SIN 124
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
Magreth akaichomeka bastola yake kiunoni mwake na kuifunika na tisheti yake ndefu aliyo ivaa. Akatoka ndani hapo huku akisikilizia jinsi kengele ya mlangonimwake jinsi inavyo toa mlio, akafungua geti dogo na akajifanya akishangaa uwepo wa makamu wa raisi Madenge Jr.
“Muheshimiwa”
“Yaa je tuna ruhusiawa kuingia ndani?”
Makamu wa raisi Madenge Jr alizungumza huku akiwa amejawa na tanasamu pana sana usoni mwake. Magreth akawatazama walinzi hao kumi walio simama pembeni ya raisi Mtenzi na katika sekunde hizo chache akaweza kugundua uwezo wao pamoja na udhaifu wao na hata likitokea jambo lolote basi ata weza kulihimili.
ENDELEA
“Yaa karibu sana muheshimiwa. Hii ni big suprize kwangu”
“Ni kweli, sikuhitaji kuwafaamisha nikaona nije mwenyewe”
“Ume pajuaje hapa muheshimiwa?”
“Ahaa…niliagiza vijana wangu waweze kuwafwatilia. Kama muliweza kuja ikulu basi nami nikaona sio mbaya leo nije kuonana nanyi”
“Tuna shukuru sana, muheshimiwa karibu sana ndani”
Magreth alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Makamu wa raisi akaingia sebleni na walinzi wake wawili huku wengine wakibaki nje kuimarisha ulinzi.
“Shikamoo muheshimiwa”
Josephine alisalimia kwa heshima zote.
“Marahaba habari ya wewe?”
“Nina smshukuru Mungu ana saidia”
“Karibu ukae muheshimiwa”
“Nashukuru. Mume jitahidi, eneo hili ni zuri sana”
“Asante sana muheshimiwa. Je nikuandalie nini muheshimiwa?”
Magreth alizungumza kw afuraha iliyo mfanya Josephine naye kujiamini.
“Nime toka kula usiku huu, hivyo musi sumbuke sana. Ahaa Jose nime kuja kwanza kukushukuru kwa kuweza kutuonyesha ni wapi raisi Mtenzi alipo kuwa ame fukiwa na kile kifusi cha hoteli. Pili tume pata tatizo ambalo kwa kweli tuna amini kwamba wewe uta kuwa ni msaada mkubwa sana kwetu”
Makamu wa raisi alizungumza kwa sauti ya utaratibu na iliyo jaa hekima kubwa sana. Ukimtazama kwa haraka haraka una weza kusema ni mtu mwema na mwenye roho ya upendo. Ila sumu na tamaa inayo endelea kuchemka moyoni mwake kwa kweli ni jambo la hatari sana.
“Tatizo gani muheshimiwa?”
“Leo mchana raisi Mtenzi aliweza kuondolea hospitalini na watu ambao tuliweza kunyaka matikio yao kwenye cctv camera, ila kwa bahati mbaya hatukuweza kuona sura zao. Watu hao mmoja wao alikuwa ni mwanamke ambaye ana oneana ana uwezo mkubwa sana wa upambanaji na mtu wa pili ni mwanaume. Walimuondoa raisi Mtenzi hospitalini na hadi sasa hivi hatufahamu ni wapi walipo, pia nina imani kwamba ulikuwepo kwenye eneo la tukio na ulishuhudia jinsi mwanamke huyo alivyo kuwa ana wapiga wanajeshi wangu?”
“Ndio muheshimiwa na pia nili muadisia rafiki yangu juu ya jambo hilo”
“Kwa kweli, nina shinda hata hii taarifa kuitoa kwenye vyombo vya habari kwani watu wata niona kwamba sio muwajibikaji. Ila nilipo kaa sana na kutafakari, nika kumbuka kwamba upo wewe mwenye uwezo wa maono yajayo au yaliyopo. Basi kwa heshima zote, nina kuomba uweze kumuomba Mungu wako aweze kutuonyesha sehemu alipo raisi wetu mpendwa bwana Mtenzi”
Josephine akashusha pumzi huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Laiti kama ninge kuwa na uwezo wa kupambana basi ninge pambana na yule aliye muiba raisi pale hospitalini ila sikuwa na uwezo wa kupigana.”
“Ni kweli, na hata kwenye cctv camera niliweza kuona ni jinsi gani ulivyo kuwa una duwaa”
“Nita muomba mwenyezi Mungu na akinionyesha ni wapi alipo raisi Mtenzi basi nita kuambia muheshimiwa”
“Je huna hisia zozote za sehemu alipo?”
“Mmmm hapana muheshimiwa. Ila ngoja nisali kidogo”
Josephine akafumba macho yake kwa dakika moja nzima kisha akaafumbua.
“Nime pata jambo muheshimiwa”
“Jambo gani?”
“Kuna mtu alipanga kumuua raisi Mtenzi hivyo hapa malaika wa Mungu wame niambia kwamba ata kuja kuonakana akiwa na afya yake njema na ata rudi kuiongoza serikali yake kwani yey ndio chaguo sahihi la mwenyezi Mungu”
Makamu wa raisi mapigo yake ya moyo yakampasuka mithili ya mftuza lililo chomwa na pini. Mapigo yake ya moyo yakazidi kuchanganya, akahisi kijasho kina kwenda kumwagika, akatoa kitambaa chake na kujifuta usoni mwake.
“Je….je…je..je…huja onyesha huyo aliye taka kumua?”
“Mmmm acha niombe tena”
Josephine akafumba macho na kumfanya Magreth kumtazama makamu wa raisi jinsi anavyo pepesa pepesa macho kwani hapo ana hisi kwamba ana kwenda kutajwa yeye. Taratibu Josephine akafumbua macho yake na kumtazama makamu wa raisi.
“Nime onyeshwa muuaji”
“Ni..ni…nani?”
“Kuna daktari mmoja alipanga kumchoma sindano ya sumu raisi Mtenzi ila sijamfahamu kwa jina ila nikimuona basi nina weza kumtambua”
“Kweli!!?”
Makamu wa raisi alizungumza kwa mshangao huku mapigo yake ya moyo kidogo yakitulia taratibu.
“Ndio”
“Basi tuta hakikisha kwamba huyo daktari tuna mpata na ata eleza ni kwa nini alipanga kufanya hivyo. Je una weza kuona ni sehemu gani alipo raisi Mtenzi”
“Ndio nime onyeshwa”
Magreth moyo wake uka mstuka sana huku na akamtazama Josephine ambaye ana tambua kwamba janaga moyo wa kudanganya.
“Ni wapi?”
Makamu wa raisi aliuliza huku akijiweka sawa kwenye kiti chake.
“Yupo mkoani Morogoro, ila sijatambua ni sehemu ani ambayo yupo ila nina onyeshwa yupo katikati ya mashamba ya mpanga”
“Kwa hiyo yupo Morogoro?””
“Ndio ila sifahamu ni eneo gani?”
“Basi nina shukuru sana binti, acha nikatume vijana kuhakikisha wana kwenda kumtafuta. Morogoro ni eneo dogo sana hivyo tuna weza kulipata kwa muda mfupi tu”
“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi akaaga na akatoka ndani hapo, akaingia kwenye gari na kushusha pumzi.
“Vipi muheshimiwa?”
“Ilikuwa bado kidogo huyu msichana kunijua. Ila maono yake yame angukia kwa daktari”
“Duu hivi ana ona kweli?”
“Ndio, kwa maana ame juaje kama raisi alitaka kuuwawa. Alijuaje kama kuna dokta alipanga kumuu. Huyu binti anacho kifanya ni kitu cha uhakika”
“Duuu sasa tuna fanyaje?”
“Hakikisha kwamba dokta Masangi ana patikana kabla ya hili jambo halijakwenda vizuri na ameniambia kwamba raisi yupo mkoni Morogoro. Hivyo nina hitaji kuwasiliana na mkuu wa mkoa wa Morogoro aweze kuhakikisha ana tuma vijana kwenye kila sehemu yenye mashamba mkoni hapo ili kuhakikisha raisi ana patikana”
“Sawa mkuu”
Msafara huo ukaondoka nyumbani hapo kwa Magreth na kumfanya kupata amani kidogo. Akafunga geti lake kwa ndani na kurudi sebleni na kumkuta Josephine akiwa katika wasiwasi.
“Ita kuwjae akaenda Morogoro na akashindwa kumkuta?”
“Shauri yao. Kwanza ni muuaji, hapa nilipo kuwa nina mtazama kwenye macho yake niliweza kuona kabisa ana wasiwasi”
“Mmmm yaani nime ogopa sana bado nusu tu nimtaje yeye mwenyewe kwamba ndio muuaji”
“Duu. Ila ume tumia njia nzuri. Ila ina bidi kuimarisha ulinzi kwa raisi la sivyo hawa watu wana weza kurudi”
“Ni kweli je kuna mtu gani ambaye yupo serikalini una muamini?”
Magreth akashusha pumzi huku akimtazama Josephine, akatoa simu mfukoni mwake na kumpigia RPC Karata.
“Magreth habari yako”
“Salama kaka yangu upo wapo?”
“Nime rudi Dar es Salaam si una jua hali iliyo tokea”
“Sawa nina weza kukuona au ukaja nyumbani kwangu”
“Kuna tatizo?”
“Kuna jambo muhimu sana?”
“Ndio kuna jambo muhimu kaka yangu”
“Basi nina kuja si hapo Kigamboni?”
“Ndio”
“Basi dakika ishirini nita kuwa hapo kwa maana nipo kwenye patroo”
“Sawa kaka”
Magreth akakata simu, honi ya gari lake mlangoni ikamfanya atoke, akachungulia nje na kumuona Juma. Akafungua geti kubwa na akaingiza gari hilo ndani.
“Aisee barabara ina lete shinda sana”
“Pole hata sisi wenyewe tume ona. Ila gari halija leta shida?”
“Hii mashine boss sijapata shida yoyote njiani”
“Sawa”
Magreth akashusha mizogo yao na kuingiza ndani kwake. Josephine akagonga mlangoni mwa chumba alichopo dokta Masawe.
“Ni mimi”
Josephine alizungumza mara baada ya kuona dokta Masawe ana chelewa kufungua mlango huo. Taratibu Mlango wa chumba hicho ukafunguliwa.
“Vipi wame ondoka?”
“Ndio”
Dokta Masawe akashusha pumzi taratibu huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana. Dokta Masawe akatoka hadi sebleni na kuchungulia akamkuta Juma.
“Huyu ni nani?”
Dokta Masawe aliuliza huku akiwa amejwa na wasiwsi mkubwa snaa moyoni mwake.
“Huyu kijana wangu. Tafadhali nina kuomba usiwe na mashaka naye. Alafu Juma kun……..”
Magreth kabla ya kumalizia sentensi yake, akasikia honi mlangoni na akatoa na kwenda kufungua geti. Akamkuta RPC Karata akiwa ameongozana na vijana wake wanne.
“Muna weza kunisubiria”
“Sawa mkuu”
RPC Karataa akaongozana na Magreth na wakaingia ndani. Dokta Masawe akastuka mara baada ya kumuona RPC Karaka kwani wana fahamiana.
“Masawe ndugu yangu upo?”
“Nipo kaka”
“Kumbe una fahamiana na mdogo wangu”
“Ndio ndio”
“Kaka nime kuita hapa kwa jambo moja. Ila nina hitaji kufahamu mume fikia wapi katika kumtafuta raisi?”
“Bado ngoma droo. Hali ime kua sio hali ndani ya nchi”
“Je mume weza kufahamu sababu za yeye kutoweka?”
“Hapana, sijafahamu bado ila si unatambua kwamba nina fwata amri ya wakubwa wangu na wala hupaswi kuuliza sana”
“Sawa kaka yangu, kati ya binadamu ambao nina waamini naamini kwamba una tambua wewe ni mmoja wapo”
“Nashukuru kwa hilo Magreth.”
“Huyu ni dokta Masawe kama mulivyo fahamiana. Pia ni ndio daktaria anaye itazama afya ya raisi Mtenzi”
“Ana itazama kivipi?”
“Mimi ndio mtu niliye mtorosha raisi Mtenzi hospitalini.”
“Wewe!!?”
RPC Karata alizungumza kwa mshangao.
“Ndio”
“Wewe ndio ume wapiga wale wanajeshi?”
“Ndio na raisi yopo hapa”
“Kwa nini sasa ume mtorosha”
“Makamu wa raisi lisaa moja alikuwepo hapa. Ishu yake ilikuwa ni kuuliza ni wapi alipo raisi Mtenzi”
“Ana wauliza nyinyi kwa nini?”
“Ndugu yangu hapa Josephine ana uwezow a kuona maono ya sehemu alipo mtu yoyote anaye mkusudia na huyu ndio alitoa ripoti ya swala la milipuko inayo endelea na pia ndio alionyesha raisi sehemu alipo fukiwa.”
“Ahaa sasa hapo nime waelewa. Ehee kwa hiyo mume mueleza makamu wa riais kwamba raisi mupo naye?
“Hapana”
“Kwa nini sasa?”
“Kwa maana raisi yeye ndio ana husika katuka kutka kuyaondoa maisha ya raisi Mtenzi”
“NINI?”
“Ndio, ana husika na alimuagiza dokta Masawe ili amuue raisi Mtenzi na baada ya jaribio kushindikana, makamu wa raisi akatuma mlinzi wake ili kumua dokta Masawe”
“Mungu wangu, hii nchi sasa ina elekea wapi?”
“Ndio hivyo kaka yangu. Hapa ninavyo zungumza, Josephine ame wadanganya kwamba raisi Mtenzi yupo mkoani Morogoro na usishangae ikatolewa amri ya askari kuelekea mkoa wa Morogoro kumtafuta raisi Mtenzi”
RPC Karata akashusha pumzi kwani hayo anayo yasikia na jinsi anavyo mfahamu makamu wa raisi bwana Madenge Jr ni mtu mwema na ambaye hana matatizo na viongozi wa chini yake.
“Raisi yupo wapi?”
Magreth akatangulia na RPC Karata akamfwata kwa nyuma. Wakaingia katika chumba hicho na RPC Karata hakuamini kumuona raisi Mtenzi sehemu huyo. RPC Karata machozi yakaanza kumlenga lenga na kumfanya Magreth kujawa na mshangao kwani hajui ni kwa nini RPC Karata ametawaliwa na huzuni kubwa kama hiyo ikiwa yeye ni askari mkakamavu.
ITAENDELEA
Haya sasa, RPC Karata ame muona raisi Mtenzi kwa nini ame jawa na msisitizo, makamu wa raisi ame danganywa je ata weza kumpata raisi Mtenzi ili kukamilisha zumuni lake la kumuua kiongozi wake huyo? Usikose sehemu ya 125.