SIN 123
Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)
Age ……………………………………………………18+
Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188
ILIPOISHIA
“Moyo wako bado una hitaji kumuua raisi Mtenzi?”
“Hapana kwa kweli, siwezi kufanya jambo hilo kwenye maisha yangu.”
Dokta Masawe alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Magreth akampa ishara ya kusima na akatii. Wote watatu wakaondoka sebleni hapo na kuingia chumbani alichopo raisi Mtenzi. Macho yakamtoka dokta Masawe huku kwa mara kadhaa akimwatazama Josephine na Magreth usoni mwake.
“Nina kupa jukumu la kuhakikisha raisi Mtenzi ana pona endapo uta fanya ubabaishaji wowote, au akafa basi tambua kwamba na wewe nina kuua. Kama niliweza kuwapiga wanajeshi zaidi ya kumi na tano na nika mtoa raisi pale Muhimbili basi hakika kuitoa roho yako ni kitendo cha sekunde. Tumeelewana?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama dokta Masawe usoni mwake na akamfanya atingishe kichwa akimanisha kwamba ame muelewa vizuri sana.
ENDELEA
“Ila haya hali ya raisi sio salama ina weza kuleta shida”
“So una hitaji tumpeleke wapi ikiwa raisi ana hitaji kumuu”
Dokta Msangi akaka kimya huku akimtazama raisi Mtenzi aliye lala kitandani hapo huku hali yake ikiwa bado hajitambui kabisa.
“Sema tukuletee nini na nini ili kumuhudumia”
“Nikiwataji hamuto weza kuvifahamu. Nina omba muniletee kalamu na karatasi ili niwaandikie”
Josephine akatoka ndani hapo na baada ya sekunde kadhaa akarudi akiwa na kalamu na karatasi. Dokta Masawe akaorodhesha vitu vyote ambavyo ana hitaji katika kumuhudumia raisi Mtenzi.
“Vitu hivyo sio rahisi kuvipata madukani ni hadi muende kwenye hospitali kubwa kama Agakhan”
“Wao wame salimika na milipuko?”
“Yaa hawajaguswa hata kidogo nendeni pale kuna daktari mmoja ana itwa dokta Khan muambie kwamba nime agizwa na dokta Masawe hivi vitu nina uha kika ata kupatia”
Dokta Masawe alizungumza huku akimkabidhi karatasi hiyo Magreth.
“No ata kwenda Jose.”
“Sasa dokta kwa nini usimpigie kwa maana endapo nika mkuta hayupo ina kuwaje?”
“Simu yangu hapa sina, nina hisi ime angukia eneo la tukio pale tulipo shambuliwa”
Magreth akampapasa dokta Masawe na kweli hakuwa na simu yake mfukoni.
“Akikataa kunipatia?”
“Muambie ni muhimu sana na kama akihitaji kuzungumza nami basi una weza kuwasiliana na dada yako hapa na nina weza kuzungumza naye”
“Sawa. Mage nita tumia pikipiki?”
“Una weza kuiendesha?”
“Ndio, ila sio sana”
“Hivyo vitu nilivyo waagiza sio rahisi kubebwa na pikipiki, mukipata gari pickup kidogo ina weza kusaidia kubeba hivyo mizigo kwa maana ni kuna life mashine hapo kubwa itakayo weza kumsaidia raisi katika siku hizi”
“Hiyo gari ndogo hapo nje ina weza kujitahidi kubeba?”
“Hapana, ukienda kule una weza kuina”
“Basi hadi Juma arudi na gari Aud Q7 si ina beba?”
“Yaa”
Magreth akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Juma.
“Vipi?”
“Ndio nina fika hapa hotelini, funguoa ume iacha kwa nani?”
“Dada mmoja mrefu hii, ni mweupe kidogo”
“Okay nina muona ngoja nizungumze naye usikate simu”
“Sawa”
“Samahani dada, nina itwa Juma. Kuna funguo ya gari aina ya Aud q7 ime acha hapa?”
“Mmm una mtambua aliye iacha?”
“Ndio ni boss wangu”
“Ana muonekano gani?”
“Ni mwana dada mrefu, maji ya kunde na nimwembamba kiasi”
“Una weza kumpigia”
“Simu ipo hewani, una weza kuzungumza naye”
Juma alizungumza huku akimkabidhi mwana dada huyo simu.
“Haloo”
“Ni mimi, nime muagiza huyo ni kijana wangu, mpatie funguo”
“Sawa”
“Nashukuru”
Magreth alimsikia Juma akizungumza.
“Amenikabidhi”
“Una weza kufika Dar es Salaam saa ngapi?”
“Mmmm nita chukua kama masaa manne hadi matano kufika hapo nyumbani?”
“Sasa hivi ni saa mbili, okay jitahidi basi uwahi si una jua tuna mgonjwa hapa ndani?”
“Yaa natambua bosi”
“Sawa”
Magreth akakata simu hiyo.
“Hivi tatizo lake haswa ni nini?”
“Amekosa pumzi, na amevuta hewa chafu hivyo endapo hewa hivyo ita weza kutoka kwenye mapafu yake basi kidogo ana weza kuwa sawa.”
“Jose vipi mbona kama ume kosa raha galfa?”
“Hata mimi sielewi, ila nina hisi kuna ugeni uta kuja hapa nyumbani”
“Ugeni kutoka wapi?”
“Sifahamu, ila nina hisi kwamba kuna ugeni uta fika hapa”
Magreth na dokta Msangi wakatazamana kwenye nyuso zao na wakakosa kutambua ni mgeni gani ambaye ata fika nyumbani hapo.
***
“Dokta vipo hali ya mwanangu?”
Nabii Sanga aliuliza huku akiwa amejawa na simanzi.
“Tuna mshukuru Mungu ameweza kuzinduka kutoka kwenye kifo na tuta muhamisha wodi hii na kumpeleka katika wodi ya kwake peke yake”
“Ohoo asante Mungu”
“Pia mke wako amezinduka, sasa je tuwaweka katika wodi moja au tuwatenganishe”
“Wawekeni wodi moja”
“Sawa”
Daktari huyo akaingia katika chumba hicho cha ICU, akawaeleza manesi kumuandaa Julieth kwa ajili ya kumtoa katika chumba hicho cha ICU.
“Waziazi wangu wapo wapi?”
Julieth alimuuliza mmoja wa manesi hao.
“Baba yako yupo hapo nje ana kusubiria”
“Mama yangu je?”
“Naye yupo uta muona”
Walipo hakikisha wame kiandaa vizuri kitanda cha Julieth wakaanza kukisukuma ili kumtoa nje.
“Mume wnagu hali yake ina endeleje?”
“Bado ila naye muda si mrefu ata zinduka”
Julieth akamtazama Jery ambaye naye hadi sasa hivi hajitambui, kisha akwaruhusu manesi hao kumtoa katika chumba hicho. Nabii Sanga tabasamu pana likamtawala usoni mwake, taratibu akamkumbatia Julieth.
“Mama yupo wapi?”
“Yupo huku chumbani?”
Manesi wakamuingiza Magreth katika chumba alicho lazwa Mrs Sanga.
“Julieth”
Mrs Sang alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake.
“Mama”
“Bee mwanangu”
Mrs Sanga aliitikia huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Baba kaka wapo wapi?”
Nabii Sanga akamtazama mke wake ambaye kidogo akatingisha kichwa akimaanisha kwamba wasizungumze kitu chochote.
“Wame toka kidogo kuna mambo wana yashuhulikia”
“Sawa, kulitokea nini mbona tupo hospitalini?”
Nabii Sanga taratibu akashusha pumzi taratibu huku akimtazama Julieth usoni mwake.
“Mwanangu kuna moja ya shambulizi lilitokea kwenye ile hotel pale na kwa bahati mbaya mambo yame kuwa kama hivyo yalivyo kuwa je una kumbuka mara ya mwisho ulikuwa wapi?”
“Ndio, baba mke alikuja kutuita chumbani kwetu tukaingia kwenye lifti na baada ya hapo tukapata mtetemeko mkubwa na hatukujua kilicho endelea baada ya hapo. Je mume wajua walio fanya shambulizi hilo?”
“Ndio”
“Ni kina nani?”
“Al-Shabab”
“Al-Shabab!! Walikuwa wana tafuta nini kwenye harusi yetu?”
“Bado hatuja jua chanzo kamili, ila woa ndio walio husika”
“Ila baba ina bidi tufanye jambo juu ya hili. Hatuwezi kuacha hili swala lipite kirahisi hivi’
“Usijali mwanagu, kila jambo lipo chini ya uangalizi”
“Ungalizi gani baba. Watu walio tuvurugia shuhuli yetu haiwezekani kuwaacha, watumie wanachama wote email na waambie nahitaji kuonana nao kesho usiku”
Jlieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama baba yake usoni.
“Ila huja pona bado?”
“Baba, sijavunjika sehemu yoyote ya mwili wangu, ninacho kihitaji kwa sasa ni kukutana na wanachama wangu na hayo mengine muniachie mimi sawa”
“Nime kuelewa”
Nabii Sanga alijibu kwa upole kwani mwanaye Julieth amejawa na hasira mithili ya Simba jike aliye uliwa watoto wake.
***
“Muheshimiwa kila kitu kipo tayari tuna weza kuondoka sasa”
“Sawa”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr, akasimama na kuongozana na mlinzi wake huyo, wakaingia ndani ya gari na wakaondoka eneo hilo la ikulu huku wakiwa na walinzi kumi watano wakiwa gari ya mbele na watano wakiwa katika gari la nyuma.
“Muheshimiwa naweza kukuuliza swali?”
“Uliza”
“Kwa nini una kwenda kuonaan na yule msichana?”
“Kuna mambo nahitaji kumuuliza, naona ana jambo fulani ndani yake. Hivi alikufahamu yule binti ambaye ni rafiki yake?”
“Sidhani”
“Basi tukifika pale ina bidi ukae ndani ya gari sinto hitaji akuone ukiwa ume ambatana nami”
“Sawa muheshimiwa”
Gari hizo zikazidi kusonga mbele na wakafanikiwa kufika nyumbani kwa Magreth.
“Ni kina nani?”
Magreth alizungumza huku akitazama kwenye simu yake video zinazo rekodiwa kupitia cctv kamera alizo zifunga getini kwake.
“Kuna nini?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.
“Kuna gari tatu nyeusi zime simama hapo nje?”
Magreth alizungumza huku akimuonyesha Josephine video hizo.
“Mungu wangu!!”
Josepghine aliye shika simu hiyo alihamaki. Magreth akamsogele na kutazama video hiyo. Wakamuona makamu wa raisi Madenge Jr akishuka kwenye gari la katikati.
“Ame kuja kufanya nini?”
“Hata mimi sifahamu ame kuja kufanya nini?”
Magreth akakimbilia katika chumba alipo lazwa raisi Mtenzi na ndipo alipo dokta Masawe.
“Dokta kuna jambo lime tokea. Ila nakuhitaji ukae ndani ya chumba hichi na mgonjwa na mujifungie kwa ndani, sinto hitaji kukuona una toa pua yako nje. Sawa”
“Jambo gani?”
Magreth akamuonyesha dokta Masawe video hizo na kumfanya aanze kutetemeka mwili mzima.
“Ume nielewa lakini?”
“Ndio so ame kuja kufanyaje, au ame gundua kwamba nipo hapa na mgonjwa?”
“Nina imani kwamba hajajua chochote, ila kaa ndani hapa na usitoe”
“Sawa”
Magreth akatoka chumbani hapo na kwa haraka dokta Masawe akafunga chumba hicho kwa ndani. Magreth akamkuta Josephine akiwa ana haha sebleni hapo.
“Hei nahitaji utulie usionyeshe wasiwasi wa aina yoyote. Sawa”
“Sawa”
“Niangalie, endapo uta kuwa na wasiwasi basi tambua kwamba uwepo wa dokta Masawe pamoja na raisi Mtenzi uta julikana”
“Sawa”
Magreth akaichomeka bastola yake kiunoni mwake na kuifunika na tisheti yake ndefu aliyo ivaa. Akatoka ndani hapo huku akisikilizia jinsi kengele ya mlangonimwake jinsi inavyo toa mlio, akafungua geti dogo na akajifanya akishangaa uwepo wa makamu wa raisi Madenge Jr.
“Muheshimiwa”
“Yaa je tuna ruhusiawa kuingia ndani?”
Makamu wa raisi Madenge Jr alizungumza huku akiwa amejawa na tanasamu pana sana usoni mwake. Magreth akawatazama walinzi hao kumi walio simama pembeni ya raisi Mtenzi na katika sekunde hizo chache akaweza kugundua uwezo wao pamoja na udhaifu wao na hata likitokea jambo lolote basi ata weza kulihimili.
ITAENDELEA
Haya sasa, makamu wa raisin a walinzi wapo nyumbani kwa Magreth je wata fanikiwa kufahamu uwepo wa raisi Mtgenzi ambaye bado wana endelea kutafuta huku imani zao zikiamini kwamba mtu aliye mtorosha raisi Mtenzi ni mtu mbaya? Usikose sehemu ya 124.