Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Hongera, umeikimbiza.. Karibu kwenye foleni...

Jana nilikuona mahali nikakosa cha kusema juu yako ila tambua nakukubali sana tena sana...
Yaan haha sina cha kusema kabisa nineisoma na kuimaliza leo asubuhi nimewafikia

Tater asante kwa kunikubali nakushukuru kwa kujua hilo tuko pamoja
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Seheu 63

Baada ya kutoka nyumbani kwa
brigedia Frank kuchukua silaha
waliwapitia vijana ambao Obi alikuwa
amewaandaa waliokuwa na gari lao
kisha wakaongozana kuelekea kwa
akina Elvis.Walikuwa wamejianda
kwa mapambano wakiwa na silaha
kali.Watatu kati ya vijana hawa
wamewahi kupitia jeshi na
wakafukuzwa kutokanana utovu wa
nidhamu.Wote walikuwa ni wajuzi
sana katika kutumia silaha na
walikuwa na genge lao la kufanya
uhalifu wa kutumia silaha.Wengine
watano walikuwa na uzoefu pia katika
mambo ya uhalifu na hata kutumia
silaha.
"Ninaomba hiki anachonieleza
Winnie kuhusu Elvis kisiwe
kweli.Nataka kwanza nithibitishe ni
Elvis yupi huyo anayemtaja wakati Elvis amekwisha zikwa?Ni mzimu
wake ndio umerudi kutusumbua?
akajiuliza
"Nafsi yangu inakataa kabisa na
haiamini katika mambo hayo ya
mizimu.Yawezekana kuna mtu
mwingine anajiita Elvis na si Elvis yule
tuliyemuua.Lakini mbona wasifu
alionielezea Winnie unafanana kabisa
na wasifu wa Elvis? Hili suala naona
linataka kunipasua kichwa changu
lakini nitapata majibu muda si
mrefu.Usiku huu wa leo kwa namna
yoyote ile lazima nimpate Vicky kwani
yeye ndiye anayeweza kunithibitishia
kuhusu huyo mtu anayejiita Elvis"
akaendelea kuwaza Frank
Japokuwa Winnie alipita maeneo
yale usiku lakini aliweza kukumbuka
vyema mahala ilipo nyumba ya akina
Elvis na hatimaye wakawasili katika
nyumba ile Ni pale kwenye lile geti"
akaelekeza Winnie na gari zikasimama
"Una hakika ni hapa?akauliza
Frank
"Nina uhakika Frank ni hapa"
akasema Winnie
"Nataka uwe na uhakika Winnie
.Una hakika ni hapa?Frank akauliza
tena
"Nina uhakika ni hapa.Siwezi
kupotea" akasema Winnie
"Good.Obi wapange vijana wako
ili muweze kuingia ndani mimi
nitakuwa pale mbele nikiangalia
namna zoezi linavyokwenda na
endapo kutakuwa na tatizo lolote
nitatoa msaada" akasema Frank na
Obi akashuka.Frank akaenda
kuegesha gari mita kadhaa kutoka geti
la kuingilia katika nyumba ile
akaichukua bunduki yake kubwa akaiandaa kwa ajili ya lolote ambalo
lingeweza kutokea
"Winnie utakuwa umenisaidia
sana kama kweli tukifanikiwa
kuwapata hao jamaa pamoja na
Graca.Ninakuahidi baada ya kuwapata
hao jamaa basi dada yako atakuwa
huru na sintamfuatilia tena.Lakini
endapo unanidanganya utanisamehe
kwa kile nitakachokufanyia" akasema
Frank ambaye kwa wakati huu sura
yake ilionyesha ukatili mkubwa
"Ninakuambia ukweli Frank
siwezi kukudanganya.Ninafanya hivi
ili kumsaidia dada yangu aweze
kuachiwa na hawa jamaa" akasema
Winnie kwa kujiamini
Obi na vijana watano
wakafanikiwa kuruka ukuta na
kuingia ndani bila kelele.Walikuwa ni
wazoefu sana wa mambo kama haya
hivyo kuingia mle ndani iliwachukua muda mfupi tu.Kabla ya kufanya lolote
wakatulia kwa dakika mbili
wakihakiki usalama na baada ya
kuhakikisha eneo lile ni shwari na
hakuna mtu yeyote pale nje Obi akatoa
maelekezo kwa vijana watatu
watawanyike kuizunguka nyumba ile
kisha yeye na wale vijana wawili
waliobaki wakanyata kuusogelea
mlango.Taa za ndani zilikuwa
zinawaka na waliamini lazima kuna
watu ndani ila hawakusikia sauti ya
mtu akiongea.Kwa kutumia funguo
bandia wakafungua mlango na kuingia
sebuleni ambako kulikuwa kimya
kabisa.Taratibu wakafuata varanda
kuelekea vyumbani.Walipita vyumba
vyote lakini hakukuwa na mtu.Hii
ikawashangaza sana.
"Where are they? akauliza Obi
lakini vijana wake wakabaki kimya Let's search again.Safari hii tuwe
waangalifu sana kutafuta yawezekana
kuna mlango wa siri wamepita watu
hawa na kwenda kujificha" akasema
Obi na upekuzi ukaanza
upya.Walipekua sana lakini
hawakuambulia kitu.Huku akitokwa
na jasho akampigia simu Frank
"Frank hakuna mtu humu ndani"
"Nini?! akauliza Frank kwa
mshangao
"Hakuna mtu humu ndani"
"No ! Search again.They must be
there!! akasema kwa ukali
"Mzee tumerudia kupekua mara
mbili lakini hakuna mtu yeyote humu
ndani ila kunaonekana kuna watu
walikuwepo humu muda si mrefu sana
kabla ya sisi kuwasili"
"Damn it !! akasema kwa hasira
na kupiga usukani halafu akamgeukia
Winnie "Watu wako hawapo humo
ndani.Unanidanganya? akauliza Frank
kwa ukali
"Hapana Frank
sikudanganyi.Watu hawa wanaishi
humu ndani" akasema Winnie
akionekana kuogopa
"Kama wanaishi humu wako
wapi?Wamejificha wapi?
"Sifahamu ila wanaishi
humu"akasema Winnie
"Get out of the car ! akaamuru
Frank na Winnie akafungua mlango
wa gari akashuka.
"Obi nifungulie geti ninakuja
humo ndani" akasema Frank na
mlango mdogo wa geti ukafuguliwa
akamshika mkono Winnie
akamuingiza ndani
"Frank nilikwambia huyu
msichana si wa kumuamini kwani hakuna mtu yeyote humu ndani"
akasema Obi
"Nilikwisha mtahadharisha kuwa
mimi ni mtu mbaya sana
nikidanganywa na nitamtoa uhai hapa
hapa!! akasema Frank akiwa amewaka
hasira
"Mna hakika hakuna mtu yeyote
humu ndani?akamuuliza Obi
"Tumepekua mara mbili na
hakuna mtu yeyote humu ndani"
"Hakuna mlango wa siri ambao
hawa jamaa wameutumia kukimbia
baada ya kugundua uwepo wetu?
"Hakuna mzee.Tumetafuta sana
hakuna mlango wowote wa
siri"akasema Obi na Frank
akamgeukia Winnie akamtaka apige
magoti halafu akatoa bastora yake
"Ninakupa nafasi ya mwisho ya
kunieleza ukweli.Nani alikutuma uje
unieleze ongo huu?Ukishindwa kunijibu ninakutoa uhai wako sasa
hivi!! akafoka Frank
"Please dont kill me I'm telling
the truth!! akasema Winnie huku
akilia
"Mkuu huyu msichana ni muongo
kabisa.Huu ni mtego
tumewekewa.Tuondokeni haraka sana
hapa kabla hatujavamia.Nilikuwa na
wasi wasi naye muda mrefu" akasema
Obi
"Hata mimi sikuwa nikimuamini
kabisa hasa kwa namna alivyonitafuta
na kunipata.Nimebadili
mawazohHatutamuua kwani
anatumiwa na watu wanaonifahamu
vyema hivyo itakuwa rahisi kwangu
kuwafahamu kwa kumtumia
yeye.Mfungeni tunaondoka naye"
akasema Frank kwa hasira
"Frank please I'm telling the
truth!! naomba uniamini tafadhali!! akalia Winnie lakini haraka haraka
akafungwa mikono kwa kamba
"Frank tafadhali naomba
uniamini.Ninachokueleza ni kitu cha
kweli kabisa.Sijakudanganya" Winnie
akaendelea kulia
"Winnie nilikutahadharisha kuwa
sitaki kudanganywa lakini hukusikia
ukanidanganya.Siwezi kukusamehe
kwa hilo lazima nikuue!!
Kitakachokuokoa ni pale
utakaponieleza ukweli"
"Ninakueleza ukweli Frank kwa
nini hutaki kuniamini? akauliza
Winnie
"Mpelekeni katika gari ,sitaki
kumuona mbele ya macho yangu"
akasema Frank na kwa haraka Winnie
akatolewa mle ndani akabebwa juu
juu hadi katika gari la Frank
"Nini kinaendelea hapa
Frank?Obi akauliza na Frank akainamisha kichwa kwa muda
akifikiri halafu akasema
"I'm confused.Yule msichana
anaweza kuwa anasema kweli kwani
kuna maneno alinieleza ambayo
yananifanya kidogo
nimuamini.Hatutaondoka hapa sasa
hivi hadi tuhakikishe ni nani anaishi
katika nyumba hii.Tusikate tamaa
mapema"akasema Frank
"Mkuu huu unaweza kuwa ni
mtego.Huyu msichana anaweza kuwa
ametumika kukuwekea
mtego.Kumbuka Pascal ameuawa na
hatujui nani kamuua hivyo nawe pia
unaweza kuwa katika orodha ya
wanaotafutwa wauae.Nakushauri
tuondoke hapa si mahala pazuri
kwetu" akasema Obi
"No! Hatuondoki hapa.Waelekeze
vijana wako wajipange kukabiliana na
shambulio lolote ambalo litatokea hapa.Nataka niwafahamu hao watu
wanaonitafuta ni akina nani." akasema
Frank na Obi akatoka kwenda
kuwapanga vijana wake
"Sintatoa mguu wangu ndani ya
hii nyumba hadi nipate uhakika
kuhusu huyo Elvis.Mambo
niliyoambiwa na Winnie
yamenichanganya mno na hasa baada
ya kusikia jina Elvis likitajwa tena.Kila
nikilifikiria jina hili ninaishiwa nguvu
kab............" Frank akatolewa mwazoni
baada ya ujumbe kuingia katika simu
yake.Ujumbe huu ulikuwa na mlio wa
tofauti na ule wa jumbe nyingine
zinapoingia.Haraka haraka akaitoa
simu na kuusoma ujumbe ule
"Hongera.Nambayako ya siri
imefanikiwa kubadilishwa"ndivyo
ulivyosomeka ujumbe ule.Ndani ya
sekunde chache akajikuta akiloa jasho
mwilini What ?!! akasema kwa sauti
"This cant be!! Nini hiki
kinanitokea?Nani kabadilis.........."
akawaza na haraka haraka akazitafuta
namba za simu za msimamizi wake
mkuu wa shamba ambaye ndiye
mwenye funguo za kuingilia mle ndani
ya nyumba lakini simu yake haikuwa
ikipatikana.Miguu ikamtetemeka
"No ! No ! No !akasema huku
akitoka nje kwa kasi na kumfuata Obi
"Obi tuondoke haraka sana kuna
jambo limetokea"akasema Frank
"Nini kimetokea mkuu? akauliza
Obi kwa mshangao
"Wakusanye vijana wote tuwahi
haraka sana nyumba yangu
imevamiwa! akasema huku midomo
ikimtetemeka kwa hasira.Haraka
haraka Obi akawakusanya vijana wake
wakaingia katika gari na kuondoka
kwa kasi akimfuata Frank aliyekuwa akiendesha gari kama
mwendawazimu kuwahi shambani
kwake
"Ni nani hawa waliovamia
nyumba yangu na kuingia katika
katika ofisi yangu?Hawa lazima
watakuwa ni ni hawa watu
wanaonifuatilia.lazima watakuwa ni
kundi la Elvis na
wenzake.Wamefahamuje kama nina
ofisi kule shambani ambako
ninahifadhi mambo yangu nyeti?
akajiuliza
"Winnie anasema kwamba Vicky
aliwahidi kuwapeleka hao jamaa
mahala ambako ana uhakika kwamba
wanaweza wakanipata.Vicky niliwahi
kumpeleka katika nyumba yangu ya
shambani na kumficha
kule.Yawezekana ni yeye ndiye
aliyewapeleka hao jamaa kama
alivyosema Winnie? Ukiacha Vicky mwingine ambaye anafahamu
kuhusiana na nyumba yangu ya
shambani ni Graca.Tena hyu
anafahamu kama kuna ofisi ya siri
iliyoko chini ya nyumba kwani
niliwahi kumfungia kule wakati ule
nikimtisha anirejeshee kompyuta
yangu.Kama kweli Graca anaishi na
akina Elvis kama basi kuna
uwezekano mkubwa huu ni
muendelezo wa jitihada zao za
kuhakikisha kwamba wanafahamu
kila ninachokifanya na hasa kuhusu
biashara ya silaha.Naamini ni yeye
ndiye aliyewaelekeza wenzake kuhusu
ofisi yangu ya siri kwani Vicky
hafahamu chochote kuhusu ofisi
hii.Kwa nini lakini mwanangu wa
kumzaa ananifanyia haya?Haogopi
kupambana nami?Ninaanza kuhisi
Vicky na akina Graca wote ni kundi
moja na wameungana ili kupambana nami,nahisi hata huyu Winnie
ametumwa kwa lengo la kuja kwangu
ili kunipotezea muda na kuwapa
nafasi hao watu pamoja na dada yake
kuvamia nyumba yangu.Huyu
nitamtumia katika kuwatafuta Vicky
na wenzake hadi niwapate.Haya yote
yanatokea kwa sababu nilimpuuza
Pascal alipotoa wazo la kumuua Vicky
mapema.Hata madam Elizabeth
alipotoa maelekezo nimuue Vicky
sikutekeleza kwa vile tayari
nilimuhitaji Vicky kingono na hizi
ndizo athari zake.Sipaswi kumlaumu
mtu kwa haya
yanayonikuta.Nimeharibu mimi
mwenyewe na sasa natakiwa
kupambana kuhakikisha
ninarekebisha hii hali haraka sana na
nitarekebisha baada tu ya kuhakikisha
nimewapata hao watu kwa haraka
sana.Kabla ya kufika asubuhi kesho lazima niwe nimewapata Vicky na
kundi lake lote"Kichwa cha Frank
kikajaa mawazo mengi sana


*******************

Graca aliwaongoza akina Elvis
hadi katika ofisi ya baba yake
aliyoijenga chini ya ardhi.
"Hii ndiyo ofisi ya baba" akasema
Graca
"Steve pitia kwa haraka na
uchukue chochote kinachoweza
kutufaa katika uchunguzi wetu.Graca
ulisema kuna sehemu pia huwa
anahifadhi vitu vyake ni wapi?
akauliza Elvis
"Ni katika mlango ule pale"
akaelekeza Graca na Elvis akaenda
kuutazama ule mlango nao pia ulikuwa unafunguliwa kwa namba
maalum.
"Huyu jamaa amejidhatiti sana
kiusalama.Si rahisi kuingia huku
mahala anakohifadhi mambo yake."
akasema Elvis huku akivua begi lake
na kutoa kitu flani akakipachika katika
mlango halafu akabonyeza kitufe
katika kidude hicho na namba
nyekundu zikaonekana zikihesabu
kuanzia kumi na ilipofika sifuri kidude
kile kikalipuka ingawa hakikutoa
mlipuko mkubwa wenye madhara na
mlango ukafunguka
"Huku tuko chini ya ardhi hivyo
hakuna anayeweza kusikia sauti hii ya
mlipuko huko juu" akasema Elvis na
kuusukuma mlango wakaingia katika
chumba kimoja kikubwa sana kama
ukumbi wa mikutano wenye kuweza
kuchukua watu zaidi ya mia tano. What is this place" akawaza
Elvis .Akiwa na tochi wakafanikiwa
kupata sehemu ya kuwashia taa na
kukawa na mwangaza wa
kutosha.Kulikuwa na maboksi ya
mbao yamepangwa vizuri
"Nini wanahifadhi humu?
akauliza Omola.Elvis akashusha moja
ya boksi lile la mbao na kutoa mfuniko
wake akakutana na jozi za viatu vya
kiume
"Viatu? Elvis
akashangaa.Akashusha boksi lingine
akalifungua na kukuta limejaa jozi za
viatu.Wote wakazidi
kushangaa.Akashusha lingine la tatu
na kukuta kuna viatu.
"Frank anafanya biashara ya
viatu?Elvis akamuuliza Graca
"Hata mimi
nimeshangaa.Ameianza lini biashara
hii" Graca naye akashangaa Hainiingii akilini Frank afiche
jozi za viatu katika sehemu kama hii
yenye ulinzi mkubwa.Milango yote ya
hapa inafunguliwa kwa namba
maalum na haiwezekani akatumia
gharama kubwa kutengeneza sehemu
kama hii kwa ajili ya kuhifadhi vitu
kama viatu" akasema Elvis na
kumgeukia Graca
"Graca una fahamu kama baba
yako anajihusisha na biashara ya
viatu?
"Hapana sifahamu chochote
kuhusiana na baba kujihusisha na
biashara ya viatu" akasema Graca
"Tuendelee kupekua yawezekana
tukakabaini vitu vingine.Siamini
kabisa kama Frank anatumia sehemu
hii kuficha viatu" akasema Elvis na
kuanza kushusha makasha na
kuyafungua na yote yalijaa
viatu.Alishusha zaidi ya maboksi ishirini lakini yote yalikuwa na
viatu.Jasho lilimtiririka kutokana na
zoezi lile
"Inaonekana maboksi haya yote
yana viatu.Nilitegemea sehemu kama
hii angeweza kuhifadhi silaha au vitu
vingine lakini kumejaa maboksi ya
viatu" akasema Elvis na wote
wakatazamana.Elvis akaendelea
kuchunguza lakini hakufanikiwa
kupata aina yoyote ya silaha
"Twende tukamuone Steve kama
kuna kitu chochote amekipata cha
kuweza kutusaidia" akasema Elvis
wakatoka na kuingia katika ofisi
walikomuacha Steve
"Steve kuna kitu chochote
umekipata? akauliza Elvis
"Kuna hii bahasha nimeipata
katika droo ya kati ina nyaraka za
kutolea mizigo bandarini.Nyaraka
zinaonyesha kuna kontena kumi na nane zimeingia nchini mwezi uliopita
kutoka nje ya nchi.Vingi ya vitu
vilivyomo humu ni risiti mbali mbali
za malipo lakini nimekuta kompyuta
ndogo katika moja ya droo" akasema
Steve
"Vizuri.Huko ndani kuna chumba
kikubwa kama bohari la kuhifadhia
mizigo na tumekuta kuna shehena
kubwa ya viatu"
"Viatu?Hakuna silaha hata
moja?Steve akashangaa
"Hata mimi nilitegemea
tungeweza kukuta silaha lakini
tumekutana na jozi za viatu" akasema
Elvis na kumgeukia Graca
"Graca kuna sehemu nyingine
ambayo unadhani unaweza
kutupeleka na tukapata nyaraka zaidi
kuhusu baba yako na mtandao wake?
akauliza Elvis Hapa ndipo ninapopafahamu
kuwa anaficha mambo yake ya
siri.Kama mkikosa hapa kupata kitu
cha kuwasaidia sifahamu tena sehemu
nyingine" akasema Graca
"Ahsante hata hivyo umetusaidia
sana.Steve chukua hivyo
ulivyofanilkiwa kuvipata tuondokeni
kabla hawajatugundua kuwa tuko
hapa" akasema Elvis kisha wakaanza
kutoka.Walipotoka chini Elvis akapiga
piga sikio na kumuita Vicky
"Vicky unanipata?
'Ninakupata Elvis.Mpo salama?
"Salama kabisa
Vicky.Tumekwisha maliza kazi hapa
na tunaondoka.Uko salama? hakuna
hatari yoyote?
"Niko salama kabisa na hakuna
hatari yoyote"
"Good.Zima mashine ili tuweze
kutoka" akasema Elvis na hazikupita sekunde thelathni umeme ukakatika
na kwa haraka wakatoka mle ndani na
kuelekea iliko mashine ya umeme
mahala walikomuacha Vicky
"Pole sana kwa kukuacha peke
yako" akasema Elvis baada ya kufika
mahala aliko Vicky
"Mmefanikiwa kupata chochote?
"Si haba kuna vitu vichache
tumevipata na tunakwenda kuvifanyia
uchunguzi tuone kama vinaweza
kutusaidia.Washa ueme kisha tupotee
maeneo haya" akasema Elvis na
mashine ikawashwa kisha
wakaondoka wakifuata ile njia
waliyojia


*******************

Frank na vijana wake waliwasili
shambani wakiwa katika mwendo mkali sana.Walipofika katika geti la
walinzi Frank akashuka na kumkuta
mlinzi mmoja tu
"Wenzako wako wapi?akauliza
"Wamekwenda kutazama
mashine ya umeme ina matatizo"
"Matatizo?Frank akauliza
"Ndiyo bosi.Umeme umekuwa
unazima mara kwa mara usiku huu
hivyo wakaenda kutazama kama kuna
tatizo na hawajarejea"
"Tatizo hilo limeanza lini?
akauliza
"Limeanza usiku huu"
"Mbona nawapigia simu zao
hawapatikani?Wamekwenda bila
simu?
"Wamekwenda nazo bosi"
"Kuna mtu yeyote amekuja hapa
usiku wa leo?
"Hapana bosi hakuna mtu yeyote
aliyekuja hapa" Una hakika?
"Ndiyo bosi hakuna yeyote
aliyefika hapa"akajibu yule mlinzi
Frank akaingia haraka katika gari lake
na kuingia shambani akiendesha kwa
kasi ya ajabu.Alisimamisha gari nje ya
nyumba akashuka na kumtaka Obi
awaelekeze vijana wake wazunguke
nyumba kukagua kama kuna mtu
yeyote halafu yeye Obi na kijana
mmoja wakaingia ndani.Waliingia kwa
tahadhari kubwa sana.Nyumba
ilikuwa kimya kabisa.walipita sebuleni
,wakakagua vyumba vingine vya
kulala hakukuwa na mtu yeyote na
wakati wakiendelea kukagua mmoja
wa vijana wa Obi akamuita na
kumuonyesha mlango wa nyuma
ulikuwa wazi.Obi akamuita Frank na
kumuonyesha ule mlango
"Yawezekana Marwa aliufungua
mlango huu wakati akitafuta chanzo cha umeme kukatika mara kwa mara"
akasema Frank na kuchukua simu
akampigia Marwa mlinzi wake mkuu
pale shambani lakini bado simu yake
haikupatikana
"Mbona simu yake haipatikani?
akajiuliza halafu akaendelea na zoezi
la kukagua nyumba.Chumba cha
mwisho kukagua kilikuwa ni chumba
chake cha kulala.Aliingia kwa
wasiwasi mkubwa na kila kitu
kilionekana kiko sawa.Hakuna kitu
kilichoguswa
"Where are you bastard!!
akasema kwa sauti ndogo na kuingia
katika chumba cha kubadilishia nguo
na kabati lililouziba mlango wa
kuingilia katika nyumba ya chini
lilionekana kutokuguswa,akalisogelea
taratibu kulichunguza lakini
lilionekana kama vile alivyoliacha
akashusha pumzi Naona kila kitu kiko
sawa.Hakuna kitu
chocotekilichoguswa.Kama kila kitu
kiko sawa kwa nini basi nikatumiwa
ule ujumbe nikijulishwa kuwa namba
ya siri ya kufungulia mlango 34DN
imebadilishwa?akawaza halafu
akamtaka Obi na kijana wake watoke
wakaendelee kufanya uchunguzi nje
na mle chumbani akabaki peke
yake.Akalisogeza pembeni kabati na
kuingiza namba za siri za kufungulia
mlango na hapo ndipo akili zilipotaka
kumruka.Mlango uligoma kufunguka
na jibu alilopewa ni kwamba namba
aliyoingiza si sahihi.Akaingiza tena
namba zile lakini zikakataa na
ukatolewa ujumbe wa onyo kuwa
amebakisha nafasi moja tu ya kujaribu
kuufungua mlango ule kabla ya
king'ora cha hatari kulia.Frank akasimama akashika kiuno alihisi
miguu inamuisha nguvu
"Nani huyu aliyethubutu
kunifanyia kitu kama hiki? Amewezaje
kubadili namba za siri? akajiuliza
halafu akampigia simu Obi na
kumtaka aende chumbani kwake mara
moja.Obi akakimbia na kwenda
chumbani
"Obi kuna tatizo limetokea.Kuna
watu walikuwa humu chumbani"
"Wamechukua kitu gani?Walinzi
hawakufanikiwa kuwaona ?akauliza
Obi na Frank akaegemea ukuta kwani
miguu yake alihisi ikiisha nguvu
"Tukiwa kule mahala
alikotupeleka Winnie,nilitumiwa
ujumbe katika simu yangu kwamba
namba ya siri ya kufungulia mlango
wangu wa kuingia katika chumba cha
siri ninakohifadhi vitu vyangu vya siri
imebadilishwa na ndiyo maana nikataka kuja hapa haraka na kweli
namba imebadilishwa"
"Ni nani hao wanaokufuatilia
mkuu?
"Kuna watu fulani wanafuatilia
sana mambo yangu"
"Unawafahamu?
"Ninawafahamu na wengine ni
watu wangu wa karibu."
"Tunawafanya nini?Nipe
maelekezo" akasema Obi
"Tutawatafuta na kuwapata
lakini kwanza ni kuufungua mlango
huu kufahamu nini hasa walichokuja
kukitafuta humu ndani"
Frank akamchukua Obi hadi stoo
wakachukua vifaa vya kuwawezesha
kutoboa tundu kazi na kazi ya
kuutoboa ukuta ikaanza.Obi alichukua
dakika ishirini kuweza kutoboa tundu
katika ukuta lililowazewezesha
kupita.Frank akashuka ngazi huku akikimbia na Obi akimfuata
nyuma.Moja kwa moja Frank
akaelekea katika ofisi
yake.Akasimama na kushika
kichwa.Vitu vilitawanya na ilionekana
kulikuwa na upekuzi mkubwa .
"I swear I'm going to kill
them!!!..I'm going to kill...!!!! akasema
kwa hasira na kuanza kuokota
karatasi mbalimbali zilizokuwa
zimetupwa chini
"Nani hawa waliofanya kitu hiki
mkuu? akauliza Obi lakini Frank
akujibu kitu alikuwa anafungua droo
za kabati haraka haraka na kutazama
ndani.
"Oh my God!! akasema akiwa
amekata tamaa
"Nini bosi kuna kitu cha muhimu
wamechukua?akauliza Obi
"My laptop!! akasema Frank na
kukaa juu ya meza Ndani ya kompyuta hiyo kuna
mambo yoyote ya muhimu ulikuwa
umeyahifadi?
"Kuna mambo ya muhimu sana
na nyeti ambayo sikutaka mtu yeyote
ayafahamu" akasema Frank kwa
masikitiko
"Ni akina nani hawa
waliokufanyia hivi?akauliza
"Wamecheza na petroli kwenye
moto na wataijua nguvu yangu.!!!!
akasema kwa hasira Frank
"Wote waliohusika katika jambo
hili wao na familia zao hakuna
atakayesalimika.Kila walilolitenda la
kuvamia makazi yangu ni tangazo la
vita na ninaapa nitawafyeka hadi
kizazi chao.Sintakuwa na huruma
kabisa katika hili" akasema Frank
"Mungu atanisamehe kwa hiki
ninachokwenda kukifanya kwa wote
waliofanya ujinga huu!! akasema Frank na kuusukuma mlango
unaoingia katika chumba cha
kuhifadhi vitu vyake ambao ulikuwa
umepigwa na kilipuzi na ukawa wazi
akakuta makasha ya mbao yaliyojaa
viatu yakiwa yamesambazwa.
"Walikuwa wanatafuta nini hasa
mkuu hadi wakapekua namna hii?
akauliza Obi
"Stop asking question Obi.Jiandae
kwa kazi.Safari hii sitaki makosa.Sitaki
mahojiano nataka kifanyike kitu
kimoja tu.Kutoa rho ya kila
nitakayekuelekeza.Mungu
atanisamehe kwa hili" akasema Frank
"sawa bosi ninasubiri kauli
yako"akasema Obi
"Nimekwisha kwambia kwamba
jiandae kwa kazi kubwa.Roho za watu
wengi zitaondoka katika hili lakini
kabla ya yote namtaka Winnie hapa
ndani.Mleteni haraka sana" akasema Frank na biakatka baada ya dakika
tano akarejea akiwa na Winnie.Frank
akamtaka Obi amfungue awe huru na
kumuamuru atoke mle ndani
"Winnie nimekuita hapa kwa
mara ya mwisho kwani una dakika
chache sana za kuendelea kuivuta
pumzi" akanyamaza na kumtazama
Winnie aliyekuwa akitetemeka kwa
woga
"Hii ni ofisi yangu ya siri ambayo
huhifadhi nyaraka zangu za siri.Muda
mfupi uliopita imevamiwa na watu
wasiojulikana na unajionea
mwenyewe mambo
waliyoyafanya.Wamepekua kila
mahala wamevuruga ofisi yangu na
wamechukua kila walichoona
kinawafaa wakaondoka.Hili ni tangazo
la vita kati yangu na wao" akanyamaza
akavuta pumzi ndefu halafu
akaendeleaNinaamini kabisa kwamba
miongoni mwa hao jamaa waliofanya
uchokozi huu ni dada yako Vicky na
kwa kitendo hiki nimeamua kulipiza
kisasi kibaya sana kwao.Mimi huwa
sichezewi kiasi hiki.Huu ni uchokozi
uliovuka mipaka na nitawafanyia kitu
kibaya mno.Nitawateketeza wao na
familia zao.Nitakiondoa kizazi chao
hapa duniani.Mungu atanisamehe kwa
hili ninalokwenda kulifanya."akasema
kwa hasira
"Frank please dont kill me!!
Winnie akalia huku mwili wote
ukimtetemeka kwa woga.Frank
alikuwa amekasirika mno.
"Kuna kitu kimoja tu ambacho
kinaweza kukuokoa Winnie na
kunifanya nibadili adhabu yangu
kwako.Nataka unieleze ukweli ni wapi
alipo dada yako?Ukinieleza hilo
nakuahidi nitakuacha huru.Mimi ni mtu ninayetembea katika maneno
yangu hivyo nikisema nitakuacha huru
amini nitakuacha huru.Winnie wewe
bado msichana mdogo na una mambo
mengi bado ya kufanya katika
maisha,una ndoto nyingi za kutimiza
na unayapenda maisha yako lakini
utayatimiza hayo yote endapo tu
utanieleza ukweli.Chaguo ni lako
aidha unieleze ukweli uendelee kuishi
au nikutoe roho.Ninakupa sekunde
sitini za kuamua hatima ya maisha
yako"akasema Frank
"Frank sifahamu mahala pengine
ninapoweza kumpata dada kwa
wakati huu zaidi ya pale
nilipowapeleka.Tafadhali naomba
usiniue Frank nakuomba sana"akalia
Winnie
"Thirty seconds!! akasema Frank
"Frank please I'm telling the
truth!! akazidi kulia Winnie "Ten seconds!! akasema Frank
"Frank nakuomba tafadhali!!
akalia Winnie
"Five seconds!! akasema Frank
na Winnie akaongeza kulia akiomba
Frank asimuue
"Two Seconds!! akasema Frank
na kutoa bastora akamlenga Winnie
"Nimekupa nafasi ya kufanya
uchaguzi kuhusu maisha yako nawe
umechagua kufa.Kwa heri Winnie"
akasema Frank na bila huruma
akaachia risasi tatu kutoka katika
bastora yake zilizomkosa Winnie na
kuvunja kioo cha kabati Winnie
akaanguka kwa woga
"Una bahati ninahitaji bado
kukutumia vinginevyo ningeweza
kukutoa uhai"akawaza Frank akiwa
amewaka kwa hasira.Akamuita Obi Toa hii takataka nenda kaifunge
garini bado nitahitaji kumtumia"
akasema Frank
"Mkuu kuna taarifa nimepewa na
vijana waliokuwa wanazunguka
nyumba kwamba wameokota miili ya
watu wawili karibu na mashine ya
kufua umeme wakiwa hawana
fahamu"
"Wako wapi hao watu? akauliza
Frank
"Wameletwa wako hapo nje"
akajibu Obi halafu wakatoka haraka
kwenda kuwatazama watu wale ni
akina nani
"Oh my God ! Ni akina Marwa.Are
they still breating?akauliza Frank kwa
masikitiko
"Wanaonekana bado wanapumua
japo kwa mali" akasema Obi na Frank
akaagiza wapakiwe garini ili
wawakimbize hospitali.Akawataka vijana watatu wabaki pale nyumbani
wakilinda yeye na wengine wote
wakaingia katika magari na kuondoka
kuwahi hospitali kuokoa maisha ya
akina Marwa
"Ninarudia tena kwamba hakuna
aliyeshiriki katika unyama huu
atabaki salama.Swali linalonila akili ni
je watu hawa ni akina nani na kitu
gani wanakitafuta kwangu? Lakini
mkosi wote huu umeletwa na Graca na
mama yake.Kama asingeiiba
kompyuta yangu haya yote
yasingejulikana.Nilikuwa na mipango
naye mizuri sana ya kumjengea
maisha bora lakini akapuuza hayo
yote na akachagua kushirikiana na
akina Elvis" Mara tu alipokumbuka
Elvis akahisi mwili wote unamsisimka
"Bado sijapata jibu kuhuus huyu
Elvis ambaye Winnie amemtaja kuwa
ni mmoja wa watu waliomteka Vicky.Kama ni kweli huyu Elvis
ametokea wapi wakati Elvis
ninayemfahamu aliyekuwa
akinifuatilia amekwisha uawa?Kuna
Elvis wawili katika idara ya ujasusi?
Au kuna mtumwinine amejipa jina la
Elvis ?akajiuliza
"Jambo hili linazidi
kunichanganya lakini nitapata majibu
pale tu nitakapofanikiwa kumpata
Vicky.Yeye ndiye anayeweza
kunihakikishia ni Elvis yupi ambaye
Winnie amemtaja"akaendelea kuwaza
Frank.
Waliwafikisha akina Marwa
hospitali na kwa haraka wakapatiwa
huduma.Wakati wakiendelea
kuhudumiwa Frank akawataka akina
Obi waondoke kwani walikuwa na
mambo mengi ya kufanya kwa usiku
ule Tunaelekea wapi mkuu?
akauliza Obi
"Nahitaji kumuhoji zaidi
Winnie.Nikimpata dada yake
nitakuwanimepata jibu la kila
kilichotokea usiku huu.Ni yeye pekee
anayeweza kunisaidia kumpata
Vicky.Turejee kule mahala
tulikokwenda mwanzo" akasema
Frank wakaondoka pale hospitali
kurejea tena katika makazi ya akina
Elvis

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana...

Elvis anajigongea tu ngozi bila kuvuja jasho...

Doreen kaliwa, Gracia kaliwa... ila kiherehere cha Winnie kitamponza...


Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom