Riwaya: Kijijini kwa Bibi

RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA THELATHINI NA TATU.

______________
ILIPOISHIA...
______________

Mchungaji Wingo aliporudi nyumbani kwake, akakuta mlango wa mbele uko wazi, video sebuleni inawaka, akamuita binti yake, lakini hakupata jibu, akaamua aende akamuangalie chumbani kwake, alipokaribia mlango wa chumba cha binti yake, alisikia mlio wa kitanda cha binti yake kikilalamika kwa fujo,

"mh..", mchungaji Wingo aliguna...

______________
ENDELEA.....
_______________

...mh", mchungaji aliguna, kisha akagonga mlango, mlio wa kitanda ukakoma, kisha ukimya ukatawala,

we happy", Mchungaji Wingo akamuita binti yake,

"abee baba", happy akaitika,"una shughuli gani umo ndani?", Mchungaji Wingo akamuuliza, kimya kikatawala tena, ila cha sasa hivi kilikuwa kirefu kidogo,

"mbona hujibu?", Mchungaji Wingo akauliza baada ya ukimya,

"nilikuwa naa...naa...naa.., sijakusikia ulichosema baba", Happy akashindwa kujibu akawa anajiuma uma tu,

"nimekuuliza una shughuli gani umo ndani, mbona kitanda kinapiga kelele hivyo?", Mchungaji Wingo akarudia swali katika sauti ya ukali,

"nafunga neti baba", happy akajibu huku sauti ikiwa na wasiwasi,"neti tu, ndo kitanda kipige kelele namna hiyo?", Mchungaji Wingo aliongea huku akiwa anarudi sebuleni, pia alionekana hakuridhishwa na jibu la binti yake

.***************

Ndani baada ya kusikia mtu anagonga hodi, wote walishtuka, ila hawakukurupuka, wakatulia tuli, baada ya kugundua kuwa anaegonga ni mchungaji, happy aliteremka chini taratibu kisha akavaa kanga yake, akawa anamjibu baba yake, kipindi hicho chote, Omari alikuwa anajing'ang'aniza kupita dirishani bila mafanikio, baada ya majibizano ya muda mfupi, kati ya happy na baba yake, Mchungaji aliondoka mlangoni kwa happy, hapo ndipo Omari akapata sauti,

"Sasa nitatokaje nje?", Omari alimuuliza happy kwa sauti ya chini sana,

"subiri kidogo, sasa hivi anaenda kuoga", Happy alimtoa Omari hofu.

"Happy umeniponza mwenzio" Omary aliongea huku akitaka kulia,

"Acha ujinga wewe, kwani baba amejua kinachoendelea?" Happy aliuliza kwa ukali,

"Hata kama hajui, wewe unadhani nitatokaje nje?" Omary aliuliza huku akiwa anafunga vifungo vya shati yake,

"Si nimekwambia ataenda kuoga muda si mrefu" Happy aliongea,

"Sasa mimi nitaaminije?" Omary alijikuta anauliza swali la kipuuzi,

"Mimi hapa ni kwetu, najua ratiba za watu wote hapa, ebu niamini acha ujinga" Happy alimuelewesha Omary.

"Dah, tamaa nyingine mbaya sana" Omary aliongea peke yake huku akijifuta jasho ingawa ndani hakukuwa na hali ya joto,

"Unasemaje" Happy alimuuliza Omary baada ya kumuona akiongea ingawa hakumuelewa,

"Sijasema kitu bwana" Omary alijibu huku akionekana ana hasira I logic hang any in an a na hofu.

"Mwenzangu ushaanza kuwa chizi" Happy aliongea huku akimcheka Omary chinichini.

*********************

Mchungaji Wingo alipotoka mlangoni kwa binti yake, alienda sebuleni, kisha akazima luninga, alafu akamuita happy,

"Umeshamaliza kufunga chandarua?" Mchungaji Wingo alimuuliza binti yake,

"Tayari, alafu sijisikii vzuri" Happy alimwambia baba yake,

"Kwa hiyo umehisi itakuwa malaria na ndio maana ukafunga chandarua?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akitabasamu,

"Ndio hivyo, mimi nadhani itakuwa ni malaria tu" Happy alijibu huku nae akitabasamu,

"Kuna maji ya moto?" Mchungaji Wingo aliamua kubadili mada,

"Ndio, yapo...yatakosaje wakati najua watumiaji mpo?" Happy aliuliza,

"Ebu niandalie nikaoge mie" Mchungaji Wingo aliongea huku akinyanyuka,

"Sawa mzee" Happy alijibu,

"Mama bado hajarudi?" Mchungaji Wingo aliuliza huku akisimama,

"Wakiendaga mjini wanawahigi kurudi kwani?, hiyo ni mpaka saa kumi na mbili jioni" Happy alijibu baba yake,

"Huyu nae bwana, si ahache kwenda uwage unaenda wewe?, yeye ameshaanza kuzeeka" Mchungaji Wingo aliongea kwa kulalamika,

"Wivu tu huo, muache aendage yeye, maana ndio anajua mahitaji ya watoto" Happy aliongea wakati baba yake anaelekea chumbani.

Happy akaenda bafuni akachukua ndoo na kwenda nayo jikoni ambapo aliiwekea maji ya moto na kuirudisha tena bafuni.

"Maji yapo tayari baba" Happy alipaza sauti kumwambia baba yake aliyekuwepo chumbani,

"Oooh nakuja, umeshayachanganya na maji ya baridi?" Mchungaji Wingo aliuliza huku bado akiwa ndani,

"Utachanganya mwenyewe, maana Jana nilivyokuchanganyia ulilalama nimezidisha ubaridi" Happy alimwambia baba yake,

"Bora hujachanganya, maana Sikh hizi nahitaji maji ya uvugu vugu mkali kidogo" Mchungaji Wingo aliongea huku bado akiwa chumbani,

"Umeshaanza kuzeeka ndio maana unataka maji yenye joto Kali" Happy alimwambia Baba yake huku akiwa bado amesimama mlangoni,

"Kweli aisee, naona umri unanitupa mkono" Mchungaji Wingo aliongea huku akitoka ndani akiwa amejifunga taulo lake kiunoni na moja kwa moja akanyoosha mpaka bafuni.

Alipoingia, akatoa taulo lake mwilini,

"mh..kumbe sabuni imeisha?", mchungaji aliongea peke yake, baada ya kuangalia sehemu ya kuwekea sabuni ikiwa tupu mule bafuni,

Mchungaji Wingo akakata shauri la kurudi kutoka bafuni na kurudi chumbani ambapo ndipo huifadhi sabuni nyingine.

********************

Happy Binti Mchungaji alipoona kuwa baba yake kaingia bafuni, akaingia chumbani haraka,

"Tayari baba ameingia bafuni, twende nikutoe nje" Happy aliongea kwa sauti ya chini ambayo ilisikika vyema masikioni mpwa Omary,

''Sasa njia tunayotokea si ndipo lilipo bafu, akisikia hatua za watu wawili zinatembea si atagutuka?" Omary alimuuliza happy Binti Mchungaji,

"Hawezi kugundua bwana, twende acha uoga" Happy aliendelea kumwambia Omary,

"Sasa si bora nisubiri Stoke bafuni aende chumbani?" Omary aliuliza,

"Acha ujinga, mama anarudi sasa hivi na wadogo zangu, wakikukuta humu, je itakuwaje?" Happy nae aliuliza,

"He!!!! Leo kweli siku yangu, haya twende" Omary aliongea kinyonge huku akisikitika.

Happy akamshika mkono Omary, kisha akaanza kutoka nae nje kwa mwendo wa kunyata, yaani mwendo wa taratibu usiokuwa na vishindo.

Walipofika usawa wa mlango wa baf na ndio muda huo Mchungaji Wingo alikuwa anafungua mlango ili akachukue sabuni chumbani.

Ghafla tu Omary na Happy binti Mchungaji wakashuhudia mlango wa bafu ukifunguliwa na wote macho yakawatoka pima mithili ya mtu aliekwamwa na kitu kooni...

********ITAENDELEA********

the Legend☆
 
RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.

SEHEMU YA THELATHINI NA NNE.

______________
ILIPOISHIA...
______________

Happy akamshika mkono Omary, kisha akaanza kutoka nae nje kwa mwendo wa kunyata, yaani mwendo wa taratibu usiokuwa na vishindo.
Walipofika usawa wa mlango wa baf na ndio muda huo Mchungaji Wingo alikuwa anafungua mlango ili akachukue sabuni chumbani.
Ghafla tu Omary na Happy binti Mchungaji wakashuhudia mlango wa bafu ukifunguliwa na wote macho yakawatoka pima mithili ya mtu aliekwamwa na kitu kooni...

_______________
ENDELEA........
_______________

Happy akauwai mlango wa bafuni, akaushikilia, tena kwa kuwa mlango wenyewe ulikuwa unafunguka kwa nje akaamua aulalie kabisa, Omari kuona hivyo akahisi kitakachomsaidia ni nduki tu. Akatoka mbio kuelekea nje,

"we happy vipi, una nini leo?", Mchungaji Wingo alimuuliza binti yake kwa sauti yenye mshangao huku akiusukuma mlango kwa utaratibu mzuri ili asimdhuru binti yake aliyekuwa amelala,

"baba sijisikii vizuri, naona kizunguzungu", Happy aliongea huku akiwa bado amelala chini.
Baba yake akamnyanyua, kisha akamrudisha chumbani kwake,

"nikupelekee hospital mwanangu?", Mchungaji Wingo alimuuliza binti yake kwa sauti ya huruma,

"hapana baba, nafikiri ni tatizo la muda", Happy alijibu huku akijifunika shuka,

"Hapana, lazima uende hospitali, ngoja nimalize kuoga nikupeleke" Mchungaji Wingo alimwambia mwanae,

"Baba hii hali ya kawaida tu, itaisha" Happy alijibu baba yake,

"Usichukulie vitu kirahisi rahisi, we jiandae tu nikupeleke" Mchungaji Wingo aliongea huku akitoka nje.

"hii ya leo balaa, sijui baba angenichukuliaje?", Happy alijiuliza mwenyewe huku akiwa na tabasamu la mshangao na pia akimshukuru Mungu kwa kumuepusha na dhahama hii.

*******************

Omari alipotoka kwa mchungaji mbio mbio mpaka alipofika nyumbani, akasukuma mlango akaingia kwa fujo hadi ndani,

"ehe, vipi mwenzetu?", Omari alipokewa na sauti ya Sajenti Minja aliyekuwa anamshangaa,

"nilikuwa nakimbia kimbia, kuweka mwili fiti", Omari alijibu akiwa katika tabasamu la uongo huku akipumua bila mpangilio,

"haya bwana, mi nilifikiri umefumaniwa na mke wa mtu uko, maana mbio ulizokuja nazo si mchezo", Sajenti Minja aliongea na kufanya vicheko vilipuke sebule yote.

"Hanna mjomba, huku ugenini siwezi kufanya hivyo" Omary alijibu huku akijilazimisha kutabasamu,

"Sisi tutajuaje bwana, nyie vijana mna mambo mengi" Mama Kayoza aliongea,

"Hakuna mama" Omari aliongea huku akiingia ndani, akamwita Kayoza, wakaingia ndani,

"duh, jomba uko noma", Omari alianza kwa mtindo huo,

"vipi tena baab?", Kayoza akauliza kwa mshtuko,

"mchungaji kanikuta juu ya mwili wa mwanae kaka", Omari akapasua lililomkuta,

"naisi kama sijakusikia vizuri vile, ebu rudia", Kayoza akauliza kwa stahajabu,

"nimesema kuwa, mchungaji kanikuta ndani kwake", Omari akaongea tena alichomaanisha,

"ikawaje kaka?", Kayoza akauliza huku akiwa bado haamini anachoambiwa.

Omari akamsimulia yote, mpaka alipofanikiwa kukimbia.

"duh, pole mwanangu", Kayoza akampa pole Omari,

"Cha kushukuru ni kuwa nimetoka salama" Omary aliongea huku akivua fulana yake,

"Sasa huyo Happy kwa hali uliyomuacha nayo si itakuwa baba yake amejua?" Kayoza aliuliza,

"Sijui bwana, kama baba yake atahisi labda inaweza kuwa tatizo, ila kuniona hajaniona" Omary alimjibu mwenzake,

"Ila usirudie kufanya ujinga kama huo tena, yule mwanamke ni shetani angalia usiwe unamsikiliza kila anachokushawishi" Kayoza alimshauri Omary,

"haina noma, kuna mpya gani hapa?", Omari akauliza,

"kesho saa nne tutaenda kwa mganga", Kayoza akamtaharifu Omari.

"maeneo gani",Omari akauliza,

"mi mwenyewe sijajua bado", kayoza akajibu,

"Dah, Mimi nina wasiwasi yasije yakatokea kama ya kwa yule mganga" Omary aliongea,

"Sasa usiseme hivyo, cha muhimu ni kumuomba Mungu tu atusaidie" Kayoza alimwambia Omary,

"Mungu tunamuomba ila pia tahadhari lazima" Omary alimwambia Kayoza,

"Basis usiende, nitaenda Mimi na mjomba" Kayoza aliongea huku akionekana hajafurahishwa na maneno ya Omary,

"Nitaenda tu" Omary aliongea kwa upole baada ya kugundua Kayoza amepaniki,

"Sasa kama utaenda kwanini unaleta maneno ya kutishana?" Kayoza aliuliza,

"Basi yaishe kaka, nisamehe kwa maana sikudhani kama utamaindi" Omary aliamua kujishusha ili mambo yaishe,

"Hatugombani hapa, tunaeleweshana tu" Kayoza alimwambia Omary,

"Sawa nimekuelewa ndugu yangu" Omary alijibu,

"Kama umenielewa sawa, Mimi nipo sebuleni" Kayoza aliongea huku akielekea nje na kumuacha Omary akiwa amejimwaga kitandani.

.*******************

Kesho yake asubuhi Sajenti Minja aliwapitia wakina Kayoza, na safari ya kwenda kwa mganga ikaanza.

Njia nzima hakuna alieongea, ndani ya gari kulikuwa na mziki laini wa unbreak my heart ulioimbwa na mwanamama wa kimarekani anayejulikana kama Tony braxton.
Sajenti Minja alikuwa akiufatilia ule wimbo kwa sauti ya chini, Omari yeye alikuwa na mawazo yake, Kayoza pia alikuwa anafikiria anachokijua.

"Huo wimbo vipi?" Kayoza aliuliza baada ya Sajenti Minja kurudia zaidi ya mara tatu kuupiga ule wimbo,

"Si naupenda tu" Sajenti Minja alijibu kwa kifupi,

"Mimi najua mtu akiupenda wimbo lazima kuna tukio linahusihana na huo wimbo" Omary alichangia,

"Ebu acheni ujuaji, sasa mnataka niweke nyimbo gani? au niweke hayo manyimbo yenu yenye yo yo nyingi?" Sajenti Minja aliuliza,

"Wewe tuambie tu kuhusu huo wimbo, acha kujikanyaga" Kayoza alimwambia mjomba ake huku akicheka,

"Au shangazi hasomeki?" Omary akaongeza na swali,

"Ebu niacheni bwana" Sajenti Minja aliongea huku akizima redio ya gari.

Kwa mganga waliingia mishale ya saa sita kasoro robo, wakapokelewa na msaidizi wa mganga, ila kwa bahati nzuri hawakukuta foleni ndefu, watu walikuwa wachache tu.

Baada ya nusu saa, zamu yao ikafika wakaingia ndani, kile kitendo cha kayoza kuingiza mguu katika mlango wa nyumba ya mganga, pale pale akabadilika na akawa katika taswira ya kutisha sana, ila alikuwa hawezi kutembea, aliganda pale pale, Sajenti Minja alipata uoga huku akidhani kuwa zile bakora za kipindi kile zinarudi tena kwa hiyo akakaa mbali kabisa na Kayoza hata alipogundua kuwa Kayoza ameganda pale, bado alikuwa anaogopa kumsogelea. Unacheza na viboko nini.

Mganga akapelekewa taharifa kuhusu lile tukio, Mganga ikambidi atoke katika chumba chake cha kazi na kwenda mahali alipo Kayoza, alipofika akamuangalia zaidi ya dakika kumi, kisha mganga akafunga macho yake, alafu akatoa pumzi kumuelekea kayoza kwa njia ya mdomo, pale pale Kayoza akadondoka chini huku akiwa katika ile ile taswira ya kutisha.

"Mtoeni nje" Mganga akawaamuru wamtoe nje, wakambeba wakampeleka nje, wateja waliokuwa nje wanasubiria tiba wote walikimbia walipomuona Kayoza katika hali ile ya kutisha.

"Aliyekuja na huyu kijana yupo Wapi?" Mganga aliuliza huku akimuangalia msaidizi wake,

"Yule kule" Msaidizi wake aliongea huku akinyoosha kidole kuelekea alipo Sajenti Minja,

"Mbona amekaa mbali sana?" Mganga aliuliza huku akishangaa,

"Hata sisi hatujui, labda anamuogopa" Msaidizi wake alijibu,

"Kamuite" Mganga alimtuma msaidizi wake na yule bwana akaenda kumuita.

Sajenti Minja alipofika alimsalimia mganga kisha mganga akawaambia aliefuatana na Kayoza amfuate ndani, Sajenti Minja na Omari wakamfuata mganga.

Mganga alikuwa ni mwanamke wa makamo, alikuwa na macho mekundu sana, akamkazia macho Sajenti Minja, kisha mganga akasema,

"Minja mna tatizo kubwa sana" Mganga aliongea na Sajenti Minja alishtuka kusikia mganga kamtaja jina lake, ila akapata matumaini ya kumaliza tatizo,

"ila kwako naamini litaisha", Sajenti Minja alijitutumua na kumjibu mganga,

"bibi yake mzaa baba yupo hai", Mganga akamtupia swali Sajenti Minja,

"ndio mama", Sajenti Minja akajibu,

"anaishi wapi?", Mganga akauliza tena huku akiwa amemkazia macho Sajenti Minja,

"anaishi Bukoba vijijini", Sajenti Minja akajibu,

"Sasa itabidi huyo kijana apelekwe uko", Mganga akawaambia Sajenti Minja,

"tumpeleke wapi?", Sajenti Minja akauliza ili apate ufafanuzi zaidi,

"mpelekeni kijijini, kijijini kwa bibi yake" Mganga aliongea akiwa amefunga macho.........

*******ITAENDELEA********

*Kumekucha sasa, Mganga anakisema kile anachokiona, je Sajenti Minja atakubali aende Bukoba? ataagaje ofisini?

the Legend☆
 
Hahahahahahaa, Minja angeambiwa hayo mambo sidhani kama angekubali. Ila kanichekesha alivyokaa mbali na kayoza, kweli bakora si poa

the Legend☆
Wakati tunasubiria game ya Taifa...ungeshusha episode kadhaa Mkuu..
 
Mganga anausukumia Msala kwa bibi!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…