Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Ngoma inogile,frank ameshakusanya team ya vijana wake na wanaenda kuchukua silaha kwanza,nahisi hizo silaha wanaenda kuzichukulia palepale walipo kina Elvis na team yake yatazuka mapambano,hisia zangu zinazidi kunituma kwamba huo ni usiku mbaya sana kwa frank coz ameshanusa harufu ya mzimu Elvis he must die,hakuna aliyewahi kuonana na mzimu akabaki hai,huyo mume wa Elizabeth sina uhakika kama kweli amekufa inawezekana kifo kimekuwa faked,hii ngoma ni nzito na huu ni usiku wa damu,let's wait and see ,nitarudi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye kifo cha Deusdedith MM nakuunga mkono,
 
I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 64

Baada ya kutoka shambani kwa
Frank,akina Elvis walirejea katika
makazi yao.Mara tu walipofika
wakastushwa na kukuta mlango
mdogo katika geti la nyumba yao
ukiwa wazi Winnie amerejea? akauliza
Vicky lakini hakuna aliyemjibu kila
mmoja akatoa bastora
yake,wakashuka garini na kuingia
ndani kwa tahadhari
kubwa.Walizunguka nyumba yote
lakini hawakuona dalili zozote za
kuwepo mtu
"Kote kuko salama" akasema
Steve kisha wakaingia ndani na
kukuta sebuleni si kama
walivyopaacha
"Some one was here" akasema
Elvis na kwa tahadhari wakaanza
kuzungukia vyumba vyote wakakuta
milango yote iko wazi
"Yawezekana ni Winnie aliamua
kurudi na alipotukosa akaondoka
tena" akasema Vicky
"Hapana si winnie.Kuna watu
wengine wamekuja hapa wakati
hatupo na inaonekana kuna kituwalikuwa wanakitafuta.Tutaufahamu
ukweli" akasema Elvis na kuchukua
kadi ndogo ya kuhifadhia kumbu
kumbu katika kamera ndogo za siri
alizozifunga na wote wakaenda
sebuleni akaiweka kadi ile katika
kompyuta na kuanza kutazama toka
muda ule walipoondoka pale
nyumbani.Hakukuwa na mtu yeyote
aliyeonekana katika kamera hadi
zilipopita dakika hamsini ndipo
kamera iliyoelekezwa getini
ikaonyesha watu sita wakiruka ukuta
na kuingia ndani
"Hawa hapa" akasema Elvis na
kurudisha nyuma kidogo wakaanza
kuwafuatilia.Hawakuwa wameziba
nyuso zao mmoja wao akasogelea
mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni
ndipo Vicky akamtambua
"Nimemkumbuka mtu huyu.Ni
yule aliyetuvamia nyumbani asubuhi.Amenifuata hadi huku?
akasema na Steve akamtazama
akathibitisha kuwa ndiye.Kamera
iliyokuwa sebuleni ikawaonyesha
wale jamaa wakifuata korido kuelekea
vyumbani ambako hakukuwa na
kamera nyingine iliyofungwa.Baada ya
muda wakarejea sebuleni na yule
kiongozi akatoa simu akazungumza na
mtu fulani na kutoka na baada ya
dakika kama tatu hivi akarejea akiwa
ameongozana na watu ambao
waliwawafanya wote mle ndani
wapatwe na mshangao
"Baba!! akasema Graca
"Winnie? akasema Vicky
"Sasa picha limekolea.Winnie na
Frank? Wamekutana
wapi?Wanafahamiana?akauliza Elvis
akimtazama Vicky
"Frank na Winnie
wanafahamiana? akauliza Elvis Hapana hawafahamiani.Sijawahi
kumtambulisha Frank kwa Winnie
hata mara moja.Makutano yetu yote
huwa ni nje ya nyumbani.Hata mimi
nashangaa wamekutana
wapi?akasema Vicky na katika
kumbukumbu ya kamera ikaonekana
Winnie akiwa amepigishwa magoti na
Frank aliyekuwa amefura hasira
akamnyooshea bastora na ilionekana
kuna kitu alikuwa anamuuliza.Winnie
akalia akiomba na Frank akaachia
risasi zilizovunja kioo cha kabati na
Winnie akaanguka chini na baada ya
muda akafungwa mikono na kutolewa
nje.Vicky akashindwa kujizuia
akatokwa na machozi
"Jamani mdogo wangu" akasema
"Stop crying Vicky!! akasema
Elvis.Kamera ilimuonyesha Frank
akiwa sebuleni na baadae akaitoa
simu yake akasoma ujumbe kisha akatoka mbio na kamera ya nje
ikamuonyesha akitoka nje ya
geti.Hawakuonekana tena
"Walikuja hapa kutufuata
sisi.Tayari wamekwisha tufahamu
mahala tulipo na ndiyo maana wakaja
na kikosi wamejiandaa kwa
mapambano" akasema Elvis
"Lakini wamefahamuje kuhusu
sisi? Wamempataje Winnie?akauliza
Vicky
"Winnie ndiye anayepaswa
kujibu swali hilo.Kupitia kwake
tutafahamu ni vipi ameweza kukutana
na akina Frank"
"Elvis tafadhali nawaomba
tufanye kila lililo ndani ya uwezo
wetu kumuokoa mdogo wangu.I won't
forgive myself if anything bad happens
to her!! akasema Vicky huku macho
yake yamejaa machozi We'll do everything we can but
right now we have to get out of
here.Tuchukue kila kinachotufaa
tuondoke kwani mahala hapa si
salama tena.Tayari tumegundulika"
akasema Elvis
"Tunakwenda wapi? Steve
akauliza
"Tutajua baada ya kutoka hapa"
akasema Elvis na kuchukua smu yake
akampigia Meshack Jumbo
akamjulisha kilichotokea na
kumuahidi kumpigia tena simu
baadae.Akachukua kompyuta ya Frank
aliyopewa na Graca na kila kilicho
chake akavipeleka garini.Zoezi hilo
halikuchukua muda mrefu wakafunga
nyumba na kuondoka
"Tunaelekea wapi? akauliza
VickyBado sifahamu lakini tuondoke
kwanza hapa kisha tutapata sehemu
ya kwenda" akasema Elvis
"Ninayo nyumba yangu ambayo
imekamilika ninataka kuitumia kwa
biashara ya kupangisha.Iko sehemu
tulivu.Tunaweza kuhamishia makazi
ya muda hapo" akasema Vicky
"Winnie anapafahamu mahala
hapo?Elvis akauliza
"Hapana hapafahamu"
"Good.Tupeleke hapo tuweke
makazi ya muda" akasema Elvis na
kumgeukia Omola
"Omola endelea kumfuatilia
Winnie ili tufahamu mahala alipo"
akasema na Omola akawasha
kompyuta yake na kusema
"Simu yake bado imezimwa"
"Endelea kumfuatilia na kama
kuna chochote utakigundua
utujulishe" akasema Elvis na safari ikaendelea.Garini kila mmoja alikuwa
kimya akiwaza lake.Kitendo cha Frank
kugundua mahala walipo kiliwastua
sana
"Steve alinionya kuhusu
kuwakaribisha akina Vicky pale
nyumbani lakini kinapuuzia na hiki
ndicho kilichotokea.Pamoja na
kumuonya Winnie hakutaka kutusikia
akakimbia na sasa amesababisha
madhara.Amekamatwa na akina Frank
ameteswa na amewaonyesha mahala
ulipo.Ni vipi endapo atawaeleza kuwa
bado niko hai? akajiuliza na kuhisi joto
la ghafla licha ya gari kuwa na kipoza
hewa
"Kama wakigundua niko hai kila
kitu kitaharibika na nitawaweka
katika hatari watu watu wengi
akiwamo mke wangu
Patricia.Natakiwa kuchukua hatua za
haraka sana za kumnusuru Patricia.Anatakiwa ahame haraka sana
kwa akina Juliana na atafutiwe makazi
mengine na hata ikiwezekana
ahamishiwe nje ya nchi kwa muda
hado hapo mambo
yatakapotulia.Nitazungumza na
mkurugenzi baadae kuhusu jambo hili
lakini kesho asubuhi lazima Patricia
aondoke haraka sana pale kwa akina
Juliana" akaendelea kuwaza
Walifika katika nyumba ya Vicky
ambayo tayari ilikwisha kamilika na
ilikuwa ikisubiri mpangaji.
"Nyumba nzuri sana hii.Hongera
Vicky"akasema Steve mara tu
walipoingia ndani.Ilikuwa
imekamilika na ilikuwa na kila kitu
ndani
"Nyumba hii nina mpango wa
kukodisha raia wa kigeni ambao
wanakuja kufanya kazi Tanzania na
ndiyo maana nimeweka kila kitu ndani.Karibuni jisikieni nyumbani"
akasema Vicky
"Ahsante Vicky tumekwisha
karibia lakini hatuna muda wa
kupumzika tunaendelea na
kazi.Hakuna kulala leo"akasema
Elvis.Saa ilionyesha ni saa nane kasoro
dakika ishirini na mbili
"Zoezi letu limekwenda vizuri
licha ya hili lililojitokeza la Frank
kugundua makazi yetu ila nawasihi
msiogope .Tuko salama na hakuna
kitakachotokea tukashindwa
kukidhibiti.Tumepata nyaraka kadhaa
kutoka kule kwa Frank pamoja na
komputa yake ambavyo tunaamini
vinaweza kutusaidia kupata mambo
ya muhimu kuhusu mtandao wao wa
kuuza silaha.Steve weka kila kitu
mezani tuanze kupitia nyaraka
hiz😵mola wewe utaikagua kompyuta
hii ya Frank na kama kuna kituchochote cha maana utatujulisha"
akasema Elvis na Steve akaweka
mezani bahasha ile yenye nyaraka
mbalimbali na Elvis akamgawia Steve
na Vicky kila mmoja nyaraka zake
azipitie.Baada ya muda Steve akasema
"Elvis ulisema ndani ya kile
chumba mlikuta kuna shehena ya
viatu?
"Ndiyo kuna shehena kubwa ya
viatu"
"Basi hapa nina nyaraka
zinazoonyesha kuwa wiki tatu
zilizopita kuna kontena kumi na nane
za viatu zilitolewa bandarini.Kontena
hizi zote zinakwenda kwa kampuni ya
Pendeza Co.Ltd"
"Thats's interesting.Inawezekana
labda mzigo hupo wa viatu ndiyo ule
tumekuta katika kile chumba cha siri
cha Frank?akauliza Hapo ndipo tunapaswa
kuchunguza"akasema Steve
"Tuichunguze kwanza kampuni
hii ya Pendeza Co.Ltd tumfahamu
mmiliki wake ni nani na kama Frank
ana uhusika wowote katika kampuni
hii" akasema
"Guys I got something" akasema
Omola aliyekuwa akiipekua kompyuta
ya Frank,wote wakamsogelea
"Nini umekipata? akauliza
"Kuna barua pepe nimefanikiwa
kuzipata.Barua pepe hizi ni nakala
ambazo mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya McLolien anaitwa Shanon
blank alikuwa anawasiliana na mtu
anaitwa Patrice
Lwibombe.Mawasiliano yao ni kwa
lugha ya kifaransa.Katika mawasiliano
hayo Shanon anamlalamikia Patrice
kwa kuchelewesha malipo ya mzigo
waliopewa.Patrice akamuhakikishia Shanon kuwa kabla ya wiki kumalizika
watalipa pesa yote.Akaendelea
kujitetea kwamba makusanyo
hayakuwa mazuri kutokana na
mapambano makali ya vikosi vya
Serikali ya Congo vikisaidiana na vile
vya kutoka umoja wa Afrika na
kuwarudisha nyuma kidogo.Shanon
amemuahidi Patrice kwamba
watakapolipa deni lao basi
watatumiwa mzigo mkubwa haraka
sana.Frank ametumiwa nakala za
mawasiliano hayo wiki moja iliyopita"
akasema Omola
"Finaly we got them" akasema
Elvis kwa furaha.
"Subiri kidogo Elvis" akasema
Steve
"Maelezo haya ya Shanon
yametoa picha fulani.Nyaraka hizi za
kutolea mzigo bandarini zinaonyesha
kwamba zile kontena za viatu zilitumwa na kampuni ya McLorien
.Tayari picha imeanza
kujitokeza"akasema Steve
"Ni kweli Steve picha imeanza
kujitokeza na kueleweka.Hii kampuni
ya McLorien ndio waliotuma mzigo
ule wa viatu kwa kampuni ya Pendeza
Co.Ltd.Mmiliki wake Shanon Blank
ana mawasiliano na Frank na katika
mawasiliano hayo tunaona
akiwasiliana na Patrice ambaye
hakuna shaka kwamba ana mahusiano
na kundi la waasi kwani amekiri
kwamba wamechelewa kulipa fedha
kwa sababu ya mapambano makali na
vikosi vya serikali na vile vya umoja
wa Afrika.Tunaona Shanon
anamsisitiza Patrice alipe deni lao na
halafu watumiwe mzigo mwingine
ambao ninaamini ni silaha.Kwa hiyo
sasa tuna kampuni mbili ambazo
tunapaswa kuzichunguza.Kwanza ni hii Pendeza na pili ni hii
McLorien.Tunapaswa kuifahamu
vyema kampuni hii ya McLorien na
vile vile tumfahamu huyu Patrice ni
nani na yuko wapi.Tunatakiwa
kufahamu ni namna gani silaha
zinaingia hapa nchini?Omola anza
kufanya uchunguzi wa kampuni hii ya
McLorien tufahamu mmiliki wake ni
nani na inajishughulisha na nini? Vile
vile fuatilia huyu Patrice ni nani na
yuko wapi?akasema Elvis na Omola
akaenda kuketi mezani kuendelea na
kazi aliyopewa
"Wakati Omola akiendelea na
uchunguzi wa kampuni ya McLorien
sisi tutaendelea kuichunguza kampuni
ya Pendeza.Tutamtumia Mkurugenzi
kwani yeye anao uwezo wa kuingia
katika mtandao wa taasisi
yoyote.Nataka atusaidie kuingia katika
mtandao wa wakala wa kusajili biashara na makampuni ili tuifahamu
vyema kampuni hii ya Pendeza iko
wapi na mmiliki wake ni
nani?akasema Elvis na kisha akatoa
simu na kuzungumza na Meshack
Jumbo
"Mkurugenzi kuna jambo
tunahitaji msaada wako" akasema
Elvis
"Jambo gani Elvis?Mko wapi sasa
hivi?
"Tumepata hifadhi sehemu fulani
salama"akasema Elvis na ukimya
mfupi ukapita akaendelea
"Kama nilivyokueleza kuwa
tumetoka katika nyumba ya Frank
iliyoko shambani kwake na kule
tumeingia katika ofisi yake ya siri
iliyoko chini ya nyumba.Ndani ya ofisi
hiyo tumefanikiwa kupata nyaraka
kadhaa pamoja na kompyuta ndogo
ambavyo tumekwisha anza kuvifanyia uchunguzi.Ndani ya ofisi hiyo ya siri
kuna chumba kikubwa ambacho
kinatumika katika kuhifadhi vitu na
tumekuta kuna shehena kubwa ya
viatu.Katika nyaraka tulizozipata
katika ofisi hiyo ya Frank zipo
zinazoonyesha kuwa kuna mzigo wa
kontena kumi na nane umetolewa
bandarini wiki nne zilizopita ambazo
zinaonyesha ni mzigo wa
viatu.Kontena hizo zinaonekana
kutumwa na kampuni inaitwa
McLorien na kampuni iliyotumiwa
mzigo huo hapa Tanzania inaitwa
Pendeza Co.Ltd.Katika komputa
tuliyoichukua katika ofisi hiyo
tumefanikiwa kupata nakala za barua
pepe ambazo Frank ametumiwa na
mtu moja anaitwa Shanon Blank
ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa
kampuni ya McLorien ambaye alikuwa
akiwasiliana na mtu anaitwa Patrice Lwibombe.Shanon anamuuliza Patrice
kuhusu kuchelewa kuwasilisha malipo
baada ya kukabidhiwa mzigo na
Patrice akaahidi kulipa haraka sana
pesa hizo huku akijitetea kwamba
wameshindwa kulipa kwa wakati
kutokana na mapambano kuwa makali
kati yao na vikosi vya serikali
vikisaidiwa na vile vya umoja wa
Afrika"
"Ouh hizo ni habari njema
sana.Tayari tumepata mwanga.Huyu
Patrice lazima ana mahusiano na
waasi ambao wanauziwa silaha na
akina Frank"akasema Meshack Jumbo
"Ndiyo mzee.Tayari tumekwisha
anza uchunguzi kuhusiana na
kampuni hii ya McLorien pamoja na
kumfahamu huyu Patrice ni nani,yuko
wapi na anajishughulisha na
nini.Msaada tunaohitaji toka kwako ni
kuichunguza kampuni ya Pendeza Co.Ltd ya hapa Tanzania ili
tumfahamu miliki wake kwani
kampuni hii ina mashirikiano na
kampuni ya McLorien ambao
tunaamini wana mashrikiano ya
kibiashara na Patrice ambaye
tunaamini anahusiana na waasi
wanaopigana na serikali ya
Congo.Tunaomba utusaidie kuingia
katika mtandao wa msajili wa
viwanda na baishara Tanzania ili
tufahamu mmiliki wa kampuni hii ya
Pendeza Co.Ltd"akasema Elvis
"Sawa Elvis nipe dakika tano
halafu nitakupa
majibu.Ninachowataka kuanzia sasa
mnapaswa muwe makini sana kwani
hali imebadilika na kwa hiki
kilichotokea usiku huu kinaonyesha
wazi kwamba hali si salama
kwetu.Tunatajiwa kufanya haraka
sana kulimaliza suala hili kabla ya akina Frank hawajagundua kwamba
uko hai"akasema Meshack na kumtaka
Elvis amsubiri kwa dakika kadhaa ili
aweze kumpa majibu ya kuhusiana na
kampuni ya Pendeza Co.Ltd
"Elvis nini tunafanya kumpata
Winnie? akauliza Vicky ambaye
alionekana kuwa mbali sana
kimawazo.
"Vicky kwa sasa tujielekeze
kwanza katika mambo ya msingi na
baadae tutaangalia namna ya
kumtafuta Winnie ambaye
hatufahamu mahala alipo.Usihofu
Vicky tutafanya kila tuwezalo
kumpata mdogo wako" akasema Elvis
"Elvis we need to do something
quick.Tukichelewa wale jamaa
wataweza kumuua.Tumeona kwenye
kamera mambo
aliyofanyiwa.Nawaombeni jamani
tufanye haraka tukamuokoe" akasema Vicky huku macho yake yamejaa
machozi.
"Winnie ameyatafuta mwenye
haya yote yaliyompata.Kiburi chake
kimempomnza kwani hakutaka
kuamini kama alikuwa katika mikono
salama na badla yake akaamua
kuondoka na sasa ametuongezea kazi
nyingine.Tumalize kwanza mambo
mhimu ndipo tushughulike na hawa
watu wenye viburi" akasema Steve na
maneno yale yakamkera sana Vicky
"Steve ungekuwa mahala pangu
kamwe usingethubutu kutamka
maneno kama hayo.Winnie ni mdogo
wangu wa damu na siwezi kuwa na
amani kama hatapatikana akiwa
mzima.Wale jamaa wanaweza
wakamuua wakati wowote.Please we
have to save her" akasema Vicky
"Vicky vumilia kidogo tupate
majibu ya uchunguzi wetu halafu tutashughulikia suala la mdogo
wako"akasema Elvis
"Elvis they are going to kill her !!
akasema Vicky huku akilia
"Niamini Vicky hawataweza
kumuua kwani watamtumia yeye ili
kuweza kutupata.Kama si hivyo tayari
wangeweza kumuua.Naamini Winnie
ndiye aliyewaelekeza mahala pale
tulipokuwa na uliona katika kumbu
kumbu ile ya kamera namna
walivyokasirika walipokuta hakuna
mtu na ndiyo maana wakamtishia
kumuua ili aseme mahala
uliko.Niamini tafadhali kwamba
tutampata Winnie akiwa mzima.I give
you my word" akasema Elvis
"Elvis ninakuamini lakini muda
tunaoupoteza hapa wale jamaa
wanaweza wakamfanya kitu kibaya
mdogo wangu." akasema VickyVicky umekwisha hakikishiwa
kwamba mdogo wako atakapatikana
akiwa mzima sasa hofu ya nini?
Tuache tufanye kazi na tukimaliza
tutashughulikia suala la mdogo wako"
akasema Steve na Vicky akamtazama
kwa jicho la chuki
"Ninyi ndio mliosababisha haya
yote yakatokea.Kama
msingenihusisha katika kifo cha
Pascal tusingefika hapa
tulipofika.Haya yote yameanza baada
ya kunilazimisha nishiriki katika
kumuua Pascal.Kabla ya hapo maisha
yangu yalikuwa na amani na nilikuwa
nikiishi na kufanya kazi zangu kwa
amani bila matatizo yoyote lakini
nilipoanza kushirikiana nanyi ndipo
matatizo yote yalipoanza.Kama
hamtaki kunisaidia kumtafuta mdogo
wangu siendelei kushirikiana nanyi tena.I'm out of the team"akasema
Vicky kwa hasira
"Kama unataka kufanya ujinga
kama aliofanya mdogo wako hadi
akakamatwa na akina Frank be our
guest!! akasema Steve kwa ukali
"Please stop !! akafoka Elvis
"Mkitaka tufanikiwe katika hili
tunalolifanya mnatakiwa muache
mambo ya kitoto na wote muelekeze
akili zenu katika jambo zito la maana
lililoko mbele yetu.Tuna jukumu zito
sana ambalo tunapaswa kulikamilisha
na mchango wa kila mmoja wetu
aliyeko hapa unahitajika sana.I'm a
leader here and you'll all listen to
what I say.If anybody of you dont
want to listen to me or follow my
directions,is allowed to leave right
now!!akasema Elvis na kuwatazama
Steve na Vicky kwa macho makali
"I'm sorry Elvis" akasema Steve "Hakuna anayetaka kuondoka?
akauliza Elvis lakini hakuna
aliyemjibu
"Kama hakuna anayetaka
kuondoka basi acheni mambo ya
kijinga na tufanye kazi.Vicky
nimekwisha kueleza kwamba
tutafanya kila tuwezalo kumpata
mdogo wako lakini hatuwezi kuacha
kazi hii muhimu iliyoko mezani na
kuanza kuzunguka kumtafuta Winnie
ambaye hatufahamu yuko
wapi.Nimekuahidi kufanya kila
tuwezalo kumpata na ninaomba
uniamini.Kama umeshindwa
kuniamini basi ninakupo uhuru uende
ukamtafute wewe mwenyewe lakini
kama unataka mdogo wako apatikane
akiwa mzima nisikilize
ninachokuambia.Unanielewa Vicky?!
akauliza Elvis na Vicky akatikisa
kichwa kukubaliana naye Good.Lets get back to work"
akasema Elvis
"Omola kuna chochote
umekipata? akauliza
"Nipe dakika chache kuna kitu
nakifuatilia " akajibu Omola
"Wakati tukisubiri kupata majibu
kutoka kwa mkurugenzi tutafakari
namna akina Frank walivyoweza
kumpata Winnie."
"Yawezekana walimpigia simu na
kumtaka waonane" akasema Steve
"Wanafahamu njia nyepesi ya
kumpata Vicky ni kwa kumtumia
Winnie na ndiyo maana wakawekeza
nguvu katika kumsaka.Mkumbuke
mtandao huu ni mkubwa na
wanaweza wakafanya jambo lolote"
akasema Steve
"Kuna jambo moja linanipa
wasiwasi kidogo lakini sina hakika
kama linaweza kuwa na mahusiano na hiki kilichotokea" akasema Graca
ambaye toka walipofika hapa
amekuwa kimya
"Katika uchunguzi hata jambo
dogo sana linaweza kuwa na msaada
mkubwa.Tueleze hicho kinachokupa
wasi wasi" akasema Elvis
"Tukiwa chumbani nilimueleza
Winnie historia ya maisha yangu na
akashangaa sana.Akaniuliza maswali
mengi kuhusiana na baba yangu"
"Maswali gani aliyauliza?
akauliza Elvis
"Alitaka kufahamu nyumbani
kwetu,na kwa namna alivyokuwa
anauliza maswali yake ni kama vile
alikuwa anatafuta njia nyepesi ya
kuweza kuonana na baba.Mimi
sikumtilia maanani na nikamueleza
kila kitu nikiamini mimi na yeye sote
tuko katika boti moja.Nilipomuona
akiwa na baba nikakumbuka maswali yale aliyokuwa ananiuliza kuhusiana
na baba." akasema Graca
"Graca unahisi kwamba Winnie
alikwenda mwenyewe kwa
Frank?akauliza Elvis
"Exactly!! akasema Graca
"Wait" akasema Vicky
"Kuna kitu hata mimi
nimekikumbuka kuhusiana na hiki
anachokisema Graca.Jana niliporejea
kutoka kuonana na rais,Elvis alinitaka
nizungumze na Winnie na nimsihi
atulie kwani hali hii ni kwa muda tu na
baadae maisha yetu yatarejea kama
kawaida.Nilimuita chumbani
nikamuelewesha akanielewa na
ninakumbuka aliniuliza kama
ninamfahamu Frank nikamwambia
kwamba Frank ni rafiki yangu.Sikujua
kwa nini aliniuliza swali lile lakini sasa
ninaanza kupata picha ya swali
lake.Kuna uwezekano mkubwa kwamba Winnie alikwenda kumfuata
Frank yeye mwenyewe"
"Lakini kwa nini afanye hivyo?
Kwa nini akamtafute Frank wakati
tayari Graca amekwisha msimulia kila
kitu kuhusiana naye na anafahamu
kuwa ndiye anayewawinda?Steve
akauliza
"Hayo ni mawazo yangu tu lakini
majibu yote anayo yeye mwenyewe
Winnie.Tukimpata atatupa majibu
namna alivyok................." Vicky
akanyamaza baada ya simu ya Elvis
kuita,alikuwa ni Meshack Jumbo,Elvis
akaipokea haraka haraka
"Elvis nimefuatilia ile kampuni
kama ulivyonitaka na nimepata
majibu.Kampuni hii imesajiliwa hapa
Tanzania na mmiliki wake anaitwa
Irene mwabukusi.Mmiliki wake ni
moja tu na Frank hajaorodhshwa
kokote kama mmiliki wa kampuni hii.Nadhani mtu wa kumchunguza
hapa ni huyo Irene kujua namna
anavyoshiriana na Frank" akasema
Meshack
"Ahsante sana mzee kwa msaada
huo mkubwa.Tutakujulisha nini
tutakipata kutoka kwa Irene" akasema
Elvis
"Kitu kingine Elvis,tayari
nimekwisha anza kufuatilia nyumba
niliyokwambia kwamba Patricia
ataishi baada ya kumuondoa kwa
akina Juliana na kesho nitakamilisha
kila kitu kishaPatricia ahamie
hapo.Usihofu kila kitu kitakwenda
vyema.Nitawasiliana nanyi mchana
kujua mlikofikia na kuwajulisha ni
wapi nimefikia.Ninachowaomba
vijana wangu jitahidini sana kuwa
waangalifu hasa wakati huu ambao
Frank na watu wake wanamtafuta
sana Vicky" Usijali mzee tuko makini"
akajibu Elvis na kukata simu
akawageukia wenzake
"Mzee anasema kwamba mmiliki
wa kampuni ya Pendeza Co.Ltd
anaitwa Irene Mwabukusi.Anadai
Frank hahuski chochote na kampuni
hii hivyo kazi yetu sasa ni kumsaka
huyo Irene na tukimpata tumuhoji
tufahamu uhusianao wake na Frank
na mahusiano yake na kampuni ya
McLorien.Steven kesho asubuhi
itakuwa ni kazi yako ya kwanza
kumtafuta Irene na kuhakikishe kabla
ya saa nne asubuhi umekwisha mpata
na kupata majibu toka kwake."
"Sawa Elvis.Katika nyaraka hizi
kumeelekezwa mahala zilipo ofisi za
kampuni hiyo ya Pendeza.Itakuwa
rahisi kwangu kumpata"
"Good.Omola yeye ataanza kazi
yake kesho ya kumchunguza makamu wa rais.Mimi na Vicky tutashughulikia
suala la Winnie.Gracayeye ataendelea
kupumzika" akasema Elvis na
kumgeukia Omola
"Omola kuna chocte mpaka sasa
hivi?
"Kwa taarifa nilizofanikiwa
kuzipata kutoka katika mtandao ni
kwamba kampuni hii ya McLorien
imesajiliwa nchini Marekani.Ni
kampuni mama ambayo ndani yake
kuna benki na makampuni mengine
mbali mbali.Hakuna taarifa nyingi za
kutuwezesha kuifahamu kampuni hii
kiundani hata hivyo nimewasiliana
kwa barua pepe na rafiki yangu
mmoja aliyeko nchini Marekani ili
anisaidie kupata taarifa za kuhusiana
na kampuni hii ya McLorien.Kwa
kuwa tayari imeingia katika mikono
yetu lazima ichunguzwe hadi mzizi wake.Kesho tutapata jibu kuhusiana
na hii kampuni" akasema Omola
"Sawa Omola ahsante kwa kazi
nzuri.Tunaitegemea sana taarifa hiyo
ya kuhusiana na hii kampuni.Vipi
kuhusu Winnie unaweza kumtafuta
tena na kujua mahala alipo?akauliza
Elvis
"Bado simu yake imezimwa"
akajibu Omola baada ya kubofya
kompyuta yake
"Hakuna tatizo kesho tutamsaka
na kumpata.Ni usiku mwingi tayari na
ni wakati wa kupumzisha miili yetu
kujiandaa kwa siku ya kesho ambayo
itakuwa ni ndefu sana.Ahsanteni
nyote kwa ushirkiano mkubwa na
tumeweza kufanikiwa kupata mambo
ya kutusaidia katika uchunguzi
wetu.Steve utampeleka Omola hotelini
kwake akapumzike kwani kesho
asubuhi anatakiwa kuanza shughuli iliyomleta hapa Tanzania" akasema
Elvis na kuagana na Omola akangia
garini na Steve akamrejesha hotelini
alikofikia
"Vicky naendelea kukusihi
kwamba usiwe na wasi wasi hata
kidogo tutampata Wema.Kwa sasa
hawataweza kumuua kwani
wanaamini yeye ndiye njia pekee ya
kuweza kuwafikisha kwako japo
mateso atayapata"Elvis akamwamia
Vcky
"Elvis moyo wangu umekosa
amani kabisa kwa hawa jama
kumshikilia mdogo wangu.Ni vipi
kama watamtesa na akawaeleza
kwamba mimi ni mpelelezi?Sitaki siri
hii ijulikane.Elvis we have to do
whatever we can to get her back.Can
you promise me that?
Elvis akamtazama Vicky usoni na
kusema "I give you my word we'll get her
back alive"
"Thank you" akasema Vicky
"Ni wakati wa kwenda
kupumzika tuelekeze vyumba vyetu
vya kulala"
"Nyumba hii haina vyumba vingi
kama ile mliyokuwa mnaitumia ila
vilivyopo vitatutosha." akasema Vicky
na kumuongoza Elvis hadi katika
chumba watakamolala halafu yeye na
Graca wakaelekea katika chumba
kingine.Mara tu walipoingia chumbani
wakijiandaa kupumzika Graca
akamwambia Vicky kuwa kuna kitu
anataka azungumze na Elvis
akamfuata chumbani kwake akagonga
mlango na Elvis akafungua
"Graca,karibu ndani" akasema
Elvis na kumkaribisa Graca ndani
"Elvis nimekuja kukuaga mpenzi
wangu.Siwezi kulala bila kukubusu" akasema Graca na kumsogelea Elvis
akamkumbatia na kumbusu.
"Graca kama nilivyokuleza
kwamba unatakiwa uwe makini sana
watu humu ndani wasifahamu kama
mimi na wewe tunakutana.Hii ni siri
yetu.Umenielewa?
"Nimekuelewa Elvis lakini wakati
mwingine ninashindwa kujizuia kwa
mfano usiku huu sijui kama ningepata
usingizi bila kukubusu.Ninakupenda
sana Elvis zaidi ya unavyoweza
kufikiri" akasema Graca akiwa bado
amemkumbatia Elvis.Taratibu Elvis
akaitoa mikono yake na kusema
"Graca nakushukuru sana kwa
msaada wako uliotusaidia siku ya
leo.Nina imani kubwa kwamba yale
yote tuliyofanikiwa kuyagundua
ofisini kwa baba yako usiku wa leo
yatakuwa na manufaa makubwa sana
katika uchunguzi wetu" Ahsante sana Elvis.Nimejitolea
kufanya lolote lile kwa ajili yako.Ngoja
nirejee chumbani Vicky asinisubiri
sana.I love you" akasema Graca na
kumbusu tena Elvis kisha akatoka
kurejea chumbani kwao
"Kadiri muda unavyozidi kwenda
ndivyo Graca anavyozidi
kuchanganyikiwa juu
yangu.Sikupaswa kabisa kufanya naye
mapenzi lakini sikuwa na namna
nyingine ya kuweza kupata taarifa
muhimu tuliyoihitaji mno.Hili si suala
la kupuuzia na kulichukulia
kirasirahisi kwani Graca tayari
anaamini nimekubali toka moyoni
kuwa naye.Ni vipi atakapogundua
kwamba nilimdanganya ili niweze
kupata taarifa toka kwake? Hata hivyo
sitakiwi kuumizwa na jambo kama hili
wakati katika mto na kuanza
kutafakari jukumu zito lililo mbele yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom