Riwaya: Kijijini kwa Bibi

Riwaya: Kijijini kwa Bibi

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE.

______________
ILIPOISHIA...
______________

Walipofika katika sehemu ambapo kulikuwa
kumetulia na kulikuwa na kapori kidogo, ni umbali
mdogo kutoka nyumbani kwav mganga
aliyewaagiza maiti, walisimamishwa na gari
ya polisi wa doria waliokuwa wanaimarisha ulinzi
kile kipindi cha usiku.

"mnaenda wapi?" askari mmoja akawauliza,

"nyumbani" Sajenti Minja akajibu huku wasiwasi
mwingi ukiwa umemtawala,

"huku juzi tulipishana na watu nao tulipowauliza
wakasema hivyo hivyo, kesho yake tukasikia
majambazi yamepavamia na kuiba mali za watu,
na nyie msije mkawa ni miongoni mwa hao
waarifu" Askari yule akamwambia sajent Minja
huku akiwa anawatilia mashaka,

"sisi hatuwezi kuwa majambazi, afande" Sajenti
Minja akajitetea

"hatuwezi kuwaamini, hadi tuwakague" yule
askari aliongea huku akimulika upande wa ndani
wa gari kwa kutumia tochi,

"Sisi ni watu safi" Sajenti Minja aliongea huku
ndani ya nafsi yake akiomba Askari wasikague
buti ya gari,

"Na huku kuna mini?" Askari mwingine aliongea
huku akifungua buti ya gari na kuwafanya wakina
Sajenti Minja waishiwe nguvu....

____________
ENDELEA....
____________

...."ebu toa lock ya buti" Askari yule akamuamrisha Sajenti Minja baada ya kufungua buti bila mafanikio.

Sajenti Minja akaona akifanya uzembe kidogo,
anaweza kuvuliwa nguo bila kutegemea, kwa
maana kwa Sajenti kama yeye kukutwa na maiti
ndani ya gari ni aibu kubwa.

"unajua unaongea nani?" sajenti Minja akamuuliza yule askari wa doria kistaharabu,

"haijalishi, kukujua wewe nani nadhani hakutasitisha kukukagua. fungua buti bwana" yule askari akaongea kwa ukali.

"Ngoja nikuoneshe kitambulisho changu" Sajenti Minja akatoa kitambulisho chake, akamtupia yule
askari,

"alafu inaonekana una jeuri sana kijana?, unamtupia nani likitambulisho lako?" yule afande
akawa anaongea huku akiwa anamfuata Sajenti Minja akiwa na gadhabu, alipomfikia, yule askari
akamtandika sajenti Minja kibao cha nguvu.

"haya okota likitambulisho lako na unipe mikononi, sio unirushie, umeona mi limbwa
eeh!?", yule askari wa doria akahoji kwa ukali mpaka mate yakamtoka,

Sajenti Minja akaona asilete mabishano wakati wanachelewesha kazi kwa mganga, akakubali kuwa mjinga, akakiendea
kile kitambulisho, akakiokota kisha akampatia yule askari wa doria.

Yule askari akakipokea,
akashtuka baada ya kukiangalia kwa nje, maana kilikuwa cha kipolisi, alipokifungua kwa ndani, akakisoma ndani, kisha
akammulika Sajenti Minja na tochi usoni, ghafla
akampigia saluti, wale askari aliokuwa ameongozana
nao, kuona hivyo, nao wakampigia saluti Sajenti Minja.

"samahani sana mkuu, mi sikujua kabisa" yule
askari wa doria aliongea huku sura yake
ikionesha kama anataka kulia kutokana na hofu aliyokuwa nayo,

"usijali, ndio kazi inatakiwa kufanywa hivyo" Sajenti Minja ndivyo alivyomjibu, kisha
akamuuliza, "bado unataka nifungue buti?"

"ha...hapa...hapana mkuu" yule askari wa doria akajibu kwa sauti iliyojaa kitetemeshi.

"Kwa hivyo mnaweza kuturuhusu twende?" Sajenti Minja aliwauliza,

"Nenda tu mkuu, samahani sana kwa usumbufu" Askari alijibu huku akimrudishia Sajenti Minja kitambulisho chake.

Sajenti Minja akakipokea kitambulisho chake na wakaingia ndani ya gari, kisha wakaendelea na safari yao.

"wajomba pale bila kutumia akili tulikuwa tunaumbuka" Sajenti Minja alianzisha maongezi baada ya kuondoka eneo walilosimamishwa,

"Mimi ndio nilikuwa nimekata tamaa kabisa" Omari nae akachangia,

"Mimi akili niliyokuwa nayo ilikuwa ni kutoka nduki tu" Kayoza aliongea na kufanya wenzake wacheke,

"bila ya kitambulisho, sasa hivi sijui tungekuwa
wapi?" Sajenti Minja akasema huku akiwa anaipaki gari nje ya nyumba ya mganga.

Wakashuka, kisha wakaenda hadi mlangoni kwa
mganga, wakabisha hodi, wakafunguliwa na
msaidizi wa mganga,

"sisi tulijua hamuwezi kuja tena, maana giza limekuwa kubwa sana" Msaidizi wa Mganga
aliwaambia baada ya kuwagundua,

"tulipata matatizo kidogo njiani, ila yameisha" Sajenti Minja aliongea huku akiwa anaingia ndani na nyuma yake wakina Kayoza wakimfuata.

"Sasa itabidi ifanyike ingawa tumechelewa kidogo" Mganga aliongea baada ya kuwaona,

"Itakuwa vyema sana" Sajenti Minja aliongea,

"Sasa huyo kijana mwenye tatizo inabidi asogee hapa tumfanyie mambo kidogo" Mganga aliongea huku akitandika kitambaa cheusi chini. Kayoza akasogea na kuambiwa Amalie kile kitambaa cheusi na mganga akaanza kufanya matambiko.

Baada mganga kumaliza matambiko madogo pale
nyumbani, wale wasaidizi wa mganga, walikuwa
wanne, wawili wakambeba yule maiti na wawili
wengine wakabeba vifaa vya uganga, hapo
ilikuwa saa sita na dakika zake za kutosha,
mganga akawa anaongoza msafara.

"Hizi sehemu zinatisha ila mnabidi mzizoee" Mganga aliwaambia wakina Sajenti Minja wakati wakiwa njiani,

"Hizi sehemu za kutisha nimeshazizoea sana, labda vijana wangu hapa ndio wageni" Sajenti Minja alijibu,

"Kwa hivyo mambo haya ya kutembea kwa waganga ushayazoea sana?" Mganga alimuuliza Sajenti Minja,

"Hapana, kwa masuala ya kiganga mi ndio mara yangu ya kwanza" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa hata mazingira ya kutisha umeyazoeaje?" Mganga aliuliza,

"Kutokana na kazi zetu mzee wangu" Sajenti Minja alijibu,

"Kwani nyie mnafanya kazi gani?" Mganga aliwauliza,

"Hao vijana wangu wanasoma chuo, mimi ni muangaikaji tu wa sehemu mbalimbali katika kutafuta ridhiki" Sajenti Minja alijibu,

"Sasa kama huyu kijana mwenye matatizo yupo Chuo huko chuo anaishi vipi na chuo mzimu" Mganga alihoji,

"Matatizo matatizo tu na ndio maana tumemleta hapa" Sajenti Minja alijibu na ukimya ukatawala tena njiani.

Walitembea mda wa saa nzima hadi sehemu za makaburini.

" inabidi tuchague kaburi moja ambalo limetengenezwa vizuri na liwe la mwanamke" Mganga alitoa maelekezo na wale wasaidizi wake wakatawanyika kila mmoja na upande wake wakitafuta hilo kaburi zuri alilozikwa mwanamke.

"Naona hili hapa linafaa" Msaidizi mmoja wa mganga alipaza sauti na watu wote wakaelekea eneo alilopo.

Walipofika katika kaburi moja lililosakafikiwa
vizuri, Mganga alilidhika nalo baada ya kuona kila anachokihitaji kipo.

Mganga akawaamuru wasimame, kisha
akachukua kikapu cha uganga akatoa vifaa vyake
akavipanga kulizunguka lile kaburi,

"Were kijana njoo ulale hapa juu ya hili kaburi" Mganga alimwambia kayoza,

"Mi naogopa mzee" Kayoza aliongea huku akiwa na wasiwasi,

"We mpumbavu mini, ebu lala hapo kabla sijakuchapa makofi, we unafikiri utaponaje kama ukikahidi maneno ya mganga" Sajenti Minja aliongea kwa ukali, Kayoza akakubali kulala hivyo hivyo huku aakitetemeka.

Baada ya Kayoza kulala juu ya kaburi, mganga akammwagia madawa yake Kayoza kichwani, haikuchukua
hata dakika moja, Kayoza akapoteza fahamu na kulala kama maiti,

"Haya mchukueni huyo maiti na mumlaze pembeni ya huyo kijana" Mganga akawaamuru wasaidizi wake
wamchukue yule maiti na kumlaza pamoja na
kayoza, wasaidizi wakatekeleza agizo.

"Kazi ndiyo inaanza, sharti kubwa na la kuzingatia ni kwamba kazi itakapoanza haitatakiwa ionekane damu ya kitu chochote kile" Mganga aliongea,

"Hata ya mbu?" Sajenti Minja aliuliza kutokana na eneo like kuwa na mbu wengi,

"ndio, kama mbu atakung'ata hata usimuue, maana ukimuua ile damu yake inaweza kuwa tatizo kwetu" Mganga aliongea kwa msisitizo,

"Na ikionekana ni kipi kitachotokea?" Sajenti Minja aliuliza,

"Huu mzimu tunaoutoa hapa, nguvu zake zipo kwenye damu ya kila kiumbe, kwa hiyo damu itakapoonekana, mzimu atapata nguvu na kati yetu hapa hakuna atakayepona" Mganga alitoa Maelezo,

"Hilo litawezekana" Sajenti Minja alijibu,

"Na pia kama mtu ana kidonda ajitahidi akizibe kisionekane" Mganga alitilia mkazo,

"Basi kazi ifanyike tu, naona Maelezo yako yamejitosheleza" Sajenti Minja aliongea,

"Kwa hiyo hapa kazi inayofanyika ni kuutoa huu mzimu kutoka kwa kijana wenu na kuuingiza katika maiti alafu kazi itayofuata ni kuizika hivyo maiti pamoja na mzimu" Mganga alimaliza.

Mganga akaanza kazi yake, alimwaga madawa
eneo lote, kisha akaanza kuongea lugha
anayoijua yeye, alifanya kwa nusu saa, kisha
likatokea dubwana la ajabu kwenye mwili wa
Kayoza, kila mtu alipata uoga isipokuwa mganga tu.

Sasa like dubwana likawa kama linavutwa kutoka kutoka kwenye mwili wa Kayoza, ila likawa
halitaki,
hiyo hali ilienda kama saa nzima, mganga
akaanza kuona mafanikio, lile dubwana lilishatoa
mwili mzima ikawa bado miguu, na mwisho hadi miguu ilitoka na likaanza kudumbukia katika ile maiti.

Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu,
akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga
aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa

"tumekwisha...".

Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu waliolala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............

******ITAENDELEA*******

*Je mganga atafanikiwa kuutuliza mzimu uliokuwa na hasira ya kudhuriwa au mzimu ndio utawamaliza wote waliotaka kumdhuru?

the Legend☆
Jamani omary dah
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO.

______________
ILIPOISHIA...
______________
Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu.

akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa

"tumekwisha...".

Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu walioloala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............

___________
ENDELEA
___________

"Hapa sijui kama tutapona" Mganga alitamka maneno hayo, huku akiwa
kama anajitayarisha na pambano jingine.

Mzimu ulipiga kelele zilizowatisha watu wore pale, kisha ulirudi kwa kasi ndani ya mwili wa Kayoza, kisha Kayoza
akanyanyuka taratibu, alikuwa tayari
keshabadilika, alikuwa anaogepesha ukimtazama msoni, macho yalikuwa meupe yasiyo na mboni na meno ya mbele pembeni yalikuwa marefu kama ya mnyama simba.

Kayoza akawatazama wote, alafu akawa
anamfuata Omari, Omari kuona hivyo, mkojo
ukaanza kumtoka na hata kukimbia akawa anashindwa ila alibaki ametoa macho huku machozi yakimtoka ingalikuwa halii.

Kayoza alipomfikia Omary
akamuangalia kisha akaachane nae, sasa akawa
anafuata mganga ambaye muda wote alikuwa bado anafanya mambo yake ya kiganga kwa ajili ya kujaribu kuutuliza mzimu wa Kayoza.

Mganga baada ya kuona mzimu unamfuata, maamuzi aliyoyachukua ni kutoka tu
mbio, akasababisha na watu walikuwepo katika
hilo eneo nao watoke mbio
mganga hakufika hata mbali, Kayoza akamkamata,

"Wewe ni nani mpaka utake kunitoa katika nyumba yangu?" Mzimu ulimuuliza mganga huku ukiwa umemkaba katika shingo na kusababisha kucha zake ndefu zipenye kwenye shingo ya mganga,

"Mi...mii..nimeagi..zwa tu na ndugu za...ko" Mganga aliongea kwa tabu huku damu zikimchuruzika shingoni.

Ila pamoja na utetezi wake ule mzimu ulimbeba juu na kung'ata shingoni kisha aakaanza kumnyonya damu, alipomaliza akamtupa pembeni.

Kisha mzimu ukatoka mbio na kuwakuta wasaidizi wa mganga wakiwa wanakimbia na wale
wasaidizi wake pia wakanyonywa damu.

Kisha Kayoza akamfuata sajenti Minja, ambae yeye alikimbia ila mwisho akaamua asimame tu maana aliona hata kama akikimbia ni lazima tu akamatwe.

Mzimu akamkamata mkono Sajenti Minja alafu akawa anamvutia
kichakani sehemu ambayo kulikuwa na miti mingi, alipofika katika eneo lenye miti,

"Usipate kichwa kwa kuwa niliahidi kutoidhuru damu yenu, wewe ndiyo utasababisha nivunje ahadi yangu" Mzimu uliongea huku
Ukikata fimbo, na kisha ukaanza kumtandika Sajenti Minja, alimtandika
kisawa sawa, mpaka sajenti Minja akawa analia kama mtoto.

Mzimu uliporidhika na bakora alizozipata Sajenti Minja ukamuachia na Sajenti Minja akatoka mbio kama mwendawazimu na kuishika ile njia waliyokuja nayo ambayo ilikuwa inaelekea nyumbani kwa Mganga.

Mzimu ulipomuachia Kayoza, Kayoza akadondoka chini kama kifurushi na akapoteza fahamu.

Omary yeye baada ya kuachwa na mzimu wala hakukimbia, alikuwa anaangalia tu unyama unaofanywa na mzimu na hata wakati Kayoza anaanguka na kupoteza fahamu Omary aliona na akaamini tayari mzimu umemuachia rafiki yake, Maamuzi aliyoyachukua Omary ni kwenda kumpa msaada Kayoza, alipofika, akambeba Kayoza kisha akawa kwenda walipoacha gari lao ambapo ni nyumbani kwa Mganga.

Walifanikiwa kufika salama nyumbani kwa mganga na wakamkuta Sajenti Minja anaangaika kufungua mlango wa gari ili aingie,

"Vipi huyo tayari au bado?" Sajenti Minja alimuuliza Omary baada ya kumuona anakuja na Kayoza,

"Tayari amerudi katika hali yake" Omary alijibu huku akifungua mlango wa gari na kumuingiza Kayoza,

"Aisee hii siwezi kuisahau" Sajenti Minja aliongea huku akiwasha gari na kuiondoa kwa kasi.

"Hii ilikuwa hatari, ila wewe hajakudhuru" Omary aliongea huku akijua fika Sajenti Minja alipewa bakora zisizo kuwa na idadi,

"Usiseme hivyo wewe, dah yaani nimefanywa mtoto Leo, tena mtoto wa shule" Sajenti Minja aliongea kwa huzuni,

"Umefanywaje kwani mjomba?," Omary aliuliza huku akimcheka kimoyomoyo,

"Hata kuhadithia siwezi, ni kitendo cha aibu sana" Sajenti Minja aliongea,

"Si uniambie tu mjomba" Omary alikazania huku akiendelea kumcheka moyoni,

"Nitakuambia tukifika bwana" Sajenti Minja alijibu huku akiongeza mwendo wa gari.

*****************

Katika hospitali ya mkoa kulikuwa na kasheshe
kubwa sana, kuna watu waliambiwa ndugu yao
amefariki, ila walipoenda monchwari hawakuikuta
maiti ya ndugu yao, walipowafata madaktari
wakawathibitishia kuhusu kifo cha ndugu yao, na
hata babu wa monchwari alithibisha kupokea maiti
ya huyo ndugu yao, sasa cha ajabu maiti ikawa
haionekani
Polisi walipofika pale hospitali, wakamchukua
babu wa mochwari huku wakiwa na uhakika kuwa
huyu mzee anahusika kwa namna moja au nyingine
katika upotevu wa ile maiti.

Babu akachukuliwa hadi kituoni, walipomfikisha
wakaanza kumuhoji,

"Mzee kuwa mkweli, tuambie huo mwili umeupeleka wapi?" Askari alimuuliza Babu wa monchwari,

"Yaani hata mimi sielewi, ule mwili kweli niliupokea ila hata ulivyopotea mimi sijui" Babu alijibu kwa kujiamini,

"Kwani walinzi mpo wangapi pale monchwari" Askari aliuliza,

"Tupo wawili" Babu alijibu,

"Umesema wewe ndiye uliupokea mwili, he wakati mwili unapotea ilikuwa zamu ya nani kulinda?" Askari akaendelea kuuliza,

"Yaani huo mwili niliupokea Jana saa mbili usiku, na imeonekana haupo Leo saa kumi na mbili alfajiri" Babu alijibu,

"Ilikuwa zamu ya nani?" Askari aliuliza,

"Zamu yangu" Babu alijibu,

"Babu acha kutuchanganya, inaonesha wewe unajua kila kitu kuhusu kupotea kwa huo mwili" Askari aliongea huku akitabasamu ili asimtishe Babu,

"Unadhani nakutania mjukuu wangu?, kweli mimi sijui kitu, inawezekana mile chumba cha monchwari kina wachawi, si unajua wachawi wanazipenda sana maiti" Babu alijitetea na kumfanya askari acheke,

"Babu sema kweli usiogope, hata kama umeusika hatuwezi kukufunga, maana utakuwa kama shahidi, na si unajua shaidi hafungwi?" Askari alimlainisha Babu huku akiendelea kucheka,

"Kweli hamuwezi kunifunga?" Babu aliuliza huku akimuangalia Askari,

"Kama utamtaja muhusika hautofungwa mzee, ila ukishikiria msimamo wako wa kuficha ndio utakaokuingiza matatizoni" Askari alimwambia babu wa monchwari,

"Kusema ukweli aliyeuchukua ule mwili namjua kwa sura ila jina simjui" Babu aliamua kusema ukweli,

"Anakaa Wapi?" Askari aliuliza,

"Sijui ila nikimuona tu sura yake namjua hata kama nikitoka kulala" Babu aliendelea kukazania maneno yake,

"Kulikuwa na makubaliano yoyote kati yenu mpaka auchukue huo mwili?" Askari aliuliza,

"Hapana aisee" Babu alikataa,

"Sasa alichukuaje na wakati wewe mlinzi ulikuwepo?" Askari aliendelea kumbana kwa maswali,

"Alikuja na bunduki akanitishia, kisha akaingia ndani na kubeba maiti" Babu wa monchwari aliamua kusema uongo,

"Sasa kwa nini tokea mwanzo hukusema hivyo?" Askari aliuliza huku akimuangalia usoni,

"Nilikuwa siamini kama mtaniamini" Babu alijibu,

"Sawa babu, itabidi urudi ndani" Askari aliongea huku akisimama,

"Ndani tens kufanya mini?" Babu aliuliza kwa kuamaki,

"Utatoka tu babu, ila kwa sasa mtuhumiwa bado unahesabika ni wewe mpaka apatikane huyo mwingine unaedai alikuvamia na bunduki" Askari aliongea na kubonyeza kitufe kilichopo mlangoni na mlango ukafunguka wakaingia Askari wengine wawili,

"Mpelekeni selo" Askari aliwaamrisha wenzake ambayo walimshika babu huku na huku na kutoka nae nje.

wanamtoa katika chumba cha mahojiano, ili
wampeleke rumande.

****************

Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
Sajenti Minja akawarudisha wakina Kayoza kwa
mama Kayoza, kisha yeye akawa anaelekea
kituoni,
alipofika, akapaki gari lake kisha akawa anaenda
katika ofisi ya mkubwa wake, katika kolido ya
ofisi akapishana na askari watatu waliokuwa
wamemfunga pingu mzee mmoja ambae sura
yake haikuwa ngeni kwake yeye Sajenti Minja, ikabidi
ageuke amwangalie tena, na yule mzee nae
akageuka kumuangalia sajenti Minja, ndipo
sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo yule mzee monchwari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....

********ITAENDELEA*********

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA.

sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo yule mzee monchari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....
_____________
ENDELEA....
_____________

...yule babu wa mochwari akasimama, "vipi we mzee, songa mbele" askari mmoja akaongea kwa hasira.
"taratibu wanangu, nimemuona mtu kama aliekuja kununua ile maiti" yule babu akaongea kwa matumaini huku shingo yake akiitoa kwa Sajenti Minja na kuwageukia wale maaskari,

"yuko wapi?" askari mwenye hasira akauliza.
Yule babu akageukia ile sehemu aliyokuwepo sajenti Minja ili awaoneshe maaskari,

"kha!," yule babu akajikuta anashtuka kwa mshangao baada ya kutomuona tens Sajenti Minja,

"vipi babu?, tuoneshe haraka, unatuchelewesha" yule askari mwenye hasira akauliza huku amemtolea macho babu,
"alikuwepo pale" yule babu akasema huku akionesha lile eneo alilokuwepo Sajenti Minja.
"kwa hiyo hayupo?", yule askari mwenye hasira akahoji.
"alikuwepo pale", Babu akajitetea.
"hujanijibu bado, kwa hiyo hayupo" yule askari aliuliza tena huku akiwa na shauku ya kufanya kitu.
"ndio mwanangu" Babu akajibu kwa upole.
Bila kutegemea, babu alipigwa mtama mmoja mkali sana, akaangukia makalio.
"unatuchelewesha majumbani kwetu, hatujalala na wake zetu tokea juzi usiku" askari mwenye hasira aliongea huku akimnyanyua babu babu baada ya kumpiga mtama.

Sajenti Minja akacheka tu baada ya kushuhudia ule mtama aliopigwa babu kisha akaishia kujiuliza ni kwanini babu amekamatwa, akajiona mkosaji kwa kukimbia kwa maana yeye angeweza kuwa msaada wa babu, pia akaona alichokifanya kinaweza kubwa sahihi zaidi kwa kuwa huenda Babu atakuwa amekamatwa kutokana na kesi ile ya kuiba maiti, yaani inawezekana kabisa ndugu wa marehemu wamegundua kuwa wameibiwa, na mwisho akajisemea itabidi achunguze ni kitu kilichofanya mpaka yule babu awe katika mikono ya polisi.

"Vipi mbona una mawazo hivyo?" Askari mmoja aliyekuwa anatoka msalani alimuuliza Sajenti Minja aliyekuwa amezama katika bahari ya tafakuri,

"Ah, si unajua tena mawazo ni kawaida kwa binadamu" Sajenti Minja alijibu baada kushtuka kutoka katika lindi la mawazo,

"Wewe ni mgeni kituoni hapa? Maana sura yako sijawahi kuiona" Yule askari alimuuliza Sajenti Minja,
"Kabisa, inaelekea kila mtu anaefanya kazi hapa umemkariri?" Sajenti Minja aliuliza,
"Yaani wote, sisi ndio wakongwe wa hapa" Yule askari alijibu huku akitabasamu,
"Sawa bwana, mimi ndio nawasili muda huu kuja kuripoti kwa mara ya kwanza" Sajenti Minja aliongea huku nae akitabasamu,

"Bila shaka wewe ndiye Joel Minja?" Yule Askari aliuliza,
"Haswaa, umenijuaje?" Sajenti Minja aliuliza,
"Tuliambiwa Leo kuna ugeni wa askari mpelelezi kutoka Dodoma" Yule askari aliongea,
"Basi ndio huyo" Sajenti Minja aliongea,
"Umeshafika ofisini kwa mkuu?" Yule Askari aliuliza,
"Bado, yaani hapa ndo mahala pa kwanza kufika" sajenti Minja aliongea na wote wakacheka,
"Sasa ofisi ya mkuu unaijua?" Yule askari alimuuliza,
"Nitaijulia Wapi mimi?" Sajenti Minja alijibu,
"Sasa ungefikaje" Yule askari aliuliza,
"Ningefika tu, ila kwa kuwa nimekutana na wewe, mambo yatakuwa sawa" Sajenti Minja aliongea,
"Twende nikupeleke" Yule askari akaongea huku akitangulia mbele

Wakatoka katika eneo la chooni, akawa anaelekea katika ofisi ya mkubwa wake, walipofika yule askari aliyempeleka hakutaka kuingia, aliishia mlangoni na kuondoka zake na kumuacha Sajenti Minja mlangoni.

Sajenti Minja akapiga hodi kisha akaingia, aliporudishia mlango, akampa heshima yake mkuu wa polisi,
"kaa hapo sajenti" Mkuu wa polisi wa shinyanga alimuelekeza sajenti Minja sehemu ya kukaa.
sajenti Minja akasogeza kiti, kisha akakaa.
"habari yako Minja" Mkuu wa polisi akamsalimia.
"nzuri tu, shikamoo mkuu" sajenti Minja akajibu.
"Marhaba, Leo ndio siku ya kwanza kuwasili kituoni hapa" Mkuu wake alimuuliza huku akiwa jibu analo kabisa,
"Naam mkuu" Sajenti Minja alijibu kikakamavu,
"Vizuri sana, na kilichokuleta huku nadhani unakijua" Mkuu wake aliuliza tena,
"Ndio mkuu" Sajenti Minja alijibu,
"Tukupatie Askari wa huku ili msaidiane au wewe una pendekezo Gani?" Mkuu wake alimuuliza,
"Naimani peke yangu nina uwezo wa kufanikisha" Sajenti Minja alijibu,
"Kwanini hutaki msaada?" Mkuu wake aliendelea kumbana,
"Kwa sababu hata niliyofikia katika upelelezi wa hii kesi ni hatua nzuri, sasa ukinipa mtu wa kusaidiana nae itakuwa kama tunaanza upya kwa kuwa atakuja na mipango, mbinu na mawazo tofauti kuhusu hii hii kesi" Sajenti Minja alijibu,,

"Lakini kumbuka umoja ni nguvu" Mkuu wake aliongea huku akitabasamu,

" hilo nalijua mkuu, nitapohitaji msaada nitakwambia" Sajenti Minja aliongea,

"Kesi unayoifuatilia umeishia nayo wapi?" Mkuu wake aliuliza,

"Kwa kweli hata niliyopiga ni ndogo sana, bado nahitaji mwanga zaidi ili hata nijue wa kumtia hatiani" Sajenti Minja aliongea,

"Sawa, basi hapa nna habari ambazo zinaweza kukupa mwanga kidogo" Mkuu wake aliongea na kumfanya Sajenti Minja atege masikio vyema,

"Habari zipi hizo mkuu?" Sajenti Minja aliuliza,

"leo asubuhi wasamalia wema walitoa taharifa za kuwepo watu wanne ambayo walikuwa wana alama ya kung'atwa shingoni na kitu kama mnyama mwenye meno makali, tulipoenda tuliweza kukuta watatu waliokuwa wamenyonywa damu makaburini, ila habari nzuri mmoja wapo amekutwa yuko hai, lakini hali yake sio nzuri, ni wa leo au wakesho muda wowote anaweza kufa", Mkuu wa Polisi aliongea huku akiangalia baadhi ya makabrasha yaliyopo mezani kwake,
Sajenti Minja alivyosikia habari ya watu kukutwa wakiwa wamekufa kwa kunyonywa damu eneo la makaburini, moja kwa moja akajua kuwa ni yule mganga na wasaidizi wake, ila habari ya mmoja kuwa hai ndio hakuipenda,
"ndio, nakusikia mkuu" sajenti Minja akajibu baada ya ukimya wa muda mfupi,
"Sasa kwa fikra zangu za haraka haraka haya mauaji nayafananisha na yanayofanywa na mtu unaemtafuta kwa maana hata wale watu waliokutwa wamekufa katika geti la mchungaji walikuwa hivyo hivyo na hizo alama shingoni" Mkuu wake alitoa maelezo,
"Nadhani kwa kuwa huyu mmoja yupo hai basi anaweza kutusaidia tukapata mwanga kidogo" Sajenti Minja aliongea huku moyoni akiwaza hata huyo mtu afe,

"Sasa hivi yupo sehemu ya wagonjwa mahututi amepumzishwa, jioni tutaenda kuongea nae" Mkuu wake aliongea,

"Litakuwa jambo jema sana" Sajenti Minja aliongea,

"sasa ni hivi tutatoka mimi na wewe hadi katika ofisi za akari wengine ili nikutambulishe, alafu jioni ndio tutaenda hadi hospitali ili tuchukuwe maelezo ya huyo aliebakia, maana anaweza kutupa pa kuelekea" mkuu wa polisi alimalizia kuongea huku akisimama,
"sawa mkuu" sajenti Minja akajibu.

Walitoka nje ya ofisi ya mkuu na kisha muda huo sajenti Minja akaanza kutembezwa katika ofisi za askari wa ngazi mbalimbali ili atambulishwe kwa wenzake hao, na kisha pia alizungushwa katika mazingira yote ya eneo like la Polish kwa ajili ya kupata kuyaona ili hata akitoka nje ajue duka linapatikana wapi? vyoo vinapatikana wapi na mambo mengine yanayolizunguka eneo lile.
Baada ya Mkuu wake kuridhika aliamua na kumpeleka katika ofisi ambayo Sajenti Minja ataitumia muda wote ambao atakuwepo pale na kisha wakaagana huku wakikumbushiana kuwa jioni ni lazima waende hospitali kumuona huyo mtu aliyebakia ya wenzie kunyonywa damu, Sajenti Minja hakupenda kabisa hyo safari ila hakuwa na la kufanya, ilibidi atimize matakwa ya kazi yake.

************************

Jioni ilifika haraka sana kwa upande wa Sajenti Minja, alitamani hata isifike kabisa.
Mkubwa wake alimpitia na wakatoka eneo la kituoni.
Baada ya kutoka kituo cha polisi, sajenti Minja na mkuu wake wakafunga safari hadi hospitali, njia nzima sajenti Minja alikuwa anatetemeka, alijua fika kuwa anaenda kuumbuka mbele ya mkuu wake,
"vipi Minja, mbona unatetemeka sana?" mkuu wa polisi akauliza.
"leo nimeamka na homa, kwa hiyo sijisikii vema kabisa" sajenti Minja alidanganya.
"itakuwa malaria, tukifika itabidi upime kabisa" mkuu wa polisi alimshauri Sajenti Minja.

Gari ilipofika, sajenti Minja na Mkuu wa polisi wakatelemka kisha wakawa wanaelekea sehemu ilipo wodi za wagonjwa mahututi, walitumia dakika mbili mpaka kufika katika chumba ambacho alilazwa yule msaidizi wa Mganga ambae alikuwa amenusurika na kifo, ila chumba kilikuwa kitupu,

"Eh, mbona hayupo, ameshakufa nini?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akitoa macho kuangaza bila mafanikio. Kwa upande wa Sajenti Minja hiyo habari ilikuwa nzuri, alijikuta anatabasamu waziwazi mbele ya Mkuu wake,

"Mbona unacheka, unafurahia kumpoteza shahidi?" Mkuu wake alimuuliza kwa mshangao,
"Hapana mkuu, nacheka unavyopeleka imani yako katika kifo wakati hata hujaenda kuuliza kwanza kwa madaktari" Sajenti Minja alijitetea kwa njia ya uongo,

"Kweli bwana, ebu twende tukaulize" Mkuu wake aliongea huku akielekea upande zilizopo ofisi za madaktari na huku Sajenti Minja akiendelea kuomba wakifika waambiwe yule bwana amekufa.
Baada ya sekunde kadhaa walitokea sehemu zilipo ofisi za madaktari, ila kwa bahati nzuri hata kabla hawajaingia ndani, walikutana na Daktari ambae ndiye anayesimamia matibabu ya msaidizi wa Mganga,

"Ooohoo kamanda umeshawasili?" Daktari aliongea huku akimpa mkono Mkuu wa polisi,

"Vipi kuna wema kweli? mbona mgonjwa wetu hayupo kule katika wodi aliyokuwepo asubuhi?" Mkuu aliuliza huku akionesha wasiwasi,

"Wema upo, tens mkubwa sana" Daktari alijibu huku akicheka,

"Hapo kidogo umenipa nguvu, haya niambie huo wema" Mkuu aliongea huku akiwa bado yupo makini kumsikiliza Daktari,

"Mgonjwa wako amepata nafuu na hata kuongea anaongea" Daktari alitoa habari zilizokuwa nzuri kwa Mkuu wa polisi ila hizo hizo habari zilikuwa mbaya sana kwa Sajenti Minja,

"Mmempeleka wapi sasa?" Mkuu wa Polisi aliuliza,

" yuko katika wodu ileee" Daktari aliongea huku akiwaelekeza kwa kidole katika wodi ambayo amehamishiwa msaidizi wa Mganga.

Sajeni Minja na Mkuu wa Polisi baada ya kumshukuru Daktari wakawa wanaelekea kwenye wodi aliyokuwamo yule msaidizi wa mganga huku Sajenti Minja mapigo yake ya moyo yakiongezeka kasi.

wakaingia ndani ya wodi, kisha wakawa wanaelekea kwenye kitanda cha yule msaidizi wa mganga, hapo Sajenti Minja moyo ulikuwa unamkimbia ajabu, akatamani hata sura yake ibadilike au akatamani hata yule msaidizi wa Mganga awe amepoteza kumbukumbu zake, lakini haikuwa hivyo.

Walipofika katika kitanda cha yule msaidizi wa mganga, wakakuta kalala huku kawapa mgongo, yule mkuu wa polisi akamshika bega kwa lengo la kumuasha, yule msaidizi wa Mganga akageuza sura na macho yake yakagongana na macho ya Sajenti Minja........

******ITAENDELEA******

*je Msaidizi wa Mganga atalopoka na kumtaja sajenti Minja kama ni mtu mmoja wapo kati ya wale waliomsababishia matatizo?

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.

MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO.

______________
ILIPOISHIA...
______________
Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu.

akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa

"tumekwisha...".

Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu walioloala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............

___________
ENDELEA
___________

"Hapa sijui kama tutapona" Mganga alitamka maneno hayo, huku akiwa
kama anajitayarisha na pambano jingine.

Mzimu ulipiga kelele zilizowatisha watu wore pale, kisha ulirudi kwa kasi ndani ya mwili wa Kayoza, kisha Kayoza
akanyanyuka taratibu, alikuwa tayari
keshabadilika, alikuwa anaogepesha ukimtazama msoni, macho yalikuwa meupe yasiyo na mboni na meno ya mbele pembeni yalikuwa marefu kama ya mnyama simba.

Kayoza akawatazama wote, alafu akawa
anamfuata Omari, Omari kuona hivyo, mkojo
ukaanza kumtoka na hata kukimbia akawa anashindwa ila alibaki ametoa macho huku machozi yakimtoka ingalikuwa halii.

Kayoza alipomfikia Omary
akamuangalia kisha akaachane nae, sasa akawa
anafuata mganga ambaye muda wote alikuwa bado anafanya mambo yake ya kiganga kwa ajili ya kujaribu kuutuliza mzimu wa Kayoza.

Mganga baada ya kuona mzimu unamfuata, maamuzi aliyoyachukua ni kutoka tu
mbio, akasababisha na watu walikuwepo katika
hilo eneo nao watoke mbio
mganga hakufika hata mbali, Kayoza akamkamata,

"Wewe ni nani mpaka utake kunitoa katika nyumba yangu?" Mzimu ulimuuliza mganga huku ukiwa umemkaba katika shingo na kusababisha kucha zake ndefu zipenye kwenye shingo ya mganga,

"Mi...mii..nimeagi..zwa tu na ndugu za...ko" Mganga aliongea kwa tabu huku damu zikimchuruzika shingoni.

Ila pamoja na utetezi wake ule mzimu ulimbeba juu na kung'ata shingoni kisha aakaanza kumnyonya damu, alipomaliza akamtupa pembeni.

Kisha mzimu ukatoka mbio na kuwakuta wasaidizi wa mganga wakiwa wanakimbia na wale
wasaidizi wake pia wakanyonywa damu.

Kisha Kayoza akamfuata sajenti Minja, ambae yeye alikimbia ila mwisho akaamua asimame tu maana aliona hata kama akikimbia ni lazima tu akamatwe.

Mzimu akamkamata mkono Sajenti Minja alafu akawa anamvutia
kichakani sehemu ambayo kulikuwa na miti mingi, alipofika katika eneo lenye miti,

"Usipate kichwa kwa kuwa niliahidi kutoidhuru damu yenu, wewe ndiyo utasababisha nivunje ahadi yangu" Mzimu uliongea huku
Ukikata fimbo, na kisha ukaanza kumtandika Sajenti Minja, alimtandika
kisawa sawa, mpaka sajenti Minja akawa analia kama mtoto.

Mzimu uliporidhika na bakora alizozipata Sajenti Minja ukamuachia na Sajenti Minja akatoka mbio kama mwendawazimu na kuishika ile njia waliyokuja nayo ambayo ilikuwa inaelekea nyumbani kwa Mganga.

Mzimu ulipomuachia Kayoza, Kayoza akadondoka chini kama kifurushi na akapoteza fahamu.

Omary yeye baada ya kuachwa na mzimu wala hakukimbia, alikuwa anaangalia tu unyama unaofanywa na mzimu na hata wakati Kayoza anaanguka na kupoteza fahamu Omary aliona na akaamini tayari mzimu umemuachia rafiki yake, Maamuzi aliyoyachukua Omary ni kwenda kumpa msaada Kayoza, alipofika, akambeba Kayoza kisha akawa kwenda walipoacha gari lao ambapo ni nyumbani kwa Mganga.

Walifanikiwa kufika salama nyumbani kwa mganga na wakamkuta Sajenti Minja anaangaika kufungua mlango wa gari ili aingie,

"Vipi huyo tayari au bado?" Sajenti Minja alimuuliza Omary baada ya kumuona anakuja na Kayoza,

"Tayari amerudi katika hali yake" Omary alijibu huku akifungua mlango wa gari na kumuingiza Kayoza,

"Aisee hii siwezi kuisahau" Sajenti Minja aliongea huku akiwasha gari na kuiondoa kwa kasi.

"Hii ilikuwa hatari, ila wewe hajakudhuru" Omary aliongea huku akijua fika Sajenti Minja alipewa bakora zisizo kuwa na idadi,

"Usiseme hivyo wewe, dah yaani nimefanywa mtoto Leo, tena mtoto wa shule" Sajenti Minja aliongea kwa huzuni,

"Umefanywaje kwani mjomba?," Omary aliuliza huku akimcheka kimoyomoyo,

"Hata kuhadithia siwezi, ni kitendo cha aibu sana" Sajenti Minja aliongea,

"Si uniambie tu mjomba" Omary alikazania huku akiendelea kumcheka moyoni,

"Nitakuambia tukifika bwana" Sajenti Minja alijibu huku akiongeza mwendo wa gari.

*****************

Katika hospitali ya mkoa kulikuwa na kasheshe
kubwa sana, kuna watu waliambiwa ndugu yao
amefariki, ila walipoenda monchwari hawakuikuta
maiti ya ndugu yao, walipowafata madaktari
wakawathibitishia kuhusu kifo cha ndugu yao, na
hata babu wa monchwari alithibisha kupokea maiti
ya huyo ndugu yao, sasa cha ajabu maiti ikawa
haionekani
Polisi walipofika pale hospitali, wakamchukua
babu wa mochwari huku wakiwa na uhakika kuwa
huyu mzee anahusika kwa namna moja au nyingine
katika upotevu wa ile maiti.

Babu akachukuliwa hadi kituoni, walipomfikisha
wakaanza kumuhoji,

"Mzee kuwa mkweli, tuambie huo mwili umeupeleka wapi?" Askari alimuuliza Babu wa monchwari,

"Yaani hata mimi sielewi, ule mwili kweli niliupokea ila hata ulivyopotea mimi sijui" Babu alijibu kwa kujiamini,

"Kwani walinzi mpo wangapi pale monchwari" Askari aliuliza,

"Tupo wawili" Babu alijibu,

"Umesema wewe ndiye uliupokea mwili, he wakati mwili unapotea ilikuwa zamu ya nani kulinda?" Askari akaendelea kuuliza,

"Yaani huo mwili niliupokea Jana saa mbili usiku, na imeonekana haupo Leo saa kumi na mbili alfajiri" Babu alijibu,

"Ilikuwa zamu ya nani?" Askari aliuliza,

"Zamu yangu" Babu alijibu,

"Babu acha kutuchanganya, inaonesha wewe unajua kila kitu kuhusu kupotea kwa huo mwili" Askari aliongea huku akitabasamu ili asimtishe Babu,

"Unadhani nakutania mjukuu wangu?, kweli mimi sijui kitu, inawezekana mile chumba cha monchwari kina wachawi, si unajua wachawi wanazipenda sana maiti" Babu alijitetea na kumfanya askari acheke,

"Babu sema kweli usiogope, hata kama umeusika hatuwezi kukufunga, maana utakuwa kama shahidi, na si unajua shaidi hafungwi?" Askari alimlainisha Babu huku akiendelea kucheka,

"Kweli hamuwezi kunifunga?" Babu aliuliza huku akimuangalia Askari,

"Kama utamtaja muhusika hautofungwa mzee, ila ukishikiria msimamo wako wa kuficha ndio utakaokuingiza matatizoni" Askari alimwambia babu wa monchwari,

"Kusema ukweli aliyeuchukua ule mwili namjua kwa sura ila jina simjui" Babu aliamua kusema ukweli,

"Anakaa Wapi?" Askari aliuliza,

"Sijui ila nikimuona tu sura yake namjua hata kama nikitoka kulala" Babu aliendelea kukazania maneno yake,

"Kulikuwa na makubaliano yoyote kati yenu mpaka auchukue huo mwili?" Askari aliuliza,

"Hapana aisee" Babu alikataa,

"Sasa alichukuaje na wakati wewe mlinzi ulikuwepo?" Askari aliendelea kumbana kwa maswali,

"Alikuja na bunduki akanitishia, kisha akaingia ndani na kubeba maiti" Babu wa monchwari aliamua kusema uongo,

"Sasa kwa nini tokea mwanzo hukusema hivyo?" Askari aliuliza huku akimuangalia usoni,

"Nilikuwa siamini kama mtaniamini" Babu alijibu,

"Sawa babu, itabidi urudi ndani" Askari aliongea huku akisimama,

"Ndani tens kufanya mini?" Babu aliuliza kwa kuamaki,

"Utatoka tu babu, ila kwa sasa mtuhumiwa bado unahesabika ni wewe mpaka apatikane huyo mwingine unaedai alikuvamia na bunduki" Askari aliongea na kubonyeza kitufe kilichopo mlangoni na mlango ukafunguka wakaingia Askari wengine wawili,

"Mpelekeni selo" Askari aliwaamrisha wenzake ambayo walimshika babu huku na huku na kutoka nae nje.

wanamtoa katika chumba cha mahojiano, ili
wampeleke rumande.

****************

Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
Sajenti Minja akawarudisha wakina Kayoza kwa
mama Kayoza, kisha yeye akawa anaelekea
kituoni,
alipofika, akapaki gari lake kisha akawa anaenda
katika ofisi ya mkubwa wake, katika kolido ya
ofisi akapishana na askari watatu waliokuwa
wamemfunga pingu mzee mmoja ambae sura
yake haikuwa ngeni kwake yeye Sajenti Minja, ikabidi
ageuke amwangalie tena, na yule mzee nae
akageuka kumuangalia sajenti Minja, ndipo
sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo yule mzee monchwari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....

********ITAENDELEA*********

the Legend☆
Nimecheka sana sajent minja na mzimu
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA.
______________
ILIPOISHIA...
______________
Walipofika katika kitanda cha yule msaidizi wa mganga, wakakuta kalala huku kawapa mgongo, yule mkuu wa polisi akamshika bega kwa lengo la kumuasha, yule msaidizi wa Mganga akageuza sura na macho yake yakagongana na macho ya Sajenti Minja........

_____________
ENDELEA.....
______________

.. "umekuja kuniona mheshimiwa?," yule msaidizi aliongea kwa tabasamu huku akimuangalia sajenti Minja.
"ndi...ndio, unaendeleaje?" sajenti Minja akamuuliza huku akitetemeka, kiasi kwamba mkuu wa polisi akaliona hilo.
"nashukuru mungu, vipi wewe?" yule msaidizi wa mganga akamtupia swali jingine.
"mi sijisikii vizuri kabisa" sajenti Minja akajibu.
"Minja ebu twende ukapime malaria, ukimaliza utakuja kuongea nae zaidi" mkuu wa polisi akasema.
Sajenti Minja akashusha pumzi ya kushukuru kwa maana aliona amepona.
"nakuja ili tuongee zaidi" sajenti Minja akamwambia yule msaidizi wa mganga huku akiwa anatoka na mkuu wa polisi.
"inaelekea mnafahamiana?" mkuu wa polisi akamtupia swali sajenti Minja wakiwa wanaelekea katika mabenchi ya kusubiria vipimo.
"hapana, hatakuwa kanifananisha tu, au inawezekana kachanganyikiwa kutokana na kukoswa koswa kufa, yaani nimekuja Jana tu alafu nijuane na watu wa huku?" sajenti Minja akajibu kwa kumdanganya mkuu wa Polisi,
"Ila nadhani endelea kujifanya hivyo hivyo kama unamjua ili umuweke karibu maana mkiwa marafiki anaweza akakueleza mambo mengi zaidi" Mkuu wa polisi alimshauri Sajenti Minja,

"Hilo nadhani ni jambo zuri na inaweza kuwa mbinu safi" Sajenti Minja alijibu,
"Au hii kesi nimpe mtu mwingine ili wewe uifuatilie tu iliyokuleta" Mkuu wa polisi alimuuliza Sajenti Minja,

"Mi nadhani zinaufanano na kesi iliyonileta, kwa hiyo ni vyema tu niendelee nayo" Sajenti Minja alijibu,

"ok, we chukua vipimo hapa, acha mi nirudi ofisini, ukishamuhoji tu, uje unipe taharifa" mkuu wa polisi akatoa maagizo.

"Kwanini tusimpe muda kidogo wa mapumziko, tumuhoji hata kesho ili akili yake itulie kidogo" Sajenti Minja alitoa ushauri,
"Sawa, ila inabidi haya mambo yaende haraka haraka na yafanikiwe ili ionekane tunafanya kazi kwa bidii" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja,
"Kuhusu hilo wala usijali, mambo yataenda sawa tu" Sajenti Minja alijibu,
"Sawa basi, sasa wewe kachukue vipimo tu tutakutana kesho tena, maana giza linaanza kuingia" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja,
"sawa mkuu" sajenti Minja akajibu huku akijifanya anaelekea sehemu zilipo mahabara za hospitali.
"Huu ushakuwa msala, sasa huyu msaidizi wa Mganga ataniletea balaa kubwa sana uko mbele" Sajenti Minja aliongea huku akiwa bado anatembea.

***********************

Wakina Kayoza waliporudi kwa mama yao, walimsimulia yote yaliyotokea, mama kayoza alisikitika sana,
"mchungaji kashindwa, kwa mganga ndio hivyo tena bahati mbaya, mi hata sijui nifanyaje?" Kayoza aliongea kwa kulalamika.

"Mchungaji hajashindwa, vuta subira tu utapona" Mama Kayoza aliongea,

"Mama sio kwa matukio haya, maana hii imeshakuwa kesi nyingine" Kayoza aliongea,

"Mjomba yenu nae hajafanywa kitu na mzimu huko makaburini?" Mama Kayoza aliuliza na kufanya Omari aangushe kicheko baada ya kuzikumbuka zile bakora alizochapwa Sajenti Minja,
"Sasa mbona mimi nauliza wewe unacheka?" Mama Kayoza aliuliza huku akiwa amekasirika,
"Mimi sikuona ila Omari alinihadithia" Kayoza nae aliongea huku akicheka,
"Mbona mnanicheka? omary amekuhadithia nini" Mama Kayoza aliuliza huku akiwa anawaangalia kwa zamu,
"Mjomba nasikia amekula bakora za kutosha, mpaka kukaa anakaa kwa shida" Kayoza alimwambia mama yake huku akicheka,
"Sasa ndio kinachowachekesha?" Mama Kayoza aliwauliza,
"Sio tukio zuri, ila inachekesha mama, mtu mkubwa kama mjomba kutandikwa kama mtoto" Kayoza aliongea na kumfanya mama yake scheme chini chini,
"Ebu acheni upumbavu" Mama Kayoza aliongea huku akicheka,

Mara wakasikia mlango unagongwa, Mama Kayoza akaenda kuufungua
"karibu mchungaji" mama kayoza akasema huku akiacha nafasi alie nje apite.
"asante mpendwa" mchungaji alijibu huku akiingia ndani.
"vipi mgonjwa, unaendeleaje?" mchungaji akaongea huku anamtazama kayoza.
"namshukuru Mungu" kayoza akajibu.
"lazima umshukuru Mungu, kwani ye ndo muweza ya yote" mchungaji aliongea huku akikaa kwenye kochi.
"Za nyumbani?" Mama Kayoza alimuuliza Mchungaji Wingo,
"Uko ni wazima, bwana yupo pamoja nasi. Sijui nyinyi hapa?" Mchungaji Wingo alijibu na kuuliza,
"Sisi nasi ni wazima, karibu" Mama Kayoza aliongea,

"kilichonileta hapa ni kitu kimoja tu, leo usiku kutakuwa na maombi, mnakaribishwa wote mje" Mchungaji Wingo akasema kilichompeleka.
"haya mchungaji, tunashukuru kwa kutupa taharifa" mama Kayoza akajibu.
"Ndio kazi yangu" Mchungaji Wingo alijibu,
"Itakuwa usiku wa saa ngapi" Mama Kayoza aliuliza,
"Kuanzia saa mbili" Mchungaji Wingo alijibu,
Kisha mchungaji akaaga, ila alitaka asindikizwe na Kayoza.
Kayoza akaongozana na mchungaji hadi nyumbani kwake,
Pale kwa mchungaji kuna msichana ambae ni mtoto wa kwanza wa mchungaji, tokea siku ya kwanza alipomuona Kayoza, alijenga upendo juu yake,
Mchungaji alipofika akaingia chumbani kuchukua biblia, akamuacha kayoza kakaa peke yake,
mara yule binti wa mchungaji akaja, alipomuona kayoza akatabasamu,
"amani ya bwana iwe nawe" kayoza akamsalimia yule binti.
"sema mambo bwana, mi sio mlokole" yule binti akajibu kwa mbwembwe.
Kayoza akatabasamu, "mambo" kayoza akasema.
"safi, mzima?" yule binti nae akauliza uku akikaa jirani na kayoza.
"mi mzima" kayoza akajibu,
"Kayoza mimi na wewe tunajuana ingawa sio sana, si ndio" Binti mchungaji alimuuliza Kayoza,

" ndio" Kayoza alijibu.

"Basi kuna kitu kinaitwa hisia, sidhani kama zunazuilika" Binti Mchungaji aliongea na kumfanya Kayoza awe makini kidogo kumsikiliza,

"Unataka kusema nin?i" Kayoza aliuliza,

"Sitaki kupoteza muda, ninachotaka kusema ni kwamba Kayoza nakupenda" Binti akajivika ujasiri, kisha akamueleza Kayoza jinsi anavyojisikia juu yake,

"Sawa, nashukuru" Kayoza aliongea huku akimuomba Mungu amuepushe na huo mtihani,

"Ukisema unashukuru unamaanisha nini?" Binti Mchungaji aliuliza,
"Nimekuelewa" Kayoza alijibu,
"Naomba unijibu ili nijue hisia zako kwangu" Binti mchungaji aliongea,
"Usijali, kesho tutaongea vizuri" Kayoza alijibu huku akitabasamu,

"nibusu basi ili nishinde vizuri mwenzio" mtoto wa mchungaji akaongea kwa mahaba.
"kesho rafiki yangu, hivi huogopi kusema hayo maneno katika nyumba takatifu kama hii?" kayoza akamjibu kwa busara,
"si unibusu jamani wewe." yule binti akakomalia kwa sauti ya juu kidogo.
"unamwambia nani akubusu?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akiwa anaingia Sebuleni.....

*****ITAENDELEA*****

the Legend☆
 
Back
Top Bottom