Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
RIWAYA: KASRI YA MWINYI FUAD
MWANDISHI: ADAM SHAFI ADAM
IMELETWA KWENU NA: BURE SERIES
SEHEMU YA 1
KIJAKAZI alizaliwa kutokana na ukoo wa kitumwa. Baba yake na mama yake walikuwa ni miongoni mwa watumwa watiifu sana wa Bwana Malik na kama wao, Kijakazi alinuia kuwa mtumishi wake mtiifu kabisa.
Wazee wa Kijakazi walifariki alipokuwa bado mdogo. Katika kukua kwake aliamini kuwa kule kuzaliwa kwake mtumishi ndiyo majaaliwa yake. Shabaha kubwa ya Kijakazi katika maisha yake ilikuwa ni kumfurahisha bwana wake, na kwa hiyo, alikuwa tayari kumfanyia kazi yoyote ile.
Mkewe Bwana Malik, kama alivyo yeye mwenyewe, alipenda sana kumtuma Kijakazi. Kazi za Kijakazi zilikuwa za nendarudi, mara afanye hili mara afanye lile, mara aende huko mara aende kule, mara achukue hiki mara achukue kile, kutwa kucha. Mara nyingi baada ya kuifanya kazi hurejeshwa kuifanya kazi hiyo hiyo mara ya pili. Kijakazi hakuwa na mapumziko hata kidogo ndani ya nyumba ya Bwana Malik.
Ghafla Bwana Malik humwita Kijakazi na kumpigia makelele. “Weel Nenda kamfunge mbuzi apate kula majani’.”
“Nishafunga mbuzi Bwana!”
“Wacha kujibu, wewe mbwal Fanya kama unavyoambiwa!”
Kabla ya kuitimiza ile amri aliyopewa mwanzo mara Bibi Maimuna, mke wa Bwana Malik, naye hutoa yake, “Kijakazi! Hebu kanitekee maji hapo kisimani nataka kuja kukoga, ma’na’ke n’najihisi n’nanuka jasho.”
“Maji nishateka, Bibi, lakini nitakwenda kuteka tena.”
“Unakwenda wapi tena? Unafikiri huko kisimani kuna maji ya kuchezea?”
Kijakazi husimama uwanjani kwa Bwana Malik, amepigwa na mshangao, hajui aende akafunge mbnzi au akateke maji, na Bwana Malik na Bibi Maimuna wakiendelea kumfokea na kumtolea maneno makali....
Hivi ndivyo yalivyokuwa maisha ya Kijakazi; kutwa yumo mbioni kutumwa na huku akisumbuliwa.
Haya yote hayakumkera Kijakazi hata kidogo, kwa sababu aliamini kuwa ndiyo majaaliwa yake. Aliamini kwamba wajibu wakc mkubwa katika maisha yake, ulikuwa kufanya anavyoweza kumfurahisha Bwana Malik na kila aliye wake. Hakupenda hata kidogo kumwona yc yote katika watu wa Bwana Malik amekasirika, na ilipokuwa hivyo, alijiona yeye ndiye chanzo na alijilaumu sana.
Jumba la Bwana Malik lilikuwa katikati ya shamba lake huko Koani, kubwa na la fahari, halina mfano wake jirani. Vyumba vyake vingi, waliovijua ni watumishi wa ndani na Bwana Malik na mkewe tu.
Kwenye ukumbi wa jumba la Bwana Malik kulikuwa na mapambo mengi ya fahari na starehe ya pekce. Kulikuwa na viti vya mpingo vya asili vilivyochongwa kwa nakshi. vyote vimetandikwa mito ya mahameli. Kuta zilikuwa zimepambwa kwa mapicha ya wafalme wa Kiarabu wa zamani, na chini ya mojawapo ya picha hizo limemng’inizwa jambia zuri la fedha. Sakafu ya ukumbi huo ilifunikwa na zulia kubwa kutoka Uajemi, na katika pembe moja liliwekwa kasba la msaji lililonakshiwa kwa misumari ya shaba.
Hapo ndipo Bibi Maimuna alipokuwa akipotezea wakati wake mwingi, akikaa na kujitandaza jua ya vile viti vizuri vilivyotandikwa mito ya mahameli, na kujipaka mafuta ya hal-ud na manukato mengine mazuri.