Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli kabisa mfano Umetaja Kilimahewa ni Jirani kabisa na Ghana mitaa yangu pia.. nimeishi Igoma, Igogo, Ghana, kirumba, Bwiru na kuweka makazi ya kudumu Kitangiri.. hivyo naenjoy tu.Natumaini unapata picha nzuri ukioanisha mitaa na matukio.
Safi kabisa hii riwaya inachezewa Mwanza hivyo wasomaji wa Mwanza watakuwa wanaona picha ya mji wao katika maandishi.Ni kweli kabisa mfano Umetaja Kilimahewa ni Jirani kabisa na Ghana mitaa yangu pia.. nimeishi Igoma, Igogo, Ghana, kirumba, Bwiru na kuweka makazi ya kudumu Kitangiri.. hivyo naenjoy tu.
Piga kazi kjn people zinapita kimya kimya!Mdogo mdogo tunasonga. Ila comments ni chache sana, zinanikatisha tamaa.
Bonge la riwaya kakaAsante ila michango ya wasomaji ni michache sana labada riwaya si nzuri hivyo nawachosha tu!!??
Raha ya Manju ni kuona hadhira inashangilia hapo Manju anaweza madoido mpaka ukimuambia arudie alichofanya anashidwa. Na raha ya mwandishi ni kuona muitikio wa hadhira ( wasomaji). Kadri comments zinapokuwepo nani na kazana.Piga kazi kjn people zinapita kimya kimya!
Nzuri Sana mkuuTWENDE KAZI
7
Nilipoingia ukumbi wa disk nilitafuta sehemu nzuri ya kukaa, viti vingi vilikuwa wazi watu walikuwa ukumbini wakicheza mziki. Nikakaa kwenye kona moja itakayo niwezesha kuona karibu sehemu nzima ya ikumbi wa disko, niliwasha sigara na kuanza kuvuta wakati naangalia watu wakicheza na baada ya muda akapita muhudumu ambaye nilimuita na kumuagiza aniletee chupa ndogo ya pombe aina ya Long John. Aliniletea nikaendelea kunywa huku nikiwaza na kuwazua, nilikuwa nimekaa karibu saa moja na kitu hivi walipoingia wasichana wawili warembo sana na wamevaa mavazi nadhifu. Walipoingia waliongoza moja kwa moja na kuja kukaa kwenye meza iliyokuwa karibu yangu, muda mfupi baadae muhudumu aliwaletea bia za kopo aina ya Stella, nilishangaa kidogo kuona wasichana wawili tu aniletewa katoni nzima kwa mpigo. Walianza kunywa huku wakiongea taratibu na kitambo kidogo walikuwa wameisha kunywa nusu ya katoni na hapo sauti zao zilianza kupanda kiasi cha kuwasikia maongezi yao. Baada ya muda mfupi kidogo waliniomba niwaangalizie bia zao wakacheze disko, kwa kuwa waliona mimi ndio nilikuwa meza ya jirani yao.
Ulikuwa ni muziki wa rhumba uliopigwa na Oliver Ngoma ndio ulikuwa unapigwa nao waliucheza vizuri sana na kwa maringo hasa punde uliunganisha muziki uitwao Azaraki nao wa Oliver. Vimwana waliendelea kucheza name niliwaangalia kwa chati, baada ya kwisha mziki wa Azaraki walirudi kukaa sehemu yao. Walipo rudi sehemu yao walinishukuru huku wakinikaribisha nijiunge nao nami nilishukuru na kuendelea kukaa nilipokuwa wao waliendelea na maongezi yao huku wakizitimba bia.
Ghafla mawazo yalirudi kwa Sonno na Kikakika, nikajihisi vibaya kwa kutokuwa nao wakati huo, nilipoangalia saa yangu ilikuwa ni saa mbili na dakika ishirini na tano na Sonno alikuwa bado hajarudi. Nilitupa macho kwa wale wasichana nikaona mmoja wao akiangalia saa yake alafu nikamsikia akimaka, “Unajua huyu Patrick mshenzi sana”alimueleza mwenzie. Roho ikanishituka kusikia jina, nikatega masikio kunasa sauti zao zaidi.
“Hata mimi huwa namchukia, sijui kwa nini Moddy anamuona wa maana kiasi cha kuniacha nikastare peke yangu na yeye kuongozana naye. Mwenzie alichangia katika maongezi ya rafiki yake.
“Basi mimi ndio usiseme maana namchukia ile mbaya, sasa fikiria kitendo cha kuja kumchuka Zuberi kwangu mchana wakati akisubiri mlo ni uungwana huo”. Aliongea Yule msichana wa kwanza.
“Mimi nashangaa sana kuhusu huyu Patrick, toka wiki hii ianze amekuwa akimfuatafuata sana Moddy, mara ampigie simu aende kwake, wakati mwingine amuijie na gari. Kwa mfano usiku wa jana kampigia simu jioni akaenda na hakurudi mpaka saa tisa usiku ndio anarudi. Nilipomuuliza akanambia alikuwa kwenye mambo ya biashara” aliongea Yule mwingine.
“Kama ni hivyo inashangaza kwani hata mimi Zuberi aliniaga kuwa anakwenda kwa Patrick na sikumuona tena mpaka asubuhi ya leo, tena anakuja ananiambia hata kuwa na nafasi ya kunutoa out leo kwa sababu ana masula nyeti na Patrick.
Nafikiri ndugu msomaji hata kama ni wewe ungekuwa muhusika wa hili suala langu la wizi na kusikia maongezi haya yanayoendelea baina ya hawa mabinti ungegundua kitu kama wewe sio mpungufu wa akili. Nilianza kufikiri haraka nini nifanye ili hawa wasichana wanieleze anakokaa huyo Patrick bila wao kuwa na mashaka na mimi. Hapo likaja wazo kuwa nimsuburi kwanza Sonno maana ilikuwa mapema mno kuchukua muelekeo mwingine, hivyo nilikaa nikiwachunga kwa macho ili wasije wakaondoka bila kufahamu.
Disko lilikuwa linaendelea na watu walizidi kumiminika katika ukumbi huu wa Magnum, ghafla wale wasichana walikuja kwenye meza yangu na vikopo vine vya Stella walivyokuwa wamebakiza na kuviweka mezani huku wakiniomba niwaangalizie wakati wao wakicheza mziki. Walifanya hivyo kutokana na ongezeko la watu, walijua sio rahisi kuziacha mezani kwao na mimi nimudu kuziangalia kwa mbali.
Walicheza kama miziki mitatu hivi alafu wakaja wameshikana mikono mpaka kwenye meza yangu, hawakurudi kwenye meza yao kwani walivuta viti na kukaa huku wakinisogezea kopo moja la Stella na kuniambia ninywe. Ilionekana wazi kuwa pombe zilishawapanda kichwani, niliwashukuru kasha nikawambia kuwa huwa situmii kwani nimezoea pombe kali, walisikitika kwa kukataa kinywaji chao alafu wakaanza mazungumzo yao. Niliwasikiliza huku nikijifanya sina habari nao huku nikiyakata makali polepole, walikuwa wakiongea maongezi ya kawaida tu na tulidumu katika hali hiyo kama dakika tano hivi ndipo nilipowachokoza kwa maneno.
“Akina dada naona tumekaa meza moja lakini hatufahamiani.” Nilitoa kauli ambayo ilikatisha maongezi yao na kuniangalia alafu mmoja wao akasema;
“Unajua kaka tuliona kana kwamba hupendi bugudha ndio maana tukaendelea na maongezi yetu.” Aliongea mmoja wao.
“Sawa dada nafikiri hiyo ilikuwa tafsiri ya kihisia tu” nilisema na kuendelea “sijui wewe unaitwa nani?”
“Naitwa Mtuli.” Alijibu na kunyamaza.
“Na wewe dada unitwa nani?” Nilimuuliza mwingine.
“ Mie naitwa Monica” alijibu.
“Nyie ni wanyeji hapa? Niliuliza.
“Ndio” walijibu kwa pamoja alafu Monica akaunganisha swali, kwani wewe ni mgeni?
“Ndio” nilijibu kwa kudanganya.
“Unatokea wapi?” aliuliza Mtuli.
“Mbeya” niliendelea kudanganya
“Karibu sana Mwanza” alisema Mtuli.
“Nimeishakaribia ila nitashukuru sana nikipata wenyeji kama ninyi” nilijibu na kutupa kijembe.
Sikujibiwa ila niliunganishiwa swali kutoka kwa Monika.
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Lyampili Mabagala” nilijibu.
“Hapa Mwanza umekuja kutembea tu au kibiashara” nilitupiwa swali linguine.
“Nimepita tu naenda Ukerewe kumuona mdogo wangu ambaye anafanya kazi huko.”
“Kumbe unaenda Ukerewe, basi mimi ndio kwetu.” Alisema Mtuli.
“Kwenu ni sehemu gani pale ukerewe?” nilimuuliza.
“Wewe unafahamu sehemu gani huko Ukerewe?” Niliulizwa badala ya kujibiwa.
“Nafahamu Muriti, Nansio na Murutunguru.” Nilijibu.
Ahaa!! Hizo sehemu zote umewahi kufika na ukapakariri vizuri?” MTuli aliendelea kunimiminia maswali.
“Sio sana ila nazifahamu.” Nilijibu kwa mkato.
“Basi mie kwetu ni pale Muriti madukani.” Alisemsa na kuendelea. “Baba yangu ni maarufu kidogo pale Muriti kama ulikaa kidogo huenda ikawa ulimufahamu.
“Anaitwa nani?” nilimuuliza.
“Anaitwa Kazobha ndie mwenye bucha la kuchinja nguruwe pale.” Alijibu.
Kwa hakika nilikuwa namfahamu kwani kule Muriti kuna ndugu zangu hata baba yake alikuwa ananifahamu ila huyu binti sikumfahamu kabisa hata yeye hakuonyesha dalili za kunifahamu. Hapo nikavunga. “Huyo mzee niliwahi kumsikia wakati nilipotembelea pale.
Mara Sonno akaingia na kuangaza kwani alikuwa hajaniona, nikampungia mkono naye akaniona na kunihuata. Alifika na kuvuta kiti kimoja kilichosalia ili kuhitimisha mzunguko wa viti vine. Tulijuliana hali kasha akawasalimia waschana wale alionikuta nao;
“Habari zenu akina dada?” alisalimu.
“Nzuri tu, sijui wewe.” Waliongea kwa pamoja.
“ Mie poa kabisa.” Alijibu Sonno.
“Karibu.” Alisema Mtuli huku akumsogezea kopo la Stella.
Sonno alichukua na kukipachua tayari kwa kunywa, alikunywa kama funda tatu hivi na kurudisha kopo kwenye meza huku akiangaza macho ukumbini, alafu akamuita muhudumu na kumuajizia kopo sita za Stella na chupa moja ya Konyagi. Vinywaji vilipoletwa aliwapa wasichana yale makopo ya Stella na kuilaza chupa ya konyagi mezani, ikawa kama unywaji ndio umeanza. Baada ya kuwa nimewatambulisha wote na kufahamiana Sonno alinikonyeza na kutoka hapo tulipokaa, kitambo name niliwaaga hawa wasichana na kuwaambia kuwa naenda maliwatoni na hapo nilimfuata Sonno aliyekuwa ametoka nje ya jingo na kuegamia gari pale maegesho.
“Vipi?” Niliuliza punde nilipofika tu.
“Huyo mtu wako nimemkuta na amenieleza kila kitu ila nimemuachia uhai sijui nimefanya makosa.” Aliongea Sonno.
“Hapana.” Hebu nipe maelezo kwa kifupi.” Nilisema.
“nilipofika nilifanya kama nahitaji chumba hivyo nililipa na akaenda kunionyesha chumba, kulikuwa na watu wanazagaasehemu hizo. Baada ya kuonyeshwa chumba niliingia kuoga na nilipomaliza kuoga alikuwa amebaki peke yake hapo nilimuita kama vile ni shida ya dharura. Alikuja chumbani na alipoingia tu nikafunga mlango na kutoa bastola”
“Hapo nilimshinikiza kujibu maswali yangu huku nikimtishia kuwa akileta ubishi amekwisha na kwa mkwala niliachia risasi moja kwenye sakafu kuonyesha kuwa sitanii kwa kuwa bastola yangu ina kiwambo sauti haikusikika. Alibabaika na kuanza kutetemeka huku akisema. “Usiniue nitajibu.”
“Chumba namba ishirini na saba kinamilikiwa na nan?.” Nilimuhoji.
“Alikuwepo jamaa mmoja hivi ambaye katoka jioni.” Alijibu.
“Ni akina nani waliingia humo zaidi ya huyo jamaa? Alisita kidogo lakini aliponiangalia usoni akaendelea.
“walikuja watu wawili wakanipa pesa alafu wakaenda kukagua humo ndani, tulikuwa nao hawakuchukua kitu chochote.” Aliongea huyo muhudumu kwa uoga.
“Nimekuuliza ni wakina nani? Na je ndio utaratibu wenu kuruhusu wateja kukaguliwa?” niliuliza huku nikisogeza bastola sikioni kwake.
“Namfahamu mmoja tu, anaitwa Patrick Mwisongo anakaa Kigoto kwenye jumba lililo kando ya ziwa.” Alisema
“Hebu nieleze vizuri kabla sijachukia na kusambaza kichwa chako kwa risasi.” Nilizidi kumchimba mkwala.
“Ukivuka pale mwaloni soko la samaki unaendelea mbele baada ya kuacha nyumba za kawaida utakuta jumba la kifahari lenye ua wa michongoma ndio jumba la kwanza la kifahari na liko mbali nyumba nyingine upande wa kushoto kama unatokea mwaloni.” Baada ya hapo nilimwambia atulie asimwambie mtu yeyote juu ya jambo hilo alafu nikampatia sh. Elfu ishirini na kuagana naye bila tatizo. Alimalia kueleza Sonno.
Pamoja saana kiongoziJioni mtapata muendelezo