I DIED TO SAVE PRESIDANT
Sehemu 67
David alipomaliza kuzungumza
na Frank simuni akazitafuta namba za
simu za makamu wa rais akampigia
"Hallow David" akasema Dr Shaf
"Dr Shafi habari yako.Vipi mbona
sauti yako haitoki vizuri leo?
"NImepatwa na mafua ya ghafla
ila tayari nimepata dawa na
ninaendelea na kazi zangu.Kuna
taarifa zozote mpya?
"Nimetaka tu kukujulia hali na
kukujulisha kuwa leo ndiyo mambo
yanaanza rasmi.Maandalizi ya
mkutano yanaendelea na kila kitu
kimekamilika.Dr makwa ninaye hapa
nyumbani kwangu toka jana na
viongozi wengine wote wa vyama vya
siasa wako katika sehemu zao
wamejificha wakisubiri muda ufike ili
wajitokeze na mambo yaanze rasmi.Dr Shafi nitakuwa nikikujulisha kila
hatua tunayopiga ninachokusisitiza tu
usiwe na wasiwasi kila kitu
kimepangwa vizuri na kila jambo
litakwenda kama vile tunavokusudia"
"Hizo ni taarifa njema sana
David.Mimi sina wasiwasi nawe hata
kidogo kwani najua mahala ulipo
hapaharibiki kitu.Endelea kunijulisha
kila kitu kinavyoendelea ila nashauri
umakini mkubwa unatakiwa hasa
katika hatua hii.Polisi wanawawinda
sana hawa wanasiasa na endapo
watafanikiwa kumkamata hata mmoja
wao basi wanaweza wakamtesa na
akaeleza kwamba wewe ndiye
uliyekuwa nyuma ya mpango huu wa
maandamano na vurugu.Ikifika hapo
kila kitu kitakuwa kimeharbika hivyo
viongozi hawa wa siasa wawe makini
mno" Hilo nimekwisha liona na
nimezungumza nao na tumewekeana
mikakati na kutokana na mipango
yetu ilivyoandaliwa hakutakuwa na
tatizo lolote.Nitawasiliana nawe tena
jioni ya leo kukujulisha mambo
yanavyokwenda"
"Nawatakia kila la heri na
mafanikio" akasema Dr Shafi na
kukata simu
"Sasa ngoja niende katika msiba
nyumbani kwa madam Elizabeth
nikamjulishe mambo
yanavyokwenda.Mambo yote tayari
yanakwenda vyema ninachosubiri ni
muda tu ufike ili tujue mbivu na
mbichi"akawaza David na kuanza
kujiandaa kwa ajili ya kwenda msibani
nyumbani kwa Elizabeth
****************** Steve alirejea katika makazi yao
akiwa ameambatana na Omola
"Karibu sana Omola"akasema
Elvis
"Ahsante sana Elvis.Nashukuru
kila kitu kinakwenda vyema kwa
upande wagu.Vipi hapa kwenu
mambo yanakwendaje?akauliza
Omola na kabla Elvis hajajibu kitu
akatokea Steve akiwa na chupa ya
mvinyo akiwa na glasi tatu akamimina
na kuwapatia Elvis na Omola.Kila
mmoja akanywa funda moja halafu
Elvis akasema
"Kwa upande wetu mambo
yamekwenda vizuri.Kwanza kabla ya
yote nataka nikushukuru sana kwani
ile programu yako imetusaidia
tumeweza kumpata Winnie japo
alikuwa ameumizwa lakini tayari
amekwisha shughulikiwa na
anaendelea vyema" akasema Elvis na kumtazama Omola aliyekuwa
anatabasamu
"Tukiachana na
hilo,tumefanikiwa pia kumpata Irene
Mwabukusi mmiliki wa kampuni ya
Pendeza.Baada ya kumuhoji amekiri
kwamba mwenye kampuni ile ni
brigedia Frank lakini alimtumia yeye
kuanzisha na kuisimamia kwa kuwa
yeye hataki kujulikana kama anamiliki
kampuni" akasema Elvis na
kumueleza Omola kila kitu
walichoelezwa na Irene
mwabukusi.Omola akanywa funda la
mvinyo na kusema
"Haya ni mafanikio makubwa
yamepatikana ndani ya kipindi
kifupi.Ninyi ni wachapa kazi hodari
sana ninafurahi kukutana na kufanya
kazi nanyi.Nimeipenda timu yenu"
akasema na wote wakatabasamu Mpaka hapa tayari mwanga
umepatikana.Kama kampuni hii ni ya
Frank basi anatumia kama mwavuli
wa kumkinga na biashara hii haramu
ya silaha anayoifanya.Watu hawa
wanazo mbinu nyingi za kufanikisha
biashara yao.Ni mtandao mrefu na
ndiyo maana hata mizigo yao inatoka
bandarini bila hata ya
kukaguliwa.Tuendelee kuchunguza na
tutaupata ukweli wote" akasema
Omola na kumimina tena mvinyo
katika glasi akanywa halafu
akaendelea
"Nimefanikiwa kuonana na
makamu wa rais.Nashukuru Vicky
amefanya kazi nzuri na sikupata taabu
yoyote kuingia ikulu kwani taarifa
zangu tayari zilikuwepo hivyo
nikapata urahisi wa kuonana na
makamu wa rais.Sijamuona Vicky
yuko wapi? akauliza Omola.Vicky ameondoka asubuhi na
mpaka sasa hajarejea.Kinachonipa
wasiwasi hakumuaga mtu yeyote
anakwenda wapi"
"Aliondoka bila kumuaga mtu
yeyote?
"Ndiyo.Aliondoka wakati bado
tumelala na mpaka sasa
hajarejea.Msiwe na wasi wasi Vicky
atakuwa salama,anajua
kujilinda,tuendelee na kazi.Tupe
maelezo ya kazi yako ya leo" akasema
Elvis
"Sikuonana na rais ila wasaidizi
wake walipewa maelekezo
walinipeleke kwa makamu wa rais na
nikafanikiwa kuonana naye.Makamu
wa rais bado ni kijana na na
anaonekana ni msomi
mzuri.Nilijitambulisha kwake kumbe
tayari taarifa zangu alikuwa
nazo,aliambiwa na rais.Tulikunywa chai pamoja na kisha nikapata wasaa
wa kuzungumza naye kuhusu masuala
ya mazingira.Wakati nikiendelea
kumuuliza maswali huku nikimrekodi
nikafungua mkoba wangu na
kubonyeza chupa ya dawa isiyokua na
harufu ambayo humfanya mtu
kupatwa na mafua ya ghafla na
makamu wa rais akapatwa na chafya
ya ghafla.Dawa hii haikuniathiri mimi
kwani tayari nilikuwa nimepaka dawa
fulani puani ambayo huzuia
kuathiriwa na hii dawa pindi
unapoipuliza sehemu.Dr Shafi alitoka
na kuingia maliwato na mimi nikapata
nafasi ya kufanya utundu
wangu.Nilichomeka kifaa fulani
kidogo katika kalamu yake ambacho
kitarekodi mazungumzo yake
yote.Nilingiza pia proramu fulani
katika simu yake ambayo
itatuwezesha kunasa mawasiliano yake yote ya simu.Kwa kuwa alikuwa
anapiga chafya mfululizo aliniomba
radhi kwamba hataweza kuendelea na
mazungumzo yetu na akanitaka
niende tena kesho.Hapo ndipo
nilipoishia siku ya leo" akasema
Omola na kuinua glasi akanywa tena
funda lingine la mvinyo
"Hongera sana Omola umefanya
kazi kubwa na nzuri.Yale maneno yote
aliyotueleza Vicky sasa
nimeyaamini.Kuhusu kifaa hicho
ulichokiweka katika kalamu ya
makamu wa rais tutawezaje kupata
taarifa zake?Itakulazimu tena kwenda
kupata kalamu hiyo na kukipata hicho
kifaa ili kusikia mambo kiliyorekodi?
"Hatuhitajitena kuipata hiyo
kalamu kwani kifaa hicho ninaweza
kukiongoza kwa kutumia kompyuta
yangu.Tutapata kila kitu hapa hapa"akasema Omola na Steve
akainuka akampatia kompyuta yake
"Kwanza tuanze na majibu ya ule
uchunuzi niliowaomba wenzangu
wanisaidie kuichunguza kampuni ya
McLorien.Kama nilivyowaleza
kwamba majibu tayari yametumwa
katika akaunti yangu ya barua pepe"
akasema Omola huku vidole vyake
vikicheza na vitufe vya kompyuta yake
na mara akaifungua akaunti yake ya
barua pepe akazikuta barua pepe
kadhaa lakini aliyokuwa anaihitaji
kwa wakati huo ni moja tu akaitafuta
akaipata akaifungua na kuanza
kuisoma.Alipomaliza akawageukia
akina Elvis
"Kwa mujibu wa wenzangu
walionisaida kupata taarifa za
kampuni ya McLorien ni kwamba
kampuni hiyo imesajiliwa nchini
Marekani na inajishughulisha namasuala ya mavazi na
urembo.Inajulikana sana kwa uuzaji
wa nguo nzuri na viatu vya bei nafuu
sana.Mmiliki wa kampuni hii anaitwa
Shanon Blank jina ambalo tulilikuta
katika mawasiliano ya barua pepe kati
yake na Patrice Lwibombe.Kwa bahati
nzuri wamenitumia pia na picha ya
mmiliki wa kampuni hiyo na hiyo
kidogo imenistua" akasema Omola na
kuwataka akina Elvis wasogee ili
waweze kuishuhudia picha hiyo ya
Shanon Blank
"Is this true?akauliza Steve kwa
mshangao
"Huyu si Elizabeth mama yake
Juliana? akauliza
"Picha aliyotutumia Juliana ya
mama yake na hii zinaonyesha ni watu
wanaofanana sana lakini bado
hatuwezi kuwa na uhakika kama huyu ni mama yake Juliana.Tufanye kwanza
uchunguzi"akasema Elvis
"Sioni sababu ya kufanya
uchunguzi wakati hata kwa macho
unaona kabisa huyu ni Elizabeth
mama yake Juliana.Believe me
Elvis"akasema Steve
"Steve unaweza kuwa sahihi
lakini tujiridhishe kwanza kama ni
kweli ni yeye.Huyu anaitwa Shanon
Blank na mama yake Juliana anaita
Elizabeth je ni mtu yule yule lakini ana
majina tofauti?Kama ni kweli kwa nini
awe na majina tofauti?hayo ni mambo
ambayo tunapaswa kuyatafutia
majibu japo sura ni kweli inaonyesha
ni ya mama yake Juliana ingawa katika
picha hii amekuwa mweupe zaidi"
"Elvis ukumbuke pia kwamba
tulijaribu kumtafuta kwa jina lile
alilotuambia Juliana la Elizabeth lakini
hatukuweza kumpata.Hii inaonyesha kwamba hatumii jina hilo na
yawezekana akawa anatumia jina hili
la Shanon Blank.Kumbuka Juliana
alisema kwamba mama yake
amekuwa anajiusisha na biashara
haramu na hii ni staili ya watu
wanaojihusisha na biashara hizi
haramu mara nyingi hawatumii
majina yao halisi.Yawezekana jina lake
halisi ni Elizabeth lakini akabadilisha
na kujiita Shanon.Unasemaje kuhusu
hilo Elvis?akauliza Steve
"Kwa hili tulazimika kumuhitaji
Juliana.Mpigie simu tukutane
naye"akasema Elvis mara Omola
aliyekuwa anacheza na kompyuta
yake akawageukia
"Nimeingiza picha hizi mbili
katika programu yangu na matokeo
yanaonyesha kuwa huyu ni mtu
mmoja.Anachokisema Steve ni kitu cha kweli.Elizabeth ndiye huyu
Shanon" akasema Omola
"Hapa tunahitaji msaada wa
Juliana ili tuweze kumfahamu mama
yake kwa undani"akasema Elvis
"Una hakika atakubali kutupa
taarifa za mama yake?Yuko tayari
mama yake achunguzwe?akauliza
Omola
"Juliana yuko tayari mama yake
achunguzwe kwani ni yeye aliyetupa
taarifa kwamba anahisi mama yake
anajihusisha na biashara haramu na
akatutaka tuchunguze jambo hilo.Vile
vile lazima atupe ushirikiano kwa
sababu ametuomba tumsaidie kufanya
uchunguzi kwa watu waliomuua
mpenzi wake vile vile mdogo wake."
akasema Elvis na Steve aliyekuwa
amesogea pembeni akiongea na simu
akarejea Nimempata Juliana na
nimemuomba tukutane
amekubali.Ninakwenda kuonana naye
mara moja" akasema Steve
"Huwezi kwenda peke
yako,tutakwenda sote"
"Are you sure Elvis?
"Yes.Hataweza kuniona mimi
nitabaki garini na wewe utakwenda
kuzungumza naye katika gari lake na
utamtaka athibitishe kama huyu
anayeonekana katika picha ni mama
yake.Omola atakutumia picha hizi
katika simu ili Juliana aweze
kuziona.Sisi tumethibitisha kuwa ni
yeye kupitia programu ya Omola
lakini tunahitaji na yeye athibitishe
kweli huyu ni mama
yake.Akithibitisha kuwa ni mama yake
tutahiaji atusaidie kuchunguza pasi za
kusafiria za mama yake ili tulifahamu
jina lake halisi ni nani.Ni jambo gumu kidogo lakini litakuwa na msaada
mkubwa kwetu.Kama kweli ana nia ya
dhati ya kutaka kumfahamu vyema
mama yake na biashara anazozifanya
basi huu ni wakati wake.Tunahitaji
msaada wake sana"akasema Elvis
"Wakati mkienda huko mimi
nitaendelea kufuatilia kifaa kile
ambacho nimekitega katika kalamu ya
makamu wa rais nifuatilie maongezi
yake.Sifahamu kiswahili laiti Vicky
angekuwepo angenisaidia kujua kile
anachokizungumza makamu wa rais"
akasema Omola
"Usijali Omola yupo Graca hapa
atakusadia kujua kile
kinachoongelewa" akasema Elvis na
kumuita Graca akamtaka amsaidie
Omola kufahamu kile
kinachozungumzwa katika
mazungumzo ambayo kifaa
alichokitega katika ofisi ya nakamu wa rais kitayanasa.Bila kupoteza muda
Elvis na Steve wakaingia garini na
kuondoka kwenda kukutana na
Juliana
"Kama Juliana atathibitisha kweli
huyu ni mama yake basi jambo hili
litakuwa pana sana"akasema Elvis
"Mimi sina shaka kabisa kuwa
huyu ni Elizabeth lakini ni vyema
tukathibitisha kwa kumtumia mwanae
Juliana"akasema Steve na Elvis
akaendelea kuzichunguza picha zile
mbili zilizowekwa katika simu ya
Steve
"Umemuonaje Omola?akauliza
Steve huku akitabasamu
"Not now Steve.Tuko katikati ya
jambo zito masuala ya wanawake
yaweke kwanza pembeni" akasema
Elvis na safari ikaendelea
******************* Frank aliwasili nyumbani kwa
Irene,akapokewa na mtumishi wa
ndani akamkaribisha sebuleni.Baada
ya dakika tano Irene akatokea akiwa
amefunga plasta chini ya jicho na uso
wake ulionekana kuvimba.Mkononi
pia alikuwa amefunga bandeji
"Irene nini kimetokea?Umepata
ajali?
"Ni bora kama ningepata
ajali."akasema Irene huku akikaa
sofani
"Irene nieleze umepatwa na
tatiuzo gani?Umenistua sana
uliponipigia simu nikaacha kila kitu na
kuja kukuona" akasema Frank.Irene
akamtazama Frank kwa makini sana
kwa sekunde kadhaa halafu akasema
"Frank nataka leo unieleze
ukweli" Ukweli gani Irene?Kabla ya yote
nieleze nini kimekupata?
"Frank nataka kufahamu
unajihusisha na mambo gani?akauliza
Irene na Frank akastuka sana
"Sielewi unamaanisha nini Irene
unapouliza swali kama hilo wakati
unafahamu kabisa mambo
ninayojihusisha nayo.Unaifahamu kazi
yangu na unazifahamu pia biashara
zangu"akasema Frank
"Frank chochote kile
unachojishughulisha nacho ambacho
si kizuri nakuomba ukiache haraka
sana"akasema Irene.Frank akasimama
na kumtazama kwa macho makali
"Irene unanishangaza sana kwa
haya maneno yako"
"Usishangae Frank na wala sina
lengo ya kuyachimba maisha yako na
kufahamu kila unachokifanya lakini nakueleza ukweli kwamba uko katika
hatari kubwa"
"Hatari?! akauliza Frank kwa
mshangao
"Ndiyo uko katika hatari kubwa"
"Irene tafadhali sitaki uendelee
kunizunguka,nieleze ukweli kwani
umekuwa unazungumza mambo
ambayo siyaelewi"
Irene akameza mate na kusema
"Nimefuatwa na watu wawili
hapa nyumbani asubuhi ya
leo.Niliwakaribisha ndani nikijua ni
wateja wamekuja kuzungumza nami
masuala ya biashara lakini ikawa
tofauti wote wawili walikuwa na
bastora na wakaniamuru niongozane
nao kimya kimya bila kutoa ukelele
wowote"
"Oh my God! what happened
then?Who are they?Siwafahamu na sijawahi
kuwaona lakini wao wananifahamu na
walifika hadi dukani kwangu asubuhi
wakaambiwa sijafika ndiyo maana
wakanifuata huku nyumbani"akasema
Iene na Frank akagonganisha mikono
yake kwa hasira
"Walikupeleka wapi?Walikuw
wamnataka nini?
"Niliingia katika gari lao na
wakaanza kuniuliza
maswali.Waliniuliza kwamba kampuni
ya pendeza ni ya nani?Nikawajibu ni
ya kwangu lakini hawakuamini
wakaanza kunitesa humo humo ndani
ya gari.Waliniuliza tena mahusiano
yangu na wewe nikawajibu
sikufahamu na hapo ndipo walipotaka
kunitoa jicho kwa kutumia kisu
ikanilazimu kuwaeleza ukweli" Jesus Chris !! akasema Frank
kwa sauti ndogo akiwa amesimama
ameshika kiuno
"Uliwaeleza mambo
gani?akauliza
"Kila kitu kuhusiana na
kampuni.Niliwaeleza kwamba wewe
ndiye mmiliki wa kampuni na
umeniweka mimi kama msimamizi
wake.Waliniuliza pia namna
tunavyoagiza mizigo yetu
nikawaeleza"
"Kwa nini Irene umewaeleza kila
kitu?Hukuweza uvumilia
mateso?akauliza Frank kwa ukali
"Frank I'm sorry nilivumilia sana
lakini ikafika mahala nikashindwa
kuendelea kuvumilia zaidi ikanilazimu
kuwaeleza kile walichokuwa
wanakitaka.Isitoshe inaonekana tayari
walikuwa wanafahamu kila kitu kwani
walikuwa na nyaraka za kutolea mzigo bandarini ambazo wanadai walizipata
toka kwako hivyo ikanilazimu
kuwaeleza ukweli wote.I'm sorry
Frank" akasema Irene na Frank
akaonekana kuchanganyikiwa
akaanza kuzunguka zunguka mle
sebuleni halafu akasimama na kuuliza
"Nini kingine walikuuliza?
"Walitaka kufahamu kuhusiana
na kampuni ya McLorien."
"Oh my gosh !akasema Frank
akizidi kuchanganyikiwa
"Uliwajibu nini?
"Niliwajibu kwamba kampuni ya
McLorien ndiyo ambayo hutuuzia
bidhaa tunazouza katika maduka
yetu"
Frank akavuta pumzi ndefu na
kuketi sofani
"who are those people?Kwa nini
wanakuchunguza?akauliza Irene Irene samahani sana kwa
kukuingiza katika matatizo haya.Pole
kwa yote yaliyokupata kwa ajili
yangu.Watu hawa siwafahamu lakini
ninaamini lazima watakuwa
wametumwa na mahasimu wangu wa
biashara.Kuna watu ninahasimiana
nao katika mambo yetu ya biaahsra na
ndiyo hao wananichunguza na kwa
taarifa ulizowapa wamepata kitu
kikubwa sana"
"I'm sory Frank sikuwa na namna
nyingine ya kufanya.Kama
nisingewaeleza ukweli wangeweza
kuniua wale jamaa.Nisamehe sana
Frank sikujua chochote"
"Usijali Irene hilo si kosa lako
lakini watu hawa sintawaruhusu
waendelee na kutaka
kunihujmu.Nitawaonyesha
kazi.Unaweza kunieleza wasifu wa
watu hao? Mmoja alikuwa na mwili
uliojengeka na ndiye alikuwa dereva
wa gari na mwingne alikuwa
mwembamba wastani na mrefu
kidogo ila alikuwa na ndevu nyingi na
alikuwa amevaa kofia na miwani.Huyu
ndiye aliyekuwa ananitesa" akasema
Irene na Frank akaitafuta picha ya
mcheza mpira wa kikapu wa Marekani
Stephe curry na kumuonyesha Irene
"Mmoja wao anaweza kufanana
na huyu jamaa pichani?
"Hapana hakuna anayefanana
naye.Kidogo labda yule mwenye
madevu mengi anaweza kulingana
naye mwili lakini sura hawafanani
kabisa"
"Who are they?!! akajiuliza Frank
"Frank mimi na wewe ni watu
tunaoheshimiana na kuaminiana
sana.Nataka nikuombe fanya kila
uwezavyo kuwatafuta wale jamaakwani wanaonekana ni watu hatari na
wanakufahamu vyema.Kama
wameweza kupata hadi nyaraka zile
za mizigo basi tayari wanafahamu
mambo yako mengi.Watu hawa ni
hatari na si wa kuwapuuza.Please
don't mess with them.Kama unao
uwezo wa kuwadhibiti fanya hivyo
angalia bado mapema watu hawa
wanakusaka kila kona" akasema Irene
"Ahsnate sana Irene kwa taarifa
hizi.Hapa nyumbani kwako hakuna
kamera za ulinzi?
"Hakuna kamera hapa
nyumbani"
"Sawa.Nitakufungia kamera za
ulinzi hapa nyumbani na kukuwekea
walinzi wa kukulinda wewe na famlia
yako.Nakuahidi watu wale
hawatarejea tena hapa kukutisha
kwani nitawasaka kila kona na
kuhakikisha nimewapata.Pole sana Irene ila nakuomba uwe muangalifu
sana kuanzia sasa" akasema Frank
huku akiinuka
"Irene inanilazimu kuondoka
natakiwa kuanza kuwasaka hawa
jamaa haraka sana kwani ni watu
hatari mno kwangu.Kama kuna hatari
yoyote unahisi nijulishe hataka sana"
akasema Frank akaagana na Irene
akaelekea katika gari lake
"Aaaaaghhh!!! akapiga ukelele wa
hasira Frank huku akiupiga usukani
kama kawaida yake awapo na hasira
"What's happening to me?Why
now?? akajiuliza na kuwasha gari
akaondoka
"Yote haya yaliyotokea na
yanayoendelea kutokea
yamesabishwa na Graca.Kama
asingeiba kompyuta yangu na kuanza
kushirikiana na akina Elvis haya yote
yasingekuwepo.Mpaka hapa nina uhakika kwamba watu hawa
wanaoendelea kunifuatilia ni mtandao
wa Elvis.Inawezekana Elvis alikuwa
anashirikiana na wenzake katika
kunichunguza na hata baada ya yeye
kufa hao wenzake wanaendelea na
uchunguzi wao.Ninawafahamu hawa
jamaa hawatalala hadi wahakikishe
wamenichunguza na kunifahamu
kiundani.Mpaka sasa tayari
wamefahamu kuhusiana na biashara
ya silaha na kila uchao wanazidi
kunichiba zaidi wakitafuta ushahidi
zaidi.I wont let them go far.Hapa
walipofika panatosha sana" akawaza
"Wanasema watoto ni baraka
kutoka kwa Mungu lakini kwangu
imekuwa tofauti si baraka tena bali ni
laana.Graca ni laana kwangu na
amenisababishia matatizo
makubwa.Nitahakikisha ninamsaka na
kumtia mikononi na ninaapa nitamkata kiungo kimoja baada ya
kingine.Nitampa mateso makali
ambayo hajawahi kuyashuhudia"
akawaza na kusimamisha gari
pembeni akachukua simu na kumpigia
Elizabeth
"Frank unasemaje?akauliza
Elizabeth baada ya kuipokea simu
"Habari yako madam
Elizabeth?akauliza Frank
"Frank nilikukanya usinipigie
simu nilikuwa na maana yangu.Kwa
nini umepuuza agizo langu?
"Madam kuna jambo limejitokeza
I need to talk to you"akasema
Frank.Elizabeth akasikika akivuta
pumzi ndefu
"Jambo gani limetokea?
"Madam siwezi kukueleza
simuni.Naomba nije nikuone
tafadhali" akasema Frank na Elizabeth
akamruhusu aende nyumbani kwake Kwa hapa lilipofika hili suala
siwezi kulikabili peke yangu,ninahitaji
msaada kutoka kwa Elizabeth.Hili
suala limekwisha kuwa kubwa na ili
kulimaliza nguvu kubwa inahitajika"
akawaza Frank akampigia simu Obi
"Mmekwisha anza kumtesa
Vicky?Amefunguka lolote?
"Bado hatujaanza
mkuu,tunashughulikia namna ya
kuihifadhi miili ya wenzetu ndipo
tuanze lile zoezi la Vicky"
"C'mon Obi !! fanya haraka sana
uanze kumuhoji huyo mwanamke.Hali
si nzuri hata kidogo.Ikiwezekana
waachie vijana wako waendelee na
zoezi la kuwahifadhi hao wenzenu na
wewe ushughulike na suala la
Vicky.Nataka nitakapopiga tena simu
nikute tayari kuna taarifa umezipata
kutoka kwa Vicky!! Mkuu hawa waliofariki mimi
ndiye kiongozi wao hivyo lazima
nishiriki hadi mwisho
kuwahifadhi.Siwezi kuliacha jambo
hili kwa mtu
mwinvine.Nitakapomaliza nitaifanya
kazi yako lakini kama unaona
ninachelewa unaweza ukatafuta watu
wengine wakakusaidia"
Frank akatafakari na kusema
"Samahani Obi,kichwa changu
kimevurugika kabisa kwa sasa kwani
mambo mengi mazito
yananizunguka.Endelea na taratibu
zako ila nakuomba ujitahidi ufanye
kila linalowezekana kumuhoji Vicky
kwani ana taarifa muhimu
ninazozihitaji mno"
"Sawa mkuu" akajibu Obi na
kukata simu
*************** Flaviana beauty salon ndipo
mahala Juliana na Steve walipanga
wakutane.Alifika katika maegesho ya
saluni hii kubwa akashuka na kwenda
katika duka lililokuwa pembeni
akanunua pakiti za Chokolate na
kurejea garini akaendelea kumsubiri
Steve.Mara simu yake ikaita alikuwa
ni Steve
"Hallow Steve"
"Juliana mimi tayari nimefika
hapa mahala tulikopanga
tukutane.Wewe uko wapi?
"Mimi tayari nimefika kama
ronbo saa iliyopita." akasema Juliana
"Ok good.Usishuke garini
nielekeze gari lako lilipo nitakufuata"
akasema Steve na Juliana
akamuelekeza aina ya gari lake na
kukata simu Elvis na Steven wakafika katika
maegesho.Steve akaweka sikioni kifaa
cha kuwawezesha kuwasiliana
"Testing one two three,one two
three..." akasema Steve akijaribu kifaa
kile kama kinafanya kazi
"Good lucky brother" akasema
Elvis wakati Steve akishuka na
kuelekea katika gari la Juliana.Elvis
alibaki garini akiangalia kila
kilichokuwa kinaendelea pale.Alitaka
kuhakiki usalama wa Steve.
Steve alilitambua gari la Juliana
akafungua mlango na kuingia ndani.
"Habari ya mchana Steve"
akasema Juliana huku akimpatia Steve
pakiti ya chocolate Steve akatabasamu
"Samahani sana Juliana
nimekuvurugia ratiba zako mchana
huu" akasema SteveUsijali Steve.Tunaendelea na
maandalizi ya mazishi ya baba hivyo
sikuwa na kazi kubwa sana nyumbani"
"Ahsante kwa kufika.Kuna jambo
tumelipata ambalo tunahitaji msaada
wako"
"Mimi niko tayari kutoa kila aina
ya msaada muda wowote mkihitaji
hivyo msisite kila pale mtakapohitaji
msaada wangu"
"Thank you" akasema Steve
halafu akaitoa simu yake ya mkononi
na kufungua sehemu ya kuifadhi picha
"Nataka uzitambue picha hizi
mbili"akasema Steve na kumpatia
simu Juliana ambaye alitabasamu na
kusema
"Huyu ni mama yangu"akasema
Juliana
"Are you sure?
"Yes I'm sure.Huyu ni mama" Steve mwambie akuthibitishie
kwa mara nyingine kama kweli huyo
ni mama yake" Elvis aliyekuwa
anafuatilia mazungumzo ya Steve na
Juliana akamuelekeza Steve bila
Juliana kujua
"Hii ni picha ya kwanza ambayo
ulitutumia na hii ni picha ya pili
ambayo tumeipata sisi.Nataka kwa
mara nyingine tena unithibitishie
kwamba huyu ni mama yako"
akasema Steve
"Steve mbona huniamini?Huyu ni
mama yangu.Ninamfahamu kuliko
ninyi hivyo niamini ninaposema
kwamba huyu ni mama yangu japo
kuna utofauti mdogo katika picha hizi
mbili lakini amini huyu ni mama"
'Thank you so much" akasema
Steve na kuiweka simu mfukoni Nini kinaendelea?Kuna chochote
mmekipata katika uchunguzi
wenu?akauliza Juliana
"Ndiyo kuna jambo
tumelipata.Tumegundua kwamba
mama yako anamiliki kampuni
inaitwa McLorien iliyosajiliwa nchni
marekani na anatumia jina la Shanon
Blank.Unaifahamu kampuni hii?
"Mc What? akauliza Juliana
"McLorien"akajibu Steve
"Hapana siifahamu hiyo
kampuni.Ni mara yangu ya kwanza
ninasikia kwamba mama anamiliki
kampuni hiyo.Ninafahamu ana
biashara zake nchini marekani na
anafanya kwa ubia na mtu mmoja
anaitwa Joe Gregory.Niliwahi kusikia
kwamba wanataka kuanzisha biashara
ya mitumba kutoka Marekani na
kuiuza katika nchi za Afrika lakini sifahamu chochote kuhusiana na
kampuni hiyo ya McLorien."
"Joe Gregory? akauliza tena kwa
sauti ili Elvis aweze kusikia vyema
"Ndiyo anaitwa Joe Gregory.Huyu
ninamfahamu ni tajiri na inasemekana
ana makampuni kadhaa nchini
Marekani na ndiye mshirika mkubwa
wa mama katika biashara nchini
Marekani" akasema Juliana.
"Jina halisi la mama yako ni nani?
akauliza Steve
"Mimi ninamfahamu kwa jina la
Elizabeth"akajibu Juliana
"Hili jina Shanon Blank kalitoa
wapi?Kwa nini asitumie jina lake
halisi la Elizabeth? akauliza Steve
"Hata mimi ninashangaa.Kama
nilivyowaeleza awali kwamba mama
anajihusisha na mambo ambayo si
mazuri ndiyo maana nikawaomba
mnisaidie kumchunguza" Tunaendelea kumchunguza ila
na wewe tunakuomba utusaidie jambo
moja"
"Sema chochote Steve mmi niko
tayari kuwasaidia"
"Tunataka kulifahamu jina halisi
la mama yako.Tusaidie kuchunguza
kwa nini hatumii jina lake halisi na je
ana majina mengine tofauti na hili la
Shanon Blank?Unaweza kutusaidia
kwa hilo?
"Bila shaka.Kuna mtu mmoja
ambaye naamini anaweza akanipa
taarifa zote za mama.Huyu ni Robert
ambaye ni mlinzi wa mama na ni mtu
ambaye mama anamuamini mno.Siri
zake nyingi huyu anazifahamu"
"Unadhani anaweza kukubali
kukueleza siri za mama yako?
"Sina hakika sana lakini ngoja
nijaribu kwani huyu jamaa amekuwa
ananitaka sana kimapenzi lakini sijawahi kumkubalia.Nitamwambia
kwamba nimekubali ombi lake na
nitamdanganya kwamba atakapokuja
Tanzania wakati wakileta maiti ya
baba nitampa anachokihitaji"akasema
Juliana
"Muda gani nitegemee jibu ?
"Nitazungumza naye na
atakachonieleza nitakupa jibu"
"Ahsante sana Juliana kwa
ushirikiano wako mkubwa"
"Muda wowote mimi niko tayari
kutoa kila aina ya msaada kwani
nataka watu hawa walioiandama
familia yetu wajulikane na wafikishwe
katika mkono wa sheria"
"Steve muulize kuhusu Patricia"
Elvis akamwambia Steve
"Nakuhakikishia Juliana kwamba
wote walioshiriki katika mauaji hayo
siku zao zinahesabika.By the way
how's Patricia?Patricia anaendelea vyema.She's
deeply hurt but she's very
strong.Anajitahidi kwa kila namna
awezavyo kuweza kukabiliana na
ukweli kuwa Elvis hayupo tena.Ni
jeraha kubwa amelipata ambalo
litachukua muda kupona lakini
ninaamini siku moja litapona na
maisha yataendelea kama kawaida.Sisi
tulio karibu naye tunajitahidi kufanya
kila lililo ndani ya uwezo wetu
kumsaidia ili aweze kukivuka kipindi
hiki kigumu kwake.She'll be
fine.Halafu kabla sijasahau leo Patricia
atahama pale nyumbani anahamia
ikulu.Rais na mke wake
wamemuomba akaishi nao hadi hapo
atakapokuwa tayari kuishi
mwenyewe.Patricia ana nyota ya
kupendwa na watu.Rais na mke wake
wanampenda na wanamchukulia kama sehemu ya familia yao" akasema
Juliana
"Juliana ahsante sana kwa muda
wako.Tutaendelea
kuwasiliana.Usiache kunijulisha
tafadhali majibu utakayoyapata"
akasema Steve na kushuka garini
akarejea katika gari lao
"Nadhani umesikia kila kitu
tulichozungumza na Juliana"akasema
Steve
"I heard everything.." akasema
Elvis huku akiwa ameeleza macho
yake katika gari moja jeusi
'Unaliona lile gari jeusi karibu na
gari la Juliana? akauliza Elvis na
wakati huo Juliana alikuwa anaondoka
"NImeliona.Kuna nini?
"Ninahisi gari lile linamfuata
Juliana.Nimelichunguza kuna mtu
yumo mle ndani na wakati wewe
unazungumza na Juliana alikuwa anafungua dirisha na kutoa kichwa
anachungulia na kuna wakati
akashuka akajifanya
anatengene......."akanyamaza Elvis
baada ya gari lile nalo kuanza kondoka
baada ya Juliana kuwasha gari na
kuanza kuondoka
"Juliana anaondoka naye
anaondoka.Yule jamaa lazima
anamfuatilia" akasema Elvis
"Twende tumfuate tumjue ni
nani?
"Au ni mlinzi wa Juliana?akauliza
Steve
"Mpigie Juliana muulize kama
ana walinzi"akasema Elvis na Steve
akampigia simu Juliana
"Hallo Juliana samahani kwa
usumbufu.Ninataka kufahamu jambo
moja je unao walinzi wanaokulinda
kile sehemu uendako?akauliza Walinzi?akauliza Juliana na
kucheka kidogo
"Sina walinzi,mlinzi wangu pekee
ni Mungu"
"Ahsante sana."akajibu Steve na
kukata simu
"Juliana anadai hana walinzi"
"Kama si mlinzi wake basi
tufanye zoezi moja dogo tupate
uhakika kama kweli anamfuatilia
Juliana ama vipi.Mwambie Juliana
aingie barabara ya Ndovu" akasema
Elvis na Steve akampigia simu Juliana
akamtaka aingie barabara ya
Ndovu.Alipokata kuingia barabara ya
ndovu lile gari nalo likakata na
kuendelea kumfuata
"Bado anamfuata.Mwambie
aende moja moja Uchumi
supermarket" akasema Elvis na Steve
akampa maelekezo Juliana "Steve nini kinaendelea?akauliza
Juliana kwa wasi wasi
"Usiwe na wasi wasi Juliana
ninataka kuhakikisha kuwa uko
salama"akasema Steve na kukata simu
Juliana akafuata maelekezo
aliyopewa hadi alipofika Uchumi
supermarket akaingia na kwenda
katika maegesho lile gari nalo likakata
kona na kuingia hapo supermarket
"Mpaka hapa tuna uhakika yule
jamaa anamfuatilia Juliana" akasema
Elvis
"Nimefika tayari.Nifanye
nini?akauliza Juliana
"Shuka ingia ndani kununua kitu
chochote" akasema Steve na Juliana
akashuka akaingia ndani ya
supermarket.Yule jamaa naye
akafungua mlango akashuka
akajifanya anakwenda kununua maji
halafu akarejea garini. "It's our chance.Let's go get him"
akasema Elvis na wote wakashuka
wakatembea kwa tahadhari kulifuata
lile gari.Elvis akagonga kioo cha
dirisha na yule jamaa aliyekuwamo
mle ndani akashusha kioo na wakati
huo huo Steve akafungua mlango na
kuingia ndani kwa kasi ya aina yake
akamtolea bastora
"Shhh!!! akamfanyia ishara asitoe
ukelele
"Shuka taratibu nifuate" akasema
Elvis na yule jamaa akashuka na
kuongozana na Elvis katika gari
lao.Steve akabaki katika gari la yule
jamaa akipekua kama kuna kitu
chochote cha kumfaa halafu akatoka
na kurejea garini,wakawasha gari na
kuondoka
"Tell Juliana to go home"
akasema Elvis na Steve akampigia
simu Juliana Juliana you are free to go home
now" akasema Steve
"Steve kuna tatizo gani?
"Tutazungumza baadae ila kwa
sasa unaweza kwenda nyumbani"
akasema Steve na kukata simu.Yule
jamaa alikuwa amekaa kiti cha nyuma
na Elvis aliyekuwa anaichezea bastora
yake.Ndani ya muda mfupi tayari
alikuwa ameloa jasho
"Jamani mnanipeleka wapi?Ninyi
ni akina nani?akauliza lakini hakuna
aliyemjibu.Steve aliyekuwa katika
usukani akamrushia Elvis simu ya yule
jamaa akaifungua na kuikagua
akakutana na picha ambazo zilimstua
kidogo.Juliana akiwa na Patricia na
Meshack Jumbo.
"Kwa nini unamfuatilia
Juliana?Nani kakutuma
umfuatilie?akauliza Elvis Simfahamu Juliana" akasema
yule jamaa.Elvis akamnasa kibao
kikali halafu akamuonyeha picha ya
Juliana akiwa na Meshack Jumbo na
Patricia
"Hii picha umeitoa wapi?Nani
kakutuma umpige picha Juliana?
Yule jamaa akabaki kimya
"Usiponijibu utakuwa ni mwisho
wako leo!! akasema Elvis huku
akimtazama yule jamaa kwa macho
makali
"Steve naomba zana zangu"
akasema Elvis na Steve akamrushia
kiboksi kidogo chenye vifaa akatoa
koleo dogo na kukibana kidole cha
mwisho cha yule cha jamaa kwa nguvu
akapiga kelele kubwa.
"Nani kakutuma umfuatlie
Juliana? akauliza tena Elvis kwa ukali
lakini yule jamaa hakujibu This is not working.Ngoja
nikufundishe adabu.Ninawapenda
sana watu kama ninyi" akasema Elvis
halafu akamshika yule jamaa mikono
na kumfunga kwa kamba halafu kwa
kutumia ile kolea akaishika korodani
na kuiminya.Yule jamaa akapiga kelele
kubwa
"Ni madam!!...akasema na Elvis
akamuachia
"Nani kakutuma umfuatilie
Juliana? akauliza Elvis
"Ni madam Elizabeth"
"Elizabeth ni nani?
"Ni mama yake Juliana.Alinitaka
nimfuatilie Juliana kila anakokwenda
na nimpige picha kila anayekutana
naye" akasema yule jamaa.
"Lini umeanza kumfuatilia?
"NImeanza jana"akasema yule
jamaa.Elvis akamtazama na kusema Ninakupa onyo kwamba kuanzia
sasa acha kumfuatilia Juliana.Safari hii
nitakuacha hai lakini nikigundua
kwamba unaendelea na mchezo wako
wa kumfuatilia nitakuondoa uume
wako.Umenisikia!! akauliza Elvis huku
akimsindikiza na kofi kali
"Nimekusikia kaka"
"Good.Usimweleze chochote
huyo tajiri wako anayekutuma
umfuatilie Juliana kama umekutana na
sisi.Ukithubutu kufanya hivyo tutajua
na tutakutafuta na kukuua.JIna lako
nani?
"Duma"
"Duma nadhani tumeelewana"
"Nimekuelewa kaka sintarudia
tena" akasema Duma.Elvis akamtaka
Steve asimamishe gari na kumtaka
Duma ashuke.Alikuwa katika
maumivu makali sana hivyo mara tu
aliposhuka garini akajitupa katika nyasi pembeni ya barabara na akina
Steve wakaendelea na safari yao
"Elizabeth tayari ameanza kuhisi
kitu kuhusu Juliana na ndiyo maana
ameweka mtu wa kumfuatilia kwa
bahati mbaya mtu mwenyewe
aliyepewa kazi hii hana ujuzi wowote
wa kumfuatilia mtu.Nimemuonea
huruma yule kijana ni njaa tu ndiyo
inawapelekea wakafanya kazi za
namna hii"
"Si njaa Elvis ni uvivu.Ziko fursa
nyingi ambazo wangeweza kuzitumia
kujitengeneza maisha mazuri lakini
wanapenda mteremko"akasema Steve
"Hata hivyo ameipata tamu yake
na hatathubutu tena kumfuatilia
Juliana.By the way nimefurahi kusikia
Patricia anahamia ikulu leo.Ni
muhimu sana kuondoka pale kwa
akina Juliana.Tuachane na hilo,turudi
katika kazi.Picha inaendelea kujitengeneza na sasa amejitokeza
Elizabeth ambaye bado hatufahamu
jina lake halisi ni nani.Huyu mama
kwa jina lolote lile analolitumia tayari
tuna uhakika kuwa anahusiana na
Frank na anahusika pia katika
biashara ya silaha kwani ndiye
aliyekuwa anawasiliana na Patrice.
Tunaanza kupata picha mtandao huu
ulivyo mkubwa lakini pamoja na haya
yote tuliyoyapata we have to dig
deeper.Lazima tuutafute mtandao
wote na kuusafisha.Tutachimba hadi
ule mzizi wa mwisho hata kama ni
mdogo au mkubwa kiasi gani.Narudia
tena kuweka ahadi kwamba hakuna
mwenye kuhusika na mtandao huu
atabaki salama" akasema Elvis
"Itabidi nizungumze na Juliana
nimweleze awe makini sana kwa sasa
kwani mama yake tayari ameanza
kumfuatilia.Amekwisha anza kumtilia shaka na hasa baada ya kutumiwa
picha Juliana na Patricia wakiwa na
Meshack Jumbo" akasema Steve
"Kwa picha ilivyo inaonyesha
huyu Elizabeth au Shanon ndiye
kiongozi au anayo nafasi kubwa katika
mtandao huu wa kuuza silaha.Vile vile
kuna mtu wa tatu amejitokeza hapa
ambaye Juliana amemtaja Joe
Gregory.Huyu naye kama ni mshirika
wake lazima tumfanyie uchunguzi
inawezekana naye akawa anahusika
pia katika biashara hii ya silaha.Vile
vile kuna huyu mtu naitwa Patrice
lazima naye tumfahamu kwani huyu
aidha ni mmoja wa viongozi katika
kikundi hiki cha waasi au ni kiungo
baina ya waasi na akina
Frank.Tukimpata huyu tutakuwa
tumepiga hatua kubwa sana" akasema
Elvis.Waliendelea na safari yao huku wakijadiliana mambo mbalimbali hadi
walipofika katika makazi yao.
"Mambo yanakwendaje hapa?
akauliza Elvis
"Hapa kila kitu kinakwenda
vyema.Nashukuru nimerejea salama"
akasema Omola
"Mmemtazama Winnie
anaendeleaje?
"Hakuna aliyekwenda huko
kumtazama toka mlipoondoka"
akajibu Graca na Elvis akaenda katika
chumba alimokuwa amelazwa Winnie
akafungua mlango na kumkuta Winnie
bado amelala,akarejea sebuleni
"bado amelala ila anaendelea
vyema." akasema Elvis na kuketi
sofani
"Kuna lolote mmefanikiwa
kulipata kutoka kwa makamu wa
rais?akauliza Ndiyo kuna jambo
tumelipata.Graca amenisaidia sana
kuweza kufahamu maongezi
yaliyorekodiwa na ile programu
niliyoiweka katika simu ya makamu
wa rais.Kwa mujibu wa Graca mengi ni
mazungumzo ya kikazi lakini
tumefanikiwa kunasa mazungumzo ya
simu kati ya makamu wa rais na mtu
aliyemtaja kwa jina la David" akasema
Omola na kubonyeza rekodi ile ya
mazungumzo ya Dr Shafi
"Hallow David" akasema Dr Shaf
"Dr Shafi habari yako.Vipi mbona
sauti yako hitoki vizuri leo?
"Nimepatwa na mafua ya ghafla
ila tayari nimepata dawa na
ninaendelea na kazi zangu.Kuna
taarifa zozote mpya?
"Nimetaka tu kukujulia hali na
kukujulisha kuwa leo ndiyo mambo
yanaanza rasmi.Maandaliz ya mkutano yanaendelea na kila kitu
kimekamilika.Dr Makwa ninaye hapa
nyumbani kwangu toka jana na
viongozi wengine wote wa vyama vya
siasa wako katika sehemu zao
wamejificha wakisubiri muda ufike ili
wajitokeze na mambo yaanze rasmi.Dr
Shafi nitakuwa nikikujulkisha kila
hatua tunayopiga ninachokusisitiza tu
usiwe na wasiwasi kila kitu
kimepangwa vizuri na kila jambo
litakwenda kama vile
tunavyokusudia"
"Hizo ni taarifa njema sana
David.Mimi sina wasiwasi nawe hata
kidogo kwani najua mahala ulipo
hapaharibiki kitu.Endelea kunijulisha
kila kitu kinavyoendelea ila
nakushauri umakini mkubwa
unatakiwa hasa katika hatua hii.Polisi
wanawawinda sana hawa wanasiasa
na endapo watafanikiwa kumkamata hata mmoja wao basi wanaweza
wakamtesa na akaeleza kwamba
wewe ndiye uliyekuwa nyuma ya
mpango huu wa maandamano na
vurugu.Ikifika hapo kila kitu kitakuwa
kimeharibika hivyo viongozi hawa wa
siasa wawe makini mno"
"Hilo nimekwisha liona na
nimezungumza nao na tumewekeana
mikakati na kutokana na mipango
yetu ilivyoandaliwa hakutakuwa na
tatizo lolote.Nitawasiliana nawe tena
jioni ya leo kukujulisha mambo
yanavyokwenda"
"Nawatakia kila la heri na
mafanikio" akasema Dr Shafi na
kukata simu
Elvis akavuta pumzi ndefu na
kurudia kusikiliza tena rekodi ile kwa
mara ya pili. Dr Shafi anazungumza na David
kuhusiana na mkutano ulioandaliwa
na viongozi wa vyama vya siasa.David
anasikika akimtaja Dr Makwa kuwa
amelala nyumbani kwake akiogopa
kukamatwa na polisi.Dr Makwa ni
kiongozi wa chama kikubwa cha siasa
hapa nchini."akasema Elvis na
kunyamaza kidogo halafu akasema
"Katika taarifa ya habari leo
asubuhi nimemsikia mkuu wa jeshi la
polisi nchini akitoa onyo kuhusu
mkutano wa hadhara ulioandaliwa na
vyama vya siasa uliopigwa marufuku
na jeshi la polisi.Baada ya kuyasikia
mazungumzo haya ya Dr Shafi na
David ninashawishika kuamini
kwamba Dr Shafi na huyo David wako
nyuma ya huu mkutano ulioandaliwa
leo na wanasiasa wa vyama vya
upinzani.Kinachonishangaza ni
kwamba Dr Shafi yuko katika chama tawala iweje ashirikiane na wakuu wa
vyama pinzani kwa siri?Kuna nini
kinaendelea hapa?David ni nani?
akauliza Elvis
"Jamani kuna jambo linaendelea
hapa na taa nyekundu imeniwakia
tayari.Japo tuna masuala mengi
makubwa yanatukabili lakini
tusilipuuze suala hili.Wakati
tunaendelea kumchunguza makamu
wa rais kuhusiana na uhusika wake
katika mtandao wa silaha tuendelee
pia kumchunguza mahusiano yake na
wanasiasa wa vyama pinzani tujue
kuna kitu gani kinaendelea kati
yao?Mazungumzo haya tuliyoyasikia
yanaashiria kuna jambo ambalo si
zuri"akasema Elvis
"Elvis play that record again"
akasema Steve na Elvis akaicheza
tena ile rekodi.Steve akasikiliza kwa
makini Play again" akasema na
kuisikiliza tena
"Kuna kitu umekigundua
Steve?akauliza Elvis
"Elvis kuna jambo ambalo sikuwa
nimelitilia maanani sana lakini baada
ya kusikia mazungumzo haya
nimeanza kuliona kama lina maana"
"Jambo gani?
"Kwanza kabla ya yote naomba
nipate hii sauti ya David.Tunahitaji
kufahamu ni David yupi.Sauti hii si
ngeni kwangu lakini tunahitaji kupata
uhakika"
"Hata mimi hii sauti si ngeni
kwangu.Unahisi umewahi kuisikia
mahala?akauliza Elvis
"Elvis ninaomba dakika chache
tutafahamu kuhusu sauti hii" akasema
Steve na kuichukua simu yake ambayo
tayari Omola alikwisha muwekeakipande cha sauti ya David.Akatoka
nje na kumpigia simu Samira
"Summer baby" akasema Steve
baada ya Samira kupokea simu
"Hello my love.Vipi maendeleo
yako?
"Ninaendelea vyema
Samira.Ahsante sana kwa msaada
wako mkubwa kwa kumpeleka Omola
kwa makamu wa rais"
"Usijali Steve.Muda wowote
ukiwa na jambo lolote niko tayari
kukusaidia.Vipi kuhusu kazi zako
zinakwendaje?
"Kazi zangu zinakwenda vyema
ila ninahitaji msaada wako tena"
"Sema Steve unahitaji msaada
gani?
"Kuna faili nakutumia lifungue
halafu sikiliza sauti hiyo na kama
utaweza kuitambua niambie ni sautiya nani?Tafadhali nisaidie sana katika
hilo ni muhimu sana"
"Sawa Steve" akajibu Samira na
Steve akamtumia lile faili lenye sauti
ya David.Baada ya dakika moja Samira
akapiga simu
"Umeisikia sauti hiyo?Unaweza
kuitambua?akauliza Steve
"Hii ni sauti ya David."
"Are you sure?Steve akauliza
"yes I'm sure.Kuna nini
kwani?Hii rekodi umeitoa
wapi?akauliza Samira akionekana
kuwa na wasi wasi kidogo
"Ahsante sana Samira kwa
msaada wako huu
mkubwa.Nitazungumza nawe baadae"
akasema Steve na kukata simu
akarejea sebuleni
"Nimethibitisha sauti hii
iliyokuwa inazungumza na makamu wa rais ni sauio ya waziri mkuu
mstaafu David Sichoma"
"Exactly! akasema Elvis
"Sauti hii si ngeni kwangu na
nilikuwa najiuliza ni wapi nimewahi
kuisikia.David na makamu wa rais
wako nyuma ya mkutano huu
unaotarajiwa kufanyika leo na Dr
Makwa kiongozi wa chama kikuu cha
upinzani amelala nyumbani kwa
David.Kuna kitu gani hawa jamaa
wanakipanga dhidi ya
serikali?Hainiingii akilini watu
wakubwa kama hawa,makamu wa rais
na waziri mkuu mstaafu washirikiane
na viongozi hawa wa vyama vya siasa
kuandaa mkutano wa hadhara.Ndugu
zangu hapa kuna kitu kinachoendelea
ambacho hatuna budi kukifahamu"
akasema Elvis
"Awali niliwaeleza kwamba kuna
jambo ambalo sikuwa nimelitilia maanani lakini kwa sasa ninauona
umuhimu wake" akasema Steve na
kunyamaza akamtazama Elvis na
kusema
"Elvis sikuwa nimekueleza
kuhusu suala hili kwani ni suala
binafsi lakini kwa hapa tulipofika
nalazimika kuweka wazi kila kitu"
"Ni jambo gani hilo Steve?
"Samira ana mahusiano na waziri
mkuu mstaafu David Sichoma"
"Wow ! akasema Elvis na wote
wakawa kimya wakitazamana
"Nilipotoka kizuizini nimewakuta
wakiwa katika mahusiano na David
ndiye anayemgharamia Samira kwa
kila kitu.Kwa kuwa Samira
ananipenda sana alinieleza ukweli
kwamba yuko na David kwa sababu ya
fedha zake na si kwa
mapenzi.Nilimtaka Samira aachane na
David ili mimi na yeye tuyaanze maisha mapya lakini akakataa kwa
madai kwamba hawezi kuachana
ghafla na David kwani amemuahidi
mambo mengi.Kikubwa ambacho
ninakiona kwa sasa kina umuhimu ni
pale aliponiambia kwamba David ana
mipango ya kuwa rais wa Tanzania na
amemuahidi mambo mengi makubwa
endapo atakuwa rais na ndiyo maana
Samira hataki kuachana
naye.Mazngumzo yake na makamu wa
rais yamenifanya nione kauli hii ina
umuhmu mkubwa kwetu"
"Ahante Steve kwa jambo
hilo.Kauli hiyo ni nzito sana.David ni
waziri mkuu mstaafu amekwisha
achana na mambo ya uongozi lakini
kwa kauli hiyo anaonyesha kwamba
bado ana mipango ya kutaka
urais.Ataupataje huo urais?Hilo ni
swali ambalo tunapaswa kujiuliza.Je
anataka kuhama chama na kujiunga na chama cha upinzani na ndiyo
maana anashirikiana nao?Kama ndiyo
kwa nini basi asijitokeze na kutangaza
wazi kukihama chama chake na
kujiunga na upinzani?Kwa nini
anaongoza harakari zake chini kwa
chini na hataki ajulikane?akauliza
Elvis
"Elvis ninashauri wakati
tunaendelea na suala la akina Frank
basi tuendele pia kumchunguza David
na hapa tunaweza kumtumia Samira
kumchunguza kwani ni wapenzi na
David hajui kama Samira ana
mahusiano na mimi.Unaonaje suala
hilo?
"Ni wazo jema.Utazungumza na
Samira uone kama atakubali
kutusaidia kwa hilo" akasema Elvis
"Ktu kingine ambacho tunapaswa
kukumbuka ni kwamba makamu wa
rais ndiye alitoa amri ya mimi kuuawa,na vile vile akatoa amri Pascal
auawe na hata Vicky pia ni yeye
aliyetoa amri auawe.Tunapaswa
tufahamu kwa nini alitoa maelekezo
watu hawa wauae?Bado nina imani Dr
Shafi lazima atakuwa anahusiana na
mtandao wa akina Frank kwani haya
yote yalianza baada ya mimi kuipata
kompyuta ya Frank na kufahamu
kuhusu biashara ya silaha.Tutafute
kitu kitakachotupa ushahidi kwamba
Dr Shafi anahusiana na akina Frank"
akasema Elvis
"Kesho nitarejea tena kuendelea
na mazungumzo naye na
kumchunguza zaidi.Vile vile bado
tunaendelea kufuatilia mazungumzo
yake yote ya simu na kila baada ya
nusu saa tutakuwa tunaangalia
mazungumzo yaliyorekodiwa hivyo
msiwe na wasi wasi tutapata kila
tunachokihitaji" akasema Omola Ahsante Omola.Tuliweke hilo
pembeni na tuendele na uchunguzi
wetu.Kuna mtu amejitokeza anaitwa
Joe Gregory.Kwa mujbu wa Juliana ni
kwamba huyu ni mshirika mkubwa
wa mama yake wa biashara nchini
Marekani.Mchunguze huyu naye ili
ufahamu ni mtu wa namna gani vle
vile tuanze kumtafuta Patrice."
"Nina ushauri"akasema Omola
"Karibu" akasema Elvis
"Nashauri kwa sasa tuelekeze
nguvu katika kumchunguza Elizabeth
au Shanon au vyovyote vile
anavyojiita.Tunaweza kupata taarifa
nyingi za kutusaidia kutoka
kwake.Nitahitaji kuipata simu au
kompyuta yake niifanyie uchunguzi na
tutaweza kupata mambo mengi ya
kutusaidia.Ninawashauri ndugu zangu
tukitaka kumpata huyu Patrice na
kumfahamu ni nani basi tuwekeze nguvu kubwa katika kumchunguza
Elizabeth.Nina uhakika mkubwa
lazima anawasiliana na Patrice"
akasema Omola
"Hilo ni wazo zuri japo tutakuwa
tumemuweka Juliana katika hatari
kubwa na hasa kwa wakati huu ambao
mama yake tayari amekwisha anza
kumtilia mashaka kufuatiwa
kutumiwa picha akiwa na Meshack
Jumbo" akasema Steve
"Ni kweli yuko katika hatari
lakini hatuna namna lazima atusaidie
kuweza kumchunguza mama
yake.Ninaamini atakubali kufanya
hivyo kwani hata yeye anahitaji
kumfahamu mama yake na mambo
yake ya siri anayoyafanya.Naamini
tukimuomba atakubali kutusaidia"
akasema Elvis
"Sawa Elvis.Nitazungumza naye" Nitalazimika kwenda nawe
wakati unazungumza naye kuna
mambo ambayo nitapenda
kumuelekeza" akasema Omola
"Vipi kuhusu Joe
Gregory?Umekwisha anza
kumchunguza? akauliza Elvis
"Nimemtumia barua pepe rafiki
yangu wa nchini Marekani anisaidie
kupata taarifa zake.Atanipa majibu
ndani ya muda mfupi " akajibu Omola
"Guys msimame kidogo mpate
chochote cha kuweka tumboni.Toka
asubuhi mmekuwa mkifanya kazi na
mmesahau kabisa kama miili yenu
nayo inahitaji kuhudumiwa" akasema
Graca aliyeingia pale sebuleni akiwa
na sinia lenye mabakuli ya supu
"You are so fast Graca" akasema
Omola akichukua bakuli lake la supu
na kila mmoja akachukua lake.Wakati
wakiendelea kupata supu ukasikikamlio katika kompyuta ya Omola
akaangalia na kusema
"Majibu yamekuja" Omola
akaifungua barua pepe ile akaisoma
"Tumekipata tulichokuwa
tunakihitaji" akasema Omola
"Kwa mujibu wa taarifa
nilizozipata kuhusu Joe Gregory ni
kwamba huyu ni mwanajeshi mstaafu
na kwa sasa anajishughulisha na
biashara mbali mbali.Amewekeza
katika biashara za
migahawa,anamiliki pia meli kubwa za
mizigo,kwa ujumla Joe ni mtu
tajiri.Ukiwataja matajiri wa Marekani
na Joe huwezi kukosa kumtaja"
akasema Omola akameza mate na
kuendelea
"Masuala ya utajiri wake sisi
hayatuhusu lakini kuna hili moja
ambalo naamini linatuhusu sana
sisi.Joe anamiliki kiwanza cha kutengeneza bunduki kubwa na
ndogo.Katika kiwanda hicho
anatengeneza bunduki za kawaida na
hata zile za kivita.Kwa maelezo haya
tayari tunapata jibu kwamba Elizabeth
anapata silaha kutoka kwa Joe ambazo
huja kuziuza kwa waasi.Inawezekana
vile vile kwamba silaha nyingine
zinakuja kufanyiwa majaribio kwa
waasi ili kujua ubora wake"
"Oh Ahsante Mungu" akasema
Elvis
"Picha inazidi kujiunganisha na
muda si mrefu tutapata picha kamili
nani na nani wamo katika mtandao
huu wa biashara ya silaha.Nani
wanafaidika kutokana na damu isiyo
na hatia ya wananchi wa Congo
inayomwagwa na waasi wanaouziwa
silaha na mtandao huu wa akina
Frank.Watu hawa tuliowafahamu si
peke yao bado kuna wengine ambao lazima tuendelee kuwatafuta na
kuwafahamu.Wote lazima walipe uovu
wao.Huko waliko wafahamu kuwa
siku zao zinahesabika.Kama
alivyoshauri Omola nguvu kubwa kwa
sasa tuielekeze katika kumchunguza
Elizabeth ili tuweze kumfahamu huyu
Patrice ni nani hasa yuko wapi na
mahusiano yake na waasi wa
Congo.Vile vile tuendelee
kumchunguza makamu wa rais tujue
kama naye anahuska katika mtandao
huu.Wakati huo huo David naye
aendelee kuchunguzwa kama
tulivyokubaliana.Hatuhitaji kupoteza
muda mpigie simu Juliana muulize
kama amefanikiwa yale tuliyomuomba
atusaidie na vile vile na umjulishe
kuwa tunahitaji kuonana naye tena"
akasema Elvis na Steve akampigia
simu Juliana akamuomba
waonane.Steve na Omola wakaingia garini wakaondoka kwenda kuonana
na Juliana
"Bado natafakari kwa nini David
na Dr Shafi wahusike katika mkutano
wa vyama vya siasa vya upinzani na
kibaya zaidi ni kwamba licha ya
kwamba mkutano huu umepigwa
marufuku lakini bado wanaendelea
kuufadhili ufanyike.Kuna kitu gani
wanakitafuta hawa viongozi?Je
wanataka kujiunga na vama vya
upinzani?Kama ni hivyo kwa nini
wasijiunge kwa uwazi kuliko kufadhili
mikutano kama hii ambayo ni wazi
itasababisha vurugu?Steve anadai
kwamba David ana dhamira ya
kuwania urais,je hizi ni harakati zake
ameanza za kutaka kujirudisha katika
siasa kwa kufadhili mkutano huu wa
leo?akajiuliza Elvis akiwa sebuleni
peke yake baada ya akina Steve
kuondoka
Sent using
Jamii Forums mobile app