Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

Shukurani mkuu
Ingawa kuna wakati unatufanya kushinde JF "Pale arosto itukamatapo"
 
I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 44

Nashukuru sana
Steven.Uliniambia kuna jambo
unataka tuzungumze.Ni jambo
gani?
“Ninahitaji msaada
wako.Unamfahamu Vicky
mapenzi?
“Yule mwenye Angel Vick
hotel?Samira akauliza
“Ndiyo huyo”
“Ninamfahamu.Kuna shoga
yangu mmoja ni rafiki yake wa
karibu sana.Unamtaka wa nini?
“Ninataka uniunganishe naye”
“Kivipi? Akauliza Samira kwa
mshangao kidogo
“Sikiliza Samira.Kuna taarifa
fulani nazihitaji kutoka kwa Vicky
hivyo ili kuzipata lazima nijifanye
na mimi ni mteja wake na
ninamuhitaji kimwili.Ninahitaji mtu wa kuniunganisha naye na
wewe unafaa kabisa”
“Oh my Gosh Stevenn !!
Unamtaka yule kahaba?akasema
Samira kwa mshangao
“Hili ni suala la kikazi baby
summer naomba unielewe na si
vinginevyo.Anazo taarifa muhimu
sana na ambazo ili kuzipata lazima
nijifanye ninahitaji huduma yake
ya kimwili.Nafahamu yule ni
kahaba wa bei ghali sana na
hawezi kamwe kunikubali mtu
kama mimi hivyo wewe
utamwambia kwamba kuna
mfanya biashara tajiri anamtaka
na yukotayari kutoa kiasi chochote
cha pesa kwa ajili ya usiku mmoja
tu.Jaribu kunijenga kama mtu
mzito na kiasi chochote cha pesa
atakachohitaji naomba umpatie
halafu mimi nitakurejeshea.Hata kama akikuambia kwamba ana
miadi na mtu usiku wa leo panda
dau na kwa vile ana tamaa ya fedha
atakubali.Unaweza kunisaidia kwa
hilo tafadhali? Akauliza Steven
“Steven hili ni suala kubwa
umenibebesha”
“Nafahamu ni suala kubwa
lakini sina mwingine wa kuweza
kunisaidia zaidi yako.Tafadhali
Samira kubali kunisaidia” akasema
Steven.Samira akafikiria kidogo
kisha akasema
“Sawa nitakusaidia lakini na
wewe naomba ulifanyie kazi hilo
suala nililokueleza”
“Usijali nitalifanyia kazi”
akasema Steven na kisha
wakaingia bafuni kuoga na Steven
akaondoka kwenda kuifanya kazi
aliyotumwa na Samira ****************
Saa nne na dakika kumi na
mbili gari moja la kifahari aina ya
Range rover evogue lenye rangi
nyeupe likawasili katika nyumba
ya bi Tarimo mama yake
Elvis.watu hawakuwa wengi
asubuhi hii zaidi ya ndugu
waliokuwa wakisubiri kufanyike
kikao cha kuanua tanga na msiba
kumalizka.Walikuwepo pia
majirani wachache wakisaidia
kufanya shughuli za usafi wa
vyombo na mazingira.Gari lile
likasimama na baada ya sekunde
kadhaa mlango ukafunguliwa
akashuka mwanadada mmoja
mrefu wastani mwenye mwili
mwembaba.Alikuwa amevaa gauni
refu jeusi na kichwani alijifunga kitambaa cheusi chenye nakshi za
kupendeza na macho yake
aliyafunika kwa miwani mikubwa
myeusi iliyoonekana kuwa ya
gharama kubwa.Mkononi alikua na
pochi ndogo ya dhahabu na vidole
vyak evote vya mikono vilijaa pete
za thamani.Aliufunga mlango wa
gari na kuanza kutembea hatua za
kunyata kuelekea ndani.Watu
waliokuwepo pale iliwabidi
kugeuza shingo zao kumtazama
mwanamke yule mrembo na
aliyeonekana tajiri sana.
Aliwasalimu akina mama
waliokuwa wamesimama
wakizungumza akajitambulisha
kwamba yeye ni rafiki wa mjane
wa marehemu na akaomba
aelekezwe mahala aliko ili
akamsalimu.Mama mmoja
akamuongoza ndani hadi katika chumba alimo Patricia.Ndani ya
chumba kile kulikuwa na
wanawake zaidi ya saba waliokuja
kumpa pole mwenzao.
“Patricia nimekuletea mgeni”
akasema yule mama na Patricia
akainua kichwa akamtazama
mgeni yule na akajikuta akipatwa
na nguvu za ghafla akainuka na
kwenda kumkumbatia
“Dada Juliana!! Akasema na
kisha akaanza kulia.Mwanadada
yule akambembeleza Patricia
akanyamaza
“Doreen huyu ni dada Juliana
nadhani nyote mnamfahamu ni
mwanamitindo maarufu sana hapa
nchini lakini kwa kipindi kirefu
hakuwepo hapa nchini alikuwa
anaendelea na shughuli zake za
mitindo nje ya nchi.Ni mtu mwenye
msaada mkubwa sana katika maisha yangu.Ametoka nami mbali
sana na sikutegemea kama
ningeweza kuonana naye leo na
katika mazingira haya.”Patricia
akamtambulisha Juliana kwa
wenzake
“Patricia pole sana kwa
masahibu yote
yaliyokupata.Nimerejea jana hapa
nchini kwa ajili ya kuandaa
mazishi ya baba yangu aliyefariki
katika ajali ya ndege.Nilifika hadi
katika ile nyumba yenu ya zamani
ndipo nikapewa taarifa zako na
mtu anayeishi pale kwamba
umefiwa na mumeo.Patricia
tutazungumza mambo mengi sana
mimi na wewe lakini kikubwa
kilichonileta hapa ni kuja kukupa
pole kwa matatizo haya makubwa
yaliyokupat………………” Juliana
akanyamaza baada ya mama mmoja kuingia mle chumbani na
kuwataarifu kwamba kikao cha
kuanua tanga kinataka kuanza na
wao ndio wanaosubiriwa
“Nimechelewa sana kwa
sababu ya kupatafuta mahala
hapa.Hata hivyo si neno mimi
nakwenda kukusubiri garii
umalize kikao kisha tuzungumze”
akasema Juliana
“Hapana Juliana
usiondoke.Wewe ni familia yangu
pia nakuomba ubaki.Nakuhitaji
sana” akasema Patricia na Juliana
akakubali kubaki.Wote wakatoka
mle chumbani na kwenda katika
hema kunakofanyika kikao.Watu
wote wanaotakiwa kuwepo katika
kikao hicho walikuwepo hivyo
kikao kikaanza
Kiongozi wa ukoo alifungua
kikao na kutoa maelezo kadhaa ya ufunguzi na kabla ya mambo
mengine ya kimila kuanza Patricia
akaomba apewe nafasi ya kusema
neno,akaruhusiwa,akasimama na
bila kupoteza muda akasema
“Mtaniwia radhi wakubwa
zangu kwa haya nitakayoyasema
lakini imenilazimu kuyasema.Mimi
ni mjane wa marehemu.Kwa
bahati mbaya mimi na marehemu
katika kipindi chote cha maisha
yetu hatukubahatika kupata
mtoto.Kukosa mtoto imekuwa ni
kigezo cha familia ya mume wangu
kuniadhibu na kunifanya wakati
mwingine nijute kwa nini
niliolewa na mtoto
wao.Nimetukanwa sana na
kuvuliwa thamani
yangu.Nimenyanyaswa mno na
ndugu wa mume wangu na kwa
kuwa nilikuwa nampenda sana mume wangu niliyavumilia haya
yote.Ni Elvis pekee ambaye
alikuwa liwazo langu,hata pale
ndugu zake wote waliponivua nguo
kwa matusi makubwa
waliyonitukana ana kwa ana na
katika simu,lakini ni yeye
aliyesimama upande wangu na
kunipa nguvu ya kuendelea
kuvumilia manyanyaso toka kwa
ndugu hao” akanyamaza na kufuta
machozi na mingong”ono ikaanza
kusikika
“Ninawaeleza haya kwa
uchungu mkubwa kwa sababu
nimeyaweka ndani ya kifua changu
kwa miaka mingi.Mtu pekee
ambaye aliniunganisha nanyi ni
Elvis na kwa sasa amefariki na kwa
bahati mbaya sina mtoto naye
ambaye angeendelea
kuniunganisha nanyi hivyo basi nimefanya maamuzi.Mimi na
mume wangu tulipambana na
maisha tukachuma mali nyingi
lakini tayari ndugu wamekwisha
anza mikakati ya kuweza
kuninyang”anya mali zote kwa
kisingizio kwamba sina mtoto na
marehemu.Kwa bahati mbaya
kwenu mali zote Elvis alizisajili
kwa jina langu na hakuna yeyote
mwenye uwezo wa
kuninyang’anya,hata hivyo
nimeamua kuwarejeshea mali zote
ambazo mimi na marehemu mume
wangu tulizitolea jasho.Tunazo
nyumba mbili,magari
manne,miradi kadhaa na
mashamba.Sintachukau hata
kimoja wapo.Nitawaachia vyote
kwani sitaki kuendelea
kunyanyaswa nanyi.Ninawachia
kwa moyo mweupe kabisa na ninaomba baada ya mimi kuondoa
mguu wangu hapa ndani basi
mniache nikaanze maisha yangu
mengine.Mimi na ninyi tutakuwa
tumemalizana.Sitaki mnifuate na
kuendelea kuninyanyasa katika
maisha yangu mengine.Niacheni
niendelee kumlilia mume wangu
peke yangu” akasema Patricia na
kufuta machozi.Akamuomba
mwanasheria wake asogee pale
mbele akiwa na mkoba akafungua
na kutoa nyaraka kadhaa za
umiliki wa mali walizokuwa
wanamiliki yeye na mumewe
ambazo alizionyesha kwa ndugu
wote walikuwepo pale.Kulikuwa
kimya kabisa na watu wote
waliokuwepo pale hawakuamini
kilichokuwa kinafanyika.Wengi
walimshangaa sana Patricia kwa
maamuzi yale aliyoyachukua.Akamfuata mama
Elvis na kumkabidhi nyaraka zile
na alipotaka kumpa mkono mama
yule akausukuma
“Nenda zako kahaba mkubwa
wewe.Hata sisi
hatukuhitaji.Umemuacha mwanetu
akaondoka bila hata kutuachia
mtoto.!! Akasema mama yule kwa
sauti kali na bila kupoteza muda
Patricia akawataka rafiki zake
waondoke pale msibani.Juliana
akamshika mkono na kumuongoza
hadi katika gari lake.Doreen naye
akaingia katika gari lake na wale
wengine nao kila mmoja akaingia
katika gari lake wakaondoka
“Patricia inaonekana kuna
mambo mazito sana yanaendelea
katika maisha yako” akasema
JulianaDada Juliana kuna mambo
mazito sana ambayo yamenitokea
na kuna nyakati nilitamani hata
kujiondoa uhai.Ndugu wale
wamenifanyia mambo mabaya
sana na
yasiyovumilika.Nitakueleza
mambo yote lakini kwa sasa
naomba unipeleke katika kaburi la
mume wangu.Jana nilishindwa
kushuhudia wakati akizikwa
nilipoteza fahamu” akasema
Patricia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo mkuu Jackal unatuchanganya maana umefungua uzi wa hadithi ukilinganisha speed yako na Mkuu Kulubule ni Maji na Mlima….Kuwa serious mkuu na hizi kauli, zinawakatisha wadau tamaa ya kutupia vitu adimu
Samahani mkuu mbududa!
 
Shukran sana Mzee kulubule
Hii season nyingne mkubwa wee anza tu hata sekunde hii!!

Tupo tushaketi kitambo kusubiri hvyo vigongo mkubwa
 
Asante sana Mkuu Kulubule. Iko vizuri sana hii na kasi yako ni nzuri.
 
I DIED TO SAVE PRESDANT

Sehemu 45

Inaonekana Patricia
amepitia matatizo
makubwa.Maneno aliyoyaongea
pale msibani yanatosha kutoa
picha halisi ya maisha ya taabu na
mateso aliyoyapitia.Si suala jepesi
kukubali kuacha mali zote
alizochuma na mumewe lakini kutokana na manyanyaso
aliyoyapata toka kwa ndugu za
mumewe amelazimika kufanya
hivyo ili awe na amani.Japo
wengine waliongea maneno ya
kubeza na kumdharau kwa
maamuzi yale lakini mimi
namuunga mkono kwa kile
alichokifanya na hata mimi
ningekuwa mahala pake
ningefanya vile vile.Ninamfahamu
vyema Patricia ni mtu mwenye
msimamo na akiamua jambo lake
huwa hayumbi.Aliwaonyesha kitu
kikubwa kwamba hakuwa na Elvis
kwa sababu ya mali bali kwa
mapenzi ya kweli na ndiyo maana akawarudishia mali
zote.Nasikitika sana kwa kukaa
kipindi kirefu namna hii bila
kuonana wala kuwasiliana
naye.Niliondoka nchini akiwa
bado anasoma sekondari na
sikupata nafasi ya kumuaga
.Nimefurahi kuonana naye tena
japo tumekutana sote katika
matatizo lakini huyu
ninamuhesabu kama sehemu ya
familia yetu.Ni mtu aliyenivutia
toka akiwa msichana mdogo na
nikajitolea kumsaidia yeye na
mama yake.Nasikitika mama yake
alifariki bila mimi kuwa na
habari.Nilifanya kosa kukaa muda mrefu bila kuwasiliana nao na
kufahamu maendeleo
yao.Nilidhani hawahitaji tena
msaada wangu baada ya
aliyekuwa mke wa rais wa wakati
ule kuwasaidia kuwapatia kiwanja
na mtaji wa bashara na maisha
yao kuanza kwenda
vizuri,nikasahau kamba licha ya
msaada wa fedha bado Patricia
alinihitaji.Safari hii sintamuacha
tena peke yake.Nitamshauri
niende naye nje ya nchi tukaishi
huko akaanze maisha
mapya.Endapo hatakuwa tayari
kuondoka basi nitamnunulia
nyumba nzuri hapa hapa Tanzania,nitamtafutia pia gari zuri
la kutembelea.Nitamsaidia aweze
kurejea katika maisha yake
aliyoyazoea” akawaza Juliana
Waliwasili makaburini na
Doreen akamuongoza hadi katika
kaburi la Elvis ambako kulikuwa
na mafundi waliokuwa
wanaendelea na zoezi la kuweka
nakshi za kupendeza,ikawalazimu
kusimamisha shughuli kwa muda
na kumpa Patricia nafasi.Akapiga
magoti na kukilaza kichwa chake
juu ya kaburi akamwaga machozi
mengi.Baada ya dakika kumi
Juliana akamuinuaImetosha Patricia.Bado
utaendelea kuja hapa mara kwa
mara kumlilia mumeo.Kwa sasa
twende ukapumzike” akasema
Juliana akiwa amemshika mkono
Patricia akampeleka garini.
“Doreen ninyi mnaweza
kwenda kupumzika.Patricia
ninakwenda naye nyumbani
kwetu kupumzika.Huyu ni
sehemu ya familia yetu.Atakuwa
salama msihofu” akasema Juliana
“Doreen nawashukuru sana
kwa kuwa nami katika kipindi hiki
kigumu.Ninakwenda na Juliana
huyu ni dada yangu msiwe na
hofu nitakuwa salama.Nitawasiliana nawe
baadae” akasema Patricia na
kuwaaga wale rafiki zake wengine
wakatawanyika





******************

Samira na rafikiye Mwasu
waliwasili Angel Vicky hotel
wakitumia gari la kifahari la
Samira.Ukiacha uzuri wao wa
asili,wanawake hawa walikuwa
wamejiremba vilivyo na kila aliyepishana nao aligeuka
kuwatazama kwa
nyuma.Haikuhitaji nguvu kubwa
kufahamu kuwa wanawake wale
walikuwa ni wenye kujiweza sana
kiuchumi.Walielekea mapokezi na
kuchangamkiwa na
wahudumu,wakajieleza shida yao
kuwa ni kuonana na Vicky
“Mna miadi ya kuonana naye
leo? Akauliza muhudumu
“Hapana hatuna miadi naye
ila mueleze kwamba Mwasu
mzungu anahitaji kumuona”
akasema Mwasu na yule
muhudumu akainua simu
akampigia Vicky akamjulisha kuhusiana na ujio wa Mwasu naye
akatoa maelekezo kwamba
amfuate ofisini.Mwasu hakuwa
mgeni wa hoteli ile akamuongoza
Samira kuelekea katika ofisi ya
Vicky.Hii ilikuwa ni mara ya
kwanza kwa Samira kufika hapa
hotelini.Kabla ya kuingia katika
ofisi ya Vicky wakaingia kwanza
katika ofisi ya katibu muhtasi
wake ambaye alifahamiana na
Mwasu wakasalimiana halafu
wakaingia ofisini kwa Vicky
“Wow ! Karibuni
visura.Mnavyong’aa kama
malaika” akasema Vicky kwa furaha baada ya akina Samira
kuingia ofisini kwake
“Huyu anaitwa Samira ni
shoga yangu”
“Nafurahi kukufahamu
Samira.U mrembo sana.Mimi
naitwa Vicky” akasema Vicky
huku akitabasamu
“Hata mimi nafurahi sana
kuonana nawe ana kwa ana
Vicky.Nimekuwa nakuona sehemu
mbali mbali na nilitamani sana
siku moja nifahamiane nawe.Leo
ndoto yangu imetimia” akasema
Samira
“Wow that’s so sweet”
akasema Vicky kwa furaha Vicky hatutaki kuchukua
muda wako mwingi kwani wewe
ni mtu unayejali mno
muda.Tunaomba dakika chache tu
za maongezi.Tumekuja kwa
mazungumzo ya
kibiashara.Mambo ya pesa”
akasema Mwasu.Vicky akawataka
watoke mle ofisini waelekee
sehemu maalum kwa ajili ya
mazungumzo.Wakaelekea juu ya
hoteli.Wahudumu
wakawahudumia kwa vinywaji na
mazungumzo yakaanza
“Haya niambieni visura
wangu ni biashara gani
mmeniletea? Akaanzisha mazungumo Vicky.Mwasu
akamfanyia ishara Samira
azungumze
“Kuna binamu yangu mmoja
anaishi nje ya nchi amekuja hapa
nchini kwa mapumziko na
anakuhitaji kwa usiku wa leo”
akasema Samira na kunyamaza
ukapita ukimya mfupi
wakitazamana kisha Vicky
akasema
“Samira mpaka umekuja
kwangu naamini tayari
unaifahamu shughuli yangu”
“Ndiyo ninaifahamu Vicky”
“Good.Lakini kwa bahati
mbaya kwa usiku wa leo tayari nina miadi na mtu kwa hiyo huyo
binamu yako atasubiri siku
nyingine.Utanisamehe sana kwa
hilo shoga yangu”
“Vicky naomba tuzungumze
pembeni” akasema Mwasu
wakainuka na kusogea pembeni
mahala ambako Samira
asingeweza kuwasikia
“Sikiliza Vicky hii si biashara
ya kukataa.Huyo jamaa ana fedha
kama mchanga.Amemweleza
Samira kwamba yuko tayari kulala
nawe kwa usiku wa leo kwa
gharama zozote zile.Please my
dear don’t say no to this” akasema Mwasu.Vicky akafikiri tena kidogo
na kusema
“Unamfahamu huyo mtu
mwenyewe? Anaishi nchi gani?
“Samira ameniambia kwamba
anatoka nje ya nchi.Kitu kikubwa
si nchi atokako bali ni kiasi gani
anatoa”akajibu Mwasu
“Mwasu tatizo si fedha bali
mtu ambaye nina miadi naye kwa
usiku wa leo ni mtu wangu wa
muhimu na ambaye amenisaidia
sana katika mambo mengi na bado
anaendelea kunisaidia.Siwezi
kumuacha kwa sababu ya mtu
mmoja ambaye atakuwa nami kwa
usiku mmoja na kuondoka.Faida nipatazo toka kwa huyo mtu
wangu ni nyingi kuliko fedha
ambazo huyo jamaa atanilipa kwa
usiku mmoja.Kwanza ameniona
wapi?
“Sikiliza Vicky,kusema ukweli
huyo jamaa hajakuona na wala
hakufahamu ila amempa kazi
Samira ya kumtafutia mwanamke
mrembo zaidi hapa Dar es salaam
kwa ajili ya kupitisha naye usiku
wa leo kwa gharama zozote ndipo
Samira aliponifuata akanieleza na
mimi nikamuelekeza tuje
kwako.Vicky jambo hili lina
maslahi pia kwetu kwani endapo
utakubali ombi la huyo jamaa basi hata sisi kuna kiasi fulani cha
fedha tutakipata kama ahsante ya
kumpelekea mwanamke mrembo
kuliko wote Dar es
salaam.Tunaomba utusaidie na
sisi tupate walau chochote kitu
hali ngumu sasa hivi” akasema
Mwasu.Vicky akafikiri kidogo na
kuuliza
“Samira anasema huyo jamaa
ana uwezo wa kutoa kiasi gani?
Kama unavyojua mimi si wa
kiwango kidogo kama wale
makahaba wanaojipanga
barabarani.Mimi sifanyii dhiki bali
ni kitu kilichoniingia damuni na
ninafanya kwa starehe.Shilingi nhgapi anaweza akanilipa kwa
usiku mmoja huyo jamaa?
Akauliza Vicky
“Samira ameambiwa na huyo
jamaa atafute mwanamke ambaye
atamlipa kiasi chochote cha fedha
utakachokihitaji” akasema Mwasu
“Good.Huyo jamaa lazima
atakuwa tajiri sana.Sawa
nimekubali nitavunja miadi na
huyo mtu niliyekuwa nikutane
naye leo kwa kuwa umenieleza
kwamba na ninyi pia mtafadikika
endapo nitakubali.Wewe ni rafiki
yangu mkubwa na siwezi
kukuangusha”akasema Vicky
kisha wakarejea alipo Samira Samira nimekubaliana na
ombi lenu baada ya Mwasu
kunieleza kwamba na ninyi pia
mtafaidika endapo nitakubali
kulala na huyo binamu
yako.Nadhani Mwasu amekwisha
kueleza kuwa mimi hutoza
kiwango kikubwa sana na ndiyo
maana watu wangu huwa ni
matajiri wakubwa na vigogo
wakubwa wa serikali.Huyo
binamu yako atanipa kiasi gani?
“Ahsante sana Vicky kwa
kukubali kwani ni kweli hata sisi
kuna kitu ameahidi kutupa.Wewe
unahitaji kiasi gani Vicky?
Akauliza Samira Millioni tano kwa usiku
mmoja” akajibu Vicky
“Fine.Utapata hizo fedha
ndani ya muda mfupi
ujao.Nitakutumia katika simu
yako kama utapenda”
“Hapan sitaki malipo ya
simu.I need cash” akasema Vicky
“Hakuna neno.Naomba unipe
muda kidogo nikamjulishe na
anipe kiasi hicho cha fedha.Mwasu
naomba nikukute hapa hapa
nitarejea muda si mrefu” akasema
Samira na kuondoka
“Ni taarifa gani anazozihitaji
Steven hadi akawa tayari kutumia
kiasi chochote cha fedha.Hata hivyo nitamuomba awe makini
sana asithubutu kulala na
Vicky.Yule anaonekana ni kahaba
aliyekubuhu na ndiyo maisha
yake” akawaza Samira na kwenda
hadi nyumbani kwake akachukua
kiasi cha shilingi milioni sita kisha
akarejea hotelini kwa Vicky
akamkuta akiwa bado anaendelea
kupata kinywaji na Mwasu.
“Nimerejea”akasema
“Karibu”akasema Vicky
“Mambo yote yanakwenda
vizuri.Nimerejea na kila kitu”
akasema Samira akafungua mkoba
na kumkabidhi Vicky kiasi cha shilingi milioni tano na milioni
moja akamkabidhi Mwasu
“Napenda watu wa aina hii
ambao hawana tatizo katika kutoa
malipo.Utanijulisha nitakutana
wapi na huyo bilionea.Nataka iwe
ni katika hoteli yenye hadhi ya
nyota tano kutokana na hadhi
yangu” akasema Vicky
“Usijali Vicky hayo yote
yatafanyika hupaswi kuwa na
wasiwasi” akasema Samira
wakaendelea na mazungumzo
kidogo halafu Samira akaondoka
akamuacha Mwasu akiendelea na
mazungumzo na Vicky.Mara tu alipotoka hotelini kwa Vicky
akampigia simu Steve
“Niambie Summer baby”
akasema Steven baada ya
kuipokea simu
“kazi yako tayari”
“Real ?!!
“Ndiyo.Kila kitu kimekamilika
na usiku wa leo utakutana na
Vicky.Nakuomba uje hapa
nyumbani nikupe
maelekezo”akasema Samira
“Ahsante sana
Samira.Ninakuja hapo muda si
mrefu” akasema Steven na kukata
simu
******************

Alipoachana na Patricia
makaburini,Doreen hakwenda
nyumbani kwake bali akaelekea
moja kwa moja katika makazi ya
Elvis.Alihitaji sana kuonana na
Elvis.
“Sasa mpira nimebaki nao na
ni uchaguzi wangu nifunge au
nitoe nje.Ninahitaji kucheza vizuri
sana mpira huu ili niibuke mshindi.Elvis atakuwa
wangu,lazima awe wangu.Yeye na
Patricia hakuna tena
kitakachoendelea kati yao.Kwa
Patricia Elvis tayari amekwisha
fariki na kwa upande wa Elvis sina
hakika kama atakubali kujitokeza
kwa Patricia na kudai kwamba
hakuwa amekufa.Haraka sana
lazima nianze kufanya mipango ya
kuondoka naye kwenda mbali
tukaishi huko mara tu
atakapomaliza kazi yake
salama.Nimekuwa natafakari
sehemu ya kwenda lakini mpaka
sasa bado sijapata jibu niende
wapi.Nataka tukaishi sehemu salama ambako hakuna
atakayegundua kama Elvis yuko
hai.Dada Martha yuko Sweden
natamani niende huko lakini sitaki
kuishi karibu na ndugu.Nataka
nikae sehemu ambako hakuna
anayenifahamu.Kuna nchi mbili
ambazo ninazifikiria Canada na
Australia.Nitafanya uchunguzi
nijue kati ya hizo nchi mbili ni ipi
ambayo inaweza ikatufaa mimi na
Elvis kwenda kuishi” Kichwa cha
Doreen kilijaa mawazo mengi
kuhusiana na yeye na Elvis.
Alifika katika makazi ya Elvis
Graca akamfungulia geti na mara tu aliposhuka garini
wakakumbatiana.
“Graca tell me how’s Elvis?
Akauliza Doreen huku sura yake
ikionyesha wasi wasi mwingi
“Elvis is fine” akajibu Graca
“Are you sure?
“Yes .He’s fine.He did
it”akasema Graca na Doreen
akamkumbatia tena huku sura
yake ikiwa imejaa tabasamu
“By the way you look so
pretty today” akasema Doreen
“Thank you”
“You are amazing.U msichana
mzuri sana Graca.” Akasema
Doreen kisha wakaelekea ndani na moja wa moja Doreen
akaelekea chumbani kwa Elvis
akagonga mlango na kuruhusiwa
kuingia ndani.
“Oh Elvis ! akasema Doreen
baada ya kuingia mle ndani
akakimbia na kumkumbatia Elvis
kwa nguvu na kumbusu
“Vipi hali yako Elvis? Akauliza
Doreen huku machozi yakimtoka
“Mimi naendelea vyema”
akajibu Elvis
“Elvis please don’t do that
again.Umeniweka katika wakati
mgumu sana.Nilipokuona ndani ya
jeneza nilishindwa kuvumilia na
kuangusha machozi na sikuamini kama ungeweza kuamka
tena.Tafadhali usirudie tena kitu
kama kile” akasema Doreen
“Patricia anaendeleaje?
“Hali ya Patricia siwezi
kuzema ni nzuri kwani amepata
jeraha ambalo halitaweza kupona
na ambalo litamtesa hadi sku
atakapoingia kaburini.Sikufichi
Elvis Patricia ameumia
sana.Sifahamu maisha yake
yatakuaje lakini yule ni
mwanamke jasiri atajitahidi
maisha yaende ila hatakuwa na
furaha tena.Wewe ndiye
uliyekuwa kila kitu kwake” akasema Doreen .Elvis
akainamisha kichwa
“Nimemuumiza mno
Patricia.Sikutegemea kama siku
moja ningeweza kumuumiza
namna hii.Hata hivyo baada ya
operesheni hii kumalizika
nitafanya kila niwezalo ili niweze
kuungana naye
tena.Nitamuelewesha atanielewa
kwamba nililazimika kufanya vile
ili kuweza kuikamilisha vyema
operesheni yangu”
“No ! akasema Doreen
“Don’t do that.” Akasema
Doreen na Elvis akainua kichwa akamtazama kwa sekunde chache
na kuuliza
“Kwa nini?
“Patricia tayari anafahamu
umekufa na amekwisha kubaliana
na hilo kwa hiyo utakapojitokeza
na kudai kwamba hukuwa
umekufa utazidi kumchanganya
na kumuumiza zaidi na hata
mapenzi yenu hayataweza kurejea
kama awali.Hakuna mwanamke
atakayekubali kuwa na
mwanaume ambaye
hamuelewi.You are dead to her so
let her move on.It’s over between
you.Kuibuka kwako na kumueleza
ukweli kwamba hukuwa umekufakutaleta mtafaruku mkubwa sana
na sisi wote tunaofahamu jambo
hili tutakuwa katika matatizo
makubwa sana.Please Elvis don’t
do that” akasema Doreen
“Doreen hakuna wa
kunipangia maisha
yangu.Sikupenda kufanya hivi
,sikupenda kumuumiza Patricia
mwanamke ambaye niliapa mbele
ya madhabahu kuwa naye katika
shida na raha,mwanamke ambaye
ninathubutu kusema kwamba
ninampenda kuliko wanawake
wote katika dunia hii,mwanamke
ambaye siwezi kumaliza
kumuelezea sifa zake njema.Uamuzi wangu baada ya
operesheni hii kumalizika na mimi
nikiwa bado hai lazima nimtafute
Patricia nikaishi naye hata kama
ni nje ya nchi mbali na hapa lakini
lazima niishi naye.Katu siwezi
kukubali kumpoteza.Nimetoka
naye mbali sana” akasema Elvis
“Elvis sikupangii kuhusu
maisha yako bali kama mtu wako
wa karibu ninakushauri kwamba
halitakuwa jambo jema kurudiana
tena na Patricia.Laiti ungefahamu
ulivyomuumiza,usingekuwa na
wazo la kutaka kujitokeza kwake
na kudai kwamba hukuwa
umekufa.Kwanza hatakuamini tena,na vile vile utakuwa
umeendelea kumuumiza zaidi na
zaidi.Hatakubali tena kuwa na
mwanaume kama
wewe.Ninakushauri kwamba
uanze kuyafikiria maisha mapya
bila Patricia.Hata yeye tayari
amekwisha kubali kwamba haupo
na hautarejea tena na tayari
amekwisha anza kujipanga kwa
maisha mapya bila ya
wewe.Ulipofanya maamuzi ya
kulifanya jambo hili naamini
ulijua kwamba utakumbana na
changamoto kama hizi.Nakushauri
usitake kuyaharibu mambo
zaidi,suluhisho pekee ni kuondoka hapa nchini na kwenda kuanza
maisha mapya mbali kabisa na
hapa ambako hakuna atakayejua
kitu ulichokifanya hapa” akasema
Doreen
“I’m confused right
now.Tuachane na hilo suala
nitafikiria taratibu nini cha
kufanya.Kwa sasa nahitaji muda
wa kujipanga vyema kwa ajili ya
kazi kubwa inayonikabili”
akasema Mathew na kuinamisha
tena kichwa akazama mawazoni
“Kuna jambo lingine ambalo
nadhani unapaswa ulifahamu
”akasema Doreen na Elvis akainua
kichwa harakaPatricia amefanya nini tena?
Akauliza
“Leo kulikuwa na kikao cha
familia ili kumalizia msiba.Katika
kikao hicho Patricia ameeleza
wazi kila kitu ambacho amekuwa
anafanyiwa na ndugu zako,namna
wanavyomnyanyasa na
kumtukana kwa kutopata
mtoto.Kwa hiyo amefanya
maamuzi magumu,mali zote
ambazo ulichuma naye
amezikabidhi kwa mama yako na
yeye ataondoka na nguo zake tu
na kila kitu amewaachia ndugu
zako” What ?!! akauliza Elvis huku
akisimama na kushika kiuno
“Ndiyo hivyo Elvis.Patricia
ameamua kuzikabidhi mali zote
mlizochuma pamoja kwa mama
yako na yeye hataondoka na kitu
chochote kile.Anataka aishi
maisha mapya.Tayari ana kidonda
kikubwa moyoni mwake na hivyo
hataki tena kuendelea kuumizwa
na kutoneshwa kidonda chake
kwa matusi ya ndugu
zako.Amefanya hivi ili aachwe
huru aendelee na maisha yake”
“That can’t be ! Kwa nini
akafanya maamuzi hayo wakati mali zangu zote nilimuandikisha
yeye?
“Ameeleza hayo yote kwamba
mali zote zimesajiliwa kwa jina
lake lakini ameamua kuziachia
kwa ndugu zako.Ameamua
kuyaanza maisha mapya na hataki
tena mahusiano yoyote na familia
yako ambayo ilikuwa
inamnyanyapaa.Amefanyiwa
mambo mengi mabaya ambayo
mengine hajaweza kukueleza
akihofia kukugombanisha na
ndugu zako.Patricia ameteseka
vya kutosha .Ameumia kwa muda
mrefu na sasa ni wakati wake wa kupumzika.Let her go Elvis”
akasema Doreen
“Dah ! Sikuwahi kutegemea
kama maisha yangu na Patricia
yangeweza kufika mwisho kwa
staili hii.Doreen anaweza kuwa
sahihi kwamba mimi na Patricia
tumefikia mwisho lakini bado
mapema sana kukubaliana na hilo
jambo.Ngoja niliweke kwanza
pembeni na nijiweke sawa kwa
ajili ya kuanza kuwakabili wale
maharamia waliosababisha
maisha yangu na mwanamke
nimpendaye kuliko wote yafike
hapa yalipofika.Ninaapa
hawatabaki salama.Nitawafagia kikatili sana mmoja baada ya
mwingine.Hakuna jiwe litasalia
juu ya jiwe” akawaza Elvis halafu
akamgeukia Doreen.
“Doreen ninashukuru sana
kwa kushirikiana nami katika
suala hili.Umefanya jambo kubwa
ambalo sijui nitakulipa nini.Hata
hivyo ni wakati wako wa kwenda
kupumzika kwani sasa ninaingia
kazini na sitaki kukuingiza katika
hatari” akasema Elvis na kumstua
Doreen
“No Elvis.Siwezi kukuacha
peke yako hapa.Suala hili ni letu
sote na s…....”Nalifahamu hilo Doreen na
ndiyo maana ninakuomba urejee
nyumbani kwako ukapumzike
kwani kinachokwenda kutokea ni
kitu cha hatari sana.Tayari
nimekwisha muumiza Patricia na
sitaki kumuumiza tena
mwingine.Msaada wako bado
ninauhitaji sana lakini
nitakuomba unisaidie ukiwa
kwako na si hapa kwani itakuwa
hatari kubwa kwako”
“Elvis…” akasema Doreen
“Doreen nakuomba usiseme
chochote kwa sasa.Kikubwa
ninachokuomba ni kuwa karibu
na Patricia.Kwa sasa anahitaji mno msaada wako.Hicho ni kitu
kikubwa sana ambacho ninataka
unisaidie kukifanya.Ukaribu wetu
utaendelea kama kawaida na
tutakuwa tukionana mara kwa
mara lakini pale tu
nitakapokujulisha kwamba
ninahitaji kukuona.Usifike hapa
nyumbani bila mimi kukuomba
uje.Patricia anakuhitaji sana kwa
sasa” akasema Elvis na machozi
yakaonekana machoni pa
Doreen.Elvis akamsogelea
akamfuta machozi
“Doreen tafadhali usilie.Hili
ninalifanya kwa ajili ya usalama
wako.Ni hatari kubwa kukaa karibu na mimi kwa sasa.Watu
ninaokwenda kupambana nao ni
watu hatari sana hivyo sitaki
wewe au mwingine yeyote aumie
ndiyo maana nakuomba kwa sasa
uende nyumbani kwako
ukapumzike.Kuwa karibu na
Patricia.By the way where is she
now?Umemuacha wapi na wewe
ukaja huku?
Doreen akafuta machozi na
kusema
“Tulipotoka nyumbani kwa
mama yako tukaelekea
makaburini na ndiko
tulikoachana.Ameondoka na
mwanamke mmoja anaitwa Juliana ni mwanamitindo ambaye
amekuja leo msibani”
“Juliana? Elvis akauliza
“Ndiyo.Unamfahamu?
“Juliana ni mtu muhimu sana
kwa Patricia na wamekuwa karibu
kwa muda mrefu toka angali mimi
na Patricia tuko shuleni.Kwa
muda mrefu amekuwa nje ya nchi
na kama amekuja basi amekuja
kwa wakati muafaka sana ambao
Patricia anamuhitaji sana.She’s in
good hands” akasema Elvis
“Simfahamu Juliana lakini
kwa namna nilivyowaona na
Patricia ninakubaliana nawe
kwamba she’s in very good hands hivyo usiwe na wasiwasi”akasema
Doreen
“Yah” akasema Elvis na
kukawa kimya.Baada ya sekunde
kadhaa Doreen akasema
“Elvis mimi na wewe
tumeianza operesheni hii
pamoja.Uliniamini ukaniita
nikufuate Mbeya na mimi kwa
kukuthamini nikaacha kila kitu na
kukufuata mara moja.Elvis niko
tayari kufanya chochote
utakachoniamuru kukifanya hata
kama ni cha hatari ili mradi
usiniweke mbali nawe hasa kwa
wakati huu ambao naamini
unanihitaji sana” akasema Doreen Doreen nauthamini mno
mchango wako na nimeweza
kufika hapa nilipo kutokana na
msaada wako mkubwa.Nakuhitaji
sana lakini kwa hali halisi ilivyo
hairuhusu uwe karibu yangu
kwani haitakuwa salama kwako
hata kidogo.Sitaki niyaweke
maisha yako katika hatari Doreen
ndiyo maana ninakuomba kwa
wakati huu uwe mbali nami
kidogo ili niweze kupambana na
hawa maharamia lakini kwa
wakati huo nitakuomba uwe
karibu sana na Patricia kwani
anahitaji mno mtu wa kuwa naye
karibu .Nitakuwa nawasiliana nawe mara kwa mara kujua
maendeleo yako na muda wowote
nitakapohitaji msaada wako
nitakujulisha haraka sana”
akasema Elvis..
“Nimekuelewa Elvis,nitafanya
kama ulivyoelekeza lakini nina
ombi moja kwako.Ninaomba
walau mara moja kwa wiki nije
hapa kuwajulieni hali na
kuhakikisha kwamba nyote mko
salama.Tafadhali naomba
usinizuie kwa hilo Elvis”
Elvis akatafakari kwa muda
na kusema
“Hakuna tatizo unaweza kuja
siku za jumapili kutujulia hali ila ujapo hakikisha hakuna anayejua
unakwenda wapi na kama ukiona
kuna mtu anakutilia shaka usije
tafadhali.Ninaomba unijulishe kila
kinachoendelea katika maisha ya
Patricia”
“Ahsante sana Elvis.Mungu
akulinde na akuongoze katika kazi
hii kubwa na ya hatari na
uikamilishe salama.Nina mambo
mengi ya kuzungumza nawe lakini
nitasubiri hadi hapo mambo
yatakapokuwa
yamekamilika.Kama kuna kitu
chochote utakihitaji hata kiwe cha
hatari kiasi gani nijulishe nami
nitahakikisha unakipata” Nashukuru sana Doreen kwa
kunielewa.Tafadhali usiache kuwa
karibu na Patricia”
‘Nitafanya hivyo Elvis.Basi
sitaki kupoteza muda wako ngoja
niende nyumbani nikapumzike
nikuache uendelee na mipango ya
operesheni yako.Tafadhali
wasiliana nami mara kwa mara”
“Nitafanya hivyo Doreen”
akajibu Elvis na Doreen akatoka
mle chumbani Elvis akamsindikiza
hadi garini kabla hajaingia garini
akageuka na kumkumbatia
Elvis,akambusu
“Elvis I’ll miss you a lot.Please
be safe for me and Patricia” akasema Doreen na Elvis
akatabasamu na kusema
“I will.Tafadhali hakikisha
Patricia anakuwa salama”
‘Usihofu Elvis.She’ll be fine”
akasema Doreen wakabusiana
tena ,Elvis akamfungulia mlango
wa gari akaingia na kuondoka
“Nilidhani Elvis anatania
aliposema kwamba hataki Doreen
aendelee kukaa hapa,kumbe
alikuwa anamaanisha
alichokisema” akawaza Graca
aliyekuwa dirishani akitazama
Doreen akiondoka.Uso wake ulijaa
tabasamuSasa nimebaki peke yangu
na mpira,nishindwe mwenyewe
kufunga.Sipaswi kufanya
makosa.Natakiwa kufanya kila
niwezalo kuhakikisha Elvis
anakuwa wangu.Sitaki kujilaumu
baadae kwamba nilipata nafasi
nikashindwa kuitumia.Huu ni
wakati wangu wa kuyaanza
maisha mapya nikiwa na
Elvis.Mwili wote unanisisimka
natamani hata sasa nimweleze
Elvis kwamba ninataka kuishi
naye lakini ngoja nivute subira
niendelee kuandaa mazingira ya
kuhakikisha Elvis anakuwa
wangu.Mwanaume kama huyu mwenye mapenzi ya kweli kwa
mke wake ni kazi ngumu kumnasa
lakini nitafanya kila niwezalo
kuhakikisha ninamshawishi.Japo
sina uzoefu sana katika masuala
hayo ya mapenzi lakini
nitajitahidi” akawaza Graca na
kumuona Elvis akirejea ndani
akamfuata
“Mbona Doreen amekuja na
kuondoka? Graca akauliza
“Nilikueleza awali kwama
sitaki ukaribu mkubwa na Doreen
hasa kwa wakati huui ambao
Patricia anaamini
nimekufa.Nalifahamu lengo la
Doreen ni kutaka kutumia nafasihiyo kuanzisha mahusiano ya
kimapenzi nami jambo ambalo
silikubali.Patricia bado ni
mwanamke pekee ambaye
nampenda kuliko wote na
nitaendelea kumpenda” akasema
Elvis na kuketi sofani Graca
akaenda kuketi pembeni yake
“Elvis naomba nikuulize kitu
ila utajibu kama utajisikia kujibu”
“Uliza Graca” akasema Elvis
“Kwa hivi sasa kila mtu
anafahamu kwamba umefariki.Ni
watu wachache tunaofahamu
kwamba uko hai.Sifahamu nini
mipango yako baada ya kuimaliza
operesheni hii lakini naaminihaitakuwa rahisi kujitokeza kwa
watu waliokuzika kaburini an
kudai kwamba hukuwa
umekufa.Hata kama ukiamua
kufanya hivyo itakuchukua muda
kidogo na hata mimi sikushauri
ufanye hivyo kwani ni hatari
kwako na kwetu pia lakini swali
langu ni kwamba kwa muda huo
wote utaishi vipi bila kuwa na
mwenzi au mtu wa kukuliwaza?
Elvis akatabasamu baada ya
swali lile la Graca
“Kwa nini umeuliza hivyo
Graca?
“Huhitaji mtu wa
kukuliwaza?Graca akauliza Unaamaanisha nini Graca?
“Ninamaanisha huhitaji mtu
wa kukuliwaza katika wakati huu
mgumu ili akili yako iweze kutulia
na kufanya kazi sawa sawa?
Elvis akatabasamu na kusema
“Kwa sasa sihitaji mambo
hayo.Nina mambo mazito
yanayonikabili hivyo masuala ya
mapenzi ninayaweka
kand😵peresheni iliyoko mbele
yangu ni nzito sana na lazima
nifanye kila lililo ndani ya uwezo
wangu kuweza kuwafagia
maharamia hawa wanaosababisha
mamia ya watu wanauawa bila
hatia huko mashariki ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Sidhani
kama kuna mwanamke
anayeweza kuniliwaza na
kunisahaulisha kuhusu mke
wangu Patricia.”
“Elvis nafahamu wewe ni mtu
jasiri lakini hata uwe jasiri vipi
ukweli utabaki pale pale kwamba
unahitaji mtu wa
kukuliwaza.Tunasoma katika
historia hata wale watawala
waliowahi kuwa majasiri
wakubwa lakini walihitaji pia
faraja kutoka kwa wake zao kwa
hiyo hata wewe unahitaji faraja
Elvis.You need someone by your
side especially at this time” Graca I’m at war and right
now I need only soldiers by my
side.I need people with ugly
faces,people who are trained to
fight and kill !! akasema Elvis
“You need more” akasema
Graca
“You need a sweet voice
every morning to tell you that
things will be fine.Hiyo ni silaha
kubwa sana Elvis.Unahitaji mtu
wa kukutia moyo hata pale
ambapo unahisi mambo hayaendi
sawa au hata pale unapohisi
kushindwa.Usiwaze sana kuhusu
hilo,I’m right here.I’ll comfort
you,I’ll encourage you,I’ll do everything to make sure you are
fine.Nitasimama nawe hata pale
mambo yatakapokuwa magumu
hivyo usijihesabu kwamba uko
peke yako.Nitakusaidia
kupambana ingawa sintakuwa na
silaha” akasema Graca na Elvis
akajikuta akitabasamu
“Graca ahsante sana kwa
maneno hayo yenye kunipa nguvu
zaidi.Una ujasiri mkubwa
sana.Ninakuahidi kwamba
nitakulinda kwa kila uwezo nilio
nao na nitahakikisha kwamba
unakuwa salama na maisha yako
yanakuwa na furaha siku zote” akasema Elvis.Graca akamsogelea
karibu zaidi na kumkumbatia
“Thank you Elvis.You are so
nice” akasema na kumtazama
Elvis usoni kwa muda wa sekunde
kadhaa
“Elvis ngoja nikuache
ujiandae.If you need anything let
me know” akasema Graca na
kuinuka akaelekea chumbani
kwake
“Mara ya kwanza
nilipomuona Graca sikutegemea
kama anaweza kuwa ni binti
mwenye ujasiri wa namna
hii.Ninafurahi kwamba hali yake
imeanza kuimarika na kurejea katika maisha ya kawaida.Leo
ameamka na furaha kubwa na
nimeshangaa hata kwa maswali
ambayo amekuwa ananiuliza
kuanzia asubuhi.Ametaka sana
kufahamu kuhusiana na maisha
yangu ya kimapenzi.Kwanza
alitaka kufahamu kuhusu mimi na
Doreen .Licha ya kujaribu
kumdanganya lakini kumbe tayari
anafahamu kila kitu kwamba mimi
na Doreen tumekuwa tunakutana
kimapenzi.Hii si picha nzuri hata
kidogo na ndiyo maana nimeamua
kumuondoa Doreen hapa ili jambo
lile lisiendelee.Sasa hivi
ameniuliza kama nitahitaji mtu wa kunifariji.Yuko sahihi ninahitaji
sana mtu wa kunisaidia kukiweka
sawa kichwa changu lakini
mwanamke pekee mwenye uwezo
huo ni Patricia .Hakuna
mwanamke mwingine anayeweza
kuchukua nafasi yake ndani ya
moyo wangu .Dah ! Ngoja
niachane na suala hili nijielekeze
zaidi katika kupanga mipango ya
kukabiliana na hawa maharamia”
akawaza Elvis
Alipotoka sebuleni Graca
alieleka moja kwa moja chumbani
kwake akakaa kitandani huku uso
wake ukiwa na tabasamu kubwa Mhh ! mambo hayatakuwa
rahisi.Kumpata Elvis si jambo
rahisi hata kidogo.Mawazo yake
yote bado ni kwa mkewe Patricia
na sijui nifanye nini niweze
kumbadili mawazo hata hivyo
sikati tamaa nitaendelea na
harakati zangu hadi
ntakapofanikiwa.Nimeanza
vizuri.Siku zote Simba
mwendapole ndiye mla nyama na
mimi sipaswi kuwa na
papara.Nitakwenda taratibu hadi
nihakikishe nimefanikiwa kuingia
katika kichwa cha
Elvis.Nikifanikiwa katika hili
nitakuwa ni mwanamke mwenye furaha sana katika maisha yangu
yote.Kuna nyakati namuonea wivu
hata huyo mke wake kwa kuwa na
mwanaume kama huyu ambaye
anampenda kwa moyo wake
wote” akaendelea kuwaza Graca

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom