I DIED TO SAVE MY PRESDENT
SEHEMU YA 14
MTUNZI : PATRICK.CK
ILIPOISHIA
ukweli mtu mwalimu.Hauna
mtu mwingine anayefahamu suala
hili hapa shuleni zaidi yangu”
“ Jesus Christ !!..Patricia
!!!..bado siamini kama anaweza
kweli akafanya jambo kama hili”
“ Naomba uniamini mwalimu
Anna”
“ Kwa nini alikimbilia kwenda
kuitoa hiyo mimba bila hata kuja
kuniuona na kuniomba ushauri?
Siku zote nimekuwa mlezi
wao.Nimejishusha na kuwa kama
rafiki yao ili wakiwa na tatizo
lolote wasisite kunieleza kwa nini
hakunifuata akanieleza tatizo lake
nimsaidie ?
“ Mwalimu Anna suala hili ni
gumu na alikuwa
amechanganyikiwa kwa hiyo
akaona njia pekee ya kufanya ni
kwenda kuitoa”
“ Ulifahamu kila kitu kwa nini
basi na wewe hukuja kunieleza hadi umesubiri hali imekuwa
mbaya?
“ Mwalimu ,hili ni suala
linalomuhusu mtu na siwezi
kufanya lolote bila ruhusa yake”
“C’mon Elvis,she’s your friend
and you need to be there for
her.What’s the meaning of
friendship if you cant help each
other in times like this? Akauliza
mwalimu Anna.Elvis akashindwa
kujibu
“Hiyo mimba aliitolea wapi?
“Alikwenda kutolea Tanga
mjini.Mimi sikuambatana
naye.Huyo rafikiye aliyempa
ujauzito ndiye aliyekuja
kumchukua na kumpeleka
kwenda kuitoa hiyo mimba”
“Nyie watoto mnafanya mambo
ya hatari sana.Hili si suala la
kufanyia mchezo hata kidogo.Ni
suala zito sana.Inaonekana mimba
hiyo alitolewa vichochoroni na mtu
ambaye si mtaalamu .Kama ni hivyo inabidi aende akasafishwe
upya vinginevyo anaweza
akapoteza maisha.Ouh jamani
mambo gani haya yanamtokea
mwanafunzi ninayempenda?
Akasema mwalimu Anna
“ Mwalimu Anna ndiyo maana
nimekuja hapa kukuomba utafute
namna yakumsaidia Patricia ili
aweze kusafishwa na pili suala hili
lisifike kwa uongozi wa shule
.Wewe ndiye mama unayetulea
hapa shuleni tukiwa na matatizo
kama haya wewe ndiye kimbilio
letu.Naomba ulichukue suala hili
kama mama na umsaidie Patricia
aweze kupona na aendelee na
masomo yake .Bila msaada wako
hali yake itakuwa mbaya na
tunaweza tukampoteza” akasema
Elvis
“ Elvis umeichanganya sana na
sijui nifanye nini.Patricia ni
mwanafunzi ninayempenda mno
na siku zote ndoto yangu ni kuona akitimiza ndoto zake.Ouh
jamani Patricia” akasema
mwalimu Anna na kuvuta pumzi
ndefu.Akainama akafikiri na
kusema
“ Elvis suala hili ni gumu na
siwezi kutoa jibu la moja kwa moja
ni namna gani nitaweza kumsaidia
Patricia.Kesho nitampeleka
hospitali na kule atafanyiwa
uchunguzi ili kubaini ni jambo
gani linalomsumbua.Baada ya
uchunguzi wa madaktari ndipo
tutajua ni namna gani ya
kumsaidia”
“ Hapondipo penye tatizo
mwalimu Anna.Endapo atapimwa
na ikagundulika kwamba ametoa
mimba taarifa hii inaweza
kumletea matatizo kwa uongozi wa
shule na familia yake pia.Mwalimu
Ana suala hili halitakiwi kufika
kwa uongozi wa shule au mtu
mwingine .Nimekuja hapa
kukuomba kama mama tafadhali msaidie Patricia ili aweze kupona
na aendelee na masomo yake”
“ Elvis kama nilivyosema siwezi
kutoa jibu la moja kwa moja
kuhusu namna gani nitaweza
kumsaidia Patricia.Naomba
uniache kwa usiku huu nitafakari
nini nitafanya.Kesho asubuhi
tayari nitakuwa na jibu.Hata mimi
ninampenda Patricia na nitafanya
kila niwezalo kumsaidia . Mama
yake amekuwa akinipigia simu
mara kwa mara na kuniuliza
maendeleo ya mwanae,ana
matumaini makubwa sana na
mwanae huyu wa pekee.Kama
mama nitamsaidia wmanamke
mwenzangu ili mwanae aweze
kupona” akasema mwalimu Anna
“Mwalim Anna kuna ambo
lingine nataka kukuomba”
“ Jambo gani Elvis?
“ Ninaomba kesho
utakapompeleka Patricia hospitali
,niambatane nawe” Usijali kuhusu hilo.kama uko
tayari tutakwenda sote”
“ Ahsante sana mwalimu Anna
na samahani kwa taarifa hizi
nilizokuletea ambazo najua
zimekustua sana lakini wewe
ndiye mama yetu mlezi hapa
shuleni kwa hiyo tunapokuwa na
matatzio wewe ndiye mtu pekee
tunayeweza kukukimbilia”
“ Ahsante kwa Elvis kwa taarifa
hizi.Umefanya jambo la maana
sana kuja kunieleza lakini
ulipaswa kunieleza mapema ili
nione namna gani ya
kumsaidia.Ningejua mapema
yasingefika hapa yalipofika”
akasema mwalimu Ana na Elvis
akaondoka
“ Watoto hawa kwa nini
wanafanya mambo ya hatari
namna hii kuhatarisha maisha
yao?Bado siamini kama Patricia
mtoto mwenye bidii kubwa na akili
ya ajabu anataka kuyaharibu maisha yake.Itanilazimu nifanye
kila niwezalo ili kumsaidia.Kama
asiposaidiwa kila alichokifanyia
kazi kwa miaka hiyo yote
kitapotea” akawaza mwalimu Anna
halafu akaifungua bahasha
aliyopewa na Steve na kukuta
bunda la noti nyekundu akastuka
“ Hizi za nini tena?akajiuliza
huku akizihesabu fedha zile.
“ Elvis hakupaswa kunipa
fedha hizi ili nimsaidie
Patricia.Hata bila ya fedha
nilazima nimsaidie Patricia lakini
kwa vile amenipa mwenyewe
siwezi kuzikataa” akawaza walimu
Anna halafu akatoka na kuelekea
katika bweni la wasichana
kuangalia maendeleo ya Patricia..
********************
Uso wa mwalimu Anna
ulionyesha mstuko mkubwa
wakati akitoa katika chumba cha daktari mkuu wa hospitali ya
mkoa ambako Patricia alipelekwa
kwa ajiliya kufanyiwa
uchunguzi.Alionekna
kuchanganyikiwa.Elvis ambaye
alikuwa nje akimsubiri
akashangazwa na hali ile ya
mwalimu Anna akamsogelea
“ Mwalimu Anna daktari
anasemaje? Vipimo vinasemaje?
Akauliza Elvis.Mwalimu Anna
hakusema kitu akamshika Elvis
mkono na kuelekea katika benchi
la kupumzikia wakakaa
“ Elvis nimechangnyikiwa na
sijui nifanye nini”
“ Kwa nini mwalimu Anna?
Daktari anasemaje?
“ Elvis tatizo ni kubwa sana
tofauti na tulivyokuwa tukifikiria”
“ Daktari anasemaje? Vipimo
vinaonyeshaje?
“ Elvis nimetetemeka sana kwa
taarifa ya daktari” Niambie mwalimu
Anna.Daktari anasemaje? Patricia
na tatizo gani?
“ Tatizo la Patricia ni
kubwa.Imegundulika kwamba
daktari aliyemtoa mimba
hakumsafisha vizuri hivyo
kupelekea kizazi chake kuoza”
“ Ouh Mungu wangu..!!....Elvis
akastuka na kuweka mikono yake
kichwani
“ Kwa hiyo daktari
anasemaje?Watamsafisha upya?
“ Suluhisho pekee hapa la
kuyanusuru maisha ya Patricia ni
kumfanyia upasuaji na kuondoa
kizazi”
“ What ?! …Patricia atolewe
kizazi? Ina maana hatakuwa na
uwezo wa kupata mtoto katika
maisha yake yote?
“ Ndiyo Elvis.Kama akiondolewa
kizazi basi hatakuwa na uwezo wa
kupata mtoto katika maisha yake
yote yaliyobaki” Ouh Masikini Patricia.kwa nini
yanamtokea haya? Ndoto yake
nyingine kubwa ni siku moja kuwa
na familia.Kama akitolewa kizazi
ndoto hii haitatimia.Jamani
Patricia ataishi vipi? Akawaza
Elvis na kumgeukia mwalimu
Anna aliyekuwa ameinama
akitafakari
“ Mwalimu Anna hakuna njia
nyingine ya kuweza kumsaidia
Patricia zaidi ya kuondoa kizazi?
Akauliza Elvis
“ Hakuna Elvis.Hakuna njia
nyingine ya kumsaidia
Patricia.Kwa mujibu wa daktari ni
kwamba hali yake si nzuri na
inatakiwa afanyiwe upasuaji huo
haraka iwezekanavyo.”
“ Tutafanya nini basi mwalimu
Anna? Wewe umaeamua nini?
“ Patricia atalazwa hapa
hospitali.Taratibu zinafanyika ili
aweze kupelekwa wodini .Suala la
upasuaji itabidi lisubiri kwanza hadi mzazi wake na uongozi wa
shule ufahamishwe.Hili ni suala
kubwa na kwa ngazi iliyofikia sasa
inabidi wazazi na uongozi wa
shule wafahamu” akasema
mwalimu Anna
“Mwalimu Anna hatuwezi
kuendelea kulifanya jambo hili
kuwa siri? Nina wasi wasi mkubwa
endapo taarifa hizi zitamfikia
mama yake na uongozi wa shule”
akasema Elvis
“ Elvis hili ni suala zito na
linalohusisha uhai wa wanafunzi
ambaye mimi ndiye mlezi wake
kwa hiyo jukumu langu ni kutoa
taarifa sahihi kwa wazazi na
walimu.Endapo nitaficha juu ya
ugonjwa wa Patricia na baadae
ikagundulika kwamba nilisema
uongo nitajiweka katika matatizo
makubwa.Wewe unataka tufanye
nini Elvis? Akauliza mwalimu
Anna ninachotaka ni kuendelea
kulifanya suala hli liendelee kuwa
siri.Ongea na daktari na aandike
tatizo lingine kabisa ili
kumuepusha Patricia na matatizo
mengine.Mama yake hatakiwi
kujua chochote”
“ Elvis hilo ni suala gumu kwa
sasa.Kwanza sina hakika kama
daktari atakubali ,pili hata kama
akikubali nani ambaye
atamuuguza Patricia hapa
hospitali? Patricia atafanyiwa
upasuaji mkubwa kwa hiyo
anahitajika mtu wa karibu wa
kumuuguza hadi hapo
atakapopona.Kazi hii anatakiwa
kufanya mtu wake wa karibu
“ Usiogope kuhusu hilo
mwalimu Anna.Hapa Tanga mjini
ninaye binamu yangu moja
anafanya kazi katika benki ya
NMB.Ni mtu ambaye ninaelewana
naye sana kwani amekulia
nyumbani kwetu.Endapo nitaongea naye nina hakika lazima
atakubali kumsaidia Patricia kwa
sababu kwa hivi sasa yuko likizo
kwa hiyo atakuwa na nafasi nzuri
ya kumuhudumia .Kuhusu
daktari usiwe na shaka wale
tutaongea nao kwa pesa tu”
“ Hapana Elvis usifanye
hivyo,.Naomba usitumie pesa
yoyote tafadhali.Pesa uliyompa
jana inatosha kabisa”
“ Usijali mwalimu Anna,pesa ile
ya kwako .Nisubiri dakika mbili
niende hapo nyuma” akasema
Elvis na kutoka mbio kueleka
katika ATM ilikuwa pale hospitali
akachukua fedha kiasi cha shilingi
laki tatu na kurejea akamkabidhi
mwalimu Anna
“ Elvis kwa nini unafanya haya
yote?
“kwa sababu Patricia ni rafiki
yangu na nilimuahidi kwamba
nitakuwa naye katika nyakati
zote,lazima nitimize ahadi yangu.Muda unakwenda mwalimu
Anna nenda kaonane na daktari ili
tujue atatusaidiaje.Mimi
nawasiliana na binamu yangu
nimfahamishe kuhusu sula hili”
akasema Elvis mwalimu Anna
akainuka na kuelekea ofisini kwa
daktari.Elvis akachukua simu na
kumpigia binamu yake Scola
“ hallow Elvis habari ya
shule?Nimepanga nije wiki hii
kukusalimia hapo shguleni
nikuletee na zawazi zako” akasema
Scola baada ya kupokea simu
“ Habari nzuri Scola.Nimekuja
mjini leo.Niko hapa hospitali ya
mkoa”
“ Uko hospitali? Kuna nini?
Unaumwa? Akauliza Scola
“ Hapana siumwi Scola,ni rafiki
yangu ndiye anayeumwa.Uko wapi
hivi sasa?
“ Niko Saluni natengeneza
kucha”
“ Unaweza kuja hapa hospitali? Kuna tatizo gani?
“ Siwezi kukueleza katika
simu.Naomba uje sasa hivi hapa
hospitali” akasema Elvis
“ Ok nakuja sasa
hivi.Umeniogopesha sana Elvis”
akasema Scola na kukata simu
“ Elvis akaenda kukaa katika
bench lililokuwa nje ya ofisi ya
daktari.Baada ya kama dakika
ishirini muuguzi akaja na kitanda
cha magurudumu na kuingia
nacho ofisini kwa daktari na
baada ya muda akatoka
akikisukuma kitanda kile
ambacho juu yake alikuwa
amelala Patricia.Daktari pamoja
na mwalimu Anna nao wakatoka
,mwalimu Anna akamuomba Elvis
waongozane kuelekea wodini
ambako Patricia akapewa
kitanda.Wakati akiwa nje ya
wodi,simu yake ikaita ,alikuwa ni
Scola,akamuelekeza amfuate
katika wodi Elvis kuna nini? Mbona uko
huku? Unaumwa? Akauliza Scola
ambaye alikuwa na sura iliyojaa
wasiwasi.Elvis akamvuta pembeni
na kumueleza kila kitu kuhusiana
na matatizo ya Patricia
“ Ouh my gosh ! anaendeleaje?
Akauliza Scola kwa wasi wasi
“ hali yake si nzuri” akasema
Elvis na mara mwalmu Anna
akatoka mle wodini.Elvis
akamtambulisha kwa Scola
wakasalimiana
“ mwalimu Anna daktari
amesemaje? Akauliza Elvis
“ Amepokea ule mzigo na
amekubali kutusaidia.Kutokana
na hali ya Patricia kuendelea kuwa
mbaya usiku wa leo itabidi
afanyiwe upasuaji. Kwa maana
hiyo itanilazimu nisirejee shuleni
leo ili niendele kufuatilia sula hili”
akasema mwalimu Anna na wote
wakabaki kimya Napatwa na wasi wasi sana
mtoto wa watu kufanyiwa upasuaji
mkubwa namna hii bila ya mzazi
wake kufahamishwa.”akasema
mwalimu Anna
“ Usihofu wmalimu
Anna.Patricia mwenyewe hataki
mama yake afahamu kuhusu
suala hili.”
“Kwa hivi sasa Patricia yuko
katika maumivu makali na hana
uwezo wa kufanya maamuzi
yoyote kuhsu suala hili” akasema
mwalimu Anna
“ Kama ni hivyo basi sisi ndio
tunapaswa kubeba jukumu
lote.Tunatakiwa tuwe majasiri na
tukubaliane na chochote
kitakachotokea” akasema Scola
MIEZI MITATU BAADAE
Miezi mitatu imekwisha pita
toka Patricia afanyiwe upasuaji na
tayari amekwisha pona na kurejea masomoni.Hali yae ilikuwa nzuri
na hakuna aliyefahamu chochote
kuhusiana na kilichokuwa
kinamsumbua na kusababisha
afanyiwe upasuaji.Ilibaki ni siri
yao pekee yeye Patricia,Elvis ,
mwalimu Anna na Scola binamu
yake Elvis ambaye alifanya kazi
kubwa sana ya kumuuguza
Patricia wakati alipofanyiwa
upasuaji.
Japokuwa alikuwa anaendelea
vizuri na masomo yake lakini kuna
jambo moja kubwa ambalo
lilikuwa linamtesa sana.Ni suala la
kutoweza kupata mtoto tena
katika maisha yake
yaliyobakia.Elvis ambye
aliifahamu siri hii alijitahidi sana
kumpa moyo na kumfariji
Siku zilikatika na hatimaye
ukafika wakati wa kumaliza
shule.Bado ukaribu wao ulikuwa
mkubwa sana.Pale shuleni kila
mtu alifahamu kwamba lazimaPatricia na Elvis wana mahusiano
ya kimapenzi lakini ukweli ni
kwamba walikuwa marafiki wa
kawaida na hawakuwa wapenzi
kama watu
walivyodhani.Japokuwa Elvis
aliendelea kumpenda Patricia kila
uchao lakini alivuta subira ili
kuacha kwanza kidonda cha
Patricia kipone.Hakutaka
kumuingiza tena kwa haraka
katika mahusiano kwani siku zote
katika maongezi yao Patricia
aliweka wazi ni jinsi gani
anavyoyachukia mapenzi.Aliweka
wazi kwamba hatapenda tena
kwani haoni umuhimu wa kuingia
mapenzini na kuumizwa tena
“ Yalikuwa ni makosa yangu
hadi nikawa katia hali hii.Nastahili
niubebe mzigo huu mimi
mwenyewe” Hiyo ndiyo ilikuwa
kauli ya kila mara ya Patricia
wakiwa katika maongezi yenye
kuhusisha mambo ya mahusiano. Elvis aliyaona mateso na
machungu ya moyo aliyokuwa
nayo Patricia kila alipofikiria
kwamba hataweza kupata mtoto
katika maisha yake
yote,akaumuoea huruma
sana.Patricia alizidi kumuingia
moyoni na ndiye mwanamke pekee
ambaye aliupeleka mbio moyo
wake.Hakuwahi kutokea
mwanamke aliyempenda kama
alivyompenda Patricia na aliweka
nadhiri ya kuhakikisha
anafanikiwa kuwa naye maishani
Jioni moja wakiwa wamekaa
bustanini sehemu waliyopenda
sana kukutana ,Patricia
akamuuliza swali Elvis
“ Elvis,kuna jambo limekuwa
linanikwaza sana na
kunishangaza”
“ jambo gani Patricia?
“ Toka nimekufahamu siku zote
nimekuwa nikitegemea kwamba
lengo lako kubwa ni kuwa mwana sayansi,daktari au mhandisi na
sikutegemea hata simu moja
kwamba unataka kusoma mambo
hayo ya upelelezi unayotaka
kwenda kuyasomea.Kwa nini
usiwe daktari au hata rubani? Au
kwa nini usiwe mhandisi?Mimi
binafsi hainiingii akilini kwa mtu
kama wewe kwenda kusomea
mambo kama hayo sijui ya ujasusi
sijui mnayaitaje..” akasema
Patricia na kumfanya Elvis acheke
kicheko kikubwa
“ Patrcia si wewe peke yako
unayeniuliza swali hili.Hivi sasa
nina ugomvi na mama yangu
kuhusiana na maamuzi yangu ya
kutaka kujiunga na mafunzo ya
usalama wa taifa.Ukweli ni
kwamba nilipenda sana kufanya
kazi hii toka nikiwa mtoto
mdogo.Baba yangu alikuwa kanali
wa jeshi kwa hiyo nilipenda sana
mambo haya ya usalama na ndiyo
maana ndoto yangu kubwa ni kuingia katika kazi hii ya
ujasusi.Ninaipenda kazi hii toka
moyoni na kuna baba yangu
mdogo anayefanya kazi katika
idara ya usalama wa taifa
amekuwa ananipa moyo sana
kwamba kama ninaipenda kazi hii
basi atakuwa tayari kunisaidia”
akasema Elvis
“ Sikuzuii kuifanya kazi hiyo
Elvis lakini sina hakika kama
umefanya chaguo
sahihi.Muonekano wako si mtu wa
kufanya kazi kama hizo ambazo ni
za hatari kubwa.”
“ Usihofu Patricia.Ninaipenda
kazi hii na ndiyo pekee ambayo
ninataka kuifanya katika maisha
yangu” akasema Elvis na
kumfanya Patricia aendele
kumtazama kwa macho makali.
***********************
Hatimaye baada ya kumaliza
masomo yao ya kidato cha sita
Elvis na Patricia walifanikiwa
kupata kazi ya muda katika hoteli
ya kitalii wakati wakisubiri
matokeo yao .Kwa sasa Elvis
alikuwa akiishi jijini Dar es
salaam katika nyumba yao iliyoko
Mbezi.Urafiki baina yao uliendelea
kuwa mkubwa na wakaribu zaidi
hata baada ya kumaliza masomo.
Ilikuwa ni siku ya ijumaa wote
wawili wakiwa katika zamu ya
usiku siku ambayo wageni
walikuwa wachache sana hapo
hotelini hivyo Patricia na Elvis
wakapata wasaa wa kukaa pamoja
na kuzungumza mambno yao ya
maisha.Walienda kukaa katika viti
vya kupumzikia pembeni ya
bwawa la kuogelea.Siku hii
Patricia alionekana kuwa na
mawazo mengi
“ Patricia unawaza nini?
Akauliza Elvis bada ya kumuona Patricia yuko kimya na
ameyaelekeza macho yake juu
angani.
“ Ninawaza mambo mengi
sana.Nawaza kuhusu safari yangu
ya maisha.Nafikiria ndoto zangu
nyingi ambazo natakiwa nizitimize
,nyingine hazitawezekana tena
lakini nitajitahidi niweze kutimiza
asilimi 98 ya malengo yangu.”
Akasema Patricia
“ Patricia wewe ni mwanamke
wa aina yake na usiyekubali
kushindwa na jambo.Toka
nimekufahamu nimejifunza
mambo mengi kupitia
kwako.Umenifundisha namna ya
kupambana kufikia malengo ya
maisha.Nimejifunza kupambana
na changamoto zozote
zinazojitokeza katika
kuyakamilisha malengo
binafsi.Nashukuru sana kwa
elimu hii ya bila darasa”akasema Elvis .Patricia akatabasamu na
kumshika mkono Elvis
“ Elvis haya yote yamewezekana
kwa sababu yako ya watu wenye
mapenzi na mimi ukiwamo
wewe.Huwezi kujua una nafasi
gani kwangu.Wewe ndiye
umekuwa kama malaika wangu
mlinzi.Umekuwa nami hata katika
nyakati zile ngumu ambazo
hakuna mtu ambaye angeweza
kuwa nami lakini wewe ulisimama
pamoja nami,ulihuzunika
nami,ukacheka na kufurahi
nami.Kuna nyakati huwa
ninajiuliza kwa nini unanifanyia
haya yote? Ninajiuliza bila kupata
jibu nitakulipa kitu gani kwa
mambo haya makubwa
uliyonifanyia.Nimekuwa nikitafuta
siku nyingi nafasi ya kukuuliza ni
kwa nini unanifanya haya? Why
me? akauliza Patricia.Elvis
akatabasamu halafu akakohoa
kidogo na kusema Patricia may be its right time
now to know the truth”
“ Truth ?! What truth? Akauliza
Patricia huku sura yake
ikionyesha wasi wasi
“ Itis the truth about me and my
heart” akasema Elvis huku
Patricia akimuangalia kwa
wasiwasi.Elvis akameza mate na
kusema
“Patricia kwa muda mrefu
nimekuwa nikitafuta nafasi kama
hii ambayo nitakueleza kile
kilichomo moyoni mwangu na kwa
nini nimeyafanya haya yote
niliyoyafanya.Sikuweza kukueleza
mapema kutokana na na
kukabiliwa na mambo mengi ya
masomo na kimaisha” Elvis
akatulia kidogo akamtazama
Patricia halafu akaendelea
“ Patricia ni ukweli huu
nitakaokwambia ndio
utakaoniweka huru toka
kifungoni” Ni ukweli gani huo Elvis?
Please tell me” akasema Patricia
“ Patricia Mungu ametuumba na
kutuweka duniani tufurahi na
kuutukuza uumbaji wake na
katika maisha haya ametupa kila
mmoja na mtu wake ambaye
ataambatana naye na kuwa mwili
mmoja.Patricia moyo wangu
umekuona wewe na kutua kwako
kiasi ambacho hauwezi
kubanduka tena.Ninakupenda
Patricia kwa moyo wangu wote
Nina hakika kwamba wewe ndiye
mwanamke pekee katika dunia hii
ambaye umeumbwa kwa ajili
yangu.Nguvu ya pendo langu
kwako ndiyo inayonifaya niweze
kusimama nawe hata katika
nyakati zile ngumu.Tafadhali
Patricia naomba uufungue moyo
wako na unikubalie niwe mpenzi
wako” akasema Elvis.Patricia
akabaki ameduwaa alikosa neno la
kuongea.Walitazamana kwa dakika kadhaa kisha Patricia
akasema
“ Elvis nmekosa neno la
kusema.Sijui nikujibu nini .”
akasema Patricia na mara macho
yake yakajaa machozi.
“ Tafadhali usitoe machozi
Patricia.Futa machozi halikuwa
lengo langu kukukwaza.” akasema
Elvis
“ Hujanikwaza Elvis lakini
nimepatwa na mstuko mkubwa
sana kwa mtu kama wewe
kunipenda mtu kama
mimi.Siamini na haikuwahi
kuniingia akilini hata siku moja
kwamba utatokea kunipenda.
Ahsante kwa kunipenda Elvis
lakini nasikitika kwamba
umeniambia ukweli wako kwa
kuchelewa”
“ Kwa nini unasema hivyo
Patricia?
“ Kwa sababu moyo wangu
hauna hata chembe ya mapenzitena kwa mwanaume yeyote.Zaidi
ya yote Elvis unahitaji kuwa na
mwanamke mwenye mapenzi ya
kweli nawe,ambaye anatoka katika
familia bora kama yako
,mwanamke amb……..” akasema
Patricia lakini Elvis akamkatisha
“ Sikiliza Patricia,sihitaji
mwanamke mwingine ,nakuhitaji
wewe pekee.Siko tayari kuwa na
mpenzi ambaye si wewe” akasema
Elvis.Patricia akafuta machozi na
kusema
“ Elvis you were there beside me
all the time and you know exactly
what I went through.I don’t think
I’m the right woman for you”
Akasema Patricia.Elvis
akatabasamu na kusema
“ Patricia ni kwa sababu ya
upendo wangu usiopimika kwako
ndiyo maana niko nawe toka
tulipofahamiana na ni kwa sababu
ya upendo huo huo ndio maana
niko nawe hapa sasa hivi