Riwaya: Janga

Riwaya: Janga

RIWAYA: JANGA

MTUNZI: richard MWAMBE



Kontena zilizobaki zilizuiwa bandarini kwa uchunguzi, watu wakapiga kelele, waandishi wakaandika, hapo ndipo Mustafa Bashiru alipopata umaarufu kwa kisa hicho, alichimbachimba, akaweka vitu hadharani, Watanzania wakafunguka macho. Vipodozi hivyo vyenye sumu viliingiaje madukani? Wakajiuliza. Kwani serikali na idara ya ukaguzi wa ubora wa bidhaa za kutumia binadamu zilikuwa wapi wakati haya yote yakitokea? Maswali hayo na mengine mengi hayakupata majibu. Mahakama ikaamuru kontena hizo zisiingie kwenye mzunguko wa matumizi ya binadamu, kesi ikaunguruma, ikiwa hukumu inakaribia, Jaji aliyekuwa na dhamana ya kesi hiyo akafa kwa ajali ya gari pale Mnazi Mmoja, utata.



SEHEMU YA 11



Miezi mitatu iliyopita…

“Mr Mwakitalu, umeshakamilisha mchakato wa vile vipodozi?” Mkurugenzi katika kitengo cha uchakataji wa viwango vya bidhaa mbalimbali Bwana Kajaze akamwuliza kijana wake.

“Ndiyo, imekamilika lakini kuna tatizo kubwa, ile bidhaa haifai kabisa kutumika na binadamu, lazima iteketezwe yote,” akajibu.

“Kweli?”

“Kweli kabisa, tazama karatasi hizi,” akamwonesha, “Haya ni matokea ya kipi kimepatikana, kuna kemikali mbaya sana, ambazo zikifika kwenye mwili wa mwanadamu, atadhurika vibaya yaani nashindwa kueleza,” Mwakitalu akakaa vyema kitini.

“Sawa, sasa subiri kidogo, kaa na hivyo vipimo kisha nitakupa maelekezo ya nini cha kufanya,” kajaze akamwambia Mwakitalu.

“Khaa! Inamaana kuna maelekezo mengine zaidi ya kuteketeza?”

“Nimekwambia subiri upate maelekezo mengine,” Bwana Kajaze akasisitiza.

“Ok, basi majibu haya hapa!” akampatia zile karatasi na kuondoka zake. Bwana Kajaze akajishika kichwa na kuipitisha mikono yake kuanzia utosini mpaka kisogoni, akashusha pumzi na kutulia. Baada ya kama dakika tano za kufikiria, akainua simu yake na kupiga namba fulani.

“Ee Mheshimiwa, nahitaji kukuona kidogo, ile results imetoka,” akamwambia mtu wa pili.

“Ok, njoo afisini, nakusubiri,” yule Mheshimiwa, upande wa pili akamwambia.

Dakika thelathini baadae….

Bwana Kajaze, akaketi kwa mtindo wa kutazamana na Mheshimiwa Waziri Thomas Kalembo katika afisi yake iliyoko katikati ya jiji. Kila mmoja alikuwa kimya kabisa bila kuongea lolote. Kalembo akajikohoza na kukata kimya kile.

“Unajua pale kuna pesa nyingi sana ambayo hatuwezi kuiacha ipotee, lazima mzigo huo uingie sokoni piga ua. Naomba umwambie mkemia wako abadilia hiyo taarifa ili ile bidhaa ipate kibali cha ubora na kutumika,” Kalembo akaeleza na wakati huo huo mlango ukafunguliwa, watu wawili wakaingia na kuketi jirani katika makochi yaliyokuwa ndani ya afisi hiyo.

“Karibuni wadau,” Kalembo akawakaribisha watu hao walioonekana kutakata kwa pesa. Kajaze akawatupia macho na kuona kuwa walikuwa Watanzania wenye asili mbili tofauti. Kalembo akawaeleza kwa kifupi juu ya taarifa ile ya mkemia wa idara ya viwango.

“Sasa sisi iko nafanyaje?” mmja akauliza

“Tumeweka fesa nyingi bhana pale, fanya kitu bhana wewe ni mkubwa serikalini na kumbuka nawe umeweka chchte bhana, nataka mali ile teketea bure?” akalalamika yule Mhindi.

“Hapana, ndiyo maana nikawaita,” akawatoa hofu, kisha akamtazama yule mkurugenzi.

“Hawa ndiyo business partiners wangu, ambao sote kwa pamoja tunamiliki ule mzigo, na wewe ni mtu wa kwanza kujua hilo hivyo funga kinywa chako,” akavuta mtoto wa meza na kuchomoa bahasha iliyonona akamkabidhi Bwana kajaze.

“Hizi ni milioni kumi, kahakikishe hayo majibu yamebadilika kwa sababu tuntaka tuanze kujenga mazingira ya utoaji zile kontena,” akamwambia na kumkabidhi. Kwa mikono iliyojawa kitetemeshi akapokea bahasha ile huku akisitasita.

“Usihofu kijana, kamata mshiko kajenge maisha na wenzio, Waswahili tunasema penye udhia penyeza rupia, nafikiri umenielewa,” akamwambia.

“Ndiyo mheshimiwa,”

“Ok utanipa mrejesho, waweza kwenda,” akamruhusu na Yule bwana akaondoka na kuwaacha watatu mle ndani.

“Msiwe na wasiwasi, hili litaisha tu,” akawaambia.

“Aaah sisi hapana shida kabisa, naamini wewe,” yule Mhindi akamjibu kwa furaha.

“Vipi kule forodhani mmekamilisha?” akawauliza.

“Aaa tayari tumeongea na ile bwana ya ushuru, imesema hamna tabu kabisa, hatutalipa isipkuwa tumtafutie ya boga tu, tukamalizana naye badala ya ushuru kuwa milioni miambili sasa mempa yeye milioni ishirini keshasini document hii hapa, tazama,” wakampa ile dkument akaitazama na kutabasamu.

Hii ndiyo nchi yetu bwana, mambo yanakwenda tu ilimradi uwe nazo basi, Kalembo akawaza huku akijikuna tumbo lake. Mazungumzo machache yakwafanya wale mabwana waweke mambo yao sawa.

Bwana Kajaze aliketi afisini kwake huku mikguu yake ikiwa katika mtindo wa 4, mluzi uliotoka kinywani mwake hata haukuwa na mpangilio sawasawa. Sura yake mara ilikuwa na shaka na mara ikawa na furaha ilimradi tu ilibadili mwonekano wake, akachukua simu ya mezani na kubofya tarakimu kama tatu hivi na kuiweka sikioni.

“Eee Mwakitalu, una ratiba gani jioni hii?” akaongea na mtu wa upande wa pili.

“Aaaa nikitoka hapa mi ni nyumbani tu,”

“Tunaweza kuonana sehemu? Maana hata siku moja hatujawahi kukaa pamoja,” akamwambia.

“Aaa ni kweli, lakini si unajua tena mimi na wewe madaraja hayafanani hivyo hata vijiwe vya kuketi havitafanana,”

“Tuyaache hayo, tuonane Club Africando Mwnanyamala Komakoma kuna mambo tuzungumze kidogo,” akamwambia.

“Bila shaka mkuu!”

CLUB AFRICANDO – saa 1:17 usiku

Mwakitalu aliegesha gari yake nje ya ukumbi huo na mara tu baada ya kuizima injini, alijikuta kazungukwa na ma-dada poa waliovaa kihasarahasara wakimtangazia biashara ya ngono.

Haya ndo mi siyataki daima, akawaza huku akipenye kati kati yao na kupotelea ndani ya kilabu hiyo. Watu walikuwa ni wengi sana waliokuwa wakipata vinywaji, nyama choma na mambo mengi yanayozunguka maeneo kama hayo. Mwakitalu akavipita viti kadhaa na kupenya katika moja ya kichochoro kisha akaingia katika mlango wa kioo kizito uliopambwa kwa maneno VIP.

“Oh karibu kijana!” Kajaze akamkariisha huyo bwana huku akimwonesha kiti cha kukaa. Pembeni ya mkurugenzi huyu kulikuwa na mwanamke wa haja, aliyeumbwa akaumbika, sura nzuri iliypangwa vyema, midomo mipana na macho ya kusinzia, ukimwona harakaharaka kama ametulia bila kujitikisa basi unaweza kujua kuwa amechorwa lakini sivyo.

Hivi hawa binadamu wapo? Mwakitalu akajiuliza huku akijiweka sawa lakini jicho lake halikubanduka kabisa kwa mwanadada huyo, paja lililjaa nyama lilikuwa ikimetameta kwa mafuta na harufu ya manukato iikijaza chumba hicho. Sasa mtu kama huyu akijipaka vile vipodozi si ndiyo atapululuka uzuri wote na mwisho nyama ya udongo, akajiseme anfsini mwake.

“Mwakitalu mbona kama haupo vile?” Kajze akamwuliza.

“Aaa nipo mkuu si unajua macho yalikuwa yakipata burudani kidogo…”

“Anhaaa kwa huyu motto mzuri, aaaa usijali humu ndani wapo wengi ukitaka tu unaitiwa,” Kajaze akamtaka yule mwanadada kuwapisha kidogo ili wafanye mazungumzo yao. Akanyanyuka na kuondoka, akawaacha wawili wale mle ndani.

“Ndiyo kiongozi nimeitikia wito, inaonekana kuna jambo zuri kaka,” Mwakitalu akaanzisha mazungumzo.

“Sure! Hivi ile taarifa uliyonionesha nani mwingine ameiona kwa pale kazini?” Kajaze akauliza.

“Hamna, baada tu ya kukamilisha zile sampuli na kupata matokeo nikakuletea wewe,”


ITAENDELEA
 
RIWAYA: JANGA
MTUNZI: Richard MWAMBE
SEHEMU YA 12
ILIPOISHIA…


“Hamna, baada tu ya kukamilisha zile sampuli na kupata matokeo nikakuletea wewe,”
ENDELEA

“Good!” akaingiza mkono katika mfuko wa koti lake na kutoa bulungutu la noti nyekundu nyekundu tupu.
“Milioni kumi hizo hakikisha ile ripoti imebadilika ndani ya saa nane kuanzia kesho saa mbili asubuhi,” Kajaze akamwekea mbele zile pesa zilizobanwa vyema kwa rababendi. Mwakitalu akabaki anashangaa pasi na kusema lolote. Hakujua achukue au asichukue.
“Za nini hizi?” akauliza.
“Acha ujinga wewe! Hizo ni za kununulia wino wa kubadilisha ile dokumenti, kwani ni mara ya kwanza wewe kupokea pesa?” Kajaze akamwambia na kumtwanga swali. Kumbe watu hawa ilikuwa ni mara nyingi kwao kupokea pesa na kupitisha vyakula au dawa zisizo na ubora kwa wananchi. Baada ya muda wananchi wakianza kujenga makaburi ya ndugu zao, wao wanajenga majumba mapya na makubwa. Wananchi wakinunu marumaru za makaburi ili ndugu zao walale kwa amani, wao wanabandika maraumaru chooni, jikoni na kila wanapopataka.
Rushwa, rushwa ni adui wa haki, nchi zetu zinakosa huduma za msingi kwa sababu ya mdudu rushwa, nani atajayethubutu kumkemea na kumwangamiza? Badala ya kumwangamiza unajikuta unaangamizwa mwenyewe, janga. Madawa mabovu, vyakula vibovu, vipodozi hatari vyote vinawafikia wananchi na kuwaangamiza vibaya. Vinapitaje bandarini, vinathibitishwaje kwenye viwango kabla ya mwanadamu kutumia? Rushwa. Mbaya zaidi, watumiaji wakishatumia, wakapata madhara, wakienda hospitalini majibu hayabadiliki.
‘Dawa hatuna nendeni mkanunue duka la pale sokoni’ muuguzi atakwambia, ukijiangalia pesa yako haitoshi, basi, mgnjwa wako atafumba macho na kusema buriani. Ukijaaliwa kufika dukani hata leseni si ajabu usiione, kama ukiiona basi tazama jina la mmiliki, ni yule yule aliyekwambia ‘kanunue dawa paleeee’, tutafika?
“Kiongozi hili janga,” Mwakitalu akamwambia Kajaze.
“Kivipi?”
“Sikatai, mara nyingi pesa huja, na tunapitisha mzigo, lakini mizigo ile huwa haina madhara sana kama huu. Mkuu hili ni anagamizo, yaani tukiingiza hii kitu tunatengeneza janaga baba, tutakula pesa, sawa, lakini hapo kuna kifungo. Hii kontena yote ni mbovu kiongozi,” Mwakitalu akalalama kwa sauti ya wastani.
“Naona usharidhika na maisha Mwakitalu. Hizi biashara za wakubwa kijana, unakataa hii pesa, utabadili hiyo dkumenti kwa vitisho tena bure, si unawajuwa madigala wakiamua. We funika kombe mwanaharamu apite,” Kajaze akashawishi.
Chukua pesa hiyo! Oh no janga hilo kaka, utaingia mkenge. Sauti hizo zilibishana ndani ya moyo wa Mwakitalu, zikagombana na kuvutana mashati, hazikupata muafaka zaidi zilimfanya mwenye mwili huo kuzidi kuchanganyikiwa. Nyumba yako haujamaliza, mawazo yake yakamkumbusha. Ile gari uitakayo muda wowote itapakiwa melini kama ukiichukua hiyo pesa, mawazo yakamshawishi.
“Aaaaaaaa ok!” akakubali na kuvuta kile kitita, akakipachika mfukoni.
“Naomba niende!” akamwambia Kajaze.
“Hunywi kidogo?”
“Aaaah nimeacha siku hizi. By the way, tutaishughulikia kesho, na kila kitu kitakuwa ok,” Mwakitalu akamwambia Kajaze na wakati huo tayari alikuwa keishasimama. Wakaagana na Bwana Kajaze yeye akabaki kuendelea kuponda raha.
Haikuwa kazi kubwa siku iliyofuata kubadili dokumenti zile, Mwakitalu alibonyeza hapa na pale na kifaa chake cha kuprinti kikato karatasi kama ile isipokuwa tu hapa na pale palibadilishwa. Akavuta kibompoli chake na kusaini dokumenti ile kisha akaipeleka kwa bosi wake ambapo ilipokelewa kwa bashasha.
Bwana Kajaze akaikagua, iko sawa, naye akavuta peni na kuisaini.
“Safi sana kijana, mambo ndiyo haya,” akamwambia na kumpa mkono kisha Mwakitalu akaondoka zake.
Umefanya nini? Akahisi kama mtu akimuuliza lakini kila alipogeuka hakumwona, kwa nukta kadhaa nafsi yake ikahangaika sana kwa kile alichokifanya lakini basi hakuna jinsi kama ni maji yeshamwagika.

Rejea Vingunguti …
Kile alichokuwa akikisubiri Amata kikatukia, geti likafunguliwa kama mida ya saa kumi na nusu hivi. Jeepe Cherokee ikaibuka kutoka ndani na kuikamata Barabara ya Nyerere. Akawasha gari na kukunja kulia, akaambaa na barabara ya pembeni mpaka maeneo ya Kalakana, pae akaingia barabara jubwa na kujikuta jirani kabisa na gari ya yule amtafutaye. Dakika tatu tu, taa zikaruhusu, msafara ukaondoka. Tazara, ile Jeep ikakunja kushoto na kuchukua Barabara ya Mandela na ilipofika Buguruni ikakunja kulia na kukamata Barabara ya Uhuru mpaka Ilala Boma, pale ikakunja kushoto na kuchukua Barabara ya Kawawa kuelekea Magomeni. Muda wote huo Kamanda Amata alikuwa nyuma ya gari kama mbili hivi akiifuata hiyo ya huyo mdosi. Nusu saa iliyofuata ile gari iakegeshwa katika Hoteli ya Bushtreka.
“Bushtreka!” Amata akajisemea mwenyewe na wakati huo kama hakuyaamini macho yake kwa kumuona Gina akipita kidogo na kumpita pale pale akasimama kama mita hamsini mbele karibu na gereji ya Wachina.
Kila mmoja alibaki katika gari yake, hakuna aliyeteremka, ni macho tu yaliyokuwa yakitalii huku na kule. Amata akachukua kijitabu chake na kuandika mambo kadhaa kisha akawasha gari tayari kuondoka kwani hakujua watu hao watamaliza saa ngapi.
“Piiiii!” honi kali za gari kutoka nyuma yake zikapiga kumwashiria kuwa kuna gari. Akageuka na kuitazama, Toyota Prado nyeupe ilikuwa ikiingia katika maegesho ya ndani kabisa na kisha akashuka Mheshimiwa Kalembo na kupotelea ndani ya hoteli hiyo.
“Huyu mzee anafuata nini huku?” Amata akajiuliza kwa sauti lakini hakupata jibu.
“Hapa si pa kuondoka, inawezekana kuna misheni inayosukwa, huko huko leo, hata kama sina njaa nitakula tu,” akajisemea kwa sauti ya kujisikia mwenyewe na kushuka kwenye gari.
Gina naye akamwona Amata akashuka, akampa kama dakika mbili hivi kisha nay eye akashuka na kumfuata, akapita kwenye ukorido mrefu na kutokea kwenye ukumbi nadhifu wa chakula. Ni watu wachache tu waliokuwa katika ukumbi huo, Gina akamwona Amata kwa mbali, akatabasamu na kumfuata, baada ya kuomba ruhusa ya kuketi na kuruhusiwa, Gina akajibweteka kitini na kuagiza chakula.
“Vipi?” Amata akaulza.
“Safi, umemuona mheshimiwa?” Gina naye akauliza.
“Yap, ndiyo maana nimeshuka kuja kujua yuko na wajamaa au vipi, maana huyu naye kwa urafiki wa mashaka hajambo!” Amata akaongezea.
“Ndo hivo,”
Amata na Gina walikuwa pale wakizungumzia mambo mengi sana juu ya sakata hilo na mengine mengi waliayokwisha kuyapitia, wakiwa wamezama katika mazungumzo hayo, wakamwona mheshimiwa Kalembo akitoka ndani na kuondoka zake huku akisalimiana na wachache wanaomfahamu. Na baadaye kidogo wale wafanyabiashara nao wakaondoka zao.
“Gina hapa kazi nafikiri imeisha kwa leo, maana hatujui kama hawa watatu wanaubia au vipi, tufanye hivi, maada tumewaona hapa, ii kuhakikisha tuuchunguze ukaribu wao kama upo,” Amata akaeleza mpango kazi.
“Sawa, maana hata mimi nilitaka nikwambie hilo. Sasa tunaenda wapi?” Gina akaanza ubembe wake.
“Kila mtu kwake saa hii,” Amata akamwambia
“Aah no, please haujamaliza kuniweka sawa turudi nyumbani,”
“Nina kika cha kikazi usiku huu nitachelewa kurudi,” akamwambia Gina.
“Au una mwanamke mwingine?”
“Wivu kidonda Gina! Nenda kanisubiri nyumbani kwako, leonakuja kulala huko,” akamwambia.
“Ok,” wakaachana na kila mmoja akashika njia yake.
Kamanda Amata alipoachana na Gina, moja kwa moja akawahi nyumbani kwake maeneo ya Kinondoni. Akabadili nguo zake na kuvaa za kazi. Suruali nyeusi ambayo ukiitazama utafikiri ni jinzi lakini kumbe ilikuwa ni suruali ya mpira mpana. Akafungua kabati na kutoa fulana nyingine nayo nyeusi akaivalia na ikamkaa vyema, raba anazoziamini kwa kazi za usiku. Alipoona amejiweka sawa, akachukua pesa kidog kwa ajili ya hili au lile. Bastola zake ndogo mbili kazibana kiunoni kiasi kwamba hata ufanyeje huwezu jua. Dakika chache tu akawa yupo kikazi. Akaingia stoo na kuondoa turubai lililfunika pikipiki yake aipendayo kwa kuwa ni muda mrefu hakuitumia. Akaikagua hapa na pale na kisha akaiwasha na kuingia mjini.
Saa zikapita na dakika zikayoyoma, alipoitazama saa yake mkononi akagundua kuwa kumbe usiku mwingi ulikuwa umeshafika kwa mara nyingine. Akatoka taratibu na kuvuka barabara. Upande ule alikoelekea, kama nyumba ya nne hivi ndipo ilipo nyumba ya marehemu Shekibindu. Nyumba hiyo ilikuwa kimya kabisa, vyumba vyote taa zilikuwa zimezimwa. Akajongelea karibu na ukuta kisha kwa umakini na ufundi akapanda ukuta huo na kutua ndani ya ua wa nyumba hiyo kubwa bila kufanya ukulele wowote. Alipoona utulivu upo, taratibu akatembea kuutafuta mlango utakaoweza kumfikisha ndani ya kasri hilo pweke.
Mlango wa jikoni ndiyo uliyomkaribisha Amata baada ya kutikiswa mara mbili tu, akasogea mpaka karibu kabisa na milango ya vyumbani. Katika kijibegi chake kilichokuwa mgongoni, akachomoa kijichupa kidogo kama cha pafyumu kisha akavuta hatua katika mlango mmoja baada ya mwingine na kunyunyiza hewani huku yeye akivaa kifaa maalumu cha kukinga dawa hiyo isimdhuru. Ilikuwa dawa mbaya kabisa ya usingizi ambayo ukiivuta tu hewa yake basi utalala kama pono. Dakika mbili baadae akaanza kupekuwa nyumba hiyo bila wasiwasi wowote. Alipita hapa, akapita pale, akashika hiki na kushika kile, vyote vya sebuleni havikumfaa. Safari ikaanza kwenda chumbani ambako Shekibindu alikuwa akilala na mama watoto wake. Siku hii katika kitanda kikubwa alikuwa mwanamke huyo peke yake. Akafunga mlango nyuma yake na kumtazama mama huyo. Hakuwa mzee wala mtu mzima sana, ila ni wa makamo kati ya miaka thelathini na tano hadi arobaini, mwenye shepu hasa ya kinyamwezi. Na kwa jinsi alivyolala pale kitandani, lo!
Hakuja kwa hilo japo damua ilianza kumchemka na sehemu fulani za mwili zilizolala zilianza kuchukua uhai. Shuka lilikuwa kando kidogo na kuuacha nusu ya mwili wa mama huyo wa watoto wawili ukiwa wazi, nyama tamu ya paja mpaka karibu na kiuno ilikuwa nje. Jicho halina pazia, Amata aiyaburudisha macho yake kwa sekunde kadhaa kisha akamfunika na shuka ile nyepesi. Akavuta hatua kwenye makabati na kuanza kupekua hapa na pale, zaidi ya nguo na vipodozi hakukuwa na kitu kingine cha maana. Akakata tamaa na kuamua kutoka, lakini kabla hajaufikia mlango, akili yake ikamzuia na kumgeuza upande wa pili, kulikuwa na mlango mmoja. Choo, akawaza lakini akatii hisia zake na kuuendea, alipofungua, ndani yake akakuta milango mingine miwili inayotazamana, akafungua wa kwanza, kweli ni choo, wa pili, umefungwa kwa funguo. Akatabasamu na kutoa funguo yake isiyoshindwa, mzunguko mmja tu kitasa kikatii na mlango ukafunguka.
Ilikuwa ofisi ya wastani, si kubwa wala si ndogo, mafaili kadhaa yalikuwa mezani, kwa haraka haraka ilionekana wazi kuwa afisi ile haijaguswa kwa muda kwani kitu kama vumbi kilitanda juu ya kabrasha zile. Kamanda Amata akaketi na kufungua moja baada ya jingine, yote hayo hayakuwa na tija kwake. Faili kama la nne hivi ndilo hasa alikuwa akilitafuta. Na kwa kuwa mwenyewe alikwishakufa, hakuona haja ya kuliacha, akalitia begini. Kompyuta kubwa iliyokuwa hapo mezani hakuahangaika hata kuiwasha zaidi zaidi aliufumua mfuniko wa system unit na kung’oa hard disk akaitia begini. Kwa mwendod wa taratibu akatoka ndani ya chumba kile, alipenda sana apate kitabu cha kumbukumbu lakini haikuwa hivyo. Nitakuja tena kumsalimu mjane, akawaza na kuondoka zake.

ITAENDELEA…
 
RIWAYA: JANGA

MTUNZI: richard MWAMBE





Ilikuwa ofisi ya wastani, si kubwa wala si ndogo, mafaili kadhaa yalikuwa mezani, kwa haraka haraka ilionekana wazi kuwa afisi ile haijaguswa kwa muda kwani kitu kama vumbi kilitanda juu ya kabrasha zile. Kamanda Amata akaketi na kufungua moja baada ya jingine, yote hayo hayakuwa na tija kwake. Faili kama la nne hivi ndilo hasa alikuwa akilitafuta. Na kwa kuwa mwenyewe alikwishakufa, hakuona haja ya kuliacha, akalitia begini. Kompyuta kubwa iliyokuwa hapo mezani hakuahangaika hata kuiwasha zaidi zaidi aliufumua mfuniko wa system unit na kung’oa hard disk akaitia begini. Kwa mwendod wa taratibu akatoka ndani ya chumba kile, alipenda sana apate kitabu cha kumbukumbu lakini haikuwa hivyo. Nitakuja tena kumsalimu mjane, akawaza na kuondoka zake.



“Umenifanya nini jana Amata?” Gina alilalama kwenye simu alfajiri ya siku hiyo.

“Aaaaa samahani nilichelewa kurudi kutoka huko nilikokuwa,” akamjibu.

“Sawa naju tu, una mwingine!”

“Kazi kwanza mwanamke, mapenzi baadae,” akamwambia, “Tukutane afisini kuna jambo la kuangalia pamoja,” akaongeza.

“Ok, hamna shaka boss!” simu ikakatika.



SEHEMU YA 13

SHAMBA

Mchana wa siku hiyo TSA walikutana katika ofisi yao ya siri huko Gezaulole ambako kwa kificho walipaita Shamba. Jingo hilo lilifanyiwa kazi nyingi za kiusalama na watu wa idara hii nyeti. Ni wao sita tu waliokuwa wanaifahamu, wengi walioingia hapo hawakuingia na macho yao yakiwa wazi wala hawakutoka katika hali hiyo.

Madam S, Kamanda Amata na Gina walikuwa katika chumba kidogo cha mikutano ndani ya nyumba hiyo kongwe.

“Sasa kwa mawazo yangu, nimeanza kuitambua hii kesi, hili hapa faili la hukumu ambalo marehemu Shekibindu alikuwa ameliandaa, bahati mbaya hakuwahi kulifanyia kazi mpaka mauti inamchukua. Madam S akalivuta na kuanza kulisoma kwa sauti huku Gina na Amata wakimsikiliza. Alitumia dakika ishirini na moja kumaliza hukumu ile. Akalifunga lile faili na kuwatazama wawili wale.

“Amata!” akaita kwa sauti ya chini kana kwamba hakutaka watu fulani wamsikie.

“Vipi?” Amata akajibu kwa swali.

“Nimeelewa, Shekibindu kauawa kwa asilimia sabini. Hili faili linajieleza, hawa jamaa inaonekana hawkautaka kabisa kupteza matrilioni yao. Na kama wamemuua, hukumu inayokuja inakuja kuwapa ushindi, na kama itawapa ushindi basi si kingine ni rushwa…”

“Naam!” Gina akaitikia, “Nani bingwa wa kutoa rushwa zaidi ya Ankhit na Suleiman? Ni wafanya biashara gani ambao wana urafiki sana na viongozi wa serikali zaisi ya hao wawili?” akaongeza maswali.

“Shekibindu alitaka kuteketeza haya mavipodozi yote, na zoezi hilo alitaka mahakama isimamie kabla ya kutoa hukumu halisi ambapo hapa aikuwa anawafunga maisha na kuwangia leseni za biashara,” Madam akasema.

“Ina maana Shekibindu hakuwa na urafiki nao?” Kamanda akaauliza.

“Bila shaka, hakuwa na urafiki na mtu. Unakumbuka alivyomweka ndani yule Mturuki aliyekuwa akiingiza dawa za kulevya, wakati kesi ile imepigwa danadana miaka nenda rudi,” Madam akaongea kwa uchungu.

Kama walimshawishi kwa rushwa basi alikataa, na vipi kama huyu Tulabayo hajaingia kwenye mtego huo…”

“Aaaaaaaahhh! Madam sasa umeniunganishia matukio,” Amata akamwambia Madam kisha akaanza kumsimulia siku ya jana yote ilivyokwenda jinsi walivywafuatilia Ankhit na mwenzake mpaka walipomwona Waziri Kalembo kule Bushtracker.

“Amata, unataka kunambia Kalembo atakuwepo kwenye sakata hili?” Madam akauliza.

“Ndiyo nataka kufanya uchunguzi kwa kuwa huyu waziri haeleweki, ana biashara haramu nyingi sana, ameshitakiwa kwa kesi nyingi lakini zote anashinda katika mazingira ya kutatanisha, fisadi, mpenda pesa, mfalme,” Kamanda Amata akaongea kwa hasira.

“Subiri Amata, nammezea mate sana huyu jamaa, nataka upeleleze ujue nini kinaendelea kati ya hawa wafanyabiashara, Kalembo na huyo Tulabayo. Kesho hii kesi inaendelea pale Kisutu, Gina hakikisha unakuwa pale, kila kitu kikimalizika, jioni saa kumi na mbili wote muuwache mji peke yake mje hapa, Chiba na Jasmine watakuwepo pia kazi yao wamemaliza kule Zimbabwe,” Madam akaeleza.

Akafungua bahasha yake na ndani yake akatoa picha kadhaa na kuziweka mezani, picha zile zilikuwa za watu tofauti kama wane hivi.

“Mmewahi kuwaona watu hawa?” akawauliza. Gina na Amata wakazitazama.

“Hapana!” wakajibu kwa pamoja.

“Ok, achana nazo, tutazijadili siku nyingine, ila kwa sasa karirini hizo sura nilizowaonesha kwenye picha,” akawaagiza.

“Lakini Madam mi bado nakumbusha mara kwa mara, kama sasa tunaona wazi kuwa Shekibindu atakuwa ameuawa, vipi kuhusu Mustafa Bashiru?” Gina akauliza.

“Oh sure! Huyu mtu ni muhimu kujua yuko hai au vipi, nafikiri hilo niachieni mimi, ninyi fanyeni niliyowaagiza,”

“Ok Madam! Copy that,” Amata akajibu na kile kikao kikafungwa, kila mmoja akaendelea na mambo yake ndani ya jingo hilo.

“Ngrrrrrrrrrrrrr! Ngrrrrrrrrrrr!” simu ya mezani kwa Inspekta Simbeye ikaita, mzee huyu alikuwa akiufunga mlango kwa nje tayari kwa kuondoka.

“Aaaaa shit! Nani huyo saa hii?” akaongea kwa sauti ya chini huku akiuma meno. Akatulia na ile simu ikakatika, alipokiachia kitasa tayari kwa kuondoka ile simu ikaita tena kwa nguvu ile ile, akarudi na kuufungua mlango, akaiwahi kabla haijakatika na kuiweka sikioni.

“Inspekta Simbeye hapa…”

“Alfa!” Madam akajibu kwa kutaja code yao ya siri sana ambayo huashiria simu hiyo si ya kawaida.

“Nakusoma!”

“Kuna fax yako itaingia ofisini sasa hivi, usitoke!” Madam S akasema kisha ukimya ukatawal kati yao kwa sekunde kadhaa.

“Omega!” akaongeza tena. Na ile simu ikakatika. Simbeye akarudi na kufunga mlango kwa ufunguo kisha akaketi kusubiri. Sekunde kadhaa akasikia mlio kama wa mdudu ukitoka kwenye ile mashine na karatasi ya ujumbe mfupi ikaanza kujitokeza, akaisubiri, ilipomalizika, akainyakuwa na kuisoma kwa shauku.

Atafutwe, Mustafa Bashiru, mwandishi wa habari gazeti la Mbalamwezi, ametoweka tangu jana na hajulikanai alipo.

Mtu huyo ni ana funguo ya sanduku letu la siri.

Clear!

Ujumbe ule ukakatikia hapo, Simbeye akausoma tena na tena akaikunja ile karatasi na kuichanachana vipande kisha akaitia kinywani na kutafuna vibaya. Baada ya sekunde kadhaa akainua simu yake na kupiga tarakimu moja tu.

“Kaunta namba moja!” ile simu ikajibiwa na mwanadada.

“Ofisi namba tano inaongea, naomba mumrudishe Chatu mara moja hapa nina shida naye,” akamaliza na kukata simu. Hakukaa hata sekunde kumi, akaichukua redio yake na kuiwasha, na ikakrma mara mja mbili akasikia ujumbe alioutuma ukifanyiwa kazi kupitia simu hiyo ya upepo.

“…Chatu, Chatu. Chatu, Chatu, ova!”

“…Chatu anakusikia, ova!”

“…Chatu anatakiwa kurudi mtoni mara moja, ova!”

“…Ujumbe umepokelewa na unafanyiwa kazi, ova!”

Simbeye kutoka afisini kwake akatikisa kichwa baada ya kujua kuwa vijana hao wako njiani muda huo.

Akiwa macho yake yamezama kabisa katika habari iliyokuwa ikitangazwa katika luninga ambayo iliwekwa ofisini kwake, mbisho wa hodi ukamgutusha.

“Shit, hawa watu wanaweza kuua, kupiga gani hodi huko sasa?” akajisemea na kuinuka kwenda kufungua.

“Jambo afande!” kijana mmoja wa makamo, mwenye mwili ulioshupaa misuli, alimsalimu inspekta huyo huku akiwa kabana mikono kiukakamavu kabisa.

“Jambo!” Simbeye akajibu kisha akamruhusu kuingia ndani, wakaketi kwa kutazamana.

“Jose, upo Chatu?” Simbeye akauliza.

“Ndiyo afande, nimeanza duty wiki hii,” akajibu.

“Ok good! Sasa kuna kazi nataka kikosi chako kiifanye kwa haraka sana,”

“Ndiyo afande!”

“Kuna mtu anaitwa Mustafa Bashiru!” Simbeye akamwambia huyo kijana afande.

“Ndyo ni mwandishi wa Mbalamwezi…”

“Yeah yeah namkumbuka si ndiyo aliokotwa akidaiwa ametekwa sijui nini,” Jose akaeleza.

“Huyo huyo, sasa huyu mtu ametoweka tangu jana hajaonekana, nataka mfanye uchunguzi, mjue alipo, awe hai ama amekufa,” akatoa amri.

“Timamu afande!” akainuka na kusimama kwa ukakamavu, alipogeuka tu na kutaka kutoka akaitwa na kugeuza mwili wake tena, kisha akasimama kwa ukakamavu.

“Habari zote utakazokusanya za huyo mtu, nipe mimi mara moja na si kwa mtu mwingine!”

“Sawa” akajibu na kuondoka zake.

Siku hiyo msako mzito ukaanza dhidi ya mtu huyo, vijana hao wa polisi ambao daima huzurua na Land Cruiser yao walitumia mbinu nyingi kutafuta habari za Mustafa, kila kona walihakikisha wanafanya zoezi hilo.

Jioni hiyo hiyo Ngishu na kundi lake walikutana bandani kule ambako walimpeleka Mustafa mara ya kwanza walipomteka.

“Tumemkosa?” Ngishu akauliza.

“Ndiyo, tena inaonekana hayupo kabisa mjini hapa!” Kadoda akajibu. Ukimya ukachukua nafasi yake kisha Ngishu akaendelea, “Mnajua ni hatari sana kutojua mtu huyo alipo, na hii ni kwa sababu hatujua yuko kwa nani, vipi kama akiwa mikononi mwa polisi? Si ataweza kuwasaidi sisi kukamatwa!”

“Sasa tunafanyaje Ngishu?” Kebby akauliza.

“Kwanza, kama kajua tunamsaka, kajuaje? Au hapa kuna mamluki, nashindwa kuelewa, kwa sabau siku ile ya juzi alikuwepo mjini lakini nilipopewa tu maagizo ya kumshughulikia yule mtu hakuonekana tena…”

“Hilo jambo rahisi Ngishu, mlipokuwa mnaongea mlikuwa wangapi?” Kebbya akamkatisha kwa swali.

Ngishu akatulia kimya kwa nukta kadhaa kisha akafungua kinywa chake, “Wawili, tulikuwa ndani zaidi ya hapo ni secretary ambaye alikuwa afisi ya pili,” akawaambia.

“Baasss! Umejaribu kumchunguza huyo secretary?” Kebby akauliza.

“Hawezi, kwanza afisi zile zilivyo hawezi kusikia kitu…”

“Sasa kwa nini utufikirie sisi wa mbali umuwache huyo secretary wa karibu hapo?”

“Mh!” Ngishu akaguna na kujaribu kuvuta kumbukumbu, hakuna kitu zaidi ya kukumbuka alivyoingia na kutoka, japo tofauti ilikuwa ni kutazamwa kwa jicho baya pindi alipokuwa akitoka.

Possible! Akawaza na kuwatazama wengine.

“Ok guys, tuonane kesho mahakamani, kila mtu aje kwa siri kwa sababu kama yule mjinga yupo mjini hapa, atajitokeza tu, si unajua anataka habari,” Ngishu akawaambia wenzake.

“Ndiyo,” Kebby akajibu huku akisimama kutoka pale alipokuwa ameketi.

Baada ya kikao hicho, Ngishu akawapatia posho yao ya kazi, pesa iliyonona, wakaagana na kila mmoja akachukua hamsini zake.

Kamanda Amata akazima gari na kushusha mguu wake taratibu ardhini, alipokwishakusimama vyema akaufunga mlango, kisha hatua zake zikamfikisha katika ukumbi mkubwa wa Club Ambiance, Sinza. Akasogea na kupishana na watu waliojaa ndani humo, akapata nafasi na kuketi huku muziki wenye makelele ukipigwa na watu wakiselebuka usiku huo kana kwamba hawana familia nyumbani.

“Umesikilizwa kaka?” sauti ya kukwaruza ya mwanamke ikayafikia masikio yake, akainua uso kumtazama.

“Hapana, niletee safari moja baridi, bila glass!” akamwagiza na yule mwanadada akapotea eneo hilo. Macho ya Amata yakaangaza ukumbi mzima kwa muda mfupi sana, kutokana na taa za rangi rangi hakuweza kuona vizuri.

“Nakwambia leo utaondka na mimi!!”

“Sitaki bwana!!”


ITAENDELEA
 
RIWAYA:JANGA
MTUNZI: Richard MWAMBE
SEHEMU YA 14
“Yaani unywe bia zangu tu! Lazima ukalipe, la, nakuua”
Kelele hizo zikatokea katikati ya watu waliokuwa wakicheza muziki, Amata akamsogeza pembeni Yule dada mhudumu maana tayari alikuwa ameleta kinywaji. Akatazama ile vurugu ya mwanaume huyo na Yule msichana wakivutana huku na huko huku wakiyapata matusi ya walevi waliokuwa wakiharibiwa starehe zao.
“Unabisha, unabisha? Nikuue, nikuueeeeee?”
Sauti ya Yule mwanaume ikapaa wakati huo akiwa kaingiza mkono ndani ya jaketi lake la jinzi.
“Nani yule?” akamwuliza yule mhudumu.
“Huyu kaka huwa anakuja hapa mara kadhaa, tena leo yuko peke yake, akishalewa ndiyo wa hivyo hivyo,” akajibu.
“Na Yule mwanamke ni nani?” akatupa swali linguine.
“Aaaa madada poa hao, keshakunywa bvia zake sasa anagoma kwenda kutoa mzigo,” yule Mhudumu akajibu huku tayari akiondoka. Amata akapiga funda moja refu la bia ile huku jicho lake likiwa linaangalia ule mchezo.
Mh, hii ndiyo Dar es salaam usiku! Akawaza na wakati uo huo akatoa miwani yake na kuivaa kisha akamtazama Yule kijana kwa umakini, miwani ile ilimwezesha kumwona mtu kama ana kitu chochote cha chuma, ilikuwa na madini ambayo hayaoni nguo wala hayaoni nyama, huona mifupa na vitu vya vyuma. Kwa miwani hiyo akagundua yule kijana ana bastola na kisu. Kitu kile kikamgutusha Kamanda. Bastola kwenye starehe? Akajiuliza moyoni. Mara yule kijana akamvuta yule mwanamke kwa nguvu na kutoka naye nje ya klabu ile ya usiku. Amata naye akanyanyuka, taratibu akatoka kwenda kutazama mchezo ule unaishia wapi.
Nje ya ile klabu bado yule kijana alikuwa anatumia nguvu kumswaga yule dada poa, wakafika kwenye gari moja, Noah nyeusi, akamtupia ndani na kuufunga mlango. Kengele za hatari zikagonga kichwani mwa Amata, akaikumbuka ile gari, ilikuwa inawafuata mchana, akaisogelea kwa chati kuitazama namba zake maana alizikariri, yeah, sawa, ni ile ile. Damu ikamchemka, akatazama huku na kule, hakukuwa na watu wengine zaidi ya wadada poa wanaojiuza na walevi wengine.
Ile Noah ikawashwa na kuondoka eneo lile kwa kasi, Amata akawahi kuingia katika gari yake akawasha naye akaifuata. Wakaingia barabara ya Shekilango na kurudi Sinza Lego. Yule kijana akawa anaendesha gari kwa fujo, na Amata naye alihakikisha hamwachi, akapita Lego na kutokea Barabara ya Morogoro akakunja kushoto na kuifuata Manzese. Baada ya kuvuka daraja tu, akaingia kulia kama anakwenda Mburahati kisha akasimama mbele ya nyumba moja ya wageni, taa za gari yake zilipomulika getini Amata akasoma, ‘Magunia Lodge’.
Geti likafunguliwa, ile Noah ikaingia ndani na likafungwa tena. Amata akapita bila kusimama mpaka nyumba ya nne hivi akasimama. Akazima gari na kutulia kama dakika tatu hivi, akajua kwa jinsi yule bwana alivyopania kulipwa pesa yake, muda huo tayari atakuwa anavunja amri ya sita kimabavu. Akafunga gari yake, akaicha pale pale kisha taratibu akarudi kwenye ile lodge, akaminya kengele ikaita, kidirisha kikafunguliwa.
“Nani?” sauti ya mlinzi ikauliza.
“Vyumba vipo?” Amata akauliza.
“Vipo, karibu sana,” yule mlinzi akafungua mlango na Amata akaingia ndani, mkononi akiwa na kijibegi kidogo ambacho ndani yake kulikuwa na viatu na dawa ya usingizi. Akapokelewa na kupewa chumba. Wakati anaandika kwenye leja ya wageni, akatazama aliyetangulia kaingia chumba gani, hakuona kusajiliwa. Akaandika jina la uongo, kabila la uongo, atokako, aendako kwa uongo.
“Namba nane!” akaambiwa na mhudumu wa kike aliyeonekana kusongwa na usingizi mwingi. Baada ya kukabidhi funguo, yule mwanadada akajibwaga kwenye godoro na kulala. Amata akapita taratibu kwenye milango. Naam mlango namba sita ulisikika ukulele wa kitanda kilicholegea kikipata shida, akajua kwa vyovyote wako humu.
Akaingia kwenye chumba alichopewa, chumba cha wastani, kitanda cha nne kwa sita, akaketi kwanza na kupanga mambo yake.
Hapa ndipo pa kuanzia, akajiegesha kusubiri muda kidogo maana alijua wawili hao hawawezi kulala humo ila wakimaliza mambo yao wataondoka, na yeye hakutaka hilo. Akachukua mkoba wake na kuufungua, akato ile dawa ya usingizi kisha akavua viatu na kubaki na sox miguuni. Akachukua miwani yake na kuivaa, akatoka taratibu kwa mwendo wa kunyata mpaka katika chumba cha mapokezi, akapuliza ile dawa na kisha akachukua funguo yake mfuko mwingine, akazunguka mlango wa nyuma na kutoka nje, kwa hatua za minyato akamfikia mlinzi aliyekuwa kasinzia huku kaegemea ukuta, akambana macho na kumpulizia puani. Ijapokuwa mlinzi huyo aijifanya kujitutumua lakini alilegea taratibu. Hapo hakuna ujanja, alijua wataamka baada ya masaa matano. Akaingia ndani kwa mlango wa nyuma na kukiendea kile chumba, hakubeba silaha yoyote, alipachika ufunguo wake na kuusukuma ule wa ndani, kisha akafungua bila kuchelewa.
Jicho la Amata likatua kitandani, yule jamaa akiwa kijasho kinamtoka kama anakimbizwa na mwanamke naye akiwa haeleweki kama hizo kelele ni za kukataa au kufuarahia.
“We nani? Unaingia bila hodi?” yule jamaa akajinasua mwilini mwa mwanamke na kujirusha kando, Amata akajua kuwa anakimbilia nguo zake ambazo kuna kisu na bastola. Kwa mruko mmoja, Amata alimfiki na kumpa pigo takatifu, jamaa akashuka chini taratibu bila kelele. Yule mwanamke akajikurupua naye na kujiviriga shuka, alipotaka kupiga kelele Amata akamnyoshea kidole cha kimya.
“Aaaaaa, aaaaah we nani?” Yule bwana akauliza.
“Usitake kunijua mi nani, ila wewe ndo unambie ni nani, nani aliwatuma kutoboa mipira ya gari yangu jana?” swali hilo kidogo likamgutusha yule jamaa, akatoa macho.
“Mi-mimi? Ulinio-na mi-mi?” jamaa akauliza kwa tabu.
“Kama ningewaona ningeruhusu mtoboe? Nieleze kwani mlikuwa mnanifuata na ninyi ni nani?” akamwuliza swali lakini yule jama akaonekana jeuri.
“Siwezi kukwambia asee, siwezi ni bora kufa,”
“Ok, bora kufa eee!” Amata akavuta sourual ya yule bwana pale mezani akachukua kisu, akakirusha na kukidaka kisha akakishusha kwa nguvu kwenye nyama ya paja ya yule jamaa, kikazama chote.
“Aaaaaaaaaaiiiiiiiiggggghhhhhh!!! Aaaaaaaaaaaaa, nassss-nase… aiyayayay!” akapiga yowe la uchungu, Amata hakujali alimtazama tu.
“Sema boss wako anaitwa nani?”
“Ngishu! Ngishu! Ngishu!”
“Anaishi wapi?”
“Sijui aseee, sijui mimi, mi ananituma tu, aiiii naumia bwana,” akalia.
“Usilie, ndiyo uanaume huo! Ninyi ndiyo mlimteka Mustafa?”
“We-we umejua-je eeeeee?” akauliza, kwa jibu hilo Amata akajua kuwa ni wao walimteka.
Akakichomoa kile kisu na mara Yule mwanamke akakurupuka na kuchukua bastola, Amata akainuka na kugeuka kwa upande ule.
“Mwache mwenzio!” akapiga kelele huku bastola yenye akitetemeka kuishika. Mara Yule jamaa kutoka pale chini, akajiinua na mguu wake ule mzima ukaupiga mkono wa Amata, kile kisu kikamchomoka na kutua mbavuni mwa ule mwanadada. Amata akageuka na pigo moja matata, ambalo lilimpeleka jamaa ukutani, akajigonga kwa nguvu na kwenda chini kimya huku macho yamemtoka.
Kamanda akawahi kugeuka kwa yule mwanamke, damu zilikuwa zimetapakaa eneo kubwa na mwili wake ukiwa chini bila nguo. Akaziendea nguo za huyo jamaa akazipekuwa mifukoni, hakuna cha maana zaidi ya noti za shilingi elfu kumi kumi kama kumi hivi, akazirudisha, akachukua simu na kuiwasha, haina jina hata moja, akaichukua na kuondoka nayo. Chumbani kwake akaweka kibegi chake vizuri, ile simu akaifungua na kuiweka vipande vipande, akavaa viatu vyake, na kubeba kijibegi tayari kwa safari. Akahakikisha haachi hata alama moja, akatoka kwa kufungua milango kama kawaida na kurudi kwenye gari yake.
Siku iliyofuata…
MAHAKAMA YA KISUTU
Shauku ya Watanzania ilikuwa ni kusikia juu ya kesi hiyo, waandishi walijaa si wamagazeti au wa televisheni kila kona walikuwapo. Wananchi wa kawaida nao hawakuwa nyuma hata kidogo, walihakikisha wanasikiliza kila kitakachosemwa. Kamanda Amata na Gina walikuwepo katika kona tofauti.
“Cooooorrrrrtttt!” sauti ikasikika na kila mmoja akasimama na Jaji mwenye dhamana akaingia katika sehemu yake, na wote wakaketi, mahakama ikaanza.
Mwendesha mashitaka akasimama na kuanza kusoma shitaka la mshitakiwa mmoja mmoja kati ya wale wawili yaani Ankhit na Suleiman. Shitaka lile lilisomwa kwa dakika kumi na saba kwa kila mmoja.
Jaji Tulabayo akiwa ameketi kitini na vazi lake jekundu huku kichwani kavaa kitu cheupe mfano wa kofia, akajiweka vyema na kuwauliza watuhumiwa mmoja baada ya mwingine kama wamekubali hilo kosa, wakakana. Kila mtu mle ndani ya Mahakama akaguna kimoyomoyo. Upande wa mashitaka ukatoa ushahidi wa kuwatia hatiani, ushahidi ule ule ambao ulisomwa siku zile za Shekibindu ndiyo uliyosomwa tena ukiambatana na vidhibiti vya madaktari bingwa juu ya nini kilipatikana katika vipimo vya postmortem za wale wanawake waliokufa wakidaiwa kutumia vipodozi hivyo hatari.
Jaji Tulabayo, baada ya kuisikiliza kwa makini kesi hiyo, akaihairisha mpaka baada ya wiki mbili akiutaka upande wa washitakiwa nao walete ushahidi wao dhidi ya kadhia hiyo. Minong’ono ilikuwa mingi katika jingo hilo mara tu Jaji alipotoka, wengi wao wakionekana kutoridhishwa na uendeshwaji wa kesi hiyo.
“Hawa ilitakiwa wahukumiwe tu, ni wauaji,” alisikika mtu mmoja akiwaambia wenzake nao wakakubaliana naye na kuanzishwa mazungumzo huku wakitaja vifungu vya sheria vilivyotumiwa na Jaji Shekibindu kuwatia hatiani na sasa walikuwa wanajiuliza vifungu gani vya sheria hiyo hiyo ambavyo vimetumika na Tulabayo, mkanganyiko.
Katika upande mwingine wa jingo hilo la mahakama, vijana wawili walikuwa wameketi ndani ya gari moja nyeupe, Subaru. Hawakuwa wakiongea na ukimya wao ulikuwa na ishara fulani kwani hawakuwa kimya cha kawaida. Baada kama ya dakika kumi hivi za ukimya wao mmoja akamgeukia mwenzake na kushusha pumzi.
“Uhhhhh!”
“Vipi?” mwingine akauliza.
“Boban,” akataja jina moja.
“Achana na huyo fala, ye anajua tuna kazi ngumu siku hizi, sijui kaenda wapi mpaka saa hii hata gari hajaleta, si ajabu yuko na Malaya tu,” Kadoda akamwambia huyo rafiki yake.
“Ndiyo hivyo, yaani jamaa akipata hela anachanganyikiwa kabisa, sijui alipozaliwa alikuta hela zinataga mayai!” yule wa pili akamwambia Kadoda.
“Mwache, leo akiibuka tu lazima akae tunduni, Ngishu keshasema!” akiwa katika kumalizia sentensi hiyo, simu yake ikaita, akainyanyua na kutazama kioo chake.
“Ngishu!” akasema kwa sauti ya chini iliyosikika vyema kwa mwenzake. Akabofya kitufe chekundu cha simu hiyo na kuiweka sikioni.
“Yeah man!” akaita.
“Tukutane kwenye ufukwe wa Ocean Road tafadhali, kuna kazi imejitokeza yapaswa kufanyiwa kazi,” Ngidhu akawaambia wale vijana. Kadoda aliyekuwa nyuma ya usukani akaiwasha ile Slubaru na kuionda katika viwanja vile huku akiyapita makundi ya watu yaliyokuwa bado yakitoka mahakamani hapo na kuendelea kujadili juu ya kesi hiyo ilivyokuja kinyume na matarajio.

RIWAYA HII INAPATIKANA KWA S 4000 TU. WASILIANA NA MWANDISHI 0766974865

Kila mmoja akiwa katika shughuli zake ndani ya viwanja vya mahakama, TSA walihakikisha wanaelewa kila kinachopita mbele yao. Kariu kabisa na lango la kutokea nje ambalo moja kwa moja hukutana na makutano ya Barabara za Maktaba na Bibi Titi, kulikuwa na gari moja, Toyota Carina juu ikiwa na bango kubwa lililoandikwa TAX. Ndani ya gari hiyo kulikuwamo watu wawili, Madam S na Scoba. Mara tu ile Subaru ilipotoka, Scoba alimshtua Madam S, mwanamama huyo akaitazama ile gari ikiondoka, akaiandika namba zake kwa haraka kisha akamwambia Scoba kuwa wataifuatilia.
Gina, mara tu baada ya kuona ukumbi ule umekuwa tupu akavuta hatua kuelekea nje, akiwa katika ujia mpana uliokuwa ukimwongoza nje, Gina akakutana uso kwa uso na mwendesha mashitaka wa kesi ile.
“Kama nakufahamu!” yule baba akamwambia Gina.
“Inawezekana!” Gina akajibu huku akimtazama mzee huyo kwa jicho pembe.
“Nilikuwa nakuona pale UDSM miaka mine nyuma,”
“Ni kweli, nilikuwa nachukua digrii ya kwanza ya sheria,” Gina akajibu.
“Oh ndiyo, sawasawa kabisa, karibu sana mi huwa nakuwa hapa mara nyingi sana nafanya kazi Mwendesha Mashitaka wa serikali. Ulishapata kazi?” Yule baba akamwuliza Gina.
Gina akatabasamu, swali lile alilielewa vyema maana yake nini.
“Bado, ndiyo nahangaika huu mwaka wa tatu sasa!” akajieleza.
Yule baba akatulia kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema, “Sawa, nitakusaidia, utapata usijali, sasa nipe namba yako nitakupigia baadaye nikitoka tuongee vizuri ili nijue tunafanyaje”.
Gina akampa namba zake za simu kisha wakaagana naye akatoka nje ya Mahakama na kuelekea kwenye maegesho.
“Ingia, ila ujue kuwa una kesi ya kujibu,” Kamanda Amata akamwambia Gina huku akimfungulia mlango na mwanamke huyo akaingia. Gina alielewa maana ya kauli ya Amata, akatabasamu tu huku gari ikiondoka na kutoka nje ya viwanja hivyo.

NINI KITAENDELEA?
 
RIWAYA: JANGA

MTUNZI: richard MWAMBE

SEHEMU YA 15

Yule baba akatulia kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema, “Sawa, nitakusaidia, utapata usijali, sasa nipe namba yako nitakupigia baadaye nikitoka tuongee vizuri ili nijue tunafanyaje”.

Gina akampa namba zake za simu kisha wakaagana naye akatoka nje ya Mahakama na kuelekea kwenye maegesho.

“Ingia, ila ujue kuwa una kesi ya kujibu,” Kamanda Amata akamwambia Gina huku akimfungulia mlango na mwanamke huyo akaingia. Gina alielewa maana ya kauli ya Amata, akatabasamu tu huku gari ikiondoka na kutoka nje ya viwanja hivyo.

UFUKWE WA OCEAN ROAD

Ile Subaru ikaegeshwa taratibu kwenye miti ya mivinje iliyozunguka fukwe hiyo, hawakushuka, walibaki ndani humo na sekunde kumi zilikuwa nyingi, Ngishu na Kebby wakaingia ndani ya gari hiyo. Macho ya Ngishu na Kebby yalikuwa yanafanana kwa rangi, yote yalikuwa mekundu na yaliyotona kwa machozi ya mbali.

“Vipi wazee, mbona kama mependeza mchana huu?” Kadoda akawauliza.

“Dah! Boban amekufa,” Kebby akasema.

“Nini!!! Unasema nini wewe, aiyaaaaaaaa!” Kadoda alijikuta anapiga unyende wa nguvu.

“Tulia wewe, mbona una kelele?” Ngishu akamwambia.

Kadoda akatulia huku akipiga kichwa chake juu ya usukani kwa uchungu, akajikuta chozi likimdondoka, kisha akamwatama Kebby na Ngishu.

“Mnajua washikaji acheni utani,” Kishasha akawaambia.

“Boban ameuawa, maiti yke imekutwa Magunia Lodge asubuhi ya leo kwa maelezo ya polisi wa Magomeni,” Kebby akawaeleza.

“Itakuwa mwanamke tu, tena gesti kabisa aaaaah!” Kadoda akazidi kuchanganyikiwa.

“Inatuchanganya kwa sababu hata mwanamke aliyekuwa naye kakutwa kafa chumbani humo, inaonekana kuna mtu wa tatu hapa,” Kebby akaeleza.

“Sasa mlinzi, mhudumu wa gesti wanasemaje?”

“Sijui!” Kebby akaeleza. Ukimya ukapita kwa sekunde chache kisha Ngishu akakohoa na kushuka kwenye ile gari, akatazama kupitia dirishani, “Hakikisheni mnapata hiyo habari mapema ili muuaji asakwe leo hii hii,” akawaambia kisha akaondoka, Kebby naye akafungua mlango na kutoka, akamfuata Ngishu aliyekwenda kuketi chini ya mvinje.

“Mi nilijua tu, kutokumpata Mustafa kutatugharimu ndiyo hii sasa!” Kadoda akang’aka na kujiegemeza kwa nguvu kitini.

Afisi ya Waziri Thomas Kalembo ilikuwa kimya kabisa, ijapokuwa kulikuwa na watu watatu ndani yake jioni hiyo, lakini bado ukimya ulishika hatamu.

“Sasa tunajipanga vyema, ile taarifa ya uchunguzi mmeshaipata siyo?” waziri huyo akauliza.

“Yeah, imefika tayari, sasa tumpatia mwanasheria wetu yeye naifanyia kazi mara moja,” Ankhit akajibu huku Suleiman akiwa kimya.

Kikao hicho kifupi safari hii kilifanyika katika afisi ya Kalembo mara tu baada ya kazi, ilikuwa ni mkakati wa kujipanga sasa kwa ajili utetezi wao katika mahakama itakayofuata.

“Kwa ujuma kesi tumeshashinda!” Kalembo akawaambia wale washirika wake. Nao wakafiki hilo. Lakini habari ya kifo cha kijana wao mmoja kilikuwa ni shtusho la moyo kwao.

“Nani itakuwa ua yeye?” Ankhit akauliza.

“Bado hatujajua, vijana wanafanya uchunguzi,” Kalembo akajibu.

“Hapana shaka, Kalembo najua vyema kazi, tapata hiyo mutu tu,” akaongea kwa lafudhi yake ya Kihindi.

Baada ya kuachana na swahiba zake, Kalembo alikutana na vijana wake katika maficho yao ya siri. Huko hakukuwa na hoja nyingine zaidi ya kifo cha Boban.

“Boban kauawa, no way, hapa kuna mambo mawili makubwa tu, ama kafumaniwa na mume wa huyo mwanamke au kuna adui yetu nyuma yake!” Ngishu akaeleza huku akifuta machozi mara kwa mara.

Kalembo alikuwa na vijana wake, wakijaribu kuangalia wigo wa kifo hicho wasipate jibu.

“Yule mhudumu anasema hajui chochote kwa sababu yeye alilala alipoamka na akaona kwenye mlango wa wateja wake hao ambao hawakutakiwa kulala kuna kitu kama damu, ndipo akafungua na kukuta mauaji hayo, mlinzi naye anaeleza hadithi hiyohiyo,” Kebby akasema. Mara baada ya kuachana pale Ocean Road Kebby na Ngishu walichukua jukumu la kwenda polisi kuulizia nini hasa kinaendelea juu ya mauaji hayo na ndipo walipokutana na habarai hiyo.

“Lakini wanasema kuna mteja alichukua chumba namba sita usiku huo, hakuonekana asubuhi, hivyo polisi wanamsaka maana jina wanalo ila hawakuweza kutupatia,” Kebby akaongeza.

“Sawa, sasa swala la mfu tuwaachie ndugu zake, sisi tujiangalie wenyewe, naamini kuwa muuaji atapatikana tu,” Kalembo aliyekuwa kava sox usoni aliwaeleza vijana wale, daima alipenda kuvaa hivi kila akutanapo na vijana hawa isipkuwa Ngishu pekee ndiye alikuwa akimjua sura mheshimiwa huyu.

“Kwa hiyo mna wasiwasi Mustafa anaweza kufanya kisasi na sisi? Lakini kumbukeni hakuziona sura zenu sasa atawajuaje? Hilo halina mashiko,” akaongeza kusema huku akiinuka na kuondoka eneo lile, kabla hajapotelea katika vyumba vilivyo katika banda hilo akasimama na kuwageukia, “Msipoteze muda kuhusu kuzikwa kwa marehemu, nduguzake watamzika, ninyi endeleeni na mikakati, fanyeni kama hakuwepo vile, muuaji atapatikana tu,” akawaambia na kuondoka.

Vijana hao nao wakaondoka mara baada kikao hicho wakiwekeana mikakati ya kukamilisha kazi inayowakabili. Pesa walikuwa nayo ya kutosha, hawakuwa na tabu, wangetumia watakavyo, lakini kila mmoja alipokuwa akikumbuka Boban, alihisi kama kesho ni zamu yake.

Simu ya Kebby ikaita, akaichomoa mfukoni na kuitazama namba, ilikuwa nmba ya Boban, marehemu. Akatoa macho kama fundi saa anayetafua skrubu iliyopotea.

“We vipi?” Kadoda akauliza.

“Boban!”

“Kafanya nini?”

“Anapiga simu, hii hapa,” akampa Kadoda.

“Shiiiit!” akang’aka na kuwatazama wenzake kwa zamu, simua ikakatika, kila mmoja akashusha pumzi.

Kishasha akaegesha gari pembeni katika barabara ya Bagamoy eneo la Boko Basihaya.

“Muuaji ana simu ya marehemu, hamuoni kama ni rahisi kumpata?” Kishasha akawaambia.

“Kivipi?”

“Tumtegee mtego,” akawaambia kwa kusisitiza.

“Tutamtegaje?” Kadoda akauliza.

“Si tunamt…”

Kabla hajamaliza kusema simu ile ikaita tena, Kebby akaichukua na kuipokea, akaiweka sikioni huku akihema kwa nguvu.

“Hello,” sauti nzito ikasikika ndani ya chombo hicho, kila mtu kwenye ile gari alikuwa kimya kabisa akisikiliza kile ambacho kilikuwa kikitoka katika simu hiyo mara baada ya Kebby kuweka sauti ya juu.

“Natumai unanisikia vyema, usiku huu ni zamu yako,” ile simu ikakatika. Kebby akajikuta anatetemeka mwili mzima. Kila mtu akajibwaga vyema kitini mwake huku akishusha pumzi ya nguvu.

“Kajikamatisha huyo!” Kadoda akawa wa kwanza kuzungumza.

“Kivipi?” Kishasha akauliza.

“Si kasema leo zamu ya Kebby, sasa tunamtega, Kebby akiwa nyumbani kwake, sisi tunatega nje, akijifanya kuja tu amekwisha!”

“Hivi Kado, muuaji gani atakwambia anakuja kukuua then aje kwako, vipi kama atamvizia njiani au sasa hivi keshafika kwake anamsubiri?” Kishasha akauliza na kumfanya Kadoda ajione masikini wa fikra.

Kishasha akaondoa gari na kuendelea na safari yao huku kila mmoja akiwa na mawazo yake kichwani. Saa moja iliyofuata iliwakuta katikati ya jiji, wakaamua kutafuta sehemu japo wapate chakula cha jioni, lakini Kebby hakuwa na raha kabisa.



10

Kamanda Amata akacheka sana na kuitia ile simu mfukoni. Mtapata tabu leo, akawaza na kuwasha gari kisha akaingia barabarani na kuondoka kwa fujo akiacha watu wakimtukana kimoyomoyo. Mtajiju! Akajisemea kwa sauti ya tumboni maana alilijua hilo. Mwendo wa kasi wa gari yake ulimshangaza kila mtu katika kila eneo alilopita. Akiwa katika mwendo huo mkono wake wa kushoto ulikuwa ukifungua redio kusikiliza taarifa ya habari ya saa mbili.

Dar es salaam

Watu wawili zaidi wamefariki dunia leo baada ya kupatwa na ugonjwa mbaya wa ngozi. Kamanda wa polisi mkoa amethibitisha vifo hivyo kutokea katika hospitali mbili tofauti jijini. Akiongea na waandishi wa habari, Kamanda huyo amekiri kuwa vifo hivyo vinafanana kabisa na vile vilivyotokea kwenye hospitali ya Amana wiki kadhaa zilizopita. Aidha amewataka wakina mama kuacha mara moja kutumia vipodozi vinavyosemekana kuwa ni hatarishi.Miili ya marehemu hao inafanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Muhimbili.

Ile taarifa ikamfanya Amata ajisikie ganzi, akawasha indiketa na kutoa gari nje ya barabara na kuigeuza kurudi alikotoka.

Ninaenda wapi Amata? Akajiuliza huku akiiacha barabara hiyo Mbozi na kukamata ya Chang’ombe kuelekea mjini. Hata kabla hajafika makutano ya Barabar za Kawawa na Nyerere, simu yake ikaita, alipoitoa akakuta ni Madam S anampigia.

“Yes Mom!”

“Ofisi ndogo,” kisha simu ikakatika. Amata akakunja kuli na kuingia Barabara ya Nyerere baada ya kuvuka Makutano ya Nyerere na Msimbazi katika eneo la Kamata, badala ya kwenda Mnazi Mmoja akakunja kushoto na kuchukua ile Barabara ya Nkurumah.

Dakika kumi na tano tu aliegesha gari nje ya ofisi ya Madam S, na kuteremka, akazikwea ngazi kwa haraka na kuingia katika ofisi hiyo nyeti, inayoendesha kazi za siri.

“Keti!” Madam akamwambia.

“Asante, we huendi nyumbani?” akamwuliza Madam.

“Niwahi nini ilhali sina mume…”

“Eh yaishe!” Amata akakatisha mada.

“Nipe ripoti kijana maana naona hii kazi sasa inataka kuanza kunoga,” Madam S akamwambia Amata huku akijiweka sawasawa kitini, “maana najua siku nzima hii utakuwa umeshakusanya vingi vya kutosha,” akaongeza.

“Ni kweli, ulivyonipigia simu nilikuwa njiani kuelekea Muhimbili kuona hiyo miili ya hao marehemu waliotangazwa usiku huu,” akamwambia bosi wake.

“Oh, kumbe umechelewa kupata habari, wamekufa tangu saa saba mchana, na nimetoa amri wasizikwe…”

“Kwa nini?” Kamanda akauliza.

“Kwa sababu, nataka sasa tufanye vipimo sisi wenyewe na kujiridhisha, kisha nitakwambia kinachofuata,” akamwambia.

“Sawa nakuunga mkono. Madam, nimeshaitikisa ngome ya adui nahisi kuwa muda si mrefu tutajua Musatafa yuko wapi,” Amata akasema.

“Kivipi sijakupata hapo,”

“Jana nimepambana na mmoja wa vijana ambao bila shaka wapo jirani na kiini cha habari hii,”

“Ulimjuaje?” Madam akauliza.

“Sikuwa na shida naye lakini kilichotokea ni kuwa aliingia baa na silaha, akachukua mwanamke na kulazimisha kuondoka naye, walipotoka nikawafuatilia, kufika nje ndipo nakutana na gari ile iliyokuwa inatufuatilia mchana wa jana kuanzia Segerea, sikumwacha nikaondoka naye,” Amata akaeleza habari ile kwa kirefu sana, Madam S naye akasikiliza kwa makini vile vile.

“Sasa huyo mtu yuko wapi?” akamuuliza.

“He! Yuko mchwari, uzembe wake ulisababisha kifo chaken na mpenzi wake”.

Madam S akakaa kimya akimwangalia kijana wake, kisha akatikisa kichwa huku na kule.

“Ok, amekwambia nini?”

“Amenambia bosi wake ni Ngishu,”

“Ngishu! Ok,” Madam akajibu kwa mkato na kuvuta motto wa meza, akatoa bahasha ile ile aliyoitoa jana yake. Akachambua picha na kumpa moja ya kijana wa Kihindi. Amata akaipokea na kuitazama.

“Huyo ndiyo Ngishu!” Madam S akamwambia. Amata akaitazama ile picha kwa makini sana kisha akaiweka mezani.

“Kuna mchezo mzito nyuma ya kitu hiki, huyu mtoto wa Kihindi nahisi ana kikosi cha wauaji au watekaji,” Madam akamwambia Amata.

“Usijali Madam, nakuhakikishia kila kitu kitajulikana tu,” akasema kwa kujiamini.

“Ok, abort!” Madam akamwambia Amata na kijana huyo akaelewa mara moja anachoambiwa, akazungusha kiti chake na kukaa kiupandeupande huku akimpa mwanamama huyo ubavu. Mlango ukafunguliwa, na aliyeingia hakuwa mwingine bali ni Daktari Jasmine. Huyu alikuwa ni daktari bingwa katika kitengo hiki cha siri, cheo chake kilijulikana kama TSA 3.

Amata akanyanyuka na kumlaki, akambusu maslhavuni na kumkaribisha kiti. Jasmine akapeana mikono na Madam S, baada ya salamu hizo za bashasha kwa watu hawa kutokuonana kwa miaezi kadhaa, Jasmine aliketi akitazamana na Kamanda Amata.

“Pole kwa safari, naona umenenepa sana, Amerika imekupenda ee?” Madam akamtania.

“Haijanipenda huu unene ni kwa sababu ya kula maplastiki kila siku,” Jasmine akawaambia na wote wakaangua kicheko.

ITAENDELEA
 
RIWAYA:JANGA
MTUNZI: Richard MWAMBE
SEHEMU YA 16
Daktari Jasmine, aliondoka na kwenda Marekani kwa ajili ya masomo ya ziada katika kituo cha uchunguzi cha John Hopkins, safari yake ya kwenda huko ilikuwa ni ya kikazi ili kuboresha zaidi idara hiyo katika kazi zake. Lakini pia kulikuwa na mvutano kati ya Madam S na Rais wan chi kuhusu daktari huyo kijana. Ikulu ilimtaka awe daktari wa Rais pia awe katika moja wa walinzi wake wa karibu. Madam hakukubaliana na hilo kutokana na kwamba kitengo chake kingekuwa na kazi ngumu ya kumpata mtu mwingine nah ii ni kwa kuhofia uvujaji wa siri nyingi za kitengo hicho nyeti.
“Nimerudi Madam!”
“Good, umerudi na kazi ipo mezani, ukiimaliza ndipo nitakupa likizo,” Madam S akamwambia, kisha akavuta droo nyingine na kuto faili, akamkabizi mwanadada huyo. Jasmine akalitazama kwa kuligeuza na juu ya jalada kulikuwa na maandishi makubwa ya wino mweusi, JANGA. Akalifungua na kuanza kulisoma taratibu huku, Amata na Madam wakiendelea na habari nyingine kabisa.
Katika ukumbi mkubwa wa chakula, ndani ya Hoteli ya Serena, Gina alikutana na mwenyeji wake ambaye mchana wa siku hiyo walikutana pale Mahakama ya Kisutu. Huyu alikuwa mwendesha mashitaka wa serikali, mtu mzima lakini alionekana wazi kuwa ni mpenda ngono, rushwa ya ngono ili akusaidie. Mara baada ya kupewa namba na Gina mchana ule, akaona wazi kapata kimwana, na alichanganyikiwa zaidi aliptazama ubarikio alioupata Gina sehemu za nyuma za mwili wake.
Simwachi! Akajisemea moyoni na jioni hiyo akampigia simu akimtaka wakutane Serena. Serena? Ndiyo Serena, kwa sababu alikuwa na mambo mawili kwa msichana huyo ambayo yeye mwenyewe Gina alijua moja tu, kutafutaiwa kazi.
Alifika mapema, akapanga chumba kwa Dola 200 kwa usiku mmoja akijihakikishia kumpata mrembo huyo.
Kazi atapata tu, ila lazima nifaidi kama kwa wale wengine, akajisemea na kujiaminisha. Rushwa, rushwa ya ngono, wanawake wengie wananasa katika rushwa hii wakiahidiwa kazi, wapo wanaopata na wengine wanaishia patupu na kubaki kutumiwa na huyu na yule pasi na wao kugundua kuwa ni mchezo. Hili ni janga lingine, janga kubwa kwa dada zetu, vyuoni hawasomi kazi kwenda disco, akitegemea kumpa penzi mwalimu ili apate alama za juu na GPA za maana, ngono. Anapomaliza chuo cheti chake kinamuuza kuwa ni mwenye akili, kumbe mbumbumbu, ‘kiuno’ ndiyo CV yake, janga.
Gina aliingia katika hoteli hiyo majira ya saa mbili akisingizia usafiri ulikuwa shida kutoka kwa Gongo la Mboto. Mwenyeji wake alikuwa tayari.
“Karibu sana miss…”
“Miss Rose!” akadanganya jina, “Subiri kidogo, tunaketi wapi?” akauliza.
“Aaaa kwenye ukumbi wa chakula, kuna tatizo?”
“Hakuna tatizo, ila mimi hupenda kuwa muwazi sana, mimi navuta sigara, hivyo naomba nivute hapa moja kisha tuingie huko,” Gina akamwambia mwenyeji wake ambaye mpaka hapo alikwishamsoma mawazo yake.
“Sawa!” akajibiwa.
Gina akachukua kijikebe kidogo katika pochi yake, akachomoa sigara moja na kuiwasha kisha akapiga pafu nne tu akaimaliza.
“Twen’zetu!” wakaingia ndani ya ukumbi huo.
Hakukuwa na watu wengi, taa za rangi ya dhahabu zilipendezesha ukumbi huo kwa kupenyeza miali yake katika mapambo yaliyotengezwa kwa vioo vya mikato mbalimbali. Hatua kama ishirini hivi ziliwafikisha wawili hao katika meza ndogo yenye viti viwili vya kupendeza.
“Kula unachotaka,” Gina akaambiwa.
“Aii jamani, mambo mengine haya wenzenu ushamba,” Gina akajibu huku akishangaashangaa huku na kule.
“Enhe mrembo…”
“He mrembo tena, usiniite hivyo, jina langu Rose,” Gina akaongea kwa aibu.
“Aaaa usihofu, hilo ni jina tunalowaita wasichana wote wenye uzuri asili kama wewe! Nami naitwa Dastan Majoti,” yule jamaa akaongea kwa sauti nzito na laini.
“Mmh, nambie, mpaka sasa hujapata kazi, umenishangaza sana,” yule jamaa akaanzisha mazungumzo.
“Kazi ngumu baba ‘angu, nimeomba weeeee lakini nazungushwa tu,” Gina akazungumza kwa huzuni.
Vyakula vikaja na vinywaji vya kutosha, pombe kali zilikuwepo, Gina aligundu kuwa huyo mwenyeji wake anammezea mate kwa jinsi alivyokuwa akipepesa macho yake na kushindwa kumtazama mwanamke huyo usoni.
“Hongera, nimeona unavyounguruma mahakamani,” Gina akamwambia huku akijifanya kama pombe inataka kumchukua. Majoti akastuka kidogo na kumtazama mwanadada huyo.
“Aaaa kawaida tu, mimi wananitegemea sana kwenye kesi ngumu kama hizi…”
“Lakini uelekeo unauonaje, wanashinda au la?” Gina akauliza.
“Aaaa wanashinda wale, kwa sababu serikali haina ushahidi wa kutosha wa kuwatia hatiani,” Majoti akajibu.
“By the way ulikuja kufanya nini pale?”
“Nilikuja kumcheki rafiki yangu Sauda, nimesoma naye Mlimani,”
“Oooh good! Nitakusaidia, na utapata mara moja. Unapenda serikalini au kwenye ofisi binafsi?”
“Serikalini,” Gina akajibu.
Danstan Majoti, akatikisa kichwa juu chini kuashiri kuwa ameelewa, akameza funda moja la mate, akainua simu yake na kubofya tarakimu kadhaa kisha akaweka sikioni.
“Eh, Comrade, habari za siku?” Majoti akamsalimia mtu wa upande wa pili.
“Nipo kabisa, umepotea sana vipi hujapata kimeo?” upande wa pili ukauliza.
“Hapana, kuna mdogo wangu asee vipi utumishi hapo univushie,”
“Keshatuma barua?”
“Bado,”
“Mwambie alete kesho saa nne, anikabidhi mwenyewe mkononi,” upande wa pili ukajibu.
Dastan akakata simu na kuiweka mezani. “Kazi imekwisha mtoto mzuri!” akamwambia Gina.
“Yaani kirahisi tu!” akashangaa na kutamka kwa sauti.
“Yeah, haya mambo tunajua wenyewe tunavyocheza, ila kama hujui, utazungukaaaa we na mabahasha yako hupati chochote, utatuma maombi mpaka stamp ziishe posta, utabaki hapo hapo,” Majoti Dastan akajigamba. Gina akasikitika moyoni kusikia hayo, akasikiri ni vijana wangapi wanaoteseka kutembea maofisini kutapeliwa pesa na wajanja wanaojifanya watawapa ajira lakini wanabaki hawana kitu.
Rushwa ya kila aina ilikuwa inaziba haki za wananchi, pesa, ngono na mengine kibao.
“Nitatakiwa kukupa shi’ngapi?” Gina akauliza.
“Ingekuwa nahitaji pesa kwako nisingekuita hapa Rose…”
“Kwa hiyo unanisaidia tu?” Gina akachokonoa.
“Aaaa msomi wewe, unaelewa mazingira, sikutaka pesa kutoka kwako kwa sababu najua nawe unatafuta pesa kwa kuwa huna ajira”.
“Aiii jamani, sijui nikulipe nini mimi…”
“Usiumize kichwa, msaada tu wa kibinadamu, maisha ni kusaidiana Rose, nimekodi chumba hapo juu, nategemea hutoniangusha japo kwa usiku mmoja tu,” Majoti akaongea lugha iliyosafirisha ujumbe wa mapenzi, Gina akamtazama mtu mzima huyo kwa jicho pembe, alilitegemea hilo.
“Unajua Rose, hii kazi yetu inalipa, akiingia mjinga unapiga hela. Nakuhakikishia mwezi ujao tu unaanza kukunja kitita chako. Kama hii kesi ya leo tumepiga hela ndefu sana, ndefu sana yaani, mi sasa ninja nyumba tano, gari nne za kutembelea, nalala nnapotaka,” akajieleza, tayari kinywaji kilikuwa kikifanya kazi.
“Asee, ila mi nilisikitika juu ya Shekibindu, nilikuwa nampenda yule baba!”
“Aaaa yule mzee mjinga mpaka umri ule alikuwa anakaa nyumba ya serikali, mi nilikuwa sipendi kufanya kazi naye yaani hupati pesa. Sikiliza, hii kesi alishika yeye, alikuwa haingiliki, alipokufa aaaa kila mtu akasema afadhali, akachukua rafiki yangu Tulabayo, siku nne tu mipesa hii hapa, watashinda kesi watatambaa zao,” Majoti akabwabwaja bila kujua anayeongea naye kuwa ni moja Polisi, mbili Usalama wa Taifa, TSA 5, kwa ujumla alikuwa ni mtu hatari kuliko hatari yenyewe.
“Nimechoka, nahiyaji kupumzika!” Gina akajilegeza na kuyashuhudia meno meupe ya Majoti yakionekana baada ya kukenua kwa furaha ya kusikia neon hilo.
“Hata mimi pia, twende tukapumzike bebi,” akalalama.
“Ai jamaani, usiniite bebi, nina mchumba mimi…”
“Aaaa hakuna mchumba asiyetaka maendeleo, twende,” Majoti akasimama huku kidogo akiyumba, wakakokotana na Gina huku mtu mzima yule akijitahidi kupapasa mtiti ya Gina. Chumba kikubwa, ghorofa ya pili, Majoti akafungua mlango kwa taabu kidogo, kila mara alikuwa akishindwa kutumbukiza funguo mahala pake.
“Hah! Hah! Hah! Aaaa unashindwa kulenga tundu la ufunguo, na vingine utaweza?” Gina akamtania.
“Aaa hii ni funguo, vingine hata gizani nalenga…” wote wakaangusha kicheko na mlango ukafunguka. Moja kwa moja wakaangukia kitandani na kubiringishana.
“Rose unaonekana unayaweza ee?”
“Yaani leo utashindwa wewe, na hizo pombe zako, utazimia,” Gina akamwambia. Majoti akamkumbati Gina kwa nguvu pale kitandani, akapeleka kinywa chake kwa mwanamke huyo, Gina akafanya kama anaupokea ulimi wa huyo bwana.
“Subiri! Hivi watu wanasema kuwa Shekibindu ameuawa ni kweli?” akauliza
“Aaaaaa Rose!!! Swali gumu hilo,”
“Nijibu bebiiiii!” Gina akambembeleza huku mkono wake ukilipapasa dume hilo kwenye dhakari yake.
“Oooh! Rose, aaaaah! Polepole mama. Ni kweli jamaa walimfanyia mpango. Shhhhhh! Nikisikia umemwambia mtu nakumaliza,” Majoti akajikuta akijibu bila kipingamizi. Achana na mapenzi bwana, ukibanwa kitandani utajibu na kutoa kila siri, Gina aliitumia nafasi hiyo kwa kuuliza maswali ya kutosha na yote akapata majibu sawasawa.
“Mtandao ni mkubwa na kila watu wana kazi yao,” akamalizia kusema. Mara simu ya Gina ikaanza kuita kwenye mkoba wake.
“Samahani!” akamwambia kisha akachukua simu yake na kuitazama.
“Nani?”
“Mchumba wangu!”
“Mwambie upo kwenye usahili wa kazi…”
“He! Kumbe huu ni usahili!” Gina akajifanya kushangaa huku akiifyatua ile simu.
“Hello!”
“Uko wapi mrembo wangu?”
“Nipo kwenye usahili wa kazi, nitachelewa kurudi,”
“Ok sawa!” Amata akajibu upande wa pili, akajua tu kwa vyovyote Gina kuna kazi nyeti anayoifanya.
“Sasa baby, wapi tena?” Majoti alimwambia Gina, wakati mwanadada huyo alipotoka kitandani na kuelekea bafuni.
“Najiweka, sawa tuanze mambo au siyo? Nawe jiandae basi,” Gina akmwambia kwa sauti ya deko iliyomtekenya mwanaume huyo mpaka kwenye nyayo.
Gina akaingia bafuni, akafunga mlango kwa ndani, na kushusha pumzi, akachomoa kifaa cha kurekodia sauti, akakikuta bado kinafanya kazi, akasevu faili, akakizima na kukificha kwenye sidiria kama mwanzo, akatoka bafuni na kumkuta jamaa tayari kabaki na bukta.
“Uko tayari kwa mchezo?” Gina akauliza.
“Karibu kitandani!” Majoti akajibu na kuivuta shuka karibu.
“Ok!” Gina akajibu, akavua fulana na kubaki na sidiria na jinzi aliyovaa, akamtupia jicho Majoti na kumkuta katumbua macho.
“Fanya haraka, nazidiwa mwenzio,” Majoti akasisitiza.
“Usiwe na haraka, utakula mpaka utasaza,” Gina akajibu, akauendea mkoba wake, akachukua kimkebe chake cha sigara, “Naomba nivute kidogo, nipate stimu!” akamwambia huku akiketi kitandani.
“Bila shaka!”
Gina akaketi kitandani, Majoti, akaamka na kukaa jirani yake huku mkono wake akiwa kauzungusha kiunoni mwa mrembo wake; akachukua sigara na kubana kwa midomo yake, akachukua kiberiti na kukiwasha, sekunde mbili tu ile sigara ikawa imewaka. Akaibana kwa vidole na kuitoa kinywani, akamtazama Majoti usoni, akarudisha sigara kinywani na kuvuta pafu moja kubwa, kisha akampulizia moshi mtu mzima huyo usoni. Kilichofuata hapo ni vikohozi mfululizo kutoka kwa Majoti.
“We vipi?” Gina akauliza.
“Nimepaliwa na sigara yako, koh! Koh! Koh!” akazidi kukohoa. Gina akainuka na kujifanya anakwenda kuizima sigara hiyo, “Samahani!” akamwambia. Alipogeuka nyuma alimkuta mtu yule kajibwaga kitandani anathema kwa nguvu, Gina akamrudia na kumtazama.
“Samahani sana, sikujua kama moshi unakudhuru,” akamwambia na kumpulizia tena, Majoti akahisi kama anakabwa, akakosa pumzi, macho yakawa mazito, akazidiwa na kuchukuliwa na usingizi mzito. Gina akavaa fulana yake, akainua mkoba wake na kupotelea nje. Tayari ilikuwa saa tano usiku alipokuwa nje ya hoteli hiyo.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom