Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Mtunzi usisahau kututoa kweny hii alosto ya riwaya hii...
 
Vicha vya HABARI VINGINE... YAANI KIMAONESHA AMESHAKUFA HALAFU NDIO ANAYEYOA SIMULIZI... WAKATI NO MAREHEMU TAYARI
 
I DIED TO SAVE
PRESIDENT

PART 2

MAWASILIANO
0764294499

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Samahani sana
mzee.Nimelazimika kuja kukuona
kuna jambo nataka kuongea
nawe.Nahitaji tena msaada wako”
Mkurugenzi akamtazama kwa
makini na kusema
“ Evis kuna kitu gani
unachokifuatilia?Kitu gani
kinachoendelea ambacho hutaki
kuniambia?
Elvis akavuta kiti na kuketi
halafu akasema
“ Mzee najua unahitaji sana
kujua kitu
ninachokichunguza.Nahitaji sana
kukueleza ni kitu gani lakini
inaniwia ugumu kwa sababu hata
mimi mwenyewe bado sijapata
undani hasa wa kile ninachokifuatilia.Nahitaji
uchunguzi zaidi ili niweze kupata
taarifa zenye kutosheleza na ndipo
nitakapokuja kwako kukueleza ”
akasema Elvis.Mkurugenzi
akamtazama na kusema
“ Elvis ninakuamini sana
kijana wangu na niko tayari
kukusaida msaada wowote
unaouhitaji lakini nimeanza
kuingiwa na shaka kuhusiana na
usiri wako katika jambo hilo
unalolichunguza”
“ Mzee nafahamu kwamba
ninakwenda kinyume na taratibu
kwa kuchunguza jambo bila
kukushirikisha kwanza
wewe.Jambo ninalolichunguza ni
jambo kubwa na ninahitaji bado
kufahamu mambo kadhaa ili
niweze kulileta mezani kwako likiwa limekamilika .Naomba
muda kidogo ili niweze
kukamilisha uchunguzi
wangu”akaomba Elvis.Meshack
Jumbo akasema
“ What do you need this time?
“Nahitaji kwenda Afrika ya
kusini”akasemaElvis
“ Afrika ya kusini?
“ Ndiyo mzee
“Kufanya nini?
“ Kuna mtu ambaye nahitaji
kwenda kumuhoji.Nina uhakika
yeye ndiye mwenye majibu yote ya
kile ninachokichunguza”akasema
Elvis
“ Kwa hiyo unahitaji nini?
“ nahitaji ruhusa ya kwenda
huko na endapo nitahitaji msaada
wowote nikiwa huko basi
nitakufahamisha.Mzee suala hili ni muhimu sana.Utimilifu wa
jambo zima ninalolichunguza
unategemea sana safari hii”
akasema Elvis .Mkurugenzi
akafikiri kidogo na kusema
“ Umeniacha nikiwa sina
uamuzi mwinginezaidi ya
kukuruhusu uende huko afrika ya
kusini.Pamoja na hayo ukumbuke
siku zote kwamba ninakuamini
kila unachoniambia kwa niyo
pindi ukamilishapo uchunguzi
wako ujekwangu mara moja
kunieleza”
“ Mzee ahsante sana kwa
kuniamini .Nakuahidi
nitakaporejea nitakuwa na kitu
muhimu cha kuweka mezani
kwako” Akasema Elvis
“ Elvis Kitu kingine
ninachotaka kukufahamisha ni kwamba safari hii ni ya siri kati
yangu nawe na haitakuwepo
katika orodha ya kazi za ofisi kwa
hiyo jitahidi asifahamu mtu
mwingine yeyote..” akasema
mkurugenzi
“ Ahsante sana
mzee.Ninategemea kuondoka
kesho asubuhi na baada ya siku
mbili nitarejea.”
“ sawa Elvis.Nakutakia kila la
heli. Nitaongea na Bongani
Makath ambaye ni mtu wetu kule
afrika kusini na atakupatia kila
aina ya msaada unaouhitaji ukiwa
kule”
“ Ahsante sana
mzee.Tutaonana nitakaporejea”
akasema Elvis na kuondoka ili
kuanza maandalizi ya safari yake
ya kuelekea afrika kusini.ENDELEA……………………..
Saa tano za asubuhi ndege ya
shirika la ndege la afrika ya kusini
ikatua katika uwanja wa ndege wa
kimtaifa wa Oliver thambo jijini
Johannesburg Afrika ya kusini.Ni
siku ya Ijumaa iliyopendezeshwa
na kijua kitamu .Elvis akiwa ni
mongoni mwa abiria waliosafiri na
ndege hii kutokea jijini Dar es
salaam alishuka ndegeni na
kukamilisha taratibu za
kiuhamiaji halafu akatoka na
kupokelewa na Bongani Makath
wakala wa idara ya ujasusi ya
Tanzania nchini Afrika ya
kusini.Kisha salimiana wakaongia garini na safari ya kuelekea
nyumbani kwa Bongani ikaanza.
Bongani alikuwa na jumba
kubwa na zuri.Elvis
akakaribishwa ndani na maongezi
ya kikazi yakaanza.
“ Elvis karibu sana afrika ya
kusini” akasema Bongani
‘ Ahsante sana
Bongani.Nyumba yako nzuri sana
nimeipenda” akasema Elvis
“ Ahsante sana Elvis.Habari
za Dar es salaam? Ni muda mrefu
hatujaonana”
“ Dar es salaam kwema.Ni
kweli ni muda mrefu hatujaonana”
akasema Elvis.Kikapita kimya
kifupi Bongani akasema
“ Nimelifanyia kazi lile suala
ulilonieleza na tayari nimekwisha
ongea na uongozi wa hospitali ile na wametoa ruhusa ya kuonana
na mgonjwa unyemtaka.Kwa
mujibu wa melezo yao ni kwamba
mgonjwa huyo hali yake
inaendelea vizuri kwa sasa na ana
uwezo wa kuhojiwa jambo
lolote”akasemaBongani
Bila kupoteza muda Bongani
na Elvis wakaingia garini na safari
ya kuelekea hospitali ikaanza
*****************
Saa saba za mchana katika
uwanja wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam dege
la shirika la ndege la Qatar
airways linatua .Miongoni mwa
abiria walioshuka walikuwepo
watu wawili waliokuwa wamevalia nadhifu sana.Watu wale
walikamilisha taratibu za uhamiaji
na kuruhusiwa kuingia
nchini.Katika sehemu ya
kupokelea abiria wanaowasili watu
wane walikuwa wakiwasubiri wale
jamaa wawili na walipowaona
wakawapokea na kuwaongoza hadi
katika gari mbili zilizokuwa nje ya
uwanja wakaingia na kuondoka na
moja kwa moja wakaelekea
Silvano hoteli moja ya hoteli
inayosemekana kwamba ni kubwa
na ya ghali kuliko zote nchini
Tanzania.
Dakika kama ishirini toka
wawasili pale hotelini gari moja
jeusi likawasili na akashuka
Brigedia Jenerali Frank Kwaju
akiwa ameongozana na watu
wawili na miongoni mwao alikuwepo Pascal
Situmwa.Chrispine Akwite
akawapokea na kuwaongoza hadi
ghorofa ya juu waliko wale wageni
wawili.Brigedia Frank na ujumbe
wake wakasalimiana na wale
jamaa
“ Karibuni sana Tanzania”
akasema Frank
“ Ahsante sana
Frank.Tunashukuru” wakajibu
wale jamaa kwa pamoja
“ Habari za Tanzania? Mambo
yanakwendaje hapa? Akauliza
mmoja wa wale jamaa
“ Habari za hapa ni nzuri na
kila kitu kinakwenda kama
kawaida.Mheshimiwa Daudi
Sichoma tayari nimekwisha
wasiliana naye na jioni ya leo
tutakuwa naye katika kikao.Msiwe na wasi wasi kila kitu kitakwenda
vizuri.” Akasema Frank .Baada ya
maongezi kidogo wakaagana kwa
ajili ya kwenda kujiandaa na kikao
kitakachofanyika jioni ya siku
hiyo.Frank akiongozana na Pascal
pamoja na mtu mwingine
wakaingia garini na kuondoka
“ Frank wewe ni rafiki yangu
na kila kitu tunafanya pamoja
lakini nashangaa mpaka sasa hivi
hujanieleza chochote kuhusiana
na wale jamaa.Who are they?
Frank akamtazama na kusema
“ Usiwe na haraka
Pascal.Utafahamu kila kitu katika
kikao cha pamoja leo jioni”
Pascal akavuta pumzi ndefu
na kusema
“ Frank mimi na wewe
tumekuwa ni washirika wakubwa sana na kwa muda mrefu.Kila
jambo tumekuwa tukilifanya
pamoja na hatujawahi kufichana
jambo lolote.Kama mshirika na
mtu wako wa karibu nina haki ya
kufahamu ni kitu gani
kinachoendelea kabla hata ya
hicho kikao” akasema Pascal
“ Pascal ni kweli wewe ni
mshirika wangu mkubwa lakini
nasikitika kwamba sintaweza
kukueleza kwa sasa ni kitu gani
kinachoendelea.Naomba uvute
subira hadi jioni kuna jambo zuri
sana utalifahamu” akasema Frank
“ Frank
unanishangaza.Haijawahi tokea
hata siku moja ukanificha
jambo.Kuna nini kinachoendelea?
Halafu umenistua sana
ulipomtaja Daudi Sichoma kwamba naye atahusika katika
kikao cha jioni.Huyu ni waziri
mkuu mstaafu anahusikaje na
sisi? Tafadhali naomba uniweke
wazi Frank”akasema Pascal
“ Pascal naomba usiwe na
haraka sana lakini kwa
kukudokeza tu ni kwamba kuna
jambo zito lililowaleta wale jamaa
na ndiyo maana waziri mkuu
mstaafu Daudi Sichoma naye
atashiriki katika kikao.Vuta subira
kidogo tu na utafahamu kilakitu”
akasema Frank na Pascal
hakutaka kuuliza tena
wakaendelea na safari yao
********************
Geti la hospitali ya magonjwa
ya akili iliyopo nje kidogo ya jiji la Johannesburg likafunguliwa na
gari aina ya range rover yenye
rangi nyeupe ikaingia na
kusimama katika kibanda cha
walinzi kwa ajili ya ukaguzi.Mlinzi
mmoja aliyevalia sare za kampuni
binafsi ya ulinzi akalisogelea lile
gari na Bongani aliyekuwa
akiendesha akashusha kioo
akasalimana naye kwa lugha ya
kizulu wakaongea kidogo halafu
akamruhusu apite
“ Unafahamiana na yule
mlinzi?akauliza Elvis
“ Hapana sifahamiani
naye.Nimemchangamkia tu ili
kujenga mazoea naye.Siku zote
ukitaka watu kama hawa
wasikubughudhi basi jishushe na
ujiweke chini yao”akasema
Bongani na kuegesha gari katika maegesho ya hospitali kisha
wakashuka na kuingia katika
jengo la utawala .Moja kwa moja
wakanyoosha hadi katika mlango
uliokuwa na kibao kidogo juu Dr
Susan Ndaba Dlamini.Bongani
akagonga mlango na sauti toka
ndani ikawaruhusu
wapite.Wakaingia na kukutana na
mwanamke mmoja mrembo sana
mwenye tabasamu la
kuvutia.Aliwasalimu kwa furaha
na kukakaribisha
“Karibuni sana” akasema Dr
Susan
“ Ahsante sana Susan.Huyu
hapa ni yule mwenzangu toka
Tanzania anaitwa Elvis.Tumekuja
kuhusiana na lile suala
nililokwambia .Tunataka kuongea
machache na Graca” akasema Bongani.Dr Susan akaweka chini
kalamu yake na kuwatazama
akina Elvis kwa makini kisha
akasema
“ Hali ya Graca kwa sasa
inaendelea vizuri na anazidi
kuimarika siku hadi siku tofauti
kabisa na wakati
alipoletwa.Kinachonishangaza
kidogo ni kwamba kuna nyakati
anakuwa mzima kabisa na kuna
nyakati huwa ana badilika na
kumshangaza kila
mtu.Nikimuangalia sana Graca
ninahisi kuna jambo analo
moyoni.Haonekani kama ni
mgonjwa wa akili
niliowazoea.Ninasema hivyo kwa
sababu nimekuwa karibu naye
sana toka alipoletwa na
ninamfaamu vizuri” Akasema Dr Susan na kuinuka na kuwaomba
akina Elvis
wamfuate.Waliongozana hadi
katika bustani kubwa iliyokuwa
na viti vizuri na maua ya
kupendeza.Kulikuwa na sehemu
nyingi za kukaa kupumzika na
baadhi ya wagonjwa walionekana
wakiwa wamekaa na madaktari
wao.Dr Susan akawaambia akina
Elvis waketi katika mojawapo ya
sehemu za kupumzikia na
wamsubiri akamlete Graca
“ Unafahamiana na Dr
Susan?akauliza Elvis baada ya Dr
Susan kuondoka.Bongani
akatabsamu na kusema
“ Ndiyo ninafahamiana naye
ni mtu wangu wa karibu sana
ndiyo maana umeona imekuwa
rahisi kuruhusiwa kuingia huku na kuonana na mgonjwa.Kwa
kawaida kuja kumuona mgonjwa
hapa huwa ni jambo lenye
utaratibu mrefu kidogo lakini
kwetu sisi imekuwa rahisi”
akasema Bongani huku
akitabasamu
“ Hata mimi nimeshangaa
kutokana na urahisi
huutulioupata tofauti kabisa na
nilivyokuwa nimetazamia”
akasema Elvis na mara kwa mbali
akatokea Dr Susan akiwa
amemshika mkono binti mmoja
mrefu mwembamba
mweupe.Walikuwa wakitembea
huku wakiongea na kucheka kama
marafiki wakubwa
“ Thats Graca” akasema
Elvis.Bongani akamtazama na
kusema Unasemaje Elvis?
“ Sikutegemea kama ni binti
mzuri kiasi hiki”akasema Elvis
huku bado akiendelea kumkodolea
macho Graca aliyekuwa akija
taratibu akiongozana na Dr
Susan.Baada ya kufika mahali
pale walipokuwa wamekaa
Bongani na Elvis
wakasimama,Elvis akamvutia
Graca kiti akaketi .Dr Susan
akakohoa kidogonakusmea
“ Bongani na Elvis huyu ndiye
Graca.Ni
mrembosana.Mnamuonaje?
akatania Dr Susan na wote
wakatabasamu
“Ni kweli ni mrembo sana”
akasema Elvis huku akiendela
kumkodolea macho niti yule
mwenye macho ya aibu.Graca alikuwa anaonekana ni mzima wa
afya na ilikuwa vigumu kuamini
kwamba alikuwa mgonjwa wa akili
“ She’s so pretty” akawaza
Elvis akiendelea kumtazama
Graca kwa macho ya kuibia
“ Graca hawa ni wageni wako”
akasema Dr Susan
“Huyu hapa anaitwa Mr
Bongani ni mwenyeji wa
Johannesburg na huyu hapa
anaitwa Elvis toka jijini Dar es
salaam.” Dr Susan akafanya
utambuliso
“ Karibuni sana” akasema
Graca kwa sauti ndogo na laini
“ Ahsante sana” wakajibu kwa
pamoja Elvis na Bongani
“ Elvis nadhani itakuwa
vyema tukiwaacha wewe na Graca
muongee.Graca hana matatizo yuko katika hali nzuri leo na
atakujibu kila kitu unachokihitaji
toka kwake” akasema Dr Susan
halafu yeye na Bongani wakainuka
wakaelekea katika benchi
lililokuwa mbali kidogo.
“ Pole sana
Graca.Unaendeleaje ? akaanzisha
maongezi Elvis
“ Ahsante sana
Elvis.Ninajisikia vizuri
sana.Umetokea Tanzania?
Akauliza Graca
“ Ndiyo nimetokea Tanzania.”
“Umenifahamuje? Tumewahi
kuonana?
“ Hatujawahi kuonana ila
nimekufahamu kupitia kwa David
Elifariji”
Graca akastuka mno baada
ya kusikia jina la David likitajwa. Umesema David Elifariji?
Unamfahamu? ”akauliza Graca
“ Ndiyo ninamfahamu
.Nmeonana naye kabla sijaja
huku”
“ Anaendelaje? Akauliza
Graca
“ Anaendelea vizuri” akajibu
Elvis.Graca akainamisha kichwa
machozi yakamtoka
“ Ninaitwa Elvis
tarimo”akasemaElvis na Graca
akainua kichwa akamtazama
“Ninafanya kazi katika idara
ya ujasusi nchini
Tanzania.Nilihitimu mafunzo ya
kijeshi na David halafu
nikaondoka kuelekea nchini
Marekani kwa mafunzo zaidi” Elvis
akanyamaza akamtazama Graca
kisha akasema “ Hivi majuzi kulitokea tukio
moja ambapo mwanamke mmoja
alipoteza fahamu kwa muda wa
miezi miwili.Alipozinduka
nilifanikiwa kumuhoji na akasema
kwamba aliyeamrisha apigwe hadi
auawe ni mwajiri wake ambaye ni
mfayakazi wa idara ya usalama
wa taifa.Nilimfanyia uchunguzi
mtu huyo na ndipo nilipogundua
kwamba alikuwa na mahusiano ya
karibu na baba yako Brigedia
jenerali Frank kwaju.Nilijiuliza
maswali mengi kuhusiana na
ukaribu huo na ndipo
nilipomkumbuka David.Wakati
naondoka kuelekea Marekani kwa
mafunzo,kesi ya David ilikuwa
bado ikiunguruma kwa hiyo
sikujua hatima yake.Ilinilazimu kumfuata David gerezani na
kuonana naye” akasema Elvis
“ Nimeonana na
David,nimeongea naye na
amenieleza mambo mengi
.Amenieleiza mkasa mzima
uliompelekea afungwe
gerezani.Toka ndani kabisa mwa
moyo wake amekiri kwamba
hakutenda lile kosa na
alibambikiwa ile kesi ya
ubakaji.Nilimuamini na kuahidi
kumsaidia na ndiyo maana
nimelazimika kuja kuonana
nawe.Kuna mambo ambayo
nahitaji kuyafahamu toka kwako
ambayo yatatusaidia katika
kumsaidia David anayetumikia
kifungo cha miaka thelathini
gerezani” akasema Elvis.Graca akainama na kutoa machozi na
kusema
“ Unataka nini toka kwangu?
“ Graca nimelisoma faili la
kesi.Kuna ushahidi mzito
uliotolewa ukiwemo wa daktari
aliyekufanyia uchunguzi na
kuthibitisha kwamba ni kweli
ulibakwa na David.Daktari huyo
aliyeithibitishia mahakama tayari
amekwishafariki na inasemekana
alifariki kwa sumu.Kilichonileta
hapa ni kufahamu ukweli toka
kwako kwani wewe ndiye
muhusika mkuu wa sakata hili.Ni
kweli David alikubaka? Ni kweli
wewe una matatizo ya akili kama
faili lako linavyoonyesha? akauliza
Elvis.Graca akainama na kuanza
kulia.Elvis akatoa kitambaa kisafi
na kumpatia Futa machozi .naomba
tafadhali nieleze kila kitu
unachokifahamu kuhusiana na
sakata hili.Ukweli wako ndio
utakaonipa nguvu ya kumsaida
David kutoka gerezani” akasema
Elvis.Graca akafuta machozi na
kusema
“ Sifahamu chochote
.Ulichokisoma katika faili ndicho
sahihi” akasema Graca huku
machozi yakimtoka.
Elvis alimtazama Graca kwa
makini na kisha akasema
“ Graca please tell me the
truth.Nimelipitia faili la kesi na
nimegundua mambo mengi
ambayo nina mashaka
nayo.Nimeongea na David amekiri
kwamba hakutenda lile kosa and I
do believe him.Ninataka nisikie pia na kwa upande
wako,unasemaje? Ninataka
nimsaidie David ambaye
anateseka gerezani kwa kosa
ambalo naamini hakulitenda
.Tafadhali naomba unieleze
ukweli” akasema Elvis.Graca
akaendelea kulia.Elvis akainuka
na kwenda kumshika bega.
“ Please Graca I need to know
the truth” akasema Elvis.Graca
akamtazama Elvis kwa makini
usoni na kusema
“ Kwa sababu ya David
nitakueleza ukweli”
“ Ahsante GracaYou are doing
the right thing”
Sekunde kadhaa zikapita
Graca akiwa kama mtu
anayekumbuka jambo halafu
akasema kwanza kabisa naomba
nikuweke wazi kwamba hauongei
na mgonjwa wa akili.Mimi si
mgonjwa wa akili na sikuwahi
kuwa na ugonjwa huo” akasema
Graca
“ Reall !!? Elvis akashangaaa
“ usishangae Elvis.Hakuna
anayejua jambo hili zaidi yangu na
nitakueleza baadae ni kwa nini
nimeletwa kutibiwa katika
hospitali hii ya magonjwa ya
akili”akasema Graca
“ tell me everything” akasema
Elvis
Graca akamtazama Elvis
usoni na kuendelea
“ Siku moja mama alifanikiwa
kuingia katika chumba cha baba
ambacho hukitumia kama ofisi
yake ndogo awapo nyumbani.Katika chumba hicho
hakuna yeyote ambaye
anaruhusiwa kuingia.Sifahamu
aligundua nini lakini alinipa
mkoba uliokuwa na kompyuta
ndogo mkononi akaniomba
nikaufiche mahala ambako
hakuna yeyote anayeweza
kuona.Jioni ya siku hiyo
kulitokea mzozo mkubwa baina ya
baba na mama.Nilimsikia mama
akimlaumu baba kwa kujiingiza
katika biashara haramu
.Sikuelewa mara moja ni biashara
zipi alizokuwa akiongelea mama
.Baada ya siku tatu toka utokee
mzozo ule mama alifariki dunia
katika ajali ya gari akiwa safarini
kuelekea Morogoro.Gari lake
lilipasuka tairi na kupinduka” Graca akainama na kufuta
machozi halafu akaendelea
“ Baada ya mama
kufariki,baba alinifuata na
kuniuliza endapo mama aliwahi
kunipa mzigo wowote
nikaufiche.Nilikataa kumweleza
ukweli ikamlazimu atumie vitisho
na ndipo nilipochukua lile begi na
kwenda kulificha kwa David
ambaye kwa wakatio huo tulikuwa
katika mahusiano ya
kimapenzi.Vitisho vilizidi na siku
moja baba alinikamata na
kunitesa sana akatishia kuniua
endapo nisingemuonyesha mahala
lilipo begi lake.Alinitesa sana
usiku huo.Kulipopambazuka
alfajiri nilidamka na kwenda
kuchukua lile begi kwa
David.Sikujua kama kuna watu waliokuwa
wananifuatilia.Nilipotoka niliona
kuna watu wawili wakishuka
garini.Niliwafahamu watu wale ni
washirika wa baba ikanilazimu
kupenya dirishani na kukimbia
na kwenda kulifcha begi lile
sehemu ninakojua.Saa tatu za
asubuhi nilipata taarifa kwamba
David amekamatwa kwa kosa la
ubakaji.Niliogopa sana kwani baba
alikwisha ahidi kufanya jambo
lolote kuhakikisha kwamba begi
lake linapatikana.Kwa namna
alivyonitesa na kunitisha niliogopa
kuna uwezekanao anaweza hata
kuniua hivyo ikanilazimu
kujifanya kama
nimechanganyikiwa hivyo
kuwafanya watu wamtaarifu baba
ambaye alinikamata na kunipeleka katika hospitali ya taifa kitengo
cha magonjwa ya akili.Pamoja na
kulazwa pale bado baba aliendelea
kuwasisitiza madaktari kwamba
wajitahidi ili niweze kupata nafuu
haraka lengo lake nikamuonyeshe
mahala lilipo begi lake.Niliendelea
kujifanya mgonjwa wa akili na
sikuonyesha dalili zozote za
kupata nafuu na ndipo baba
alipoamua kunileta huku afrika ya
kusini na kunitupa hapa.Toka
aliponileta hajawahi hata siku
moja kuja kuniangalia au hata
kunijulia hali.”akasema Graca na
kuanza kulia.Elvis akainuka na
kumshika bega akambembeleza
anyamaze.Graca akafuta machozi
na kuendela.
“Ukweli ni kwamba David
hakutenda kosa hilo alilodaiwa kulifanya,hakunibaka na wala
asingeweza kufanya hivyo kwa
sababu upendeo wake kwangu
hauna kipimo.Ninasikitika sana
Elvis kwa kuishi maisha haya
.Ninapewa madawa mengi makali
na kunifanya nidhoofu namna
hii.Sielewi nitaishi hivi mpaka
lini.Sitaki kujifanya nina nafuu
kwani baba atatarifiwa naatakuja
kunitoa hapa” Graca akashindwa
kujizuia kuangua kilio.Elvis
akainuka tena na kwenda
kumbembeleza
“ Nyamaza kulia Graca.”
akasema Elvis
“ Inauma sana Elvis.Ninasikia
maumivu makali ya
moyo.Uchungu ninaoupata
huelezeki” Pole sana Graca”akasema
Elvis halafu ukimya ukatawala
“ Kwa sasa nina hakika
lazima katika hilo begi kuna siri
nzito ambayo inamfanya brigedia
Franka asiwe hata na huruma kwa
mwanae.Mpaka Graca kuamua
kujifanya ni mgonjwa wa akilini
wazi aligundua kwamba baba yake
angeweza hata
kumuua.Ninachotaka kufahamu
toka kwa Graca kuna nini ndani
ya hilo begi? akawaza Elvis halafu
akakohoa kidogo na kuita kwa
sauti ya upole
“ Graca !!..
Graca akainua kichwa
akamtazama Elvis .
Machoyake yalikuwa mekundu .
“ Graca nimechomwa sana na
maelezo yako .Naelewa uko katka kipindi kigumu na cha mateso
makubwa.Nakuahidi kufanya kila
lililo ndani ya uwezo wangu
kukusadia wewe na David na
kuwaondoa katika mateso haya
mliyo nayo” akasema Elvis halafu
akavishika viganya vya mikono ya
Graca na kusema
“ Please trust me.I’ll do
anything I can to help you.I give
you my word” akasema Elvis
“ Ahsante sana Elvis .Naomba
kama una uwezo wa kunisaidia
tafadhali nisaidie.Mateso
ninayoyapata ni
makubwa.Nimechoka kuishi
maisha haya ya mateso lakini
naogopa kuondoka hapa kwani
baba akinipata atanifanyia jambo
baya.Nina hakika mpaka aleo hii
bado atakuwa akitaka kufahamu
 
Back
Top Bottom