Riwaya: SIN

Riwaya: SIN

SIN 118


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188







ILIPOISHIA


“Sihitaji umfikirie tena Magreth”
Jinsi Maimuna mara baada ya kuzungumza hivyo, akampulizia Evans pumzi ailiyo ingia hadi ndani ya moyo wake na kusabaisha chuki kubwa sana juu ya Magreth na hata mawazo yake mazuri yakabadilika na kuwa mabaya.
“Magreth ni adui yako nauna paswa kumuua yeye na yule rafiki yake”
Jini Maimuna alizidi kumpandikiza Evans chuki hadi akatamani kumuua Magreth wakati huo huo.
“Nita muua Magreth na rafiki yake sehemu yoyote nitakayo muona”
Evans alizungumz akwa msisitizo huku akimtazama jini Maimuna usoni mwake na kumfanya atabasamu kwa maana uwezo alio kuwa nao rafiki wa Magreth ni mkubwa sana na una weza kumkwamisha kwenye mipango yake mingi.





ENDELEA


“Bado wana jeshi wana endelea kufukua kisiki kwani hii ndio sehemu ya mwisho ambayo raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania bwana Chinas Mtenzi alikuwepo na familia yake katika harusi ya kijana wake.”
Evans na jini Maimuna wote walimsikiliza muandishi huyo wa habari anaye onekena kwenye luninga huku akionyesha jinsi wanajeshi wakeindelea kufanya jitihada katika kuhakikisha wana upate mwiliwa raisi Mtenzi.


“Yule si Mage na rafiki yake?”
Evans alizungumza huku macho yakiwa yame mtoka.


“Ndio, sija jua wana fanya nini pale”
“Twende basi”
“Ngoja kwanza hatuwezi kwenda Dar es Salaam usiku huu acha kupambazuke”
Jini Maimuna alizungumza kwa msisitizo na kumfanya Evans kukubaliana na kila jambo.


***


Jitihada zikazidi kuongezeka na wakafanikiwa kuikuta lifti lilyo fukikwa na kifusi hicho. Wakaanza wakaanza kumtoa raisi Mtenzi ambaye yupo kwenye hali mbaya sana, wakamtoa Julieth pamoja na mume wake kisha wakawafwatia walinzi huko wote wakiwa wamezimia. Kila mmoja akajikuta akimuamini Josephine kwani ndio mtu wa pekee aliye walekeza kwamba raisi Mtenzi ata kuwepo eneo hilo.


“Binti je wana familia wengine wapo hai?”
Makamu wa raisi alimuuliza Josephine huku akimtazama usoni mwake. Josephine akafumba macho yake huku Nakijaribu kumuomba Mungu kumuonyesha ni nani ambaye ame salimika katika jengo hilo.


“Vipi?”
Makamu wa raisi aliluliza mara baada ya Josephine kufumbua macho.
“Hakuna wote walio baki ni marehemu”
Makamu wa raisi akashusha pumzi huku akitazama jengo hilo la gorofa lililo vunjika vibaya sana.
“Muheshimiwa ina bidi kwa sasa uelekee ikulu.”
Mlinzi wa makamu wa raisi alizungumza.
“Ikulu haijapata madhara?”
“Hapana”
“Nahitaji kuondoaka na huyu binti”
Makamu wa raisi alizungumza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Mimi nime ongozana ndugu yangu muheshimiwa hivyo kama ni kwenda nahitaji twende wote”
“Hakuna shaka”
“Sisi tuna usafiri wa pikipiki”
Magreth alizungumza na makamu wa raisi. Magreth na Josephine wakapanda pikipiki na kuanza kuelekea ikulu huku raisi na wapambe wake wakipanda helicopter na kuelekea ikulu. Magreth na Josephine wakafika ikulu na kupokelewa na makamu wa raisi.
“Ahaa samahani muheshimiwa ninge penda kufahamu lengo la wewe kutuita hapa”
Josephine alimuuliza makamu wa raisi huku wakiwa wamekaa kwenye ofisi ya raisi Mtenzi.
“Nahitaji kufahamu raisi ata pona?”
“Ndio hato kufa”
“Ata kaa kitandani kwa muda gani?”
“Muda mfupi hawajapata majeraha ya kuwafanya wakae kitandani kwa kipindi kirefu”
“Je mke wake na wana familai wake wengine ime kuwaje?”
“Wote wame kufa”
Josephine alizungumza kwa kukiamini na kumfaya makamu wa raisi kuzidi kumuamini kwa kila jambo.
“Una weza ni wapi tunapo weza kuwapata wahusika wa kundi hili la kigaidi”
“Hilo ina nibidi nimuombe Mungu ili aweze kunionyesha”
“Basi nina kuomba ufanye hivyo. Hii ni namba yangu ya mawasiliano, chochote utakacho onyeshwa basi hakikisha kwamba una wasiliana na mimi”
Josephine akaipokea bussines card hiyo.
“Sawa muheshimiwa”


“Kwa sasa muna jishuhulisha na nini?”
“Nina mgahawa”
Magreth aliwahi kulijibu swali hilo huku akimtazama makamu wa raisi usoni.
“Basi nina shukuru kwa muda wenu”
“Asante nawe muheshimiwa”
Magreth na Josephine wakaondoka ikulu majira ya saa kumi na moja alfajiri na moja kwa moja wakaelekea kwenye nyumba ya Magreth iliyopo Kigamboni na kwa bahati nzuri mtaa wao hakuweza kupata madhara ya aina yoyote.


“Hili jambo Josephine siwezi kuliacha kilapita hivi hivi. Ina tupasa kuisaidia nchi yetu kwa kila jambo”
“Ni kweli ila watu ambao wana shuhulika na hili jambo kwao hawaogopi kabisa kufa. Kufa ni dhawabu kwa mwenyezi Mungu”
“Potelea pote ila ni heri kuwaua kuliko hichi walicho kifanya hapa Dar. Wewe mwenyewe una ona ni jinsi gani raisi wasio na hatia walivyo fariki”
“Mmmmm acha tuone huko mbeleni mambo yatakuwa vipi”
Hapakuwa na hata mmoja wao aliye patwa na usingizi, kwani hali walio iona kwa kweli ina wanyima usingizi.
***


Huduma zikazidi kuendelea kwa raisi Mtenzi, Jery, Julieth na walinzi wake wawili. Madaktari wa hospitali ya taifa ya Muhimbili wakazidi kujitahidi wana hakikisha kwamba wana wanaokoa maisha yao pamoja na wananchi wanao letwa hapo wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana. Nabii Sanga muda wote hakuweza kukaa kabisa kwani ana tamani hata kusikia sauti ya mwanaye Julieth kwa mara nyingine.


Majira ya saa mbili asubuhi wakatolewa katika vyumba vya matibabu na kuingizwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.
“Mwanangu hali yake ipo vipi dokta?”
Nabii Sanga alimuuliza daktari huyo.
“Wana endelea salama, ni jambo la kumuomba Mungu hali zao ziweze kurudi na kuwa fiti”
“Nashukuru dokta”
Nabii Sanga alizungumza huku akichungulia kwenye kioo cha dirishani jinsi Julieth anavyo wekewa mashine za kumsaidia kuhema vizuri. Mrs Sanga akafika hospitalini hapo na wakakumbatiana na mume wake hukua kilia sana
“Vipi watoto wetu wengine hawajapatikana?”
“Ndio mke wangu”
Nabii Sanga alijibu kwa upole na hakuhiji kumueleza mke wake kwamba wame fariki kwani ana weza kumsababishia mke wake huyo matatizo ya presha.
“Wamesemaje juu ya Julieth?”
“Ana endelea vizuri hapa tumuembe Mungu”
Tv iliyopo kwenye kordo hiyo inayo rusha matangazo mabalimbali ikaanza kuwafanya watu kadhaa walipo hapo kutulia kutazama video hiyo.


‘TUME LIPIZA KISASI CHA KARNE. TANZANIA ILITUSHAMBULIA KATIKA BANDARI YETU SASA HICHO WALICHO KIPATA NI HAKI YAO INAYO WASTAHILI.”


Video hiyo fupi ya mkuu wa kikundi cha Al-Shabab ikaishia hapo na kumfanya kila mtu aliye iona video hiyo kukasirishwa.


“Ina maana Al-Shabab ndio walio tushambulua hivi?”
Mrs Sanga alimuuliza mume wake.
“Ndio”
Nabii Sanga alijibu kwa ufupi kisha akaanza kutembea akitoka hapo na kuelekea nje huku mke wake akimfwata kwa nyuma. Nabii Sanga akatafuta namba ya vijana wake wakazi ambao wana fanya kazi za kijasusi.


“Ohoo tuna shukuru Mungu muheshimiwa upo salama”
“Nina imani kwamba mume weza kuona hiyo video iliyo tangazwa kwenye tv?”
“Ndio muheshimiwa ndio tume iona”
“Wame haribu harusi ya binti yangu na wame sababisha maafa ya vifo vya ndugu zangu na wana familia yangu. Ninacho kihitaji musambaratishe kikundi hicho ila namuhitaji kiongozi wao akiwa hai. Mume nielewa”
“Ndio muheshimiwa”
Nabii Sanga akakata simu huku akiwa amejawa na hasira na uchugu mwingi sana.
“Mume wangu una hisi wana weza kuifanya hiyo kazi?”
“Ndio”
“Ila wale ni drugs dealers. Una wapa majukumu magumu sana mume wangu. Hembu jaribu kulifikiria hilo mara mbili mume wangu”
“Sasa una taka mimi nifanye nini ikiwa wewe mwenyewe ume ona hili jambo lilivyo tuharibia kila kitu tulicho kuwa tume panga”
“Ndio nime ona ila mume wangu hii vita sio ya sisi peke yetu. Vita hii ni ya nchi nzima na lazima serikali ita fanya jambo kwenye hili. Hembu jaribu kuwaza hili”
Mrs Sanga alizungumza kwa msisitizo, akachukua simu ya mume wake na kumpigia kijana wake.


“Bory”
“Ndio madam”
“Musifanye chochote hadi pale nitakapo waambia. Ume nielewa?”
“Ndio, ila kwa ni nini ikiwa muheshimiwa ame toa amri?”
“Ame itoa akiwa na hasira. Hatuhitaji kuwapoteza na nyinyi pia”
“Sawa madam”
Mrs Sanga akakata simu na kuanza kuelekea ndani na kumfanya mume wake kumtazama kwa macho makali laiti kama ange jua kwamba ange jua wanaye wa kiume wame fariki basi asinge wazuia vijana hao.
***


“Muheshimiwa una uha kika hiyo video haito tuletea shida?”
Msaidi za karibu wa kiongozi cha Al-Shabab alizungumza huku akimtazama bosi wake ambaye ameituma video hiyo kwenye mitandao ya kijamii dakika kadhaa zilizo pita.


“Najua wata tutafuta ila kwa sasa ina tubisi kubadilisha makazi yetu”
“Una hitaji twende wapi?”
“Leo tuna elekea nchini Nigeria na tuta ungana na kundi la Boko haramu”
“Mmmmm muheshimiwa, ume kubali tuwe chini yao?”
“Ni kwa muda, hili sekeseke likiisha basi tuta hakikisha kwamba tuna rudi kwenye mamlaka yetu”
“Ila muheshimiwa tume jipalia makaa ya moto. Kuna nchi kama Marekani ni mshirika mzuri sana wa Tanzania na raisi wa Marekani ni siku kadhaa alikuwa nchini Tanzania. Huoni wata tuwinda”
“Hatuwezi kukamatwa. Niamini mimi, vijana wame maliza kufunga kila kitu?”
“Ndio mkuu”
“Ni muda wa kuondoka sasa”
Mkuu huyo wa kundi la Al-Shabab aliwamba vijana wake na safari ya kueleke nchini Nigeria kwenye kundi la Boko Haramu ikaanza huku ikiwa hiyo ndio shabaha yao ya mwisho kabisa katika kujificha ili kukimbia hili mikono ya usalama.
***


“Hili swala la vikundi vya kigaidi vya bara la Afrika sasa lime fikia pabaya sana. Japo sisi tupo mbali sana ila ina tupasa kuhakikisha tuna saidiana na ndugu zetu katika kuteketeza na kuvifuta kabisa vikundi kama Al-Shabab , Boko haramu na vikundi vingene vinavyo fanania na hivyo”
Raisi wa Marekani alizungumza na washauri wake.
“Ndio muheshimiwa, hilo ni wazo zuri sana. Je tuna anzia wapi ikiwa hadi sasa hivi serikali ya Tanzania haijatoa statement ya aina yoyote?”
“Tuwape muda, kwani raisi pia alikumbwa na shambulizi hilo.”
“Muheshimiwa una weza kuwasha tv”


Sekretari wa raisi wa Marekeni alizungumza akiingia ofisini hapo. Raisi akawasha tv iliyopo ofisini kwake hapo. Wakatazama makamu wa raisi wa nchi ya Tanzania akizungumza na waandishi wa habari.


“Ndugu zangu Watanzania. Ni majonzi makubwa sana ambayo kwa sasa tuna kabiliana nayo. Tume weza kufahamu adui yetu aliye sababisha, ndugu zetu, rafiki zetu, wazazi wetu na watoto wetu kufa vifo vya kinyama sana.”
“Ninacho kwenda kuwaahidi. Sisi kama serikali ya jamuhuri na Muungano wa Tanzania. Tuta kwenda kuhakikisha tuna lipa kwa haya yote yaliyo tokea. Tuta watafuta Al-Shabab iwe ni ardhini, majini, angani au nchi kavu nina wahakikishia kwamba tuta wapata. Tuta tumia nguvu na uwezo wote ambao tunao kuhakikisha tuna watawanyisha kundi lote la Al-Shabab.”
Makamu wa raisi alizungumza kwa msisitizo.


“Familia zote ambazo zime patwa na matatizo ya kufiwa na wapendwa wao au kuharibikiwa na rasilimali zao ikiwemo makazi yao ya kuishi. Serikali yangu ita hakikisha kwamba ina toa ushirikiano wa asilimia mia moja ili kuijenga Dar es Salaam mpya na Tanzania mpya. Mungu ibariki Tanzania na Mungu ibariki Afrika, asante kwa kunisikiliza”
Hotuba hiyo fupi ikaishia hapo.
“Mpigieni simu makamu wa raisi wa Tanzania nahitaji kufahamu hali ya rafiki yangu raisi Mtenzi”
“Sawa muheshimiwa”
Simu ikapigwa na sekretari. Ikapokelewa na sekretari wa Tanzania ambaye kwa haraka akaiunganisha simu hiyo na simu ya ofisi ya raisi ambayo kwa sasa makamu wa raisi ndio anaye iongoza.


“Muheshimiwa makamu wa raisi yupo hewani”
Raisi wa Marekani akachukua mkonga wa simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Habari yako makamu wa raisi?”
“Nina shukuru muheshimiwa”
“Nime toka kuona hotuba yako yako na waandishi wa habari sasa hivi. Mimi pamoja na wananchi wote wa Marekani tuna toa pole kwa nchi yako ya Tanzania”
“Nina shukuru sana muheshimiwa”
“Natambua kwa sasa ni kipindi kigumu ambacho muna pitia. Vipi hali ya rafiki yangu Mtenzi ina endeleaje?”
“Hali yake bado yupo ICU. Ila madaktari wame tuhakikishia kwamba ana weza kurusi kwenye hali yake hivi karibuni”
“Kama hali yake ipo mbaya sana nina kuomba aweze kuletwa nchini Marekani kwa matibabu zaidi. Tuta hakikisha kwamba tuna fanya kila liwezekanalo hali yake ina rudi na kuwa salama”
“Sawa muheshimiwa, nita kujulisha muda wowote kuanzia hivi sasa”
“Pia nahitaji kutoa msaada wa kijeshi. Nahitaji kutuma jeshi langu lije nchini kwako kuhakikisha wana toa msaada wa ujenzi wa majengo ya kisasa na afya kwa ujumla”
“Nina shukuru sana muheshimiwa na nina wakaribisha muda wowote ule”
“Sawa basi nita wasiliana nawe baada ya masaa mawili”
“Karibu sana muheshimiwa”
Raisi wa Marekeni akakata simu na kuwatazama washauri wake na akaachia tabasamu kwani kile alicho kuwa ana kihitaji kutoka Tanzania sasa kina kwenda kutimia.
ITAENDELEA


Haya sasa, ni kitu gani ambacho raisi wa Marekani ana kihitaji kutoka nchini Tanzania? Usikose sehemu ya 119.
 
SIN 119


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Kama hali yake ipo mbaya sana nina kuomba aweze kuletwa nchini Marekani kwa matibabu zaidi. Tuta hakikisha kwamba tuna fanya kila liwezekanalo hali yake ina rudi na kuwa salama”
“Sawa muheshimiwa, nita kujulisha muda wowote kuanzia hivi sasa”
“Pia nahitaji kutoa msaada wa kijeshi. Nahitaji kutuma jeshi langu lije nchini kwako kuhakikisha wana toa msaada wa ujenzi wa majengo ya kisasa na afya kwa ujumla”
“Nina shukuru sana muheshimiwa na nina wakaribisha muda wowote ule”
“Sawa basi nita wasiliana nawe baada ya masaa mawili”
“Karibu sana muheshimiwa”
Raisi wa Marekeni akakata simu na kuwatazama washauri wake na akaachia tabasamu kwani kile alicho kuwa ana kihitaji kutoka Tanzania sasa kina kwenda kutimia.


ENDELEA


“Nahitaji viongozi wote wa ngazi za juu wa muwaarifu juu ya kikao hichi cha dharura. Sawa”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Sekretari akatoka ndani hapo na kumuacha raisi na washauri wake.
“Tuna kwenda kujenga magorofa ya kisasa, ila kuna hadithina kubwa ipo chini ya ardhi ya Dar es Salaam. Hadhina hiyo ita tuongezea utajiri mara dufu na huu tulio nao kwa maana Watanzania wenyewe hawajui kama kuna mali nyingi sana zipo katika mji huo”
Raisi wa Marekani alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana, kwani ziara yake aliyo ifanya Tanzania miezi kadhaa ilikuwa ni kuchunguza juu ya hadhina hiyo na hakujua ni jinsi gani anaweza kumshawishi raisi Mtenzi katika kuitoa hiyo hadithina.


***


Kengele ya getini ikawafanya Magreth na Josephine kutazamana.
“Ni nani huyo?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth. Magreth akatoa simu yake mfukoni na kuangalia upande wa video za cctv kamera na akamuona Juma akiwa ame simama mlangoni hapo. Magreth kwa haraka akatoka nje na kufungua geti lake.


“Juma”
Magreth alizungumza kwa kuhamaki na akakumbatiana na Juma.
“Bosi upo salama?”
“Ndio, wewe je?”
“Nimepo salama, ila jengo la mgahawa wetu nalo lime angukaka”
Juma alitoa taarifa iliyo mstua kidogo Magreth.
“Ila kati ya wafanyakazi wetu hakua aliye poteza maisha?”
“Yaa wengi niliweza kuwadanganya na kwenda nao Bagamoyo hivyo tulikuwa salama japo wapo walio wapoteza ndugu zao”
“Ohoo Mungu wangu. Karibu ndani”
“Nashukuru”
Wakaingia hadi sebleni, Josephine akasalimiana na Juma huku wote wakiwa wamejawa na furaha kwa maana kila mmoja ana hisia za kimapenzi na mwenzake, ila wana ogopa kuambiana ukweli.
“Upo salama Juma”
“Ndio wewe je?”


“Mimi nipo salama kabisa. Ahaa jana niliwaona kwenye tv ndio nika hisi kwamba asubuhihi hii muna weza kuwa hapa”
“Ni kweli, tulikuwa katika hoteli ambayo raisi alifukiwa”
“Ahaaa sawa sawa”
“Juma uta kula nini?”
“Chochote tu bosi”
Magreth akanyanyuka na kuelekea jikoni na kuwaacha wawili hao ambao ana tambua kwamba wana penda. Ukimya ukatawala kati yao huku macho yao wote wakiwa wame yageuzia kwenye tv iliyopo sebleni hapo.
“Ahaa mgahawa wetu ume lipuliwa”
“Weee kweli?”
“Ndio”
“Poleni sana, ila si muliondoka kama tulivyo waambia?”
“Ndio”
“Duu maisha ni bora kuliko majengo”
“Ni kweli”
Magreth akarudi akiwa amebeba glasi tatu za juisi na kuziweka mezani.
“Japo ni asubuhi, ina bidi tupate juisi kidogo au kuna mtu ana hitaji chai hapa?”
“Hapana juisi ina tosha”
Juma alizungumza huku akipokea glasi hiyo ya juisi. Josephine akachukua glasi yake kitendo cha kuanza kuiepeleka glasi hiyo mdomoni mwake akajikuta mkono wake huo wa kulia ukitetemeka sana na glasi hiyo ikaponyoka na kuanguka chini na kuwashangaza Magreth na Juma.


“Vipi?”
Magreth alimuuliza Josephine. Josephine akafumba macho yake kwa haraka huku akiaanza kuonyeshwa kitu kingine ambacho kika mfanya astuke sana. Josephine akafumbua macho yake huku mapio yake ya moyo yakimuenda kasi sana hadi akajihisi maumivu.
“Kuna nini Josephine”
Juma aliuliza huku akiwa amejawa na mshangao.
“Raisi”
Kauli hiyo ika mstua sana Magreth.


“Raisi ame fanyaje?”
“Ina bidi tumsaidie raisi sasa hivi”
“Kwa nini?”
“Kuna mtu ame pangwa kumuua raisi”
Josephine alizungumza huku jasho likimtiririka usoni mwake na kuwafanya Magreth na Juma wote wakajawa na mshangao.


***


“Natambua hii kazi ninayo kupatia ni ngumu ila nina hitaji uweze kuifanya kikamilifu”
Makamu wa raisi alizungumza huku akimtazama mmoja wa madaktari wana muhudumia raisi Mtenzi.
“Kazi gani muheshimiwa?”
“Nahitaji umchome sindano ya sumu raisi Mtenzi ambayo ita muua taratibu ndani ya msaa sita na isitokee mtu yoyote kuweza kufahamu kwamba ame kufa kwa sindano hiyo ya sumu”
Daktari huyo akastuka sana, hakuamini kama makamu wa raisi bwana Madenge Jr ana weza kumuambia maneno kama hayo.


“Usistuke hii pia ita kuwa nafasi kwako kupanda cheo na kuwa daktari mkuu wa hospitali au uihitaji hiyo nafasi?”
“Na…itaka”
“Basi kazi hiyo hakikisha una ifanya leo. Ila nahitaji iwe siri yako na mimi tu. Ume nielewa?”
“Ndio muheshimiwa”
“Nime kuandalia milioni mia moja pamoja na kazi kukupandisha cheo. Ukishindwa basi kila kitu kina yayuka”
Dokta Masawe, akatingisha kichwa huku akiwa amejawa na tamaa ya pesa hizo ambazo kwenye maisha yake ya utendaji wa kazi haja wahi kufanikiwa kushika kiwango kikubwa kama hicho cha pesa.
“Sawa muheshimiwa nita ifanya ila nina kuomba ahadi iwe ya kweli”
“Nina imani kwamba una nifahamu vizuri si ndio?”
“Ndio”
“Basi mimi ni mtu wa kutimiza ahadi zangu. Fanya hivyo”
“Sawa”
“Kazi njema na kazi itakapo malizika basi hakikisha kwamba tuna onana uso kwa uso na usinipigie simu na kunieleza habari kama hizo”
“Sawa muheshimiwa”
Dokta Masawe akapena mkono na makamu wa raisi Madenge kisha akatoka ofisini hapo. Taratibu makamu wa raisi akanyanyuka na kuitazama ofisi hiyo ilivyo nzuri.


‘Siku zote nilikuwa nina tamani sana kukalia hichi kiti. Sasa huu ni wakati wangu, Mtenzi hapo ulipo fikia sinto ruhusu urudi tena duniani’


Dokta Masawe akaingia kwenye gari lake na kuondoka ikulu hapo huku akilini mwake akifikiria ni jinsi gani anavyo weza kuitekeleza kazi hiyo kwa maana raisi Mtenzi yupo chini ya uangalizi mkali sana wa jopo kubwa la madaktari wezake na mara kwa mara huwa wana ifwatilia afya ya raisi.


‘Ila nilazima niondoke na hichi kitita cha pesa. Nime fanya kazi miaka yote ila sija wahi kushika kiasi hicho kwa kumkupuo ni lazima nizishike sasa’


Dokta Msangi aliendelea kujifariji huku akipita kwenye barabara ambayo haijaadhirika na mashambulizi hayo ya mabomu.


***


“Ni nani huyo ambaye ame panga kumuua raisi?”
Magreth alizungumza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Sijajua na sijaonyeshwa ni nani, ila kuna mtu ame kusudia kabisa kumuua raisi Mtenzi.”
“Ohoo Mungu wangu ni nini hichi tena”
“Samahani bosi na Josephine. Ume juaje kama raisi ana taka kuuwawa?”
Juma aliuliza kwa maana hatambui kabisa uwezo wa Josephine.


“Nina uwezo wa kuona maono ya mambo yanayo taka kutokea kabla hata hayajatokea”
“Mmmmm!!”
“Anacho kizungumza Jose ni kweli, ana uwezo huo”


“Mage hatuna muda wa kutosha ina tupasa kwenda Muhimbili kumsaidia raisi”
“Sawa, ila ni lazima tuwe na plan nina imani kwamba raisi ana lindwa sana”
“Ndio ana lindwa, ila hatuna jinsi na hatujui ni nani ambaye ata muua”
Magreth akajikuta akikaa kwenye sofa huku akijaribu kutafakari ni jambo gani ambalo ana weza kulifanya kama ni kazi basi hiyo ina kwenda kuwa kazi ngumu sana. Magreth akatoa simu yake mfukoni na kuitafuta namba ya Levina, akampigia, ila kwa bahati mbaya akakuta simu ya Levina ikiwa haipo hewani. Akajaribu kupiga tena ila simu yake bado haipatikani.


‘Huyu naye amepatwa na nini?’


Magreth alizugumza huku akijaribu kumpigia simu Levina kwa mara ya tatu na majibu yakawa ni yake yale.
“Nina wazo”
Juma alizungumza na kuwafanya Josephine na Magreth kumtazama.
“Kama ni kumuokoa raisi ina bidi tutafute mavazi ya madaktari wa hospitali ya Muhimbili na tuhakikishe kwamba tuna mtoa ndani ya hospitali pasipo mtu yoyote kuweza kuona”
“Ni wazo zuri, ila nina fikiria ni jinsi gani ambavyo tuna kwenda kumtoa ingali wewe mwenyewe una jua hali hakisi iliyopo hivi sasa?”
“Mage sisi twendeni tuta jua huko huko”
Josephine alisisitizia na Magreth hakuwa na kipingamizi. Wakatoka ndani hapo na kuingia kwenye gari ndogo ya Juma ambayo ameinunua siku za hivi karibuni na wakaianza safari ya kuelekea hospitali ya Muhimbili.
***
“Wakija wale wezangu wawili uta wakabidhi funguo. Muda wetu wa chumba si bado haujaisha?”
“Ndio bado hauja isha”
“Basi uta wakabidhi funguo”
“Sawa”
Levina alizungumza na muhudumu huyo kisha akaondoka eneo la mapokezi huku akiburuza begi lake la matairi lenye nguo zake pamoja na vifaa vyake muhimu. Akaingiza begi hilo ndani ya gari lake, akazunguka upande wa dereva, akafungua mlango na kuingia ndani. Akatoa hati zake tatu za kusafiria ndani ya pochi yake, akaanza kuzipitia moja baada ya nyingine.


‘China pata nifaa’


Levina alizungumza kimoyo moyo kisha akawasha gari na kuanza safari ya kueleke katika kiwanja cha ndege KIA, huku simu yake ya mkononi akiwa ameizima na kuicha ndani ya chumba hicho cha hoteli. Kiwango cha pesa ambacho walishirikiana na wezake kukipata, ana amini kita mfanya kuishi maisha ya starehe hadi kufa kwake katika nchi hiyo ya china.


“Siwezi kuwa na watu ambao akili zao haziwazi yale ninayo yawaza mimi”
Levina alizungumza huku akizidisha mwendo kasi wa gari lake ili kuwahi kufika Moshi kabla ya mambo haya rafiki zake hao hawaja stukia juu ya wizi huo ambao ana ufanya.


***
“Mzee”
Daktari mmoja alimuita nabii Sanga na wakasogea pembeni na kumuacha mke wake aliye kaa kwenye kiti akiendlea kusali ili mwanaye Julieth aweze kupata nafuu.
“Ndio”
“Nina kuomba tuongozane kama hotajali”
“Tuna kwenda wapi?”
“Nahitaji kukuonyesha baadhi ya maiti ili uweze kutambua wana ndugu wako”
Nabii Sanga akamtazama mke wake ambaye ana onekana kukosa raha, kisha msogele mke wake.


“Mke wangu nina kuja sasa hivi”
“Una kwenda wapi?”
“Nazungumza na daktari mara moja”
“Sawa”
Nabii Sanga na dokta huyo wakaondoka eneo hilo na wakaongozana hadi kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Hakika ndani ya chumba hicho kume jaa maiti nyingi sana hadi baadhi zime lazwa sakafuni kwani watu walio fariki ni wengi na hadi sasa idadi yao haijaweza kufahamika.
“Kuna hizi maiti hapa zime letwa kutoka kwenye jengo la hoteli hivyo tuna kuomba uweze kuzitambua kama zina husia na wewe”
Daktari akafungua shuka la maita ya kwanza na kumfanya nabii Sanga kufumba macho yake kwani huyo aliye muona hapo ni mdogo wake wa tumbo moja ambaye ni wa kike.


“Nina mjua ni dada yangu”
Nabii Sanga alizungumza kwa kujikaza ila machozi yana mlanga lenga usoni mwake.”
Daktari akamuagiza muhudumu wa chumba hicho kuapachika kibao cha namba maiti huyo. Akafunua shuka la pili nabii Sanga akahisi moyo wake ukiraruriwa na kitu chenye ncha kali sana. Hakuamini kumuona mwanaye wa kwanza akiwa amelala eneo hilo huku kifua chake kikiwa ime fumuka na mbavu zote zime chomoza nje.
“Ni…ni…first born wangu”
Nabii Sanga alizungumza kwa uchungu sana na huku akishindwa kabisa kuyazuia machozi yake. Akafuniliwa maiti ya tatu na kumfanya nabii Sanga kushindwa kustahimiki kabisa na kuanza kuangua kilio kwa sauti kwani mwanaye wa pili wa kiume naye mwili wake ume pondeka pondeka vibaya na hapo alipo kiwili wili cha kuanzia kiunoni kuelekea miguuni hakipo kabisa.
ITAENDELEA


Haya sasa, nabii Sanga ame shuhudia maiti za vijaan wake, ambao siku iliyo pita tu walikuwa hai na wenye furaha sana, ila leo hii wapo kwenye hali kama hizo, ni kitu gani ata fana nabii Sanga kwa wasababishaji wa vifo hivyo vya wana familia yake? Usikose sehemu ya 120.
 
Duh! Hadi huruma jamani yani kama kweli vile. Hizi episode mbili nimezisoma yaan bas tu
 
SIN 120


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


“Nina mjua ni dada yangu”
Nabii Sanga alizungumza kwa kujikaza ila machozi yana mlanga lenga usoni mwake.”
Daktari akamuagiza muhudumu wa chumba hicho kuapachika kibao cha namba maiti huyo. Akafunua shuka la pili nabii Sanga akahisi moyo wake ukiraruriwa na kitu chenye ncha kali sana. Hakuamini kumuona mwanaye wa kwanza akiwa amelala eneo hilo huku kifua chake kikiwa ime fumuka na mbavu zote zime chomoza nje.
“Ni…ni…first born wangu”
Nabii Sanga alizungumza kwa uchungu sana na huku akishindwa kabisa kuyazuia machozi yake. Akafuniliwa maiti ya tatu na kumfanya nabii Sanga kushindwa kustahimiki kabisa na kuanza kuangua kilio kwa sauti kwani mwanaye wa pili wa kiume naye mwili wake ume pondeka pondeka vibaya na hapo alipo kiwili wili cha kuanzia kiunoni kuelekea miguuni hakipo kabisa.





ENDELEA


Daktari akataka kufunua shuka lililo funikia maiti nyingine ila nabii Sanga hakuwa na uvumilivu wa kuendelea kutazama. Akatoka nje hakufika mbali katika jengo hili akajikuta akiinama na kuanza kutapika huku akilia kwa uchungu sana.
“Mzee upo sawa”
Daktari alimuuliza nabii Sanga, jicho alilo tazamwa na nabii Sanga likawa ni jibu tosha kwamba hayupo sawa. Nabii Sanga akajjifuta mdomo wake huku yaswira za maiti za watoto wake wa kiume pamoja na dada yake zina endelea kumrudia mara nyingi kichwani mwake hadi akatamani kupiga makelele ila ana shindwa.


“Ndani paking za magari zime jaa”
Juma alizungumz ahuku aki simisha gari lake nje ya geti la hospitali ya Muhimbili. Akaanza kushuka Josephine huku akiangaza angaza eneo hilo la hospitalini. Honi iliyo pigwa nyuma ya gari lao ika mfanya Juma kutazama nyuma. Dokta Masawe akashusha kioo cha gari lake na kuchungulia nje.


“Binti mwambie dereva aingize gari ndani”
Dokta Masawe alimuambia Josephine na kumfanya Josephine kumtolea macho daktari huyo. Mapigo yake yakaanza kumuenda kasi sana.
“Binti vipi mbona una nitumbulia macho?”
Dokta Masawe alizungumza kwa ukali sana. Juma akashuka kwenye gari huku akiongozana na Magreth.
“Mzee ndani paking zime jaa”
“Sasa ndio usimamishe gari getini. Litoea bwana”
Dokta Masawe aliendelea kufoka.


“Juma litoe tu gari”


Magreth alizungumza. Juma akaingia ndani ya gari na kulitoa gari hilo, mlinzi akafungua geti hilo na taratibu akaliingia gari hilo ndani ya eneo hilo la hospitali. Askari wa ulinzi akamuelekeza Juma ni eneo gani anapo weza kulisimamisha gari lake.
“Mage Mage”
Josepghine aliita huku akiwa amejawa na wasiwasi mkubwa sana.


“Nini?”
“Nime Muangalia yule mzee mapigo yangu yana nienda kasi sana”
“Mzee gani?”
“Si yule aliye kuwa ana foka kwenye gari”
“Mmmm labda ni kutokana na kufoka kwake au kuna kitu umeweza kuona kwake?”
“Hapana, ila nime jikuta tu mapigo yangu ya moyo yakinienda kasi”
“Tuachane naye. Magreth alizungumza huku akisimama na kumtazama Juma anaye shuka ndani ya gari lake.
“Raisi yupo wapi?”
Juma aliuliza, Josephine akatazama majengo hayo kisha akanyooshea mkono jengo moja la gorofa. Wakaanza kutembea kuelekea katuka jengo hilo.


“Ulinzi ni mkali sana”
Juma alizungumza huku akitazama wanajeshi wanao katiza katiza katika jengo hilo.


“Musiogope”
Magreth alizungumza huku wakiingia ndani ya jengo hilo, wakaanza kupandisha ngazi kuelekea juu gorofani. Wakafika katika kordoa mbayo moja ya chumba ndipo alipo lazwa raisi Mtenzi, Julieth na Jery.


“Duu wapo wanajeshi arobaini”
Juma alizungumza huku akiwa amesha hesabu idadi ya wanajeshi walipo eneo hilo.


“Jose tuna kutegemea wewe?”
“Ngojeni kwanza….Yule si mrs Sanga?”
“Ndio”


Magreth alijibu huku wakimtazama mrs Sanga aliye kaa kwenye moja ya kiti huku akiwa amejiinamia.


“Nisubirini hapa”
Josephine alizungumza huku akielekea katika eneo alilo kaa mrs Sanga. Baadhi ya wanajeshi wana mfahamu Josephine kwani yeye ndio mtu wa pekee aliye waonyesha ni wapi alipo kuwa raisi.


“Shikamoo mama”


Josephine alizungumza kwa heshima zote huku akikaa pembeni ya mrs Sanga.
“Marahaba Jose. Ume salimika?”
“Ndio mama nipo hai vipi baba yupo wapi?”
“Ame ondoka hapa na daktari. Nashukuru nasikia kwamba kwa kupitia maono yako uliweza kusaidia kupatikana kwa raisi mwanangu na mkwe wangu”
“Sifa ni kwa Mungua ambaye yeye ndio amenipatia kipawa hichi. Si kwa uwezo wangu wa kibinadamu”
“Ni kweli, je katika lile jengo ukiachilia na hao walipo patikana je kuna watu wengine ambao wame salimika?”
Josephine akashusha pumzi huku akimtazama mrs Sanga kwani anavyo onekana hafahamu kama watoto wake wa kiume pamoja na ndugu zake wengine wamefariki dunia.
***


“Hali inayo endelea nchini Tanzania hivi sasa nina imani kila mmoja wenu ameweza kuiona”
Raisi wa Marekani alizungumza na viongozi wa ngazi za juu ikiwemo viongozi wa kijeshi. Huku wengine waliopo mbali wakifwatilia kikao hicho nyeti kwa njia ya video call.
“Kama unavyo fahamu ziara yangu ya mwisho nilikwenda nchini Tanzania. Tuna hitaji sana kuhakikisha tunawasaidia ndugu zetu kwa hali na mali”
“Muheshimiwa raisi, tuna tambua ni nguvu gani ambayo nchi yetu inayo. Ila hatuta weza kupelekea majeshi yetu tukaingia vita na vikundi vya ajabu alafu tuka shindwa kunufaika na chochote. Ina tupasa tunufaike na misaada yetu”
Makamu wa raisi alizungumza pointi iliyo mfanya raisi kutabasamu.


“Ni kweli, katika jiji la Dar es Salaa kuna hadihina kubwa ambayo ipo chini ya ardhi. Hadihina hiyo ina weza ika tufanya tuzidi kuwa matajiri mara dufu. Ndio maana tume ridhia katika kutoa majeshi pamoja na pesa za kutosha kwa kwenda kujenga jiji jipya la Dar es Salaam”
“Je wanajeshi wetu wata pambana na hivyo vikundi vya kigaidi?”
“Ndio, mission yetu ni kuifanya dunia kuwa sehemu salam”
“Muheshimiwa raisi, mimi nina pinga hilo. Kumbuka ni juzi tu tume weza kuwarudisha wanajeshi wetu kutoka Iraq na Telebani. Wanajshi wetu wameweza kufariki, wengine kupoteza viongo vyao, muheshmiwa raisi ifikie hatua wanajeshi wetu waweze kupumzika na familia zao.”
Mkuu wa jeshi alizungumza na kuwafanya viongozi wengine kuungamkono jambo hilo.


“Kama lengo ni kwenda na kujenga mji wao na kupata hadhina hiyo basi hatuwezi kubisha. Hilo la kupambana na Al-Shabab tafadhali tuwa pumzishe wana jeshi wetu”
“Sawa nime waelewa na wanejeshi wetu wata fanya kama tulivyo zungumza”
“Sawa mkuu”
Kikao hicho kikashia hapo na raisi akarudi ofisini kwake pamoja na wasaidizi wake ambao ni washauri wake.
“Mpigieni makamu wa raisi wa Tanzania”
“Sawa muheshimiwa”
Sekretari akapiga simu kwa makamu wa raisi wa Tanzania na simu hiyo ikapokelea.


***


“Ndio muheshimiwa raisi”
“Tume kaa na viongozi wezangu na tume fikia muafaka wa kutoa msaada wa wanajeshi wetu katika ujenzi wa Dar es Salaam na kuimarisha ulinzi wa jiji hilo hadi pale litakapo kamilika”
“Nashukuru sana muheshimiwa. Nimeitisha kikao na wakuu wa usalama kisha nita kufahamisha ni kiipi tulicho kubaliana na lini muweze kuja nchini kwentu”
“Sawa nina subiria makubaliano yako”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr akakta simu kisha akanyanyuka. Akaongozana na sekretari wake hadi kwenye ofisi ukumbi wa kikao. Akamkuta waziri mkuu pamoja na viongozi wengine wa ngazi za juu ambao siku ya jana ya shambulizi hawakuwepo jijini Dar es Salaam.


“Habari za muda huu”
“Salama muheshimiwa”
“Tume weza kupokea maombi mawili kwa marafiki zetu Marekeni. Ombi la kwaza kabisa ni kuleta vikosi vya vya jeshi katika kujenga mji wetu ambao ume haribika na kama munavyo fahamu, nchi yetu haina Malighafi za kutosha katika kulirudisha jiji letu liwe kama lilivyo kuwa awali. Pili wana hitaji raisi Mtenzi kupelekwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu zaidi. Je mume afikiana na hilo”
“Makamu wa raisi nina swali moja tu?”
“Uliza waziri mkuu”
“Ina kuwaje wana tuletea wana jeshi ikiwa nchi kama ya kwao ina makampuni mengi yenye ubunifu mkubwa wa ujengaji wa majengo”
“Wanajeshi wana jitolea, sidhani kama kuna kampuni ita kuwa tayari katuka kujenga bure ikiwa wata tumia vifaa vyao. Nina imani waziri mkuu nime kujibu vizuri”
“Ndio muheshimiwa”
“Jiji letu lina paswa kurudi katika ubora wake. Mukumbuke kwamba jiji hili ni jiji la kibiashara. Likiendelea kuwa kama magofu hakika uchumi wetu uta dhorota”
“Sawa muheshimiwa, je afya ya raisi ina endeleaje?”
“Bado yupo ICU hadi sasa hivi bado sijapata ripoti yoyote ya afya yake”
“Sawa muheshimiwa kwa upand wangu mimi sina pingamizi katika hilo”
“Hata mimi sina pingamizi”
Viongozi wote wakakubali kwamba wanajeshi wa Marekani waweza kufika nchini Tanzania kwa ajili ya kulijenga upya jiji la Dar es Salaam ambalo lime shambuliwa vibaya sana. Makamu wa raisi akajibu makubaliano hayo kwa barua pepe ili kutulia usisitizo katika makubaliano hayo ya kujengwa kwa jiji la Dar es Salaam.


***


“Niambie tu ukweli”
Mrs Sanga alizungumza kwa upole huku akimtazama Josephine usoni mwake. Kabla Josephine hajazungumza chochote nabii Sanga akafika eneo hilo huku macho yake yakiwa mekundu sana.
“Mume wangu vipi?”
Mrs Sanga alizungumza huku akisimama. Nabii Sanga akamkumbatia mke wake huku akimwagikwa na machozi hali iliyo mfanya mrs Sanga kujawa na wasiwasi mwingi sana.


“Mume wangu kuna nini?”
“Tumepoteza watoto wetu wa kiume”
Mrs Sanga taratibu akamuachia mume wake huku macho yakiwa yamemtoka. Mrs Sanga taratibu akakaa chini huku mapigo yake ya moyo yakimuenda kasi.
“Una…na….taka kuniambia wanangu wame kufa?”
Mrs Sanga alizungumza kwa wasiwasi.”
“Ndio mke wangu”
Mrs Sanga akashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio kwa sauti ya juu na kuwafanya wanajeshi wote kumtazama. Nabii Sanga hakuweza hata kumbembeleza mke wake kwani hilo walilo lipata ni pigo kubwa sana.


“Masikini wee”
Juma alizungumza huku wakimtazama mrs Sanga kwa mbali.
“Nahisi ata kuwa ame fiwa”
“Na nani?”
“Sija jua”
Josephine akarudi sehemu alipo simama Juma na Magreth.


“Vipi nani ame kufa?”
“Watoto wao wa kiume wame fariki”
“Duuu”
“Yaa sasa hapa ina bidi turudi kwenye plan yetu. Kumtoa raisi pale ni ngumu sana ila ina bidi mutafute makoti nyinyi wawili ili muweze kuingia katika chumba cha dokta”


Josephine alizungumza huku akiwatazama Juma na Magreth.
“Sawa”
“Mimi nita kuwepo pale kwa mrs Sanga na mume wake. Chumba kile ndipo eneo lilipo lazwa raisi Mtenzi, Jery na Julieth”
“Sawa”
Juma na Magreth wakaondoka eneo hilo na kuanza kutafuta chumba cha kuhifadhia makoti ya madaktari wote.
“Aisee mimi huwa siijui vizuri hii hospitali”
Magreth alizungumza huku wakiendelea kuangaza angaza kila eneo la gorofa hilo.
“Tuingie hapa”
Juma alizungumza huku akifungua mlango ulio andikwa dreasing room. Wakaingia ndani na kwa habahati nzuri wakakuta makoti ya madaktari ambayo yame fuliwa, yapo ndani ya chumba hicho.
“Ina bidi mimi nivalie kama nesi”
“Yaa ita pendeza”
Juma akachukua koti jeupe na kulivaa huku Magreth akivalia kiji gani ambacho ni kifupi ambacho kidogo kime acha maeneo ya mapaja yake kuwa wazi. Dokta Masawa akafungua droo ya ofisini kwake, akachukua chupa ndono ya sumu ambayo ina weza kumuua mtu ndani ya msaa matatu. Akakiingiza kichupa hicho katika mfuko wa koti lake, akatoka ofisini kwake na kuanza kuelekea katika chumba cha wagonjwa mahututi. Akafika nje ya chumba hicho na kumkuta mrs Sanga akiendelea kulia kwa uchungu sana.
“Ahh samahani sana, muna weza kumsogeza mama mbali na hapa kwa maaana hili eneo halitakiwi kuwa na kelele kabisa”
Dokta Masawe alizungumza, kitendo cha Josephine kumtazama mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda kasi, huku wasiwasi ume mjaa na kujikuta akimshangaa hadi dokta Msawe akahisi binti huyo ata kuwa ame hisi jambo ambalo wote wawili hawalifahamu.


ITAENDELEA


Haya sasa, Josephine na dokta Masawe wame kutana uso kwa uso je Josephine ata fahamu juu ya mpango mchafu alio nao dokta Msawe? Usikose sehemu ya 121.
 
SIN 121


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188





ILIPOISHIA


Juma akachukua koti jeupe na kulivaa huku Magreth akivalia kiji gani ambacho ni kifupi ambacho kidogo kime acha maeneo ya mapaja yake kuwa wazi. Dokta Masawa akafungua droo ya ofisini kwake, akachukua chupa ndono ya sumu ambayo ina weza kumuua mtu ndani ya msaa matatu. Akakiingiza kichupa hicho katika mfuko wa koti lake, akatoka ofisini kwake na kuanza kuelekea katika chumba cha wagonjwa mahututi. Akafika nje ya chumba hicho na kumkuta mrs Sanga akiendelea kulia kwa uchungu sana.
“Ahh samahani sana, muna weza kumsogeza mama mbali na hapa kwa maaana hili eneo halitakiwi kuwa na kelele kabisa”
Dokta Masawe alizungumza, kitendo cha Josephine kumtazama mapigo yake ya moyo yakaanza kumuenda kasi, huku wasiwasi ume mjaa na kujikuta akimshangaa hadi dokta Msawe akahisi binti huyo ata kuwa ame hisi jambo ambalo wote wawili hawalifahamu.





ENDELEA


“Samahani dokta”
Josephine alizungumza kwa kujiamini huku akimtazama dokta Masawe usoni mwake. Gafla mrs Sanga akaangukana kuzimia. Kitendo hicho kikamfanya dokta Masawe kugairi kuingia ndani hapo, akamkimbilia mrs Sanga na kuanza kumpatia huduma ya kwanza.


“Mke wangu amepatwa na nini?”
“Nabii Sanga alizungumza huku macho yakiwamekundu sana usoni mwake kwani tukio hilo lina zidi kumkosesha amani.


“Tulia nina muhudumia”
Dokta Masawe alizungumza na akawaomba wanajeshi wamsaidia kumbebea mrs Sanga na kumuingiza kwenye moja ya chumba.


“Mbona wanajeshi wame pungua?”
Juma aliuliza huku wakiwa wana tambea kwenye kordo hiyo ya kuelekea kwenye chumba cha ICU alipo lazwa raisi Mtenzi huku nyoso zao wakiwa wamezifunika na vitambaa vyeupe ambavyo wana vitumia madaktari wengi katika kipindi hicho ambacho hali ya kuwapokea wagonjwa ni wengi sana.


“Sifahamu kume tokea jambo gani”
Magreth alizungumza huku wakizidi kuwapita baadhi ya wanajeshi wanao imarisha ulinzi eneo hilo. Magreth akamkonyeza Josephine kisha wakaingia katika chumba hicho chenye wagonjwa watano, mmoja wapo akiwa ni raisi Mtenzi. Magreth akatembea hadi dirishani na kuchungulia..


“Hapa hatuwezi kumshusha ni mbali sana”
Magreth alizungumza huku akitazama umbali ulipo dirishani hapo.


“Sasa tuna fanya nini?”
“Ngoja kwanza”
Magreth alizungumza hukua kiangaza angaza kila sehemu ya chumba hicho. Akamsogelea raisi Mtenzi na kumuangalia jinsi mashine za kupimulia zinavyo msaidia katika kuhema.
“Nahitaji kusafisha njia na wewe huku nyuma hakikisha kwamba una toka na kitanda cha raisi”
“Una maanisha nini?”
Magreth akamtazama Juma kwa sekunde kadhaa, kisha akajifunga kitambaa hicho cha usoni ambacho kimebakisha macho pamoja na paji lake la uso. Akatoka kwenye kordo hiyo, akampiga mwanajeshi mmoja ngumi nzito ya shingoni mwake na kumfanya mwanayeshi huyo kuweweseka na akaanguka chini huku akiwa ana shika koo lake. Kitendo hicho kikawashangaza wanajeshi wengine pamoja na Josephine, mshangao huo wa wanajeshi, ukazidi kumpa Magreth kasi ya kuwashambulia kwa kuwapiga sehemu muhimu ambazo hawatoweza kusimama katika muda huo.


Juma akachungulia nje ya chumba hicho na akaona shuhulia ya Magreth inavyo kwenda na akajikuta akimshangaa bosi wake jinsi anavyo piga wanajeshi hao wambao ni wauame walio shiba kisawa sawa. Juma kwa haraka akaikweka kitanda alicho lazwa raisi Mtenzi sawa akaitoa mashine hiyo inayo msaidia kupumua, puani mwake. Akategesha saa yake dakika kumi kuhakikisha kwamba ndani ya dakika kumi hizo ana pata kifaa cha hewa ya oksijeni kitakacho msaidi raisi Mtenzi kupumua.


Juma akakisukuma kitanda hicho hadi mlangoni, akachungulia nje na kuwakuta wanajeshi wote wakiwa chini. Juma akakisukuma kitanda hicho na kwa haraka akaanza kukisukuma kwenye kordo hiyo huku wakisaidiana na Magreth anaye mwagikwa na jasho jingi. Wakamuingia raisi Mtenzi kwenye moja ya chumba wakamkalisha kwenye kiti cha magurudumu na kutoka ndani hapo huku wakiwa wame mfunika na koti jeupe mwili mzima ili watu wasimtambue.


“Ina tubidi tumtafutie mashine yoyote ya oksijeni pasipo kufanya hivyo ana weza kufa”
Juma alizungumza huku wakiendelea kuelekea nje. Wakakuta gari moja ya wagonjwa ikiwa ime washwa, huku dereva akiwa hayupo. Magreth akafungua mlango wa nyuma na wakakuta kitanda na kwa bahati nzuri gari hiyo ya wagonjwa ina kitanda ndani na ina mashine ndogo inayo weza kumsaidia mtu kupumua. Juma akamuingiza raisi Mtenzi ndani ya gari hilo, akamuwekea mashine hiyo na upumuaji wake ukaendelea kama kawaida. Magreth akawasha gari hilo na wakaondoka eneo hilo.


“Kume tokea nini?”
Dokta Masawe alizungumza huku akimtazama Josephine ambaye muda wote wa matukio hayo yaliyo endelea alibaki kuwa kama mshangaaji na hakutaka kujihusisha hata kidogo kuhofia kuhisiwa kwamba yeye naye ana husika kwenye jambo hilo.
“Aisee kume tokea nini?”
Dokta Masawe alimuuliza mwana jeshi mmoja aliye kaa chini huku akisikilizia maumivu hayo ya kupigwa na mtu ambaye hawamfahamu. Mwajeshi huyo alinyoosha mkono kwenye chumba cha ICU. Dokta Masawe kwa haraka akasimama na kukimbilia chumbani hapo. Macho yakamtoka mara baada ya kukuta kitanda cha raisi Mtenzi akiwa hayupo ndani hapo.
“Mungu wangu raisi hayupo”
Dokta Masawe alizungumza huku akikimbilia kipaza sauti akaminya batani na kuanza kuzungumza.


“Kume tokea tatizo, raisi ame toweka chumba cha ICU narudi raisi ametoweka chumba cha ICU. Wana jeshi wote na wana usalama wote tusaidiane katika kumtafuta”


Dokta Masawe mara baada ya kutoa taarifa hiyo akatoka ndani hapo huku akiwa amechanganyikiwa. Wanajeshi, askari pamoja na madaktari wakaanza msako wa kimtafuta raisi Mtenzi kika kona ya hospitali hiyo pasipo kufahamu kwamba tayari alisha tolewa hospitali hapo.


Josephine akaondoka eneo hilo, akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Magreth.


“Ndio”
“Mupo wapi?”
“Tumesha toka siku nyingi hapo”
“Muna kwenda wapi?”
“Tuta kuambia. Wewe chukua pikipiki uelekee nyumbani”
“Sawa”
Josephine akakata simu, akamkodisha muendesha pikipiki mmoja na wakaondoka eneo hilo huku akiwaacha wanajeshi, madaktari wakiwa katika hali ya wasiwasi mkubwa sana.


“Nilikuambia usinipigie simu ukimaliza kazi”
“Nalitambua hilo muheshimiwa. Hadi ninavyo zungumza hivi sasa, raisi ametowesha hapo hospitalini na watu wasio julikana”
“Nini?”
“Ndio ame toweshwa na watu wasio julikana”
“Ila kazi ume ifanya?”
“Sija ifanya muheshimiwa”
“Shitii mtafuteni hadi muumpate mume nielewa?”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr alizungumza kwa ukali sana kwani mpango wake ume kwenda vibaya. Dokta Masawe akakata simu huku woga ukiwa ume mtalawa sana.


***


“Boss tuna kwenda wapi?”
Juma alizungumza huku akimtazama raisi Mtezi aliye lala kimya.


“Tuna elekea nyumbani kwangu, ndio eneo salama zaidi”
“Kwako, hawato tufwata?”
“Hakuna ambaye ana weza kutufwata huko”
“Sawa”


Magreth akasimamisha gari hilo nje ya geti lake wakamshusha raisi Mtenzi na kumuingiza ndani, wakamlaza katika chumba cha Josephine wakamuweka mashine hiyo ya kupumulia waliyo ikuta ndani ya gari kisha Magreth akaliondoa gari hilo na kwenda kulitelekeza kwenye moja ya eneo ambalo lime pata majanga ya kuharibiwa na milipuko. Akarudi nyumbani kwake na kumkuta Josephine akiwa amesha rudi.


“Vipi hospitalini?”
“Wee kume chachamaa. Wanajeshi wana katiza kila sehemu, yule daktari woga ume mjaa alafu nina hisi yule doktaa na jambo la kufanya katika hili”
“Dokta yupi?”
“Yule mzee aliye kuwa ana foka pale getini kumbe ni dokta. Ila nilipo muona moyo wangu ulinienda kasi kama mara ya kwanza.”
“Kwa nini?”
“Sijui ikiwa watu wa kawaida ukiwaangalia nina kuwa sawa tu”
“Ina bidi tumpate yule dokta”
Magreth alizungumza kwa msisitizo.
“Tumpate wa nini?”
“Mashaka ya Levin….nani Josephine ni lazima kuna jambo yule dokta atakuwa ana lifahamu juu ya mpango wa raisi Mtenzi kuuwawa”
“Hata mimi nina hisi hivyo”
Josephine alitilia mkazo.
“Alafu huyu mjinga hadi sasa hivi hajatutafuta”
“Nani?”
Juma aliuliza.


“Levina”
Josephine akafumba macho yake kidogo na akajikuta akistuka.


“Nini?”
“Nime ona Levina ana panda ndege inayo kwenda Kenya”
“Ina maana ana toroka au?”
“Ndio ana toroka”
“Huyu mtoto chok** kweli vipi pesa zetu”
Magreth alizungumza kwa ukali huku akionekana kuchanganyikiwa kwani usaliti alio ufanya Levina una yeyusha ndoto zao zote za kumiliki pesa nyingi zime toweka.
Levina akajawa na tabasamu pana mara baada ya ndege aliyo ipanda kuanza kuiacha ardhi ya Tanzania taratibu. Ndege hiyo ilipo kaa sawa, akafungua mkanda wa siti yake na kujikalisha vizuri kwenye siti hiyo huku akiaanza kuwaza ni jinsi gani anavyo weza kuanza kuzitumia pesa hizo alizo wadhulumu na wezake.
Akafungua laptop yake na kuanza kutafuta hoteli ambazo zina patikana nchini China. Akapata hoteli moja ambayo watalii wengi wana fikizia, akafanya malipo ya awali akiamini kwamba ndani hato kaa muda mrefu nchini Nairobi.


“Tuna fanyaje sasa ili tumpate Levina?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Josephine usonimwake.


“Hatuna namna na pesa yetu ndio imesha kwenda hivyo”
“Duuu huyu mjinga haki ya Mungu niki mshika nita muu. Una namba ya pale hotelini?”
“Ndio”
Magreth akainakili namba hiyo kwa haraka ndani yas imu yake kisha akaipiga. Simu ikapokelewa.
“Nina itwa Magreth nilipangisha chumba kwenye hoteli yenu hapo majuzi”
“Ndio dada Magreth”
“Huyo rafiki yetu tuna jaribu kumpigia ila hatumpati hewani kuna tatizo lolote?”
“Ohoo rafiki yenu aliondoka asubuhi ya leo. Ila ame acha funguo”
“Basi nina kuja chumba chetu si kipo salama?”
“Ndio”
Magreth akakata simu, akaingia bafuni akaogo. Akabadilisha nguo haraka haraka kisha akanza safari ya kuelekea mkono Morogoro kwa kutumia pikipiki yake.
“Hivi huo uwezo wako una utolea wapi?”


Juma aliuliza huku akimtazama Josephine usoni mwake.
“Hahaa, ni kipawa ambacho mwenyezi Mungu alinipatia toka utotoni”
“Ahaa hicho kipawa chako hakiendani na swala la kukoko?”
“Yaa ila ina nibidi niwe sana karibu na Mungu kwani yeye ndio anayesha mambo yajayo na yanayo weza kutika sasa hivi”
“Ahaa sawa sawa”


Ukimya ukatawala katikati yao huku kila mmoja akimtazama mwenzake kwa macho ya aibu. Juma akashusha pumzi na taratibu akahamia kwenye sofa alilo kaa Josephine. Akamshika Josephine katika paja lake la kushoto na kumfanya Josephine kukaa kimya kidogo. Juma akazidi kujikaza japo mapigo yake ya moyo yana muenda kasi sana. Akasogeza lispi zake karibu na lispi za Josephine na akaanza kumnyonya na Josephine hakuwa na ujanja wa aina yoyote zaidi ya kutulia na kumruhusu Juma afanye anacho jisikia


***


Macho yakazidi kumtoka makamu wa raisi Madenge Jr. Video iliyo rekodi tukio zima lililo fanyika katika kordo ya kuelekea katika vyumba vya ICU. Mapigo waliyo kuwa wana pigwa wanajeshi walio kuwa wame imarisha ulinzi wa eneo hilo hakika yakazidi kumuacha mdomo wazi makamu wa raisi.
“Huyu hadi sasa hivi hamjamjua huyu mwanamke ni nani?”
Makamu wa raisi alimuuliza daktari mkuu wa hospitali ya taifa Muhimbili.
“Hapana muheshimiwa”
“Sio mfanyakazi wenu?”
“Hapana sio mfanyakazi wetu”
“Hakikiesheni huyu binti muna mpata.”
Makamu wa raisi alitoa maagizo hayo kwa mkuu wa kiosi cha wanajeshi walio kuwa wana mlinda raisi Mtenzi hospitalini hapo.
“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi na walinzi wake wakatoka ofisini hapo. Akamtazama dokta Msangi kisha akamuita kwa ishara, akasogea eneo ambalo halina mtu yoyote ambaye ana weza kuwaisikia chochote.
“Ulishindwaje kumdhuru?”
“Muheshimiwa nilichelewa kufika eneo la tukio. Samahani sana kwa hilo”
“Sasa funga kinywa chako na usijaribu kumueleza mtu yoyote juu ya hili swala na kuanzia hivi sasa mpango wa kumuua Mtenzi haupo tena mikononi mwako. Umenielewa?”
Makamuwa raisi alizungumza kwa suati ya chini ila iliyo jaa umsisitizo ndani yake.
“Ndio muheshimiwa”
Makamu wa raisi akaondoka eneo hilo na kumuacha dokta Masawe akiyang’ata meno yake kwa hasira kwani hakutarajia kama dili hilo lina weza kukatishwa ikiwa alisha anza kuipangia bajeti pesa hiyo.


ITAENDELEA


Haya sasa, dili la dokta Masawe lime katishwa je ata jitahidi kuhakikisha kwamba ana muua raisi Mtenzi ambaye hadi sasa hivi hajulikani ni wapi alipo? Usikose sehemu ya 122.
 
SIN 122


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188






ILIPOISHIA


“Sawa muheshimiwa”
Makamu wa raisi na walinzi wake wakatoka ofisini hapo. Akamtazama dokta Msangi kisha akamuita kwa ishara, akasogea eneo ambalo halina mtu yoyote ambaye ana weza kuwaisikia chochote.
“Ulishindwaje kumdhuru?”
“Muheshimiwa nilichelewa kufika eneo la tukio. Samahani sana kwa hilo”
“Sasa funga kinywa chako na usijaribu kumueleza mtu yoyote juu ya hili swala na kuanzia hivi sasa mpango wa kumuua Mtenzi haupo tena mikononi mwako. Umenielewa?”
Makamuwa raisi alizungumza kwa suati ya chini ila iliyo jaa umsisitizo ndani yake.
“Ndio muheshimiwa”
Makamu wa raisi akaondoka eneo hilo na kumuacha dokta Masawe akiyang’ata meno yake kwa hasira kwani hakutarajia kama dili hilo lina weza kukatishwa ikiwa alisha anza kuipangia bajeti pesa hiyo.





ENDELEA


“Hakikisha kwamba dokta huyu ana toweka duniani”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr alimuambia mlinzi wake huku akiingia ndani ya gari na kuondoka eneo hilo la hospitalini.


***


Magreth akafika mkoni Morogoro. Akaingia eneo la mapokezi na kukutana na muhudumu wa hoteli.


“Habari yako”
“Salama dada. Funguo yako hii hapa”
“Nashukuru”
Magreth akapandisha gorofani na kuingia kwenye chumba chao. Kila kitu chao akakikuta chumbani hapo kasoro vitu vya Levina. Magreth akakusanya vitu vyake na vitu vya Josephine, akaviingiza kwenye gari lake. Alipo hakikisha kwamba vitu vyao vyote vipo kwenye gari, akampigia simu Josephine.


“Vipi?”
“Nimefika n anime mkuta hayupo. Sasa naliancha hili gari hapa, hembu mpatie simu Juma”
“Ndio boss”
“Naacha gari langu hapa Morogoro, nina hitaji uje kulichukua”
“Ahhaa sawa bosi so nipande basi?”
“Hivi kuna mabasi yanago anza safari kutoka Dar?”
“Hapana, ina bidi nikapandie Mlandizi naona basi zote zinazo tokea mlandizi”
“Sawa fanya hivyo mimi nina rudi Dar es Salaam na fungua nina iacha mapokezi hapa”
“Sawa”
“Mage”
“Nina hitaji kwenda Muhimbili nita hitaji kumpeleleza yule dokta uliye na mashaka naye”
“Njoo kwanza nyumbani”
“Poa”
Magreth akamkabidhi muhudumu wa mapokezi funguo ya gari lake na akaianza safari ya kurudi jijini Dar es Salaam. Ikamchukua masaa manne kufika Dar es Salaam.


“Juma alisha ondoka?”
Magreth alimuuliza Josephine mara baada ya kuingia ndani.


“Ndio aliondoka muda ule ule ambao ulimpigia simu”
“Una onekana una furaha sana vipi?”


Swali la Magreth likamfanya Josephine kubaki akitabasamu.


“Au mume sha kubaliana nini?”
Magreth aliendelea kumtania Josephine.
“Bwana Mage”
“Haya bwana vipi raisi ame jitingisha hata kidogo?”
“Hapana ina bidi tumtafute daktari la sivyo ana weza kufa humu ndani”
“Sasa ni dokta gani ambaye ana weza kumfanyia matibabu?”
“Hata mimi sifahamu kwa kweli, au kumachukue yule dokta ninaye mtilia mashaka”
“Sasa kama una mtulia mashaka akija hapa si ina weza kuwa ni shida kwetu”
“Yule yule ndio anaye tufaa sisi”
“Mmmm sawa”
Magreth na Josephine wakakubaliana kumpata dokta Masawe. Magreth akaelekea hospitali ya Muhimbili na kwa bahati nzuri akafanikiwa kumuona dokta Masawe akiwa ana elekea kwenye maegesho ya magari. Mlinzi wa makamu wa raisi aliye kabidhiwa kazi ya kumuua dokta Masawe ili kuhakikisha siri ya kumuua raisi Mtenzi haivuji naye yupo eneo hilo la maegesho huku akiwa amevalia kofia nyeusi kuificha sura yake.


“Samahani dokta”
“Magreth alimuita dokta Masawe aliye shika fungu mkononi mwake kwa ajili ya kufungua mlango wa gari hilo.


“Bila samahani”
“Ahaa nina weza kupata dakika moj…..”
Gafla Magreth akamuangusha dokta Masawe chini na risasi iliyo kuwa imefyatuliwa kwa ajili ya kumpiga dokta Masawe, ikapiga kwenye kioo cha gari lake na kika pasuka. Tukio hilo Magreth alilifanya kwa uharaka sana kwani aliweza kumuona muuaji kwa kupitia kioo hicho ambacho kwa sasa kime funja.


“Nini?”
“Lala chini”
Magreth alizungumza huku akijaribu kuchungulia. Mlinzi wa makamu wa raisi bwana Madenge Jr akafyatua risasi mfululizo na uzuri ni kwamba bastola yake ameifunga kiwambo ambacho kina zuia sauti kutoka hivyo watu wengine walio eneo la hospitali wana endelea na shuhuli zao. Magreth akabundigika chini ya uvungu wa gari la pembeni aina ya Ford Range. Akatokea upande wa kijana huyo. Akamvuta mguu kijana huyo na akaanguka chini. Kabla Magreth hajafanya shambulizo lolote, kijana huyo akampiga teke la shingo na kumfanya Magreth kuona mawenge mawenge. Kijana huyo akasimama na kukimbia eneo hilo huku akimuacha dokta Masawe akimfwata Magreth aliye alal chini kwa ajili ya kumpa huduma ya kwanza.


“Una jisikiaje?”
Dokta Masawe alizungumza hukua kimuamsha Magreth.
“Kidogo nafuu”
“Wana taka kuniua washenzi hawa”


Dokta Masawe alizungumza kwa hasira.
“Kina nani?”
Dokta Masawe akaka kimya kwa maana bado hamuamini Magreth.


“Ahaa acha tu”
Dokta Masawe kalizunguka gari hilo, akatoa chupa ya maji na kumkabidhi Magreth kwa ajili ya kunawa uso wake kwani ume chafuka kidogo.
“Nashukuru binti”
“Usijali dokta. Nina mgonjwa wangu yupo nyumbani nina kuomba sana uweze kwenda kumfanyia matibabu”
“Ana sumbuliwa na nini?”
“Naye aliweza kuudhurika na mashambulizi ya mabomu.”
“Sasa kwa nini usimlete hospitalini”
“Nina imani hata wewe mwenyewe una ona jinsi gani ambavyo hospitali zilivyo jaa na wagonjwa wa kawaida huwa hawapati kipaumbele kama jinsi wenye huwezo na mali wanavyo pewa kipaumbele”
Dokta Masawe akamtazama kwa sekunde kadhaa Magreth.


“Alafu wewe kama nina kujua. Wewe si yule mmiliki wa ule mgahawa pake Kinondoni?”
“Ndio”
“Ahha mimi ni mteja wenu huwa mara kwa mara huwa nina pata chakula pale. Basi ingia kwenye gari langu twende”
“Mmmm kule ninapo ishi mimi kidogo barabara ime haribika. Kama ina wezekana tuondoke na pikipiki yangu”
Dokta Masawe akajishauri kwa sekunde kadhaa kisha akakubaliana na Magreth.


“Hivi ni wapi ume sema?”
“Kigomboni”
“Ahaa sawa sawa twende.”
Magreth na dokta Masawe wakaondoka eneo hilo huku matarajio ya Magreth yame kwenda kiwepesi sana tofauti na alivyo kuwa ana fikiria.


Nabii Sanga akamtazama mke wake aliye wekewa mashine na kumsaidia kupumua mstuko alio upata kwa kweli ni mkubwa sana. Taratibu nabii Sanga akasimama na kutoka ndani hapo, hapo ndipo akaanza kutambua kwamba utajiri wake hauwezi kufanya kila jambo kwani, laiti kama roho zinge kuwa zina nunuliwa basi ange wanunulia vijana wake roho ambazi zinge wafanya warudi tena duniani. Akaitoa simu yake mfukoni, akaingia upande wa video na kuanza kuangalia video za sherehe ya send off ya mwanaye. Furaha iliyo kuwa ime watawala watoto wake hao watatu hakika ika zidi kumfanya moyo wake kupatwa na maumivu ambayo kwenye maisha yake yote hakuwahi kuyapata.


Madaktari wanne wakiwa wana kimbia wakingia katika chumba cha ICU na kumfanya nabii Sanga kusimama na kuanza kuelekea karibu na chumba hicho.
“Huruhusiwi kuingia ndani hapa”
Daktari mmoja alizungumza huku akimtoa nabii Sanga ambaye ana mshuhudia Julieth akiwa ana jirushua rusha kitandani mithili ya mtu mwenye kifafa huku mashine inayo msiaida kupumua ikitoa mlio wa kuashiria uhatari wa hali ya mgojwa. Nabii Sanga akazidi kuchanganyikiwa kwa maana hatambui ni jambo gani ambalo lina msumbua mwanaye hadi hali hiyo kumtokea.


***


“Vipi ume fanikiwa?”
Makamu wa raisi aliuliza mara baada ya mlinzi wake huyo kuingia ofisini kwake.


“Ime shindikana”
“Ime shindikana vipi ikiwa ni kazi rahisi sana”
“Aliweza kusaidia na yule binti ambaye jana alikuwa na mwenzake aliye onyesha eneo ambalo raisi alifukiwa”
“Yule msichana mrefu, maji ya kunde”
“Ndio muheshimiwa”
“Ilikuwaje hadi amsaidie”
“Walikuwa wana zungumza eneo la maegesho ya magari na laiti kama ninge mkosa pale nisinge mpata tena”
“Bado huja nijibu alimsaidia vipi?”
“Alimkumba na akaanguka pembeni na risasi zilimkosa”
“Hakikisha kwamba una mpata huyu mpumbavu ume nielewa”
“Ndio muheshimiwa”
Makamu wa raisi alizungumza kwa hasira na kijana wake akatoka ndani hapo kwani kama ni mpango wake sasa una anaza kuwa mgumu.


“Je una fahamu ni sehemu gani ambapo yule binti ambaye ni mtabiri tabiri ana ishi?”
“Sifahamu ila tuna weza kupapata”
“Nitamfutie leo usiku nahitaji kwenda kuonana naye na kuzungumza naye”
“Sawa”
Mlinzi wake huyo akatoka ofisini hapo na baada ya dakika kumi akarudi akiwa ame tambua ni eneo ganiambalo Josephine ana ishi.


***
“Karibu sana dokta hapa ndio nyumbani”
Magreth alizungumza hukuwakishuka kwenye pikipiki. Dokta Masawe akamtazama kwa sekunde kadhaa Josephine na akamkumbuka.
“Wewe leo ulikuwepo pale hospitalini?”
“Ndio, nilikuwepo”
Dokta Masawe akamtazama Magreth aliye muonyeshea ishara ya kuingia ndani. Dokta Masawe taratibu akaanza kutembea kuelekea ndani huku akimuacha Josephine akifunga geti hilo vizuri. Wakamkaribisha sebleni hapo, Magreth akaingia ndani kwake, akachomeka bastola yake kiunoni na kurudi sebleni.
“Dokta ni nani aliye hitaji kukua na kwa nini alihitaji kukuua?”
Swali la Magreth kidogo likamstua dokta Masawe.
“Ahaa ni watu fulani ambao kidogo tumepisha kwenye mambo ya kibiashara kwa maana ukiachilia kazi yangu ya udaktari, pia nina nina fanya biashara.


“MUONGO”
Josephine alizungumza kwa kujiamini na kumfanya dokta Masawe kumshangaa.
“Samahani binti naamini hatujuani. Nime kuja hapa kwa ajili ya msaada alio utenda dada yako sijui nani yako, ila tambua kwamba sijakuja kuhojiwa”
Magreth akachomoa bastola yake na kumnyooshea dokta Masawe na kumfanya aanze kutetemeka mwili mzima.


“Ukweli wako ndio utakufanya uwe huru. Niambie ni kwa nini ulihitaji kuuwawa?”
Dokta Masawe akaanza kutetemeka mwili mzima.
“Ku…mb….e na nyinyi ni wale wale?”
“Dokta nijibu sina utani nita kifumua kichwa chako ukidanganya?”
“Ni…i…ima kamu wa raisi”
“Makamu wa raisi ana nini?”
“Yeye ndio ameagiza mtu kwa ajili ya kuniua mimi”
Josephine na Magreth wakajawa na mshangao mkubwa sana.


“Kwa nini ana hitaji kukuua?”
“Dokta Masawe macho yakamtoka huku akiogopa sana kutoa siri hiyo ambayo aliapa kwamba hato itoa.
“Zungumza dokta kumbuka kwamba maisha yako mimi ndio muamuzi sasa hivi. Ufe au uendelee kuishi”
“Ni…ni..ni kutokana na…na….”
“Na na na na nini?”
“Alihitaji nimchome sindano ya sumu raisi Mtenzi ili afe”
Macho yakawatoka Josephine na Magreth.
“Acha utani wewe”
Magreth alizungumza huku akitabasamu huku akihisi kwamba anacho kizungumza dokta Masawe ni uongo.


“Haki ya Mungu dini yangu ni mkristo. Makamu wa raisi aliniahidi kunipandisha cheo na kunipa milioni mia moja ikiwa kama malipo ya kazi hiyo”
Taratibu Magreth akaishusha bastola hiyo.


“Ndio maana nilipo kuwa nina kutazama mapigo yangu ya moyo yalikuwa yana kwenda kasi sana”
Josephine alizungumza huku akimtazama dokta Masawe.


“Moyo wako bado una hitaji kumuua raisi Mtenzi?”
“Hapana kwa kweli, siwezi kufanya jambo hilo kwenye maisha yangu.”
Dokta Masawe alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Magreth akampa ishara ya kusima na akatii. Wote watatu wakaondoka sebleni hapo na kuingia chumbani alichopo raisi Mtenzi. Macho yakamtoka dokta Masawe huku kwa mara kadhaa akimwatazama Josephine na Magreth usoni mwake.
“Nina kupa jukumu la kuhakikisha raisi Mtenzi ana pona endapo uta fanya ubabaishaji wowote, au akafa basi tambua kwamba na wewe nina kuua. Kama niliweza kuwapiga wanajeshi zaidi ya kumi na tano na nika mtoa raisi pale Muhimbili basi hakika kuitoa roho yako ni kitendo cha sekunde. Tumeelewana?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama dokta Masawe usoni mwake na akamfanya atingishe kichwa akimanisha kwamba ame muelewa vizuri sana.


ITAENDELEA


Haya sasa, dokta Masawe amepewa jukumu la kumuhudumia raisi Mtenzi je ata fanikiwa kumfanya arudi kwenye hali yake ya kawaida au tamaa ya milioni mia moja ita mrudia tena moyoni mwake? Usikose sehemu ya 123.
 
SIN 123


Muandishi…………………………………………….EDDAZARIA G.MSULWA(G.Authour)


Age ……………………………………………………18+


Simu………………………………………………… 0657072588(whatsapp) au 0768516188






ILIPOISHIA


“Moyo wako bado una hitaji kumuua raisi Mtenzi?”
“Hapana kwa kweli, siwezi kufanya jambo hilo kwenye maisha yangu.”
Dokta Masawe alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Magreth akampa ishara ya kusima na akatii. Wote watatu wakaondoka sebleni hapo na kuingia chumbani alichopo raisi Mtenzi. Macho yakamtoka dokta Masawe huku kwa mara kadhaa akimwatazama Josephine na Magreth usoni mwake.
“Nina kupa jukumu la kuhakikisha raisi Mtenzi ana pona endapo uta fanya ubabaishaji wowote, au akafa basi tambua kwamba na wewe nina kuua. Kama niliweza kuwapiga wanajeshi zaidi ya kumi na tano na nika mtoa raisi pale Muhimbili basi hakika kuitoa roho yako ni kitendo cha sekunde. Tumeelewana?”
Magreth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama dokta Masawe usoni mwake na akamfanya atingishe kichwa akimanisha kwamba ame muelewa vizuri sana.





ENDELEA


“Ila haya hali ya raisi sio salama ina weza kuleta shida”
“So una hitaji tumpeleke wapi ikiwa raisi ana hitaji kumuu”
Dokta Msangi akaka kimya huku akimtazama raisi Mtenzi aliye lala kitandani hapo huku hali yake ikiwa bado hajitambui kabisa.
“Sema tukuletee nini na nini ili kumuhudumia”


“Nikiwataji hamuto weza kuvifahamu. Nina omba muniletee kalamu na karatasi ili niwaandikie”
Josephine akatoka ndani hapo na baada ya sekunde kadhaa akarudi akiwa na kalamu na karatasi. Dokta Masawe akaorodhesha vitu vyote ambavyo ana hitaji katika kumuhudumia raisi Mtenzi.
“Vitu hivyo sio rahisi kuvipata madukani ni hadi muende kwenye hospitali kubwa kama Agakhan”
“Wao wame salimika na milipuko?”
“Yaa hawajaguswa hata kidogo nendeni pale kuna daktari mmoja ana itwa dokta Khan muambie kwamba nime agizwa na dokta Masawe hivi vitu nina uha kika ata kupatia”
Dokta Masawe alizungumza huku akimkabidhi karatasi hiyo Magreth.


“No ata kwenda Jose.”
“Sasa dokta kwa nini usimpigie kwa maana endapo nika mkuta hayupo ina kuwaje?”
“Simu yangu hapa sina, nina hisi ime angukia eneo la tukio pale tulipo shambuliwa”


Magreth akampapasa dokta Masawe na kweli hakuwa na simu yake mfukoni.
“Akikataa kunipatia?”
“Muambie ni muhimu sana na kama akihitaji kuzungumza nami basi una weza kuwasiliana na dada yako hapa na nina weza kuzungumza naye”
“Sawa. Mage nita tumia pikipiki?”
“Una weza kuiendesha?”
“Ndio, ila sio sana”
“Hivyo vitu nilivyo waagiza sio rahisi kubebwa na pikipiki, mukipata gari pickup kidogo ina weza kusaidia kubeba hivyo mizigo kwa maana ni kuna life mashine hapo kubwa itakayo weza kumsaidia raisi katika siku hizi”
“Hiyo gari ndogo hapo nje ina weza kujitahidi kubeba?”
“Hapana, ukienda kule una weza kuina”
“Basi hadi Juma arudi na gari Aud Q7 si ina beba?”
“Yaa”


Magreth akatoa simu yake mfukoni na kumpigia Juma.
“Vipi?”
“Ndio nina fika hapa hotelini, funguoa ume iacha kwa nani?”
“Dada mmoja mrefu hii, ni mweupe kidogo”
“Okay nina muona ngoja nizungumze naye usikate simu”
“Sawa”
“Samahani dada, nina itwa Juma. Kuna funguo ya gari aina ya Aud q7 ime acha hapa?”
“Mmm una mtambua aliye iacha?”
“Ndio ni boss wangu”
“Ana muonekano gani?”
“Ni mwana dada mrefu, maji ya kunde na nimwembamba kiasi”
“Una weza kumpigia”
“Simu ipo hewani, una weza kuzungumza naye”
Juma alizungumza huku akimkabidhi mwana dada huyo simu.


“Haloo”
“Ni mimi, nime muagiza huyo ni kijana wangu, mpatie funguo”
“Sawa”
“Nashukuru”
Magreth alimsikia Juma akizungumza.
“Amenikabidhi”
“Una weza kufika Dar es Salaam saa ngapi?”
“Mmmm nita chukua kama masaa manne hadi matano kufika hapo nyumbani?”
“Sasa hivi ni saa mbili, okay jitahidi basi uwahi si una jua tuna mgonjwa hapa ndani?”
“Yaa natambua bosi”
“Sawa”
Magreth akakata simu hiyo.
“Hivi tatizo lake haswa ni nini?”
“Amekosa pumzi, na amevuta hewa chafu hivyo endapo hewa hivyo ita weza kutoka kwenye mapafu yake basi kidogo ana weza kuwa sawa.”
“Jose vipi mbona kama ume kosa raha galfa?”
“Hata mimi sielewi, ila nina hisi kuna ugeni uta kuja hapa nyumbani”
“Ugeni kutoka wapi?”
“Sifahamu, ila nina hisi kwamba kuna ugeni uta fika hapa”
Magreth na dokta Msangi wakatazamana kwenye nyuso zao na wakakosa kutambua ni mgeni gani ambaye ata fika nyumbani hapo.
***


“Dokta vipo hali ya mwanangu?”
Nabii Sanga aliuliza huku akiwa amejawa na simanzi.
“Tuna mshukuru Mungu ameweza kuzinduka kutoka kwenye kifo na tuta muhamisha wodi hii na kumpeleka katika wodi ya kwake peke yake”
“Ohoo asante Mungu”
“Pia mke wako amezinduka, sasa je tuwaweka katika wodi moja au tuwatenganishe”
“Wawekeni wodi moja”
“Sawa”
Daktari huyo akaingia katika chumba hicho cha ICU, akawaeleza manesi kumuandaa Julieth kwa ajili ya kumtoa katika chumba hicho cha ICU.
“Waziazi wangu wapo wapi?”
Julieth alimuuliza mmoja wa manesi hao.
“Baba yako yupo hapo nje ana kusubiria”
“Mama yangu je?”
“Naye yupo uta muona”
Walipo hakikisha wame kiandaa vizuri kitanda cha Julieth wakaanza kukisukuma ili kumtoa nje.
“Mume wnagu hali yake ina endeleje?”
“Bado ila naye muda si mrefu ata zinduka”
Julieth akamtazama Jery ambaye naye hadi sasa hivi hajitambui, kisha akwaruhusu manesi hao kumtoa katika chumba hicho. Nabii Sanga tabasamu pana likamtawala usoni mwake, taratibu akamkumbatia Julieth.
“Mama yupo wapi?”
“Yupo huku chumbani?”
Manesi wakamuingiza Magreth katika chumba alicho lazwa Mrs Sanga.
“Julieth”
Mrs Sang alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake.


“Mama”
“Bee mwanangu”
Mrs Sanga aliitikia huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Baba kaka wapo wapi?”
Nabii Sanga akamtazama mke wake ambaye kidogo akatingisha kichwa akimaanisha kwamba wasizungumze kitu chochote.


“Wame toka kidogo kuna mambo wana yashuhulikia”
“Sawa, kulitokea nini mbona tupo hospitalini?”
Nabii Sanga taratibu akashusha pumzi taratibu huku akimtazama Julieth usoni mwake.


“Mwanangu kuna moja ya shambulizi lilitokea kwenye ile hotel pale na kwa bahati mbaya mambo yame kuwa kama hivyo yalivyo kuwa je una kumbuka mara ya mwisho ulikuwa wapi?”
“Ndio, baba mke alikuja kutuita chumbani kwetu tukaingia kwenye lifti na baada ya hapo tukapata mtetemeko mkubwa na hatukujua kilicho endelea baada ya hapo. Je mume wajua walio fanya shambulizi hilo?”
“Ndio”
“Ni kina nani?”
“Al-Shabab”
“Al-Shabab!! Walikuwa wana tafuta nini kwenye harusi yetu?”
“Bado hatuja jua chanzo kamili, ila woa ndio walio husika”
“Ila baba ina bidi tufanye jambo juu ya hili. Hatuwezi kuacha hili swala lipite kirahisi hivi’
“Usijali mwanagu, kila jambo lipo chini ya uangalizi”
“Ungalizi gani baba. Watu walio tuvurugia shuhuli yetu haiwezekani kuwaacha, watumie wanachama wote email na waambie nahitaji kuonana nao kesho usiku”
Jlieth alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama baba yake usoni.
“Ila huja pona bado?”
“Baba, sijavunjika sehemu yoyote ya mwili wangu, ninacho kihitaji kwa sasa ni kukutana na wanachama wangu na hayo mengine muniachie mimi sawa”
“Nime kuelewa”
Nabii Sanga alijibu kwa upole kwani mwanaye Julieth amejawa na hasira mithili ya Simba jike aliye uliwa watoto wake.


***
“Muheshimiwa kila kitu kipo tayari tuna weza kuondoka sasa”
“Sawa”
Makamu wa raisi bwana Madenge Jr, akasimama na kuongozana na mlinzi wake huyo, wakaingia ndani ya gari na wakaondoka eneo hilo la ikulu huku wakiwa na walinzi kumi watano wakiwa gari ya mbele na watano wakiwa katika gari la nyuma.
“Muheshimiwa naweza kukuuliza swali?”
“Uliza”
“Kwa nini una kwenda kuonaan na yule msichana?”
“Kuna mambo nahitaji kumuuliza, naona ana jambo fulani ndani yake. Hivi alikufahamu yule binti ambaye ni rafiki yake?”
“Sidhani”
“Basi tukifika pale ina bidi ukae ndani ya gari sinto hitaji akuone ukiwa ume ambatana nami”
“Sawa muheshimiwa”
Gari hizo zikazidi kusonga mbele na wakafanikiwa kufika nyumbani kwa Magreth.
“Ni kina nani?”
Magreth alizungumza huku akitazama kwenye simu yake video zinazo rekodiwa kupitia cctv kamera alizo zifunga getini kwake.


“Kuna nini?”
Josephine aliuliza huku akimtazama Magreth usoni mwake.


“Kuna gari tatu nyeusi zime simama hapo nje?”
Magreth alizungumza huku akimuonyesha Josephine video hizo.
“Mungu wangu!!”
Josepghine aliye shika simu hiyo alihamaki. Magreth akamsogele na kutazama video hiyo. Wakamuona makamu wa raisi Madenge Jr akishuka kwenye gari la katikati.


“Ame kuja kufanya nini?”
“Hata mimi sifahamu ame kuja kufanya nini?”
Magreth akakimbilia katika chumba alipo lazwa raisi Mtenzi na ndipo alipo dokta Masawe.


“Dokta kuna jambo lime tokea. Ila nakuhitaji ukae ndani ya chumba hichi na mgonjwa na mujifungie kwa ndani, sinto hitaji kukuona una toa pua yako nje. Sawa”
“Jambo gani?”
Magreth akamuonyesha dokta Masawe video hizo na kumfanya aanze kutetemeka mwili mzima.
“Ume nielewa lakini?”
“Ndio so ame kuja kufanyaje, au ame gundua kwamba nipo hapa na mgonjwa?”
“Nina imani kwamba hajajua chochote, ila kaa ndani hapa na usitoe”
“Sawa”
Magreth akatoka chumbani hapo na kwa haraka dokta Masawe akafunga chumba hicho kwa ndani. Magreth akamkuta Josephine akiwa ana haha sebleni hapo.
“Hei nahitaji utulie usionyeshe wasiwasi wa aina yoyote. Sawa”
“Sawa”
“Niangalie, endapo uta kuwa na wasiwasi basi tambua kwamba uwepo wa dokta Masawe pamoja na raisi Mtenzi uta julikana”
“Sawa”
Magreth akaichomeka bastola yake kiunoni mwake na kuifunika na tisheti yake ndefu aliyo ivaa. Akatoka ndani hapo huku akisikilizia jinsi kengele ya mlangonimwake jinsi inavyo toa mlio, akafungua geti dogo na akajifanya akishangaa uwepo wa makamu wa raisi Madenge Jr.
“Muheshimiwa”
“Yaa je tuna ruhusiawa kuingia ndani?”


Makamu wa raisi Madenge Jr alizungumza huku akiwa amejawa na tanasamu pana sana usoni mwake. Magreth akawatazama walinzi hao kumi walio simama pembeni ya raisi Mtenzi na katika sekunde hizo chache akaweza kugundua uwezo wao pamoja na udhaifu wao na hata likitokea jambo lolote basi ata weza kulihimili.


ITAENDELEA


Haya sasa, makamu wa raisin a walinzi wapo nyumbani kwa Magreth je wata fanikiwa kufahamu uwepo wa raisi Mtgenzi ambaye bado wana endelea kutafuta huku imani zao zikiamini kwamba mtu aliye mtorosha raisi Mtenzi ni mtu mbaya? Usikose sehemu ya 124.
 
Back
Top Bottom