Riwaya: Senyenge

Riwaya: Senyenge

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Posts
1,941
Reaction score
2,044
JINA: SENYENGE
MWANDISHI: CHIAMARO MOKIRI
MAWASILIANO: Chiamaro.llc@gmail.com / +255 (0)763 170 858

UTANGULIZI.
Maisha ya Hook Hobie yalikuwa na siri nzito aliyoificha kwa zaidi ya miaka thelathini. Uhuru wake, Wadhifa wake, Mali zake na kila kitu alichokimiliki kilitegemea siri yake hiyo. Na kama mtu yeyote aliye makini, Hook Hobie, alikuwa tayari kufanya lolote ili kuilinda siri yake. Kwasababu ingetokea ikavuja basi maisha yake yote yangekuwa yameharibika.

Njia aliyoitumia kuhakikisha siri yake hiyo haivuji kwa zaidi ya miaka thelathini ilitegemea mambo mawili - mambo ambayo kila mtu huyatumia kujilinda dhidi ya hatari. Mambo ambayo taifa huyatumia kujilinda dhidi ya maadui zake: Kuhisi na kuanza mwitikio. Hatua ya kwanza, hatua ya pili. Kwanza unalihisi tishio, halafu unaweka mwitikio.

Hatua ya kwanza ilikuwa ni kama onyo kwake na ilikuwa ikibadilika mwaka hadi mwaka kutokana na mazingira yalivyobadilika. Ilihusisha tabaka mbili kama fensi mbili ziizungukayo nyumba. Fensi ya kwanza ilikuwa maili elfu kumi na moja kutoka nyumba ilipo. Hii ilikuwa ni kama onyo la kwanza. Ingemuambia adui zako wanakaribia kukufikia. Fensi ya pili ilikuwa maili elfu tano karibu na nyumba, lakini bado ingekuwa maili elfu sita kutoka fensi ya kwanza ilipo. Hii ingemuambia adui zako wapo karibu sana kukufikia. Ingemuambia hatua ya kwanza imeisha. Ingemuambia ni muda wa hatua ya pili.

Hatua ya pili ilikuwa ni mwitikio. Alikuwa amepanga vyema nini atafanya kipindi onyo la pili litakapofikiwa. Alikuwa ametumia karibu miaka 30 akifikiria, lakini kulikuwa na jibu moja tu sahihi - Mwitikio ungekuwa ni kukimbia. Kupotea kabisa. Yeye mwenyewe alikuwa ni mtu asiyeendeshwa kwa hisia bali tafakari kali. Na maisha yake yote alijivunia ujasiri na uthubutu wake. Kila ilipohitajika kufanyika jambo, kama lingekuwa na faida kwake, basi angelifanya bila kusitasita. Lakini alijua siku atakaposikia maonyo kutoka kwenye fensi alitakiwa kuondoka kwasababu hakuna mtu ambaye angeweza kuhimili kilichokuwa kinakuja. Hayupo. Hata yeye pamoja na ujasiri wake asingeweza.

Hatari ya siri yake kuvuja ilipita na kutambaa kama mawimbi kwa miaka mingi. Alikuwa akitumia muda mwingi akijua mambo yataharibika saa yeyote, lakini haikuwa hivyo. Muda mrefu ulipita kiasi kwamba hisia zikamwambia yupo salama. Miaka thelathini sio mchezo! Lakini kuna nyakati aliiona miaka thelathini ni kama kufumba na kufumbua macho tu.

Hivyo akawa analisubiria onyo la kwanza akipanga namna atakavyokimbia. Picha ya tukio zima litakavyokuwa ilikuwa kichwani mwake. Kwanza, Onyo la kwanza lingekuja mwezi mmoja kabla ya onyo la pili. Huo mwezi mzima angeutumua kujiandaa. Angezifuta nyayo zilizokuwa zinaonekana, angehamisha mali zake na angelipa visasi kama vilikuwepo. Halafu muda ambao onyo la pili lingekuja angeondoka bila kusita wala kugeuka nyuma.

Lakini kupanga huwa ni jambo moja na uhalisia ni jambo lingine. Muda ulipofika onyo la kwanza na lile la pili vilikuja kwa pamoja. Kwa wakati na siku moja. Mbaya zaidi onyo la pili ndilo lilitangulia. Yaani fensi iliyokuwa karibu na nyumba ndiyo ilikuwa imevamiwa kwanza. Na Hook Hobie hakukimbia. Alipuuza mipango yote aliyoipanga kwa miaka thelathini na kuamua kukabiliana na kilichokuwa kinakuja kwake uso kwa uso.

SEHEMU YA KWANZA
 
SEHEMU YA KWANZA:
Jack Reacher alimuona mwanaume mmoja akiingia baani hapo kupitia mlango ambao haukuwa mlango, bali ukuta ulio wazi tu. Baa ilikuwa ikitazamana na barabara wanapopita watembea kwa miguu. Nje na ndani kulikuwa na meza na viti vilivyofunikwa na mwamvuli mkubwa uliolipa eneo lote kivuli na utulivu wa kutosha.

Yule mwanaume alisimama kwa dakika kadhaa ili kuyaruhusu macho yake yazoee giza lililokuwemo mule ndani baada ya kutoka kwenye mwanga mkali wa jua huko nje ya mitaa ya Key West. Ilikuwa ni mwezi wa sita, saa kumi kamili alasiri kusini kabisa mwa Amerika. Jua kali na joto lisilozoeleka. Reacher alikiegemea kiti chake vizuri na kupiga funda moja la maji halafu akatulia kuona nini kitafuata.

Yule mwanaume alianza kuzungusha macho yake kupakagua mule ndani. Baa yenyewe ilikuwa imetengenezwa kwa kutumia bodi zilizoonekana ni kama zimetolewa kwenye meli iliyokufa. Kwenye pembe moja kulikuwa na mkusanyiko wa vitu kama neti zilizochoka. Vifaa vya kuvulia, Reacher alihisi ingawa katika maisha yake yote hakuwahi kuvua samaki achilia mbali kupanda hata mtumbwi.

Yule mwanaume alianza kupiga hatua kuelekea ilipokuwa kaunta. Alikuwa mzee pengine wa miaka sitini. Urefu wa wastani na unene kidogo. Daktari angeweza kumuweka kundi la waliopitiliza uzito wa kawaida.

Alikuwa amevaa kama mtu wa kaskazini aliyeshtuliwa na safari ya ghafla. Suruali laini ya kijivu - Juu pana, chini nyembamba, Shati jeupe na koti la kijivu juu yake. Chini alikuwa na soksi nyeusi na viatu vya kimjinimjini. Mtu wa New York au Chicago, Reacher aliwaza. Pengine mtu wa Boston aliyekulia maisha ya kiyoyozi na nguo kama hizi huzivaa mara mojamoja pale inapobidi.

Yule mwanaume alifika kaunta na kutoa waleti kwenye mfuko wa koti lake. Reacher alikuwa bado anamtazama akiifungua waleti na kuigeuzia kwa mhudumu huku akiuliza swali. Mhudumu aliangalia pembeni bila kujali kama aliyetukanwa. Yule mwanaume akairudisha waleti yake mfukoni na kuongea jambo na mhudumu akainama akaibuka na kinywaji kutoka kwenye dumu la barafu. Yule mwanaume akakipokea na kukitazama huku akitabasamu.

Reacher akapiga fundo lingine la maji. Yeye alikuwa amekutana na watu wengi waliokuwa fiti na imara, lakini hakuwahi kukutana na mtu imara kama mwanajeshi mmoja wa kiBelgiji aliyeapa kuwa fanya chochote kile unachotaka kufanya alimradi unakunywa lita tano za maji ya madini kila siku, basi utakuwa fiti na imara. Reacher akagundua lita tano ni sawa na kigaloni kidogo na kwa kuwa yule mwanajeshi alikuwa na mwili mdogo yeye ilimfaa. Lakini yeye alihitaji lita kumi za hayo maji kila siku. Na tangu alipofika mitaa ya Keys alikuwa akiifuata hiyo ibada na ilikuwa ikimpa matokeo mazuri. Kila siku ilipohitimu saa kumi kamili angeitembelea baa hii na kukaa kwenye kona akinywa maji. Na alikuwa amejenga uraibu wa maji kama ilivyo pombe kwa mlevi.

Yule mwanaume alikuwa bado amesimama akishushia kinywaji chake kukata kiu huku akizungusha macho kama kutafuta uamuzi akae wapi. Ukitoa mhudumu, Reacher tu ndiye aliyekuwemo baani humo. Yule mwanaume akainua bia yake kama ishara ya kumwomba Reacher wakae pamoja. Reacher alitikisa kichwa. Yule mwanaume alisogea kuketi. Alipokaa akaanzisha mazungumzo.

"Wewe ndiyo Jack Reacher?" Aliuliza.

Hakuwa mtu wa Chicago. Alikuwa ni mtu wa New York. Sauti na lafudhi yake vilimfanya Reacher agundue hilo.

"Jack Reacher?" Aliuliza tena.

Kwa ukaribu, macho yake yalionesha ana maswali mengi. Reacher hakujibu baadala yake alichukua chupa yake na kupiga funda la maji.

"Wewe ni Jack Reacher?" Yule mwanaume aliuliza tena kwa mara ya tatu.

Reacher aliishusha chupa yake mezani halafu akatingisha kichwa chake.

"Hapana." Alidanganya.

Mabega ya yule mwanaume yakashuka chini. Akanyanyua mkono wake kutazama muda halafu akanyanyuka, lakini akarudi kukaa kama vile muda ulikuwa umemwambia aendelee kukaa.

"Saa kumi na moja tayari." Alisema.

Reacher akatikisa kichwa kukubali. Yule mwanaume akamuoneshea mhudumu chupa kama ishara ya kuomba aongezewe kinywaji.
"Joto," Alisema baada ya mhudumu kuondoka. "Kuna joto sana."

Reacher akatikisa kichwa chake kukubali halafu akapiga fundo lingine la maji.

"Unaweza ukawa unamfahamu mtu anaitwa Jack Reacher mitaa hii?" Yule mwanaume aliuliza.

Reacher akaguna. "Unaweza ukamwelezea muonekano wake labda nitamjua kwa kumuona ila sio kwa jina."

Yule mwanaume alikuwa anapiga funda refu la bia yake. Alipoishusha chupa akajifuta mdomo wake.

"Sina kwa hakika," Alianza kuongea. "Ninachofahamu ana mwili mkubwa na ndiyo maana nikahisi ni wewe."

Reacher alitikisa kichwa na kuongea, "Kuna watu wengi wenye miili mikubwa kuliko hata mimi kila sehemu."

"Lakini hata jina hujawahi kulisikia?"

"Ni lazima niwe nimelisikia?" Reacher aliuliza.

Yule mwanaume akaguna.

"Naitwa Costello," alijitambulisha kama kukwepa swali aliloulizwa kuepusha makubwa. "Nafurahi kukutana na wewe."

Reacher alitikisa kichwa na kuinua chupa yake na kuonesha alama ya cheers na kuanza kuongea, "Unafanya kazi ya kutafuta watu wanaotoroka?"

"Hapana, Mimi ni mpelelezi wa kujitegemea." Costello alisema.

"Na unamtafuta mtu anaitwa Reacher?" Reacher aliuliza. "Amefanya nini?"

Costello akainua mabega, "Hakuna alichokifanya. Nimepewa tu maelekezo ya kumtafuta."

"Na unahisi yupo huku?"

"Wiki iliyopita alikuwepo huku," Costello alianza kuelezea. "Anayo akaunti ya benki Virginia na amekuwa akituma hela huko."

"Kutokea huku Key West?"

Costello akatingisha kichwa kukubali, "Kila wiki kwa muda wa miezi mitatu sasa."

"Kwahiyo?"

"Kwahiyo anafanya kazi huku," Costello alisema. "Amekuwa akifanya kazi huku kwa miezi mitatu. Unahisi kuna mtu anaweza akawa anamfahamu?"

"Sidhani." Reacher alijibu.

Costello akatikisa kichwa kukataa, "Nimeuliza kuanzia Duval, ambako ndiyo pamechangamka na kwa bahati nzuri nikakutana na msichana mmoja kwenye bar f'lani akaniambia kuna mtu mwenye sifa hizo nilizokuambia na huwa anakunywa maji hapa kwenye baa hii kila saa kumi." Halafu akakaa kimya huku akimuangalia Reacher machoni kama anayetangaza pambano. Reacher akapiga funda lingine la maji halafu akamtazama Costello machoni pia.

"Sadfa." Reacher alisema.

Costello akatikisa kichwa na kuongeza, "Nadhani."

"Unajua kuna idadi kubwa ya watu wanaoingia na kutoka hapa Keys kila leo. Ni ngumu kujua nani ni nani." Reacher alisema.

"Nadhani." Costello alijibu.

"Lakini nitakuwa macho na masikio wazi." Reacher alisema.

"Nitashukuru sana."

"Kwani anatafutwa na nani?"

"Mteja wangu," Costello alisema. "Mwanamke mmoja anaitwa Mrs Jacob."

Reacher akapiga fundo la maji. Jina la Mrs. Jacob halikuwa na maana yeyote kwake. Jacob? Hakuwahi kusikia au kukutana na mtu mwenye jina hilo.

"OK, Kama nitapata fununu au kukutana naye nitamwambia, lakini usinitegemee sana kwasababu sikutani na watu wengi." Reacher alisema.

"Unafanya kazi gani?"

"Nachimba bwawa za kuogelea." Reacher alijibu.

Costello akawa kama anayetafakari kama mtu aliyejua bwawa za kuogelea ni nini lakini hakujua kwanini watu wa huku waliyahitaji.

"Unaendesha mitambo ya kuchimbia, sio?"

Reacher akatabasamu na kutingisha kichwa kukataa. "Huku tunachimba kwa mikono."

"Kwa mikono?" Costello aliuliza kwa mshangao. "Na koleo au?"

"Ndiyo." Reacher alijibu.

Costello akatikisa kichwa kama aliyeridhika na majibu na kuongeza, "Basi kwa hakika huwezi kumfahamu huyu Reacher. Kwa mujibu wa maelezo ya mteja wangu, Jamaa alikuwa ni mwanajeshi na nimeangalia nikakuta ni kweli. Medani za kutosha tena polisi wa wanajeshi mkubwamkubwa. Mtu kama huyo huwezi kumkuta anachimba mabwawa ya kuogelea tena kwa mikono."

Reacher akapiga funda lingine la maji ili kuficha msisimko wake. "Kwahivyo utamkuta anafanya nini?"

"Kwa huku?" Costello alianza kueleza. "Sina uhakika. Pengine atakuwa mkuu wa ulinzi kwenye hoteli kubwa au anafanya biashara."

"Wewe unahisi kwanini kati ya sehemu zote achague kuja huku?"

"Inashangaza," Costello alijibu. "Huku ni kuzimu, lakini ndiko aliko. Hilo halina ubishi. Aliachana na jeshi miaka miwili iliyopita akaweka pesa zake karibu na Pentagon halafu akapotea. Kuanzia hapo akawa anatoa hela karibu kila sehemu unayoijua halafu ghafla miezi mitatu iliyopita ameanza kuweka pesa kutokea huku. Hiyo inamaanisha amezunguka sana ameamua atulie hapa. Nitampata tu."

Reacher akatikisha kichwa. "Unahitaji msaada wangu kumtafuta?"

Costello akatingisha kichwa. "Usijali," Alisema halafu akanyanyuka kutoka kwenye kiti. Akawekwa pesa ya bili inayodaiwa mezani na kuanza kuondoka.

Reacher alimtazama akiondoka. Maongezi yao yalikuwa yametumia dakika 15.

Lisaa limoja baadae Reacher alikuwa anakatisha mitaa ya Duval huku maswali matatu yakiwa kichwani mwake. Kwanza ni atumie mkakati upi ili kuondoa taarifa zake za benki kupatikana kwa urahisi. Pili alikuwa anajiuliza ni wapi atapata chakula cha jioni mapema na akikipata atakula nini. Na tatu alikuwa akijiuliza ni kwanini alimuongopea Costello. Haikumchukua muda akapata majibu ya maswali yake. Kwanza kuanzia muda ule na kuendelea asingetumia tena benki kuhifadhi pesa hata kama iwe nyingi kiasi gani. Pili ni kwamba angeenda kwenye mgahawa wake wa kila siku na kufuata ushauri wa mwanajeshi mmoja kuhusu chakula kwa jioni hiyo. Swali la tatu jibu lake lilikuwa rahisi: Alimdanganya Costello kwa sababu hakukuwa na sababu ya kuacha kumdanganya.

Pia hakuwa na sababu kwanini mpelelezi kutoka New York awe anamtafuta. Hakuwahi kuishi New York. Au miji yeyote ya kaskazini. Au kuiweka sahihi, hakuwahi kuishi mahali popote. Hiyo ndiyo ilikuwa moja ya maana ya maisha yake. Ndiyo sababu mojawapo kati ya nyingi iliyomfanya awe alivyo. Alikuwa amezaliwa kwa Afisa wa jeshi la maji na alikuwa ametembea sehemu tofautitofauti tangu siku ambayo alitoka kwenye tumbo la mama yake katika hospitali moja huko Berlin. Hivyo maisha yake yote yalikuwa ni ya kwenye kambi tofautitofauti za jeshi. Alipokuwa akajiunga na jeshi hadi kuwa polisi wa wanajeshi na akaishi na kuhudumu kwenye kambi zilezile hadi mkataba wa amani uliposainiwa na jeshi likapunguza idadi ya watu ikiwemo yeye mwenyewe. Akaamua kurudi Amerika kuzungukazunguka kama mtalii asiye na hela za kutosha hadi alipofika chini kusini huku hela alizotegemea zikiwa zinaenda kuishi. Akaamua atafanya kazi kwa siku chache. Siku chache zikawa wiki na wiki ikawa miezi na bado alikuwa yupo hadi alipotokea Costello.

Hakuwa na ndugu wala jamaa mahala popote. Hakuwa akidaiwa na mtu yeyote. Hakuwahi kuiba, au kusema uongo. Alikuwa ni kama kiumbe kisichoonekana. Na kwenye maisha yake hakuwahi kufahamiana na mtu anaitwa Jacob. Hilo alikuwa na uhakika nalo. Hivyo alichohitaji Costello yeye kilikuwa hakimhusu.

Yote hii ilikuwa ni kwa sababu kutokutambulika ilikuwa imekuwa kama jadi yake na ilikuwa imemkaa kwenye ubongo wake wa mbele. Miaka miwili iliyopita kila kitu kiligeuka chini juu. Alibadilika kutoka kuwa papa hadi kuwa si chochote kwenye bahari. Kutoka kuwa kiongozi mkubwa na aliyeheshimika kwenye jamii ya wanajeshi hadi kuwa mmoja kati ya raia milioni miambili na sabini wasiojulikana. Hisia zake zilimwambia ni jambo la ajabu lakini kuna muda nafsi yake ilifurahia hio hali. Alipenda kutokujulikana. Ilimpa kujiamini na uhakika f'lani kama bima. Kila alipokutana na watu aliweka ucheshi na urafiki nao bila kusema mengi kuhusu yeye mwenyewe. Alikuwa ni mtu wa kulipa Cash na usafiri wake ulikuwa ni barabarani. Hakuna ndege wala cheki. Hakuwahi kumwambia mtu yeyote jina lake. Hata alipofika West Key alijitambulisha kama Harry Truman kwenye nyumba ya kulala wageni alipopanga chumba. Na kwavile West Key hawakujali nani ni nani alivutiwa napo. Akavutiwa kiasi cha kusahau alikuwa anatakiwa aondoke.

Alizunguka mtaani kwa muda wa lisaa limoja hadi akafika kwenye mgahawa alipozoea kula chakula.
Sahani ya chakula chake ililetwa na mhudumu ikiwa na nyama, mayai na mchanganyiko wa mboga za majani. Baadae ililetwa Ice cream ya chocolate na karanga. Alipomaliza kuila akanywa vikombe viwili vya kahawa kama kitindamlo na kushushia maji chupa mbili za lita mojamoja.

"Hapo safi?" Aliuliza mhudumu huku akitabasamu aina la tabasamu wanalotoa wafanyabiashara pale unapowapa hela.

"Imenishuka kunako kabisa." Reacher alijibu.

"Naona."

"Ndiyo. Najisikia vizuri sasa."

Na ilikuwa ni kweli. Siku yake ya kuzaliwa iliyokuwa inafuata ingemfanya awe na miaka 39, lakini bado alikuwa imara na mwenye nguvu. Hili lilimfanya ajisikie vizuri.

"Usiku unaenda kazini?" Yule mhudumu aliuliza.

Reacher akatabasamu. Alikuwa anafanya kazi nyingi. Ukitoa kuchimba bwawa za kuogelea, aliwafundisha watu pia mazoezi na usiku alifanya kazi ambayo wanaume wengi wangefurahi kuifanya bure kabisa. Alikuwa ni mlinzi kwenye baa moja ya maonesho ya utupu wa wanawake. Kazi yake ilikuwa ni kusimama akiwa kifua wazi, akinywa vinywaji vya ofa vya bure huku akihakikisha wanawake waliokuwa watupu hawabugudhiwi na mtu yeyote. Na mwisho wa siku angepewa dola hamsini.

"Ndiyo," Reacher alijibu. "Ninaenda."

Yule mhudumu akacheka. Reacher alinyanyuka akalipa hela yake na kuingia mtaani tena kuelekea bar alikokuwa akifanyia kazi ambako kuna jambo lilikuwa linamsubiria.

SEHEMU YA PILI BOFYA HAPA
 
Sawa ndugu ninafuatilia
Naash Nash

Sent from my TECNO-L5 using JamiiForums mobile app
 
SEHEMU YA PILI
Takribani maili 15 kaskazini kutoka alipokuwepo Reacher, chini ya jengo moja kubwa jijini New York, Mkurugenzi mkuu wa kampuni moja alikuwa amepanda lifti kuelekea ilipokuwa ofisi ya Mkurugenzi wa fedha. Wanaume hawa wawili waliingia kwenye ofisi ya ndani na kusimama nyuma ya meza kubwa. Ilikuwa ofisi ya kifahari na samani zake zilikuwa ni za gharama pia. Ilikuwa imesheheni mapambo ya kila namna ikiwemo michoro maarufu kutoka Italia na sehemu nyingine nyingi. Mezani kulikuwa na Kompyuta kubwa ambayo iligharimu pesa kubwa kuliko ilivyopaswa. Kompyuta yenyewe ilikuwa inawaka ikisubiri kuingiziwa nywira. Mkurugenzi mkuu aliandika maneno kwa kicharazio halafu akabonyeza kitufe cha enter na skrini ikafungua jedwali kubwa kama kutii amri. Lilikuwa ni jedwali lililobeba ukweli wote kuihusu kampuni na ndiyo maana lilitunzwa kwa nywira.

"Unadhani tutafanikiwa?" Mkurugenzi mkuu alihoji.

Hiyo ilikuwa siku ya kufanya maamuzi magumu. Siku ya kupunguza wafanyakazi. HR wa kampuni naye alikuwa bize tangu asubuhi akionana na huyu na yule na kumpa maneno ya asante na kwaheri.

"Unadhani tutafanikiwa?" Alihoji tena baada ya ukimya kidogo.

Sio kwamba mkurugenzi wa fedha hakumsikia, hapana. Alikuwa anaandika tarakimu kubwakubwa kwenye karatasi iliyokuwa mkononi mwake. Alikuwa akitoa na kujumlisha moja baada ya nyingine. Alipomaliza akainua macho kuitazama kalenda halafu akakunja uso.

"Kwa nadharia inaonesha tutafanikiwa." Alianza kuongea. "Lakini kiuhalisia haiwezekani."

"Haiwezekani?"

"Ndiyo. Muda unatubana," Mkurugenzi wa fedha alianza kueleza ili bosi wake huyo amuelewe. "Ni kweli tunafanya jambo zuri kupunguza watu kwa asilimia 80 na hilo litatuokolea pesa nyingi ukizingatia hata tuliowaacha ni wale ambao wanapokea mshahara kidogo. Lakini tuliowafukuza tumewalipa mafao yao hadi mshahara wa mwezi ujao. Kwahivyo mtiririko wa fedha hautakaa vizuri hadi muda wa wiki sita zijazo."

Mkurugenzi akaguna na kuuliza, "Kwani tunahitaji kiasi gani cha pesa?"

Mkurugenzi wa fedha akashika kielekezi cha kompyuta na kubonyezabonyeza hadi lilipofunguka jedwali lingine ndipo akaongea "Dola milioni moja nukta moja," alisema na kuongeza, "Ndani ya wiki sita."

"Benki hawawezi kutupatia hio hela?"

"Sahau," Mkurugenzi wa fedha akafoka kidogo. "Tunalo deni kubwa tu ambalo bado hatujalilipa sasa tukienda kuomba tena mkopo watatucheka."

"Lakini kuchekwa ni bora kuliko...."

Hakumaliza kauli yake Mkurugenzi wa fedha akamuingilia, "Pointi siyo hiyo. Pointi ni kwamba watagundua hatuko vizuri kwa sasa na wataomba tuwalipe madeni yao muda huohuo."

Mkurugenzi mkuu akaishika meza kwa nguvu, "Nitauza baadhi ya hisa." Alisema.

"Bado haiwezekani," Mkurugenzi wa fedha alionya. "Ukiziweka hisa sokoni bei itashuka muda sio mrefu na mikopo yetu yote inategemea hizo hisa. Hiyo inamaanisha hisa hazitakuwa na thamani tena na mabenki yatakuja kutufirisi muda sio mrefu."

Mkurugenzi mkuu akawa kama anatafakari jambo. Ukapita ukimya kidogo kabla hajaongea tena, "Sitakubali kupoteza kila kitu kwa sababu ya dola milioni moja tu. Haiwezekani. Hiyo pesa ni kidogo sana."

"Pesa kidogo ambayo hatuna."

"Tukitafuta hatuwezi kukosa."

Mkurugenzi wa fedha hakujibu chochote. Lakini uso wake ulionesha kama kuna jambo alitaka kusema.

"Unawaza nini?" Mkurugenzi mkuu aliuliza kama aliyeyasoma mawazo ya Msaidizi wake.

"Kuna maongezi nikiyasikia pahali fulani," Mkurugenzi wa fedha alianza kuongea "Kuna jamaa anatoa mkopo wa dharura - dakika za kufa na kupona. Tunaweza kwenda kujaribu."

"Anaaminika?"

"Kwa nilivyosikia naweza kusema ndiyo. Jamaa ana wadhifa na ofisi yake ipo kwenye jengo la WTC na ndiyo shughuli zake."

Mkurugenzi Mkuu akamtazama mkurugenzi wa fedha kama ambaye hajaelewa. "Shughuli zipi?"

"Kama hizi," Mkurugenzi wa fedha alieleza. "Wakati ambao unaenda kufilisika na mabenki hayajali."

Mkurugenzi alitikisa kichwa na kuanza kuzungusha macho kuitazama ofisi ile. Ilikuwa ofisi nzuri. Yeye mwenyewe ofisi yake ilikuwa ghorofa ya juu ya hii mkono wa kulia na ilikuwa nzuri zaidi. Kuvipoteza ingekuwa fedheha kubwa sana.

"Sawa," Alisema baada ya tafakari kidogo. "Onana naye atupatie hiyo fedha."

"Mimi siwezi kuonana naye. Jamaa huwa hadili na wafanyakazi au wanabodi, ila wakurugenzi tu. Itakubidi wewe ndiye uende ukamuone."

SEHEMU YA TATU BOFYA HAPA
 
SEHEMU YA TATU:
Ulikuwa ni usiku mtulivu kwenye baa aliyolinda Jack Reacher. Pengine kwasababu ilikuwa ni katikati ya wiki na watu hawakuwa wengi. Kama wangehesabiwa basi idadi yao isingevuka arobaini. Kulikuwa na wasichana wawili nyuma ya kaunta na wengine watatu wakichezacheza kuwaburudisha wateja. Baa yenyewe ilikuwa ni ghorofa ya pili. Yeyote aliyetaka kuingia ilimbidi apande ngazi kutokea chini kwanza. Reacher alikuwa akimtazama msichana mmoja aliyeitwa Crystal. Kuna muda alihisi hilo halikuwa jina lake halisi, lakini hakuthubutu kumuuliza. Hii ilikuwa ni Key West na watu hawakushughulika na majina ya watu wengine. Crystal alikuwa akiingiza kiasi kikubwa cha pesa kuliko mshahara aliokuwa akilipwa Reacher kwa mwezi alipokuwa jeshini. Na Crystal alijipenda hivyo alijizawadia gari aina ya Porsche.

Reacher alikuwa amesimama karibu na mlango wa kuingilia ndani ya baa sehemu ambayo ilimruhusu kila anayeingia amuone na kwa wale waliokuwa ndani wasimshahau. Kwa pale alipokuwa amesimama aliona wanaume wawili wakiwa wamefika kwenye mlango wa kuingilia baa. Walionekana wametokea kaskazini. Umri zao zilikuwa kwenye miaka ya thelathini. Walikuwa wamevaa suti na viatu vya gharama kubwa. Ni kama walikuwa wamekuja huku kwa ghafla na kwa kazi ya haraka. Walikuwa wamesimama wakibishana na mtu wa kuuza tuketi mlangoni. Reacher alisogea kuona kilichokuwa kinaendelea.

"Kuna tatizo?" Aliuliza.

Hayo maneno mawili mara nyingi yalitosha kuwaogopesha wanaume wengi wakorofi, Lakini hawa wawili hawakushtuka hata kidogo. Ni kama walikuwa na mchanganyiko wa kujiamini na kiburi. Ni kama walifanya walichotaka kwa namna waliyotaka wao. Lakini pia walikuwa wapo ugenini na ukiwa ugenini baadhi ya tabia zako unaziweka kando.

"Hakuna tatizo, Tarzan." Jamaa aliyekuwa amesimamia mkono wa kushoto aliropoka.

Reacher alitabasamu. Alikuwa ameitwa majina mengi ya ajabu, lakini Tarzan lilikuwa jipya kwake. "Kama unataka kuingia utalipia dola 3 kwa kila kichwa au muondoke maana kukaa nje ni bure kabisa."

"Kuna mtu tunataka kuongea naye haraka tu." Jamaa wa kulia alijibu.

Namna walivyoongea ilionesha wote ni watu wa New York. Reacher akainua mabega.

"Sauti ya muziki ni kubwa humu ndani sidhani kama mtu wenu mtaelewana." Reacher alisema.

"Jina lako ni nani?" Jamaa wa mkono wa kushoto aliuliza.

"Tarzan." Reacher alijibu.

"Tunamtafuta mtu anaitwa Reacher," Jamaa wa kulia alisema. "Jack Reacher. Unamfahamu?"

Reacher akatikisa kichwa chake kukataa. "Sijawahi hata kulisikia hilo jina."

"Basi tunaomba uturuhusu tuongee na wahudumu wa hapa, tumeambiwa wanaweza wakawa wanamfahamu."

Reacher akatikisa kichwa tena kukataa. "Hapana hawamjui."

"OK, Bwana Tarzan, tunapita kwa nguvu." Jamaa wa kulia alisema.

"Unajua kusoma?" Reacher alimuuliza huku akisonta kibao kikubwa kilichokuwa kimening'inizwa kikisomeka 'UONGOZI UNAYO HAKI YA KUKUBALI AU KUKATAA MTU KUINGIA NDANI.'

"Mimi ndiyo uongozi," Reacher alisema baada ya kuridhika kuwa wamesoma kilichoandikwa. "Na nimekataa kukuruhusu kuingia."

Yule jamaa wa kushoto alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi.

"Unataka nikutafsirie iwe katika lugha nyepesi?" Reacher alimuuliza. "Hiyo inamaanisha mimi ndiye bosi hapa na sitaki kukuona."

"Acha kelele, Tarzan." Jamaa wa kulia alijibu huku akianza kupiga hatua kuingia ndani. Reacher alimsubiri hadi walipokaribiana bega kwa bega halafu akainua mkono wake wa kushoto na kushika kiwiko cha yule jamaa kwa kasi ya ajabu kama radi akawa anakikandamiza kwa nguvu zake zote. Yule jamaa alianza kuruka kama anayepigwa shoti.

"Ondokeni," Reacher alimnong'oneza masikioni.

Yule jamaa mwingine alikuwa anapiga hesabu ya nafasi za kushambulia alizonazo. Reacher aliligundua hilo hivyo akainua mkono wake wa kulia uliojengeka vizuri - Ulikuwa mkono mkubwa na yule jamaa alipata ujumbe uliokusudiwa asithubutu ujanja wowote. Reacher alipomuachia yule jamaa walianza kuondoka.

"Tutaonana tena muda sio mrefu, Tarzan." Jamaa aliyekuwa amebanwa mkono alisema.

"Ukija tena ukumbuke kuwaalika marafiki zako wote," Reacher alimjibu. "Msisahau kuja na dola tatutatu za kiingilio kwa kila kichwa."

Alipohakikisha wametoka kabisa akaanza kurudi alipokuwa amekaa. Alipogeuka akakutana uso kwa uso na Crystal.

"Walikuwa wanataka nini?" Crystal aliuliza.

"Kuna mtu wanamtafuta."

"Reacher?"

Reacher alitingisha kichwa kukubali.

"Hii ni mara ya pili," Crystal alisema baada ya ukimya kidogo. "Kuna mzee mmoja pia alikuja anamtafuta Reacher. Unatakiwe uwafuatilie ujue wanataka nini?"

Reacher alisita. Crystal alikuwa ameshika shati lake akampatia mkononi. "Nenda," Crystal alisema. "Sisi tutakuwa sawa kwa usiku wa leo hata usijali."

Reacher alilipokea shati lake na kuanza kuligeuza.

"Asante, Crystal." Alisema huku akilivaa shati lake na kuanza kuzifuata ngazi kushuka chini.

"Usijali, Reacher." Crystal alijibu.

Key West majira ya saa tano usiku inakuwa imechangamka sana. Kuna baadhi ya watu wanakuwa ndiyo wamemaliza siku yao, lakini wengi ndiyo kwanza wanaianza. Duval ndiyo mtaa mkubwa na ulikuwa umepambwa kwa mwanga na kelele. Hivyo Reacher hakuwa anawahofia wale jamaa wawili. Kama wangetaka kumlipizia kisasi basi lazima wangechangua eneo lisilo na mashahidi wengi.

Hivyo alianza kutembea kwa kasi kutafuta maeneo yasiyokuwa na mkusanyiko wa watu kuona kama atawabahatisha huko. Baada ya mwendo wa kujifichaficha akaingia katikati ya barabara ili kuruhusu kuonekana. Hakuwa anahofia kupigwa risasi kwa sababu wale jamaa hawakuwa na bunduki. Suti zao zilikuwa zimemthibitishia hilo. Zilikuwa zimewabana kiasi cha kutowaruhusu kuficha bunduki na pia walionekana ni watu waliokuja kusini kwa haraka na ingekuwa vigumu kuambatana na bunduki kwenye ndege kwa ghafla.

Baada ya mwendo mrefu alikata taamaa ya kuwaona. Ni kweli Duval ilikuwa mji mdogo, lakini kubwa sana kuhifadhi watu wawili. Alikata kona ya kwanza na ya pili. Alipoingia barabara la upande mwingine aliona kitu cha ajabu. Aliona mtu akiwa amelala barabarani. Haikuwa kawaida ya watu wa Keys kulala barabarani. Pamoja na hayo kulikuwa na mambo mengine mawili: Jambo baya na jambo zuri.

Jambo baya ni kwamba mkono wa yule jamaa ulikuwa haueleweki kwa staili uliyokuwa umekaa. Jambo zuri ni kwamba Reacher alizifahamu nguo alizokuwa amevaa yule mtu aliyelala. Koti la kijivu na suruali nyepesi ya kijivu. Reacher aliangalia kuona kama kuna mtu alikuwa anamtazama. Aliporidhika hakukuwa na mtu alianza kutembea kwa hadhari kuelekea yule mtu alipokuwa amelala.

Alikuwa ni Costello na hakuwa amelala. Alikuwa amekufa! Uso wake ulikuwa umejaa damu kama uliochunwa ngozi. Reacher alikadiria alikuwa amekufa kwa zaidi ya lisaa limoja lililopita.

Hapo aliingiza mkono kwenye mifuko ya koti la Costello. Hakukuta kitu chochote. Hata ile waleti aliyomuona nayo kule baa haikuwemo.

Akamgeuza kwa nyuma kuangalia mikono yake. Hapo aliona kitu kingine cha ajabu. Mikono yote miwili ilikuwa imekatwa vidole vyote kumi. Ilionesha waliofanya hii kazi walitumia kisu chenye makali kama ya nyembe mpya iliyotoka kiwandani na walijua kwa hakika walichokuwa wanakifanya.

Reacher akajua shughuli imeanza. Lakini hakujua ni shughuli ipi!

SEHEMU YA NNE
 
SEHEMU YA NNE
"Najihisi nina hatia," Reacher alisema.

Crystal alitikisa kichwa chake kama ishara ya kupinga. "Sio wewe uliyemuua," Aliongea kumfariji Reacher.

"Ni kweli, lakini nimesababisha kifo chake," Reacher alisema na kuongeza. "Sioni kama kuna utofauti hapo."

Baa ilikuwa imefungwa na ndani walikuwa wamekaa Reacher na Crystal tu. Hakukuwa na taa zinazowaka wala mziki wala sauti yeyote isipokuwa muungurumo wa kiyoyozi kilichokuwa kinafukuza hewa ya jasho iliyoachwa na wanywaji waliokuwa wameondoka.

"Tatizo nilimdanganya," Reacher alianza kuongea tena. "Pengine kama ningemwambia ukweli ningeyaokoa maisha yake. Angefahamu ni mimi angeondoka na asingeendelea kubakia hadi kuuawa."

Crystal alikuwa amevaa tisheti nyeupe ndefu iliyofunika mapaja yake. Hakuwa amevaa kitu kingine isipokuwa hiyo tisheti.

"Kwanini unajihangaisha na kosa ambalo siyo lako?"

Lilikuwa ni aina ya swali la watu wa Keys. Aina ya watu ambao walikuwa hawajali mambo ya watu wengine.

"Kwasababu najihisi nina hatia kwa namna moja au nyingine," Reacher alisema.

"Hapana hupaswi kusema hivyo," Crystal alimfariji tena. " Sio wewe uliyemuua."

"Hata nisiposema haileti utofauti wa ninavyojisikia. Au kuna tofauti?" Reacher alimuuliza.

"Ndiyo. Tena tofauti kubwa sana," Crystal alijibu. "Kwani yeye alikuwa ni nani?"

"Aliniambia ni mpelelezi wa kujitegemea na alikuwa ananitafuta mimi." Reacher alisema.

"Alikuambia kwanini anakutafuta?"

Reacher alitikisa kichwa kukataa. "Hapana na mimi pia sijui kwanini!"

"Na wale jamaa wawili je? Ni wenzake?" Crystal aliuliza tena.

"Hapana," Reacher alianza kueleza. "Wale jamaa wawili ndiyo waliomuua."

Crystal alimtazama kwa jicho la mshangao na hofu. "Umejuaje?"

"Ni hisia tu," Reacher alianza kueleza. "Wale hawakuwa wenzake kwa sababu hata mionekano yao ni tofauti kabisa. Suti zao zilikuwa za gharama lakini nguo zake zilikuwa za bei ya kawaida tu. Na ninahisi pia walikuja kumfuatilia na katika kumshughulisha ndiyo akataja alikuwa amekuja kumtafuta mtu anaitwa Reacher na wao ndiyo wakaanza kumtafuta."

"Itabidi uwashirikishe polisi." Crystal alishauri.

Reacher alitikisa kichwa kukataa.

"Usiporipoti kwao watachunguza halafu watakuja kukutafuta wewe kama mhusika wa mauaji."

"Sio leo wala kesho," Reacher alisema. "Jamaa hana kitambulisho chochote wala alama za vidole. Mpaka wanakuja kugundua alikuwa nani na alifuata nini muda utakuwa umeenda sana."

"Kwahivyo utalipotezea hili suala kama hakijatokea kitu."

"Hapana;" Reacher alisema. "Naenda kumtafuta Mrs. Jacob aliyemtuma Costello."

"Unamfahamu?"

"Simfahamu, lakini nitampata."

"Kwanini?"

"Nahitaji kujua nini kinaendelea." Reacher alijibu.

"Kwanini?" Crystal aliuliza tena.

"Kwasababu kuna mtu kafa kwaajili ya jina langu. Hicho ndicho kinanifanya nihusike."

"Lakini utaanzia wapi na humjui hata huyo Mrs. Jacob?"

"Nitaanzia ofisini kwa kwa Costello," Reacher alisema. "Pengine katibu muhtasi wake anaweza kuwa na msaada."

"Unafahamu ofisi yake ilipo?"

"Sijui," Reacher alisema na kuongeza. "Lakini nahisi ni New York kutoka na lafudhi ya Costello ilivyokuwa. Na kwakuwa nalifahamu jina lake na ninafahamu alikuwa ni askari mstaafu sidhani kama itakuwa ngumu kumpata."

"Alikuwa polisi mstaafu?" Crystal aliuliza. "Umefahamu vipi?"

"Wapelelezi wanaojitegemea wote huwa ni polisi wastaafu, hiyo ni moja ya sharti la kuwa mpelelezi wa kujitegemea." Reacher alisema.

Crystal alitabasamu kwa mshangao. Alikuwa amevutiwa na namna Reacher alivyofahamu mambo mengi. Ili kuridhisha udadisi wake akamuuliza Reacher, "Umeyajuaje haya unayonieleza?"

"Mimi nilikuwa mpelelezi," Reacher alisema. "Nilikuwa polisi wa wanajeshi kwa miaka kumi na tatu na niliiweza shughuli."

"Usijisifu. Acha watu wakusifu." Crystal alitania. "Unategemea kuanza kufuatilia hili suala lini?"

Reacher aliyazungusha macho yake mule ndani halafu akamtazama Crystal. "Sasa hivi. Natakiwa niende Miami nikapande ndege ya New York."

"Utafika vipi Miami usiku huu na hakuna magari," Crystal aliuliza.

Reacher alitabasamu halafu akaongea kwa kujiamini, "Utanipeleka kwa gari lako."

"Ngoja nibadilishe nguo kwanza."

"Hiyo uliyovaa ipo sawa. Twende."

Waliongozana kwenda hadi sehemu ya maegesho ilipopaki gari ya Crystal. Reacher alifungua milango wakaingia ndani na Crystal akaanza kuyakanyaga mafuta. Walizipita barabara za Key West na Reacher muda wote aliifurahia safari yake. Crystal naye alikuwa akitabasamu kimyakimya kwa namna alivyoimudu gari kwa ufasaha kutoka sehemu moja hadi nyingine na hatimaye walifika uwanja wa ndege.

"Nashukuru kwa lifti." Reacher alisema.

Crystal alitabasamu, "Nafurahi pia kukubeba."

Reacher alifungua mlango na kutoka nje. "OK," Alisema. "Tutaonana tena."

Crystal alitikisa kichwa kukataa. "Mimi sio mtoto mdogo," Alisema. "Watu wa hirimu yako huwa hawarudi wakiondoka."

Reacher alitabasamu na kuinama dirishani kilipo kichwa cha Crystal. Hapo walibusiana kwenye midomo yao na kukaa hivyo kwa dakika tano. Walipoachiana Crystal alikuwa wa kwanza kuongea.

"Kwaheri, Reacher." Alisema. "Nafarijika hatimaye nimelifahamu jina lako la kweli."

"Mimi pia nitafarijika nikilifahamu la kwako?" Reacher alisema.

"Crystal." Crystal alisema na kucheka. .

Reacher alicheka pia halafu akainuka kutoka dirishani. Crystal akalitia moto tena gari lake na kuondoka akimuacha Reacher akiliiangalia gari lilivyomezwa na umbali. Lilipoondoka kabisa kwenye macho yake akajua anayo shughuli mbele yake.

SEHEMU YA TANO
 
SEHEMU YA TANO
New York, takribani maili hamsini kutoka alipokuwa amesimaa Reacher, Yule mkurugenzi mkuu alikuwa amelala kitandani. Hakuwa amefumba macho. Alikuwa anatazama dari la nyumba yake iliyokuwa imepigwa rangi siku sio nyingi. Alikuwa amewalipa wapaka rangi hela nyingi kwa kazi ya masaa kumi tu kuliko hela aliyowalipa baadhi ya wafanyakazi wake kwa mwezi. Kiuhalisia sio yeye aliyekuwa amelipa hela. Kampuni ndiyo iliyokuwa imelipa hela huku ikiainishwa ni gharama za matengenezo ya majengo ya kampuni. Kufanya hivyo kuliirudhuru kampuni kama mzigo mzito unavyoweza kuzamisha meli.

Jina lake lilikuwa ni Chester Stone. Jina la baba yake lilikuwa ni Chester Stone. Na jina la babu yake lilikuwa ni Chester Stone. Babu yake ndiye aliyeanzisha biashara ya kampuni yao miaka mingi iliyopita kipindi ambacho hesabu zilikuwa zinafanywa kwa mkono na sio kikokotoo au kompyuta. Yeye alikuwa ni fundi saa tu ambaye alibahatika kuiona fursa iliyokuwepo kwenye kiwanda cha filamu. Aliutumia ujuzi wake kuanza kutengeneza projekta za kutumika kwenye kumbi za sinema. Halafu akatafuta watu wa kusaidiana nao. Kwa pamoja wakaliteka soko na kutengeneza hela nyingi sana. Wakauza Projekta mamia kwa mamia. Kwenye kitabu cha mapato na madeni, Jedwali lilionesha mapato yalikuwa makubwa kuliko madeni.

Halafu Chester wa kwanza akafa na teknolojia yake. Zikavumbuliwa televisheni. Sinema zikakosa masoko na wateja wa projekta wakawa wachache. Lakini Chester wa pili alikuwa na akili hivyo akalisoma soko pia na kuendana nalo. Faida ikawa maradufu na mpaka wakati anafariki hadi Chester wa tatu kuchukua mikoba kampuni ilikuwa katika hali nzuri. Utajiri na mafanikio. Kufunga harusi ya kifahari. Kuhamia kwenye kasri na kununua magari ya kifahari. Huyo alikuwa Chester wa tatu. Na wakati wake zama zikabadilika tena. Ukaanza ushindani kutoka makampuni makubwa ya nchi kama Japan, Korea, Taiwan na Ujerumani. Soko lilikuwa linahitaji teknolojia ambayo Chester hakuwa anaifahamu...

Mke wake aligeukia upande wake. Akayafumbua macho yake na kugeuza kichwa kulia na kushoto. Kwanza kuangalia muda halafu kumuangalia mume wake ambaye alikuwa anashangaa dari.

"Haujalala tu?" Aliuliza kwa sauti ya upole na mshangao kwa pamoja.

Chester hakujibu. Mke wake akatazama pembeni. Jina lake lilikuwa Marilyn. Marilyn Stone. Alikuwa amefunga ndoa na Chester kwa siku nyingi sana. Siku nyingi sana kiasi cha kuelewa na kujua kila kilichoendelea. Alikuwa anajua kila kitu. Hakuwa na ushahidi au taarifa kamili, lakini alikuwa anajua. Ingewezekana vipi asijue? Alikuwa ni mwanamke mwenye akili na macho. Na ulikuwa umepita muda mrefu bila kuona bidhaa zinazotengenezwa na kampuni ya mumewe zikiwa kwenye maduka yeyote yale. Ulikuwa umepita muda mrefu bila wao kualikwa kwenye hafla yeyote kusherehekea mauzo au kupewa pongezi tu. Na ulikuwa umepita muda mrefu bila mume wake kulala usiku kwa amani. Hivyo alijua.

Lakini hakujali. Kwenye shida, kwenye raha ndicho kilikuwa kiapo chake. Na siku aliyoapa alimaanisha. Utajiri ulikuwa mzuri. Hivyo umaskini ungekuwa mzuri pia. Na hata hivyo sio kwamba wangekuwa maskini sana, hapana. Pia bado walikuwa ni vijana. Hawakuwa wadogo sana na wala hawakuwa wazee sana. Walikuwa na afya. Chester alikuwa bado na muonekano mzuri tu na walipendana. Na ni kweli Marilyn alikuwa na miaka arobaini, lakini aliamini kichwani mwa Chester umri wake ulikuwa ni miaka ishirini na kitu tu. Kila kitu kilikuwa sawa tu. Hakukuwa na haja ya kuwaza sana. Marilyn alivuta shuka lake akajifunima vizuri kulala. Ilikuwa ni saa kumi na moja na dakika tano alfajiri. Chester alikuwa bado yupo macho analitazama dari la nyumba yake.

SEHEMU YA SITA
 
Back
Top Bottom