RIWAYA : KIJIJINI KWA BIBI.
MTUNZI : ALEX KILEO.
SEHEMU YA AROBAINI NA NANE.
__________________
ILIPOISHIA....
------------------------------
Kayoza alipoingia ndani, Martha akaubana mlango na funguo kisha funguo akaidumbukiza ndani ya kifua chake, kisha akamgeukia Kayoza,
"Kayoza hakuna panya, ila ninachotaka toka kwako unakijua, Kayoza unaumiza moyo wangu sana, nifanyaje ili ujue nakupenda, eee?",Martha aliongea huku machozi yakimtoka,
"Dah, Martha si nilishakuambia haiwezekani lakini?" Kayoza aliuliza baada ya kukaa muda mrefu akimuangalia Martha kwa hasira,
"Naomba tu iwezekane, mpaka Mimi kufikia hata hii ya kukutamkia maneno haya, ujue hisia zangu zimenishinda" Martha aliongea huku akipiga magoti,
"Sawa nimekuelewa, naomba unifungulie mlango nitoke nje" Kayoza aliamua kumkubalia ili amridhishe Martha,
"Hapana sitaki utoke" Martha aliongea kwa hisia huku akimtazama Kayoza...
mara sauti ya Mkuu wa Polisi ambaye ndiye Baba yake Martha ikasikika mlangoni,
"we Martha unaongea na nani uko chumbani? Ebu nifungulie mlango"
**********ITAENDELEA***********
..."hakuna kitu daddy",Martha alimjibu Mkuu wa polisi,
"kwa hiyo unaongea peke yako uko"Mkuu wa polisi akamtupia mwanae swali jingine,
"si naongea na simu",Martha akajibu.
"Fungua basi mlango niingie" Mkuu wa polisi akamwambia mwanae,
"Daddy navaa bwana, kwani unataka nini huku?" Martha alimjibu baba yake huku akideka.
Hivyo ndivyo alivyolelewa na wazazi wake, amelelewa malezi ya kujibishana na wazazi wake kama rafiki zake,
"Si nilitaka nikuone mwanangu, au vibaya mama?" Mkuu wa polisi aliuliza huku akiwa mlangoni,
"Nakuja sebulebi daddy, mammy umemuacha wapi?" Martha aliuliza,
"Nimerudi nae, ameenda kuoga" Mkuu wa polisi alijibu huku akiamua aondoke zake, na kurudi sebuleni kuongea na Sajenti Minja,
"naweza kupata juice",Sajent Minja alimuuliza Mkuu wa polisi alipokua anakaa,
"mhmm..sidhani kama ipo, ebu ngoja, we Martha, marthaa",Mkuu wa polisi alijibu kisha akamuita mwanae,
"nakuja daddy" Sauti ya Martha ilisikika kutoka chumbani kwake.
Baada ya sekunde chache Martha akawa mbele ya Sajenti Minja na baba yake,
"shikamoo anko",Martha alimsalimia Sajenti Minja,
"marhabaaa anko, kuna juisi?",Sajenti Minja aliitikia, kisha nae akauliza swali,
"ipo anko,",Martha alijibu,
"naomba unipe ya pera",Sajenti Minja aliwasilisha ombi lake, mmmh, ya pera hamna, ipo ya orange, strawberry,mango na passion",Martha alijibu,
"nipe ya chungwa na maji ya baridi",Sajenti Minja aliagiza na martha akamletea,
"Vijana wangu hawajaja leo?" Sajenti Minja alimuuliza Martha, alikuwa akiwaulizia wakina Kayoza,
"Hawajafika anko" Martha alijibu huku nafsi yake ikimsuta kwa maana aliongea uongo,
"Leo naona watakuwa wamechoka" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja,
"Wamechoka wapi, itakuwa wameona nimeshapona kwa hiyo hawaoni umuhimu wa kuja kunijulia hali" Sajenti Minja aliongea,
"Acha wapumzike, maana wale watoto walikuwa wanashinda hospitali mpaka nikawa nawahurumia" Mkuu wa polisi aliwatetea wakina Kayoza,.
"Hakuna haja ya kuwahurumia, hilo ndilo lilikuwa jukumu lao, mama yao umri wake umeshakwenda, anatakiwa apumzike" Sajenti Minja aliongea,
"Wameshawahi kuishi Dodoma ee?" Mkuu wa polisi aliuliza swali lililomshtua Sajenti Minja,.
"Nani alikwambia?" Sajenti Minja aliuliza huku akijifanya anacheka ili kuuficha mshtuko wake, ila tayari Mkuu wa polisi alikuwa ameshamsoma,
"Waliniambia wenyewe, wakadai wamemaliza pale UDOM ila hawajachukua vyeti vyao" Mkuu wa polisi alizidi kutiririka na kuendelea kumshtua Sajenti Minja,.
"Yah ni kweli walimaliza pale" Sajenti Minja alijibu kifupi,
"Sasa ni kwanini hawajachukua vyeti?" Mkuu wa polisi aliuliza swali la kumtega Sajenti Minja ili zone kama jibu lake litafanana na la wakina Kayoza,
"Hawajachukua vyeti?, mbona Mimi hawajaniambia kama hawajachukua vyeti vyao?" Sajenti Minja alijifanya kushangaa huku akiuliza,
"Alah!!! Kumbe hujui?" Mkuu wa polisi aliuliza,
"Aisee hawakuniambia, labda wamefanya makosa wanaogopa kuniambia, au wamekula ada?" Sajenti Minja aliamua kumuigizia sasa Mkuu wa polisi, alivyokuwa anaongea utasema kweli yaani,
"Wameniambia wameshindwa kulipa ada ndio maana hawajachukua" Mkuu wa polisi aliamua kumwambia ukweli,
"Wanekudanganya, niliwapa pesa yote, itakuwa wamefeli au wamekula ada...yaani awa watoto awa, utakuta hata mama yako hajui kama hawana vyeti" Sajenti Minja alijifanya kusikitika,
"Kwani walikuwa wanasomea nini?" Mkuu wa polisi aliuliza swali jingine lilimuweka mtegoni Sajenti Minja,
"Hawajakwambia?" Sajenti Minja alimuuliza mkuu wa polisi huku akijitahidi kuvuta kumbukumbu ya masomo waliyokuwa wanasoma wakina Kayoza,
"Hawakuniambia" Mkuu wa polisi alijibu huku akibonyeza controller ya runinga,
"Mi hata nilikuwa sifuatilii wanachukua kozi gani, ili mradi nilikuwa nawalipia ada wamalize tu chuo" Sajenti Minja alilipangua swali la Mkuu wa polisi,
"Ulikuwa unatakiwa uwafuatilie bwana" Mkuu wa polisi alimwambia Sajenti Minja,
"Shauri yao bwana kama walichezea masomo, ngoja nikajimwagie maji" Sajenti Minja alijibu huku akinyanyuka na kuondoka ili kuyakwepa maswali ya Mkuu wa polisi, maana yalimpa mashaka na akahisi inawezekana babu wa monchwari alimchoma.
Kuanzia hapo akaanza kuishi kwa wasiwasi akihisi kuwa inawezekana kabisa Mkuu wa polisi anawapeleleza wakina Kayoza pasipo wao kujua.
*******************
Baada ya Martha kumuhudumia Sajenti Minja, Martha alirudi chumbani kwake, usiku ulikuwa umeshaingia,
"sasa mimi nitatokaje humu?",Martha alipokelewa na swali la Kayoza ambae alikuwa yuko ndani ya kabati,
"subiri bwana, sasa hivi wanaenda kulala, sebule itakuwa haina mtu",Martha alimjibu Kayoza kwa kujiamini,
"Alafu mbona unajiamini sana, we huogopi kuniingiza mwanaume chumbani kwako?" Kayoza aliuliza huku akiwa ana hasira,
"Lazima nijiamini, sasa nimuogope nani wakati nipo kwetu?" Martha alijibu kwa nyodo huku akitandika vizuri kitanda chake,
"Usiwe unajiamini kwa kila kitu, vingine vitakutokea puani, shauri yako" Kayoza aliongea kwa hasira huku akichungulia dirishani,
"Nikuletee chakula?" Martha alimuuliza Kayoza,
"Hapana, sihitaji" Kayoza alijibu huku akionekana amesusa,
"Ukisusa sisi twala" Martha aliongea kwa madaha huku akielekea sebuleni.
Martha alibeba chakula kingi na kwenda kulia chumbani kwake kwa lengo la kula pamoja na Kayoza.
"Njoo rule bwana K, usiwe unasusa Susa kama mtoto wa kike" Martha alimwambia Kayoza huku akimpa kijiko, lakini Kayoza hakutaka hata kujisumbua kupokea, badala yake alikaa tu kitandani huku mkono ukiwa shavuni.
Baada ya masaa mawili, kila mtu aliyekuwa sebuleni alienda kulala, sebule ikabaki tupu.
Ilikuwa ni mishale ya saa nne usiku, katika chumba cha Martha kulikuwa na sauti za mabishano ambazo zilikuwa zinasikika kwa chini chini sana,
"Martha niachie niende, mama atakua na wasiwasi nyumbani",Kayoza alimlalamikia Martha,
"ni vigumu kutoka Kayoza, lazima mlinzi kesho atamwambia baba alafu iwe msala kwako",Martha alijibu akiwa na lengo la kumzuia Kayoza asiondoke ili atimize azma yake ya kufanya nae mapenzi,
"kulala na wewe ni kitu ambacho akiwezekani Martha, kwanza tulikubaliana kuwa watu wakienda kulala ndio unanitoa, ona sasa unaleta sababu nyingine",Kayoza aliongea kwa kulalamika,
"isiwe tabu mwenzangu, wewe lala kitandani mimi nitalala chini",Martha aliongea huku akikunjua godoro jingine alilolitoa juu ya kabati.
"Nani kakwambia anataka kulala hapa?" Kayoza aliuliza kwa jazba,
"Alafu usiongee kwa sauti kubwa, Baba akisikia itakuwa tabu kwako, shauri yako" Martha alimtisha Kayoza,
"Basi nitoe nje niende kwetu" Kayoza aliongea kwa sauti ndogo,
"We lala, ikifika saa saba au saa sita nitakutoa, mlinzi atakuwa amesinzia" Martha alimlaghai Kayoza, ikambidi alale, ila kwa sharti moja, wasilale pamoja, ambapo Martha alikubali na kutandika godoro chini na kitandani alilala Kayoza.
Ilimchukua saa moja tu Kayoza kupata usingizi, akalala fofofo huku akikoroma, saa sita ikafika, ikapita na saa saba ikafika na kupita na sasa ilikuwa saa Tisa usiku,
Martha akakurupuka kutoka katika godoro la chini, taratibu akavua nguo zake zote, kisha akapanda kitandani kwa hadhari ya kutomshtua Kayoza, akaingia ndani ya blanketi, kisha akaanza kufungua zipu ya suruali ya Kayoza,
"mmmh, mbona yuko hivi?",Martha aliguna baada ya kumuona Kayoza kalegea kama mtu aliepoteza fahamu, ila hiyo haikumzuia kuendelea na anachokifanya, akafanikiwa kuishusha suruali ya Kayoza hadi miguuni, sasa akawa anajiweka sawa ili atimize lengo lake, Kayoza aliinuka kama mshale, kwa kasi ya mwanga na meno yake yakapenya sawia katika shingo ya Martha,
"mamaaaaaaaa nakufaaaaaaaaa",sauti ya Martha ilisikika kwa nguvu na kuwaamsha watu wote waliolala mpaka majirani..............
****"*****ITAENDELEA************
*kwa Mara nyingine tena Kayoza ameharibu, tena ameharibu ndani ya nyumba ya Mkuu wa polisi, je kelele alizotoa Martha zitasababisha Kayoza akamatwe?
*Mkuu wa polisi amemtuma mtu ili amchunguze Omary huku na yeye akianza kumchunguza Sajenti Minja, je atafanikiwa kupata anachokitaka?
the Legend☆