Riwaya: Jina langu ni Pheady

Riwaya: Jina langu ni Pheady

Naash nash kiongozi
Ukitaka bei ya soft copy sio dhambi pia
 
KAZI IENDELEE



" mbali kivipi?" Alihoji Sonno.
"Huyu mzungu tulikuwa nae katika mfunzo ya mapigano huko Cambodia." Niliamua kujibu kwa kudanganya.
"Ahaa! Hebu niangalie hiyo picha." Alisema huku huku akichukua picha niliyokuwa nimeishikilia mkononi. Baada ya kuitupia macho aligeuka na kuniulizia, " Vipi naye alikuwa anayaweza mapambano au la?"
"Ndio alikuwa mzuri sana kwa mapigano lakini nasikia ameishakufa, sasa kinachonishangaza ni hii picha kuwa hapa kwa hawa watu." Nilisema.
"Hilo lisikupe tabu labda kabla ya kufa alikuwa akifahamiana na hawa watu au walifanya kazi pamoja." Alisema Sonno.
"Kama mawazo yako ni sahihi kwa nini picha yake ikae pamoja na yangu wakati mimi sifahamiani nao?" Nilimhoji Sonno nipate mawazo yake.
"Kwa hiyo unataka kusema kuwa ndio waliomuua kwa sababu wewe wewe wanakutafuta wakuue na picha yako ipo kundi moja na ya huyo mzungu." Alisema Sonno.
"Haswaaa!? Ndio mawazo yangu yanavyonituma" na nilieleza huku nikijua wazi kuwa mimi ndie niliyemuua.
"Kama ni hivyo hizo picha zote wameshakuwa maiti au wako mbioni kuwa maiti." Alisema Sonno.

Kabla hatujaendelea mlango mlango uligongwa alafu akaingia dada chumbani. "Pheady twendeni tukale chakula tayari" alisema dada. Tuliongozana na dada mpaka chumba cha chakula. Tulikula huku tukipiga porojo za hapa na pale baada ya chakula tulienda kukaa sebuleni na muda huo ilikuwa imeishatimia saa mbili na dakika ishirini na saba usiku.
"Pheady, leo nimekuletea mkanda mzuri wa video wa Double Impact" Alisema dada huku akiweka mkanda ili tuweze kuangalia.
"Du" umenipatia sana dada maana huyo Sterling Van Damme huwa napenda anavyopigana." Nilisema.
"Mie nikijua tu kwa jinsi ninavyokufahamu lazima umpende Damme." Alisema huku akimalizia kuweka mkanda na kurudi kukaa kwenye sofa tuliangalia huku tukiwa na mazungumzo ya kawaida mpaka ilipotimia saa tatu na nusu aliamka na kuwachukua watoto kwenda kulala.
"Kama mkichoka mtazima, mie naenda kupumzika najisikia mchovu." Alisema dada huku akiondoka hapo sebuleni.
"Sawa, usiku mwema" nilimjibu.
"Kwa heri kaka" alimuambia Sonno.
"Asante dada, uwe na usiku mwema." Sonno alijibu.
Baada ya dada kuondoka tuliendelea kuangalia ile video ilipokwisha tulizima na kwenda kulala.

Huko uwanja wa ndege ilipofika saa tano kasoro dakika saba Patrick aliegesha gari maegesho na kwenda kukaa sehemu ya kupokea wageni huku akifyonza pombe kali aina ya Power No 1. Kifupi toka jana Patrick amekuwa ni mtu asiyependa ulevi upungue kichwani mwake, alikosa amani bila pombe kichwani kutokana na vitendo vilivyomsibu kwa mda mfupi uliopita kitu ambacho hakutegemea.

Ilipofika saa tano kasoro dakika tatu ndege inayokuja na wageni iligusa ardhi na baada ya mzunguko ikawa imetulia. Wasafiri walianza kushuka wakati huo Patrick alikuwa makini na watu wanaoshuka. Baada ya kuwa wameteremka watu kama tisa hivi wa kumi alikuwa Mr Wanna See akiongozana na kijana mmoja wa kiafrika aliyekuwa amevaa suti ya kijivu na miwani ya jua. Wanna See alivaa suruali ya jeans na T shirt huko akiwa amepakata mkoba. Walishuka wakaongoza sehemu ya ukaguzi baada ya muda kidogo wakawa wametokeza sehemu ya mapokezi. Patrick aliwalaki kwa kukumbatiana. Baada ya kuwa wamesalimiana Patrick aliwaongoza mpaka kwenye gari lake ambapo walipanda na kuanza safari kuelekea mjini Mwanza. Wakati wapo njiani Mr Wanna See alimuambia Patrick kuwa watafikia kwake kwa hiyo awapeleke kwake, nae aliwaongoza mpaka huko kwake Kirumba. Walipofika walikaa na kuanza kujadili masuala yaliyowaleta, hawakutaka kupoteza muda.

"Bwana Patrick hapa tulipo tumekuja tayari kwa kazi tupo watatu, mwenzetu hukumuona lakini yupo yeye atakuwa Hotel. Nafikiri baada ya kuwa amemaliza mipango ya kupata chumba atatupigia simu, namba za simu anazo. Kwa hiyo kuanzia sasa inabidi tuwe kazini. Sikuja kwa ajili ya kupata hizo dhahabu za Mr Catto ila Kuna suala lililojitokeza kuhusu huyo mtu uliyenionyesha picha zake kwamba amehusika na upolaji wa dhahabu. Huyo mtu anatafutwa na shirika ja ujasusi Afrika Kusini na anajulikana huko kama Lyampili Mabagala raia wa Uganda. Na nyie mnadai anaitwa Pheady mwenyeji wa kisiwani Ukerewe, Mwanza, Tanzania. Ila kitu kimoja ni kuwa picha za hayo majina mawili tofauti zinaonyesa ni mtu yule yule. Hivyo ni wazi alitumia jina bandia na uraia bandia alipokuwa Afrika Kusini. Kutokana na tuhuma zinazomkabili huko Afrika Kusini, zimetolewa dola milioni ishirini kwa mtu atakayempata na kumuua au kumpeleka akajibu mashitaka yake. Hivyo mimi nimechukua jukumu hilo kutokana na urahisi uliopo kwetu kumpata. Mtu huyu mnaemuita Pheady anatuhumiwa kwa kuwaua wenzie wawili na kutokomea kusikojulikana, wakati walipotumwa hapa Tanzania kuja kulipua bomba la mafuta la TAZAMA. Maiti ya mmoja ilipatikana huko Dar ikiwa imepigwa risasi ya aina ile ile ya bastola walizopewa kwenda kufanyiwa kazi na shirika hilo la ujasusi. Maiti ya mwingine ambaye yeye Pheady alisafiri naye kwa gari toka huko Afrika Kusini haijawahi kupatikana ila shirika la ujasusi lina uhakika aliuwawa na kutupwa mahali pasipo julikana. Baada ya kuona hiyo picha ya Pheady na kulinganishwa na ya Lyampili ikagundulika mtu ni Yule yule kasoro majina ni tofauti " Alipofika hapo Mr Wanna See alivuta mkoba wake na kuufungua akachambua ndani ya mkoba na kutoa picha mbili alizompatia Patrick.
Patrick aliziangalia alafu akasema" Ni kweli kabisa huyu mtu ni yule yule kasoro majina."
"Kwa hiyo kazi iliyopo ni ya kumtoa roho huyu mshenzi. Malipo ya awali tumeisha chukua kwa kazi hiyo na fungus lako tumekuja nalo tukijua lazima tutafanikiwa. Sasa kabla hatujaendelea na mipango mingine nipe maendeleo ya kazi ya kwanza ilipofikia." Alimaliza Wanna See na kunyamaza wakati, wakati wote huo yule mwenzake alikuwa kimya akisikiliza tu.

Patrick alieleza jinsi ilivyokuwa mpaka mwisho tulivyokuja kumuokoa Kikakika na mikakati aliyokuwa amepanga mpaka wakati huo. Alipomaliza maelezo yake Wanna See alimuuliza hao vijana wake wangeonekana saa ngapi kuleta taarifa ya huyo mtu waliyemteka jana. Patrick alimuambia watakuwa hapa wote ifikapoa saa tisa na kama kutakuwa na dharura tutawasiliana nao kwa njia ya simu maana mitambo yetu ya mawasiliano imeharibiwa.
"Sawa ngoja tuwasubiri hao watu watuletee taarifa, kama kutakuwa hakuna lolote lililopatikana tunaweza kumfuata kwake huko Ukerewe tukamsagie huko huko maana yeye ndie muhimu kufa." Alisema wanna see.

Walipomaliza hayo maongezi waliomba waonyeshwe vyumba vya kulala ili wajipumzishe na uchovu wa safari wakati wakiwasubiri akina Gilly na wenzake. Patrick aliwaonyesha wakaenda kupumzika.

Patrick alikaa Sebuleni na kuwasha runinga, akuwa anaangalia runinga huku akiwa na kinywaji aina ya Long John karibu akiendelea kufyonza taratibu. Mara simu iliita akanyanyua mkono wa simu na kuweka sikioni. "Hallo Patrick hapa nani mwenzangu?" Aliuliza.
"Huwezi kunijua hata kama nikitaja jina langu, ila kwa kifupi ni kuwa mimi nimefika na Wanna See. Nilitaka kujua kama mmefika maana tulipanga niwapigie simu nikishapata chumba. Na tayari chumba ninacho hapa Mwanza Hotel chumba namba 36, kwa hiyo nipe niongee na Wanna See" ilisikika sauti kwenye simu.
"Wanna See na mwenzie wamepumzika maana tumefika kitambo kidogo hapa nyumbani na tumeishajadili masuala mawili matatu hivi kuhusiana na kazi iliyopo" Alisema Patrick.
"Sawa Kama ni hivyo basi watakapoamka wambie wanipigie simu hapa mie nitakuwepo tu au kama ni vipi waje Mwanza Hotel" Alisema yule mtu wa kwenye simu.
"Okey, nitafanya hivyo." Alisema Patrick.
"Haya kwa heri." Aliongea yule mtu wa kwenye simu na kukata.
 
Back
Top Bottom