Riwaya: SIN

SIN 124


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


Magreth akaichomeka bastola yake kiunoni mwake na kuifunika na tisheti yake ndefu aliyo ivaa. Akatoka ndani hapo huku akisikilizia jinsi kengele ya mlangonimwake jinsi inavyo toa mlio, akafungua geti dogo na akajifanya akishangaa uwepo wa makamu wa raisi Madenge Jr.
“Muheshimiwa”
“Yaa je tuna ruhusiawa kuingia ndani?”


Makamu wa raisi Madenge Jr alizungumza huku akiwa amejawa na tanasamu pana sana usoni mwake. Magreth akawatazama walinzi hao kumi walio simama pembeni ya raisi Mtenzi na katika sekunde hizo chache akaweza kugundua uwezo wao pamoja na udhaifu wao na hata likitokea jambo lolote basi ata weza kulihimili.





ENDELEA


“Yaa karibu sana muheshimiwa. Hii ni big suprize kwangu”
“Ni kweli, sikuhitaji kuwafaamisha nikaona nije mwenyewe”
“Ume pajuaje hapa muheshimiwa?”
“Ahaa…niliagiza vijana wangu waweze kuwafwatilia. Kama muliweza kuja ikulu basi nami nikaona sio mbaya leo nije kuonana nanyi”
“Tuna shukuru sana, muheshimiwa karibu sana ndani”
Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Makamu wa raisi akaingia sebleni na walinzi wake wawili huku wengine wakibaki nje kuimarisha ulinzi.


“Shikamoo muheshimiwa”
Josephine alisalimia kwa heshima zote.
“Marahaba habari ya wewe?”
“Nina smshukuru Mungu ana saidia”
“Karibu ukae muheshimiwa”
“Nashukuru. Mume jitahidi, eneo hili ni zuri sana”
“Asante sana muheshimiwa. Je nikuandalie nini muheshimiwa?”
Magreth alizungumza kw afuraha iliyo mfanya Josephine naye kujiamini.
“Nime toka kula usiku huu, hivyo musi sumbuke sana. Ahaa Jose nime kuja kwanza kukushukuru kwa kuweza kutuonyesha ni wapi raisi Mtenzi alipo kuwa ame fukiwa na kile kifusi cha hoteli. Pili tume pata tatizo ambalo kwa kweli tuna amini kwamba wewe uta kuwa ni msaada mkubwa sana kwetu”
Makamu wa raisi alizungumza kwa sauti ya utaratibu na iliyo jaa hekima kubwa sana. Ukimtazama kwa haraka haraka una weza kusema ni mtu mwema na mwenye roho ya upendo. Ila sumu na tamaa inayo endelea kuchemka moyoni mwake kwa kweli ni jambo la hatari sana.


“Tatizo gani muheshimiwa?”
“Leo mchana raisi Mtenzi aliweza kuondolea hospitalini na watu ambao tuliweza kunyaka matikio yao kwenye cctv camera, ila kwa bahati mbaya hatukuweza kuona sura zao. Watu hao mmoja wao alikuwa ni mwanamke ambaye ana oneana ana uwezo mkubwa sana wa upambanaji na mtu wa pili ni mwanaume. Walimuondoa raisi Mtenzi hospitalini na hadi sasa hivi hatufahamu ni wapi walipo, pia nina imani kwamba ulikuwepo kwenye eneo la tukio na ulishuhudia jinsi mwanamke huyo alivyo kuwa ana wapiga wanajeshi wangu?”
“Ndio muheshimiwa na pia nili muadisia rafiki yangu juu ya jambo hilo”
“Kwa kweli, nina shinda hata hii taarifa kuitoa kwenye vyombo vya habari kwani watu wata niona kwamba sio muwajibikaji. Ila nilipo kaa sana na kutafakari, nika kumbuka kwamba upo wewe mwenye uwezo wa maono yajayo au yaliyopo. Basi kwa heshima zote, nina kuomba uweze kumuomba Mungu wako aweze kutuonyesha sehemu alipo raisi wetu mpendwa bwana Mtenzi”
Josephine akashusha pumzi huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Laiti kama ninge kuwa na uwezo wa kupambana basi ninge pambana na yule aliye muiba raisi pale hospitalini ila sikuwa na uwezo wa kupigana.”
“Ni kweli, na hata kwenye cctv camera niliweza kuona ni jinsi gani ulivyo kuwa una duwaa”
“Nita muomba mwenyezi Mungu na akinionyesha ni wapi alipo raisi Mtenzi basi nita kuambia muheshimiwa”
“Je huna hisia zozote za sehemu alipo?”
“Mmmm hapana muheshimiwa. Ila ngoja nisali kidogo”
Josephine akafumba macho yake kwa dakika moja nzima kisha akaafumbua.
“Nime pata jambo muheshimiwa”
“Jambo gani?”
“Kuna mtu alipanga kumuua raisi Mtenzi hivyo hapa malaika wa Mungu wame niambia kwamba ata kuja kuonakana akiwa na afya yake njema na ata rudi kuiongoza serikali yake kwani yey ndio chaguo sahihi la mwenyezi Mungu”
Makamu wa raisi mapigo yake ya moyo yakampasuka mithili ya mftuza lililo chomwa na pini. Mapigo yake ya moyo yakazidi kuchanganya, akahisi kijasho kina kwenda kumwagika, akatoa kitambaa chake na kujifuta usoni mwake.
“Je….je…je..je…huja onyesha huyo aliye taka kumua?”
“Mmmm acha niombe tena”
Josephine akafumba macho na kumfanya Magreth kumtazama makamu wa raisi jinsi anavyo pepesa pepesa macho kwani hapo ana hisi kwamba ana kwenda kutajwa yeye. Taratibu Josephine akafumbua macho yake na kumtazama makamu wa raisi.


“Nime onyeshwa muuaji”
“Ni..ni…nani?”
“Kuna daktari mmoja alipanga kumchoma sindano ya sumu raisi Mtenzi ila sijamfahamu kwa jina ila nikimuona basi nina weza kumtambua”
“Kweli!!?”
Makamu wa raisi alizungumza kwa mshangao huku mapigo yake ya moyo kidogo yakitulia taratibu.


“Ndio”
“Basi tuta hakikisha kwamba huyo daktari tuna mpata na ata eleza ni kwa nini alipanga kufanya hivyo. Je una weza kuona ni sehemu gani alipo raisi Mtenzi”
“Ndio nime onyeshwa”
Magreth moyo wake uka mstuka sana huku na akamtazama Josephine ambaye ana tambua kwamba janaga moyo wa kudanganya.


“Ni wapi?”
Makamu wa raisi aliuliza huku akijiweka sawa kwenye kiti chake.


“Yupo mkoani Morogoro, ila sijatambua ni sehemu ani ambayo yupo ila nina onyeshwa yupo katikati ya mashamba ya mpanga”
“Kwa hiyo yupo Morogoro?””
“Ndio ila sifahamu ni eneo gani?”
“Basi nina shukuru sana binti, acha nikatume vijana kuhakikisha wana kwenda kumtafuta. Morogoro ni eneo dogo sana hivyo tuna weza kulipata kwa muda mfupi tu”
“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi akaaga na akatoka ndani hapo, akaingia kwenye gari na kushusha pumzi.


“Vipi muheshimiwa?”
“Ilikuwa bado kidogo huyu msichana kunijua. Ila maono yake yame angukia kwa daktari”
“Duu hivi ana ona kweli?”
“Ndio, kwa maana ame juaje kama raisi alitaka kuuwawa. Alijuaje kama kuna dokta alipanga kumuu. Huyu binti anacho kifanya ni kitu cha uhakika”
“Duuu sasa tuna fanyaje?”
“Hakikisha kwamba dokta Masangi ana patikana kabla ya hili jambo halijakwenda vizuri na ameniambia kwamba raisi yupo mkoni Morogoro. Hivyo nina hitaji kuwasiliana na mkuu wa mkoa wa Morogoro aweze kuhakikisha ana tuma vijana kwenye kila sehemu yenye mashamba mkoni hapo ili kuhakikisha raisi ana patikana”
“Sawa mkuu”
Msafara huo ukaondoka nyumbani hapo kwa Magreth na kumfanya kupata amani kidogo. Akafunga geti lake kwa ndani na kurudi sebleni na kumkuta Josephine akiwa katika wasiwasi.
“Ita kuwjae akaenda Morogoro na akashindwa kumkuta?”
“Shauri yao. Kwanza ni muuaji, hapa nilipo kuwa nina mtazama kwenye macho yake niliweza kuona kabisa ana wasiwasi”
“Mmmm yaani nime ogopa sana bado nusu tu nimtaje yeye mwenyewe kwamba ndio muuaji”
“Duu. Ila ume tumia njia nzuri. Ila ina bidi kuimarisha ulinzi kwa raisi la sivyo hawa watu wana weza kurudi”
“Ni kweli je kuna mtu gani ambaye yupo serikalini una muamini?”
Magreth akashusha pumzi huku akimtazama Josephine, akatoa simu mfukoni mwake na kumpigia RPC Karata.
“Magreth habari yako”
“Salama kaka yangu upo wapo?”
“Nime rudi Dar es Salaam si una jua hali iliyo tokea”
“Sawa nina weza kukuona au ukaja nyumbani kwangu”
“Kuna tatizo?”
“Kuna jambo muhimu sana?”
“Ndio kuna jambo muhimu kaka yangu”
“Basi nina kuja si hapo Kigamboni?”
“Ndio”
“Basi dakika ishirini nita kuwa hapo kwa maana nipo kwenye patroo”
“Sawa kaka”
Magreth akakata simu, honi ya gari lake mlangoni ikamfanya atoke, akachungulia nje na kumuona Juma. Akafungua geti kubwa na akaingiza gari hilo ndani.
“Aisee barabara ina lete shinda sana”
“Pole hata sisi wenyewe tume ona. Ila gari halija leta shida?”
“Hii mashine boss sijapata shida yoyote njiani”
“Sawa”
Magreth akashusha mizogo yao na kuingiza ndani kwake. Josephine akagonga mlangoni mwa chumba alichopo dokta Masawe.
“Ni mimi”
Josephine alizungumza mara baada ya kuona dokta Masawe ana chelewa kufungua mlango huo. Taratibu Mlango wa chumba hicho ukafunguliwa.
“Vipi wame ondoka?”
“Ndio”
Dokta Masawe akashusha pumzi taratibu huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana. Dokta Masawe akatoka hadi sebleni na kuchungulia akamkuta Juma.
“Huyu ni nani?”
Dokta Masawe aliuliza huku akiwa amejwa na wasiwsi mkubwa snaa moyoni mwake.


“Huyu kijana wangu. Tafadhali nina kuomba usiwe na mashaka naye. Alafu Juma kun……..”


Magreth kabla ya kumalizia sentensi yake, akasikia honi mlangoni na akatoa na kwenda kufungua geti. Akamkuta RPC Karata akiwa ameongozana na vijana wake wanne.
“Muna weza kunisubiria”
“Sawa mkuu”
RPC Karataa akaongozana na Magreth na wakaingia ndani. Dokta Masawe akastuka mara baada ya kumuona RPC Karaka kwani wana fahamiana.
“Masawe ndugu yangu upo?”
“Nipo kaka”
“Kumbe una fahamiana na mdogo wangu”
“Ndio ndio”
“Kaka nime kuita hapa kwa jambo moja. Ila nina hitaji kufahamu mume fikia wapi katika kumtafuta raisi?”
“Bado ngoma droo. Hali ime kua sio hali ndani ya nchi”
“Je mume weza kufahamu sababu za yeye kutoweka?”
“Hapana, sijafahamu bado ila si unatambua kwamba nina fwata amri ya wakubwa wangu na wala hupaswi kuuliza sana”
“Sawa kaka yangu, kati ya binadamu ambao nina waamini naamini kwamba una tambua wewe ni mmoja wapo”
“Nashukuru kwa hilo Magreth.”
“Huyu ni dokta Masawe kama mulivyo fahamiana. Pia ni ndio daktaria anaye itazama afya ya raisi Mtenzi”
“Ana itazama kivipi?”
“Mimi ndio mtu niliye mtorosha raisi Mtenzi hospitalini.”
“Wewe!!?”
RPC Karata alizungumza kwa mshangao.
“Ndio”
“Wewe ndio ume wapiga wale wanajeshi?”
“Ndio na raisi yopo hapa”
“Kwa nini sasa ume mtorosha”
“Makamu wa raisi lisaa moja alikuwepo hapa. Ishu yake ilikuwa ni kuuliza ni wapi alipo raisi Mtenzi”
“Ana wauliza nyinyi kwa nini?”
“Ndugu yangu hapa Josephine ana uwezow a kuona maono ya sehemu alipo mtu yoyote anaye mkusudia na huyu ndio alitoa ripoti ya swala la milipuko inayo endelea na pia ndio alionyesha raisi sehemu alipo fukiwa.”
“Ahaa sasa hapo nime waelewa. Ehee kwa hiyo mume mueleza makamu wa riais kwamba raisi mupo naye?
“Hapana”
“Kwa nini sasa?”
“Kwa maana raisi yeye ndio ana husika katuka kutka kuyaondoa maisha ya raisi Mtenzi”
“NINI?”
“Ndio, ana husika na alimuagiza dokta Masawe ili amuue raisi Mtenzi na baada ya jaribio kushindikana, makamu wa raisi akatuma mlinzi wake ili kumua dokta Masawe”
“Mungu wangu, hii nchi sasa ina elekea wapi?”
“Ndio hivyo kaka yangu. Hapa ninavyo zungumza, Josephine ame wadanganya kwamba raisi Mtenzi yupo mkoani Morogoro na usishangae ikatolewa amri ya askari kuelekea mkoa wa Morogoro kumtafuta raisi Mtenzi”
RPC Karata akashusha pumzi kwani hayo anayo yasikia na jinsi anavyo mfahamu makamu wa raisi bwana Madenge Jr ni mtu mwema na ambaye hana matatizo na viongozi wa chini yake.
“Raisi yupo wapi?”
Magreth akatangulia na RPC Karata akamfwata kwa nyuma. Wakaingia katika chumba hicho na RPC Karata hakuamini kumuona raisi Mtenzi sehemu huyo. RPC Karata machozi yakaanza kumlenga lenga na kumfanya Magreth kujawa na mshangao kwani hajui ni kwa nini RPC Karata ametawaliwa na huzuni kubwa kama hiyo ikiwa yeye ni askari mkakamavu.


ITAENDELEA


Haya sasa, RPC Karata ame muona raisi Mtenzi kwa nini ame jawa na msisitizo, makamu wa raisi ame danganywa je ata weza kumpata raisi Mtenzi ili kukamilisha zumuni lake la kumuua kiongozi wake huyo? Usikose sehemu ya 125.
 
SIN 125


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188




ILIPOISHIA


“Mungu wangu, hii nchi sasa ina elekea wapi?”
“Ndio hivyo kaka yangu. Hapa ninavyo zungumza, Josephine ame wadanganya kwamba raisi Mtenzi yupo mkoani Morogoro na usishangae ikatolewa amri ya askari kuelekea mkoa wa Morogoro kumtafuta raisi Mtenzi”
RPC Karata akashusha pumzi kwani hayo anayo yasikia na jinsi anavyo mfahamu makamu wa raisi bwana Madenge Jr ni mtu mwema na ambaye hana matatizo na viongozi wa chini yake.
“Raisi yupo wapi?”
Magreth akatangulia na RPC Karata akamfwata kwa nyuma. Wakaingia katika chumba hicho na RPC Karata hakuamini kumuona raisi Mtenzi sehemu huyo. RPC Karata machozi yakaanza kumlenga lenga na kumfanya Magreth kujawa na mshangao kwani hajui ni kwa nini RPC Karata ametawaliwa na huzuni kubwa kama hiyo ikiwa yeye ni askari mkakamavu.





ENDELEA


“Huyu mzee kipindi nilipo kuwa depo alinilelea kama kijana wake. Alinipenda sana kwa maana nilikuwa mchapakazi na pia alinipa kazi ambayo kusema kweli haiwezi kufutika kwenye ufahamu wangu wa akili”
“Kazi gani?”
Magreth alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama RPC Karata usoni mwake.
“Mwanaye wa kwanza alikuwa ni jambazi katika mkoa wa Kagera. Alijihusisha na maswala ya utekaji wa magari na mambo mengi sana ya kihalifu. Kipindi hicho muheshimiwa alikuwa ni RPC Katika mkoa huo wa Kagera. Alinipa kazi ya kumuua mwanaye na genge lake hivyo nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha nina lisambaratisha genge hilo na niliweza kufanikiwa”
“Duu kwa hiyo alijua kabisa kwamba una muua mwanaye?”
“Ndio, hapakuwa aliye amini kama muheshimiwa atatoa ruhusa hiyo. Isitoshe ana watoto wawili tu wa kiume mmoja ni yule niliye muua na mwengine ni huyu Jery ambaye kwa kipindi hicho alikuwa bado mdogo sana”
“Ahaa kwa hiyo Jery na kaka yake walipishana kwa miaka mingi?”
“Yaa walipishana miaka mingi. Baada ya hapo mimi ndio nikawa mwanaye wa hiyari na nina muheshimu kama baba yangu hadi leo”
RPC Karata alizungumza huku akijifuta machozi usoni mwake.
“Una uhakika kwamba makamu wa raisi alihitaji kumuua raisi?”
“Ndio na Josephine ndio aliye weza kuliona jambo hilo na baada ya hapo tuka fanya jitihada za kwenda kumuokoa katika hospitali ya Muhimbili. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuhakikisha kwamba ina pambana na wale wanajeshi na nilifanikiwa kumtoa raisi pale hospitalini. Endapo tunge chelewa kutekeleza jambo hilo basi nina uhakika wa asilimia mia moja sasa hivi raisi ange kuwa maiti kwani dokta Masanja ame kiri kabisa kwamba yeye ndio alipewa dili hilo la kumuua raisi Mtenzi.”
“Masawe huyu?”
“Ndio yeye ndio alipewa jukumu la kumuua raisi Mtenzi tena kwa kumchoma sindano ya sumu”


RPC Karata macho yakamtoka. Akachomoa bastola yake kiunoni na kutoka chumbani hapo huku akiwa amejawa na hasira kali sana. Akatoka chumbani hapo na breki ya kwanza kufika sebleni, akamkwida dokta Masawe shati lake maeneo ya kifuani huku bastola yake akiwa ameiweka chini ya kidevu ya dokta huyo. Juma na Josepgine macho yakawatoka huku wakiwa hawaelewi ni kwa nini RPC Karata ana amuua kufanya hivyo kwa mtu ambaye walikuwa wana changamkiana dakika chache zilizo pita.


“Niambie ni kwa nini ulihitaji kumuua raisi?”
Dokta Masawe mwili mzima ukaanza kumetetemka haja ndogo akashindwa kuizuia na kujikuta akilowanisha suruali yake. Magreth hakuhitaji kuingilia ugomvi huo na zaidi alihitaji RPC Karata aweze kusika ukweli wa jambo hilo.
“Ni…n…ni…m….a..ka..mu wa…raisi alinipa kazi..ya kumuua”
“Alikuahidi kukupatia nini?”
“Mi..li…oni mi…a na kuni…pandi.sha cheo”
Dokta Masawe alizungumza kwa sauti iliyo jaa kigugumiza sana.
“Ulikula kiapo hichi ndio ulicho kiamua kukifanya. Milioni mia moja na cheo kwa uhai wa kiongozi mkubwa wa nchi. Raisi eheee?”
RCP Karata aliendelea kufoka na dokta Masawe akakosa majibu.
“Watu kama nyinyi hamstahili kuishi kabisa”
RPC Karata alizungumza na kumsukumia dokta Masawe kwenye sofa akakoki bastola yake kwa kuziruhusu risasi ziwete kutoka.
“NAOMBA UNISAMEHEE NDUGU YANGU NIPO TAYARI KUMUHUDUMIA RAISI HADI APONE. NAOMBA NAFASI NYINGINE”
Dokta Masawe alizungumza huku akiwa amepiga magoti chini na kuvifumbata viganja vyake kwa pamoja huku akilia kwa uchungu sa kujutia kwa kutanguliza tama ayake mbele pasipo uzalendo.
“Endapo baba yangu mlezi ata kufa. Basi wewe nawe uta kufa na sinto kuacha. Fala wewe”
RPC Karata mara baada ya kumaliza kuzungumza hivyo akachomoa magazine ya bastola yake na kuirudisha kiunoni huku magazine akiichomeka mfuko wake wa nyuma.
“Nashukuru sana”
Dokta Masawe alizungungumza kwa huzuni kubwa sana hadi Juma na Josephine wakamuonea huruma.


“Mage nina kupa ruhu ya kumuya huyu mpumbavu, endapo ata dhubutu kutoroka, au kumuua raisi. Sawa”
“Sawa kaka”
“Nina ondoka nina endelea na patrol ya mji. Nikiendelea kukaa hapa nina weza kumuua huyu mpumbavu”
“Sawa sawa. Alafu kuna vifa aliagiza dokta Masawe kwa ajili ya kumtibu raisi. Nina omba kama ita wezekana uwende na Josephine Agakhan kuna daktari mmoja dokta Masanja ame agiza muonana neya ata pewa hivyo vifaa. Ukiwepo na wewe nina imani kwamba ita tia uzito sana juu ya upatkikanaji wa vifaa hivyo”
Magreth alizungumza na ushawishi wake ukamfanya RPC Karata kumtazama kwa sekunde kadha akisha kisha akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ame kubali.


Josephine na RPC Karata wakaondoka nyumbani hapo na kuelekea hospitali ya Agakhan. Magreth akamtazama dokta Masawe pamoja na mikojo yake iliyo tapakaa kwenye sakafu hiyo. Akaingia chumbani kwake, akatoka na pensi pamoja na tisheti ambazo zilikuwa zina valiwa na Evans kipindi ana ishi naye.
“Bafu lipo hapo. Una weza uka oga”
“Nashukuru”
Dokta Masawe alijibu kwa upole huku aibu ikiwa ime mtawala kisawa sawa. Akaondoka sebleni na Magreth akasafisha sebleni kwake.


“Huyu RPC ana undugu na raisi?”
“Ni baba yake wa hiyari”
“Ahaa ndio maana ame kasirika?”
“Wee acha jamaa likuwa an afumuliwa ubongo leo”
“Yani niliogopa, nilijua banamu banamwagika”
Kauli hiyo ya Juma ikamfanya Magreth kucheka sana.


***


“Nime sikia kwamba una uwezo wa kuona mambo yajayo au yanayo tokea”
RPC Karata alimuuliza Josephine huku akimtazama usoni mwake.


“Ndio”
“Je mke wa raisi Mtenzi yupo wapi kwa sasa?”
“Muhimbili”
“Wodi gani?”
“Mochwari”
RPC Karata akastuka kidogo huku akimkazia macho Magreth.
“Una taka kuniambia kwamba yule mama ame fariki?”
“Ndio ame fariki. Kwenye lile gorofa walio pona ni waty watano Tu. Jery, baba yake, mke wake pamoja na walinzi wawili.
“Tuelekeeni Muhimbili”
RPC Karata alizungumza kwa msisitizo wake na dereva wake akabadilisha muelekeo wa gari.
“Ila imetupasa kuelekea Agakhan”
“Nataka kwenda kuhakikisha kwa macho yangu”
RPC Karata alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Wakafika hospitai ya Muhimbili. Ashuka kwenye gari na kuongoza njia ya kueleka katika jengo la kuhifadhia maiti. Josephine hakuitaji kushuka kwenye gari hilo kwamanaa ni muoga sana wa kushuhudia maiti za watu.


“Mwili wa first lady upo wapi?”


RPC Karata alimuuliza mtu anaye shuhulika na kuhifadhi maiti hizo.
“Huku”
Jamaa huyo mwenye rasta zilizo simama na macho yake yaliyo tawaliwa na uwekundu wa kuvuta bangi. Hakujibu chochote zaidi ya kuanza kuingia ndani ya jengo hilo huku akiziruka ruka maiti za watu walio fariki katika mashambulizi ya mlipuko. Akafungua moja ya friji kubwa na akavuta moja ya droo ya friji hilo.


“Huyu hapa”
RPC Karata macho yakamtoka, hakumuamini mwana mama ambaye amejaliwa kuwa na roho nzuri na mwenye kumcha Mungu leo hii yupo kwenye sanduku hilo la kuhifadhia maiti.
“Mwili wake ume dhibitishwa na dokta kwamba ame kufa?”
RPC Karata alizungumza huku akiwa amejawa na mchozi hata swali hilo alilo liuliza hakulitarajia kama ata liuliza hivyo.
“Mzee baba mtu akidanja hakuna haja ya kudhibitishwa na dokta. Mdano huyu mama”
Muhudumu huyo akavuta droo hiyo yoye nje na akafunua shuka eneo la kiunoni, RPC Karata ujasiri wote uka muishia kwani mkewa raisi Mtenzi eneo la kuanzia miguuni mwake lote lime pondeka pondeka vibaya sana. RPC Karata akatoka ndani hapo hauku akiwa na machungu mengi sana. Hata wasaidizi wake waliweza kuligundua hilo kwa haraka na jambo la pekee walilo lifanya ni kumrudisha kwenye gari kwani ana mwagikwa na mchozi mithili ya mtoto mdogo.


***


“Ndio muheshimiwa makamu wa raisi”
“Nime pata habari kutoka kwa mtu ninaye muamini. Watu wana sadikika kwamba wame mtekea raisi Mtenzi kwa sasa wapo mkoa wa Morogoro. Hivyo hakikisheni kwamba muna kwenda kuwasaka mkoa mzima. Ume nielewa RC?”
“Ndio muheshimiwa nime kuelewa”
“Nahitaji hadi kukipambazuka muwe mume nipatia jibu la wapi alipo raisi”
“Sawa”
Makamuwa wa raisi bwana Kadenge Jr akakata simu huku akiwa amejawa na hasira kwani mipango yake ya kumalizia kuamuua raisi Mtenzi ina kwenda kuwa migumu.
“Hawa walio mchukua raisi nikiwapata haki ya Mungu nita waua kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
“Ila muheshimia kwa namna moja ama nyinngine wata kuwa wame kupunguzia kazi”
“Kazi kivipi?”
“Hatujio walio mchukua ni watu wa aina gani. Ila kwa asilimia kubwa nina hisi kwamba ni watu ambao ni wabaya na walio kuwa na mpango wa kumuua raisi kwa bomu. Sasa wame ona kwamba wameshindwa hivyo wame amua kumchukua wao wenyewe wakamlazie”
Mlinzi wa makamu wa raisi alizungumza huku akimtazama mkuu wake.
“Etii ehee?”
“Ndio mkuu, hii ishu ni personal na ime garimu maisha ya watu wengi sana. Wewe mwenyewe ume iona ile clip ya Al-Shabab. Wame kiri kuhusika na hili shambulizi kwa sasabu moja tu, walishambuliwa kwenye bandari yao. Nao wameona wamefanya malipizi kwa jiji zima la Dar tena siku ya harusi ya mtoto wa raisi. Hivyo usiumize kichwa kiongozi wangu. Endapo mwezi wa kwanza uta pita, mwezi wa pili uta pita mwenzi wa tatu mkuu una chukua nchi”


Makamu wa raisi akajikuta akitabasamu kwa maana tamaa yake kubwa ni kuhakikisha kwamba ana pata madaraka ya kuwa kiongozi wa juu kabisa kwenye nchi hii ya Tanzania.
“Hapo kidogo ume nifumbua akili yangu”
“Ndio muheshimiwa hatupaswi kutumia nguvu nyinngi sana katika hili swala.”
“Ila hakikisha una mpata dokta Masawe na kumuua”
“Usijali muheshimiwa, nita dili naye. Alafu kuna habari muhimu nime ipata ambayo ita zidi kukupatia wewe nguvu”
“Habari gani?”
“Nime sikia kwamba mke wa raisi naye ame fariki dunia”
“Weee?”
“Ndio, nime ipata habari hiyo kutoka kwa askari mmoja msaidizi wa RPC Karata na ameniambia kwamba wamedhibitisha kabisa kuuona mwili wa mrs Mtenzi”
“Kwa hiyo mke wangu rasmi naye ana kwenda kuwa first lady”
“Ndio muheshimiwa”
Makamu wa raisi akajikuta akichia kicheko cha kejeli kwani malengo yake ya kuiongoza Tanzania hayato kuwa na mpinzani wa aina yoyote.
***


RPC Karata akashuka kwenye gari huku Josephine akiwa ana mfwata kwa nyuma.
“Mkuu”
Josephine aliita na kumfanya RPC Karata kugeuka kusimama na kugeuka kwa nyuma.


“Nina jambo la naomba nikueleze”
“Zungumza”
“Yule kijana wako mrefu na mweusi. Usimuambie kabisa juu ya hili jambo la uwepo wa raisi Mtenzi ndani ya nyumba ya Magreth”
“Kwa nini?”
RPC Karata alizungumza huku akimtazama kijana wake huyo aliye simama eneo la nje kuhakikisha ana endelea kuimarisha ulinzi wa mkubwa wake huyo.
“Ana penyeza siri kwa kila kinacho endelea kwa mlinzi wa makamu wa raisi ambaye ndio alipewa jukumu la kumuua dokta Masawe ili siri yao isivuje. Isitoshe habari ya kufariki kwa mrs Mtenzi amesha ifikisha kwa mlinzi huyo”
“Pumbavu kweli huyu”
RPC Karata akataka kumfwata kijana wake huyo ila Josephine akamshika mkono.


“Nini?”
“Usimkasirikie ila muombe simu yake uta dhibitisha kile ninacho kuambia”
RPC Karaka akashusha pumzi iliyo punguza jazba yake kidogo. Akamuita kijana huyo kwa ishara na akawafwata hadi walipo simama.
“Nipe simu yako, kuna mtu nahitaji kumpigia”
“Sawa muheshimiwa”
Jamaa huyo akatoa simu yake pasipo kufahamua na pelelezwa.


“Ina neno la siri”
RPC Karata alizungumza na kijana huyo akatoa neno hilo la siri kisha akamkabidhi mkuu wake simu hiyo. RPC Karata akajifanya ana ingiza namba huku wakiondoka eneo hilo na Josephine. Wakafika mapokezi na kumuulizia dokta Khan na wakaelekezwa ofisi yake ilipo. RPC Karata akajikuta akisimama huku akisoma meseji za kijana wake ambazo zime mstua sana na kujikuta akichomoa bastola yake taratibu huku hasira ikiendelea kumtafuna moyoni mwake kisawa sawa.


ITAENDELEA


Haya sasa, ni mesjeji gania mbazo zina ufanya moyo wa RPC Karata kutwafunwa na hasira kali namna hiyo? Usikose sehemu ya 125.
 
SIN 126


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188






ILIPOISHIA


“Nipe simu yako, kuna mtu nahitaji kumpigia”
“Sawa muheshimiwa”
Jamaa huyo akatoa simu yake pasipo kufahamua na pelelezwa.


“Ina neno la siri”
RPC Karata alizungumza na kijana huyo akatoa neno hilo la siri kisha akamkabidhi mkuu wake simu hiyo. RPC Karata akajifanya ana ingiza namba huku wakiondoka eneo hilo na Josephine. Wakafika mapokezi na kumuulizia dokta Khan na wakaelekezwa ofisi yake ilipo. RPC Karata akajikuta akisimama huku akisoma meseji za kijana wake ambazo zime mstua sana na kujikuta akichomoa bastola yake taratibu huku hasira ikiendelea kumtafuna moyoni mwake kisawa sawa.





ENDELEA


Josephine akwahi kumshika RPC Karata mkono wake kwani kuba baadhi ya watu walisha anaza kumtolea macho huku wakiwa wemejawa na wasiwasi.
“Muheshimiwa hapa ni hospitali watu wana kushangaa”
Josephine alizungumza kwa sauti ya upole na iliyo jaa unyeyekevu mkubwa sana. RPC Karata akamkabidhi Josephine simu hiyo ili aweze kusoma mesji hizo.


‘Bado nina endelea kupeleleza nyendo za RPC’


‘Hakikisha una fahamu kila kitu kinacho endelea kwa maana huyo tuna mjua ni mpambe wa raisi Mtenzi’


‘Ni kweli, je uma niahidi nini kwenye hili’


‘Uta kuwa RPC wewe mara baada ya makamu wa raisi kuchukua nafasi ya uraisi’


‘Sawa je raisi akipatikana’


‘Hawezi patikana na pia ikiwezekana ukipata nafasi muue mkuu wako ili njia yako iwe nyeupe’


Josephine macho yakamtoka. Kitendo cha kunyanyanyua uso wake ili kutazama alipo RPC Karata, hakuweza kumuona.


“Mungu wangu”
Josephine alizungumza na kuanza kukimbilia kuelekea nje. Akamkuta vijana wengine wa RPC Karata wakiwa wame mshikilia kijana huyo huku wakiwa wame mpokonya bunduki yake na wame mfunga pingu.


“Una taka kuniua mimi kwa ajili ya madaraka eheee?”
RPC Karata alizungumza huku akimshushia ngumi ya uso kijana wake huyo aliye wekwa chini ya ulinzi mkali.
“Hapana bosi sijui unacho zungumzia”
RPC Karata kwa haraka aka mkwapua Josephine simu hiyo na kuwaonyesha vijana wengine meseji hizo. Kila aliye soma alijawa na mshangao ime kuwaje rafiki yao ame ingingia kwenye msafara wa mamba ikiwa yeye ni Kenge.


“Muingizeni kweye gari alafu na huyo mpumbavu mwenzako nita hakikisha nina shuhulika naye.”
Vijana hao wa RPC Karata wakatekeleza agizo hilo la bosi wao na wakamuingiza ndani ya gari kijana huyo kisha RPC Karata na Josephine wakaelekea kwenye ofisi ya dokta Khan.


‘Mbona nyinyi ingia bila bisha hodi’


Dokta Khan alizungumza kwa ukali huku akiwakazia macho RPC Karata na Josephine walio simama mbele yake. RPC Karata hakuzungumza kitu chochote zaidi ya kunyoosha mkono wake kwa Josephine ambaye alielewa kusudio la RPC Karata. Akatoa karatasi hiyo aliyo kabidhiwa na dokta Msangi na akamkabidhi RPC Karata ambaye moja kwa moja akaiweka mezani kwa dokta Khan.


“Nahitaji hivi vifaa?”
Dokta Khan akaichukua karatasi hiyo, akaivaa miwani yake na kuangalia kilicho andikwa kwenye karatasi hiyo.
“Mimi siwezi toa vifaa vya hospitali hii peleka kwa hospitali ya serikali pasipo malipo yoyote”
“Dokta Masawe ndio ame tuagiza”
Josephine alijibu.


“Jua vizuri dokta Masawe, ila vifaa hivyo ni very expensive.”
“Kwa hiyo una tupa au hutupi?”
RPC Karata aliuliza kwa sauti ya kukoroma.
“Siwezi toa, lazima tufanye negotiatios ili tujue na sisi tuna nufaika vipi?”
RPC Karata akachomoa bastola yake na akamvuta dokta Khan karibu yake huku bastola hiyo akiwa ameiweka shavuni mwake.
“Una nijua mimi ni nani?”
“Nd..i…i..o”
“Mimi ni nani?”
“RPC”
“Una jua nina shuhulika na watu na waina gani?”
“Wahalifu”
“Sasa usitake na wewe nika kuvisha joho la uhalifu. Nchi ipo kwenye shida, wewe una taka kutuletea maswala ya pesa au una hitaji kesho uka panda ndege na kurudi kwenu India?”
“A..haa…hapana”
“Basi tupatie vifaa vyote vilivyo andikwa hapa tena vikiwa katika ubora mzuri. Umenielwa?”
“Ndi….io muheshimiwa”
Dokta Khan alijibu kwa unyeyekevu uliyo jaa woga mwingi sana kiburi chote alicho kuwa ana kionyesha awali kime potea. Wakatoka ofisini hapo na wakaelekea katika stoo ya kuhifadhia vifaa vya hospitali hiyo. Dokta Khan akaanza kuonyesha vivaa walivyo agizwa. RPC Karata akwaita viajana wake wawili kwa kutumia simu ya upepo. Wakaingia kwneye stoo hiyo na kuanza kutoa vivaa hivyo na kuvipeleka kwenye gari.
“Vita rudishwa lini?”
Dokta Khan aliuliza kwa sauti ya upole sana.


“Sijui”
RPC Karata alijibu kwa ufupi na wakaondoka eneo hilo. Wakaingia kwenye gari na kuianza safar ya kuelekea nyumbani kwa Magreth. Juma akafungua geti na gari hilo likaingia ndani, askari hao wakashusha vifaa hivyo na kuviingiza hadi sebleni.
“Magreth nina kuomba”
RPC Karata akatoka nje na Magreth akamfwata kwa nyuma.
“Hii ni simu ya kijana wangu. Alikuwa ana chati na yule bodyguard wa makamu wa raisi”
RPC Karata alizungumza huku akimpa Magreth simu hiyo. Akaanza kusoma meseji hizo ambazo hata yeye zili mshangaza sana.


“Ana taka kukua kisa cheo?”
“Ndio maanayake”
“Daa sasa yupo wapi kijana mwenyewe”
RPC akafungua mlango wa gari na kumuonyesha kijana huyo aliye kaa siti ya nyuma huku akiwa ameimarishiwa ulinzi na vijana wengine wawili.
“Huyo mpumbavu ndio anaye hitaji kunia”
“Aisee uso wake wala hauonyeshi kama ni muuji”
“Ndio hivyo. Rafiki yako ndio aliye weza kunistua kwenye jambo hilo ndio maana ume ona tume mtia nguvuni”
Magreth akafunga mlango wa gari hilo.


“Hyu ni tamaa tu ndio zime mkamata. Ina bidi abaki chini ya ulinzi. Alafu sisi tudili na huyu mlinzi wa makamu wa raisi kwa maana yeye moja ndio mtu aliye taka kumuua dokta Masawe na pili tuki mkamta basi tuna weza kupata siri nyingi sana kutoka kwa makamu wa raisi ambazo ana mpango wa kuzifanya.”
“Hilo ni wazo zuri. Je tuta mpata vipi?”
“Niachie hiyo kazi mimi. Wewe kadili na kijana wako na mimi nidili na huyu mshenzi ambaye kama ingekuwa sio uwezo nilio nao ange tuu”
“Sawa hilo nina kuachia wewe. Ila nina kuomba sana usi muue hiyo kijana pasipo mimi kuonana naye”
“Sawa kaka”
“Nina imani vifaa hivyo vina hivyo ndio sahihi?”
“Labda nimuulize dokta”
“Muulize kwa maana vifaa vyenyewe tume vipata kwa tabu sana”
Magreth akarudi ndani na kuwakuta dokta Masawe na Juma wakisaidiana katika kuingiza vivaa hivyo kwenye chumba alicho lazwa raisi Mtenzi.


“Vifa ahivyo ndio sahihi?”
“Ndio nina shukuru”
“Poa”
Magreth akatoka nje na kumjibu RPC Karata jibu hilo la dokta Masawe. RPC Karata akaaga na akaondoka nyumbani hapo na vijana wake huku simu ya kijana wake ambaye ni msaliti akiicha mikononi mwa Magreth.


“Jose”
“Bee”
“Kuna hii kazi nime achiwa hapa ya kumpata msaidizi wa makau wa raisi una ona jambo gani mbeleni.”
“Ngoja kwanza nisali”
Josephine akafumba macho yake kwa sekunde kadhaa kisha akayafumbua.
“Nime pewa jambo la tofauti kabisa”
“Jambo gani?”
“Nimeonyeshwa majeshi ya Marekani yana kuja nchini Tanzania. Ila lengo la majshi hayo ni kuingia nchini ni kuchukua hadhina kubwa sana ambayo ipo chini ya ardhi ya posta. Endapo adhina hiyo tukiipata nchi yetu ina kwenda kutajirika na kuwa mara elfu moja na hapa ilipo”
Magreth macho yakamtoka kwa mshangao.
“Mara elfu moja na hapa tulipo?”
“Ndio ni hadhina kubwa sana ambayo ime achwa kwa miaka elfu moja iliyo pita.”
“Ohoo Mungu wangu. Sasa ina kuwaje?”
“Mission iliyopo sasa hivi ni kuhakikisha kwamba Wamarekani hawaipati hadhina hiyo kwani wakiipata, wana kwenda kutajirika mara dufu na wata kuwa na nguvu kubwa sana hapa duniani”
Magreth akajikuta akishusha pumzi kwa maana hakuwa na habari kabisa na najambo hilo. Meseji ikaingia kwenye simu hiyo na akaifungua, kwa bahati nzuri kijana huyo alitoa neno la siri na kuiacha simu yake kubaki kuwa huru pasipo ulinzi wa neno hilo la siri.


‘Oya kijana mume fikia wapi?’


“Jose kuna meseji ime ingia kutoka kwa yule mshenzi”
“Nani?”
“Mlinzi wa makamu wa raisi”
Josephine akaisoma meseji hiyo kisha akamtazama Magreth.


“Huyu mjinga nahitaji kudili naye sasa hivi”
“Basi muambie muonane”
Magreth akaka kimya kwa sekunde kadhaa kisha akaijibu meseji hiyo.


‘Kaka nina habari nyeti tuna weza kuonana usiku huu?’


‘Ina husiana na nini?’


‘Raisi Mtenzi na hii habari nime ipata kutoka kwa RPC. Sasa kaka fanya tukutane’


‘Poa poa. Wapi sasa tuonane’


“Nikutane naye wapi?”
“Sehemu yoyote ambayo una hisi kwamba ni nzuri kwa usiku huu”
Magreth akajifikiria kisha akamuandikia meseji mlinzi huyo wa makamu wa raisi sehemu ya kukutana. Magreth akaingia chumbani kwake na kuvaa mavazi yake ambayo ana yatumia kwenye kazi zake hizo. Akababa silaha zake zote na akatoka ndani hapo. Juma macho yakamtoka mara baada ya kuuona bosi wake akiwa kwenye mavazi hayo.
“Siri yako usimuambie mtu”
Magreth alizungumza na akatoka ndani hapo. Josephine akamfungulia geti na akatoka ndani hapo na pikipiki yake na kuanza kuelekea eneo kuwahi kabla ya mlinzi huyo wa raisi kufika.


***


“Evans amka amka?”
Jini Maimuna alimuasha Evans na taratibu akanyanyuka kitandani huku akiwa amejawa na lepe kubwa la usingizi.
“Vipi ume kuja saa ngapi?”
“Muda wote huwa nipo karibu na wewe. Sasa sikia kuna habari muhimu sana ambayo nina hitaji kukupatia”
“Habari gani?”
“Kuna hadhina kubwa sana ambayo ipo kwenye eneo la Posta. Hadhina hiyo Wamarekani wame panga kuichukua na endapo wakiichukua nchi yao ita kuwa ni tajiri mara dufu”
“Kwa hiyo mimi nifanyaje?”
“Nahitaji hadhina hiyo ibaki ndani ya nchi hiyo na endapo uta fanikiwa kumuonyesha Makamu wa raisi ni wapi hadhina hiyo ina patikana basi uta fanikiwa kuwa tajiri mkubwa sana duniani kwa maana na wewe uta pata kiasi chako chochote ukitakocho”
Evans akaka vizuri kitandani, huku uchu wa utajiri ukimtawala.


“Una sema nita kuwa tajiri mkubwa duniani?”
“Ndio tena una weza kuwa tajiri hata namba moja duniani na utajiri wako hauto kwisha kabisa, na vizazi vyako zaidi ya saba vina weza kufurahia utajiri huo”
“Duu sasa niambie nini nifanye”
“Nahitaji asubuhi uanze safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam. Moja kwa moja uende hadi Ikulu na ukakutane na makamu wa raisi na endapo uta kutana naye basi uta mueleza juu ya hiyo habari”
“Hato nisaliti?”
“Hawezi kukusaliti kwa manaa mimi nita kuwa nyuma yako.”
Evans akatazama saa ya kwenye simu yake na kukuta ni saa nane na dakika ishirini usiku.
“Naweza kuianza safari hii usiku huu huhu. Asubuhi niwe mimesha timba ikulu pale au una onaje?”
“Hakuna shaka ila jambo ni moja. Moja kubwa na gumu sana”
“Jambo gani”
“Ili hadhina hiyo iweze kupatina ni lazima kupatikane mwanamke mwenye maono makubwa sana na damu yake ndio ina weza kufungua mlango wa kuelekea eneo ilipo hadhina hiyo”
“Sasa huyo mwana mke tuna mpatia wapi?”
“Tanzania mwanamke huyo yupo mmoja tu na endapo akifa basi mwanamke mwengine ambaye ana weza kutokea na kuwa na uwezo kama yeye ni baada ya miaka mia moja. Nina imani miaka hiyo mia moja utakuwa umesha kufa ila mimi nita kuwepo hai”
“Niambie sasa huyo mwanamke ana patikana wapi ili hata kwa kumpatia pesa ina bidi tumrubuni na awe upande wetu. Hadhina hiyo ni utajiri una jua”
“Ndio, ila mwanamke huyo ni ngumu sana kwa mimi kumsogelea kwa manaa ana uwezo mkubwa kuliko mimi japo yeye ni bina damu”
“Mmmmm”
“Ndio endapo ange kuwa hana uwezo wa kunishinda basi ninge mchukua kirahisi”
“Niambie ni nani kwa maana kama ni pesa ina weza kutumika na nika mpata kirahisi”
“Ana itwa Josephine ni rafiki wa karibu sana na Magreth na msichana huyu tulikutana naye ile siku pale barabarani tulipo kutana na Magreth.”
Evans akastuka kidogo.


“Yule demu aliye kuwa naa mlazimisha Magreth waondoke?”
“Yap. Yule ndio ufunguo wa hadhina hiyo. Bila yeye, hata Wamarekani wenyewe hawawezi kupata hata jiwe moja la dhababu”
Jini Maimuna alizungumza kwa sauti ya upole na kumfanya Evans kushusha pumzi huku akitafakari ni jinsi gani anavyo weza kumpata Josephine ili wawe wa kwanza kupata hadhina hiyo.


ITAENDELEA


Haya sasa, Josephine ndio ufunguo wa kupata hadhina hiyo je wata faikiwa kumpata Josephine ambaye ana uwezo mkubwa kuliko jini Mimuna? Usikose sehemu ya 127.
 
SIN 127


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Mmmmm”
“Ndio endapo ange kuwa hana uwezo wa kunishinda basi ninge mchukua kirahisi”
“Niambie ni nani kwa maana kama ni pesa ina weza kutumika na nika mpata kirahisi”
“Ana itwa Josephine ni rafiki wa karibu sana na Magreth na msichana huyu tulikutana naye ile siku pale barabarani tulipo kutana na Magreth.”
Evans akastuka kidogo.


“Yule demu aliye kuwa naa mlazimisha Magreth waondoke?”
“Yap. Yule ndio ufunguo wa hadhina hiyo. Bila yeye, hata Wamarekani wenyewe hawawezi kupata hata jiwe moja la dhababu”
Jini Maimuna alizungumza kwa sauti ya upole na kumfanya Evans kushusha pumzi huku akitafakari ni jinsi gani anavyo weza kumpata Josephine ili wawe wa kwanza kupata hadhina hiyo.





ENDELEA


“Njia rahisi ninayo hisi kwamba ita tusaidia ni kuwa karibu na Magreth”
“Alafu?”
“Nita weza kuweka ukaribu na Josephine na nita weza kumchukua na kumpeleka eneo hilo la hadhina”
“Jambo hili halipaswi kuchukua zaidi ya wiki kwa maana jeshi la Marekani lina kuja Dar es Salaam kwa ajili ya ujenzi wa jiji hilo. Hivyo macho yao yatakuwa yana angalia sana eneo la Posta.
Evans akajikuta akikuna kicha chake kwa maana dili hili kwa kweli ni kubwa na yeye ana hitaji utajiri kwa namna yoyote ile.


“Poa acha kwanza nionane na makamu wa raisi kisha tuta jua nini cha kufanya. Huyo demu hata kwa kumteka tuna weza kufanya hivyo”
Jini Maimuna akajikuta akitabasamu.
“Nini?”
“Hivi una mjua Magreth vizuri?”
“Ndio, ni muuza maandazi ambaye nili msaidia kuto bwakwa na vibaka”
“Uliwahi kujitokeza ile siku ila endapo usinge jitokeza wale vibaka wange pata tabu sana.”
“Sija kuelewa”
“Uta elewa ukikibaliana na makamo wako wa raisi katika dili hilo. Safari njema”
Jini Maimuna akapotea na kumfanya Evans kuanza kuanza kujiandaa haraka haraka. Akabeba kila kilicho chake, na kutoka ndani ya chumba hicho. Akakabishisha funguo mapokezi akaingia kwenye gari lake na kuondoka eneo hilo na kuianza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam.


***


Magreth akafika katika eneo alilo kubaliana na mlinzi wa makamu wa raisi. Akasimamisha pikipiki yake eneo ambalo sio rahisi kwa mtu mwengine kuiona, isitoshe giza lililopo eneo hili. Lilisaidia sana pikipiki hiyo kuto onekana kwa urahisi. Baada ya dakika ishirini, gari aina ya Range rover vorge ika fika eneo hilo ila ika simama eneo la mbali kidogo kutoka sehemu alipo jificha Magreth.


‘Njoo kwenye gari’


Meseji hiyo ikamfanya Magreth kushusha pumzi kidogo kwa maana alitarajia kwamba mtu huyo atakapo vika sehemu hiyo ata shuka. Magreth akatoa silaha ndogo vilivyo kaa katika muundo wa nyota. Akaanza kuvizurusha kwenye tairi za gari hilo jambo lililo mfanya mlinzi huyo wa makamu wa raisi ajulikaney kwa jina la Boko kustushwa sana.


Boko akaiandaa bastola yake vizuri, huku akizima taa za gari hilo kwa maana kuendelea kuziwasha ni **** nafasi adui kuweza kumuona eneo alipo. Kuzima kwa taa za gari hizo, ikawa ni nafasi nzuri sana kwa Magreth kulikimbilia gari hilo. Akavunja kioo cha nyuma kwa kutumia mpini wa upanga wake ulio tengenezwa kwa chuma. Boko akaanza kufyatua risasi nyuma ya gari lake huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana. Gafla akastukukia kioo cha upande wake kikivunjwa. Kabla hajafanya chochote akastukia akipigwa ngumi ya kichwa na kumfanya aweweseka. Magreth kwa haraka akafungua mlango wa gari hili na akamchomoa Boko na kumpiga kigoti cha kifuani na akamuangusha chini. Boko akajaribu kujitutumua ila akajikuta akipikoe kipigo kitakatifu kilicho na ndani ya dakika mbili akawa hajiwezi kabi. Magreth akawasha tochi ya simu ya kijana wa RPC Karata,akamulika ndani ya gari hilo na akachukua simu mbili zilizomo ndani hapo. Akazima tocho hiyo na akamaburuza Boko hadi ilipo pikipiki yake.


‘Nambebeje huyu mjinga?’


Magretg aliwaza huku akimtazama Boko aliye tebwereka mithili ya embe bonyoa. Magreth akatoa simu yake mfukono na kumpigia RPC Karata.
“Ndio”
“Nime mpata na nina kuhitaji”
Magreth akamtajia RPC Karata eneo alipo na hazikupita dakika ishirini. RPC Karata akafika eneo hilo huku akiwa peke yake.
“Ni wewe?”
RPC Karata alimuuliza Magreth aliye valia nguo zilizo ificha hadi sura yake.
“Yap. Mtu wako ukihitaji kumuhoji ni wewe”
RPC Karata akachuchumaa na kumtazama Boko.
“Tumpeleke ufukweni ata zungumza vizuri”
“Sawa”
RPC Karata akamuingiza Boko ndani ya gari hilo na kuanza kuondoka. Magreth akapanda kwenye pikipiki yake na kuanza kuwafwata kwa nyuma. Wakafika kwenye fukwe ambayo haitumiki, wakamshusha Boko na jambo zuri linalo wasaidia ni mwanga wa mbalamwezi unao angaza sana eneo hilo.


“Hee hee”
RPC Karata alizungumza huku akimuamsha Boko.
“Nina imani kwmaba una nijua si ndio?”
Boko akamtazama kwa sekunde kadha kisha akatingisha kichwa akimaanisha kwamba ana amfahamu.
“Kwa nini mume hitaji kumuua raisi Mtenzi”
Boko akastuka sana kwa maana aliamini siri hiyo ipo kwa watu watatu. Yeye, dokta Masawe na makamu wa raisi amabaye ndio ame panga yote hayo.


“Sijui una zungumzia nini?”
“Ana kuchukulisha muda wako”
Magreth alizungumza huku akichomoa kisu kifefu kidogo akamchoma Boko kisu hicho kwenye paja la mguu wa kulia na kumfanya alia kwa uchungu sana.


“Kwa nini ulihitaji kumuua raisi Mtenzi?”
Magreth alilirudia swali hilo huku akiwa amejawa na hasira kali sana.
“Ni makamu wa raisi ndio amepanga kumuua kwa manaa naa hitaji kiti cha uraisi”
Mazungumzo yote hayo anayo yazungumza Boko, RPC Karata aliyarekodi ikiwa ni ushahidi ambao baadaye ana weza kuutumia kwa ajili ya kumstaki makamu wa raisi.


“Kwa hiyo makamu wa raisi ndio ame husika”
“Ndio yeye ndio amehusika kwa asilimia mia moja, mimi ni msaidizi wake tu na nina fwata amri yake tu”
Boko alizungumza huku akilia sana kwani maumivu anayo tapata ka kwenye paja lake hilo sio ya mchezo. Magreth akamtazama RPC Karata, ana RPC Karaka akanyoosha dole gumba la mkono wake wa kulia, taratibu akageuzia kidole gumba hicho chini, ikiwa ni ishara ya kumpa ruhusa Magreth kumuua Boko.


Magreth akachomoa upanga wake huo mrefu na kuikata shingo shingo ya Boko na akatengenisha mwili na kiwili wili chake.


“Nime rekodi mazungumzo haya. Nina imani kwamba mazunumzo haya yatamuingiza makamu wa raisi kifungoni”
“Sawa hakikisha una yatunza na hakikisha una itunza siri yangu ya muonekano huu”
“Usijali kuanzia hivi sasa tuta kuwa tuna shirikiana kwenye kila jambo la usalaama. Nina kuomba uweze kumlinda raisi”
“Sawa. Mimi nina ondoka”
Magretha akaeleke eneo alipo iacha pikipiki yake na akapanda pikipiki yake na kuondoka eneo hilo. RPC Karata akauchukua mwili wa Boko na kuutupia baharini. Akakichukua kichwa cha Boko na kuondoka nacho. RPC Karata akafika katika nyumba kwake. Akatafuta boksi, akakiweka kichwa cha Boko kwenye mfuko wa lailoni na kukiingiza kwenye boksi hilo. Akalifunga vizuri boksi hilo mithili ya zawadi, kisha akaandika kwa nje maandishi yanayo someka, ‘ZAWADI KWA MAKAMU WA RAISI’. Akalibeba boksi hilo na kurudi nalo kwenye gari, akafika eneo la karibu na ikulu, akashuka. Akawatazama omba omba walio lala nje ya moja ya duka, akamfwata mmoja na kumuamsha.
“Vipi?”
“Poa”
“Nahitajiji upeleke hili boksi kwenye geti la ikulu”
“Sasa hivi?”
“Ndio kuna elfu kumi hii. Nina kusubiria hapa”
Omba omba huyo pasipo kujali akababe boksi hilo na akakimbia hadi kwenye geti la ikulu. Akaliweka boksi hilo na akaanza kukimbia. Kitendo hicho kikawafanya wanajeshi wanao linda kuanza kumsimamisha kwa kumkemea kwa sauti kali. Ila omba omba huyo hakuhitaji kabisa kusimama. Mwanajeshi mmoja hakufanya makosa akampiga risasi ya mgongo na omba omba huyo akaanguka na akafariki hapo hapo.


Mlio wa risasi uka mstua RPC Karata pamoja na walinzi wengine kwa ikulu. Wakakimbilia getini na kuwakuta wanajeshi hao wakiusogelea mwili wa omba omba huyo.
“Ame kufa”
Mwanajeshi huyo aliye mpiga risasi ombaomba huyo alizungumza mara baad ay kumgeuza upande wa pili kwani alianguka kifudi fudi.


“Hilo boksi lina nini?”
Kiongozi wa wanajeshi hao aliuliza.


“Hatufahamu mkuu, huyu omba omba aliliteka akalitupa hapa na akakimbia. Tulijaribu kumsiihi asimame ila hakudhubutu. Nika mpiga risasi”
“Isije ikawa ni bomu?”
Ndio hivyo muheshimiwa “
“Hembu lifungue”
Mwanajeshi mmoja akalisogelea boksi hilo. Atatoa kisu kidogo mfukoni mwake na kuanza kulichana boksi hilo kwa utaratibu.
“Kuna nini?”
Mkuu huyu aliuliza huku akiwa ame simama mbali kidogo akitamtazama mwanajeshi wake huyo.


“Kuna mfuko mweusi na eneo la nje kume andikwa zawadi kwa makamu wa raisi.


“Hembu fungua huo mfuko”
Mwanajeshi huyo alitii amri ya bosi wake huku akitetemeka mwili mzima na jasho likimwagika usoni mwake. Mwanajeshi huyo akajikuta akirudi nyuma kidogo huku akiwa amejawa na mstuko mkubwa sana.


“Ni nini wewe?”
Mkuu huyo aliuliza huku akimkazia macho kijana wake.


“Ni kichwa mkuu”
“Kichwa cha nini?”
“Binadamu”
Mkuu huyo akawatazama wanajeshi wengine. Akapiga hatua hadi kwenye boksi hilo. Macho yakamtoka kwa maana kichwa hicho ni cha mtu anaye mfahamu kabisa.
“Mungu wangu”
“Mkuu ina bidi muheshimiwa aweze kuona hili kwa maana ime andikwa ni zawadi yake”
“Muheshimiwa ame lala?”
“Sifahamu mkuu”
“Beba hilo biksi unifwate”
Mkuu huyo alimuambia kijana wake huko huku akitanguliak uelekea ndani. Moja kwa moja akaelekea hadi katika chumba cha makamu wa raisi. Akagonga na baada ya muda kidogo akafunguliwa mlango.


“Samahani muheshimiwa kwa kukuamsha muda huu”
“Bila sahamani kuna nini?”
Mkuu huyo akamtazama mwanajeshi huyo aliye baba boksi hilo.
“Una ujasiri mkuu”
“Ndio maana nime kuwa makamu wa raisi. Ninge kuwa sina ujasiri nisinge kuwa sehemu hii”
“Samahani muheshimiwa sizungmzii ujasiri huo”
“Ujasiiri upi una unungumzia”
“Kijana wako hatupo naye tena”
“Kijana wangu nani?”
“Boko”
“Ame patwa na nini?”
Mkuu huyo akampa ishara mwanayeshi wake huyo aliye baba boksi. Akasogea hadi sehemu alipo simama makamu wa raisi, kisha akalifunua na kumuonyesha makamu wa raisi kichwa cha Boko jinsi kilivyo wekwa ndani ya boksi hilo, kitendo kilicho mfanya makamu wa raisi bwana Madenge Jr kanza kutetemekwa mwili mzima kwani ni masaa machache tu ame toka kuachana na Boko, mlinzi wake namba mojana anaye muamini na kumfichia siri zake nyingi ikiwemo ya kutaka kumuua raisi Mtenzi.


ITAENDELEA


Haya sasa, makamu wa raisi ame letewa kichwa cha mlinzi wake anaye mpenda kuliko wengine, je ata endelea na mpagago wake kutaka kumuua makamu wa raisi? Usikose sehemu ya 128.
 
SIN 128


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188



ILIPOISHIA


“Kijana wangu nani?”
“Boko”
“Ame patwa na nini?”
Mkuu huyo akampa ishara mwanayeshi wake huyo aliye baba boksi. Akasogea hadi sehemu alipo simama makamu wa raisi, kisha akalifunua na kumuonyesha makamu wa raisi kichwa cha Boko jinsi kilivyo wekwa ndani ya boksi hilo, kitendo kilicho mfanya makamu wa raisi bwana Madenge Jr kanza kutetemekwa mwili mzima kwani ni masaa machache tu ame toka kuachana na Boko, mlinzi wake namba mojana anaye muamini na kumfichia siri zake nyingi ikiwemo ya kutaka kumuua raisi Mtenzi.





ENDELEA


“Ni…n…ani…ame kileta?”
Makamu wa raisi aliuliza huku akiwa amejawa na kigugumizi kikali sana.
“Ni omba omba mmoja ndio ame kiletea, mara ya kwanza vijana wangu walihisi ni bomu. Ombaomba yule alikimbia mara baada ya kulitupia boksi getini na akakimbia. Alivyo jaribu kusimamishwa akaendelea kukimbia na vijana wangu walimpiga risasi”
“Kwa hiyo hamjui ni nani ambaye ame husika na kumuua mlinzi wangu”
“Ndio muheshimiwa”
“Kakitunzeni hicho kichwa, kisha nahitaji muutafute mwili wake popote ulipo ili tumzike kwa heshimwa”
“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi akarudi chumbani kwake huku machozi ya hasira yakimwagika usoni mwake. Akajikuta akimwaga vitu vilivyopo meza ya kioo na vikavunjika vunjika.
***


Maji ya bomba la mvua taratibu yakaendelea kumwagika Magreth usoni mwake. Kumbumbu ya mauaji aliyo yafanya muda mchache uliyo pita, bado ina endelea kupita kwenye ubongo wake mithil ya mkanda wa video za tape.


‘Mungu wangu nina kuomba unisamehe’


Magreth alizungumza huku akisikilizia maji ya bomba hilo jinsi yanavyo endelea kumwagikia, akiwa ndani ya bafu la chumbani kwake hapo. Akajitazama kwenye kioo kikubwa kilichopo hapo chooni na kujiona jinsi umbo lake lilivyo umbika vizuri. Mazozi anayo yafanya mara kwa mara kidogo yana muomuondoa manyama uzembe. Taratibu Magreth akaanza kujitomasa maziwa yake na kujikuta akipata msisimko mkali sana.


‘Ahaa sitaki kufanya hivi’


Magreth alizungumza kimoyo moyo. Akajipaka sabuni mwili wake wote, akaoga haraka haraka kisha akatoka bafuni hapo. Akamkuta Josephine akiwa amejilaza kitandani.
“Juma yupo wapi?”
“Amenijalaza sebleni”
“Ahaaa sawa”
“Alafu Mage ume lifikiria swala la hadhina ambayo ipo chini ya ardhi ya Posta.”
“Nisiwe muongo rafiki yangu. Sijafikiria chochote, je tuta ipata vipi hiyo hadhina?”
“Ipo kwene mapango yaliyo chini ya ardhi hiyo. Pia eneo hilo ni eneo lenye nguvu kubwa za giza kwa maana watu walio weka hadhina hizo ni wafalme wa zamani sana”
“Wafalme gani?”
“Sifahamu ila ni hadhina ambazo wafalme hao waliziweka kwa nguvu za giza na pia kuna kiumbe kimesha fahamu juu ya hadhini hiyo”
“Kiumbe gani?”
“Una mkunbuka yule mwanamke ambaye tulimkuta na Evans ndani ya gari lake?”
“Ndio”
“Yule dada ni jini”
“Jini!!!?”
Magreth aliuliza kwa mshangao.
“Ndio ni jini na tena ndio anaye muwezesha Evans katika mipango yake ya kutaka kuanzisha kanisa ambalo halito kuwa kanisa la kumtumikia Mungu, bali litakuwa ni kanisa la kumuabudu jini huyo. Katika kanisa hilo watu watakuwa wana pokea miujiza ya kila namna na wata muona Evans kama mtumishi anaye tumiwa na Mungu, kumbe nyuma yake kuna jini”
“Mmmmm”
“Ndio, na jini huyotayari amesha tambua hizo hazini na amesha mueleza Evans. Evans ata shirikiana na makamu wa raisi na wata nihitaji mimi katika kuwafungulia katika eneo hilo”
“Wewe?”
“Ndio. Mimi ndio mwenye nguvu za kufungua eneo hilo kwa kutumia ndamu yangu. Hakuna binadamu yoyote mwenye uwezo wa kufungua eneo hilo”
Maneno ya Josephine yakamshangaza sana Magreth. Akajikuta akishusha pumzi huku akimtazama rafiki yake huyo.


“Ila msaada wako ndio uta weza kunisaidia mimi kuto ingia mikononi mwao. Endapo Evans na makamu wa raisi wata pata hizo mali basi tusahau kuhusiana na raisi Mtenzi kurudi Madarakani kwa maana makamu wa raisi bwana Madenge ata kuwa na nguvu kubwa sana ya kiuchumi na ataweza kuwarubuni wanajeshi kwa kutumia pesa atakazo zipata. Ana weza kuipindua nchi hata kama raisi Mtenzi ata weza kurudi madarakani”
Magreth akashusha pumzi taratibu huku akimtazama Josephine anaye zungumza kwa huzuni kubwa sana.
“Tunapo endea huko mbele tuta pata tabu sana Mage. Wakati ni wa sisi kuhakikisha kwamba tuna zuia hilo jambo”
“Sasa hizo hazini zipo vipi?”
“Ni eneo ambalo lime tengenezwa kwa madini ya kila aina ya madini yote yenye thamani kubwa duniani yapo hapo. Pia jeshi la Marekani ambalo lina kuja nchini Tanzania wiki ijayo pia lita kuja kwa lengo la kuhitaji hayo madini”
“Mungu wangu daa”
“Ndio hivyo ina bidi tujitahidi katika hilo”
“Tupumzike hadi asubuhi alafu tuta jua nini cha kufanya. Sawa”
“Sawa”
Magreth akavaa suruali yepesi ya kulalalia, akajifunga tenge kifuani mwake na kutoka chumbani hapo. Akaelekea katika chumba alicho lazwa raisi Mtenzi. Akamkuta dokta Masawe akiwa tayari amesha muwekea raisi Mtenzi mashine za kumsaidia kupumua pamoja na mashine inayo hesabu mapigo yake ya moyo.


“Ana endeleaje muheshimiwa?”
“Hali yake nina weza kusema kwamba ina endelea vizuri kwa maana nime weza kumpima na kukuta kuna babadiliko na pale alivyo kuwa ameletwa Muhimbili”
“Sawa nahitaji uhakikishe kwamba ana kuwa katika uangalizi mzuri kwa maana ana paswa kurudi kwenye kiti chake haraka iwezeanavyo”
“Sawa sawa”
Magreth akamtazama dokta Masawe usoni mwake kisha akatoka ndani hapo, akamkuta Juma akikoroma sebleni hapo. Akatoka nje na kuhakikisha kwamba ulinzi wa nyumba yake upo vizuri. Alivyo ridhika arudi ndani kwake na kujipumzisha.
***


Asubuhi na mapema Jery akazinduka kutoka katika usingizi huo wa nusu kifo. Akafumbua macho yake na kuangaza eneo hilo na kujikuta akiwa amelala kwenye kitanda na upande wake wa kulia kukiwa na walinzi wa baba yake ambao nao pia wame wekewa mashine za kuwasaidia katika kupumua.


Baada ya dakika kumi akaingia daktari ambaye ana wafwatilia afya zao kwa ukaribu sana. Daktari alipo muona Jery amezinduka kwa haraka akamsogelea.
“Nipo wapi hapa?”
“Upo hospitali ya Muhimbili muheshimiwa”
“Mama na baba yangu wapo wapi?”
Daktara akapata kigugumizi cha kumjibu jibu hilo.


“Kwanza una jisikiaje?”
“Najisikia vizuri. Nahitaji kumuona mama yangu na baba yangu. Pia nahitaji kumuona mke wangu”
“Ngoja nika muangalie mke wako kwa maana yupo hapa hospitalini”
“Sawa”
Daktari Richard akatoka ndani hapo na kuelekea katika wodi aliyo lazwa Mrs Sanga na Julieth ambao afya zao zina endelea vizuri.
“Habari za asubuhi”
“Salama tu”
“Ahaa mkwe wenu ame weza kudinduka na ana kuhitaji bi Josephine”
Josephine mara baada ya kusika hivyo, akashuka kitandani hapo haraka haraka huku akisukumba bomba lenye matairi ambalo lime ning’iniziwa dripu la maji alilo chomwa mkono wake wa kushoto.


“Kuwa makini”
Daktari alizungumza na Julietha akaendelea na harakati ya kuelelekea ICU. Nabii Sanga naye hakuwa nyuma kuelekea katika chumba hicho. Wakaingia ndani ya chumba hicho na Juliet kwa haraka akakumbatiana na Jery huku wakiwa katika hisia kali za kimapenzi.
“Upo salama mke wangu”
“Ndio mume wangu. Wewe je?”
“Nashukuru Mungu, najisikia vizuri”
Taratibu wakaanza kunyaonya ndimi zao.
“Wazazi wangu wapo wapi?”


Swali la Jery likanfanya nabii Sanga kumtazama daktari huyo kwa maana wote wawili wana fahamu ukweli wa jambo lililo tokewa ka raisi Mtenzi.
“Kuna tatizo ambalo lime wapata wazazi wangu?”
Jerya aliuliza huku akiwa amemkazia macho daktari huyo.
“Niambieni kama kuna tatizo lime wapata wazazi wangu?”
Jery alizungumza kwa kufoka na kumfanya Julieth kumtazama.


“Mkwe kuna matatizo yalijitokeza kidogo sio mazuri. Subiri hali yako ikiwa vizuri, nita kuambia”
“No baba mkwe mimi ni mtoto wa kiume. Niambieni ni kitu gani kilicho tokea kwa wazazi wangu”
Jery aliendelea kusisitizia na kumfanya nabii Sanga kuwasogelea kwa ukaribu.
“Baada ya mlipuko ule wa jana. Muliweza kufukuliwa kwenye kifusicha hoteli ile. Baba yako aliweza kupatikana kwa manaa mulikuwa naye nyinyi wawili pamoja na walinzi hawa. Baba yako aliletwa hapa na kwa habati mbaya inavyo sadikika hadi sasa hivi yupo mikononi mwa Al-Shabab kwa maana walivamia hospitalini hapa, wakawapiga walinzi na wakamchukua baba yako. Hadi sasa hivi hakuna anaye fahamu kwamba kama mzee wako yupo hai au amekufa”
“Una taka kuniambia walio sababisha milipuko kwenye harusi yangu ni hao Al-Shabab?”
“Ndio mkwe”
“Wapumbavu hawa nita waaua. Haki ya Mungu nita waua”
Jery alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.


“Je mama yangu”
“Ahaa muheshimiwa endapo uta lia sana muheshimiwa hali yako ina weza kuwa mbaya zaidi”


Daktari alizungumza huku akimtazama Jery usoni mwake.
“Nijibu mama yangu yupo wapi?”
“Ahaa….a….a”
“Baba mkwe mama yangu yupo wapi?”
Jery alibadilisha swali hilo mara baada ya kumuona daktari ana babaika babaika.
“Mama yako bado sija pata habari zake. Labda hilo jambo umuuliza daktari”
Nabii Sanga alizungumza kitu anacho kifahamu kwa manaa na yeye hafahamu juu ya mrs Mtenzi.
“Dokta usinitumbulie macho niambie mama yangu yupo wapi?”
“Mama yako ame fariki”
Taarifa hiyo ikawastua watu wote ndani hapo. Jery macho yakamtoka huku yakizidi kukolea wekundu utokanao na kulia kwa muda mrefu pamoja na hasira.


“Haiwezekani mama yangua kafariki”
Jery alizungumza hukua kishuka kitandani, akachomoa vitu vyote vilivyo kuwa vime wekwa kifuani mwake.
“Mochwari yenu upo upande gani?”
“Mume wangu tulia kidogo”
Julieth alizungumza huku naye machozi yakimwagika usoni mwake.


“Nahitaji kufahamu mochwari yenu ipo wapi?”
“Kule muheshimiwa”
Daktari alimuonyesha jengo hilo kwa kupitia dirishani. Jery hakujali kama miguuni mwake hana viatu wala ndala. Akaanza kutembea kuelekea nje na kumfanya nabii Sanga naye kumfwata kwa nyuma pamoja an Julieth. Wakakutana na mrs Sanga mlangoni.
“Mkwe vipi?”
Jery akampita mama mkwe wake huyo pasipo kumjibu chochote.
“Hayupo sawa mke wangu”
Nabii Sanga alijibu hukua kimtazama Jery na Julieth wanao elekea mochwari huku wakiwa katika mwendo wa haraka hadi wakamshinda dokta huyo. Wanajeshi nao hawakumuacha Jery kwani bado ana lindwa kama mtoto wa raisi.
“Ana kwenda wapi?”
“Mochwari kumuangalia mama yake”
“Mungu wangu kwani mama yake ame fariki?”
“Ndio”
“Ohooo mume wangu kamzuie. Ana weza kuchanganyikiwa kijana wa watu”
“Hapana kwa sasa yupo kwenye hali mbaya ambayo endapo mtu yoyote ata mzuia ana weza kumfanya chochote na kumbuka mimi ni mkwe wake, sihitaji kuombana naye. Wewe rudi chumbani kwako sawa”
“Sawa”
Nabii Sanga akaanza kukimbilia eneo wanapo elekea Jery.


“Jery Jery, vaa viatu basi”
Julieth alizungumza na mwanajeshi mmoja kamakabidhi Jery viatu na akakivaa. Wakafika katika jengo hilo la kuhifadhia maiti na wakakuta watu wakiendelea kuangua vilio wengine wakiwa wamezia eneo la nje kwa mana matatizo yaliyo tokea yame wagusa wana Dar es Salaam wengine pamoja na Watanzania kwa ujumla.
“Nahiji kumuona mama yangu”
Jery alimuambia muhifadhi maiti huyo ambaye kwa wingi wa maiti alizo zipokea zikiwa katika hali mbaya, zime mfanya kuongeza kiwango chake cha kuvuta bangi kwa siku kwa maana pasipo kufanya hivyo hato weza kabisa kuifanya kazi hiyo. Kijana huyo akaongoza moja kwa moja hadi kwenye friji kubwa lenye makabati mengi ya kuhifadhia maiti.


“Una ujasisi?”
Jama alizungumza huku akitoa moshi mwingi wa bangi hiyo anayo ivuta puani mwake.
“Fungua”
Jamaa akavuta droo hilo. Jery na Julieth wote wakamshuhuda mrs Mtenzi akiwa amelazwa kwenye droo hiyo inayo fuka moshi wa ubaridi mkali unao gandisha maiti hizo ili zisioze.


“Mama yako, kiwili wili chake cha chini kime pondeka vibaya sana. Je una weza kukiona?”
Swali la muhudumiaji huyo likamfanya Jery kukaa kimya huku machozi yakimwagika. Julieth naye machozi ya uchungu na hasira yakaendelea kumwagika kwani mwana mama huyo alikuwa akimpenda sana na kumjali na alimchukulia kama mwanaye wa kumzaa.
***


“Muheshimiwa raisi tume fanikiwa kuupata mwili wa Boko, ume tupwa baharini huku kichwa chake kikiwa kime gawanyishwa na mwili wake”
Ripoti hiyo ikamfanya makamu wa raisi bwana Madenge kusimama wima kutoka kwenye kiti alicho kikali.
“Yupo wapi?”
“Mwili wake upo kwenye gari muheshimiwa”
Makamu wa raisi akaongozana na kijana wake huyo hadi kwenye gari lililo beba mwili wa Boko, ambao una pelekwa hospitali kwa ajili ya kuhifadhiwa. Wakamfunua shuka lake na makamu wa raisi akadhibitisha kwamba ni mwili wa Boko.
“Mpelekeni hospitalini na mumuwekee na kichwa chake”


Makamu wa raisia lizungumza huku machozi yakimwagika kwani kuondoka kwa kijana wake huyo ni pigo kubwa sana kwake.
“Sawa muheshimiwa”
“Nendeni mukaniletee yule msichana anaye onyeshwa mambo yajayo. Nataka aje anitajie ni nania liye muua Boko. Mume nielewa”
“Sawa muheshimiwa”
Agizo hilo la kwenda kuletwa kwa Josephine likatekelezwa na vijana hao ambao kwa haraka wakaingia kwenye gari na kuainza safari ya kuelekea nyumbani kwa Magreth kwa ajili ya kumchukua Josephine.


ITAENDELEA


Haya sasa, makamu wa raisi ame agizwa Josephine kuletewa ikulu, je Josephine ata mtaja Magreth ambaye ndio ame muu Boko au ita kuwaje? Usikose sehemu ya 129.
 
SIN 129


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188



ILIPOISHIA


Makamu wa raisi akaongozana na kijana wake huyo hadi kwenye gari lililo beba mwili wa Boko, ambao una pelekwa hospitali kwa ajili ya kuhifadhiwa. Wakamfunua shuka lake na makamu wa raisi akadhibitisha kwamba ni mwili wa Boko.
“Mpelekeni hospitalini na mumuwekee na kichwa chake”


Makamu wa raisia lizungumza huku machozi yakimwagika kwani kuondoka kwa kijana wake huyo ni pigo kubwa sana kwake.
“Sawa muheshimiwa”
“Nendeni mukaniletee yule msichana anaye onyeshwa mambo yajayo. Nataka aje anitajie ni nania liye muua Boko. Mume nielewa”
“Sawa muheshimiwa”
Agizo hilo la kwenda kuletwa kwa Josephine likatekelezwa na vijana hao ambao kwa haraka wakaingia kwenye gari na kuainza safari ya kuelekea nyumbani kwa Magreth kwa ajili ya kumchukua Josephine.





ENDELEA


Gari mbili kutoka ikulu, zilizo jaa wanajeshi zikasimama getini mwa nyumba ya Magreth. Wakashuka wanajeshi sita na kusimama getini hapo. Mmoja wapo akaminya kitufe cha kengele na wakasubiriwa kwa ajili ya kufunguliwa. Magreth kwa haraka akatoa simu yake mfukoni na kutazama video za kamerza zilizo fungwa getini kwake.


“Hawa ni walinzi wa makamu wa raisi”
Magreth alizungumza huku akimatzama Juma na Josephine walio kaa sebleni hapo.
“Wamekuja kufanya nini?”
“Sijajua na sijamuona makamuwa raisi. Juma ingia ndani kwenye chumba cha daktari na hakikisha kwamba dokta Masawe hatoki ndani na wala hamjulikani kama mupo humu ndani”
“Sawa bosi”
Magreth akatoka nje na kufungua geti dogo.
“Habari zenu”
“Salama, tuna muhitaji Josephine ana hitajika ikulu kwa maagizo ya makamu wa raisi”
“Samahani naomba nione vitambulisho vyenu”
Mmoja wa wanajeshi hao akatoa kitambulisho chake na kumkabidhi Magreth akakisoma na umrudishia.
“Kama hamtojali nita kwenda naye ndugu yangu kwa maana siwezi kumuacha muka ondoka naye peke yake”
“Sawa hakuna shaka”
Magreth akafunga geti hilo na kurudi ndani.
“Vipi”
“Tuna elekea ikulu, si upo vizuri?”
“Ndio”
Magreth akaingia katika chumba alichopo Juma.
“Tuna kwenda Ikulu sasa hivi. Hakikisha kwamba dokta na mgonjwa wana kuwa salama”
“Sawa”
“Dokta kumbuka macho yangu yote yana kuangalia wewe, hakikisha mgonjwa ana kuwa salama”
“Sawa muheshimiwa”
Dokta Masawe alijibu kwa unyonge. Magreth na Josephine wakatoka nje na kuingia kwenye moja ya gari la wanajeshi hao na kuainza safari ya kuelekea Ikulu. Wakafika ikulu na moja kwa moja wakapelekewa katika ofisi ya makamu wa raisi.
“Karibuni na samaani kwa kuwakurupusha ila nime waita hapa nina hitaji kujua jambo moja tu”
Makamu wa raisi alizungumza bila hata ya kuwasalimia Magreth na Josephine.


“Jambo gani muheshimiwa?”
Magreth aliuliza.
“Kwanza kaeni”
“Asante”
Magreth na Josephine wakaka kwenye viti hivyo viwili vilivyopo mbele ya meza ya makamu wa raisi.
“Jana usiku kijana wangu au kwa lugha nyingine, mlinzi wangu wa karibu ameuwawa kifo cha kikatili sana. Ame katwa kichwa chake na nikaletewa hapa ikulu kama zawadi yangu”
“Mungu wangu!!”
Magreth alijikuta akistuka kana kwamba hafahamu kilicho tokea.
“Ndio, nina hitaji kufahamu ni nani aliye husika na kifo hicho. Wewe kama mtabiri unaye ona mambo yaliyo jificha nina hitaji uniambie ni nani ambaye eme husika na kifo hicho”
Josephine na Magreth wakatazamana.
“Samahani muheshimiwa, je ukiwaauliza wachunguzi wako wana dai nini?”
“Hadi sasa hivi sija fwatilia juu ya uchunguzi wao ila nina kuhitaji wewe uweze kuniambia ni nani ambaye eme husika”
Josephine akashusha pumzi taratibu kisha akafumba macho yake kwa sekunde kumi na tano kisha akayafumbua.
“Ume ona nini?”
“Kijana wako ame uwawa na Al-Shabab na wata muua kila mmoja ambaye ana hitaji kushikilia kiti cha uraisi. Wamekutumia zawadi hiyo ili kukuonyesha kwamba wana uwezo wa kukusogelea karibu na kukuua hata kama una lindwa na maelfu ya wanajeshi”
Josephine alimuongopea makamu wa raisi na kumfanya ajawe na wasiwasi mkubwa sana hadi akajikuta akisimama kwenye kiti chake.


“Una taka kuniambia ni Al-Shabab?”
“Ndio muheshimiwa siwezi kukuongopea”
“Mungu wangu, sasa niambie nifanye nini?”
“Ufanye nini muheshimiwa?”
“Kwa sas amimi ndio nina ongoza nchi. Sasa ita kuwaje wakiniua na mimi?”
“Najua ni nafasi ngumu sana muheshimiwa. Ila simamia nafasi ambayo Mungu amekuchagua, ukihitaji nafasi nje ya hiyo ambayo Mungu ame kuchagua kifo chako kita kuwa mapema sana na huto fanikiwa kwenye hiyo nafasi unayo ifikiria”
Josephine alizungumza kimafumbo na kumfanya bwana Madenge Jr kukaa tena kwenye kiti chake huku akiishiwa nguvu kabisa.
“Ina maana….kwamba….ahaahaha sawa, je raisi Mtenzi ata rudi?”
“SIku atakayo patikana ndio siku atakayo rudi”
“Si ume sema yupo mkoa wa Morogoro?”
“Ndio yupo mkoa wa Morogoro. Ila ina bidi muhakikishe kwamba muna ongeza jitihada za kumtafuta”
“Sawa nita fanya hivyo. Nina shukuru kwa maono yako”
“Nashukuru nawe pia muheshimiwa.”
Makamu wa raisi akamuita dereva wake na kumuagiza awarudishe Magreth na Josephine nyumbani kwao. Wakiwa kwenye kordo Magreth hakuamini kumuona Evans akiwa ana ana kuja mbele yao huku akiwa ameongozana na wanajeshi wawili. Walipo karibiana Magreth akasimama na kumfanya Josephine pamoja na dereva huyu kusimama.
“Tumekutana huku pia?”
Evans alianza kuzungumza hukua akiwa amejawa na tabasamu pana sana usoni mwake.


“Ndio, ume kuja kufanyaje hapa ikulu?”
“Nime kuja kwa kazi zangu. Naamini hata wewe ume kuja kwa shuhuli zako”
Taratibu Josephine akamsogelea Evans na kusimama karibu kabisa na sikio lake.


“Natambua jini wako Maimuna ame kuagiza uje kuzungumza upuuzi hapa kwa makamu wa raisi. Ila tambua hujui una dili na mambo ya aina gani na endapo uta kwenda ndani hapo na kuzungumzia kuhisiana na hadhina hiyo. Uta kufa mikononi mwangu na huyo jini wako Maimuna hato kuwa na uwezo wa kukusaidia na familia yako pamoja na lile gorofa ulilo jenga kwanu kwa pesa za kijini vita teketea na utamuacha mama yako kwenye hali ya umasikini mara saba ya umasikini walio kuwa nao mara ya wanza. Chaguo ni lako, kufunga bakuli lako au kupoteza kila ulicho nacho sasa”
Josephine alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza ambayo ni Evans pekee ndio alikuwa ana isikia. Woga ukamjaa sana Evans, hamu na shahuku yote iliyo mleta ikulu ikampotea. Akawatazama Magreth na Josephine wanao endelea na safari yao ya kuelekea nje huku nyuma yao wakifwata na dereva wa makamu wa raisi.
“Hei twende”
Mlinzi huyo alimsisitizia Evans ambaye muda wote macho yake ame wakodolea Magreth na Josephine hadi wakapotea kwneye upeo wa macho yake. Akaongozana na walinzi hao hadi ofisini kwa makamu wa raisi.
“Mkuu huyu kijana ana itwa Evans ameo omba kuonana na wewe””
“Una nini cha kuzungumza na mimi?”
“Ahaa…muheshimiwa kuna…kuna”
“Kuna kuna kuna nini? Acha kubabaika kama huna cha kuzungumza mtoeni ofisni kwangu bwana akili yangu haipo sawa”
Bwana Madenge Jr alizungumza kwa hasira kali sana huku akiwatazama walinzi wake hao. Evans akamuona jini Maimuna akiwa pembeni yake.


“Muheshimiwa nina imani kwamba una hitaji nafasi hii na una pata wakati mgumu sana wa kujihakikishia kuichukua hii nafasi”
Evans alizunugmza kimafumbo na kumfanya bwana Madenge Jr kustuka kidogo.


“Naomba mutupishe”
Bwana Madenge Jr alizungumza huku taratibu akiishusha hasira yake. Walinzi hao wakatoka ofisini hapo.
“Rudia ulikuwa una sema”
“Natambua kwamba una hitaji nafasi ya uraisi na mpinzani wako ni raisi Mtenzi ambaye hadi sasa hivi hufahamu ni sehemu gani alipo, si ndio?”
“Wewe ni nani?”
“Nina itwa Evans Shika ni mtumishi wa Mungu ambaye nina uwezo wa kuona maono makubwa sana yajayo na hata nikikutazama wewe nina weza kuona kwamba ni kitu gani unacho kiwaza”
Makamu wa raisi akamkazia macho Evans anaye jibaragazua mbele yake.


“Una jua nina waza nini sasa hivi?”
“Ndio?”
“Niambie”
“Uta wezaje kuwashinda Al-Shabab ambao wame kuwa ni kikwazo kikubwa sana cha nafasi yako ya uraisi kwa ni wame muua mlinzi wako na wemekuletea kichwa”
Maneno yote anayo yazungumza Evans yana toka kwa jini Maimuna ambaye hata yeye ameweza kupotezwa katika maono yake na Josephine ambaye ana uwezo wa kuomba chochote kwa Mungu na akajibiwa wakati huo huo.
“Nipe njia ya kupambana nao?”
“Nahiyaji unihakikishie jambo”
“Jambo gani?”
“Uta nipa nafasi kubwa kwneye nchi ya kutengeneza kanisa langu kubwa na vikwazo vyote ambavyo niliwekewa katika uanzilishi wa kanisa langu vina futwa.”
“Vikwazo gani?”
“Moja raisi Mtenzi alihitaji kunia akishirikiana na mwanaye Jery”
“Nikuamini vipi?”
“Nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Julieth mkwe wa Mtenzi hivyo walihitaji kunia ikuwa ili kuto kuniaona duniani ili kulinda ndoa hiyo”
Makamu wa raisi akashusha pumzi huku akimtazama Evans usoni mwake.


“Ishu ni wewe kujenga kanisa pekee?”
“Na kulipiza kisasi kwa Jery na Julieth”
“Kwa hiyo una nihakikishia kwamba nita pata kiti cha uraisi?”
“Ndio”
“Kijana mimi sio mtu wa masihara. Endapo sinto pata kiti hichi cha uraisi, nita kuua mimi mwenyewe. Umenielewa?”
“Ndio muheshimiwa”
“Basi ume pata unacho kihitaji. Hao unao hitaji kuwalipizia kisasi kazi ni kwako mimi sinto jihusisha, ume nielewa?”
“Nashukuru muheshimiwa”
“Niambie sasa raisi Mtenzi kwa sasa yupo wapi?”
Jini Maimuna akamnong’oneza Evans masikoni mwake.
“Yupo mkoani Morogoro”
Jibu hilo la Evans likazidi kumfanya makamuwa raisi kumuamini Evans kwani hata utabiri wa kwanza wa Josephine ame mueleza kuhusiana na mkoa wa Morogoro, kitu ambacho ni uongo kwani raisi Mtenzi yupo ndani ya jiji hilo hilo la Dar es Salaam.
***


Magreth na Josephine wakashuka kwenye gari getini kwao na dereva huyo akaondoka zake. Wakaingia ndani huku Josephine akionekana hana furaha kabisa.


“Mbona uso wako una onekana haun furaha?”
“Nahitaji kuingia kwenye vita Mage”
“Vita gani?”
“Vita ya kumuangamiza jini Maimuna. Nimeweza kumdhibiti kwa sasa katika kuona kile ambacho nina kiona mimi. Kwa sasa ana ona yale yote ambayo ni nina zungumza kwa kuganganya na hayo ndio anayo yaona yeye. Kwenye hilo nime fanikiwa ila nahitaji kumrudisha kuzimu kwa maana ana weza kuleta madhara makubwa sana”
“Sasa hiyo vita nita kusaidije?”
“Sio vita ya kuonana na macho Mage. Nina imani kwamba una jua vita za kiroho jinsi zinavyo kuwa”
“Ndio”
“Nahitaji kufunga kwa siku saba kavu”
“Bila kula chochote?”
“Ndio, mbona sio mara moja kufanya hivyo. Nahitaji kuingia kwenye maombi ya nguvu kuhakikisha kwamba nina muondoa kabisa jini Maimuna kwenye huu ulimwengu”
“Sawa sawa”
Baada ya mazungumzo hayo wakaingia ndani. Wakamkuta Juma akiwa sebleni akitazama luninga.
“Vipo ume pata kfingua kinywa?”
“Hapana nina wasubiria nyinyi”
“Vipi mgonjwa hali yake?”
“Kama mulivyo ondoka ipo vile vile, dokta yupo chumbani kwake.”
Josephine akaingia kwenye chumba alicho lazwa raisi Mtenzi. Akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akamsogelea kitandani hapo.
“Maisha ya raisi yapo hatarini dokta. Natambua una jua uwezekano wake wa kupona ni mdogo snaa si ndio”
Dokta Masawe akashusha pumzi taratibu kwa maana ana tambua fika kwamba uwezekano wa raisi Mtenzi kupona ni mdogo sana.


“Ndio”
“Natambua una fanya kazi kwa shinikizo la kuogopa kuuwawa si ndio?”
“Ndio”
“Nahitaji kukaa ndani hapa na raisi kwa wiki moja”
“Sija kuelewa?”
“Najua huja nielewa. Ila kwa matibabu yako hayo ni kwamba lazima raisi ata kufa ndani ya siku mbili zijazo. Nahitaji kumuomba Mungu kumpatia nafasi nyingine aweze kuishi hivyo sitaki ubebe lawama ambayo ita kuepekea wewe kifo. Umenielewa”
“Ndio”
Magreth na Juma wakaingia ndani ya chumba hicho.


“Jose nime sikia vibaya au?”
Magreth aliuliza huku akimtazama Josephine aliye simama pembezoni mwa kitandani alicho lazwa raisi Mtenzi.
“Huja sikia vibaya, huo ndio ukweli. Nina kiona kifo cha raisi Mtenzi ndani ya siku mbili zijazo. Kifo ambacho kita ipelekea nchi katika mateso makubwa sana, zaidi ya haya ambayo tuna yapitia kwani maana makamu wa raisi kwa sasa kinacho muongoza ni tamaa na ata fanya kila liwezekanalo kuipata nafasi ya uraisi”
Magreth na Juma wakajawa na wasiwasi.


“Hichi ninacho kwenda kukifanya sifahamu kama Mungu ata nijibu au laa, ila nime ona kwamba kesho kutwa ata kufa na endapo ata kufa dokta Masawe muta muua pasipo sababu ya msingi hivyo nina waomba kuanza hivi sasa munipe nafasi, nita kaa ndani hapa kwa maombi ya siku saba. Chochote kitakacho tokea nikiwa katikati ya maombi tafadhali musi fanye jambo la aina yoyote. Tume elewana”
“Ndio”
“Ninaomba muniache na mgonjwa sasa”
Josephine alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Magreth, dokta Masawe na Juma wakatoka ndani hapo huku kila mmoja akiwa amejawa na huzuni kubwa kwa maana hawajui ni n ini kitatokea mara baada ya raisi Mtenzi kufariki duniani.


ITAENDELEA


Haya sasa raisi Mtenzi ata fariki siku mbili zijazo je maombi ya Josephine yana weza kufanya kazi au ata shindwa? Usikose sehemu ya 130.
 
SIN 130


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188







ILIPOISHIA


“Hichi ninacho kwenda kukifanya sifahamu kama Mungu ata nijibu au laa, ila nime ona kwamba kesho kutwa ata kufa na endapo ata kufa dokta Masawe muta muua pasipo sababu ya msingi hivyo nina waomba kuanza hivi sasa munipe nafasi, nita kaa ndani hapa kwa maombi ya siku saba. Chochote kitakacho tokea nikiwa katikati ya maombi tafadhali musi fanye jambo la aina yoyote. Tume elewana”
“Ndio”
“Ninaomba muniache na mgonjwa sasa”
Josephine alizungumza huku machozi yakimlenga lenga. Magreth, dokta Masawe na Juma wakatoka ndani hapo huku kila mmoja akiwa amejawa na huzuni kubwa kwa maana hawajui ni n ini kitatokea mara baada ya raisi Mtenzi kufariki duniani.





ENDELEA


“Dokta ni kweli raisi Mtenzi ata fariki?”
Magreth alimuuliza dokta Msawe kwa sauti ya upole sana.
“Hali yake ilifikia kwa kweli ni mbaya na pia ni hali ambayo kwa hapa ndani na mimi peke yangu siwezi kumuhudumia.”
“Una shaurije?”
“Kwa kuwa Mungu hashindwi na jambo la aina yoyote basi nasi tuendelee kumuomba aweze kupona”
“Sawa”
Kengele ya getini iliyo anza kutia mlio ikamfanya Magreth kutoa simu yake mfukoni mwake na kuangalia ni nani anaye bisha hodi. Akamona RPC Karata akiwa amesimama mlangoni hapo, akatoka nje na kumfungulia.
“Karibu sana kaka”
“Nashukuru, una endeleaje?”
“Nina meshukuru Mungu”
“Karibu ndani?”
“Mimi sio mkaaji sana. Nime pita mara moja kukujuza kwamba kume tolewa taarifa ya kumsaka mtu aliye fanya mauaji ya yule kijana”
“Nina uhakika kwamba hawato weza kufahamu si ndio?”
“Yaa kwa maana mimi ndio nilikipeleka kichwa cha yule kijana ikulu na nina imani kwama muheshimiwa ameweza kuchanganyikiwa”
“Mmmm ume kipeleka vipi?”
“Nilikiweka kwenye boksi na kumpa omba omba mmoja ambaye alikwenda kukitupa katika geti la ikulu, kwa bahati mbaya alipo kuwa ana kimbia alipigwa riasi na akafariki hivyo ushahidi uliweza kufutika”
“Masikini wee”
“Ndio hivyo no way out. Sasa nina hitaji kumfikishia hii audio ya mahojiano na nita mshinikiza aweze kuachia nafasi yake ya umakamu wa raisin a ikiwezekana waziri mkuu aweze kuiongoza nchini”
“Mmmmm ata kuua”
“Najua ata niua ila sinto ipeleka mimi kama mimi. Nitakacho jaribu ni kumtumia kwa mtando na hato weza kufahamu ime tokea wapi”
“Sawa ila kuwa makini, wewe si una jua hii hali inavyo endelea”
“Ndio ndio. Vipi hali ya raisi ina maendeleo yoyote?”
“Josephine ameweza kuona kifo cha raisi Mtenzi”
“Nini?”
“Yaa tena ame dai kwamba baada ya siku mbili ana weza kufa. Ila alicho kifanya ni kujifungia chumbani kwa raisi Mtenzi na kumuomba Mungu aweze kumuepushia raisi Mtenzi kifo hicho”
“Dokta Masawe hajafanya upumbavu wake?”
“Hapana haja fanya chochote kwa kweli, ila tumuache Mungu afanye kazi yake kwa maana hata madaktari huwa wana shindwa kuzuia kifo. Nina muamini Josephine ana weza kufanya jambo katika hili”
“Acha nikamuone raisi?”
“Hapana, Josephine emeomba kujifungia ndani hapo ili kuhakikisha kwamba ana yata kuwa maombi ya siku sana bila kula chochote”
“Duu sawa sawa. Acha mimi nika endelee na majukumu mengine”
“Sawa kaka”
RPC Karata akaingia kwenye gari lake na akaondoka na Magreth akarudi ndani.


***


“Nahitaji kuelekea ikulu”


Jery alimwambia mmoja wa walinzi wanao mlinda.
“Ila muheshimiwa bado madaktari hawajakupatia ruhusa?”
“Ndio nina litambua hilo ila nina hitaji kwenda ikulu sasa hivi”
Jery alizungumza kwa msisitizo na mwanajeshi huyo akakubaliana na ombi hilo.
“Nahitaji ubaki hapa nina kwenda ikulu mke wangu”
Jery alimuambia Julieth huku akimtazama usoni mwake.
“Mume wangu haupo sawa. Twende wote”
Jery akamtazama kwa sekunde kadhaa Julieth kisha akamtazama nabii Sanga.
“Muna weza kwenda pamoja mwanangu”
Nabii Sanga alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Jery usoni mwake.
“Sawa”


Jery, Julieth na walinzi sita wakaondoka hospitalini hapo na kuelekea ikulu. Ukimya ndani ya gari hilo ukazidi kutawala, taratibu Julieth akamshika mkono Jery.


“Be stronger mume wangu”
“Haya”
Jery alijibu kwa ufupi huku akitazama geti la Ikulu linavyo funguliwa. Gari hizo mbili zika simama na wanajeshi hao wakashuka. Jery akajifikiria kwa sekunde kadhaa kisha wakashuka kwa pamoja na mke wake kwenye gari hilo.Jery akaanza kuongoza njia huku Julieth pamoja na walinzi hao wakimfwata kwa nyuma. Jery na Julieth wakajikuta wakisimama huku wakimtazama Evans anaye kuja mbele yao.


“Ume kuja kufanya nini hapa?”
Jery alimuuliza Evans huku akimshika shati lake.
“Tafadhali una nichafua”
Jibu la Evans alikamfanya Jery amtandike ngumi Evans kichwa cha uso huku akimuachia na kumfanya aweweseke huku akiyumba sana. Jery akataka kumvamia ila walinzi wake wakamzuia kwa ili kuepusha mtafaruku huo.
“Mkamateni mshenzi huyo”
“Hawezi kukamatwa”
Mlinzi ambaye alikuwa akimsindikiza Evans alijibu kwa kujiamini na kumfanya Jery kumshangaa sana.
“Una semaje wewe?”
“Nime sema kwamba hakamatwi na nyote sihitaji mumshike huyu kijana”


“Una zungumza wewe kama nani?”
“Kama mlinzi wa kiongozi wa nchi. Tuna weza kuendelea”
Mlinzi huyo alizungumza huku akimshika mkono Evans na wakaanza kuondoka eno hilo. Evans akamkonyesha Julieth na kumfanya Jery kuzidi kujawa na hasira sana. Evans akapiga hatua kadhaa kisha akasimama, taratibu akarudi sehemu alipo simama Jery na kumsogelea karibu yake.


“Ulinitesa kipindi kile kisa huyo malaya hapo. Ila kwa sasa kibao kimekugeukia wewe hivyo usinitishe”
Maneno hayo ya Evans hayakumpendaza kabisa Jery. Akamvaa Evans na kumuangusha chini akaanza kumshambulia kwa kumpiga ngumi mvululizo. Walinzi wa Jery hawakuhitaji kuamua ugomvi huo kwani Evans ndio aliye rudi na hawajui ni kitu gani alicho kizungumza na kumfanya Jery kukasirika. Mlinzi wa makamu wa raisi akataka kuamua ugomvi huo ila walinzi wa Jery wote wakamnyooshea bunduki zao.
“Usiwaguse”
Walinzi wengine wanao fanya kazi chini ya makamu wa raisi wakafika eneo hilo na kila mmoja akaanza kuwanyooshea bunduki walinzi wa Jery. Julieth akatamani kuamua ugomvi huo ila akajikuta akishindwa kwani kiuhalisia Evans ndio mwanaume wake wa kwanza kumtoa usichana wake. Evans hakuhitaji kuwa mnyonge, akamgeuza Jery na kumuweka chini, akaanza kumshindilia ngumi mfululizo.


“Ni nini kinacho endelea hapo?”
Makamu wa raisi alizungumza kwa kufoka huku akitembea kwa haraka eneo hilo la ugomvi.
“Waamueni”
Hapakuwa na mlinzi aliye weza kupinga amri hiyo ya makamu wa raisi. Wakaachanisha Jery na Evans ambao kila mmoja ana mwagikwa na damu puani mwake.


“Nitakuu wewe mwana haramu?”
Jery aliendelea kufoka huku akijitahidi kujitoa mikononi mwa walinzi wake.
“Jaribu uone, mimi sio Evans yule mnyonge wa kipindi kile nita kuua na wewe”
“Muondoeeni huyo”


Makamu wa raisi alizungumza na Evans akatolewa nje kabisa ya jengo la ikulu. Gari lake likatolewa na akaamrishwa aondoke eneo hilo.
“Daktari aletwe na mpelekeani Jery ndani kwao”
“Sawa mkuu”
Jery akapelekwa katika nyumba wanayo ishi.
“Nita muua yule mshenzi”
Jery aliendelea kufoka huku damu zikimwagika puani mwake. Julieth akachukua moja ya kitambaa na akaanza kufuta Julieth damu hiyo inayo mwagika. Daktari akaingia ndani hapo na akaanza kumpatia huduma Jery ambaye bado ana fura kwa hasira.


“Mume wangu tuliza hasira najua ni jinsi gani tuta dili naye yule mshenzi”
“Lazima nimuue”


Jery aliendelea kulalama. Akaingia makamu wa raisi na kukaa kwenye moja ya sofa.
“Jery mwanangu mbona una kuwa mgomvi kiasi hicho?”
Bwana Madenge Jery alizungumza huku akimtazama Jery usoni mwake.


“Yule ni mshenzi sana”
“Ame faya kosa gani?”
Jery akamtazama Julieth kwa sekunde kadhaa.


“Baba mdogo hayo achana naye. Mume fikia wapi kumpata baba yangu?”
“Bado tuna endelea kumtafuta na wana jeshi wana fanya msako kwenye mkoa wa Morogoro.”
“Kwani ndipo alipo pelekwa?”
“Ndio”
“Ume fahamu kama mama yangu ame fariki?”
“Ndio nina fahamu”
“Nahitaji uwaue wote walio husika kwenye mauaji hayo. Umeinielewa baba mdogo?”
“Nime kuelewa endapo tuta wakamata wahusika basi tuta shuhulika nao kisawa sawa”
“Tukiachana na hayo Evans Shika ame kuja kufanya nini hapa ikulu?”
“Ahaa alikuja kutoa pole”
“Pole kwa nani ikiwa wahusika wa hii ikulu hatupo?”
“Jery kumbuka kwamba raisi anapo kuwa hayupo madarakani mimi ndio nina ichukua nafasi yake”
“Ila na wewe si una ikulu yako kwa nini usiende kuifanyia kazi yako yote kwenye ikulu?”
Jery alizungumza kwa kufoka sana.


“Kumbuka una zungumza na nani Jery. Pia wewe huna mamlaka yoyote kwenye hii nchi, wewe ni mtoto wa raisi na sio raisi. Usilisahau hilo”
“Mume wangu tuliza jazba. Baba mdogo msamehe mume wangu, naamini kwamba hayupo kwenuye wakati mzuri”
“Nina kwenda kuendelea na majukumu yangu. Endapo uta kuwa sana, nipo ofisini”
Makamu wa raisi akatoka ndani hapo.
“Hivi vidonge uta kunywa utakapo jisikia maumivu ya kichwa”
Dokta akamkabidhi vidonge hivyo Julieth kisha akatoka ndani hapo.
“Mume wangu huyu ni baba yako mdogo kweli?”
“Hapana nime zoea kumuita baba mdogo tu. Alafu huyu mzee huwa simuamini sana”
“Humuamini kivipi?”
“Ni mtu mwenye tamaa, ina wezekana ana fahamu ni wapi alipo baba yangu ila ana zingua. Ila ngoja kuna kifaa ambacho ni cha siri sana ambacho ana kifahamu mimi, mama na baba. Kifaa hicho huwa kina muonyesha raisi ni eneo gani alipo”
“Una fahamu kilipo?”
“Ndio nina fahamu ni wapi kilipo”
Jery na Julieth wakaingia katika chumba cha raisi Mtenzi. Jery moja kwa moja akasogeza kitanda, akatoa zulia lililopo chini ya zulia hilo na kukuta mfuniko wa chuma ambao ni mdogo na una batani za kuingiza namba za siri. Jery akaingiza namba za siri na akafungua kimlango hicho. Akakitoa kifaa hicho kilocho kaa kama simu. Akakiwasha, na kikahitaji neneo la siri na akaandika jina la mama mzaa baba yake.


“Hapa sasa ni sawa”
Jery alizungumza huku wote wakikitazama kofaa hicho. Baada ya sekunde kadhaa alama ya kijani ikaonekana.
“Yes baba yupo hai”
“Ume juaje?”
“Endapo ingeonyesha alama nyekundu basi baba angekuwa amesha kufa”
“Weee”
“Ndio na alama inaonyesha baba yupo hapa hapa Dar es Salaam”
“Muambie basi baba yako mdogo ili aweze kutuma jeshi?”
“Hapana tuna kwenda sisi wenyewe”
“Kama watakuwa ni watu wabaya ndio wame mchukua ita kuwaje mume wangu”
“Julieth ninapo kuambia kwamba huyu makamu wa raisi simuamini na kwenye maisha yako sheria namba moja usimuamini mtu yoyote hapa ikulu. Hujui ni sumu ya aina gani ambayo makamu wa raisia me mezeshwa yule mshenzi Evans.”
“Sawa mume wangu”
Jery na Julieth wakaingia katika chumba cha Jery wakabadilisha nguo na Julieth akavaa nguo za Jery ambazo zina mtosha. Wakaondoka eneo hilo la ikulu pasipo walinzi na kuanza kufwata amelekezo ya kifaa hicho sehemu kinapo waelekeza kuelekea.
“Kunja kushoto hapo”
Julieth alizungumza na Jery akakunja kona ya ya barabara inayo inagi kwenye mtaa ambao una majumba mengi ya kifahari.


“Simama simamisha gari”
Julieth alizungumza mara baada ya alama hiyo ya kijani kuanza kucheza cheza kipindi tu walipo fika usawa na nyumba anayo ishi Magreth.


ITAENDELEA


Haya sasa Julieth na Jery wamegundua ni sehemu gani raisi Jery yupo je Magreth akilitambua hilo kwama maadui zake wame fika hapo hususani Julieth ata fanya nini? Usikose sehemu ya 131.
 
SIN 131


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188




ILIPOISHIA


Jery na Julieth wakaingia katika chumba cha Jery wakabadilisha nguo na Julieth akavaa nguo za Jery ambazo zina mtosha. Wakaondoka eneo hilo la ikulu pasipo walinzi na kuanza kufwata amelekezo ya kifaa hicho sehemu kinapo waelekeza kuelekea.
“Kunja kushoto hapo”
Julieth alizungumza na Jery akakunja kona ya ya barabara inayo inagi kwenye mtaa ambao una majumba mengi ya kifahari.


“Simama simamisha gari”
Julieth alizungumza mara baada ya alama hiyo ya kijani kuanza kucheza cheza kipindi tu walipo fika usawa na nyumba anayo ishi Magreth.





ENDELEA


“Alama inaonyesha ni hapa”
Julieth alizungumza na wote wakalitazama geti hilo lililo fungwa.


“Ina kuwaje?”
Julieth alizngumza huku akitazama geti hilo.
“Ina kuwaje kivipi?”
“Hii nyumba ana ishi dada mmoja ana itwa Magreth”
“Una taka kusema yeye ndio ame mteka baba?”
“Sija jua ila ngoja tugonge tuone”
Wakashuka kwenye gari hilo na wakalisogelea geti hilo. Juilieth akaminya kitufe cha kengele walicho kiona kwenye geti hilo. Magreth macho ya mshangao yakamtoka jambo lililo mfanya Juma atambue juu ya mstuko huo.
“Mbona una onekana una wasiwasi?”
“Jery na Julieth wapo hapa?”
“Ndio kina nani?”
“Jery ni mtoto wa raisi Mtenzi na Julieth ni mtoto wa nabii Sanga”
“Wame juaje kama raisi yupo hapa?”
“Kwa kweli sifahamu. Hembu ngoja kwanza?”
Magreth akampigia simu RPC Karata.
“Mage vipi?”
“Jery na Julieth wapo getini kwangu wana gonga je ume weza kuwaleza uwepo wa raisi Mtenzi eneo hili?”
“Hapana, kwani wamesha toka hospitalini?”
“Ndio, sasa sijui ime wame juaje?”
“Hembu wasikilize wana weza wakwa wame kuja labda kuulizia huduma ya Josephine”
“Etii ehe?”
“Yaa kwani wame kuja na walinzi?”
“Hapana nina waona wakiwa wapo wao peke yako”
“Basi wata kuwa wamekuja kumuulizia huyo rafiki yako”
“Basi ngoja niwasikilize”


Magreth akakata simu na kumgeukita dokta Masawe.
“Una weza kwenda jikoni ili wasikukute hapa kwa maana bado hatujui ni nani wa kumuamini”
“Sawa”
Dokta Masawe akaelekea jiko na Magreth akatoka ndani na kufungua geti dogo.


“Habari yako”
Jery alianza kusalimia.
“Salama, niwasaidie nini?”
“Nisikilize Mage, alama ina onyesha kwamba baba yangu mkwe yupo hapa. Tume kuja kiamani na hatujawahulisha askari na endapo tunge wajulisha basi tungekuja na majeshi. Hivyo tuambie kama baba mkwe wangu yupo au hayupo?”
Julieth alizungumza kwa sauti ya msisitizo na iloyo jaa hasira kidogo.
“Una zungumzia nini wewe?”
“Julieth tulia. Dada mimi nina itwa Jery Mtenzi, ni mtoto wa raisi Mtenzi. Nina imani una nifahamu?”
“Yaa nilikuona kwenye tv?”
“Baba yangu aliweza kutoroshwa hospitali ya Muhimbili alipo kuwa amelazwa. Hivyo tafadhali dada yangu, hiki ni kifaa maalumu ambacho kina muonyesha raisi sehemu alipo na kama unavyo ona kina wakia eneo hili kama unavyo kiona.”
Jery alizungumza kwa sauti ya upole huku akimtazama Magreth usoni mwake. Magreth akanyoosha mkono wake na Jery akamkabidhi kifaa. Magreth akatazama alama hiyo jinsi inavyo waka waka na kweli ramani ina onyesha kwamba raisi Mtenzi yupo hapo.
“Ingieni ndani”
Magreth alizungumza huku akimkabidhi Jery kifaa hicho. Wakaingia ndani na akawakaribisha sebleni hapo.
“Kifaa hicho kilikuwa wapi?”
“Ni mali maalumu inayo milikiwa na raisi hivyo watu wake hususani wana familia yake ndio watu wa pekee ambao wana fahamu hilo.”
Magreth akashusha pumzi huku akimtazama Juma ambaye ana yafwatilia mazungumzo hayo vizuri.


“Raisi yupo hapa ila hali yake sio nzuri”
“Una maana gani kuzungumza hivyo kwamba hali yake sio nzuri?”
Jery aliuliza kwa sauti ya upole na iliyo jaa heshima kubwa sana.
“Ajali muliyo ipata ilikuwa ni mbaya sana. Ila jambo ambalo lilikuwa lina kwenda kumtokea lilikuwa ni zaudi ya ubaya”
“Jambo gani?”
“Alipangwa kuuwawa kwa kuchomwa sindano ya sumu akiwa hospitalini kwenye hali hiyo. Ila ndugu yangu aliweza kupata maono juu ya jambo hilo na kitu cha kumshukuru Mungu ni kwamba tulifanikiwa kumuokoa kutoka kwenye tatizo hilo na ndio nika mleta nyumbani hapa”
“Ni nani aliye taka kumuua?”
Julieth aliuliza kwa shahuku ya kuhitaji kufahamu juu ya jambo hilo.
“Makamu wa raisi alihitaji kumuua”
“NINI……!!?”
Jey aliuliza kwa mshangao mkubwa sana.


“Ndio alimpatia tenda mmoja wa madaktari wa Muhimbili katika kutekeleza tukio hilo. Ila kwa bahati mbaya akataka kumuua yule daktari mara baada ya kushindwa kutekeleza jambo hilo.”
“Mke wangu si una kumbuka nilicho kuambia?”
“Ndio mume wangu nina kumbuka”
“Kwa hiyo wewe ndio uliye mtorosha?”
“Mimi na kijana wangu hapa tulishirikiana katika kuifanya kazi hiyo. Maisha ya raisi na uzalendo ni kwanza japo mimi na familia ya mkwe wako hatuna maelewano. Sikutaka kutumia matatizo yangu na familia ya nabii Sanga kumuacha raisi kupata kifo ambacho sio haki yake.”
“Kabla sijamuona baba yangu ila nina kushukuru sana dada Magreth”
Jery alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Usijali, dokta Msawe”
Magreth aliita na dokta Msawe akafika sebleni hapo.
“Una weza kuketi dokta”
Dokta Masawe akaketi huku akimtazama Jery usoni mwake.


“Huyu ndio dokta aliye nusurika kifo kutoka mikononi mwa makamu wa raisi”
“Mzee wangu wewe ndio ulipewa jukumu la kumuua baba yangu?”
“Ndio”
“Una uhakika?”
“Asilimia mia moja. Malipo yangu ilikuwa ni milioni mia moja pamoja na kupandishwa cheo. Nilishindwa kutekeleza hili ikiwa wewe nawe ulikuwa ndani ya chumba kile kile pamoja na mke wako na wale walinzi wawili. Nilipo muambia kwamba nime shindwa, akahitaji kunia. Huyo binti ndio aliye nisaidia na kuanzia siku hiyo tuna ishi hapa na muheshimiwa. Huko nje endapo nita utoa uso wangu basi nita uwawa”
Maneno ya dokta Masawe yakamfanya Jery kububujikwa na machozi ya hasira. Unyama ambao ulitendeka kwenye harusi yake makamu wa raisi ana ona hautoshi hadi ana hitaji kumalizia kabisa baba yake.
“Yote aliyefanya ili iweje?”
“Ili apate uraisi”
“Ohoo alishindwa kusubiria baba yangu amalize muda wake na agombanie yeye. Mbona binadamu hatuna shukrani sisi”
Jery alizungumza kwa huzuni kubwa sana huku akiendelea kulia kwa uchungu sana hadi Magreth akamuonea huruma.


“Mama yangu ame kufa, baba yangu hali yake ndio hiyo. Hivi kweli kweli, huyu makaku wa raisi ana paswa kufanya hivi?”
“Usilie mume wangu, jambo la msingi ni kumshukuru Mungu kwamba tume mpata baba”
Julieth alimbembeleza Jery anaye lia kama mtoto mdogo. Kila aliye muona Jery alijikuta akijawa na huzuni kubwa sana.
“Naweza kumuona baba yangu?”
“Ndio ila kwa sasa ana fanyiwa maombi ya siku saba. Ndugu yangu ambaye aliweza kuona jambo hilo kwenye maono pia ame weza kuona kifo cha baba yako baada ya siku mbili ndio maana ame amua kufanya maombi ya mfululizo kwa ajili ya kumuombea baba yako kurudi kwenye uzima.”
“Nionyeshe tu”


Magreth akasimama na kwa ishara akamuomba Jery amfwate. Wakafika kwenye chumba alichopo raisi Mtenzi. Magreth akachukua moja ya stuli na akapanda na kuchungulia kwa kupitia eneo la juu la mlango huo ambalo lina kioo. Akamuona Josephine akiwa amepiga magoti pembeni ya kitanda cha raisi Mtenzi hukua akiomba kwa unyenyekevu mkubwa sana.
“Una weza kumuona kupitia hapa. Muombaji ame omba kuto sumbuliwa hadi siku saba zitakapo kwisha”
Taratibu Jery akapanda na kuchungulia ndani hapo, hakumini kumuona baba yake akiwa amelala kitandani huku mashine za kumsaidia kupumua zikiwa puani mwake. Unyenyekevu ambao ana uonyesha Josephine uka mfanya Jery kuelewa ni kitu gani kinacho endelea kwenye maombi hayo. Jery akaendelea kulia kwa uchungu sana, furaha, amani na upendo ambao alikuwa akionyeshwa na wazazi wake wote ume potea. Julieth uvumilivu uka mshinda, akafika eneo hilo na kumkuta Jery akiwa ana chungulia ndani hapo. Taratibu Jery akashuka na kujikuta akishindwa kuizuia sauti yake ya kulia. Julieth kwa haraka haraka akapanda kwenye stuli hiyo na kuchungulia ndani, akajidhibitishia jambo walilo kuwa wakielezwa na Magreth. Akashuka taatibu huku akiwa mnyonge sana kwani alikuwa ana mchukulia Magreth ni aduia yake mkubwa sana.


Julieth akamshika mkono Jery na wakarudi sebleni wote watatu.
“Mage”
Jery aliita huku akifuta machozi yake.
“Ndio”
“Baba yangu akipona nina kuhakikishia zawadi kubwa sana. Hili ulilo lifanya ni jambo la kishujaa, nina imani kwamba uta kuwa una tafutwa kwa kufanya tukio hilo?”
“Ndio ila hawakunijua. Pia huyo ndugu yangu hapo ndani aliweza kuwaambia eneo ambalo raisi amepelekwa ni mkoani Morogoro “
“Sasa napata picha”
Jery alizungumza huku akimtazama Magrth usoni mwake.
“Picha gani?”
“Makamu wa raisi alituambia kwamba wana jeshi na askari wapo mkoani Morogoro na wana mtafuta raisi”
“Yaa japo hapaswi kundaganya ila ilimpasa kufanya hivyo ili mradi kuhakikisha kwamba maisha ya raisi yanakuwa salama”
“Dada Mage, nina kuamini, nina amini baba yangu yupo mikono salama. Ila siwezi kuendelea kukaa hapa, nahitaji kufanya kitu kwa ajili ya kuhakikisha bwana Madenge ana lipa juu ya hili alilo lifanya kabla ya kwenda kwa hao Al-Shabab walio ua maelfu ya watu ambao hawana hatia”
“Sawa ila Jery kumbuka kwamba endapo uta kuwa ni kikwazo kwa makamu wa raisi basi ana weza kuku. Kuwa makini sana kwenye hilo”
“Usijali dada, kwa kuwa nimesha jua ni adui yangu ni nani basi nita jua ni namba gani ya kutumia uwezo wangu kuhakikisha kwamba nina muondoa makamu wa raisi kwenye hicho kiti anacho kikalia. Ikitokea hata baba yangu ame kufa, ni heri aka patikana kiongozi atakaye ingia madarakani kwa mapenzi ya Mungu kuliko kiongozi atakaye ingia kwa ajili ya tamaa zake yeye mwenyewe”
“Sawa nime kuelewa”
Jery akasimama na akapeana mikono na Magreth, Juma pamoja na dokta Masawe. Julieth naye aka fanya hivyo hivyo kisha wakaondoka nyumbani hapo.


“Bosi hii haitoo leta uhatari wa usalama wetu kwa maana sasa hili jambo sio siri tena?”
Juma alizungumza huku akimtazama huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana.
“Akitoa siri hii basi atakaye kufa ni baba yake. Ila jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba tuna mlinda raisi ndani ya hizi siku ambazo Josephine ana fanya maombezi. Akipona sawa asipo pona pia tuta mshukuru Mungu kwa maana kwenye haya maisha hakuna mtu atakaye ishi milele.”
Magreth alizungumza kwa sauti ya upole ambayo dhahiri ina onyesha amejiandaa kukubaliana na kila jambo litakalo kwenda kutokea mbele yake.
***


“Tuna kwenda wapi mume wangu”
Julieth aliuliza huku akimtazama Jery anaye ongeza mwendo kasi wa gari hilo analo liendesha.
“Kwa waziri mkuu”
“Kufanya nini?”
“Yeye ndio mtu ninaye muamini”
“Mume wangu, una tambua ni hali gani inayo endelea. Waziri mkuu naye kwa mafano akikugeuka ita kuwaje ehee?”
Julieth alimuuliza mume wake kwa msisitizo huku akimtazama usoni mwake. Taratibu Jery akapunguza mwendo kasi wa gari hilo na kulisimamisha pembezon mwa barabara. Akaanza kuupiga piga mskani wa gari hilo kwa hasira kali sana, hukua akilia kwa uchungu sana.
“Nita muua kila mmoja aliye husika kwenye hili, haki ya Mungu nita muua”
Jery aliendelea kufoka kwa hasira sana. Julieth akatamani kumueleza Jery juu ya uwezo na nguvu iliyopo nyuma yake ila ana ogopa sana kwa maana chanza cha matatizo haya yote yanayo tokea sasa hivi ni kutokana na vijaa wake kuwaangamiza askari wa baharini na kesi hiyo wakaichonganisha na kundi la kigaidi la Al-Shabab.


‘Ehee Mungu wangu nita fanya nini mimi?’


Julieth alizungumza kimoyo moyo huku akimtazama Jery aliye inamisha kichwa chake kwenye mskani wa gari hilo huku akiendelea kulia kama mtoto mdogo.


“Mume wangu”
“Mmmmm”
“Nina mpango katika hili, je upo tayari tushirikiane?”
Jery taratibu akanyanyua kichwa chake na kumtazama Julieth usoni mwake kisha akatingishwa kichwa akimaanisha kwamba ame kubaliana na chochote atakacho kizungumza mke wake huyo ambaye hawajapata mapumziko ya faragha toka walipo funga ndoa yao kanisani na mapunziko yao yame angukia kwenye matatizo yanayo umiza mioyo yao.


ITAENDELEA


Haya sasa Julieth amepata mpango je ni mpango gani au ata muonyesha Jery nguvu ya genge kubwa la madawa ya kulevya analo limiliki kisiri sana kutoka mikoni mwa baba yake nabii Sanga? Usikose sehemu ya 132.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…