I DIED TO SAVE PRESIDANT
sehemu 68
Najaribu kutafakari dhamira ya
wanasiasa hawa kulazimisha mkutano
wao ufanyike wakati jeshi la polisi
limeupiga marufuku?Endapo mkutano
huo utafanyika ni wazi kutazuka
vurugu kati ya wafuasi wao na jeshi la
polisi na kila mara kunapotokea
vurugu kati ya polisi na wafuasi wa
vyama vya siasa lazima maisha ya
watu kadhaa yapotee kwani hufika
mahala ambapo polisi hulazimika
kutumia nguvu kubwa zaidi baada ya
wafuasi hao kugoma kutii amri."
Akawaza Elvis halafu mara jambo
likamjia akilini
"Kuna wazo linanijia.Yawezekana
labda dhana ya wanasiasa hawa ni
kulazimisha kufanyika kwa mkutano
usio kuwa na kibali wakiamini kabisa
kwamba kutatokea vurugu kwani
lazima jeshi la polisi liwatawanye
wafuasi wao na kitokea vurugukunaweza kutokea vifo na majeruhi na
hii inaleta sifa mbaya kwa serikali
kwamba inakandamiza demokrasia na
kuua raia wake.Sioni kama kuna lengo
lingine zaidi ya hilo kwa wanasiasa
hawa kulazimisha kufanyika kwa
mkutano wao leo licha ya kupigwa
marukufu na jeshi la polisi.Ninahisi
kwamba hizi ni njama chafu za David
na washirika wake za kutaka
kuichafua serikali iliyoko madarakani
ionekane haifai na utakapofika wakati
wa uchaguzi basi agombee urais kwa
tiketi ya chama cha upinzani.Kwa
David inawezakana lengo lake likawa
hilo lakini vipi kuhusu Dr Shafi?Yeye
ana ajenda gani?Kwa nini ashirikiane
kwa siri na David na hawa
wanasiasa?Yawezekana kuna zaidi ya
ninavyofikiri.Tutapata jibu baada ya
kufanya uchung....." Graca akaingia pale sebuleni akiwa na glasi ya juisi
akamuweka Elvis mezani
"Elvis my love karibu kinywaji."
akasema Graca huku akimsugua sugua
Elvis mgongoni
"Ahsante sana Graca.Umekuwa ni
msaada mkubwa kwetu" akasema
Elvis
"Usijali Elvis.Nina furahi na mimi
kuwa na mchango wangu hata mdogo
katika jambo hili" akasema Graca na
kumbusu Elvis akaanza kumpapasa
kifuani
"Graca not now" akasema Elvis
"Elvis you have to
relax.Umekuwa ukifanya kazi
mfululizo toka jana usiku na
inakulazimu upumzike.Mwili nao
unahitaji mapumziko ili uweze
kuhimili mikiki mikiki hii
inayoendelea" Graca hatuna muda wa
kupumzika kwani watu tunaowatafuta
hawapumziki hata kidogo.Kila dakika
wako kazini wakihakikisha kwamba
hatufanikiwi .Hatuwezi kuwapa nafasi
hata ndogo wakafanikiwa kutoroka
kwani tayari tumepiga hatua
kubwa.Tayari tumefanikiwa
kuwafahamu vinara wakubwa wa
biashara hii ya silaha na tayari
tunafahamu mahala zinakotoka na
namna zinavyosafirishwa.Bado
tunaendelea kufanya uchunguzi
kuubaini mtandao huu wote.Tunahisi
bado kuna watu wengine wakubwa
ambao hatujawabaini lakini kwa
mwendo tunaokwenda nao
tutawabaini wote.Mafanikio haya yote
yametokana na wewe"
"Ni furaha kubwa kusikia kuhusu
mafanikio hayo makubwa
mliyoyafikia.Ninawaombea muweze kulimaliza salama suala hili.Mimi niko
tayari kwa msaada wowote ule muda
wowote ule nitakapohitajika kufanya
hivyo"akasema Graca
"Endelea na shughuli zako
ninakwenda kumuangalia Winnie"
akasema Elvis na kwenda katika
chumba alimo Winnie
"Winnie"akaita Elvis na Winnie
akafumbua macho.Tayari alikwisha
amka.Elvis akamsogelea karibu zaidi
"Unajisikiaje sasa hivi?
"Nina maumivu makali kichwani
na mwili wote unauma.Where am I?
akauliza Winnie
"Usiogope uko sehemu
salama.Tumekutoa katika hatari"
akasema Elvis na Winnie akataka
kuinuka lakini akauma meno kwa
maumivu Elvis akamsogelea na
kumsaidia kuinuka akakaa kitandani.Akamtazama Elvis na
machozi yakaanza kumtoka
"Nyamaza kulia Winnie.Uko
sehemu salama"akasema Elvis
"I'm sorry...I'm very sorry!!
Elvis akakaa kitandani
akamshika Winnie mkono
"Usilie Winnie.Nieleze tafadhali
nini kilitokea?Kwa nini uliondoka?
Wale jamaa wamekupataje? akauliza
Elvis na Winnie akaendelea kulia
"Nieleze tafadhali"akasema Elvis
lakini bado Winnie aliendelea
kulia.Elvis akatoka akaelekea jikoni na
kurejea na bakuli la supu akakaa
kitandani na kumnywesha Winnie
ambaye alionekana kuwa na
njaa.Alihakikisha amekunywa supu
yote
"Haya nieleze nini kilitokea?Kwa
nini ukaamua kuhatarisha maisha
yako wakati tulikwishakueleza kwamba huko nje ni hatari kuna watu
wanawatafuta?Elvis akauliza
"Samahani sana.Dada yangu yuko
wapi?
"Vicky aliondoka asubuhi na
hajarejea tena hadi mida hii.Hakuaga
mtu na hatujui mahala aliko" akasema
Elvis na Winnie akastuka sana
akaweka mikono kichwani
"Oh my God Elvis,find my
sister.She's in danger!!
"In danger?How do you know
she's in danger? akauliza Elvis
"I'm sorry Elvis kwa hiki
nitakachokueleza.Nilijipeleka
mwenyewe kwa Frank"
"What ?!!!
"I'm sorry Elvis I wanted to save
my sister"akasema Winnie na kuanza
kulia
"Relax Winnie .Nieleze kila kitu" Winnie akamueleza Elvis kila kitu
alichokifanya.Elvis akavuta pumzi
ndefu
"Kwa nini ulifanya vile
Winnie?kwa nini hukusikia kile
tulichokueleza?Huoni kwamba kwa
kufanya hivyo umehatarisha maisha
yetu na hata dada yako maisha yake
umeyaweka hatarini? akauliza Elvis
"I'm sorry Elvis.Nilidhani kwa
njia ile nitamsaidia dada yangu aweze
kuachana na kazi hii.Sikujua kama
wale jamaa ni wabaya kiasi kile"
"Umefanya kosa kubwa sana
Winnie.Nataka kufahamu kitu
kimoja,wakati mnazungumza ulinitaja
hata mara moja kwa jina? akauliza
Elvis na Winnie akaonekana kuogopa
kujibu
"Nijibu Winnie ni muhimu sana
kwangu kujua" Winnie akatikisa kichwa
kukubali,Elvis akasimama
"I'm sorry Elvis" akasema Winnie
"It's ok Winnie dont cry.Nataka
nikueleze kwamba ulichokifanya
hakikuwa sahihi na umeongeza
matatizo badala ya kuyapunguza.Watu
wale uliokwenda kuonana nao si watu
wazuri hata kidogo.Ni watu makatili
na wasio na utu.Sisi na dada yako tuko
katika operesheni ya kuwatafuta na
kuwafikisha katika sheria kwani
wanajihusisha na biashara haramu ya
silaha.Wanawauzia silaha waasi
wanaoua watu huko mashariki mwa
Congo.Tunataka tuufute kabisa
mtandao wao.Watu hawa baada ya
kufahamu kuwa tumewagundua
walitaka kuniua na ikanilazimu
kughushi kifo changu na hivi sasa
wanaamini kuwa nimekufa.Nimefanya
hivi ili niweze kupata nafsi nzuri zaidi ya kuufahamu mtandao wao na
kuwafagia wote.Kitendo cha
kufahamu kuwa niko hai kitavuruga
kila kitu kwani watajificha na
nitashindwa kufanikisha uchunguzi
wangu"
"I'm sorry Elvis..I'm real very
sorry" akasema Winnie.Chumba
kikawa kimya.Elvis alionekana
kuzama mawazoni.Akatafakari halafu
akamgeukia Winnie
"Unahisi dada yako atakuwa
wapi?
"Sina hakika lakini yawezekana
akawa katika hatari.Tafadhali Elvis
nisaidieni kumtafuta dada yangu"
akasema huku machozi yakiendelea
kumtoka.
"Ok.Let me see what we can do to
find her.Endelea kupumzika" akasema
Elvis na kutoka mle chumbani.Alihisi
kuchanganyikiwa Kwa hili alilolifanya Winnie
anastahili hata kukatwa kichwa.Kwa
nini akafanya vile na kurudisha nyuma
kile tulichojitolea maisha yetu
kukipigania?Kwa maelezo aliyowapa
akina Frank ni wazi hivi sasa
watakuwa na mashaka kama kweli
nimefariki dunia.Hii itafanya kazi yetu
iwe ngumu wakati tumekwisha fika
hatua nzuri." akawaza akielekea
chumbani kwake
"Ngoja niwasubiri akina Steve
wareje tujue namna ya kufanya kwani
tayari huyu Winnie ameharibu kila
kitu.Natamani nikamchape vibao
lakini haitasaidia kitu.Kilichopo hapa
ni kutafuta namna ya kuendelea na
operesheni yetu licha ya huyu
limbukeni kuharibu kila kitu" akawaza
Elvis na kukaa kitandani akaweka
mikono kichwani akazama mawazoni *******************
Frank aliwasili nyumbani kwa
Elizabeth.Hali iliyokuwapo mahala
hapa ni kama vile hakukuwa na
msiba.Watu hawakuwa wengi kama
ilivyozoeleka mahala kunapokuwa na
msiba.Walikuwepo ndugu wachache
na wengine ni wafanyabiashara
marafiki wa familia wa hapa nchini na
wengine wa kutoka nje ya
nchi.Waombolezaji wote walikuwa
wamekaa katika bustani kubwa na
nzuri na huko kila kitu
kilipatikana.Kulikuwa na vyakula na
vinywaji vya kila aina.Watu walikuwa
wakila na kunywa kama vile hakuna
jambo la huzuni linaloendelea .
Frank alipofika akapokewa na
walinzi na kuelekzwa sehemu ya
kuegesha na aliposhuka tu akakutana na mwanadada maalum ambaye kazi
yake ilikuwa ni kuwapokea wageni
waliokuwa wakifika pale msibani na
kuwaelekeza sehemu za kuketi
"Poleni sana" akasema Frank
baada ya kushuka garini na kupokewa
na mwanadada yule aliyekuwa
amevalia gauni refu jeusi lililomkaa
vyema
"Tunashukuru sana mzee"
akasema Yule mwanadada ambaye
kila alipotabasamu vishimo
vilionekana katika mashavu
yake.Akamuelekeza sehemu ya
kwenda kuketi lakini kabla hajaelekea
huko Frank akasema
"Ninahitaji kuonana na madam
Elizabeth.Yuko sehemu gani?
Yule mwanadada akampeleka
mahala waliko waombolezaji wengine
halafu akaenda kumjulisha Elizabeth
kuhusu Frank.Elizabeth akawaomba radhi watu aliokuwa amekaa nao
akaongozana na yule mwanadada hadi
mahala alikokaa Frank.Elizabeh
akamtaka amfuate wakaelekea ndani
"Karibu Frank"akasema
Elizabeth wakiwa katika chumba cha
mazungumzo.
"Madam utanisamehe sana kwa
kuja mida hii lakini imenilazimu nije
kutokana na suala la dharura
lililotokea" akasema Frank
"Nini kimetokea Frank?
"Madam kuna jambo limetokea
ambalo naona limevuka mikono yangu
na linahitaji nguvu ya ziada
kulimaliza."
"Nieleze Frank ni jambo
lipi?Usiniambie umeharibu tena kwani
safari hii sintakusamehe" akasema
Elizabeth kwa sauti ya juu kidogo
"Jana usiku nilipigiwa simu na
binti mmoja akajitambulisha kwamba anaitwa Winnie ni mdogo wake na
Vicky"
"Bado unaendelea na masuala ya
Vicky?Nilikukanya uachane na
masuala hayo!!! akasema Elizabeth
"Sikuwa naendelea na suala hilo
naomba unisikilize madam"
"Endelea"akasema Elizabeth
"Winnie alinitaka
tuonane.Nikamuelekeza sehemu ya
kukutana na tulipoonana akanieleza
mambo ambayo yalinistua kidogo"
"Alikueleza nini?akauliza
Elizabeth
"Alikuja kuniomba nimsaidie
dada yake.Alidai kwamba dada yake
hahusiki chochote na kifo cha
Pascal.Anasema kwamba kuna watu
wawili ambao walimtumia dada yake
katika kumuua Pascal.Walifahamu
kuwa ana ukaribu na Pascal hivyo
wakamtaka amuite pale hotelini na wakatishia kumuua asipofanya
hivyo.Vicky akampigia simu Pascal na
kumtaka afike pale hotelini na wale
jamaa wakamuua"
Sura ya Elizabeth ikabadilka kwa
maneno yale ya Frank akakunja
sura.Frank akaendelea
"Winnie anadai kwamba wale
jamaa waliwapeleka katika nyumba
fulani wakawafungia na Winnie
akasikia wale jamaa wakimlazimisha
Vicky awapeleke sehemu ambako
wanaweza wakanipata na ninahisi
lengo lao lilikuwa ni kunimaliza na
mimi pia.Walitishia kumuua mdogo
wake endapo atakataa na Vicky
akashindwa kukataa akakubali
kuwapeleka sehemu ambako
anaamini wanaweza
wakanipata.Usiku huo wakaondoka na
kumuacha Winnie hapo katika hiyo
nyumba na akafanikiwa kutoroka ndipo aliponitafuta na kunitaka
nimsaidie kumuokoa dada
yake.Nilimtaka anipeleke katika hiyo
nyumba walimokuwa wamefungwa
tukaenda huko lakini hatukufanikiwa
kukuta mtu.Tukiwa pale nikapata
ujumbe katika simu kuwa namba za
kufungulia mlango wa ofisi yangu ya
siri katika nyumba yangu ya shambani
imebadilishwa nikahisi kuna watu
wamevamia nikaenda haraka sana na
kukuta kweli ofisi yangu imevamiwa
na kuvurugwa sana.Sikufanikiwa
kuwapata hao jamaa.Nilirejea tena
katika ile nyumba lakini hakukuwa na
mtu nikalazimika kuwaacha vijana
wawili wachunguze nani watakaokuja
pale.Niliondoka na Winnie na
kumpeleka mafichoni" Frank
akanyamaza na kumtazama Elizabeth
aliyekuwa amewasha sigara akivuta
mfululizo.AkaendeleaAsubuhi ya leo nikapigiwa simu
na Vicky akanitaka
tuonane.Tulipoonana nikamtaka
anieleze wale watu waliomteka ni
akina nina wako wapi lakini akakana
kutekwa wala kuwafahamu hao
jamaa.Nilishangaa kwa kauli zao
zinazokinzana ikanilazimu
kumchukua Vicky kumpeleka mahala
nilikomficha Winnie ili nikaupate
ukweli na nilipofika pale nikakuta
vijana waliokuwa wanamlinda Winnie
wamekufa na Winnie hayupo.Nikiwa
hapo nkapigiwa simu na Irene
akanitaka nionane naye.Nikaenda
kuonana naye na akanieleza kwamba
kuna watu wawili walifika nyumbani
kwake asubuhi na wakamtisha kwa
bastora na kumtaka angozane
nao.Walianza kumuhoji kuhusiana na
kampuni ya Pendeza na wakaanza
kumtesa ikamlazimu kuwaeleza ukweli kwamba kampuni ile ni ya
kwangu.Walikuwa na nyaraka
tulizotolea mzigo wa mwisho
bandarni na wakauliza maswali mengi
kuhusiana na mizigo yetu namna
tunavyoisafirisha na Irene akawaeleza
kila kitu kisha wakamuachia na ndipo
aliponipigia simu"
Elizabeth akaitupa chini sigara
aliyokuwa anaivuta na kuisigina kwa
kiatu kisha akamtazama Frank kwa
hasira
"Frank nimechoka sitaki tena
kusikia upuuzi kutoka kwako.Hii ni
mara ya mwisho kusikia ukinieleza
ujinga unaoendelea kuufanya.Next
time I'll shoot you right here!!!..Nina
mambo mengi yananikabili kwa sasa
hivyo inuka nenda karekebishe
makosa yako.Make sure before sunset
you find those bastards and kill them.You understand?!! akasema
Elizabeth kwa ukali
"Madam Elizabeth nimekuja
kwako kukueleza na kukuomnba
msaada kwa sababu ni suala ambalo
limevuka nguvu yangu."
"Unashindwaje kuwatafuta hao
jamaa?How could you let them enjoy
doing what they like?Umekuaje siku
hizi Frank?Ukishindwa katika hili
hutakuwa unanifaa tena nitatafuta
mtu mwingine anayeweza kufanya
kazi!! akasema Elizabet na maneno
yale yakamkera Frank akasimama
"Madama Elizabeth sitaki
nikuvnjie heshima lakini nimekuja
hapa nina tatizo ambalo linatuhusu
sote hivyo nataka unisikilize hadi
nitakapomaliza.Jambo hili
ninalokueleza ni muhimu sana na
endapo utalipuuza we'll all go down so
sit there and listen to me" akasemaFrank.Elizabeth akamtazama Frank
kwa hasira na kusema
"Frank toka lini umeanza kunipa
amri?Mapembe hayo yameota
lini?Unafahamu unazungumza na
nani?Mimi si kama hao wanawake
zenu,mimi ni mtu mwingine tofauti
kabisa.Ninaogopwa sana na hata na
magenge makubwa ya
kimafia.Ninaweza hata sasa nikaamua
usitoke tena nje na maisha yako
yakaishia humu humu ndani.Dont play
with me.Na hii ni nafasi ya mwisho
usithubutu tena kuniamuru
chochote.Umesikia Frank? akauliza
Elizabeth.Frank akapiga magoti na
kuomba msamaha
"Nisamehe madam Elizabeth
sintarudia tena utovu wa nidhamu"
akasema Frank
"Stand up.Malizia unachotaka
kunieleza kisha uondoke.Nina mambo mengi sana ya kufanya.Wakati wangu
wa kukutana nawe na kusikiliza
upuuzi wako bado haujafika" akasema
Elizabeth na Frank akaketi
"Nataka unieleze kwa nini hawa
jamaa wamekushinda?Hauna nyenzo
za kukuwezesha kuwapata?
"Madam hukuniacha nimalizie
nilichotaka kukueleza.Tuna tatizo
madam.Kwa mujibu wa maelezo
aliyonipa Winnie ni kwamba moja kati
ya watu hao wawili waliokuwa
wamewashikilia na ambao ninaamini
ndio waliovamia ofisi yangu shambani
na ndio waliomteka Irene na kuwaua
wale vijana wawili na kumchukua
Winnie ni Elvis"
"Elvis?!! akauliza Elizabeth kwa
mshangao mkubwa
"Elvis yupi?Kuna Elvis mwingine
ameibuka ukimuacha yule
aliyekufa?akaulizaKwa wasifu aliouelezea
Winnie,Elvis huyo anafanana sana na
Elvis yule aliyekufa.Elvis anafanana na
mcheza mpira wa kikapu wa Marekani
Stephe curry na hicho ndicho kitu cha
kwanza alichokielezea Winnie
nilipomuuliza kuhusu huyo
Elvis.Kingine ambacho kilinipa tatizo
ni pale aliponieleza kwamba
mwanangu Graca naye yumo katika
hiyo nyumba walimokuwa
wamefungwa na hao watu aliowataja
kwa majina ya Elvis na
Steve.Ukumbuke ni Elvis
aliyemtorisha Graca kutoka Afrika
kusini kwa hiyo taarifa hiyo ikanipa
shida kidogo"
"That must be a ghost.That
woman isn't telling the truth"
akasema Elizabeth
"Lakini Winnie hakuonekana
kama anadanganya.Nilimtazama machoni na alikuwa anasema
kweli"akasema Frank na ukimya
ukatanda na Elizabeth akawasha
sigara akavuta mikupuo kadhaa,Baada
ya dakika mbili akauliza
"Are you sure Elvis died?
Swali lile likambabaisha kidogo
Frank
"Answer me Frank" akasema
Elizabeth
"Elvis alikufa"
"Nani alithibitisha?
"David alithibitisha hilo na hata
mimi na Pascal tulikuwepo msibani na
jeneza lenye mwili wa Elvis likaletwa
na watu wakatoa heshima zao za
mwisho"
"You saw him in the coffin?
akauliza Elizabeth
"I didnt.Waliobahatika kutoa
heshima za mwisho ni marafiki na
ndugu wachache kwani alikuwa ameumizwa vibaya kwa risasi maeneo
ya kichwani hivyo hawakuruusu kila
mmoja amuangalie" akasema
Frank.Elizabeth akawa kimya kwa
muda akatafakari halafu akamgeukia
Frank
"Ulinieleza kwamba David ndiye
aliyeshughulikia mpango mzima wa
kumuua Elvis?
"Ndiyo madam" akajibu Frank
"Nisubiri hapa ninakuja sasa
hivi.David tayari yuko hapa" akasema
na kutoka akamucha Frank peke yake
mle ndani.Baada ya dakika saba
Elizabeth akarejea na safari hii akiwa
ameongozana na David Sichoma
"David nimekuleta hapa ili kwa
pamoja tuzungumze suala muhimu
sana ambalo limejitokeza na linahitaji
kushughulikiwa haraka sana"
akasema ElizabethNini kimetokea Madam?
akauliza David kwa wasi wasi
"Kabla sijakueleza chochote
nataka unijibu.Are you sure Elvis
died? akauliza Elizabeth na swali lile
likamshangaza kidogo David
"Yes he died.Why? akauliza
David
"Are you sure?
"Yes I'm sure.Elvis tayari
amekufa na kuzikwa.Kuna nini
kwani?akauliza David
"Ulihakiki kama kweli amekufa?
"Frank aliponiomba nimsadie
kumuua nilimuomba makamu wa rais
anisaidie naye akamkabidhi jukumu
hilo mkurugenzi wa idara ya ujasusi
Meshack Jumbo na kumtaka
ahakikishe Elvis anakufa na ndivyo
ilivyokuwa.Elvis akafa na makamu wa
rais akajulishwa naye
akanijulisha.Nilituma watu wangu kuhakiki kama kweli Elvis amekufa na
wakahakiki kweli amekufa na
kuzikwa"akasema David
"Ahsante David kwa taarifa hiyo
na kutuhakikishia kwamba Elvis
amekufa lakini kuna taarifa nyingine
ambayo amekuja nayo Frank.Elvis
ameonekana akiwa hai."
"What?!! David akashangaa
"That's impossible.Elvis
amekwisha kufa na kuzikwa.Anayedai
kumuona ameona kivuli chake japo
sitaki sana kamini katika mambo
hayo.Elvis hataonekana tena" akasema
David kwa kujiamini
"David pamoja na maelezo hayo
uliyoyatoa nataka ufanyike uchunguzi
mkubwa kwamba kweli Elvis
amekufa?Nataka mtu aliyepewa
jukumu la kumuua Elvis apatikane ili
tupate uhakika kama kweli Elvis
amekufa au vipi" Madam Elizabeth una wasiwasi
labda Elvis hakufa?
"Ninakuamini sana David lakini
siwezi kuzipuuza taarifa za Elvis
kuonekana hai.Anza kulishughulikia
hilo na mpaka jioni ya leo nataka huyo
mkurugenzi wa ujasusi aliyepewa
jukumu la kumuua Elvis awe
amepatikana na atuthibitishie
kwamba kweli Elvis amekufa.Achana
na kila unachokifanya nenda
kalishughulikie hilo na jioni ya leo
nataka majibu" akasema Elizabeth na
David akainuka na Elizabeth
akamsindikiza nje kisha akarejea
ndani
"Sasa ni zamu yako.Nataka
mpaka jioni ya leo hao watu wawili
ambao wanaanza kuonekana kuwa
kikwazo kwetu wawe wamepatikana
na tuwajue ni akina nani .Mtumie
huyo Vicky kupata taarifa muhimu za kuwahusu hao jamaa.Kama mpaka saa
kumi na mbili jioni ya leo hautakuwa
umefanikiwa kuwapata mimi
mwenyewe nitabeba jukumu na
nitazungumza na huyo Vicky na
asiombe jambo hili lifike huko.Nenda
kaanze kazi mara moja na saa kumi na
mbili kamili nipigie simu nijulishe
umefikia wapi" akasema Elizabeth na
Frank akaondoka.Elizabeth akaenda
moja kwa moja chumbani kwake
akawasha sigara na kuanza kuvuta
mfululizo
"Kwa mara ya kwanza katika
maisha yangu ninahisi uoga kutokana
na taarifa za kukinzana kuhusiana na
kifo cha Elvis.Ninahisi woga kwa
sababu huyu jamaa tayari anafahamu
kuhusu biashara ya silaha ambayo
Frank anaisimamia na endapo
atachimba kwa undani zaidi anaweza
akagundua mambo mengine ambayo hatakiwikuyafahamu.Mdogo wake
Vicky anadai kwamba Elvis yupo hai
na ndiye aliyewateka yeye na dada
yake.Vicky yeye anadai kwamba
hakuna jambo kama hilo na David
naye anathibitisha kuwa Elvis
amefariki.Nani kati yao anasema
kweli?akawaza na kuvuta mkupuo
mkubwa wa sigara
"Kuna mtu mmoja tu ambaye
anaweza akatuthibitshia kuwa Elvis
amekufa au vipi naye ni mkurugenzi
wa idara ya ujasusi.Kwa mujibu wa
David huyu ndiye aliyepewa jukumu la
kuhakikisha Elvis anakufa na ndiye
aliyemthibitishia makamu wa rais
kuwa Elvis amekufa.Huyu lazima
apatikane leo hii.Vile vile kuna
ulazima wa kumuhoji tena Vicky naa
kufahamu kuhusiana na hao watu
waliokuwa wamemteka ni akina
nani.Jambo lingine ambalo limenistua ni baada ya nyaraka kuibwa ofisini
kwa Frank.Watu hawa wakiachiwa
watapiga hatua kubwa sana na
kuvuruga kila kitu kinachoendelea
hivi sasa." akawaza Elizabeth
**********************
Kichwa cha David kilijaa mawazo
mengi sana baada ya kutoka
nyumbani kwa Elizabeth
"Kwa nini madam Elizabeth
anadhani Elvis hajafariki dunia? Frank
kaitoa wapi taarifa hiyo kuwa Elvis
yuko hai?Huu si ukweli hata kidogo
kwani Elvis tayari amekufa na
kuzikwa.Makamu wa rais hawezi
kunieleza kitu ambacho hana uhakika
nacho.Hata hivyo ngoja nifanye
uhakiki kama anavyotaka madam" akawaza David na kuchukua simu
akampigia makamuwa rais Dr Shafi
"Samahani kwa kukusumbua
tena Dr Shafi"akasema David baada ya
Dr Shafi kupokea simu
"Bila samahani David.karibu"
akasema Dr Shafi
"Ahsanate sana.Dr Shafi kuna
taarifa ambayo nimeipata imenistua
kidogo na ndiyo maana nimelazimika
kukupigia simu."
"Ndiyo David" akasema Dr Shafi
"Kuna taarifa za kustusha kidogo
zinadai kwamba Elvis ameonekana
akiwa hai"
"Elvis?!! Dr Shafi akastuka sana
"Ndiyo Dr Shafi"
"Taarifa hizo zimetoka
wapi?Kaonekana wapi na lini?
"Kuna mtu ambaye ametoa
taarifa hizo kwa mmoja wa washirika
wangu kuwa Elvis yuko hai" Thats not true.Elvis amekwisha
fariki dunia na hayupo tena
duniani.Mimi mwenyewe nilihudhuria
mazishi yake na nilikuwa miongoni
mwa watu wachache waliofanikia
kumuona Elvis akiwa ndani ya jeneza
iweje leo aonekane akiwa hai?Hilo
haliwezi kutokea David labda huyo
aliyetoa taarifa hizo ameona mzimu au
mtu aliyefanana na Elvis lakini si Elvis
halisi.He's dead"akasema Dr Shafi na
David akavuta poumzi ndefu
"Dr Shafi utanisamehe kwa hili si
kwamba sikuamini lakini unaonaje
endapo tutafanya uchunguzi ili
kujiridhisha na taarifa hizi kuwa si za
kweli?akauliza David
"Unataka tufanyaje
David?Tufukue kaburi?
"Hapana sijamaanisha tufukue
kaburi bali tumpate mtu aliyepewa
jukumu hilo la kumuua Elvis na atuthibitishie kuwa kweli Elvis
amekufa.Mimi na wewe hatuna wasi
wasi kuhusu suala hili lakini
wenzangu katika umoja wetu wana
wasiwasi sana na wanataka
uthibitisho kuwa Elvis
amekufa.Tukimpata huyu
aliyethibitisha kifo cha Elvis
atatusaidia kuondoa mkanganyiko
huu."
"Niliyemkabidhi jukumu la
kumuua Elvis ni Meshack Jumbo na
ndiye aliyenithibitishia kuwa Elvis
amekufa na akanitumia hadi picha za
maiti yake.Kwa hiyo unataka tumpate
Meshack Jumbo?
"Ndiyo Dr Shafi.Tunapaswa
kumpata na ili athibitishe kuwa kweli
Elvis amekufa"
"Hili sasa ni suala lingine.Huyu ni
kiongozi mkuu wa idara ya ujasusi na
kumpata kwake si kazi nyepesi hata hivyo niachie jambo hili nione namna
nitakavyofanya.Nitawatuma vijana
kumteka ili isijulikane kuwa ni sisi na
kisha atapelekwa mahala pa siri na
huko atahojiwa kuhusianana kifo cha
Elvis.Kama hatutaupata ukweli basi
itatulazimu kufukua kaburi la Elvis na
kujiridhisha kama kweli
amekufa.Nitawaandaa vijana kuifanya
kazi hiyo na pale watakapokuwa
tayati nitakujulisha"
"Ahsante sana Dr Shafi.Bado
ninaendelea kufuatilia hali ya mambo
na nitaendelea kukujulisha kila
kinachoendelea huku" akasema David
na kukata simu
Dr Shafi alipomaliza kuzungumza
na David simuni akaegemea kiti chake
akionekana kuwa na mawazo mengi
"Hili jambo limeanza kuchukua
sura mpya.Kwa nini wameanza kuhisi
kuwa Elvis hajafa?Kaonekana wapi? Sidhani kama suala hili linaweza kuwa
limeibuka tu hewani lazima lina
msingi wake na halitakiwi kupuuzwa
kwani katika dunia ya sasa lolote
linawezekana.Atakapopatikana
Meshack Jumbo ataeleza ukweli wote"
akawaza Dr Shafi
*****************
Juliana aliwasili mahala
alikopanga kukutana na
Steve.Akampigia simu na kumbe
tayari Steve alikwisha wasili muda
mchache uliopita akamuelekza mahala
alipo Juliana akamfuata
"Karibu Juliana" akasema Steve
ambaye alikuwa ameongozana na
Omola
"Habari yako dada" akasema
Juliana akimsalimu Omola Huyu anaitwa Omola ni
mwenzetu anatoka nje ya nchi bado
hafahamu kiswahili" akasema Steve
"Omola huyu ni Juliana ambaye
tumekuja kuonana naye" akasema
Steve akianza kutumia lugha ya
kiingereza ili Omola aweze kuelewa
"Juliana,nafurahi kukufahamu"
"Hata mimi nimefurahi kukutana
nawe Omola.Karibu sana Tanzania"
akasema Juliana
"Juliana awali ya yote nikuombe
samahani kwa usumbufu huu mkubwa
tunaoendelea kukupatia"akasema
Steve
"Usijali Steve hakuna
usumbufu.Muda wowote ule mkihitaji
msaada wangu niko tayari
kuwasaidia"
"Ahsante sana.Kabla
hatujakueleza kilichotuleta hapa
nataka kufahamu umefikia wapi kuhusiana na ile kazi tuliyokuomba
utusaidie?
"Baada ya kufika nyumbani
nimewasiliana na yule mtu
niliyekueleza na akakubali
kunisaidia.Kama nilivyokueleza huyu
jamaa ni mtu wa karibu sana na mama
na anazifahamu siri zake
nyingi.Amenieleza kwamba mama
anatumia majina mbali mbali katika
shughuli zake.Hata yeye mwenyewe
halifahamu jina lake halisi kwani
mama ana vyeti vya kuzaliwa zaidi ya
vitano vyenye majina tofauti na
vimetolewa katika nchi tofauti
tofauti.Jina Shanon Blank ni moja ya
majina yake anayoyatumia katika
mambo yake ya biashara nchini
marekani.Kila nchi anakowekeza
hutumia jina tofauti.Hata pasi za
kusafiria anazo zaidi ya kumi za nchi mbali mbali.Hilo ndlio nililofanikiwa
kulipata"
"Ahsante sana Juliana huo ni
msaada mkubwa umetupa.Kama
ulivyohisi ni kweli mama yako
anajihusisha na mitandao ya kihalifu
na ndiyo maana anatumia majina
tofauti ili isiwe rahisi
kujulikana.Tumewahi kumtafuta kwa
jina lake la Elizabeth lakini
hatukufanikiwa kwani hakuna rekodi
zozote za jina hilo.Majibu haya
yametupa mwanga mkubwa na
tutayafanyia kazi"akasema Steve
"Tukiachana na hilo kuna lingine
ambalo nataka nikujulishe.Baada ya
kuachana muda ule
tulipokutana,tuligundua kwamba
kuna mtu anakufuatilia na ndiyo
maana nikawa ninakupa
maelekezo.Tulifanikiwa kumpata mtu
huyo na akakiri kweli ametumwa na mama yako akufuatilie.Katika simu
yake tulimkuta ana picha yako ukiwa
na Meshack Jumbo na Patricia.Aliipiga
picha hiyo na kumtumia mama
yako.Nimeona nikueleze jambo hili ili
uwe makini sana kwani tayari mama
yako ameanza kukutilia mashaka
nyendo zako"
"Dah ! nimestuka sana.Sikujua
kama mama ameanza
kunifuatlia.Nitajitahidi sana kuwa
makini kuanzia sasa.Huyo jamaa
aliyetumwa kunifuatilia yuko wapi?
'Tulimuacha aende zake lakini
alichokipata hatathubutu tena
kukufuatilia"
"Ahsanteni sana"
"Kubwa ambalo tumekuitia hapa
tunahitaji tena msaada wako"
"Hakuna tatizo nielezeni
mnahitaji nini na mimi nitawasaidia" Nadhani sijakueleza lakini mimi
na wenzangu tunachunguza mtandao
wa watu wanaofanya biashara
haramu ya silaha na waasi
wanaopigana na serikali ya
Congo.Kwa muda mrefu kumekuwa
kunaibuka vikundi vya waasi
vikipambana na serikali ya Congo na
maisha ya watu wengi yamepotea na
wengine kukimbia nchi yao na
kwenda kuishi nchi za ugenini kama
wakimbizi.Watu wanaofanya biashara
hii wapo hapa nchini na ni mtandao
mrefu unaohusisha watu matajiri na
wengine ni viongozi katika serikali ya
Tanzania na Congo.Katika uchunguzi
wetu tumebaini kwamba Shanon
Blank ambaye ni mama yako ndiye
kinara katika biashara hii ya silaha"
"Jesus Christ!!! akasema Juliana
kwa mshangao mkubwa Nilijua mama anajihusisha na
mambo haramu lakini sikuwahi kuhisi
kama anaweza akajihusisha katika
biashara kama hii" akasema Juliana
"Shanon Blank..." Steve
akaendelea
"Anashirikiana na Joe Gregory
ambaye ulitueleza ndiye mshirika
wake mkuu wa biashara nchini
Marekani.Huyu Joe ni tajiri sana
anamiliki biashara kadhaa kubwa na
ana kiwanda cha kutengeneza
bunduki kubwa na ndogo na silaha
nyingine.Kwa kutumia kampuni ya
McLorien inayomilikiwa na mama
yako hutuma silaha ambazo huja kama
bidhaa za nguo na viatu na hutumwa
katika kampuni ya Pendeza ambayo
inamilikiwa na mtu mmoja anaitwa
brigedia Frank na huyu ndiye
anayefanya harakati zote za
kuhakikisha mzigo unafika nchini Congo kwa waasi.Tumefanikiwa
kupata mawasiliano kati ya Shanon na
mtu mmoja anaitwa Patrice Lwibombe
ambaye tunaamini ana mahusiano na
waasi kwani katika mawasiliano hayo
tuliyoyanasa Shanon anamtaka Patrice
kuharakisha malipo ya mzigo
walioupokea ambao tunaamini ni
silaha,Patrice akamjibu kwamba
wamechelewa kufanya makusanyo
kutokana na mapambano kuwa makali
baina ya vikosi vyao na vile vya
serikali vikisaidiwa na vile vya umoja
wa Afrika.Huyu ndiye ambaye
tunamsaka tumjue ni nani na yuko
wapi na vile vile mahusiano yake na
waasi" akasema Steve na kunyamaza
akamtazama Juliana
"Siamini eti kwa sababu ya pesa
mama ameamua kujiingiza katika
biashara kama hii.Huu ni uuaji kwani
silaha wanazowauzia hao waasi ndizo zinatumika kuua watu wasio na hatia"
akasema Juliana na kwa mbali macho
yake yakaonekana kulengwa machozi
"Juliana tunataka kuusafisha
mtandao huu na kuimaliza kabisa hii
biashara hivyo tunahitaji msaada
wako"
"Niambie chochote mnachohitaji
na mimi nitakifanya.Nimepata hasira
sana kwa haya anayoyafanya
mama.Ninaona aibu hata kuzaliwa
katika familia kama hii.Niambie
tafadhali mnataka nifanye nini?
"Tunataka kumfahamu Patrice
Lwibombe ni nani na yuko wapi.
Tutaweza kulifanikisha hilo endapo
tutafanikiwa kuipata kompyuta au
simu ya mama yako.Nina imani lazima
mama yako anawasiliana na Patrice
kwa simu au kwa barua pepe hivyo
tukiweza kupata kimojawapo kati ya
simu yake ya mkononi au kompyuta anayotumia tutaweza kupata mambo
mengi yanayohusiana na mtandao
huu na hata kuwafahamu wengine
ambao hatujawagundua bado.Can you
do that for us? akauliza Steve.Juliana
akainamisha kichwa kwa muda
akatafakari halafu akasema
"Chumbani kwa mama si rahisi
kuingia lakini siwezi kushindwa
nitatafuta namna ya kufanya hadi
niweze kufanikiwa kupata kimoja
wapo.Mama ana simu zaidi ya tatu ila
kompyuta mpakato anazo
mbili.Nitajitahidi niweze kupata hivyo
vyote ili muweze kuvifanyia
uchunguzi"
"JItahidi kuipata simu yake
anayotumia sasa na ukishaipata
unipigie nitakupa maelekezo namna
ya kufanya.Tutaingiza programu
fulani katika simu hiyo na
itaunganishwa katika hii kompyuta yangu na tutakuwa na uwezo wa
kusikia mazungumzo yake yo.." Omola
akanyamaza baada ya mlio fulani
kutokea katika kompyuta
yake.Akamtaka Steve asogee karibu
"Nimepata tena mazungumzo
mengine ya makamu wa rais
yaliyorekodiwa kwa muda wa nusu
saa iliyopita.Tafadhali sikiliza halafu
utanieleza amesema nini" akasema
Omola na kuanza kucheza rekodi
zile.Yalikuwa ni mazungumzo ya
makamu wa rais akizungumza na
watu mbali mbali kupitia simu yake
.Mara sura ya Steve ikabadilika baada
ya kusikia rekodi mbili za mwisho
"Kuna nini Steve mbona
umestuka? akauliza Omola.Steve
akamuelezea kila kitu kuhusiana na
mazungumzo yale ya makamu wa rais
na David Mpigie simu Elvis mueleze kila
kitu ili hatua za haraka zichukuliwe
kumuokoa Meshack" akasema Omola
"Steve subiri kidogo.Mimi pia
nimesikiliza hicho ulichokuwa
unakisikiliza na nimestuka kusikia
habari za Elvis.Ni Elvis yupi
anayezungumziwa?akauliza
Juliana.Steve na Omola wakatazamana
"Oh my God ! akasema Steve kwa
sauti ndogo
"Tafadhali nieleze Steve ni Elvis
yupi anayezungumziwa?Ni Elvis yupi
ambaye alikufa lakini ameonekana
akiwa hai? akauliza Juliana
"Tumefanya nini?Juliana
hakutakiwa kabisa kusikia au
kufahamu jambo lolote kuhusiana na
Elvis.We've done a huge
mistake.Tumejisahau na
tukazungumza mambo haya mbele
yake wakati tukifahamu kabisa huyu ni mtu wa karibu na Patricia.What am
I going to do?akawaza Steve
"Steve mbona hunijibu?Hawa
ambao wamesikika wakizungumza ni
akina nani?Kwa nini
wanamzungumzia Elvis?Ni Elvis yupi
anazungumzia?Nieleze ukweli
tafadhali bila kunificha" akasema
Juliana
"Steve muda unakwenda na
tukiendelea kuchelewa hapa
tutasababisha Meshack aingie katika
hatari kwani hajui chochote
kinachoendelea dhidi yake.Mjibu
Juliana swali lake tuondoke"
"Nijibu Steve" akasema Juliana
"Sawa Juliana sina namna hivyo
lazima nikueleze ukweli kwani wewe
kwa sasa ni mwenzetu na sioni sababu
ya kukuficha kitu.Hawa uliowasikia
wakizungumza ni makamu wa rais na
waziri mkuu mstaafu David Sichoma.Tumegundua kwamba
makamu wa rais ana mahusiano na
mtandao wa akina Frank wa kuuza
silaha lakini bado tunaendelea
kumchunguza na ndiyo kazi
anayoifanya Omola.Kuna programu
ameitega katika simu ya makamu wa
rais ambayo hurekodi mazungumzo
yote na kutupa taarifa kila baada ya
nusu saa.Kwa upande wa David huyu
tumegundua kwamba anashirikiana
na wanasiasa wa vyama vya upinzani
katika kuandaa mkutano wa hadhara
utakaofanyika leo mkutano ambao
umepigwa marufuku na jeshi la polisi
lakini wao wanadai kwamba mkutano
huo utafanyika kama
ulivyopangwa.David tumeanza
kumchunguza tufahamu nini dhamira
yake ya kuungana na wanasiasa
ingawa tayari tunazo taarifa kuwa ana mipango ya kuwania urais nadhani
katika uchaguzi ujao"
"Subiri kidogo Steve,kuna jambo
umelifungua kichwani kwangu"
akasema Juliana
"David waziri mkuu mstaafu ni
rafiki wa mama na jana nilimkuta
nyumbani mama akanitambulisha
kwake.Baada ya kuondoka mama
akaniambia kwamba David alikuja
pale kwa maongezi na akadai kwamba
katika mazungumzo yao David
alimwambia anataka kuchukua nafasi
ya urais na akamuahidi kwamba
endapo akipata urais mimi ataniteua
kuwa waziri wa maliasili na utalii"
"Kweli?! akauliza Steve
"Kweli kabisa Steve.David na
mama ni marafiki.Sikuwa nalifahamu
hilo hadi jana nilipomkuta nyumbani"
"Juliana kama nilivyokueleza
awali kwamba mtandao huu wa mama yako unahusisha watu wakubwa.Nina
imani urafiki wao si wa bure kuna
jambo linaendelea kati yao na kwa
kuwa tumeanza kumchunguza David
tutafahamu kila kitu anachokifanya"
"Naomba sasa kufahamu kuhusu
Elvis aliyekuwa anazungumziwa na
makamu wa rais na David"akasema
Juliana na zikapita sekunde kadhaa
Steve akitafakari halafu akasema
"Sina ujanja Juliana lazima
nikueleze ukweli.Elvis
anayezungumziwa hapa ni mume wa
Patricia"
"What?!!..Are you serious?
akauliza Juliana kwa mshangao
"Juliana Elvis mume wa Patricia
hajafa yuko hai"
Juliana akapatwa na mshangao
mkubwa akasimama na kumtazama
Steve kwa macho makali Steve ninakuheshimu sana
lakini naomba usinitanie namna
hiyo"akasema Juliana na Steve
akamuomba aketi
"Elvis aligundua kuwepo kwa
biashara ya silaha kupitia kwa Graca
mtoto wa Frank.Walipofahamu kuwa
tayari wamegundulika wakataka Elvis
auawe hivyo wakamtumia makamu
wa rais ambaye naye alimuachia
jukumu hilo Meshack na hapo ndipo
ulipochezwa mchezo wa Elvis
kughushi kifo chake na watu wote
wakaamini kwamba amekufa.Alifanya
hivi ili akina Frank waendelee na
biashara zao bila hofu na yeye apate
nafasi nzuri ya kuwatafuta na
hatimaye kuufutilia mbali mtandao
huu.Kwa bahati mbaya tayari
wameanza kuwa na wasiwasi kwamba
yawezekana Elvis hajafa na hii
imetokana na hatua kubwa ambayo imekwisha pigwa katika
kuwachunguza hawa jamaa ndani ya
kipindi kifupi.Kwa hiyo Juliana huo
ndio ukweli halisi,Elvis hajafa na
anaendelea na mapambano
kuhakikisha kwamba anaufagia
mtandao wote wa akina Frank.Hii ni
siri kubwa na tunaofahamu ni sisi
watu wachache.Nimekwambia wewe
kwa sababu ni mwenzetu na umejitoa
kupambana pamoja nasi hivyo
hatuwezi kukuficha kitu"
"Dah ! haya ni maajabu ya
Musa.Patricia anafahamu chochote
kuhusu jambo hili?
"Hapana Patricia hafahamu
chochote.Juliana muda unakwenda
tutazungumza zaidi tukipata nafasi
tunakuomba uyafanyie kazi hayo
tuliyokueleza na ukifanikiwa
tuwasiliane mara moja.Onyo ninakupa
hapaswimtu yeyote kufahamu kuhusu suala ili la Elvis kuwa hai hasa
Patricia" akasema Steve wakaagana
"Wamefahamuje kama Elvis yuko
hai? akauliza Omola
"Hata mimi ninashangaa kwa
sababu hii ni siri kubwa ambayo
tunaoifahamu ni sisi wachache.Sijui
wamefahamu vipi.Ngoja nimpigie
Elvis nimfahamishe tulichokipata"
akasema Steve na kupunguza mwendo
wa gari akampigia Elvis simu
"Elvis mambo yameharibika"
"Kuna nini Steve? Mmeonana na
Juliana?akauliza Elvis
"Wameanza kuwa na wasi wasi
kwamba haujafa"
"Tayari ninafahamu jambo hilo"
"Unafahamu?Umefahamuje?akau
liza Steve
"Ni Winnie ndiye aliyewaeleza
akina Frank kuwa niko hai.Ninyi
mmefahamuje? Tumenasa mazungumzo ya
makamu wa rais na David muda mfupi
uliopita.David anamueleza makamu
wa rais kwamba wafanye uchunguzi
kuthibitisha kifo chako kwani
umeonekana ukiwa hai na
wamekubaliana kwamba wamteke
Meshack Jumbo wamuhoji ili aseme
ukweli.Elvis tufanye haraka sana
kumuokoa mkurugenzi yuko katika
hatari kubwa"
"Oh my God !! mko wapi sasa
hivi?
"Tumeachana na Juliana muda si
mrefu na tumeanza safari ya kurejea
nyumbani"akajibu Steve
"Endelea na safari mimi ngoja
niwasiliane na mkurugenzi halafu
nitakujulisha nini tufanye" akasema
Elvis na kukata simu na haraka haraka
akampigia Meshack Jumbo.Simu ikaita na kukatika bila kupokelewa.Akapiga
tena
"C'mon Jumbo pokea simu"
akasema Elvis kwa sauti ndogo huku
mapigo ya moyo yakimwenda kasi
aliingiwa na woga mwingi kuhusu
maisha ya Meshack.Mara simu
ikapokelewa na Elvis akashusha
pumzi
"Hallo" ikasema sauti ya Meshack
Jumbo
"Mzee uko wapi?
"Nimetembelewa na wageni
wanatoka afrika kusini niko nao hapa
Venus hotel ambako tunapata chakula
cha mchana"
"Mzee nakuomba uondoke hapo
haraka sana.Hauko salama" akasema
Elvis
"Elvis usihofu kuhusu mimi.Hapa
kuna usalama wa kutosha na isitoshe tunao walinzi wetu wanaotulinda.Vipi
huko mnaendeleaje?
"Mzee Jumbo huu si utani
nakuomba tafadhali ondoka hapo sasa
hivi si salama kwako kwa sasa"
"Kwa nini unasema
hivyo?akauliza Meshack na mara
akaingia ujumbe katika simu yake.
"Elvis I'll get back to you"
akasema Meshack
"Mzee list......" akasema Elvis
lakini tayari simu ilikwisha katwa.
Meshack akaufungua na kuusoma
ujumbe ule
"Hotel Yvona room 83...Be there
before 2.00 pm.It's important
Mbutolwe
"Huyu binti ana tatizo gani hadi
asisitize nikaonane naye kabla ya
muda huo .Kuna taarifa anazo za
muhimu?akajiuliza Meshack Yawezekana kuna taarifa za
muhimu sana amezipata kwani
alikuwa kiongozi wa timu niliyoiunda
kuchunguza kifo cha mke wa waziri
wa zamani wa ulinzi wa Rwanda
aliyeuawa katika hoteli moja hapa
Tanzania.Inawezekana kuna taarifa
nyeti amezipata na anataka
kunishirikisha na ndiyo maana
amenitumia ujumbe hu.."Mara simu ya
Meshack ikaita alikuwa ni Mbutolwe
"Hallo" akasema Meshack
"Mzee natumai umeupata
ujumbe wangu"akasema Mbutolwe
"Nimeupata"
"Naomba tekeleza ujumbe
unavyotaka" akasema Mbutolwe na
kukata simu
"Lazima kuna jambo la muhimu
sana ananiitia ngoja nikamtazame"
akawaza Meshack akirejea ukumbi wa
chakula ambako wageni wake walikuwa wanaendelea kupata
chakula.Elvis aliendelea kupiga simu
mfululizo lakini Meshack
hakupokea.Alipoona mkurugenzi
hapokei simu yake akampigia Steve
"Steve nimempigia simu
mkurugenzi kumuonya kuwa yuko
katika hatari lakini hanielewi
nimeendelea kumpigia simu hapokei
tena.Something is wrong we need to
hurry" akasema Elvis
"Amekueleza yuko wapi?
"Yuko Venus hotel,ile iko karibu
na Mawingu tower.Steve elekeeni
hapo haraka sana mimi nami ninakuja
sasa hivi nitawakuta hapo" akasema
Elvis na kuingia haraka chumbani
kwake na kwa haraka akabadili
mwonekano wake kwa kuweka ndevu
bandia akavaa kofia na kuchukua
silaha zake akaziweka katika mkoba
mdogo na kumuaga Graca kisha akatoka na kutembea kwa kasi
akielekea katika hoteli moja iliyoko
umbali wa kama dakika kumi
hivi.Alitembea haraka haraka na kuna
wakati alikuwa anakimbia hadi
alipofika katika hoteli ile ambako
kulikuwa na taksi kadhaa akaingia
katika mojawapo ya taksi na kumtaka
dereva ampeleke Venus hotel
Meshack Jumbo alimaliza
kupata chakula na wageni wake
akawaomba radhi kuwa amepata
dharura ikabidi waagane kwani
wageni wale walikuwa na safari ya
kuelekea Arusha jioni ya siku
ile.Baada ya kuagana nao akaondoka
hadi katika gari lake na kumtaka
dereva wake ampeleke Yvona hotel.
Akiwa garini akakumbuka Elvis
alimpigia simu na kumtaka aondoke
pale hotelini haraka kwani yuko
katika hatari Elvis alikuwa anamaanisha nini
aliponitaka niondoke haraka pale
hotelini niko katika hatari?Is
something going on?akajiuliza halafu
akachukua simu na kumpigia Elvis
"Mzee uko wapi?
"Nimekwisha ondoka pale Venus
hotel kwa sasa ninaelekea Yvona hotel
Mbutolwe ameniita pale kuna jambo
anataka kunieleza.Kuna nini
kinaendelea nakumbuka kuna jambo
ulinieleza lakini sikukuelewa"
"Una hakika umeitwa na
Mbutolwe?
"Ndiyo.Kuna kazi nilimpa na
kuna jambo anataka kunieleza hivyo
ninakwenda kuonana naye Yvona
hotel nikitoka hapo nitakupigia
unielekeze mahala mlikohamia nije
niwatembelee na kujua
mnaendeleaje"akasema Meshack na Elvis akawa kimya hakusema
chochote kwa sekunde kadhaa
"Elvis" akaita Meshack
"Mbutolwe anafanya nini hapo
hotelini?akauliza Elvis
"Sijafahamu bado anafanya nini
lakini amenitumia ujumbe na kunitaka
nikaonane naye hapo.Amenielekeza
nimkute chumba namba 83"
"Sawa mzee ukitoka hapo
unijulishe ili nikuelekeze mahala
tunakoishi hivi sasa"akasema Elvis
"Kuna jambo ulinieleza
uliponipigia simu lakini
hukunifafanulia,ni jambo gani
hilo?Kuna hatari gani?
"Usijali mzee tutazungumza
utakapokuja hapa" akasema Elvis na
kukata simu
"Simuelewi Elvis alikuwa
anamaanisha nini aliposema kuwa
niko katika hatari ?Mbona hajanifafanulia ni hatari ipi hiyo
iliyokuwa inanikabili? akajiuliza
Meshack Jumbo
Mara tu alipokata simu Elvis
akampigia simu Steve
"Steve, mzee amekwisha ondoka
Venus hotel,anaelekea hotel Yvona
anakwenda kuonana na
Mbutolwe.Tuelekee huko.Mko wapi
hivi sasa?
"Tupo barabara ya Umoja na
tumefika hapa katika ubalozi wa
Urusi"
"Good.Ingia bara bara ya Sambaa
halafu nisubirini pale karibu na kanisa
la Mashahidi wa Yehova.Ninakuja na
taksi" akasema Elvis na kumtaka
dereva aongeze mwendo
Dereva wa ile taksi alikuwa
mzoefu sana wa barabara za jiji la Dar
hivyo haikuchukua muda mrefu
wakawasili mahala Elvis alikopanga
Sent using
Jamii Forums mobile app