RIWAYA:JANGA
MTUNZI: Richard MWAMBE
SEHEMU YA 16
Daktari Jasmine, aliondoka na kwenda Marekani kwa ajili ya masomo ya ziada katika kituo cha uchunguzi cha John Hopkins, safari yake ya kwenda huko ilikuwa ni ya kikazi ili kuboresha zaidi idara hiyo katika kazi zake. Lakini pia kulikuwa na mvutano kati ya Madam S na Rais wan chi kuhusu daktari huyo kijana. Ikulu ilimtaka awe daktari wa Rais pia awe katika moja wa walinzi wake wa karibu. Madam hakukubaliana na hilo kutokana na kwamba kitengo chake kingekuwa na kazi ngumu ya kumpata mtu mwingine nah ii ni kwa kuhofia uvujaji wa siri nyingi za kitengo hicho nyeti.
“Nimerudi Madam!”
“Good, umerudi na kazi ipo mezani, ukiimaliza ndipo nitakupa likizo,” Madam S akamwambia, kisha akavuta droo nyingine na kuto faili, akamkabizi mwanadada huyo. Jasmine akalitazama kwa kuligeuza na juu ya jalada kulikuwa na maandishi makubwa ya wino mweusi, JANGA. Akalifungua na kuanza kulisoma taratibu huku, Amata na Madam wakiendelea na habari nyingine kabisa.
Katika ukumbi mkubwa wa chakula, ndani ya Hoteli ya Serena, Gina alikutana na mwenyeji wake ambaye mchana wa siku hiyo walikutana pale Mahakama ya Kisutu. Huyu alikuwa mwendesha mashitaka wa serikali, mtu mzima lakini alionekana wazi kuwa ni mpenda ngono, rushwa ya ngono ili akusaidie. Mara baada ya kupewa namba na Gina mchana ule, akaona wazi kapata kimwana, na alichanganyikiwa zaidi aliptazama ubarikio alioupata Gina sehemu za nyuma za mwili wake.
Simwachi! Akajisemea moyoni na jioni hiyo akampigia simu akimtaka wakutane Serena. Serena? Ndiyo Serena, kwa sababu alikuwa na mambo mawili kwa msichana huyo ambayo yeye mwenyewe Gina alijua moja tu, kutafutaiwa kazi.
Alifika mapema, akapanga chumba kwa Dola 200 kwa usiku mmoja akijihakikishia kumpata mrembo huyo.
Kazi atapata tu, ila lazima nifaidi kama kwa wale wengine, akajisemea na kujiaminisha. Rushwa, rushwa ya ngono, wanawake wengie wananasa katika rushwa hii wakiahidiwa kazi, wapo wanaopata na wengine wanaishia patupu na kubaki kutumiwa na huyu na yule pasi na wao kugundua kuwa ni mchezo. Hili ni janga lingine, janga kubwa kwa dada zetu, vyuoni hawasomi kazi kwenda disco, akitegemea kumpa penzi mwalimu ili apate alama za juu na GPA za maana, ngono. Anapomaliza chuo cheti chake kinamuuza kuwa ni mwenye akili, kumbe mbumbumbu, ‘kiuno’ ndiyo CV yake, janga.
Gina aliingia katika hoteli hiyo majira ya saa mbili akisingizia usafiri ulikuwa shida kutoka kwa Gongo la Mboto. Mwenyeji wake alikuwa tayari.
“Karibu sana miss…”
“Miss Rose!” akadanganya jina, “Subiri kidogo, tunaketi wapi?” akauliza.
“Aaaa kwenye ukumbi wa chakula, kuna tatizo?”
“Hakuna tatizo, ila mimi hupenda kuwa muwazi sana, mimi navuta sigara, hivyo naomba nivute hapa moja kisha tuingie huko,” Gina akamwambia mwenyeji wake ambaye mpaka hapo alikwishamsoma mawazo yake.
“Sawa!” akajibiwa.
Gina akachukua kijikebe kidogo katika pochi yake, akachomoa sigara moja na kuiwasha kisha akapiga pafu nne tu akaimaliza.
“Twen’zetu!” wakaingia ndani ya ukumbi huo.
Hakukuwa na watu wengi, taa za rangi ya dhahabu zilipendezesha ukumbi huo kwa kupenyeza miali yake katika mapambo yaliyotengezwa kwa vioo vya mikato mbalimbali. Hatua kama ishirini hivi ziliwafikisha wawili hao katika meza ndogo yenye viti viwili vya kupendeza.
“Kula unachotaka,” Gina akaambiwa.
“Aii jamani, mambo mengine haya wenzenu ushamba,” Gina akajibu huku akishangaashangaa huku na kule.
“Enhe mrembo…”
“He mrembo tena, usiniite hivyo, jina langu Rose,” Gina akaongea kwa aibu.
“Aaaa usihofu, hilo ni jina tunalowaita wasichana wote wenye uzuri asili kama wewe! Nami naitwa Dastan Majoti,” yule jamaa akaongea kwa sauti nzito na laini.
“Mmh, nambie, mpaka sasa hujapata kazi, umenishangaza sana,” yule jamaa akaanzisha mazungumzo.
“Kazi ngumu baba ‘angu, nimeomba weeeee lakini nazungushwa tu,” Gina akazungumza kwa huzuni.
Vyakula vikaja na vinywaji vya kutosha, pombe kali zilikuwepo, Gina aligundu kuwa huyo mwenyeji wake anammezea mate kwa jinsi alivyokuwa akipepesa macho yake na kushindwa kumtazama mwanamke huyo usoni.
“Hongera, nimeona unavyounguruma mahakamani,” Gina akamwambia huku akijifanya kama pombe inataka kumchukua. Majoti akastuka kidogo na kumtazama mwanadada huyo.
“Aaaa kawaida tu, mimi wananitegemea sana kwenye kesi ngumu kama hizi…”
“Lakini uelekeo unauonaje, wanashinda au la?” Gina akauliza.
“Aaaa wanashinda wale, kwa sababu serikali haina ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani,” Majoti akajibu.
“By the way ulikuja kufanya nini pale?”
“Nilikuja kumcheki rafiki yangu Sauda, nimesoma naye Mlimani,”
“Oooh good! Nitakusaidia, na utapata mara moja. Unapenda serikalini au kwenye ofisi binafsi?”
“Serikalini,” Gina akajibu.
Danstan Majoti, akatikisa kichwa juu chini kuashiri kuwa ameelewa, akameza funda moja la mate, akainua simu yake na kubofya tarakimu kadhaa kisha akaweka sikioni.
“Eh, Comrade, habari za siku?” Majoti akamsalimia mtu wa upande wa pili.
“Nipo kabisa, umepotea sana vipi hujapata kimeo?” upande wa pili ukauliza.
“Hapana, kuna mdogo wangu asee vipi utumishi hapo univushie,”
“Keshatuma barua?”
“Bado,”
“Mwambie alete kesho saa nne, anikabidhi mwenyewe mkononi,” upande wa pili ukajibu.
Dastan akakata simu na kuiweka mezani. “Kazi imekwisha mtoto mzuri!” akamwambia Gina.
“Yaani kirahisi tu!” akashangaa na kutamka kwa sauti.
“Yeah, haya mambo tunajua wenyewe tunavyocheza, ila kama hujui, utazungukaaaa we na mabahasha yako hupati chochote, utatuma maombi mpaka stamp ziishe posta, utabaki hapo hapo,” Majoti Dastan akajigamba. Gina akasikitika moyoni kusikia hayo, akasikiri ni vijana wangapi wanaoteseka kutembea maofisini kutapeliwa pesa na wajanja wanaojifanya watawapa ajira lakini wanabaki hawana kitu.
Rushwa ya kila aina ilikuwa inaziba haki za wananchi, pesa, ngono na mengine kibao.
“Nitatakiwa kukupa shi’ngapi?” Gina akauliza.
“Ingekuwa nahitaji pesa kwako nisingekuita hapa Rose…”
“Kwa hiyo unanisaidia tu?” Gina akachokonoa.
“Aaaa msomi wewe, unaelewa mazingira, sikutaka pesa kutoka kwako kwa sababu najua nawe unatafuta pesa kwa kuwa huna ajira”.
“Aiii jamani, sijui nikulipe nini mimi…”
“Usiumize kichwa, msaada tu wa kibinadamu, maisha ni kusaidiana Rose, nimekodi chumba hapo juu, nategemea hutoniangusha japo kwa usiku mmoja tu,” Majoti akaongea lugha iliyosafirisha ujumbe wa mapenzi, Gina akamtazama mtu mzima huyo kwa jicho pembe, alilitegemea hilo.
“Unajua Rose, hii kazi yetu inalipa, akiingia mjinga unapiga hela. Nakuhakikishia mwezi ujao tu unaanza kukunja kitita chako. Kama hii kesi ya leo tumepiga hela ndefu sana, ndefu sana yaani, mi sasa ninja nyumba tano, gari nne za kutembelea, nalala nnapotaka,” akajieleza, tayari kinywaji kilikuwa kikifanya kazi.
“Asee, ila mi nilisikitika juu ya Shekibindu, nilikuwa nampenda yule baba!”
“Aaaa yule mzee mjinga mpaka umri ule alikuwa anakaa nyumba ya serikali, mi nilikuwa sipendi kufanya kazi naye yaani hupati pesa. Sikiliza, hii kesi alishika yeye, alikuwa haingiliki, alipokufa aaaa kila mtu akasema afadhali, akachukua rafiki yangu Tulabayo, siku nne tu mipesa hii hapa, watashinda kesi watatambaa zao,” Majoti akabwabwaja bila kujua anayeongea naye kuwa ni moja Polisi, mbili Usalama wa Taifa, TSA 5, kwa ujumla alikuwa ni mtu hatari kuliko hatari yenyewe.
“Nimechoka, nahiyaji kupumzika!” Gina akajilegeza na kuyashuhudia meno meupe ya Majoti yakionekana baada ya kukenua kwa furaha ya kusikia neon hilo.
“Hata mimi pia, twende tukapumzike bebi,” akalalama.
“Ai jamaani, usiniite bebi, nina mchumba mimi…”
“Aaaa hakuna mchumba asiyetaka maendeleo, twende,” Majoti akasimama huku kidogo akiyumba, wakakokotana na Gina huku mtu mzima yule akijitahidi kupapasa mtiti ya Gina. Chumba kikubwa, ghorofa ya pili, Majoti akafungua mlango kwa taabu kidogo, kila mara alikuwa akishindwa kutumbukiza funguo mahala pake.
“Hah! Hah! Hah! Aaaa unashindwa kulenga tundu la ufunguo, na vingine utaweza?” Gina akamtania.
“Aaa hii ni funguo, vingine hata gizani nalenga…” wote wakaangusha kicheko na mlango ukafunguka. Moja kwa moja wakaangukia kitandani na kubiringishana.
“Rose unaonekana unayaweza ee?”
“Yaani leo utashindwa wewe, na hizo pombe zako, utazimia,” Gina akamwambia. Majoti akamkumbati Gina kwa nguvu pale kitandani, akapeleka kinywa chake kwa mwanamke huyo, Gina akafanya kama anaupokea ulimi wa huyo bwana.
“Subiri! Hivi watu wanasema kuwa Shekibindu ameuawa ni kweli?” akauliza
“Aaaaaa Rose!!! Swali gumu hilo,”
“Nijibu bebiiiii!” Gina akambembeleza huku mkono wake ukilipapasa dume hilo kwenye dhakari yake.
“Oooh! Rose, aaaaah! Polepole mama. Ni kweli jamaa walimfanyia mpango. Shhhhhh! Nikisikia umemwambia mtu nakumaliza,” Majoti akajikuta akijibu bila kipingamizi. Achana na mapenzi bwana, ukibanwa kitandani utajibu na kutoa kila siri, Gina aliitumia nafasi hiyo kwa kuuliza maswali ya kutosha na yote akapata majibu sawasawa.
“Mtandao ni mkubwa na kila watu wana kazi yao,” akamalizia kusema. Mara simu ya Gina ikaanza kuita kwenye mkoba wake.
“Samahani!” akamwambia kisha akachukua simu yake na kuitazama.
“Nani?”
“Mchumba wangu!”
“Mwambie upo kwenye usahili wa kazi…”
“He! Kumbe huu ni usahili!” Gina akajifanya kushangaa huku akiifyatua ile simu.
“Hello!”
“Uko wapi mrembo wangu?”
“Nipo kwenye usahili wa kazi, nitachelewa kurudi,”
“Ok sawa!” Amata akajibu upande wa pili, akajua tu kwa vyovyote Gina kuna kazi nyeti anayoifanya.
“Sasa baby, wapi tena?” Majoti alimwambia Gina, wakati mwanadada huyo alipotoka kitandani na kuelekea bafuni.
“Najiweka, sawa tuanze mambo au siyo? Nawe jiandae basi,” Gina akmwambia kwa sauti ya deko iliyomtekenya mwanaume huyo mpaka kwenye nyayo.
Gina akaingia bafuni, akafunga mlango kwa ndani, na kushusha pumzi, akachomoa kifaa cha kurekodia sauti, akakikuta bado kinafanya kazi, akasevu faili, akakizima na kukificha kwenye sidiria kama mwanzo, akatoka bafuni na kumkuta jamaa tayari kabaki na bukta.
“Uko tayari kwa mchezo?” Gina akauliza.
“Karibu kitandani!” Majoti akajibu na kuivuta shuka karibu.
“Ok!” Gina akajibu, akavua fulana na kubaki na sidiria na jinzi aliyovaa, akamtupia jicho Majoti na kumkuta katumbua macho.
“Fanya haraka, nazidiwa mwenzio,” Majoti akasisitiza.
“Usiwe na haraka, utakula mpaka utasaza,” Gina akajibu, akauendea mkoba wake, akachukua kimkebe chake cha sigara, “Naomba nivute kidogo, nipate stimu!” akamwambia huku akiketi kitandani.
“Bila shaka!”
Gina akaketi kitandani, Majoti, akaamka na kukaa jirani yake huku mkono wake akiwa kauzungusha kiunoni mwa mrembo wake; akachukua sigara na kubana kwa midomo yake, akachukua kiberiti na kukiwasha, sekunde mbili tu ile sigara ikawa imewaka. Akaibana kwa vidole na kuitoa kinywani, akamtazama Majoti usoni, akarudisha sigara kinywani na kuvuta pafu moja kubwa, kisha akampulizia moshi mtu mzima huyo usoni. Kilichofuata hapo ni vikohozi mfululizo kutoka kwa Majoti.
“We vipi?” Gina akauliza.
“Nimepaliwa na sigara yako, koh! Koh! Koh!” akazidi kukohoa. Gina akainuka na kujifanya anakwenda kuizima sigara hiyo, “Samahani!” akamwambia. Alipogeuka nyuma alimkuta mtu yule kajibwaga kitandani anathema kwa nguvu, Gina akamrudia na kumtazama.
“Samahani sana, sikujua kama moshi unakudhuru,” akamwambia na kumpulizia tena, Majoti akahisi kama anakabwa, akakosa pumzi, macho yakawa mazito, akazidiwa na kuchukuliwa na usingizi mzito. Gina akavaa fulana yake, akainua mkoba wake na kupotelea nje. Tayari ilikuwa saa tano usiku alipokuwa nje ya hoteli hiyo.
ITAENDELEA