HaMachiach
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 3,417
- 6,149
- Thread starter
- #921
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Imekwisha poteza ladha mkuu..ngoja tuamie upande wa pili mana huku magumashi sana.tantalilaaaaa nyiiingi sana.kulubule Mungu anakuona
Hama uwasalimieImekwisha poteza ladha mkuu..ngoja tuamie upande wa pili mana huku magumashi sana.tantalilaaaaa nyiiingi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Episode mbili bado unaona magumashiImekwisha poteza ladha mkuu..ngoja tuamie upande wa pili mana huku magumashi sana.tantalilaaaaa nyiiingi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
kuwa na moyo wa shukuraniImekwisha poteza ladha mkuu..ngoja tuamie upande wa pili mana huku magumashi sana.tantalilaaaaa nyiiingi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 66
Vicky alitoka chumbani kwake
baada mlango wa sebuleni kugongwa
akaenda kuufungua akakutana na
mlinzi
"Kuna watu wanakuuliza
mama"akasema yule mlinzi
"Waruhusu waingie
ndani"akasema Vicky na mlinzi yule
akaenda kuwafungulia geti wakaingia
ndani.Kutoka ndani ya gari wakashuka
watu wanne wakiongozwa na
Obi.Vicky akahisi woga
"Hallo Vicky.Tumekutana
tena.Uko tayari?akauliza Obi
"Mnanipeleka wapi?
"Unakotakiwa kwenda.Kama uko
tayari ingia garini tuondoke" akasema Obi na Vicky akaongozana nao hadi
katika gari lao akaingia na
kuondoka.Mara tu walipovuka geti Obi
ambaye alikuwa amekaa kiti cha
nyuma pamoja na Vicky akamuomba
kijana aliyekuwa amekaa mbele
ampatie vifaa vyake
"Mnataka kunifanya nini?
akauliza Vicky kwa wasi wasi
"Relax Vicky.This is just a
procedure.Hutakiwi kufahamu mahala
unakoelekea hivyo naomba usiwe
mbishi" akasema Obi na kutoa sindano
katika mkoba ule akavuta dawa fulani
katika kichupa na kumchoma Vicky
katika .Hazikuisha sekunde thelathini
Vicky akalala usingizi mzit😵bi
akatoa simu na kumpigia Frank
"Mkuu tayari tunaye Vicky"
"Good.Fanyeni kama
nilivyowaelekeza hakikisheni
mnachukua kila aina ya tahadhari kwani watu wanaomtumia wana
mbinu nyingi"akasema Frank
"Tuko makini sana.Tutakujulisha
tukifika" akasema Obi na kukata
simu.Walikuwa makini sana katika
kuangalia kama kuna mtu yeyote
aliyekuwa anawafuata
nyuma.Walikwenda hadi katika
nyumba moja maeneo ya Mijiwe na
kuingia ndani.Haraka haraka Vicky
akashushwa na kupakiwa katika gari
lingine ambalo lilipita katika geti la
nyuma na kupita katika njia
iliyokuwemo shambani halafu
wakatokea katika barabara kubwa
wakaendelea na safari
"Kama walikuwa wanatufuatilia
kwa namna yoyote ile hapa
tumewalamba chenga ya mwili"
akasema Obi huku akicheka.
Waliendelea na safari hadi katika
nyumba ambayo Winnie aliletwa usiku wa jana wakaingia na Vicky
akapelekwa katika chumba akafungwa
pingu miguu na mikono kisha
akamchoma sindano nyingine na
wakaamuacha azinduke.Obi
akamjulisha Frank kuwa tayari
wamekwishamfikisha Vicky sehemu
husika
"Good Job Obi.Sasa jipeni muda
wa kuchunguza kama hakuna yeyote
anayemfuatilia mimi niko njiani
ninakuja hapo"akasema Frank
******************
Jina mtaa wa viwanda lilitokana
na eneo hilo kutengwa maalum kwa
ajili ya viwanda.Kulikuwa na viwanda
vikubwa zaidi ya kumi vinavyofanya
kazi na vingine vikiwa katika hatua mbali mbali za ujenzi.Kulikuwa na
majengo makubwa makubwa na
mengine yalizungushiwa ukuta
mkubwa.Steve aliendesha gari
taratibu huku Elvis akitumia
programu ile katika kompyuta
kutafuta mahala alipo Winnie.
"Ni maeneo haya hapa" akasema
Elvis baada ya kufika katika eneo la
kilichokuwa kiwanda cha saruji
ambacho kwa sasa hakifanyi
kazi.Mwekezaji wa kiwanda hiki
alishindwa kukiendeleza
akakitelekeza na kung'oa mashine
zote muhimu na kubaki magofu.Elvis
na Steve wakashuka garini na
kuangaza angaza.Watu waliokuwa
njiani hawakuwa wengi kutokana na
muda huo wengi kuwa makazini.
"Programu inatuonyesha ni eneo
hili la kushoto ambako kuna hiki
kiwanda cha saruji" akasema Elvis Ukuta uliozunguka kiwanda hiki
ulibomoka bomoka na hivyo
kupafanya kuwa ni sehemu ambayo
vijana hupenda kujificha na kuvuta
bangi.Doria za mara kwa mara za
polisi ndizo ziliowakimbiza vijana hao
eneo hili na kuondoa kitisho
kilichokabili raia hasa wafanyakazi
waliokuwa wanafanya kazi katika
viwanda vilivyoko eneo hili
waliokuwa wakiporwa fedha na mali
zao kila uchao.
Steve na Elvis wakaambaa na
ukuta wakakuta sehemu iliyoanguka
wakaingia ndani.Walitembea kwa
tahadari kubwa wakipita majengo
kadhaa yaliyotelekezwa bila kukutana
na mtu yeyote na mara wakatokea
katika jengo kubwa la ghorofa moja
ambalo lilionekana kama awali
lilitumika kama ofisi ingawa kwa sasa
hakukuwa na madirisha wala milango.Lilibaki gofu.Steve aliyekuwa
ametangulia mbele akasimama na
kumsukuma Elvis arejee nyuma
"Kuna nini? akauliza Elvis
"Kuna mtu amejificha pembeni
ya lile jengo anavuta sigara" akasema
Steve
"Good.Zunguka kwa nyuma mimi
nitamuwahi kwa mbele" akasema
Elvis na Steve akanyata akapita
pembeni ya mtambo mmoja mkubwa
uliotelekezwa pembeni ya jengo lile
bila kuonekana akazunguka nyuma ya
lile jengo akaruka dirisha na kuingia
ndani akaanza kupanda ngazi
kuelekea juu alikokuwa yule jamaa
akivuta sigara.Elvis akamuona Steve
akipanda ngazi taratbu naye akaiweka
sawa bastora yake iliyofungwa
kiwambo cha kuzuia sauti.Yule jamaa
alikuwa ameegemea ukuta akivuta
sigara akionekana kujisahau kabisa.Mara akastuliwa na sauti ya
kitu kama jiwe lililoanguka nyuma
yake.Akaitupa sigara na haraka
akageuka nyuma kutazama kuna nini
lakini hakuona chochote
"Peter ! akaita lakini
hakujibiwa.Haraka haraka akatumia
ngazi zilizokuwa nje akaanza kushuka
haraka haraka lakini kabla hajafika
cini akatokea Elvis na kumtaka
asimame alipo.Yule jamaa kwa woga
akageuka na kutaka kurudi juu lakini
akakutana na Steve akiwa na
bastora.Kwa ujasiri na wepesi wa aina
yake akaitoa bastora kwa lengo la
kupambana na akina Steve lakini Elvis
tayari alikwisha kiona kitendo kile na
hakumpa nafasi kwani kwa shabaha
ya aina yake akaupiga risasi mbili
mkono ule uliokuwa umeshika
bastora akaanguka chini.Steve
akamuwahi na kumvuta juu akamuingiza ndani.Elvis akaangaza
kila upande na hakuona mtu
yeyote.Akapanda ngazi haraka haraka
akamfuata Steve kule juu
"Tuambie wewe ni nani na
unafanya nini hapa? akauliza Steve
"Jamani naombeni msiniue.."
"Hatutakuua kama utatueleza
wewe ni nani na unafanya nini hapa?
akauliza Elvis lakini yule jamaa
hakujibu kitu alikuwa anagugumia
kwa maumivu huku damu nyingi
ikiendelea kutoka katika jeraha.
Elvis akamkanyaga katika jeraha
la yule jamaa ambaye alipiga ukelele
mkubwa wa maumivu.
"Beka !! ikasikika sauti ikiita.Elvis
akamuinamia yule jamaa
"Huyo ni nani anakuita?akauliza
kwa sauti ndogo
"Ni mwenzangu tuko naye hapa"
akajibu yule jamaa Muite aje hapa haraka sana
lakini usimueleze kama tuko hapa"
akasema Elvis na kumnyooshea
bastora.
"Peter njoo huku! akasema yule
jamaa kwa sauti iliyojaa
maumivu.Steve na Elvis wakajificha na
mara Peter akaingia mle ndani
"Peter kimbiaaaaa!!! akasema
Beka na Peter akataka kugeuka
akimbie lakini Steve akacheza vizuri
na bastora yake na kumpiga risasi
mbili za mgongo akaanguka
chini,akamuwahi na kuichukua
bastora yake.Akamgeuza akamtazama
lakini alikuwa katika dakika zake za
mwisho.
"Can he make it? Elvis akauliza
"No he won't" akasema Steve
"Mwenzako roho yake
inachukuliwa na ziraili muda huu
nawe utamfuata muda si mrefu endapo hautatueleza ninyi ni akina
nani na mnafanya nini hapa?Kwa nini
mna silaha?
"Msiniue jamani.Sisi tuko hapa
tumepewa kazi ya kufanya"
"Kazi gani na nani kawapa kazi
hiyo?
"Kuna mtu tunamlinda
hapa.Tumepewa kazi na Obi"
"Yuko wapi huyo mtu
mnayemlinda?Kafanya nini?akauliza
Steve
"Ni msichana na hatujui kafanya
nini.Sisi tumepewa kazi ya
kumlinda.Obi ndiye anayefahamu
kafanya nini"
"Inuka haraka tupeleke mahala
alipo huyo msichana" akasema Elvis
na Steve akamshika mkono
akamuinua yule jamaa ambaye
akawapeleka katika chumba
walimomfungia mtu ambaye walikuwa wanamlinda.Msichana
mmoja aliyechafuka damu akiwa
ameinamisha kichwa alikuwa
amefungwa kamba katika
kiti.Haikuhitaji nguvu kubwa
kugundua kwamba yule msichana
alikuwa ameteswa sana
"Winnie !! akaita Elvis na kwa
taabu Winnie akainua kichwa.Hakuwa
na nguvu kabisa.Elvis akamgeukia
yule jamaa na kumtandika ngumi
iliyompeleka hadi chini.
"Mnawezaje kufanya ukatili huu
kwa msichana huyu asiye na kosa
lolote? akasema kwa ukali Elvis na
Steve akaanza kumfungua Winnie
kamba alizofungwa
"Nisaidieni jamani mnipeleke
hospitali."akalia yule jamaa ambaye
jeraha lake liliendelea kutoa damu.
"Elvis !! akasema Winnie kwa
sauti dhaifu baada ya kufunguliwa Winnie you'll be fine" akasema
Elvis na kumuinua Winnie akaanza
kushuka naye chini.
"Jamani nitakufa nipelekeni
hospitali" akalia yule jamaa.Steve
akamtazama kwa hasira na kuchomoa
bastora yake
"You'll go to hospital in hell!!
akasema na kuachia risasi nne na
kuuondoa uhai wa yule jamaa
"Hizi ni salamu kwa hao
wanaowatuma mpambane na watu
msiowafahamu" akasema na kushuka
ngazi haraka haraka kumfuata Elvis
"Umemuacha yule jamaa?
"I killed him"
"Good" akasema Elvis
wakitembea haraka haraka hadi
walipofika katika gari lao .Kulikuwa
na watu wachache wakipita
barabarani lakini hawakuwajali wakampakia Winnie na kuondoka
eneo lile
"Wamemtesa sana"akasema
Steve
"Winnie hakupaswa kupitia haya
yote aliyoyapitia.Mateso haya ni
makubwa sana kwake.Hakustahili"
akasema Elvis
"Naamini kwa haya yaliyomkuta
atakuwa amejifunza akiambiwa
asifanye kitu fulani basi atii.Kama
angesikia tuliyomweleza
yasingemkuta haya yaliyomkuta.Nini
kinafuata baada ya hapa? akauliza
Steve
"Kwa sasa tumshughulikie
Winnie hali yake iboreke halafu
tusubiri taarifa kutoka kwa
Omola"akasema Elvis na kumpigia
simu Dr Philip akamuelekeza mahala
walikohamia na kumtaka afike haraka
sana *****************
Samira na Omola waliwasili
ikulu na hawakupata taabu katika
kuingia kwani taarifa za kuwasili kwa
Omola tayari zilikuwepo.Wasaidizi wa
rais wakamjulisha Omola kwamba rais
hataweza kuonana naye kwa muda ule
kwani alikuwa katika kikao muhimu
hivyo alitoa maelekezo kwamba
atakapofika apelekwe moja kwa moja
kwa makamu wa rais ambaye tayari
amekwisha zungumza naye.Omola na
wasaidizi wale wa rais wakaelekea
moja kwa moja hadi katika ofisi ya
makamu wa rais ambako ilimlazimu
Omola kusubiri kwani tayari makamu
wa rais alikuwa na mazungumzo na
watendaji kadhaa wa ofisi yake.Saa
nne na nusu ndipo makamu wa rais
alipomaliza mazungumzo na watendaji wake na akataarifiwa
kwamba Omola tayari amekwisha
wasili akaelekeza aingie ofisini kwake.
"Karibu sana" akasema makamu
wa rais akimkaribisha Omola.Uso wa
Dr Shafi ulionyesha tabasamu baada
ya kumuona mrembo yule ambaye
kwa wajihi alioutengeneza alionekana
kweli mwandishi wa habari
"Nashukuru sana mheshimiwa
makamu wa rais"akajibu Omola
"Naitwa Omola Otola ni
mwandishi wa habari za
mazingira.Ninafanya kazi na shirika
lisilo la kiserikali ambalo kazi yake ni
kutunza na kuhifadhi mazingira.Katika
shirika letu kuna kitengo cha habari za
mazingira na tuna jarida la mazingira
litokalo kila mwezi hivyo tunazunguka
sehemu mbalimbali duniani kutafuta
habari za mazingira na kuziandika
katika jarida letu.Kikubwa tunachoangalia katika nchi
tunazozitembelea ni namna
wanavyotunza na kuhifadhi
mazingira.Ni mara ya kwanza tunafika
Tanzania kuandika habari za
mazingira.Katika Afrika ni nchi ya
kwanza kuitembelea na tumeamua
kuandika habari za Tanzania katika
jarida letu kwa sababu ni nchi
inayokua kwa kasi kiuchumi.Takwimu
zinaonyesha kuwa kumekuwa na
ongezeko kubwa la shughuli mbali
mbali za kiuchumi hususan viwanda
na katika shughuli hizi za kiuchumi
uchafuzi wa mazingira hauwezi
kukosekana hivyo ni muhimu kujua
namna serikali ya Tanzania
inavyokabiliana na suala la uchafuzi
wa mazingira,namna inavyotunza
mazingira ya fukwe,namna
inavyotunza na kuhifadhi misitu na
vyanzo vya maji.Kwa ujumla tunataka
kufahamuu mazingira kwa upana
wake hapa Tanzania" akasema Omola
"Omola ninashukuru sana
kukufahamu.Mheshimiwa rais
amenipigia simu na kuniueleza
kwamba utakuja kuonana nami hivyo
nikupe ushirikiano.Ni kweli ofisi
yangu ndiyo inayoshughulika na
masuala yote ya mazingira na
nitakueleza kwa upana wake
kuhusiana na mazingira kwa
ujumla.Utaniwia radhi kwani kwa sasa
ninahitaji kupata mapumziko kidogo
halafu tutapata wasaa wa
kuzungumza utaniuliza maswali na
mimi nitakujibu na nitakuelekeza pia
kwa watu wangu wanaohusika na
mazingira na utapata mambo mengi
kupitia kwao.Kama hutojali naomba
tuongozane kupata chai" akasema
makamu wa rais na Omola hakujivunga akakubali wakaongozana
na Dr Shafi kupata chai.
"Karibu sana Tanzania Omola.Ni
mara yako ya kwanza kufika
Tanzania?akauliza Dr Shafi
"Ndiyo mheshimiwa makamu wa
rais.Ni mara yangu ya kwanza kufika
Tanzania.Ni nchi nzuri
nimeipenda.Nimekuwa nikizisikia sifa
zake kwa muda mrefu na leo
nimefurahi kuwa hapa.Nimekutana na
watu wakarimu sana kama vile
nilivyokuwa nikisikia kwamba
waTanzania ni watu wakarimu
mno.Kikubwa kilichonifurahisha ni
namna serikali ya Tanzania
inavyojitahidi kuupaisha uchumi
wake.Hatua zinazochukuliwa na
serikali ya Tanzania katika kuinua
uchumi zinazaa matunda na sasa
uchumi wa Tanzania ni moja ya chumi
za mfano barani Afrika na duniani kwa ukuaji wake wa kasi"akasema Omola
na Dr Shafi akatabasamu
"Ni kweli Omola,uchumi wa
Tanzania unakua kwa kasi kubwa
sana kwani hii ni mipango ya serikai
kwamba kabla ya kufika 2025
Tanzania iwe imeingia katika uchumi
wa kati na kwa namna uchumi
unavyoendelea tunaamini tutafika
lengo hilo" akasema Dr Shafi
wakaendelea na mazungumzo
mengine na wakati wakiendelea
kupata chai makamu wa rais
akafuatwa na kujulishwa kwamba
kuna waziri amekuja anahitaji
kuzungumza naye.Dr Shafi akamtaka
radhi Omola kwamba amepatwa na
dharura na akamuomba aendelee
kumsubiri amalize mazunumzo yake
na waziri aliyemtembelea.Baada ya Dr
Shafi kuondoka Omola akapata nafasi
na kumpigia simu Elvis Omola mambo yanakwendaje
huko? akauliza Elvis baada ya kupokea
simu
"Tayari nimeonana na makamu
wa rais na muda mfupi uliopita
nimekuwa naye ila hatujafanya
mazungumzo yoyote amepata dharura
kuna waziri amekuja ana
mazungumzo naye ila akimaliza
tutazungumza"
"Vipi kuhusiana na ile taarifa ile
kuhusiana na kampuni ya McLorien
ambayo uliahidiwa kuipata leo?
akauliza Elvis
"Oh! Ahsante kwa
kunikumbusha.Nipe muda kidogo
niwasiliane na mtu wangu kama ana
taarifa zozote amezipata kuhusu hiyo
kampuni"akasema Omola na kukata
simu akachukua kijitabu kidogo
kutoka katika mkoba wake akazitafuta
namna fulani nakupiga akazungumza kwa dakika moja na kukata simu
halafu akampigia Elvis
"Elvis mtu wangu amenijulisha
kwamba tayari amekwisha nitumia
taarifa katika barua pepe
yangu.Nitakapokuja jioni tutaifungua
tujue nini amekipata kuhusiana na
kampuni hiyo ya McLorien"
"Sawa Omola.kazi njema.Kama
kuna msaada wowote unauhiaji
nijulishe tafadhali" akasema Elvis
akaagana na Omola na kukata simu na
Omola akaendelea kumsubiri makamu
wa rais hadi alipomaliza kikao na
waziri kisha akamuita Omola ofisini
kwake wakaanza
mazungumzo.Makamu wa raia
akampa Omola muhtasari wa hali ya
mazingira ulivyo hapa nchini na
akamueleza namna
wanavyoshughulikia suala la uharibifu
wa mazingira.Ulikuwa ni muhtsari mrefu na wakati akiendelea Omola
akaomba samahani kwani kifaa kile
kidogo alichokuwa anakitumia
kurekodia kilionyesha
kujaa.Akafungua mkoba wake na
kukiminya kichupa kidogo mithili ya
kichupa cha uturi halafu akachukua
kifaa kingine cha kurekodia
akakiweka mezani akaendelea
kumrekodi makamu wa rais.Sekunde
chache makamu wa rais akaanza
kupiga chafya.
"Oh sorry" akasema Dr Shafi na
kutoa kitambaa mfukoni
"Tunaweza kuendelea" akasema
lakini ghafla akaanza tena kupiga
chafya mfululizo
"Excuse me" akasema na kuinuka
akaelekea katika mlango mdogo
ulioonekana kama maliwato.Kwa
muda wote ambao alikuwa amekaa na
makamu wa rais aliweza kumsoma vizuri na kugundua kwamba alikuwa
anatumia kalamu nyekundu ambayo
aliitoa katika mfuko wake wa koti.Kwa
kasi ya ajabu akafungua mkoba wake
na kutoa kitu fulani kidogo na
kukiweka ndani ya kalamu ile
aliyokuwa anaitumia makamu wa rais
halafu akatoa kitu fulani kama kichupa
cha dawa akakiweka puani kama vile
anavuta hewa ya kile kilichokuwamo
ndani ya ile chupa kisha akatoa tena
kichupa kile mithili ya kichupa cha
uturi na kukipuliza karibu na meza ya
makamu wa rais.Baada ya muda
kidogo makamu wa rais akarejea
"Samahani sana
Omola.Nimepatwa na hii chafya ya
ghafla" akasema makamu wa rais na
,mara tu alipoketi akaanza tena kupiga
chafya mfululizo.
"Pole sana mheshimiwa makamu
wa rais"akasema Omola Usijali Omola.Naomba samahani
sana kwa hali hii iliyonitokea"
akasema makamu wa rais na kuinuka
akaingia tena maliwat😵mola akaiona
mezani simu ya mkononi akaichukua
na kuifungua akatoa kadi ndogo ya
kuhifadhia kumbu kumbu
iliyokuwamo na kuingiza kadi yake
halafu akabonyeza namba kadhaa na
programu fulani ikaingia katika ile
simu ya makamu wa rais.Haraka
haraka akaitoa ile kadi yake na
kuirejesha ile ya makamu wa rais na
kuiweka simu mahala
ilipokuwa.Kitendo kile kilichukua
muda mfupi sana.Sekunde chache tu
baada ya kuirejesha simu,mlango
ukafunguliwa na makamu wa rais
akarejea.
"Omola utanisamehe sana
ninaona hali yangu imebadilika ghafla
hivyo ninahitaji kuonana na daktari wangu mapema.Nadhani itakuwa
vyema kama tukiendelea na
mazungumzo zaidi kesho"
"Sawa mhesimiwa,nitakuja tena
kesho.Pole sana" akasema Omola na
kutoka.Bado Samira alikuwa garini
akimsubiri wakaondoka
*******************
Frank aliwasili katika nyumba
alikopelekwa Vicky,akawakuta vijana
wa Obi wakiwa wameimarisha ulinzi
"Kazi nzuri Obi.Mna hakika
hakuna yeyote aliyekuwa
anawafuatilia?akauliza Frank
"Hapana mkuu hakuna yeyote
aliyetufuatilia"
"Are you sure Obi? akauliza
Frank Ndiyo mkuu.Tumechukua kila
aina ya tahadhari hadi kufika
hapa.Nimewatuma vijana wamefanya
uchunguzi wa eneo lote kuzunguka
hapa hakuna hatari yoyote"
"Vipi kuhusu Vicky,
mmemchunguza hajafungwa kifaa
chochote cha kurekodi mazungumzo?
akauliza Frank
"Hana kifaa chochote
tumemfanyia uchunguzi wa kutosha"
"Good.Where is she?akauliza
Frank na Obi akampeleka katika
chumba alimokuwamo Vicky.Mlango
ukafunguliwa na taa ikawashwa Vicky
tayari alikwisha zinduka.
"Hallow Vicky.Dunia imekuwa
ndogo sana hatimaye tumeonana
tena" akasema Frank huku
akitabasamu
"Winnie yuko wapi? Not so fast pretty
lady.Tunakwenda taratibu hatua kwa
hatua.Mimi nawe tuna mazungumzo
marefu sana siku ya leo" akasema
Frank na kumuita Obi akamtaka
amfungue Vicky pingu alizokuwa
amefungwa.
"Samahani sana Vcky kwa
kukuleta hapa kwa staili hii lakini
imenibid kufanya hivi kwa ajili ya
tahadhari"
"I'm so dissapointed with you
Frank.Kwa nini umenifanyia hivi?Kwa
nini ukamtuma huyu mtu wako kuja
kututeka?Kwa nini umemteka mdogo
wangu na kumpa mateso? Nijibu
Frank kwa nini umenifanyia
haya?Dont you trust me
anymore?akasema Vicky huku
akilengwa na machozi
"Ninakuamini Vicky lakini kwa
mambo yaliyotokea ndani ya siku mbili hizi nimepata mkanganyiko na
sina hakika kama nitakuamini tena"
akasema Frank
"Kitu gani kinakufanya
usiniamini?
"Ninataka unishawishi nikuamini
tena.Nataka unieleze kwa nini
ulimuua Pascal?Nimeumia sana kujua
kamba umeshiriki katika kifo
chake.Tuanzie hapo nieleze kitu gani
kimekufanya umuue Pascal? akauliza
Frank na macho yake yakaanza
kubadilika na kujaa ukatili
"Una hakika ni mimi ndiye
niliyemuua Pascal?Kwa nini
unanihusisha na jambo kama
hili?Mimi ninawezaje kumuua mtu
wangu wa karibu?Wewe na Pascal ni
watu wangu wa karibu na hata mimi
nimeumizwa vile vile na kifo
chake.Tafadhali nakuomba
usinihusishe na jambo kama hilo.Mimi si muuaji.Nilikubali kumuua kanali
Norman kutokana na fedha nzuri
aliiniahidi Deus lakini mimi si
muuaji.I'm not a kiler" akasema
Vicky.Frank akainuka na kumsogelea
"Vicky tell me the trust.Kwa nini
ulimuua Pascal?
"Frank please I'm not a killer"
akasema Vicky
"C'mon Vicky tell me the truth
why you killed him? Who sent you to
kill him?akauliza Frank huku akipiga
kitanda kwa mikono,tayari hasira
zilianza kumpanda
"Frank mambo haya yote
umeyatoa wapi?Aliyekwambia
kwamba mimi nimemuua Pascal
amekudananya.Siwezi kufanya jambo
kama hilo.I'm not a killer like you"
akasema Vicky.Frank akamtazama
kwa hasira Vicky naomba unisikilize
vyema.Frank huyu unayezungumza
naye hapa si Frank yule ambaye
umemzoea.I'm real Frank the killer!
Hivyo nakupa angalizo kuwa makini
sana unapozungumza nami.Nipe
majibu ya maswali yangu
ninayokuuliza or else I'll destroy
you.Dont force me to do that. I'm
asking again why you killed Pascal and
who sent you?
"Frank nimekwisha kueleza
kwamba sihusiki na jambo
hilo.Naomba unieleze kwa nini
unamshikilia mdogo wangu?Where is
she?
"Vicky please I dont want to
destroy you my dear.Tell me the trut.I
swear I'll understand and let you
go.Ninaamini huwezi kufanya jambo
kama hili wewe mwenyewe lazima
kuna mtu amekutuma na huyo ndiye ninayetaka kumjua.Huyo ndiye
ninayemuhitaji" akasema Frank
"Frank nakuomba tusiendelee
kupoteza muda wakati unafahamu
fika kwamba sijahusika na siwezi
kujihusisha na jambo kama
hilo.Naomba usiyachoshe masikio
yangu kwa jambo hilo.Nataka nimone
Winnie" akasema Vicky
"C'mon Vicky.Usitake kulifanya
suala hili likawa gumu zaidi .Tell me
the truth!! akafoka Frank
"There is no truth!! Vicky naye
akafoka.Frank akamtazama kwa
hasira halafu akasema
"Nisikilize vyema.Usijidanganye
kwamba sifahamu
ulichokianya.Ninajua kila kitu.Tayari
nimefuatilia na nimegundua wewe
ndiye uliyempigia simu Pascal
ukamuita aje kule hotelini na huko
ukamuua.Nani alikutuma ufanye hivyo? akauliza Frank.Maneno yale ya
Frank yakamstua Vicky lakini
akajikaza ili Frank asigundue.
"Thats not true.Sijawasiliana na
Pascal kabla ya kifo chake" akasema
Vicky na kuzidi kumpamdisha hasira
Frank akamnasa kofi kali
"Yes you called him !!!akafoka
Frank
"If you don't tell me the trruth I
swear I'm going to destroy you and
Winnie!!
Vicky aliyekuwa ameanguka
kitandani kufuatia kofi kali la Frank
akainuka aliposikia jina Winnie
likitajwa
"Dont dare touch her!!! akasema
Vicky
"Kama hutanieleza ukweli nani
alikutuma umuue pascal nitamuua
Winnie tena mbele ya macho yako.Ninakupa nafasi ya mwisho
.Niambie ukweli !!
"Frank tafadhali nakuonya
usimguse mdogo wangu.Cheza na
mimi utakavyo lakini si
Winnie.Uliyekuwa unanitafuta ni mimi
na si Winnie.Yeye hahusiani kwa
lolote na wewe ndiyo maana
nimejileta kwako ili umuachie
Winnie.Please let her go!! akasema
Vicky
"Uhai wa Winnie uko mikononi
mwako.Wewe ndiye utakayeamua
kumuua au kumuacha hai.Kama
utanieleza ukweli Winnie ataendelea
kuwa hai lakini kama utanificha
nitaanza kwanza kumtoa uhai Winnie
na wewe utafuata tena kwa mateso
makali mno"
"Ni ukweli upi unautaka Frank? Tell me everything.Niambie nani
kakutuma umuue Pascal?Nani
unashirikiana nao?
"Nimekwisha kwambia hakuna
mtu yeyote aliyenituma na wala
ninayeshirikiana naye"
"Where is Elvis?!!! akauliza Frank
kwa ukali
"Elvis?!! Vicky akashangaa
"Ni nani huyo Elvis?akauliza
"Usijifanye humjui Elvis.Yule
jamaa aliyekufuata akaanza
kukuchunguza kuhusiana na kifo cha
kanali Norman"
"That man is dead!.Isn't he? Tena
wewe mwenyewe ndiye uliyeniambia
kwamba mmemuua sasa iweje
uniulize yuko wapi wakati unafahamu
mahala alipo?akauliza Vicky
"Vicky unajifanya mjanja sana
siyo?Kwa taarifa yako tayari Winnie
ametueleza kila kitu.Ametuelezakuhusu Elvis na mwenzake Steve
ambao waliwateka na kukulazimisha
uwaonyeshe mahala nilipo.Kwa nini
hutaki kunieleza ukweli kuwa ni wao
ndio waliokutumia ili kumpata
Pascal?Kwa nini unanificha jambo hilo
wakati tayari ninalifahamu?akauliza
Frank na Vicky akatoa kicheko
"Do you believe her?akauliza
"Winnie amekudanganya"
"Hapana
hajanidanganya.Alifahamu kwamba
ninakutafuta kwa ajili ya kufahamu
kwa nini ulishiriki katika mauaji ya
Pascal na akanieleza kwamba wewe
huhusiki bali ulilazimishwa kumuita
Pascal hotelini.Alinieleza kila kitu ili
niweze kukuacha huru kwani ana
wasiwasi wale jamaa wanaokushikilia
wanaweza wakakuua. Alinitaka
nikuokoe kutoka katika mikono ya hao
jamaa aliowataja kwa majina ya Elvis na Steve.Kama haitoshi alinieleza pia
kwamba katika nyumba hiyo
mliyokuwa mnashikiliwa yupo pia
mwanangu Graca ambaye alitoroshwa
na Elvis kutoka afrika ya
kusini.Nilimtaka akanionyeshe mahala
hapo mnaposhikiliwa tukaenda na
hatukukuta mtu yeyote.Ninataka
kuwafahamu hao jamaa ni akina
nani?Kwa nini
wananitafuta?Ninavyofahamu ni
kwamba Elvis aliyemtorosha Graca
kutoka Afrika kusini tayari amefariki
dunia nataka kujua ni Elvis yupi huyo
aliyekuwa anakushikilia?Ninahitaji
sana kuwafahamu hawa jamaa ni
akina nani na wako wapi.Sina shida
yoyote na wewe Vicky.Ninakuomba
tafadhali nieleze ukweli kuhusu hawa
jamaa ninawahitaji sana" akasema
Frank Frank narudia tena kukueleza
kwamba Winnie
amekudanganya.Nashangaa mambo
haya yote aliyokueleza ameyatoa
wapi.Hakuna mtu yeyote aliyetuteka
zaidi ya yule aliyekuja kutaka
kututeka nyumbani ambaye ninaamini
wewe ulimtuma ukiamini kwamba
nimehusika katika kumuua
Pascal.This is a big lie.Hakuna Elvis
wala Steve ninaowafahamu.It's a lie"
akasema Vicky
"Vicky tafadhali huu si wakati wa
utani.Nieleze ukweli tafadhali."
akasema Frank
"Ukweli upi unaouhitaji
Frank?Nimekueleza kila kitu kwamba
Winnie alikudanganya"
"Hapana.Hakunidanganya.Sina
mahusiano yoyote na Winnie na sina
hakika kama ananifahamu lakini
alinipigia simu akahitaji kuonana nami na tulipoonana akanieleza haya yote
akiomba nikusaidie kwani uko katika
matatizo" akasema Frank na
kumtazama Vicky kwa hasira halafu
akauliza
"Where were you last night?
"Last night? akauliza Vicky
"Ndiyo ulikuwa wapi?
"Hayo ni masuala yangu binafsi
ambayo hutakiwi
kuyafahamu"akasema Vicky
"I need to know Vicky.Kwa
mujibu wa Winnie uliwaahidi hao
jamaa kwamba utawapeleka mahala
ambako unaamini wanaweza kunipata
na jana usiku nikiwa katika nyumba
ambayo Winnie alinipeleka akidai
ndiko mlikokuwa mnashikiliwa
nikataarifiwa kwamba kuna watu
wamevamia katika nyumba yangu ya
shambani na wakaingia katika ofisi
yangu ninamohifadhi mambo yangu ya siri wakachukua kila walichoona
kina wafaa.Ninaamini waliofanya
hivyo ni hao jamaa waliokuwa
wanakushikilia na ninaamini wewe
ndiye uliyewapeleka huko kwani
uliwaahidi kufanya hivyo.Vicky
ninarudia tena kukuomba kwa mara
ya mwisho hawa watu ni akina nani na
wanataka nini kwangu?Ninataka
kujua huyo mtu anayeitwa Elvis ni
yupi?
"Frank sitaki kuendelea
kuzungumza tena masuala hayo
ambayo nimekwisha kueleza kwamba
si ya kweli.Tafadhali nionyeshe alipo
Winnie!!Let her go!! akasema Vicky
huku akihisi mwili unamtetemeka
kwa ndani.Frank akazidi kumtazama
kwa hasira
"Vicky sikutaka kukufanyia hivi
lakini umenilazimisha wewe
mwenyewe nikuharibu and I'll destroy you!! akasema na kutoka akamkuta
Obi amesimama nje ya mlango
"Obi huyu mwanamke bado
mgumu kusema chochote.Sikutaka
kumtesa lakini amenilazmisha
kufanya hivyo.Ninataka umfunge na
twende naye kule aliko mdogo
wake.Nitamtesa na atasema kila kitu
na hata ikibidi kumuua mdogo wake
nitafanya hivyo.Leo lazima niupate
ukweli!! akasema Frank na Obi
akaingia ndani ya kile chumba
akamfunga Vicky kitambaa
usoni,akamfunga pingu za mikono
akamtoa mle ndani na kumfungia
katika buti ya gari wakaondoka
kuelekea mahala walikomuacha
Winnie
****************Elvis na Steve walimpitia Dr
Philip mahala walikopanga wakutane
wakaelekea moja kwa moja katika
makazi yao mapya.Elvis akamueleza
kila kitu kilichotokea na mahala
walipofikia katika uchunguzi wao
"Poor girl.Ameingia katika
matatizo ambayo
hakuyategemea.Hakupaswa
kufanyiwa ukatili wa namna hii.Watu
hawa wana roho za kinyama
sana"akasema Dr Philip huku
akimuangalia Winnie namna
alivyochafuka kwa damu
"Ni watu makatili sana lakini siku
zao zinahesabika.Tayari tumepata
mwangaza mkubwa kuhusiana nao na
nina uhakika muda si mrefu sana
tutakuwa tumepata taarifa kamili za
kuhusiana na mtandao wao" akasema
Elvis na safari ikaendelea hadi
walipofika katika makazi yao.Haraka Winnie akashushwa na kuingizwa
ndani Dr Philip akaanza
kumuhudumia.Wakati Winnie
akiendelea kuhudumiwa Elvis
akamuita pembeni Graca
"Vicky hajarejea?akamuuliza
"Hapana hajarejea"akajibu Graca
na taarifa ile ikamshangaza sana
Elvis.Steve akatoka haraka kwenda
kununua mahitaji kwani hawakuwa
wamepitia sehemu yoyote wakiwahi
kumpatia huduma Winnie
"Vicky amekwenda wapi?Kwa
nini hakuaga tujue anakwenda wapi?
akajiuliza Elvis na kutolewa mawazoni
baada ya simu yake kuita.Mpigaji
alikuwa Omola
"Omola mambo
yanakwendaje?akauliza Elvis
"Mambo yanakwenda
vizuri.Tayari nimeondoka kwa
makamu wa rais na ninaelekea hotelini.Naomba aje mtu kunichukua"
akasema Omola na muda huo huo
Elvis akampigia simu Steve akamtaka
akamchukue Omola hotelini kwake.
"Anaendeleaje?Elvis akauliza
baada ya kuingia katika chumba alimo
Winnie
"Anaendelea vyema.Tumuache
apumzike na akiamka ataendelea
kutumia dawa za kumsaidia kutuliza
maumivu.Amepata michubuko kwa
nje lakini haionyeshi kama
ameumizwa kwa ndani hivyo dawa
hizi zitamsaidia" akasema Dr Philip na
kwa kuwa alimaliza kazi yake
aliyoitiwa akaagana na akina Elvis
akaondoka.Hakuwa amekuja na gari
hivyo ikamlazimu kutembea kwa
miguu kutafuta taksi.Wakati
akiwasubiri akina Omola,Elvis
akaenda kujipumzisha chumbani
kwake Vicky amekwenda wapi?Kwa
nini akaondoka kimya kimya bila
kuaga?Staili yake ya kuondoka inanipa
mashaka sana hata hivyo ngoja
tuendelee kumsubiri.Kingine
kinachoniumiza kichwa ni namna gani
akina Frank walivyoweza kumpata
Winnie?Amewaeleza mambo
gani?Atatueleza kila kitu
atakapoamka.Imekuwa ni jambo zuri
kumshirikisha Omola katika
operesheni hii kwani bila yeye
tusingeweza kumpata Winnie kwa
haraka namna hii..." Elvis akatolewa
mawazoni baada ya mlango wake
kufunguliwa akaingia Graca
"Elvis poleni sana na hongereni
kwa kufanikiwa kumpata Winnie"
akasema Graca na kukaa karibu na
Elvis
"Tumewahi kumpata kabla ya
wale jamaa hawajamuumiza sana" Vipi kuhusu zile nyaraka
tulizozipata jana ofisini kwa
baba,kuna maendeleo yoyote
yamepatikana?
"Nyaraka zile ni muhimu sana na
uchunguzi wake
unaendelea.Zimetusaidia tumepiga
hatua kubwa na tumepata mwangaza
kuhusiana na biashara hii ya
silaha.Tumefanikiwa kumpata Irene
mwabukusi ambaye nyaraka
zinaonyesha ndiye mmiliki wa
kampuni ya Pendeza Co.Ltd .Irene
amekiri kwamba kampuni ya Pendeza
ni kampuni ya Frank lakini yeye ndiye
msimamizi mkuu.Mizigo imekuwa
inatumwa kutoka kampuni ya
McLorien kuja katika kampuni ya
Pendeza na muagizaji mkuu wa mizigo
hiyo ni David.Ikifika Tanzania mizigo
hiyo hutolea bila kufanyiwa ukaguzi
na kisha David huipeleka mahala ambako hutoa silaha na kisha
hupeleka mali katika maduka
yake.Irene anadai kwamba Pendeza
Co.Ltd iko pia katika nchi za Congo na
Burundi.Tunahisi kuwa David
anatumia kampuni hii ya Pendeza
kupitishia mizigo ya silaha.Tunataka
tuichunguze pia kampuni ya McLorien
ambayo inaonekana ndiyo inayotuma
mizigo kwa kampuni ya
Pendeza.Tunamsubiri Omola ambaye
aliomba msaada kwa wenzake
wamsaidie kuichunguza kampuni hii
ya McLorien na tayari amekwisha
tumiwa majibu katika barua pepe
akifika ataifungua na tutajua nini
wamekipata kuhusiana na kampuni
hii.Graca mambo yanakwenda vizuri
usiwe na hofu tutahakikisha yeyote
anayejihusisha na mtandao huu
anafikishwa mbele ya sheria" Sina cha kusema
Elvis,ninawaombea wewe na wenzako
mfanikiwe katika suala hili ili na mimi
niweze kuwa huru kwani bila baba na
mtandao wake kumalizwa nitaendelea
kuishi maisha kama ya ndege ya
kujificha ficha.Lakini kwa kuwa niko
nawe karibu siogopi tena.Elvis
nakuomba usiivunje ahadi uliyonipa
kwani ukifanya hivyo utauvunja moyo
wangu vipande.Nimepitia mengi
magumu,nimepita katika giza nene na
sasa nimeanza kuona mwangaza
katika maisha yangu hivyo sihitaji
kuumizwa tena.Lizingatie hilo"
akasema Graca na kumbusu Elvis
akaelekea chumbani kwake
"Graca anasema kweli,amepitia
mengi magumu na hapaswi kuumizwa
tena na mimi nimekwisha muahidi
kwamba nitakuwa naye kimapenzi na
tayari amechanganyikiwa juu yangu.Nitafanya nini wakati bado
ninampenda Patricia?Ngoja niyaweke
pembeni masuala haya ya wanawake
nimalize kwanza masuala muhimu
kisha nitajua nini cha kufanya."
akawaza Elvis
"Nina uhakika mkubwa kwamba
Frank anaitumia kampuni hii ya
Pendeza kupitishia silaha.Ndani ya
makontena hayo yanayotumwa
ninaamini ndimo silaha hupakiwa na
ndiyo maana makontena hayo
hutolewa bila kufanyiwa ukaguzi
wowote ili kuficha kile kilichomo
ndani yake.Frank huyapeleka katika
shamba lake na kule hupakua silaha
na kisha huzisafirisha kwenda nchini
Congo.Tayari mwanga huo nimeupata
lakini bado nahitaji ushahidi
zaidi.Nahitaji kuwafahamu wote
waliomo katika mtandao huu"
akaendelea kuwaza Elvis ****************
Frank na Obi wakiwa na vijana
wao wakawasili eneo la viwanda
ambako Winnie alikua
amepelekwa.Baada ya kufika katika
jengo alimokuwamo Winnie,Vicky
akashushwa toka katika buti ya gari
na kufunguliwa kitambaa.
"Hapa ni wapi? akauliza huku
akitetemeka
"Quiety!! akasema Frank na
kumtaka Vicky apandishwe
ghorofani.Vijana wawii wakamshika
Vicky na kuanza kumpandisha juu
Frank na Obi wakiwa wametangulia
mbele.Obi akamuongoza Frank katika
chumba alimokuwa amefungiwa
Winnie lakini wote wakapatwa na
mshangao mkubwa sana baada ya kukuta chumba kitupu na kamba
alizofungiwa zilikuwa zimekatwa na
kutupwa
"beka!!!! akaita Obi lakini
hakujibiwa
"Peter !!! akaita tena lakini
akajibiwa na ukimya mkubwa
"Somehing is wrong ! akasema
Obi kwa sauto ndogo na kutoka
haraka mle chumbani
"Obi nini kimetokea?Wako wapi
vijana?Winnie yuko wapi? akauliza
Frank akimfuata Obi nyuma.Ghafla Obi
akasimama kama mtu aliyekutana na
kitu cha kutisha akahisi miguu
inamuisha nguvu akapiga magoti na
kushika kichwa
"Oh my God!! akasema Obi na
mara Frank naye akaingia mle ndani
ya kile chumba na kuwakuta vijana
wawili wakiwa wamekufa kwa
kupigwa risasi Who did this !!! akasema Frank
kwa mshangao na kwa hasira
akamfata Vicky akamuwekea bastora
kichwani
"Utanieleza wapi walipo watu
uliowasaidia kumuua Pascal? akasema
na kumshika Vicky nywele
akampeleka katika chumba kile
walichouawa wale vijana wawili
"You see this?!akauliza
"Waliofanya hivi ni hao wenzako
unaoshirikiana nao.Ukitaka nikuache
hai nieleze wako wapi?
"Winnie yuko wapi? Siwezi
kusema chochote bila kumuona
Winnie.Show me Winnie and I'll tell
you everything" akasema Vicky Frank
akapandwa na hasira akamrushia
ngumi nzito iliyompeleka chini
akamkalia juu na kuanza
kumporomoshea makonde Mkuu imetosha.Utamuumiza
huyu na tutakosa kila kitu" akasema
Obi na kumvuta Frank ambaye
alikuwa amepandwa na hasira isiyo
kifani.Uso wa Vicky uliloa damu na
mara simu ya Frank ikaita.Akaitoa
mfukoni na kutazama mpigaji alikuwa
ni Irene akasogea pembeni
"Irene" akasema baada ya
kuipokea
"Frank where are you? I need to
see you !! akasema Irene
"Kuna tatizo Irene? akauliza
Frank
"Chochote unachokifanya achana
nacho nakuhitaji hapa nyumbani sasa
hivi.Kuna jambo la msingi sana"
"Irene ni jambo gani hilo?Huwezi
kunieleza simuni?
"Frank believe me acha kila
unachokifanya na uje hapa nyumabani
ninakusubiri.Usipuuze tafadhali"akasisitiza Irene.Frank
akazama katika tafakari
"Frank !! akaita Irene
"I'm coming there" akasema
Frank na kumtaka Obi wazungumze
"Obi kuna dharura imejitokea
ninahitajika sehemu fulani.Take care
of everything here.Mrudisheni Vicky
na hakikisha anaongea.Do everything
you can to make her tell us
everything!! akasema Frank na
kuondoka haraka haraka akionekana
kuchanganyikiwa
"Bastard !! akapiga usukani wa
gari baada ya kukumbuka miili ya
wale vijana wawili waliouawa na
Winnie kutoweka
"Nani huyu aliyefanya
haya?Amefahamuje kama Winnie
yuko pale? Winnie alikuwa ni muhimu
sana kwetu kwani bila yeye Vicky
hawezi kutueleza jambo lolote.I'm back to square one.Watu hawa tayari
wanaonekana kunifuatilia kila
mahala,na wanafahamu kila
ninachokifanya.I must find them
immediately!! akawaza akiendesha
gari kuelekea nyumbani kwa Irene
"I think Winnie and Vicky are
playing a game with me.Kauli zao
zinakinzana.Winnie anadai kwamba
walikuwa wametekwa na watu ambao
amewataja kwa majina na mmoja wa
watu waliotajwa ni Elvis lakini Vicky
amekana kutekwa na watu hao.Winnie
ametupeleka hadi mahala walikokuwa
wanashikiliwa lakini hatukukuta mtu
yeyote mahala hapo na tukiwa hapo
ofisi yangu shambani ikavamiwa na
mpaka sasa hakuna mtu yeyote
aliyeonekana akiingia ndani ya
nyumba hiyo.Leo tena Vicky
amejitokeza na kukana kila kile
alichokisema Winnie na kama haitoshi Winnie akatoroka.What kind of game
are they playing?How could I be such
a fool?!! How could I let them fool me
like this?! akawaza na kuupiga
usukani kwa hasira
"Vicky atanieleza kila kitu
leo.Nitampa kila aina ya mateso hadi
atakaponieleza ukwe.." Frank
akatolewa mawazoni baada ya simu
yake kuita.Alikuwa ni David
"Hallow David" akasema Frank
" Hallo Frank.Habari za leo?Vipi
maendeleo yako ?
"Ninaendelea vyema.Vipi wewe?
"Hata mimi ninaendelea
vyema.Nimekupigia kukujulia hali
kwani toka asubuhi sijaipata simu
yako.Tuko katika hatua kubwa sana
hivi sasa tunapaswa kuwa na
mawasiliano ya karibu na kupeana
taarifa za mara kwa mara juu ya kile
kinachoendelea kujiri.Dr Makwa amelala nyumbani kwangu kwa
kuhofia kukamatwa na amekuwa
akiwasiliana na wenzake kuhusiana
na kinachoendelea na taarifa
anazoendelea kupokea ni kwamba kila
kitu kinakwenda vyema na maandalizi
yanaendelea ya mkutano wa leo.Jioni
ya leo lazima tuwe na kikao tujadili
kuhusu mambo yalivyokwenda na
kinachoendelea.Baada ya mkutano wa
leo tutapata picha kamili ya namna
operesheni yetu inavyokwenda"
akasema David
"Sawa David.Tutakutana jioni ili
tupeane taarifa zaidi kuhusu
operesheni hii" akasema Frank
"Frank are you ok today?akauliza
David
"Why?Frank naye akauliza
"Unaonekana hauko sawa.Vipi
kuhusu mazishi ya pascal? Ni kweli siko sawa David kuna
jambo fulani linaniumiza kichwa
sana.Kuhusu Pascal bado sijapata
taarifa kamili ni lini anazikwa.Nitapita
msibani baadae kupata taarifa kisha
nitakujulisha"
"Frank umesema kwamba kuna
jambo linakuumiza kichwa.Ni jambo
lipi?Linahusiana na hili suala
letu?Kama linahusiana na sisi liweke
wazi tulifanyie kazi haraka.Hatutaki
kikwazo chochote kwa sasa"
"Ni suala binafsi ninaweza
kulishughulikia"
"Sawa Frank tutawasiliana
baadae"akasema David na kukata
simu
"Sijui kwa nini nimeanza
kumchukia David.Huyu jamaa ninahisi
anaweza akahusika pia katika kifo cha
Pascal.Lakini suala ili la kifo cha Pascal
bado lina ukakasi.Winnie aliwataja Elvis na Steve kwamba walimteka
Vicky na kumlazimisha kumuita Pascal
pale hotelini kisha wakamuua.Madam
Elizabeh naye akadai kwamba yeye
ndiye aliyemuua
Pascal.Ninaposhindwa kupata jibu ni
je madam Elizabeth ameshirikiana na
hao akina Steve?Nilimuuliza kuhusu
kushirikiana na Vicky na akadai
kwamba ndiyo alishirikiana na Vicky
..oh gosh I'm confused.Ngoja niliendee
taratibu hili suala nikiliendea kwa
pupa litanichanganya.Mwenye majibu
yote juu ya suala hili ni Vicky.Nina
uhakika nikimtesa atanieleza ukweli
wote kama kweli alitumwa na madam
Elizabeth au vipi.Kama kweli
alimtuma nitachunguza nijue Pascal
alifanya jambo gani hadi
akauawa?akaendelea kuwaza.
Sent using Jamii Forums mobile app[/QUOTE
Afadhar asee
Mkuu, mi huwa nasoma novel za page 500 mpaka 700 mfululizo bila kupumzika. Novel za Chess nilikuwa namaliza moja kila Siku... Hit and run, naingia lay her along the lily, ... I will fix zote kwa siku moja.
The genius... Umetisha Sana mkuuTaarifa za Irene zitamfanya Frank achanganyikiwe kabisa. Atalazimika kumwambia Elizabeth. Elizabeth atatafuta namna ya kummaliza Frank. Vicky lazima atoke Salama huko matesoni kwa namna gani haijulikani. Pia mawasiliano ya David na Makamu Rais yatanaswa yakuhusu maandamano ya wanasiasa. Mambo yanazidi kunoga. Bila shaka tupo episode za mwisho mwisho.
Mkuu bure ni ghali mnoImekwisha poteza ladha mkuu..ngoja tuamie upande wa pili mana huku magumashi sana.tantalilaaaaa nyiiingi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo hamzingatii na mda si kila mara mtu yupo online kuna life nje ya jfMkuu bure ni ghali mno