Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

Riwaya: Kasri ya Mwinyi Fuad

SEHEMU YA 18



“Hapana kosa lo lote kuifanya kazi yako vizuri. Sidhani kama kuna mtu atakayekufukuza hapa na pia sioni sababu kwa nini ufanye kazi kama mnyama!” Mkongwe alimwambia Kijakazi.

“Siku zote nimekuwa hivi! Sasa hata sihisi kama ninafanya kazi kwa sababu nimelemaa kufanya kazi namna hii. “Kijakazi alijibu.

Siku nyingi Mkongwe alifanya kazi pamoja na Kijakazi na hakuacha kusema naye ili afanye kazi kibinaadamu, lakini jawabu lilikuwa lile lile, “Mimi nimeanzia hapa nitamalizikia hapa.”

Mwisho Mkongwe alichoka na alibaki kumtazama tu.

Msimu wa karafuu ulipofika, Fuad aliajiri vibarua wengi shambani kwake kuja kumchumia. Jamaa zake pia walikuja kutoka mjini kwa ajili ya kazi za kuweka hesabu. Kambi za wachumaji karafuu zilipigwa na wafanya kazi wote wa kawaida wa Fuad waliachishwa zile kazi zao ili wajiunge katika kuchuma karafuu. Fuad alishughulika sana kwani hizo ndizo siku za kuchuma pesa. Katika siku hizo alikuwa mkali kupita siku zote na yule aliyezidharau hata chembe mbili tu za karafuu alishika adabu yakc kwa matusi ya Fuad.

Usiku mmoja Kijakazi na Mkongwe walikuwa wamekaa juu ya jamvi wameelekezana nyuso zao na kati yao ipo chungu ya karafuu mbichi wanazichambua.

Mkongwe hakuvunjika moyo katika kufanya kazi. Mara alianza kumpamba kwa maneno.

“Hivyo Bi Kijakazi utaendelea kufanya kazi namna hii mpaka lini?” Mkongwe aliuliza.

Kijakazi alishtuka kwani hakupata kuitwa bibi hata siku moja maishani mwake. Bibi aliyemjua yeye duniani ni Bibi Maimuna tu ambaye alifariki zamani.

“Umesemaje vile? Umeniita Bibi? Tafadhali usiniite hivyo; mimi na Kijakazi tu.”

“Mimi nimekwita bibi kwa ajili ya kukuheshtmu, kwa ajili ya umri wako, nakuona sawa sawa na mama yangu aliyenizaa. Nakuuliza tena kama hukusikia Bi Kijakazi, utafanya kazi namna hii mpaka lini?” Mkongwe aliuliza.

“Mpaka mwisho wa maisha yangu yote.”

Mara Mkongwe alianza kumweleza kwa urefu na kumwambia “Sikiliza Bi Kijakazi, na lazima ufanye kazi kidesturi, ufanye kazi huku ukijifikiria kama wewe ni binaadamu. Ukiendelea kufanya kazi namna hiyo utatuharibia sisi sote kwani mara kwa mara humsikia Bwana Fuad akisema “Unamwona Kijakazi namna anavyofanya kazi?” Kwa sababu yako wewe ndiyo ikawa Fuad anatutaabisha sisi sote hapa. Wewe ndiwe umekuwa mfano katika kila kazi na katika kustahamili mateso. Mimi sitakubali kutumwa kama wewe!”

Kijakazi alistushwa na maneno hayo na aliyasikia kama sauti zilizokuwa zikisema naye akiwa katika ndoto kwani hapana hata siku moja aliyopata kuambiwa yeye mwenyewe na Fuad kuwa anafanya kazi vizuri. Sifa zote alizopewa Kijakazi alipewa wakati hayupo kwani akiwa uso kwa uso na Fuad, yalikuwa ni yale yale tu ya Fuad kuukunja uso wake na kumtolea maneno ya usafihi na matusi kama alivyofanya marehemu Bwana Malik.

“Ah! Kweli Bwana Fuad anasema hivyo?” Kijakazi aliuliza kwa sauti ya furaba kubwa.

“Bi Kijakazi mimi sipendi kukutukana lakini sina budi kukwambia uache upumbavu wako! Sisi ni lazima tupumzike kwani ni binaadamn sawa sawa na Fuad! Huoni kuwa huyo Bwana Fuad wako ni mtu asiye na fadhila na mwizi wa nguvu za watu?” Mkongwe alisema huku akiwa amekasirlka sana.

Maneno yote aliyoyasema Mkongwe yalipita kwenye masikio ya Kijakazi kama upepo. Fikra yake yote ilikuwa katika kuwaza kwamba ijapokuwa siyo mbele yake yeye mwenyewe, baada ya muda mrefu, tena mrefu sana, Fuad amemtaja kuwa anamfurahisha kwa kazi yake nzuri.

Kijakazi alijiuliza mwenyewe kwa nini hakusifiwa na Fuad mbele ya uso vvake? Kwa nini hata siku moja hakuambiwa neno zuri kutoka kinywani mwa Fuad?
 
SEHEMU YA 19


Hata siku moja Fuad hakupata kumwambia anafanya kazi vizuri au hata kucheka naye tu. Yeye aliyachukulia yote hayo kuwa si kitu kwani Fuad ni mtoto kwake yeye. mtoto aliyemlea mwenyewe. Ue kuambiwa na Mkongwe kuwa alimsifu mbele ya wafanyakazi wengine kulimpa furaha maalum iliyofidia yote aliyokuwa akifanya.

Mkongwe hakutaka tena kuendelea na mazungumzo hayo. Waliendelea kuchambua karafuu mpaka saa sita za usiku na hapana mmoja kati yao aliyezungumza na mwenzake. Baada ya hapo kila mmoja alikwenda kulala.

Kwa ajili ya vuguvugu la siasa ya kuwapinga mamwinyi na mabwana shamba, mabwana shamba walizidisha chuki zao kwa wakulima. Wao walichukua hatua za kikatili katika kulipiza kisasi.

Kwa sababu hii, hali ya maisha kwa wapagazi wanaofanya kazi kwa Fuad na kwa mabwana shamba wengine ilizidi kuwa mbaya. Wakulima wengi walifukuzwa kutoka mashambani kwa mabwana shamba na wengine walitiliwa moto konde zao au kung’olewa mazao yao ilhali bado machanga.

Wakulima wengi waliteremkia mjini na wengi wao walikuwa wakikutana pahala pamoja paitwapo Kijangwani. Katika jumla ya mazungumzo yao wakati walipokutana hapo ilikuwa kuhusu maisha yao na vipi wangeweza kuyatatua matatizo yao. Hawakuwa tena na ardhi ya kulima, kwa hiyo hawakuwa na msingi wa maisha yao.

Yaliyokuwa yakizungumzwa hapo hayakubaki hapo hapo kwani habari ziliwafika wakulima wengine wa sehemu za mbali na jambo hili liliweza kuleta mafaham’’aDO makubwa kati ya wakulima tokea wale waliofukuzwa mashambani mpaka wasiofukuzwa.

Mara moja moja walipopata nafasi, wale wakulima waliokuwa bado kufukuzwa mashambani walipenya na kwenda mjini. Huko walipewa taarifa juu ya yale yaliyokubaliwa miongoni mwa wakazi wa mjini wasiokuwa na kazi na kwa hiyo wasiokuwa na chakula wala mahali maalum pa kuishi.

Lakini hayo yalimhusu nini Fuad? Aliamka alfajiri aweze kujitayarisha kwa safari ya kwenda mjini kuuza karafuu. Aliingia chooni na kukoga, na baadaye aliingia chumbani kwake na kuanza kuvalia. Alijipaka mafuta kichwani akazichana nywele zake vizuri na kuzipasua njia upande. Alichukua kila kichupa cha mafuta mazuri kilichokuwapo juu ya meza ndogo chumbani humo na kujipaka mafuta yake. Alisimama mbele ya kioo akajitazama, na alipoona amependeza kama alivyotaka, alitoka.

Gari la Fuad lilikwisha pakiwa karafuu tokea usiku na sasa Fuad yu tayari kwenda zake mjini kuuza karafuu zilizokwisha kukauka.

“Yuko wapi huyu tena? Hebu nendeni mkamtafutel” Fuad alimpigia kelele mfanyakazi wake aliyekuwa amekwisha ingia katika sehemu ya nyuma ya gari amekalia magunia ya karafuu.

Kabla hajawahi kushuka garini kwenda kumwita, dereva wa gari alifika mwenyewe, na hapo hapo alilitia gari moto wakaelekea mjini. Fuad mwenyewe alikaa mbele na dereva na wachukuzi wa yale magunia wakakaa nyuma.

Siku kama hii huwa siku ya furaha kubwa kwa Fuad. Siku ya kuleta karafuu mjini kuja kuuza ndiyo siku ya kustarehe huko mjini na kwa sababu hii ile kanzu na kofia, kivazi cha kawaida cha Fuad anapokuwa sbamba, huvuliwa. Leo Fuad amevaa shati la mikono mirefu, suruali ndefu ya sufi rangi ya kiJivujivu na viatu vya buti vyeusi vilivyong’arishwa vizuri na Kijakazi tokea jana.

Haikuwa safari ndefu kutoka Koani mpaka mjini kwenye soko la karafuu na mara walifika hapo wakawakuta wanunuzi wako tayari wanaingojea mali tu.

“Gunia ishirini zote mali safi,” alisema yule dalali aliyezipima karafuu za Fuad huku akiyasukuma mawe ya mizani yake hapa na pale baada ya kwisha kupima.

Alimwandikia kikaratasi Fuad naye pale pale akaenda kuchukua fedha zake kwenye ofisi ya tajiri aliyekuwapo hapo hapo karibu na soko Malindi. Baada ya muda alirejea pale lilipomngojea gari lake na wafanyakazi wake walikuwa wamekwishaingia ndani ya gari.

“Nyie tangulieni, mimi mtakuja jioni kwa teksi.” Fuad aliwaambia wafanyakazi wake kwa furaha, jambo lililokuwa si la kawaida.

Alitia mkono mfukoni akatoa pesa na kumpa kila mfanyakazi shilingi mbili.
 
SEHEMU YA 20



Wafanyakazi wale walibakia ndani ya gari. Fuad alipokuwa akienda zake, walimsindikiza kwa macho wakimwona akilifuata jia Ulilotokea Malindi kuelekca Forodhani na walipokwisha ona kwamba Fuad amekwisha ingia mjini kabisa walitoka garini.

Hawakuwa na wasiwasi wo wote kwani siku kama hiyo, siku ambayo Fuad huja mjini kuaza karafuu, huwa ni siku ya kutegea kazi kwa wafanyakazi wote wa Fuad. Siku kama hiyo, mwenye safari yake huenda, mwenye kutaka kupalilia konde lake haweza kufanya hivyo na mwenye kutaka kupumzika hupumzika. Kazi huwa nayo Kijakazi peke yake mwenye kutaka kuonyesha utiifu kwa bwana wake mpaka mwisho wa umri wake.

Siku kama hiyo, Fuad huzama katika starehe za mjini na anaporejea nyumbani huwa yu chopi hajali kitu cho chote.

Kila mmoja katika wafanyakazi wale alishika njia yake na kwenda kufanya shughuli zake.

Hiyo ilikuwa ni fursa kubwa kwa kina Vuai kwani siku hiyo hiyo palikuwa na mkutano mkubwa wa hadhara hapo Kijangwani.

Vuai na kikundi chake walikuwa wamejijaza kibandani wengine wakiwa wamekaa juu ya vipande vibovu vya mikeka, wengine wamekaa juu ya makozi na wengine wamekalia nazi zisizofuliwa. Baada ya mazungumzo mafupi tu ya kiasi cha kuulizana hali Vuai alitoa shauri. “Unajua wewe! Leo lazima mmoja wetu afike Kijangwani akasikilize cho chote kile.”

“Si bora u’kenda wewe, alau mwenyeji huko kidogo,” alitoa shauri mfanyakazi mwingine.

Hakupoteza wakati, Vuai alikwenda barabaram na kwa bahati alipofika tualiikuta gari inayotokea Mchangani na kuingia kwa safari ya mjini.

Fuad alifanya kazi zake zote zilizo za lazima hapo mjini na alipomaliza hakupoteza wakati. Alimpitia rafiki yake wa hapo mjini, Nassor.

Nassor alikuwa ni kijana aliyejuana tu na Fuad. Hawakuwa na urafiki mkubwa. Baba yake Nassor pia alikuwa. Bwana Shamba lakim alikufa ghafla baada ya shamba lakc kufilisiwa na bepari wa Kihindi aliposhindwa kullpa deni la pesa alizokopa kuchumia karafuu.

Baba yake Nassor alipokufa hakuacha kitu cho chote na yeye Nassor alikumbwa na lile wimbi linalowakumba wakulima na kuwatupa mjini kuja kutafuta maisha.

Fuad hakupenda kufuatana na mtu ye yote anapofika mjini ila Nassor tu. AIipenda kufuatana naye si kwa kitu cho chote bali kwa ajili ya uwenyeji aliokw’sha kuupata mjini. Nassor alimwelewa mwahala motc mwa starehe na haya ndiyo aliyoyataka Fuad.

Nassor na Fuad walikwenda zao mpaka Lusitania Bar hapo karibu na Minara miwili. Waliingia ndani na kuwakuta watu wanajiburudisha kwa vinywaji namna mbali mbali. Fuad alifanya masihara na watu wawili watatu aliojuana nao na baada ya hapo yeye na Nassor walikaa pahala pembeni peke yao.

“Utakunywa nini?” Fuad alimwuliza Nassor baada ya wote kwisha kukaa.

“Bia, laldni moto.”

Fuad aliagiza bia moja moto na moja baridi. Bia hizo zilimalizika zikaagizwa nyingine. Ziliagizwa nyingine na nyingine, na Fuad alipoona bia zishamchosha alitoa amri tu. “Sasa tutakunywa wiski!”
 
SEHEMU YA 21



Fuad alikwisba zoea kuamrisha na unapomjia tu ubwana hutaka kuamrisha bila kujali anazungumza na nani.

Haikuchukua muda mara wiski mbili zililetwa baada va Fuad kuziagizia.

Nishai zilikuwa zishampanda Fuad na kidogo kidogo alianza ule ukarimu wa kilevi. Alimnunulia ulevi kila aliyemsalimu. Muda ulivyopita ndivyo meza ya Fuad ilivyojaa watu na ilipofika saa tisa juu ya meza yake palikuwa oa msitu wa chupa zilizojaa aina tofauti za ulevi.

Nishai zilikuwa kubwa na walijistarehesha kwa kuimba nyimbo za Kiarabu, za Kihindi na nyimbo za taarabu za Kiswahili.

Walilewa mpaka magharibi na baada ya hapo Nassor na Fuad waliteremkia ng’ambo kwa starehe zao nyingine.

Baada ya kumaliza starehe zote alizozitaka, Fuad alikodi teksi na kurejea kwake.

Huko nyumbani Kijakazi alikuwa na wasiwasi juu ya bwana wake. Hakujua nini lilimtokea huko mjini na tangu saa.kumi na mbili alisimama nje akitazama njia itokayo mjini kwa matumaini kuwa Fuad atarejea salama. Kiasi cha saa tatu za usiku teksi ilifika pale nyumbani kumleta Fuad. Baada ya kufika tu aliingia chumbani kwake na kujitupa juu ya kitanda na nguo zake bila ya hata kuvua viatu.

“Oh! Haijambo bwana amerudi salama!” Kijakazi alisema akishusha pumzi na kupumua.

Alinyemelea ndani kidogo kidogo ili apate kuhakikisha kama Fuad ni mzima na alipofika chumbani kwake alimkuta amelala chali anakoroma udenda unamtoka. Sehemu ya kichwa ilikuwa kitandani miguu ameining’iniza.

Kijakazi alijitahidi kumwinua Fuad na kumlaza sawa na halafu alimvua viatu na soksi. Alitaka hata kumvua nguo lakini alikuwa mzito sana na Kijakazi hakuweza kumwinua. Alimkunjulia chandarua na baada ya hapo alisimama kwa unyongs pembeni ya kitanda na kumtazama bwana wake mpenzi halafu alizima taa na kufunga mlango akimwacha Fuad amelala kama aliyekufa fofofo.

Kwa bahati Vuai alirejea mapema kutoka mjini kuliko Fuad lakini hakutaka kuwaambia kitu wenzake mara moja. Alitaka akutane nao kwa nafasi wakati Fuad atapokuwa amekwisha lala; kwa hivyo. aliwaambia wakutane barabarani wakati wa usiku kama kawaida wanapokutana hapo kwa mazungumzo.

Baada ya Vuai kuhakildsha kwamba Fuad amekwisha lala na wala hana tamaa tena ya kuamka kwa usiku ule, alikwenda barabarani ambako aliwakuta wenzake wanamngojea kwa hamu kubwa. Baada ya kufika tu hata kabla ya kukaa, mmoja katika watu wale waliokuwa wakimngojea alimwuliza, “Enhe, wanasemaje huko mjini?”

“He! Ngojea nikae basi, mbona una pupa namna hiyo?” Vuai alikaa na baada ya kujuliana nao hali alianza kuwaelezca aliyoyasikia mjini. “Nasikia litanunuliwa shamba na wale waliofukuzwa kutoka kwenye mashamba ya mabwana shamba wote watapatiwa ardhi ya kulima.”

“Pesa za kununulia hilo shamba watazipata wapi?” Aliuliza mmoja kati ya wale waliokuwa wakimsikiliza Vuai kwa makini.

“Ah, hayo mimi siyajui: watayajua wenyewe huko mjini.” aliiibu.

“Wazee wanasema, ukimwona mwenzako ananyoa basi wewe tia majL Je, sisi tuliopo hapa kwa Fuad unafikiri nini Vuai?” aliuliza mwingine.

“Ah, si tutakuwa kama hao waliokwisha kufukuzwa tu?”

“Na hawa wanaofukuzwa hasa hufukuziwa nini?” aliuliza mkulimamwingine, mzee.
 
SEHEMU YA 22

“Eh! Watu wamechoka kutumwa Mzee Usi!” alijibu Vuai.

Mazungumzo yaliendelea mpaka usiku wa manane na walipochoka kila mtu alikimbilia bandani kwake kwenda kulala

Nishai za asubuhi zilimwelekeza Fuad aende zake mjini kumaliza starehe alizozibakisha jana.

Baada ya kwisha kukoga mbio mbio alimtuma mkulima mmoja kwenda mwita dereva wake na baada ya muda dereva alifika na gari lake akifikiri kuna shchena nyingine ya karafuu inayotaka kupelekwa mjini.

Gari lilikwenda mjini abiria akiwa Fuad peke yake. Hakuzungumza. na dereva wake nj’a nzima. Fikra mbali mbali zilikuwa zikimwendea kichwani mwake.

Alifikiri ulwa aliokuwa nao, pesa alizokuwa nazo, amri aliyokuwa nayo kwa wapagazi wote shambani kwake. Lakini halafu zilimjia fikra kwamba juu ya yote hayo alikuwa hastarehe kama anavyotaka yeye.

Aliwaza kwamba yeye awe anaranda mji mzima huku akiendesha mwenyewe gari zuri kubwa ambalo kila atakayeliona atalitumbulia macho. Aliona si kiasi chake, kijana mwenye pesa nyingi kama yeye kupanda gari la kubebea mizigo, yeye pamoja na watwana wake. Al’jihisi amechoka kupanda teksi na kuendeshewa gari na dereva asiyeweza kumwamuru kama anavyotaka yeye.

Siku chache baadaye, Fuad alinunua gari kubwa la aina ya Rambler ienye rangi ya bahari.

Hili halikuwa jambo kubwa kwake kwani pesa alikuwa nazo na hakuwa na tabia ya ubakhili katika kuzitumia kama aliyokuwa nayo baba yake. Marehemu Bwana Malik alihesabu hata senti moja. Pesa alizitumia kwa mipango. Fuad hakuzionea uchungu pesa alizokuwa nazo. Yeye amezirithi tu pesa hizo. Amefumbua macho siku moja akajiona yeye ni bwana mkubwa mwenye watwana kadhaa chini yake akiwatuma kama anavyotaka.

Alistarehe kama kijana ye yote yule mwenye pesa nyingi.

Vijana wote walimhusudu alipoingia na gari lake mjini. Alikuwa maarufu miongoni niwa mabwana shamba wote wanaoishi mjini na kila aliyekuwa na mtoto wa kike alimvutia kwake ili amwoze. Aliingia ndani ya nyumba zao kwa mapana na marefu na alipata kila fursa ya kuwaona watoto hao waliong’aa kwa weupe kwa kufichwa ndani.

Fuad mwenyewe alikuwa na azma ya kuoa. Starehc za ujana zilianza kumchosha akaamua kutafuta mchumba atakayekuwa mke wake.

Hapo hapo Koani palikuwa na wasichana wengi wa mabwana shamba wengine, laidni wasichana hao pamoja na wale aliowaona mjini wote hapana hata mmoja aliyempenda kwa kumwoa.

Fuad alitaka rake aliye mzuri bila ya kifani. Kila msichana aliyemwona hakuwa mzuri kama alivyotaka yeye mwenyewe. Kwa sababu hii, safari za mjini zilikuwa hazimwishi. Safari hizi mwenyewe aliziita safari za kutafuta mchumba. Akitoka huko Koani mbio na gari lake na kuranda kila sehemu ya mji akimtupia jicho kila msichana aliyemwona.
 
SEHEMU YA 23


“He! Mtoto huyu na gari lile!” Kijakazi akikaa na kujisemea kila alipomwona Fuad akilitia Rambler moto.

Ndani ya moyo wake, Kijakazi alimtakia Fuad mafanikio na salama kat’ka kila alilokuwa akilifanya. Hakupenda kumwona ndani ya gari lile, ambalo aliliendesha mbio sana. Kijakazi alikuwa na wasiwasi mkubwa moyoni mwake.

“Hebu fikiri Fuad akipinduka na dubwasha lile! Sijui itakuwa vipi? Ataumia maskini!”

Fikra mpya za kumwudhi zilimwingia Kijakazi moyoni. Kila Fuad anapoondoka shamba na gari lake kwa ajili ya safari zakc za kutafuta mchumba basi Kijakazi huwa hana fura’na mpaka anapomwona Fuad amerejea nyumbani salama.

Siku nyingi zilip ta na hali ya wakuiima ilikuwa inazidi kuwa mbaya. Mateso ya mabwana shamba ambao waliungwa mkono na wakoloni yalizidi. Ilikuwa hakuna lo lote la kufanya isipokuwa kutafuta njia ya kuepukana na mateso hayo.

Vuai hakuchoka kwenda mjini kusikiliza kila lililozungumzwa katika mipango ya wakulima na vipi wataweza kubadilisha maisha yao. Kila aliposikia kuwa viongozi wa siasa watafanya mkutano wa hadhara pahala po pote pale ikiwa mjini au shamba basi Vuai alifanya kila njia ili afike huko apate kuja kuwahadithia wenzake. Fuad naye aliyajua vizuri yaliyokuwa yakitcndeka na alikuwa na chuki kubwa kwa ye yote yule aliyemsikia akizungumza cho chote kuhusu kuwapigania wakulima na watu wa chini.

Jumapili moja palikuwa na mkutano mkubwa sana wa hadhara hapo Raha Leo na Vuai hakutaka mkutano huu umpite. Alifanya kila ujanja mpaka akafika. Ulihudhuriwa na maelfu ya wafanyakazi na wakulima. Vuai alisikiliza hotuba zilizotolewa na viongozi katika mkutano huo kwa hamu. Ulipomalizika tu upesi upesi alijihimu kurejea Koani.

Ulipofika usiku, saa za kwenda kuzungumza barabarani. Vuai alifika mapema, kabla ya wakati wa kawaida. Midomo ilikuwa ikimwasha kwa kutaka kusimulia aliyoyasikia mkutanoni huko.

Baraza lilipotimia tu, Vuai alianza, “Mkutano wa leo ulikuwa mkubwa sana, na mambo yaliyozungumzwa ni yakufurahisha kweli kweli. Ama niliyoyasikia leo mazuri sana. Wale jamaa wanaotusaidia leo walikuwa na mkutano hapo penye uwanja wa Raha Leo na maneno aliyoyasema msemaji mmoja yalikuwa mazuri na yaliniingia sana,” Vuai alisema.

Enhe, kimesemwa nini huko?” aliuliza mkulima mwingine.

“Mambo makubwa na pindi yakiwa basi mateso ya Fuad hayatatupata tena. Kwanzainasemwa kwamba haya yote hayawezi kubadilika mpaka kwanza wakoloni watoke katika nchi hii. Na baada ya hapo wakulima wenyewe watachukua hatua ya kuyabadilisha maisha yao,” alieleza Vuai.

“Ehe!’

“Alisema wakulima ni binaadamu kama walivyo binadamu wote basi lazima ifanywe kila njia wakulima wawe na maisha ya kibinaadamu; nyumba nzuri za kisasa zikiwa na taa za umeme na hiyo ardhi ya mabwana shamba...” hapo hakuweka wazi; alisita na halafu alisema, “hayo ya ardhi yatasawazishwa akishatoka mkoloni.” Vuai alizidi kueleza.

“Lakini ukitazama hayo ni kweli. Hawa mabwana shamba wanatutesa sana lakini ndio hatuna la kufanya. Ndio tulivyojaaliwa,” alisema kijana mmoja katika kundi la watu waliokaa kizani wakimsikiliza Vuai akieleza.......

Mawazo aliyokuwa akija nayo Vuai kutoka mjini hayakuenea miongoni mwa wafanyakazi wa Fuad tu, bali katika kila pembe ya Koarii mpaka Mwera. Yaliyokuwa yakizungumzwa na wakulima yalikuwa m hayo hayo. Fikra za wakulima zilikuwa zikichemka na walihitaji uongozi tu kwani walikuwa tayari kufanya jambo lo lote. Walikuwa wamechoka. Kufa, au kuishi katika hali hii, kwao ilikuwa ni sawa.
 
SEHEMU YA 24



Sasa Vuai na wenzake walikuwa wamechoka kuwa wasikilizaji tu wa yanayozungumzwa mikutanoni na mara hii walikubaliana watafute mahusiano makubwa zaidi na wale ndugu huko mjini wenye kuwaonea huruma.

“Nikipata nafasi nitakwenda kuwatafuta hao wanaoielewa mipango hiyo zaidi hapo Kijangwani!” alisema Vuai akizungumza na mkulima mwenzake walipokuwa wakipalilia mikarafuu shambani kwa Fuad. Alikuwa aldsubiri tu itokee ile fursa yake ya kawaida, yaani Fuad aende mjini kuuza karafuu. Haikuchukua muda mrefu fursa hiyo ilitokea. Baada ya kuondoka tu na Rambler lake, gari lililochukua karafuu likiwa limetangulia mbele. Vuai aliondoka na kwenda mjini.

Saa tano juu ya alama Vuai alifika Kijangwani. Alikwenda kwenye kijumba kidogo cha mawe kilichokuwa hapo ambacho kilionyesha kama ni olisi. Alitaka kuingia mle ndani lakini alisita kidogo.

Watu walikuwa wakiingla na kutoka ndani ya kijumba hicho na wengi kwa namna walivyovalia walionyesha ni watu waliotoka sehemu za mashamba kama yeye Vuai.

“Ati Bwana, mtu anaweza kuonana na nani hapa akiwa na tatizo lo lote?” Vuai alimwuliza mtu mmoja aliyetoka ndani ya kijumba kile.

“Una shida? Je, ushafukuzwa shambani nini?” aliuliza yule mtu.

“Si hayo, ni mengine kabisa,” Vuai alijibu.

Hakutaka kumwambia mtu ye yote yale aliyokuwa nayo moyoni ila tu kwa yule aliyehusika.

“Ingia hapo ndani mkono wa kulia utaona mlango. Ing’’a humo na utamkuta mtu na huyo utaweza kumwelezea shida zako,” alisema yule mtu.

“Ahsante Bwana.”

Yule mtu alikwenda zake na Vuai aliingia ndani ya kile kijumba. Aligonga mlango na alipata amri ya kuingia ndani. Alifungua mlango na mbele yake alimkabili kijana mmoja aliyekuwa amekaa juu ya kiti na meza mbelc yake. Alikuwa anashughulika na kuandika hata hakumtazama yule aliyeingia ndani.

Baadaye yule kijana aliinua uso wake akamwona Vuai amesimama miangoni.

“Karibu ndugu,” alisema yule kijana.

Alimkaribisha kukaa juu ya kiti kimoja katika viti vilivyozungushwa chumbani mle na mara yule kijana alianza kumsaili Vuai.

“Je, naweza kukusaidia ndugu?” aliuliza yule kijana.

“Bwana shida yangu niliyo nayo ni ndogo tu,” alianza. Vuai.

“Kwanza ndugu napenda uelewe hapa hapana ‘Bwana’. Sisi sote ni ndugu; ndugu tulioungana kuwapiga vita mabcpari na mabwana shamba,” yule kijana alimwambia Vuai.

“Ahsante Bwana nimesikia, “alijibu Vuai.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 25



Alikwisha zoea kumwita ‘Bwana’ kila aliyemhisi amemzidi, kwani alikuwa ameishi kwa mamwinyi siku nyingi na alikwisha zoea kumtetemekea kila mtu. Yule kijana aliyaelewa haya na alimwacha aendelee kumwita Bwana ijapokuwa yule kijanamwenyewe hakupenda.

“Mimi Bwana natokea Koani, nafanya kazi katika shamba la Bwana Fuad. Mara nyingi nahudhuria mikutano inayofanywa hapa mjini na mimi na wenzangu wa huko Koani tuna mambo fulani hatuyafahamu.”

“Umefanya uzuri kuja,” alianza yule kijana. “Sisi tunawatafuta hasa watu kama nyinyi ambao wana mambo hawayafahamu na wanataka kufahamishwa; kusema kweli hukukosea kuja hapa kwani hayo ndiyo madhumuni ya ofisi hii...” yule kijana alimwelezea Vua.

“Umesema uko shambani kwa nani vile?”

“Kwa Bwana Fuad.”

“Fuad! Fuad! Fuad!” yule kijana aliendelea kulitamka jina la Fuad kama kwamba linamkumbusha kitu. “Aha” Fuad! Tunazo habari. zake hapa. Hebu ngoja kidogo.”

Yule kijana aliondoka pale juu ya kiti alipokuwa amekaa na kwenda kwenye kabati kubwa lililokuwa hapo penye pembe ya meza. Alitoa bunda la makaratasi na kuanza kuyapekua.

“Aha, Fuad, ndiyo! Tunazo habari zake hapa. Bwana shamba huyu aliwahi kutaka kumkamata kwa nguvu msichana mmoja aliyekuwa akifanya kazi shambani mwake.” alielezea yule kijana. “Huko shambani mnakofanya kazi hapakuwa na msicbana mmoja aitwaye Mariam?”

“Mariam? Yeye alikimbia siku moja, nafikiri alitaka kupigwa na Fuad, mana’ake siku hiyo alipokimbia alianza kutolewa maneno na kutukanwa na Fuad,” alieleza Vuai.

“Basi ukweli wa mambo ni kwamba alitaka kumkamata na kumnajisi ndiyo maana akakimbia.”

“Hivyo?” aliuliza Vuai akistaajabu sana.

“Sasa sikiliza. Wenzako ulio pamoja nao huko shambani kwa Fuad ni watu madhubuti au ndio hivyo tu?” aliuliza yule kijana.

“Wako waliokuwa madhubuti na wako ambao si barabara.” alijibu Vuai.

“Sasa mambo gani hasa mnataka kuyajua, wewe na weozako?”

“Sisi tunataka kuyajua mambo yote ambayo tunayasikia kuhusu maisha yetu sisi wakulima,” Vuai alisema.

“Sikiliza, nenda ukaonane na wenzako uwaambie kuwa maisha ya wakulima yatabadilika Fuad akitaka asitake. Vile vile ilawa mnaweza kufanya mipango minu naweza kuja huko huko Koani ili kuzungumza na watu wa huko kwa jumla. PeDgine hilo litakuwa jambo la maana zaidi.”

“Anasema Fuad akitaka asitake maisha yetu yatabadilika,” Vuai aliwaeleza wenzake waliokuwa wakimsikiliza kwa makini walipokuwa wamekaa pale barabarani, usiku, wakizungumza.
 
SEHEMU YA 26


“Akitaka asitake namna gani: kwa nguvu?” aliuliza mkulima mmoja.

“Sijui kama kwa nguvu au kwa hiari, mimi kaniambia Fuad akitaka asitake maisha yetu yatabadilika.”

“Ah, mambo ya ajabu hayo,” alisema yule mkulima.

“Hata mimi naona ajabu!” alitilia mkazo mkulima mwingine.

Mazungumzo ya akina Vuai na wenzake yalikuwa yamebadilika kabisa. Hawakuwa tena wakizungumza habari za ngoma na wanawake wazuri. bali kila walipokutana walikuwa wanazungumza matatizo muhimu kuhusu maisha yao.

Fikra za Vuai zilibadilika kabisa. Aligeuka kuwa ni mwalimu wa kuwasomesha wenzake juu ya maisha na wapi ulimwengu unakoeodea. Kuna waliokubaliana naye na kuna wale ambao hawakuamini aliyokuwa akiyasema. Hata hivyo, hakukasirika hata kidogo na wale wasiokubaliana naye. Aliamini kuwa kila mmoja katika wao alitaka mabadiliko katika hali ya maisha yake. Kila mtu alikuwa amekwisha choka na mateso ya mabwana shamba.

Huko mjini mambo yalikuwa ya moto kwani habari za vishindo walivyokuwa wakivifanya wafanyakazi ziliwafika akina Vuai na wakulima wengineo wa sebemu mbali mbali za Unguja.

“Sasa lazima tufanye mpango yule kijana aweze kuja hapa ili aweze kuzungumza nasi,” alisema Vuai katika mazungumzo yao hapo barabarani.

“Vipi ataweza kuja huku na kuonana nasi? Bwana Fuad siku hizi kawa mkali zaidi kuliko zamani.” Alisema mkulima mmoja.

“Tutafanya mipango. Hivyo Fuad mmoja ndiyo anaweza kutushinda sisi aote kwa akili?” Vuai aliuliza.

“Mipango gani? Hapana hata mmoja kati yetu mwenye pahala penye nafasi ambapo tutaweza kukutana na huyo kijana.

“Nafasi ni kitu cha kutengenezwa. Muhimu tukubaliane tu. Na nafikiri haina haja ya kujificha kwani Fuad mwisho atayajua tu haya, na sidhani kama kuna haja ya kumwogopa.” Vuai aliwaelezea wenzake.

“Si suala la kumwogopa lakini sharti tuchukue hadhari mana’ake tukifukuzwa hapa...”

Kabla yule mkulima mwinginc aliyekuwa akisema kumaliza maneno yake Vuai aliyakatiza kati kati.

“Sikiliza Umari. wenzetu kadha wa kadha kutoka sehemu mbali mbali washafukuzwa na mpaka leo wanaishi. Mimi nafikiri madhalitumedhamiria kulifanya jambo natulifanye haidhuru kitokee cho chote. Tahadhari ni lazima kuchukua kwani haina haja ya kufanya mambo kiendawazimu; lakini kikitokea kitu hatuna budi kukikabili.

“Basi tumwite huyo kijana. Tutafanya kila njia ili tuweze kukutana naye ijapokuwa mwituni,” alisema Umari. “Sasa lini utakwwenda tena mjini?” aliuliza.
 
SEHEMU YA 27


“Kama kawaida, akitoka tu Fuad kwenda kuuza karafuu na mimi nitaondoka....”

Siku ile Fuad alirejea kutoka mjini saa sita za usiku amelewa chopi. Aliliendesha gari mbio na alipofika hapo kwake aliiliza honi ya motokaa yake kwa makelele na kila mmoja aliamka lakini hapana aliyemjali.

Huko mjini wakati alipokuwa bar akilewa, alisikia mazungumzo mengi kuhusu kikundi cha walu waliodhamiria kuwapia mabwana shamba. Maneno haya yalimkera sana na alikula yamini kwamba yuko tayari hata kumwua ye yote atakayelota habari kama hizo shambani kwake.

Makelele ya honi ya gari lake hayakumshughulisha mtu isipokuwa Kijakazi aliyekatiza usingizi wake na kuja mbio kumsikiliza Bwana wake mpenzi. Alikwenda mpaka lilipo lile gari na kumkuta Fuad yumo ndani amekaa humo mlango ameufungua. Aliinyemelea ile gari kidogo kidogo lakini mara aliisikia sauti ya kilevi ya Fuad ikiuliza,

“Unataka nini hapa saa hizi?”

“Ah! Bwana, nimekuja kukusikiliza; nikifikiri umefikwa na jambo!” alijibu Kijakazi kwa sauti ya hofu.

“Ha! ha!” alicheka Fuad kwa sauti kubwa na kusema.

“Hata nikifikwa na jambo utafanya nini kizee kama wewe. Toka hapa nenda zako, mpumbavu mkubwa we!”

Kijakazi aligeuka upesi upesi na kurejea alikotokea lakini mara aliisikia sauti ya Faud ikiita tena.

“Lakini hebu njoo!”

Kijakazi alirejea tena kwa Fuad na mara Fuad alianza kumwuliza.

“Mkongwe yuko wapi.”

“Nafikiri amekwisha lala Bwanal” alijibu Kijakazi.

“Mmm! Basi nenda zako.”

Fuad alitoka garini akafunga milango yote halafu akakaa hapo kwa muda kidogo ak’liegemea, Siku ile ulevi wake ulimwelekeza kwa Mkongwe na kutoka hapo alikwenda mpaka lilipokuwa banda lake.

Hakubisha hata hodi alipofika hapo. Aliusukuma mlango wa kumbesa uliokuwa umezuiliwa kwa kisiki cha mti. Mkongwe alishituka na kuruka kutoka pale kitandani alipokuwa amelala akipiga makelele.

“Mwizi! Mwizi! Mwizi!”

Usiku ulikuwa mkubwa na kelele za Mkongwe ziliweza kusikilizana mbali.

Watu walitoka vibandani mwao kila mtu na silaha yake mkononi, mwenye panga. mwenye mngu, mwenye mtalimbo au silaha yo yote aliyoweza kuipata. Wote waliloka nje na kuelekea kule yalikotokea yale makelele.

“Yuko wapi huyo mwizi!” walianza watu kuulizana.
 
SEHEMU YA 28


Mara walisikia sauti ya Fuad ikijibu, “hakuna mwizi! Mwizi gani atakayethubutu kuja shambani kwangu. Huyu Mkongwe anataka kukuhangaisheni tu.”

“Ala, Bwana Fuad! Mbona saa hizi uko huku?” aliuliza Vuai aliyekuwamo katika kundi lililokwenda kumkamata mwizi.

“Haya nendeni mkalale, upesi!” Fuad aliamuru.

Fuad hakuwahi kulifanya alilotaka kulifanya na aliona bora arejee nyumbani kwake akalale kwani nishai za ulevi zilikuwa zinamzidi.

Mkongwe hakulala kucha usiku ule. Alidhani Fuad angerudi tena saa yo yote ile lakini kwa bahati hakuja tena.

Ilipofika asubuhi kila mtu aliendelea na kazi yake kama kawaida na minong’ono ya hadithi ya Fuad ilitapakaa kote. Kwa Vuai hayakuwa mapya kwani alikwisha kuambiwa yale aliyotaka kumfanyia Mariam. Wafanyakazi wa shambani kwa Fuad hawakuonyesha kama walishughulishwa na mambo ya Fuad lakini kila mtu alikuwa na lake moyoni.

Fuad hakutahayari wala kuona vibaya kwa yale aliyoyafanya kwani hakuwajali bata kidogo wote wale waliokuwa wakiishi shambani kwake Alihisi anaweza kufanya jambo lo lote bila ya kujali cho chote. Bali, hakuhisi tu alifanya hasa mambo mengi ya utovu wa adabu.

Vuai na wcnzake walitayarisha mipango madhubuti ya kumwita yule kijana kutoka mjini ili aje kuzungumza nao. Walijaribu kutafuta pahala lakini mwisho waliona wakutane pale pale barabarani wanapofanyia baraza lao la kawaida nyakati za usiku. Waliamini kwamba hapana ye yote ambaye angewatilia shaka akiwakuta pale.

Kiasi cha saa mbili za usiku yu’e kijana alifika Koani, Baada ya kupatafuta kidogo tu pale alipoelekezwa na Vuai, aliwakuta watu kiasi ya kumi wamekusanyika barabarani wanamngojea. Hawakuonyesha kama wanamngojea mtu, na adui ambaye angetokea ghafla angelifikiri walikuwa katika mazungumzo ya kawaida tu kama ilivyo desturi ya washamba kukaa barabarani na kuzungumza.

Yule kijana alifika hapo kwa baskeli yake na baada ya kufika tu aliiweka pembeni. Alivalia kama wanavyovalia wakulima wengine ili asijulikane kama yu mgeni.

Vuai alikuwa wa kwanza kumtambua yule kijana. Alirakaribisha na wote wakakaa kwenye pembe ya barabara.

“Je, ndugu habari ya hapa?” aliuliza yule kijana.

“Habari za hapa nd’o kama tulivyokwisha kuzungumza Bwana,” alijibu Vuai.

“Kama mnavyojua, mimi m mjumbe kutoka huko mjini. Nimeletwa kwenu na ndugu zenu baada ya huyu ndugu kuja kuonana na sisi,” alisema yule kijana huku akimwonyesha kidole Vuai.

“Mimi jina langu Vuai.”

“Ala! Mimi naitwa Marijani,” alisema yule kijana.
 
SEHEMU YA 29


“Basi Bwana Marijani nd’o kama tulivyokwisha zungumza huko ofisini kwako. Sisi tunakusubiri hapa kwa hamu kubwa na siku ya leo ni siku ambayo tumeisubiri siku nyingi. Wenzangu wana mengi wanayotaka kujua, kwa hiyo, baada ya kuwazungumza nafikiri bado watakuwa na maswala mengt ya kukuuliza.”

“Sikilizeni,” alianza Marijani, amezungukwa, amewekwa kati kati kila mtu ana hamu ya kumsikiliza atasema nini. “Shida mlizo nazo nyinyi nd’zo shida walizo nazo wakulima wote nchini. Kuna wengine, shida zao zimezidi zenu kwani wao washafukuzwa mashambani. Mimi mwenyewe kwetu ni shamba, kule Donge, na ijapokuwa sasa naishi mjini wazec wangu bado wako huko huko na nawatembelea kila wiki. Kwa hiyo, matatizo yenu nayaelewa vizuri.”

“Lakini Bwana...” alisema mkulima mmoja lakini mara Marijani alimkatiza maneno yake.

“Sikilizeni tafadhali msiniite Bwana, Mimi ningelipendelea mniite ndugu, man’ake naona fahari zaidi kuitwa hivyo.”

Marijani aliendelea na maneno yake. “Sisi tuna mipango madhubuti kuhusu maisha ya wakulima kwa jumla Si kama tunataka kukudaeni kwa mabwana shamba halafu wao wakuoneeni huruma, hasha. Wao hawana huruma, na haina maana kuzitaka huruma pahali zisipokuwa. Tuna mipango mizuri zaidi ya hapo baadaye, lakini habari hii tutazungumza tukisha fahamiana vizuri. Jambo muhimu ambaio napenda mlijue ni kwamba wakulima wote waliofukuzwa mashambani washapata ardhi na wanaendesha maisha huko na kila atakaye fukuzwa kutoka kwa bwana shamba atapatiwa ardhi ya kumtosha.”

Wote walikuwa wakisikiliza kwa hamu, wamemfumbul’a macho ili wamwone katika giza lililokuwa limetawala usiku huo. Kimya; mara moja moja tu ilisikika sauti ya bundi au ya komba, wakiimba baada ya kunyvva tembo. Marijani pekee ndiye aliyekuwa akisema. Kila alipopita mtu kwenye mkutano wao wa siri Marijani aiikatisha mazungumzo yake mpaka mtu huyo atoe salam, ajibiwe na aende zake.

“Mnajua ndugu; sasa sina budi niondoke nirejee mjini mana’ke wakin.’ona napita usiku huu pale polisi Mwera wataanza matala yao,” Marijani aliwaambia wenzake.

“Nani hao walakaokufanyia matata?” aliuliza Vuai.

“Askari wanatutabisha sana, lak’ni haidhuru!”

“Basi ye yote katika nyinyi akipata nafasi anaweza kupenya na kuja mjini siku yo yotc ile,” alisema Marijani huku akiwashika mikono na kuaga.

Marijani na Vuai walikutana tena na tena hapo Kijangwani na walipanga mipango mingi. Kila alilozungumza na Marijani, Vuai aliwaarifu wenzake na mahusiano kati ya ofisi kuu ya wakombozi wa wananchi yalikuwa mazuri.

Haya yote yalifanyika kwa siri bila ya Fuad kujua. Si kama kwamba hakuielewa ile chuki iliyokuwapo kati ya wakulima na mabwana shamba katika nchi kwa jumla. Aliloshindwa kufikiria tu ni kwamba lingekuwapo vuguvugu la mwamko wa wakulima na zaidi ya hivyo kwamba hilo vuguvugu lingewakumba hata watwana wale shamban’ kwake.

Baada ya mwezi tu tokea Marijani kuonana na kikundi cha wakulima wa huko Koani, wakombozi wa wananchi walitangaza kuwapo kwa mkutano mkubwa hapo hapo Kijangwani mbele ya ofisi yao. Siku hiyo Fuad naye alikuwa na safari ya kwenda mjini, sio kwa sababu ya kuhudhuria mkutano huo, bali kwa sababu ya kufuatia starehe zake.
 
SEHEMU YA 30


Vuai hakutaka fursa hiyo impite na alifanya kila jambo ili afike. Baada ya Fuad kuondoka alijitahidi kutafuta gari lakini hakufanikiwa.

Kwa kawa’da Magari mengi yalikuwa yakipita nj’a hiyo ya Koani lakini siku hiyo bahati ilikuwa mbaya haikutokea gari yo yote kwa muda mrefu. Vuai aliupiga mguu na hakupata gari mpaka baada ya kutembea maili nne na kufika pale Ms’kit’makufuli. Alipofika Kijangwani alikuta watu washaanza kukusanyika. Wengi wao walikuwa wamevaa nguo chafu; dalili ya kuwa walitokea makazini na hawakuwahi kufika majumbani kwao.

Mkutano ulikuwa wa kusisimua na wakati ulipita b la ya Vuai kutanabahi kwamba anatarajiwa kurudi Koani kwa haraka. Mkutano ulimalizika saa kumi na mbili magharibi na hata baada ya kumalizika Vuai alibaki hapo hapo na kuzungumza na watu aliokwisha kujuana nao kwa kuja kwake sana hapo Kijangwani.

Hata alipotanabahi, ilikuwa saa moja na nusu usiku na hapo Vuai alianza tena kuutwanga mguu kurejea shamba. Mara hii alikwenda kwa mguu kitambo kirefu na usiku ulimkuta njiani. Alipofika hapo karibu ya Mweia, kwa mbali aliziona taa za motokaa zilizomulika mwanga mkali. Alikata shauri kuisimamisha tu hata ikiwa gari ya nani.

“Ho! Ho! Ho!” Vuai alilipigia kelele lile gari lilipofika karibu yake.

Ama siku hiyo kweli ilikuwa ni siku ya bahati mbaya kwa Vuai. Gari lile lilikuwa la Fuad! Kwa bahati mbaya zaidi Fuad alisimama kwa jeuri akitaka kujua ni “mbvva” gani yule aliyethubutu kumsimamisha. Alikuwa amelewa lakini si sana na aliweza kuzungumza na mtu bila ya ulevi wake kutambuliwa ila labda kwa yule anayeijua harufu ya ulevi.

“We nani wewe?” aliuliza Fuad baada ya kusimamisha gari yake.

Ilikuwa kiza. Fuad hakumwona vizuri Vuai. Dimbidi atoe kichwa nje ya gari kumwangalia aliyemsimamisha.

Vuai alikwishaitambua gari ya Fuad. Lo, hakuwa na hila yo yote ya kufanya ili asitambuliwc.

“Wewe unafanya nini huku saa hizi?” aliuiiza Fuad kwa hamaki.

Vuai aliduwaa kimya. Hakuwa na la kujibu wala bakuweza kuzua uwongo wo wote ule ambao ungelimnusuru.

“Ala, kumbe ndiyo desturi yenu hiyo; tutaonana.”

Fuad aliliondoa gari lake ambalo alikuwa hakulizima moto alipokuwa akizungumza na Vuai na kumwacba pale pale.

Vuai hakusitushwa na maneno ya Fuad na baada ya hapo aliamua kutembea taratibu tayari kulikabili lo lote litakalomtokea. Haukupita muda baada ya Fuad kupita alitokea mwenye baiskeli na Vuai akamwomba amsaidie. Huyu bwana mwenye baiskeli alikubali akampakia kwenye kibao cha nyuma na kumchukua mpaka Koani ambako alimkuta Fuad amekwisha kwenda zake kulala.

Usiku ule Vuai alirejea nyumbani amechoka. Hakwenda barazani ijapokuwa wenzake walikuwa wakimngojea kwa hamu kubwa. Hakusimama po pote ila alifululiza bandani kwake kwenda kupumzika.
 
SEHEMU YA 31


Fuad alikuwa si mpumbavu wa kuelewa basira za wakulima zilivyo dhidi ya mamwinyi na alikuwa na hakika kwamba ile haikuwa mara ya kwanza kwa Vuai kutoroka shambani kwenda mjini.

Kitendo cha Vuai kilimkasirisha sana na alikichukulia kuwa ni utovu wa adabu mkubwa kwa Vuai kutoroka. Joto la moyo lilimpanda na usiku kucha hakulala kila alipofikiri kwamba hata wapagazi wake sasa hawana woga na wanathubutu bata kutoroka. Baada ya kupambazuka Fuad alitoka na gari lake mpaka mjini. Aliranda mjini na kuangalia mandhari ya asubuhi na alipofika kiasi cha saa tatu alifika Darajani.

Alilisimamisha gari lake mbele ya jumba kubwa la kizamani lililotengenezwa vizuh.

Chini ya jumba hilo walionekana watu wakiingia na kutoka. Pembeni ya mlango wa jumba hilo palikuwa na meza na kijanaaliyekuwa amekaa nyuma ya meza hiyo alikuwa amezongwa na watu kadha wakimpa pesa na yeye akiwaandikia hati za stakabadhi.

Alipofika tu mlangoni Fuad alikabiliana na mtu mmoja aliyevalia vizuri. Alikuwa amevaa kofia ya mkono, iliyokaa vizuri juu ya kichwa chake, koti zuri la lasi na kanzu ya dorya.

“Salam alaikum,” Fuad alimsalimu yule mtu.

“Alaiku musalam, khabari za asubuhi?”

“Nzuri,” alijibu Fuad huku akionyesha mwenye haraka.

“Je, Bwana Marejebi nimemkuta?”

“Sasa hivi nilimwona hapa,” alisema yule mtu huku akiangaza huku na huku kama kumtafuta yule aliyeulizwa. “Hebu mtazame juu; labda amepanda huko,” aliendelea.

Fuad pale pale alipanda juu na kwa haraka aliyokuwa nayo alipanda ngazi mbili mbili. Alipofika juu alimwuliza mtu wa kwanza aliyekutana naye na mtu huyo alimpeleka mpaka ofisini kwa Bwana Marjebi. Fuad aligonga mlango, akakaribishwa, na kuingia ndani.

Alimkuta Bwana Marjebi ameuziba uso wake gubi gubi kwa gazeti alilokuwa akilisoma. Alikuwa amekaa juu ya kiti cha kuzunguka, akijizungusha huku na huku. na huku akisoma gazeti lile.

“Salam alaikum,” Fuad alimsalimu Bwana Marjebi aliyekuwa bado amejigubika kwenye gazeti kama kwamba hakusikia mtu akiingia ofisini mle. Bwana Marjebi alijifunua lile gazcti na alipomwona Fuad alisema kwa Furaha, “Ah, ya Bin Malik!”
 
SEHEMU YA 32



Aliliweka lile gazeti juu ya mcza kubwa iliyokuwa mbele yake na kujitandaza zaidi juu ya kiti chake cha kuzunguka.

Meza iliyokuwa mbele yake ilikuwa inang’ara na imepambwa kwa mabuku makubwa yaliyopangwa vizuri katika kila pembe ya meza ile. Katikati ya mabuku yale palikuwa na kidau kizuri cha wino na kalamu ndcfu iliyotoswa ndani ya kidau kile.

“Unasemaje Bin Malik? Leo naona umetamani kuja kututembelea ofisini kwetu; karibu kaa kitako.” Bwana Marjebi alimkaribisha Fuad kukaa juu ya kiti k’moja ya viti viwili vilivyokuwa mbele ya meza ile.

“Ahsante Bwana, ahsante.”

“Je, nini khabari Bin Malik? Sikupata kukuona hata siku moja ofisini kwetu; je, kumezidi nini tena leo?

“Khabari Bwana Marjebi, nimekuja, nataka unieleze khassa, mana’ake hawa ...” Fuad alisita kidogo na kumtazama Bwana Marjebi huku akitafuta neno la kusema, “ng’ombe hawa, nisameh Bwana Marjebi sijakusudia kutukana mbele yako, lakini sina vingine vyo vyote vya kuwaita ila hivyo - hawa siku hizi wamekuwa hata hawaogopi”

“Nani tena hao wanaokushughulisha akili yako,” aliuliza Bwana Marjebi huku akiichezeachezea tai iliyomkaba vizuri rohoni.

“Si hawa wanaojidai, sijui, wakombozi. Jana nimemkuta mpagazi wangu mmoja anatoka mjini kwa miguu. Nafikiri alikuwa anatoka huko huko kwa hao wakombozi. Sasa naona Bwana Marjebi mambo yamezidi hata hawaogopi tena. Alla - izza, hata vile vitwana vya shambani kwangu vimekuwa haviogopi. Zamani ilikuwa hathubutu kuondoka mtu kwenda hata hatua mbili bila ya amri yangu. Ati nasikia wanadai usawa - usawa gani wanataka hawa? Hata Mungu hakuumba vidole sawa. Hawa, Wallahi...”

“Sikiliza Bin Malik,” Bwana Marjebi alianza kumtuliza Fuad aliyekuwa kahamaki. “Hawa watwana wasikushughulishe akili yako; wamoja havai mbili. Wao washajaaliwa kuwa nyuma, watakuwa nyuma maisha yao. Wakombozi, wakombozi, wakikomboe nini hawa. Hawana lao jambo. Ati wanataka wapewe nchi waongoze! Unafikiri wana wanaloliweza hawa; hawawezi cho chote,” Bwana Marjebi alisema kwa hasira. “Wewe Bin Mal’k unafikiri Mwingereza mpumbavu awape nchi wale wapumbavu waiongoze. Uchaguzi tushawashinda; uhuru tunautia mkononi tarehe tisa Disemba; usitie wasi wasi wo wote - Chama cha Raiat-el-Sultani kiko imara hapana khof,” Bwana Marjebi alisema na kumtia moyo Fuad, lakini pale pale aligeuza sauti yake na kuuliza huku akitabasamu

“Kwanza mchango wa sherehe za uhuru ushatoa?”

“Bado Bwana, lakini azma n’nayo.”

“Basi. la-takhaf bin Malik, nenda zako kafanye kazi zako. Ukimwona yo yote katika hao wapagazi wako anajidai kutaka kuwa mkombozi, naye mfukuzilie mbali tu.”
 
SEHEMU YA 33



“Ahsante, ahsante, Bwana Marjebi; na kesho nikijaaliwa nitaleta mchango wa sherehe za uhuru.”

“Tena usiwache kuleta, babu-el-hadid peke yake kaleta shilingi alf.”

“Stoacha Bwana. Haya fi-amani-llah”

Fuad aliondoka pale akiwa mwingi wa furaha. Angelionekana mwendawazimu tu kama si hivyo, angelipiga chereko pale pale. Alishuka chini mbio moja kwa moja mpaka ndani ya gari yake akaitia moto na kuirejesha nyuma mbio, na baada ya kuigeuza, hakusimama mpaka Koni.

Siku ile hakutaka kuzungumza na mtu, kwani aliona akifanya hivyo ataichafua furaha yote aliyokuwa nayo moyoni.

Asubuhi ya siku ya pili Fuad aliamka mkali kuliko kawaida yake. Alip’ga makclele na kutukana ovyo. Haya yalikuwa matayarisho ili atakapokutana na Vuai awe ameshakuwa mkali kama anavyotaka yeye mwenyewe.

Alikuwa akifuata kij’a kimoja kinachotokea nyuma kwake na kuelekea kule iliko kambi ya wachumaji karafuu alipokutana na Mkongwo ambaye hakuweza kumpita bila ya kumsemesha kwa namna anavyomwashiki.

Mkongwe alikuwa amechukua furushi la majani kwapani amekazana kwenda kuwalisha ng’ombe. Alikuwa amejifunga kanga mbili zilizo kongwe, moja kichwani na moja amejiandaa. Mzuri wa kimaumbile, Fuad alipomtupia macho hakujizuia kumsemesha.

“Unakwenda wapi?” Fuad alimwuliza Mkongwe kwa hamaki.

“Si unaniona nimechukua majani? Basi mwenyewe huwezi kukisia kama natoka kuchuma majani?” Mkongwe alimjibu huku woga na hasira vimemjaa kila akifikiri siku ile Fuad alipotaka kumwingilia ndani ya kibanda chake kwa nguvu.

“Ebo! Wewe unathubutu kunijibu mimi namna hivyo?” Fuad alipiga kelele huku akitaka kumkamata.

Mkongwe alimkwepa na kukimbilia mbio bandani mwa ng’ombe, furushi lake la majani kwapani.

“Yuko wapi mbwa yule?” Fuad aliuliza bila ya hata kujua anamwuliza nani.

Alikuwa akipiga makelele peke yake na hasa aliomba akutane na Vuai apate kummiminia hamaki zote zilizokuwa moyoni mwake.

Vuai ambaye alikuwa akipiga majalbe kwenye miche michanga ya mikarafuu alikuwa amekwisha zisikia kelele za Fuad lakini aliendelea na kazi yake kama kawaida. Alikwisha kata shauri Ia kumjibu Fuad kweli tupu na amtazame atafanya nini.

Mara Fuad alimwona Vuai anashughulika, jembe mkononi, ameinamia pale pale palipo na kazi yake. Vuai naye alikwisha baini kwamba Fuad yupo pale lakini hata hakutaka kujipa taabu ya kumtazama.

“Wewe! Wcwe! Mimi nakutafuta wewe tokea saa ile!” alianza Fuad huku akimwelekezea kidole chake cha shahada. Fuad aliendelea na makelele aliyoyaanza tokea alipotoka kwake.
 
SEHEMU YA 34


Vuai alisita na kazi yake na kumtazama Fuad bila kuonyesha kustuka wala kutaharaki. Alikuwa amesimama, moyo wake tanda kabisa. akingojea nini Fuad atasema.

Mara Fuad aliendelea na makelele yake. “Juzi ulikuwa unatokea wapi?”

“Mkutano” alijibu Vuai bila ya kumwita Fuad Bwana’ kama ilivyo kawaida yao.

“Mkutano? Mkutano gani?” alizidi kuuliza Fuad.

“Mkutanoni pale Kijangwani,” alijibu Vuai.

Kijangwani palikuwa pashakuwa pahala maarufu sana na ni watu wachache tu wasiopata kusikia habari zakc. Si wakulima tu waliopaelewa Kijangwani bali hata mabwana shamba na mabepari walikuwa wanapaelewa vizuri. Mara nyingi Fuad alikwishazisikia hadithi za Kijangwani lakini aliwaona wote waliofika pahala pale kwa haja yo yote kama watu wajinga wasioweza kufanya jambo lo lote.

Fuad alianza kumvaa Vuai kwa maneno, “Ala, na wewe pia,! Na wewe p’a ushakuwa mkombozi wa wananchi? Wacheni upumbavu wenu huo Nyie mnafikiri mnaweza kufanya n’ni?”

Chuki ilikuwa imemjaa. Alikwishazisikia hadithi nyingi za wakuiima waliohudhuria mikutano ya hapo Kijangwani kutoka kwa mabwana shamba wenzake wakati wanapokuwa katika starehe zao huko mjini au hata mashamba wanapotembeleana. Pale pale aliamua kumfukuza Vuai shambani mwake.

“Hilo jembe liwache hapo hapo na uondoke shambani mwangu sasa hivi. Usichukue kitu cho chote, uondoke wewe tu!”

Haya hayakumshitua Vuai kwani hata mwenyewe alikuwa akitumainia kwamba iko siku moja atafukuzwa kutoka shambani kwa Fuad. Alifanya kama alivyoambiwa. Bila ya kumwambia Fuad kitu cho chote alifuata njia na kuja zake mjini.

Vuai alizidisha idadi ya wakulima wallofukuzwa mashambani. Na si yeye peke yake. Haya yaliwafika wakulima wengi kutoka kila pembe ya kis’wa cha Unguja. Wote waliishia hapo Kijangwani. Vuai alikuwa mwenyeji hapo na alipofika tu alijua akaonanc na nani.

Alimkuta Marijani chumba kile kile alichomkuta siku ile katika hali ile ilekainamia makaratasi, kalamu mkononi; mara aitazame karatasi hii mara aitazame karatasi ile. Alisimama mlangoni na kugonga.

“Je, ndugu nini khabari?”

Marijani alisimama pale alipokuwa amekaa na kuja kumsalimu Vuai.

“Jamaa wote hawajambo huko?” Marijani alimwuliza Vuai huku akimvuta mkono na kumwongoza kukaa juu ya kiti.

Wote wawili walikaa bega kwa bega na kabla Marijani hajasema kitu cho chote Vuai alianza kusema bila ya kujibu yale aliyoulizwa.

“Ndugu, mimi nimekwisha fukuzwa kutoka huko shambani kwa Fuad. Alinikuta njiani nikirejea kutoka ule mkutano uliokuwepo juzi. Tena siku hizi mambo yake yamefurutu ada, manaake amezidi kuwa hana adabu. Siku ile uliniambia kwamba alitaka kumkamata Mariam kwa nguvu, basi hivi majuzi alitaka kumwingilia Mkongwe kibandani mwake usiku. Mkongwe alipiga kelele na sote tulitoka na silaha zetu.”
 
SEHEMU YA 35



Vuai alisita kusema kidogo na kutikisa kichwa, mara aliendelea na hadithi yake.

“Ah, ama kijana yule bado zake zipo. Ingelikuwa hakujitambulisha kwetu kama ni yeye, basi nafikiri tungelimvaa kwa mapanga.”

Vuai alikuwa anazungumza kwa hasira kubwa, kipovu kinamtoka mdomoni. Jasho jombamba lilimiminika kutoka usoni kwake na mara kwa mara alikuwa akilipangusa kwa mikono yake iliyojaa vumbi la udongo. Jasho hilo liliteremka mpaka kifuani na kulowanisha shati la mardufu bovu lisilokuwa na kifungo hata kimoja alilolivaa.

Marijani alikaa kimya akimsikiliza Vuai na hata mara moja hakumwingilia katika mazungumzo yake. Alitaka aseme mpaka amalize yote aliyotaka kusema. Lakini mara Vuai alisita na kuonyesha kama amekwisha maliza kusema maneno yake.

“Enhe!” Marijani aliingilia kati kama kumtaka Vuai aendelee na maelezo yake.

“Basi alinijia na kuniuliza nilikuwa nikitoka wapi pale aliponikuta nik’rejea kutoka mjini kwa miguu. Mimi sikutaka kumficha na nilimwambia wazi wazi kwamba nilikuwa nikitoka kwenye mkutano wa wakombozi wa wananchi.

“Alisema nini ulipomwambia hivyo?” mara Marijani aliingilia kati kuonyesha hamu ya kutaka kujua.

“Kwa hakika sikumwambia kuwa ulikuwa mkutano wa wakombozi wa wananchi. Nilimwambia tu kuwa nilikuwa mkutanoni Kijangwani.”

“Ah, wewe ulipomtajia Kijangwani tu lazima mwenyewe alifahamu ulikuwa mkutano gani,” Marijani alisema.

“Sikiliza ndugu,” Marijani aliendelea, “wewe una mke na watoto?”

Vuai aliukunjua kidogo uso wake uliokuwa umejaa hamaki na kutabasamu. “Mimi mjane bado. Wazee wangu walitaka kunipa mke mwaka jana lakini niliikataa na ulikuwa ugomvi mkubwa baina yangu na wao lakini...”

Marijani hakutaka kujua zaidi juu ya ugomvi wa Vuai na wazee wake kwa kukataa kupewa mke. Aliingilia kati ya maelezo hayo na kusema, “Kama huna mke na watoto ni vizuri zaidi. Leo kiasi cha saa hedashara itakuja gari hapa, na mimi na wewe tutakwenda pahala, na hapo utawakuta wenzako wengi ambao naamini utapenda kuishi nao. Utajifunza mambo mengi buko. Sasa kama una kazi zako za kufanya hapa mjini unaweza kwenda kuzifanya na tukutane hapo saa hizo nilizokwambia.”

“Mimi sina kazi yo yote ya kufanya. Nitasubiri pale nje chini ya miti mpaka zitakapotimia hizo saa.”

“Sawa sawa,” Marijani alijibu.

Vuai alitembea temboa na kufanya mambo madogo madogo aliyotaka kuyafanya na ilipofika saa nane alifika Kijangwani.

Uwanja wa Kijangwani ulikuwa umezungukwa na miti mirefu ya mikungu, miembe na mizambarau. Ijapokuwa joto lilikuwa kali, uwanjani hapo palivuma upepo wa kuburudisha na miti yote hiyo kwa umoja ilitupa vivuli vyake uwanjani hapo. Kwa mtu aliyechoka na hata kwa asiyechoka, palikuwa ni pahala pazuri pa kupumzikia na kupunga upepo. Watu wengi walikuwa wakipita hapo.

Vuai alikaa chini ya mti na mara usingizi ulimchukua.

Haikuwa saa kumi na moja kama walivyoagana. Marijani alichelewa kiasi cha nusu saa. Alipofika alimkuta Vuai amekaa chini ya mti bado anapunga hewa nzuri ya Kijangwani. Marijani alifika na mwenzake aliyekuwa akiendesha hilo gari. Lilikuwa gari dogo, kongwe, lililokuwa wazi nyuma, lcnyc nafasi ya kuchukua kama watu wanane. Wote watatu walikaa sehemu ya mbele na bila ya kupoteza vvakati walianza safari yao.
 
Back
Top Bottom