuna chochote kinahitajika
nitaarifu nami nitatoa”
Mara tu alipomaliza kuongea
na MeshackJumbo Dr Shafi
akampigia simu waziri mkuu
mstaafu David Mlingo hallow Dr Shafi” akasema
David baada ya kupokea simu
“David nimekupigia
kukufahamisha kwamba ile kazi
imekamilika.Yule kijana tayari
amekwisha ondolewa kwa hiyo
amani imetamalaki.Mambo yote
sasa yanakwenda vizuri”
Akiwa ndani ya gari David
akashusha pumzi na usoni
pakajengeka tabasamu zito.
“Ahsante sana Dr Shafi kwa
taarifa hizi nzuri.Sasa kazi zetu
zitafanyika vizuri bila ya
kipigamizi .Good job Dr Shafi”
akasema Davidf
“Sawa David.Hata hivyo vijana
wote wanane waliotumwa kuifanya
kazi hii wameuawa.Yule kijana
alikuwa hatari mno” Usijali kuhusu hilo Dr
Shafi.Haijalishi ni vijana wangapi
tumewapoteza lakini kikubwa ni
kwamba wamefanikiwa
kumuondoa Elvis ambaye alikuwa
ni kikwazo kikubwa sana
kwetu.Kinachotakiwa kufanyika ni
kuhakikisha kwamba hakuna
uchunguzi wowote utakaofanyika
kuhusiana na vifo hivyo.Endapo
wakifanya uchunguzi wanaweza
wakafika mbali na kugundua
mambo mengine ya siri ambayo
hawapaswi kuyajua.Unatakiwa
kulidhibiti hilo”
“Usijali David .Suala hilo liko
ndani ya uwezo wangu na
nitalishughulikia.Ninachowaomba
kila mmoja kwa upande wake
afanye namna
inavyotakiwa.Endapo kuna jambo lolote ambalo unadhani ninaweza
kulitatua kwa upande wangu
usisite kunijulisha mara moja”
“Nimekuelewa Dr Shafi tuko
makni sana na jambo hili na
tunajitahidi kufanya kazi kwa
kujituma na nina uhakika mpango
wetu utafanikiwa.Jioni ya kesho
tutakuwa na kikao na
nitakufahamisha yale yote
yatakayoongelewa katika kikao
hicho” akasema David kisha
wakaagana
“Hii ni hatua kubwa mno
tumeipiga.Elvis alikuwa mtu
hatari kwetu na alihatarisha
mpango wetu.Kwa sasa tuko huru
kuendelea na mpango
wetu.Ninaanza tena kupata
matumaini ya kuingia ikulu
nikiwa rais wa Tanzania” akawaza David huku akizitafuta namba za
brigedia Frank akampigia
“hallow david” akasema Frank
baada ya kupokea simu
“Frank nimepata taarifa sasa
hivi toka kwa Dr Shafi.Elvis tayari
ameondolewa japokuwa
tumewapoteza vijana wetu
wote.Kikwazo kimeondolewa
tuitumie vyema nafasi hii kuweka
sawa mipango”
“Hizi ni taarifa nzuri
sana.Nilikuwa na wasi wasi
mwingi kwani ninasikia Yule
kijana alikuwa na uwezo wa hali
ya juu.Kwa sasa naweza kusema
njia ni nyeupe na tunaweza
kuendelea na mipango yetu bila
vipingamizi vikubwa”
“Kweli kabisa
Frank,tunatakiwa tuongeze kasi tufanye mambo yaende haraka
haraka.Nadhani katika kikao cha
jioni ya kesho tutaongea zaidi juu
ya suala hili na hatua inayofuata”
akasema David wakaagana na
kukata simu
“Nashukuru yule
mwanaharamu amekufa.Alikuwa
ananipa mawazo sana.kwa sasa
natakiwa kujua mahala alipo
Graca.Yule naye bado ni hatari
kwangu.Naamini kumpata
itakuwa kazi nyepesi kwani mtu
aliyekuwa anamtegemea
amefariki.Huyu ndiye aliyeuza siri
zetu kwa Elvis” akawaza Frank
******************
Hali ya simanzi ilitawala
katika jengo zima la ofisi za idara ya ujasuri baada ya taarifa za kifo
cha Elvis kuwafikia wafanyakazi
wenzake.Haikuwa rahisi kuamini
kama kweli Elvis amekufa hadi
walipothibitishiwa na Albert
namna alivyoshambuliwa
MeshackJumbo aliwasili
ofisini na kukuta shughuli
zimesimama na watu
wamesimama kivikundi
wakijadiliana kuhusiana na kifo
cha Elvis.Meshackakawaita wote
katika ukumbi wa mikutano
“Naamini tayari nyote mnazo
taarifa za kile kilichotokea leo”
akanyamaza kidogo na kuendelea
“Asubuhi ya leo nilipokea
taarifa inayomuhusu mtu
tunayemtafuta kwa muda mrefu
ambaye anatuhumiwa kuratibu
mashambulio ya mabomu katikajiji la Arusha ambaye ni Abdullah
Abdullah.Kwa mujibu wa taarifa
hiyo niliyoipata ni kwamba
Abdullah amejificha katika msitu
wa Ngezi.Niliitisha kikao cha
dharura na baada ya
majadiliano.Mimi,Elvis ,Albert na
Rosa tulikubaliana kwenda
kufanya uchunguzi katika msitu
huo kuhusiana na hizo
taarifa.Pamja nasi alikuwepo pia
daktari wetu Dr Phlip.Tulipofika
msituni tulijipanga na kuanza kazi
lakini wakati tukiendelea ilisikika
milio ya risasi ikatulazimu
kuingia ndani ya msitu kumsaidia
Elvis aliyekuwa ametangulia
.Tulipomfikia hakuweza kuongea
chochote kwani alikuwa
ameshambuliwa kwa risasi nyingi
.Tulimpakia garini ili kumkimbiza hospitali tukijaribu kuokoa
maisha yake lakini hakuweza
kufika hospitali.Amefariki dunia
tukiwa njiani kuelekea hospitali”
MeshackJumbo akanyamaza na
kuinamisha kichwa.
“Shambulio lile” akaendelea
“Linatufanya tuamini kwamba
inawezekana ni kweli Abdullah
alikuwa anautumia msitu wa
Ngezi kama maficho
yake.Tutamsaka Abdullah kokote
aliko na tutahakikisha tunampata
akiwa hai au amekufa”
akanyamaza tena kidogo halafu
akaendelea
“Taratibu za msiba
zinaendelea na
tutawataarifuni.Ndugu zangu
nafahamu nyote mmeumizwa sana
kwa taarifa hizi kwani Elvis alikuwa ni kipenzi wa kila mmoja
hapa ofisini lakini tujikaze na
tuendelee na kazi” akasema
MeshackJumbo halafu akaelekea
ofisini kwake akajiegemeza katika
kiti na kuelegeza tai
“Uuuuphh !!akashusha pumzi
“Hatua ya kwanza
imemalizika.We saved Elvis.Kila
mtu kwa sasa anaamini Elvis
tayari amekufa.Kinachofuata ni
hatua ya pili ambayo ni ngumu
zaidi nayo ni kumzika na
kuwafanya watu wote waamini
kwamba Elvis amekufa na
kuzikwa” Akawaza MeshackJumbo
“kabla ya yote natakiwa
kwanza kumtaarifu mke wake
Patricia kuhusiana na tukio
hili.Najua ni jambo zito mno
kwake lakini hakuna namna lazima ajue.Natumai huko mbeleni
ataelewa na watasemeheana”
Mzee jumbo akainuka kitini
akatoka mle ofisini akaingia katika
gari lake na kuondoka.Ilimchukua
zaidi ya dakika arobaini kufika
katika hospitali anayofanya kazi
Patricia.Alielekezwa mahala
anakoweza kumpata Dr
Patricia.Toka mapokezi akatembea
kwa haraka kuelekea katika jengo
aliloelekezwa iliko ofisi ya Dr
Patricia
Ilimlazimu kumsubri kidogo
kwani kwa muda huo alikuwa
katika kazi ya dharura.Baada ya
kama nusu saa hivi akatokea
“Mhh !! what a pretty woman”
akawaza Meshackbaada ya
kumuona Patricia“Shikamoo mzee” Patricia
akamsalimu
“Marahaba Patricia.Pole na
kazi”
“Ahsante mzee.karibu sana”
“Nashukuru Dr Patricia”
Akasema MeshackJumbo halafu
kikapita kimya
kifupi.MeshackJumbo hakujua
aanzie wapi kumweleza Patricia
.Akakohoa kidogo na kusema
“Uhhmm,Patricia mimi naitwa
MeshackJumbo ni mkuu wa kazi
wa mumeo Elvis” akaanzisha
maongezi mzee Jumbo.Sura ya
Patricia ikaonyesha wasiwasi
kidogo
“Nafurahi kukufahamu mzee”
akasema Patricia
“Patricia nimekuja mimi
mwenyewe kuongea nawe kukupa taarifa muhimu.Najua wewe ni
mwanamke jasiri na ninakuomba
uendelee kuwa jasiri” Jumbo
akanyamaza na kumeza
mate.mapigo ya moyo ya Patricia
yalibadilika na kuanza kwenda
kasi.Mzee Jumbo akaendelea
“Nadhani unaifahamu kazi
anayoifanya mumeo na
ninathubutu kusema kwamba
taifa linajivunia kuwa na mtu
kama Elvis.Ni kijana wa aina yake
aliyefanya mengi katika nchi
hii.Nathubutu kusema kuwa
katika idara yetu yeye ndiye
tegemeo” akanyamaza kidogo na
kuendelea
“Kazi zetu zinezungukwa na
hatari nyingi muda wote na hivyo
kutufanya tusiwe na maisha ya
kawaida.Nadhani utakubaliana nami kuhusu hilo” akanyamaza
tena akamtazama Patricia aliyejaa
wasiwasi kisha akaendelea
“leo asubuhi kuna kazi
iliyojitokeza na ambayo ilimlazimu
Elvis kwenda kuishughulikia
.Katikati ya shughuli hiyo
aliyokuwa anaifanya lilitokea
shambulio la ghafla toka kwa watu
aliokuwa anawafuatilia .Watu hao
wanne walimshambulia Elvis hata
hivyo kwa umahiri na uwezo
mkubwa aliokuwa nao aliweza
kupambana nao wote kuwaua
wote na yeye kuumizwa vibaya
sana”
Kauli ile ya mzee Jumbo
ikamstua Patricia akajikuta
amesimama na kushika
kichwa.Kijasho chembamba cha
woga kikamtoka Where is my husband? is he
okay? Akauliza Patricia kwa
woga.MeshackJumbo akasimama
na kumtuliza akamsihi
aketi.Tayari machozi yalianza
kumdondoka
“Tafadhali niambie
mzee,mume wangu yuko wapi?
Ana hali gani? Akauliza Patricia
huku akilia
“Please Patricia you have to be
strong” akasema Meshack.Patricia
akamtazama MeshackJumbo kwa
macho makali na kusema
“Tell me where’s my
husband?I want to see him now !!!
“Patricia..” akasema mzee
Jumbo na kunyamaza
“Elvis alikuwa ameumizwa
sana ,tulimpakia garini ili
kumkimbiza hospitali na kwa bahati mbaya hakuweza kufika
hospitali akafariki du…………”
Mzee Jumbo hakumaliza
sentesi yake,Patricia akaanguka
na kupoteza fahamu
“Inauma sana lakini lazima
tufanye hivi” akawaza
MeshackJumbo na kuomba
msaada kwa wauguzi waliokuwa
karibu
******************
Tayari kiza kimekwisha tanda
na ilipata saa mbili kasoro za
usiku Elvis alipofumbua macho
baada ya kuchomwa sindano ya
kumzindua
“Oh ,thank God.He’s awake”
akasema Dr Philip huku
akishusha pumzi.Pembeni yakealikuwepo Dr Rajesh patel mmiliki
wa hospitali hii kubwa.Philip na
patel ni marafiki wakubwa wote
walikutana masomoni nchini
Cuba.Wamekuwa marafiki
wakubwa kwa muda mrefu na
ndiyo sababu haikuwa vigumu
kwa Dr patel kukubali kumsaidia
Dr Philip katika mpango ule
“Pole sana Philip.Hili ni jambo
zito na la hatari hata hivyo
tutafanikiwa” akasema Dr Rajesh
“Ahsante.Ni jambo la hatari
lakini lazima lifanyike” akajibu
Philip huku akichuku kipimo na
kumpima Elvis
“Kila kitu kinakwenda vizuri”
Akasema Dr Philip
“Kinachofuata sasa ni
kumpeleka nyumbani
kumpumzisha kwani bado fahamu hazijamrejea sawa sawa” Dr Philip
na Dr Rajesh walijadiliana kwa
dakika kadhaa namna
watakavyoweza kumtoa Elvis pale
hospitali .Dr Rajesh akatoka na
baada ya dakika kadhaa akarejea
akiwa na gari la wagonjwa .Elvis
akafunikwa shuka na kuwekwa
katika kitanda cha magurudumu
na kwa haraka wakamtoa mle
ndani ya chumba maalum
alimokuwa amewekwa na
kuingizwa garini na gari
likaondoka
“Rajesh ahsante sana
.Ninauthamini mno mchango wako
katika operesheni hii”
“Usijali Dr Philip.Huu ni
msaada mdogo ukilinganisha na
mengi ambayo umekuwa
unanisaidia .Umenisaidia mambo mengi sana na zaidi ya yote suala
hili ni kwa ajili ya usalama wa
nchi yetu na majirani zetu”
akasema Dr Rajesh
Toka Rajesh
hospital,walielekea Yamazuka
Hospitali ambako Dr Philip
hufanya kazi katika muda wa
ziada.Elvis akashushwa na
kuingiza moja kwa moja ofisini
kwa Dr Philip na kupumzishwa
kitandani.Dr Philip na Rajesh
wakaagana Rajesh
akaondoka.hakuna mtu yeyote
aliyemtilia shaka wala kumuuliza
kuhusu mgonjwa aliyekuja naye
Dr Philip kwani ni kawaida yake
kuja na wagonjwa mbali mbali na
kuwatibu kisha kuondoka.Baada
ya Rajesh kuondoka Dr Philp
akampigia simu MeshackJumbo Hallow Dr Philip” akasema
Mzee Jumbo
“Mzee mambo yamekwendaje
huko? Akauliza dr Philip
“Mambo yanakwenda vizuri
japokuwa si rahisi kama
tulivyotarajia.Sijapata bado hata
muda wa kupumzika.Kwa sasa
niko hapa nyumbani kwa mama
yake Elvis ulipo msiba.Mke wake
bado anapatiwa msaada wa
kitabibu kwani amekuwa
anapoteza fahamu mara kwa mara
toka alipopata taarifa hizi.Philip
jambo hili limewaumiza watu
wengi lakini hatuna namna
nyingine ya kufanya.Nina imani
huko mbeleni watatusamehe
baada ya kugundua nini lilikuwa
lengo la kufanya hivi.Wewe uko
wapi sasa hivi? Akauliza Jumbo “Niko hapa ofisini kwangu
Yamazuka .Elvis amekwisha
zinduka japokuwa bado
hajarejewa na fahamu zake
kamili.Nimempumzisha hapa kwa
muda kabla ya kumpeleka
nyumbani kwake.Msaada
ninaouhtaji kwa sasa ni namna ya
kumtoa hapa na kumpepeleka
mahala anakoishi kwani
sipafahamu”
“Kazi nzuri sana Dr Philp.Hizi
ni dalili njema kwamba
tutafanikiwa zoezi letu.Mpaka sasa
wale jamaa wamekwisha amini
kwamba Elvis amekufa na
nilimtumia makamu wa rais picha
za Elvis akiwa eneo la tukio kule
Ngezi na ameamini.Kuhusu
kumpeleka kwake nitamtuma
Steven aje hapo sasa hivi.Mimi bado nitaendelea kukaa hapa
nikisaidiana na ndugu za Elvis
kuweka sawa mambo.Nikitoka
hapa nitaelekea moja kwa moja
hospitali kujua maendeleo ya
Patricia.Hiki ni kipindi ambacho
yatupasa kusahau kabisa usingizi
na kufanya kazi usiku na mchana”
“Ok mzee tutakutana
nyumbani kwa Elvis” akasema Dr
Philip na kukata simu
Alipomaliza kuongea na Dr
Philip,MeshackJumbo akampiga
simu Steven na kumpa taarifa
kuhusu Elvis na kumuelekeza
aende Yamazuka Hospital
akamchukue
“Sipati picha namna watu
hawa wanaopoteza fahamu kiasi
hiki wakigundua kwamba jambo
hili ni la uongo.Sijui nini kitatokea” akawaza Meshackbaada
ya kurejea ndani na kuona watu
kama sita hivi wakiwa
wanapepewa baada ya kupoteza
fahamu huku wengine wakilia kwa
uchungu
*****************
Steven na Dr Philip
walisaidiana kumuingiza Elvis
garini halafu wakaondoka .Safari
ilikuwa ya kimya kimya hadi
walipowasili nyumbani.Taratibu
Elvis akatembea kuingia
ndani.Doreen aliyekuwa
amesimama mlangoni
akamkimbilia kutaka
kumkumbatia lakini Steven
akamzuia na kumuingiza ndani,
akampeleka chumbani kwake.Graca alibaki anashangaa
kumuona Elvis akiwa katika hali
ile.
“Dada Doreen kitu gani
kinaendelea?Elvis amepatwa na
nini hadi akawa katika hali
ile?Mbona anaonekana mgonjwa
sana? Graca akamuuliza Doreen
ambaye alikuwa ameegemea ukuta
“Relax Graca.He’s fine”
akajibu Doreen
“Relax ?!! Graca akahamaki
“Something is wrong with him
and I know you know what’s going
on but you don’t tell me.Toka
asubuhi nimekuwa nikikuuliza
alipo Elvis umekuwa unanipa
majibu ya mkato.Nataka
kufahamu Elvis ana matatizo
gani?Nijibu tafadhali kwani Elvis
ndiye pekee ninayemtegemea sasa hivi.Usalama wangu unamtegemea
yeye”
Doreen akamfuata akamshika
mkono na kumketisha sofani
“Ni kweli Graca kuna jambo
linaendelea hapa lakini Elvis
amenizuia nisikueleze
chochote.Atakueleza yeye
mwenyewe nini kinaendelea”
Doreen akasema.Graca
akamtazama kwa wasi wasi
mkubwa
“Usiwe na wasi wasi
Graca.Elvis yuko sawa”
“Dada Doreen nashindwa
kujizuia kutokuwa na wasiwasi
kwa sababu yeye ndiye kila kitu
kwangu.Usalama wa maisha
yangu unamtegemea yeye kwa
kiasi kikubwa” Nalifahamu hilo Graca na
ndiyo maana ninakuhakikishia
kwamba Elvis yuko sawa”
“Na hawa jamaa alioongozana
nao ni akina nani? Unawafahamu?
Akauliza Graca
“Wale ni wafanyakazi
wenzake.Usiwe na shaka nao hata
kidogo” Akasema Doreen na mara
Steven akaingia pale sebuleni
akastuka alipokutanisha macho
na Graca
“Mhh !! Elvis anawatoa wapi
watoto wazuri kama hawa? Nahisi
huyu ndiye yulebinti aliyeniambia
alienda kumchukua afrika
kusini.She’s amazing” akawaza
Steve halafu akakohoa kidogo na
kusema
“Doreen tunahitaji chakula
chepesi kwa ajili ya Elvis” Kwa haraka Doreen akainuka
na kuelekea jikoni akawaacha
Steven na Graca pale sebuleni
“Naitwa Steven” Akasema
Steven huku akimtazama Graca
“Naitwa Graca”
“Nafurahi kukufahamu
Graca.Mimi ni rafiki wa
Elvis.Tunafanya kazi pamoja kwa
hiyo tutaendelea kuonana kwani
nitakuwa nikikaa hapa kwa siku
kadhaa.Usihofu kuhusu Elvis.He’s
fine” akasema Steven kwa sauti ya
upole halafu akaondoka kuelekea
chumbani kwa Elvis
Wakati Elvis akiendelea
kulishwa taratibu na Doreen
Steven akampigia simu
MeshackJumbo akampa taarifa za
Elvis na kumuelekeza mahala
walipo *******************
MeshackJumbo aliwasili
mahala wanakoishi akina
Elvis,akapokewa na Steven
ambaye alimtambulisha kwa akina
Doreen na Graca halafu
akampeleka moja kwa moja
chumbani kwa Elvis
“Welcome back to the world”
MeshackJumbo akamtania Elvis
aliyekuwa amekaa sofani.Elvis
akatabasamu
Dr Philip akatoa maelezo ya
maendeleo ya Elvis halafu
MeshackJumbo akataka kusema
kitu lakini Elvis akamzuia
“Mzee nataka kwanza
kufahamu mke wangu
anaendeleaje? Usihofu Elvis nitakueleza kila
kitu” akasema MeshackJumbo na
kumueleza Elvis kila kitu
kilivyoenda .Michirizi ya machozi
ikaonekana mashavuni mwa Elvis
“Elvis huu si wakati wa wewe
kuangusha chozi.Ni wakati ambao
unahitaji ujasiri wa aina yake
kuliko wakati mwingine wowote
katika maisha yako”akasema
Meshack
“Mzee naumia sana nikifikiria
mateso anayoyapata mke wangu
sasa hivi “
“Elvis ili tufanikiwe mpango
wetu lazima uyasahau hayo yote
kwa sasa na tuelekeze akili zetu
zote katika suala hili” akasema
MeshackJumbo na Elvis akafuta
machozi Hatua ya kwanza
imemalizika na Elvis tayari
amefariki.Nini hatua ya pili?
Akauliza Steven
“kwa mujibu wa mpango
ulivyo,keshi tutaanza
kushughulikia jeneza pamoja na
kaburi atakamozikwa Elvis.Kila
kitu kiko tayari vifaa vimekwisha
andaliwa.Mazishi yatafanyika lini?
“Kesho kutwa.Kikao cha
familia kimekaa na mimi
nikawashauri mazishi yafanyike
kesho kutwa kama tulivyokuwa
tumepanga.Nimewaambia
washughulikie masuala mengine
yote lakini suala la jeneza na
kaburi watuachie sisi
tutashughulikia.Dr Philip
umejipangaje kuhusu jeneza?
Akauliza MeshackJumbo Kesho nitakuwa na kazi ya
kulishughulikia suala hilo na
mpaka jioni kila kitu kitakuwa
tayari”
“Vizuri.Mimi kesho
nitakutana na ndugu wa Elvis
tena kumalizia baadhi ya
maandalizi ya mazishi.Nataka
tulimalize jambo hili la msiba kwa
haraka ili Elvis aanze kuifanya
kazi yake haraka kwani hawa
maadui zetu hawalali wakipanga
mipango yao na sisi tunapaswa
twende nao sambamba” akasema
MeshackJumbo
Majadiliano yaliendelea hadi
ilipotimu saa saba za usiku
ambapo MeshackJumbo aliondoka
kurejea kwake na Dr Philip yeye
alibaki pale pale kwa Elvis kwani
kulikuwa na nafasi ya kutosha Baada ya watu wote kutoka
mle chumbani Elvis akajilaza
kitandani huku akihisi kichwa
kizito sana.Aliwaza mambo mengi
kuhusiana na mpango ule
unaoendelea lakini kubwa
lililomtesa kichwa chake ni mke
wake Patricia.Taratibu kijiusingizi
kikaanza kumnyemelea na mara
kwa mbali akasikia kama mlango
unafunguliwa taratibu.Akafumbua
macho na kukutana na Doreen
“Doreen badio hujalala hadi
mida hii? Akauliza Elvis kwa sauti
ya uchovu
Doreen hakujibu kitu
akamfuata Elvis pale kitandani
akamkumbatia
“Elvis unajisikiaje?
“Najisikia vizuri japo kichwa
kinaniuma sana” Pole sana Elvis” akasema
Doreen
“Ahsante sana.Ahsante kwa
kila kitu” akasema Elvis kikapita
kimya
“Graca
anaendeleaje?Nilimuona wakati
nikiingia namna alivyopatwa na
mshituko”
“Ni kweli Graca amekwisha
gundua kuna jambo linaendelea
na hatujamwambia.Toka asubuhi
amekuwa ananiuliza kama
ninafahamu kinachoendelea
nilimkatalia kwamba sijui
chochote.Usiku huu alipokuona
ukiingia wasiwasi wake
umeongezeka na akanifuata
tena.Safari hii nilishindwa
kukataa na nikamwambia
kwamba ni kweli kuna jambo linaendelea lakini utamweleza
wewe mwenyewe.Ana wasi wasi
mkubwa na usalama wa maisha
yake”
“Usijali kuhusu hilo,she’ll be
fine.Nitaongea naye kesho”
akasema Elvis halafu akazama
mawazoni.Doreen akamuangalia
na kusema
“Unamuwaza Patricia?
“Ndiyo.Nashindwa
kutomuwaza.Nimemsababishia
mateso makali kwa kitendo cha
kudanganya kuhusu kifo changu”
akasema Elvis
Doreen akajisogeza karibu
yake na kusema
“Elvis usimuwaze Patricia kwa
sasa.She’ll be ok.Huko mbeleni
atakusamehe baada ya kugundua
kwa nini ulifanya hivi.Unachotakiwa ni kuelekeza
akili yako yote katika kazi nzito
iliyoko mbele yako.Bila wewe
mtandao huu wa vigogo
wanaofanya biashara haramu ya
silaha hutakoma na raia wasio na
hatia wataendelea kupoteza
maisha kila uchao huko Congo”
Elvis akamtazama Doreen
akatabasamu na kusema
“Ahsante sana Doreen kwa
ushirikiano wako.Ni wakati wa
kupumzika kesho itakuwa siku
ndefu mno”akasema
Doreen akatabasamu na
kumbusu Elvis akajilaza pembeni
yake
ELVIS ANAFANIKIWA
KUTENGENEZA KIFO
CHAKE JE MPANGOWAKE HUU
UTAFANIKIWA?
MPANGO WA
KUIANGUSHA SERIKALI
UTAFANIKIWA?
NINI KITATOKEA KATI YA
PATRICIA NA MUMEWE
ELVIS?
HARAKATI ZA DOREEN
KUMPATA KIMAPENZI
ELVIS MUME WA RAFIKI
YAKE ZITAFANIKIWA?
MPENZI MSOMAJI
USIKOSE SEHEMU
IJAYO..