Riwaya: Senyenge

Nimetoka sasa hivi kucheck movie ya Jack Reacher muda sio mrefu ya tom cruise sijui ndo yenyewe
 
Ndugu wasomaji, nilipata matatizo ya kuharibikiwa na hard disk iliyokuwa inahifadhi vitu vyangu. So muda ambao nilikuwa kimya nilikuwa najaribu kuiandika tena hii riwaya kwa kumbukumbu - ninaendelea vizuri, naamini siku sio nyingi tutaendelea na burudani yetu. Naomba mniwie radhi.
 
Nilipoona umePost nilijua umeweka vitu nikaja faster kumbe porojo!
 
SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA
"Kwahivyo tunafanya nini sasa?" Reacher aliuliza.

Walikuwa bado wapo kwenye maegesho ya nje ya ofisi ya McBannerman, huku jua likiimulika ile Bravada ya Jodie. Kiyoyozi kilikuwa kimewashwa pia. Hii ilimfanya Reacher aisikie vyema harufu ya unyunyu aliokuwa ameuvaa Jodie. Kwa wakati huo, Reacher alikuwa ni mwanaume mwenye furaha kuliko wanaume wote akiishi kwenye kuimbukumbu ya zamani. Miaka ya nyuma, mara kwa mara angewaza ingekuwaje kama angekuwa na Jodie katika umbali wa kugusana siku akiwa mkubwa. Ni jambo ambalo hakuwahi kutarajia lingeweza kutokea. Alidhani wangepotezana tu na wasingewahi kuonana tena. Alidhani hisia zake zingeyeyuka na kufifia. Lakini leo alikuwa hapo, akivuta hewa ya unyunyu wake, akimuangalia miguu kwa jicho la wiziwizi. Zamani alidhani Jodie angekuwa akawa mwanamke wa kawaida tu, lakini sasa hivi alikuwa anajihisi mwenye hatia kwa kuuchukulia poapoa uzuri wa Jodie.

"Ni tatizo tayari," Jodie alisema. "Siwezi kwenda huko kesho muda hauniruhusu."

Miaka kumi na tano. Ilikuwa ni muda mrefu au muda mfupi? Huo muda unaweza kumbadilisha mtu? Kwa Reacher miaka kumi na tano aliiona kama muda mfupi. Hakujisikia kama amebadilika sana. Alikuwa ni mtu yuleyule, anaefikiria vilevile na mwenye uwezo wa kufanya vitu kama miaka kumi na tano iliyopita. Ni kweli alikuwa ameongeza uzoefu wa mawili matatu kwa muda huo, alikuwa amezeeka lakini kiujumla alikuwa ni mtu yuleyule. Lakini alihisi Jodie angekuwa amebadilika. Hakuna wasiwasi. Miaka yake kumi na tano iliyopita ilikuwa ni ya mazingira tofautitofauti. Shule ya sekondari, chuo, shule ya sheria, ndoa, talaka. Lazima angekuwa mtu tofauti. Reacher alihisi alikuwa anashughulika na mambo matatu kwa wakati mmoja: Uhalisia wa Jodie kama mtoto miaka kumi na tano iliyopita, halafu namna Reacher alivyotarajia atakuwa, na mwisho kabisa namna alivyomkuta amekuwa. Alikuwa na uhakika wa mambo mawili ya kwanza, ila sio jambo la tatu. Alikuwa anamjua Jodie kama mtoto, alikuwa anamjua Jodie kama mtu mzima aliyemuumba kwenye fikra zake. Lakini hakuwa anajua Jodie wa sasa jambo ambalo lilimtia mashaka kwasababu hakuwa tayari kufanya kosa lolote la ajabu mbele ya Jodie.

"Itabidi uende mwenyewe," Jodie alisema. "Ni sawa?"

"Ni kweli," Reacher alijibu. "Lakini hilo sio tatizo hapa, tatizo ni kwamba unatakiwa uwe makini sana."

Jodie alitikisa kichwa kukubali. "Sawa. Nitakuwa makini."

"Ofisi yako ipo wapi?"

"Wall Street na Lower Broadway."

"Lower Broadway ndipo unaishi?"

"Ndiyo. Huwa natembea kufika nyumbani. Navuka nyumba kama 15 tu."

"Kuanzia kesho nitakuwa nakuendesha kwa gari. Hautakiwi kutembea tena."

Jodie alionesha mshangao. "Utaniendesha?"

"Ndiyo." Reacher alijibu. " Kuvuka nyumba kumi na tano kwa mguu ni hatari zaidi. Wanaweza kukukwapua mtaani, vipi ofisi yako ipo salama kweli?"

Jodie alitikisa kichwa kukubali. "Hakuna mtu anaruhusiwa kuingia bila kitambulisho au bila kuwa na miadi na mtu wa mule."

"Ok, kwahivyo nitakuwepo nyumbani kwako usiku wote na asubuhi nitakuendesha mlango hadi mlango kabla sijaja kuonana na familia ya Hobie. Na wewe utatakiwa ubaki ofisini hadi nitakapokuja kukuchukua tena."

Jodie alibaki kimya. Reacher akayapitia maneno aliyoyasema.

"Namaanisha kwako lazima una chumba cha wageni?"

"Ndiyo," Jodie alijibu.

"Basi sawa."

Jodie alitikisa kichwa kukubali.

"Kwahivyo?" Reacher aliuliza.

Jodie aligeuza uso kumtazama halafu akatabasamu. "Tunaenda shopping."

"Shopping? Unataka kununua nini?"

"Siyo ninataka kununua nini," Jodie alisema. "Ila ni wewe unataka nini!"

Reacher alimtazama Jodie kwa jicho la wasiwasi. "Ninataka nini?"

"Nguo mpya," Jodie alisema. "Itakuwa jambo la ajabu kwenda kuwatembelea wale wazee huku unaonekana kama mzimu. Na tunahitaji kupita duka la dawa pia. Jeraha lako halitopona kwa muujiza."



"UNAFANYA UJINGA GANI?" Mkurugenzi wa fedha alifoka.

Alikuwa kwenye mlango wa ofisi ya Chester Stone, ghorofa ya juu ilipo ofisi yake mwenyewe. Alikuwa ameshikilia fremu ya mlango akihema kwa nguvu na uchovu. Hakuwa amekuja kwa lifti. Kuisubiria kungemchelewesha. Alikuwa amepanda ngazi kwa kukimbia. Stone alikuwa anamuangalia kwa mshangao.

"Wewe mwehu," alifoka tena. "Nilikuambia usifanye huu upuuzi."

"Nisifanye nini?" Stone aliuliza.

"Kuweka hisa sokoni. Nilikuambia usifanye huo upuuzi."

"Mbona sijaweka hisa sokoni," Stone alisema.

"Basi hisa zipo sokoni na watu wanazikimbia kama ni bomu au mvua ya tindikali."

"Nini?"

Mkurugenzi wa fedha alivuta pumzi ndefu. Akamkodolea macho mwajiri wake. Hapo akaona mwanaume mnyonge aliyevaa suti ya gharama ya uingereza akiwa amekaa kwenye dawati ambalo lilikuwa la bei ghali kuliko pesa zilizomilikiwa na kampuni.

"Wewe ni mjinga na nilikuambia usifanye huu upuuzi. Ni mara mia ungeita waandishi wa habari ukatangaza 'kampuni yangi haina thamani yoyote' kuliko huu upuuzi."

"Unaongelea nini. Sikuelewi."

"Mabenki yananipigia simu," Mkurugenzi wa fedha alianza kueleza. "Wanasema wanafuatilia kwa karibu. Hisa zako zimeingia sokoni lisaa limoja lililopita na bei inaporomoka tu. Haziuziki. Ni kama umetuma meseji kuwaambia wewe ni tatizo na wanakudai zaidi ya milioni kumi na sita kwa dhamana ya vitu ambavyo thamani yake hata senti kumi na sita haifiki."

"Sijaziweka hisa sokoni," Chester alisema.

Mkurugenzi wa fedha alitikisa kichwa kwa dharau. "Kwahivyo nani ameziweka. Mzimu wa Santa?"

"Hobie," Stone alisema. "Lazima ni yeye. Yesu wangu! Kwanini?"

"Hobie?" Mkurugenzi wa fedha alirudia.

Stone alitikisa kichwa kukubali.

"Hobie? Kwanini ulimpa hisa?"

"Sikuwa na jinsi." Stone alijitetea.

"Shit. Unaona anachokifanya sasa?" Mkurugenzi wa fedha alifoka.

Stone alitikisa kichwa kwa uoga. "Tunafanyaje sasa?"

Mkurugenzi wa fedha alishusha mikono yake chini kutoka kwenye fremu ya mlango. "Sahau kuhusu mimi. Hakuna neno tunafanyaje ni unafanyaje wewe, mimi ninaacha kazi. Hili tatizo utalimaliza mwenyewe."

"Lakini wewe ndiye ulimpendekeza huyu jamaa." Stone alifoka pia.

"Ni kweli, lakini sikupendekeza umpatie hisa wewe mwehu." Mkurugenzi wa fedha alifoka pia. "Wewe ni chizi kumbe. Inamaana nikipendekeza utembelee mbuga za Serengeti uwaone simba utaenda mbali zaidi kuwashika sharubu halafu unilaumu mimi?"

"Lakini nahitaji msaada wako," Stone alisema.

Mkurugenzi wa fedha alitikisa kichwa kukataa. "Mimi nimeacha kazi. Kwa sasa hivi ushauri wangu ni uende ilipo ofisi yangu ukapokee simu zinazoingia uwajibu maswali yao."

"Subiri," Stone alifoka tena. "Ninahitaji msaada wako."

"Dhidi ya Hobie? Endelea kuota rafiki yangu." Mkurugenzi wa fedha alisema.

Halafu akawa ameondoka. Aligeuka nyuma na kutokomea tu. Stone alinyanyuka kutoka kwenye dawati lake na kusimama mlangoni na kumtazama akiondoka. Ofisi ikawa kimya. Katibu muhtasi wake pia alikuwa ameondoka. Mapema zaidi ya alivyotarajia. Stone alitoka nje kusimama kwenye korido. Ofisi ya mauzo ilikuwa tupu. Mashine zilikuwa kimya. Akapanda kwenye lifti na kushuka ghorofa ya chini peke yake. Ofisi ya mkurugenzi wa fedha ilikuwa tupu. Droo zilikuwa tupu na baadhi ya vifaa binafsi vilikuwa vimeondolewa. Kompyuta ilikuwa imezimwa na simu ilikuwa inaita. Akaipokea.

"Hello?" Alisema kwenye maiki ya simu. "Mimi ni Chester Stone."

"Bwana Stone, tafadhali subiri uunganishwe na mkurugenzi."

Ukapita mziki kidogo kabla sauti ya Mkurugenzi haijaja kwenye spika za simu.

"Bwana Stone," ilikuwa sauti nzito. "Mkurugenzi hapa."

"Hello," ndilo neno pekee aliloweza kufikiria Chester.

"Nadhani unaelewa nafasi yetu kwa sasa, hatuna budi kuchukua hatua." Sauti ilisema.

"Ok," Chester alikuwa anawaza hatua zipi hizo. Jela? Mahakama?

"Tutatoka nje ya msitu pengine kuanzia kesho,"

"Nje ya msitu? Kivipi?"

"Tunaliuza deni." Sauti ilisema.

"Mnauza deni? Sijaelewa."

"Hatuhitaji kuendelea kukudai. Naamini unaelewa nafasi yetu, kwasababu hili suala limetoka nje ya mipaka. Kwahivyo tunaliuza deni. Na hicho ndicho watu hafanya, sio? Wakiwa na kitu ambacho hawakihitaji tena wanakiuza, sio?"

"Mnamuuzia nani?" Stone aliuliza.

"Kampuni moja inajiita Caymans. Wametoa ofa nzuri."

"Kwahivyo hilo suala linatuacha sisi wapi?"

"Sisi?" Sauti ilisema tena. "Haituachi popote kwa maana jukumu letu kwako limevunjwa. Hakuna sisi tena. Uhusiano wetu umekufa. Na ushauri wangu ni kwamba usiwahi kujaribu kuufufua. Tutauchukulia kama tusi kwa majeruhi. Umenielewa?"

"Kwahivyo nadaiwa na nani sasa hivi?"

"Kampuni ya Cayman," Sauti ilijibu kwa upole. "Nina uhakika anayehusika nayo atakutafuta muda sio mrefu."

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
 
Hongera mkuu Chachasteven.
Maneno ndio haya!
 
Okay! Changamoto za hapa na pale zimeisha. Nitakuwa naweka kila baada ya siku mojamoja yaani masaa 24 kuanzia kesho asubuhi saa 4 mapema mzigo unakuwa hewani....
Ahadi ni deni mkuu.Sasa hivi tunaelekea saa 7 mchana bado bilabila!
 
Okay! Changamoto za hapa na pale zimeisha. Nitakuwa naweka kila baada ya siku mojamoja yaani masaa 24 kuanzia kesho asubuhi saa 4 mapema mzigo unakuwa hewani....
Kwa watani zangu wakurya saa nne haijafika bado poti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…