Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 41

C’mon Elvis wake up !!
akasema Dr Philip kwa wasi wasi
wakiwa chumbani kwa Elvis
wakimsubiri azinduke baada ya
muda walioutarajia kupita.Wote
walikuwa kimya wakitazama saa
zao.Mashine ya kuonyesha mapigo
ya moyo ilionyesha mwenendo
mzuri na hata mifumo mingine
ilionyesha kwenda vizuri.Kengele
ya getini ikalia na Steven akaenda
kufungua geti akakutana na
Mesahck Jumbo akamkaribisha
ndani
“Mambo yanakwenaje hapa?
Akaulia Meshack Jumbo baada ya
kukuta hali ya ukimya mle ndani.
“Mambo hapa yanakwenda
vyema lakini mpaka sasa bado
Elvis hajazinduka licha ya muda uliokuwa unatakiwa kupita.Hata
hivyo mifumo yote ya miwli
inaonyesha kwenda vyema”
akasema Dr Philip
“Msiwe na wasiwasi
atazinduka.Elvis ni jasiri na
atazinduka.Naomba niwatoe
wasiwasi.Nina furaha sana kwa
operesheni hii
kukamilika.Halikuwa jambo rahisi
kwetu lakini tumeweza
kulifanikisha na kwa sasa Elvis ni
marehemu.Hii ni jambo kubwa
sana kwetu.Napenda nichukue
nafasi hii kuwashukuru sana kwa
kazi kubwa mliyoifanya” akasema
Meshack Jumbo na mara mlango
ukagongwa Steven akaufungua na
kukutana na Graca ambaye macho
yake yalikuwa yamevimba.
“Graca karibu.Kuna tatizo
lolote? Akauliza Steven Bado Elvis hajazinduka?
Akauliza Graca
“bado hajazinduka ila
anaendelea vyema na muda
wowote atazinduka”
Akasema Steven
“Who is that? Akauliza
Meshack Jumbo
“Huyu ni Graca”
“Let her in” akasema Meshack
na Graca akaruhusiwa kuingia
ndani,akashindwa kuyazuia
machozi kumtoka alipomuona
Elvis pale kitandani.
“Pole sana Graca” akasema
Meshack Jumbo
“Ahsante sana mzee”akajibu
Graca huku akifuta machozi
“Graca mimi naitwa Meshack
Jumbo ndiye mkuu wa kazi wa
Elvis.Mimi na wewe hatujapata
nafasi ya kuzungumza ana kwa ana lakini tayari Elvis amekwisha
nieleza kila kitu kuhusu wewe na
ninapenda kuchukua nafasi hii
kukupa pole sana kwa yale yote
uliyoyapitia.Wewe ni binti jasiri
mno na unastahili
kupongezwa.Wewe ni chimbuko la
operesheni hii.Bila wewe
tusingeweza kufahamu kuhusu
mambo yanayofanywa na baba
yako na genge lake hivyo kwa
niaba ya serikali napenda
nikuahidi kwamba tutafanya kila
linalowezekana kukusaidia
kuanza maisha mapya yenye
furaha ana amani na hautalia tena”
“Ahsante sana mzee” akajibu
Graca
“Operesheni ya leo
imekwenda vizuri na kila kitu
kimekwenda kama
tulivyotarajia.Nakutoa wasi wasi kwamba Elvis atazinduka muda
wowote hivyo usihofu” akasema
Meshack na kuwataka akina
Steven watoke mle chumbani na
kumuacha Graca peke yake na
Elvis
“Graca tunakuacha na
Elvis.Unaweza ukamueleza jambo
lolote lile kwani
anakusikia.Itapendeza endapo
akizinduka na kukukuta ukiwa
pembeni ya kitanda chake”
akasema Meshack Jumbo na kisha
wakatoka wote na kumuacha
Graca peke yake akiwa na Elvis
“Huyu binti anapaswa
kulindwa sana kwani ndiye
chimbuko la haya yote
yaliyotokea.Mipango inaendelea ili
kumhamishia Marekani akaishi
kule kwani hapa Tanzania baba
yake anamsaka amuue.Ni binti anayepaswa kupewa msaada
mkubwa,maisha yake
yameharibiwa na baba yake hivyo
tunapaswa sisi kuyajenga
upya.Ananifurahisha ni binti jasiri
mno”akasema Meshack
“Ni mrembo pia” akaongeza
Steven
“Steven tabia zako chafu
ziweke mbali kabisa na binti huyu
! akasema Meshack Jumbo
“Samahani mzee niliongeza
utani kidogo” akasema Steven na
kutabasamu
“Tuachane na hayo napenda
kwa mara nyingine tena
niwashukuru kwa kazi kubwa
mliyoifanya siku ya leo.Ni vigumu
kuamini kwamba tumefanikiwa
kuifanya operesheni kubwa na
hatari kama hii.Tumeuaminisha
umma kwamba Elvis amekufa.Huu ni mzigo mkubwa tumeubeba
lakini ni kwa manufaa mapana ya
taifa.Jukumu letu kubwa kwa sasa
ni kufahamu kwamba katika hali
ya kawaida Elvis tayari amekufa
hivyo tunapaswa kuhakikisha
inakuwa hivyo hadi hapo
atakapokamilisha operesheni
hii.Kitakachofuata baada ya zoezi
hili kukamilika ni operesheni nzito
ya kusafisha genge lote
linaloongozwa na brigedia Frank
na wenzake ambao ndiyo chanzo
cha maisha ya Elvis kubadilika
namna hii.Hakuna jiwe
litakalosalia juu ya jiwe hii ni kauli
ya Elvis”akasema Meshack Jumbo
“Nakuhakikishia mzee
kwamba nitafanya kazi bega kwa
bega na Elvis na tutahakikisha
tunaufyeka mtandao wote wa
hawa jamaa.Hakuna mwenye mkono wake katika mtandao huu
atabaki salama” akasema Steven
“Ninaufahamu uwezo wako
Steven na ukiungana na Elvis kwa
pamoja mnaweza mkafanya jambo
kubwa sana”
“kama unaufahamu uwezo
wangu mzee kwa nini ukakubali
nikakaa kizuizini kwa muda huu
wote? Hukujua kama naweza kuwa
na msaada siku moja? Akauliza
Steven
“Steven tuachane na hayo
mambo.Kitu kikubwa na cha
msingi ni kwamba kwa sasa
umekwisha toka kizuizini na yale
yote ya nyuma yamepita.Usirudie
tena yale mambo yaliyokufanya
ukaingia kizuizini.Huu ni wakati
wa kuyajenga maisha yako.Miaka
inakwenda na unapaswa kuwa na
familia.Ishi kama mwenzako Elvis ambaye amekuwa ni mfano wa
kuigwa kutokana na maisha
anayoishi yeye na mke wake
Patricia hadi lilipotokea suala hili
na kuyaharibu maisha yao.Sina
hakika kama ile furaha yao ya
ndoa itajirudia tena baada ya
jambo hili”
“Nini itakuwa hatima ya Elvis
baada ya operesheni kumalizika?
Atajitokeza na kudai kwamba
hakuwa amekufa? Unadhani jamii
itamuelewa? Steven akauliza
“Hilo ni jambo linaoumiza
mno kichwa changu lakini naamini
huu utakuwa ni mwisho wa Elvis
kuonekana kwani nashauri baada
ya operesheni kumalizika aondoke
hapa chini na kwenda kuishi mbali
nje ya nchi kwa maisha yake
yaliyobaki” Unadhani Elvis atakubali
kumuacha mkewe Patricia? Dr
Philip akauliza
“Ni vigumu mno hasa kwa
namna Elvis anavyompenda mke
wake laini hakuna namna lazima
aachane naye kwani endapo
ikigundulika kwamba kifo kile
hakikuwa cha kwali sote tutaingia
matatizoni.Ili kuepusha hayo
lazima Elvis aondoke hapa nchini
na kwenda kumalizia maisha yake
nje ya nchi.Nitahakikisha anapata
kila kitu kwa ajili ya maisha yake
mapya.Hata hivyo ninamuonea
huruma sana mke wake.Msibani
amezimia zaidi ya mara tatu na
hakuweza hata kumuaga
mumewe.Ni jambo kubwa hili
tumelifanya.Tumesababisha
vidonda visivyopona kwa watu
wengi na hasa Patricia mwanamkeambaye Elvis kwa mdomo wake
amewahi kunitamkia kwamba
anampenda kuliko wote
duniani.Tuachane na hayo
tutapata wasaa mzuri na wa
kutosha kuyajadili pale
tutakapokuwa na Elvis.Tuendelee
kumuombea aweze kuzinduka”
akasema Meshack Jumbo
“Makamu wa rais ndiye
aliyenitaka nihakikishe Elvis
anauawa” Meshack akaendelea
“Nikiwa msibani leo alinipigia
simu na kunitaka nitakapomaliza
shughuli za mazishi nimpigie simu
kuna jambo la muhimu sana
anataka kuniambia na ndiyo
maana nikahisi yawezekana labda
amegundua kuhusu mpango wetu
au amesikia kuhusu Stevenn
kutolewa kizuizini ndiyo maana
nikamtaka Steven asionekane msibani.Nimempigia simu usiku
huu na akanieleza kile alichokuwa
ananiitia” akanyamaza kidogo na
kuendelea
“Kuna mtu mmoja anaitwa
Pascal situmwa mfanyakazi wa
idara ya usalama wa taifa
anatakiwa auawe mara moja”
“Pascal situmwa? Akauliza
Steven
“Ndiyo.Unamfahamu? akauliza
Meshack Jumbo
“Hili jina si geni kwangu
nimewahi kulisikia mahala
likitamkwa ila sina kumbukumbu
ni wapi.Kafanya nini huyu
jamaa?akauliza Steven
“Hajaniambia kafanya nini
huyu jamaa na wala sikutakiwa
kuhoji.Ninachotakiwa ni
kutekeleza maagizo ya
kumuondoa.Anataka hadi ikifika siku ya kesh…………..” Meshack
akanyamaza baada ya kusikia
vishindo vya mtu.Kwa kasi ya aina
yake Steven akatoa bastora na
mara akatokea Graca pale sebuleni
akihema na kabla hajasema
chochote watu wote pale sebuleni
wakatoka mbio kuelekea katika
chumba alimo Elvis na kumkuta
amezinduka
“Patricia.!! ..Patricia !! Hilo
ndilo neno alilokuwa analitamka
Elvis kwa sauti dhaifu.Haraka
haraka Dr Philip akampima ili
kuhakikisha kila kitu kinakwenda
vyema.Akamtundikia chupa ya
maji iliyochomwa dawa ya kumpa
nguvu kisha akamuagiza Graca
atengeneze uji haraka ili wampe
Elvis kwani hakuwa amekula kitu
kuanzia asubuhiElvis !! akaita Dr Philip.Elvis
akageuza macho akamtazama.
“Elvis unaweza kunitambua
mimi ni nani? Akauliza Dr
Philip.Elvis akafumba macho
halafu akayafumbua akatazama
tena.
“Elvis unaweza ukanitambua
mimi ni nani? Akauliza Dr
Philip.Elvis hakumjibu kitu
akaendelea kumtazama.
“Patricia !! akasema Elvis kwa
sauti dhaifu
“Bado hajazinduka
vizuri.Tumuache kwa muda
fahamu zimrejee vizuri” akasema
Dr Philip
******************
Wengi wa watu walikuwepo
nyumbani kwa bi Tarimo usiku
huu ni ndugu na majirani
wakiendelea kuwafariji
wafiwa.Watu walikaa vikundi
vikundi wakizungumza na wengine
wakicheza bao na karata.Baadhi ya
akina mama walikuwa ndani na
wengine wakiendelea na shughuli
mbalimbali za kupika na usafi wa
vyombo.Kutokana na hali yake
kuwa dhaifu Patricia alikuwa
amelala katika chumba maalum na
pembeni yake akiwepo rafiki yake
kipenzi Doreen.
“Patricia tafadhali nakuomba
ujaribu kula chakula hiki
nimekuandalia mimi
mwenyewe.Nimekuletea supu ya
kuku.Inuka ule upate nguvu.Mwili wako umekuwa dhaifu sana”
Doreen akambembeleza Patricia
ale chakula.Akamshika mkono na
kumsaidia kukaa kisha akaanza
kumnywesha ile supu ya
kuku.Doreen alijitahidi na
kuhakikisha Patrcia amemaliza
bakuli zima la supu
“Doreen nimemkosea nini
Mungu hadi akaniadhibu kiasi
hiki? Patricia akamuuliza Doreen
“Patricia usiwaze hayo mambo
tafadhali.Jitahidi upate
mapumziko ya kutosha.Hii ni
mitihani ya maisha ambayo lazima
tuipitie” akasema Doreen na
Patricia akaonekana kuzama
mawazoni
“Nilifanya jambo baya wakati
nikiwa nasoma shule.Niliwahi
kutoa mimba na kwa tendo lile la
uuaji ninaamini Mungu ananiadhibu mpaka leo.Kwa tendo
lile la kuua kiumbe asiye na hatia
nimepoteza uwezo wangu wa
kuzaa,sina kizazi tena na Mungu
anaendelea kuniadhibu na sasa
amenichukulia hadi ile nguzo
yangu kuu niliyokuwa
nimeegemea.Elvis alikuwa ni kila
kitu kwangu.Yeye ndiye aliyekuwa
nguzo yangu,mfariji wangu,rafiki
yangu na furaha yangu.Dunia
nzima wangeweza kuniacha lakini
si Elvis.Alinipenda kuliko kitu
chochote.Nitafanya nini bila yeye?
Nitaishi vipi bila yeye? Doreen
sikufichi rafiki yangu sioni tena
sababu ya kuendelea kuishi kwani
maisha yangu hayatakuwa na hata
chembe ya furaha.Sina thamani
tena katika hii dunia kwani mtu
peke aliyekuwa ananithamini ni
Elvis na kwa kuwa ameondokasiioni tena thamani yangu”
akasema Patricia kwa uchungu na
kumfanya Doreen adondoshe
machozi
“Patricia tafadhali usiseme
hivyo.Mungu hakuadhibu
anatupenda sote na ndiyo maana
pamoja na makosa mengi
tunayomkosea bado anatupa
zawadi hii ya uhai.Kufa ni jambo la
kawaida ambalo sote
tutalipitia.Inauma kwa sababu
Elvis ametutangulia.Ninafahamu
uchungu ulionao sasa hivi lakini
nakuomba usijione uko peke
yako.Bado watu wengi tuko nyuma
yako nakuhakikisha kwamba
unakivuka salama kipindi hiki
kigumu.Nakuahidi katu
hatutaweza kukuacha.Tutasimama
nawe katika kila gumu
utakalopitia”akasema Doreen “Ninakushukuru sana Doreen
kwa kusimama nami katika
kipindi hiki kigumu mno katika
maisha yangu.Ninao watu wengi
wanaonifahamu lakini
ninashukuru kwa kuwa na watu
wachache ambao ninawaamini
ambao katika kila tatizo
linalonikumba hufumba macho na
kusimama nami katika
maombi.Sina cha kuwalipa watu
hao ila ni Mungu pekee
atakayewalipa.Tatizo linakuja kwa
ndugu wa Elvis ambao toka angali
mtoto wao yuko hai walikuwa
wananiona takataka nini kitatokea
wakati mtoto wao amefariki?
Wewe mwenyewe umeona namna
nilivyobaguliwa hapa msibani hadi
kufikia hatua ya kutengwa katika
chumba changu peke
yangu.Namshukuru sana yule mzee Meshack ambaye ndiye
aliyehakikisha na mimi ninapewa
kipaumbele vinginevyo
nisingeweza hata kupewa fursa ya
kumuaga Elvis” akanyamaza na
kumtaka Doreen ambaye alikuwa
anatoa machazi asiendelee kulia
“Doreen nyamaza kulia tayari
tumekwishalia vya kutosha na hata
kama tutalia hadi sauti zikauke
hatutaweza kumrejesha tena
Elvis.He’s gone and will never
come back.Kinachofuata sasa ni
kujipanga kukabiliana na maisha
bila yeye.Nimepata donda
lisiloweza kupona hadi siku
nitaingia kaburini hivyo sitaki tena
kuendelea na maisha ambayo
yataniongezea maumivu katika
kidonda changu hivyo nimefanya
maamuzi.Naamini kesho kikao cha
familia kitakaa ili kuhitimisha shughuli za msiba na katika kikao
hicho mali zote ambazo nilichuma
na marehemu nitaziwasilisha kwa
mama yake.Sitaki maisha ya
kuendelea kusemwa na kuumizwa
moyo wangu kwani watu hawa bila
kujali majonzi niliyonayo
walinilifuta na kunitaka
kuorodhesha mali
zilizopo.Nimeumizwa mno na
jambo hili kwani mali zile
haziwahusu chochote”
“Patricia !! akasema Doreen
lakini Patricia akamzuia
“Doreen tayari nimeamua
hivyo.Nafahamu mali hizo ni haki
yangu lakini sitaki maneno.Mali
zinatafutwa na nina uhakika
nitaweza kupata mali
nyingine.Nataka niishi kwa amani
nikiendelea kumlilia mume wangu.Sitaki kujiongezea
matatizo” akasema Patricia
“Kwa upande mwingine
Patricia ninaweza kukuunga
mkono katika maamuzi haya.Kama
bila kujali majonzi uliyo nayo
wamethubutu kukuhoji kuhusu
mali za marehemu watu hawa ni
wanyama kabisa.Waachie mali zao
na sisi tutakusaidia kuweza kupata
mali nyingine”
“Ahsante Doreen kwa
kuniunga mkono.Kikubwa
ninachoshukuru ni kwamba bado
ni mzima ninao uwezo wa kufanya
kazi kwa bidii na kupata mali
nyingine.Nakushauri rafiki yangu
usikubali kuolewa kama
unafahamu kwamba hauna uwezo
wa kuzaa kwani manyanyaso
utakayoyapata toka kwa ndugu wa
mume ni makubwa sana.Ni mengi nimeyapitia ambayo mengine
sikutaka kumueleza hata Elvis kwa
kuogopa kumkosanisha na ndugu
zake.Si mara moja nimekuwa
ninapigiwa simu na ndugu zake
Elvis wakinitukana sana
wakinitaka niachane na ndugu
yao.Ni mateso makubwa sana
nimeyapitia na kuna nyakati
nilijuta kwa nini niliolewa”
akasema Patricia
“Pole sana Patricia kwa
mateso yote uliyopitia.Mungu
anaona kila kitu na atakusaidia
kuweza kuipata furaha ya maisha
yako.You’ll be happy again.Usikate
tamaa” akasema Doreen
“Haya ni malipo ya uovu
nilioufanya.Mungu ananiadhibu.I’ll
never be happy.My happiness is
gone.Elvis ndiye aliyekuwa furaha
yangu na baada ya kuondoka kwake sintakuwa na furaha
tena.Hakuna mwanadamu
atakayetokea na kunipa furaha
kama aliyonipa Elvis”
“Patricia usiwaze sana kuhusu
mambo haya kwa sasa.Huwezi
kujua Mungu ana mipango gani
nawe.Kila jambo hutokea kwa
sababu maalum.Tunaelekezwa na
maandiko kwamba tushukuru kwa
kila jambo”akasema
Doreen.Patricia akainama akafikiri
kwa muda na kusema
“Doreen do you believe there
is God? Akauliza Patricia na
kumstua Doreen
“Patricia tafadhali nakuomba
usiwaze sana hadi ukafikia hatua
ya kukufuru.Haya yote ni mapenzi
ya Mungu.Yeye ndiye mwenye
kutoa na hutwaa kwa muda
anaotaka yeye hata kama bado tunawahitaji wapendwa
wetu.Tunaelekezwa kumshukuru
kwa kila jambo hata kama ni
jambo la kutuumiza hata pale
anapowachukua wale tuwapendao
na kuwategemea” akasema Doreen
na Patricia akafuta machozi
“I don’t think there is God”
akasema
“Patricia tafadhali usiseme
hivyo.Mungu yupo.Tafadhali lala
na usiache kichwa chako kikajawa
mawazo mengi na
kumkufuru”akasema Doreen
“Where is he? Kama kweli
yupo haoni kama Elvis ndiye
furaha yangu ya pekee hapa
duniani na akamchukua? Why he
wants me to suffer? Akauliza
Patricia.Doreen hakujibu kitu
akafungua mkoba wake na kutoa
pakiti ya dawa akachukua dawa nne na kumpa Patricia
ameze.Miongoni mwa dawa zile
zilikuwemo pia dawa za
usingizi.Haukupita muda akalala
“Patricia ana uchungu
uliopitiliza hadi akaanza
kuzungumza maneno kama yale
akihoji uwepo wa Mungu.Inaumiza
sana.Kuna nyakati hata mimi
ninajikuta nikishindwa kuvumilia
na kutamani kumueleza ukweli
kwamba Elvis hajafa lakini
ninashindwa.Kwa nini lakini Elvis
akaamua kumtesa Patricia kiasi
hiki? Laiti angeweza kupata picha
ya namna mke wake alivyoumizwa
na kifo hiki sijui angefanya
nini.Hata hivyo kwa upande wa pili
hata yeye hakupenda kufanya hivi
bali amelazimika kufanya hivi kwa
ajili ya kusaidia watu wanaoteseka
na kuuawa bila hatia.Elvis anampenda sana Patricia na laiti
kama angekuwa na namna
nyingine ya kufanya basi angeweza
kufanya lakini hakuwa na njia
nyingine ya kufanya zaidi ya
kughushi kifo chake” akawaza
Doreen na kumtazama Patricia
aliyekuwa amelala kitandani
“Namuonea huruma sana
Patricia.Swali ninalojiuliza ni je
nini kitafuata baada ya Elvis
kumaliza operesheni yake?Je
atajitokeza na kudai kwamba
hakuwa amekufa? Jamii
itamuelewa kwamba kweli hakuwa
amekufa? Kama asipojitokeza je
utakuwa ndiyo mwisho wake na
Patricia?Kama ikiwa hivyo hiyo
itakuwa ni fursa yangu ya kuwa na
Elvis atakuwa wangu
daima.Naomba iwe hivyo na hilo
ndilo dua langu usiku na mchana.Nitafanya mpango tuhame
hapa nchini na kwenda nje ya nchi
kuanza maisha mapya na
hatutarejea tena Tanzania”
akawaza Doreen na kujilaza
pembeni ya Patricia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 41

C’mon Elvis wake up !!
akasema Dr Philip kwa wasi wasi
wakiwa chumbani kwa Elvis
wakimsubiri azinduke baada ya
muda walioutarajia kupita.Wote
walikuwa kimya wakitazama saa
zao.Mashine ya kuonyesha mapigo
ya moyo ilionyesha mwenendo
mzuri na hata mifumo mingine
ilionyesha kwenda vizuri.Kengele
ya getini ikalia na Steven akaenda
kufungua geti akakutana na
Mesahck Jumbo akamkaribisha
ndani
“Mambo yanakwenaje hapa?
Akaulia Meshack Jumbo baada ya
kukuta hali ya ukimya mle ndani.
“Mambo hapa yanakwenda
vyema lakini mpaka sasa bado
Elvis hajazinduka licha ya muda uliokuwa unatakiwa kupita.Hata
hivyo mifumo yote ya miwli
inaonyesha kwenda vyema”
akasema Dr Philip
“Msiwe na wasiwasi
atazinduka.Elvis ni jasiri na
atazinduka.Naomba niwatoe
wasiwasi.Nina furaha sana kwa
operesheni hii
kukamilika.Halikuwa jambo rahisi
kwetu lakini tumeweza
kulifanikisha na kwa sasa Elvis ni
marehemu.Hii ni jambo kubwa
sana kwetu.Napenda nichukue
nafasi hii kuwashukuru sana kwa
kazi kubwa mliyoifanya” akasema
Meshack Jumbo na mara mlango
ukagongwa Steven akaufungua na
kukutana na Graca ambaye macho
yake yalikuwa yamevimba.
“Graca karibu.Kuna tatizo
lolote? Akauliza Steven Bado Elvis hajazinduka?
Akauliza Graca
“bado hajazinduka ila
anaendelea vyema na muda
wowote atazinduka”
Akasema Steven
“Who is that? Akauliza
Meshack Jumbo
“Huyu ni Graca”
“Let her in” akasema Meshack
na Graca akaruhusiwa kuingia
ndani,akashindwa kuyazuia
machozi kumtoka alipomuona
Elvis pale kitandani.
“Pole sana Graca” akasema
Meshack Jumbo
“Ahsante sana mzee”akajibu
Graca huku akifuta machozi
“Graca mimi naitwa Meshack
Jumbo ndiye mkuu wa kazi wa
Elvis.Mimi na wewe hatujapata
nafasi ya kuzungumza ana kwa ana lakini tayari Elvis amekwisha
nieleza kila kitu kuhusu wewe na
ninapenda kuchukua nafasi hii
kukupa pole sana kwa yale yote
uliyoyapitia.Wewe ni binti jasiri
mno na unastahili
kupongezwa.Wewe ni chimbuko la
operesheni hii.Bila wewe
tusingeweza kufahamu kuhusu
mambo yanayofanywa na baba
yako na genge lake hivyo kwa
niaba ya serikali napenda
nikuahidi kwamba tutafanya kila
linalowezekana kukusaidia
kuanza maisha mapya yenye
furaha ana amani na hautalia tena”
“Ahsante sana mzee” akajibu
Graca
“Operesheni ya leo
imekwenda vizuri na kila kitu
kimekwenda kama
tulivyotarajia.Nakutoa wasi wasi kwamba Elvis atazinduka muda
wowote hivyo usihofu” akasema
Meshack na kuwataka akina
Steven watoke mle chumbani na
kumuacha Graca peke yake na
Elvis
“Graca tunakuacha na
Elvis.Unaweza ukamueleza jambo
lolote lile kwani
anakusikia.Itapendeza endapo
akizinduka na kukukuta ukiwa
pembeni ya kitanda chake”
akasema Meshack Jumbo na kisha
wakatoka wote na kumuacha
Graca peke yake akiwa na Elvis
“Huyu binti anapaswa
kulindwa sana kwani ndiye
chimbuko la haya yote
yaliyotokea.Mipango inaendelea ili
kumhamishia Marekani akaishi
kule kwani hapa Tanzania baba
yake anamsaka amuue.Ni binti anayepaswa kupewa msaada
mkubwa,maisha yake
yameharibiwa na baba yake hivyo
tunapaswa sisi kuyajenga
upya.Ananifurahisha ni binti jasiri
mno”akasema Meshack
“Ni mrembo pia” akaongeza
Steven
“Steven tabia zako chafu
ziweke mbali kabisa na binti huyu
! akasema Meshack Jumbo
“Samahani mzee niliongeza
utani kidogo” akasema Steven na
kutabasamu
“Tuachane na hayo napenda
kwa mara nyingine tena
niwashukuru kwa kazi kubwa
mliyoifanya siku ya leo.Ni vigumu
kuamini kwamba tumefanikiwa
kuifanya operesheni kubwa na
hatari kama hii.Tumeuaminisha
umma kwamba Elvis amekufa.Huu ni mzigo mkubwa tumeubeba
lakini ni kwa manufaa mapana ya
taifa.Jukumu letu kubwa kwa sasa
ni kufahamu kwamba katika hali
ya kawaida Elvis tayari amekufa
hivyo tunapaswa kuhakikisha
inakuwa hivyo hadi hapo
atakapokamilisha operesheni
hii.Kitakachofuata baada ya zoezi
hili kukamilika ni operesheni nzito
ya kusafisha genge lote
linaloongozwa na brigedia Frank
na wenzake ambao ndiyo chanzo
cha maisha ya Elvis kubadilika
namna hii.Hakuna jiwe
litakalosalia juu ya jiwe hii ni kauli
ya Elvis”akasema Meshack Jumbo
“Nakuhakikishia mzee
kwamba nitafanya kazi bega kwa
bega na Elvis na tutahakikisha
tunaufyeka mtandao wote wa
hawa jamaa.Hakuna mwenye mkono wake katika mtandao huu
atabaki salama” akasema Steven
“Ninaufahamu uwezo wako
Steven na ukiungana na Elvis kwa
pamoja mnaweza mkafanya jambo
kubwa sana”
“kama unaufahamu uwezo
wangu mzee kwa nini ukakubali
nikakaa kizuizini kwa muda huu
wote? Hukujua kama naweza kuwa
na msaada siku moja? Akauliza
Steven
“Steven tuachane na hayo
mambo.Kitu kikubwa na cha
msingi ni kwamba kwa sasa
umekwisha toka kizuizini na yale
yote ya nyuma yamepita.Usirudie
tena yale mambo yaliyokufanya
ukaingia kizuizini.Huu ni wakati
wa kuyajenga maisha yako.Miaka
inakwenda na unapaswa kuwa na
familia.Ishi kama mwenzako Elvis ambaye amekuwa ni mfano wa
kuigwa kutokana na maisha
anayoishi yeye na mke wake
Patricia hadi lilipotokea suala hili
na kuyaharibu maisha yao.Sina
hakika kama ile furaha yao ya
ndoa itajirudia tena baada ya
jambo hili”
“Nini itakuwa hatima ya Elvis
baada ya operesheni kumalizika?
Atajitokeza na kudai kwamba
hakuwa amekufa? Unadhani jamii
itamuelewa? Steven akauliza
“Hilo ni jambo linaoumiza
mno kichwa changu lakini naamini
huu utakuwa ni mwisho wa Elvis
kuonekana kwani nashauri baada
ya operesheni kumalizika aondoke
hapa chini na kwenda kuishi mbali
nje ya nchi kwa maisha yake
yaliyobaki” Unadhani Elvis atakubali
kumuacha mkewe Patricia? Dr
Philip akauliza
“Ni vigumu mno hasa kwa
namna Elvis anavyompenda mke
wake laini hakuna namna lazima
aachane naye kwani endapo
ikigundulika kwamba kifo kile
hakikuwa cha kwali sote tutaingia
matatizoni.Ili kuepusha hayo
lazima Elvis aondoke hapa nchini
na kwenda kumalizia maisha yake
nje ya nchi.Nitahakikisha anapata
kila kitu kwa ajili ya maisha yake
mapya.Hata hivyo ninamuonea
huruma sana mke wake.Msibani
amezimia zaidi ya mara tatu na
hakuweza hata kumuaga
mumewe.Ni jambo kubwa hili
tumelifanya.Tumesababisha
vidonda visivyopona kwa watu
wengi na hasa Patricia mwanamkeambaye Elvis kwa mdomo wake
amewahi kunitamkia kwamba
anampenda kuliko wote
duniani.Tuachane na hayo
tutapata wasaa mzuri na wa
kutosha kuyajadili pale
tutakapokuwa na Elvis.Tuendelee
kumuombea aweze kuzinduka”
akasema Meshack Jumbo
“Makamu wa rais ndiye
aliyenitaka nihakikishe Elvis
anauawa” Meshack akaendelea
“Nikiwa msibani leo alinipigia
simu na kunitaka nitakapomaliza
shughuli za mazishi nimpigie simu
kuna jambo la muhimu sana
anataka kuniambia na ndiyo
maana nikahisi yawezekana labda
amegundua kuhusu mpango wetu
au amesikia kuhusu Stevenn
kutolewa kizuizini ndiyo maana
nikamtaka Steven asionekane msibani.Nimempigia simu usiku
huu na akanieleza kile alichokuwa
ananiitia” akanyamaza kidogo na
kuendelea
“Kuna mtu mmoja anaitwa
Pascal situmwa mfanyakazi wa
idara ya usalama wa taifa
anatakiwa auawe mara moja”
“Pascal situmwa? Akauliza
Steven
“Ndiyo.Unamfahamu? akauliza
Meshack Jumbo
“Hili jina si geni kwangu
nimewahi kulisikia mahala
likitamkwa ila sina kumbukumbu
ni wapi.Kafanya nini huyu
jamaa?akauliza Steven
“Hajaniambia kafanya nini
huyu jamaa na wala sikutakiwa
kuhoji.Ninachotakiwa ni
kutekeleza maagizo ya
kumuondoa.Anataka hadi ikifika siku ya kesh…………..” Meshack
akanyamaza baada ya kusikia
vishindo vya mtu.Kwa kasi ya aina
yake Steven akatoa bastora na
mara akatokea Graca pale sebuleni
akihema na kabla hajasema
chochote watu wote pale sebuleni
wakatoka mbio kuelekea katika
chumba alimo Elvis na kumkuta
amezinduka
“Patricia.!! ..Patricia !! Hilo
ndilo neno alilokuwa analitamka
Elvis kwa sauti dhaifu.Haraka
haraka Dr Philip akampima ili
kuhakikisha kila kitu kinakwenda
vyema.Akamtundikia chupa ya
maji iliyochomwa dawa ya kumpa
nguvu kisha akamuagiza Graca
atengeneze uji haraka ili wampe
Elvis kwani hakuwa amekula kitu
kuanzia asubuhiElvis !! akaita Dr Philip.Elvis
akageuza macho akamtazama.
“Elvis unaweza kunitambua
mimi ni nani? Akauliza Dr
Philip.Elvis akafumba macho
halafu akayafumbua akatazama
tena.
“Elvis unaweza ukanitambua
mimi ni nani? Akauliza Dr
Philip.Elvis hakumjibu kitu
akaendelea kumtazama.
“Patricia !! akasema Elvis kwa
sauti dhaifu
“Bado hajazinduka
vizuri.Tumuache kwa muda
fahamu zimrejee vizuri” akasema
Dr Philip
******************
Wengi wa watu walikuwepo
nyumbani kwa bi Tarimo usiku
huu ni ndugu na majirani
wakiendelea kuwafariji
wafiwa.Watu walikaa vikundi
vikundi wakizungumza na wengine
wakicheza bao na karata.Baadhi ya
akina mama walikuwa ndani na
wengine wakiendelea na shughuli
mbalimbali za kupika na usafi wa
vyombo.Kutokana na hali yake
kuwa dhaifu Patricia alikuwa
amelala katika chumba maalum na
pembeni yake akiwepo rafiki yake
kipenzi Doreen.
“Patricia tafadhali nakuomba
ujaribu kula chakula hiki
nimekuandalia mimi
mwenyewe.Nimekuletea supu ya
kuku.Inuka ule upate nguvu.Mwili wako umekuwa dhaifu sana”
Doreen akambembeleza Patricia
ale chakula.Akamshika mkono na
kumsaidia kukaa kisha akaanza
kumnywesha ile supu ya
kuku.Doreen alijitahidi na
kuhakikisha Patrcia amemaliza
bakuli zima la supu
“Doreen nimemkosea nini
Mungu hadi akaniadhibu kiasi
hiki? Patricia akamuuliza Doreen
“Patricia usiwaze hayo mambo
tafadhali.Jitahidi upate
mapumziko ya kutosha.Hii ni
mitihani ya maisha ambayo lazima
tuipitie” akasema Doreen na
Patricia akaonekana kuzama
mawazoni
“Nilifanya jambo baya wakati
nikiwa nasoma shule.Niliwahi
kutoa mimba na kwa tendo lile la
uuaji ninaamini Mungu ananiadhibu mpaka leo.Kwa tendo
lile la kuua kiumbe asiye na hatia
nimepoteza uwezo wangu wa
kuzaa,sina kizazi tena na Mungu
anaendelea kuniadhibu na sasa
amenichukulia hadi ile nguzo
yangu kuu niliyokuwa
nimeegemea.Elvis alikuwa ni kila
kitu kwangu.Yeye ndiye aliyekuwa
nguzo yangu,mfariji wangu,rafiki
yangu na furaha yangu.Dunia
nzima wangeweza kuniacha lakini
si Elvis.Alinipenda kuliko kitu
chochote.Nitafanya nini bila yeye?
Nitaishi vipi bila yeye? Doreen
sikufichi rafiki yangu sioni tena
sababu ya kuendelea kuishi kwani
maisha yangu hayatakuwa na hata
chembe ya furaha.Sina thamani
tena katika hii dunia kwani mtu
peke aliyekuwa ananithamini ni
Elvis na kwa kuwa ameondokasiioni tena thamani yangu”
akasema Patricia kwa uchungu na
kumfanya Doreen adondoshe
machozi
“Patricia tafadhali usiseme
hivyo.Mungu hakuadhibu
anatupenda sote na ndiyo maana
pamoja na makosa mengi
tunayomkosea bado anatupa
zawadi hii ya uhai.Kufa ni jambo la
kawaida ambalo sote
tutalipitia.Inauma kwa sababu
Elvis ametutangulia.Ninafahamu
uchungu ulionao sasa hivi lakini
nakuomba usijione uko peke
yako.Bado watu wengi tuko nyuma
yako nakuhakikisha kwamba
unakivuka salama kipindi hiki
kigumu.Nakuahidi katu
hatutaweza kukuacha.Tutasimama
nawe katika kila gumu
utakalopitia”akasema Doreen “Ninakushukuru sana Doreen
kwa kusimama nami katika
kipindi hiki kigumu mno katika
maisha yangu.Ninao watu wengi
wanaonifahamu lakini
ninashukuru kwa kuwa na watu
wachache ambao ninawaamini
ambao katika kila tatizo
linalonikumba hufumba macho na
kusimama nami katika
maombi.Sina cha kuwalipa watu
hao ila ni Mungu pekee
atakayewalipa.Tatizo linakuja kwa
ndugu wa Elvis ambao toka angali
mtoto wao yuko hai walikuwa
wananiona takataka nini kitatokea
wakati mtoto wao amefariki?
Wewe mwenyewe umeona namna
nilivyobaguliwa hapa msibani hadi
kufikia hatua ya kutengwa katika
chumba changu peke
yangu.Namshukuru sana yule mzee Meshack ambaye ndiye
aliyehakikisha na mimi ninapewa
kipaumbele vinginevyo
nisingeweza hata kupewa fursa ya
kumuaga Elvis” akanyamaza na
kumtaka Doreen ambaye alikuwa
anatoa machazi asiendelee kulia
“Doreen nyamaza kulia tayari
tumekwishalia vya kutosha na hata
kama tutalia hadi sauti zikauke
hatutaweza kumrejesha tena
Elvis.He’s gone and will never
come back.Kinachofuata sasa ni
kujipanga kukabiliana na maisha
bila yeye.Nimepata donda
lisiloweza kupona hadi siku
nitaingia kaburini hivyo sitaki tena
kuendelea na maisha ambayo
yataniongezea maumivu katika
kidonda changu hivyo nimefanya
maamuzi.Naamini kesho kikao cha
familia kitakaa ili kuhitimisha shughuli za msiba na katika kikao
hicho mali zote ambazo nilichuma
na marehemu nitaziwasilisha kwa
mama yake.Sitaki maisha ya
kuendelea kusemwa na kuumizwa
moyo wangu kwani watu hawa bila
kujali majonzi niliyonayo
walinilifuta na kunitaka
kuorodhesha mali
zilizopo.Nimeumizwa mno na
jambo hili kwani mali zile
haziwahusu chochote”
“Patricia !! akasema Doreen
lakini Patricia akamzuia
“Doreen tayari nimeamua
hivyo.Nafahamu mali hizo ni haki
yangu lakini sitaki maneno.Mali
zinatafutwa na nina uhakika
nitaweza kupata mali
nyingine.Nataka niishi kwa amani
nikiendelea kumlilia mume wangu.Sitaki kujiongezea
matatizo” akasema Patricia
“Kwa upande mwingine
Patricia ninaweza kukuunga
mkono katika maamuzi haya.Kama
bila kujali majonzi uliyo nayo
wamethubutu kukuhoji kuhusu
mali za marehemu watu hawa ni
wanyama kabisa.Waachie mali zao
na sisi tutakusaidia kuweza kupata
mali nyingine”
“Ahsante Doreen kwa
kuniunga mkono.Kikubwa
ninachoshukuru ni kwamba bado
ni mzima ninao uwezo wa kufanya
kazi kwa bidii na kupata mali
nyingine.Nakushauri rafiki yangu
usikubali kuolewa kama
unafahamu kwamba hauna uwezo
wa kuzaa kwani manyanyaso
utakayoyapata toka kwa ndugu wa
mume ni makubwa sana.Ni mengi nimeyapitia ambayo mengine
sikutaka kumueleza hata Elvis kwa
kuogopa kumkosanisha na ndugu
zake.Si mara moja nimekuwa
ninapigiwa simu na ndugu zake
Elvis wakinitukana sana
wakinitaka niachane na ndugu
yao.Ni mateso makubwa sana
nimeyapitia na kuna nyakati
nilijuta kwa nini niliolewa”
akasema Patricia
“Pole sana Patricia kwa
mateso yote uliyopitia.Mungu
anaona kila kitu na atakusaidia
kuweza kuipata furaha ya maisha
yako.You’ll be happy again.Usikate
tamaa” akasema Doreen
“Haya ni malipo ya uovu
nilioufanya.Mungu ananiadhibu.I’ll
never be happy.My happiness is
gone.Elvis ndiye aliyekuwa furaha
yangu na baada ya kuondoka kwake sintakuwa na furaha
tena.Hakuna mwanadamu
atakayetokea na kunipa furaha
kama aliyonipa Elvis”
“Patricia usiwaze sana kuhusu
mambo haya kwa sasa.Huwezi
kujua Mungu ana mipango gani
nawe.Kila jambo hutokea kwa
sababu maalum.Tunaelekezwa na
maandiko kwamba tushukuru kwa
kila jambo”akasema
Doreen.Patricia akainama akafikiri
kwa muda na kusema
“Doreen do you believe there
is God? Akauliza Patricia na
kumstua Doreen
“Patricia tafadhali nakuomba
usiwaze sana hadi ukafikia hatua
ya kukufuru.Haya yote ni mapenzi
ya Mungu.Yeye ndiye mwenye
kutoa na hutwaa kwa muda
anaotaka yeye hata kama bado tunawahitaji wapendwa
wetu.Tunaelekezwa kumshukuru
kwa kila jambo hata kama ni
jambo la kutuumiza hata pale
anapowachukua wale tuwapendao
na kuwategemea” akasema Doreen
na Patricia akafuta machozi
“I don’t think there is God”
akasema
“Patricia tafadhali usiseme
hivyo.Mungu yupo.Tafadhali lala
na usiache kichwa chako kikajawa
mawazo mengi na
kumkufuru”akasema Doreen
“Where is he? Kama kweli
yupo haoni kama Elvis ndiye
furaha yangu ya pekee hapa
duniani na akamchukua? Why he
wants me to suffer? Akauliza
Patricia.Doreen hakujibu kitu
akafungua mkoba wake na kutoa
pakiti ya dawa akachukua dawa nne na kumpa Patricia
ameze.Miongoni mwa dawa zile
zilikuwemo pia dawa za
usingizi.Haukupita muda akalala
“Patricia ana uchungu
uliopitiliza hadi akaanza
kuzungumza maneno kama yale
akihoji uwepo wa Mungu.Inaumiza
sana.Kuna nyakati hata mimi
ninajikuta nikishindwa kuvumilia
na kutamani kumueleza ukweli
kwamba Elvis hajafa lakini
ninashindwa.Kwa nini lakini Elvis
akaamua kumtesa Patricia kiasi
hiki? Laiti angeweza kupata picha
ya namna mke wake alivyoumizwa
na kifo hiki sijui angefanya
nini.Hata hivyo kwa upande wa pili
hata yeye hakupenda kufanya hivi
bali amelazimika kufanya hivi kwa
ajili ya kusaidia watu wanaoteseka
na kuuawa bila hatia.Elvis anampenda sana Patricia na laiti
kama angekuwa na namna
nyingine ya kufanya basi angeweza
kufanya lakini hakuwa na njia
nyingine ya kufanya zaidi ya
kughushi kifo chake” akawaza
Doreen na kumtazama Patricia
aliyekuwa amelala kitandani
“Namuonea huruma sana
Patricia.Swali ninalojiuliza ni je
nini kitafuata baada ya Elvis
kumaliza operesheni yake?Je
atajitokeza na kudai kwamba
hakuwa amekufa? Jamii
itamuelewa kwamba kweli hakuwa
amekufa? Kama asipojitokeza je
utakuwa ndiyo mwisho wake na
Patricia?Kama ikiwa hivyo hiyo
itakuwa ni fursa yangu ya kuwa na
Elvis atakuwa wangu
daima.Naomba iwe hivyo na hilo
ndilo dua langu usiku na mchana.Nitafanya mpango tuhame
hapa nchini na kwenda nje ya nchi
kuanza maisha mapya na
hatutarejea tena Tanzania”
akawaza Doreen na kujilaza
pembeni ya Patricia

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ushukuriwe
 
Back
Top Bottom