Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESDANT

Sniehemu 40

fedha usiumize kichwa kwani
bado tunazo nyingi.Yawezekana
kweli David ameweza kutuzidi
akili na kuongeza fedha katika
mchanganuo ule wa wanasiasa
lakini bado tunazo fedha za
kutosha na mimi ndiye ninayetia
saini fedha itoke hivyo bado
tunayo nafasi ya kupiga hela
Pascal.Usiumie kwa vijihela hivi
vidogo alivyotupiga.Tuna trilioni
sita zimetengwa kwa ajili yetu
hivyo usijali tutakuwa mabilionea
hivi karibuni.Tuepushe
malumbano yasiyo na tija hasa
kwa wakati huu ambao mambo
yetu yanakwenda vizuri sana”
akasema Frank “Ninakuelewa Frank
lakini…………...”Pascal akataka
kusema kitu Frank akamzuia.
“Hakuna lakini Pascal,mjadala
kuhusu jambo hili nimeufunga na
sitaki uendelee tena.Mbona
hukunihoji mimi nilipotaja fedha
wanazohitaji viongozi wa jeshi
niliowashawishi wajiunge nasi?
“Wewe nakuamini Frank na
siwezi kuwa na shaka nawe hata
kidogo ila huyu David nina
mashaka naye sana”
“Pascal itakulazimu
kumuamini kwani mimi
ninamuamini David na sioni tatizo
lake.Mchango wake ni mkubwa
sana katika kufanikisha
operesheni hii hivyo kama kunatatizo lolote kati yako naye basi
liweke pembeni kwanza tumalize
operesheni yetu hii muhimu.Kesho
yule kenge Elvis anazikwa hivyo
inatubidi tuhudhurie na tufanye
utafiti kama tunaweza kumuona
Graca.Ninaamini lazima
atakuwepo kushuhudia nguzo
yake ikizikwa”
“Sawa Frank utanijulisha ni
muda gani tunakwenda huko
mazishini” akajibu Pascal na
kukata simu
“Pascal anaweza kuwa sahihi
kuhusiana na kiwango kile cha
fedha za kugharamia operesheni
mafuta yetu lakini sioni tatizo
kwani fedha bado ziko nyingi na
kila mmoja atapata.David anataka mimi na yeye tutafute namna ya
kuweza kuchota shilingi trilioni
mbili kutoka katika zile fedha
tulizotengewa.Hili ni wazo zuri
lakini tutawezaje kuchota fedha
hizo bila ya wengine
kufahamu?Amesema atakuja na
mpango ngoja nisubiri nione
mpango huo ili tufanye
maamuzi.Kama tukifanikiwa
katika huo mpango nitakuwa
bilionea na hata ile biashara ya
silaha nitaachana nayo kwani
tayari imeingia mdudu.Mpango wa
mapinduzi nao ukifanikiwa
nitakuwa waziri wa ulinzi.Mambo
yanazidi kuninyookea.Huu ni
mwaka wangu” akawaza Frank
*****************
Kumepambazuka na tayari
kijua kimeanza kuchomoza.Ni siku
ambayo Elvis anatakiwa
kuzikwa.Hadi kunapambazuka
Elvis alikuwa macho.Hakuweza
kupata usingizi kutokana na
mawazo mengi aliyokuwa nayo
kuhusiana na kile kinachokwenda
kutokea siku hii.Akiwa katika
mawazo mengi akasikia kengele ya
getini ikilia kwa nguvu akainuka
na kwenda kwa tahadhari
kuangalia mgongaji akakutana na
Steven.
“Steven umelala wapi
leo?akauliza “C’mon Elvis mbona unauliza
swali kama vile hufahamu mji huu
ni wangu?
“Steven ninataka
kukukumbusha kwamba bado uko
katika uangalizi wangu.Mambo
yako utayafanya pale
nitakapokuacha uende lakini kwa
sasa utalazimika kufuata kile
nitakachokuelekeza.Umelala
mahala kusiko julikana ni vipi
endapo ungefikwa na jambo baya
huko?
“I’m sorry Elvis.It wont
happen again” akasema Steven
“Jitahidi lisijitokeze tena
jambo kama hili.Zingatia nidhamu
katika kazi” Nimekuelewa Elvis.Vipi
unaendeleaje?
“Ninaendelea vyema”
“Good to hear that”akasema
Elvis.Steve akamtazama machoni
kwa muda na kusema
“Elvis japokuwa machoni
hauonyeshi lakini moyoni
nafahamu una hofu
kubwa.Ninakuomba ondoa
hofu.Sisi sote tuko nyuma
yako.Sote tuko pamoja na
tutafanya kila lililo ndani ya uwezo
wetu kuhakikisha mpango huu
unafanikiwa kama
tulivyoupanga.You’ll be fine
brother” akasema Steven
“Thank you Steven.I’ll be fine”
akasema Elvis “Dr Philip na akina Doreen
wamekwisha amka?
“Dr Philip bado amelala ila
Doreen hakurejea hapa amelala
msibani .Lazima awe karibu na
Patricia”
“Oh ! kumbe Doreen na
Patricia ni marafiki?
“Steven haya mambo
hayakuhusu.Nenda kamuamshe Dr
Philip tuanze kujiandaa kwa siku
kubwa ya leo.Usisahau kubadili
shati kuna alama za rangi ya
mdomo” akasema Elvis na kuingia
chumbani kwake akajilaza
kitandani na kuzama tena
mawazoni.Baada ya kama dakika
kumi hivi akasikia kengele ya
mlangoni ikilia akainuka na kwenda kuangalia nani alikuwa
getini akakutana na mkurugenzi
wake Meshack Jumbo akamsalimu
na kumkaribisha sebuleni.
“Vipi hali yako Elvis?
“Naendelea vyema mzee”
“Uko tayari kuikabili siku ya
leo?
“Niko tayari mzee usihofu.Vipi
huko msibani mambo
yanakwendaje? Akauliza Elvis na
kabla Jumbo hajajibu kitu Steven
na Dr Philip wakaingia pale
sebuleni na kumsalimu
“Habari zenu vijana
wangu.Nimepita mara moja kuja
kujua maendeleo yenu hapa”
“Tunaendelea vyema
mzee.Maandalizi kwa karibu asilimia tisini yanakwenda
vizuri.Jeneza liko tayari na
tumelifanyia majaribio liko
safi.Upande wa kaburi kuna
mambo machache ya kumalizia na
Steven ataelekea huko asubuhi hii
kuhakikisha kila kitu kimekwenda
vizuri” akasema Dr Philip.
“Vizuri sana.Huko msibani
mambo yanakwenda vizuri
pia.Ndugu wa muhimu wote tarai
wamewasili na ratiba
haijabadilika,mazishi ni
leo.Niliwaomba wanipe suti kwa
ajili ya kumvisha marehemu na iko
katika sanduku lile nililokuja
nalo.Kwa ujumla kule msibani
mambo yote nimeyaweka sawa.Nataka kujua mpangilio
wenu huku umekaaje?
“Mpangilio wa leo umekaa
hivi.Tutaondoka hapa saa saba za
mchana na kuelekea nyumbani
kwa Dr Rajeshi na pale ndipo
shughuli itakapoanzia.Elvis
atachomwa sindano ya kumlaza na
kupakiwa katika gari la wagonjwa
kuelekea hospitali ambako
taratibu za kumuweka katika
jeneza zitafanyika.Saa tisa alasiri
litakuja gari maalum na kuubeba
mwili kisha kuupeleka nyumbani
ambako tutafika mida ya saa kumi
au kumi na moja.Tutachelewa
kuupeleka mwili nyumbani,kwani
sindano atakayochomwa Elvis
itamchukua zaidi ya saa tano au
sita na tunataka tufike makaburini
jioni ili shughulizi fanyike haraka
haraka na watu watawanyike na kuwaacha mafundi wakiendelea na
shughuli za kulifunika kaburi na
hapo ndipo tutakapopata na sisi
nafasi ya kuweza kumtoa Elvis na
kuondoka naye kwani wakati huo
tayari kiza kitakuwa kimeingia.Sisi
ratiba yetu imekaa hivyo.Wewe
ndiye utakayeshughulikia ratiba
ya nyumbani” akasema Dr Philip
“Vizuri.Ni ratiba nzuri na
inakwenda kama tulivyokwisha
kubaliana.Kuhusu kule nyumbani
msiwe na wasi wasi wowote.Kila
kitu kitakwenda sawa.Najua
kutaibuka maswali kwa nini mwili
umechelewa kufika msibani lakini
nitatafuta kisingizio
chochote.Baada ya kufika mwili
ndugu wachache wataaga mwili
huo ndani pamoja na viongozi
wachache na wafanyakazi kisha itasomwa ibada fupi na kuelekea
makaburini”
“Angalizo lingine,jeneza
libabebwa na watu maalum tu
walioandaliwa na hakuna mtu
mwingine kusogelea
jeneza.Shughuli zote watuachie
sisi” akasema Dr Philip
“Hilo tayari nimekwisha
wajulisha na
wanalifahamu.Shughuli zote za
kuandaa mwili hadi kuuingiza
kaburini ni la kwetu hivyo
hakutakuwa na tatizo lolote”
akasema Meshack Jumbo na kutoa
maelekezo mengine kisha
akaondoka kuelekea msibani na
kuwaacha vijana wake
wakiendelea na maandalizi
***************
Saa tano za asubuhi ,waziri
mkuu mstaafu David Sichoma
akiwa katika ofisi yake ya
nyumbani simu yake
ikaita,alikuwa ni Dr Makwa
“Habari yako Dr Makwa?
Akasema David baada ya kupokea
simu ile
“habari nzuri ndugu
David.Natumai u mzima wa afya”
“Mimi mzima kabisa.Sijui nyie
huko mnaendeleaje?
“Tunaendelea vyema”
“Nafurahi kusikia hivyo”
akasema David na sekunde kadhaa
za ukimya zikapita
“Bwana David nimekupigia ili
kupata ufafanuzi toka kwako
baada ya kushindwa kuelewana na
mjumbe uliyemtuma kwangu” Mjumbe?!! David akashangaa
“Ndiyo.Yule kijana
uliyemtuma aje kupata ufafanuzi
wa kina kuhusiana na ule
mchanganuo wa operesheni
mafuta yetu niliokukabidhi jana na
tukaufikia muafaka,iweje leo
umtume kijana aje kutaka maelezo
ya kina? Kama hukuridhishwa na
mchanganuo wetu ungetueleza
toka jana kuliko hili la kututaka
tuandike mchanganuo mwingine
na kupunguza gharama.Dont you
trust us David?Dr Makwa akauliza
“Dr Makwa kabla sijasema
chochote kwanza nakuomba
ondoa hasira ili tuweze
kuzungumza hiki
kilichotokea.Naomba usikasirike
ndugu yangu”
“Nitaachaje kukasirika David
wakati umeshindwa kutuamini nakuamua kunitumia kijana
jeuri.Nashangaa umeshindwa hata
kunipigia simu tukazungumza
badala yake ukaamua kunitumia
kijana yule?
“Dr makwa uko wapi sasa
hivi? Akauliza David
“Niko hapa katika ofisi kuu ya
chama ila nitatoka muda si mrefu
ninakwenda kukutana na
wenyeviti wenzangu ambao kwa
pamoja tumeandaa operesheni
mafuta yetu ili tukalijadili suala
hili na kutoa maamuzi.Hakuna
maana ya kushirikiana tena na mtu
ambaye hatuamini”akasema Dr
makwa akionyesha kuwa na hasira
“Dr Makwa tafadhali
nakuomba usifanye jambo lolote
kwa sasa.Naomba tuonane hapa
nyumbani kwangu.Ninakusubiri
hapa naomba uje tuzungumze ndugu yangu nakuomba sana”
akasema David
“Sawa David.Ninakuja hapo
kwako sasa hivi” akajibu Dr
Makwa na kukata simu
“Nani huyu aliyekwenda kwa
Dr Makwa na kutaka ufafanuzi wa
ule mchanganuo wa operesheni?
Naamini lazima atakuwa ni mmoja
wa watu tunaoshirikiana katika
operesheni mapinduzi.Ni nani kati
yao? Akajiuliza David
“Huyu anaweza kuwa
Pascal.Lazima atakuwa ni
yeye.Jana hakuonyesha
kuridhishwa na mchanganuo wa
operesheni mafuta yetu.Naamini
atakuwa ndiye aliyemfuata Dr
Makwa na kutaka ufafanuzi akidai
ametumwa na mimi.Haya ndiyo
madhara ya kushirikiana na vijana
wenye tamaa kama hawa katika mambo mazito kama haya.Kama
kweli ni yeye ndiye aliyefanya hivi
atakuwa amevuka mstari na
ninaapa ataiona nguvu
yangu.Haikuwa kazi nyepesi
kuingia makubaliano na wale
wanasiasa na baada ya mambo
kwenda vizuri huyu kijana
mshenzi anataka kuharibu kila
kitu kwa tamaa zake.Kama ni yeye
nitamuonyesha,siwezi katu
kukubali aharibu ndoto zangu za
kuwa rais.Ngoja nimsubiri Dr
Makwa ili nimfahamu huyo mtu
aliyekwenda kwake na kudai
ametumwa na mimi” akawaza
David na kumuagiza mtumishi
wake amletee pombe kali
Dakika thelathini na tano
zilikatika ndipo Dr makwa
akawasili nyumbani kwa David namoja kwa moja wakaeleka
bustanini
“Dr makwa awali ya yote
nakuomba samahani sana kwa
usumbufu huu mkubwa
uliotokea.Naomba nifahamu nini
hasa kilitokea? Nieleze kila kitu
tafadhali”
“Nikiwa ofisini kwangu nikiwa
na mazungumzo na watendaji wa
chama,nikataarifiwa kwamba kuna
mgeni toka kwako nikajua kuna
jambo la muhimu nikaahirisha
kikao na watendaji
nikamkaribisha yule mtu
wako.Alitoa katika mkoba wake
kitabu cha mchanganuo
nilichokukabidhi jana.Alisema
kwamba umemtuma ili apate
maelezo ya kina kuhusiana na
mchanganuo ule.Nilishangaa sana
lakini nikalazimika kuchukua muda kumpa ufafanuzi japo kwa
ufupi ili aweze kupata picha
namna mpango wetu ulivyokaa
lakini hata baada ya kumpa
maelezo hayo akasema kwamba
mchanganuo ule haufai na
tuandike upya.Naomba nikueleze
ukweli nimefadhaishwa sana na
kitendo hiki David.Sikutegemea
kabisa kama ungeweza kutufanyia
hiki ulichotufanyia.Tulikuheshimu
tukajua tumepata mshirika lakini
kumbe nawe huna
msimamo.Tayari nimeitisha kikao
na wenyeviti wa vyama na
kikubwa tunakwena kuwaeleza
hali halisi na kisha tukubaliane
kutokuendelea na operesheni hii”
akasema Dr Makwa na David
akavuta pumzi ndefu
“Dr Makwa toka uliponipigia
simu na kunieleza kuhusu jambo hili,akili yangu imeshindwa
kutulia kabisa na ndiyo maana
unaniona na hii chupa ya mvinyo
nikijaribu kuweka kichwa
sawa.Naomba uniamini ndugu
yangu kwamba huyo kijana
aliyekufuata mimi sijamtuma.Katu
siwezi kufanya jambo la kijinga
namna hiyo” akasema David
“Hukumtuma?!! Dr makwa
akashangaa
“Ndiyo.Sijamtuma kwako”
“Kama hukumtuma amepataje
kile kitabu cha mchanganuo
nilichokukabidhi jana?
“Huyo kijana yukoje?
Alijitambulisha anaitwa
nani?David akauliza
“Ni mrefu wastani
mwembamba na ndevu zake
amezitengeneza kwa mtindo wa
duara kuzunguka kidevu chake.Alijitambulisha anaitwa Joel
Kupaya”
Sura ya David ikabadilika na
kupandwa na hasira
“That bastard !! akasema kwa
hasira
“Tayari nimekwisha
mfahamu.Jina lake ni Pascal na si
Joel kama alivyokueleza.Naomba
uniamini Dr Makwa kwamba huyo
jamaa mimi sijamtuma”
“David ninakuamini sana
lakini kwa hili inaniwia ugumu
kukuamini kwa sababu huyo
jamaa alikuwa na kitabu cha
mchanganuo ambacho
nilikukabidhi jana.Amefahamuje
kuhusu mpango wetu wa kuandaa
operesheni mafuta yetu?Kama
kweli hukumtuma nieleze
amefahamuje kuhusu jambo hili la
siri? David akamimina mvinyo
katika glasi akanywa na kusema
“Dr Makwa kwa hapa ilipofika
sina ujanja zaidi ya kukueleza
ukweli ila nakuomba na kukuonya
kwamba yale nitakayokuambia
yatabaki kuwa siri yako na
hapaswi mtu mwingine
kuyafahamu.Chunga sana mdomo
wako na uufunge kabisa”
“Niamini David” akasema Dr
Makwa
David akamueleza Dr makwa
kila kitu kuhusiana ule mpango wa
mapinduzi.Dr Makwa akajikuta
akilazimika kuvua koti baadaya
kuhisi joto
“Kwa nini ukanificha jambo
hili David? Kwa nini hukunieleza
kilicho nyuma ya pazia? Akauliza
Dr Makwa “Huu ni mpango wa siri kubwa
na ambao huwezi kumueleza kila
mtu .Kitu cha muhimu ni kwamba
tayari umeufahamu hivyo nataka
uufumbe mdomo wako na pili
uhakikishe kwamba operesheni
mafuta yetu inafanyika na
kufanikiwa.Nakuahidi Dr Makwa
kama mipango yetu itakwenda
vizuri na tukafanikiwa kuchukua
nchi basi wewe ndiye utakayekuwa
waziri mkuu” akasema David na
kukawa kimya
“Unasemaje kuhusu hilo Dr
Makwa? Akauliza David
“I’m speechless.Nashindwa
niseme nini ila nashukuru kwa
kuamua kunieleza ukweli na
kuniahidi nafasi ya uwaziri
mkuu.Nakuahidi ushirikiano
mkubwa na operesheni yetu
itaendelea na itakuwa moto zaidi kuliko hata tulivyopanga
awali.Pamoja na haya kuna jambo
bado linanipa mashaka
sana.Inakuaje katika operesheni
nzito kama hii ukamuhusisha
kijana mshenzi kama yule?
“Sikuwa nikifahamu chochote
hadi nilipoitwa na brigedia Frank
Kwaju ambaye ni rafiki yangu wa
muda mrefu nikahudhurie kikao
muhimu na ndipo nilipokutana na
watu hao na huyo jamaa Pascal
akiwemo.Si mimi niliyemchagua
awemo katika timu bali ni brigedia
Frank kwani ni rafiki yake
mkubwa.Ni kijana mshenzi sana
wa tabia na jana tu katika kikao
nilipowasilisha mchanganuo wenu
ndipo mambo
yalipoanza.Hakukubaliana na kiasi
cha fedha nilichokitaja cha
kugharamia operesheni mafuta yetu na ndiyo maana leo hii
amekufuata ili ajiridhishe”
“Frank nakushauri rafiki
yangu,get rid of him.Fanya kila
uwezalo kumuondoa katika
timu.Hii ni operesheni nzito mno
na mtu kama yule hapaswi kuwa
katika timu” akasisitiza Dr Makwa.
“Usihofu Dr Makwa.Yule
kijana ni kama vumbi tu ambalo
naweza kulipuliza muda wowote
na likapotea
hewani.Nitamshughulikia na
hatakuwa tena kikwazo kwetu”
“Litakuwa jambo la busara
sana”
“Dr Makwa narudia tena
kukusisitiza kwamba jambo hili ni
la siri kubwa na hata mke wako
hapaswi kulifahamu.Wote tuliomo
katika mpango huu tumekula
kiapo cha kutokutoa siri na yeyote atakayethubutu kutoa siri hii
tutamuua”
“Usiwe na hofu yoyote kuhusu
mimi siwezi kutoa siri kwa jambo
nyeti kama hili wakati mimi
mwenyewe usiku na mchana
ninaota kuwa na madaraka
makubwa.Hii ni nafasi ya pekee ya
kutimiza ndoto yangu ya muda
mrefu ya kushika nafasi
kubwa.Naomba uwe na amani
David siri hii iko salama” akasema
Dr Makwa halafu wakaendelea na
mazungumzo yao mengine.
*****************
Mshale wa saa ulionyesha
tayari imetimu saa saba za
mchana.Ni muda ambao Elvis
alipaswa kuondoka katika makazi
yake na kuelekea nyumbani kwa Dr Rajesh ambako shughuli
ingeanzia hapo.Tayari alikwisha
jiandaa alikuwa amevaa ile suti
aliyoletewa na Meshack
Jumbo.Graca hakutaka kabisa
kumuona Elvis wakati akiondoka
alikuwa amejifungia chumbani
kwake.Elvis akawaomba akina
Steven wamsubiri kwa dakika
chache akamuage Graca.Mlango
ulikuwa umefungwa,akakiminya
kitasa mlango ukafunguka
akaingia ndani na kumkuta Graca
amekaa kitandani na mkononi
akiwa ameshika kitambaa
kilicholoa machozi yaliyokuwa
yanamtiririka.Alipomuona Elvis
machozi yakazidi.Elvis akamfuata
na kuketi pembeni yake
“Tafadhali usilie Graca.Wewe
ni mwanamke jasiri sana.Umepitia
mambo mengi mazito kwa hiyo naamini hata hili utaweza
kulihimili.Tafadhali futa machozi
na badala ya kulia tumuombe
Mungu ili jambo hili liende vizuri
kwani ni kwa manufaa ya wengi”
akasema Elvis na kumpatia Graca
kitambaa kingine.
“Futa machozi na uzame
katika maombi” akasema Elvis na
Graca akafuta machozi
akamtazama Elvis
“Elvis are you sure you want
to do this?
“Yes.I have to do this.Hakuna
namna nyingine ya kulimaliza
suala hili zaidi ya kufanya hivi.I
have to die Graca”
“What about me ? Graca
akauliza
“Come here” akasema Elvis na
kumkumbatia Graca huku
akimpiga piga mgongoni Nilikuahidi utakuwa salama
hivyo niwepo au nisiwepo bado
ahadi yangu iko pale pale.Tayari
suala lako liko katika mikono
salama hivyo ikitokea operesheni
ikashindwa kufanikiwa basi wapo
watu ambao watalishughulikia
suala lako lakini nina uhakika
mkubwa kwamba kila kitu
kitakwenda vizuri.Jioni ya leo
ikimpendeza Mungu tutakula
chakula cha usiku
pamoja.Nimekuja kukuaga Graca
muda umefika wa mimi kwenda”
akasema Elvis
“Elvis najua siwezi kukuzuia
usifanye jambo hili ila kabla
hujaondoka ninapenda nikwambie
kwamba wewe ni mtu muhimu sna
kwangu.Wewe ni zaidi ya ndugu au
rafiki.Sijawahi kukutana na
binadamu mwenye roho ya huruma kama wewe na ndiyo
maana machozi hayakauki
nikifikiria kwamba nimekufahamu
kwa kipindi kifupi na sasa
unaingia katika jambo ambalo
linaweza kusababisha ukapoteza
uhai endapo hata kosa dogo
litafanyika,pili jambo hili
likifanikiwa maisha yako
yatabadilika kabisa na hautaishi
kama ulivyokuwa ukiishi
awali.Mambo haya mawili
yananiumiza mno lakini kama
ulivyosema ni kwamba lazima
ufanye jambo hili.Nimepitia mengi
magumu lakini hili limekuwa
gumu mno kwangu hata hivyo
nitadumu katika maombi na nina
imani utakuja kula chakula
nitakachokuandalia.Tafadhali
niahidi kwamba utarejea salama” akasema Graca huku michirizi ya
machozi ikionekana machoni pake
“Graca ..” Elvis akataka
kusema kitu na kunyamaza baada
ya mlango kugongwa
“Graca this is it.I have to go
now” akasema Elvis na
kuinuka.Graca naye akasimama
akamkumbatia Elvis na kumbusu
“I love you Elvis.Please don’t
die” akasema na kumuachia Elvis
akaenda kukaa kitandani.Elvis
akamtazama na bila kusema
chochote akafungua mlango na
kutoka
“Muda unakimbia sana
Elvis.We have to go” akasema
Steven aliyekuwa amesimama nje
ya chumba cha Graca.Tayari jeneza
lilikwisha pakiwa katika gari lenye
vioo vyeusi . Are you ready Elvis? Akauliza
Dr Philip aliyekuwa katika usukani
“I’m ready.Let us go ! akasema
Elvis na safari ikaanza
“I love you Elvis.Please don’t
die” maneno haya ya Graca
yakajirudia kichwani kwa Elvis
“Nimemuweka Graca katika
wakati mgumu sana.Ananitegemea
sana mimi katika kujenga upya
maisha yake hivyo kitendo cha
mimi kwenda kuzikwa kimempa
wasiwasi sana.Ana hofu na hatima
ya maisha yake endapo
nitakufa.Naamini mambo
yatakwenda vizuri ili niweze
kurejea na kumsaidia huyu binti
mwenye uzuri wa kipekee kabisa”
akawaza Elvis na picha ya Patricia
ikamjia
“Leo ni siku ngumu sana kwa
Patricia.Mume,rafiki,faraja yake,nguzo yake anakwenda
kuwekwa kaburini.Sipati picha ni
uchungu kiasi gani
alionao.Nimemsababishia donda
ambalo haliwezi kupona.Mimi
nilikuwa kila kitu kwake na kuna
uwezekano asione thamani ya
kuendelea tena kuishi bila mimi.Ni
mwanamke anayenipenda
kupindukia.Ninajuta kwa nini
sikuyasikiliza mawazo yake pale
aliponiuliza kwanini katika kazi
zote nikachagua kuifanya kazi hii?
Haya ndiyo matokeo yake.Hata
hivyo sipaswi kujilaumu sana
kwani jambo hili ninalokwenda
kulifanya ni kwa manufaa ya nchi
na watu wasio na hatia wanaouawa
kutokana na silaha zinzouzwa na
genge la akina Brigedia
Frank.Huko waliko waanze
kujiandaa kwani kiama chao kinakuja.Wao ni sababu ya mimi
kutunga uongo huu mkubwa na
kuwaumiza wengi hasa mke wangu
Patricia.Hakuna ambaye
anahusika na mtandao huu
atakayebaki salama.Hakuna jiwe
litasalia juu ya
jiwe.Nitawasambaratisha
wote.Waombe nilale usingizi wa
moja kwa moja lakini kama
nikifanikiwa kuamka basi
wamekwisha” akawaza Elvis
******************
Dr Makwa Tusangira alimaliza
mazungumzo na waziri mkuu
mstaafu David Sichoma na
kuondoka.David akiwa na hasira
zisokifani akaichukua chupa ya
mvinyo na bila kumimina katika
glasi akagugumia kwa pupa.Mambo aliyoelezwa na Dr
makwa yalimkasirisha mno
“Pascal umevuka mstari na
siwezi kukuvumilia zaidi ya
hapa.Umekosea sana kutaka
ushindani na mimi.Inaonekana
bado hujanifahamu vyema.Katu
siwezi kukubali mambo yangu
yakaharibika kwa sababu
yako.Huko uliko vuta pumzi ya
mwisho mwisho kwani hutaliona
jua la kesho” akawaza David na
kuchukua simu akazitafuta namba
za makamu wa rais Dr Shafi
Abdulkareem Omar akampigia
“Habari yako mheshimiwa
David” akasema Dr Shafi baada ya
kupokea simu
“Nzuri kabisa mheshimiwa
makamu wa rais.Pole na
majukumu” “Ahsante sana .Vipi mambo
yanakwendaje?
“Mambo yanakwenda vyema
Dr Shafi usihofu.Nimekupigia
kukujulisha kwamba nitakuwa na
kikao nawe kesho jioni ili nikupe
kwa kina maendeleo ya ule
mpango wetu.Ningeomba tukutane
hapa nyumbani kwangu mida ya
jioni”
“Nashukuru sana mhshimiwa
David.Nitafika bila kukosa hiyo
kesho”
“Sawa Dr Shafi.Kuna jambo
lingine nahitaji msaada wako”
“Sema David nikusaidie nini?
“Kuna mtu mmoja anaitwa
Pascal Situmwa ni mfanyakazi wa
idara ya usalama wa taifa.Huyu
anaweza kuwa kikwazo kikubwa
sana katika kufanikisha mipango
yetu.Naomba aondolewe haraka sana .Hili ni jipu ambalo hatupaswi
tusubiri litumbuke
lenyewe.Nahitaji litumbuliwe
haraka sana”
“Umesema anaitwa Pascal
Situmwa? Dr Shafi akauliza
“Ndiyo.Anaitwa Pascal
Situmwa”
“Sawa nitamshughulikia kama
yule mwingine.Endapo kuna mtu
yeyote anayeonekna kuwa
kikwazo nijulishe mara moja ili
tuweze kumshughulikia haraka”
“Ahsante sana Dr
Shafi.Tutaonana hiyo kesho jioni”
akasema David na kukata simu
Mara tu alipomaliza
kuzungumza na David ,Dr Shafi
akazitafuta namba za simu za
Meshack Jumbo na kumpigia Meshack Jumbo habari yako
mzee wangu” akasema Dr Shafi
baada ya Meshack kupokea simu
“Habari nzuri sana
mheshimiwa makamu wa rais”
“Nafurahi kusikia hivyo.Uko
wapi mida hii?
“Niko kwenye msiba wa
Elvis,leo ndiyo mazishi yake”
“Sawa Meshack.Naomba baada
ya shughuli za mazishi kumalizika
uwasiliane nami kuna jambo
nataka kuzungumza
nawe.Tafadhali usilale bila
kwasiliana nami”
“Nitafanya hivyo mheshimiwa
rais” akasema Meshack
“Good” akajibu Dr Shafi na
kukata simu
“Dr Shafi ana tatizo gani?
Jambo gani anataka kuniambia?Au
kuna jambo amelihisi kuhusiana na kifo cha Elvis? Au amepata
taarifa kuhusu Steven kuondolewa
katika kizuizi? Meshack akajiuliza
“Nitafahamu kila kitu hiyo
jioni nitakapokutana naye lakini
Steven anapaswa kuwa katika
tahadhari na asionekana hapa
msibani kwani wengi wa watu
anaofanya nao kazi watakuwepo
hapa”
Meshack akachukua simu na
kuzitafuta namba za Dr Philip
akampigia
“Philip mambo yanakwendaje
huko? Akauliza baada ya Dr Philip
kupokea simu
“Huku mambo yanakwenda
vyema.Vipi huko mambo
yanakwendaje? Nipe habari
mmefikia wapi? Tumefika hapa nyumbani
kwa Dr Rajesh na muda si mrefu
Elvis ataingizwa katika usingizi”
“Vizuri sana.Kuna jambo
nataka ulizingatie.Steven
asionekane hapa msibani.Nina
wasi wasi taarifa za yeye kutoka
katika kizuizi tayari zimejulikana
hivyo yatupasa kuwa
makini.Shughuli ikimalizika hapo
nyumbani kwa Rajesh arejee
katika makazi yao akaendelee
kupumzika na mambo mengine
yote akuachie wewe”
“Sawa nimekuelewa
mzee.Tutafanya
hivyo.Nitawasiliana nawe baada ya
mambo kukamilika hapa” akasema
Dr Philip na kukata simu
“Meshack Jumbo anahisi
taarifa za Steven kutoka kizuizini
zimevuja hivyo anamtaka Steven asionekane msibani” Dr Philip
akawaeleza akina Elvis
“Nini kimetokea hadi akahisi
hivyo? Elvis akauliza
“Ndugu zangu,nilitolewa
kizuizini kwa ajili ya kusaidia
katika operesheni hii hivyo lazima
niishiriki kikamilifu hadi mwisho
wake.Nitafika msibani lakini
sintashuka garini.Lolote linaweza
kutokea hapo msibani hivyo
yatupasa sote tuwepo karibu na
Elvis kwa ajili ya kutoa msaada wa
haraka pale utakapohitajika”
akasema Steven
“Wazo la Steven ni
zuri.Tunahitajika wote kushiriki
operesheni hii hadi mwisho hivyo
lazima awepo msibani lakini
atabaki garini” akasema Dr Philip
“Sawa.Tuendelee na mipango
yetu.Muda unakwenda sana” akasema Elvis.Dr Philip akatoa
kichupa cha dawa na kuivuta
katika bomba la sindano
akahakikisha ameweka kipimo
sahihi
“Elvis this is it.Kuna kitu
chochote unataka kukisema kabla
sijakuchoma sindano hii?
Elvis akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Endapo itatokea bahati
mbaya nikalala usingizi wa moja
kwa moja fikisheni ujumbe huu
kwa mke wangu Patricia kwamba
ninampenda sana.Pili nataka Graca
asaidiwe.Atolewe hapa nchini na
apelekwe nje ya nchi.Yeye ndiye
chimbuko la operesheni hii na
nilimuahidi kumsaidia kuyaanza
upya maisha yake hivyo naomba
mnisaidie kuitimiza ahadi
hiyo.Mkurugezni tayari analifahamu jambo hili” akasema
Elvis
“Anything else ? Steven
akauliza.Elvis akamtazama
akatabasamu na kusema
“Kama nikifariki,Steven
nakuonya usijenge mazoea na mke
wangu.Kaa naye mbali
kabisa.Nakufahamu wewe ni
kiumbe mchafu wa tabia” akasema
Elvis na wote wakacheka
“I’m ready” akasema Elvis na
Dr Philip akamchoma sindano
“Hesabu kuanzia kumi
kushuka chini” akasema Dr Philip
“Ten! Elvis akaanza kuhesabu
“Nine…..Eight…..Seven….SS..Si
…..Sixxx…..” Hilo ndilo lilikuwa
neno la mwisho Elvis
kulitamka.Kitanda kikaletwa
akapakiwa katika gari la wagonjwa kisha safari ya kuelekea hospitali
ikaanza
*******************
Saa nane na dakika kumi za
mchana,mke wa rais aliwasili
nyumbani kwa Bi Tarimo
akimuwakilisha rais katika
mazishi ya Elvis.Watu walikuwa
wengi sana.Nyimbo za kuwafariji
waombolezaji zilikuwa zinapigwa
wakati mwili wa marehemu
ukisubiliwa kuwasili hapo
nyumbani.Picha mbalimbali za
maisha ya Elvis zilikuwa
zinaonyeshwa kupitia runinga
kadhaa zilizosambazwa katika
sehemu walizokaa waombolezaji
Meshack Jumbo aliyekuwepo
pale msibani kuhakikisha mambo
yanakwenda kama walivyopanga alimtaarifu mwongozaji shughuli
kwamba mwili utachelewa kidogo
kuwasili pale nyumbani hivyo
ikalazimu zoezi la chakula
liendelee.Wakati watu
wakiendelea kupata
chakula,Meshack akakutana na
kamati ya mazishi na kuwajulisha
kwamba mwili utachelewa
kuwasili pale nyumbani hivyo
italazimu ratiba ifupishwe ili
kuwahi mazishi.Ilimlazimu
kutunga sababu za uongo za mwili
kuchelewa na akaeleweka
Saa kumi na dakika nane gari
maalum lililobeba mwili wa Elvis
likawasili likiwa limeongozana na
gari la wagonjwa ambamo ndani
yake alikuwepo Dr Philip na Dr
Rajesh.Kulikuwepo pia na gari
lingine aina ya V8 ambalo
alikuwemo Steven na rafikiye Ben na mwisho kulikuwa na gari
lililobeba wafanyakazi nane
kutoka kampuni ya kushughulikia
mazishi ambao tayari walikwisha
pewa maelekezo maalum ya nini
cha kufanya pale msibani
Muongozaji shughuli
akawajulisha waombolezaji
kuwasili kwa mwili wa marehemu
na vilio vikaamka.Meshack jumbo
akatoka na kukutana na Dr Philip
na Rajesh akawapa maelekezo na
mwili wa Elvis ukashushwa katika
gari na wale jamaa waliovalia sare
maalum ambazo ni suruali nyeusi
na makoti meupe.Hakuna
aliyeruhusiwa kubeba jeneza zaidi
yao
Jeneza liliingizwa moja kwa
moja katika chumba maalum
kilichoandaliwa kwa ajili ya ndugu
wa karibu kutoa heshima za mwisho.Vilio vilikuwa vikubwa
sana pale jeneza lilipoingizwa
ndani.Ilimlazimu Meshack Jumbo
kuchukua kipaza sauti na kutoa
maelekezo
“Ndugu zangu waombolezaji
mtatuwia radhi sana kwa mwili
kuchelewa kuwasili hapa
nyumbani.Hii ni kutokana na
sababu zilizo nje ya uwezo
wetu.Kutokana na kuchelewa huko
itatulazimu kufupisha ratiba yetu
hapa nyumbani ili tuweze kuwahi
makaburini kumpumzisha ndugu
yetu.Zoezi la kuuaga mwili wa
marehemu litafanywa na watu
wachache tu ambao ni ndugu wa
karibu,viongozi wa serikali na
wafanyakazi wenzake
wachache.Wengine wote
mtawakilishwa na hao.Hii ni
kutokana kwanza kuokoa muda,vile vile mwenzetu aliumia
vibaya hasa sehemu za
kichwani.Baada ya zoezi hilo
kumalizika jeneza litatolewa nje
na ibada itafanyika kisha salamu
za rambi rambi zitatolewa haraka
haraka.halafu sote tutaelekea
makaburini kumpumzisha ndugu
yetu.naomba tuheshimu ratiba
hiyo tafadhali” akasema Meshack
Jumbo kwa msisitizo
Jeneza likafunuliwa kwa ajili
ya watu maalum kutoa heshima
zao za mwisho.Elvis alikuwa
amelala ndani ya jeneza kama
mfu.Hakuwa na fahamu.Kuanzia
puani hadi shingoni alifungwa
bandeji ambao kwa mujibu wa
maelezo ya Meshack aliyoyatoa
kwa ndugu ni kwamba iliwekwa
maalum kwa ajili ya kuziba
sehemu ambayo iliharibiwa vibaya kwa risasi.Juu ya jeneza kulikuwa
na kioo ambacho kilizuia watu
wasiweze kumgusa Elvis akiwa
ndani ya jeneza.
Wa kwanza kuaga mwili
alikuwa ni bi Tarimo mama mzazi
wa Elvis.Aliangua kilio kikubwa
sana alipomuona mwanae wa
pekee akiwa amelala ndani ya
jeneza.Wa pili kuaga alikuwa ni
Patricia mke wa Elvis.Hakuwa na
nguvu hivyo alitegemezwa na
akina mama wanne akiwamo
Doreen rafiki yake mkubwa.Mara
tu alipolifikia jeneza lenye mwili
wa mumewe akapoteza fahamu
hivyo ikabidi kumtoa nje kwa ajili
ya huduma
Zoezi liliendelea kwa viongozi
wa serikali waliokuwepo pale
ndugu na wafanyakzi wenzake
wachache kutoa heshima zao za mwisho kisha jeneza likafungwa
na kutolewa nje kwa ajili ya
ibada.Hakukuwa na utulivu tena
eneo lile la msiba kwani vilio
vilisikika kila kona.Ilibidi
zifanyike jitihada kubwa
kuwanyamazisha watu na ndipo
ibada ikaanza.Kutokana na
kuchelewa sana kwa ratiba ibada
haikuwa ndefu.baada ya ibada
kumalizika zikafuata salamu za
rambi rambi toka kwa watu na
makundi mbali mbali zikatolewa
haraka haraka na saa kumi na
moja na dakika ishirini safari ya
kuelekea makaburini
ikaanza.Wengi walilaumu sana
kwa mambo kuchelewa namna ile
lakini kwa Meshack Jumbo na
vijana wake haya yalikuwa ni
mafanikio kwao kwani mambo
yalikwenda kama walivyotarajia. Saa kumi na mbili na dakika
saba msafara wa magari ukawasili
katika makaburi ya Mbuyuni
ambayo ni makaburi mapya.Jeneza
likashushwa na kuweka pembeni
ya kaburi maalum lililojengwa kwa
ustadi wa aina yake.Kila aliyeliona
alimsifu mjenzi wa kaburi lile.kwa
mara nyingine tena jeneza
likafunguliwa ili kumpa nafasi ya
mwishoi mjane wa marehemu
kuweza kuuaga mwili wa mumewe
kwani hakuweza kufanya hivyo
nyumbani baada ya kupoteza
fahamu.Patricia akasaidiwa
akasogelea jeneza na safari hii pia
alishindwa kumuaga Elvis kwani
alipoteza fahamu tena.Hakukuwa
na ratiba ndefu hapo makaburini
kwani tayari jua lilikwisha anza
kupoteza nuru na kukipisha kiza
hivyo jeneza likashushwakaburini.Ukawekwa mfuniko wa
muda na watu mbalimbali
wakaweka shada za maua na zoezi
hilo lilipokamilika watu wote
wakaombwa kurejea nyumbani
kwa ajili ya kuendelea na
maombolezo hadi kesho yake
tanga litakapoanuliwa.Taratibu
umati wa watu ukaondoka pale
makaburini na kuwaacha mafundi
wa kutoka kampuni ya ujenzi
anayomiliki Ben wakianza
maandalzi ya kazi ya kulifunika
kaburi.watu wote walipoondoka
Steven ambaye wakati shughuli
hizi zote zinafanyika alikuwa
garini akafika pale kaburini na
kuwaita pembeni Ben,Dr Rajesh na
Dr Philip
“Mpaka hapa mambo yote
yamekwenda vizuri
sana.Hongereni kwa kulisimamia vyema zoezi zima,sasa
tumebakiwa na kazi moja tu
kubwa.Kumtoa Elvis ndani ya
jeneza na kumzindua.Ben itabidi
uwaondoe hawa mafundi wako
kwa muda ili tuweze kuifanya kazi
hiyo kwa haraka” akasema Steven
na bila kupoteza muda Ben
akawaita mafundi wake
akawaeleza kwamba kuna mambo
ya kimila yanakwenda kufanyika
pale katika kaburi la Elvis kwa
muda wa saa moja akawataka
waondoke eneo lile wakapate
kinywaji na chakula kisha
atawapigia simu warejee mambo
yatakapokuwa
yamekamilika.Akawapatia fedha
ya chakula kiasi cha shilingi
milioni moja na laki tatu
wakafurahi sana na kuondoka. Sasa ni wakati wetu”
akasema Dr Philip baada ya wale
mafundi kuondoka.Haraka haraka
Dr Rajesh,Dr Philip na Steven
wakaingia kaburini na kulifungua
jeneza.Taratibu za kumzindua
Elvis zikaanza.kwanza alitolea
ndani ya jeneza likafungwa
vizuri.Tayari kulikuwa na kiza
mahala pale.Wakambeba Elvis na
kumpeleka katika gari la
wagonjwa lililokuwapo pale
makaburini.Mashine alizokuwa
amefungwa kwa ajili ya kumsaidia
kupata hewa safi zikatolewa na
kuunganishwa katika mashine
nyingine iliyokuwamo mle garini
ya kumsaidia kuvuta
hewa,ikaunganishwa pia mashina
ya kupima mwenendo wa mapigo
yake ya moyo.Kila kitu
kilikuonekana kwenda vizuri. Ben akawapigia simu mafundi
wake warejee kwa ajili ya
kumalizia ujenzi wa kaburi.Steven
na akina Dr Philip wakaondoka
zao.
“Ee Mungu tusaidie Elvis
aweze kuamka” akaomba Dr Philip
huku akimtazama Elvis.
Walifika hadi nyumbani kwao
na Elvis akashushwa garini na
kuingizwa ndani.Graca aliyefungua
geti alipatwa na furaha ya ajabu
alipomuona Elvis akishushwa
garini
“Anaendeleaje? Akamuuliza
Steven
“Bado hana fahamu.Tuko
katika jitihada za kumzindua”
akasema Steven .
Wakiwa wanaendelea
kumsubiri Elvis azinduke Meshack
Jumbo akapiga simu Dr Philip nipe ripoti mambo
yanakwendaje huko? Akauliza
Meshack baada ya Dr Philip
kupokea simu
“Mambo yamekwenda
vizuri.Kila kitu kimekwenda kama
tulivyopanga.Ahsante sana kwa
kusimama vyema hapo nyumbani
na kila kitu kikaenda vyema kama
tulivyotarajia.Hivi sasa tayari
tumekwisha ondoka makaburini
tuko hapa nyumbani tukimsubiri
Elvis azinduke.Mafundi
wanaendelea na kazi ya kufunika
kaburi”
“Good job.Mmefanya kazi
nzuri sana.Mimi bado niko hapa
msibani na utanijulisha mambo
yanavyokwenda hapo” akasema
Meshack na kukata
simu.Alipomaliza kuzungumza na Dr Philip akampigia simu makamu
wa rais Dr Shafi
“Habari za jioni mheshimiwa
makamu wa rais” akasema
Meshack baada ya Dr Shafi
kupokea simu
“Habari nzuri Meshack
Jumbo.Mambo yamekwendaje leo?
“Mambo yamekwenda
vyema.Tayari tumempumzisha
yule kijana wetu.Hivi sasa bado
niko hapa msibani kuendelea
kuwafariji wafiwa nimeona
niwasiliane nawe kama
ulivyonitaka.”
“Mesahck Jumbo kwanza
kabisa napenda kukushukuru sana
kwa kazi kubwa
uliyoifanya.Ninakuahidi kwamba
sintakusahau kwa jambo hili
kubwa na siku moja utaiona faida ya hili ulilolifanya” akasema Dr
Shafi
“Nashukuru sana” akasema
Meshack Jumbo
“Nilihitaji kuonana nawe
usiku huu ana kwa ana lakini
sintaweza kwa kuwa kuna sehemu
nahitajika kufika usiku huu hivyo
nitakupa maagizo muhimu katika
simu na ninaomba uyafanyie kazi
kwa haraka.”
“Sawa mkuu nitalitekeleza
agizo lolote utakaponipa kwa
haraka”
“Good.Kuna kijana mmoja
anaitwa Pascal Situmwa nahitaji
naye aondolewe haraka sana.Huyu
kijana anafanya kazi idara ya
usalama wa taifa.Nataka hadi
kufika kesho jioni niwe nimepata
taarifa kwamba tayari amekwisha
uawa.Unaweza ukaniahidi kwamba utalifanyia kazi jambo
hilo kwa haraka?
“Sawa mheshimiwa makamu
wa rais nitalifanyia kazi jambo hilo
kwa haraka kama ulivyoagiza”
akasema Meshack Jumbo.
“Good.Kesho kijana atakuletea
mzigo wako nyumbani” akasema
Makamu wa rais na kukata simu
Meshack Jumbo akatoa
kitambaa na kufuta jasho.
“Mauaji mengine!! Akawaza
Meshack Jumbo na kwenda kuketi
akionekana kuwa na mawazo
mengi.
“Pascal Situmwa.! Akawaza
“Jina hili si geni kwangu.Kuna
mahala nimewahi kulisikia
likitamkwa.Huyu naye amefanya
nini? Kama ni mfanyakazi wa idara
ya usalama wa taifa yawezekana
kabisa kuna jambo ameligundua kuhusiana na mtandao aliomo
makamu wa rais na ndiyo maana
wanataka kumuua haraka.Je
nifuate maelekezo ya makamu wa
rais na kumuua? Akajiuliza
“Kabla ya yote nahitaji
kumfahamu zaidi huyu Pascal
Situmwa ni nani na ndipo nifanye
maamuzi.Kwa kuwa shughuli hapa
zimemalizika ngoja niage
niondoke zangu nikaanze
kulifuatilia jambo hili” akawaza
Meshack akainuka na kuwaaga
ndugu na jamaa waliokuwepo pale
msibani usiku ule kisha
akaondoka .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom