Riwaya: I died to save my President

Kudadeki.....patamu hapo Pascal na Vicky wanakuwa wakwanza kukutana na mtu alikufa na kuzikwa.....nasubiri kuona Frank pia akikutana na Elvis pamoja mkurugezi wa ujasusi...atakapo sema good job vijana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iko nzuri sana, Vicky hajui kuwa ukiona mzimu lazima ufe, hawezi kwenda mtaani kusimulia mzimu wa Elvis. Lazima watapike yote.

Mtihani hapo ni namna ya kutoka nao nje ya hoteli.
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 49

No !! this is not true.You?!!
akasema Pascal kwa mshangao
midomo ikimtetemeka
"It's true Pascal.It’s me
Elvis.Mimi ni halisi na wala si
mzimu kwa hiyo usiifanye akili
yako ione kama vile uko ndotoni"
akasema Elvis na kuinua glasi ya
mvinyo iliyokuwa mezani
akanywa
"Nadhani sasa hauna wasi
wasi tena.Mimi ni halisi kwani
mzimu hauli wala kunywa lakini
mimi nimekunywa mvinyo mbele
yako"
“You are dead !! akasema
Pascal
"No I'm not." akasema Elvis
na uso wa Pascal ukaonekana kuloa jasho.Ghafla macho yake
akayaelekeza mlangoni
"Vic........" kabla hajamaliza
sentensi yake mara risasi
mfululilzo kutoka katika bastora
iliyofungwa kiwambo cha sauti
zikamiminika kichwani kwa
Pascal na kumuodoa uhai pale
pale.Elvis na Steve kila mmoja
akaruka upande wake
kujinusuru.Vicky alisimama akiwa
na bastora mkononi ikifuka
moshi.Kwa haraka na kwa
shabaha ya aina yake Elvis
akaulenga mkono wa Vicky
uliokuwa na bastora ikaanguka
chini.Wakati Vicky akiwa chini
akigugumia kwa maumvi makali
Steve akaruka na kumuwahi
akamnyooshea bastora .Elvis akaenda kumtazama Pascal tayari
hakuwa na uhai.Kichwa chake
kilifumuliwa kwa risasi.
"Can he make it? Steve
akauliza
"No he's gone" akasema Elvis
na kumfuata Vicky pale chini
"What have you done?!!
akauliza lakini Vicky hakujibu
kitu.Alikuwa anagugumia kwa
maumivu makali ya risasi
"Kill me you bastard!!
akasema kwa ukali.
"We cant kill you.We need
you” akasema Elvis na kwa haraka
akalifungua sanduku alilokuja
nalo lililokuwa na vifaa mbali
mbali akachukua dawa na kuivuta
katika bomba la sindano kisha
akamchoma Vicky karibu na mahala alipopigwa risasi na
kumfanya asihisi maumivu makali
pamoja na kuzuia damu isiendelee
kutoka.
“Steve kila kitu kimeharibika
we have to get out of here now
lakini kabla hatujaondoka lazima
tuhakikishe tumepaacha salama
mahala hapa. Mlaze Pascal hapa
mahala damu ya Vicky
ilipomwagika ili zichanganyike
halafu hakikisha hakuna mahala
ulikoacha alama zako za
vidole.Pangusa kila sehemu
haraka haraka" akasema Elvis na
kumuinua Vicky akampeleka
bafuni akamuamuru aoage aondoe
damu iliyotapakaa mwilini.Wakati
Elvis na Vicky wakiwa bafuni
Steve akaanza kufuta alama za vidole katika sehemu zote ambazo
aliamini amezishika kwani
hakuwa amevaa kitu chochte
mkononi tofauti na Elvis
aliyekuwa amevaa glovu.Baada ya
kuoga na kujifuta damu Elvis
akalifunga jeraha la Vicky halafu
akamtaka avae koti la Steve ili
jeraha lile la risasi lisionekane
"We're going out.Utakuwa
kimya na kufuata maelekezo
yetu.You'll smile like nothing
happened.Ukienda kinyume na
sisi kwa namna yoyote ile you are
finished.Kichwa chako
nitakifumua kwa risasi kama
ulivyomuua Pascal.Umenielewa !!
akauliza Elvis kwa ukali
"Nimekuelewa lakini
naombeni mnipeleke hospitali " akasema Vicky.Elvis na Steve
wakatazamana
"Everything ok? Can we go
now? Elvis akauliza
"Tunaweza kuondoka.Kila
kitu kiko sawa." akasema Steve
wakazima taa na kutoka mle
chumbani.Elvis alikuwa
amemshika kiuno Vicky
wakionekana kama wapenzi.Steve
alikuwa nyuma yao hatua kadhaa
akiangalia kwa makini kama kuna
hatari yoyote nyuma
yao.Walishuka kwa kutumia lifti
halafu wakaingia katika ukumbi
wa chakula na kutoka wakaelekea
maegesho ya magari.Hakuna
yeyote aliyewatilia shaka au kuwa
na wasi wasi nao.Kwa upande wa
Elvis ilikuwa vigumu kutambulikahasa kutokana na vitu bandia
alivyokuwa amevaa na kuubadili
kabisa mwonekano wake.
Vicky akaingizwa katika gari
la Elvis na kukaa kiti cha pembeni
na kwa tahadhari mikono yake
ikafungwa pingu zile alizokuwa
amefungwa Pascal na kuondoka
mahala pale huku Steve akiwa
nyuma yao kuhakikisha
wanakuwa salama.Baada ya
kuingia barabarani Elvis
akampigia simu Dr Philip na
kumtaka wakutane nyumbani
kwake haraka sana usiku ule kuna
dharura imetokea halafu
akampigia simu Meshack Jumbo
na kumtaka pia afike nyumbani
kwake usiku ule kuna jambo
limetokea. Elvis akageuza shingo na
kumtazama Vicky ambaye uso
wake ulikuwa mkavu sana na
hakuonyesha hata chembe ya wasi
wasi kana kwamba hakuna
kilichokuwa kimetokea muda
mfupi uliopita
"Who is this woman? Siamini
kama ni kahaba kwa namna
alivyoweza kuitumia silaha kwa
wepesi ule.Hakuna kati yetu
aliyekuwa na mawazo kama
angeweza kufanya kitu kama kile
na akaitumia fursa wakati sisi
tukiwa tumeelekeza akili zetu kwa
Pasal akachukua bastora na
kumuua.Bastora ile aliitoa wapi?
Ni ya kwake? Kwa nini akamuua
Pascal? akajiuliza Elvis huku
akiongeza mwendo wa gari Ukimtazama alivyo na
kitendo alichokifanya hawaendani
kabisa.Hakuna atakayeamini
akiambiwa kwamba mwanamke
huyu ametoka kutoa uhai wa mtu
kikatili muda mfupi uliopita.Huyu
ni mwanamke hatari na kuna
mambo mengi tutayafahamu
kupitia kwake.Lazima ipo sababu
iliyopelekea akamuua Pascal.Huu
ni mwanzo tutafahamu mambo
mengi yaliyojificha.Nimekwisha
weka ahadi kwamba hakuna jiwe
litakalosalia juu ya
jiwe.Tutawaangusha wote
waliomo katika mtandao haramu
wa kuuza silaha kwa waasi wa
Congo DRC.Je na huyu mwanamke
naye ni mmoja wa watu waliomo
katika mtandao huo? akajiuliza Elvis na kulipita gari lililokuwa
mbele yake
"Ninahisi hata huyu naye ni
moja wao kwa sababu kwa mujibu
wa barua pepe nilizozikuta katika
kompyuta ya Frank,mtu anayejiita
Deusdedith MM alitoa maelekezo
kwamba kahaba huyu atumike
katika mauaji ya kanali
Norman.Kuna uwezekano
mkubwa mwanamke huyu naye
akawa ni mmoja wao au akawa ni
muuaji anayetumiwa na watu
hawa kuua kimya
kimya.Inashangaza sana kahaba
kuwa na utajiri mkubwa kama
alionao huyu Vicky.Atatueleza kila
kitu" akawaza Elvis na kujitazama
tena Vicky ambaye alikuwa ameegemea kitini akionekana
kupitiwa na kijiusingizi.
Waliwasili katika makazi yao
na Graca akawafungulia geti.Vicky
akashushwa na kuingizwa katika
moja wapo ya chumba
kilichokuwa kimeandaliwa
akalazwa kitandani na kufungwa
pingu mkono wake wa kushoto na
miguuni katika kitanda cha
chuma.
"Please take me to hospital"
akasema Vicky
"Hapa uko hospitali usihofu"
akasema Elvis na kutoka mle
chumbani akaufunga mlango
"Elvis nimefurahi umerejea
salama.Kila kitu kimekwenda
vizuri? akauliza Graca Kila kitu kiko sawa
Graca.Nenda chumbani
ukapumzike sisi bado tunaendelea
na kazi" akasema Elvis na Graca
akaenda kupumzika chumbani
kwake
"Good job Steve" akasema
Elvis huku akichukua glasi ya maji
"Elvis kilichotokea pale
ninaona kama filamu.Bado
najaribu kutafakari lakini inaniwia
vigumu kuamini kama kweli Vicky
ndiye aliyefanya kitendo kile na
kwa wepesi ule" akasema Steve
"Ni kweli ni kitu ambacho
kinashangaza sana.Hatukuwa
tumetegemea kama Vicky
angeweza kufanya kitendo cha
namna ile na ndiyo maana
hatukuwa tumeelekeza macho yetu kwake na akatumia mwanya
huo kufanya alichokifanya.Swali
ambalo tunapaswa tulitafutie jibu
ni kwa nini amemuua
Pascal?lazima ipo sababu
iliyomfanya akamuua
Pascal.Alifahamu kuwa
tutamfanyia mahojiano Pascal na
kuna mambo tutayafahamu hivyo
akaamua kumuua ili tusiweze
kumuhoji.Tumemkosa Pascal
lakini tumempata mtu ambaye
naamini ni muhimu sana
atakayetusaidia kupata majibu ya
maswali yetu"akasema Elvis
"Mwanamke yule ni hatari
sana.Angeweza hata kutumaliza
sote" akasema Steve
"Nahisi lengo lake lilikuwa
hilo kutumaliza sote kwani bastora yake bado ilikuwa na
risasi za kutosha na kama
tusingekuwa makini angeweza
kutumaliza na kutokomea
zake.Siku zote nimekuwa
nikikufundisha Steve usiwaamni
sana wanawake hasa hawa wenye
uzuri wa kimalaika.Wanaweza
kuwa hatari kuliko hata
shetani.Mtazame Vicky huwezi
hata kuhisi kama amewahi
kuigusa hata silaha lakini ndani ya
sekunde chache ameweza kuutoa
uhai wa mtu kikatili.Anaonekana
ni mzoefu sana katika mambo……"
Elvis akanyamaza baada ya
kengele ya getini kulia Steve
akaenda kwa tahadhari kubwa na
kumkuta ni Dr Philip karibu sana Dr Philip"
akasema Steve baada ya Philip
kushuka garini
"Nimeitika wito kwa haraka
Elvis.Is everything ok here?
akauliza Dr Philip baada ya
kuingia ndani
"Kazi imeanza Dr Philip na
kuna mtu anahitaji huduma yako
ya haraka amepigwa risasi
mkononi" akasema Elvis na
kumsimulia Dr Philip
kilichotokea.Bila kupoteza muda
Philip na Elvis wakaenda katika
chumba alimo Vicky.Dr Philip
akalitazama jeraha la Vicky kisha
akaelekeza afunguliwe na baadhi
ya vitu viandaliwe ili aweze
kumfanyia upasuaji wa
mkono.Meza kubwa ya chakula ikaletwa mle chumbani na
kuwekwa godoro juu yake Vicky
akalazwa na kuchomwa sindano
ya kuondoa maumivu kisha Dr
Philip akaanza kuufanyia upasuaji
mkono ule kuondoa
risasi.Lilikuwa ni zoezi la dakika
thelathini halafu akashona jeraha
na kumchoma Vicky Sindano
nyingine.Wakiwa katika hatua za
mwisho mlango ukafunguliwa na
Meshack Jumbo akiwa na Steve
wakaingia
"Karibu sana mzee"akasema
Elvis na kumuacha Dr Pilip na
Steve mle chumbani akaongozana
na Meshack kuelekea sebuleni
"Elvis habari za hapa? mambo
yanakwendaje? Nilikuwa na siku
ndefu iliyokabiliwa na mambo mengi na ndiyo maana sikuweza
tena kurejea hapa.Ila nilihudhuria
kikao cha mwisho cha kuhitimisha
msiba na..."
"Tayarini ninafahamu kila
kitu kilichotokea mzee.Doreen
naye alikuwepo na amenieleza
kila kitu"akasema Elvis
"Vizuri kama tayari unazo
taarifa.Alichokifanya Patricia
kimesikitisha wengi.Inaonekana
kuna mambo mengi aliyokuwa
anafanyiwa na ndugu zako hadi
akaamua kuchukua uamuzi ule
mgumu .Tuachane na hayo
ninataka kufahamu
kinachoendelea hapa.Yule
mwanamke mle ndani ni nani na
kafanya nini? akauliza Meshack na Elvis akamsimulia kila kitu
kilichotokea usiku ule.
"Elvis nimesisimkwa mwili
kusikia kitu alichokifanya yule
mwanamama.Mmekwisha
mfahamu ni nani?
"Hapana bado.kwanza
tunamtibu kumuondoa risasi
halafu tutamfanyia mahojiano
tumfahamu ni nani ila lazima ni
mtu hatari na ni mzoefu wa silaha
kwa namna alivyoweza kumuua
Pascal.Alimlenga risasi za kichwa
na lengo likiwa ni kumuua kwa
haraka ili tusiweze kupata
chochote kutoka kwake"
"Kwa mtazamo wangu
mtandao wa hili genge ni mkubwa
na kuna uwezekano hata huyu mwanamke naye akawa ni mmoja
wao." akasema Meshack
"Kwa mujibu wa barua pepe
nilizozipata kutoka katika
kompyuta ya Frank iliyoibwa na
Graca,mtu anayeitwa Deusdedith
MM anaonekana kutoa maelekezo
mengi kwa Frank na ambaye
anaonekana ndiye kiongozi wao
alimuelekeza Frank amtumie
Vicky katika mauaji ya kanali
Norman kwa hiyo basi huyu
mwanamke ni muhimu sana
kwetu kwani anafahamu mambo
mengi kuhusiana na mtandao huu
.Ni yeye ambaye anamfahamu
Deusdedith MM na atatuongoza
kujua mahala alipo.Kuna
uwezekano pia mwanamke huyu
akawa ni muuaji anayetumiwa na akina Frank kuua watu kimya
kimya kwa kutumia uzuri
wake.Tutayafahamu haya yote
ndani ya kipindi kifupi.Zama zake
tayari zimekwisha" akasema Elvis
"Mimi ngoja niwasiliane na
makamu wa rais nimjulishe
kwamba tayari Pascal ameuawa
kama alivyoagiza" akasema
Meshack na kumpigia simu
makamu wa rais akamjulisha
kwamba tayari Pascal ameuawa.
"Kazi nzuri sana Meshack
.Hizi ni taarifa njema kabisa.Kesho
ule mzigo niliokuahidi utaletwa
ofisini kwako" akasema makamu
wa rais Dr Shafi na kuagana na
Meshack
"kwa nini makamu wa rais
atake Pascal auawe? Elvis akaulizaHilo ni swali ambalo
tunapaswa kulitafutia
majibu.Alitaka wewe uuawe kwa
sababu tayari ulikwishaingia
katika anga za vigogo lakini huyu
Pascal sijafahamu yeye alifanya
nini hadi ikaamriwa auawe"
akasema Meshack
"Pascal na Frank ni marafiki
wakubwa na bishara ya silaha
wanaifanya kwa
pamoja.Inawezekana makamu wa
rais ni mmoja wa washirika wa
mtandao huu na ndiyo maana kila
pale maslahi yao yanapoguswa
anatumia nguvu yake kuondoa
vikwazo.Kama ni hivyo kwa nini
Pascal atakiwe kuuawa wakati ni
mwenzao. Je Frank anaweza
kumtoa kafara swahiba wake mkubwa kama Pascal? kama jibu
ni ndiyo basi lazima kuna jambo
kuwa limetokea kati yao kwa
maana hiyo lazima kumchunguza
pia Frank kujua kama kuna jambo
lolote limetokea kati yake na
Pascal lakini kabla ya hayo yote
lazima kwanza tuufahamu
ukubwa wa mtandao huu na
tuwajue wahusika wote kisha
tuanze kuubomoa hatua kwa
hatua.Hakuna atakayesalia hata
mmoja" akasema Elvis.
"Mara nyingi viongozi
wakubwa kama hawa
wanaposhiriki katika magenge
kama haya yenye kufanya
biashara haramu huwa
hawajihusishi moja kwa moja bali
uhusika wao huwa wa siri na inawezekana kukawa na ugumu
wa kuthibitisha kama makamu wa
rais ni mmoja wa
wahusika.Inawezekana akawa si
mmoja wao ila kuna kitu
anakipata kutoka kwa wakuu wa
mtandao huu na akawa
akiwasaidia kutekeleza maagizo
yao mbali mbali.Haya yote
yanawezekana na yanatakiwa
yachunguzwe."
"Usemayo ni ya kweli kabisa
mzee na tutayafanyia kazi ili
kuufahamu ukweli.Ahadi yangu ni
ile ile siku zote kwamba kaika
suala hili hakuna jiwe litasalia juu
ya jiwe.Yeyote anayehusika katika
biashara hii akiwa hapa nchini
lazima atajulikana na hatua stahiki zitachukuliwa" akasema
Elvis.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha linazidi kunoga [emoji39] [emoji39] [emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…