I DIED TO SAVE PRESDENT
Sehemu 33
Ilimlazimu Dr Philip kutumia
usafiri wa pikipiki ya kukodi
kumfikisha Samawati beach hotel
kwani mkurugenzi wake
MeshackJumbo alimtaka asitumie
gari.Alimlipa kijana wa piki piki
akaangaza pande zote kuhakiki
usalama wake halafu akaingia
hotelini akaelekea moja kwa moja
mahala alikokuwa MeshackJumbo
“Karibu sana Dr
Philip.Nashukuru umefika kwa
wakati”
“Imenilazimu kutumia
bodaboda” akajibu Philip
“good.Umefanya jambo
zuri.Una hakika hakuna
aliyekuwa anakufuatilia huko
utokako?
“Hakuna mzee.Ni salama
kabisa” akasema Dr Philip “Mzee uliniambia uko na
Elvis,mbona simuoni hapa?
Akauliza DrPhilip
Kabla MeshackJumbo
hajajibu kitu Elvis
akatokea,akasalimiana na Dr
Philip na maongezi yakaanza
“Dr Philip hatuna muda
mwingi mahala hapa kutokana na
jukumu kubwa lililoko mbele yetu”
akasema Meshackakanyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Sina shaka nawe hata kidogo
Dr Philip na ndiyo maana
nimekuita hapa kukushirikisha
jambo kubwa .Nina imani
utakuwa ni msaada mkubwa
kwetu kwani jambo
ninalotakakukushirikisha ni la siri
kati yetu sisi tuliopo hapa”
akanyamaza tena na kumtazama Philip ambaye alitikisa kichwa
kukubaliana na kile alichokisema
Mechack Jumbo.
“Alfajiri ya leo nimeitwa na
makamu wa rais nyumbani
kwake.Jambo aliloniitia ni zito na
la kustusha.Kuna mtandao wa
watu unaofanya biashara haramu
na ndani ya mtandao huo wamo
vigogo wa serikali na baadhi ya
wafanya biashara wakubwa.Elvis
amegundua biashara
wanazozifanya na baada ya
kugundua kwamba wamekwisha
fahamika wanataka wamuue Elvis
kwani tayari amekuwa kikwazo
kwao”
Dr Philip akapatwa na
mstuko mkubwa.Kimya cha
sekunde kadhaa kikapita. Mzee umenistua sana kwa
hiki ulichokisema .Ninaomba
unifafanulie kidogo nilifahamu
jambo hilikwa kina” akasema
DrPhilip
“Ni hivi” akasema Elvis
“Katika siku za karibuni
nimefanikiwa kugundua
kuhusiana na mtandao unaofanya
biashara ya kuwauzia silaha wasi
wanaopambana na serikali ya
Congo.Mtandao huo
unawahusisha watu waliomo
ndani ya serikali hapa Tanzania
na ndaniya serikali ya
Congo.Silaha hizo huagizwa nje ya
nchi na kupita katika bandari yetu
halafu huishia mikononi mwa
waasi wanaopigana na serikali ya
Congo ambao huzinunua kwa pesa
nyingi na wakati mwingine kubadilishana na
madini.Uchunguzi wa mtandao
huu na hii biashara bado
unaendelea lakini wakati
uchunguzi ukiendelea hawa jamaa
wamegundua kwamba
wamefahamika na suluhisho
pekee walilonalo ni kuniua ili
wawe salama.Leo alfajiri
mkurugenzi ameitwa na makamu
wa rais nyumbani kwake na
akapewa maagizo ya kuhakikisha
ninauawa siku ya leo” akasema
Elvis.
“Sijawahi kupata taarifa
mbaya na ya kustusha kama hii
toka nimeanza kazi.Wanataka
kumuua Elvis?!! Akasema kwa
mshangao Dr Philip.
“Najua umestuka sana Dr
Philip lakini naomba nikutoe wasiwasi kamba lengo lao haliwezi
katu kufanikiwa.Nilipoanza
kulichunguza jambo hili
nilitegemea kitu kama hiki
kingeweza kutokea kwa hiyo
nilikwisha jiandaa kisaikolojia.Hizi
ni changamoto tunazokumbana
nazo katika hizi kazi zetu”
akasema Elvis.
“Elvis mimi kwa mara ya
kwanza nimekasirishwa mno na
hiki kitendo kinachotaka
kufanywa na hawa
vigogo.Sikutegemea kama watu
hawa wanaweza kufikia maamuzi
makubwa namna hii ya kutaka
kukuua mtu kama wewe.Elvis
hawa watu kama dhamira yao ni
kutaka kukuua basi hawatalala
usingizi hadi wahakikishe mpango
wao umetimia.Elvis you have to run.Go far away from here”
akasema Dr Philip
Elvis akatabasamu kidogo na
kusema
“Ahsante kwa ushauri
DrPhilip na hata mkurugenzi
alinieleza hivyo kwamba nikimbie
lakini mimi siwezi
kukimbia.Lazima nipambane
nao.Nimekwisha gundua biashara
yao haramu lazima niifikishe
mwisho.Nitapambana nao hadi
dakika ya mwisho.Kukimbia si
suluhu kwani hata huko
nitakakokimbilia wanaweza
wakanisaka na kunipata
wakaniua”
“Elvis mtandao huu ni
mkubwa na una watu wenye
nguvu kubwa.Kama maelekezo ya
kukuua yametoka kwa makamu wa rais ni wazi mtandao huu ni
mkubwa na unaweza kufanya
jambo lolote walitakalo kwa wakati
wowote.You have to run brother”
akasema Dr Philip
“Dr Philip nataka lengo lao
litimie”
“Lengo gani? Akauliza
DrPhilip
“Wanataka kuniua basi
lazima nife ili wawe na amani na
waendelee na biashara zao kama
kawaida” akasema Elvis na kuzidi
kumchanganya Dr Philip
“Nashindwa kukuelewa
Elvis.Watu hawa wanataka
kukuua na wewe bila wasi wasi
unakubali wakuue?Kifo chako
kitakuwa na msaada gani kwa
watu wasio na hati wanaoendelea
kuteseka huko jamhuri ya kidemokrasia ya Congo? Tafadhali
lifikirie upya hili suala na
usilifanyie mzaha!!akasema Dr
Philip
“Hakuna mzaha katika hili
DrPhilip .Kutokana na umuhimu
wake ndiyo maana nimekuita hapa
ili kwa pamoja tujadiliane namna
nitakavyokufa .Ninataka
nitengeneze kifo changu ili watu
hawa wanaoniwinda wawe na
amani na wendelee na shughuli
zao.Nataka wawe na uhakika
kwamba sipo tena duniani na hiyo
itakuwa ni fursa kwangu ya
kuwachuguza vizuri na
kuufahamu mtandao wao wote”
Dr Philip akatikisa kichwa na
kusema
“Kidogo sasa ninaanza
kukuelewa Elvis unachomaanisha.Tayari nilikwisha
taharuki kusikia kwamba unataka
kufa” akasema Dr Philip
“Ahsante kwa kunielewa Dr
Philip.Ni kweli kifo changu
kitakuwa cha kutengeneza lakini
chenye uhalisia mkubwa.Mpango
wenyewe umekaa hivi.Mkurugenzi
atapigiwa simu na mtu ambaye
atajitambulisha kwamba anatoka
katika chombo cha usalama na
atampa habari kwamba mtu
anayetafutwa sana na serikali kwa
kuratibu mashambulio mawili ya
mabomu jijini Arusha Abdullah
Abdullah ameonekana katika
msitu wa Ngezi.Baada ya kuipokea
taarifa hiyo mkurugenzi atanituma
mimi niende huko Ngezi kufanya
uchunguzi wa taarifa hizo ambako
tayari kuna watu watakuwa wamewekwa ili wanimalize pindi
tu nikitokea” akasema Elvis.
“Huo ni mpango walioupanga
wao ili wanimalize.Sisi mpango
wetu ni huu.Akishapokea simu
hiyo toka kwa hao jamaa
,mkurugenzi atanituma katika
msitu wa Ngezi.Mkurugenzi
akiambatana nawe mtanifuata
kwa nyuma.Katika eneo
nitakaloelekezwa atakuwepo
Steven Mugo yeye ndiye
nitakayeshirikiana naye katika
operesheni hii.Mimi na Steve
tutapambana na hao jamaa
watakaokuwa wamewekwa hapo
kunimaliza na kisha nitawataarifu
wewe na mkurugenzi mtafika pale
mara moja na wewe kama daktari
wa idara utathibitisha kwamba
nimekufa na kisha nitapelekwakatika hospitali ya St Clara
ambako watathibitisha pia
kwamba nimekufa.Katika hatua
hiyo wewe ndiye utakayechukua
nafasi kubwa kwani itahusisha
sana utaalamu wa hali ya juu na
ndiyo maana tumekuita hapa ili
kwa pamoja tujadili namna ya
kufanya kuufanikisha mpango
huu” akasema Elvis.
Dr Philip akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Nimeusikia mpango Elvis ni
mzuri lakini unahitajika utaalamu
mkubwa sana na endapo kutaokea
kosa hata dogo tu basi tunaweza
tukakupoteza moja kwa
moja.Naomba niwatoe wasiwasi
kwamba jambo hili linawezekana
kabisa kukafanyika na kwa
upande wangu ninaweza kufanya kila lililo ndani ya uwezo wangu
kuufanikisha.Kuna dawa inaitwa
Mephotexis II ambayo hutumiwa
na majasusi.Hii ni dawa ambayo
inampoteza mtu fahamu kwa
muda mrefu na mtu yeyote
akimuona mtu aliyepotezwa
fahamu kwa dawa hii atahisi
amekufa.Dawa hii ni hatari na
endapo ikikosewa hata kidogo
ikazidishwa basi hautaamka
tena.Baada ya tukio la msituni
kumalizika nitakuchoma dawa
hiyo na utaonekana kama
mfu.Mimi ndiye daktari wa idara
nikishathibitisha kwamba
umekufa hakuna atakayehoji
tena.Mkurugenzi atatoa taarifa
rasmikwamba umekufa.Baada ya
hapo umechagua hosptali ya St
Clara lakini napendekezatusiitumie hospitali ile kwani kuna
watu wa dini pale na inaweza
kuwa vigumu kuwashawishi
wakubali kujiunga nasi katika
mpango wetu.Nashauri tutumie
hospitali ya Rajesh Memorial
hospital.Mmiliki sa hospitali ile Dr
Rajesh ni rafiki yangu na nina
uhakika lazima watakubaliana
nami kirahisi.Tutakupeleka pale
nao pia watatoa ripoti yao
kuthibitisha kwamba ni kweli
umekufa.Baada ya hapo
nitakuzindua na kukutibu jeraha
utakalokuwa umelipata la risasi
kisha utaenda mapumzikoni
ukisubiri siku ya mazishi”
Dr Philip akanyamaza
akamtazama Elvis na mzee
Meshackkisha akasemaHakuna yeyote
atakayeruhusiwa kukuona katika
chumba cha maiti hadi siku ya
mazishi ambayo napendekeza
yafanyike haraka kesho
kutwa.Kitakachofanyika siku ya
mazishi ni kwamba katika jeneza
utakamowekwa kutafungwa kifaa
maalum cha kukusaidia
kupumia.Mirija miwili midogo
itatoka katika kifaa hicho na
kuingia mdomoni mwako.Hii ni
kwa ajili ya kuingiza hewa safi
mwilini.Hakuna atakayeweza
kuiona mirija hii kwani itakuwa
imefunikwa na bendeji
itakayofungwa kuanzia puani hadi
shingoni kwa kisingizio kwamba
sehemu hiyo imeharibiwa kwa
risasi.Kaburi utakamozikwa
litajengwa kitaalamu sana ili kuruhusu hewa kuingia
ndani.Kwa kigezo kwamba
umeumia vibaya sana kwa risasi
mwili wakohautaonyeshwa
hadharani isipokuwa kwa watu
wachache sana wa karibu
wakiwemo viongozi ili upatikane
ushahidi kwamba ni kweli
umekufa.Shughuli za mazishi
itabidi zichelewe kidogo ili hadi
tutakapofika makaburini kijua
kiwe kinazama.Kwa kuwa muda
utakuwa umekwenda shughuli
zitafanyika haraka haraka hapo
makaburini na watu wataombwa
kurejea majumbani na kuwaacha
mafundi wakilifunika
kaburi.Baada ya watu kuondoka
mafundi hao nao wataondolewa
kwa kigezo cha kufanya mambo ya
kiusalama na hapo ndipo Stevenatakapoingia na gari lenye jeneza
lingine na tutalibadilisha jeneza
kisha kaburi litafunikwa na picha
itaishia hapo”
Kimya kikatawala.Baada ya
muda Elvis akasema
“Una mpango mzuri sana Dr
Philip.Ahsante kwa mchanganuo
huo mzuri.Binafsi ninakubaliana
na mpango huo japo kuna baadhi
ya vitu tutaviongeza ili kuuweka
mpango huu vizuri zaidi”
“hata mimi sikutegemea kama
Dr Philip unaweza kuwa mwepesi
wa kufikiri namna hii.Nimeupenda
mpango huu.Natumai kama
ukienda vizuri basi lengo letu
litafanikiwa” akasema mzee
MeshackJumbo
Majadiliano marefu
kuhusiana na mpango ule yaliendelea na hatimaye
wakatawanyika ili kwenda kuanza
maandalizi.Dr Philip akaelekea
Rajesh memorial hospital kuonana
na Dr Rajesh ,mzee
MeshackJumbo na Elvis
wakaelekea katika nyumba
alikofungwa Steven Mugo.
******************
“Sasa nayakumbuka maneno
ya Patricia ambayo amekuwa
akiniambia mara kwa mara
kwamba katika kazi zote za dunia
hii kwa nini niliamua kufanya kazi
hii?Ninaipenda sana kazi hii lakini
kwa sasa ninaanza kuyaonja
machungu yake.Ni kazi iliyojaa
hatari kila kukicha.Wanataka
kuniua.Nitakufa kama wanavyotaka lakini hawajui kama
nitarejea kama mzimu na
kuwawinda usiku na
mchana.Hawatapata usingizi na
mwisho wa yote nitahakikisha
mtandao wao wote
unasambaratishwa.Sintafumba
jicho hadi pale nitakapohakikisha
mtu wa mwisho katika mtandao
huu ametiwa nguvuni.Siwezi
kukimbia na kwenda kujificha
mbali wakati ndugu zetu wa
Congo wakiangamia kwa silaha
zinazouzwa na genge hili la
maharamia.Lazima nipambane
nao hadi mwisho” akawaza Elvis
na kumkumbuka Patricia akahisi
kuumia moyoni
“Masikini Patricia mke wangu
sipati picha atakuwa katika hali
gani pindi akipata taarifa za kifo changu.Pamoja na yote yaliyotokea
katika ndoa yetu lakini kuna kitu
kimoja tu ninachokiamini,Patricia
ananipenda mno na atakapopata
taarifa za mimi kufariki maisha
yake hayatakuwa sawa tena.She”ll
never be the same ! nifanye nini
sasa? Akajiuliza Elvis wakiwa
garini
“Jambo hili la kifo changu
litawaumiza watu wengi sana hasa
mke wangu kipenzi na mama
yangu,pia ndugu zangu,lakini sina
namna nyingine ya kufanya zaidi
ya kutengeneza kifo changu ili
niweze kuumaliza mtandao huu
hatari.Hata nikiamua nikimbie
bado maisha yangu hayatakuwa
na amani na nitakimbia hadi
lini?Kitu pekee hapa ni kutulia na
kupambana.Nisipofanya hivi maisha ya watu wengi yataendelea
kupotea .Hawana mwingine wa
kuwaokoa zaidi yangu” akawaza
Elvis
“Nina imani Patricia
atanielewa nitakapokuja
kumueleza dhumuni la kufanya
hivi.Japokuwa itakuwa na ugumu
kuelewa lakini nitajitahidi hadi
aelewe kwamba nilifanya hivi kwa
ajili ya kuwaokoa mamia ya watu
wasio na hatia wanaopoteza
maisha katika nchi jirani ya
Congo” Akaendelea kuwaza Elvis
“Najaribu kutengeneza picha
namna Patricia
atakavyoumia.Sikutegemea kama
itatokea siku nitamuumiza
Patricia kiasi hiki.Naomba Mungu
aniwezeshe nimalize kazi hii
salama na baada ya kazi hii sitaki tena kuendelea nayo.Nataka
nitulie na mke wangu nimfute
machozi na kumrejesha katika
hali yake ya kawaida.Nataka kuwa
huru niishi maisha yenye furaha
na mke wangu Patricia” Elvis
akaendelea kuumiza kichwa kwa
mawazo.Muda wote toka
wametoka Samawati hoteli mzee
MeshackJumbo amekuwa kimya
na hakuongea lolote.Alionekana
kusongwa na mawazo mengi.Elvis
aliligundua hilo akageuza shingo
na kumtazama mzee
Meshackaliyekuwa ameinamisha
kichwa
“Mzee !! akaita Elvis na
kumstua MeshackJumbo toka
mawazoni Usiwaze sana mzee haya mni
mambo ya kawaida katika kazi
zetu” akasema Elvis
“Ndiyo Elvis ni mambo ya
kawaida lakini nashindwa kujizuia
kuwaza kwa sababu jambo
tunalokwenda kulifanya ni kubwa
na la hatari sana.Endapo
tutakosea kidogo tu basi
tutapelekea mauti yako jambo
ambalo sitaki litokee”
Elvis akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Ni kweli mzee.Jambo hili ni
la hatari sana na kosa dogo tu
basi nitakwenda moja kwa moja
lakini kitu kimoja kinachonipa
matumaini ni kwamba namuamini
sana Dr Philip.Nina imani
atasimamia zoezi hili na litakuwa
na mfanikio” Hata mimi namuamini sana
Dr Philip lakini kuna makosa ya
kibinadamu yanaweza yakatokea
na kusababisha maafa.Sitaki
jambo lolote likutokee Elvis na
ndiyo maana nathubutu kusema
kwamba mpango huu ni mzuri
lakini moyo wangu hauna amani
kabisa .Vipi kuhusu
mkeo?Utamuacha katika hali
gani?Ni vipi endapo atagundua
kwamba ulimdanganya kuhusu
kifo chako?Ndugu zako je
watakuchukuliaje pindi
wakikuona ukiwa hai hali
walihakikisha kwamba umefariki
dunia na wakakuzika kaburini?
Elvis haya ni maswali ambayo
nimekuwa najiuliza kuhusiana na
mpango huu tunaotaka
kuufanya.Mimi bado nakushauri Elvis kama inawezekana
ukubaliane na mpango wangu wa
kuondoka kwenda mbali wewe na
mkeo na nitawasaidia kwa kila
kitu ili muweze kuyaanza upya
maisha yenu huko mbali na
uachane kabisa na kazi
hizi.Ninakupenda sana kijana
wangu na ndiyo maana
ninakuomba ufanye hivi” akasema
mzee MeshackJumbo
“Mzee ondoa hofu.Nilikwisha
sema kwamba siwezi kukimbia
kabisa na wala kukimbia si
suluhu ya matatizo haya.Nitabaki
hapa na tutaendelea na mipango
yetu kama
tulivyoipanga.Nitapambana na
hawa watu na kama ikitokea
nikafariki basi nitakuwa nimekufa
kishujaa kwa kutetea damu zawananchi wanyonge wa Congo
wasiendele kuuawa.Kuhusu mke
na ndugu zangu ni kweli
wataumia na hata mimi ninaumia
sana moyoni kila nikivuta picha
namna mke wangu Patricia
atakavyoumia lakini hakuna
namna nyingine ya kufanya
kuwasaidia ndugu zetu wa Congo
zaidi ya kufa.Ninaamini zoezi hili
likikamilika basi nitamuelewesha
na atanielewa tu lakini kuna
jambo moja nataka nikufahamishe
mzee wangu” akasema Elvis
“Jambo gani?
“Baada ya operesheni hii
kumalizika na wote tukawa
salama hii itakuwa ndiyo kazi
yangu ya mwisho.Nataka
kuachana na kazi hii na kuanza
maisha mapya” Elvis kazi hii huwezi
kuiacha.Ni kama vile ukipakwa
mafuta ya kichungaji huwezi
kuacha uchungaji utaendelea hadi
kifo chako.Kwa hiyo sahau kabisa
kuhusu kuacha kazi
hii.Tunakutegemea sana na hata
taifa bado linakuhitaji hivyo ni
mapema sana kuanza kufikiria
kuacha kazi hii” akasema mzee
Jumbo
“Mzee msimamo wangu ndio
huo kwamba hii ni kazi yangu ya
mwisho .Nimefanya maamuzi haya
kwa ajili ya mke wangu Patricia
ambaye ameteseka kwa muda
mrefu kutokana na kazi
hii.Nimekosa muda wa kutosha wa
kuwa naye.Naomba unielewe mzee
wangu” akasema Elvis.mzee Jumbo akafikiri kwa muda na
kusema
“Sawa tutaangalia lakini sijui
kama itawezekana” akasema
Jumbo na kumuelekeza Elvis njia
ya kupita kuelekea mahala
alikofungwa Steven Mugo.Ni watu
wachache tu aliokuwa
wakifahamu mahala aliko
Steven,hata Elvis mwenyewe
hakuwa akipafahamu
Waliwasili katika nyumba
iliyozungushwa ukuta mrefu
wenye rangi nyeupe.Kuuzunguka
ukuta ule kulipandwa nyasi nzuri
za kupendeza .Elvis akasimamisha
gari katika geti kubwa
jeusi.MeshackJumbo akashuka
garini na kwenda katika nguzo
moja ya geti ambako kulikuwa na
kifaa Fulani mithili ya mita ya umeme wa luku akabonyeza
namba kadhaa halafu ukatoka
mwanga na kummulika
usoni.Baada ya muda geti likaanza
kujifungua na toka ndani
akaonekana mtu mmoja aliyekuwa
amevaa suti
nyeusi.Meshackakamfanyia ishara
Elvis aingize gari ndani.Mzee
Jumbo akasalimiana na yule
jamaa aliyekuwa ndani Elvis
akashuka garini na kuwafuata
“Elvis kutana na Meja Adolf
kutoka jeshi la polisi .Yeye ndiye
anayesimamia ulinzi wa nyumba
hii” Akatambulisha Mzee Jumbo
kisha akamgeukia Adolf
“Meja Adolf kutana na
Elvis,yuko katika ofisi yangu”
Meja Adolf akatabasamu Oh,kumbe wewe ndiye
Elvis.Nimekusikia mara kwa mara
lakini sikuwahi kupata bahati ya
kukutana nawe ana kwa
ana.Karibu sana Elvis” akasema
Meja Adolf.Mzee Jumbo
akamuomba Elvis waongozane
kuelekea ndani
“Nadhani ni mara yako ya
kwanza kufika hapa Elvis”
akasema mzee Meshackwakipiga
hatua kuelekea ndani zaidi
“Ndiyo mzee ni mara yangu ya
kwanza.Sijawahi kufika mahala
hapa”
“Hapa ni mahala pa siri
ambako huwa tunawahifadhi watu
mbali mbali kwa mfano rais wa
Burundi aliyepinduliwa na
kukimbilia Tanzania aliishi hapa
,baadhi ya viongozi wengine wandani na nje pia wamewahi kuishi
hapa.Kwa sasa Steven Mugo pekee
ndiye anayeishi humu ndani akiwa
chini ya uangalizi maalum wakati
uchunguzi wa suala lake
unaendelea” akasema mzee Jumbo
huku akiufungua mlango wa
chumba kimojawapo na kuingia
katika sebule nzuri.Jumbo
akamuomba Elvis amsubiri pale
sebuleni halafu akaelekea katika
chumba anakolala Steven Mugo
akabisha hodi mara tatu na sauti
toka ndani ya chumba kile
ikamruhusu aingie ndani.Taratibu
akakinyonga kitasa na kuingia
ndani.Steven Mugo alikuwa
amejilaza kitandani huku akivuta
sigara.Alipomuona MeshackJumbo
akachukua gazeti na kuanza
kusoma.Hakutaka kumtazama usoni.Mzee Jumbo akaketi katika
sofa lilokuwamo mle chumbani
akavuta pumzi ndefu na kusema
“Habari yako Steven”
Steven hakujibu kitu
akaendelea kusoma gazeti lake
“ Najua hukutegemea kama
ningekuja kukuona muda huu na
ninafahamu kwamba hautaki
kabisa kuiona sura yangu
hapa.Ninafahamu mimi nawe
hatutazamani usoni hasa
kutokana na jambo lililotokea
lakini kilichonileta hapa si
kulionelea suala hilo ila kuna mtu
nimemleta anahitaji kukuona”
Steven Mugo akaliweka chini
gazeti lake na kumtazama mzee
Jumbo
“Mgeni gani? Kwa mara ya kwanza baada
ya karibu mwaka mmoja na nusu
toka amefungwa katika nyumba
hii Steven akamsemesha Jumbo
“Ni mtu ambaye hukutegemea
kabisa kumuona.Uko tayari
kuonana naye?
Steven Mugo akafikiri kwa
muda na kusema
“sawa,mlete nionane naye”
MeshackJumbo akatoka kwa
haraka na kumfuata Elvis
“Steven amekubali kuonana
nawe.Nafasi ni yako Elvis ongea
naye na tafadhali mshawishi
akubali kujiunga nawe” akasema
MeshackJumbo.Elvis akainuka na
kuingia katika chumba alimo
Steven.
Kwa sekunde kadhaa Elvis na
Steve walikuwa wanatazamana.Kila mmoja
alikuwa anamshangaa
mwenzake.Steven akainuka pale
kitandani alipokuwa amekaa na
kumfuata Elvis wakakumbatiana
kwa furaha
“Elvis ! akasema Steven kwa
mshangao
“Siamini kama hisia zngu
zilikuwa za kweli.Nilijua tu lazima
siku moja utakuja.Niliwahi kuota
kwamba wewe ndiye utakayekuwa
mkombozi wangu na leo ndoto ile
niliyoota imetimia na Elvis umetia
mguu wako hapa .karibu sana”
akasema Steven na kumkaribisha
Elvis katika sofa lililokuwamo mle
chumbani kisha akaenda sebuleni
na kurejea na chupa kubwa ya
mvinyo na glasi mbili akamimina mvinyo katika glasi zile na
kumpatia moja Elvis
“Pole sana Steven” akasema
Elvis
“Ahsante Elvis.Nashukuru
umekuja kuniona na ujio wako
huu ninaamini utakuwa na neema
kubwa kwangu.Elvis nimekuwa
nikiishi katika jumba hili kwa
miaka kadhaa sasa na hakuna
mtu aliyewahi kuja kunitazama
zaidi ya huyu mzee wenu na
walinzi wa hapa
wanaonilinda.Japo ninapata kila
ninachokihitaji lakini ni mateso
makubwa kuwamo ndani ya
jumba hili” akasema Steven.
“Pole Steven.Mambo haya
yatakwisha tu usihofu” akasema
Elvis Elvis ninateseka bila
kosa.Nina hakika unazifahamu
tuhuma ninazokabiliana nazo
lakini naomba nikuweke wazi
kwamba sikufanya hicho
ninachotuhumiwa kukifanya.Sina
kosa lolote nimefungwa hapa
bure.Please Elvis help me
brother.Bila wewe kunisaidia
nitafia ndani ya jumba hili
.Nadhani kuna watu wanataka
kuniangamiza bila kosa lolote.Do
you believe me Elvis?” akauliza
Steven.Uso wake ulionyesha
huruma.
“I do believe you Steven and
I”m here to help you .I”m here to
take you out of here” akasema
Elvis. Steven akashindwa kujizuia
kwa furaha aliyoipata akainuka na
kumpa mkono Elvis
“Ahsante Elvis kwa kuja
kunitoa kifungoni.Nimeteseka
mno.Tafadhali naomba usiniache
humu ndani leo” akasema Steven
kwa furaha
Elvis akamueleza Steven kila
kitu kuhusiana na kinachoendelea
baina yake na mtandao wa akina
Frank.Steven akavuta pumzi
ndefu na kusema
“Dah,hawa watu nina hasira
nao sana.Usijali Elvis mimi niko
pamoja nawe na nitafanya kila
niwezalo ili mpango huu
ufanikiwe.Nina hasira sana na
hawa viongozi wenye kutumia
madaraka yao kukandamiza
wanyonge.I swear this time I’m going to show them who I real am”
akasema Steven kwa hasira
“Ahsante Steven kwa
kukubali kujiunga nami.Nina
imani kubwa nawe na nina
uhakika vita hii
tutashinda.Naomba unipe dakika
mbili nizungumze na mkurugenzi”
akasema Elvis na kutoka
akaelekea sebuleni alikokuwapo
MeshackJumbo
“Vipi mambo yamekwendaje?
Akauliza Mzee Jumbo
“mambo mazuri mzee.Steven
amekubali kushirikiana nami”
“Good” akasema mzee Jumbo
halafu akamtazama Elvis kwa
makini na kusema
“Elvis kabla hatujatoka hapa
una uhakika na hiki unachotaka
kukifanya kuhusu kumtumia Steven katika operesheni hii?
Akauliza.Elvis akatabasamu
kidogo na kusema
“Ndiyo mzee nina uhakika na
ninachotaka
kukifanya.Ninamfahamu vyema
Steven Mugo na ndiyo maana
nikamchagua yeye ashirikiane
nami.Ondoa hofu mzee kila kitu
kitakwenda vizuri”
“Nashukuru kusikia hivyo
kwani siku zote ninayaamini
maneno yako lakini mambo
yakienda vinginevyo tutakuwa
tumejiingiza katika hatari kubwa
sana.Tafadhali naomba usimuache
Steven afanye jambo lolote la
kijinga na kutuletea matatizo sisi
tuliomtoa humu hasa mimi”
akasema Mzee Jumbo. “mzee naomba usihofu
chochote.Tafadhali niamini”
akasema Elvis
“Nakuamini Elvis” akasema
mzee Jumbo kisha akaongozana
na Elvis wakaingia chumbani kwa
Steven
“Steven mkurugenzi ana
jambo anataka kukueleza”
akasema Elvis na Steven
akamtazama mzee Jumbo kwa
jicho la chuki .Mzee Jumbo
akakohoa kidogo na kusema
“Steve nadhani Elvis
amekwisha kuelekeza kila kitu
kinachoendelea na kwa nini
tumekuja hapa hapa kwa hiyo
sitaki kupoteza muda kwa
kuyarudia yale uliyokwisha
elezwa.Ni kutokana na suala hilo
alilokueleza Elvis nimeamuakufanya maamuzi magumu sana
ya kukutoa humu ndani.Naomba
ufahamu kwamba maamuzi haya
niliyoyafanya yataniletea matatizo
makubwa lakini kutokana na uzito
wa jambo tunalokwenda kulifanya
na baada ya kuhakikishiwa na
Elvis kwamba wewe ndiye pekee
anayekuhitaji katika operesheni
hii nimelamika kukutoa humu
ndani.Ninachokuomba ni kwamba
tafadhali usifanye jambo lingine
lolote tofauti na kile
atakachokuelekeza Elvis.Vile vile
naomba usijaribu wala kufikiria
kutoroka kwani kwa………………”
“Usihofu mzee” Steven
akamkatisha mzee Jumbo
“Siwezi kutoroka .Kama
ningetaka kutoroka ningekwisha
ondoka kitambo sana lakini ninaziheshimu mamlaka
zilizoniweka humu ndani na ndiyo
maana mpaka leo hii niko humu
ndani.Siwezi kutoroka kwa sababu
sikuwahi kufanya kosa lolote la
kunifanya nikimbie.Nitaendelea
kuipigania haki yangu hadi pale
nitakapoipata .Kama hakuna
kingine cha kuniambia tunaweza
kuondoka? Akauliza Steven.Elvis
na MeshackJumbo wakatazama
“Elvis mnaweza kwenda mimi
nitabaki hapa kuna mambo
nataka kuyaweka sawa.Usijali
kuhusu usafiri nitatumia gari la
Meja Adolf.Nenda kajiandae kwani
muda wowote toka sasa shughuli
itaanza” akasema kwa sauti ya
chini mzee Jumbo.Elvis na Steven
wakatoka na kuingia katika gari wakaondoka kurejea kwa Salhat
alikoliacha gari lake.
“Namchukia sana Yule
mzee.Kwa zaidi ya mwaka sasa leo
hii ameweza kusikia sauti
yangu.laiti angekuja peke yake
ningeweza hata kumfumua
magumi.yeye ni sababu ya mimi
kuteseka namna hii.Anafahamu
kabisa kwamba sina kosa lolote
lakini ameshindwa kunitetea”
akasema Steven
“Usijali Steven mambo haya
yatakwisha tu.Ninakuahidi baada
ya mambo haya kumalizika basi
tutaanza kulishughulikia suala
lako na utasafishwa dhidi ya
tuhuma zinazokukabili.Mpaka
hapa hesabu tayari suala lako
limekwisha” Sijui nikushukuruje Elvis
kwa kuja kunisaidia .Bila wewe
ningefia katika ile nyumba.Hata
hivyo sitaki tena kuendelea na hii
kazi.Nafikiria kuanza shughuli
nyingine .Nitafungua biashara na
nitaishi maisha mazuri tu”
akasema Steven
“Wazo lako ni sawa na
langu.Mimi ninaipenda kazi hii
lakini nitaachana nayo kwa ajili ya
kuwa karibu na Patricia”
“Oh ,anaendeleaje mkeo?
Tayari mmekwisha pata mtoto?
Akauliza Steven na Elvis akahisi
kama kuna kitu kimemgonga
kichwani.
“ Bado hatujapata mtoto”
akajibu
“mnasubiri nini Elvis?
Unataka ufe bila kuacha ukumbusho duniani? Nyie
mliobahatika kuoa mnatakiwa
kuwa na watoto kwa sababu hizi
kazi zetu hazitabiriki muda
wowote unaweza poteza maisha”
akasema Steven
“Ni kweli hayo uyasemayo na
ndiyo maana nimefanya maamuzi
kwamba hii ni kazi yangu ya
mwisho ili nipate muda mzuri wa
kuwa na mke wangu.Yeye ndiye
kila kitu kwangu.Nitaacha kila
kitu nikipendacho kwa sababu
yake” akasema Elvis
“Patricia anafaa kujivunia
sana kuwa na mwanaume
anayempenda kama wewe.Toka
nimekufahamu ukiwa na Patricia
sijawahi kukuona ukiwa na
mwanamke mwingine wa pembeni
au hata kusikia sifa zako mbaya.Hata mkeo ni mwanamke
mtulivu sana.Mna bahati ninyi
kukutana.Uamuzi unaotaka
kuuchukua Elvis ni uamuzi sahihi
na mimi nitakusaidia
tutapambana hadi tuhakikishe
kwamba tunawafyeka hawa wote
wanaosababisha maisha ya ndugu
zetu huko Cogo yanapotea kila
uchao huku wao matumbo yao
yakishiba kwa mauzo ya silaha
wanazowauzia waasi”
“Mimi na Patricia tuna
historia ndefu na ndiyo maana
ninasema niko tayari kuacha kila
kitu nikipendacho kwa ajili yake”
akasema Elvis na mara
akakumbuka mambo
alioyoyafanya na Doreen na
akakumbuka namna alivyomkuta
Patricia akitoka hotelini akiwambaya.Hata mkeo ni mwanamke
mtulivu sana.Mna bahati ninyi
kukutana.Uamuzi unaotaka
kuuchukua Elvis ni uamuzi sahihi
na mimi nitakusaidia
tutapambana hadi tuhakikishe
kwamba tunawafyeka hawa wote
wanaosababisha maisha ya ndugu
zetu huko Cogo yanapotea kila
uchao huku wao matumbo yao
yakishiba kwa mauzo ya silaha
wanazowauzia waasi”
“Mimi na Patricia tuna
historia ndefu na ndiyo maana
ninasema niko tayari kuacha kila
kitu nikipendacho kwa ajili yake”
akasema Elvis na mara
akakumbuka mambo
alioyoyafanya na Doreen na
akakumbuka namna alivyomkuta
Patricia akitoka hotelini akiwatu na ilikuwa ni bahati
mbaya.Sikuwa nimedhamiria
kufanya kitu kama kile japokuwa
Doreen amekuwa akihitaji sana
kufanya mapenzi nami toka
alipopewa ruhusa hiyo na Patricia
kwa kusudi la kuzaa mtoto na
mimi.Sijui nilikuwa nawaza wapi
hadi nikajikuta nikinasa katika
mtego wa Doreen.Ni vipi kama
akija leo na kunieleza kwamba ana
mimba yangu?Nitakataaje wakati
nimefanya naye mapenzi? ”
akawaza Elvis