Riwaya: I died to save my President

Riwaya: I died to save my President

I DIED TO SAVE PRESIDANT

Sehemu 51

Inakaribia saa sita za usiku
Elizabeth na Juliana wakiwa garini
wakitoka katika kikao cha ndugu
ambacho walifikia muafaka
kuhusiana na mazishi ya Deus
mume wa Elizabeth.
"Juliana kuna jambo
ninalifikiria kuhusu yule rafiki
yako Patricia"
"Jambo gani mama?
"Ninataka nimuweke awe
msimamizi wa miradi yetu mbali
mbali.Kwa sasa baada ya kufiwa
na mumewe atakuwa katika
upweke mkubwa.Kwa kuwa tunamiradi sehemu mbali mbali
duniani atakuwa akisafiri mara
kwa mara na hii itamsaidia sana
katika kusahau machungu ya kifo
cha mumewe.Unaonaje kuhusu
wazo hili?
"Wazo lako ni zuri mama
lakini hapana.Sitaki Patricia
ahusishwe kwa namna yoyote
katika miradi ya familia
yetu.Kwanza yule ni msomi mzuri
na ana kazi yake.Amesomea
udaktari na hana elimu ya
biashara.Hatafuti kazi kwani
anaweza kujimudu kutokana na
kazi yake anayoifanya na hana
shida ya kutafuta kazi
nyingine.Pili miradi ya familia
yetu imekuwa na mabalaa mengi” sura ya Elizabeth
ikabadilika.Juliana akaendelea
“Sintasahau kifo cha
Godson.Alipoteza uhai baada ya
kumshirikisha katika miradi ya
familia.Godson alikuwa msomi na
mwenye kazi nzuri sana lakini
mkamshawishi aachane na kazi
aliyokuwa anaifanya asimamie
miradi ya familia lakni matokeo
yake ni kukatwa pumzi kikatili
namna ile.Patricia amepitia
mambo mengi sana na sitaki
kumuongezea matatizo
mengine"akasema Juliana
"Juliana tafadhali
usinikumbushe kuhusu
Godson.Mpaka leo kidonda
kilichotokana na kifo chake
hakijapona."akasema Elizabeth Sote bado tunatibu majeraha
yaliyosababishwa na kifo cha
Godson.Patricia ni muhimu sana
kwangu hivyo sitaki kuongeza
tena kidonda kingine"
"Juliana tafadhali naomba
unielewe sina leno baya na
Patricia bali ninatafuta
msaidizi.Wewe umekwisha kataa
kusimamia miradi ya
familia.Mdogo wako Sekela naye
yuko masomoni na kwa sasa
baada ya baba yako kufariki
nimebaki peke yangu hivyo
nahitaji msaidizi ambaye ni mtu
wa karibu na familia yetu.Patricia
anafaa sana"akasema Elizabeth
"mama tafadhali kama
unahitaji mtu wa kufanya shughuli
zako tafuta mtu mwingine na si Patricia.I dont want to involve her
in your dirty business"akasema
Juliana na Elizabeth akastuka na
kumtazama kwa macho makali
"What you've just said?
akauliza Elizabeth kwa ukali
"I dont want Patricia to be
involved in your dirty businesses"
akasema Juliana.Elizabeth
aliyekuwa katika usukani
akalazimika kupunguza mwendo
wa gari na kuegesha kandoni mwa
barabara halafu akainamisha
kichwa chini .
“Kuna nini mama mbona
tumesimama? akauliza
Juliana.Elizabeth akavuta pumzi
ndefu na kusema
"Sikutegemea kabisa kusikia
neno kama hilo likitoka kinywani mwako my dear daughter"
akasema Elizabeth huku
akimtazama Juliana kwa macho
makali
“Unathubutuje kutoa kauli
kama hiyo Juliana? akauliza
Elizabeth
"Kwani si kweli mama?Mimi
ni mtu mzima ninaelewa mambo
mengi japo sijawahi kukueleza
chochote kuhusiana na mambo
mnayoyafanya wewe na baba
lakini ninafahamu kuwa kuna
mambo machafu mnayafanya na
ndiyo maana sitaki kushiriki
katika biashara zetu" akasema
Juliana huku akilengwa na
machozi
"Kila siku taswira ya Godson
inanijia namna alivyoshambuliwa na mwili wake kuharibiwa kwa
risasi.Yalikuwa ni mauaji ya
kinyama sana.Japo hamtaki
kusema lakini ukweli ni kwamba
yalisababishwa na mambo yenu
ya siri"
Elizabeth akavuta pumzi
ndefu na kuwasha gari
wakaendelea na safari kimya
kmya hadi walipofka
nyumbani.Mara tu Juliana
aliposhuka mama yake akamuita
"Juliana we need to talk!!
"Mama nimechoka
tutazungumza siku nyingine"
"Hakuna siku nyingine.We
need to talk now! akasema
Elizabeth kwa ukali.Juliana
hakutaka malumbano na mama
yake wakaongozana hadi katika chumba cha maongezi.Elizabeth
akamtazama Juliana kwa muda
halafu akasema
"Arlight .Its true,me and your
father we have some dirty
business"akanyamaza na baada ya
sekunde chache akaendelea
"You are who you are,
because of the dirt businesses me
and your father are doing.Ni kwa
sababu ya biashara hizo unazozita
haramu,umeishi maisha
mazuri,umesoma vizuri na
umejulikana.Mimi na baba yako
hatukuwa na maisha haya
mnayoishi ninyi.Tumehangaika na
kujiingiza katika mambo mengine
mabaya kwa ajili yenu hivyo
unapaswa kuwa na shukrani kwa
maisha haya unayoyaishi leo.Hujawahi kukosa kitu
chochote unachokihitaji katika
maisha yako nini kingine
unakihitaji?Ninataka leo iwe ni
mwanzo na mwisho kusikia
unalitamka neno kama
hilo.Nataka uwe kimya na
uendelee kuyafurahia
maisha.Niambie chochote
unachokihitaji nitakupatia lakini
usithubutu kutaka kuingia katika
mambo yangu.Sitaki kukupoteza
kama nilivyompoteza Godson."
akasema Elizabeth kwa ukali na
Juliana akawa kimya
"Unafahamu ni hatari ngapi
mimi na baba yako tumezipita ili
ninyi muwe salama na muishi
maisha ya kifahari kama
haya?akauliza Elizabeth halafu akavua gauni alilovaa na
kumuonyesha Juliana makovu
kumi na moja ya risasi mwilini .
"Huu ni ushahidi kwamba
nimepitia magumu mengi hadi
kufika hapa nilipo.Nilitegemea
ungenishukuru kwa mambo haya
yote niliyowafanyia lakini badala
yake umenibeza.Kama mtoto
wangu wa kwanza sikutegemea
kabisa kama siku moja ungeweza
kutamka maneno kama yale"
"I'm sorry mother" akasema
Juliana
"Juliana nakubali I'm not a
perfect mother lakini ninaweza
kujivunia kwamba kwa asilimia
kubwa wanangu nimehakikisha
wanapata maisha bora.Siku moja
utaelewa kwamba haya yoteninayoyafanya ni kwa ajili
yenu,utanitafuta unishukuru
lakini utakuwa umekwisha
chelewa.Siaki kukuingiza katika
mambo yangu ila nataka ufurahie
maisha wewe na mdogo
wako.Tazama baba yako
ameondoka,mimi mwenyewe
hakuna ajuaye pengine muda
wowote ninaweza kuondoka pia
hivyo ninajitahidi kuwawekea
misingi mizuri ili kwamba hata
nikifa leo muendele kuwa na
maisha mazuri wewe na mdogo
wako.Kuna mambo mazuri
ninayaandaa kwa ajili yako.Nataka
nikuibie siri ila naomba uufunge
mdomo wako na usimwambie mtu
yeyote.Skutaka kukueleza lakini
imenilazmu nikueleze ili ujue kwamba mimi silali nikiwaza
mambo mazuri kwa ajili
yako"akasema Elizabeth na
kunyamaza kwa muda halafu
akasema
"David kuna jambo alikuja
kunieleza.Kuna mpango
unaendelea wa kumuondoa rais
wa sasa madarakani na yeye
David ataapishwa kuwa rais wa
mpito na akishafanikiwa kuwa
rais atakuteua uwe waziri wa
maliasili na utalii.Jambo hilo
tumekwisha lijadili na
tumekubaliana .Nilitaka iwe
suprise kwako lakini
umenilazimisha nikueleze kabla
ya wakati" Juliana akamtazama mama
yake akakosa neno la kusema.Uso
wake ukajenga tabasamu
"Say something
Juliana"akasema Elizabeth
"What can I say mother?
Nimekosa neno la kusema ila
nimepokea taarifa hiyo kwa
mstuko kwani mimi sina uzoefu
wowote na mambo ya
siasa.Nitawezaje kuimudu nafasi
kubwa kama hiyo?Halafu naomba
ufafanuzi kuhusu hilo jambo la
kumuondoa madarakani rais
kwani kwa ninavyofahamu mimi
rais huchaguliwa kila baada ya
miaka mitano na rais aliyepo
madarakani hajamaliza kipindi
chake cha pili cha miaka mitano
wanamuondoaje?Wanataka kumuua?akauliza Juliana
akionyesha kuwa na wasi wasi
mkubwa
"Hapana hakuna mapinduzi
yoyote au kumuua rais wa
sasa.Kwa maelezo aliyonipa David
ni kwamba kuna mchakato
unaendelea ndani ya chama chake
wa kumuondoa rais madarakani
kwa kushindwa kumudu vyema
majukumu yake.Chama
hakiridhishwi na uongozi wake
hivyo wanataka kumtoa na
kumuweka mtu mwingine kwa
muda na mtu huyo tayari
ameandaliwa ni David.Pindi
akipata urais na wewe utangia
katika baraza la mawaziri.Huu ni
mwanzo wa safari yako ya kuwa
mwanamke mwenye nguvu na utakapoingia katika nafasi kubwa
ndipo utakapoelewa mimi
ninafanya nini.Usihofu kwamba
hufahamu siasa.Si kila waziri au
mbunge anaifahamu vyema
siasa.Kila kitu utakifahamu huko
huko mbele ya safari.Hukupaswa
kulifahamu hili kwa sasa lakini
kwa kuwa umekwisha lifahamu
anza kufanya maandalizi.Si muda
mrefu sana utakuwa
mheshimiwa.Hizi zote ni juhudi
zangu za kuhakikisha unakuwa na
maisha mazuri na mafanikio
makubwa.Juliana mimi na wewe
hatupaswi kuwa na
tofauti.Tunapaswa kuwa kitu
kimoja.Umechoka sana Juliana
nenda kapumzike tutazungumza
mambo mengi baada ya mazishi" Juliana akaondoka na moja
kwa moja akaelekea chumbani
kwa Patricia akagonga mlango.
Patricia ambaye hakuwa na
usingizi akainuka na kwenda
kuufungua mlango
“Dada Juliana karibu”
“Ahsante Patricia.Samahani
kwa kukusumbua usiku
huu.Tayari ulikwisha lala?
Akauliza Juliana
“Hapana dada.Sina
usingizi.Ahsante sana kwa ule
mvinyo ulioniletea umenisaidia
sana.Vipi huko utokako mambo
yamekwendaje?akauliza
Patricia.Juliana akamimina
mvinyo katika glasi akanywa
funda kubwa kisha akasema Huko mambo yamekwenda
vizuri na tumefikia
makubaliano.Mazishi ni jumanne
ijayo.Msiba utakuwa hapa
nyumbani na kesho kutwa
jumatatu mwili utawasili na siku
ya jumanne tutazika.Kuanzia
kesho hapa nyumbani patakuwa
ni mahala penye heka heka nyingi
za maandalizi”
“Imekuwa vyema mmefikia
makubaliano”akasema Patricia
“Ni kweli Patricia imekuwa
vyema kwani hata wao hawakuwa
wakielewana lakini kwa msiba
huu umewaleta pamoja na
wamemaliza tofauti zao” akasema
Juliana na ukimya
ukatanda.Patricia akasema Dada Juliana kuna jambo
nataka nikueleze.”
Juliana akainua kichwa na
kumtazama Patricia
“Nimepigiwa simu na mke wa
rais akanijulisha kwamba
wamejadiliana na rais na
wamekubaliana kwamba niende
nikaishi nao ikulu kwa muda hadi
hapo nitakapokuwa tayari kuanza
shughuli zangu.Nimefikiria
nimeona ni jambo jema hivyo
baada ya mazishi ya baba
nitakwenda kuishi
ikulu.Nakuomba usinielewe
vibaya kwani hata hapa ni
nyumbani na ninapata kila
ninachokhitaji lakini wale wazee
wameniomba sana nikaishi nao na
nimeshindwa kukataa” Hakuna tatizo kuhusu hilo
Patricia.Hayo ni maamuzi yako
lakini siku zote kumbuka kuwa
hapa ni nyumbani kwako na
milango iko wazi kwako muda
wowote” Akasema Juliana.Ukapita
ukimya kisha Patricia akauliza
“Dada Juliana baada ya
mazishi ya baba utaondoka tena
kurejea huko ulikokuwa?
“Hapana sintaondoka tena.I’m
back for good.This time I wont run
again” akasema Juliana
“ Run?!! Akauliza Patricia
“ Patricia kuna mambo mengi
yalinikuta na kunifanya
nikakimbia nchi.Sikuondoka kwa
kupenda.Ninapenda sana
nyumbani lakini nililazimika
kuondoka bila kupenda” Nini kilitokea dada Juliana?
akauliza Patricia.Juliana
akaichukua chupa ya mvinyo
akaitingisha halafu akagugumia
mvinyo wote uliobaki
“Wewe ni mdogo wangu na
nitakueleza,ila yote
nitakayokueleza yabaki katika
kifua chako.Hatakiwi mtu
mwingine yeyote kuyafahamu”
“Usiwe na wasi wasi nami
Juliana” akasema Patricia.Juliana
akavuta kumbu kumbu halafu
akasema
“Sikuwahi kukuonyesha
mpenzi wangu wakati ule lakini
nilikuwa na mpenzi anaitwa
Jose.Tulipendana mno na tulikuwa
na mipango mingi sana ya maisha
yetu ya usoni.Ni mwanaume pekee ambaye nilimpenda kwa
moyo wangu wote na hadi leo hii
bado ninaamini kwamba
hatatokea mwingine kama
yeye.Jose alikuwa ni mtoto wa
kigogo mmoja wa serikali na
familia yao walikuwa wenye
kujiweza sana kifedha kama sisi.”
Akanyamaza kwa sekunde kadhaa
na kuendelea
“Yuko wapi kwa hivi sasa?
Mliachana? Akauliza Patricia
“Mapenzi yetu yalikuwa
mazito sana na tusingeweza
kuachana.Aliuawa”
“Aliuawa? Nani alimuua?
“Mpaka leo sifahamu ni nani
walimuua Jose lakini alikatwa
shingo na kichwa
kikatenganishwa na mwili kishamwili wake ukaenda kuwekwa
katika geti la nyumbani kwa
wazazi wake na pembeni yake
kukiwa na barua ya onyo kwamba
nitakayefuata ni mimi.Kwa haraka
sana wazazi wangu
wakanikimbiza na kwenda
kunificha nje ya nchi ambako
nimeishi toka wakati ule na
sijawahi kurejea Tanzania.Msiba
wa baba umenirejesha tena hapa
na ndiyo maana ninasema
kwamba safari hii siwezi kukimbia
tena.Nimechoka kuishi nchi za
watu.Kama ni kuniua waniue tu
siwezi kuogopa tena”akasema
Juliana akionekana kuwa na
hasira na uchungu mwingi
“Pole sana Juliana.Ninajiona
nimepitia matatizo lakini kumbe ya kwako ni mazito kuliko
yangu.Pole sana.Ni nani hao
waliomuua Jose? Walifanikiwa
kukamatwa?
“Mpaka leo imebaki ni fumbo
gumu kufumbuliwa”
“Hakuna aliyewahi
kukamatwa kuhusiana na mauaji
hayo? Akauliza Patricia
“Hakuna aliyewahi
kukamatwa.Hii inaniumiza mno.”
“Kuna kitu kinanishangaza
sana dada Juliana" akasema
Patricia
"Kitu gani Patricia?
"Ulisema kwamba Godson
aliuawa kwa kupigwa risasi nyingi
na watu wasiojulikana na mpaka
leo watu hao hawajawahi
kukamatwa.Kama haitoshi na mpenzi wako Jose naye aliuawa
kikatili na mpaka leo hii wauaji
wake hawajawahi
kukamatwa.Wewe mwenyewe
ulichukuliwa na kwenda kufichwa
nje ya nchi na hiyo ndiyo salama
yako kwani vinginevyo na wewe
ungekwisha uawa.Hudhani kama
kuna watu wanailenga familia
yenu?Haya yanaonekana ni mauaji
ya kulipiza kisasi.Mmewahi
kulifikisha suala hili katika
vyombo husika? akauliza Patricia
"Patricia uko sahihi kabisa.Ni
wazi wauaji hawa wana lengo
baya na familia yetu.Mdogo wangu
wa mwisho aliwahi kunusurika
kuuliwa kwa risasi na ndiyo
maana ikawalazimu wazazi
kumtafutia walinzi wa kuongozana naye kila sehemu .Ni
majanga matupu katika familia
yetu.Matukio haya yote
yanapotokea wazazi husema
wanashughulikia lakini mpaka leo
hakuna majibu yoyote ya nani
waliofanya mauaji haya mabaya
.Jambo hili limekuwa linaniumiza
sana kwa miaka mingi na ndiyo
maana safari hii sitaki kukimbia
nataka nibaki hapa hapa nchini ili
niwafahamu watu hao ni akina
nani na sababu ya kuiandama
familia yetu?
"I’m going to help you"
akasema Patricia
"Patricia no! Dont involve
yourself in this" akasema Juliana
"Juliana wewe ni dada yangu
umenisadia mambo mengi kwa wakati ule ambao nilikuwa na
shida sana na mpaka sasa bado
uko nami.Ninao wajibu wa
kukusaidia pia"
"Patricia nauthamini sana
mchango wako lakini katika hili
hapana.Sitaki ujihusishe nalo.Ni
jambo la hatari kubwa.Tayari una
matatizo mengi yanayokukabili
kwa sasa na sitaki uongeze
matatizo.Nimekueleza tu kama
mdogo wangu ili uwe na picha ya
masahibu ninayoyapitia"
"Juliana tafadhali naomba
ukubali nikusaidie dada
yangu"Patricia akasisitiza
"Unataka kunisaidia vipi
Patricia?
"Ninaweza kukuunganisha na
watu ambao wanauwezo wa kufanya uchunguzi na kuwabaini
wauaji.Ninafahamiana na rafiki
zake Elvis na nikiwaomba
wataniskiliza.Hata bosi wao mzee
Meshack Jumbo ninafahamiana
naye na ni mtu mwema.Amekuwa
nami toka msiba ulipotokea na
hadi jana katika kikao cha familia
alikuwepo nikimuomba anisaidie
kuhusu suala hili hawezi kukataa"
akasema Patricia na Juliana
akainamisha kichwa akazama
mawazoni
"Juliana" akaita Paricia
"Unasemaje kuhusu wazo
hilo?
"Wazo hilo si baya lakini..."
"Mbona una wasi wasi dada
Juliana?akauliza Patricia.Juliana
akafikiri kidogo na kusema Kuna tatizo lipo Patricia."
"Tatizo gani?
"Japo sina bado uthibitiso au
ushahidi wa kutosha wa
kuhusiana na hili lakini ninahisi
wazazi wangu ni chanzo cha haya
yaliyotokea.Nahisi kuna mambo
wanajihusisha nayo kuna
uwezekano familia yetu inalengwa
na mahasimu wao wa kibiashara
ndiyo maana tunauawa kama
kuku.Endapo nitakubali kuruhusu
uchunguzi ufanywe kuna
uwezekano yakaibuka mambo
mengine kuhusu familia
yangu.Sitaki jambo hilo litokee"
akasema Juliana
"Juliana usiogope katik
akuipigania haki.Ndugu yako
Godson na mpenzi wako Joseph waliuawa kikatili na wewe
mwenyewe ukanusurika.Una
uhaika gani kama hao wauaji
wamekwisha acha kukusaka? Uko
tayari kuwaacha wauaji hawa
waendelee kutamba na kuwafanya
muishi kwa hofu kana kwamba
hakuna vyombo vya kuwasaidia?
Tafadhali usikubali kuwaacha hivi
hivi.Pambana hadi haki ipatikane.
na wote waliohusika katika mauaji
haya watiwe nguvuni.Kama
usipowapata watu waliofanya
mauaji haya basi hata wewe
hautakuwa na amani na bado
utaendelea kuwa
hatarini.Wakifahamu umerudi
lazima watakusaka na
kukuua.Usihofu kama kuna
mambo yataibuka yanayowahusu wazazi wako kama wanahusika
kwa namna yoyote na
kusababisha vifo hivyo lazima nao
wapate haki yao.Hili ni jambo
gumu sana kwa wengi lakini mimi
ushauri wangu kwako ni huo dada
yangu ila kama unaona hakuna
ulazima wa kutafuta haki na
kuwaacha wauaji hao waendelee
kutamba basi hakuna haja ya
kufanya uchunguzi lakini kama
unataka kuufahamu ukweli na
kuwajua wauaji ili na wewe
uendelee kuwa salama kubali
nikusaidie na ukweli uwekwe
bayana.Piga moyo konde fumba
macho na uitafute haki hata kama
itakubidi kuwaigiza wazazi wako
katika matatizo lakini kama
wanahusika kwa namna moja au nyingine sheria lazima ichukue
nafasi.Hii ni kutafuta haki kwa
wale waliouawa bila hatia"
akasema Patricia
"I'm confused Patricia and I
dont know what to do.Ninataka
sana kuwafahamu wauaji hawa na
kuona haki ikitendeka lakini kwa
upande mwingine ninahofia
kuhusu familia yangu.Ninaweza
kuwaingiza katika matatizo
makubwa kitu ambacho sitaki
kukifanya"
"Unahisi ni mambo gani
mabaya ambayo wazazi wako
wanashiriki usiyotaka yajulikane
?Patricia akauliza
"I'm not sure yet but I know
they are doing dirty
businesses.Godson aliuawa baada ya kuanza kushiriki katika
biashara za familia.Alikuwa na
kazi yake nzuri sana na yenye
mshahara mkubwa ila wazazi
wakamshauri aachane na kazi
hiyo ili asimamie miradi ya familia
na ndipo alipouawa kikatili.Siku
kadhaa kabla ya kifo chake aliwahi
kunieleza kwamba kwa namna
yoyote ile nisithubutu kujiingiza
katika miradi ya
familia.Hakunifafanulia kwa kina
kwa nini aliniambia vile ila
ninaamini kuna mambo aliyaona
na ndiyo maana akanitaka
nisijihusishe kabisa katika
biashara zile"akasema Juliana
"Juliana mapema uliniambia
kwamba mpaka sasa bado
hujapata mbadala wa mpenzi wako Jose.Ulimpenda kwa dhati
ya moyo wako.Kama kweli
unampenda kiasi hicho ni wakati
sasa wa kupambana kwa ajili yake
na mdogo wako Godson.Ni wakati
wa kuhakikisha haki
inapatikana.Pambana kwa ajili
yao.Elvis amenifundisha jambo
kubwa sana siku zote unapaswa
kupambana kwa ajili ya yule
unayempenda.Elvis aliwahi
kudiriki hata kukorofishana na
mama yake mzazi kwa sababu
yangu. Wewe pia unapaswa
kupambana kwa ajili ya wale
uwapendao ambao walinyimwa
haki yao ya kuishi na hivyo
kukunyima wewe furaha ya
maisha yako.Kama Jose
asingeuawa hivi sasa ungekuwa na furaha na amani wala
usingeikimbia nchi.Unapombana
kwa ajili ya haki unapaswa
kufumba macho na kuhakiksha
wale wote waliohusika wanatiwa
nguvuni hata kama ni watu wa
muhimu kwako."akasema
Patricia.Juliana akainuka
akazunguka zunguka mle
chumbani na baada ya dakika tano
akaketi
"Patricia umeniambia
maneno mazito sana leo hii na
macho yangu yamefumbuka,ule
woga umekwisha.Naomba
unikutanishe na huyo mtu
unayesema anaweza akanisaidia"
akasema Juliana
"Are you sure ?Patricia
akauliza Yes.I want to find
justice.Siwezi kuliacha jambo hili
likaishia hewani.Potelea mbali
litakalotokea"
"Vizuri.Kesho ni jumamosi
siku ya mapumziko nitampigia
simu mzee Meshack asubuhi na
kumuomba tuonane na
nitamuomba tukutane naye”
akasema Patricia
"Ahsante sana Patricia.Sasa
ngoja nikuache ulale tutaonana
hiyo asubuhi" akasema Juliana na
kuondoka akaelekea chumbani
kwake
"Aliyoyasema Patricia ni
mambo ya kweli kabisa.Ni wakati
sasa wa kuutafuta ukweli wa nani
aliwaua mpenzi wangu Joseph na
mdogo wangu Godson.Nilifikiria muda mrefu kulichunguza suala
hili nikaogopa,nashukuru Patricia
amenipa moyo na sasa nataka
kuwafahamu wauaji waliomuua
Godson na Jose.Mama hatafurahi
akilifahamu jambo hili lakini sina
namna nyingine ya kufanya lazima
niwajue watu hao ni akina nani
kwani hata mimi walitaka
kuniua.Kama si wazazi
kunikimbiza nje ya nchi lazima na
mimi wangekwisha niua.Halafu
nimekumbuka jambo huu ni
wakati pia wa kufahamu mambo
ambayo mama anayafanya
.Ninaamini kuna mambo haramu
anayafanya ila ni hodari sana wa
kuyaficha hivyo ni wakati wa
kufanya uchunguzi na
kuyajua.Amekiri mwenyewe kwamba ni kweli kuna mambo
haramu anayafanya kakini
hakutaka kuniweka wazi.Ni
wakati wa kumuondoa katika
biashara hizo haramu.Nililazimika
kumkubalia yote aliyoniambia
likiwamo la eti kutaka kunichagua
kuwa waziri wa maliasili na
utalii.Siwezi kukubali uteuzi kama
huu utakaofanywa na genge lao ili
wanitumie katika mambo yao
haramu" akawaza Juliana.


*****************


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom