I DIED TO SAVE MY PRESDENT
Sehemu 18
Ni saa tano za asubuhi,siku
ya jumapili bado Patricia na Elvis
wako kitandani wakijipumzisha
kutokana na uchovu wa siku
iliyotangulia.Wote walikunywa
pombe nyingi katika sherehe ya
kuzaliwa Patricia.Mlio wa simu
liyokuwa ikiita ndio uliomstua
Elvis akainuka na kwenda
mezani.Ilikuwa ni simu ya Patricia
iliyokuwa ikiita.Katika kioo cha
simu iliandika “ Dharura kaziniElvis akaichukua simu ile na
kumuamsha mke wake
“ mmhh my darling,niache
nilale kidogo .Nimechoka sana”
akasema Patricia huku macho
yake yakionyesha wazi kwamba
alikuwa na uchovu mwingi
“ Pokea simu hii
darling,imepigwa katika namba ya
dharura ya kazini kwako”
akasema Elvis.Neno dharura
likamstua Patricia akainuka
haraka na kuichukua simu
akabonyeza kitufe cha kupokelea
“ Hallow “ akasema
“ Dr Patricia kuna dharura
imetokea”
“ Jambo gani limetokea
Amanda?akauliza
“ Cindy amezinduka”
“ Cindy?!! Patricia
akashangaa Ndiyo amezinduka sasa hivi”
“ Anaweza kuongea?
Anajifahamu?
“ Ndiyo anafahamu zake na
anaweza kuongea japo anasikika
kwa mbali ”
“ Ok nakuja sasa hivi”
akasemaPatricia na kukata simu
.Akavuta pumzi ndefu
“ Kuna nini kimetokea?
Akauliza Elvis
“ Kuna mgonjwa mmoja
ambaye aliletwa pale hospitalini
kwetu akitokea hospitali ya taifa
ya Muhimbili akiwa hana
fahamu.Kwa mujibu wa taarifa
iliyotoka Muhimbili ni kwamba
mwanadada huyo aliokotwa na
wasamaria wema na kupelekwa
pale akiwa hana fahamu .Baada
ya kumchunguza wakaamua
kumleta pale kwetu ili tumfanyie uchunguzi wa kina kuhusianana
nini kinamsumbua kichwani”
“ Nini kilimpelekea apoteze
fahamu? Akauliza Elvis
“ Kwa mujibu wa uchunguzi
tuliomfanyia,alipoteza fahamu kwa
sababu ya kupigwa sana hasa
sehemu za kichwani.Inaonekana
watu waliompiga walikuwa na
lengo la kumuua.”
“ Dah jamani dunia hii imejaa
watu makatili sana”: akasema
Elvis
“ Kwa muda wa miezi miwili
amekaa bila fahamu na katika
muda huo wote hakuna hata
ndugu yake mmoja aliyejitokeza
ndiyo maana nikaamua kumpa
jina la Cindy” akasema Patricia
“ So are you going there?
Akauliza Elvis Yes ! I have to go there”
akasema Patricia
“ I’ll go with you.Umechoka
sana na siwezi kukuacha
ukaendesha gari ukiwa katika
hali hii.Nitakupeleka kazini na
kukurudisha” akasema Elvis
.Wakaingia bafuni kuoga kisha
wakaelekea katika chumba cha
kulia chakula wakapata kifungua
kinywa
“ Sylvie,Doreen bado
hajaamka? Patricia akamuuliza
mtumishi wao wa ndani
“ Aliamka ,akaomba kahawa
kisha akarudi tena kulala” akajibu
Sylvie
“ Ok ngoja nikamuangalie
kabla hatujaondoka.Jana alikuwa
amelewa sana” akasema Patricia
na kuinuka akaelekea katika
chumba cha wageni alikolala Doreen.Bila kubisha hodi Patricia
akaingia chumbani na kumkuta
Doreen amejilaza kitandani
“ Bado umelala? Inaonekana
shughuli ya jana ilikuwa nzito
sana” akasema Patricia huku
akitabasamu.Doreen akainuka na
kunyoosha mikono akamfanyia
ishara Patricia akae kitandani
“ Enhee nipe habari
shoga.Mambo yalikwendaje?
“ Mhhhhh..!!!!” Doreen
akaguna
“ Mbona unaguna?
“ Mambo hayakwenda kama
tulivyopanga” akasema Doreen
“ What happened?
Doreen akainuka na kukaa
kisha akasema
” Nilijitahidi sana kadiri
niwezavyo bila mafanikio.Elvis alikuwa amelala fofofo.Alikuwa
amezidiwa na kilevi”
“ Dah ! So what happened?
Alikuona?
“ Nilijikuta nimepitiwa na
usingizi na nikastuka asubuhi
Elvis akiwa amewasha taa
ananishangaa.Shoga ninasikia
aibu sitaki hata kuonekana huko
nje hadi atakapoondoka.Sijui
nitamtazamaje Elvis usoni “
“ Alisemaje alipokuona?
Akauliza Patricia huku sura yake
ikionyesha wasiwasi mwingi
“ Alistuka sana.Sura yake
ilipata wasiwasi
mkubwa.Hakuamini
kilichotokea.Nilimuomba
samahani nikaondoka haraka kuja
huku.Patricia tumefanya jambo la
aibu sana.Nasikia aibu mno”
akasema Doreen “ samahani sana Doreen kwa
kukuingiza katika jambo hili”
“ Usijali Patricia ,yote hii
ilikuwa ni katika kutafuta
suluhisho la matatizo yako.”
Patricia akakaa kimya akafikiri na
kusema
“ So what are we going to do
now? Akauliza
“ I don’t know Patricia.I’m so
scared to do it again” akasema
Doreen.Patricia akainama
akatafakari na kusema
“ Ahsante Doreen kwa
kujitolea kunisaidia.kwa sasa
naelekea hospitali kuna dharura
imetokea.Nitakuja kukuona jioni
tutaongea zaidi”akasema Patricia
“ Elvis naye anatoka?
Ninaogopa hata kumtazama usoni”
akasema Doreen “ Elvis naye anaondoka.Ndiye
anayenipeleka hospitali.”
“ Ok hata mimi ngoja
nijiandae niondoke niende
nyumbani nikapumzike .Leo
sintatoka kabisa” akasema Doreen
Patricia akatoka mle
chumbani akamuelekeza
mtumishi wake kazi za kufanya
kisha yeye na mumewewakaingia
garini na kuondoka kuelekea
hospitali
‘ Patricia ,hivi Doreen anaishi
na nani?akauliza Elvis.Patricia
akastushwa kidogo kwa swali lile
“ Unauliza Doreen anaishi na
nani..?
“ Ndiyo.Doreen anaishi na
nani? Ana mume?
“ Hana mume anaishi peke
yake.Kwa nini umeuliza? Nilihitaji tu kufahamu kwa
sababu nilishangaa uliponiambia
kwamba alilala pale nyumbani
nikajiuliza angewezaje kufanya
hivyo kama tayari ana mume
wake”
Patricia akacheka kidogo na
kusema
“ Doreen hana mume na
ndiyo maana yuko huru kufanya
jambo lolote”
“ Ok sawa.Uliionaje sherehe
ya jana?
“ Sherehe ilipendeza sana
kiasi kwamba siwezi hata
kuielezea.Japokuwa matatizo
madogo madogo kama ya kulewa
kupitiliza yalikuwepo lakini kwa
ujumla wake shertehe ilikuwa
nzuri sana.”
“ jana ulikunywa pombe
nyingi sana” akasema Elvis Kweli nilikunywa
sana.Baada ya wageni kuondoka
tulibaki tunaendelea kunywa mimi
na Doreen na sikumbuki hata
mwenzangu aliondoka saa ngapi
kwenda kulala.Sitaki tena kurudia
unywaji pombe wa namna ile”
akasema Patricia.Elvis akacheka
kidogo na kusema’
“ Kitugani kilikufanya unywe
pombe namna ile?
“ Ni furaha tu niliyokuwa
nayo jana.Nilitaka nifurahi kwa
sababu kwa siku za hivi karibuni
kichwa changu kimekuwa na
mambo mengi sana kwa hiyo jana
nikaona ni bora niitumie siku ile
kujisahaulisha mambo yote na
kufurahi.” Akasema Patricia.Elvis
akageuza shingo na kumtazama
mkewe Patricia naomba tafadhali
usiwaze chochote kuhusiana na
mambo yale aliyokwambia
mama.Niachie mimi suala hili
nitalishughulikia kama
nilivyokuahidi.” akaema
Elvis.Patricia akatabasamu bila
kusema chochote safari ikaendelea
Walifika hospitali Patricia
akampeleka mumewe sehemu ya
kupumzikia akamuomba amsubiri
pale
“ I must do something”
akawaza Elvis halafu akachukua
simu yake na kuzitafuta namba za
simu za Doreen akampigia
“ Hallow Elvis” akasema
Doreen baada ya kupokea simu
“ Doreen nahitaji kukuona
,umeshaondoka hapo nyumbani? Nimeshaondoka niko njiani
kuelekea nyumbani kwangu.Kuna
tatizo lolote Elvis?
“ Hakuna tatizo ila nahitaji
kukuona.We need to talk”
“ Sawa Elvis,unataka tuonane
wapi? Nielekeze sehemu
unakotaka tukutane”
“ Usisumbuke Doreen
ninakuja nyumbani kwako”
akasema Elvis huku akishuka
ngazi na kuelekea lilipo gari lake.
“ Najua Elvis anataka
kuongelea kuhusiana na lile tukio
la jana.Niliuona uso wake namna
alivyokuwa akinitazama.Patricia
ameniingiza katika mgogoro
mkubwa.I’m so stupid.Nimekubali
kufanya jambo kama lile na
kujidhalilisha namna ile.Ninaona
aibu sana na sijui nitamtazamaje
Elvis”akawaza Doreen lakini maraakatabasamu baada ya
kukumbuka kitu
“ Pamoja na mambo
kutokwenda kama tulivyotaka
lakini kuna jambo nililiona usoni
kwa Elvis.Japokuwa alistuka sana
aliponiona lakini alikuwa
ananitamani.Kuna kila dalili
kwamba Elvis alitamani sana
kufanya nami mapenzi lakini
alikuwa akimuogopa mke
wake.Yawezekana hilo ndilo jambo
linalomleta kwangu.” Akawaza
Doreen na kukumbuka picha ya
tukio la jana
“ Mwili wangu ulipogusana na
Elvis nilipatwa na msisismko wa
aina yake.Nilihisi ni kama
nimelala na mwanaume
wangu.Elvis ni mwanaume
anayesisimua sana.Tayari
tulikwisha anza kufanya mapenzi kama nisingepiga ule ukulele kwa
raha ya ajabu niliyoisikia basi
asingestuka..Sijui nitafanya nini
kumpata Elvis tumalizie pale
tulipoishia .Ouh jamani sijui kwa
nini mawazo kama haya
yananijia.Lakini yote haya
ameyataka Patricia mwenyewe ”
akawaza Doreen na kukumbuka
msisimko alioupata wakati
akizichezea nyeti za Elvis.
“ Ni muda mrefu nilimtamani
Elvis lakini sikuwa na mawazo
yoyote kwamba siku moja mimi na
yeye tunaweza kulala kitanda
kimoja tena katika hali ya
utupu.Elvis ni mume wa rafiki
yangu kipenzi na siku zote
nimeliheshimu hilo..Ni Patricia
mwenyewe ndiye
anayenisbabishia niwaze mawazo
ya namna hii baada ya kunitaka nilale na mumewake.Japokuwa
Elvis ni mwanaume
ninayemtamani sana lakini sikuwa
tayari kulala naye lakini Patricia
alinilazimisha sanahadi nikakubali
na baada ya Elvis kuuona utupu
wangu sina cha kuogopa
tena.Lazima ndoto yangu
itimie.Lazima nitembee naye.”
akawaza Doreen wakati akikata
kona kuingia nyumbani kwake
.Martha mtumishi wake wa ndani
alimfungulia geti akaingiza gari
halafu akaelekea moja kwa moja
chumbani kwake ambako alioga
haraka haraka na kujiandaa kwa
ajili ya kukutana na
Elvis.Alipomaliza kujiandaa
akapanda kitandani na
kujilaza.Picha ya tuko la jana
haikuacha kumjia kichwani. Nina hakika kinachomleta
Elvis ni kuhusianana tukio la
jana tu.yawezekana anataka kuja
kuende………….”alikatishwa
mawazo yake na mtu aliyebisha
hodi katika mlango
wake.Akainukana kwenda
kuufungua Alikuwa ni mtumishi
wake wa ndani
“ Dada yule mgeni uliyesema
akija nimkaribishe sebuleni tayari
amekwisha fika” akasema Martha
mtumishi wa ndani wa Doreen
“ Ok Martha mpeleke katika
chumba cha maongezi” akasema
Doreen kisha akaufunga mlango
wake na kuuegemea.Mapigo ya
moyo wake yalibadilika na kuanza
kwenda kasi
“ Naona aibu sana kukutana
tena ana kwa ana na Elvis.”
Akawaza halafu akaenda katika meza yake ya vipodozi akajitazama
usoni
“lakini kwa nini niogope w
akati ni mke wake ndiye
aliyesababisha haya yote? Sikuwa
nikihitaji jambo kama hili litokee
lakini Patricia amelazimisha hadi
limetokea.Elvis amekwisha uona
utupu wangu na nina hakika
hataacha kunifuata kama nyuki
.Potelea mbali litakalotokea
nalitokee tu siwezi kuendelea
kumuogopa ,kama akitaka penzi
mimi nitampatia tu kwani tayari
nimeruhusiwa na mke wake na
hata hivyo Elvis ni mwanaume
niliyemtamani siku nyingi sana.”
Akawaza Doreen kisha akafungua
mlango akatoka na kuelekea
katika chumba cha maongezi aliko
Elvis Elvis ! karibu sana”
akasema Doreen huku
akijilazimisha kutabasamu
“ Doreen samahani sana kwa
kukusumbua .Najua muda huu
ulikuwa unapumzika”
“ Usijali Elvis,karibu sana.”
Akasema Doreen huku akijitahidi
kuyaficha macho yake yasikutane
na yale ya Elvis.
“ Uhhm Doreen nimelazimika
kuja kukuona ili tuzungumzie
suala lile lililotokea jana
usiku.Bado ni….” Akaanzisha
mazungumzo Elvis lakini Doreen
akamkatisha
“ Elvis utanisamehe sana kwa
tukio lile la aibu.Hata mimi
mwenyewe sielewi
lilitokeaje.Naomba samahani sana
Elvis na tafadhalinaombausimweleze Patricia “ akasema
Doreen
“ Doreen najua ni pombe
mlizokunywa jana ndizo
zilizosababisha jambo lile
litokee.Sote tulikuwa tumelewa
sana jana.Lakini ninachojiuliza ni
kwa nini ukaacha vyumba vingine
vyote na kuingia kwangu? Ni kwa
nini ukanivua hadi nguo yangu ya
ndani na kunipandisha hisia ili
tufanye mapenzi? Kwa nini
ulifanya vile? Doreen ni sisi pekee
tunaofahamu nini kilitokea na
wala sintomueleza mke wangu
kwa hiyo tafadhalinaomba
unieleze ukweli,ni kweli ulikuwa
umelewa au ulidhamiria kufanya
vile? Niambie ukweli nitakuelewa
Doreen “ akasema Elvis
“ Elvis kusema ukweli sikuwa
nikijitambua kutokana na pombe nilizokuwa nimekunywa.Baada ya
sherehe kumalizika na wageni
wote kuondoka nilikuwa nimelewa
sana na kwa hiyo Patricia
akanishauri kwamba nilale pale
pale nyumbani.Tuliendelea
kunywa pombe hadi usiku mwingi
nikamwambia Patricia anionyeshe
chumba nikalale lakini alikuwa
amelewa hajitambui hivyo
nikainuka mwenyewe na kuanza
kutafuta chumba kilipo nikajikuta
nimeingia katika chumba
chenu.Elvis sina maelezo ya
kutosha kulielezea jambo hili kwa
sababu kuna mambo hata mimi
sikumbuki yalitokeaje”akasema
Doreen
“ Natamani sana kukubaliana
nawe Doreen lakini kitu ambacho
hakiniingi akilini ni kwamba kama
ulikuwa umelewa kiasi chakutojitambua kwa nini basi
ukavua nguo zako zote na
kuziweka sofani kisha ukapanda
kitandani mtupu? Pale kitandani
ulimkuta mtu amelala kwa nini
ukaanza kumchezea kwa
madhumuniya kufanya mapenzi?
Akauliia Elvis.Swali lile
likambabaisha Doreen
akashindwa kujibu
“Naomba unijbu Doreen.Ni
kweli ulikuwa umelewa au
ulidhamiria kufanya vile?
Akauliza Elvis
“ Elvis,..” Doreen akataka
kusema kitu lakini akaogopa
“ Tell me please” akasisitiza
Elvis
“ Naomba uniambie
ulijisikiaje uliponiona asubuhi ni mimi ndiye niliyelala nawe na si
mkeo Patricia?
Elvis akamuangalia Doreen kwa
mshangao mkubwa
“ I was angry,very angry….”
Doreen akatabasamu kidogo na
kusema
“ No Elvis,hukuwa
umekasirika.Ulikuwa unamuogopa
mkeo Patricia asijue .I saw your
face.You needed it.You needed me
,right? Akasema Doreen na
kumfanya Elvisi azidi
kumshangaa.
“ Doreen mambo gani hayo
unayasema.Wewe ni rafiki mkuwa
wa mke wangu,unadhani Patricia
angesema nini endapo angekukuta
chumbani kwake tena ukiwa
mtupu? Halafu ulijua kabisa
kwamba umelala kitandani na
mume wa rafikiyako kipenzi na wakati nikijiandaa kufanya tendo
la ndoa nikidhani niko na mke
wangu wala hukuonekana
kustuka.Ni wazi ulikuwa
umedhamiria jambo lile
litokee.Kwa nini Doreen.kwa nini
ulitakakufanya vile? Kwanini
ulitaka kumsaliti rafiki yako
kipenzi? Akauliza Elvis.Doreen
akamtazama na kuuliza
“ Elvis why are you here?
Akauliza Doreen huku
akimsogelea Elvis.
“ I’m here to find answers”
akajibu Elvis
“ No Elvis.You are not here for
answers” akasema Doreen huku
akimkaribia zaidi Elvis na
kukigusisha kifua chake katika
kifua cha Elvis na kuyafanya
mapigo ya moyo ya Elvis
yabadilike You are here because you
need something.Tell me what do
you want Elvis?Usiogope Elvis
tuko hapa peke yetu,mkeo hayupo
wala hakuna anayetuona.So tell
me what do you want?” akasema
Doreen .Elvis aliendelea
kumtazama akashindwa aseme
nini.
“ Why are you doing this
Doreen.” Akauliza Elvis
“ Elvis mbona unauliza
maswali mengi sana.Niambie bila
kunificha ni kitu gani umekifuata
hapa kwangu?Kama hutaki
kuniambia basi nitakwambia .”
Akasema Doreen na taratibu
akafumba macho na kuusogeza
mdomo wake karibu na mdomo wa
Elvis,akambusu na ghafla Elvis
kama mbogo majeruhi akamshika Doreen kwa nguvu na kuanza
kunyonyana nadimi.
Doreen tayari alipandisha
mashetani yake ,alikuwa akihema
haraka haraka.Hakutaka
kupoteza muda akaanza kufungua
vifungo vya shati la Elvis.Ghafla
Elvis akakurupuka na
kumsukuma
“ Elvis,why? What happened?
“ No I cant do this.I real cant”
“ Elvis,usinifanyie hivyo
tafadhali.Nafahamu umekuja
kunifuata mimi.Sasa unaogopa
nini? Hakuna atakayefahamu na
wala mkeo Patricia hatajua
lolote.Please Elvis I need you”
akasema Doreen huku
akimsogelea Elvis
“ No Doreen stop.!..akasema
kwa ukali Elvis huku akihema
kwa nguvu. Walisimama kwa sekunde kadhaa
wakitazamana kila mmoja
akihema kwa nguvu.Vifungo vya
nguo aliyokuwa ameivaa Doreen
vilikuwa vimefunguka na hivyo
kuifanya sehemu ya matiti yake
mazuri kuonekana na kumpa
wakati mgumu sana Elvis
“ Hili ni jaribu kali sana.Sijui
ni kitu gani hasa kilichonileta
huku kwa Doreen.” Akawaza Elvis
huku akiendelea kumtumbulia
macho Doreen
“ Elvis tafadhali naomba
usiogope kitu.Nafahamu
unanitaka lakini
unaogopa.Hakuna atakayefahamu
chochote kuhusiana na jambo
hili.I need you and I’ll give you
everything that you want hata vile
ambavyo umeshindwa kuvipata
kwa mkeo kwangu nitakupa” akasema Doreen .Kauli ile
ikamstua kidogo Elvis akauliza
“ Doreen,kuna jambo lolote
ambalo Patricia amekueleza kwa
siku hizi za karibuni?
“ Jambo gani hilo?
“ Hajakueleza jambo lolote
kuhusiana na mambo ya ndani ya
ndoa yetu?
“ Kuna jambo Fulani
alinieleza”
” Jambo gani? “
“ Ni kuhusiana na yeye
kutopata mtoto”
Elvis akashusha pumzi
akamuangalia Doreen na
kumuuliza
“ Alikueleza sababu za yeye
kutokupata mtoto?
“ Ndiyo alinieleza kila kitu”
Elvis Akakaa kimya kidogo kisha
akasema siku chache zilizopita
,ndugu zangu wakiongozwa na
mama walianza kuhoji kuhusiana
na kwa nini toka tumeoana hadi
leo hii hatujafanikiwa kupata
mtoto.Hakuna anayefahamu ni
kwa nini sisi hatuna mtoto hadi
leo hii.” akanyamaza kidogo
akatazama chini halafu akainua
kichwa na kuendelea
“ Kitendo cha ndugu zangu
kuanza kuulizia kuhusiana na
masuala ya mtoto kimemkosesha
amani mke wangu .Juzi
aliniambia kitu ambacho
kilinishangaza sana.Aliniambia
kwamba yuko tayari mimi nizae na
mwanamke mwingine nje ya
ndoa.Nilimkatalia kuhusiana na
jambo hilo lakini hakuonekana
kuridhika.Tukio lililtokea jana
linanifanya nianze kuhisi kwamba yawezekana mlikuwa mmepanga
litokee.Hiyo ndiyo sababu
nimekuja hapa kwako ili niweze
kuupata ukweli wa tukio lile.Ni
kweli mlikuwa mmepanga na
Patricia kwamba nilale nawe?
Naomba usinifiche Doreen”
akasema Elvis.Doreen alionyesha
wasi wasi mwingi.Alishindwa ajibu
nini.Kwa mbali macho yake
yakaonekana kulengwa na
machozi
“ Elvis naomba nikwambie
ukweli.” Akasema Doreen halafu
akainama akafikiri kwa muda na
kusema
“ Elvis tafadhali naomba
usikasirike lakini ukweli
nikwamba lile lilikuwa ni tukio la
kupangwa..Tulilipanga mimi na
Patricia.” Ouh Mungu wangu
!!akasema Elvis na kusimama
akashika kichwa chake.Doreen
akaendelea
“ Patricia alinifuata akanieleza
matatizo yake na namna
anavyoteseka kwa kukosa
mtoto.Aliniambia kwamba anataka
uwe na furaha maishani mwako
na furaha hiyo ingekamilika
endapo tu ungekuwa na
mtoto.Patricia anaogopa kwamba
siku moja shinikizo toka kwa
ndugu zako litazidi na utaamua
kuzaa na mwanamke ambaye yeye
hamfahamu na hivyo kuhatarisha
ndoa yenu na kwa sababu
anakupenda ndiyo maana akaona
ni vyema kama atakupa nafasi ya
kuweza kuzaa na mwanamke
ambaye yeye anamuamini
.Ulipokataa kufanya hivyo alikuja kwangu na kuniomba nimsaidie
katika tatizo lake hili,.Aliniomba
nizae nawe .Nilimuuliza kama uko
tayari kwa jambo hilo akasema
kwamba alikueleza lakini
haukuwa tayari.Kwa upande
wangu sikuwa tayari kufanya
jambo kama hili hasa kutokana na
namna tunavyoheshimiana lakini
Patricia alinililia sana nikamuonea
huruma na kukubali kumsaidia
ndipo tulipopanga ule mpango na
yakatokea yale yaliyotokea.Elvis
naomba unisamehe sana,nilifanya
vile kwa ajili ya kumsaidia rafiki
yangu “ akasema Doreen.Elvis
akamtazama kwa macho makali
na kusema
“ Siamini kama ni kweli
mmefikia hatua hii.How could you
do this?Mnafahamu madhara
yake? Nilikwisha mwambia Patricia kwamba asiumize kichwa
chake na jambo hili lakini hataki
kunielewa,.What else should I do
to prove to her that I love her with
all my heart? Akasema Elvis kwa
ukali.Jambo lile lilionekana
kumchukiza mno.
“ Elvis tulikuwa tunajaribu
kutafuta suluhu ya tatizo hili.Cant
you see how Patricia is suffering
right now? Akasema Doreen naye
sauti yake ilionekana kuanza
kuwa kali
“ so this is the solution? You
are making things worse than
solving the problem.” Akasema
Elvis
“ Elvis,Patricia loves you so
much na ndiyo maana yuko tayari
kufanya jambo kama hili kwa ajili
ya kukupatia wwewe furaha.Do you think this is easy for her?
Akauliza Doreen
“ Nafahamu mke wangu
ananipenda sana na lengo lake ni
kuniona nikiwa na furaha lakini
njia hii anayotaka kuitumia si
sahihi hata kidogo.Mimi
ninampenda kwa jinsi alivyo na
wala suala la kukosa mtoto
halipunguzi hata chembe moja ya
upendo wangu kwake.Siku zote
nimekuwa nikimuasa kwamba
maneno mengi yatasemwa lakini
anatakiwa awe mvumilivu .Kukosa
mtoto si mwisho wa maisha”
akasema Elvis.Doreen
akamtazama kwa makini na
kusema
“ Hongera kwa msimamo huo
lakini nina hakika moyoni mwako
utakuwa ukiumia sana kwa
kukosa mtoto japokuwa hutaki kuweka wazi.Nina hakika vile vile
kwamba siku moja itafika
utashindwa kuvumilia na
utaamua kuzaa nje ya ndoa
yako.Patricia tayariamekwisha
liona hilo na ndiyo maana
amekubali kwamba uwe na mtoto
wan je ya ndoa lakini toka kwa
mwanamke anayemfahamu na
kumuamini na katika hilo
amenichagua mimi.” akasema
Doreen.Elvis akainama akafikiri
na kusema
“ Iwas there when it
happened.Nilikuwepo na
kushuhudia wakati Patricia
anapoteza uwezo wa
kuzaa.Nilisimama pamoja naye
.Nilimpenda hata kabla ya
matatizo yale kumkutana
nitaendelea kumpenda siku zote
za uhai wangu.Nilimuoa Patricia kwa sababu ninampenda kwa
moyo wangu wote na siumizwi kwa
hali yake ya kukosa mtoto kwa
sababu nililifahamu jambo hili
toka awali na nikawa tayari
kukabiliana nalo.Kuhusu kuzaa
mtoto na mwanamke mwingine
hilo ni jambo ambalo sintaweza
kulifanya.Sijali kama ni yeye
anayetaka ama nani lakini siwezi
kufanya hivyo.”akasema Elvis
“ Kwa nini unafanya hivyo
Elvis? Kwa nini hutaki kumsikiliza
mkeo? Kwa nini hutaki kumuona
Patricia akiwa na furaha? I beg
you, do what she wants you to do
and you can make her happy”
akasema Doreen
“ Ninampenda sana mke
wangu na ndiyo maana sitaki
kufanya hivyo anavyotaka nifanye
kwa sababu ninafahamu lazima ataumia sana moyoni.Halafu ni
kwa nini unanisisitiza sana
kuhusu kufanya jambo hili?
Akauliza Elvis
“ Its because I’m a woman
and I know how a woman feels
pale anapundua kwamba hana
uwezo wa kuzaa mtoto” akasema
Doreen
“ Think about it Elvis and if
you want to do what your wife
wants ,I’ll be right here waiting”
akasema Doreen.Elvis akamtzama
usoni akataka kusema jambo
lakini kabla hajatamka chochote
simu yake ikaita,akaitoa mfukoni
akatazama mpigaji.Alikuwani
Patricia mke wake
“ Hallow Patricia”
“ Elvis uko wapi? Mbona
sikuoni hapa nilipokuacha?
Akauliza Patricia Elvis akamtazama Doreen
halafu akasema
“ Nimetoka kidogo kuna mtu
nimekuja kumtazama mara
moja.Tayari umeshamaliza
shughuli nije nikuchukue?
“ Elvis kuna tatizo
limejitokeza na hakuna mtu
mwingine ninayeweza kumueleza
zaidi yako”
“ Tatizo gani Patricia?
“ Ni kuhusiana na huyu
msichana Cindy niliyekuja
kumtazama.Ni kweli amezinduka
na anaweza kuongea kidogo
.Wakati niko naye nikimuhudumia
kuna jambo amenieleza limenistua
kidogo”
“ amekueleza nini” akauliza
Elvis.
“ Ameninong’oneza kwamba
anataka nimsaidie kumuondoa pale hospitali kwani maisha yake
yako hatarini”
“Maisha yake yako hatarini?
Kivipi?
“ Anadai kwamba kuna watu
wanaotaka kumuua.Anasema
kwamba endapo atagundulika
yuko pale hospitalini basi lazima
atauawa..”
“ Amekueleza nini sababu ya
maisha yake kuwa hatarini na ni
akina nani wanaotaka kumuua?
“ Hapana hajanieleza
chochote.How are we going to help
her?
Elvis akafikiri kidogo na kusema
“Nakuja hapo sasa hivi “
akasema na kukata simu
“ Kuna tatizo limetokea?
Akauliza Doreen
“ Kuna mtu ana tatizo ngoja
nikamuangalie” akasema Elvis Before you go” akasema
Doreen.Elvis akageuka na
kumtazama
“ Nahitaji unijibu kwa nini
umemdanganya mkeo alipokuuliza
uko wapi? Kwa hukumweleza
ukweli kwamba uko na mimi?
“ Sitaki ajue kama nimekuja
kwako na ninaomba Doreen suala
hili Patricia asilifahamu”
“ Usijali Elvis,hakuna
atakayejua .Hata kama tutafanya
Patricia hatajua chochote”
akasema Doreen na kumstua
kidogo Elvis
“ Umesema nini Doreen?
“ Nimesema kwamba muda
wowote ukinihitaji niko hapa
nakusubiri” akasema Doreen
“ stop this Doreen.I have to
go.We’ll talk later” akasema Elvis
na kuondoka Namlaumu sana Patricia
kwa kitu anachotaka
kukifanya.Hakupaswa kufanya
vile kwa sababu ninampenda na
sikuzote atakuwa ni mwanamke
peke e ninayempenda kuliko wote
hapa duniani na siko tayari kuzaa
mtoto na mwanamke
mwingine.Najua alifikia maamuzi
haya kutokana na maneno
yanayoanza kusemwa na
ndugu.Nitasimama imara siku
zote kumtetea na sintakubali mtu
yeyote yule amseme vibaya mke
wangu” akawaza Elvis akiwa
njiani kuelekea hospitalina mara
sura ya Doreen ikamjia
akatabasamu
“ Sielewi ni kwa nini Doreen
alikubali kirahisi namna hii ombi
la Patrica la kutaka kuzaa na
mimi. Si jambo rahisi kwa mwanamke kukubali kuzaa mtoto
na mume wa mtu lakini kwa
Doreen ameonekana kutokuwa na
tatizo lolote kuhusiana na suala
hili .Napata mashaka kama kweli
ana nia ya dhati ya kumsaidia
rafikiyake au ana sababu zake
kwani hata maongeziyake
ukiyasikia unagundua kabisa
kuna kitu anakitafuta.Hata hivyo
dah ! Doreen is so hot.Anasisimua
sana.Kwa mara ya pili leo kama
nisingekuwa jasiri basi ningefanya
naye mapenzi leo kwani tayari
mashetaniyangu yalikwisha
amka.Ananiweka katikamajaribu
makubwa ” Akawaza Elvis halafu
akakumbuka jambo aliloambiwa
na Patricia
“ Huyo msichana ana
matatizo gani? Nani anayetishia
maisha yake? Ngoja nikamsikilizenione kama nitaweza kumsaidia
lakini ninahisi ni suala ambao
linatakiwa kuripotiwa polisi.”
Akawaza Elvis
Alifika hospitali akamtaarifu
mkewe ambaye alfika mara moja
akamchukua na kumpeleka hadi
sehemu Fulani
“ Hii ni sehemu pekee
ambayo hakuna kamera za ulinzi
zilizoelekezwa tofauti na kila kona
ya majengo ya hospitali
hii”akasema Patricia
“ Elvis kuna jambo yule
msichana amenieleza limenistua
kidogo”
“ Jambo gani hilo?
amekwambia nini?
“ Msichana yule ana matatizo
na anahitaji msaada.Amenieleza
kwamba maisha yake yako hatarini na kwamba kuna watu
wanaomtafuta ili kumuua”
“ Ni watu gani hao wanaotaka
kumuua na kwa nini?
“ Hajanieleza kwa undani
kuhusu suala hilo ila ameniomba
nimtoe hapa hospitali kwani
anaogopa wanaomtafuta
wakigundua kwamba yuko hapa
basi watafika na kumuua”
“ Patricia ninapata wasiwasi
kidogo kama huyo msichana tayari
amekwisha rejewa na fahamu
zake kamili.” Akasema Elvis
“ Hakuna tatizo katika
fahamu zake.Anakumbuka kila
kitu na nimemfanyia vipimo yuko
safi.Kumbukumbu zake zote ziko
sawa”
“ Anakumbuka ni kitu gani
kilimsababisha apoteze fahamu
kwa muda wa miezi miwili? Nimejaribu kumuuliza lakini
anaonekana kukumbuka jambo
Fulani halafu huogopa na kuanza
kulia.Anaonekana kuna kitu
ambacho hataki kukiweka wazi”
Elvis akafikiri na kusema
“ Naweza kuruhusiwa
kumuhoji kidogo ili nione ni
namna gani tunavyoweza
kumsaidia?
“ Kwa sasa itakuwa vigumu
kumuhoji kutokana na mazingira
ya hospitali kwanihutaruhusiwa
kuingia mahala aliko kama si
daktari au muhusika wa hospitali
hii.”
“ So what are we going to do?
Akauliza Elvis
“ I don’t know Elvis”
Elvis akainama akafikiri kwa
muda kisha akasema “ Are you sure you want to
help her?akauliza
“ Elvis msichana yule
anaonekana wazi ana tatizo kubwa
na inaonekana kuna kitu kikubwa
anakifahamu na ndiyo maana
amenililia na kuniomba nimsaidie
.Nadhani kuna ulazima wa
kumsaidia”
“ Vizuri kama uko tayari
kumsaidia basi njia pekee ni
kumuondoa hapa hospitali.Hilo
linawezekana ?
“ Anaweza kuruhusiwa lakini
kuna taratibu za kufuata”
“ Hapana hatuwezi kusubiri
hizo taratibu zikamilike
.Yawezekanani kweli anaweza
kuwa katika hatari kubwa.We
have to save her”
“What are we going to do?
Akauliza Patricia Kama kweli tunataka
kumsaidia tunatakiwa tumuondoe
hapa hospitali kimya kimya bila ya
mtu kufahamu “
“ Hilo ni jambo gumu sana
Elvis.Kamera za ulinzi zimefungwa
kila kona ya hospitali hii kwa hiyo
hatuwezi kumtorosha bila ya
kuonekana.I’mso confused”
“ Anaweza kutembea japo
kidogo?
“ nadhani anaweza kutembea
japo bado dhaifu sana”
“ Ok good.Kitu cha kufanya
hapa mvue mavazi yale ya
wagonjwa na umvishe mavazi ya
kawaida.Baada ya hapo mtoe nje
kwa kisingizio kwamba
anakwenda kupunga upepo
.Utampeleka hadi chini ya ule mti
uliopo eneo la megesho.Mimi
nitalitoa gari nje ya geti halafu nitamtuma kijana wa piki piki
ambaye atamfuata na kumtoa nje
kisha nitampakia garini na
kuondoka naye.Hakuna mtu
yeyote ambaye atahisi kwamba
umemtorosha mgonjwa bali
itaonekana ametoroka
mwenyewe”akasema Elvis .Patrcia
akafikiri kidogo kisha akasema
“ Ok ! Ngoja tufanye hivyo ili
kumsaidia yule
msichana.Anaonekana ni kweli
ana tatizo kubwa”
**********************
“ Cindy yuko wapi? Akauliza
Patricia baada ya kuwasili
nyumbani akiwa katika gari ya
kukodi.Gari lao aliondoka nalo
Elvis katika harakati za
kumtorosha Cindy Yuko chumba cha wageni
anapumzika.Vipi hospitali hakuna
tatizo lolote? Akauliza Elvis
“ Hakuna tatizo
lolote.Nimeripoti kwa uongozi
kwamba mgonjwa amepotea.Na
jambo zuri nimeripoti kwamba
mgonjwa aliyepotea ana matatizo
ya akili.Hakuna mtu anayetilia
maanani kupotea kwako hasa
baada ya kusikia kwamba ana
matatizo ya akili” akasema Patricia
na kuvuta pumzi ndefu
‘ Umefanya jambo zuri sana
la kijasiri Patricia.”
“ Ahsante sana Elvis.Ni kweli
tumefanya jambo la kijasiri
japokuwa halikuwa rahisi.Ahsante
kwa kunipa ujasiri wa kulifanya
jambo lile nilikuwa naogopa
sana.Kwa sasa Cindy yuko huru na ni jukumu letu kufahamu
kilichomsibu na kumsaidia”
“ Nadhani ni wakati muafaka
wa kumuhoji na kujua kila kitu
kumuhusu yeye.Tufahamu
ametokea wapi na akina nani
wanaotaka kumuua..” akasema
Elvis kisha wakainuka na
kuelekea katika chumba cha
wageni alimokuwamo Cindy
ambaye alikuwa amekaa kitandani
“ Unajisikiaje hivi sasa?
Akauliza Patricia
“ Ninajisikia afadhali
sana.Kidogo ninajisikia kupata
nguvu.Ahsante sana dokta kwa
msaada wako” akasema Cindy
“ Vizuri sana.Utapona tu
usiwe na wasi wasi” akasema
Patricia .Cindy akamshika mkono
na kusema Dokta ninarudia tena
kukushukuru kwa msaada wako
.Umeyaokoa maisha yangu.Watu
wale wangejua niko pale hospitali
wangenifuata na kuniua” akasema
Cindy .Patricia akageuka na
kumtazama Elvis halafu
akamshika Cindy begani
“ Cindy huyu hapa ni mume
wangu anaitwa Elvis.Kwa pamoja
tumeguswa sana na tatizo lako na
tuko tayari kukusaidia lakini ili
tukupe msaada unaostahili
tunataka tulifahamu tatizo
lako.Tunataka tufahanu nini
kilikutokea na kusababisha
upoteze fahamu kwa muda wa
miezi miwili? Tunataka kufahamu
ni akina nani wanaotaka kukuua
na kwa nini? Tafadhali kuwa
muwazi kwetu na usiogope kitu
hapa uko katika mikono salama.” Akasema Patricia.Cindy akafumba
macho kana kwamba kuna kitu
anakumbuka.Michirizi ya machozi
ikaonekana mashavuni
“ Usilie Cindy.Kuwa
jasiri.Tueleze kitu gani kilikusibu?
Akasema Patricia.Cindy akakohoa
kidogo na kusema
“Jina langu naitwa
Elizabeth.Nilitokea Iringa na kuja
kufanyakazi za ndani jijini Dar e s
salaam.Nilifanya kazi kwa mama
mmoja anaitwa mama Shamim na
alipoondoka kwenda arabuni
akanikabidhi kwa mtu mmoja
anaitwa Pascal Situmwa ambaye
mke wake alikuwa amefariki na
kumuachia watoto wawili
wadogo.Pascal alikuwa akitafuta
mtu wa kuwalea watoto wake.”
“ Hebu ngoja kwanza
Elizabeth.” akasema Elvis huku sura yake ikionyesha mshangao
Fulani
“ Unasema ulikabidhiwa kwa
Pascal Situmwa?
“ Ndiyo .Nilikabidhiwa kwa
Pascal Situmwa.Nilikuwa nafanya
kazi kwake.” Akasema Elizabeth
kwa sauti dhaifu.Elvis akafikiri
kidogo kisha akasema
“ Endelea”
“ Vipi mbona umestuka Elvis
? Do you know him? Akauliza
Patricia
“ hapana simfahamu” akajibu
Elvis.Elizabeth akaendelea
“ Nilianza kufanya kazi kwa
Pascal Situmwa na aliniamini
sana.Niliwalea watoto wake vizuri
bila matatizo.Siku moja Pascal
alikuja na rafiki zake wakanywa
sana pombe sebuleni hadi usiku
mwingi.Asubuhi nilipoamka niliokota pochi ndogo sebuleni
nikaifungua na kuangalia
kilichokuwamo ndani
yake.Kulikuwa na kadi tatu mfano
wa kadi za benki,fedha taslimu
shilingi laki tatu pamoja na dola
mia mbili za marekani.Vile vile
kulikuwa na kitu Fulani kama
memory kadi ya simu halafu
kukawa na flash disc yenye GB
8.Sikuwa na shida na vifaa vile
shida yangu mimi ilikuwa ni zile
fedha tu.Sikutaka kuziweka fedha
zile chumbani kwangu
nikaichukua ile pochi na kwenda
kuifukia chini ya mti nyuma ya
nyumba.Pascal alipoamka asubuhi
alianza kuitafuta ile pochi
akaniuliza lakini nilikana
kuiona.Aliendelea kutafuta pochi
ile kila mahali lakini
hakuipata.Baada ya kuitafuta sana na kuikosa akaniita na
kunionya kwamba niirudishe
pochi ile kwani hakuna mtu
mwingine anayeweza kuichukua
pochi ile zaidi yangu.Alinipa muda
wa dakika thelathini niwe
nimeirudisha pochi
yake.Niliendelea kukataa kwamba
sifahamu mahala iliko hiyo pochi
yake.Baada ya nusu saa akaja
tena na kuniomba nimrudishie
vitu vilivyokuwamo ndani ya ile
pochi ila fedha
nizichukue.Niliendelea kukataa
akanishika na kunipeleka
chumbani kwangu akaanza
kupekua kila mahala lakini
hakuiona pochi wala
hela,akanivua nguo zote na
kunisachi kila mahala hadi
sehemu za siri lakini hakuona
kitu.Hakunisemesha kitu tena.Ilipofika saa tisa alasiri
wakaja watu wanne ambao
sikuwahi kuwaona wakanichukua
na kunipeleka sehemu Fulani
katika shamba moja wakanitesa
sana wakanipiga sana ili
niwaeleze mahala ilipo pochi hiyo
.Walinipiga mno hadi nikapoteza
fahamu na sikujua tena kitu
chochote kilichoendelea hadi
nilipozinduka na kujikuta pale
hospitali.Wale watu walidhamiria
kuna kabisa kwani kabla
sijapoteza fahamu niliwasikia
wakijadiliana mahala
watakapokwenda kunitupa baada
ya kuniua” akasema Elizabeth
.Elvis na Patricia wakatazamana.
“ Pole sana Elizabeth.Kuanzia
sasa usiwe na wasi wasi wowote
kuhusu maisha yako.Hapa uko
sehemu salama na hakuna mtu atakayejua kama uko hapa.Kwa
sasa pumzika tutaongea zaidi
baadae” akasema Elvis halafu
akatoka na kulekea chumbani
akamuacha Patricia akimpa dawa
Elizabeth.Kichwa chake kiliwaza
jina moja tu Pascal Situmwa
“ Pascal Situmwa !..akasema
Elvis kwa sauti ndogo
“ Pascal Situmwa kwa nini
atake kuua Elizabeth kwa sababu
tu ya pochi? Katika pochi hiyo
kulikuwa na nini? Nashawishika
kuamini kwamba katika pochi
hiyo kuna jambo kubwa
.Ninamfahamu Pascal
Situmwa,mpaka afikiri hatua ya
kutaka kumuua huyu msichana
lazima iko sababu
kubwa.Inawezekana kuna jambo
analificha ambalo anahisi pengine
huyu msichana amelifahamu” akawaza Elvis na mara Patricia
akaingia
“ Elvis mbona ulistuka
uliposikia Elizabeth akilitaja jina
la aliyekuwa mwajiri wake? Do you
know him? Akauliza .Elvis
akamshika mkono mkewe na
kumketisha kitandani
“ Ninamfahamu Pascal
Situmwa.Ni mfanyakazi wa idara
ya usalama wa taifa.Ana nafasi
kubwa katika idara ile”
“ Kwa nini basi atake kumuua
Eliza? Hivyo vitu vilivyokuwa
ndani ya hiyo pochi yake vina
thamani gani?
“ I dont know my love but I
need to find out “ akasema Elvis
na kumstua mke wake
“ Find out ? How? akauliza
Patricia