Riwaya: Kijijini kwa Bibi

Riwaya: Kijijini kwa Bibi

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE.

______________
ILIPOISHIA...
______________

"nibusu basi ili nishinde vizuri mwenzio" mtoto wa mchungaji akaongea kwa mahaba.
"kesho rafiki yangu, hivi huogopi kusema hayo maneno katika nyumba takatifu kama hii?" kayoza akamjibu kwa busara,
"si unibusu jamani wewe." yule binti akakomalia kwa sauti ya juu kidogo.
"unamwambia nani akubusu?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akiwa anaingia Sebuleni.....

____________
ENDELEA..,.
_____________

..."hakuna kitu baba" binti mchungajibu akajibu.
"kwa hiyo nimesikia vibaya?" Mchungaji Wingo akauliza huku anamuangalia binti yake.
"nilikuwa namsimulia filamu moja hivi ilioneshwa jana ." binti wa Mchungaji akajibu huku akiangalia chini kwa aibu,

"Umekalia kuangalia filamu tu, badala ukazane kusoma biblia ili uongeze imani unakalia kuongeza ujinga tu" Mchungaji Wingo alimwambia binti yake aliyekuwa amesimama mbele yake
"Nisamehe baba, ila hiyo filamu ilikuwa na Mafundisho tu mazuri" Binti Mchungaji alijitetea,

"Ebu tupishe bwana" Mchungaji Wingo akamwambia mwanae na binti akaondoka haraka,
"Huyu mwanangu ni muongeaji sana, yupo tofauti na wenzake kabisa" Mchungaji Wingo aliongea huku akimgeukia Kayoza na usoni akikunjua tabasamu,

"Ila ni mcheshi sana, yaani amenizoea muda mfupi sana" Kayoza nae alijibu,

Kisha mchungaji na kayoza wakawa wanaongea, ila jambo kubwa ambalo mchungaji alimsisitiza Kayoza asikose katika maombi ya usiku.
Kayoza akarejea kwao kujumuika na mama yake.
"vipi mwenzetu, mchungaji alikuwa anakuambia nini?" mama kayoza alimuuliza mwanae.
"tulikua tunaongea mambo ya kawaida tu" kayoza akajibu.
Kisha mama kayoza akaenda jikoni kutayarisha chakula.
"eh, mwana leo nimekutana na vituko" Kayoza alianza namna hiyo kumuelezea Omari.
"wapi tena shee" Omari akauliza kwa shauku .
"si kwa mchungaji mwanangu, kuna binti yake mkubwa amedata na flag yangu"Kayoza aliongea huku akitabasamu
"kwa hiyo unataka kufanyaje?" Omari akauliza huku amekunja sura.
"nitafanyaje ndugu yangu, na hili dubwana linanibana" Kayoza alijibu kwa upole
"aah, ok, we mshiti au kama ana mahamu nitajaribu kumseti mimi" Omari aliongea, na kusababisha wote wakacheka.

"Poa mi ntakupigia pande, we si mwanangu bwana" Kayoza aliongea huku akicheka...

*****************

Sajenti Minja hakwenda kupima, alimfuatilia mkubwa wake mpaka alipomuona anapanda gari na kuondoka, naye akarudi ndani moja kwa moja hadi katika kitanda cha msaidizi wa mganga..
"vipi, unaweza kukaa" Sajenti Minja alimuuliza yule msaidizi wa mganga.
"kwanini nisiweze?, naweza tu" Msaidizi wa mganga akajibu,
"kuna maswali machache nataka nikuulize" Sajenti Minja akaongea kwa upole.
"kwani wewe ni polisi" Msaidizi wa mganga aliuliza ili apate uhakika, kwa sababu alimuhisi.
"ndio" sajenti Minja alijibu.
"sasa unataka kuniuliza nini wakati tulikuwa wote kuanzia mwanzo hadi mwisho" Msaidizi wa mganga alijibu huku akionekana akimshangaa Sajenti Minja,
"najua ndugu yangu, ila naomba unisaidie kitu kimoja" Sajenti Minja aliongea huku akisubiri sauti itakayomruhusu aendelee .
"endelea" Msaidizi wa mganga alijibu.
"naomba polisi yeyote atakaekuuliza kuhusu yale mambo yaliyötokea kule, mjibu hujui chochote, sawa?" Sajenti Minja aliwasilisha ombi lake huku akiwa hana uhakika wa kukubaliwa,
"kwanini tufiche ukweli?" Msaidizi wa mganga aliuliza kwa mshangao,

"Ukiongea ukweli utakuwa umeniharibia kila kitu katika maisha yangu, yaani hata kufungwa nitafungwa" Sajenti Minja aliongea kwa huruma ili kumshawishi Msaidizi wa Mganga akubaliane nae,

"Kwa maana hiyo wewe umependa lile tukio lililotokea siku ile?" Msaidizi wa Mganga alimuuliza Sajenti Minja,

"Tukio sasa, maana yalikuwa mengi" Sajenti Minja aliuliza,

"La wenzangu kuuawa kinyama?" Msaidizi wa Mganga aliuliza,

"Hapana, nitalifurahia vipi wakati lilikuja kuharibu tiba ya ndugu yangu na nikampoteza mtu ambaye ndiye nilikuwa nategemea yeye atamponya ndugu yangu?" Sajenti Minja aliongea kwa upole na machozi yakimtoka kwa mbali ili kumshawishi tu Msaidizi wa Mganga asiseme ukweli mbele ya Polisi wengine,

"Sasa kwanini nifiche?" Msaidizi wa Mganga akauliza tena ila kipindi hiki aliuliza kwa upole,

"Kuwa na utu ndugu yangu, maana unachotaka kukifanya ni kuniharibia maisha tu" Sajenti Minja aliendelea kumlalamikia Msaidizi wa Mganga,

"Sio nakuharibia maisha, mbona mimi maisha yangu yameshaharibika?" Msaidizi wa Mganga aliongea huku anamkodolea macho Sajenti Minja,

"Yameharibikaje sasa wakati upon hai na upon huru?" Sajenti Minja alimuuliza,

"Hill sio tatizo, tatizo ni kwamba yule Mganga nilimchukulia kama mkombozi wangu kutokana na maisha yangu" Msaidizi wa Mganga aliongea,

" kivipi yaani?" Sajenti Minja alimuuliza,

"Yaani nilikuwa sina mbele wala nyuma, ila yule mzee aliniokota tu mjini na kunichukua kisha akawa ananifundisha uganga na akawa ananipa kipato kidogo angalau nikajiona mtu" Msaidizi wa Mganga aliongea,

"Hilo sio tatizo, ngoja upone tutaongea zaidi, mimi nitakusaidia" Sajenti Minja aliongea kwa huruma huku akichomoa noti nyingi kutoka katika mfuko wake wa suruali na kumpa msaidizi wa Mganga,

"Za nini hizi?" Msaidizi wa Mganga aliuliza huku akiwa anaziangalia zile hela akiwa hataki kuzipokea,

"Zitakusaidia kununua vitu vidogo vidogo kipindi upo hapa Hospitali" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado amezishikilia zile pesa,

"Wewe ni ndugu yangu bwana, tusaidiane" Sajenti Minja aliongea kwa upole,

"Ngoja nitoke hospitali tutaongea vizuri ndugu yangu" Msaidizi wa Mganga aliongea huku akizitia pesa zile mfukoni,

"Nikununulie chakula gani kabla sijaondoka" Sajenti Minja alimuuliza,

"Chochote tu, mimi mswahili bwana sichaguagi chakula" msaidizi wa Mganga aliongea,

"Wewe mgonjwa bwana, itabidi ule minyama nyama, ngoja nikakutafutie kuku bosi" Sajenti Minja aliongea kwa furaha huku akitoka nje na akiamini tayari ameshamteka hisia yule Msaidizi wa Mganga.

**"***********

Babu wa monchwari alivyopigwa ule mtama ile asubuhi kumbe aliteguka mguu maeneo ya nyuma ya paja chini ya kiuno ila alivumilia na hakuwaambia kitu chochote wale polisi kwa sababu walikuwa na hasira muda ule, ila ilivyofika jioni maumivu yalimzidia na Babu wa monchwari akawaambia polisi ila walimpuuza tu, masikini Babu wa watu maumivu yalimzidia mpaka akawa Amalia kwa sauti kubwa kama mtoto, kilio kikamfikia mkuu wa polisi na kuja kuangalia kuna nini,

" mbona huyo mzee analia?" Mkuu wa polisi aliwauliza askari aliowakuta hapo ambayo walibaki wakitazamana bila kutoa jibu,

"Anamaumivu nadhani" Askari mmoja alijibu,
"Babu una tatizo gani?" Mkuu wa Polisi aliamua amuulize mwenyewe,
"Mguu nahisi umevunjika, nawaambia wanisaidie ila wananitukana" Babu alijibu huku akiendelea kulia,
"Umevunjikaje, umeanguka?" Mkuu wa Polisi aliuliza,
"Hao wenyewe walinipiga asubuhi" Babu alijibu,
"Hata mambo ya kuwapiga watuhumuwa si tulishawakataza?, tena mnampiga mzee kabisa..ebu chukueni gari ya doria mumpeleke hospitali" Mkuu wa Polisi aliongea kwa ukali na vijana wake wakanyanyuka haraka,

"Kwani yupo hapa kwa kosa gani" Mkuu wa polisi akauliza,

"Huyu ndiye yule mlinzi wa monchwari" Askari mmoja akajibu,
"Hata mumpeleke hospitali akapatiwe matibabu na mumrudishe hapa," Mkuu wa polisi aliongea na kuondoka huku akiwaacha vijana wake wakimbeba Babu monchwari na kumpeleka kwenye gari na safari ya hospitali ikaanza.

Iliwachukua dakika chache kufika hospitali, walimshusha Babu na kumpeleka kupata matibabu.

Babu akapatiwa huduma kisha kwa Saa nzima na akaonekana ni mfupa tu ulikuwa umehama eneo lake, madaktari wakafanya jitihada na kumtibu bila tatizo na kuwaruhusu askari waondoke nae.
Askari walipotoka nje walienda moja kwa moja mpaka kwenye gari yao, wakapanda gari ili warudi kituoni, kwa bahati mbaya gari yao ilipata itilafu ikawa haiwaki, ikabidi wapige simu kwa mkuu wao ili wapate msaada, mkuu wao akawapa namba ya sajenti Minja na kuwaambia yuko pale hospitali kwa hiyo wampigie awape msaada wa kuwarudisha kituoni kwa maana Sajenti ana gari.
Sajenti Minja baada ya kupigiwa simu akawaelekeza mahali gari lake lilipo, wale askari na Babu wa mochwari wakafika mahali gari lilipo, kisha wakawa wanamsubiri sajenti Minja atoke ndani ili awarudishe kituoni, na Babu wa monchwari ndio kabisa alikuwa anaangalia katika mlango wa kutokea hospitali ambayo ndio njia anayokuja nayo Sajenti Minja..

***"***"ITAENDELEA******""

*Kwa Mara nyingine tena Sajenti Minja anakutana na mtihani wa kukutanishwa na Babu wa monchwari, je nini kitatokea?

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO.

______________
ILIPOISHIA...
______________
Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu.

akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa

"tumekwisha...".

Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu walioloala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............

___________
ENDELEA
___________

"Hapa sijui kama tutapona" Mganga alitamka maneno hayo, huku akiwa
kama anajitayarisha na pambano jingine.

Mzimu ulipiga kelele zilizowatisha watu wore pale, kisha ulirudi kwa kasi ndani ya mwili wa Kayoza, kisha Kayoza
akanyanyuka taratibu, alikuwa tayari
keshabadilika, alikuwa anaogepesha ukimtazama msoni, macho yalikuwa meupe yasiyo na mboni na meno ya mbele pembeni yalikuwa marefu kama ya mnyama simba.

Kayoza akawatazama wote, alafu akawa
anamfuata Omari, Omari kuona hivyo, mkojo
ukaanza kumtoka na hata kukimbia akawa anashindwa ila alibaki ametoa macho huku machozi yakimtoka ingalikuwa halii.

Kayoza alipomfikia Omary
akamuangalia kisha akaachane nae, sasa akawa
anafuata mganga ambaye muda wote alikuwa bado anafanya mambo yake ya kiganga kwa ajili ya kujaribu kuutuliza mzimu wa Kayoza.

Mganga baada ya kuona mzimu unamfuata, maamuzi aliyoyachukua ni kutoka tu
mbio, akasababisha na watu walikuwepo katika
hilo eneo nao watoke mbio
mganga hakufika hata mbali, Kayoza akamkamata,

"Wewe ni nani mpaka utake kunitoa katika nyumba yangu?" Mzimu ulimuuliza mganga huku ukiwa umemkaba katika shingo na kusababisha kucha zake ndefu zipenye kwenye shingo ya mganga,

"Mi...mii..nimeagi..zwa tu na ndugu za...ko" Mganga aliongea kwa tabu huku damu zikimchuruzika shingoni.

Ila pamoja na utetezi wake ule mzimu ulimbeba juu na kung'ata shingoni kisha aakaanza kumnyonya damu, alipomaliza akamtupa pembeni.

Kisha mzimu ukatoka mbio na kuwakuta wasaidizi wa mganga wakiwa wanakimbia na wale
wasaidizi wake pia wakanyonywa damu.

Kisha Kayoza akamfuata sajenti Minja, ambae yeye alikimbia ila mwisho akaamua asimame tu maana aliona hata kama akikimbia ni lazima tu akamatwe.

Mzimu akamkamata mkono Sajenti Minja alafu akawa anamvutia
kichakani sehemu ambayo kulikuwa na miti mingi, alipofika katika eneo lenye miti,

"Usipate kichwa kwa kuwa niliahidi kutoidhuru damu yenu, wewe ndiyo utasababisha nivunje ahadi yangu" Mzimu uliongea huku
Ukikata fimbo, na kisha ukaanza kumtandika Sajenti Minja, alimtandika
kisawa sawa, mpaka sajenti Minja akawa analia kama mtoto.

Mzimu uliporidhika na bakora alizozipata Sajenti Minja ukamuachia na Sajenti Minja akatoka mbio kama mwendawazimu na kuishika ile njia waliyokuja nayo ambayo ilikuwa inaelekea nyumbani kwa Mganga.

Mzimu ulipomuachia Kayoza, Kayoza akadondoka chini kama kifurushi na akapoteza fahamu.

Omary yeye baada ya kuachwa na mzimu wala hakukimbia, alikuwa anaangalia tu unyama unaofanywa na mzimu na hata wakati Kayoza anaanguka na kupoteza fahamu Omary aliona na akaamini tayari mzimu umemuachia rafiki yake, Maamuzi aliyoyachukua Omary ni kwenda kumpa msaada Kayoza, alipofika, akambeba Kayoza kisha akawa kwenda walipoacha gari lao ambapo ni nyumbani kwa Mganga.

Walifanikiwa kufika salama nyumbani kwa mganga na wakamkuta Sajenti Minja anaangaika kufungua mlango wa gari ili aingie,

"Vipi huyo tayari au bado?" Sajenti Minja alimuuliza Omary baada ya kumuona anakuja na Kayoza,

"Tayari amerudi katika hali yake" Omary alijibu huku akifungua mlango wa gari na kumuingiza Kayoza,

"Aisee hii siwezi kuisahau" Sajenti Minja aliongea huku akiwasha gari na kuiondoa kwa kasi.

"Hii ilikuwa hatari, ila wewe hajakudhuru" Omary aliongea huku akijua fika Sajenti Minja alipewa bakora zisizo kuwa na idadi,

"Usiseme hivyo wewe, dah yaani nimefanywa mtoto Leo, tena mtoto wa shule" Sajenti Minja aliongea kwa huzuni,

"Umefanywaje kwani mjomba?," Omary aliuliza huku akimcheka kimoyomoyo,

"Hata kuhadithia siwezi, ni kitendo cha aibu sana" Sajenti Minja aliongea,

"Si uniambie tu mjomba" Omary alikazania huku akiendelea kumcheka moyoni,

"Nitakuambia tukifika bwana" Sajenti Minja alijibu huku akiongeza mwendo wa gari.

*****************

Katika hospitali ya mkoa kulikuwa na kasheshe
kubwa sana, kuna watu waliambiwa ndugu yao
amefariki, ila walipoenda monchwari hawakuikuta
maiti ya ndugu yao, walipowafata madaktari
wakawathibitishia kuhusu kifo cha ndugu yao, na
hata babu wa monchwari alithibisha kupokea maiti
ya huyo ndugu yao, sasa cha ajabu maiti ikawa
haionekani
Polisi walipofika pale hospitali, wakamchukua
babu wa mochwari huku wakiwa na uhakika kuwa
huyu mzee anahusika kwa namna moja au nyingine
katika upotevu wa ile maiti.

Babu akachukuliwa hadi kituoni, walipomfikisha
wakaanza kumuhoji,

"Mzee kuwa mkweli, tuambie huo mwili umeupeleka wapi?" Askari alimuuliza Babu wa monchwari,

"Yaani hata mimi sielewi, ule mwili kweli niliupokea ila hata ulivyopotea mimi sijui" Babu alijibu kwa kujiamini,

"Kwani walinzi mpo wangapi pale monchwari" Askari aliuliza,

"Tupo wawili" Babu alijibu,

"Umesema wewe ndiye uliupokea mwili, he wakati mwili unapotea ilikuwa zamu ya nani kulinda?" Askari akaendelea kuuliza,

"Yaani huo mwili niliupokea Jana saa mbili usiku, na imeonekana haupo Leo saa kumi na mbili alfajiri" Babu alijibu,

"Ilikuwa zamu ya nani?" Askari aliuliza,

"Zamu yangu" Babu alijibu,

"Babu acha kutuchanganya, inaonesha wewe unajua kila kitu kuhusu kupotea kwa huo mwili" Askari aliongea huku akitabasamu ili asimtishe Babu,

"Unadhani nakutania mjukuu wangu?, kweli mimi sijui kitu, inawezekana mile chumba cha monchwari kina wachawi, si unajua wachawi wanazipenda sana maiti" Babu alijitetea na kumfanya askari acheke,

"Babu sema kweli usiogope, hata kama umeusika hatuwezi kukufunga, maana utakuwa kama shahidi, na si unajua shaidi hafungwi?" Askari alimlainisha Babu huku akiendelea kucheka,

"Kweli hamuwezi kunifunga?" Babu aliuliza huku akimuangalia Askari,

"Kama utamtaja muhusika hautofungwa mzee, ila ukishikiria msimamo wako wa kuficha ndio utakaokuingiza matatizoni" Askari alimwambia babu wa monchwari,

"Kusema ukweli aliyeuchukua ule mwili namjua kwa sura ila jina simjui" Babu aliamua kusema ukweli,

"Anakaa Wapi?" Askari aliuliza,

"Sijui ila nikimuona tu sura yake namjua hata kama nikitoka kulala" Babu aliendelea kukazania maneno yake,

"Kulikuwa na makubaliano yoyote kati yenu mpaka auchukue huo mwili?" Askari aliuliza,

"Hapana aisee" Babu alikataa,

"Sasa alichukuaje na wakati wewe mlinzi ulikuwepo?" Askari aliendelea kumbana kwa maswali,

"Alikuja na bunduki akanitishia, kisha akaingia ndani na kubeba maiti" Babu wa monchwari aliamua kusema uongo,

"Sasa kwa nini tokea mwanzo hukusema hivyo?" Askari aliuliza huku akimuangalia usoni,

"Nilikuwa siamini kama mtaniamini" Babu alijibu,

"Sawa babu, itabidi urudi ndani" Askari aliongea huku akisimama,

"Ndani tens kufanya mini?" Babu aliuliza kwa kuamaki,

"Utatoka tu babu, ila kwa sasa mtuhumiwa bado unahesabika ni wewe mpaka apatikane huyo mwingine unaedai alikuvamia na bunduki" Askari aliongea na kubonyeza kitufe kilichopo mlangoni na mlango ukafunguka wakaingia Askari wengine wawili,

"Mpelekeni selo" Askari aliwaamrisha wenzake ambayo walimshika babu huku na huku na kutoka nae nje.

wanamtoa katika chumba cha mahojiano, ili
wampeleke rumande.

****************

Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
Sajenti Minja akawarudisha wakina Kayoza kwa
mama Kayoza, kisha yeye akawa anaelekea
kituoni,
alipofika, akapaki gari lake kisha akawa anaenda
katika ofisi ya mkubwa wake, katika kolido ya
ofisi akapishana na askari watatu waliokuwa
wamemfunga pingu mzee mmoja ambae sura
yake haikuwa ngeni kwake yeye Sajenti Minja, ikabidi
ageuke amwangalie tena, na yule mzee nae
akageuka kumuangalia sajenti Minja, ndipo
sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo yule mzee monchwari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....

********ITAENDELEA*********

the Legend☆
Aisee nimecheka sana, minja kakutana na fimbo za kufa mtu.
Jamani panya nae sijui alitokea wapi khaa...!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA NANE.

______________
ILIPOISHIA...
______________

"nibusu basi ili nishinde vizuri mwenzio" mtoto wa mchungaji akaongea kwa mahaba.
"kesho rafiki yangu, hivi huogopi kusema hayo maneno katika nyumba takatifu kama hii?" kayoza akamjibu kwa busara,
"si unibusu jamani wewe." yule binti akakomalia kwa sauti ya juu kidogo.
"unamwambia nani akubusu?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akiwa anaingia Sebuleni.....

____________
ENDELEA..,.
_____________

..."hakuna kitu baba" binti mchungajibu akajibu.
"kwa hiyo nimesikia vibaya?" Mchungaji Wingo akauliza huku anamuangalia binti yake.
"nilikuwa namsimulia filamu moja hivi ilioneshwa jana ." binti wa Mchungaji akajibu huku akiangalia chini kwa aibu,

"Umekalia kuangalia filamu tu, badala ukazane kusoma biblia ili uongeze imani unakalia kuongeza ujinga tu" Mchungaji Wingo alimwambia binti yake aliyekuwa amesimama mbele yake
"Nisamehe baba, ila hiyo filamu ilikuwa na Mafundisho tu mazuri" Binti Mchungaji alijitetea,

"Ebu tupishe bwana" Mchungaji Wingo akamwambia mwanae na binti akaondoka haraka,
"Huyu mwanangu ni muongeaji sana, yupo tofauti na wenzake kabisa" Mchungaji Wingo aliongea huku akimgeukia Kayoza na usoni akikunjua tabasamu,

"Ila ni mcheshi sana, yaani amenizoea muda mfupi sana" Kayoza nae alijibu,

Kisha mchungaji na kayoza wakawa wanaongea, ila jambo kubwa ambalo mchungaji alimsisitiza Kayoza asikose katika maombi ya usiku.
Kayoza akarejea kwao kujumuika na mama yake.
"vipi mwenzetu, mchungaji alikuwa anakuambia nini?" mama kayoza alimuuliza mwanae.
"tulikua tunaongea mambo ya kawaida tu" kayoza akajibu.
Kisha mama kayoza akaenda jikoni kutayarisha chakula.
"eh, mwana leo nimekutana na vituko" Kayoza alianza namna hiyo kumuelezea Omari.
"wapi tena shee" Omari akauliza kwa shauku .
"si kwa mchungaji mwanangu, kuna binti yake mkubwa amedata na flag yangu"Kayoza aliongea huku akitabasamu
"kwa hiyo unataka kufanyaje?" Omari akauliza huku amekunja sura.
"nitafanyaje ndugu yangu, na hili dubwana linanibana" Kayoza alijibu kwa upole
"aah, ok, we mshiti au kama ana mahamu nitajaribu kumseti mimi" Omari aliongea, na kusababisha wote wakacheka.

"Poa mi ntakupigia pande, we si mwanangu bwana" Kayoza aliongea huku akicheka...

*****************

Sajenti Minja hakwenda kupima, alimfuatilia mkubwa wake mpaka alipomuona anapanda gari na kuondoka, naye akarudi ndani moja kwa moja hadi katika kitanda cha msaidizi wa mganga..
"vipi, unaweza kukaa" Sajenti Minja alimuuliza yule msaidizi wa mganga.
"kwanini nisiweze?, naweza tu" Msaidizi wa mganga akajibu,
"kuna maswali machache nataka nikuulize" Sajenti Minja akaongea kwa upole.
"kwani wewe ni polisi" Msaidizi wa mganga aliuliza ili apate uhakika, kwa sababu alimuhisi.
"ndio" sajenti Minja alijibu.
"sasa unataka kuniuliza nini wakati tulikuwa wote kuanzia mwanzo hadi mwisho" Msaidizi wa mganga alijibu huku akionekana akimshangaa Sajenti Minja,
"najua ndugu yangu, ila naomba unisaidie kitu kimoja" Sajenti Minja aliongea huku akisubiri sauti itakayomruhusu aendelee .
"endelea" Msaidizi wa mganga alijibu.
"naomba polisi yeyote atakaekuuliza kuhusu yale mambo yaliyötokea kule, mjibu hujui chochote, sawa?" Sajenti Minja aliwasilisha ombi lake huku akiwa hana uhakika wa kukubaliwa,
"kwanini tufiche ukweli?" Msaidizi wa mganga aliuliza kwa mshangao,

"Ukiongea ukweli utakuwa umeniharibia kila kitu katika maisha yangu, yaani hata kufungwa nitafungwa" Sajenti Minja aliongea kwa huruma ili kumshawishi Msaidizi wa Mganga akubaliane nae,

"Kwa maana hiyo wewe umependa lile tukio lililotokea siku ile?" Msaidizi wa Mganga alimuuliza Sajenti Minja,

"Tukio sasa, maana yalikuwa mengi" Sajenti Minja aliuliza,

"La wenzangu kuuawa kinyama?" Msaidizi wa Mganga aliuliza,

"Hapana, nitalifurahia vipi wakati lilikuja kuharibu tiba ya ndugu yangu na nikampoteza mtu ambaye ndiye nilikuwa nategemea yeye atamponya ndugu yangu?" Sajenti Minja aliongea kwa upole na machozi yakimtoka kwa mbali ili kumshawishi tu Msaidizi wa Mganga asiseme ukweli mbele ya Polisi wengine,

"Sasa kwanini nifiche?" Msaidizi wa Mganga akauliza tena ila kipindi hiki aliuliza kwa upole,

"Kuwa na utu ndugu yangu, maana unachotaka kukifanya ni kuniharibia maisha tu" Sajenti Minja aliendelea kumlalamikia Msaidizi wa Mganga,

"Sio nakuharibia maisha, mbona mimi maisha yangu yameshaharibika?" Msaidizi wa Mganga aliongea huku anamkodolea macho Sajenti Minja,

"Yameharibikaje sasa wakati upon hai na upon huru?" Sajenti Minja alimuuliza,

"Hill sio tatizo, tatizo ni kwamba yule Mganga nilimchukulia kama mkombozi wangu kutokana na maisha yangu" Msaidizi wa Mganga aliongea,

" kivipi yaani?" Sajenti Minja alimuuliza,

"Yaani nilikuwa sina mbele wala nyuma, ila yule mzee aliniokota tu mjini na kunichukua kisha akawa ananifundisha uganga na akawa ananipa kipato kidogo angalau nikajiona mtu" Msaidizi wa Mganga aliongea,

"Hilo sio tatizo, ngoja upone tutaongea zaidi, mimi nitakusaidia" Sajenti Minja aliongea kwa huruma huku akichomoa noti nyingi kutoka katika mfuko wake wa suruali na kumpa msaidizi wa Mganga,

"Za nini hizi?" Msaidizi wa Mganga aliuliza huku akiwa anaziangalia zile hela akiwa hataki kuzipokea,

"Zitakusaidia kununua vitu vidogo vidogo kipindi upo hapa Hospitali" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado amezishikilia zile pesa,

"Wewe ni ndugu yangu bwana, tusaidiane" Sajenti Minja aliongea kwa upole,

"Ngoja nitoke hospitali tutaongea vizuri ndugu yangu" Msaidizi wa Mganga aliongea huku akizitia pesa zile mfukoni,

"Nikununulie chakula gani kabla sijaondoka" Sajenti Minja alimuuliza,

"Chochote tu, mimi mswahili bwana sichaguagi chakula" msaidizi wa Mganga aliongea,

"Wewe mgonjwa bwana, itabidi ule minyama nyama, ngoja nikakutafutie kuku bosi" Sajenti Minja aliongea kwa furaha huku akitoka nje na akiamini tayari ameshamteka hisia yule Msaidizi wa Mganga.

**"***********

Babu wa monchwari alivyopigwa ule mtama ile asubuhi kumbe aliteguka mguu maeneo ya nyuma ya paja chini ya kiuno ila alivumilia na hakuwaambia kitu chochote wale polisi kwa sababu walikuwa na hasira muda ule, ila ilivyofika jioni maumivu yalimzidia na Babu wa monchwari akawaambia polisi ila walimpuuza tu, masikini Babu wa watu maumivu yalimzidia mpaka akawa Amalia kwa sauti kubwa kama mtoto, kilio kikamfikia mkuu wa polisi na kuja kuangalia kuna nini,

" mbona huyo mzee analia?" Mkuu wa polisi aliwauliza askari aliowakuta hapo ambayo walibaki wakitazamana bila kutoa jibu,

"Anamaumivu nadhani" Askari mmoja alijibu,
"Babu una tatizo gani?" Mkuu wa Polisi aliamua amuulize mwenyewe,
"Mguu nahisi umevunjika, nawaambia wanisaidie ila wananitukana" Babu alijibu huku akiendelea kulia,
"Umevunjikaje, umeanguka?" Mkuu wa Polisi aliuliza,
"Hao wenyewe walinipiga asubuhi" Babu alijibu,
"Hata mambo ya kuwapiga watuhumuwa si tulishawakataza?, tena mnampiga mzee kabisa..ebu chukueni gari ya doria mumpeleke hospitali" Mkuu wa Polisi aliongea kwa ukali na vijana wake wakanyanyuka haraka,

"Kwani yupo hapa kwa kosa gani" Mkuu wa polisi akauliza,

"Huyu ndiye yule mlinzi wa monchwari" Askari mmoja akajibu,
"Hata mumpeleke hospitali akapatiwe matibabu na mumrudishe hapa," Mkuu wa polisi aliongea na kuondoka huku akiwaacha vijana wake wakimbeba Babu monchwari na kumpeleka kwenye gari na safari ya hospitali ikaanza.

Iliwachukua dakika chache kufika hospitali, walimshusha Babu na kumpeleka kupata matibabu.

Babu akapatiwa huduma kisha kwa Saa nzima na akaonekana ni mfupa tu ulikuwa umehama eneo lake, madaktari wakafanya jitihada na kumtibu bila tatizo na kuwaruhusu askari waondoke nae.
Askari walipotoka nje walienda moja kwa moja mpaka kwenye gari yao, wakapanda gari ili warudi kituoni, kwa bahati mbaya gari yao ilipata itilafu ikawa haiwaki, ikabidi wapige simu kwa mkuu wao ili wapate msaada, mkuu wao akawapa namba ya sajenti Minja na kuwaambia yuko pale hospitali kwa hiyo wampigie awape msaada wa kuwarudisha kituoni kwa maana Sajenti ana gari.
Sajenti Minja baada ya kupigiwa simu akawaelekeza mahali gari lake lilipo, wale askari na Babu wa mochwari wakafika mahali gari lilipo, kisha wakawa wanamsubiri sajenti Minja atoke ndani ili awarudishe kituoni, na Babu wa monchwari ndio kabisa alikuwa anaangalia katika mlango wa kutokea hospitali ambayo ndio njia anayokuja nayo Sajenti Minja..

***"***"ITAENDELEA******""

*Kwa Mara nyingine tena Sajenti Minja anakutana na mtihani wa kukutanishwa na Babu wa monchwari, je nini kitatokea?

the Legend☆
Sajenti Minja jinamizi bado linakufuatilia, usihofu mzimu utakutoa kwenye msala [emoji28][emoji28][emoji28]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TISA.

______________
ILIPOISHIA...
______________
Sajenti Minja baada ya kupigiwa simu akawaelekeza mahali gari lake lilipo, wale askari na Babu wa mochwari wakafika mahali gari lilipo, kisha wakawa wanamsubiri sajenti Minja atoke ndani ili awarudishe kituoni, na Babu wa monchwari ndio kabisa alikuwa anaangalia katika mlango wa kutokea hospitali ambayo ndio njia anayokuja nayo Sajenti Minja.

____________
ENDELEA...
____________

....Sajenti Minja wakati anatoka ndani ya hospitali, akawaona wale polisi na yule babu wa mochwari kupitia dirishani, akasita, kisha akili yake ikafanya kazi haraka.
akarudi kisha akawapigia simu wale askari na kuwaambia kuwa yeye bado ana shughuli anazifanya katika eneo like la hospitali, kwa hiyo askari mmoja amfuate ndani ili akampe ufunguo,
mmoja kati ya wale polisi akaenda alipoelekezwa na sajenti Minja, akapewa ufunguo, kisha akaambiwa arudishe gari pale hospitalini baada ya kazi zao

***********************

Sajenti Minja aliingia katika nyumba ya dada yake saa mbili usiku, baada ya salamu wakakumbushana mambo yaliyowakuta usiku uliopita, wakafurahi na kuhuzunika pia,
Ila habari iliyowashtua wote ni kupatikana kwa wale maiti na mtu mmoja akiwa mzima, pia sajenti Minja akawaambia namna alivyofundisha yule msaidizi wa mganga kukana kujua lolote.
Mama kayoza kidogo akashusha presha baada ya kusikia hivyo,
"Kitu kingine kibaya ni kwamba hata yule babu wa monchwari aliyetusaidia kuiba ile maiti nae amekamatwa ila sijajua kwa kesi gani?" Sajenti Minja aliendelea kutoa habari mbaya,

"Ni hiyo hiyo ya kupotea kwa maiti, asubuhi si nilikuwa hospitali nilienda kumuona mtu, ndio nikakutana na hizo habari, ila maiti yenyewe imeshapatikana uko makaburini ilikutwa pamoja na hiyo miili ya waganga wenu" Mama Kayoza aliwapa habari,

"Kama maiti imepatikana itakuwa afadhali kwa Babu" Kayoza aliongea,

"Hujui sheria mjomba, Babu hawezi kuachiwa mpaka ipatikane au ijulikane sababu za kuuza ile maiti" Sajenti Minja aliongea huku akimuangalia Kayoza,

"Sababu iliyomfanye auze si ni pesa?" Kayoza alijibu kiutani na wenzake wacheke,

"Haya mambo mazito msiyachukulie kiutani utani hivyo" Mama Kayoza aliongea huku akionekana kutofurahishwa na jibu la Kayoza,

"Mama inabidi tujifurahishe tu, ukisema uegemee sana upande wa yanayotukuta, tutakuwa watu wa machozi kila siku" Kayoza alimwambia Mama yake,

"Ujinga huo, badala uangalie namna ya kujisaidia unakalia kuongea vitu visivyo na kichwa wala miguu" Mama Kayoza aliendelea kumshambulia mwanaye,

"Vitu vya maana kama vipi?, ngoja nijiandae niende kanisani" Kayoza aliongea kwa hasira huku akiondoka sebuleni,

"Ana hasira kama babu yake, mzee John Minja" Sajenti Minja aliongea huku akicheka,

"Mjinga tu, hasira ananiletea Mimi badala ya kumpelekea bibi yake uko kijijini" Mama Kayoza aliongea,

"Kayoza anaenda kanisani?" Sajenti Minja aliuliza,

"Leo kuna maombi, tena na wewe itabidi uende ili bwana akakupe wepesi uenda kazi ya kumsaidia mjomba wako itatimia haraka" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja,

"Sawa itabidi tuongozane, kwani maombi yataisha saa ngapi?" Sajenti Minja akauliza,

"Tunakesha" Mama Kayoza alijibu,

"Mh..sasa si itabidi niende nyumbani nikabadili nguo" Sajenti Minja aliongea,

"Kwani hizo ulizovaa zina ubaya Gani? Mama Kayoza aliuliza,

"Mimi naona sio vizuri kwenda Nazi kwa sababu nimeshinda nazo kutwa nzima" Sajenti Minja alijibu,

"Hiyo sio sababu, nenda kaoge uende kanisani" Mama Kayoza aliongea,
"Sawa basi, nirudi baada ya muda gani?" Sajenti Minja aliuliza huku akiinuka,

"Hakuna kuondoka, nilipokwambia ukaoge nilimaanisha uingie bafuni, sasa unavyotaka kuondoka unadhani bafu lipo kwako tu?" Mama Kayoza aliuliza,

"Sawa bwana, basi ngoja nikajitayarishe" Sajenti Minja aliongea huku akielekea vilipo vyumba vya wakina Kayoza,

Baada ya saa moja na nusu wote walikuwa wamejiandaa mpaka Omary wakaanza kwenda eneo la maombi.
Walienda kwa miguu tu kwa maana ni eneo jirani na wanapoishi.
Walifika na muda ulipofika waumini walikuwa wengi sana kanisani, walianza kwa kuimba nyimbo mbalimbali za kutukuza.

Baada ya saa zima Mchungaji Wingo aliingia, akakaa katika kiti anachopaswa kuwepo. Nyimbo ziliimbwa kisha waimbaji wakamaliza, sala zilianza, walisali muda mrefu sana mpaka kayoza akachoka kutokana na kwamba yeye sio mtu aliyezoea sana kwenda kanisani,
"oya kaka, tusepe" kayoza alimwambia Omari ambae alikuwa anasinzia tu muda wote.
"wapi sasa" Omari akauliza kivivu huku akijinyoosha,
"maskani dogo, we unasinzia tu bila ya mpango, usije ukaharibu hewa bure" Kayoza aliongea kwa utani.
"aah wapi, mimi nina kontroo wewe" Omari akajibu kisha wote wakacheka.
Wakatoka nje ya kanisa wakawa wanaelekea nyumbani, ilikuwa kama saa saba usiku hivi, kwa mbali wakaona msichana anawakimbilia, alikuwa yule binti wa mchungaji,
"habari jamani" Binti akawasalimu.
"nzuri" wakajibu kwa pamoja.
"Kaka unaweza kutupisha kidogo?" Binti Mchungaji aliongea huku akimuangalia Omary,
"Sawa" Omary alijibu huku akitangulia mbele na kuwaacha Kayoza na Binti Mchungaji wakiwa wamesimama,
"vipi jibu langu Kayoza" Binti Mchungaji alimuuliza kayoza huku akiwa hana chembe ya aibu.
"kesho nitakujibu" Kayoza akajibu kwa ufupi.
"jamani mbona unanifanyia hivyo, au kwa kuwa nimekwambia nakupenda?" Binti Mchungaji alilalamika kwa huruma.
"sikia binti, hapa unapoteza muda wako bure, kiukweli kabisa mi siwezi kukubalia ombi lako" Kayoza aliongea kwa ujasili kwa maana aliona bora amueleze ukweli tu kuliko kumpotezea muda, Binti Mchungaji alijishusha sana, alafu akajenga chuki kali sana kwa Kayoza.
"Kwanini umeamua kufanya hivyo? au kwa kuwa nimeamua kukueleza hisia zangu?" Binti Mchungaji aliongea huku machozi yanamtoka,
"Nimefanya hivi kwa sababu nakupenda na najipenda pia" Kayoza aliongea kwa sauti ya chini kisha akaondoka kumfuata Omary,

"anajiona mzuri kumbe hana lolote, ni shetani tu ananyonya damu za watu, na kesho nitaitoa taharifa polisi ili nipate yale mapesa waliyotangaza" Binti Mchungaji aliongea kimoyo moyo huku akiwa anarudi kanisani na hasira kibao zikiwa zimemtawala.

*******

"kaka umeniangusha" Omari aliongea huku akitabasamu
"achana nae, mtoto wa mchungaji alafu anaendekeza ukicheche" Kayoza alijibu.
"Ila mpaka mwanamke akuambie maneno nayo, ujue anakupenda kweli" Omary alimwambia Kayoza,
"Akampende baba yake na mama yake, mimi sina taimu nae" Kayoza alijibu kijeuri,

"Sawa bwana, kufanya hivyo umemuepusha na kifo",Omary aliongea,

"Sijamuepusha, sema nimemsogezea mbele kifo kwa maana kifo hakiepukiki" Kayoza aliongea wakati wanafika eneo la nyumbani kwao.

**""""***************

Ilipofika alfajili, Sajenti Minja aliondoka kanisani na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwake kupumzika, kwa kuwa alichelewa sana kulala alijikuta anautandika usingizi mzito.
Mida ya saa nne akakurupuka kitandani kwake, ni kawaida yake kujisachi anapoamka, hasa pale anapolala na nguo alizotoka kutembea nazo,
alipojisachi, akakuta hana kitambulisho cha ofisini,
"mh, kitakuwa wapi, ila ngoja nikakicheki kwa dada kule na nidoee chai kabisa" sajenti Minja alijiongelesha peke yake.

Akaenda kuoga na kujisafisha kinywa kisha akajiandaa ili aende kwa Dada yake.
Akatoka nje akawasha gari, akaondoka

**********************

Binti wa mchungaji aliamka ana hasira sana siku hiyo, aliamka saa tatu, ila mpaka saa nne alikuwa ameshawapiga makofi wadogo zake wawili kutokana na hasira alizonazo. Tena aliwapiga kwa makosa madogo madogo tu yasiyo na msingi.

Binti Mchungaji alipomaliza kazi zake, akaenda kuoga, kisha akanywa chai, akavaa viwalo vyake vilivyompendeza, akamuaga mama yake kuwa anaenda kununua nguo.
"leo ndio mwisho wake, anaringa kama hana dhambi!" Binti Mchungaji aliongea kimoyo moyo wakati akitoka ndani ya geti la nyumba yao na kuishika barabara iendayo sehemu kilipo kituo kikubwa cha polisi cha mkoa,
"nikifika pale polisi namueleza askari yeyote, hata wasiponipa hela sawa, nataka tu nimkomeshe" Binti Mchungaji aliendelea kujiongelesha Mwenyewe, mara akasikia gari inapiga breki miguuni kwake, alishtuka na kuruka pembeni mpwa barabara, maana alikuwa na mawazo kiasi kwamba hakujua kama anatembea katikati ya barabara,

"punguza mawazo dada, mbona we bado mdogo tu" yule dereva wa ile gari alimwambia binti wa mchungaji.
"samahani kaka yangu" binti wa mchungaji alijitetea.
Kisha yule dereva wa gari akashuka ili kuiangalia gari yake iko salama, maana breki aliyoipiga ilikuwa Kali sana.
"aha! Kumbe polisi!" Binti Mchungaji alijikuta anahamaki baada ya kumuona yule dereva wa ile gari amevaa gwanda za polisi.
"ee, kwani vipi?" yule polisi aliuliza huku akimuangalia Binti wa Mchungaji,
"kuna habari njema nataka kukwambia" Binti Mchungaji alisema huku furaha yake ikionekana dhahiri machoni pake,
"habari gani hiyo?" yule polisi akamuuliza huku akiwa na shauku ya kutaka kujua,
Yule binti akageuka nyuma kuangalia kama kuna mtu anakuja, aliporidhka kuwa hakuna mtu, akasema,

"yule kijana anayenyonya damu za watu anakaa palee" Binti Mchungaji akasema huku akiionyeshea nyumba ya Mama kayoza ambayo ilikuwa inaonekana kwa mbali kidogo.

"Una uhakika binti?" Askari aliuliza huku akiwa ahamini anachoambiwa,
"Twende unipeleke" askari aliongea huku akimfungulia Mlango binti Mchungaji ambayo aliingia kwenye gari kwa madaha kwa maana alishaimaliza kazi aliyokusudia kuifanya....

******ITAENDELEA******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA THELATHINI.

______________
ILIPOISHIA...
_______________

ENDELEA..
______________

Binti Mchungaji akaingia ndani ya gari na kukaa siti ya mbele,

"Wewe umejuaje kuwa huyo kijana ndiye mnyonya damu?" Askari aliuliza huku akimuangalia Binti Mchungaji machoni,

"We hutakiwi kuniuliza, unachotakiwa ni kwenda kumkamata" Binti Mchungaji aliongea,

"Akikataa kuwa sio yeye unafikiri tutafanyaje, inatakiwa uniambie umejuaje kuwa ndiye yeye ili ninapoenda kumkamata niwe na ushahidi" Askari aliuliza,

"Ameshawahi kuja kanisani kwetu ili tumuombee ili apone na ahachane na hayo mambo ya kuua kwa kunyonya damu" Binti Mchungaji alijibu,

"Kumbe hata yeye hapendi we kunyonya damu na kuua?" Askari aliuliza huku akimtazama,

"Itakuwa hapendi, na ndio maana alikuja kanisani kuombewa" Binti Mchungaji alijibu,

"Sasa kama hata yeye hapendi kuua kuna haja gani ya kumkamata na wakati anaonekana ni mtu mwema?" Askari aliuliza,

"Wewe kaka ni hakimu au askari? Maana unauliza tu badala ya kwenda kumkamata mtuhumiwa, au unaogopa kunyonywa damu?" Binti Mchungaji aliuliza kwa hasira,

"Samahani, naomba nikuulize swali la mwisho kabla sijaenda kumkamata" Askari alitoa ombi,

"Sitaki swali, kama hauendi niambie nishuke, mbona askari mpo wengi tu, nitaenda kuwaambia Askari wengine" Binti Mchungaji aliongea kwa jeuri huku akiangalia pembeni,

"Naomba uniruhusu tu nikuulize hill swali, baada ya hapo sitokuuliza tena" Askari aliongea kwa upole,

"Na liwe la mwisho kweli, haya uliza" Binti Mchungaji aliongea kwa mbwembwe,

"Je huyo mnyonya damu angekua ndugu yako ungetoa taharifa polisi?" Askari aliuliza huku akiwasha gari,

"Inategemea na undugu wenyewe, kama ni wa mbali namchomea tu" Binti Mchungaji aliongea huku akifurahi gari kuwashwa kwa maana alipata uhakika wa kutimiza malengo yake,

"Angekuwa mtoto wa Dada yako au wa kaka yako je?" Askari aliuliza huku akiliondoa gari,

"Huo ni undugu wa karibu kabisa, siwezi kwenda kumsemea polisi kamwe" Binti Mchungaji aliongea huku akijitengeneza nywele vizuri, akiwa bado anajiweka vzuri alishangaa yule askari akisimamisha gari na kumpiga Kofi zito la usoni,

"Unanipigia nini sasa?" Binti Mchungaji aliuliza huku akiwa amejishika uso, ila yule Askari hakumjibu, akamuongeza jingine la uso tena pale pale alipopapiga mwanzo,

"Unanipigia nini sasa?" Binti Mchungaji aliuliza huku akisikilizia maumivu,

"Hiyo tabia yako ndio imekuponza" Askari aliongea huku akitabasamu,

"Tabia gani jamani" Binti Mchungaji alilamika huku akiwa amejishika shavu,

"Umbea, sio kila kitu kinatolewa taharifa" Askari aliongea huku akimuongezea kofi na kisha akafungua mlango wa gari ili yule msichana ashuke.

Binti akatelemka haraka haraka na yule Askari akaiondoa gari kwa spidi ya juu.

Gari la yule askari lilipopotea, yule binti mchungaji nae akahairisha safari yake,

"akha mwenzangu, huyu mmoja tu nimekutana nae njiani kanipiga vibao namna hii, je nikienda huko polisi si wataniua kabisa?" yule binti wa mchungaji aliongea huku akiwa ameshika njia ya kwenda kwao.

***********************

Sajenti Minja aliingia kwa Dada yake asubuhi na kuwakuta wakiwa wamekaa,

"Hivi huyu Mchungaji wenu ana binti mkubwa?" Sajenti Minja aliuliza baada ya salamu,

"Anae binti mkubwa kabisa, kwani vipi?" Mama Kayoza aliuliza,

"Aisee yule sio mtu mzuri kwetu, so nimekutana nae hapo njiani akanisimamisha na kuanza kunipa habari za Kayoza" Sajenti Minja aliongea,

"Eeeh, makubwa, amekwambiaje?" Mama Kayoza aliuliza,.

"Ooh Mara mnyonya damu namjua, alikuja kanisa kwetu na kuombewa, ooh Mara sijui nini, yaani inaonekana anamjua vzuri Kayoza" Sajenti Minja aliongea,

"Ikawaje sasa?" Mama Kayoza akauliza,

"Aisee nimemuwasha mabanzi, sijui hata kama atarudia tena kusema" Sajenti Minja aliongea huku akicheka,

"Usiseme hivyo, anaweza kwenda kituoni yule, maana ameshaonekana sio mtu mzuri" Mama Kayoza aliongea,

" hata akienda atakuwa hana Maelezo ya kutosha" Sajenti Minja aliongea kwa dharau,

"Tatizo lako wewe ni mpuuzi" Mama Kayoza aliongea kwa hasira baada ya kumuona Sajento Minja ana dharau

"Sasa Dada mbona unanitukana tena?" Sajenti Minja aliuliza,.

"Mpuuzi sio tusi, mtu anayepuuza jambo ndio huitwa mpuuzi" Mama Kayoza alimjibu ndugu yake,

"Sijapuuza hill jambo, mimi bado namfuatilia huyo binti ila sidhani kama ataenda kutoa taharifa polisi" Sajenti Minja aliongea,

"Haya bwana" Mama Kayoza aliongea kinyonge,

"Jana niliangusha kitambulisho changu, alafu hata sijui nilipokiangushia" Sajenti Minja aliamua kubadilisha mada,

"Kipo ndani, ulikiangushia hapa" Mama Kayoza alijibu,

"Afadhali, maana nilishapatwa na wasiwasi wa kukipoteza" Sajenti Minja aliongea.

Baada ya kukichukua kitambulisho chake aliaga na kwenda moja kwa moja hospitali kwa ajili ya kwenda kumuona Msaidizi wa Mganga.

Alifika mapema na moja kwa moja akaenda kumjulia hali Msaidizi wa Mganga, baada ya kumjulia hali mgonjwa wake, Sajenti Minja alifarijika kumuona mgonjwa wake amepata nguvu na anatembea kama kawaida.

Bila kupoteza muda, sajenti Minja akamtafuta daktari, kisha akapewa ruhusa ya kuondoka na mgonjwa wake, akamchukua hadi nyumbani kwake. Kisha akampa taharifa mkuu wa polisi kuwa yule msaidizi wa mganga ametoka hospitali na anakaa nae nyumbani kwake, mkuu akafurahi kusikia hivyo.

***********************

Kayoza na Omari walijua sababu kubwa ya binti wa mchungaji kutaka kwenda polisi ni kutokana na kukataliwa na Kayoza kuwa mpenzi wake,

Omari akaamua amchukue yeye, ikawa kila siku ni lazima aende kwa mchungaji, tena gia aliyokuwa anaenda nayo ni kununua maziwa, taratibu mazoea yakaanza hadi wakazoeana kabisa, mwisho kabisa Omari akamtongoza binti wa mchungaji, bila iyana alikubaliwa kwa roho safi, na sasa Omary na Binti Mchungaji wakawa Wapenzi rasmi.

***********************

Siku moja mkuu wa polisi alikuwa anafungua mlango wa ofisini kwake, ndio akawaona askari watatu wakiwa wameongozana na babu aliyefungwa pingu. Alikuwa ni yule Babu wa monchwari, akawaita, kisha akaingia ofisini, wale askari na yule babu nao wakaingia,

"hii kesi ya huyu mzee mbona mnaiendesha pole pole sana". Mkuu wa polisi aliwauliza wale askari.

"ushaidi ndio unatuchelewesha mkuu" Askari mmoja alijibu

"niambieni katika uchunguzi wenu mmefikia wapi" Mkuu wa Polisi akawatupia swali jingine,

"hakuna mwanga wowote tuliopata" yule askari akamjibu tena mkuu wa polisi.

"nyie wazembe kweli, ile maiti iliyoibiwa si iliokotwa pamoja na zile maiti zilizonyonywa damu?" Mkuu wa polisi akauliza kwa jazba,

"ndio mkuu" wale askari wakajibu kwa pamoja,

"mlienda kumuhoji yule mtu aliekutwa hai?" Mkuu wa Polisi akawapa swali jingine.

"hapana mkuu" akajibu yule Askari ambae siku zote uso wake utawaliwa na hasira.

"kwanini" mkuu wa polisi akaendelea kuwabana na maswali.

"yule anahusika na kesi ya sajenti Minja" yule askari akajitetea kipumbavu.,

"ok, sasa hii kesi ya huyu babu nampa sajenti Minja kwa sababu mmesema zinaingiliana, basi atazishughulikia zote" Mkuu wa polisi alimaliza kisha akawaamuru watoke ofisini kwake, wamuache babu wa monchwari peke yake, wakamtii kisha wale askari wakaondoka.

Kisha mkuu wa polisi akachukua simu yake ya mkononi alafu akapiga,
"hallow Minja uko wapi?"mkuu wa polisi aliuliza. Baada ya kujibiwa akaendelea,

"Nipo ofisini kwangu" Sajenti Minja alijibu huku akishangaa ile simu ya ghafla kutoka kwa mkubwa wake,

"ok, njoo ofisini kwangu" Mkuu wa Polisi aliongea kisha akakata simu.

"nakukabidhi kwa mtu anaejua kazi" Mkuu wa polis alimwambia babu wa mochwari,

"Nashukuru sana kwa kunijali mwanangu" Babu wa monchwari aliongea huku akiangalia chini.

"Sio nakujali, huo ndio utaratibu wa kazi" Mkuu wa Polisi aliongea.

************

Sajenti Minja baada ya simu aliyopigiwa na mkuu wake kukatwa,
akatoka ofisini kwake huku akiwa na maswali kibao juu ya kuitwa kwake na Mkuu wa Kituo.

Akawa anaelekea ofisi ya mkuu wa polìsi, alipofika mlangoni akagonga hodi,

"yes, come in" sauti ya mkuu wake kutoka ndani ilimjibu,

Sajent Minja akashika kitasa cha mlango akanyonga kwa nia ya kufungua mlango.....

******ITAENDELEA*******

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA.

______________
ILIPOISHIA...
_______________

Sajenti Minja baada ya simu aliyopigiwa na mkuu wake kukatwa,

akatoka ofisini kwake huku akiwa na maswali kibao juu ya kuitwa kwake na Mkuu wa Kituo.

Akawa anaelekea ofisi ya mkuu wa polìsi, alipofika mlangoni akagonga hodi,

"yes, come in" sauti ya mkuu wake kutoka ndani ilimjibu,

Sajent Minja akashika kitasa cha mlango akanyonga kwa nia ya kufungua mlango.....

_____________
ENDELEA..
______________

...sajenti Minja akanyonga kitasa, haikuonekana dalili ya mlango kufunguka, mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani, mara akasikia mlango unafunguliwa, akatoka mkuu wa polisi,

"minja nisubiri ndani mara moja, naenda msalani dakika moja", mkuu wa polisi alipofungua mlango aliongea maneno hayo huku akiwa anatembea kumuacha sajenti Minja, mlango ulikuwa bado uko wazi, Sajenti Minja akanyanyua mguu wa kulia ili kuingia ndani,

"jesus christ" alijikuta anasema kwa sauti ya chini baada ya kugundua kuwa aliekuwa ndani ni babu wa mochwari, ila bahati nzuri ni kwamba yule babu alikuwa ameinamia chini, kwa hiyo hakuweza kumgundua Sajenti Minja.

Sajenti Minja alirudi nje kwa kasi, kisha akaurudishia mlango huku anahema kwa fujo kama katoka kukimbia mbio ndefu,

"vipi Minja, mbona unaonekana hauko kawaida", sauti ya mkuu wa polisi ilimshtua Sajenti Minja,

"nimepigiwa simu, nyumbani kuna matatizo" Sajenti Minja alitumia uongo,

"ila kulikuwa na kazi nataka kukupa, tuingie ndani kuna kesi nataka kukupa, alafu utaendelea na ratiba zako", Mkuu wa Polisi alimwambia Sajenti Minja,

"samahani mkuu, niko chini ya miguu yako, naomba hiyo kesi unipe baadae, uko nyumbani sio kwema kabisa", Sajenti Minja aliongea uku akiwa ameweka sura ya huzuni,

"mmmh, ok, sawa, ukimaliza ya nyumbani, unijulishe, maana nataka nikupe kesi ya mzee mmoja hivi", Mkuu wa polisi alimkubalia,

"Nikimaliza nitakujulisha na asante mkuu kwa kunikubalia niende nyumbani, nikirudi nitakufahamisha" , Sajenti Minja alijibu huku akiwa anaanza kuondoka,

"Minja" Mkuu wa Polisi aliita tena wakati Sajenti Minja anaanza kuondoka,

"naam mkuu" Sajenti Minja aliitikia baada ya kuitwa,

"unaondoka tu, ila hujaniambia nyumbani kuna tatizo gani", Mkuu wa Polisi alihoji,

"kuna kajomba kangu, ambacho ni katoto ka dada yangu ambae nilikuambia anaishi hapa, nimeambiwa amegongwa na gari na hali yake sio nzuri", Sajenti Minja aliendelea kutunga uongo mbele ya bosi wake,

"ooh, poleni sana, haya bwana wahi,"Mkuu wa Polisi alimruhusu sajenti Minja kwa mtindo huo.

Sajenti Minja aliondoka kwa mwendo wa haraka haraka mpaka gari yake ilipokuwepo,

"mhm, nimesevu so hadi raha, leo nilikua nahaibika mbele ya bosi", Sajenti Minja aliongea wakati anajipakia kwenye gari yake.

********************

"duh, mama ujue mi nashindwa kuelewa, naona kama ndio mmeniacha niendelee kuwa katika hali hii", Kayoza alimwambia mama yake wakiwa wanapata chakula cha mchana,

"ebu, acha uwendawazimu uko, mzazi gani anaependa mwanae awe katika matatizo?, we msubiri mjomba ako arudi labda atakuwa na mpya", Mama kayoza alimjibu mwanae huku akiwa anasafisha mikono yake kwa maji,

"lakini mama", Kayoza kabla hajamaliza kuongea, ilisikika sauti ya mtu ikigonga mlango,

"sukuma, mlango uko wazi", Mama Kayoza aliongea kwa sauti ya juu kidogo, ili mgongaji amsikie,

"hodi mpaka ndani, eeh, nina mguu mzuri kweli, yaani nimefika wakati wa mahakuli", Sajenti Minja aliongea huku akiurudishia mlango

,"karibu anko, ingawa ndo kinaisha", Omari alimwambia sajenti Minja, kisha wote wakacheka,

"ebu tuachane na hayo, leo kidogo nipate aibu ya mwaka mbele ya bosi wangu", Sajenti Minja alibadilisha stori,

"ehe, nini tena?", Mama Kayoza aliuliza kwa shauku.Sajenti Minja aliwaeleza mwanzo mpaka mwisho,

"kwa hiyo inavyoonekana anataka na kesi ya yule babu wa mochwari iwe chini yako?" Mama Kayoza aliuliza,

"ndio hivyo" Sajenti Minja alijibu kinyonge,

"sasa utafanyaje" Mama Kayoza aliuliza,

"nitamkimbia kimbia hivyo hivyo mpaka achoke", Sajenti Minja alialiongea,

"Mimi naona bora uichukue na hiyo kesi hili uweze kuwadhibiti vizuri wahusika" Omary alichangia

"Hapana, mimi nitajitahidi niikwepe tu" Sajenti Minja aliongea,

"Ichukue hiyo kesi kwa maana huwezi jua mipango ya Mungu" Mama Kayoza aliongea,

"Tutajua uko mbele ya safari. jamani kuna kaugali kalichobaki?" Sajenti Minja aliuliza,

"ugali upo, ila mboga ndo imeisha, ngoja wajomba zako wakakununulie maziwa kwa mchungaji", Mama kayoza alimjibu Sajenti Minja huku akimpa kayoza hela ya maziwa,

"Kwani hatuwezi kununua mboga nyingine zaidi ya maziwa" Sajenti Minja aliuliza,

"Mbona tunaweza kununua hata maharage au nyama, tatizo tukiinjika mpaka viive si utakuwa umeshakufa na njaa yako?" Mama Kayoza aliongea,

"Kweli Dada, basi nyie wahini, maana njaa niliyonayo ni ya hatari...

******ITAENDELEA********

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI.

______________
ILIPOISHIA...
______________
"Kwani hatuwezi kununua mboga nyingine zaidi ya maziwa" Sajenti Minja aliuliza,

"Mbona tunaweza kununua hata maharage au nyama, tatizo tukiinjika mpaka viive si utakuwa umeshakufa na njaa yako?" Mama Kayoza aliongea,

"Kweli Dada, basi nyie wahini, maana njaa niliyonayo ni ya hatari...

______________
ENDELEA......
_______________
baada ya wakina kayoza kutoka, Sajenti Minja na dada yake waliendelea na maongezi yao.

"afadhali umekuja mwenzangu, maana mjomba ako kanichachamalia hapa", Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja

"kachachamaa na nini tena?"Sajenti Minja akauliza,

"eti anadai tuko kimya katika kufuatilia matatizo yake", Mama Kayoza akajibu,

"kuna askari niliongea nae jana, akaniambia kuna mtaalam wa jadi ana uwezo mkubwa wa kusaidia watu", Sajenti Minja alimwambia dada yake

,"kwa hiyo ulimwambia una ndugu yako ananyonya damu?", mama Kayoza aliuliza kwa mshtuko,

"kwani mi sina hakili mpaka nimwambie hivyo?, nilimdanganya natokewa na mauzauza kila nikitaka kulala", Sajenti Minja akamjibu dada yake,

"ataweza kweli kumtibia kayoza?", Mama kayoza akamtupia mdogo wake swali jingine,

"dada nawe kwa maswali!, tutajua uko uko kama ataweza au lah", Sajenti Minja alimjibu dada yake,

"lini mtaenda uko", mama Kayoza akauliza tena

"nafikiri kesho, kama nitapata nafasi", Sajenti Minja alijibu

"haya bwana, wacha nikakutayarishie chakula jikoni", mama kayoza aliongea huku akinyanyuka kwenye kochi,

"hayo ndo mambo sasa, kama kuna pilipili niwekee", Sajenti Minja alisema na kumfanya mama kayoza ahangue kicheko.

"Sasa hiyo pilipili utaiweka katika maziwa?" Mama Kayoza aliuliza huku akicheka,

"Nitaitafunia tu na ugali" Sajenti Minja alijibu,

"Ngoja nikutafutie kama ntaipata" Mama Kayoza aliongea huku akiingia jikoni.

"Sema siku hizi umekuwa mswahili kweli Dada yangu" Sajenti Minja aliongea huku akitabasamu,

"Kwanini unasema hivyo?" Mama Kayoza aliuliza huku akisimama,

"Naona nawe unakubali tu tumpeleke mwanao kwa waganga sio kama zamani ulivyoshikilia msimamo wako wa kanisani" Sajenti Minja alimwambia Dada yake,

"Ujue Mungu hana njia moja ya kukupa mafanikio, unatakiwa upitie njia nyingi lakini ukimuamini yeye tu na sio vitu vingine" Mama Kayoza alimwambia Sajenti Minja,

"Sawa mama mchungaji, inabidi na wewe ujenge kanisa lako sasa" Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,

"Ebu kwenda zako uko, kwanza ulivyosema mchungaji umenikumbusha awa wendawazimu waliofuata maziwa, mbona wamechelewa hivyo?" Mama Kayoza aliuliza,

"Wana mambo mengi wale vijana, usikute wanamnyatia yule binti wa mchungaji" Sajenti Minja aliongea kwa utani huku akicheka,

"Acha uwendawazimu wako, watoto wa mchungaji wana maadili wewe" Mama Kayoza aliongea,

"Sio wote, kama yule binti mcharuko niliekutana nae juzi ni bure kabisa, bora angeishi uswahilini tu" Sajenti Minja aliongea huku akicheka,

"Kwani ana kosa gani? Si alikuwa anaenda polisi kusema habari za ukweli" Mama Kayoza aliongea huku akitabasamu,

"We si ni mlokole? Nenda na wewe polisi kaseme hizo hizo habari kuwa mwanao muuaji" Sajenti Minja alimwambia Mama Kayoza,

"Mtoto anauma bwana, mtoto mwenyewe ndio huyo huyo mmoja kama roho" Mama Kayoza aliongea huku akicheka,

"Nenda jikoni bwana, maana story zimezidi mpaka unasahau kuwa mimi njaa inaniuma" Sajenti Minja alimwambia Dada yake,

"Hata baba, usije ukanifia bure kwa njaa" Mama Kayoza aliongea huku akielekea jikoni.

*********************

Baada ya mkuu wa polisi kurudi ndani, alimpgia simu askari mwingine na kumwambia amrudishe rumande Babu wa mochwari,

"jamani nitakaa huku mpaka lini, nina mke na watoto mimi",Babu wa mochwari aliongea huku machozi yakimtoka,

"usijali mzee wangu, upepelezi utakamilika hivi karibuni", Mkuu wa polisi alimjibu Babu wa mochwari kwa huruma.

"Mwanzo askari wako waliniambia nikiri kosa ili niachiwe, nikakiri kosa kuwa ni kweli mwili umeibwa, lakini hawajaniachia, naambulia kipigo tu mpaka viungo vinateguka" Babu wa monchwari alilalamika,

"Mzee ujue upelelezi sio kitu cha kukurupuka tu, inahitajika muda mrefu wa kuchunguza na kujiridhisha na jibu la kile kilichopelelezwa, na hapo sasa ndipo sisi tutaachana na wewe na kesi yako itakuwa mahakamani" Mkuu wa polisi alimuelewesha Babu wa monchwari,

"Mahakamani tena?, si nitafungwa jamani mie?" Babu wa monchwari aliuliza huku akilalamika,

"Sasa sisi hatutaki ufungwe, na ndio maana tunaendelea kukuhifadhi ili utusaidie kumpata huyo aliyeichukua hiyo maiti" Polisi alimwambia Babu wa monchwari,

"Sasa mbona sioni juhudi zozote ukizifanya kumtafuta huyo mtu na nilishawahi kumuona eneo hili huyo mtu mwenyewe" Babu wa monchwari aliongea na kumfanya Mkuu wa polisi ashtuke kidogo,

"Alikuwa anafanya nini na kwa nini hukuwaambia Askari?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akimshangaa,

"Kitu ninachokishangaa ni kwamba alipotea ghafla, inawezekana kabisa yule bwana si mtu wa kawaida, atakuwa mshirikina tu" Babu wa monchwari aliongea,

"Kumbe ukimuona kwa sura unamjua vizuri tu?" Mkuu wa polisi aliuliza,

"Vizuri sana tu, hata akiwa mbali namtambua" Babu wa monchwari aliuliza,

"Ulivyomuona alivaaje, au alivaa kiaskari?" Mkuu wa polisi alimdadisi Babu wa monchwari,

"Hajavaa kiaskari, na kwanza hawezi kuwa askari yule, ana ndevu kabisa" Babu wa monchwari alijibu,

"Basis usijali babu, tunaendelea kufuatilia" Mkuu wa Polisi aliongea,

Kisha yule askari aliepigiwa simu aliingia na kisha akamchukua Babu wa mochwari na kumrudisha rumande.

***********************

Wakina kayoza walipofika kwa Mchungaji Wingo, walimkuta Binti wa mchungaji anafagia fagia

"karibuni", Binti wa mchungaji aliwakaribisha alipowaona,

"asante, za hapa?", Omari alijibu alafu akamjulia hali,

"poa my husband, Kayoza mambo?", baada ya kujibu salamu ya Omari, binti wa mchungaji akamgeukia Kayoza,

"poa, kuna maziwa ya mtindi?" Kayoza akamjibu kwa mkato, kisha akasema kilichompeleka,

"yapo, mnataka kiasi gani?" Binti Mchungaji akauliza,

"nusu lita" Kayoza alijibu huku akimpatia pesa, Binti wa mchungaji akachua hela kisha akaingia ndani kuwapimia maziwa.

"kaka uko siriazi, hutaki hata kucheka nae", Omari alimwambia kayoza huku akijichekesha

"boya sana huyu demu", Kayoza aliongea akiwa na chuki za wazi kwa binti wa mchungaji.

Baada ya dakika tano binti wa mchungaji alitoka, akawapa maziwa

,"Omari baki, kuna kitu kizuri nataka kukwambia", Binti wa mchungaji alisema,

"nibaki?, kwani ndani uko na nani?", Omari alimuhoji Binti wa mchungaji,

"niko peke yangu, wote wameenda mjini, ila baba kaenda kanisani", ndivyo alivyojibu,

"Boy we tangulia, mimi ninakuja" Omary alimwambia Kayoza,

"Sasa nikifika peke yangu mama si ataniuliza?" Kayoza alihoji,

"Utajua namna ya kumdanganya, ila hata sitochelewa" Omary aliongea,

"Poa, jitahidi kuwahi bwana" Kayoza aliongea huku akianza kuondoka.

"Twende ndani basi" Binti Mchungaji alimwambia Omary huku akimvuta mkono,

"Huogopi?" Omary aliuliza huku akijatahidi kutosogea zaidi ya pale alipo,

"Twende ommy, utaniudhi ujue" Binti Mchungaji aliongea sauti ya kudeka na kumfanya Omary alegeze msimamo,

"Una hatari sana" Omary aliongea huku akipiga hatua kumfuata binti mchungaji

"Twende usiogope, awa hawarudi sasa hivi" Binti Mchungaji aliongea huku akifungua mlango wa chumbani kwake,

"Bora ungenipeleka sebuleni, huku ndio pabaya kabisa" Omary aliongea huku akiingia katika chumba cha Mchungaji,

"Kelele bwana, kaa hapo mimi nakuja sasa hivi" Binti Mchungaji aliongea huku akimkalisha Omary kitandani,

"Uwahi basi" Omary aliongea wakati Binti Mchungaji akitoka,

"Nakukuja sasa hivi, kuna kazi naenda kuimalizia chap chap" Binti Mchungaji aliongea na kisha akatoka nje baada ya kuurudishia mlango, Omary akabaki chumbani peke yake huku macho yake yakitalii katika kila kona ya chumba kile cha Binti Mchungaji.

Baada ya Binti mchungaji kumaliza kazi, akaenda kujisafi mwili, kisha akarudi chumbani kwake na kufunga mlango kwa ndani,

"we mtoto huogopi?, Omari alimuuliza huku akiwa na sura ya wasiwasi, Binti wa mchungaji badala ya kujibu, yeye akaitoa ile khanga aliyotokanayo kuoga na kubaki mtupu kama alivyozaliwa, Omari akili ilimruka na uoga wote ukamtoka, bila kutarajia akamvuta binti wa mchungaji kitandani, na kuamia katika ulimwengu mwingie.

Mchungaji Wingo aliporudi nyumbani kwake, akakuta mlango wa mbele uko wazi, video sebuleni inawaka, akamuita binti yake, lakini hakupata jibu, akaamua aende akamuangalie chumbani kwake, alipokaribia mlango wa chumba cha binti yake, alisikia mlio wa kitanda cha binti yake kikilalamika kwa fujo,

"mh..", mchungaji Wingo aliguna...

*******ITAENDELEA*******

*haya sasa Mchungaji anakuta utata katika chumba cha mwanaye, je nini kitatokea?

*Sajenti Minja amepata habari za kuwepo kwa mganga mwingine kiboko, je huyo mganga atamponesha Kayoza?

the Legend☆
 
Back
Top Bottom