I DIED TO SAVE MY PRESDENT
Sehemu 25
****************
Pamoja na kurejea nyumbani
saa kumi alfajiri lakini Pascal
alishindwa kabisa kupata usingizi
.Kichwa chake kilikuwa na
mawazo mengi sana lakini mawili
makubwa yaliyokuwa
yakimsumbua kichwa ni mpango
ule wa kuiangusha serikali na pili
ni taarifa za kuonekana kwa Elvis
akiwa na Graca nchini afrika ya
kusini.Hizi ni taarifa zilizomstua
sana kwani anafahamu vizuri Elvis
mpaka akaonane na Graca lazima
kuna kitu ambacho alikuwa
anakifuatilia
“ Damn !! akasema Pascal
kwa hasira na kuinua glasi ya
mvinyo akanywa
Hadi kunapambazuka bado
alikuwa macho.Akaoga na
kuelekea kazini.Akiwa njiani
aliwasiliana na Arafa mmoja wa wafanyakazi wa idara ya ujasusi
anakofanya kazi Elvis
“ Hallow Pascal” akasema
Arafa baada ya kupokea simu
“ hallow Arafa uko wapi sasa
hivi? Akauliza Pascal
“ Ninaelekea kazini
Pascal.wewe uko wapi?
“ Hata mimi ninaeleka kazini.”
“ Kulikoni Pascal leo
umenipigia simu asubuhi namna
hii? Akauliza Arafa
“ Nilitaka kuja ofisini kwenu
leo hii lakini sintaweza kwa hiyo
ninahitaji msaada wako”
“ Msaada gani Pascal?
“ Ninahitaji kuonana na
Elvis.Kuna taarifa ninataka
kumpa lakini kuna mtu aliniambia
kwamba Elvis hayupo.Sina uhaika
sana na jibu hilo kwa hiyo naomba
unisaidie kuthibitha kama ni kweli
hayupo.Kama yupo usimweleze
chochote nitaarifu nitamtafuta mimi mwenyewe kwa wakati
wangu” akadanganya Pascal
“Hauna mawasiliano na Elvis?
Akauliza Arafa
“ Hapana sina .Elvis ni mtu
ambaye sijazoeana naye kiasi cha
kuwa na mawasilino naye
japokuwa tunafahamiana.”
Akasema Pascal .Arafa akafikiri
kidogo kisha akasema
“ OK nitakutaarifu nikifika
ofisini” akasema Arafa na kukata
simu
“ Leo lazima nipate uhakika
kuhusu Elvis kuonekana afrika ya
kusini.Huyu mtu ananiweka
tumbo joto sana.Elvis ni mtu
hatari na lazima tumdhibiti
mapema” akawaza Pascal
Alifika ofisini kwao na
alionekana ni mwenye mawazo
mengi .Aliendelea na kazi na saa
tatu na robo Arafa akampigia simu
“ Halow Arafa” akasema Pascal
“ Pascal ni kweli Elvis hayupo
yuko nje ya mkoa kikazi”
“ Amekwenda mkoa gani na
atarudi lini?
“ Siwezi kujua yuko wapi na
anafanya nini na atarudi lini
kwani kiwango change si cha
kufahamu mambo kama
hayo.Atakaporejea
nitakufahamisha mara moja”
“Ahsante sana Arafa .Naomba
unitaarifu atakaporejea ila
tafadhali naomba usimfahamishe
chochote kama nilikuwa
namtafuta”
“ usijali Pascal” akajibu Arafa
na kukata simu
“ Kwa sasa nina uhakika
kwamba Elvis amekwenda nchini
Afrika ya kusini na si nje ya mkoa
kama alivyoniambia Arafa.Lakini
kwa nini akaenda kuonana na
Graca? Hili ndilo swali la kutafutiamajibu haraka sana” akawaza
Pascal na kutoka nje ya jengo
akampigia simu Brigedia Frank
“ hallow Pascal “ akasema
Frank
“ Frank tayari nimepata
uhakika kwamba Elvis ana safari
ya kikazi lakini mtu aliyenipa
taarifa hizo hakuweza kunieleza
amekwenda wapi na ni kazi gani
amekwenda kufanya.Mpaka hapa
hakuna shaka kwamba ni kweli
Elvis alikwenda Afrika ya kusini.”
Akasema Pascal halafu kimya
kifupi kikapita Frank akasema
“Kinachoniumiza kichwa ni
kwamba kwa nini alikwenda
kuonana na Graca? Nina hakika
kuna kitu anakitafuta.Ni kitu gani
basi alikuwa anakitafuta kwa
Graca?Amempeleka wapi Graca?
Mpaka hivi sasa sijapokea taarifa
zozote kuhusiana na zoezi la
kumtafuta mwanangu” Frank hata mimi jambo hilo
limekuwa linaniumiza sana
kichwa changu.Tunatakiwa
tutafute jibu la haraka sana la
swali hili” akasema Pascal
“ OK vizuri.Bado uko ofsini?
Akauliza Frank
“ Ninajiandaa kuondoka ili
kuwahi kikao cha leo mchana
“ Good.Kikao cha leo mchana
ni muhimu sana kwani ndicho
kitakachotupa muelekeo mzima
wa mkakati wetu .Wageni wetu
tayari nimewasindikiza
wameondoka .Utanipitia hapa
nyumbani ili tuongozane wote
kuelekea kikaoni” akasema Frank
“ Ok Frank nakuja sasa hivi”
akasema Pascal
***************** Jumba la kifahari la aliyewahi
kuwa waziri mkuu wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Daudi
sichoma lilizungukwa na bustani
iliyotengenezwa kwa ustadi
mkubwa,iliyosheheni miti mizuri
na maua ya kupendeza. Ndege
wazuri wa kila rangi waliruka
katika miti yenye maua mazuri na
kuzidi kuifanya bustani ile iwe na
mandhari ya kipekee sana.Daudi
Sichoma ni mmoja kati ya viongozi
wanaosemekana kujilimbikizia
utajiri mkubwa sana ndani na nje
ya nchi.Alimiliki mahoteli
makubwa ndani na nje ya nchi,pia
anamiliki shirika la ndege na vile
vile ana hisa nyingi katika
makampuni mengi makubwa ya
ndani na nje ya nchi.Kiwango cha
utajiri wake kimebaki kuwa siri
kutokana na kumiliki miradi
mingine mingi kwa siri
Eneo litakalotumika kwa ajili ya kikao liliandaliwa vizuri sana
katikati ya bustani hii nzuri.Kabla
ya kukaa katika meza ya kikao
kulikuwa na sehemu iliyoandaliwa
maalum kwa ajili ya wajumbe
kupata chakula kabla ya kuanza
kwa kikao.
Mpaka saa saba mchana
karibu wajumbe wote waliotakiwa
kuhudhuria kikao kile tayari
walikwisha wasili.Daudi
akawaongoza wajumbe wale hadi
katika sehemu kulikoandaliwa
chakula na wajumbe wakaanza
kujipatia mlo wa mchana.Kilikuwa
ni chakula kizuri kilichoandaliwa
na wapishi mahiri waliotoka
katika mojawapo ya hoteli
anayomiliki Daudi.Baada ya
chakula wajumbe wakaelekea
sehemu kulikokuwa
kumeandaliwa kwa ajili ya
kikao.Eneo lote lilikuwa kimya
sana. Ni milio tu ya ndege iliyokuwa ikisikika katika bustani
ile.Brigedia Frank ambaye ndiye
aliyekuwa mwenyekiti wa kikao
kile akafungua kikao kwa
kuwashuku wajumbekwa kufika
kwao
“ napenda niwataarifu
kwamba wale wageni wetu
tuliokuwa nao jana wameondoka
leo asubuhi kurejea makwao na
majukumu yote ya ule mpango
yako juu yetu kwa hiyo hatuna
muda wa kupoteza tunatakiwa
tuanze mara moja mikakati ya
kutekeleza mpango huu
mkubwa.wao tutakuwa
tukiwatumia mihutasari ya kila
kikao tunachokifanya na
utekelezaji wa kila jambo.Fedha
zitawekwa katika akaunti maalum
na kila pale tutakapokuwa
tukihitaji fedha hatutakuwa na
upungufu wowote.Ndugu zangu
hiki ni kikao cha chetu cha kwanza cha kuweka mikakati ya
kuelekea Tanzania
mpya.Mnakaribishwa kwa mawazo
tukianza na mheshimiwa Daudi
ambaye ana uzoefu mkubwa wa
kuwepo serikalini na atatusaidia
sana kimawazo” akasema Brigedia
Frank .Daudi sichoma
akatabasamu na kukohoa kidogo
akasema
“ Awali ya yote napenda
kuwashukuru nyote kwa kufika
kwenu.Namshukuru sana Frank
kwa uamuzi wake wa
kunishirikisha katika mpango huu
muhimu.Nasema ni mpango
muhimu kwa taifa letu kwani
endapo utafanikiwa basi utaleta
neema kwa watanzania na maisha
yao yataboreka tofauti na hali
ilivyo sasa.Sote tuliwasikia akina
Alhafidh na maelezo waliyotupatia
.Ukiyachambua kwa undani
maelezo yale utagundua kwamba kuna kila ulazima wa kuiondoa
kwa lazima serikali iliyopo
madarakani.Hatuwezi kuiondoa
kwa njia za kdemokrasia bali kwa
kufanya mapinduzi.” Akasema
Daudi na kunyamaza kidogo kisha
akaendelea
“ Tukirejea maelezo ya
Alhafidh tunagundua kwamba
mipango yote inayofanyika hivi
sasa kuhusiana na uwekezaji
mkubwa katika sekta ya mafuta
na gesi inalenga katika
kuwanufaisha viongozi walioko
madarakani.Hakuna hata mpango
mmoja utakaowanufaisha
wananchi wa hali ya chini.Kitu
cha pili ni kwamba viongozi hawa
wanataka kuipeleka Tanzania
katika machafuko kwa sababu
endapo marekani watajenga kituo
chao cha kijeshi hapa nchini basi
Tanzania itakuwa ni moja ya
shabaha za magaidi.Nchi haitakuwa salama
tena.Tunatakiwa tuhakikishe
kwamba hilo halitokei kwa kuja na
mikakati mizito sana ambayo
itakuwa na faida kwa watanzania
na hata tutakapofanikiwa
kuiangusha serikali basi
watanzania watuamini kwamba
tuna nia ya dhati ya kufanya
mageuzi makubwa ya maisha
yao.Endapo kila mtanzania
ataiona na kufurahia faida ya
kuwa na gesi na mafuta nchini
Tanzania basi mapinduzi
tutakayoyafanya yatakuwa na
manufaa na watanzania
watatupenda na kutuunga
mkono.Makampuni ya kiarabu
tutayapa udhibiti wa biashara ya
mafuta na yatatuletea faida kubwa
sana na tutahakikisha kila
mwananchi wa nchi hii mkubwa
kwa mdogo wanafaidika
nayo.Tutakuza uchumi tutaboresha maisha ya
mwananchi mmoja moja na kila
raia wanchi hii atakuwa na uso
wenye tabasamu.Hiyo ndiyo ndoto
yangu ya muda mrefu sana ya
kumfanya Mtanzania afurahi
kuwapo Tanzania” akasema Daudi
na wajumbe wote wakampigia
makofi kumuunga mkono David
akaendelea
“ Ndoto yangu ya miaka mingi
ni kuwa rais wa nchi hii.Lengo si
kutaka kutafuta utajiri au
umaarufu au kuabudiwa lakini
lengo langu kubwa ni kutaka
kumfanya kila raia wa nchi hii awe
na furaha ,ayamudu maisha yake
,watoto wetu wasome na ajira
zipatikane.Hayo yote
yanawezekana tu kwa kuwa na
koongozi jasiri kama mimi.Nyote
mnafahamu mambo niliyoyafanya
na kuleta mabadiliko katika jamii
.Ni mambo hayo niliyoyafanya ndiyo yanayofanya nikawa na
maadui wengi kisiasa na
nikaondolewa madarakani.Pamoja
na kuondolewa katika nafasi
yangu ya uwaziri mkuu bado
wameendelea kunifuata fata na
kuhakikisha kwamba wananizika
kabisa na kwa hilo naweza
kusema kwamba wamefanikiwa
kwani sionekani tena katika
medani za siasa.Ninamshukuru
Frak kwa kunishirikisha tena
kaika mpango huu ambao nina
hakika lazima utafanikiwa.”
Wajumbe wakapiga makofi
halafu akaendelea
“ Naomba niweke wazi kwenu
kwamba kama ilivyo ndoto yangu
ya muda mrefu na endapo mpango
huu utafanikiwa basi naombeni
mimi niwe rais.Naomba
tukubaliane toka awali kwamba
tukifakiwa mimi ndiye
nitakayekuwa rais” Daudi akasema na kuwatazama
wajumbe .Kimya kifupi kikapita
Frank akasema
“ Mimi sina kipingamizi na
hilo.Nafahamu wananchi wengi
bado wanakuhitaji sana ili
uwaongoze.wewe ndiye
utakayekuwa rais wetu”
Wajumbe wengine nao
wakaungana na Frank na wote
wakakubaliana kwamba endapo
mapinduzi yatafanyka basi Daudi
awe ndiye rais
“ Ahsanteni sana ndugu
zangu kwa kunikubalia ombi
langu.Kwa sasa nitatoa
ushirikiano wa kila namna ili
kufanikisha mpango huu”akasema
Daudi huku akitabasamu na
wajumbe wakampigia makofi
“ Ndugu zangu kuiangusha
serikalini ni mpango mpana sana
na wa siri kubwa.Ili tufanikiwe
kuna watu ambao lazima uwe nishirikishi .kwanza kabisa lazima
tutafute uungwaji mkono toka kwa
makamanda wa vikosi vya jeshi
ambao watatengeneza mtandao wa
askari watakaofanya uasi.Jeshi
litaipindua serikali na kukabidhi
madaraka kwa mtandao wetu kwa
maana hiyo lazaima tupate
makamanda wa jeshi ambao
watakuwa tayari kushirikiana
nasi.Pili tunatakiwa kuchochea
uhasama mkubwa na chuki kwa
raia dhidi ya serikali
yao.Tunatakiwa tulete aina Fulani
ya machafuko ambapo jeshi la
polisi litalazimika kutumia nguvu
kubwa katika kuyatuliza na
kusababisha vifo na katika
machafuko hayo sisi yatakuwa na
faida kwetu .Serikali itaonekana
imeshindwa kuwalinda raia wake
na inakiuka haki za binadamu na
hivyo wananchi hawatakuwa na
imani nayo tena.Tanzaniaitachafuka katika jumuia ya
kimataifa na hiyo itakuwa ni
sababu nyingine ya kutosha
kabisa kwa sisi kufanya
mapinduzi.Tutakapoingia
madarakani ndani ya kipindi
kifupi tutarejesha halali ya amani
na hivyo wananchi watakuwa na
imani na matumaini makubwa na
sisi.Katika kipengele hiki
tutawatumia wanasiasa wa vyama
vya upinzani.Hawa watapandikiza
chuki kwa katika jamii kwamba
serikali imewazuia mafuta wa
marekani na hivyo kuongoza
maandamano na migomo isiyo na
kikomo kuishinikiza serikali
iliyoko madarakani kuachia
ngazi.Migomo na maandamano
hayo yataandamana na vurugu na
hivyo kuilazimisha serikali
kutumia nguvu
kubwa.Tutawawezesha wanasiasa
hawa kifedha na watazunguka nchi nzima kuifanya kampeni
hii”David akanyamaza wajumbe
wakampigia makofi kwa mawazo
yake mazuri. Kisha wakaendelea
“ wanasiana hawa
wanachokipigania wa watanzania
bali maslahi yao binafsi kwa hiyo
kwa kutumia ushawishi wa fedha
tutaviunganisha vyama vyote vya
upinzani hiyo itaturahishishia
kutimiza lengo letu.Mimi nitawaita
viongozi hao wa vyama vya siasa
vya upinzani na kufanya nao
mkutano wa siri.Nitawashawishi
na watakubaliana
nami.Sintawaeleza kuhusiana na
mpango wetu wa kuiangusha
serkali lakini nitawahakikishia
kwamba endapo watafanya
kampeni hiyo na serikali iliyoko
madarakani ikaondolewa basi
mimi nitagombea urais kupitia
muungano wa vyama vya
upinzani.Baada ya mapinduzi viongozi hawa wa vyama vya siasa
tutawapatia nyadhifa mbalimbali
katika serikali ikiwa ni njia ya
kuwafunga midomo”akanyamaza
akainua glasi yake ya maji
akanywa na kuendelea
“ Kipengele cha tatu ambacho
tunatakiwa kukifanya ni
kuwashirikisha baadhi ya
viongozi kadhaa kutoka serikali
kuu,idara ya usalama wa
taifa.Jeshi la polisi na sehemu
yoyote ambayo tutayaona ina
manufaa.kwa upande wa serikali
kuu kuna mtu ambaye tunaweza
kumtumia.Makamu wa rais ndugu
Shafi Abdulkhareem Omari.Mzee
huyu hana maelewano mazuri na
rais na si mara moja kumetokea
mikwaruzano.Mzee huyu atatufaa
sana na atatusaidia katika mambo
mengi.Baada ya mapinduzi mzee
huyu ataendelea na wadhifa wake
wa makamu wa rais” akanyamaza tena na kuwatazama wajumbe
halafu akaendelea
“ hayo ndiyo mambo matatu
makubwa ambayo tunatakiwa
kuyafanya iwapo tunataka
mpango wetu ufanikiwe,Jeshi,
wanasiana na viongozi wachache
wa serikali na idara za usalama
.Tukifanikiwa kuzidhibiti sehemu
hizo basi tujue kwamba mpango
wetu utafanikiwa asilimia mia
moja .Kwa upande wangu mimi
nitashughulika na viongozi wa
vyama vya siasa na kuwaweka
chini na
watanisikiliza.Nitashughulika pia
na makamu wa rais pamoja na
vongozi wengine.Wote hawa nina
hakika ya kuwashawishi na
wakajiunga nasi.Upande wa jeshi
na sehemu nyingine
itakayoonekana kuwa na
umuhimu zitashughulikuwa na
watu wengine” akamaliza kutoa maoni yake Daudi .wajumbe
wakampigia makofi
“ Ahsnte sana mheshimwa
rais” akasema Frank na wote
wakacheka
“ tafadhali msicheke.Huyu
ndiye rais wetu mtarajiwa kwa
maana hiyo hakuna haja ya
kusubiri hadi mapinduzi yafanyike
ndipo tuanze kumuita rais.Mambo
yanaanza sasa kwani uhakika wa
kuchukua serikalini ni mkubwa
sana” akasema Frank
“ Nadhani nyote mmesikia
mheshimiwa David yeye ana
uzoefu mkubwa katika serikali na
ametupa mwangaza mkubwa sana
na muelekeo mkubwa.Bado
tunaendelea kuchukua maoni na
mitazamo ya kila mmoja wetu
hapa.Kabla sijaendelea zaidi
naomba na mimi niweke wazi
mbele yenu kwamba
nitashghulikia suala la jeshi.Nina ushawishi mkubwa kwa
makamanda wa vikosi mbalimbali
vya jeshi kwa hiyo naomba suala
hili niachiwe mimi na nitaliweka
sawa.Licha ya nguvu ya ushawishi
lakini mkumbuke pia kwamba
tuna fedha nyingi sana kwa ajili ya
kazi hii.kwa hiyo lazima fedha
itumike na panapo fedha hakuna
kinachoharibika” akasema Frank
na kisha wakaendelea na mjadala
******************
Kengele ya mlango wa
chumba cha Elvis ikalia na
kumuamsha toka usingizini.Toka
walipopata chakula cha mchana
alikuwa amelala kutokana uchovu
wa safari ndefu.Akajiinua kwa
uchovu na kutazama saa yake
.Ilipata saa kumi na mbili za
jioni.Akainuka akavaa shati na
kuelekea mlangoni.Akaufunguamlango na kukutana na
muhudumu
“ samahani kaka yule mgeni
wako uliyesema tumuandalie
chumba tayari amewasili”
akasema muhudmu
“ Doreen ?!!
“ Ndiyo kaka.Yupo mapokezi
anakusibiri”
“ Ok ahsante sana nakuja
sasa hivi”akasema Elvis na kuvaa
viatu vya wazi vilivyokuwamo mle
chumbani akatoka na kuelekea
mapokezi.Doreen alikuwa amekaa
katika sofa jeusi la pale mapokezi
na mara tu alimpomuona Elvis
akasimama na kumkumbatia
“ Elvis !! akasema Doreen
huku akiendelea kumkumbatia
Elvis kwa nguvu
“ Ahsante sana Doreen kwa
kuja.Karibu sana mbeya”
“Ahsante sana Elvis
.Ninashukuru nimefika salama.Njia nzima nilikuwa na
mawazo mengi sana kama uko
salama.”
“ Niko salama
Doreen.Hukupatwa na tatizo lolote
njiani?
“ Hapana sikupata tatizo
lolote .Gari hili bado jipya kabisa”
akasema Doreen
“ Patricia anaendeleaje?
Ulimweleza chochote kuhusiana
na safari hii?
“ Patricia anaendelea vizuri na
sikumweleza chochote kuhusiana
na safari hii na wala hajui kama
nimesafiri” akasema Doreen
“ Ahsante sana Doreen.Kwa
sasa naomba ujimwagie maji
halafu tupumzike kidogo kisha
tutapata chakula cha usiku.Tuna
maongezi marefu kidogo baada ya
chakula,” akasema Elvis na
kumpeleka Doreen katika chumba
alichokuwa amemuandalia Ouh jamani ! kwa nini
linapokuja suala la Elvis najikuta
siwezi kumkatalia kitu chochote ?
Nimeendesha gari toka Dar hadi
huku bila kujua nini
ananiitia”akawaza Doreen baada
ya Elvis kutoka mle
chumbani.Akavua koti na kulitupa
kitandani kisha akavua gauni lake
na kubakiwa na nguo ya ndani
“ Its cold like hell .Baridi
sana huku mbeya.Natamani kama
ningepata nafasi ya kulala na Elvis
leo..” Akawza Doreen akajifunga
taulo na kuingia bafuni akafungua
maji ya moto na kuoga
“ Kitendo cha patricia
kunitaka nizae na mume wake
Elvis kimeniweka katika wakati
mgumu sana .Kuna hisia za
tofauti nimeanza kuzipata kuhusu
elvis.Toka nilipolala naye siku ile
na kuyashika maungo yake nyeti
kila nikimuona mwili wote hunisisimka” akawaza Doreen
huku akiendelea kuoga.Picha ya
usiku ule akiwa mtupu amelala
kitandani kwa Elvis ikamjia
kichwani akatabasamu
“ Natamani usiku kama ule
ujirudie leo hii tena tukiwa huku
mbali ambako hakuna mtu wa
kumuogopa.” Akaendelea kuwaza
Doreen huku akijifuta maji
akarejea chumbani na kujilaza
kitandani akajifunika blanketi
kulikuwa na baridi kali na
taratibu kijiusingizi kikamchukua.
**************
Akiwa usingizini kwa mbali
alisikia kama mlango wa chumba
chake unagongwa.Mwanzoni
alidhani labda anaota lakini
mlango ulipoendelea kugongwa
akafumbua macho.Ni kweli kunamtu alikuwa anagonga
mlango.Akainuka na kuelekea
mlangoni akaufungua na
kukutana na sura yenye
tabasamu ya Elvis.Kwa muda wa
sekunde kadhaa Elvis alibaki
anakodolea macho kifua cha
Doreen .Kuna kitu kilimvutia pale
kifuani.Doreen aligundua kwamba
Elvis alikuwa amevutika na
sehemu ile ya kifua naye akabaki
amesimama na kumuacha Elvis
aendee kukisaili kifua chake.Elvis
akakohoa kidogo na kusema
“ Pole sana na uchovu Doreen
na samahani kwa kukuamsha”
“ Ahsante sana Elvis.Kuna
baridi sana huku na ndiyo maana
nikapitiwa na kijiusingizi.Karibu
ndani”
“ Doreen nimekuja kukutaarifu kwamba ni muda wa
kupata chakula cha usiku sasa.”
“ Ahsante sana Elvis.Nilikuwa
nimejisahau kabisa kuhusu
chakula.Karibu ndani Elvis na
mimi nijiandae twende “
“ Ahsante sana Doreen .Mimi
natangulia hotelini utanikuta
kule”
“ No Elvis.tafadhali nisubiri
tuongozane wote.karibu ingia
ndani”
“ Ok Doreen niko hapa nje
ninakusubiri”
“ Ingia ndani Elvis.Are you
afraid of me? C’mon I’m not a
ghost.Please come in” akasema
Doreen
“ ahsante Doreen.Badilisha
nguo na utanikuta hapa nje”
“ Ok Mr shy guy.Just wait for me here .I wont take long”
akasema Doreen na kuufunga
mlango akamuacha Elvis
amesimama pale nje
akimsubiri.Baada ya dakika tano
akatoka akiwa amevaa nguo nzito
za baridi wakaongozana hadi
sehemu ya chakula .Hakukuwa na
watu wengi zaidi ya raia wachache
wa kigeni .Elvis akamuongoza
Doreen hadi katika meaza moja
iliyokuwa pembeni ambayo
msichana mmoja mwenye umbo
dogo alikuwa amekaa
“ karibu Doreen” akasema
Elvis na kumvutia Doreen kiti
akaketi.Doreen na Graca
wakatazamana .Elvis akatabsamu
na kusema
“ Doreen samahani
sikukutaarifu toka mwanzo lakini katika safari yangu hii
nimeambatana na mtu
mwingine.Tafdhali kutanana
Graca Frank,Ni mtanzania
aliyekuwa nchini afrika ya kusini
na kwa sasa anaelekea Dar es
salaama” akasema Elvis halafu
akamgeukia Graca
“ Graca kutana na Doreen.Ni
mmoja kati ya marafiki zangu
wakubwa”
Doreen na Graca
wakasalimina na kisha
wakaendelea kupata mlo wa
usiku.Ni Elvis na Doreen pekee
waliokuwa wazungungumzaji pale
mezani.Graca alikuwa
kimya.Pengine ni kwa sababu ya
kutokuwa na mazoea nao ya
karibu
Baada ya kumaliza chakula Elvis akamsindikiza Graca hadi
chumbani kwake
“ kesho alfajiri na mapema
tunaanza safari ya kuelekea Dar
es salaam.Doreen amekuja na gari
ambalo ndilo tutalitumia.Sikutaka
tupande magari makubwa ya
abiria kwani sitaki uonekanae.
Kwa hiyo nitakuamsha alfajiri na
mapema kwa ajiili ya kuanza
safari.
“ Ahsante sana Elvis kwa
msaada wako .Sikujua kama una
moyo wa huruma namna
hii.Nakuahidi nikifika sehemu
salama nitakueleza kila kitu
ninachokifahamu”
“ Usihofu Graca.Uko salama
na utaendelea kuwa
salama.Nitakulinda siku zote na
hakuna mtu yeyote atakayekudhuru.Kwa sasa endelea
kupumzika” akasema Elvis na
kugeuka akaanza kuondoka.
“ is she yur girlfriend?
Akauliza Graca .Elvis ambaye
tayari alikwisha ushika mlango
akageuka
“ Unasemaje Graca? Akauliza
“ Doreen.Is she your
girlfriend? Akauliza tena Graca
“ We’re friends.Good friends”
akajibu Elvis
“ You look good together.Ok
Good night Elvis” akasema Graca
“ Good night” akasema Elvis
huku akitabasamu akaufunga
mlango na moja kwa moja
wakaelekea chumbani kwa Doreen
akagonga mlango Doreen
akaufungua .Elvis akaingia ndani
na kwenda kuketi sofaniKuna baridi sana
Elvis.Ninahisi nahitaji kupata
mvinyo” akasema Doreen akapiga
simu hotelini wamletee
mvinyo.Baada ya dakika mbili
muhudumu akawasili akiwa na
chupa ya mvinyo na glasi
mbili.Doreen akamimina mvinyo
ule katika glasi na kumpatia Elvis
glasi moja.
“Ni mara yangu ya kwanza
kufika Mbeya.Sikujua kama kuna
baridi kiasi hiki”akasema Doreen
huku naye akiketi sofani karibu
na Elvis
“ Mbeya ni mkoa wenye
baridi kali sana.Nimewahi kufika
mara kadhaa kwa hiyo
ninapafahamu vyema na ndiyo
maana nikakusisitiza usisahau
nguo za baridi” “Ahsante sana kwa
kunikumbsha.Bila hivyo sijui
ningefanya nini japokuwa hata
hivi sasa bado naisikia baridi kali
sana.” Akasema Doreen
“ Ok tuachane na hayo.Pole
sana na uchovu wa safari ndefu”
akasema David
“Ni safari ndefu
sana.Nashukuru nimefika salama
na sikupatwa na tatizo lolote
njiani”
Hongera kwa kuendesha gari kwa
umahiri mkubwa,wanawake wengi
hawawezi kuendesha gari kwa
umbali mrefu namna hii”
“Mimi nimekwisha zoea
kuendesha gari umbali
mrefu.Huwa ninaendesha gari
hadi Nairobi hadi Kampala bila
matatizo.” Akasema Doreen halafu kimya kikapita
“ Patricia aliniambai kwamba
umekwenda afrika ya kusini
lakini nikastuka uliponipigia na
namba za Zambia.Uliamua kurudi
kwa kutumia njia ya gari?akauliza
Doreen
“ Nlilazimika kutumia njia ya
gari badala ya ndege.Hii ni kwa
sababu ya Graca”
“Graca?! Doreen akashangaa
“ Graca amefanya nini?
“ Kilichonipeleka afrika ya
kusini ilkuwa ni kumfuata binti
huyu.”
“ Kwani Graca ni nani?
Kafanya nini? Akauliza Doreen
“ Siwezi kukueleza kwa
undani sana kuhusu yeye kwa
sababu ni mambo ya ndani sana
ya kikazi lakini kwa ufupi ni kwamba Graca ana taarifa
muhimu sana na maisha yake
yako hatarini na ndiyo maana
imenilazimu kumuondoa kule
afrika ya kusini”
“ wanataka kumuua ? !
Doreen akashangaa
“ Kwa miaka kadhaa sasa
amekuwa akiishi kwa mateso
makubwa na kwa taarifa alizonazo
lazima nichukue dhamana ya
kumlinda.”
“ Ouh Elvis pole sana”
“ Ahsante sana Doreen.lakini
hii ni mojawapo ya kazi
zangu.Nimekwisha zoea mambo
kama haya”
“ hao wanaotaka kumuua
wako wapi? Unawafahamu?
Akaulizia Doreen
“ wako afrika ya kusini na wengine wako hapa nchini na
ndiyo maana sikutaka kutumia
usafiri wa kawaida wa abiria kwa
nia ya kumficha.Toka afrika ya
kusini nimepita naye katika njia
za uficho ili asionekane.Baada ya
kufika hapa nimeona nitafute mtu
ambaye ninamuanini wa
kunisaidia na nimekuchagua
wewe.Ninakuamini sana Doreen
and please don’t let me down”
Doreen akatabasamu na
kusema
“ Elvis ahsante sana kwa
kuniamini.Naomba kuahidi
kwamba katu siko tayari
kukuangusha .Sijawahi na
sintofanya hivyo kamwe.Chochote
utakachokitaka toka kwangu
nitakupatia na ndiyo maana niko
hapa muda huu kwa sababu ulinitaka nije hapa.Feel free to tell
me anything,I mean anything”
akasema Doreen na uso wa Elvis
ukajenga tabasamu
“ nashukuru kwa maneno
yako mazito.Nitaendelea
kukuamini kwa siku zote za uhai
wangu.Kitu kikubwa nilichokuitia
hapa ni kwamba Graca anahitaji
msaada.kwanza kusafirishwa kwa
siri hadi Dar e s salaam na pili
kuhifadhiwa sehemu salama.Mtu
anayetishia maisha yake ni baba
yake mzazi ambaye ni afisa
mkubwa jeshini .Kuna mambo ya
siri anayoyafahamu Graca
kuhusiana na baba yake na
tumekubaliana kwamba ili
anieleze mambo hayo lazima
nihakikishe anakuwa
salama.Akisha nieleza nitamfanyia mpango wa kumuhamisha nchi na
kumtafutia makazi nchi nyingine
akaendelee na maisha yake .Kwa
mambo hayo mawili ninahitaji mtu
ambaye nina muamini sana”
akasema Elvis
Doreen akamtazama Elvis
usoni.Macho yalionyesha uoga
Fulani
“ Mbona unaogopa Doreen”
akauliza Elvis
“ Elvis I’m so scared” akasema
Doreen.Elvis akamsogelea
akamshika mkono na kumtazama
usoni
“ Do you trust me Doreen?
Akauliza
“ Ofcourse I do. I trust you”
akasema Doreen.
“ Thank you .That the only
thing I wanted to hear from you.So don’t be scared.You are
more than safe around me”
akasema Elvis na kumfanya
Doreen atabasamu
“ Tell me Elvis.What do
yuwant me to do?
“ kesho tutarejea dar es
salaam.Nataka sehemu ya
kumficha Graca,sehemu ambayo
hakuna watu wengi wanaingia
.Ninataka Graca akae nyumbani
kwako kwa muda wakati
ninamtafutia makazi mazuri”
“ Ahsante sana Elvis kwa
kuniamini na kuchagua Graca
akae kwangu.Sipingani na
mawazo yako lakini ninadhani
unahitaji kutafuta sehemu
ambayo ni salama zaidi .Pale
kwangu ni sehemu salama lakini
watu wengi huingia .Mimi ni mtu mwenye mazoea na watu wengi
kwa hiyo kuwazuia watu ghafla
wasifike nyumbani kwangu
kunaweza kuleta udadisi kidogo
na wakataka kujua kulikoni.Lakini
kuna wazo nimelipata”
“ wazo gani? Akauliza Elvis
“ Kuna rafiki yangu mmoja
ameolewa na mzungu na kwa sasa
mzungu huyo anarejea kwao.Kwa
kuwa anaondoka na mke wake
wameamua wauze kila kitu chao
hapa Tanzania .Nyumba yao ni
nzuri sana na yenye usalama wa
kutosha.Ina uzio mkubwa na ina
kila kitu ndani hadi bwawa la
kuogelea.Kama tukiona inafaa
tuinunue nyumba ile hata kwa
kulipa pesa nusu na baadae
tutamaliza deni taratibu.Nadhani
hii itakuwa ni sehemu nzuri sana kumuhifadhi Graca”akasema
Doreen na Elvis akatabasamu
“Hilo ni wazo zuri sana na
nyumba kama hiy ndiyo ambayo
ninaitafuta.Inauzwa shilingi ngapi
hiyo nyumba?
“ Mimi aliniambia kwamba
endapo ningempatia milioni
themanini basi angeweza
kunipatia nyumba hiyo kwa
sababu ni rafiki yangu lakini
thamni yake ni zaidi ya milioni
mia moja na hamsini.Ni rafiki
yangu mkubwa na tunaelewana
sana .Ninaweza kuongea naye na
bei ikashuka hata zaidi ya hapo na
tnaweza hata kumlipa kwa
awamu.”
“ kama ni hivyo hakuna haja
ya kusubiri zaidi .Ongea naye sasa
hivi na mwambie kwamba tutampaia shilingi milioni ishirini
za kuanzia na zitakazobaki
tutamlipa taratibu” akasema
Elvis.Doreen akachukua simu
yake na kumpigia huyo rafiki
yake wakaongea kwa zaidi ya robo
saa
“ Imekuwa bahati sana kwani
mpaka sasa hivi bado hajaiuza na
kesho wanaondoka kuelekea
Denmark.Amekubali kuchukua
kiasi hicho kilichopo cha fedha na
kilichobaki tutamlipa kwa kuwa
anaondoka kesho asubuhi sana
amesema kwamba funguo
nitaikuta katika kampuni ya ulinzi
ambayo wana mkataba wa
kumlindia.Kila kitu amekiacha
pale ndani hadi gari.
“ wow ! that’s great
news”akasema Elvis Naomba unipatie kompyuta
yako .Amekupa namba za akaunti
yake ya benki?
“ Amesema atanitumia muda
si mrefu”akasema Doreen huku
akilifungua begi lake na kutoa
kompyuta yake ndogo na muda
huo huo ujumbe mfupi ukaingia
katika simu yake
“ Tayari amenitumia akaunti
yake” akasema Doreen huku
akiziandika namba zile na
kumpatia Elvis ambaye alianza
mara moja zoezi la kuhamisha
pesa toka katika akaunti yake na
kuzipeleka katika katika akaunti
ya rafiki yake Doreen aitwaye
Amanda.Alihamisha kiasi cha
shilingi million ishirini na baada
ya dakika kumi Amanda akapiga
simu na kuthibitisha kwamba kiasi kile cha fedha tayari
kimeingia katika akaunti yake
“ Huu ndio uzuri wa
teknolojia.Imerahisisha sana
ufanyaji wa biashara.Ingekuwa ni
zamani ingenilazimu mpaka
kwenda benki na kuchukua kiasi
hicho kikubwa cha fedha.Ahsante
sana Doreen kwa msaada
wako.Umenisaidia kitu kikubwa
sana”akasema Elvis.Doreen
akatabasamu ,kikapita kimya
kifupi Doreen akasema
“ Arent you going to involve
Patricia in this ? akauliza
Doreen.Elvis akainama akafikiri
na kusema
“ Nitamfahamisha lakini si
sasa”
“ kwa nini hutaki
kumshirikisha katika suala hili? Don’t you trust her? Akauliza
Doreen
“ I trust her lakini kwa sasa
sitaki kumuhusisha katika suala
hili sitaki kumuongezea
matatizo.Ana mzigo mzito
unaomuelemea hivi sasa,sitaki
kumbebesha mzigo zaidi.Alionao
sasa unamtosha sana” akasema
Elvis kwa uchungu
“ Nakubaliana nawe Elvis
.matatizo aliyonayo Patricia ni
makubwa na hahitaji kuongezewa
matatizo zaidi” akasema Doreen
kimya kikapita
“ Unafikiria nini Elvis
kuhusiana na suala hili?
“ Suala gani Doreen?
“ Suala la Patricia”
“ Doreen suala la Patricia
kukosa mtoto sina namna ya kulitafutia ufumbuzi na hakuna
namna ya kufanya ili aweze
kupata mtoto.Patricia ni rafiki
yako mkubwa na nina imani
amekwishakueleza tatizo lake
kwamba hawezi kubeba
mimba.Kizazi chake kilikwisha
ondolewa.I was there when it
happened.Hakuna wa kumlaumu
kwa kilichotokea kwani bila
kufanya vile angepoteza
maisha.Ninampenda Patricia na
nilimpenda huku nikiyafahamu
matatizo yake na nilipomuoa
nilikwisha jiandaa kisaikolojia
kwamba sintakuwa na mtoto
maishani kwa sababu mke wangu
hana uwezo wa kunizalia
mtoto.Suala hili mimi haliniumizi
kichwa hata kidogo
.Kinachomsumbua Patricia kwa sasa ni maneno ambayo yameanza
kujitokeza toka kwa ndugu zangu
wakidai kwamba tumechukua
muda mrefu toka tulipooana bila
ya kuwa na mtoto.Ndugu zangu
wanadai mtoto .Haya ni matatizo
ya kawaida na ambayo
ninauhakika baada ya suala hili
kumalizika nitayaweka
sawa.Sintampa nafasi ndugu
yeyote kuingilia ndoa yangu.Huu
ni upepo tu naamini utapita na
mimi na mke wangu tutabaki
salama” akasema Elvis
“ yah ! hata mimi naomba iwe
hivyo.Patricia anateseka sana.”
“ usijali suala hili litakwisha
tu”akasema Elvis ingawa
ilionekana wazi kwamba alikuwa
akiumia sana moyoni.Doreen
akasema Elvis nafahamu unampenda
sana patricia na kwa hilo siwezi
kupingana nawe.Pamoja na hayo
naomba uwe muwazi kwangu ni
kweli hautaki kuwa na mtoto
katika maisha yako?Hautaki
kuitwa baba katika maisha yako?
Hautaki kumpata mrithi wa mali
zako? Please be honest with me”
Elvis akaninama na
kuonekana kuzama katika
mawazo.Suala aliloulizwa na
Doreen lilionekana kumchanganya
sana
“ Answer me Elvis” akasema
Doreen baada ya ukimya kutawala
mle chumbani.Elvis akainuka na
kwenda dirishani akafunua pazia
na kutazama nje halafu akageuka
na kwenda kuchukua glasi yake
na mvinyo akanywa kidogo. “ Doreen swali uliloniuliza ni
gumu sana na sijui nikujibu nini”
" Just be Honest with me”
akasema Doreen.Elvis akafikiria
tena kidogo na kusema
“ Ukweli ni kwamba hakuna
mwanandoa ambaye hapendi
kuwa na mtoto.Kila mmoja
angependa apate mtoto tena hata
zaidi ya mmoja.Kuna nyakati
huwa najitazama namna
ninavyoishi na mke wangu na
ninaona furaha yetu ingekuwa
maradufu endapo tungepata
mtoto.Kwa wazazi wangu mimi ni
mtoto wao wa pekee na hawana
mtoto mwingine.Kabla hajafariki
baba yangu alituachia mali nyingi
na mrithi pekee ni
mimi.Ningependelea kuwa na
mtoto ambaye angerithi mali hizi zote lakini uwezo huo haupo.Mke
wangu wa ndoa hana uwezo wa
kupata mtoto.Hili si suala dogo
hata kidogo ni suala zito lakini
ninamshukuru Mungu kwa
kunipa nguvu na uwezo wa
kulikabili suala hili.Toka awali
nilikwisha jitayarisha kisaikolojia
kwamba sintakuwa na mtoto
ingawa kuna nyakati huwa
ninatamani sana mtoto lakini
uwezo huo haupo tena:” akasema
Elvis .Doreen aliyekuwa kimya
akimtazama akainua Glasi yake ya
mvinyo akanywa na kusema
“ Pole sana Elvis.Ahsante pia
kwa kuwa muwazi kwangu.Najua
ni suala gumu lakini bado
unaweza kulipatia ufumbuzi”
“Ufumbuzi gani Doreen?
“Patricia anakupenda sana na amekwisha usoma moyo wako na
akafahamu kabisa kwamba
unatamani kuwa na mtoto na
ndiyo maana akakupa ruhusa ya
kutafuta mwanamke uzae naye
mtoto.Huu si uamuzi mwepesi
lakini ameweza kuufanya ili
maisha yenu yaweze kuwa na
nuru na furaha,”
“ I cant do that Doreen,I
swear I cant” akasema Elvis
“ kama mkeo tayari
amekwisha kuruhusu unashindwa
nini? Kwa nini uendelee kumtesa
mkeo?
“ Siwezi kufanya hivyo kwa
sasa nafahamu atateseka zaidi
pale nitakapozaa nje ya
ndoa.Niliapa mbele ya altare
kwamba nitampenda Patricia
katika shida na raha .Tuko katika wakati wa shida hivyo lazima
niishi kiapo change cha kumpenda
zaidi hasa wakati wa
shida”akasema Elvis
“ Patricia hawezi kuteseka
kwani tayari amekwisha jiandaa
kwa hilo na kizuri zaidi
amekwambia kwamba
atakutafutia mwanamke
anayemuamini na akanichagua
mimi.Hata hapo bado
haiwezekani?
“Doreen nimekwisha kwambia
kwamba siwezi kufanya hivyo hata
awe nani na hakuna
atakayenishawishi nifanye hivyo”
Doreen akamtazama kidogo na
kuulzia
“ Elvis be honest with
me.Kinachokufanya ulipinge suala
hili kwa nguvu zote ni kwa sababu ya upendo wako kwa Patricia au
there is something else?
“What ?! akauliza Elvis
“ Ina maana hujanisikia?
Nimekuuliza kwamba
kinachokufanya ulipinge suala hili
la kutafuta mtoto nje ya ndoa
wakati mkeo amekwisha kupa
ruhusa hiyo ni upendo wako kwa
Patricia au kuna sababu nyingine?
“ Kwa nini unaniuliza hivyo
Doreen wakati jibu unalifahamu
kwamba nilimpenda Patricia kwa
namna alivyo na ndiyo maana
siwezi kufanya kitendo kama
hicho anachonitaka nifanye.Siwezi
kufanya jambo lolote kinyume na
kiapo cha kanisani”
“ Elvis you are my friend
.Please be honest with me”
“Be honest with you? yes be honest with me .Is
everything ok with you?
“Doreen sikuelewi
unamaanisha nini kuniuliza
hivyo?
“ Namaanisha kuhusu uwezo
wako wa kumpa mimba
mwanamke.Una hakika uko sawa?
“ I am ok.Una wasi wasi naweza
kuwa na kasoro ndiyo maana
ninalipinga wazo la kuzaa nje ya
ndoa? Ondoa shaka kuhusu
hilo.Hata kama ingekuwa ni kweli
basi ingebaki kuwa ni siri yangu
na mke wangu lakini kukujibu
swali lako ni kwamba mimi sina
kasoro ni rijali kama wengine na
uwezo wangu siutilii mashaka
hata kidogo” akasema Elvis
“ Mhhh ! I nina mashaka”
akasema Doreen “ Kwa nini unakuwa na
mashaka Doreen?
Doreen akanywa kidogo kinywaji
na kusema
“ Nina wasi wasi kwa nini
hutaki mtoto wakati mke wako
amekwisha kupa ruhusa ya
kutafuta mtoto nje ya ndoa. Kama
ungekuwa huna kasoro
usingekataa”
“ Doreen mbona unasisitiza
sana kwamba nina matatizo? Sina
tatizo lolote .Mimi ni mzima
kabisa”
“ Can you prove that to me?
“ Prove what ? akauliza Elvis
“ That you are ok”
“ kwa nini nidhihirishe
kwako? Wewe hupaswi kufahamu
masuala kama hayo na hata kama
nikiwa na tatizo ni suala langu la ndani na hapaswi mtu mwingine
kufahamu”
“ Mhh ! I’m curious” akasema
Doreen na kumsogelea Elvis
“ Usiogope Elvis.Please come
closer” Akasema Doreen
“ Unataka kufanya nini
Doreen? Akauliza Elvis lakini
tayari Doreen alikwisha upeleka
mkono wake kunako ikulu na
muda ule ule ikulu
kukachachamaa
“ stop that Doreen.what are
you dong?akasema Elvis kwa sauti
ya juu.Doreen akatabasamu na
kusema
“ relax Elvis.Nilitaka tu
kuhakikisha mambo yako
sawa.Nimeamini uko sawa.”
Elvis akamtazama Doreen
usoni na kusema Doreen kwa nini
unaf…………” kabla hajamalizia
sentensi yake Doreen akasema
“ Relax Elvis,relax.Hakuna
tatizo kila kitu kiko ok” akasema
Doreen.
Bado Elvis aliendelea
kumtazam Doreen usoni kwa
macho makali.Hakuamini kama
angeweza kufanya kitendo kama
kile cha kumshika maeneo nyeti
“ Ok Elvis,let us get back to
our serious business” akasema
Doreen
“ Subiri kwanza.Doreen kwa
nini umefanya kitendo kile?
Akauliza Elvis.Doreen akainua
glasi yake akanywa na kusema
“ Ok Elvis ,unataka kufahamu
ni kwa nini nimefanya vile? Huu
hapa ni ukweli.Ukotayati kuufahamu? Akauliza
“ Ndiyo.Niambie kwa nini
umefanya kitendo kile ?
“ Ukweli ni kwamba nilihitaji
kuwa na uhakika kama kila kitu
kiko vizuri na hauna kasoro
yoyote.Ninahitaji ukubali kuzaa na
mimi mtoto kwa ajili ya
Patricia.Anateseka sana kwa
jambo hili.Sielewi ni kwa nini
unakuwa mgumu sana
kukubaliana na mke wako kuhusu
suala hili.Mimi nimekwishakubali
kumsaidia Patricia na niko tayari
muda wowote kuzaa na wewe
lakini kwako limekuwa ni suala
gumu .Kwa nini Elvis? Akauliza
Doreen
Elvis akavuta pumzi ndefu na
kusema
“ How much she paid you? Elvis namba usinielewe
vibaya .Nilikubali kwa moyo
mweupe kumsaidia Patricia na
wewe pia kumpata mtoto na si
kwa sababu ya pesa.I have my
own money,I have millions of
money na sina shida ya
pesa.Nimejitolea tu kumsadia
rafiki yangu anayeteseka sana na
wala usione ninakulazimisha
ukadhani labda nina mapungufu
ama ninataka kuwa mke wako wa
pili la hasha .Sina lengo hilo bali
nia yangu ni kuwasaidia ninyi
,wewe na mkeo kupata mtoto ili
ndoa yenu iwe na furaha.Mkeo
yuko tayari kwa jambo hilo wewe
ndiye unayekwamisha“ akasema
Doreen.Chumba kikawa kimya
kabisa.Kila mmoja alikuwa
akiwaza lake.Elvis akasema I don’t know what to say
Doreenm,wewe na Patricia
mmeniweka katika wakati mgumu
sana”akasema Elvis
“ You don’t have to say
anything Elvis.Unachotakiwa
kufanya ni maamuzi tu.Ingia
katika moyo wa Patricia na
uangalie ni namna gani anateseka
kwa kukosa mtoto.Kwa taarifa
yako hakuna kitu kinachomtesa
mwanamke kama kukosa
mtoto.Think carefully about this”
akasema Doreen
“ I don’t know Doreen.I real
don’t know what t do right now.I’m
so confused” akasema
Elvis.Doreen akamshika bega na
kusema
“ Elvis suala ni gumu na
linahitaji maamuzi magumu so think like a man and make
decision like a man.I’m not forcing
you to do it but promise me that
you’ll think about this” akasema
Doreen
Elvis akaniama akafikiri kidogo
na kusema
“ Ok Doreen.I’ll think about
that” akasema Elvis
“ Ahsante sana Elvis.Sasa
naomba ukapumzike kwani kesho
tuna safari ndefu ya kurejea Dar ”
akasema Doreen .Elvis akainuka
“ Ahsante sana Doreen .Ngoja
nikapumzike.Nitakuamsha kesho
alfajiri na mapema kwa ajili ya
safari” akasema Elvis huku
akianza kupiga hatua kuelekea
mlangoni.Akaufungua mlango na
kabla hajatoka Doreen akamuita
“ Elvis !! .Elvis akageuka Sweet dreams” akasema Doreen
“ Goodnight Doreen’ akasema
Elvis na kuufunga
mlango.Taratibu akatembea
kueleka katka chumba chake
akaingia na kujtupa kitandani
“Najua Patricia anaumia sana
na suala hili lakini sina namna ya
kufanya.Siwezi kuzaa nje ya ndoa
hata kama yeye ameridhia nifanye
hivyo.Sijui ni kitu gani
kimemuingia Patrcia na kumfanya
awaze mambo haya na kunitaka
nizae na rafiki yake Doreen.Lakini
ngoja kwanza niliweke pembeni
suala hili nishughulike na suala
zito lililoko mbele yangu la
Graca.Nitakaa na patricia na
kuongea naye kwa kina kuhusiana
na suala hili na nitamuelewesha
athari zake.Hata mimi sipendi kumuona akiumia lakini huu ni
msalaba wetu lazima tuubebe
wote” akawaza Elvis na kulala