Riwaya: Jina langu ni Pheady

Riwaya: Jina langu ni Pheady

Niwieni ladhi kidogo nimepata dharura ya safari hivyo jumatano ndio nitawapatieni haki yenu hapa
Mkuu junatano ndio leo shusha mzigo mchana huu na baada ya mechi ya Yanga shusha mzigo mwingine kusindikizia maumivu au ushindi wa Yanga.

Naamini hutotuangusha.
 
Ni majukumu tu. Huwa sivunji ahadi. Nilishasema lazima iishe hapo. Liwe juwa iwe nvua
 
KAZI IENDELEE



"Subiri," sauti ya upande wa pili ilisikika.
Baadae kidogo sauti ilisikika tena: "Hallo Norack hapa".
Patrick ninaongea, habari za asubuhi?"
"Nzuri, sijui wewe!"
"Mie poa tu, vipi kuna lolote lililotokea huko?
"Hapana ila yule mgonjwa wenu mliyemleta naye kaondoka." Alisema Norack.
"Hilo nalifahamu, tunaye hapa, vipi unatoka saa ngapi?"
"Natoka saa kumi na mbili jioni hii, hivyo nina muda wa saa nzima mbele."
"Ok, tutaonana kama tulivyopanga. Alisema Patrick.
"Sawa hakuna tatizo." Norack alijibu.

Baada ya maongezi hayo Patrick alikata simu, alikuwa ameishapata alichotaka kwani kama utakumbuka waliishaahidiana wakutane usiku lakini Patrick alitaka kujua muda wa kutoka kazini ili afanye ajuavyo.
Ilikuwa saa kumi na mbili wakati Norack alipotoka. Patrick aliweza kumuona vizuri sana, alikuwa kwenye gari ambalo Norack halijui. Norack alichepuka barabara na kuanza kutembea akielekea barabara inayotoka mjini kwenda kirumba. Patrick alipoona anaelekea huko alitia gari moto na kupita barabara nyingine alipofika mbele aliegesha gari sehemu ambayo alijua Norack atapita tu. Baada ya muda si mrefu alionekana Norack akitokeza na kupita karibu na ile gari. Patrick ambaye alikuwa katika kibanda pembeni akinywa soda alipokuwa usawa wa gali. Norack alisikia na kugeuka kuangalia, ndipo alipoiona sura ya Patrick akimjia akasimama kumsubiri.
"Vipi," Norack aliuliza baada ya kuwa karibu.
"Natoka kumsindikiza rafiki yangu ndio nikaona nipate soda hapa na kukuona wewe unapita.
"Ahaa! Mie ndio natoka kazini hivyo.
"Ok, kama ni hivyo panda kwenye gari twende zetu." Patrick alisema huku akifungua mlango wa gari iliyokuwa karibu yao.
"Ohoo! Ndio usafiri ulionao huu sio?" Alisema Norack huku akitazama kwa makini ile gari maana ilikuwa bado mpya. Alipanda kwenye gari na na Patrick akawasha na kuanza safari.
"Nafikiri tungepitia nyumbani kwangu kabisa nikakupe mzigo wako huenda tusionane tena. Baadae nitakuwa na wageni alafu kesho naweza kusafiri" Patrick alimuambia Norack gari ilipokuwa imekamata barabara.
"Sawa, hakuna tabu kwani sina jambo la muhimu kwa sasa, nilikuwa nafikiria appointment yetu tu." Alisema Norack

Patrick aliendelea na barabara na alipofika pale Hospital ya Hindu Mandal aligeuza gari na kurudi walikotokea. Aliongoza moja kwa moja mpaka kwake na kuingiza gari getini ambapo aliegesha pembeni ya nyumba. Walishuka kwenye gari na kuongozana ndani, Norack hakuwa mgeni pale. Patrick alisukuma mlango na kuingia ndani, walifika sebuleni na kuwakuta Wanna See na wenzake wakiwa wanakunywa mvinyo huku wakiangalia mkanda wa video ya American ninja 4. Norack aliwasalimia na kukaa kwenye sofa ya watu watatu ambayo haikukaliwa na mtu. Patrick alifululiza mpaka chumbani kwake baadae kidogo baada ya muda kidogo akatoka akiwa amevaa pajama huku ameshikilia chupa ya bia mbili mkononi. Alifika na kukaa sofa moja na Norack alafu akavuta stuli iliyokuwa karibu na kuweka zile bia.
"Kachukue birauli hapo kwenye kabati." Patrick alimuambia Norack. Wakati Norack ananyanyuka kwenda kuchukua birauli Patrick alisema tena: "Nichukulie na chupa ya John Walker kwenye jokofu hapo." Norack alifanya mambo yote hayo na kurudi kukaa karibu na Patrick. Wakati wote huo Wanna See na wenzake waliendelea kunywa huku wakionyesha kuwa makini na ule mkanda wa video.

Patrick alifungua bia na kummiminia mpenziwe kwenye birauli alafu yeye akajimiminia John Walker na wakaanza kunywa. Norack alipomaliza bia ya kwanza akasema hajisikii vizuri hivyo anataka kuoga kwanza. Patrick alimuambia afanye anavyojisikia, hivyo Norack aliondoka na kuingia chumbani kwa Patrick. Baada ya muda kidogo alirudi akiwa tayari ameishaoga, unywaji ukaendelea kama jadi. Baada ya ule mkanda wa video kufika mwisho, Wanna See na wenzake wakaondoka na kuingia vyumbani mwao

Sebule ilibaki na Patrick na Norack waliendelea kunywa, Patrick alikuwa akimchanganyia bia na John Walker Norack, hivyo baada ya muda mfupi Norack alishaanza kulewa. Patrick alianza kumchezea maungo yake huku akimpapasa mipapaso mikali iliyoanza kumrusha pumzi Norack, alisikika akihema bila mpangilio. Baada ya huo mchezo kuwa umekolea walijikuta wakihamia chumbani. Ilikuwa ni kitandani ambapo walikuwa wamemalizia ngwe ya mchezo wa kwanza hivyo waliamua kuingia ngwe ya pili. Patrick alimuambia wabafilishe uwanja na kwenda kwenye meza iliyokuwa humo chumbani. Norack aliilalia meza kwa tumbo huku niuno akiwa amekibinua ipasavyo na Patrick alikuwa nyuma yake akibembea huku akimpapasa na kupikicha chuchu za Norack. Ilikuwa ni wakati wa kilele cha mchezo Norack alipozidisha kukata kiuno ndipo Patrick alipochomoa upanga uliokuwa pembeni ya meza, Norack hakuwa na habari na yanayojili kwani alikuwa amenogewa na utamu. Ghafla kama umeme Patrick alishusha ule upanga shingoni mwa Norack na kutenganisha vipande viwili kichwa kilibaki mezani na kiwiliwili kilijirusha kilianguka sakafuni. Yalikuwa ni mauaji ya kinyama yasiyostahili katika jamii ya binadamu. Kichwa kilionekana kikitoa macho kwa kurembua alafu kikafumba. Patrick alitabasamu tabasamu la kiuaji, hakupendeza na hilo tabasamu lake, kweli alichukiza. Damu zilitapakaa sehemu kubwa ya chumba na katika maungo yake Patrick. Alichukua maji baridi toka kwenye jokofu na kuvimwagia vile vipande vya mwili wa Norack ili kupunguza uvujaji wa damu, baada ya hapo alifanya usafi humo chumbani na kuoga.

Ilikuwa ni saa mbili na nusu hivi alipokuwa amemaliza kutekeleza unyama wake huo. Alitoka chumbani mwake na kwenda sebuleni ambapo aliwakuta wakina Wanna See wakila vyakula vya kwenye makopo.
"Hallo kazi uliyoitaka nimemaliza." Alisema huku akimuangalia Wanna See.
"Alaa!! Ushamtoa mtu uahai mara hii!?" Wanna See alisema.
"Ndio, twendeni mkaangalie" Patrick alisema kwa kusisitiza utafikiri alilofanya ni la maana. Kweli alionekana kama kichaa kwani mtu mwenye akili timamu hawezi furahia kumuua mpenzi wake. Walisimama wote na kuongozana chumbani kwa Patrick, walipofika waliangalia vipande vya maiti iliyo uchi. Wote walitabasamu kifedhuri alafu akasikika yule mzungu mwingine akisema; "Kweli wewe ni mpiganaji wa hali ya juu, unamuua mtu kwa upanga bila hata kutoa sauti!!". Walitoka mle ndani na kujaza upepo mtumbwi wao alafu wakapakia ile maiti na kuifunga jiwe, kichwa nacho kikafungwa jiwe. Walipiga kasia na kwenda kuitumbukiza kina kirefu cha maji ziwa Victoria.

Ilipofika saa saba usiku walikuwa wameisha maliza mambo yao, hivyo walikuwa wanaanza safari ya kuelekea kwa mzee Magesa kama walivyopanga. Safari ilianza kwa kutumia gari mbili, Wanna See alikuwa peke yake kwenye gari la nyuma wakati Patrick na yule mzungu mwingine pamoja na yule mzulu walikuwa katika gari moja lililokuwa mbele. Mwendo ulikanyagwa kuelekea kwa mkuu wetu wa ofisi za hapa Mwanza, kwa kuwa ilikuwa usiku gari ziliongozana kwa kuachiana nafasi kubwa kwani kulikuwa hakuna magari mengi wakati huo. Patrick alifika mbele ya ile nyumba na kutoa ishara ya kumjulisha Wanna See kuwa ni hapo alafu akapitiliza na kwenda kuegesha mbali kidogo. Walitelemka na kuanza kurudi kwa mguu, Wanna See alipoona ile ishara aliegesha kule kule nyuma gari lake nae akatoka na kuanza kutembea kwa mguu. Usiku ulikuwa umetulia, haukuonyesha dalili za viumbe hai kuwa macho maeneo hayo. Wanna see ndie alikuwa wa kwanza kuifikia nyumba ile, alizunguka kwa pembeni ya ua kama mpita njia huku akiaangalia kwa makini eneo la hiyo nyumba. Wakati wote mkono mfukoni ukichezea bastola.

Kutokana na kuwa taa zilikuwa zinawaka sehemu zote kuzunguka nyumba, haikuwa kazi kuona ndani ya ua na kubaini kuwa hakukuwa na ulinzi. Alipokuwa kwa nyuma alimuona Patrick akichepuka kichocholoni na kuelekea upande aliokuwepo, alimsubiri kwa kujikinga sehemu yenye giza. Alipokuwa amekaribia sehemu hiyo Wanna See alijitokeza na kumfanyia ishara amfuate. Patrick alimkaribia na kumsikiliza; "Nenda uwachukue wenzio mpitie kwa mbele hakuna ulinzi, ila muwe makini inaweza kuwa mtego. Mimi nitawachunga, nitakuwa tayari nimeisha ingia ndani ya ua" alimaliza maelezo na Patrick akatekeleza. Wanna See alijisogeza nyuma kidogo alafu akavuta pumzi alijirusha katika mtindo wa kujiviringisha hewani na kujigeuza mara mbili hewani akawa ametua ndani ya ua huku kachuchumaa. Alitua bila kishindo chochote huku masikio yake yakiwa makini kwa kusikiliza aina yoyote ya mjongeo au sauti. Alipotua chini tu alikuwa ameishaangaza mazingira yote ya pale, hivyo alilala chini na kutembelea tumbo mpaka ukuta wa nyumba. Alikuwa amefikia chini ya dirisha kwa nyuma huku akiwa hatua chache kutoka kwenye mlango wa nyuma. Aliendelea kujivuta kwa tumbo na kuufikia mlango, alichungulia kwa chini ya mlango ambapo kulikuwa na nafasi kidogo lakini hakuona kitu wala kuhisi kitu. Alijivuta mpaka kwenye pembe ya ukuta na kuchungulia sehemu ya mbele ya nyumba, aliwaona Patrick na wenzake wakiwa wanaruka geti lililokuwa limefungwa kwa ndani.

Baada ya kutumbukia ndani walikimbia kwa tahadhari hukua wakiwa wameinama mpaka kwenye ukuta wa nyumba na kujibanza sambamba na ukuta. Walisikilizia kidogo alafu wakapeana ishara ya kutawanyika kuzunguka nyumba huku wakikagua sehemu za madirisha. Patrick yeye alibaki mlango wa mbelea. Baada ya kuzunguka wale wawili walikutana nyuma ya nyumba na Wanna See ambaye wakati wote alikuwa makini. Walipoonana kule nyuma Wanna See alimuambia yule mzulu akamuambie Patrick wanaingilia nyuma hivyo awe makini kwa ulinzi huko mbele, kama atasikia purukushani afanye atakavyo fikiri linafaa. Yule mzulu alifanya hivyo na kurudi nyuma ambapo aliwakuta wenzie wakiwa wanajaribu kufungua mlango na funguo malaya.
Mara mlango ulikubali, kitasa kikaachia Wanna See akawaambia wenzie wakae tayari kwa lolote yeye anajitosa ndani. Wakati yote hayo yanatokea Mzee Magesa na vijana wake watatu walikuwa wanawaaikia wakiwa sebuleni nyuma ya sofa huku wakiwa tayari kwa mashambulizi. Hiyo ilitokana na kuwa baada ya shambulizi la mchana pale kwake alijua wale watu hawataridhika wangeweza kurudi usiku.
Hivyo alikuwa ametoa familia yake baada ya kuwa imerudi na kuipeleka katika nyumba yao nyingine iliyoko Nyamanoro. Baada ya kufanya hivyo akawachukua vijana watatu wanaofanya kazi chini ya ofisi ya hapo Mwanza ili waweze kumsaidia katika ulinzi wa hapo nyumbani kwake. Hakuona sababu ya kukimbia nyumba iliyo yake. Kwa hiyo wakati funguo zinaingia na kutekenya mlango walizisikia na kuvuta pumzi huku wakisubiri kitakachotokea. Walikuwa katika mfumo wa ulinzi uitwao " kimya cha ulinzi" ni ulinzi unaokutaka usieleweke kama upo katika mazingira hayo.
Wanna See alisukuma mlango na kujirusha ndani kwa kutanguliza mguu wa kushoto huku bastola mikononi, alitua ndani akiwa amegeuka kuangalia nyuma alikotokea. Hakuona kitu nyuma ya mlango kama alivyofikiri, alimuona yule mzulu akiwa pembeni ya mlango kwa nje akimulinda yeye. Aligeuka na kuangaza akagundua yuko kwenye korido ambapo pembeni yake kulikuwa na mlango wa chumba huku korido ikiendelea sebuleni. Alitoa ishara kwa yule mzulu naye mzulu akamnong'oneza yule mzungu alafu yule mzungu akaingia ndani, kule ndani kwa nyuma alibaki yule mzulu kwa ulinzi. Yule mzulu alipomfikia Wanna See alimuambia akae tayari alafu akaujaribu mlango ulikuwa wazi na kuonyesha hiyo ilikuwa ni sehemu ya jikoni, aliingia ndani kwa tahadhari na kuangaza lakini hakuona cha maana. Alitoka na kumuambia yule mwenzie wasonge mbele. Walifika mwisho wa korido ambapo mbele yao kulikuwa na sebule. Waliangaza sebuleni huku wakiwa wamejibanza ukutani, hawakuweza kuona dalili za mtu katika sebule na kwa pembeni kidogo kulikuwa na mlango ambao walihisi ni wa chumba cha kulala. Wanna See alijiviringisha chini mfano wa tairi na kufika pale mlangoni akiwa amechuchumaa. Alizungusha macho kwa haraka chini ya zile vungu za sofa na kuona watu, palepale alijirusha hewani na kutua nyuma ya jokofu huku akikoswakoswa na risasi. Yule mwenzie alimuona mtu aliyemvurumishia risasi Wanna See na akamuwahi na risasi kama tatu za shingoni na kuwa maiti palepale.

Naam! Tayari mapambano yalikuwa yameiva, yule mzungu aliendelea kuvurumisha risasi upande ule ili kimlinda Wanna See. Naye Wanna See aliendelea kukaa nyuma ya jokofu huku akichemsha akili kwa haraka, wakati huo Magesa Alisha tembelea tumbo na kuwa chini ya sofa lililo karibu na korido. Wale vijana wa Magesa alishakufa mmoja hivyo walibaki wawili, mmoja nae alitembelea tumbo kunyemelea jokofu na mwingine alijibu mashambulizi ya yule mzungu huku akiwa nyuma ya sofa.
Magesa alimuona yule mzungu na kunyanyua bastola yake, risasi iliyoachiwa na Mzee Magesa ilimpata yule mzungu usawa wa kichwa na kumrusha. Juu, alipotua chini alikuwa maiti tayari. Wanna See alipomuona mwenzie akianguka chini alipandwa na mori na kujirusha kwa namna ya ajabu huku akijiviringisha hewani. Ni kitendo ambacho Magesa na vijana wake hawakukitegemea, akiwa hewani alimuona yule kijana aliyekuwa akitembelea tumbo kumfuata akampiga risasi tatu akiwa huko huko hewani. Alipofika chini aligusa tu na kujirusha tena kurudi nyuma ya jokofu. Yule kijana wa Magesa aliyekuwa nyuma ya sofa alimuona Wanna See alivyofanya, alijisogeza sehemu nzuri na kuanza kutupa risasi kuelekea kwenye jokofu. Wakati wote huo Patrick alishahisi vurumai ndani ya nyumba pamoja na kuwa walikuwa wakitumia bastola zenye viwambo vya kuzuia sauti. Patrick alitoka pale mlangoni na kijisogeza kwenda dirisha walilokuwa wamerukia wenzie mchana na kukutana na mauti. Alipolifikia alikuta kioo kikiwa kimepasuka hivyo aliingiza mkono kwa tahadhari na kuvuta pazia. Aliweza kuona ndani na kukuta yule kijana wa Magesa akiwa anavurumisha risasi upande wa jokofu. Alimlenga na bastola na kumpigia risasi ya kichwa iliyomrusha na kuangukia juu ya sofa. Wanna See alishituka baada ya kuona mkatiko wa mashambulizi, alichungulia kwa pembeni ya jokofu kwa tahadhari ndipo alimuona mzulu akiambaaambaa pembeni mwa ukuta kwenye korido kuelekea sebuleni. Ghafla aliona mkono ukichomoza chini ya sofa ukiwa umeshikilia bastola ukimuelekea yule mzulu ambaye alikuwa hajaona. Kitendo bila kuchelewa Wanna See aliwahi kuupiga risasi ule mkono na bastola iliyokuwa imeshikiliwa na ule mkono ikaanguka pembeni. Ulikuwa ni mkono wa Mzee Magesa ambaye baada ya kupata dhoruba hiyo aliguna na kujiviringisha chini ya sofa akawa nyuma ya ya sofa. Mkono wake wa kulia ulikuwa umevunjwa kwa risasi, alichomoa bastola nyingine kwenye Sox kwa kutumia mkono wa kushoto alafu akaishika barabara tayari kwa kuendelea na mapambano. Wanna see alimuonyesha ishara yule mzulu abaki hukohuko. Mzee Magesa akinyanyuka huku akiwa ameinama usawa wa sofa na kuanza kijisogeza pembeni mwa sofa, mahesabu yake ilikuwa aingie chumbani mwake ili atoroke kwa kutumia dirisha lake maalumu ambalo lilikuwa chumbani kwake. Bahati mbaya alikuwa amechelewa kwani wakati anakaribia ukingoni mwa sofa Patrick alimuona kwa dirishani na kumpigia risasi ya mkono uliokuwa umeshikilia bastola. Alitoa ukelele na kujirusha juu huku akijiviringisha hewani na kutua katikati ya korido huku mikono yote ikiwa imeishavunjwa kwa risasi. Alinyanyua mguu kutaka kukimbilia mlango wa chumbani lakini Wanna See aliwahi kujirusha alipo na kumpigia teka la mzunguko lililompata shingoni na kumpeleka chini, yule mzulu alifika bastola mkononi na kumuelekezea kifuani akiwa pale chini. Mzee Magesa alijua siku zake zimefika akatulia, nyumba kilinuka harufu ya damu, maiti nne zilikuwa mle ndani zikivuja damu. Patrick aliyaona yote yale akatathimini hali ya usalama alafu akafungua dirisha na kujirusha ndani. Wote walimzunguka Mzee Magesa na kuanza kumuuliza maswali kuhusu mimi Pheady.
Kutokana na hali aliyokuwa nayo Mzee Magesa haikuwawia kazi ngumu kumshurutisha, naye aliwaeleza yote anayoyafamu kunihusu. Baada ya hapo walihitimisha maisha yake kwa risasi tatu za kifuani na kuanza kupekua nyumba nzima mpaka kule kulikofichwa maiti za wenzao. Baada ya kumaliza shughuri ya upekuzi walichukua petrol na kumwaga kuzunguka nyumba na nyingine ilimwagwa vyumbani. Petrol nyingine ilibaki kwenye dumu ambapo walichomeka kamba ya katani alafu wakatoka huku wakiitandaza, walipofika nje ya geti waliiwasha moto na moto ukaongoza kufuata ile kamba mpaka kwenye dumu ambapo kulitoke mlipuko na moto ukaanza kuwaka kuzunguka nyumba.
Walikimbia na kuingia kwenye magari yao na kutia moto na kurudi zao. Walikuwa wamebaki watatu kwani mmoja wao mauti ilimkuta kule kwa mzee Magesa. Hivyo walibaki; Patrick, Wanna See na yule kijana wa kizulu. Walipofika nyumbani kwa Patrick walipanga kwenda Ukerewe ili wanimalize mimi Pheady. Ilikuwa ni saa tisa na nusu usiku walipoingia vitandani kusubiri kesho ifike ili wanifungie kazi.
 
Back
Top Bottom