Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,941
- 2,044
JINA: SENYENGE
MWANDISHI: CHIAMARO MOKIRI
MAWASILIANO: Chiamaro.llc@gmail.com / +255 (0)763 170 858
UTANGULIZI.
Maisha ya Hook Hobie yalikuwa na siri nzito aliyoificha kwa zaidi ya miaka thelathini. Uhuru wake, Wadhifa wake, Mali zake na kila kitu alichokimiliki kilitegemea siri yake hiyo. Na kama mtu yeyote aliye makini, Hook Hobie, alikuwa tayari kufanya lolote ili kuilinda siri yake. Kwasababu ingetokea ikavuja basi maisha yake yote yangekuwa yameharibika.
Njia aliyoitumia kuhakikisha siri yake hiyo haivuji kwa zaidi ya miaka thelathini ilitegemea mambo mawili - mambo ambayo kila mtu huyatumia kujilinda dhidi ya hatari. Mambo ambayo taifa huyatumia kujilinda dhidi ya maadui zake: Kuhisi na kuanza mwitikio. Hatua ya kwanza, hatua ya pili. Kwanza unalihisi tishio, halafu unaweka mwitikio.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni kama onyo kwake na ilikuwa ikibadilika mwaka hadi mwaka kutokana na mazingira yalivyobadilika. Ilihusisha tabaka mbili kama fensi mbili ziizungukayo nyumba. Fensi ya kwanza ilikuwa maili elfu kumi na moja kutoka nyumba ilipo. Hii ilikuwa ni kama onyo la kwanza. Ingemuambia adui zako wanakaribia kukufikia. Fensi ya pili ilikuwa maili elfu tano karibu na nyumba, lakini bado ingekuwa maili elfu sita kutoka fensi ya kwanza ilipo. Hii ingemuambia adui zako wapo karibu sana kukufikia. Ingemuambia hatua ya kwanza imeisha. Ingemuambia ni muda wa hatua ya pili.
Hatua ya pili ilikuwa ni mwitikio. Alikuwa amepanga vyema nini atafanya kipindi onyo la pili litakapofikiwa. Alikuwa ametumia karibu miaka 30 akifikiria, lakini kulikuwa na jibu moja tu sahihi - Mwitikio ungekuwa ni kukimbia. Kupotea kabisa. Yeye mwenyewe alikuwa ni mtu asiyeendeshwa kwa hisia bali tafakari kali. Na maisha yake yote alijivunia ujasiri na uthubutu wake. Kila ilipohitajika kufanyika jambo, kama lingekuwa na faida kwake, basi angelifanya bila kusitasita. Lakini alijua siku atakaposikia maonyo kutoka kwenye fensi alitakiwa kuondoka kwasababu hakuna mtu ambaye angeweza kuhimili kilichokuwa kinakuja. Hayupo. Hata yeye pamoja na ujasiri wake asingeweza.
Hatari ya siri yake kuvuja ilipita na kutambaa kama mawimbi kwa miaka mingi. Alikuwa akitumia muda mwingi akijua mambo yataharibika saa yeyote, lakini haikuwa hivyo. Muda mrefu ulipita kiasi kwamba hisia zikamwambia yupo salama. Miaka thelathini sio mchezo! Lakini kuna nyakati aliiona miaka thelathini ni kama kufumba na kufumbua macho tu.
Hivyo akawa analisubiria onyo la kwanza akipanga namna atakavyokimbia. Picha ya tukio zima litakavyokuwa ilikuwa kichwani mwake. Kwanza, Onyo la kwanza lingekuja mwezi mmoja kabla ya onyo la pili. Huo mwezi mzima angeutumua kujiandaa. Angezifuta nyayo zilizokuwa zinaonekana, angehamisha mali zake na angelipa visasi kama vilikuwepo. Halafu muda ambao onyo la pili lingekuja angeondoka bila kusita wala kugeuka nyuma.
Lakini kupanga huwa ni jambo moja na uhalisia ni jambo lingine. Muda ulipofika onyo la kwanza na lile la pili vilikuja kwa pamoja. Kwa wakati na siku moja. Mbaya zaidi onyo la pili ndilo lilitangulia. Yaani fensi iliyokuwa karibu na nyumba ndiyo ilikuwa imevamiwa kwanza. Na Hook Hobie hakukimbia. Alipuuza mipango yote aliyoipanga kwa miaka thelathini na kuamua kukabiliana na kilichokuwa kinakuja kwake uso kwa uso.
SEHEMU YA KWANZA