HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
- Thread starter
- #1,041
I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 72
"Dr Philip endelea kushughulikia
kila kitu kuhusiana na kuuhifadhi
mwili wa Vicky kuna suala
tunaendelea kulishughulikia na baada
ya kukamilika tutaungana nawe hapo
hospitali.Mpe pole sana Winnie"
akasema Elvis na kukata simu
"One soulder down......." akasema
Steve
"But we have to continue
fighting.We must save president.."
akasema Elvis na ukimya wa zaidi ya
dakika mbili ukapita kila mmoja
akitafakari lake kisha Elvis akasema
"She's gone too soon
.Tulimuhitaji sana Vicky katika wakati
huu" akasema na kunyamaza
akatazama chini kwa muda kisha
akainua kichwa na kusema
"Steve kwa heshima ya Vicky
lazima tuhakikishe tunalimaliza suala
hili usiku wa leo.Tuhakikishe kwamba tunawapata wale wote
wanaojihusisha na biashara ya silaha
na vile vile kuwapata wale wote
waasisi wa machafuko haya
yaliyoanza leo yenye lengo la
kuiondoa serikali madarakani."
akasema Elvis sura yake ikiwa na
hasira za hali ya juu
"Kuna watu wawili tu ambao
tukiwapata wataweza kutoa majibu ya
maswali yetu yote ambao ni David na
Elizabeth.Hawa wanafahamu kila
kitu.David anafahamu nani yuko
nyuma ya mpango wa mapinduzi na
Elizabeth atatusaidia kufahamu
mtandao wote unaojihusiaha na
biashara ya silaha"akasema Steve
"Kila kitu kinamalizika usiku wa
leo!! akasema Elvis
"Vipi kuhusu
Omola.Tutamwambiaje kuhusu Vicky? Hatutamwambia kitu chochote
kwa sasa hadi hapo tutakapokuwa
tumemaliza misheni yetu" akasema
Elvis kisha wakamfuata Omola
aliyekuwa chumbani akijipumzisha
"Vipi hali ya Vicky? akauliza
Omola
"Bado hatujapokea tararifa
zozote kutoka kwa Dr
Philip.Tunaamini atapona.Omola
kuna jambo ambalo tumeamua
kulifanya usiku huu.Baada ya
kugundua kwamba watu wanaopanga
mpango wa kuipindua serikali ni wale
wale wanaojihusiaha na biashara ya
silaha tumeamua tuwakamate wote na
kuwafikisha sehemu
husika.Operesheni yetu tunaimaliza
usiku wa leo.Watu pekee ambao
tunaamini wanaweza wakatupa
majibu ya maswali yetu yote ni wawili
tu,David na Elizabeth.Tukiwapata hawa tutamaliza kila kitu.Kwa hiyo
tunataka kwanza kuwafahamu mahala
walipo.Tuliwatumia ujumbe kupitia
simu ya Frank ili wakutane sehemu
moja na ninaamini wote watakuwa
wamekutana mahala hapo na
yawezekana hadi muda huu tayari
watakuwa wamegundua kwamba
Frank amekufa.Kifo cha Frank
kitawafanya wabuni mbinu mpya za
kuendeleza mipango yao lakini kabla
hawajafanya hivyo wanatakiwa wawe
katika mikono yetu" akasema Elvis
"Itabidi tupate namba za simu
anayotumia Elizabeth ili tuweze
kumfuatilia na kujua mahala
alipo.Namba za David tunazo tayari"
akasema Omola na Elvis akamtaka
Steve ampigie simu Juliana
"Hallo Steve.Nimefika salama na Juliana baada ya kupokea simu ya
Steve
"Hilo ni jambo jema sana.Juliana
nimekupigia kujua kama umefika
salama vile vile kukujulisha jambo
moja."
"Nakusikiliza Steve"akasema
Juliana
"Tumeamua kumaliza kila kitu
usiku wa leo.Tumegundua kwamba
mama yako Elizabeth au vyovyote vile
anavyoitwa anahusika yeye na
mtandao wake katika vurugu za
kisiasa zinazoendelea hivi sasa
zilizopelekea vifo vya vijana wengi
huko mtaani.Lengo lao kuu ni
kuipindua serikali iliyoko
madarakani.Ukiacha hilo,tumegundua
pia kwamba mama yako anajihusisha
na biashara ya silaha kwa waasi wa
Congo.kwa hiyo basi tumeamua
kumtia nguvuni usiku wa leo na tumeona tusifanye hivyo kabla
hatujakujulisha wewe kwanza"
akanyamaza baada ya kusikia Juliana
akivuta pumzi ndefu
"Juliana are you ok?
"I'm ok Steve.Endelea"
"Tunahitaji kufahamu mahala
alipo mam a yako hivi sasa hivyo
tunaomba utusaidie kutupatia namba
yake ya simu anayotumia sasa ili
tuweze kumtafuta na kujua mahala
alipo na tumtie nguvuni"
"Steve hizi ni taarifa njema japo
zinastusha lakini tayari nilikwisha
jiandaa kwa jambo hili kwa hiyo
ninatoa baraka zangu mama
akamatwe na ahojiwe kuhusiana na
mambo yote haramu ambayo
amekuwa akiyafanya yeye na
wenzake.Kufikia hatua ya kutaka
kuipindua serikali huu ni uhalifu
uliovuka mipaka.Wanatakiwawakamatwe haraka sana.Pamoja na
hayo yote ambayo mmeyagundua
kwake lakini nahitaji sana ahojiwe
kuhusiana na vifo vya mdogo wangu
na mpenzi wangu.Ninaamini
anafahamu sababu ya vifo hivyo na
lazima atakuwa anawafahamu
wahusika hivyo awataje na
wafikishwe mbele ya sheria.Sintajali
kama mama yangu akifungwa kifungo
hata cha maisha,ninachojali mimi ni
haki itendeke"
"Ahsante sana
Juliana.Tunakuahidi tutafanya kila
linalowezekana kuhakisha kuwa
anatueleza kila kitu kuhusiana na vifo
hivyo.Tukiacha hayo kuna jambo
lingine ambalo tunaomba utusaidie
kulifahamu.Kuna mtu anaitwa Patrice
Lwibombe ambaye ana mahusiano na
waasi na bado hatujafahamu yuko
wapi.Tunaomba utusaidie tuweze kumfahamu ni nani na yuko wapi?
akasema Steve na Juliana akamuahidi
kulifanyia kazi suala hilo akampatia
namba za simu za mama yake na
kukata simu.Steve akampatia namba
zile Omola ili aanze kuzifanyia kazi
*****************
David na Elizabeth wakiwa garini
baada ya kuondoka katika ile nyumba
alimouliwa Frank ,simu ya David
ikaita mpigaji alikuwa makamu wa
rais Dr Shafi.David akaipokea haraka
haraka
"Hallo Dr Shafi.Nimekutafuta
sana siku ya leo bila mafanikio"
akasema David
"Toka wakati ule tumekuwa na
vikao mfululizo na rais na ndiyo maana simu yangu ilikuwa
imezimwa.Vipi maendeleo huko?
"Huku mambo yanakwenda
vyema .Tayari moto umewashwa na
unaendelea kusambaa kila sehemu na
hadi kufikia kesho baadhi ya mikoa
maandamano yataanza na ndani ya
muda mfupi nchi nzima itakuwa
imesambaa maandamano"
"Vizuri sana,nafurahi kusikia
hivyo.Katika kikao tulichokaa na rais
hakuna jambo lolote ambalo
wameligundua hadi sasa.Rais
ameelekeza kwamba wale wote
walioandaa machafuko haya akina Dr
Makwa na wenzake watiwe nguvuni
na ameagiza jeshi la polisi kutotumia
nguvu kubwa ili kuepuka maafa zaidi
kwani hadi jioni hii taarifa za vifo ni
watu arobaini na mbili na polisi kumi
na watatu.Mnatakiwa kuendelea
kushawishi vurugu zaidi na
nimerejesha zile kompyuta mahala
pake.Mama bado hajarejea"akasema kuwalazimisha polisi watumie nguvu
kubwa.Vipi wanajeshi wako
tayari?akauliza Dr Shafi
"Dr Shafi kabla hatujafika huko
nataka kufahamu kuhusiana na
Meshack Jumbo.Tayari
amepatikana?Ni muhimu sana kwetu
kumpata yule mzee"
"I'm sorry David.Taarifa
nilizozipata mara tu baada ya kutoka
katika kikao ni kwamba wale vijana
niliowatuma kwenda kumchukua
Meshack wamekutwa wameuawa
katika hoteli moja.Ninasubiri taarifa
rasmi ili tujue wamekufaje na
uchunguzi uanze mara moja.Mpaka
sasa Meshack Jumbo hajakamatwa na
hajulikani alipo"
"Oh my God !! akasema David
"I'm so sorry David lakini
ninakwenda kuunda timu nyingine
usiku huu na watamtafuta Meshack usiku kucha hadi
apatikane.Hakutapambazuka kesho
kabla Meshack Jumbo
hajapatikana.Naomba uniamini"
akasema Dr Shafi
"Ninakuamini Dr Shafi lakini
nakusistiza tena kwamba Meshack ni
muhimu mno kwetu kwani anazo
taarifa za muhimu sana kuhusiana na
Elvis.Huyu kijana tuna wasiwasi
mkubwa yuko hai bado.Taarfa za
kuonekana kwake zinatuumiza vichwa
sana na hatuwezi kuzipuuza.Endapo
ni kweli huyu jamaa yuko hai basi
mipango yetu inaweza kushindikana
ndiyo maana ninahitaji kumpata
Meshack Jumbo ili kujiridhisha kuwa
Elvis yuko hai au amefariki na
kuzikwa"
"Nitajitahidi David na kwa timu
nitakayoiunda ninaamini hadi kufika asubuhi tayari tutakuwa tumempata
Meshack na kuufahamu ukweli"
"Good.Kuhusu wanajeshi
kumetokea tatizo kidogo lakini
haliwezi kutuzuia katika mipango
yetu.Kuna mtu mmoja anaitwa
Brigedia Frank Kwaju ambaye alikuwa
anashughulikia kuandaa wanajeshi
watakaochukua nchi na tayari kila kitu
amekwisha kiweka vizuri ila kwa
bahati mbaya jioni hii tumekuta
ameuawa.Hili si tatizo sana kwani
hata mimi ninaweza kulishughulikia
hilo la wanajeshi"
"Nani kamuua?Unadhani kifo
chake kimesababishwa na hili suala
letu? akauliza Dr Shafi kwa wasiwasi
"Bado hatufahamu nani kamuua
ila tunafanya uchunguzi wa haraka
kumbaini muuaji"
"David mnapaswa kuwa makini
mno.Muuaji huyo anapaswa atafutwe haraka sana na apatikane tujue kwa
nini kamuua huyo Frank.Huu si wakati
wa kufanya mzaha hata kidogo.Jambo
hili likivuja we'll all go down.Tafadhali
kuweni makini sana.Mimi
nitawasiliana nawe muda wowote
nitakapopata jambo ambalo naamini
linatufaa"akasema Dr Shafi
wakaagana na kukata simu
"Bad news" akasema David
"Meshack Jumbo bado
hajapatikana mpaka mida hii.Ile timu
iliyotumwa kwenda kumkamata wote
wamekutwa wamekufa" akasema
David na Elizabeth akaupiga usukani
kwa hasira
"Damn it !!!
"Kwa nini kila tunachokipanga
hakiendi tunavyotaka?Kuna tatizo
gani?Lakini haya yote yanatokea kwa
sababu ya kukosa umakini.Laiti
ningelishughulikia suala hili mwenyewe haya yote
yasingejitokeza.It was my mistake and
now I have to fix it!! akasema kwa
hasira.Safari ikaendelea kimya kimya
na baada ya muda Elizabeth akauliza
"Meshack Jumbo is well
protected.Hatutaweza kumpata
kirahisi kama anavyosema huyo
makamu wako wa rais.Unafahamu
alipozikwa Elvis?
"Kwa taarifa nilizo nazo ni
kwamba Elvis amezikwa katika
makaburi ya Mkwajuni"
"Are you sure?
"Hivyo ndivyo niliambiwa"
akasema David.
"You are not sure.Ndiyo maana
mambo yanakwenda
kombo.Hamjiamini na kila
mnachokifanya.Niliwaamini nikijua
mtaweza kuhakikisha kila kitu
kinakwenda vyema lakini hakuna mlichokifanya,kila kitu kinakwenda
hovyo.Nakuonya David kama
operesheni hi itashindikana I'll Kill
you.Sikutanii katika hili.Tazama
mwenzako Frank ameuliwa kikatili
kutokana na uzembe wake.Kutokuwa
kwake makini kumegharimu maisha
yake" akasema Elizabeth kwa hasira
na kuchukua simu akampigia Juliana
"Juliana uko nyumbani?
"Ndiyo mama niko na wageni"
"Sawa mimi nimetoka kuna mtu
nimekuja kuonana naye nitachelewa
kidogo.Uko karibu na Patricia?
"Samahani mama sikukujulisha
mapema kutokana na kutingwa na
wageni,Patricia amekwisha ondoka"
"Ameondoka?Amekwenda wapi?
"Ameitwa na rais akaishi
ikulu.Patricia ni daktari wa mke wa
rais hivyo kufuatia kifo cha mume
wake rais na mke wake wakaona ni vyema endapo watamchukua na
kuishi naye ikulu"
"Oh sawa.Kuna jambo nataka
unisaidie kama unaweza kulifahamu"
"Jambo gani mama?
"Unafahamu Elvis mume wa
Patricia amezikwa katika makaburi
gani?
"Elvis amezikwa makaburi ya
Mkwajuni.Kwani kuna nini mama?
"Kuna mtu nilikuwa nazungumza
naye hapa anamfahamu Elvis na
hakujua amezikwa wapi.Endelea
kukaa na wageni nitakuja muda si
mrefu sana" akasema Elizabeth na
kukata simu
"Tunaelekea makaburi ya
Mkwajuni kutafuta ukweli kuhusu
Elvis.Tutalifukua kaburi lake ili tujue
kama kweli yuko hai au alifariki
dunia"
"Madam...." David sitaki ushauri wowote
kwa sasa nimeamua kuushika usukani
na kila kitu kitakwenda kama
ninavyotaka mimi.Vijana watakwenda
kutafuta zana na tutalifukua kaburi
kuubaini ukweli" akasema Elizabeth.
Walifika Rosana hotel wakapata
chakula wakati walinzi wao
wanakwenda kutafuta zana na
waliporejea wakaondoka kuelekea
makaburi ya Mkwajuni kutafuta
ukweli kuhusu Elvis
*******************
Wakati Omola akiendelea
kuwatafuta David na Elizabeth kwa
kutumia programu yake, Elvis na
Steve wakaenda kumtazama Meshack
Jumbo ambaye alikuwa amezinduka
na kujiegemeza ukutani. "Mkurugenzi" akasema Elvis na
Meshack Jumbo akamtazama kwa
macho makali yaliyojaa hasira
"Elvis ni wewe kweli
unayenifanyia mimi hivi?akauliza
"Samahani sana mzee wangu
lakini sikuwa na namna nyingine ya
kufanya zaidi ya kukufungia
humu.Mzee tumetafakari mimi na
wenzangu na tumeamua kulimaliza
suala usiku wa leo na halafu
utamtaarifu rais kama ulivyokuwa
unahitaji.Kabla hatujafanya hivyo
tunapaswa kuwa na ushahidi wa
kutosha usio na shaka yoyote
kuhusiana na jambo hili na vile vile
kuwapata wahusika wakuu wote.Kwa
hiyo mzee tunakwenda kuwatafuta
David na Elizabeth ambao ndio vinara
katika mpango huu wa
mapinduzi.Tunaamini kuwa
tukiwapata hawa basi mpango wote utakuwa umefika mwisho.Wakati
mimi na Steve tukienda kuwatafuta
akina David kuna jambo nataka nawe
ulifanye" akasema Elvis na
kumtazama mzee Jumbo
"Unataka nifanye nini? akauliza
"Tunaye hapa ndani Dr Makwa
Tusangira mwenyekiti wa chama
kikuu cha upinzani hapa nchini na
ametueleza kila kitu kuhusiana na
mpango huu namna
walivyoupanga.Nimemuahidi
kumsaidia kumuondoa katika kesi hii
endapo atakubali kushirikiana
nasi.Tayari amekwisha piga simu kwa
washirika wake na kuzuia mipango
yote isiendelee na sasa kuna kitu
nataka akifanye.Nataka awapigie simu
wakuu wenzake wa vyama vya siasa
ambao hivi sasa wamejificha sehemu
mbali mbali na awatake wakutane
katika hoteli ambako hukutana kwa ajili ya mikutano yao na wakifika hapo
wote watiwe nguvuni"
"Unataka niombe msaada wa
polisi?akauliza Meshack
"Hapana mzee.Hili suala bado
halijafika mahala pa kuwajulisha
polisi.Baada ya kuhakikisha kwamba
tumepata kila tunachokihitaji ndipo
tutawajulisha jeshi la polisi na
kuwakabidhi watuhumiwa wote kwao
ili taratibu nyingine
zianze.Utakachofanya utatuma vijana
wako ambao watakwenda katika hiyo
hoteli na kuwatia nguvuni wanasiasa
wote halafu watafungwa mahala pa
siri ili tuweze kuwafanyia mahojiano
na kuupata ukweli na kukusanya
ushahidi zaidi"
"Huo ni mpango mzuri.Let's end
this" akasema Meshack Jumbu huku
akijitahidi kuinuka na Steve
akamsaidia Nimechoka sana nadhani muda
wa kupumzika umekaribia.Baada ya
suala hili kumalizika nitaanza taratibu
za kustaafu kwani umri wa kustaafu
kwa hiyari umekwishafika" akasema
Meshack Jumbo halafu wakatoka mle
chumbani wakaeleka katika chumba
alimokuwamo Dr Makwa Tusangira
"Am I free to go now? akauliza Dr
Makwa baada ya akina Elvis kuingia
mle ndani
"Not yet Dr Makwa.Kuna suala
nataka ulifanye.Nataka uwapigie simu
wenzako wote mlioandaa
maandamano haya ambao hivi sasa
wamejificha sehemu mbali mbali na
uwatake mkutane katika hoteli
ambayo huwa mnakutana kupanga
mipango yenu."
"Unataka kufanya nini ?akauliza
Dr Makwa kwa wasi wasi Are you going to do it or
not?akauliza Steve huku akimsogelea
na Dr Makwa akaogopa
"NItafanya hivyo mnavyotaka ila
naombeni mtunze ahadi yenu ya
kunisaidia" akasema Dr makwa na
kuchukua simu yake akaanza
kuwasiliana na wenzake
"Mzee wakati Dr Makwa
anawasiliana na wenzake tuma timu
ya vijana iende hapo hotelini ili
kujiweka tayari na muda wowote
watakapokuwa wametimia utawapa
maelekezo wawatie nguvuni" akasema
Elvis na mara simu ya Steve ikaita
alikuwa ni Juliana
"Hallo Juliana" akasema Steve
"Steve kuna kitu kimetokea muda
si mrefu sana nimeona
nikujulishe.Mama kanipigia simu
akaniuliza mahala alikozikwa Elvis nikamuelekeza.Sijui ameuliza hivyo
kwa lengo gani hasa" akasema Juliana
"Ahsante sana Juliana kwa taarifa
hizo ambazo naamini zitatusaidia
sana.Vipi kuna kitu chochote
umekigundua kuhusu Patrice
Lwibombe?
"Hapana bado.Nitakujulisha
nitakapopata jambo lolote" akasema
Juliana
"Sawa Juliana na sisi tunaendelea
na lile zoezi na likikamilika
tutakujulisha"
"Steve naomba msitumie nguvu
kubwa sana wakati mnamkamata
mama" akaomba Juliana
"Tutalizingatia hilo" akajibu
Steve na kukata simu
"Juliana anadai kwamba mama
yake amempigia simu na kumuuliza
kuhusu mahala alikozikwa
Elvis"akasema Steve na mara akatokea Omola na kuwaita
wakaelekea sebuleni
"Kuna mambo mawili
nimeyapata.Kwanza David na
Elizabeth wote wako sehemu moja."
akasema na kuwaonyesha akina Elvis
mahala walikokuwapo akina David
"Haya ni maeneo ya Mpeteni na
huku ndiko yaliko makaburu ya
Mkwajuni ambayo muda si mrefu
Elizabeth alikuwa anamuuliza Juliana"
akasema Steve
"Jambo la pili nimepata tena
mazungumzo kati ya makamu wa rais
na David" akasema Omola na
kuyacheza mazungumzo yale ya
makamu wa rais na David.
"Ahsante sana Omola kwa
msaada wa proigramu hii kwani
tumeweza kupata mambo ambayo
ingetuchukua muda mrefu
kuyafahamu.Kumbe tayari kunawanajeshi wameandaliwa kuchukua
nchi.Hawa jamaa wamejipanga na
wamedhamiria kweli kuchukua
nchi.Kumbe Frank alikuwa ni mtu
muhimu sana kwao kwani ndiye
aliyefanikiwa kuwashawishi
wanajeshi wakubali kufanya uasi na
kuchukua nchi.Watu hawa ni
wanyama sana na hawapaswi
kuonewa huruma.Tuwawahi kabla
hawajaendelea na mipango yao zaidi"
akasema Elvis
"Kufuatia mazungumzo hayo ya
David na Dr Shafi kuna kitu
nimekipata.David na Elizabeth
wanataka kwenda katika makaburi ya
Mkwajuni ili kujiridhisha kama kweli
nimekufa"akasema Elvis
"Unadhani wanataka kufukua
kaburi?Meshack Jumbo akauliza
"Bila shaka lengo lao ni
hilo.Tunatakiwa kufanya haraka kuwawahi" akasema Elvis wakaanza
kujiandaa haraka haraka.walichukua
kila walichoona kingeweza kuwafaa
halafu wakaondoka wakimuacha
Omola alinde usalama pale nyumbani
******************
Makaburi ya Umoja Mkwajuni ni
makaburi mapya kabisa ambayo
yalikuwa katika mfumo mpya wa
kulipia hivyo kupafanya mahala hapo
kuwa sehemu nzuri na ya kuvutiwa
kutokana na uangalizi wake
mzuri.Eneo la ndani ya makaburi
kulipangwa vizuri na bado maboresho
yalikuwa yanaendela ili kupafanya
mahala pale pavutie zaidi ikiwa ni
pamoja na kuweka taa ili hata usiku
shughuli za mazishi ziweze kufanyika. David na Elizabeth wakiwa na
walinzi wao wakawasili katika
makaburi yale na kuelekea moja kwa
moja katika geti la walinzi
"David stay in the car.Let me
finish this" akasema Elizabeth na
kushuka garini akawafuata wale
walinzi,akawasalimu na wakataka
kufahamu shida yake
"Samahani ndugu zangu,ninaitwa
Sarah ninaishi Dubai.Nilipata taarifa
za kifo cha rafiki yangu ikanibidi
kufunga safari kutoka Dubai kufika
hapa kumbe tayari amekwisha
zikwa.Kesho ninasafiri kurejea Dubai
alfajiri na mapema hivyo nimekuja
hapa ili niweze kupata nafasi walau
nilione na kuweka maua katika kaburi
lake.Tafadhalini naombeni mnisaidie"
akasema Elizabeth kwa sauti ya upole
iliyowafanya walinzi wale waamini
alichokuwa anakisema Mama kwanza pole sana kwa
msiba wa rafiki yako,lakini hapa tuna
taratibu zetu zilizowekwa.Ikifika saa
moja jioni haruhusiwi mtu yeyote
kuonekana ndani ya eneo la makaburi
kwani bado hakuna taa.Tungeweza
kukuruhusu ukaingia huko lakini
wakuu wetu wakikukuta huko sisi
hatutakuwa na kazi tena" akasema
mmoja wa jamaa aliyeonekana kama
ndiye mkubwa wa zamu ile ya ulinzi
"Jamani nawaombeni
mnisaidie.Sintachukua muda mrefu"
akabembeleza Elizabeth
" Hapana mama hatutaweza
kukusaidia kwa hilo kwani tunalinda
ajira zetu.Tafuta wakati mwingine
uweze kuja kuliona kaburi la rafiki
yako" akasema yule jamaa.Elizabeth
akafungua mkoba wake na kutoa
bunda la noti akampatia yule mkubwa ambaye alitumbua macho asiamini
alichokiona.
"Kwani ndugu yako anaitwa
nani? akauliza yule jamaa huku
akiingia katika ofisi yake na kuzifungia
fedha zile katika droo
"Anaitwa Elvis"
Yule jamaa akafungua kitabu
chake kikubwa chenye orodha ya
watu wote wanaozikwa hapo
akalitafuta jina la Elvis akalipata
"Anaitwa Elvis Tarimo.Amezikwa
kitalu B.Twende nikupeleke" akasema
yule jamaa na kuchukua funguo
akamtaka mwenzake aliyekuwa naye
aendelee kulinda wakati yeye
akimpeleka Elizabeth
ndani.Alipofungua tu geti ghafla
Elizabeth akatoa bastora yenye
kiwambo cha kuzuia sauti na
kumtandika risasi mbili akaanguka
chini halafu akamgeukia yule mwenzake naye akampiga risasi ya
kichwa akaanguka chini kisha
akawaita vijana wake wakawabeba
wale walinzi na kuwaficha ndani
katika maua.Ndani kulikuwa na vibao
vya maelekezo,kulikuwa na kibao
kinaelekeza kitalu A na kingine
kinaonyesha kitalu B wakafuata njia
inayoelekea kitalu B wakayakuta
makaburi na kisha wakaanza
kulitafuta kaburi la Elvis
wakalipata.Tayari lilikuwa limejengwa
kwa ustadi na kuwekwa urembo na
kulifanya livutie sana.Haraka haraka
Eizabeth akawaelekeza wale vijana
waliokuwa na vifaa waanze kulibomoa
lile kaburi.
"David muda si mrefu
tutaufahamu ukweli" akasema
Elizabeth ambaye hakuwa na hata
chembe ya wasi wasi tofauti na David
ambaye alikuwa mkimya na alionekana mwenye woga
mwingi.Haikuwa kazi nyepesi
kulitindua zege lile lililotumika
kufunika kaburi na baada ya kuona
kazi inazidi kuwa ngumu,Elizabeth
akaamuru kaburi lichimbwe kwa
pembeni .
Elvis na Steve waliwasili katika
makaburi ya Mkwajuni,wakaegesha
gari lao mita kadhaa kutoka eneo lile
la makaburi halafu wakatembea kwa
miguu kulifuata geti huku
wakiendelea kupewa maelekezo na
Omola aliyekuwa akiwafuatilia akina
David kupitia kompyuta yake.Walifika
karibu na geti la kuingilia ndani na
wakayakuta magari mawili
yameegeshwa nje.
"Haya lazima ni magari yao"
akasema Elvis kisha akamtaka Steve
amkinge, akatembea kwa tumbo
kuelekea eneo kulikoegeshwa zile gari mbili.Akazifikia na kuchungulia ndani
hakukuwa na mtu yeyote kisha kwa
kutumia bastora yake yenye kiwambo
cha sauti akayapiga risasi matairi
kadhaa yakatoka upepo halafu
akarejea kwa Steve
"Elvis hapa kuna ulinzi lakini
sijaona hata mlinzi mmoja katika
sehemu yao" akasema Steve
"Hiyo ni ishara kuwa tayari
wamekwisha wateka au
kuwaua.Twende ndani" akasema Elvis
wakatembea kwa tahadhari hadi
katika ofisi ya walinzi ambayo ilikuwa
tupu na Steve akagundua kitu.
"Damu!!.Inaonekana tayari
walinzi wamekwisha uawa" akasema
Steve wakaingia ndani ya
makaburi.Kulikuwa giza lakini Steve
alifahamu mahala alikozikwa Elvis
akamuongoza wakatembea kwa
tahadhari kubwa.Mara kwa mbali wakaona mwangaza wa tochi na
vishindo vya watu kuchimba kitu
kigumu
"We got them.Wanaharibu kaburi
wanataka kujua kama nimo kaburini
ama vipi" akasema Elvis kwa sauto
ndogo.Wakapeana maelekezo namna
ya kuwakabili watu wale kisha kila
mmoja akapita sehemu yake wakiwa
wanatambaa kwa tumbo kuelekea
sehemu walipo wale jamaa
Kazi ya kulichimba kaburi la Elvis
iliendelea kwa kasi huku Elizabeth
akiwahimiza wafanye kwa bidii
kubwa.Alikuwa amesimama pembeni
kidogo akiwa na David huku bastora
yake ikiwa mkononi.Sehemu kubwa
ya juu ilikwisha ondolewa
"Aliyejenga kaburi hili anastahili
pongezi" akasema David
"Nadhani alifahamu kuwa
hakuna mtu ndani yake ndiyo maana akajen....." kabla hajamaliza sentensi
yake zikasikika sauti za risasi kutoka
katika bastora yenye kiwambo na
vijana wanne waliokuwa wakichimba
kaburi lile la Elvis wakaanguka chini.
"What happened? akauliza David
kwa wasi wasi huku yeye na Elizabeth
wakichuchumaa chini
"Stanley !! akaita Elizabeth lakini
mara akajikuta akiguswa na kitu cha
baridi sikioni mwake.
"Tupa chini silaha yako na uinue
mikono yako juu!!! ikamuamuru sauti
kali kutoka nyuma yake.Elizabeth alitii
amri aliyopewa na kunyoosha mkono
wake taratibu kuipeleka chini bastora
yake lakini ghafla akageuka na kutaka
kumkabili yule jamaa aliyekuwa
nyuma yake ambaye ni Elvis lakini
Steve alikiona kitendo kile na kuachia
risasi tatu zilizotua katika kiganja cha
mkono ule wenye bastora akaanguka chini.Elvis akamuwahi na
kumkanyaka kichwani huku Steve
akiwahi kumdhibiti David
Bila kupoteza muda Steve akatoa
pingu na kumfunga Elizabeth halafu
wakamwagia dawa katika jeraha lile la
risasi mkononi mwa Elizabeth ili
kuzuia damu kutoka kwa wingi na
kisha wakamchoma sindano ya
usingizi na hazikuputa sekunde
kadhaa akalala.Steve akamuweka
begani Elvis akamuongoza David
wakaondoka
"Jamani msiniue..msiniue
jamani..Mimi ni waziri mkuu
mstaafu..Ninazo fedha nying............"
"Shut up!! akafoka Elvis
Wakatoka nje ya eneo la
makaburi na Steve akaenda kulileta
gari lao wakawapakia Elizabeth na
David wakaondoka "Tumewapata kirahisi sana
tofauti na nilivyokuwa nimetegemea."
akasema Steve
"Hakuna lenye mwanzo likakosa
mwisho.Baada ya muda mrefu wa
kuishi kama wako peponi sasa ni
muda wao wa kuishi kama wako
motoni hasa huyu mwanamke leo
atajuta kuzaliwa binadamu!! akasema
Elvis huku akiuma meno kwa hasira
'Tafadhali vijana wangu
naombeni msiniue.Nitawapa kila kitu
mkitakacho.Niambieni mnataka nini
vijana wangu,kama fedha ninazo
nyingi sana na nitawapa kiasi
chochote mkitakacho" akasema David
aliyekuwa amefungwa mikono kwa
nyuma.Steve aliyekuwa amekaa naye
nyuma akamnasa kibao kizito
"Hii ni picha tu ya kitu
unachokwenda kukutana nacho huko
uendako" akasema Steve Walifika katika makazi yao
wakamshusha Elizabeth aliyekuwa
katika buti.Dr philip akaitwa haraka
sana ili kuja kumuhudumia kabla
hawajamfanyia mahojiano.David
akatupwa katika chumba cha stoo
"Mzee tumefanikiwa kuwapata
wote wawili,David na Elizabeth.Vipi
huku mmefanikisha lile zoezi?
akauliza Elvis
"Zoezi limefanikiwa na wote
wamekamatwa na nimewaelekeza
vijana wakawafunge katika ile nyunba
alimokuwa amefungwa Steve kisha
tutawafanyia mahojiano.Hongereni
sana vijana wangu kwa kazi hii kubwa
na ngumu.Kupitia watu hawa wawili
tutaweza kupata taarifa
zote.Tafadhalini vijana fanyeni kila
muwezalo kuhakikisha kwamba
mnapata taarifa kutoka kwao." Usijali mzee tutapata taarifa
zote."
"Vizuri.Vipi kuhusu suala la
kumtaarifu rais?akauliza Meshack
Jumbo
"Bado kuna kitu tunapaswa
kukifahamu.Ni nani aliye nyuma ya
mpango huu wa mapinduzi?Naamini
hawa jamaa hawakuwa peke yao
lazima kuna watu wako nyuma
yao.Tukiwapata hao basi tutamjulisha
rais.Kwa sasa tujielekeze katika
kupata taarifa kwa kina zaidi"
akasema Elvis halafu wakaenda katika
chumba alimo Dr Makwa
"Hallo Dr Maka" akasema Elvis
"Nimemaliza kazi
yenu.Mnanisaidiaje kuniondoa katika
sakata hili? akauliza Dr Makwa.Elvis
akamtazama kwa sekunde kadhaa
halafu akatoa kicheko kidogo cha
dharau You are so stupid Dr
makwa.After all you've done do you
think we're going to let you go?Mpaka
sasa idadi ya watu waliokufa kutokana
na vurugu ulizoziasisi
haijulikani,unataka tukuache
uondoke?Familia yako inafurahia hivi
sasa wakila na kunywa kwa raha zao
huko nje ya nchi wakati familia za
wengine hivi sasa kuna vilio baada ya
watoto wao kupoteza maisha kufuatia
vurugu ulizozianzisha kwa tamaa zako
za fedha na madaraka.You want me to
let you go!!..akasema Elvis huku
akimtazama Dr Makwa kwa hasira
"Uliniahidi hivyo kwamba
nikikueleza ukweli utanisaidia
kuniondoa katika hili sakata.Tafadhali
nakuom......" Hakumaliza sentensi yake
Elvis akamnasa kibao kizito
kilichompeleka chini.Steve akamuinua
na kumtandika kichwa kilichomfanya apepesuke na kujigonga ukutani
akaanguka chini.Akachukua panga
lililokuwa karibu lakini Elvis akamzuia
"Hatutakiwi kumuua.Huyu bado
tunamuhitaji sana.Ni shahidi muhimu
sana.Mfunge kabisa asije akajiua"
akasema Elvis halafu akampigia simu
Juliana kwa kutumia simu ya Steve
"Hallo Juliana ni mimi Elvis hapa
ninaongea.Tafadhali usitamke jina
langu kama uko na watu karibu"
"Nimekuelewa.Vipi maendeleo ya
lile zoezi mmelifanikisha? akauliza
"Zoezi tumelifanikisha lakini
mama yako ameumizwa kidogo
mkononi ila anaendelea
vyema.Daktari anakuja kumtibu
jeraha kisha tutaanza kumuhoji"
akasema Elvis
"Hongereni sana Elvis.Tafadhali
hakikisheni mumemuhoji na kupata
taarifa zote mnazozihitaji na vile vile msisahau kuhusiana na kupata taarifa
ya vile vifo"
"Tutafanya hivyo
Juliana.Umepata chochote kuhusiana
na Patrice Lwibombe?
"Hapana bado
sijafanikiwa.Nilikuwa na wageni ndiyo
maana nikakosa hata muda wa
kufanya upekuzi" akasema Juliana
"Juliana nina ombi moja
kwako.Kwa kuwa mama yako tayari
tunaye huku tunataka kufanya
upekuzi chumbani kwake ili tuone
kama tutaweza kupata kitu cha
kutusaidia katika uchunguzi wetu"
"Hakuna tatizo kabisa kuhusu
hilo.Mnakuja wote?
"Hapana anakuja Steve peke yake
mimi nitabaki hapa" akasema Elvis
"Sawa ninamsubiri hapa"
"Vipi kuhusu Patricia?Una taarifa
zozote kuhusiana na maendeleo yake? Amenipigia simu muda si mrefu
sana anadai anaendelea
vyema.Usihofu nitakuwa naye karibu
sana"
"Ahsante sana"akajibu Elvis na
kukata simu
Elvis akamuelekeza Steve aende
kwa Juliana na kufanya upekuzi
chumbani kwa Elizabeth .Dr Philip
alifika na kuanza kumuhudumia
Elizabeth ambaye bado hakuwa na
fahamu.Baada ya kulitibu jeraha lile
Elvis akamuita Omola wakaenda
sebuleni na kumtaka Dr Philip
amueleze ukweli kuhusiana na
Vicky.Omola alilia machozi mengi sana
kufuatia kifo kile cha rafiki yake
mkubwa Vicky.Elvis akamtaka aende
chumbani akapumzike
"Sasa ni muda wa kazi" akasema
Elvis akaelekea katika chumba
alimofungwa David akamtoa na kumpeleka sebuleni.Meshack Jumbo
na Dr Philip nao pia
walikuwepo.Alikuwa ameloa jasho
mwili mzima.
"Hallo mheshimiwa David.Usiwe
na hofu.Hapa tumekuleta na
tutazungumza kama marafiki.Take a
deep breath" akasema Elvis na David
akavuta pumzi ndefu
"Again take a deep breath !
"Good.Relax now.You need
something to drink?Whisky
,wine,water or coffee? akauliza Elvis
"W..wa..ter.." akasema huku sauti
yake ikikwama.Elvis akamletea glasi la
maji akamfungua pingu akanywa
"Sintakufunga tena pingu nataka
tuzungumze kwa amani.Kabla ya yote
naomba nifanye utambulisho.Huyu
pembeni yangu anaitwa Dr Philip ni
daktari kutoka idara ya ujasusi,yule
mzee pale ni mkurugenzi wa idara ya ujasusi anaitwa Meshack Jumbo
naamini mnafahamiana kwani
alihudumu pia hata katika wakati
ukiwa waziri mkuu.Mimi naitwa Elvis
Tarimo." akasema Elvis na David
akatamani ageuke upepo
apotee.Alitumbua macho na miguu
yake ikaonekana ikitetemeka
"Pale makaburini mlikuwa
mnataka kuthibitisha kama
nimekufa,I'm not dead !!
"No ! No !..I can't believe this !!
You are a ghost ! a ghost !! akapiga
ukelele wa woga.Elvis akatabasamu na
kumimina mvinyo katika glasi
akanywa
"Nadhani sasa umethibitisha
kwamba mimi ni halisi na si mzimu
kwani mzimu hauna tumbo na wala
haunywi mvinyo" Bwana ndiye mchungaji
wangu..." akasema David na Elvis
akamkatisha
"Huo ulikuwa utangulizi sasa ni
wakati wa mazungumzo.Nitakuuliza
maswali na ninaomba unijibu kila kitu
na endapo utashindwa kuonyesha
ushirikiano basi huu utakuwa ni
mwisho wako.Hauta liona tena jua la
kesho asubuhi.Hauta muona tena
mpenzi wako Samira"akasema Elvis
na kumstua sana David alipotaja jina
la Samira
"David wewe ni waziri mkuu
mstaafu,umehudumu katika jamhuri
ya muungano wa Tanzania kwa
kipindi cha miaka kumi na kabla ya
hapo umeshika nyadhifa kadhaa
katika serikali,ni mtu mwenye
heshima kubwa katika jamii na hata
sasa baada ya kustaafu siasa bado
umeendelea kuheshimika sana ndani na nje ya nchi.Kitu gani hasa
kimekushawishi utake kurejea katika
siasa?tuanzie hapo tafadhali"akasema
Elvis
"Mimi..." akasema David na sauti
ikakwama akakohoa kidogo
kurekebisha koo halafu akaendelea
"Mimi nimekwisha staafu siasa
na sijihusishi tena na mambo hayo"
akajibu David
"Tunafahamu umestaafu siasa
lakini kwa siku za hivi karibuni
umerejea tena katika siasa kwa
mlango wa nyuma na umekuja na
mikakati mizito ya kuhakikisha
unakuwa rais wa Tanzania.Swali langu
nini au nani kakushawishi urejee tena
katika siasa tena safari hii ukitaka
kushika nafasi kubwa zaidi ya uongozi
pasi na kufuata taratibu?
Swali lile likambabaisha David. Jibu David nani kakushawishi
urejee tena katika siasa wakati
umekwisha staafu?
"Si kweli kwamba ninataka
kuwania urais.Mambo hayo
nimekwisha achana nayo" akasema
David
"David inuka twende! akasema
Elvis na kumshika mkono David
akampeleka katika chumba alimo Dr
Makwa.
"Unamfahamu huyu? akauliza
Elvis.David alipatwa na mstuko
mkubwa na ghafla sehemu ya mbele
ya suruali yake ikaloa alikuwa
amejisaidia haja ndogo.Hakutegemea
kabisa kumkuta Dr Makwa mle
chumbani
"Unamfahamu huyu? akauliza
Elvis
"Uhhm..uhhmm..." David
akajiuma uma na kushindwa kutoa jibu.Elvis akamnasa kibao kikali
kilichompeleka chini kwani miguu
yake haikuwa na nguvu.
"Unamfahamu huyu?
"Ndiyo" akajibu David kisha Elvis
akamrejesha sebuleni
"Dr Makwa tumemchukua
nyumbani kwako na tayari ametueleza
kila kitu kuhusiana na mipango yenu
yote.Mpaka dakika hii maandamano
na mipango yote ya vurugu
imesitishwa na aliyefanya hivyo ni
muandaaji mkuu wa maandamano
ambaye ni Dr Makwa.Mpaka dakika hii
wenyeviti wote wa vyama vya siasa
ambao wameshiriki katika
kuhamasisha vurugu za leo
wamekwisha kamatwa na
wanakwenda kuhojiwa kuhusiana na
mipango yenu ya kuiangusha
serikali.Its over David.Kila kitu kimekwisha.Tamaa zako zote
zimekutokea puani." akasema Elvis
"I'm sorry." akasema David huku
akiweweseka kama mwendawazimu
"David hili nikosa la uhaini na
unafahamu adhabu ya kosa kama
hili.Awali ilikuwa ni kifo lakini kwa
sasa ni adhabu ya maisha
gerezani.Usiku huu nitakukabidhi kwa
vyombo husika ili taratibu za
kuwafungulia mashitaka wewe na
wenzako zianze mara moja kwani
tayari tunao ushahidi wa kutosha wa
mipango yenu miovu.Tunafahamu kila
kitu unachokipanga wewe na wenzako
akiwamo makamu wa rais Dr Shafi."
David akazidi kuchaganyikiwa
alipopewa habari za Dr Shafi
"Tunafahamu kuwa wewe ndiye
uliyempa maelekezo Dr Shafi kwamba
mimi niuawe,wewe ndiye
uliyemuelekeza Dr Shafi,mzee Meshack Jumbo auawe pia.Tunazo
rekodi za mazungumzo yako yote ya
simu na Dr Shafi na muda si mrefu
makamu wa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania atatiwa
mbaroni kwa tuhuma za uhaini.It's
over David but I can help you if you
choose to cooperate with
me.Ninaweza kukusadia David
kuondokana na adhabu inayoweza
kukukabili endapo utafikishwa mbele
ya vyombo vya sheria"
"Please help me!! akasema David
huku ameloa jasho kama vile
amemwagiwa ndoo ya maji
"What do you want? Kitu
chochote nitakupa tafadhali naomba
unisaidie"akasema David
"Nataka kufahamu jambo moja
tu.Nani walio nyuma ya mpango
huu?Nani wanafadhili mapinduzi
haya? akauliza Elvis Nitakuwa na uhakika gani
kwamba utatimiza ahadi yako ya
kuniondoa katika jambo hili?akauliza
David
"Right now I'm your only hope so
you either choose to tell me what I
want or to end your life in prison"
akasema Elvis
"Ok ok nitakueleza"
"I real dont know them ila
nilialikwa katika kikao na Frank na
huko ndiko nilikowakuta watu fulani
wawili wenye asili ya kiarabu na
wakajieleza kwamba wao ni
wawakilishi wametumwa na mataifa
makubwa ambayo chumi zake
zinategemea mafuta"David
akawaeleza akina Elvis kila kitu
kilicotokea katika kikao kile cha
kwanza ambapo mipango ya
mapinduzi ilianza kuandaliwa Baada ya mkutano huo ndipo
kila kitu kikaanza"akaendelea
"Nilimfuata makamu wa ais Dr
Shafi na kumshawishi akubali
kujiunga nasi ili hapo tutakapokuwa
tumeichukua nchi yeye aweze kuwa
rais wa Zanzibar.Vile vile
nikawashawishi viongozi wa vyama
vya siasa kuanzisha maandamano na
vurugu na wakati huo huo baadhi ya
wanajeshi walikuwa wanaandaliwa ili
kuweza kuchukua nchi pale vurugu
zitakapokuwa zimezidi."David
akaeleza mipango yao yote
waliyokuwa wameipanga
"David maelezo yako marefu
lakini bado swali langu hujalijibu.Ni
nani hawa ambao walileta mpango
huu kwenu?
"Nilichowaeleza ni kitu cha kweli
kabsa.Watu hao siwafahamu undani
wao" akasema David David this is the last chance to
save yourself.Tell me the truth"
akasema Elvis
"Elvis huu ni ukweli mtupu"
"David ninataka sana kukusaidia
lakini kwa kuwa umeshindwa
kunieleza ukweli nitalazimika
kukuunganisha na wenzako na gazeti
la kesho asubuhi litapambwa na picha
zenu wewe na makamu wa rais mkiwa
katika mikono ya polisi mkituhumiwa
kwa uhaini.Inuka haraka !! akaamuru
Elvis na David akasimama
"Elvis tafadhali usinipeleke
huko.Nisaidie tafadhali.Meshack
Jumbo I'm so sorry.Nisamehe mzee
wangu !! akasema David.Elvis
akamtaka amfuate
"Elvis kuna kitu nimekikumbuka"
"Sema haraka"
"Watu wale siwafahamu kiundani
lakini huyu mwanamke Elizabeth mliyenikamata naye anawafahamu na
ndiye aliyewaelekeza kwa Frank."
akasema David na Elvis akamtaka
aketi na amueleze kwa kituo
kuhusiana na Elizabeth kujihusiaha na
mpango ule wa mapinduzi
"Elizabeth alinipiga simu na
kunitaka nikamuone akanieleza
kwamba amekuja kwenye mazishi ya
mumewe Deusdedith.Elizabeth
akanieleza kwamba watu wale yeye
ndiye aliyewatuma.Alisema kwamba
kabla ya kuja huku watu wale
walimfuata kwanza yeye na wenzake
wakawaeleza kuhusu mpango wao wa
kuipindua serikali na ndipo
alipomuelekeza Frank aanze kuandaa
timu itakayoandaa
mapinduzi.Elizabeth ndiye
anayewafahamu watu hao ni akina
nani,mkimuhoji yeye atawaeleza kila
kitu" Ok good.Umekuwa rafiki
mkubwa wa Elizabeth.Tueleze
anajishughulisha na mambo gani?
"Elizabeth ni mfanya biashara
mkubwa.Anazo biashara katika nchi
mbali mbali duniani"
"Nafahamu ni mfanya biashara
lakini nafahamu kuna ambo
anajihusisha nayo tofauti na biashara
.Ni mambo gani hayo?Nieleze
tafadhali.Ukweli wako ndiyo msaada
wako"
David akainamisha kichwa
akafikiri kwa muda kisha akasema
"Elizabeth anajihusisha na
magenge ya kimafia.Mumewe
Deusdedith alikuwa kiongozi wa
genge mojawapo na baada ya kufariki
Elizabeth ameshika uongozi.Fedha
zake nyingi anazipatia katika biashara
zake hizi.Ana mtandao mkubwa katika nchi mbali mbali.Mkimuhoji
atawaeleza ukweli."
"Unamfahamu Patrice
Lwibombe?
"Patrice Lwibombe?akauliza
David
"Ndiyo .Unamfahamu?
"Lwibombe ni mtoto wa
aliyekuwa kiongozi wa kikundi kimoja
cha waasi wa Congo ambaye
amefungwa kifungo cha maisha nchini
Congo.Baada ya baba yake kufungwa
Patrice ameendeleza mapambano
dhidi ya serikali ya Congo"
"Anaishi wapi Patrice?
"Kwa taarifa nilizonazo Patrice
anaishi nchini Ubelgiji"
"Ahsante sana kwa taarifa hizo
David sasa nenda kapumzike na
tutaendelea nawe baadae" akasema
Elvis na kumpeleka David chumbani.
Sehemu 72
"Dr Philip endelea kushughulikia
kila kitu kuhusiana na kuuhifadhi
mwili wa Vicky kuna suala
tunaendelea kulishughulikia na baada
ya kukamilika tutaungana nawe hapo
hospitali.Mpe pole sana Winnie"
akasema Elvis na kukata simu
"One soulder down......." akasema
Steve
"But we have to continue
fighting.We must save president.."
akasema Elvis na ukimya wa zaidi ya
dakika mbili ukapita kila mmoja
akitafakari lake kisha Elvis akasema
"She's gone too soon
.Tulimuhitaji sana Vicky katika wakati
huu" akasema na kunyamaza
akatazama chini kwa muda kisha
akainua kichwa na kusema
"Steve kwa heshima ya Vicky
lazima tuhakikishe tunalimaliza suala
hili usiku wa leo.Tuhakikishe kwamba tunawapata wale wote
wanaojihusisha na biashara ya silaha
na vile vile kuwapata wale wote
waasisi wa machafuko haya
yaliyoanza leo yenye lengo la
kuiondoa serikali madarakani."
akasema Elvis sura yake ikiwa na
hasira za hali ya juu
"Kuna watu wawili tu ambao
tukiwapata wataweza kutoa majibu ya
maswali yetu yote ambao ni David na
Elizabeth.Hawa wanafahamu kila
kitu.David anafahamu nani yuko
nyuma ya mpango wa mapinduzi na
Elizabeth atatusaidia kufahamu
mtandao wote unaojihusiaha na
biashara ya silaha"akasema Steve
"Kila kitu kinamalizika usiku wa
leo!! akasema Elvis
"Vipi kuhusu
Omola.Tutamwambiaje kuhusu Vicky? Hatutamwambia kitu chochote
kwa sasa hadi hapo tutakapokuwa
tumemaliza misheni yetu" akasema
Elvis kisha wakamfuata Omola
aliyekuwa chumbani akijipumzisha
"Vipi hali ya Vicky? akauliza
Omola
"Bado hatujapokea tararifa
zozote kutoka kwa Dr
Philip.Tunaamini atapona.Omola
kuna jambo ambalo tumeamua
kulifanya usiku huu.Baada ya
kugundua kwamba watu wanaopanga
mpango wa kuipindua serikali ni wale
wale wanaojihusiaha na biashara ya
silaha tumeamua tuwakamate wote na
kuwafikisha sehemu
husika.Operesheni yetu tunaimaliza
usiku wa leo.Watu pekee ambao
tunaamini wanaweza wakatupa
majibu ya maswali yetu yote ni wawili
tu,David na Elizabeth.Tukiwapata hawa tutamaliza kila kitu.Kwa hiyo
tunataka kwanza kuwafahamu mahala
walipo.Tuliwatumia ujumbe kupitia
simu ya Frank ili wakutane sehemu
moja na ninaamini wote watakuwa
wamekutana mahala hapo na
yawezekana hadi muda huu tayari
watakuwa wamegundua kwamba
Frank amekufa.Kifo cha Frank
kitawafanya wabuni mbinu mpya za
kuendeleza mipango yao lakini kabla
hawajafanya hivyo wanatakiwa wawe
katika mikono yetu" akasema Elvis
"Itabidi tupate namba za simu
anayotumia Elizabeth ili tuweze
kumfuatilia na kujua mahala
alipo.Namba za David tunazo tayari"
akasema Omola na Elvis akamtaka
Steve ampigie simu Juliana
"Hallo Steve.Nimefika salama na Juliana baada ya kupokea simu ya
Steve
"Hilo ni jambo jema sana.Juliana
nimekupigia kujua kama umefika
salama vile vile kukujulisha jambo
moja."
"Nakusikiliza Steve"akasema
Juliana
"Tumeamua kumaliza kila kitu
usiku wa leo.Tumegundua kwamba
mama yako Elizabeth au vyovyote vile
anavyoitwa anahusika yeye na
mtandao wake katika vurugu za
kisiasa zinazoendelea hivi sasa
zilizopelekea vifo vya vijana wengi
huko mtaani.Lengo lao kuu ni
kuipindua serikali iliyoko
madarakani.Ukiacha hilo,tumegundua
pia kwamba mama yako anajihusisha
na biashara ya silaha kwa waasi wa
Congo.kwa hiyo basi tumeamua
kumtia nguvuni usiku wa leo na tumeona tusifanye hivyo kabla
hatujakujulisha wewe kwanza"
akanyamaza baada ya kusikia Juliana
akivuta pumzi ndefu
"Juliana are you ok?
"I'm ok Steve.Endelea"
"Tunahitaji kufahamu mahala
alipo mam a yako hivi sasa hivyo
tunaomba utusaidie kutupatia namba
yake ya simu anayotumia sasa ili
tuweze kumtafuta na kujua mahala
alipo na tumtie nguvuni"
"Steve hizi ni taarifa njema japo
zinastusha lakini tayari nilikwisha
jiandaa kwa jambo hili kwa hiyo
ninatoa baraka zangu mama
akamatwe na ahojiwe kuhusiana na
mambo yote haramu ambayo
amekuwa akiyafanya yeye na
wenzake.Kufikia hatua ya kutaka
kuipindua serikali huu ni uhalifu
uliovuka mipaka.Wanatakiwawakamatwe haraka sana.Pamoja na
hayo yote ambayo mmeyagundua
kwake lakini nahitaji sana ahojiwe
kuhusiana na vifo vya mdogo wangu
na mpenzi wangu.Ninaamini
anafahamu sababu ya vifo hivyo na
lazima atakuwa anawafahamu
wahusika hivyo awataje na
wafikishwe mbele ya sheria.Sintajali
kama mama yangu akifungwa kifungo
hata cha maisha,ninachojali mimi ni
haki itendeke"
"Ahsante sana
Juliana.Tunakuahidi tutafanya kila
linalowezekana kuhakisha kuwa
anatueleza kila kitu kuhusiana na vifo
hivyo.Tukiacha hayo kuna jambo
lingine ambalo tunaomba utusaidie
kulifahamu.Kuna mtu anaitwa Patrice
Lwibombe ambaye ana mahusiano na
waasi na bado hatujafahamu yuko
wapi.Tunaomba utusaidie tuweze kumfahamu ni nani na yuko wapi?
akasema Steve na Juliana akamuahidi
kulifanyia kazi suala hilo akampatia
namba za simu za mama yake na
kukata simu.Steve akampatia namba
zile Omola ili aanze kuzifanyia kazi
*****************
David na Elizabeth wakiwa garini
baada ya kuondoka katika ile nyumba
alimouliwa Frank ,simu ya David
ikaita mpigaji alikuwa makamu wa
rais Dr Shafi.David akaipokea haraka
haraka
"Hallo Dr Shafi.Nimekutafuta
sana siku ya leo bila mafanikio"
akasema David
"Toka wakati ule tumekuwa na
vikao mfululizo na rais na ndiyo maana simu yangu ilikuwa
imezimwa.Vipi maendeleo huko?
"Huku mambo yanakwenda
vyema .Tayari moto umewashwa na
unaendelea kusambaa kila sehemu na
hadi kufikia kesho baadhi ya mikoa
maandamano yataanza na ndani ya
muda mfupi nchi nzima itakuwa
imesambaa maandamano"
"Vizuri sana,nafurahi kusikia
hivyo.Katika kikao tulichokaa na rais
hakuna jambo lolote ambalo
wameligundua hadi sasa.Rais
ameelekeza kwamba wale wote
walioandaa machafuko haya akina Dr
Makwa na wenzake watiwe nguvuni
na ameagiza jeshi la polisi kutotumia
nguvu kubwa ili kuepuka maafa zaidi
kwani hadi jioni hii taarifa za vifo ni
watu arobaini na mbili na polisi kumi
na watatu.Mnatakiwa kuendelea
kushawishi vurugu zaidi na
nimerejesha zile kompyuta mahala
pake.Mama bado hajarejea"akasema kuwalazimisha polisi watumie nguvu
kubwa.Vipi wanajeshi wako
tayari?akauliza Dr Shafi
"Dr Shafi kabla hatujafika huko
nataka kufahamu kuhusiana na
Meshack Jumbo.Tayari
amepatikana?Ni muhimu sana kwetu
kumpata yule mzee"
"I'm sorry David.Taarifa
nilizozipata mara tu baada ya kutoka
katika kikao ni kwamba wale vijana
niliowatuma kwenda kumchukua
Meshack wamekutwa wameuawa
katika hoteli moja.Ninasubiri taarifa
rasmi ili tujue wamekufaje na
uchunguzi uanze mara moja.Mpaka
sasa Meshack Jumbo hajakamatwa na
hajulikani alipo"
"Oh my God !! akasema David
"I'm so sorry David lakini
ninakwenda kuunda timu nyingine
usiku huu na watamtafuta Meshack usiku kucha hadi
apatikane.Hakutapambazuka kesho
kabla Meshack Jumbo
hajapatikana.Naomba uniamini"
akasema Dr Shafi
"Ninakuamini Dr Shafi lakini
nakusistiza tena kwamba Meshack ni
muhimu mno kwetu kwani anazo
taarifa za muhimu sana kuhusiana na
Elvis.Huyu kijana tuna wasiwasi
mkubwa yuko hai bado.Taarfa za
kuonekana kwake zinatuumiza vichwa
sana na hatuwezi kuzipuuza.Endapo
ni kweli huyu jamaa yuko hai basi
mipango yetu inaweza kushindikana
ndiyo maana ninahitaji kumpata
Meshack Jumbo ili kujiridhisha kuwa
Elvis yuko hai au amefariki na
kuzikwa"
"Nitajitahidi David na kwa timu
nitakayoiunda ninaamini hadi kufika asubuhi tayari tutakuwa tumempata
Meshack na kuufahamu ukweli"
"Good.Kuhusu wanajeshi
kumetokea tatizo kidogo lakini
haliwezi kutuzuia katika mipango
yetu.Kuna mtu mmoja anaitwa
Brigedia Frank Kwaju ambaye alikuwa
anashughulikia kuandaa wanajeshi
watakaochukua nchi na tayari kila kitu
amekwisha kiweka vizuri ila kwa
bahati mbaya jioni hii tumekuta
ameuawa.Hili si tatizo sana kwani
hata mimi ninaweza kulishughulikia
hilo la wanajeshi"
"Nani kamuua?Unadhani kifo
chake kimesababishwa na hili suala
letu? akauliza Dr Shafi kwa wasiwasi
"Bado hatufahamu nani kamuua
ila tunafanya uchunguzi wa haraka
kumbaini muuaji"
"David mnapaswa kuwa makini
mno.Muuaji huyo anapaswa atafutwe haraka sana na apatikane tujue kwa
nini kamuua huyo Frank.Huu si wakati
wa kufanya mzaha hata kidogo.Jambo
hili likivuja we'll all go down.Tafadhali
kuweni makini sana.Mimi
nitawasiliana nawe muda wowote
nitakapopata jambo ambalo naamini
linatufaa"akasema Dr Shafi
wakaagana na kukata simu
"Bad news" akasema David
"Meshack Jumbo bado
hajapatikana mpaka mida hii.Ile timu
iliyotumwa kwenda kumkamata wote
wamekutwa wamekufa" akasema
David na Elizabeth akaupiga usukani
kwa hasira
"Damn it !!!
"Kwa nini kila tunachokipanga
hakiendi tunavyotaka?Kuna tatizo
gani?Lakini haya yote yanatokea kwa
sababu ya kukosa umakini.Laiti
ningelishughulikia suala hili mwenyewe haya yote
yasingejitokeza.It was my mistake and
now I have to fix it!! akasema kwa
hasira.Safari ikaendelea kimya kimya
na baada ya muda Elizabeth akauliza
"Meshack Jumbo is well
protected.Hatutaweza kumpata
kirahisi kama anavyosema huyo
makamu wako wa rais.Unafahamu
alipozikwa Elvis?
"Kwa taarifa nilizo nazo ni
kwamba Elvis amezikwa katika
makaburi ya Mkwajuni"
"Are you sure?
"Hivyo ndivyo niliambiwa"
akasema David.
"You are not sure.Ndiyo maana
mambo yanakwenda
kombo.Hamjiamini na kila
mnachokifanya.Niliwaamini nikijua
mtaweza kuhakikisha kila kitu
kinakwenda vyema lakini hakuna mlichokifanya,kila kitu kinakwenda
hovyo.Nakuonya David kama
operesheni hi itashindikana I'll Kill
you.Sikutanii katika hili.Tazama
mwenzako Frank ameuliwa kikatili
kutokana na uzembe wake.Kutokuwa
kwake makini kumegharimu maisha
yake" akasema Elizabeth kwa hasira
na kuchukua simu akampigia Juliana
"Juliana uko nyumbani?
"Ndiyo mama niko na wageni"
"Sawa mimi nimetoka kuna mtu
nimekuja kuonana naye nitachelewa
kidogo.Uko karibu na Patricia?
"Samahani mama sikukujulisha
mapema kutokana na kutingwa na
wageni,Patricia amekwisha ondoka"
"Ameondoka?Amekwenda wapi?
"Ameitwa na rais akaishi
ikulu.Patricia ni daktari wa mke wa
rais hivyo kufuatia kifo cha mume
wake rais na mke wake wakaona ni vyema endapo watamchukua na
kuishi naye ikulu"
"Oh sawa.Kuna jambo nataka
unisaidie kama unaweza kulifahamu"
"Jambo gani mama?
"Unafahamu Elvis mume wa
Patricia amezikwa katika makaburi
gani?
"Elvis amezikwa makaburi ya
Mkwajuni.Kwani kuna nini mama?
"Kuna mtu nilikuwa nazungumza
naye hapa anamfahamu Elvis na
hakujua amezikwa wapi.Endelea
kukaa na wageni nitakuja muda si
mrefu sana" akasema Elizabeth na
kukata simu
"Tunaelekea makaburi ya
Mkwajuni kutafuta ukweli kuhusu
Elvis.Tutalifukua kaburi lake ili tujue
kama kweli yuko hai au alifariki
dunia"
"Madam...." David sitaki ushauri wowote
kwa sasa nimeamua kuushika usukani
na kila kitu kitakwenda kama
ninavyotaka mimi.Vijana watakwenda
kutafuta zana na tutalifukua kaburi
kuubaini ukweli" akasema Elizabeth.
Walifika Rosana hotel wakapata
chakula wakati walinzi wao
wanakwenda kutafuta zana na
waliporejea wakaondoka kuelekea
makaburi ya Mkwajuni kutafuta
ukweli kuhusu Elvis
*******************
Wakati Omola akiendelea
kuwatafuta David na Elizabeth kwa
kutumia programu yake, Elvis na
Steve wakaenda kumtazama Meshack
Jumbo ambaye alikuwa amezinduka
na kujiegemeza ukutani. "Mkurugenzi" akasema Elvis na
Meshack Jumbo akamtazama kwa
macho makali yaliyojaa hasira
"Elvis ni wewe kweli
unayenifanyia mimi hivi?akauliza
"Samahani sana mzee wangu
lakini sikuwa na namna nyingine ya
kufanya zaidi ya kukufungia
humu.Mzee tumetafakari mimi na
wenzangu na tumeamua kulimaliza
suala usiku wa leo na halafu
utamtaarifu rais kama ulivyokuwa
unahitaji.Kabla hatujafanya hivyo
tunapaswa kuwa na ushahidi wa
kutosha usio na shaka yoyote
kuhusiana na jambo hili na vile vile
kuwapata wahusika wakuu wote.Kwa
hiyo mzee tunakwenda kuwatafuta
David na Elizabeth ambao ndio vinara
katika mpango huu wa
mapinduzi.Tunaamini kuwa
tukiwapata hawa basi mpango wote utakuwa umefika mwisho.Wakati
mimi na Steve tukienda kuwatafuta
akina David kuna jambo nataka nawe
ulifanye" akasema Elvis na
kumtazama mzee Jumbo
"Unataka nifanye nini? akauliza
"Tunaye hapa ndani Dr Makwa
Tusangira mwenyekiti wa chama
kikuu cha upinzani hapa nchini na
ametueleza kila kitu kuhusiana na
mpango huu namna
walivyoupanga.Nimemuahidi
kumsaidia kumuondoa katika kesi hii
endapo atakubali kushirikiana
nasi.Tayari amekwisha piga simu kwa
washirika wake na kuzuia mipango
yote isiendelee na sasa kuna kitu
nataka akifanye.Nataka awapigie simu
wakuu wenzake wa vyama vya siasa
ambao hivi sasa wamejificha sehemu
mbali mbali na awatake wakutane
katika hoteli ambako hukutana kwa ajili ya mikutano yao na wakifika hapo
wote watiwe nguvuni"
"Unataka niombe msaada wa
polisi?akauliza Meshack
"Hapana mzee.Hili suala bado
halijafika mahala pa kuwajulisha
polisi.Baada ya kuhakikisha kwamba
tumepata kila tunachokihitaji ndipo
tutawajulisha jeshi la polisi na
kuwakabidhi watuhumiwa wote kwao
ili taratibu nyingine
zianze.Utakachofanya utatuma vijana
wako ambao watakwenda katika hiyo
hoteli na kuwatia nguvuni wanasiasa
wote halafu watafungwa mahala pa
siri ili tuweze kuwafanyia mahojiano
na kuupata ukweli na kukusanya
ushahidi zaidi"
"Huo ni mpango mzuri.Let's end
this" akasema Meshack Jumbu huku
akijitahidi kuinuka na Steve
akamsaidia Nimechoka sana nadhani muda
wa kupumzika umekaribia.Baada ya
suala hili kumalizika nitaanza taratibu
za kustaafu kwani umri wa kustaafu
kwa hiyari umekwishafika" akasema
Meshack Jumbo halafu wakatoka mle
chumbani wakaeleka katika chumba
alimokuwamo Dr Makwa Tusangira
"Am I free to go now? akauliza Dr
Makwa baada ya akina Elvis kuingia
mle ndani
"Not yet Dr Makwa.Kuna suala
nataka ulifanye.Nataka uwapigie simu
wenzako wote mlioandaa
maandamano haya ambao hivi sasa
wamejificha sehemu mbali mbali na
uwatake mkutane katika hoteli
ambayo huwa mnakutana kupanga
mipango yenu."
"Unataka kufanya nini ?akauliza
Dr Makwa kwa wasi wasi Are you going to do it or
not?akauliza Steve huku akimsogelea
na Dr Makwa akaogopa
"NItafanya hivyo mnavyotaka ila
naombeni mtunze ahadi yenu ya
kunisaidia" akasema Dr makwa na
kuchukua simu yake akaanza
kuwasiliana na wenzake
"Mzee wakati Dr Makwa
anawasiliana na wenzake tuma timu
ya vijana iende hapo hotelini ili
kujiweka tayari na muda wowote
watakapokuwa wametimia utawapa
maelekezo wawatie nguvuni" akasema
Elvis na mara simu ya Steve ikaita
alikuwa ni Juliana
"Hallo Juliana" akasema Steve
"Steve kuna kitu kimetokea muda
si mrefu sana nimeona
nikujulishe.Mama kanipigia simu
akaniuliza mahala alikozikwa Elvis nikamuelekeza.Sijui ameuliza hivyo
kwa lengo gani hasa" akasema Juliana
"Ahsante sana Juliana kwa taarifa
hizo ambazo naamini zitatusaidia
sana.Vipi kuna kitu chochote
umekigundua kuhusu Patrice
Lwibombe?
"Hapana bado.Nitakujulisha
nitakapopata jambo lolote" akasema
Juliana
"Sawa Juliana na sisi tunaendelea
na lile zoezi na likikamilika
tutakujulisha"
"Steve naomba msitumie nguvu
kubwa sana wakati mnamkamata
mama" akaomba Juliana
"Tutalizingatia hilo" akajibu
Steve na kukata simu
"Juliana anadai kwamba mama
yake amempigia simu na kumuuliza
kuhusu mahala alikozikwa
Elvis"akasema Steve na mara akatokea Omola na kuwaita
wakaelekea sebuleni
"Kuna mambo mawili
nimeyapata.Kwanza David na
Elizabeth wote wako sehemu moja."
akasema na kuwaonyesha akina Elvis
mahala walikokuwapo akina David
"Haya ni maeneo ya Mpeteni na
huku ndiko yaliko makaburu ya
Mkwajuni ambayo muda si mrefu
Elizabeth alikuwa anamuuliza Juliana"
akasema Steve
"Jambo la pili nimepata tena
mazungumzo kati ya makamu wa rais
na David" akasema Omola na
kuyacheza mazungumzo yale ya
makamu wa rais na David.
"Ahsante sana Omola kwa
msaada wa proigramu hii kwani
tumeweza kupata mambo ambayo
ingetuchukua muda mrefu
kuyafahamu.Kumbe tayari kunawanajeshi wameandaliwa kuchukua
nchi.Hawa jamaa wamejipanga na
wamedhamiria kweli kuchukua
nchi.Kumbe Frank alikuwa ni mtu
muhimu sana kwao kwani ndiye
aliyefanikiwa kuwashawishi
wanajeshi wakubali kufanya uasi na
kuchukua nchi.Watu hawa ni
wanyama sana na hawapaswi
kuonewa huruma.Tuwawahi kabla
hawajaendelea na mipango yao zaidi"
akasema Elvis
"Kufuatia mazungumzo hayo ya
David na Dr Shafi kuna kitu
nimekipata.David na Elizabeth
wanataka kwenda katika makaburi ya
Mkwajuni ili kujiridhisha kama kweli
nimekufa"akasema Elvis
"Unadhani wanataka kufukua
kaburi?Meshack Jumbo akauliza
"Bila shaka lengo lao ni
hilo.Tunatakiwa kufanya haraka kuwawahi" akasema Elvis wakaanza
kujiandaa haraka haraka.walichukua
kila walichoona kingeweza kuwafaa
halafu wakaondoka wakimuacha
Omola alinde usalama pale nyumbani
******************
Makaburi ya Umoja Mkwajuni ni
makaburi mapya kabisa ambayo
yalikuwa katika mfumo mpya wa
kulipia hivyo kupafanya mahala hapo
kuwa sehemu nzuri na ya kuvutiwa
kutokana na uangalizi wake
mzuri.Eneo la ndani ya makaburi
kulipangwa vizuri na bado maboresho
yalikuwa yanaendela ili kupafanya
mahala pale pavutie zaidi ikiwa ni
pamoja na kuweka taa ili hata usiku
shughuli za mazishi ziweze kufanyika. David na Elizabeth wakiwa na
walinzi wao wakawasili katika
makaburi yale na kuelekea moja kwa
moja katika geti la walinzi
"David stay in the car.Let me
finish this" akasema Elizabeth na
kushuka garini akawafuata wale
walinzi,akawasalimu na wakataka
kufahamu shida yake
"Samahani ndugu zangu,ninaitwa
Sarah ninaishi Dubai.Nilipata taarifa
za kifo cha rafiki yangu ikanibidi
kufunga safari kutoka Dubai kufika
hapa kumbe tayari amekwisha
zikwa.Kesho ninasafiri kurejea Dubai
alfajiri na mapema hivyo nimekuja
hapa ili niweze kupata nafasi walau
nilione na kuweka maua katika kaburi
lake.Tafadhalini naombeni mnisaidie"
akasema Elizabeth kwa sauti ya upole
iliyowafanya walinzi wale waamini
alichokuwa anakisema Mama kwanza pole sana kwa
msiba wa rafiki yako,lakini hapa tuna
taratibu zetu zilizowekwa.Ikifika saa
moja jioni haruhusiwi mtu yeyote
kuonekana ndani ya eneo la makaburi
kwani bado hakuna taa.Tungeweza
kukuruhusu ukaingia huko lakini
wakuu wetu wakikukuta huko sisi
hatutakuwa na kazi tena" akasema
mmoja wa jamaa aliyeonekana kama
ndiye mkubwa wa zamu ile ya ulinzi
"Jamani nawaombeni
mnisaidie.Sintachukua muda mrefu"
akabembeleza Elizabeth
" Hapana mama hatutaweza
kukusaidia kwa hilo kwani tunalinda
ajira zetu.Tafuta wakati mwingine
uweze kuja kuliona kaburi la rafiki
yako" akasema yule jamaa.Elizabeth
akafungua mkoba wake na kutoa
bunda la noti akampatia yule mkubwa ambaye alitumbua macho asiamini
alichokiona.
"Kwani ndugu yako anaitwa
nani? akauliza yule jamaa huku
akiingia katika ofisi yake na kuzifungia
fedha zile katika droo
"Anaitwa Elvis"
Yule jamaa akafungua kitabu
chake kikubwa chenye orodha ya
watu wote wanaozikwa hapo
akalitafuta jina la Elvis akalipata
"Anaitwa Elvis Tarimo.Amezikwa
kitalu B.Twende nikupeleke" akasema
yule jamaa na kuchukua funguo
akamtaka mwenzake aliyekuwa naye
aendelee kulinda wakati yeye
akimpeleka Elizabeth
ndani.Alipofungua tu geti ghafla
Elizabeth akatoa bastora yenye
kiwambo cha kuzuia sauti na
kumtandika risasi mbili akaanguka
chini halafu akamgeukia yule mwenzake naye akampiga risasi ya
kichwa akaanguka chini kisha
akawaita vijana wake wakawabeba
wale walinzi na kuwaficha ndani
katika maua.Ndani kulikuwa na vibao
vya maelekezo,kulikuwa na kibao
kinaelekeza kitalu A na kingine
kinaonyesha kitalu B wakafuata njia
inayoelekea kitalu B wakayakuta
makaburi na kisha wakaanza
kulitafuta kaburi la Elvis
wakalipata.Tayari lilikuwa limejengwa
kwa ustadi na kuwekwa urembo na
kulifanya livutie sana.Haraka haraka
Eizabeth akawaelekeza wale vijana
waliokuwa na vifaa waanze kulibomoa
lile kaburi.
"David muda si mrefu
tutaufahamu ukweli" akasema
Elizabeth ambaye hakuwa na hata
chembe ya wasi wasi tofauti na David
ambaye alikuwa mkimya na alionekana mwenye woga
mwingi.Haikuwa kazi nyepesi
kulitindua zege lile lililotumika
kufunika kaburi na baada ya kuona
kazi inazidi kuwa ngumu,Elizabeth
akaamuru kaburi lichimbwe kwa
pembeni .
Elvis na Steve waliwasili katika
makaburi ya Mkwajuni,wakaegesha
gari lao mita kadhaa kutoka eneo lile
la makaburi halafu wakatembea kwa
miguu kulifuata geti huku
wakiendelea kupewa maelekezo na
Omola aliyekuwa akiwafuatilia akina
David kupitia kompyuta yake.Walifika
karibu na geti la kuingilia ndani na
wakayakuta magari mawili
yameegeshwa nje.
"Haya lazima ni magari yao"
akasema Elvis kisha akamtaka Steve
amkinge, akatembea kwa tumbo
kuelekea eneo kulikoegeshwa zile gari mbili.Akazifikia na kuchungulia ndani
hakukuwa na mtu yeyote kisha kwa
kutumia bastora yake yenye kiwambo
cha sauti akayapiga risasi matairi
kadhaa yakatoka upepo halafu
akarejea kwa Steve
"Elvis hapa kuna ulinzi lakini
sijaona hata mlinzi mmoja katika
sehemu yao" akasema Steve
"Hiyo ni ishara kuwa tayari
wamekwisha wateka au
kuwaua.Twende ndani" akasema Elvis
wakatembea kwa tahadhari hadi
katika ofisi ya walinzi ambayo ilikuwa
tupu na Steve akagundua kitu.
"Damu!!.Inaonekana tayari
walinzi wamekwisha uawa" akasema
Steve wakaingia ndani ya
makaburi.Kulikuwa giza lakini Steve
alifahamu mahala alikozikwa Elvis
akamuongoza wakatembea kwa
tahadhari kubwa.Mara kwa mbali wakaona mwangaza wa tochi na
vishindo vya watu kuchimba kitu
kigumu
"We got them.Wanaharibu kaburi
wanataka kujua kama nimo kaburini
ama vipi" akasema Elvis kwa sauto
ndogo.Wakapeana maelekezo namna
ya kuwakabili watu wale kisha kila
mmoja akapita sehemu yake wakiwa
wanatambaa kwa tumbo kuelekea
sehemu walipo wale jamaa
Kazi ya kulichimba kaburi la Elvis
iliendelea kwa kasi huku Elizabeth
akiwahimiza wafanye kwa bidii
kubwa.Alikuwa amesimama pembeni
kidogo akiwa na David huku bastora
yake ikiwa mkononi.Sehemu kubwa
ya juu ilikwisha ondolewa
"Aliyejenga kaburi hili anastahili
pongezi" akasema David
"Nadhani alifahamu kuwa
hakuna mtu ndani yake ndiyo maana akajen....." kabla hajamaliza sentensi
yake zikasikika sauti za risasi kutoka
katika bastora yenye kiwambo na
vijana wanne waliokuwa wakichimba
kaburi lile la Elvis wakaanguka chini.
"What happened? akauliza David
kwa wasi wasi huku yeye na Elizabeth
wakichuchumaa chini
"Stanley !! akaita Elizabeth lakini
mara akajikuta akiguswa na kitu cha
baridi sikioni mwake.
"Tupa chini silaha yako na uinue
mikono yako juu!!! ikamuamuru sauti
kali kutoka nyuma yake.Elizabeth alitii
amri aliyopewa na kunyoosha mkono
wake taratibu kuipeleka chini bastora
yake lakini ghafla akageuka na kutaka
kumkabili yule jamaa aliyekuwa
nyuma yake ambaye ni Elvis lakini
Steve alikiona kitendo kile na kuachia
risasi tatu zilizotua katika kiganja cha
mkono ule wenye bastora akaanguka chini.Elvis akamuwahi na
kumkanyaka kichwani huku Steve
akiwahi kumdhibiti David
Bila kupoteza muda Steve akatoa
pingu na kumfunga Elizabeth halafu
wakamwagia dawa katika jeraha lile la
risasi mkononi mwa Elizabeth ili
kuzuia damu kutoka kwa wingi na
kisha wakamchoma sindano ya
usingizi na hazikuputa sekunde
kadhaa akalala.Steve akamuweka
begani Elvis akamuongoza David
wakaondoka
"Jamani msiniue..msiniue
jamani..Mimi ni waziri mkuu
mstaafu..Ninazo fedha nying............"
"Shut up!! akafoka Elvis
Wakatoka nje ya eneo la
makaburi na Steve akaenda kulileta
gari lao wakawapakia Elizabeth na
David wakaondoka "Tumewapata kirahisi sana
tofauti na nilivyokuwa nimetegemea."
akasema Steve
"Hakuna lenye mwanzo likakosa
mwisho.Baada ya muda mrefu wa
kuishi kama wako peponi sasa ni
muda wao wa kuishi kama wako
motoni hasa huyu mwanamke leo
atajuta kuzaliwa binadamu!! akasema
Elvis huku akiuma meno kwa hasira
'Tafadhali vijana wangu
naombeni msiniue.Nitawapa kila kitu
mkitakacho.Niambieni mnataka nini
vijana wangu,kama fedha ninazo
nyingi sana na nitawapa kiasi
chochote mkitakacho" akasema David
aliyekuwa amefungwa mikono kwa
nyuma.Steve aliyekuwa amekaa naye
nyuma akamnasa kibao kizito
"Hii ni picha tu ya kitu
unachokwenda kukutana nacho huko
uendako" akasema Steve Walifika katika makazi yao
wakamshusha Elizabeth aliyekuwa
katika buti.Dr philip akaitwa haraka
sana ili kuja kumuhudumia kabla
hawajamfanyia mahojiano.David
akatupwa katika chumba cha stoo
"Mzee tumefanikiwa kuwapata
wote wawili,David na Elizabeth.Vipi
huku mmefanikisha lile zoezi?
akauliza Elvis
"Zoezi limefanikiwa na wote
wamekamatwa na nimewaelekeza
vijana wakawafunge katika ile nyunba
alimokuwa amefungwa Steve kisha
tutawafanyia mahojiano.Hongereni
sana vijana wangu kwa kazi hii kubwa
na ngumu.Kupitia watu hawa wawili
tutaweza kupata taarifa
zote.Tafadhalini vijana fanyeni kila
muwezalo kuhakikisha kwamba
mnapata taarifa kutoka kwao." Usijali mzee tutapata taarifa
zote."
"Vizuri.Vipi kuhusu suala la
kumtaarifu rais?akauliza Meshack
Jumbo
"Bado kuna kitu tunapaswa
kukifahamu.Ni nani aliye nyuma ya
mpango huu wa mapinduzi?Naamini
hawa jamaa hawakuwa peke yao
lazima kuna watu wako nyuma
yao.Tukiwapata hao basi tutamjulisha
rais.Kwa sasa tujielekeze katika
kupata taarifa kwa kina zaidi"
akasema Elvis halafu wakaenda katika
chumba alimo Dr Makwa
"Hallo Dr Maka" akasema Elvis
"Nimemaliza kazi
yenu.Mnanisaidiaje kuniondoa katika
sakata hili? akauliza Dr Makwa.Elvis
akamtazama kwa sekunde kadhaa
halafu akatoa kicheko kidogo cha
dharau You are so stupid Dr
makwa.After all you've done do you
think we're going to let you go?Mpaka
sasa idadi ya watu waliokufa kutokana
na vurugu ulizoziasisi
haijulikani,unataka tukuache
uondoke?Familia yako inafurahia hivi
sasa wakila na kunywa kwa raha zao
huko nje ya nchi wakati familia za
wengine hivi sasa kuna vilio baada ya
watoto wao kupoteza maisha kufuatia
vurugu ulizozianzisha kwa tamaa zako
za fedha na madaraka.You want me to
let you go!!..akasema Elvis huku
akimtazama Dr Makwa kwa hasira
"Uliniahidi hivyo kwamba
nikikueleza ukweli utanisaidia
kuniondoa katika hili sakata.Tafadhali
nakuom......" Hakumaliza sentensi yake
Elvis akamnasa kibao kizito
kilichompeleka chini.Steve akamuinua
na kumtandika kichwa kilichomfanya apepesuke na kujigonga ukutani
akaanguka chini.Akachukua panga
lililokuwa karibu lakini Elvis akamzuia
"Hatutakiwi kumuua.Huyu bado
tunamuhitaji sana.Ni shahidi muhimu
sana.Mfunge kabisa asije akajiua"
akasema Elvis halafu akampigia simu
Juliana kwa kutumia simu ya Steve
"Hallo Juliana ni mimi Elvis hapa
ninaongea.Tafadhali usitamke jina
langu kama uko na watu karibu"
"Nimekuelewa.Vipi maendeleo ya
lile zoezi mmelifanikisha? akauliza
"Zoezi tumelifanikisha lakini
mama yako ameumizwa kidogo
mkononi ila anaendelea
vyema.Daktari anakuja kumtibu
jeraha kisha tutaanza kumuhoji"
akasema Elvis
"Hongereni sana Elvis.Tafadhali
hakikisheni mumemuhoji na kupata
taarifa zote mnazozihitaji na vile vile msisahau kuhusiana na kupata taarifa
ya vile vifo"
"Tutafanya hivyo
Juliana.Umepata chochote kuhusiana
na Patrice Lwibombe?
"Hapana bado
sijafanikiwa.Nilikuwa na wageni ndiyo
maana nikakosa hata muda wa
kufanya upekuzi" akasema Juliana
"Juliana nina ombi moja
kwako.Kwa kuwa mama yako tayari
tunaye huku tunataka kufanya
upekuzi chumbani kwake ili tuone
kama tutaweza kupata kitu cha
kutusaidia katika uchunguzi wetu"
"Hakuna tatizo kabisa kuhusu
hilo.Mnakuja wote?
"Hapana anakuja Steve peke yake
mimi nitabaki hapa" akasema Elvis
"Sawa ninamsubiri hapa"
"Vipi kuhusu Patricia?Una taarifa
zozote kuhusiana na maendeleo yake? Amenipigia simu muda si mrefu
sana anadai anaendelea
vyema.Usihofu nitakuwa naye karibu
sana"
"Ahsante sana"akajibu Elvis na
kukata simu
Elvis akamuelekeza Steve aende
kwa Juliana na kufanya upekuzi
chumbani kwa Elizabeth .Dr Philip
alifika na kuanza kumuhudumia
Elizabeth ambaye bado hakuwa na
fahamu.Baada ya kulitibu jeraha lile
Elvis akamuita Omola wakaenda
sebuleni na kumtaka Dr Philip
amueleze ukweli kuhusiana na
Vicky.Omola alilia machozi mengi sana
kufuatia kifo kile cha rafiki yake
mkubwa Vicky.Elvis akamtaka aende
chumbani akapumzike
"Sasa ni muda wa kazi" akasema
Elvis akaelekea katika chumba
alimofungwa David akamtoa na kumpeleka sebuleni.Meshack Jumbo
na Dr Philip nao pia
walikuwepo.Alikuwa ameloa jasho
mwili mzima.
"Hallo mheshimiwa David.Usiwe
na hofu.Hapa tumekuleta na
tutazungumza kama marafiki.Take a
deep breath" akasema Elvis na David
akavuta pumzi ndefu
"Again take a deep breath !
"Good.Relax now.You need
something to drink?Whisky
,wine,water or coffee? akauliza Elvis
"W..wa..ter.." akasema huku sauti
yake ikikwama.Elvis akamletea glasi la
maji akamfungua pingu akanywa
"Sintakufunga tena pingu nataka
tuzungumze kwa amani.Kabla ya yote
naomba nifanye utambulisho.Huyu
pembeni yangu anaitwa Dr Philip ni
daktari kutoka idara ya ujasusi,yule
mzee pale ni mkurugenzi wa idara ya ujasusi anaitwa Meshack Jumbo
naamini mnafahamiana kwani
alihudumu pia hata katika wakati
ukiwa waziri mkuu.Mimi naitwa Elvis
Tarimo." akasema Elvis na David
akatamani ageuke upepo
apotee.Alitumbua macho na miguu
yake ikaonekana ikitetemeka
"Pale makaburini mlikuwa
mnataka kuthibitisha kama
nimekufa,I'm not dead !!
"No ! No !..I can't believe this !!
You are a ghost ! a ghost !! akapiga
ukelele wa woga.Elvis akatabasamu na
kumimina mvinyo katika glasi
akanywa
"Nadhani sasa umethibitisha
kwamba mimi ni halisi na si mzimu
kwani mzimu hauna tumbo na wala
haunywi mvinyo" Bwana ndiye mchungaji
wangu..." akasema David na Elvis
akamkatisha
"Huo ulikuwa utangulizi sasa ni
wakati wa mazungumzo.Nitakuuliza
maswali na ninaomba unijibu kila kitu
na endapo utashindwa kuonyesha
ushirikiano basi huu utakuwa ni
mwisho wako.Hauta liona tena jua la
kesho asubuhi.Hauta muona tena
mpenzi wako Samira"akasema Elvis
na kumstua sana David alipotaja jina
la Samira
"David wewe ni waziri mkuu
mstaafu,umehudumu katika jamhuri
ya muungano wa Tanzania kwa
kipindi cha miaka kumi na kabla ya
hapo umeshika nyadhifa kadhaa
katika serikali,ni mtu mwenye
heshima kubwa katika jamii na hata
sasa baada ya kustaafu siasa bado
umeendelea kuheshimika sana ndani na nje ya nchi.Kitu gani hasa
kimekushawishi utake kurejea katika
siasa?tuanzie hapo tafadhali"akasema
Elvis
"Mimi..." akasema David na sauti
ikakwama akakohoa kidogo
kurekebisha koo halafu akaendelea
"Mimi nimekwisha staafu siasa
na sijihusishi tena na mambo hayo"
akajibu David
"Tunafahamu umestaafu siasa
lakini kwa siku za hivi karibuni
umerejea tena katika siasa kwa
mlango wa nyuma na umekuja na
mikakati mizito ya kuhakikisha
unakuwa rais wa Tanzania.Swali langu
nini au nani kakushawishi urejee tena
katika siasa tena safari hii ukitaka
kushika nafasi kubwa zaidi ya uongozi
pasi na kufuata taratibu?
Swali lile likambabaisha David. Jibu David nani kakushawishi
urejee tena katika siasa wakati
umekwisha staafu?
"Si kweli kwamba ninataka
kuwania urais.Mambo hayo
nimekwisha achana nayo" akasema
David
"David inuka twende! akasema
Elvis na kumshika mkono David
akampeleka katika chumba alimo Dr
Makwa.
"Unamfahamu huyu? akauliza
Elvis.David alipatwa na mstuko
mkubwa na ghafla sehemu ya mbele
ya suruali yake ikaloa alikuwa
amejisaidia haja ndogo.Hakutegemea
kabisa kumkuta Dr Makwa mle
chumbani
"Unamfahamu huyu? akauliza
Elvis
"Uhhm..uhhmm..." David
akajiuma uma na kushindwa kutoa jibu.Elvis akamnasa kibao kikali
kilichompeleka chini kwani miguu
yake haikuwa na nguvu.
"Unamfahamu huyu?
"Ndiyo" akajibu David kisha Elvis
akamrejesha sebuleni
"Dr Makwa tumemchukua
nyumbani kwako na tayari ametueleza
kila kitu kuhusiana na mipango yenu
yote.Mpaka dakika hii maandamano
na mipango yote ya vurugu
imesitishwa na aliyefanya hivyo ni
muandaaji mkuu wa maandamano
ambaye ni Dr Makwa.Mpaka dakika hii
wenyeviti wote wa vyama vya siasa
ambao wameshiriki katika
kuhamasisha vurugu za leo
wamekwisha kamatwa na
wanakwenda kuhojiwa kuhusiana na
mipango yenu ya kuiangusha
serikali.Its over David.Kila kitu kimekwisha.Tamaa zako zote
zimekutokea puani." akasema Elvis
"I'm sorry." akasema David huku
akiweweseka kama mwendawazimu
"David hili nikosa la uhaini na
unafahamu adhabu ya kosa kama
hili.Awali ilikuwa ni kifo lakini kwa
sasa ni adhabu ya maisha
gerezani.Usiku huu nitakukabidhi kwa
vyombo husika ili taratibu za
kuwafungulia mashitaka wewe na
wenzako zianze mara moja kwani
tayari tunao ushahidi wa kutosha wa
mipango yenu miovu.Tunafahamu kila
kitu unachokipanga wewe na wenzako
akiwamo makamu wa rais Dr Shafi."
David akazidi kuchaganyikiwa
alipopewa habari za Dr Shafi
"Tunafahamu kuwa wewe ndiye
uliyempa maelekezo Dr Shafi kwamba
mimi niuawe,wewe ndiye
uliyemuelekeza Dr Shafi,mzee Meshack Jumbo auawe pia.Tunazo
rekodi za mazungumzo yako yote ya
simu na Dr Shafi na muda si mrefu
makamu wa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania atatiwa
mbaroni kwa tuhuma za uhaini.It's
over David but I can help you if you
choose to cooperate with
me.Ninaweza kukusadia David
kuondokana na adhabu inayoweza
kukukabili endapo utafikishwa mbele
ya vyombo vya sheria"
"Please help me!! akasema David
huku ameloa jasho kama vile
amemwagiwa ndoo ya maji
"What do you want? Kitu
chochote nitakupa tafadhali naomba
unisaidie"akasema David
"Nataka kufahamu jambo moja
tu.Nani walio nyuma ya mpango
huu?Nani wanafadhili mapinduzi
haya? akauliza Elvis Nitakuwa na uhakika gani
kwamba utatimiza ahadi yako ya
kuniondoa katika jambo hili?akauliza
David
"Right now I'm your only hope so
you either choose to tell me what I
want or to end your life in prison"
akasema Elvis
"Ok ok nitakueleza"
"I real dont know them ila
nilialikwa katika kikao na Frank na
huko ndiko nilikowakuta watu fulani
wawili wenye asili ya kiarabu na
wakajieleza kwamba wao ni
wawakilishi wametumwa na mataifa
makubwa ambayo chumi zake
zinategemea mafuta"David
akawaeleza akina Elvis kila kitu
kilicotokea katika kikao kile cha
kwanza ambapo mipango ya
mapinduzi ilianza kuandaliwa Baada ya mkutano huo ndipo
kila kitu kikaanza"akaendelea
"Nilimfuata makamu wa ais Dr
Shafi na kumshawishi akubali
kujiunga nasi ili hapo tutakapokuwa
tumeichukua nchi yeye aweze kuwa
rais wa Zanzibar.Vile vile
nikawashawishi viongozi wa vyama
vya siasa kuanzisha maandamano na
vurugu na wakati huo huo baadhi ya
wanajeshi walikuwa wanaandaliwa ili
kuweza kuchukua nchi pale vurugu
zitakapokuwa zimezidi."David
akaeleza mipango yao yote
waliyokuwa wameipanga
"David maelezo yako marefu
lakini bado swali langu hujalijibu.Ni
nani hawa ambao walileta mpango
huu kwenu?
"Nilichowaeleza ni kitu cha kweli
kabsa.Watu hao siwafahamu undani
wao" akasema David David this is the last chance to
save yourself.Tell me the truth"
akasema Elvis
"Elvis huu ni ukweli mtupu"
"David ninataka sana kukusaidia
lakini kwa kuwa umeshindwa
kunieleza ukweli nitalazimika
kukuunganisha na wenzako na gazeti
la kesho asubuhi litapambwa na picha
zenu wewe na makamu wa rais mkiwa
katika mikono ya polisi mkituhumiwa
kwa uhaini.Inuka haraka !! akaamuru
Elvis na David akasimama
"Elvis tafadhali usinipeleke
huko.Nisaidie tafadhali.Meshack
Jumbo I'm so sorry.Nisamehe mzee
wangu !! akasema David.Elvis
akamtaka amfuate
"Elvis kuna kitu nimekikumbuka"
"Sema haraka"
"Watu wale siwafahamu kiundani
lakini huyu mwanamke Elizabeth mliyenikamata naye anawafahamu na
ndiye aliyewaelekeza kwa Frank."
akasema David na Elvis akamtaka
aketi na amueleze kwa kituo
kuhusiana na Elizabeth kujihusiaha na
mpango ule wa mapinduzi
"Elizabeth alinipiga simu na
kunitaka nikamuone akanieleza
kwamba amekuja kwenye mazishi ya
mumewe Deusdedith.Elizabeth
akanieleza kwamba watu wale yeye
ndiye aliyewatuma.Alisema kwamba
kabla ya kuja huku watu wale
walimfuata kwanza yeye na wenzake
wakawaeleza kuhusu mpango wao wa
kuipindua serikali na ndipo
alipomuelekeza Frank aanze kuandaa
timu itakayoandaa
mapinduzi.Elizabeth ndiye
anayewafahamu watu hao ni akina
nani,mkimuhoji yeye atawaeleza kila
kitu" Ok good.Umekuwa rafiki
mkubwa wa Elizabeth.Tueleze
anajishughulisha na mambo gani?
"Elizabeth ni mfanya biashara
mkubwa.Anazo biashara katika nchi
mbali mbali duniani"
"Nafahamu ni mfanya biashara
lakini nafahamu kuna ambo
anajihusisha nayo tofauti na biashara
.Ni mambo gani hayo?Nieleze
tafadhali.Ukweli wako ndiyo msaada
wako"
David akainamisha kichwa
akafikiri kwa muda kisha akasema
"Elizabeth anajihusisha na
magenge ya kimafia.Mumewe
Deusdedith alikuwa kiongozi wa
genge mojawapo na baada ya kufariki
Elizabeth ameshika uongozi.Fedha
zake nyingi anazipatia katika biashara
zake hizi.Ana mtandao mkubwa katika nchi mbali mbali.Mkimuhoji
atawaeleza ukweli."
"Unamfahamu Patrice
Lwibombe?
"Patrice Lwibombe?akauliza
David
"Ndiyo .Unamfahamu?
"Lwibombe ni mtoto wa
aliyekuwa kiongozi wa kikundi kimoja
cha waasi wa Congo ambaye
amefungwa kifungo cha maisha nchini
Congo.Baada ya baba yake kufungwa
Patrice ameendeleza mapambano
dhidi ya serikali ya Congo"
"Anaishi wapi Patrice?
"Kwa taarifa nilizonazo Patrice
anaishi nchini Ubelgiji"
"Ahsante sana kwa taarifa hizo
David sasa nenda kapumzike na
tutaendelea nawe baadae" akasema
Elvis na kumpeleka David chumbani.