sinyora
JF-Expert Member
- Nov 21, 2016
- 970
- 1,638
yan bora angebaki nyumban na mama kayonza aiseeeOmary nae bingwa wa kuchomesha...
Aliwachomesha wenzake kwa polisi, makaburini kachomesha tena..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
yan bora angebaki nyumban na mama kayonza aiseeeOmary nae bingwa wa kuchomesha...
Aliwachomesha wenzake kwa polisi, makaburini kachomesha tena..
Asante sana dear na pole kwa majukumuWakuu nimeweka episodes nyingi kidogo sababu sitakua kabisa hewani kwa siku mbili hizi mpaka Ijumaa.
So kwa wale wanaoifuatilia riwaya hii tukutane Ijumaa, na episode nyingine ya Mkono wa Chuma itatoka pia siku hiyo.
the Legend☆
Jamani omary dahRIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE.
______________
ILIPOISHIA...
______________
Walipofika katika sehemu ambapo kulikuwa
kumetulia na kulikuwa na kapori kidogo, ni umbali
mdogo kutoka nyumbani kwav mganga
aliyewaagiza maiti, walisimamishwa na gari
ya polisi wa doria waliokuwa wanaimarisha ulinzi
kile kipindi cha usiku.
"mnaenda wapi?" askari mmoja akawauliza,
"nyumbani" Sajenti Minja akajibu huku wasiwasi
mwingi ukiwa umemtawala,
"huku juzi tulipishana na watu nao tulipowauliza
wakasema hivyo hivyo, kesho yake tukasikia
majambazi yamepavamia na kuiba mali za watu,
na nyie msije mkawa ni miongoni mwa hao
waarifu" Askari yule akamwambia sajent Minja
huku akiwa anawatilia mashaka,
"sisi hatuwezi kuwa majambazi, afande" Sajenti
Minja akajitetea
"hatuwezi kuwaamini, hadi tuwakague" yule
askari aliongea huku akimulika upande wa ndani
wa gari kwa kutumia tochi,
"Sisi ni watu safi" Sajenti Minja aliongea huku
ndani ya nafsi yake akiomba Askari wasikague
buti ya gari,
"Na huku kuna mini?" Askari mwingine aliongea
huku akifungua buti ya gari na kuwafanya wakina
Sajenti Minja waishiwe nguvu....
____________
ENDELEA....
____________
...."ebu toa lock ya buti" Askari yule akamuamrisha Sajenti Minja baada ya kufungua buti bila mafanikio.
Sajenti Minja akaona akifanya uzembe kidogo,
anaweza kuvuliwa nguo bila kutegemea, kwa
maana kwa Sajenti kama yeye kukutwa na maiti
ndani ya gari ni aibu kubwa.
"unajua unaongea nani?" sajenti Minja akamuuliza yule askari wa doria kistaharabu,
"haijalishi, kukujua wewe nani nadhani hakutasitisha kukukagua. fungua buti bwana" yule askari akaongea kwa ukali.
"Ngoja nikuoneshe kitambulisho changu" Sajenti Minja akatoa kitambulisho chake, akamtupia yule
askari,
"alafu inaonekana una jeuri sana kijana?, unamtupia nani likitambulisho lako?" yule afande
akawa anaongea huku akiwa anamfuata Sajenti Minja akiwa na gadhabu, alipomfikia, yule askari
akamtandika sajenti Minja kibao cha nguvu.
"haya okota likitambulisho lako na unipe mikononi, sio unirushie, umeona mi limbwa
eeh!?", yule askari wa doria akahoji kwa ukali mpaka mate yakamtoka,
Sajenti Minja akaona asilete mabishano wakati wanachelewesha kazi kwa mganga, akakubali kuwa mjinga, akakiendea
kile kitambulisho, akakiokota kisha akampatia yule askari wa doria.
Yule askari akakipokea,
akashtuka baada ya kukiangalia kwa nje, maana kilikuwa cha kipolisi, alipokifungua kwa ndani, akakisoma ndani, kisha
akammulika Sajenti Minja na tochi usoni, ghafla
akampigia saluti, wale askari aliokuwa ameongozana
nao, kuona hivyo, nao wakampigia saluti Sajenti Minja.
"samahani sana mkuu, mi sikujua kabisa" yule
askari wa doria aliongea huku sura yake
ikionesha kama anataka kulia kutokana na hofu aliyokuwa nayo,
"usijali, ndio kazi inatakiwa kufanywa hivyo" Sajenti Minja ndivyo alivyomjibu, kisha
akamuuliza, "bado unataka nifungue buti?"
"ha...hapa...hapana mkuu" yule askari wa doria akajibu kwa sauti iliyojaa kitetemeshi.
"Kwa hivyo mnaweza kuturuhusu twende?" Sajenti Minja aliwauliza,
"Nenda tu mkuu, samahani sana kwa usumbufu" Askari alijibu huku akimrudishia Sajenti Minja kitambulisho chake.
Sajenti Minja akakipokea kitambulisho chake na wakaingia ndani ya gari, kisha wakaendelea na safari yao.
"wajomba pale bila kutumia akili tulikuwa tunaumbuka" Sajenti Minja alianzisha maongezi baada ya kuondoka eneo walilosimamishwa,
"Mimi ndio nilikuwa nimekata tamaa kabisa" Omari nae akachangia,
"Mimi akili niliyokuwa nayo ilikuwa ni kutoka nduki tu" Kayoza aliongea na kufanya wenzake wacheke,
"bila ya kitambulisho, sasa hivi sijui tungekuwa
wapi?" Sajenti Minja akasema huku akiwa anaipaki gari nje ya nyumba ya mganga.
Wakashuka, kisha wakaenda hadi mlangoni kwa
mganga, wakabisha hodi, wakafunguliwa na
msaidizi wa mganga,
"sisi tulijua hamuwezi kuja tena, maana giza limekuwa kubwa sana" Msaidizi wa Mganga
aliwaambia baada ya kuwagundua,
"tulipata matatizo kidogo njiani, ila yameisha" Sajenti Minja aliongea huku akiwa anaingia ndani na nyuma yake wakina Kayoza wakimfuata.
"Sasa itabidi ifanyike ingawa tumechelewa kidogo" Mganga aliongea baada ya kuwaona,
"Itakuwa vyema sana" Sajenti Minja aliongea,
"Sasa huyo kijana mwenye tatizo inabidi asogee hapa tumfanyie mambo kidogo" Mganga aliongea huku akitandika kitambaa cheusi chini. Kayoza akasogea na kuambiwa Amalie kile kitambaa cheusi na mganga akaanza kufanya matambiko.
Baada mganga kumaliza matambiko madogo pale
nyumbani, wale wasaidizi wa mganga, walikuwa
wanne, wawili wakambeba yule maiti na wawili
wengine wakabeba vifaa vya uganga, hapo
ilikuwa saa sita na dakika zake za kutosha,
mganga akawa anaongoza msafara.
"Hizi sehemu zinatisha ila mnabidi mzizoee" Mganga aliwaambia wakina Sajenti Minja wakati wakiwa njiani,
"Hizi sehemu za kutisha nimeshazizoea sana, labda vijana wangu hapa ndio wageni" Sajenti Minja alijibu,
"Kwa hivyo mambo haya ya kutembea kwa waganga ushayazoea sana?" Mganga alimuuliza Sajenti Minja,
"Hapana, kwa masuala ya kiganga mi ndio mara yangu ya kwanza" Sajenti Minja alijibu,
"Sasa hata mazingira ya kutisha umeyazoeaje?" Mganga aliuliza,
"Kutokana na kazi zetu mzee wangu" Sajenti Minja alijibu,
"Kwani nyie mnafanya kazi gani?" Mganga aliwauliza,
"Hao vijana wangu wanasoma chuo, mimi ni muangaikaji tu wa sehemu mbalimbali katika kutafuta ridhiki" Sajenti Minja alijibu,
"Sasa kama huyu kijana mwenye matatizo yupo Chuo huko chuo anaishi vipi na chuo mzimu" Mganga alihoji,
"Matatizo matatizo tu na ndio maana tumemleta hapa" Sajenti Minja alijibu na ukimya ukatawala tena njiani.
Walitembea mda wa saa nzima hadi sehemu za makaburini.
" inabidi tuchague kaburi moja ambalo limetengenezwa vizuri na liwe la mwanamke" Mganga alitoa maelekezo na wale wasaidizi wake wakatawanyika kila mmoja na upande wake wakitafuta hilo kaburi zuri alilozikwa mwanamke.
"Naona hili hapa linafaa" Msaidizi mmoja wa mganga alipaza sauti na watu wote wakaelekea eneo alilopo.
Walipofika katika kaburi moja lililosakafikiwa
vizuri, Mganga alilidhika nalo baada ya kuona kila anachokihitaji kipo.
Mganga akawaamuru wasimame, kisha
akachukua kikapu cha uganga akatoa vifaa vyake
akavipanga kulizunguka lile kaburi,
"Were kijana njoo ulale hapa juu ya hili kaburi" Mganga alimwambia kayoza,
"Mi naogopa mzee" Kayoza aliongea huku akiwa na wasiwasi,
"We mpumbavu mini, ebu lala hapo kabla sijakuchapa makofi, we unafikiri utaponaje kama ukikahidi maneno ya mganga" Sajenti Minja aliongea kwa ukali, Kayoza akakubali kulala hivyo hivyo huku aakitetemeka.
Baada ya Kayoza kulala juu ya kaburi, mganga akammwagia madawa yake Kayoza kichwani, haikuchukua
hata dakika moja, Kayoza akapoteza fahamu na kulala kama maiti,
"Haya mchukueni huyo maiti na mumlaze pembeni ya huyo kijana" Mganga akawaamuru wasaidizi wake
wamchukue yule maiti na kumlaza pamoja na
kayoza, wasaidizi wakatekeleza agizo.
"Kazi ndiyo inaanza, sharti kubwa na la kuzingatia ni kwamba kazi itakapoanza haitatakiwa ionekane damu ya kitu chochote kile" Mganga aliongea,
"Hata ya mbu?" Sajenti Minja aliuliza kutokana na eneo like kuwa na mbu wengi,
"ndio, kama mbu atakung'ata hata usimuue, maana ukimuua ile damu yake inaweza kuwa tatizo kwetu" Mganga aliongea kwa msisitizo,
"Na ikionekana ni kipi kitachotokea?" Sajenti Minja aliuliza,
"Huu mzimu tunaoutoa hapa, nguvu zake zipo kwenye damu ya kila kiumbe, kwa hiyo damu itakapoonekana, mzimu atapata nguvu na kati yetu hapa hakuna atakayepona" Mganga alitoa Maelezo,
"Hilo litawezekana" Sajenti Minja alijibu,
"Na pia kama mtu ana kidonda ajitahidi akizibe kisionekane" Mganga alitilia mkazo,
"Basi kazi ifanyike tu, naona Maelezo yako yamejitosheleza" Sajenti Minja aliongea,
"Kwa hiyo hapa kazi inayofanyika ni kuutoa huu mzimu kutoka kwa kijana wenu na kuuingiza katika maiti alafu kazi itayofuata ni kuizika hivyo maiti pamoja na mzimu" Mganga alimaliza.
Mganga akaanza kazi yake, alimwaga madawa
eneo lote, kisha akaanza kuongea lugha
anayoijua yeye, alifanya kwa nusu saa, kisha
likatokea dubwana la ajabu kwenye mwili wa
Kayoza, kila mtu alipata uoga isipokuwa mganga tu.
Sasa like dubwana likawa kama linavutwa kutoka kutoka kwenye mwili wa Kayoza, ila likawa
halitaki,
hiyo hali ilienda kama saa nzima, mganga
akaanza kuona mafanikio, lile dubwana lilishatoa
mwili mzima ikawa bado miguu, na mwisho hadi miguu ilitoka na likaanza kudumbukia katika ile maiti.
Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu,
akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga
aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa
"tumekwisha...".
Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu waliolala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............
******ITAENDELEA*******
*Je mganga atafanikiwa kuutuliza mzimu uliokuwa na hasira ya kudhuriwa au mzimu ndio utawamaliza wote waliotaka kumdhuru?
the Legend☆
YaaniOmary nae bingwa wa kuchomesha...
Aliwachomesha wenzake kwa polisi, makaburini kachomesha tena..
Hatuendelei jamani dear hata kidogo tuAsante dear
the Legend☆
Soon tunaendelea dear, usiwazeHatuendelei jamani dear hata kidogo tu
Ndio mana nakupenda mmSoon tunaendelea dear, usiwaze
the Legend☆
Nimecheka sana sajent minja na mzimuRIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.
SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO.
______________
ILIPOISHIA...
______________
Mara ghafla panya akatokea
kichakani, alikuwa kama anakimbizwa na kitu.
akawa anaelekea kwenye miguu ya Omary, katika
jitihada za kumkwepa, Omary akajikuta anamkanyaga yule Panya,
damu ikaenea katika viatu vya Omari, mganga aliliona lile tukio,
akajikuta anasema kwa sauti iliyokata tamaa
"tumekwisha...".
Na wakati huo huo mzimu ukachomoka kutoka katika mwili wa maiti na huku ukifoka kwa hasira kiasi kwamba ndege na wadudu walioloala maeneo Yale ya makaburini waliamka na kukimbia hovyo..............
___________
ENDELEA
___________
"Hapa sijui kama tutapona" Mganga alitamka maneno hayo, huku akiwa
kama anajitayarisha na pambano jingine.
Mzimu ulipiga kelele zilizowatisha watu wore pale, kisha ulirudi kwa kasi ndani ya mwili wa Kayoza, kisha Kayoza
akanyanyuka taratibu, alikuwa tayari
keshabadilika, alikuwa anaogepesha ukimtazama msoni, macho yalikuwa meupe yasiyo na mboni na meno ya mbele pembeni yalikuwa marefu kama ya mnyama simba.
Kayoza akawatazama wote, alafu akawa
anamfuata Omari, Omari kuona hivyo, mkojo
ukaanza kumtoka na hata kukimbia akawa anashindwa ila alibaki ametoa macho huku machozi yakimtoka ingalikuwa halii.
Kayoza alipomfikia Omary
akamuangalia kisha akaachane nae, sasa akawa
anafuata mganga ambaye muda wote alikuwa bado anafanya mambo yake ya kiganga kwa ajili ya kujaribu kuutuliza mzimu wa Kayoza.
Mganga baada ya kuona mzimu unamfuata, maamuzi aliyoyachukua ni kutoka tu
mbio, akasababisha na watu walikuwepo katika
hilo eneo nao watoke mbio
mganga hakufika hata mbali, Kayoza akamkamata,
"Wewe ni nani mpaka utake kunitoa katika nyumba yangu?" Mzimu ulimuuliza mganga huku ukiwa umemkaba katika shingo na kusababisha kucha zake ndefu zipenye kwenye shingo ya mganga,
"Mi...mii..nimeagi..zwa tu na ndugu za...ko" Mganga aliongea kwa tabu huku damu zikimchuruzika shingoni.
Ila pamoja na utetezi wake ule mzimu ulimbeba juu na kung'ata shingoni kisha aakaanza kumnyonya damu, alipomaliza akamtupa pembeni.
Kisha mzimu ukatoka mbio na kuwakuta wasaidizi wa mganga wakiwa wanakimbia na wale
wasaidizi wake pia wakanyonywa damu.
Kisha Kayoza akamfuata sajenti Minja, ambae yeye alikimbia ila mwisho akaamua asimame tu maana aliona hata kama akikimbia ni lazima tu akamatwe.
Mzimu akamkamata mkono Sajenti Minja alafu akawa anamvutia
kichakani sehemu ambayo kulikuwa na miti mingi, alipofika katika eneo lenye miti,
"Usipate kichwa kwa kuwa niliahidi kutoidhuru damu yenu, wewe ndiyo utasababisha nivunje ahadi yangu" Mzimu uliongea huku
Ukikata fimbo, na kisha ukaanza kumtandika Sajenti Minja, alimtandika
kisawa sawa, mpaka sajenti Minja akawa analia kama mtoto.
Mzimu uliporidhika na bakora alizozipata Sajenti Minja ukamuachia na Sajenti Minja akatoka mbio kama mwendawazimu na kuishika ile njia waliyokuja nayo ambayo ilikuwa inaelekea nyumbani kwa Mganga.
Mzimu ulipomuachia Kayoza, Kayoza akadondoka chini kama kifurushi na akapoteza fahamu.
Omary yeye baada ya kuachwa na mzimu wala hakukimbia, alikuwa anaangalia tu unyama unaofanywa na mzimu na hata wakati Kayoza anaanguka na kupoteza fahamu Omary aliona na akaamini tayari mzimu umemuachia rafiki yake, Maamuzi aliyoyachukua Omary ni kwenda kumpa msaada Kayoza, alipofika, akambeba Kayoza kisha akawa kwenda walipoacha gari lao ambapo ni nyumbani kwa Mganga.
Walifanikiwa kufika salama nyumbani kwa mganga na wakamkuta Sajenti Minja anaangaika kufungua mlango wa gari ili aingie,
"Vipi huyo tayari au bado?" Sajenti Minja alimuuliza Omary baada ya kumuona anakuja na Kayoza,
"Tayari amerudi katika hali yake" Omary alijibu huku akifungua mlango wa gari na kumuingiza Kayoza,
"Aisee hii siwezi kuisahau" Sajenti Minja aliongea huku akiwasha gari na kuiondoa kwa kasi.
"Hii ilikuwa hatari, ila wewe hajakudhuru" Omary aliongea huku akijua fika Sajenti Minja alipewa bakora zisizo kuwa na idadi,
"Usiseme hivyo wewe, dah yaani nimefanywa mtoto Leo, tena mtoto wa shule" Sajenti Minja aliongea kwa huzuni,
"Umefanywaje kwani mjomba?," Omary aliuliza huku akimcheka kimoyomoyo,
"Hata kuhadithia siwezi, ni kitendo cha aibu sana" Sajenti Minja aliongea,
"Si uniambie tu mjomba" Omary alikazania huku akiendelea kumcheka moyoni,
"Nitakuambia tukifika bwana" Sajenti Minja alijibu huku akiongeza mwendo wa gari.
*****************
Katika hospitali ya mkoa kulikuwa na kasheshe
kubwa sana, kuna watu waliambiwa ndugu yao
amefariki, ila walipoenda monchwari hawakuikuta
maiti ya ndugu yao, walipowafata madaktari
wakawathibitishia kuhusu kifo cha ndugu yao, na
hata babu wa monchwari alithibisha kupokea maiti
ya huyo ndugu yao, sasa cha ajabu maiti ikawa
haionekani
Polisi walipofika pale hospitali, wakamchukua
babu wa mochwari huku wakiwa na uhakika kuwa
huyu mzee anahusika kwa namna moja au nyingine
katika upotevu wa ile maiti.
Babu akachukuliwa hadi kituoni, walipomfikisha
wakaanza kumuhoji,
"Mzee kuwa mkweli, tuambie huo mwili umeupeleka wapi?" Askari alimuuliza Babu wa monchwari,
"Yaani hata mimi sielewi, ule mwili kweli niliupokea ila hata ulivyopotea mimi sijui" Babu alijibu kwa kujiamini,
"Kwani walinzi mpo wangapi pale monchwari" Askari aliuliza,
"Tupo wawili" Babu alijibu,
"Umesema wewe ndiye uliupokea mwili, he wakati mwili unapotea ilikuwa zamu ya nani kulinda?" Askari akaendelea kuuliza,
"Yaani huo mwili niliupokea Jana saa mbili usiku, na imeonekana haupo Leo saa kumi na mbili alfajiri" Babu alijibu,
"Ilikuwa zamu ya nani?" Askari aliuliza,
"Zamu yangu" Babu alijibu,
"Babu acha kutuchanganya, inaonesha wewe unajua kila kitu kuhusu kupotea kwa huo mwili" Askari aliongea huku akitabasamu ili asimtishe Babu,
"Unadhani nakutania mjukuu wangu?, kweli mimi sijui kitu, inawezekana mile chumba cha monchwari kina wachawi, si unajua wachawi wanazipenda sana maiti" Babu alijitetea na kumfanya askari acheke,
"Babu sema kweli usiogope, hata kama umeusika hatuwezi kukufunga, maana utakuwa kama shahidi, na si unajua shaidi hafungwi?" Askari alimlainisha Babu huku akiendelea kucheka,
"Kweli hamuwezi kunifunga?" Babu aliuliza huku akimuangalia Askari,
"Kama utamtaja muhusika hautofungwa mzee, ila ukishikiria msimamo wako wa kuficha ndio utakaokuingiza matatizoni" Askari alimwambia babu wa monchwari,
"Kusema ukweli aliyeuchukua ule mwili namjua kwa sura ila jina simjui" Babu aliamua kusema ukweli,
"Anakaa Wapi?" Askari aliuliza,
"Sijui ila nikimuona tu sura yake namjua hata kama nikitoka kulala" Babu aliendelea kukazania maneno yake,
"Kulikuwa na makubaliano yoyote kati yenu mpaka auchukue huo mwili?" Askari aliuliza,
"Hapana aisee" Babu alikataa,
"Sasa alichukuaje na wakati wewe mlinzi ulikuwepo?" Askari aliendelea kumbana kwa maswali,
"Alikuja na bunduki akanitishia, kisha akaingia ndani na kubeba maiti" Babu wa monchwari aliamua kusema uongo,
"Sasa kwa nini tokea mwanzo hukusema hivyo?" Askari aliuliza huku akimuangalia usoni,
"Nilikuwa siamini kama mtaniamini" Babu alijibu,
"Sawa babu, itabidi urudi ndani" Askari aliongea huku akisimama,
"Ndani tens kufanya mini?" Babu aliuliza kwa kuamaki,
"Utatoka tu babu, ila kwa sasa mtuhumiwa bado unahesabika ni wewe mpaka apatikane huyo mwingine unaedai alikuvamia na bunduki" Askari aliongea na kubonyeza kitufe kilichopo mlangoni na mlango ukafunguka wakaingia Askari wengine wawili,
"Mpelekeni selo" Askari aliwaamrisha wenzake ambayo walimshika babu huku na huku na kutoka nae nje.
wanamtoa katika chumba cha mahojiano, ili
wampeleke rumande.
****************
Mida ya saa tano asubuhi, ndio sajenti Minja
alikurupuka, akaangalia simu yake, akukuta
missed call 12 za mkubwa wake wa polisi,
akawaamsha wakina Kayoza, kisha wakaenda
kujiswafi, wakatengeneza chai wakanywa.
Sajenti Minja akawarudisha wakina Kayoza kwa
mama Kayoza, kisha yeye akawa anaelekea
kituoni,
alipofika, akapaki gari lake kisha akawa anaenda
katika ofisi ya mkubwa wake, katika kolido ya
ofisi akapishana na askari watatu waliokuwa
wamemfunga pingu mzee mmoja ambae sura
yake haikuwa ngeni kwake yeye Sajenti Minja, ikabidi
ageuke amwangalie tena, na yule mzee nae
akageuka kumuangalia sajenti Minja, ndipo
sajenti Minja akamkumbuka, ni yule mzee mochwari na hapo pia ndipo yule mzee monchwari akamkumbuka kuwa yule wanaepishana nae ndiye aliyemuuzia maiti na kumsababishia madhira Yale, Babu wa Monchwari akasimama huku akiwa bado amemgeuzia shingo Sajenti Minja ....
********ITAENDELEA*********
the Legend☆
[emoji23][emoji23][emoji23]bakora za mzimu sio poaNimecheka sana sajent minja na mzimu
mzimu wenyewe jeuri, umechimba biti minja hadi jamaa kagwaya[emoji23][emoji23][emoji23]bakora za mzimu sio poa
the Legend☆
Hahahahaamzimu wenyewe jeuri, umechimba biti minja hadi jamaa kagwaya
Vipande vya leo vimenichekesha, Sajenti ana wakati mgumu kuliko hata KayonzaHahahahaa
the Legend☆
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Vipande vya leo vimenichekesha, Sajenti ana wakati mgumu kuliko hata Kayonza
Sent using Jamii Forums mobile app