I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 70
Dr Makwa Tusangira kiongozi
mkuu wa chama kikuu cha upinzani
nchini Tanzania aliingiia katika
chumba cha maongezi alimokuwamo
waziri mkuu mstaafu David
Sichoma,akajimimnia mvinyo katika
glasi akagugumia wote akamtazama
David na kusema
"David nakuona una wasi wasi
sana.Usihofu ndugu yangu jambo hili
litafanikiwa .Tumejipanga vizuri na
hata sasa nimetoka kuzungumza na
wenzangu kila kitu kiko vizuri na ni
wakati wa kuondoka kwenda kuanza
harakati kwani muda umefika"
"Dr Makwa sina wasiwasi nawe
hata kidogo ninaamini kila kitu
kitakwenda kama tulivyotarajia.Kuna chochote kingine utahitaji kabla
hujaondoka?
"Kila kitu kiko sawa endapo kuna
chochote nitakihitaji kwa dharura
nitakujulisha" akasema Dr Makwa
huku akiongeza tena mvinyo katika
glasi na kunywa funda kubwa
"This is it David.Ukombozi
unaanza.Wish me lucky" akasema Dr
Makwa na kumkumbatia David
wakaagana.Dr Makwa akaingia katika
gari maalum aliloandaliwa na David
huku akisindikizwa na magari mawili
ya walinzi aliopewa na David
akaondoka katika makazi yale ya
waziri mkuu mstaafu na kwenda
kuungana na wenzake katika mkutano
wa hadhara waliopanga kuufanya
katika viwanja vya jamhuri.
Toka ilipotimu saa nane za
mchana tayari watu walianza
kujitokeza katika viwanja vya jamhuri kwa ajili ya kuitikia wito wa viongozi
wao kuja kuhudhuria mkutano
mkubwa waliouitisha.Polisi
walikuwepo eneo la tukio ili kuwazuia
watu kukusanyika lakini kadiri muda
ulivyozidi kusonga ndivyo idadi ya
watu ilivyozidi kuongezeka na kuwapa
wakati mgumu polisi
kuwatawanya.Maelekezo yakatolewa
na viongozi wakuu wa jeshi la polisi
kwamba wasiwafanye chochote
wananchi hao waliokusanyika bali
wawasubiri viongozi wao walioitisha
mkutano ule bila kibali wawatie
nguvuni.Hadi ilipotimu saa kumi
tayari viwanja vya jamhuri vilikuwa
vimefurika watu.Kulikuwa na shamra
shamra nyingi na watu wakiendelea
kuimba nyimbo za hamasa
wakiwasubiri viongozi wao.Saa kumi
na nusu mmoja wa wahasishaji
akapanda juu ya gari lililotengezwa mfano wa jukwaa akashika kipaza
sauti na kutoa salamu ya hamasa kisha
kusema
"Ndugu zangu kutokana na ulinzi
uliopo hapa viwanjani viongozi wetu
hawataweza kufika hapa kwani
wanasubiriwa wakamatwe na jeshi la
polisi hivyo tumeelekezwa kwamba
tuanze maandamano kuelekea katika
ofisi zetu za chama na huko
tutawakuta viongozi wetu
wanatusubiri.Mpo tayari?
"Ndiyoooooooooooo!!!!! ikapigwa
kelele kubwa
"Mpo tayariiiiiiiiiiii...!!!!akauliza
tena
"Ndiyooooooooooooooo!!!
wakajibu wanachama
"Ahsanteni sana.Ninawasihi
msiogope chochote tunaandamana
kwa amani bila kufanya vurugu
kuelekea katika makao makuu ya chama.Tanzania ni nchi huru hivyo ni
haki yetu kuandamana na kufanya
mikutano yetu ya siasa.Ukombozi
unaanza leo ndugu zangu.Narudia
tena kuwasihi msiogope bali twendeni
kwa amani tukiimba hadi katika ofisi
za chama tukakutane na vongozi
wetu" akasema yule muhamasishaji na
kumalizia kwa salamu ya hamasa
kubwa na kisha kuyaanzisha
maandamano kuelekea katika ofisi za
chama chao
Yalikuwa ni maandamano
makubwa kutokana na uwingi wa
watu waliokuwa wamehudhuria
katika viwanja vya jamhuri na hivyo
ililazimika shughuli mbali mbali
kusimama barabarani ili
waandamanaji waweze kupita na hii
ilisababisha usumbufu mkubwa hasa
kwa wasafiri ambao walikuwa
wanarejea majumbani kwao jioni hii.Maandamano yalianza kwa amani
wakipita barabara ya mzee Juma kisha
wakaingia barabara ya Arusha na
huku kote walikopita ililazimu magari
na shughuli nyingine kusimama kwa
muda.Maandamano yalipofika katika
maungio ya barabara ya Mbuni na
Mbuyuni yakakutana na kikosi cha
polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa
wamejipanga kuwazuia wafuasi wale
wasiendelee na maandamano yao.
Jeshi la polisi lilifuata taratibu
zake za kuwataka waandamanji wale
watawanyike kwani maandamano
yale hayakuwa halali lakini
waandamanaji waliendelea kuimba
huku wakitoa maneno ya kejeli kwa
jeshi la polisi na hata wengine kuanza
kuwarushia mawe.Licha ya
waandamanaji kugoma kutawanyika
bado jeshi la polisi likaendelea
kutumia busara na kuwataka watawanyike kwa amani lakini bado
waandamanaji waliendelea kugoma
na ndipo polisi walioanza
kuwatawanya kwa kutumia gesi za
machozi.Waandamanaji walifahamu
kinachoweza kutokea hivyo wakawa
wamejiandaa kwa chupa za maji kwa
ajili ya kunawa usoni na hapo ndipo
vurugu kubwa zikaanza.Matairi
yakakusanywa na kuchomwa hivyo
kulianya eneo hili lenye maduka
makubwa makubwa kutanda moshi
mzito mweusi.Mapambano kati ya
polisi na waandamanaji yakaendelea
na ghafla polisi watatu wakaanguka na
kufa papo hapo na mara moja
wakagundua kwamba polisi wale
walikuwa wamepigwa risasi ndipo
amri ikatolewa kwamba polisi
wajihami kwa risasi za mpira kwani
miongoni mwa waandamanaji
walikuwepo pia wenye silaha za moto.Polisi wakapiga juu risasi za
baridi ili kuwaogpesha waandamanaji
lakini hawakuogopa na badala yake
polisi wengine wanne wakaanguka na
kufa kwa kupigwa risasi na hapo
ndipo walipolazimika kuanza kutumia
risasi za moto.
Katika makao makuu ya chama
alikuwapo Dr Makwa na wenzake
wakataarifiwa kwamba mambo tayari
yameharibika hivyo kwa haraka
wakatawanyika kwenda mafichoni
kila mmoja alipoajua yeye.Dr Makwa
akarejea nyumbani kwa David
"Tayari mambo yameanza na
nimetaarifiwa mpaka sasa zaidi ya
polisi kumi wamekwisha fariki dunia
na waandamanaji wengi wanaonekana
chini wakiwa wamekufa kufuatia
kupigwa risasi na polisi.Kwa sasa
ninaanza kuwahamasisha na watu wa
mikoani pia wajiandae kwani vugu vugu hili halitaishia tu Dar es salaam
bali litasambaa nchi nzima" akasema
Dr Makwa
"Kazi nzuri sana Dr
Makwa.Usihofu kuhusu usalama
wako.Hapa uko salama na endelea
kufanya kazi zako kwa uhuru ukiwa
hapa.Nataka kesho asubuhi mikoa
yote ile mikubwa iwake moto.Kote
maandamano yaanze"
"Usijali David kila kitu
kitakwenda vyema kwani tumejipanga
vizuri.Kitu cha msingi ni fedha zote
tunazozihiaji ziwepo tayari kwani
moto huu hautazimika hadi
tutakapoingia ikulu"
"Kuhusu Fedha usiwe na shaka
hata kidogo kwani zipo za
kutosha.Ngoja nishughulikie suala
hilo" akasema David na kutoka
akaelekea chumbani Safari ya kuelekea ikulu imeanza
na kwa mbali tayari nimeanza kuinusa
harufu ya jengo lile zuri.Siku si nyingi
sana toka sasa nitatangazwa rais
mpya wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Wale wabaya wangu wote
labda waote mabawa wapae
watoweke kabisa katika ulimwengu
huu kwani hakuna atakayebaki
salama.Nitahakikisha wote
ninawafyeka.Wale wote
walionihujumu kisiasa wakati wao wa
kuishi maisha magumu
umewadia.Siku zao zinahesabika"
akawaza David huku akitabasamu
akazitafuta namba za Frank akampigia
lakini simu haikupolewa,akapiga tena
bado simu haikupokelewa
"Nitampigia tena baadae.Ngoja
niwasiliane na Dr Shafi nimjulishe
kinachoendelea"akawaza David na
kumpigia simu Dr Shafi Hallo David..Mambo naona
yameanza.Nimepokea simu muda si
mrefu rais ananitaka katika kikao cha
dharura kufuatia kinachoendelea
huko mtaani hivi sasa.Una taarifa
zozote?
"Ninazo taarifa za kila
kinachoendelea huko mtaani.Mambo
yameanza vyema na yamekwenda
kama vile tulivyokuwa
tunataka.Mpaka sasa taarifa
tulizonazo ni kwamba polisi zaidi ya
kumi wamekwisha uawa na hii
imefanyika ili kuwalazimisha polisi
watumie nguvu kubwa kuwatawanya
waandamanaji .Hili limefanikiwa
kwani hadi sasa miili ya watu kadhaa
inaonekana ikiwa imezagaa
barabarani na tunategemea vurugu
hizi kuendelea usiku kucha kwani
timu ya uhamasishaji inafanya kazi
nzuri na vijana wanaendelea kuhamasiswa wasirudi nyuma bali
waendelee kupambana na polisi"
"Mwanzo mzuri David.Vipi
kuhusu akina Dr Makwana
wenzake,wako salama?
"Wote wako salama kabisa na
kila mmoja yuko mafichoni.DrMakwa
ninaye hapa na yuko salama kabisa
anaendelea na kazi zake akiwa
hapa.Kwa mujibu wa maelezo yake ni
kwamba kesho vuguvugu hili
litaendelea pia hadi mikoani na
halitakoma hadi tuhakikishe
tunaing'oa serikali madarakani"
"David ninaenda kuoanana na
rais .Tutaongea zaidi baadae .Kama
kuna chochote mtahitaji kutoka
kwangu usisite kunijulisha"
"Sawa Dr Shafi"
"Kingine David nakumbusha
kuhusu umakini mkubwa unatakiwa
katika jambo hili.Hawa wanasiasa wanatakiwa kuendelea kukaa
mafichoni hadi hapo mambo
yatakapotulia kwani naamini hivi sasa
watakuwa wanasakwa mno na jeshi la
polisi.Wakikamatwa na wakahojiwa
we'll all go down.Tafadhali hakikisha
wote wanakuwa salama.Ikilazimika
kuwaficha hata nje ya nchi nieleze
nitasaidia kwa hilo" akasema Dr Shafi
"Dr Shafi vipi kuhusu yule mkuu
wa idara ya ujasusi tayari amekwisha
patikana?
"Mpaka sasa bado sijapokea
taarifa zozote kutoka kwa vijana
niliowatuma kazi hiyo lakini naamini
bado watakuwa wanaendelea na hilo
zoezi na litakapokamilika basi
nitakujulisha"akasema Dr Shafi na
kukata simu.David akatabasamu na
kumpigia tena Frank lakini simu
haikupokelewa "Frank ana tatizo gani?Mbona
hapokei simu? Huu si wakati wa kukaa
mbali na simu hta kidogo,mambo ndio
yameanza"akawaza David
*****************
Elvis na Omola wakifuata
maelekezo ya ile programu ya
kompyuta wakafika katika nyumba
ambayo waliamini ndimo alimo Vicky
"Ni hapa" akasema Omola
akihakiki programu yake.Kabla
hawajashuka garini wakatokea watu
wawili.Elvis akamtaka Omola
washuke.Wakafungua milango na
kushuka wakawafuata wale jamaa
"Hey ! Tuwasaidie nini?akauliza
mmoja wao
"Samahani kaka,hapa ni kwa bibi
Blandina Msakwa? "Blandina?akauliza tena yule
jamaa huku akimtazama mwenzake
"Ndiyo.Ni hapa au tumepotea
nyumba?
"Nani kawaelekeza hapa?
"Tumeelekezwa na kuwa ni
hapa"
"Huyo mtu haishi hapa.Nendeni
mkaulize huko kwa majirani wengine"
akasema yule jamaa
"Samahani sana kwa
usumbufu.yawezekana aliyetuelekza
alikosea"akasema Elvis na kisha yeye
na Omola wakageuka kama vile
wanaondoka kurejea katika gari lao
lakini ghafla wakageka na kutoa
bastora wale jamaa wawili wakapatwa
na mstuko mkubwa.Mmoja akataka
kuchomoa bastora yake lakini Omola
alikiona kitendo kile na kuachia risasi
kadhaa kutoka katika bastora yake na
yule jamaa akaanguka na kutoa mguno.Yule mwenzake aliyebaki
sururali yake ya jeans rangi ya bluu
ikaloa sehemu za mbele alijisaidia haja
ndogo.Mguno ule wa kukta roho
alioutoa yule jamaa aliyepigwa risasi
ukamstua jamaa mwingine aliyekuwa
ndani akafungua mlango mdogo wa
geti na kuchungulia.Elvis alimuona na
kumvurumishia risasi lakini akawahi
kufunga mlango.
"Go after him!! akasema Elvis na
Omola akamfuata yule jamaa kwa
tahadhari kubwa.Akaufungua mlango
mdogo wa geti na kuingia ndani
akawaona watu wawili wakihangaika
kupanda ukuta ili waruke upande wa
nyuma.Mmoja wao akageuka na
kumuona Omola akamvurumishia
risasi lakini Omola akajificha nyuma
ya mti halafu kwa sabaha kali akaachia
risasi iliyompata mmoja shingoni
akaanguka chini na akabaki mmoja.Omola akajitokeza na kumtaka
ajisalimishe.Akaitupa chini bastora na
kunyoosha mikono.Akamfuata na
kuichukua bastora yake akamsachi
hakuwa na silaha nyingine.
Elvis akamuamuru yule jamaa
aliyekuwa naye nje amvute mwenzake
aliyepigwa risasi amuingize ndani
akafanya hivyo halafu
akamuunganisha na yule ambaye
alikuwa amedhibitiwa na Omola
"Mmeona kilichowatokea
wenzenu,kama mnataka kuendelea
kuishi jibuni kwa ufasaha kila
nitakacho wauliza" akasema Elvis
"Ninyi ni akina nani?Mnafanya
nini hapa?
"Sisi hapa ni walinzi
tu.Tumepewa kazi ya kuilinda hii
nyumba"
"Nani kawapa hii kazi?
"Ni Obi" Yuko wapi Obi? akaulzia Elvis
"Obi yuko ndani"
"Yuko na nani humo ndani?Wako
watu wangapi?
"Ndani kuna watu watatu,Obi na
tajiri na mwanamke mwingine
hatumjui"
"Tajiri?!akauliza Elvis
"Ndiyo.Tajiri mwenye kazi"
akasema yule jamaa
"Anaitwa nani?
"Hatumjui.Sisi tunayemfahamu ni
Obi"akasema yule jamaa halafu Elvis
akamuinua na kumtaka aelekee
mlangoni
"Fungua mlango" akaamuru Elvis
na yule jamaa akafungua mlango
ukafunguka.Sebuleni hakukuwa na
mtu yeyote na nyumba ilikuwa
kimya.Elvis akampiga yule jamaa pigo
moja la kichwani akaanguka na
kupoteza fahamu.Elvis akamfanyia ishara Omola ampoteze fahamu yule
jamaa mwingine na kufumba na
kufumbua Omola akmtadika yule
jamaa pigo zito na kumuacha akiwa
hana fahamu akatembea kwa
tahadhari kumfuata Elvis
"Kuna mtu yeyote humu
ndani?akauliza
"Nyumba iko kimya sana.Twende
kwa tahadhari hawa watu wamo
humu ndani" akasema Elvis kwa sauti
ndogo na kuanza kuzunguka ndani ya
nyumba ile na ghafla wakaona mlango
wenye mchirizi wa damu.Elvis
akamfanyia ishara Omola halafu
wakausogelea mlango ule na taratibu
Elvis akakinyonga kitasa cha mlango
na kuufungua kisha wakajitoma ndani
wakakutana na kitu cha
kustusha.Damu ilikuwa imesambaa
kila mahala na watu wawili walikuwa
wamelala katika damu hawakuonekana kuwa na uhai
tena.Pembeni ya ukuta alionekana
mwanamke mmoja akiwa amelala
sakafuni akiwa ameloa damu.Elvis
akamfuata na kugundua ni Vicky
"Vicky!! akaita Elvis na kujaribu
kumtingisha lakini Vicky hakuweza
hata kufumbua jicho.Mapigo ya moyo
wake yalikuwa chini sana.
"Omola haraka sana tumuokoe
Vicky hali yake si nzuri hata kidogo"
akasema Elvis huku akimuinua Vicky
na kutoka naye nje.Omola kabla ya
kutoka akawapiga picha wale watu
wawli waliokuwa wamelala katika
damu ambao hawakuwa na uhai tena
"Inaonekana kulikuwa na
shughuli nzito humu ndani" akawaza
Omola wakati akitoka na kukimbia
kumfuata Elvis ambaye aliondoa gari
haraka sana.Akachukua simu na
kumpigia Dr Philip Dr Philip ninakuomba uache kila
unachokifanya sasa uelekee tena
katika makazi yetu mapya kuna mtu
amejeruhiwa ana hali mbaya sana
ninakuja naye sasa hivi"
"Sawa Elvis ninafanya hivyo"
akasema Dr Philip
"Nimechunguza kwa haraka
haraka mle ndani kunaonekana
kulikuwa na shughuli nzito sana.Ni
akina nani wale jamaa wengine
waliouawa mle ndani?Inaonekana
wameuliwa kikatili sana ila nimepiga
picha maiti zao na vile vile
nimechukua simu mbili zilizokuwa
pemeni ya Vicky"akasema Omola
"Kikubwa kwa sasa tujitahidi
Vicky awe salama.Atatueleza kila kitu
kilichotokea na kwa nini alifika pale"
akasema Elvis akiendesha gari kwa
kasi Waliwasili katika makazi yao,geti
likafunguliwa na kwa haraka Vicky
akashushwa na kuingizwa
ndani.Tayari Dr Philip alikwisha fika
na kwa haraka akaanza
kumuhudumia.Winnie alipomuona
dada yake akiwa katika hali ile
akaangua kilio.Elvis akamtaka
anyamaze.Omola akamuonyesha Elvis
picha zile alizozipiga katika kile
chumba walimomkuta Vicky.
"Vicky alifikaje hapa?Inaonekana
kulikuwa na mpambano mkali sana
hadi akafanikiwa kuwaua hawa jamaa
wawili.Watu hawa ni akina
nani?Nyuso zao zote zimetapakaa
damu kiasi ni vigumu
kuwatambua.Ngoja atakapozinduka
atatujulisha nini hasa kilijiri na hawa
aliowaua ni akina nani" akasema Elvis
akachukua simu na kumpigia Steve
akamjulisha kuwa tayari wamekwisha mpata Vicky na alikuwa anaendelea
kupatiwa matibabu na Dr Pilip.Steve
akamfahamisha Elvis kwamba
walikuwa wamewasili nyumbani kwa
Doreen na muda wowote yeye na
Meshack Jumbo wataanza safari
kuelekea katika makazi yao.Elvis
akaenda katika chumba ambamo
Vicky alikuwa anaendelea kupatiwa
matibabu
"Ameumizwa sana,hata hivyo
itanilazimu kwenda kuchukua chupa
zaidi za damu kwani amepoteza damu
nyingi sana.Imekuwa vyema
mmewahi kumpata lakini
mngechelewa kidogo angepoteza
maisha" akasema Dr Philip
"Dr Philip fanya kila unaloweza
kuhakikisha Vicky anakuwa
salama.Kuna mengi tunahitaji
kuyafahamu kutoka kwake" akasema
Elvis Usijali Elvis nitafanya kila
ninaloweza na Vicky atakuwa salama"
akasema Dr Philip na kuondoka
kwenda kufuata damu ya
kumuongezea Vicky.
"Elvis ahsante sana kwa
kumukoa dada yangu.Japokuwa hali
yake si nzuri lakini ninashukuru
kwani yuko katika mikono
salama.Sina cha kukulipa Elvis na
samahani sana kwa yote
niliyoyafanya.I was so foolish.I didnt
know what I was doing" akasema
Winnie huku akilia
"Usilie Winnie kitu kikubwa kwa
sasa ni kumuombea Vicky aweze
kupata nafuu.Wewe pia bado unahitaji
mapumziko.Nenda kapumzike
nitakujulisha hali ya dada yako
inavyoendelea" akasema Elvis By the way Elvis waliofanya hivi
mmewafahamu ni akina nani?
akauliza Winnie
"Bado hatujawafahamu ni akina
nani ila mahala tulipomkuta Vicky
kulikuwa na mapambano makali na
watu wawili wamekufa naamini hao
ndio walimteka.Atakapozinduka
atatueleza mengi kuhusiana na watu
wale na nini kilitokea"
"Ahsante Elvis.Mungu akubariki
sana.Nakuomba tafadhali hakikisha
dada yangu anakuwa salama"
akasema Winnie na kwenda chumbani
kupumzika.Dr Philip akatoka katika
chumba alimokuwamo Vicky na
kumjulisha Elvis kwamba anakwenda
kuchukua damu pamoja na dawa
nyingine kwa ajili ya Vicky.Elvis
akaingia katika chumba alimo Vicky
ambaye bado hakuwa na fahamu akamtazama kwa muda halafu
akasema kwa sauti ndogo
"You are so
beautifull.Hukutakiwa kufanya kazi
kama hizi.Baada ya suala hili
kumalizika nitakushauri uachane na
hizi kazi na ujishughulishe na biashara
zako.Watoto wazuri kama ninyi ni
pambo la hii dunia hamustahili hata
kidogo kufanyiwa ukatili mkubwa
kama huu" akawaza na mara mlango
ukagongwa alikuwa ni Omola
"Anaendeleaje Vicky? akauliza
Omola akiwa ameishika kompyuta
yake
"kwa mujibu wa daktari
anaendelea vyema ila amepoteza
damu nyingi na Dr Philip amekwenda
kufuata damu zaidi pamoja na dawa"
"Vicky ni jasiri na atakuwa
salama" akasema Omola Tumuombee awe salama kwani
tunahitaji kufahamu kutoka kwake
kuhusiana na wale watu tuliowakuta
mle chumbani wamekufa ni akina
nani"
"Elvis kuna jambo nimelipata
kuhusiana na makamu wa rais na
David" akasema Omola wakatoka mle
chumbani wakaenda sebuleni
"Nimepata rekodi nyingine ya
mazungumzo kati ya makamu wa rais
na David ambayo yamefanyika muda
si mrefu sana" akasema Omola na
kumchezea Elvis mazungumzo yale ya
makamu wa rais Dr Shafi na
David.Elvis akatoa kitambaa na
kujifuta jasho.Alihisi joto
"Toka awali nilihisi lazima kuna
jambo kubwa lililoko nyuma ya
mkutano ule wa siasa na sasa tayari
tumeupata ukweli kwamba ajenda
kuu ya mkutano ule ambao ndio chanzo cha machafuko yaliyotokea leo
ni kuing'oa serikali.Makamu wa rais
na David wakishirikiana na wanasiasa
wa vyama vya upinzani lengo lao ni
kuanzisha machafuko ambayo
yataing'oa serikali iliyoko
madarakani.Huu ni uhaini.Watu hawa
ni mashetani kabisa.Watu
wanaangamia katika mapambano
kumbe lengo lao ni kupata
madaraka.Huu ni ukatili uliopitiliza
kabisa!! akasema Elvis kwa hasira
"Nadhani wanataka kuiga kile
kilichotokea katika baadhi ya nchi
ambapo kulitokea maandamani na
machafuko ya bila kukoma na serikali
zilizokuwa madarakani
zikang'oka.Lengo lao ni hilo"akasema
Omola
"Sawa kabisa Omola kwani katika
mazungumzo yao David anamsisitiza
Dr Shafi kwamba vijana wanaendelea kuhamasishwa waendeleze vurugu na
kesho vurugu hizo zitahamia pia
katika mikoa mikubwa.Lengo lao ni
vurugu zisambae nchi nzima na
serikali itatumia nguvu kubwa
kumaliza vurugu na maandamano
hayo na lengo la waandaaji wa
maandamano na vurugu hizo ni
kuilazimisha serikali kutumia nguvu
kubwa na kupelekea watu kuuawa
hivyo kuifanya jumuiya ya kimataifa
kupiga kelele kubwa na wakati
mwingine kuingilia kati kuiondoa
serikali iliyopo madarakani kwa
kisingizio cha kukiuka haki za
binadamu.Maisha ya watu hasa vijana
wadogo yanapotea kutokana na uchu
wa madaraka wa watu wachache tu "
akasema Elvis
"Kwa hiyo tunafanya
nini?akauliza Omola Watu hawa ambao wako nyuma
ya jambo hili ni hawa hawa ambao
tunaamini ndio wanaojihusisha na
biashara ya silaha kwa waasi wa
Congo.Huu unaonekana ni mtandao
mkubwa na uliosambaa sana.Nadhani
sasa itatulazimu kufanya mambo
mawili kwa wakati mmoja.Tuumalize
mtandao wote wa biashara ya silaha
na vile vile tulizime jaribio hili la
kutaka kuiondoa serikali
madarakani.Tunao ushahidi ambao
hauna mashaka kuhusiana na mpango
ya hawa jamaa na tayari
tunawafahamu ni akina nani hivyo
tunachotakiwa kufanya ni kufahamu
nani na nani wamo katika mpango
huu wa kuiondoa serikali madarakani"
"Kwa nini tusiwataarifu vyombo
vingine kama jeshi la polisi kuhusiana
na hiki tulichokigundua ili tuokoe watu zaidi wasiendelee kuuawa?
akauliza Omola
"Kitu muhimu ni sisi kuhakikisha
tumechunguza kwa kina na
kuwafahamu wahusika wote na kisha
kuwakamata na kuwakabidhi kwa
vyombo husika ili sheria ichukue
mkondo wake" akasema Elvis
"Elvis nimekumbuka kitu"
akasema Omola na kwenda katika
chumba chake na baada ya muda
akarejea
"Nilichukua simu mbili
zilizokuwa pembeni ya Vicky katika
kile chumba" akasema Omola na
kumkabidhi Elvis zile simu.Moja
ilikuwa imezima ambayo Elvis
akaitambua ni simu ya
Vicky.Akaichukua nyingine kubwa
nyeupe akaanza kuipekua.Kitu cha
kwanza alichokifanya katika simu ile
ni kufungua sehemu ya kuhifadhi picha na kustuka baada ya kuziona
picha kadhaa za Frank.
"Frank!! akasema Elvis kwa sauti
ya mshangao na kuendelea
kuzitazama picha zile.Katika picha
kadhaa Frank alionekana akiwa baa
akiwa na Pascal wakipata kinywaji
huku wakiwa na wanawake wawili.
"Umesema Frank?Omola akauliza
"Ndiyo.Kuna picha hapa katika
hii simu ambazo zinamuonyesha
Frank akiwa na Pascal wakiwa baa
wakipata kinywaji.Pia zipo picha
nyinginezo zikimonyesha Frank katika
sare za kazi"
"Je hii ni simu ya Frank? akauliza
Omola
"Ninahisi hivyo.Ichunguze laini
hii ya simu imesajiliwa kwa jina
gani?akasema Elvis na Omola
akaichukua ile simu ya Frank lakini
kabla hajafanya chochote ikaanza kuita na jina la mpigaji lilionyesha ni
David.
"Kuna mtu anapiga simu hapa
anaitwa David" akasema Omola
"David?!!.Elvis akauliza
"Ndiyo"
"Usiipokee hiyo simu ili
tuzichunguze namba hizo pia
tufahamu ni David yupi anayempigia"
akasema Elvis na simu ile ya David
ikaita na kukatika bila kupokelewa na
baada ya sekunde kadhaa ukaingia
ujumbe uliosomeka
"Frank naomba uwasiliane nami
mara tu uupatapo ujumbe huu,ni
muhimu sana"
"Tayari tumepata jibu hii ni simu
ya Frank.Je Frank ni mmoja wa watu
waliouawa mle ndani? akauliza Elvis
"Kama ni simu ya Frank basi
lazima naye ni mmoja wa watu waliouawa mle ndani.Unamfahamu
Frank kwa sura? akauliza Omola
"Hapana.lakini kuna njia rahisi ya
kufahamu kama mmoja wa watu
waliouawa mle ndani ni Frank"
akasema Elvis na kwenda kumchukua
Graca.Akaichukua simu ya Omola
akamuonyesha Graca picha alizopiga
Omola
"Ninaomba kwa makini sana
zipitie hizo picha na ujaribu kuona
kama utaweza kumtambua mmoja
kati ya watu utakaowaona katika hizo
picha.Samahani kwa picha hizi
zinatisha kidogo" akasema Elvis na
Graca akaanza kuzitazama picha
zile.Sura za watu wale zilikuwa
zimechafuka kwa damu lakini ghafla
baada tu ya kuiona picha ya pili Graca
akastuka This is my father !! akasema kwa
mstuko .Elvis na Omola
wakatazamana
"Graca itazame tena picha vizuri
na uhakikishe kama unachokisema ni
cha kweli" akasema Elvis.
"Elvis ninamfahamu baba yangu
vizuri.Hata kama nikikurupushwa
usingizini nitamtambua.Huyu ni baba
yangu Frank Kwaju.What happend to
him?Where is he?akauliza Graca
ambaye macho yake tayari yalianza
kuonyesha wasiwasi.Elvis akamshika
mkono na kumketisha sofani
"Graca you have to be
brave.Tulipokwenda kumfuata Vicky
mahala alipotuelekeza tumekuta kuna
watu wawili katika chumba
alimokuwamo.Watu hao ndio hao
unaowaona katika picha.Kwa bahati
mbaya wote wawili hawana uhai.They're both dead.I'm so sorry
Graca" akasema Elvis
"Graca pole sana" akasema
Omola na macho ya Graca yakajaa
machozi.Elvis akamkumbatia na Gaca
akikilaza kichwa chake kifuani kwa
Elvis huku machozi mengi
yakimtoka.Alikuwa analia kwa kwikwi
"Tunamsubiri Vicky azinduke ili
atueleze nini hasa kilichokuwa
kimetokea mahala pale.Yeye ndiye
anayefahamu nani waliofanya mauaji
yale ya baba yako"akasema
Elvis.Graca akainua kichwa
akamtazama Elvis
"Elvis I need to be alone now"
akasema Graca
"Kama kuna chochote unakihitaji
tafadhali nieleze"
"Ahsante Elvis" akasema Graca
na kuelekea chumbani huku akilia Anatia huruma sana
Graca"akasema Omola
"Frank alikuwa ni mkatili sana
kwa mwanae.Graca amepitia mateso
makali kutoka kwa baba
yake.Alimtesa kama si mwanae wa
damu lakini siku zote damu ni nzito
kuliko maji.Pamoja na ukatili wote
aliofanyiwa na baba yake lakini kifo
chake kimemuumiza Graca.Hawezi
kuonyesha usoni lakini moyoni
ameumia sana" akasema Elvis na
kumsimulia Omola kila kitu kuhusiana
na Graca
"Dah ! Kumbe amepitia mambo
mengi sana licha ya umri
wake.Anatuhitaji sana kwa wakati
huu.Tunapaswa tuwe naye karibu "
akasema Omola
"Tuachane na suala hilo na
tujielekeze katika kumtafuta huyu
David aliyekuwa anawasiliana na Frank ni nani?akasema Elvis na Omola
akazichukua zile namba za David
akaziingiza katika kompyuta yake
akabofya kidogo na baada ya muda
akasema
"Namba hizi ni za David
Sichoma"
"Oh my God ! Elvis akashangaa
"Huyu ni waziri mkuu mstaafu
ambaye ndiye anayewasiliana na
makamu wa rais.Kama David na Frank
wanawasiliana hii ina maana kwamba
hata David naye yumo katika mtandao
wao wa biashara ya silaha.Sasa picha
kamili imejileta yenyewe namna
mtandao huu ulivyo mkubwa na sasa
tunaona kuna mambo mengine
wanajishughulisha nayo zaidi ya
biashara ya silaha.Wana panga
mipango ya uhaini.Wanataka
kumuondoa rais aliyeko
madarakani.Hili si jambo dogo hata kidogo.Kwa nini lakini wanafanya
hivi?Kwa nini wanataka kuiondoa
serikali madarakani?Nani
kawatuma?akauliza Elvis
"Elvis maswali haya ni madogo
lakini majibu yake ni mazito sana na
tutayapa majibu endapo tutawapata
wahusika wakuu wa mtandao
huu.Tukiwapata
tukawah............."Omola akanyamaza
baada ya kengele ya getini
kusikika.Elvis akainuka akatoa
bastora yake na kueleka getini kwa
tahadhari kubwa.Akachungulia na
kumuona Steve akalifungua geti
wakaingia ndani.Steve alikuwa na
Meshack Jumbo
"Mambo yamekwenda vizuri
huko? akauliza Elvis wakiwa sebuleni
"Kila kitu kimekwenda
vizuri.Nawashukuruni sana kwa
kuniokoa mimi na familia yangu leo hii.Isingekuwa ninyi nadhani mpaka
mida hii ningekuwa nimekufa"
akasema Meshack Jumbo
"Usijali mzee,ni wajibu wetu
kufanya vile tulivyofanya" akajibu
Elvis
"Vicky anaendeleaje?akauliza
Steve
"Bado hana fahamu lakini Dr
Philip ametuhakikishia kwamba
anaendelea vyema,hajaumia sana
isipokuwa amepoteza damu nyingi"
"Nini hasa kilichotokea?Nani
waliokuwa wamemshikilia?akauliza
Meshack Jumbo.Elvis akawaelezea kila
kitu kilivyokuwa na halafu
akawaonyesha picha walizofanikiwa
kuwapiga wale watu wawili
waliokutwa wamefariki ndani ya kile
chumba walimomkuta Vicky
"Hawa ni akina
nani?Mmewatambua? akauliza Steve Tumfanikiwa kumtambua
mmoja wao.Ni brigedia Frank Kwaju"
Meshack Jumbo na Steve
wakatazamana kwa mshangao
"Frank?akauliza Meshack Jumbo
"Ndiyo.Tulipiga picha miili ile na
tukamuonyesha Graca na mara tu
alipoziona picha akamtambua baba
yake Frank.Kwa hiyo ni wazi sasa
Frank Kwaju amefariki dunia"
akasema Elvis
"dah ! akasema Steve
"Nani huyo ambaye
amemuondoa huyu jamaa duniani
kikatili namna hii?akauliza Meshack
Jumbo huku akitazama tena pichaya
Frank
"Bado hatufahamu ni nani
aliyefanya kitendo hiki tunamsubiri
Vicky yeye ndiye mwenye kufahamu
kila kitu kilichotokea.Akizinduka
atatueleza nini kilichotokea ila naamini ni yeye ndiye aliyewaua wale
jamaa"akasema Elvis
"Nilimtamani sana Frank
nikutane naye ana kwa ana" akasema
Steve
"Aliyekutana naye amefanya kile
ambacho ungekifanya pindi
ungekutana naye.Hata hivyo kuna
jambo lingine pia" akasema Elvis na
kuwachezea mazungumzo ya makamu
wa rais na David.Meshack Jumbo
akabaki mdomo wazi
"This is unbeliavable.Elvis una
hakika hizi sauti ni za makamu wa rais
na David?akauliza Meshack Jumbo
akionekana kuwa na wasi wasi
mwingi
"Usiwe na wasi wasi wowote
mzee Jumbo.Unazozisikia ni sauti za
makamu wa rais Dr Shafi na waziri
mkuu mstaafu David" "Vijana hili sijambo dogo lazima
rais afahamishwe kuhusu hili suala ili
aweze kuchukua hatua stahiki za
haraka sana kuzima mpango huu!!
akasema Meshack
"Hapana mzee hatutamtaarifu
rais mpaka hapo tutakapokuwa na
taarifa na ushahidi wa kujitosheleza
kuhusiana na hili suala.Tunapaswa
tuwafahamu wote wanaopanga njama
hizi.Huu ni mtandao mrefu hivyo
kabla ya kumjulisha rais ni lazima
kwanza tuhakikishe tumewafahamu
watu hao ni akina nani,na nani yuko
nyuma yao?Siku zote kunapokuwa na
mipango kama hii ya mapinduzi
lazima kuna watu walio nyuma ya
mipango hiyo kwa manufaa yao hivyo
hata mpango huu lazima kuna watu
walio nyuma yake ambao lazima
tuwafahamu" Elvis itachukua muda mrefu
kuwafahamu watu hao ni akina nani
kwa vile tayari tunawafahamu
wahusika wakuu ambao ni makamu
wa rais na David basi tumjulishe rais
na wakamatwe mara moja na hao
watawataja wenzao wanaoshirikiana
nao.Suala hili halipaswi kuchukua
muda mrefu.We have to do it now!!
akasema Meshack Jumbo
"Mzee suala hili ni kubwa na
zito.Hatuwezi kukurupuka na
kumuendea rais bila ya kuwa na
ushahidi wa kujitosheleza.Unadhani
rais atatuelewa kwa sababu tu ya
ushahidi wa sauti za maongezi ya
makamu wa rais na David?akauliza
Elvis na Meshack akawa kimya
"Watu hawa ni viongozi
wakubwa wa serikali hivyo
tunapowaingiza katika jambo kubwa
kama hili lazima tuwe na ushahidi usio na mashaka hata kidogo kwamba
wanahusika katika kutaka kuiangusha
serikali" akasema Elvis
"Elvis tutapoteza muda mwingi
kuwachunguza hawa jamaa wakati
wao wanaendelea na harakati zao na
maisha ya vijana wanaoingizwa
barabarani kuandamana yanaendelea
kupotea endapo hatua za haraka
hazitachukuliwa kuwadhibiti hawa
jamaa.Ukiacha hilo usalama wa rais
hivi sasa uko mashakani kwani hawa
jamaa wanaweza wakamuua hivyo
lazima tumlinde rais"
"Rais atakuwa salama
tutamlinda"akasema Elvis
"Una uhakika gani atakuwa
salama na utamlinda vipi wakati
wewe tayari umekufa na hauwezi
kuonekana mtaani?Elvis tafadhali
tusilifanye suala hili likawa
gumu,mimi maamuzi yangu ni kumjulisha rais.Naomba kusiwe na
mabishano yoyote tena kuhusu suala
hilo.Endapo litatokea jambo baya na
ikagunudlika kwamba nilifahamu
kuhusiana na mipango hii ya
mapinduzi na nikawa kimya basi
lazima na mimi nitachukuliwa
hatua.Sitaki jambo hilo linitokee hivyo
nitamjulisha rais kuhusu jambo hili
kusudi hatua za haraka
zichukuliwe"akasema Meshack Jumbo
na kutoa simu akaiwasha kwa lengo la
kumpigia rais lakini Elvis
akamnyang'anya
"Mzee ninakuheshimu sana na
ninakuomba usikilize na ufuate kile
ninachokueleza.Hii ni kazi yetu na
ninakuomba utuache tuifanye namna
tunavyoona sisi inafaa.Wewe kaa
pembeni subiri matokeo kutoka
kwetu.Tuko tayari kufanya kazi hii
kwa kila uwezo tulio nao na ninakuhakikishia tena kuwa hawa
jamaa hawatafanikiwa lengo
lao.Naomba uniamini na uiamini timu
ninayoiongoza" akasema Elvis
"Elvis nielewe kijana wangu,
maisha ya rais yako mashakani.Yuko
katika hatari kubwa ya
kuuawa.Tukifanya masihara rais
anaweza akafikwa na jambo baya
.Tunao uwezo wa kumuokoa rais dhidi
ya njama hizi ovu na lazima tufanye
sasa,si kusubiri" akasema Meshack
Jumbo
"Mzee narudia tena
kukuhakikishia kwamba rais atakuwa
salama.Watu hao hawatafanikiwa
lengo lao na ninakuhakikishia
kwamba tu......."Elvis akakatishwa na
Mzee Jumbo
"Elvis kwa nini hutaki
kunielewa?!! akauliza Meshack kwa
ukali.Elvis naye akakasirika na kusimama akamtazama Meshack kwa
hasira
"Mzee nakuonya kwa mara ya
mwisho kwamba hii ni kazi yetu.Sisi
ndio tuliobaini kuwepo kwa mipango
hii ya kuiangusha serikali na sisi ndio
tutakaohakikisha kwamba jambo hilo
halifanikiwi.This is what I died for.I
won't let my death be for nothing.I
died to save my president and thats
what I'll do!! akasema Elvis kwa ukali
"No ! akasema Meshack na
kugonga meza kwa hasira
"Ninyi nyote bado mko chini
yangu na mtafanya kila kitu kutokana
na maelekezo yangu.Hakuna
atakayekwenda kinyume na mimi!!
akasema Meshack kwa sauti
kali.Ghafla kukatokea kitu ambacho
hakuna aliyekitegemea.Elvis aligeuka
haraka kwa kasi na kumtandika
Meshack Jumbo ngumi nzito iliyomfanya apepesuke akamfuata na
kumtandika kichwa kizito Meshack
akaanguka chini.Hakuwa na fahamu
"Steve mchukue kamfungie
chumbani.Haweze kuwa kikwazo
kwetu kufanikisha kazi zetu!!
akaamuru Elvis na Steve akamvuta
Meshack Jumbo hadi chumbani
akamfungia
"Elvis wazee kama hawa
hawahitaji nguvu kubwa
kuwanyamazisha.Tayari
wamejichokea unaweza ukampiga
kichwa kizito na ukajikuta
umemmaliza kabisa.Kwa bahati nzuri
mzee huyu ana mazoezi vinginevyo
kwa kichwa kile angeweza kupoteza
kabisa maisha" akasema Steve huku
akicheka
"Kaniudhi sana yule mzee na
atakaa humo humo hadi pale
tutakapokamilisha operesheni yetu.Tuachane na hayo ya mzee
tuendelee na kazi yetu..... .." akasema
Elvis na kengele ikalia Steve akatoka
kwenda kuangalia mgongaji alikuwa
ni Dr Philip akiwa amerejea na dawa
pamoja na damu kwa ajili ya
Vicky.Hakutaka mazungumzo mengi
akaelekea moja kwa moja katika
chumba alimo Vicky akaendelea
kumuhudumia
"Tumuache Dr Philip aendelee
kumuhudumia Vicky sisi tuendelee na
kazi.Steve kuna jambo lingine
tumeligundua pia.Waziri mkuu
mstaafu David na Frank
wanafahamiana na ukitazama simu ya
Frank utagundua David amempigia
zaidi ya mara nne ila simu
haikupokelewa na akaamua kutuma
ujumbe kwamba ampigie kuna suala
la muhimu.Tayari picha imekuja kuwa
hata David naye lazima atakuwa katika mtandao wa akina Frank.Kama
David naye yumo katika mtandao wa
akina Frank hii inaaashiria kwamba
katika suala hili la mipango ya
mapinduzi hata hawa akina Frank nao
wapo pia.Tuendelee kuchunguza zaidi
na tutafahamu mambo mengi na
ndiyo maana nimemkatalia mzee
Jumbo kwamba tusimjulishe kwanza
rais kuhusiana na hili suala hadi hapo
tutakapokuwa tumepata ushahidi wa
kujitosheleza.Hili si suala la
kukurupuka na kumueleza
rais.Tumueleze pale tutakapokuwa
tayari na ushahidi wa
kutosha"akasema Elvis
"Ninakubaliana na maamuzi yako
ya kumfungia yule mzee
chumbani.Kwa maelezo haya
yaliyopatikana mchezo unazidi kuwa
mtamu.Hawa hawa ambao tulikuwa
tunawatafuta kwa uuzaji wa silaha ndio hawa hawa wanaosuka mipango
ya kuiangusha serikali.Huko mjini hivi
sasa ni heka heka kubwa.Barabara
nyingi zimefungwa kufuatia vurugu
kubwa zinazoendelea.Watu hawa
inabidi tule nao sahani moj............."
akasema Steve na kunyamaza baada
ya simu yake kuita alikuwa ni Juliana
"Juliana habari ya muda huu?Vipi
maendeleo yako?akauliza Steve
"Ninaendelea vyema
Steve.Nimekupigia kukujulisha
kwamba Patricia hayuko tena hapa
nyumbani tayari amehamia ikulu"
"Thats good news" akasema
Steve
"Jambo la pili ni kwamba mpaka
sasa sijafanikiwa kuingia chumbani
kwa mama.Chumba chake
kimefungwa na hakuna
anayeruhusiwa kuingia zaidi
yake.Ninaomba univumilie na nikipata nafasi baadae nitaingia na kuchukua
kompyuta zake"
"Sawa Juliana endapo
utafanikiwa utanijulisha ila tunaihitaji
sana kompyuta hiyo.Jitahidi kila
uwezavyo kuipata" akasema Steve na
kuagana na Juliana
"Anasemje Juliana?akauliza Elvis
"Ana taarifa mbili.Kwanza ni
Patricia'
"Kafanya nini Patricia? akauliza
Elvis
"Patricia tayari ameondoka pale
nyumbani kwao na ameelekea ikulu"
"Oh thank you Lord" akasema
Elvis
"Taarifa ya pili ni kwamba mpaka
sasa bado hajafanikiwa kuingia
chumbani kwa mama yake hivyo bado
hajaipata kompyuta ile tunayoihitaji"
akasema Steve.Elvis akafikiri kidogo
halafu akasema Frank ana mahusiano na
Elizabeth na mpaka sasa ninaamini
hajafahamu kama Frank amekufa
hivyo tutafanya jambo moja.Kwa
kutumia simu ya Frank tutamtumia
ujumbe Elizabeth na kumuelekeza
afike katika ile nyumba ulimo mwili
wa Frank na ataamini kuwa ujumbe
huo umetoka kwa Frank hivyo atafika
mahala hapo.Lengo ni kumuondoa
nyumbani ili Juliana aweze kupata
nafasi ya kuingia chumbani kwake na
kuichukua kompyuta tunayoitaka"
"Huo ni mpango mzuri
sana.Akifika pale atakutana na
mshangao wa mwaka." akasema Steve
"Haitaishia hapo.Tutamtumia pia
ujumbe David naye atafika mahala
hapo hapo na watakutana.Lengo hapa
ni kumuondoa David nyumbani ili
tuweze kumpata Dr Makwa Tusangira
ambaye amejificha nyumbani kwa David akihofia kukamatwa na
polisi.Tukimpata Makwa atatueleza
kila kitu na tutaweza kuwafahamu pia
watu wengine ambao wanashiriki pia
katika mpango huu wa kuipindua
serikali" akasema Elvis
"Huo nao ni mpango mzuri lakini
swali langu ni kwamba ni jambo lipi
hasa tunalishughulikia kwa
sasa.Kutafuta mtandao wa silaha au
kuuzima mpango wa
mapinduzi?akauliza Steve
"Kutokana na umuhimu wake na
uharaka kwa sasa tujikite zaidi katika
kulizima jaribio hili la
mapinduzi.Katika suala la silaha tayari
tumepiga hatua
kubwa.Tumewafahamu wahusika
wakuu na sasa tunaendelea kumtafuta
Patrice Lwibombe na nina uhakika
mkubwa kwamba haitachukua muda
mrefu kabla ya kumfahamu ni nani na yuko wapi.Kwa ufupi naweza kusema
kwamba tunakwenda na mambo yote
mawili kwa wakati mmoja kwani watu
hao hao wanaohusika na biashara ya
silaha ni hao hao wanaoonekana
kuhusika pia katika mpango wa
mapinduzi"
"Sawa Elvis basi tuanze
maandalizi ya kazi ya jioni ya leo
kwenda kuvamia nyumbani kwa
David na kumchukua Dr Makwa
Tusangira" akasema Steve kisha
wakaendelea na mipango kuhusiana
na kazi ya usiku ya kuvamia nyumbani
kwa David na kumchukua Dr Makwa
Tusangira.
Sent using
Jamii Forums mobile app