Riwaya: Senyenge

Riwaya: Senyenge

SEHEMU YA KUMI NA TATU
"Wewe ndiye Mrs. Jacob?" Reacher aliuliza.

Jodie Graber alitikisa kichwa kukubali.

"Ndiye mimi, Nilikuwa," Jodie alijibu. "Ni Jina la mume wangu. Tumeachana, lakini bado nalitumia kazini."

"Alikuwa ni nani?"

"Wakili, kama mimi."

"Mmedumu kwenye ndoa kwa muda kiasi gani?"

"Miaka mitatu tu. Tulikutana chuo na kuamua kufunga ndoa tulipohitimu na kupata kazi kila mmoja. Mimi nilibaki Wall Street, Yeye akaenda DC. Nasikitika alipoondoka ndoa yetu aliiacha. Hakuondoka nayo na nilikuja kujua alipotuma karatasi za kuomba tuachane. Jina lake ni Alan Jacob."

Reacher alisimama na kumuangalia Jodie. Aligundua ilikuwa huzuni kwake kusikia Jodie alikuwa ameolewa na kuachika.

Jodie alikuwa mwembamba lakini mwenye mvuto tangu akiwa na miaka kumi na tano tu, alikuwa mwenye kujiamini na mwenye soni kidogo. Reacher alikuwa ameshuhudia mara nyingi vita kati ya haya na udadisi usoni pake kila mara walipoongea kuhusu kifo na uhai na mema na mabaya enzi hizo. Halafu wangebadilisha mada na kuongea kuhusu upendo na mapenzi na wanaume na wanawake. Halafu Jodie angeona aibu na kuaga kuondoka. Reacher angebaki mwenyewe akiwa kama barafu kwa ndani. Siku chache baadaye angemuona tena Jodie akizungukazunguka kwenye mazingira ya kambi. Na sasa miaka kumi na tano baadae alikuwa ni mwanamke mkubwa, mwenye elimu ya haja ya sheria, aliyeolewa na kuachika, mzuri na mwenye busara akiwa amesimama hapo mbele yake huku wameshikana mikono.

"Umekwishaoa?" Jodie alimuuliza Reacher.

Alitikisa kichwa kukataa, "Hapana."

"Lakini una furaha?"

"Mimi nina furaha kila siku," Reacher alijibu. "Ninayo furaha tangu zamani, na nitakuwa nayo kila siku."

"Unashughulika na nini sasa?"

Reacher aliinua mabega. "Sifanyi vingi," Alijibu.

Alianza kuzungusha macho yake kwa wale waombolezaji waliokuwepo kwenye ile kadamnasi. Watu ambao wako bize muda wote. Wana maisha ya kifahari. Kazi za heshima, wote wakiwa ni watu wanaojua wanapotoka na wanapoenda. Kama mtoto anayejua vyema kuimba alfabeti A mpaka Z kwa mpangilio. Aliwatazama kwa nukta na kuwaza kama wao ndiyo walikuwa wendawazimu, au yeye ndiye alikuwa mwendawazimu.

"Nilikuwa Keys," Alisema. "Nilikuwa nachimba mabwawa ya kuogelea kwa chepeo."

Mwonekano wa uso wa Jodie haukubadilika. Jodie alijaribu kuushika mkono wa Reacher kwa nguvu. Ilikuwa kazi bure. Mkono wake ulikuwa mdogo sana ukilinganisha na kiganja cha Reacher.

Costello alikupata huko?" Jodie aliuliza.

Hakuwa akinitafuta kunialika kwenye msiba, Reacher aliwaza. "Tunahitaji kuzungumza kuhusu Costello," Alisema.

"Ni mtu makini, sio?"

Hakuwa makini sana, Reacher aliwaza tena.

Jodie aliuachia mkono wa Reacher na kuanza kuwazungukia umati wa waombolezaji. Watu walikuwa wamesimama wanasubiri kutoa pole zao kwa mara nyingine tena. Hata hivyo, vinywaji walivyokuwa wamekunywa vilianza kuwaelemea na walikuwa wakiongea kwa sauti kubwa. Reacher naye aliteleza kutoka alipokuwa amesimama hadi kwenye meza iliyokuwa imefunikwa kwa kitambaa cheupe. Hapo alichukua sahani ya karatasi na kuiwekea kuku na wali na kuchukua glasi ya maji. Kulikuwa na kiti kilichoonekana kuzeeka. Pengine ndiyo maana watu wengi walikipuuza. Reacher aliketi kwenye hicho kiti peke yake.

Alikuwa akiyazungusha macho yake kwenye ule umati wa waombolezaji huku akila taratibu. Watu walikuwa wagumu kuondoka. Hii ilithibitisha upendo wao kwa Garber ulivyokuwa mkubwa. Jodie alikuwa akitoka kwa huyu na kwenda kwa yule akitoa na kupokea mikono, huku uso wake ukiwa na tabasamu la huzuni. Kila mmoja alionekana alikuwa na kisa cha kumwambia. Kisa kuhusu moyo wa dhahabu wa Garber kwa matendo yake. Reacher angeweza kumwambia Jodie visa vingine vingi vya Garber, lakini visingekuwa na umuhimu. Jodie hakuwa anahitaji kusikia kisa chochote kujua kwamba baba yake alikuwa mtu mbele ya watu. Ni kitu alichokuwa anakifahamu. Kwa muda wa uhai wa Garber hakuwahi kumficha Jodie kitu chochote. Watu wanaishi, halafu wanakufa, na kama watayaishi maisha yao katika njia nzuri hakuna kitu cha kujutia hata wakifa.

Waliipata sehemu ya kuhifadhi gari lao mtaa wa pili, Ilikuwa sehemu yenye ukimya bila watu. Waliliegesha gari yao nyuma ya gereji ambako isingeonekana kwa urahisi. Lakini walihakikisha inakaa katika mkao wa kuondoka. Walitoa bastola zao kwenye boksi lililokuwamo kwenye gari na kuzipachika kwenye mifuko ya mikoti ya suti zao. Wakaanza kutembea kurudi barabarani kwa uangalifu mkubwa kwa kutumia njia za pembeni kidogo.

Ilikuwa ni safari fupi, lakini ngumu. Ni kweli walikuwa maili sitini kutoka Manhattan, lakini ilikuwa ni sawa na kuwa katikati ya misitu ya Borneo. Kulikuwa na majani na miti iliyozagaa kila pahali ikiwa na matawai marefu. Waliamua kutembea kwa kutanguliza migongo. Walipofika karibu na barabara iliyokuwa inaelekea kwa Garber walikuwa wakihema kwa nguvu huku vumbi la kijani likiwa limewavaa. Walilala chini ambapo wasingeweza kuonekana wakitembea. Walianza kutambaa kwa matumbo yao kama nyoka kutafuta eneo ambalo lingewaruhusu kuona vyema nini kilikuwa kinaendelea kwenye mkusanyiko uliokuwepo hapo kwa Mrs. Jacob. Wale watu waliokuwa kwa Mrs. Jacob walikuwa wanaanza kuondoka. Ilikuwa imeanza kuwa dhahiri nani haswa alikuwa Mrs. Jacob. Kama Hobie alikuwa sahihi na hii ndiyo nyumba yake, basi Mrs Jacob alikuwa ni yule mwanamke mwembamba mwenye nywele asili za njano aliyekuwa akibadilishana mikono ya kwaheri hapa na pale na wageni wake. Walikuwa wanaondoka, Yeye alikuwa anabakia. Hakuna shaka yeye ndiye Mrs. Jacob.

Walimtazama bila kusemeshana. Yeye ndiye alikuwa sababu ya umati ule. Watu wengine walianza kuelekea walipoegesha magari yao mmojammoja na hata wawiliwawili. Halafu wakaanza kuondoka kwa makundi makubwamakubwa. Magari yalikuwa yakiwashwa. Msuguano wa matairi na barabara na miungurumo ya gari hili na lile ilitawala. Kazi ilikuwa inaenda kuwa rahisi kama kipande cha mkate kwa chai. Muda sio mrefu Mrs. Jacob angebaki akiwa amesimama pale peke yake akiwa na upweke na huzuni. Halafu angepata wageni wawili zaidi. Labda angewachukulia kama waombolezaji waliofika msibani wakiwa wamechelewa. Hata hivyo, walikuwa wamevaa suti za vitambaa vyeusi na tai zao zilikuwa nyeusi ambazo kiujumla zilichukuliwa kama nguo sahihi za msiba hapo Manhattan.

Reacher aliwafuata kuwasindikiza wageni wawili wa mwisho kuondoka. Mmoja alikuwa ni koloneli na mwingine alikuwa ni jenerali tu mwenye nyota mbili begani kwake. Wote walikuwa wamevaa sare za jeshi. Haikumshangaza. Sehemu yenye chakula na vinywaji vya bure wanajeshi ndiyo huwa watu wa mwisho kabisa kuondoka hapo. Hakuwa akimfahamu yule koloneli, lakini hisia zilimwambia alikuwa amewahi kukutana mahali na yule Jenerali. Walikuwa wakitazamana kila wakati. Hata hivyo, hakuna aliyethubutu kumuuliza mwenzake kuhusu mashaka yao hayo. Hakuna haja ya kujiingiza kwenye mijadala mirefu na migumu ya kujibu swali la kwahiyo-siku-hizi-unafanya-nini.

Wale wanajeshi wawili walipanda kwenye gari moja la mwisho lililokuwa limebaki kati ya mengi yaliyokwishaondoka. Wa kwanza kufika, wa mwisho kuondoka. Muda wa amani, Hakuna vita baridi, Hakuna kazi ya kufanya kwa siku nzima. Ndiyo maana Reacher alifurahi siku alipokatwa jeshini. Na alipolitazama lile gari la kijani likiondoka alijua alikuwa sahihi kufurahi.

Jodie alikuwa amesogea hadi alipokuwa amesimama na kuupeleka mkono wake tena kugusana na wa Reacher.

"Hatimaye," Alisema kwa ukimya. "Hili nalo limeisha."

Ulipita ukimya kidogo isipokuwa kwa kelele za lile gari la wale wanajeshi wawili likiwa linaishia zake.

"Amezikwa wapi?"

"Makaburi ya mjini," Jodie alisema. "Najua angepata nafasi ya kusema azikwe wapi angechagua Arlington. Unataka ukatembelee kaburi lake?"

Reacher alitikisa kichwa kukataa. "Hakuna haja. Haiwezi kuleta utofauti wowote kwake, au inaweza? Alikuwa anajua atakapokufa nitakuwa nimepoteza mtu muhimu. Inatosha."

Jodie alitikisa kichwa kukubali.

"Ni muda tuzungumze kuhusu Costello," Reacher alisema tena.

"Kwanini?" Jodie aliuliza. "Nadhani alikwishakupa ujumbe wake."

"Hakunipa ujumbe wowote. Ni kweli alinipata, lakini nilimwambia mimi sio Jack Reacher."

Jodie alimtazama kwa macho ya mshangao. "Kwanini?"

"Tabia yangu nadhani. Sitembei nikitafuta marafiki au mahusiano. Jina la Jacob sikuwa nalifahamu kwahivyo nilimpuuza tu. Nikaendelea na hamsini zangu."

Jodie alikuwa bado anamkodolea macho Reacher.

"Nadhani ningetumia jina la Garber," Jodie alisema. "Hata hivyo lilikuwa ni suala lililomhusu baba na mimi nilitumia jina la kazini, sikuwa nafikiria utalipuuza."

"Na?"

"Na hukupaswa kulipuuza au kuongopa kwa sababu haikuwa ni suala kubwa."

"Tunaweza kwenda ndani kuongea?" Reacher aliuliza.

Jodie alipata mshtuko tena. "Kwanini?"

"Kwasababu unachosema halikuwa suala kubwa limezua mambo mazito sana."

SEHEMU YA KUMI NA NNE
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Walimuona Mrs. Jacob akimuongoza yule baunsa wa baa kule Keys aingie ndani kupitia mlango wa mbele wa nyumba. Aliifungua mlango. Mlango mkubwa wa mbao uliopakwa rangi ya brauni. Waliingia ndani na kuufunga mlango nyuma yao. Baada ya sekunde kumi ishara ya mwanga hafifu ilitokea kwenye dirisha la kushoto. Walitakadiria kile chumba chenye lile dirisha kuwa sebule au chumba f'lani cha maongezi. Kilikuwa kimezungukwa na mimea mingi kiasi kwamba ilitoa giza na kuwataka watakaoingia kukaa humo wawashe taa hata katikati ya jua kali. Wale wanaume walitambaa kusogea mbele kidogo kwa matumbo yao. Wadudu walikuwa wameanza kurukaruka kuwazunguka. Walitazamana kwa nukta bila kuongea.

Walinyanyuka kutoka ardhini na kujisogeza hadi eneo yalipokuwa yameegeshwa magari yaliyokwishakuondoka. Wakakimbiakwa kunyata hadi kuifikia nyumba ya Mrs. Jacob. Hapo waliuegemea ukuta kwa muda kidogo. Waliingiza mikono mfukoni na kutoa bastola zao. Walizishika mikononi huku midomo ya kupitisha risasi ikiwa imeangalia ardhini na kuanza kwenda mbele ya uwa mmoja baada ya mwingine. Waliungana tena na kuanza kuusogelea mlango wa mbele kila mmoja akichukua nafasi kwenye pembe mbili za mlango. Mmoja kushoto. Mwingine kulia. Bastola zilikuwa mkononi zikiwa tayari. Mrs. Jacob alikuwa ameingilia huu mlango. Hakuna ubishi atatokea mlango huohuo pia. Lilikuwa ni suala la muda tu.

"Kuna mtu alimuua?" Jodie alirudia kuuliza.

"Na katibu muhtasi wake pia ameuliwa, hakuna ubishi." Reacher alijibu.

"Siamini," Alijibu. " Kwanini?"

Jodie alikuwa amempeleka Reacher kwenye chumba kidogo kilichokuwa mwisho wa nyumba. Dirisha dogo na samani za mbao zilizokuwemo zilikipa chumba giza kidogo, hivyo Jodie aliwasha taa ndogo ya mezani ambayo ilibadilisha mandhari ya chumba chote kuwa kama ofisi ndogo alizowahi kuziona Reacher ulaya. Kulikuwa na kabati a vitabu. Kulikuwa na dawati kubwa lisilokuwa na kitu chochote juu yake.

"Sijui kwanini," Reacher alisema. " Sijui chochote. Sijui hata kwanini ulimtuma aje kunitafuta."

"Baba ndiye alikuwa anakutaka," Alijibu. "Sikuwahi kupata muda wa kujadili naye kwanini. Nilikuwa nimbanwa na kazi nyingi sana. Kulikuwa kuna kesi naishughulikia ambayo ilikuwa inaniumiza kichwa. Ninachofahamu baba alitakiwa aende kuonana na daktari wa upasuaji wa moyo. Alienda huko hospitali na kukutana na mtu ambaye nadhani kuna kitu alimweleza. Baba alikuwa kama aliyeguswa sana. Alianza kufuatilia hilo suala. Halafu baadae hali yake ilipokuwa mbaya alijua asingeweza kukamilisha alichokianza na akaanza kusema anatakiwa akutafute wewe ili ulifuatilie kwa sababu alikuwa anaamini wewe ndiye mtu sahihi ambaye ungeweza kufanya kitu. Alikuwa ananisisitizia sana ndiyo maana nikamtafuta Costello ajaribu kukutafuta uongee na baba. Huwa tunamtumia mara kwa mara ofisini kwahivyo haikuwa taabu na ndiyo kitu cha mwisho ambacho ningeweza kufanya kumsaidia baba kukupata."

Maelezo yalianza kuleta maana, Lakini swali la kwanza kichwani kwa Reacher lilikuwa ni kwanini Garber alikuwa anamtaka kwa nguvu kubwa hivyo. Aliliona tatizo la Garber. Alikuwa katikati ya jambo zito, afya yake ikiwa inayokwenda mrama, hakuwa tayari kuahirisha alichokianza na alikuwa anahitaji msaada. Garber angeweza kupata msaada kutoka sehemu yeyote. Kulikuwa na wapelelezi binafsi wengi sana Manhattan. Na kama lilikuwa tatizo ambalo ni la siri na binafsi sana Garber angeweza kunyanyua simu moja kwa rafiki zake wengi walioko kwenye taasisi ya jeshi. Mamia wakiwa tayari kufanya lolote kwaajili ya Garber. Kwahivyo Reacher alikuwa amekaa hapo akijiuliza kwanini Garber aliamua kumtafuta Reacher moja kwa moja.

"Huyo mtu aliyekutana naye huko hospitali ni nani?"

Jodie aliinua mabega juu. "Simfahamu. Nilikuwa nimebanana na sikuwahi kujadili chochote na baba kuhusu hilo suala."

"Costello aliwahi kuja kukutana na Garber?"

"Ndiyo. Nilimpigia simu na kumwambia tutamlipa kama ofisi, lakini anapaswa kuja kuchukua maelekezo huku. Aliponipigia simu siku mbili au tatu baadae alisema tayari amekwishazungumza na mzee na ombi lake lilikuwa ni kwamba akutafute wewe. Costello akawa amesisitiza nimlipe kabla ya kazi na nikawa nimemlipa."

"Ndiyo maana alisema mteja wake ni Mrs. Jacob," Reacher alisema. "Sio Leon Garber. Na ndiyo maana nilimpuuza. Na ndicho kilimpelekea akauliwa."

Jodie alitikisa kichwa kupinga na kumtazama Reacher kwa jicho la haraka. Hii ilimshangaza Reacher. Alikuwa bado anamuona kama binti wa miaka kumi na tano tu, kumbe alikuwa ni wakili aliyeshughulika na kesi nzito.

"Hakuna hatia," Jodie alisema. "Kilichotokea kipo wazi, sio? Baba alimwambia Costello hadithi yote, Costello akajaribu njia ya mkato kabla ya kuja kukutafuta wewe ambapo kwa bahati mbaya akajikuta anageuza jiwe lisilotakiwa kugeuzwa na hii ikamshtua mtu. Huyo mtu akamuua ili kujua Costello alikuwa anatafuta nini na kwanini. Kwangu mimi sioni utofauti hata kama ungecheza mpira sawa na Costello alivyouleta. Lazima wangempata tu Costello na kumuuliza ni nani alimpatia hicho anachofuatilia - Na mwisho wa siku mimi ndiye ningekuwa niliyemwingiza kwenye matatizo."

Reacher alitikisa kichwa kukataa. "Ni Leon. Kupitia wewe."

Jodie naye alitikisa kichwa kupinga kauli hiyo ya Reacher pia. "Ni yule mgonjwa kutoka hospitali ya moyo. Yeye, kupitia baba, kupitia mimi.

"Nahitaji kumpata huyo mtu."

"Haina maana kwa sasa."

"Nadhani ina maana." Reacher alisema."Kama Leon alilichukulia hilo suala kwa uzito, mimi pia ninalichukulia kwa uzito. Hiyo ndiyo ilikuwa kanuni yetu."

Jodie alitikisa kichwa kukubali. Alinyanyuka haraka na kusogea hadi ilipokuwa kabati ya vitabu. Hapo alitoa picha moja na kuitazama kwa muda mrefu kabla hajamwonesha Reacher.

"Unaikumbuka hio?" Aliuliza.

Ile picha ilikuwa na umri wa zaidi ya miaka kumi na tano. Ilikuwa ikimwonesha Garber akiwa amesimama upande wa kushoto. Reacher mwenyewe alikuwa upande wa kulia akiwa anatabasamu na sura ya ujana. Katikati yao alikuwa ni Jodie, miaka kumi na tano akiwa amevaa nguo za jua. Mkono wake mmoja ulikuwa umezunguka kiuono cha baba yake na ule mwingine kiuono cha Reacher.

"Unakumbuka hii siku? Baba ndiyo alikuwa amenunua kamera yake ya NIKON PX?"

Reacher alitikisa kichwa kukubali. Alikuwa anaikumbuka hiyo siku. Alikuwa anakumbuka vyema harufu ya nywele za Jodie. Alikuwa anakumbuka namna alivyojisikia kipindi miili yao imegusana. Alikumbuka pia namna alivyojinong'oneza mwenyewe rohoni mwake, Jikaze, rafiki. Ana miaka kumi na tano tu na ukuzingatia ni mtoto wa CO wako.

"Alipenda kuiita hii ni picha ya familia." Jodie alisema.

Reacher alitikisa kichwa kukubali. "Ndiyo ilikuwa kanuni ya jeshini."

Jodie aliitazama ile picha kwa muda, kitu f'lani kikajichora kwenye uso wake.

"Unajua na katibu muhtasi wa Costello yupo." Reacher alianza kueleza. "Lazima watamuuliza mteja wake alikuwa ni nani. Lazima atawaambia. Na hata kama hakuwaambia ni lazima watagundua tu mwisho wa siku. Kumbuka ilinichukua mimi sekunde thelathini na tano tu kwenye simu kugundua ni wapi ulipo. Watakuja kukuuliza ni nini Costello alikuwa anafuatilia."

"Lakini mimi sijui chochote," Jodie alisema.

"Unahisi wataamini hayo maneno yako?"

"Kwahivyo unashauri nini?"

"Uondoke hapa haraka iwezekanavyo," Reacher alijibu. "Hakuna ubishi. Hii sehemu imejitenga sana. Hauna sehemu ya kukaa mjini?"

"Ninayo." Jodie alijibu. "Lakini nilikuwa nina mpango wa kulala hapa usiku wote. Natakiwa kupekua kuona wosia na masuala mengine ya makaratasi. Nitaondoka kesho asubuhi."

"Fanya hayo mambo yote sasa hivi," Reacher alisema. "Fanya haraka iwezekanavyo na uondoke. Ninamaanisha kila neno ninalolisema. Hawa watu, haijalishi ni akina nani hawachezi michezo."

Muonekano katika sura ya Reacher uliongea mengi kuliko maneno aliyoyasema.

"Sawa, tuanzie kwenye makaratasi yake. Naomba nisaidie."

Kulikuwa na vyeti vyake kuanzia anamaliza shule hadi makaratasi yaliyoonesha utumishi wake jeshini. Garber alikuwa amehudumia jeshi kwa zaidi ya miaka hamsini. Kulikuwa na makaratasi yaliyoandikwa kwa mkono pia yakionesha bili za kodi, simu, umeme, mshahara wa mfanyakazi wa bustani na vifaa vingine. Pia kulikuwa na karatasi yenye mwandiko mpya. Wosia na neno la mwisho. Jodie alinyanyua makaratasi yote na kuyaweka juu ya meza na ile picha aliyokuwa ameshika ilikuwa pale. Reacher aliitazama tena.

"Ulikuwa unakubaliana naye kuhusu falsafa yake kuwa alinichukulia kama familia?"

Jodie alisimama na kutikisa kichwa kukubali.

"Nilikubaliana naye kwa kiwango cha ukichaa," Alisema. "Na siku moja nitakuambia kwanini."

Reacher alimtazama Jodie bila kusema kitu.

"Acha nichukue baadhi ya vitu muhimu," Jodie alisema. "Dakika tano, Sawa?"

Reacher alisogea lilipo kabati la vitabu na kuiweka ile picha alipokuwa ameitoa Jodie. Halafa akazima taa na kubeba begi kutoka nje. Alisimama kwenye korido na kuzungusha macho yake. Ilikuwa nyumba inayovutia. Sakafu ya mbao na samani za bei kubwa. Televisheni ya kizamani, Vitabu, Picha. Haikuwa imepambwa sana lakini ilikuwa inavutia. Inawezekana Garber alikuwa ameinunua miaka thelathini iliyopitia. Pengine kipindi ambacho mama yake Jodie alikuwa na mimba. Lilikuwa suala la kawaida. Maafisa wengi wenye familia walikuwa wakinunua nyumba zao maeneo ambayo walidhani ndiyo ingekuwa muhimili wa maisha yao. Wangenunua nyumba na kuiacha ikiwa tupu huku wakiishi ng'ambo. Pointi ilikuwa ni kuwa na eneo la kujishikisha, sehemu ambapo wangekuwa na hakika wangefikia endapo wangetoka jeshini. Au sehemu ambayo familia zao zingeishi wao wakiwa ng'ambo na huko waliko isingekuwa salama kwa familia kuwepo.

Wazazi wa Reacher hawakuwa wamechukua hiyo njia. Hawakuwahi kununua nyumba ya kukaa. Reacher hakuwahi kuishi kwenye nyumba yeyote. Sanasana aliishi kwenye kambi na mabweni ya jeshi na baadae kwenye nyumba za wageni hapa na pale za bei nafuu. Na alikuwa na uhakika hakuwa anahitaji kitu kingine. Alikuwa na hakika hakuwa anahitaji nyumba ya kuishi. Hakuna ubishi. Ilikuwa ni uzito wa majukumu kama begi alilokuwa amebeba uliomkera. Bili za kulipa, Bima na kodi za hiki na kile, Marekebisho ya paa au jiko. Kununua kapeti na zaidi ya yote kuitunza bustani. Kwanza unatumia muda na pesa nyingi kufanya majani yakuwe ili baadae uanze kutumia muda na pesa nyingi zaidi kuyapunguza urefu. Unayalaani majani kwa kukua na muda huohuo unawaza yasiwe mafupi sana na unaanza kumwagilia maji na kemikali za gharama.

Uwendawazimu!

Lakini kama kuna nyumba ambayo ingeweza kumfanya abadili mawazo basi nyumba ya Garber ndiyo ingeweza. Ilikuwa ya wastani isiyohitaji mambo mengi. Alianza kujiona akiishi hapo.

"Nipo tayari," Jodie alimshtua.

Alikuwa ametokea kwenye mlango wa sebule akiwa amebeba begi huku akiwa amevaa nguo zingine tofauti na zile za msiba. Alikuwa amevaa suruali ya Levi na kibode chenye nembo ambayo Reacher hakuwa anaifahamu. Alikuwa amechana nywele zake na sasa urembo wake ulikuwa hapo mbele ya Reacher.

Walitembea wakaivuka korido na kuufikia mlango huku wakizima baadhi ya vifaa vya umeme vilivyokuwa vinawaka. Waliporidhika waliufungua mlango wa mbele waliokuwa wameingilia dakika arobaini zilizopita.

SEHEMU YA KUMI NA TANO
 
ITAENDELEA...
Lini tena mkuu? story nzuri.
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO
Reacher alikuwa wa kwanza kutoka nje kwa sababu kadha wa kadha. Kwa kawaida angemuacha Jodie atangulie kutoka kwa sababu yeye - Reacher ni mmoja kati ya kizazi cha mwishomwisho cha vijana wa Marekani waliobeba maadili na tabia nzuri, lakini alikuwa amejifunza uungwana wa mwanaume ulioneshwa tu pale ambapo angekuwa amejua anataka kuuonesha kwa mwanamke wa aina ipi. Na pia nyumba ilikuwa ni ya Jodie, Sio ya Reacher.BNa Jodie ndiye aliyekuwa na funguo za kuufunga mlango. Kitu ambacho kiligeuza mambo juu chini. Kwahivyo sababu zote hizo ndizo zilizomfanya Reacher atangulie kutoka nje, na ndiyo maana yeye ndiye alikuwa wakwanza kuwaona wale wanaume wawili.

Mfuteni huyo baunsa na mumlete Mrs. Jacob akiwa hai, Ndivyo Hobie alivyokuwa amewaambia. Mwanaume aliyekuwa amesimama upande wa kushoto alifyatua shabaha yake akiwa amekaa. Alikuwa mwenye mori kupita kiasi. Hivyo iliufanya ubongo wake uchelewe kwa sekunde kadhaa kutafsiri kwa hakika taarifa iliyokuwa inatumwa na macho yake. Alihisi mlango wa nyumba ukifunguliwa, aliona umbile la mtu akikanyaga veranda, alimuona ni yule baunsa wa baa akiwa ametangulia na alifyatua.

Yule mwanaume wa kulia alikuwa kwenye nafasi mbaya. Hakufanya chochote.

Kwa wakati huo Reacher alikuwa akifanya matendo yake kwa hisia tu. Umri wake ulikuwa unakaribia miaka thelathini na tisa na karibu kumbukumbu zake za miaka thelathini zilikuwa sio kitu kingine, ila maisha ya kambi tofautitofauti za jeshi alizoishi. Hakuwahi kujua maana ya neno kutulia, hakuwahi hata kumaliza mwaka mzima akiwa kwenye shule moja, hakuwahi hata kufanya kazi kuanzia saa tatu hadi saa kumi na moja Jumatatu hadi ijumaa kwenye ofisi f'lani, hakuwahi kutegemea kitu chochote isipokuwa visivyotabirika. Kulikuwa na sehemu ndogo kwenye ubongo wake, kama msuli uliofanyishwa mazoezi, ambao ulikuwa umeizoea hiyo ratiba ya mambo ya ghafla ambayo ndiyo ilimfanya alipotoka nje ya mlango atazame kulia na kushoto na kwa jicho la kidadisi na kuwaona wale wanaume wawili, ambao sura zao alikuwa ameziona takribani maili elfu mbili kutoka hapo, wakiwa wamemwelekezea bastola zao aina ya pistol za milimita tisa.

Hakuonesha mshtuko, Hakuganda kwa mshangao au uoga. Hakuna kujiulizauliza, hakuna muda wa kufikiria. Ilikuwa ni mwitikio tu wa tatizo ambalo lilikuwa mbele yake kama mchoro wa hisabati uliohusisha hesabu kali ya muda zidisha eneo zidisha risasi gawia nyama laini.

Begi alilokuwa amebeba lilikuwa kwenye mkono wake wa kushoto likibembea kwenda mbele. Alifanya mambo mawili kwa wakati mmoja. Kwanza, aliliacha begi liendelee kubembea akitumia nguvu zote kwenye mkono wake wa kushoto. Pili, alimsukuma Jodie kifuani kwa nguvu kwa mkono wake wa kulia halafu risasi ya kwanza iliyotoka kwenye bunduki ya yule mwanaume wa kushoto ikalikuta begi lililokuwa linabembea. Reacher aliihisi kama imeupiga mkono wake. Alilirusha begi likampiga yule mwanaume wa kushoto kwenye uso. Alikuwa nusu ameanguka na nusu amesimama akiwa hajiwezi. Hiyo ilimtoa kwenye picha.

Lakini Reacher hakumuona alivyoanguka kwasababu macho yake yalikuwa tayari yamehamia kwa mwanamume wa kulia ambaye kwa hakika hakuwa amejiweka tayari kufyatua risasi. Reacher alijirusha kwa kasi na kumtwanga yule mwanaume usoni kwa kiwiko chake - Kiwiko ambacho kina kasi na uzito wa paundi 250 kinaweza kufanya madhara makubwa sana. Reacher alisoma madhara aliyosababisha kwenye ubongo wa yule jamaa aliyekuwa ameanguka chini na kupoteza fahamu. Halafu yule mwanaume wa kushoto alikuwa ndiyo anaanza kujiweka sawa. Mlango ulikuwa wazi na Jodie alikuwa pale anaonekana na ndiye alikuwa tatizo.

Reacher alikuwa ametenganishwa naye kwa zaidi ya futi nane na jamaa wa kushoto alikuwa katikati yao. Reacher alinyanyuka kwa kasi ya ajabu na kumsukuma pembeni yule mwanamume aliyepoteza fahamu. Alinyanyuka na kukimbia kwa kasi zaidi na kujitupa hadi alipokuwa Jodie na kuugonga mlango kuufunga. Ulilia mara tatu kwa risasi zilizoupiga nyuma yake kutoka kwa yule mwanaume wa kushoto.

'Kuna mlango wa pili?" Reacher aliuliza.

"Ndiyo."

Ilikuwa ni mwezi wa sita. Jamaa wa mkono wa kushoto alikuwa anatumia bastola aina ya M9 Beretta, ambayo hakuna shaka ingekuwa na uwezo wa kubeba risasi kumi na tano ikiwa imejaa. Na alikuwa tayari amefyatua nne, moja iliyopiga begi na tatu zilizopiga mlango. Kumi na moja ndizo risasi zilizokuwa zimebaki. Bado kulikuwa na hatari kubwa.

"Una funguo za gari?"

Jodie aliingiza mkono na kutoa funguo kwenye begi. Reacher alizichukua na kuziweka kwenye kiganja chake. Walipita na kuingia jikoni ambako ndiko kulikuwa na mlango wa pili wa kutokea nje kuelekea gereji.

"Huu mlango umefungwa?"

Jodie alitikisa kichwa kukubali. "Ufunguo wake ni huo wa kijani."

Reacher alizikagua funguo na kuuona ufunguo aliokuwa anausemea Jodie. Aliuingiza kwenye kitasa cha mlango na kuzungusha na kukitoa kichwa chake kuchungulia nje. Aliangalia kushoto, halafu kulia. Hakukuwa na dalili ya mtu anayeasubiria. Halafu akaunyofoa ufunguo kwenye kitasa na kutoka nje akimwacha Jodie ndani. Aliangalia tena mazingira. Aliporidhika aliufungua tena mlango na kumwonesha Jodie ishara ya kutoka nje. Waliingia gereji ilipokuwa na Jodie alikuwa wa kwanza kuingia.

Gereji ilikuwa na na vitu vingi ambavyo vilionekana kuwa kama vilikuwa ni vya kizamani. Kwahivyo milango ya gereji ilikuwa ni ya kufungua kwa mikono. Hakuna mlango wa automatiki. Gari la Jodie lilikuwa ni aina ya Bravada lenye rangi ya kijani. Ingeweza kuwasaidia.

"Ingia upande wa nyuma," Alisema. "Lala kwenye sakafu ya gari, Sawa?"

Jodie alifanya alivyoelekezwa. Reacher alielekea kwenye mlango wa gereji na kuufungia na kuchungulia nje. Hakuna sauti, hakuna mtu. Halafu akarudi kwenye gari na kuuingiza ufunguo kwenye gari na kuliwasha.

"Narudi baada ya dakika moja," Reacher alisema.

Reacher alienda na kuchukua nyundo ya seremala. Alitoka na kusimama kwenye mlango na kuirusha ili ipige kelele. Alihesabu hadi tano wale wanaume muda wa kuisikia na kuifuata ile sauti iliyosababishwa na nyundo. Halafu alirudi kwenye gari na kuingia na kulipiga mafuta. Gari ilitoka nje ya gereji kinyumenyume. Reacher alimuona yule mwanaume mwenye Beretta akiwa mbali kule alipoirusha nyundo akiwatazama. Alikanyaga mafuta kuelekea barabara lilipokuwa na kupiga breki.

Jodie aliinuka kutoka kutoka sakafuni mwa gari. "Tunafanya nini hapa?"

"Tunasubiria"

"Tunasubiria nini?"

"Tunawasubiria hawa watu waondoke."

Jodie alishtuka. Alikuwa katikati ya hasira na mshangao.

"Hatuwezi kuwasubiria. Tunaenda moja kwa moja hadi kituo cha polisi."

Reacher aliuzungusha tena ufunguo kuiwasha gari ili aweze kudungua vioo kusikia sauti na kuona kilichokuwa kinaendelea nje.

"Hatuwezi kwenda kituo cha polisi." Alisema bila kumwangalia Jodie.

"Kwanini?"

"Kwa sababu polisi wataanza kunihoji mimi kuhusu Costello."

"Lakini sio wewe uliyemuua."

"Unadhani watakubali kuamini hicho unachosema?"

"Lazima wakuamini kwa sababu sio wewe uliyemuua."

"Mpaka waniamini nitakuwa tayari nimepitia vitu ambavyo sio haki yangu."

Jodie alitulia kidogo kabla ya kusema, "Unajaribu kusema nini?"

"Najaribu kusema itakuwa na faida zaidi kama nikikaa mbali na polisi."

Alitikisa kichwa chake kukataa. Reacher alimuona kupitia kioo cha dereva.

"Hapana, Reacher. Tunawahitaji polisi kuliko kitu chochote kwenye hili tatizo."

Reacher alibaki amemkazia macho kupitia kioo. "Unakumbuka enzi za Garber alipokuwa akisema polisi waende kuzimu, mimi mwenyewe ni zaidi yao?"

"Ni kweli alikuwa akisema hivyo kipindi akiwa polisi. Lakini hiyo ni zamani sana."

"Sio zamani sana kama unavyoona wewe."

Jodie alinyamaza. Akasogeza kichwa chake mbele kidogo. "Hautaki kushirikisha askari, sivyo? Sio kwamba hauwez, lakini hautaki."

Reacher aligeuza kichwa ili amtazame Jodie vizuri. Aliona chozi likidondoka kutoka kwenye macho ya Jodie.

"Wakinichokoza mimi, wanajibu kwenye mahakama yangu mimi. Sio kwenye mahakama ya mtu mwingine."

Jodie alimwangalia Reacher kwa mshangao. "Unafahamu wewe ni mtu wa ajabu? Upo kama baba. Inatakiwa twende polisi moja kwa moja."

"Siwezi kufanya huo upuuzi. Wataniweka jela kwa makosa yasio ya kwangu."

"Lakini tunatakiwa kutoa ripoti." Alisema kinyonge.

Reacher alitikisa kichwa kukataa bila kusema kitu huku akimtazama Jodie kwa ukaribu zaidi. Alikuwa ni wakili ndiyo, lakini bado alikuwa ni mtoto wa Garber na alikuwa anafahamu fika mambo yalivyo kwenye ulimwengu halisi wa nje. Jodie alikaa kimya kwa sekunde chache halafu akakigusa kifua chake.

"Upo sawa?" Reacher aliuliza.

"Uliponisukuma ulinigonga kwa nguvu sana." Alijibu.

Ningetumia nguvu ingekuwaje, Reacher aliwaza.

"Wale watu ni akina nani?" Jodie aliuliza.

"Ndiyo watu waliomuua Costello."

Jodie alitikisa kichwa halafu akaguna. Akayageuza Macho yake kulia na kushoto.

"Kwahivyo tunaenda wapi?"

Reacher alitulia. Halafu akatabasamu. "Unahisi wakitaka kututafuta sehemu ya mwisho kabisa itakuwa wapi?"

"Manhattan?" Jodie alijibu.

"Hapana. Ni kwenye nyumba." Reacher alianza kueleza. "Walituona tukikimbia, sidhani kama watadhani tunaweza kurudi."

"Umechanganyikiwa. Unalifahamu hilo?" Jodie alisema.

"Tunalihitaji lile begi nililokuwa nimebeba. Lazima Leon alikuwa ameandika kitu."

Jodie alitikisa kicha chake kukataa halafu akaa kimya.

"Na pia tunahitaji kufunga milango ya nyumba yote, haswahaswa gereji. Hatutaki vibaka waingie."

Halafu Reacher akauinua mkono wake na kuweka kidole mdomoni kama ishara kwa Jodie akae kimya. Kulikuwa na sauti ya injini ikiunguruma. Kama aina ya V8 ikiwa umbali wa yadi labda themanini. Kukawa na mkwaruzano wa matairi na barabara. Halafu umbo la gari jeusi likaonekana kwa mbele likiondoka eneo hilo - Jeep kubwa nyeusi. Labda Yukon au Tahoe. Ilitegemeana sanasana kama ilikuwa na nembo ya GMC au Chevrolet kwa nyuma. Wanaume wawili ndiyo walikuwa wamekaa ndani yake wakiwa ndani ya suti nyeusi. Reacher alitoa kichwa chake nje na kusikiliza sauti ya muungurumo wa hilo gari likififia kadri lilivyozungusha matairi yake kuelekea barabara ya kuingia mjini.

SEHEMU YA KUMI NA SITA
 
Weka tuwekeee
 
Port asante sana, huduma inaridhisha
 
SEHEMU YA KUMI NA SITA
Chester stone alisubiria ndani ya ofisi yake kwa zaidi ya lisaa limoja, halafu akapiga simu ghorofa ya chini na kumfanya Mkurugenzi wa fedha aangalie salio la benki kwenye akaunti ya kampuni inayofanya kazi. Ilionesha kulikuwa na ongezeko la dola milioni moja nukta moja ambazo zilikuwaa zimetumwa dakika hamsini zilizopita kutoka ofisi za Cayman trust Company.

"Hela ipo," Mkurugenzi wa fedha alisema. "Umefaulu, mkuu."

Chester aliishika simu kwa nguvu mkononi na kushangaa alikuwa amefaulu nini haswaa.

"Nakuja ofisini kwako mara moja," Alisema. "Nataka tujadiliane kuhusu hayo mahesabu."

"Kila kitu kipo sawa, boss." Mkurugenzi wa fedha alisema. "Hata usijali."

"Hata hivyo ninakuja." Chester alisema.

Alipanda lifti iliyomshusha ghorofa mbili chini ambako aliungana na Mkurugenzi wa fedha akiyekuwa ofisini kwake. Aliingiza neno la siri na lile jedwali lenye siri za kampuni likafunguka. Halafu Mkurugenzi wa fedha aliandika kiasi kipya kilichokuwa kwenye akaunti endeshaji ya kampuni. Kompyuta ilifanya mahesabu na ikaja na ikatoa majibu ikionesha kila kitu kitakuwavipi ndani ya wiki sita zijazo.

"Unaona," Yule bwana alisema. "Safi."

"Vipi kuhusu riba tunayotakiwa kulipa?" Stone aliuliza.

"Dola elfu kumi na moja kila wiki kwa wiki sita ni kitonga."

"Lakini tutaweza kuilipa?"

Yule Mkurugenzi wa fedha alitikisa kichwa kukubali. "Ndiyo. Kuna wasambazaji wawili tunaowadai dola elfu sabini na tatu. Nadhani hatutosubiri mpaka walipe, tunaweza tukatumia hii pesa kulipa kama riba muda huo."

Alibonyeza kitu kwenye kompyuta kuonesha alichokuwa anaongelea.

"Dola elfu sabini na tatu toa elfu kumi na moja kila wiki kwa wiki sita inatuacha cha chenchi kubwa tu. Tunaweza tukawa hata tunaenda kula chakula cha jioni kila siku."

"Rudia tena kupiga hesabu, Sawa?" Stone alisema. "Angalia tena."

Yule mkurugenzi alimgeukia Stone kumtazama. Hata hivyo alifanya alichoambiwa. Haikuwa ni kampuni yake, ilikuwa ni kampuni ya Chester. Alibonyezabonyeza kicharazio hesabu zikaanza tena. Kompyuta ilionesha dola milioni moja nukta moja za Hobie zimeisha baada ya cheki kuonesha zinatiki, halafu wale wasambazaji wawili wakapata njaa na malipo baadhi yakaingia, Hobie akalipwa hela yake na wasambazaji wakalipwa tena na jedwali likaishia kuonesha kiasi kilekile cha dola elfu saba ndizo zitakazobaki kama hela halali ya kampuni.

"Usiwaze sana, Tutaweza kujiendesha kwa hii hela bila madeni baada ya wiki sita." Yule mkurugenzi alisema.

Stone alikuwa anatazama kioo akiwaza kama dola elfu saba zingetosha kumnunulia Marilyn safari ya kwenda Ulaya. Zisingeweza! Tena safari ya wiki sita ndiyo isingewezekana kabisa. Hata hivyo, lazima ingemshtua Marilyn. Ingemfanya apate wasiwasi. Angemuuliza Chester kwanini alikuwa anamtaka aende ulaya. Na ingetakiwa Chester atoe maelezo kumwambia kila kitu. Na Marilyn alikuwa na akili. Akili nyingi kiasi cha kumfanya Chester aongee kila kitu. Halafu akijua atakataa kwenda ulaya na kuambukizwa ugonjwa wa kuangalia dali usiku kucha kwa sita. Kitu ambacho Chester hakuwa anataka.

ile begi(briefcase) lilikuwa bado lipo palepale likiwa limeanguka kwenye majani. Kulikuwa na shimo moja la risasi upande ilipoingilia. Hakukuwa na shimo la kutoka kwa risasi. Lazima ile risasi ingekuwa imepita ngozi ya ile begi na kutoboa mbao zinazotengeneza briefcase kabla haijatulia kwenye makaratasi yaliyokuwamo. Reacher alitabasamu na kulibeba kwenda kuungana na Jodie aliyekuwa gereji.

Waliufunga mlango wa gereji na kwenda kuingia ndani kupitia mlango wa jikoni kama walivyokuwa wametoka mara ya mwisho. Walienda hadi sebuleni na kulichukua begi la Jodie walilokuwa wameliacha koridoni.

Reacher alifungua ile briefcase na kutoa mafaili yaliyokuwamo. Lile kasha la risasi ilidondoka chini na kutua kwenye sakafu. Reacher alilibeba mkononi mwake halafu akamuona Jodie akimuangalia. Alilizungusha na kumrushia Jodie ambaye alilidaka na kulitupa chini kama vile lilikuwa na moto.Halafu alisogea kuungana naReacher wenye sofa.

Reacher alisikia harufu ya unyunyu wake. Hakuwa anaufahamu kwa jina, lakini hakuna shaka ulikuwa ni wa kike. Kibode alichokuwa amevaa Jodie kilikuwa saizi kubwa kidogo na kiliupa muonekano mzuri mwili wake. Suruali yake pia na mkanda vilikuwa vimekipa kiuno chake muonekano mzuri zaidi. Jodie aliinama kutazama zile karatasi.

"Tunatafuta nini?"

Reacher aliinua mabega, "Tutajua tukishakipata nadhani."

Walipekua yale makaratasi kwa muda mrefu, lakini hawakupata kitu chochote. Hakukuwa na chochote. Hakukuwa na maandishi ya muda mfupi, hakukuwa na maandishi yaliyoshabihiana angalau na tatizo lao. Zaidi kulikuwa na makaratasi ya zamani yakionesha chati za matumizi ya nyumbani na bili tu. Kitu pekee ambacho kilikuwa sio cha muda mrefu ni wosia na mirathi ukiwa umefungwa kwenye bahasha yake. Mwandiko ulikuwa msafi wa taratibu. Mwandiko wa mtu ambaye alikuwa ametoka hospitali baada ya kupata shambulio la moyo. Jodie aliuchukua wosia na kuuweka kwenye mkoba wake.

"Kuna bili zozote ambazo hazijalipiwa?" Aliuliza.

Kulikuwa na mstari ulioandikwa "pending". Hakukuwa na chochote.

"Sioni," Reacher alisema. "Lakini nadhani zitaanza kuja muda sio mrefu. Kwani huwa zinakuja baada ya mwezi au mwaka?"

Jodie alimtazama na kutabasamu, "Kila baada ya mwezi. Kila mwezi bili zinakuja."

Kulikuwa na mstari mwingine ulioandikwa "medical." Huu ulikuwa umejazwa namba za risiti za hospitali na kliniki. Reacher alianza kupitiapitia.

"Yesu wangu, ina maana matibabu ya muda mfupi huo tu yamegharimu hii hela yote?"

Jodie alirudi kutazama. "Ndiyo," Alisema. "Wewe una bima?"

Reacher alimtazama kwa jicho lisilo na kitu. "Nadhani serikali inayo ya kwangu ofisini kwao,"

"Unatakiwa kuifuatilia."

"Sidhani kama naihitaji." Reacher alijibu.

"Baba alikuwa akisema hivyohivyo kwa zaidi ya miaka sitini na tatu na miezi kadhaa ndiyo maana unaona hizo gharama zote."

Ulipita ukimya kidogo. Jodie akapiga magoti na Reacher aliona tena machozi yakimdondoka kwa mara ya pili. Akaushika mkono wake.

"Leo imekuwa siku nzito sana kwako, Pole." Reacher alimwambia.

Jodie alitikisa kichwa halafu akatabasamu kidogo.

"Siku nzito sana," Alisema. "Nimemzika baba, watu nisiowafahamu wanakuja kutaka kunipiga risasi waniue, nimevunja sheria kwa kutoripoti haya mambo yote kituo cha polisi, na halafu nimejadiliana kuungana na mtu kujichukulia sheria mkononi kulipa kisasi. Unajua baba angesema nini?"

"Angesema nini?"

Jodie aliuma midomo yake kuigiza midomo ya Garber na kuweka besi, "Yote haya ndani ya siku moja, msichana? Siku moja na unaendelea. Hivyo ndivyo angeniambia."

Reacher aliguna na kuuachia mkono wa Jodie halafu akachukua karatasi moja ambayo ilikuwa na jina na anuani ya ile hospitali ya moyo.

"Twende iliko hii hospitali tukamtafute huyo mtu aliyekutana na Garber."

SEHEMU YA KUMI NA SABA
 
Asante wakunyumba

Aroo...
 
SEHEMU YA KUMI NA SABA
Kulikuwa na mjadala mkubwa uliokuwa ukiendelea ndani ya ile Tahoe nyeusi kuhusu kama wanatakiwa kurudi au la. "Kushindwa" halikuwa neno pendwa kwenye misamiati ya Hobie. Ingekuwa vyema na afadhali kama wangeondoka tu. Ilikuwa ndiyo njia nzuri, lakini kulikuwa na tatizo moja. Hobie angewatafuta na angewapata. Ingemchukua muda mrefu ndiyo, lakini angewapata. Na hicho kiligeuza njia hiyo iwe mbaya.

Kwahivyo waliamua kutumia njia nyingine. Ilikuwa wazi walitakiwa kufanya nini. Walisimama sehemu zote walizohisi ni muhimu ili kukusanya taarifa za kila walichohisi kina umuhimu. Baadae waliingia kwenye mgahawa mmoja uliopo barabara ya tisa kununua muda kidogo. Mpaka wakati ambao walifika ghorofa namba themanini na nane jengo la WTC walikuwa wamekwishayapanga maneno ya kuongea.

"Ilikuwa ngumu sana," Yule mwanaume wa kwanza alisema. "Tumesubiria kwa muda mrefu ndiyo maana tumechelewa. Kulikuwa na wanajeshi wengi waliohudhuria pale na mikononi walikuwa wamebeba silaha zao."

"Walikuwa wanajeshi wangapi?" Hobie aliuliza.

"Wanajeshi?" Mwanaume wa pili aliuliza na kujijibu. "Zaidi ya kumi na tano. Walikuwa wanazungukazunguka kila eneo la nyumba hivyo ilikuwa ngumu kidogo kuwahesabu. Ni kama walikuwa wanatoa heshima zao za mwisho."

"Mrs. Jacob aliondoka nao wakiwa wamemsindikiza," Mwanaume wa kwanza alisema. "Nadhani walikuwa wanaenda kutembelea makaburi na wakapitia hukohuko maana hawakurudi tena."

"Hamkufikiria kuwafuatilia."

"Isingewezekana," Mwanaume wa pili alisema. "Kulikuwa na msafara mkubwa wa magari yaliyokuwa yanaenda polepole. Ingekuwa ngumu kujipachika mwisho wa msafara wa msiba."

"Na yule baunsa wa keys mliyesema mlimuona?"

"Yeye aliondoka mapema kuliko wote. Tukaamua kuachana naye kama ulivyosema. Tulikuwa tumeyaelekeza macho yetu kwa Mrs. Jacob kama ulivyotuambia na tayari tulikuwa tumekwisha mjua."

"Halafu mkafanya nini tena?"

"Tuliamua kuikagua ile nyumba," Mwanaume wa kwanza alianza kueleza. "Lakini ilikuwa imefungwa - Kwahivyo tukaenda maktaba. Nyumba ilikuwa imesajiliwa kwa jina la mtu anaitwa Leon Garber. Tulipomuuliza dada wa mapokezi kama alikuwa anafahamu chochote kuhusu Leon Garber akatuonesha habari kwenye gazeti. Leon Garber ndiye alikuwa amekufa kwa shambulio la moyo. Alikuwa ni mgane na ndugu yake pekee wa karibu ni mtoto wake anayeitwa Jodie ambaye sisi tulikuwa tunamfahamu kama Mrs. Jacob. Ni binti mdogo, lakini wakili mwenye heshima wa kampuni ya Spence & Gutman iliyopo Wall Street na nyumba anayokaa ipo Broadway hapahapa New York."

Hobie alitikisa kichwa kukubali na kuliweka chuma lake juu ya meza huku akiigongagonga kwa utaratibu maalumu.

"Na huyu Leon Garber ni nani haswa?"

"Alikuwa polisi wa wanajeshi, Miltary Police." Mwanaume wa kwanza alisema.

Mwanaume wa pili aliongeza, "Amestaafu akiwa na nyota tatu na nishani zisizohesabika. Amehudumu Korea, Veitnam na kila sehemu unayoijua kwa miaka arobaini bila kupumzika."

Hobie aliacha kuligongagonga chuma lake. Aliganda kama sanamu huku rangi ikitoweka usoni kwake na kulifanya kovu lake liwe kavu.

"Askari polisi wa wanajeshi," Hobie alirudia kwa sauti ya chini.

Halafu akaganda tena na yale maneno mdomoni kwake kwa muda mrefu. Aliliinua chuma lake kutoka kwenye meza na kulisogeza karibu na uso wake. Chuma lilikuwa linatetemeka.

"Askari polisi wa wanajeshi," Alisema tena huku akiangalia chuma lake. Halafu akayahamisha macho yake kuwatazama wale wanaume wawili.

"Toka nje," Alimwambia yule mwanaume wa pili.

Yule mwanaume alimtazama mwenzake kabla ya kutoka nje na kuurudishia mlango nyuma yake taratibu. Alipotoka Hobie alisukuma kiti chake na kusimama. Aliizunguka meza yake na kwenda kusimama nyuma ya yule mwanaume wa kwanza ambaye alikuwa amekaa kwenye sofa tu bila kujichezesha wala kugeuka nyuma kumuangalia Hobie. Alikuwa amevaa Kola ya pembeni saizi ya sita ambayo iliipa shingo yake umbo la duara kamili.

Chuma la Hobie lilikuwa kama herufi J likiwa na ukubwa mzuri tu. Alilitembeza kwa kasi na kuliweka kwenye koo ya yule mwanaume kuivaa shingo yake. Akapiga hatua moja nyuma na kuanza kuvuta chuma lake kwa nguvu kutumia mwili wake wote. Yule mwanaume alitapatapa huku akilishikashika chuma la Hobie kujinyofoa bila mafanikio. Hobie alitabasamu na kulivuta kwa nguvu zaidi. Madaktari walikuwa wamefanya kazi nzuri kuhakikisha litakapoungwa halinyofoki kuachana na sehemu ndogo ya mabega ya Hobie. Hobie aliendelea kulivuta lile chuma kwa nguvu hadi yule mwanaume alipoanza kuishiwa nguvu na kulegea. Hobie alipoona hivyo alilegeza chuma lake. Halafu akasogea masikioni kwa yule mwanaume.

"Yule mwenzako niliyemtoa nje alikuwa na alama kubwa ya kupigwa na kitu kizito usoni . Imetokea wapi?"

Yule mwanaume hakujibu. Alikuwa anatafuta pumzi. Hobie alilizungusha chuma lake pale kwenye koo la yule mwanaume kwa njia ya kuifanya ncha iliyo mwisho ikae mkao wa kutoboa koromeo la yule mwanaume.

"Ile alama imetokea wapi?"

Yule mwanaume alikuwa anafahamu fika kwa namna ile ncha ilivyokuwa imekaa ingeweza kutoboa ngozi yake na kusababisha madhara makubwa kwenye taya yake. Hakuwahi kuwa mwanafunzi wa baiolojia au mfumo wa mwili wa binadamu, lakini alikuwa na hakika kifo kilikuwa karibu yake.

"Nitakuambia, Nitakuambia." Alisema.

Hobie alilivuta chuma lake kidogo na kulilegezalegeza kila mara ambapo yule mwanaume alionekana kusita kuongea jambo. Kwahivyo hadithi nzima na ukweli wote vilichukua dakika tatu tu, mwanzo hadi mwisho bila kuongeza au kupunguza nukta.

"Umeniangusha," Hobie alisema.

"Ndiyo, Tumekuangusha," Yule mwanaume alikoroma. "Lakini lilikuwa kosa la mwenzangu. Hakuthubutu kufyatua risasi kama mimi. Hakuwa na faida yeyote."

"Hakuwa na faida akilinganishwa na nini? Na wewe?"

"Ni makosa yake," Yule mwanaume alikoroma tena, "Mimi bado nina faida kwako."

"Unatakiwa unithibitishie hilo."

"Kwa vipi? Tafadhali niambie."

"Rahisi sana. Unaweza kufanya nitakachokuambia?"

"Ndiyo," Alikoroma tena. "Chochote kile."

"Niletee Mrs. Jacob." Hobie alifoka.

"Ndiyo," Sauti yake ilikuwa kama anayenong'ona kuliko kuongea.

"Na usifeli tena," Hobie alifoka tena.

"Hatuwezi kukuangusha tena. Ninakuahidi."

Hobie alianza kuzungusha tena chuma lake likiendana na kasi ya maneno aliyokuwa anasema. "Sio hamuwezi. Utakuwa peke yako kwa sababu kuna kitu kingine nataka unifanyie?"

"Kitu gani," Yule mwanaume alikoroma. "Nipo tayari."

"Mfute huyo mwenzako asiye na faida," Hobie alinong'ona kwa sauti ya chini kidogo. "Na iwe leo usiku mtakapoenda kuutupa mwili wa huyo katibu muhtasi."

Yule mwanaume alitikisa kichwa chake kwa nguvu kukubali kwa kadri chuma lilivyompatia nafasi. Hobie akalitoa kwenye shingo yake. Yule mwanaume alianza kuhema kwa kasi ya ajabu.

"Na uniletee mkono wake wa kulia kama uthibitisho," Hobie alisema.
 
SEHEMU YA KUMI NA NANE
Waligundua kwamba kliniki aliyokuwa anahudumiwa Leon Garber ilikuwa ni kitengo kidogo ndani ya hospitali kubwa ya binafsi. Kulikuwa na jengo kubwa la ghorofa lililokuwa limepakwa rangi nyeupe na majina ya kila kitengo yalikuwa yamebandikwa. Kulikuwa na ofisi za madaktari aina zote , lakini wote walifanya kazi pamoja kutegemeana na ukubwa wa tatizo la mgonjwa. Hivyo daktari aliyekuwa akimhudumia Garber alikuwa akizunguka huku na huko. Alikuwepo ICU, halafu akaenda kwenye ofisi ya wagonjwa wa nje na kurudi tena ICU kabla hajaenda ofisini kwake kuonana na wagonjwa wake wa moyo.

Jina lake lilikuwa limeandikwa kwenye risiti za Leon kama Dr. McBannerman ambaye Reacher alimfikiria angekuwa mwanaume mzee mwenye mvi na sauti nzito hadi Jodie alipomwambia McBannerman alikuwa ni mwanamke tu. Walipolipaki gari la Jodie na kushuka walienda moja kwa moja hadi zilipokuwa ofisi za kitengo cha moyo.

Dada aliyekuwepo mapokezi alikuwa mnene kuliko sauti yake ya kitoto. alimkaribisha Jodie kwa sauti yenye mchanganyiko wa huzuni. Aliwaambia wamsubiri McBannerman sehemu ya mapokezi jambo ambalo liliwapa Reacher na Jodie muda wa kutupia macho hapa na pale.

Ofisi ya McBannerman ilikuwa kama ofisi nyingi za madaktari zilivyo. Haikuwa na kelele na anga lake lilikuwa na harufu nzito ya dawa. Kulikuwa na picha za mfumo wa damu na za moyo. Jodie alikuwa akiangalia mchoro wa picha ya moyo kama anayejiuliza ni sehemu gani iliyofeli kwenye moyo wa baba yake.

Reacher pia alikuwa akiiangalia hiyo picha. alianza kuuhisi moyo wake. Ulikuwa unapiga polepole kwenye kifua chake.

Walikaa hivyo kwa dakika kumi halafu mlango wa ofisi ya ndani ukafunguliwa na Dr McBannerman akaungana nao. Alikuwa amevaa koti jeupe huku akiwa ameningi'iniza kifaa cha kupimia mapigo ya moyo, Slesoskopu, kwenye mabega yake.

"Jodie," Alisema. "Pole sana kwa msiba."

Alimaanisha kila alichokisema kwa asilimia 99%. Asilimia moja haikuwepo kwa sababu ya mashaka na wasiwasi pengine Jodie alikuja kumtaarifu anamfungulia mashtaka ya kuwa mzembe kazini, Reacher aliwaza. Mtoto wa mgonjwa aliyefariki alikuwa ni wakili na alikuwa amekuja kumuoa ofisini kwake baada ya kutoka msibani. Jodie aliyasoma mashaka ya McBannerman pia.

"Nimekuja kukushukuru," Alisema. "Umefanya kazi kubwa sana."

Presha ya McBannerman ilishuka. Alitabasamu na Jodie akayarudisha macho yake kwenye ule mchoro wa moyo tena.

"Kwahivyo ni sehemu gani iliyofeli?" Aliuliza.

"Kusema kweli, moyo wake wote ulifeli. Unajua moyo ni mashine kubwa na ngumu kuelezea. Wenyewe unadunda na kudunda kusukuma damu mara mamilioni kwa mwaka mmoja. Ukidunda kwa miaka tisini ni mapigo zaidi ya mabilioni, huo kitaalamu tunaita moyo uliyozeeka. Kama ukidunda kwa miaka sitini tunauweka kwenye kundi la moyo mchanga. Hata hivyo , punde au baadae moyo wa mtu yeyote huwa unaacha kusukuma damu."

Alimaliza maelezo yake na kumtazama Reacher kwa sekunde kadhaa. Reacher alihisi McBannerman alikuwa akiangalia kama ana dalili za maradhi ya moyo. Halafu akagundua alikuwa hajajitambulisha.

"Jack Reacher," Alisema "Ni rafiki wa muda mrefu wa Garber."

McBannerman alitikisa kichwa kukubali. "Meja Reacher, Ulikuwa haukauki mdomoni mwa Leon."

Ukapita ukimya kidogo kati yao.

"Hakuna jambo jingine alilowahi kuzungumzia?" Jodie aliuliza.

McBannerman alimtazama kwa jicho la kuhoji kama Jodie ilikuwa ameathirika kisaikolojia. Garber hakuwa bubu, kwa vyovyote vile alikuwa anaongea mambo mengi kama kufa na kuishi.

"Kitu kingine cha aina ipi?" McBannerman aliuliza.

"Sina uhakika," Jodie alieleza. "Lakini ni kama kuna mgonjwa wako mwingine aliyezungumza naye."

McBannerman aliinua mabega kuonesha hajui halafu akawa kama aliyekumbuka jambo. "Nakumbuka kuna siku alininiambia amepata shughuli muhimu na nzito."

"Shughuli ipi?"

McBannerman alitikisa kichwa "Hakunipa maelezo ya shughuli yenyewe. Kwanza alisema ataipuuzia lakini siku chache baadae alionesha kuvutiwa na hiyo shughuli."

"Ilikuwa inahusiana na mgonjwa wako mwingine?" Reacher aliuliza.

"Sifahamu kwakweli. Lakini inawezekana. Wagonjwa wangu huwa wakifika hapo mapokezi huwa wanaongeleshana kama njia ya kufarijiana kwa wanachokipitia."

"Hiyo shughuli aliyoipata alianza kuiongelea lini?" Reacher aliuliza, haraka.

"Mwezi wa tatu mwishoni au wa nne mwanzoni. Sikumbuki vizuri ila ilikuwa baada ya kumruhusu awe mgonjwa wa matibabu ya nje. Nadhani kabla hata hajaenda Hawaii."

Jodie alishtuka. "Alienda Hawaii. Sina hiyo taarifa."

"Mimi pia sikuwa nayo. Nakumbuka hakuhudhuria kliniki siku moja ndipo nikamuuliza alikuwa wapi akasema alienda Hawaii mara moja."

"Hawaii? Kwanini alienda bila kukuambia anaenda huko?" Reacher aliuliza.

"Sijui kwanini hata alienda." McBannerman alijibu.

"Afya yake ilikuwa imara kwa safari?" Reacher aliuliza.

"Hapana na ninadhani ndiyo maana alikuwa anafichaficha kuhusu safari yake hiyo."

"Kwani aliruhusiwa kuwa mgonjwa wa nje lini?"

"Mwishoni mwa mwezi wa tatu,"

"Na safari ya Hawaii?"

"Mwanzoni mwa mwezi wa nne nadhani."

"Ok," Reacher alisema. "Unaweza kutupa orodha ya wagonjwa wako wengine kati ya kipindi hicho. Machi na Aprili. Watu ambao unahisi ndiyo Garber alikuwa anawasiliana nao?"

McBannerman tayari alikuwa anatingisha kichwa chake kukataa. "Samahani. Nasikitika taratibu na maadili ya kazi yangu hayaniruhusu kutoa taarifa za wateja wangu."

Alikuwa akimwambia Jodie, maongezi kati ya daktari na wakili, mwanamke kwa mwanamke na kwa jicho la unajua fika haya mambo yanafanyika vipi.

Jodie alielewa. "Pengine tunaweza kujaribu kumuuliza huyo dada wa mapokezi kama aliwahi kumuona mzee akiwa na mahusiano ya karibu ya kuwasiliana na mgonjwa wako mweingine. Nadhani hiyo itakuwa sio kutoa siri za mteja wako - Itakuwa ni maongezi ya kawaida tu!"

McBannerman alikuwa anajua utu na muda wa kuuonesha. Alibonyeza simu yake ya mezani na kumuomba dada wa mapokezi aende ofisini kwake. Alipoulizwa swali alianza kujibu kabla swali halijaisha.

"Ndiyo, Garber alikuwa akiongea mara kwa mara na yule mzee mwenye matatizo ya mishipa ya kuingiza damu ya hewa safi.... Yule ambaye mke wake huwa anamleta na gari lililochokachoka kwa sababu ulimkataza asiendeshe gari yeye mwenyewe.... Nahisi Garber alikuwa na kitu f'lani anataka kuwasaidia.... Walikuwa wakija na picha na kumuonesha."

"Mzee Hobie?" McBannerman aliuliza.

"Ndiyo." Yule dada alijibu.

SEHEMU YA KUMI NA TISA
 
Back
Top Bottom