Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Bora leo kidgo tumepunguza ugwaduKAZI IENDELEE
Tulirudi kwa Patrick sasa:
Ilikuwa saa tatu kamili wakati Patrick na wenzake walipokuwa wamekaa katika sebule ya nyumbani kwake Patrick, nyuso zao wote zikionyesha kuwa na fikira nyingi. Ilikuwa ni wakati ambapo Wanna See alikuwa akimaliza kutoa hoja ya kuvamia pale zahanati iwapo itafika jioni ya siku hiyo bila kupata ufumbuzi wowote. Alikuwa amedhamiria kumteka upya Kikakika ili wakamlazimishe kueleza nilipo na zilipo dhahabu tulizochukua kwa Mr Catto.
Mara ghafla mlio wa ile redio iliyotegeshwa kwa mawasiliano na zahanati ukasikika, wanna See aliisogelea tayari kwa kusikiliza:
"Ehee, unasemaje? Aliuliza wanna See.
"Naomba kuongea na Patrick" ilisikika sauti ya kike.
Baada ya Gilly kuwa amefika zahanati aliamua kumuelekeza yule mpenzi wa Patrick namna ya kutumia ile redio kusudi aweze kusaidia kwa mawasiliano na kwa wakati huo ndio alikuwa anaongea. Patrick aliambiwa na Wanna See, akasogea na kuchukua hiyo redio. "Hallo Patrick hapa naongea,"
"Norack, mambo vipi mpenzi? Alisikika muuguzi.
"Safi tu, sijui una taafa gani? Maana umeniweka roho juu. Alisema Patrick.
"Wale rafiki zake na yule mtu aliyewadhurumu wapo hapa wanaongea na mwenzao. Alisema mpenzeye Patrick.
"Je wamefika muda mrefu?" Patrick aliuliza.
"Kitambo kidogo, lakini wanaonekana kuwa na wasiwasi hivyo wanaweza kuondoka wakati wowote kwani nikewasikia kwa mbali wakijadili kuondoka na mwenzao ambaye kalazwa hapa."
"Ok, nakuja huko sasa hivi, lakini usiwe na wasiwasi siwezi fanya mambo ambayo yatakufanya wewe utambulike." Alimaliza kuongea Patrick na kukata simu, tayari akili yake ilishawaza mbali.
Aliwageukia wenzake na kuwaambia: "Aisee watu tunaowatafuta wapo zahanati wanampango wa kumtoa mwenzao pale" alimaliza.
"Kama ni hivyo twende tukawawahi kabla hawajaondoka ili tuweze kuwafatilia na kutimiza lengo letu tukipata nafasi nzuri." Alisema Wanna See. Patrick na vijana wake walinyanyuka lakini Wanna See akawazuia na kusema " tutaondoka sisi Pamoja na Patrick." Vijana walitulia, Patrick akachukua bastola yake na Wanna See akaingia chumbani na kurudi na bastola tatu. Aliwapa wale wenzake wawili kila mtu bastola moja na kuwaambia twende zetu. Wanna See, Patrick pamoja na wale vijana waliokuja na Wanna See walipanda kwenya Range, maana ndio gari waliloliamini katika shughuri pevu.
Gari lilitiwa moto na Patrick maana ndie alikuwa akiufahami mji wa Mwanza vizuri, baada ya muda mfupi walikuwa wanaegesha gari pale zahanati. Ambapo yule mpenzi wake Patrick (Norack) aliwahi kutoka na kumpasha habari kuwa wametoka muda mfupi tu na mmepishana nao kwani wako kwa mguu. " Naona ndio wale kule" alimaliza kwa kuonyesha kwa mdomo kwani wakati anaongea na Patrick aligeuza shingo na kutuona.
"Okay, kwa heri, tutaonana baadae," alisema Patrick huku na kugeuza gari huku akiwaambia wenzake Kinachoendelea. Walichomoa bastola na kuziweka tayari ili watutwange risasi wakiwa kwenye mwendo. Walipofika karibu walitulenga ndio wakati huo nikaona mitutu ya bastola lakini nilikuwa nimechelewa kwani wana shabaha kama nini sijui. Risasi zilitua vifuani kwetu ni bahati tu tulivaa bullet proof. Tulijirusha na kuanguka mtaloni, kutokana na jinsi walivyoona waliendelea huku wakiamini kuwa wametuua. Patrick na wenzake walirudi nyumbani wakiwa na uhakika wa kazi waliyoifanya na baada ya kufika nyumbani waliwaeleza wenzao jinsi mambo yalivyokuwa. Wote kwa pamoja wakawa na furaha kwani walioma kazi ilikuwa imekwisha labda kummaliza mgonjwa ambaye hakuwa muhimu sana kufa ila kumteka tena ili atoe maelezo ya kina kuhusu dhahabu. Maana Wanna See alikuwa na Imani kuwa lazima anajua zilipo au watu wanaoshirikiana na Pheady.Wakati waliendelea na mjadala wao huku wengine wakiwa kwenye unywaji kwa ajili ya furaha mara mlio wa ile redio ulisikika tena. Safari hii aliyeenda kusikiliza moja kwa moja alikuwa Patrick.
"Hallo Patrick hapa naongea"
"Norack, aisee wale watu wenu wamerudi mda mfupi na kumchukua mwenzao, hivi ninavyoongea ndio wamemaliza kuondoka na gari aina ya Toyota Land cruiser Tz 1678." Alimaliza maelezo Norack na kupumua kidogo wakati Patrick hakuamini anachokisikia.
"Unasema ukweli wamerudi hapo na kumchukua huyo mgonjwa?" Patrick aliuliza kama mtoto.
"Kama nilivyokueleza ndivyo ilivyo" alijibu Norack. Patrick uso ulimbadilika, akaongea kwa kuunguruma, "mwambie huyo mtu wetu hapo aje nyumbani kwangu, alafu wewe tutaonana saa nne usiku Magnum maana leo kuna disco pale." Alimaliza na kukata mawasiliano. Alishachanganyikiwa kutokana na habari za Mimi Pheady na mwenzangu Sonno kuwa hai kutokana na shambulio walilolifanya kwetu haikuingia akilini sie kuwa hai tena bila mikwaruzo.
"Vipi mbona unatutisha kwa uso?" Aliuliza wanna See huku akimkazia macho Patrick.
"Kuna habari za kushangaza zinasema Yule mtu na Mwenzie wako hai, wamerudi pale zahanati na kumchukua mwenzao baada ya sisi kuwa tumetoka pale." Alieleza Patrick.
Wote walishikwa na butwaa, baadae kidogo Zuberi akawa kama mtu anayetoka usingizini na kuuliza: "Ina maana hawakufa?" Hakuna aliyemjibu wote walikuwa kimya.
"Inaonekana wake washenzi walikuwa wamebana bullet proof." Hatimae Wanna See alisema.
"Nafikiri kitu kama hicho,"Aliunga mkono Patrick.
"Kwa hiyo kazi imeanza upya." Alisema yule kijana wa kizungu aliyekuja na Wanna See.
"Sasa inabidi tuanze mipango mingine haraka sana, kwani kutokana na shambulio tulilowafanyia hao washenzi wanaweza kukimbia mji haraka sana." Alisema Wanna See."Namba za gari wanalotumia zimepatikana, nafikiri zinaweza kutusaidia pa kuanzia." Patrick aliongea.
Mara mlango uligongwa alafu ukasukumwa akaingia Gilly ambaye alipitiliza na kwenda kukaa kwenye sofa lililokiwa wazi pembeni. "Hali zenu waungwana" alisabahi baada ya kukaa. "Safi tu," walisema kwa pamoja alafu wakaendelea na maongezi.
"Okey, sasa inabidi tutapakae mjini na kila sehemu ya barabara kuu inayotoka katikati ya mji wa Mwanza. Kila mtu na gari lake na redio kwa ajiri ya mawasiliano, atakayeona gari hilo lenye namba hizo aina ya land cruiser awasiliane na wengine bila kuchelewa. Nafikiri hilo litakuwa ni Jambo la maana kufanyika muda huu." Alisema Wanna See.
"Sawa, hakuna tatizo," walisema kwa pamoja huku wengine wakisimama tayari kutawanyika.
"Hebu subiri kidogo" alisema Wanna See ghafla. Alafu akaendelea "yule mtu aliyekuwa anatuletea mawasiliano kutokana kule zahanati yupo kwenye mpango wa malipo yetu au ulimtumia kwa dharura tu?" Aliuliza Wanna See huku akimwangalia Patrick usoni.
" Nilimtumia kwa dharura tu, nikiwa nimemuahidi pesa na kumjengea nyumba iwapo atanisaidia. Patrick alijibu.
"Kwa hiyo unasemaje? Anaweza kuwa shahidi baadae. Wanna See alisema.
"Kwani wewe ulikuwa na maoni gani?" Aliuliza Patrick.
"Mimi naona kumzima pumzi litakuwa Jambo la maana zaidi, asije akawa mwiba baadae, kwani wanawake wasio na mafunzo maalumu huwa ni wepesi wa kufanya makosa. Alisema Wanna See.
"Sawa niachie suala hilo nitalifanyia ufumbuzi." Patrick alijibu na baada ya hapo walitawanyika kwenda kusaka gari tulilokuwa tunatumia.
Patrick gari lake kwenda mjini huku akiwa mwingi wa mawazo, alikuwa anafikiria jinsi ya kumuua Norack huku akiwa ni mpenzi wake. Roho ilimuuma sana, akapitisha uamuzi wa kumuacha hai na kumpa kila kitu atakachohitaji ili aendelee kuficha siri kuliko kumuua. Wakati huo ilikuwa saa tano na dakika kadhaa na washirika wote wa Patrick walikuwa wametapakaa Mwanza kila mtu na eneo lake. Patrick alikuwa mabatini, Wanna See na mzungu mwingine walikuwa Mwanza Hotel, yule mwenzie muafrika waliyekuja naye alikuwa kwenye bustani ya mzunguko ulio karibu na jengo la CCM makao makuu Mwanza alafu wale vijana wengine walitawanyika mjini kila mtu na eneo lake kutusaka.
Ilikuwa saa sita kasoro dakika kadhaa hivi ambapo redio ya Patrick ilionyesha kuwa mtu anaita. Patrick alibonyeza sehemu maalumu kwa kuunganishwa mawasiliano na kusogeza sikioni. "Patrick hapa," alisema. "Gilly hapa,' sauti ilisikika alafu ikaendelea; 'Nimewanasa hapa hao jamaa wana gari lao na mmoja ameingia kwenye ofisi za Tanganyika bus." Alimaliza kuongea.
"Sawa wewe wafuatilie kwa akili sana sie tutakuwa nyuma yako tuwe tunawaailiana, je? Wengine wana habari hiyo. Alimaliza maelezo na kuuliza swali. "Ndio, wamesema niwasiliane na wewe." Alijibu Gilly. "Sawa kama ni hivyo wewe endelea kuwafatilia mimi napanga namna ya kuwateketeza." Patrick alimaliza kusema na kukata mawasiliano. Hapo akaanza kuongea na vijana wengine ili kupanga namna ya kufanya ndipo walipoonana wote na Patrick akaamuru watumie Range kumufuata Gilly ambaye alikuwa anatufuata bila sisi kujua. Walitufuata mpaka tulipofika kwa Mzee Magesa ndipo walipofanikiwa kutushambulia, ni katika shambulio hilo ambapo Mr Sonno alipoteza maisha.
Katika wale watu waliotuvamia alikuwa ni Patrick ndie aliyemuua Sonno na kufanikiwa kukimbia na gari huku akiacha vijana wake wote wakiwa maiti. Alipotoka pale alikuwa mithili ya kichaa kwani hakuamini macho yake kuona vijana wake wakiteketezwa kama utani vile. Alivurumisha gari mpaka Mwanza Hotel ambapoa alijua atamkuta Wanna See, na kweli alimkuta akiwa nafasi ya wazi alikuwa amekaa na yule mzungu mwenzie huku wakinywa kahawa.
Patrick alishuka kwenye gari na kuwafuata walipokuwa wamekaa, alivuta kiti cha pembeni maana meza waliyotumia ilikuwa na viti vinne. Baada ya kukaa aliwaeleza kwamba mambo sio mazuri kwani wamepoteza vijana wote na huyo anayetakiwa kuuawa bado anaishi yaani mimi Pheady. Wanna see aliposikia hivyo alimwambia Patrick atangulie nyumbani wao wanamfuata nyuma ili wakaongee vizuri kwani mahali hapo hapakufaa kwa maongezi kama hayo. Patrick bila ajizi akinyanyuka na kuiendea gari yake alafu akatia moto huyo mpaka nyumbani kwake. Alipofika nyumbani kwake cha kwanza ilikuwa ni kwenye jokofu ambapo alitoa chupa ya John Walker na kumimina kimiminika chake kwenye birauli alafu akapiga kama funda tatu akiwa amesimama na baada ya hapo akasogea kwenye sofa na kukaa. Kwa kweli alikuwa ameghafirika, ungemuona wakati huo alitia huruma. Alikunywa ile pombe iliyokuwa kwenye birauli ilipoisha alimimina nyingine na kuendelea kunywa.
Haukipita muda mrefu Wanna see na wenzie wawili wakawa wamefika na kuchukua nafasi katika sofa, nao wakionyesha nyuso za huzuni.
"Halo Patrick hebu tupe habari kwa kifupi kuhusu kilichotokea ili tuweze kujadili Kinachoendelea, kwani naona tumebaki sisi tuliopo hapa kutekeleza kazi hii" alisema Wanna see.
"Patrick alimeza funda la pombe alafu akatia sigara na kuwasha, baada ya hapo alieleza mambo yote yalivyokuwa mpaka kufikia yeye kumuua Sonno na kukimbia.
Baada ya kuwa wamesikiliza wote kwa umakini walijadili na kukubaliana kuvamia kwa kule kwa mzee Magesa usiku, wakiwa na Imani kuwa mimi nitakuwa kule au sivyo Mzee Magesa atakuwa na cha kuwaambia kuhusu nilipo. Kwani suala muhimu ilikuwa ni kuhakikisha mimi ninakufa ili wapate pesa toka shirika la kijasusi Afrika Kusini. Wakati wanamaliza kujadili mipango yao ya kunitoa roho ilikuwa kwenye saa tisa hivi. Ghafla Wanna See alikumbuka jambo na kumuuliza Patrick; "Vipi kuhusu yule mwanamke wa mawasiliano una mpango gani naye mpaka sasa? Natumaini unaona wazi jinsi anavyoweza kuwa mwiba kwetu." Patrick akili zilishamvurugika kutokana na vifo vya wenzie hivyo hakuona sababu ya kuendelea kumthamini Norack tena. " Nina mpango wa kumuua muda mfupi ujao tena hapahapa na maiti yake mtaiona." Hatimae Patrick alijibu huku akitabasamu utafikiri anaongea kuhusu kuchinja kuku kwa ajili ya kitoweo.
"Sawa, kama ni hivyo itakuwa bora zaidi, sijui huo mpango wako unautekelezaje?" Alihoji Wanna See.
"Hiyo isiwape wasiwasi, mpango mzima ninao kichwani, nyie subirini kuona kichwa chake ifikapo saa mbili usiku. Patrick alisema kwa kujiamini, alionyesha pombe ilishamkaa kiasi. Baada ya maongezi hayo Wanna See na wenzie waliingia vyumbani kupumzika maana walijua kutakuwa na shughuri kubwa ifikapoa usiku. Patrick yeye alibaki hapo sebuleni akiwa ameegamia sofa huku akitazamana na chupa ya John Walker.
Aliendelea kukaa katika hali hiyo kwa muda mrefu huku picha ya maisha yake ikimuuijia akilini mwake kama ndoto vile. Aliwaza pindi atakapokuwa amemaliza hii kazi ya kumuua Pheady atakwenda kuishi Ulaya kwani atakuwa na pesa za kutosha vilevile ili kukwepa mkono wa sheria kutokana na mauaji yanayotokea ya watu wake wa karibu. Alijikuta akitaka kutimiza adhima ya mauaji kwa haraka sana ili apotee Tanzania. Alikuja kushtuka kutoka katika mawazo hayo aliposikia mlio wa saa ya ukutani ukiashiria saa kumi na moja jioni. Ailijinyanyua kutoka pale sebuleni na kwenda kuoga, baada ya kuoga alijiweka katika hali ya utanashati na kurudi sebuleni ambapo aliwakuta akina Wanna See wameishafika pale sebuleni. Aliliendea simu na kuzungusha namba za zahanati. Simu ilisikika ikiita upande wa pili alafu ikinyanyuliwa bila kusalimia alijikuta anaropoka "Naomba kuongea na Norack"
"Subiri," sauti ya upande wa pili ilisikika.
Ungetupia hata vipande viwili mkuu.Haahaa mkuu tuvumiliane
Uyo mzee w kimoko tuUngetupia hata vipande viwili mkuu.
Utamu koleaKAZI IENDELEE

Pamoja mkuuNiwieni ladhi kidogo nimepata dharura ya safari hivyo jumatano ndio nitawapatieni haki yenu hapa
Leta mambo mzee!!Likes na comments ndio zitaleta mwendelezo karibuni sana wapenzi wa riwaya.
Mwenye kuwajua anaruhusiwa kuwatag