Riwaya ya Kijasusi Mabaduni wa serikali

Riwaya ya Kijasusi Mabaduni wa serikali

The time is now!!!!
MABADUNI WA SERIKALI 5.

Saa nane, katikati ya usiku mnene wenye giza totoro, kuna gari nyeusi ilikuwa inaondoka katika geti la makao makuu ya Jeshi chini ya ulinzi mkali. Mbele ikitanguliwa na gari moja nyeusi aina ya Toyota Hilux Surf SSR-KD-KZN185W.

Vioo vyake vilikuwa vimefungwa na waliokuwemo ndani hawakuonekana sura zao kutokana na tinted zilizowekwa kwenye vioo hivi. Nyuma pia kulikuwa na gari ya aina ilele kama iliyopo mbele.

Gari zote tatu zilitoka eneo hili la makao makuu na kuchanja mbuga kuipita misitu kadhaa iliyokuwemo ndani ya kambi hii kubwa. Kwenye kila kizuizi ni kitambulisho tu ndio kilikuwa kikitolewa na dereva wa gari ya mbele, kisha walinzi walikuwa wakianguka saluti za kutosha na kuzipisha zipite hii ilionesha kuwa waliokuwemo hawakuwa watu wepesi bali watu wenye kilo zao mabegani.

Safari iliendelea mpaka walipokamata barabara ya Haed Road. Hii ni barabara iliyokuwa inatoka mjini Homa bay kuelekea Kaskazini mwa Songomo, lakini pia ilikuwa inapitiliza moja kwa moja kwenda nchini Jotokali kupitia mpaka wa Kabiti.

Ikiwa yapata saa kumi na robo usiku waliukaribia mpaka wa kabiti na sasa ilikuwa ni kama mita kumi hivi kulifikia Zuio la mpaka wa Kabiti, mara maaskari wenye sare za Jeshi la Songomo waliwasha tochi zenye mwanga mkali kuzielekea hizi gari ilikuwa ni dalili ya kuwa wasimame na wasisogee hatua zaidi.

Walinzi wa eneo hili walifahamika kwa umakini wao na uadilifu mkubwa waliokuwa nao wasingemruhusu mtu yeyote yule kupita bila vielelezo vilivyostahili.

Kuonesha kuwa walikuwa wanaijua kazi yao hawakuikagua gari ya mbele bali waliilenga ile ya katikati na kutaka waikague. Dereva wa ile gari hakushusha vioo wala kujitikisa.

Walinzi hawa ambao wengi wao walikuwa na insignia za First Lieutenant na Colonel wakiwa wamebeba silaha zao nzito mikononi mwao, walizidi kuonyesha ishara ya kuikagua ile gari kitendo kilichomfanya mtu mmoja kushuka kutoka kwenye ile gari ya mbele na kuja ili aongee nao.

Mtu huyu aliyeshuka alikuwa na Insignia ya Generali wa nne wa nyota moja( Brigedia General) alizipiga hatua kuwaelekea walinzi hawa akiwa kamlenga Colonel Barode.

Baada ya kumfikia, Colonel Barode alitoa heshima kwa kuanguka saluti lakini akamuonesha ishara ya kidole Brigedia General kuwa akae pembeni asiingilie utaratibu wa kazi wao wako katika majukumu yao

General alibaki akimuangalia Colonel bila kuongea chochote maana ni kweli Colonel alikuwa kwenye msitari wake wa kazi.

Baada yay a zuio hili lililoleta mtafaruku kwa takribani dakika ishirini ndipo mtu mmoja alishuka kutoka kwenye hii gari ya katikati. Mtu huyu alikuwa na sare za jeshi begani ilionesha ni cheo cha Major General.

Macho yake yalibeba umakini na mamlaka ndani yake alisimama na kuongea na Colonel kwa dakika kadhaa kwa sauti ya chini sana.

Akimsihi Colonel aruke msitari kwenye kazi yake. Colonel alikataa kata kata maana alijua kuwa kama sio kesho basi hata huko mbeleni jambo hili linaweza kurudi kumuwinda tu.

Baada ya Colonel na vijana wake kuonesha msimamo ilibidi sasa nguvu itumike na hapa ndipo vioo vya zile gari mbili vilishushwa yaani ya mbele na ya nyuma kasoro ile ya katikati ambayo bila shaka ndimo alikuwamo General Floyd Balehl.

Baada ya vioo kushushwa tu mitutu ya bunduki ilikuwa ikiwatazama Colonel na wenzake.Ndani ya gari hizi walikaa watu wa kazi tu wakiwa na tisheti nyeusi zenye mabawa vifuani na kofia nyeusi za jeshi.

Hawa ni Songomo Military special task Takers.

Kijeshi unapotamka neon “Special task” wajuvi wanajua unamaanisha nini.

Hawa ni watu wa majukumu ya ajabu na uwezo wao ni kitu kingine kabisa.

Colonel na wenzake walitambua ni kitu gani kinafuata mbele yao lakini kiapo kilisimama kwenye damu. Walijua fika kuwa wangeuawa lakini hawakutaka kuuacha msitari wa kazi maana waliapa kutouruka msitari huu hata kwa gharama ya maisha yao.

Kuna usemi kuwa kila mtu ana bei yake, lakini sio kwa Colonel Barode. Huyu mtu ni wa aina yake na masalia ya watu hawa yamebaki kwa uchache sana hapa ulimwenguni.

Amini kuwa kuna watu huwezi kuwanunua hata iweje na kadri utakavyozidi kumshawishi ndivyo utakavyozidi kumsukuma mbali zaidi na uwanja wa mapatano.

Colonel na wenzake nao walikuwa washajiandaa na silaha zao nzito na sasa ni mitutu ya bunduki walikuwa wameelekezeana.

Wakiwa wanajiandaa kutoana uhai, ndipo kwa mbele lilionekana kutua chopa jeusi lenye maandishi makubwa JISA.

Kwenye chopa alishuka mtaalamu Malone akiwa ameambatana na Team Leader wa PSU pamoja na Mwandishi Golo Zumba na hapa ndipo kalamu yangu ikang’amua kuwa kumbe Team Leader na Golo Zumba nao ni MABADUNI WA SERIKALI.mhh Ogopa sana.

Wakiwa ndani ya sare nyeusi zinazotumiwa na JISA walizisogelea zile gari ambapo baada ya kufika, Malone alizungumza na Colonel kuwa waachiwe lile jukumu hivyo Colonel na wenzake warudi kwenye eneo lao la kazi.

Colonel Barode alishusha pumzi baada ya kusikia hivyo japo hakuwa na uhakika wa hawa watu watatu kuwadhibiti hawa makamanda wa jeshi.

Colonel aliona ahueni maana asikwambie mtu kutazamana na mlango wa mauti sio kitu kidogo ujue. Ndio maana katika uwanja wa vita wengine hupata uhayawani na mawenge hali inayowapelekea kuchanganyikiwa hasa pale wanapoona wenzao wakidondoka chini bila uhai.

Nyie bakini tu kulisikia hili neno “Combat Zone” ila msiombe mkawepo. Vita huwa haupigani kwa kutumia silaha uliyonayo tu, bali vitu vinne.

Yaani, Silaha, akili, moyo na Nafsi. Ukikosa kimojawapo hapo unakimbia vitani, au unaanza kuua wenzako ili wewe utoroke.

Kitendo cha General kumuona Malone alianza kutetemeka mwili mzima na kutokwa jasho kwa wingi. Aliujua uwezo wa mtu huyu japo hawa wengine Team Leader na Golo Zumba hakuwafahamu kama nao ni Mabaduni wa Serikali.

Ujio wa hawa watu uliwafanya Makomando kushuka kutoka kwenye hizi gari tayari kwa mauaji maana hawakuwa tayari kushindwa katika jambo lao na walijiamini sana kutokana na uwezo wao kuwa wa juu sana.

Hakukuwa na haja ya mazungumzo maana aliyehitajika ni General Floyd Balehl.

Ndani ya dakika tatu tu makomando wote walikuwa chini huku roho zao zikiwa kuzimu tayari. Miili yao iliachwa ikiwa na matumbo yaliyo wazi utumbo ukiwa pembeni mchanganyiko na damu.

Midomoni meno yaling’ata ulimi uliotokeza kuja nje inchi tatu.

Ni mapigo yaliyotekelezwa kwa kutumia mikono tu bila silaha ambapo vidole vilikuwa vikizamishwa tumboni kwa nguvu na kutoka na viungo vya ndani vyote.

General alipagawa zaidi akagundua kumbe siku zote Team Leader alikuwa na Raisi Mwibale Moha akiwa nae ni miongoni mwa Mabaduni wa Serikali.

General baada ya kuona hivyo alifungua mlango wa gari na kuanza kutimua mbio asijue wapi anaelekea, huku akiwa kavalia suti kama anaekwenda kwenye hafla Fulani.

Alikimbia kurudi walikotoka na kutokana na kwamba ilikuwa ni saa kumi na moja kasoro alfajiri, kigiza Fulani bado kilikuwa kwene uso wa dunia.

Hivyo hakuwa akiona vyema anapokanyaga lakini mbio alizokuwa anatimua ni kama alikuwa anapaa, maana alijihisi mwepesi sana japo alikuwa na kitambi cha hazina kuu.

Alikimbia hadi koti la suti likafunguka vifungo vyote likawa linapepea kurudi nyuma kama bendera akawa anaongeza kasi zaidi hatimae shati nalo likachomoka maana alikuwa amechomekea, nalo likafunguka vifungo vyote na kuungana pamoja na koti kwenye kupepea.

Ungemuona ungecheka sana maana visigino vilikuwa vikigusana na kisogo kwa mbio zile, huku akiwa tumbo wazi.

Kutokana na kutoona vyema, huku akichanganywa zaidi na tochi za akina Malone nyuma yake, alijkuta kalifikia dimbwi Fulani la maji japo lilikuwa na kina kifupi cha kama futi tatu kwenda chini lakini tope lililosababishwa na maji yaliyoanza kupungua kwenye hilo dimbwi lilileta hali ya utelezi wa hatari.

Hivyo changanya na mbio zake za mawenge na hofu, alipolifikia tu hilo dimbwi lilimzoa mzima mzima na kummeza kuanzia kichwani hadi kwenye mapaja. Ikabaki miguu inapiga piga kutafuta namna ya kujinasua kutoka kwenye hayo maji yaliyochanganyikana na tope kwa chini.

Baada ya kutapatapa sana ikiwemo kumeza funda kadhaa za maji machafu, hatimae alipata upenyo akaibuka kutoka kwenye dimbwi hilo.

Sasa ile amemaliza kujipangusa macho kwa mkono wa kulia ili aone vizuri, mara anakutana na mwanga mkali wa tochi tatu kwa pamoja. Akabaki ametumbua macho tu, sasa ungemuona ndio ungecheka zaidi kwa jinsi alivyokuwa maana hata ungejizuia kucheka pengine ungejikuta unaachia hewa chafu tu. Kama akina Malone wenyewe walijikuta wakicheka wewe nani hadi ubunde?

Walimkamata wakamkokota kuelekea chopa lilipo.

Kadri walivyokuwa wakisonga mbele ndio General alibaini umbali aliokuwa amekimbia kwa muda mfupi tu, maana alishangaa wametembea mwendo mrefu sana takribani lisaa lizima na madakika. Alijishangaa mwenyewe aliwezaje kukimbia umbali mrefu hivyo kwa muda mfupi. Kwa makadirio ni kama alikuwa amekimbia kwa kasi ya Kilomita hamsini kwa lisaa. Kweli hofu juu ya kifo huleta nguvu isiyomithilika, Usipime.

Hatimae walifika mpaka pale magari na miili ilipokuwa.

General alishangaa kuona moshi mzito mweusi uliokuwa ukiishilizia na hii ni kutokana na ile miili na magari kuchomwa moto. General alishangaa sana roho walizokuwa nazo hawa watu na zaidi uwezo wao wa mapambano.

Wanajeshi waliokuwa hapo lindoni wakiongozwa na Colonel Barode walikuwa wakichimba shimo moja kubwa kwaajili ya kuyahifadhi mabaki ya miili na magari yale.

Baada ya kulifikia chopa, waliingia na chopa likapaa na kutoweka eneo hilo.

** *** ***** ******

Mwibale Moha, Murl Kamir na George Sobue walikuwa wamehifadhiwa katika Gereza la Dark Jail. Gereza hili lilikuwa ndani ya msitu mzito ambao ulikuwa umezungukwa na mito minne pande zote na kupafanya mahali hapa kuwa na mazingira magumu sana kwa maisha ya mwanadamu.

Maana nyakati za usiku mbu na baridi kali viliwanyima amani wafungwa na pia gereza hili lilijengwa kama kiwanja cha mpira kilichofunikwa kwa juu hivyo mwanga wa jua haukuwafikia waliomo ndani ya gereza.

Basi kutokana na muundo wa ujenzi wa hili gereza muda wote ndani ya gereza kulikuwa na giza na nguo hazikuwa zikikauka vizuri hivyo ilipelekea wafungwa kuambukizana magonjwa ya ngozi kwa haraka sana na ngozi zao zilikuwa nyeusi mno kutokana na baridi kali.

Ilikuwa ni bahati sana mwezi kupita bila walau vifo vya watu kumi maana mazingira hayakuwa rafiki kwa afya za wengi.

Mwibale Moha na wenzake baada ya kufika kwenye gereza hili walimkuta CL wa gereza ama Nyapara mkuu ni mtu mmoja anaitwa Limba Garuma.

Huyu Limba Garuma alifungwa kutokana na hujuma zilizotokana na siasa baada ya kuonekana akipinga wazi wazi misimamo ya Bwana Mwibale Moha na waliofanya njama mpaka akafungwa ni hawa wawili yaani Mwibale Moha akiwa Raisi na George Sobue akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Baada ya kuingia gerezani waliamrishwa kuvua nguo ili kulipa nafasi zoezi la upekuzi kufanyika.

Wakiwa bado wanajivuta vuta kuvua nguo ilisikika sauti ya kofi kali mgongoni kwa Mwibale Moha kofi lililotoka kwa nyapara mmoja hivi mfupi mwenye misuli mikononi.

Kitendo hiki kiliwashitua sana ukizingatia walikuwa hawajawahi kuingia hata kituo cha polisi zaidi ya kula mema ya nchi tu.

Kwanza ukiangalia tofauti ya umri baina ya mpiga kofi na mpigwaji ungebaini ni kama mtu mwanae kabisa lakini ni jela tu ndio watu wote hulingana, hata ukiwa mzee utapewa kazi sawa na vijana na mtatukanana kama watu wa rika moja.

Basi walivua nguo zao zote na kusimama wima, Mwibale Moha alihisi kama anaota labda, maana hakuamini kuwa ni yeye aliyekuwa anapokea amri kutoka kwa nyapara wakiwa na maaskari gereza wenye cheo cha chini kabisa cha meja.

Baada ya ukaguzi walipewa nguo zao na kuingia Admission Room ambapo walisajiliwa kama mahabusu kwa namba zilizofuatana maana walikuwa katika file moja la kesi.

Waliandikisha mpaka warithi wao kisha wakatoka na kwenda kuonyeshwa selo yao ambayo ndio ingekuwa makao yao wakiwa hapo gerezani. Waliwekwa selo moja Selo namba kumi na tatu iliyokuwa ina unyevu unyevu mwingi kutokana na Gereza hili kujengwa sehemu yenye asili ya maji maji.

Selo hii ilkuwa na jumla ya watu 45 yaani wafungwa kumi na nane na Mahabusu ishirini na saba,

Selo hii ilikuwa na Manyapara wanne yaani wawili wakiwa Manyapara wa mkanda (wa wafungwa) na wawili wakiwa wa Mahabusu.

Hivyo mahabusu walisikilizwa na manyapara wa mahabusu vivyo hivyo kwa wafungwa.

Ukiwatizama watu ndani ya hili gereza ni wazi ungedhania wote ni wagonjwa na muda si mrefu wanaweza kufa. Lakini wao walionekana kuyazoea maisha ya hapo ndani kiasi cha kupafanya kama sehemu ya amani na kawaida kwao.

Maisha ndani ya Gereza hili hayakuwa ya furaha wala amani hata kidogo kwa hawa watu watatu. Maana muda mwingi walionekana wenye mawazo mengi, kila mmoja alikuwa akimtupia lawama mwenzake kwamba kamponza.

Miili yao ilyozoea raha muda wote ilikutana na taabu ambayo haikuwa rahisi kuikabili kutokana na kutopata usingizi mzuri na lishe mbovu.

Siku moja baada ya Nyapara mkuu wa kifungo kuwa ametoka gengeni na wafungwa wengine kama ilivyo utaratibu wa magereza yote, aliwasogelea watatu hawa ambao ni Mwibale Mohan, Murl Kamir na George Sobue akawa anazungumza nao vizuri tu hakutaka kuweka chuki juu yao, maana sasa wote walikuwa sehemu moja japo yeye tayari alikuwa akitumikia kifungo chake cha miaka kumi kifungo ambacho alifungwa bila Parole kumuingiza katika mpango wa Admission Reduction yaani unatumikia siku pungufu tofauti na zile zilizopo kwenye hati ya hukumu, lakini hii ni pale ambapo mwenendo wako ndani ya gereza utakuwa wa kuridhisha. Hususani usiwe mdanganyifu juu ya afya yako kisa tu kukwepa Genge( kazi za mfungwa) usipigane hovyo na kutukana watu ndani ya gereza.

Yaani yeye alifungwa kama raia wa kigeni afungwavyo ndani ya taifa lingine.

Katika mazungumzo yao alimuuliza Mwibale Moha kuwa je atafanya nini ikiwa Itatokea kama muujiza yaani akawa ameshinda kesi na kuachiwa huru na kufanikiwa kurudi kwenye madaraka tena?

Swali hili liliibua hisia za ndani sana za huzuni kwa mwibale Moha maana alikaa kimya kama dakika nzima akiwa anatazama chini kisha alinyanyua uso ukiwa na macho yaliyojaa machozi ambayo tayari yalikwishakuanza kulowanisha mashavu yake.

Kisha kwa sauti ya unyonge sana na iliyohitaji huruma alimpigia magoti Bwana Limba na kumwambia “Nisamehe sana ndugu Limba najua ni kwa kiasi gani nimeyajeruhi maisha yako na ndoto zako, najua inaweza ikawa vigumu sana wewe kupata nafasi ya msamaha kwangu moyoni mwako. lakini nakuomba sana kwaajili ya ardhi na mbingu unisamehe ndugu yangu najuta sana kukuona ukiwa mazingira haya na sababu ikiwa ni mimi.” Aliongea akiwa amepiga magoti na hapo hapo akang’oa majani kwa mkono wake wa kulia na kuyatupa miguuni kwa Bwana Limba ikiwa ni ishara ya kusisitiza msamaha sana kwa mila na tamaduni za Songomo.

Aliongea huku machozi yakimtoka mfululizo na mate mengi yakianguka chini. Hakika alitia huruma kutokana na afya yake kudhoofika kabisa.

Ilihitaji uwe na moyo wa chuma kuweza kumnyima msamaha mtu huyu. Maana siha yake ilikuwa mithili ya mtu aliyeugua kansa ya ubongo kwa muda mrefu.

Bwana Limba aliinama tu na kumshika Mwibale Moha makwapani huku akimnyanyua juu asifanye kile anachofanya.

Akamwambia hana haja ya kumfugia chuki, maana yote yametokea kwa nafasi yake pia yamempa funzo la maisha ndani yake.

Limba alimshika mkono Mwibale Moha kwa muda mrefu sana hata yeye hakuelewa huruma kali kiasi kile ilitoka wapi kwa mtu aliyekuwa ameapa kutomsamehe abadani.

Lakini alijikuta chuki yote ikiyeyuka taratibu rohoni mwake na kujenga huruma juu ya mtu huyu hasa pale alipokuwa amebaini kuwa mtu huyu hakuwa ameipokea hii hali ya kufungwa. Maana nafsi yake haikukubali kamwe ndio maana mwili ulizidi kudhoofika kutokana na msongo wa mawazo.

Ilikuwa ni wazi kuwa mtu huyu asingedumu hata mwaka katika mazingira haya kwa hali aliyokuwa nayo, hivyo huenda akafa mapema zaidi kutokana na msongo wa mawazo.

Hali hii haikuwa kwa Mwibale Moha peke yake, bali hata washirika wake pia, Murl Kamir na George Sobue walikuwa wamedhoofika sana. Yaani ungewaona usingedhani kama ni wale makurubembe wa nchi waliokuwa wakitoa matamko ya kutikisa nchi.

Baadae walisogea ukumbini ambapo watu wote huketi kutazama televisheni na taarifa ya habari iliyokuwa ikiendelea ilitanabaisha kuwa Mtuhumiwa mwingine ambae alikuwa ni General Floyd balehl, amejiua kwa kujipiga risasi kichwani akiwa anapelekwa makao makuu ya Jeshi kwa ajili ya mahojiano baada ya kukamatwa akiwa anajaribu kutoroka nchini. Hivyo kifo cha Floyd Balehl kinafanya watuhumiwa kubakia kuwa waatatu hadi hapo baadae upelelezi utakapokuwa umekamilika.

Baadae watu hawa watatu waliongea na Nyapara mkuu ili awafanyie mpango wakutane na Bwana Jela wa hili gereza maana kuna jambo walihitaji awasaidie.

Bwana Limba alihangaika sana kujaribu kuwasilisha ombi la hawa watu kwa uongozi wa gereza. Lakini hakukuwa na matunda mazuri katika juhudi zake, ila hakukata tamaa kamwe alizidi kuwapigania watu hawa ambao sasa walibadilika na kuwa watu wake wa karibu.

Baada ya juhudi za siku tano hatimaye Bwana jela alikubali kukutana na hawa watu. Usingeamini kama huyu mtu ndie ambae alikuwa akifanya makusudi haya.

Mtu ambae hawakuwahi kudhani kuwa itatokea siku mtu huyu akawa na umuhimu kiasi hiki halafu akawaletea maringo, maana kwa nafasi walizokuwa nazo ni wazi kwamba hawakuwa hata wakifikiria kumpa maagizo maana kama ni uhitaji juu ya Parole basi walikuwa wakiongea na Mkuu wa Parole ndani ya Songomo.

Baada ya kukutana na Bwana jela walimuomba sana awafanyie utaratibu waonane na mtu mmoja kwa jina Golo Zumba Mwandishi wa habari alietukuka.

Bwana Jela aliwaahidi kulifanyia kazi ombi lao lakini wasiwe na haraka juu ya hilo.

Maana inabidi atume barua ya maombi kwenda ofisini kwa mwandishi huyo na asubiri muitikio wake ndipo awapashe na wao wawe tayari.

Hatujui watu hawa wana nini cha kumwambia Mwandishi nguli Bwana Golo Zumba lakini kalamu yangu inasita kutueleza kwa sasa basi tutajua hapo mbeleni.



***** ******* ******

Wauaji hawa walizipiga hatua kwa haraka sana kumwendea Fanton Mahal wakiwa na visu vyao mikononi lakini mara walibaki wakitetemeka huku wakiwa hawaamini wanachokiona mbele ya macho yao.

Beji ya dhahabu yenye muhuri wa Ancient Guards of the Nation ilikuwa iking’ara sana

Wauaji hawa wanaijua hii kitu vizuri kuliko kitu chochote kile maana katika assassin groups zote kumewekwa picha za hii beji kama tahadhari kuu.

Na unaambiwa usije ukajichanganya kwa mtu mwenye hiyo beji, Somo hili hutolewa sio ndani ya Songomo tu bali Ulimwenguni kote makundi yote ya Kimafia na taasisi zote za kijasusi zinafundishwa kuhusu hiyo tahadhari huku wakiwa wamepewa kipaumbele kikubwa sana katika taasisi nyingi za kijasusi.

Mfano ilipotokea mtu mwenye beji hiyo akatuma kijana wake kwenda kupewa mafunzo au kjiunga na taasisi yoyote ile iwe ya kijasusi au ya mauaji basi kijana huyo alipokelewa kwa haraka sana na kuaminiwa bila kupingwa.

Leo hii wauaji hawa wanaiona beji hii mikononi mwa mtu huyu kwanza walihisi labda itakuwa batili pengine huyu mtu anataka kuitumia tu kwa manufaa yake.

Lakini walipomtazama machoni vyema kuna kitu walikigundua, mtu huyu macho yake yalikwishakubadilika rangi na kuwa meusi ti. Bila hata weupe wowote na nywele zake zilianza kutoa moshi mweusi.

Hali hii iliwatisha sana na hawajawahi kumuona kiumbe wa aina hii zaidi ya kumsikia tu katika taasisi mbali mbali walizokwenda kuchukua mafunzo.

Walizoea kusikia habari zilizokuwa zikiwaelezea hawa malaika wa shetani namna walivyo na mabalaa yao jinsi wanavyoweza kupambana na kuhama maeneo kwa nukta kadhaa.

Baada ya kuona hivyo wauaji walipiga magoti mbele ya huyu mtu na kuinamisha vichwa vyao miguuni pake. Eeeeeeh hakukuwa na njia tofauti ya kutafuta suluhu na huyu kiumbe zaidi ya kuomba kuonewa huruma maana wauaji hutamani na kupenda waendelee kuishi. Huwa hawapendi kufa wala kufiwa.

Fanton Mahal alibaki amesimama tu vile vile maana alikuwa akitafakari ni nini awafanye watu hawa hata asiambulie chochote cha kuwafanya.

Baada ya hapo wauaji walirudi hotelini mbio mbio kwenda kuangalia hali ya majeruhi lakini moyoni wakiwa wanaomba asije akafa maana msalaba huo hawawezi kuubeba.

Walipofika kwenye mlango wa lifti, wakati inafunguka ili waingie mara wakawaona Jiga Kinamba na Mwana wakiwa wameupakata mwili wa Zurfa.

Kwakuwa king’ora cha hatari kilikwisha kulia basi kila mtu alikaa chonjo kwa tahadhari wengi wakidhani labda ni moto unataka kuzuka hapo hotelini.

Wauaji waliwalaki akina Jiga Kinamba na kuwasaidia kumbeba mwanamama huyu ambae alikuwa akivuja damu kwa wingi, wakampakia kwenye gari ile waliyokuja nayo kisha haraka wakairudia ile miili ya wenzao waliouawa pale koridoni floor namba saba kisha wakaipakia kwenye gari.

Sasa ni hivi kama kuna kitu kiliunyanyasa sana moyo wa Fanton Mahal ni kumuona huyu Bibie Zurfa akiwa mahututi tena akionekana muda wowote anaweza kupoteza maisha.

Hali hii ilimuondolea utulivu nafsini mwake akakumbuka mbali walikotoka na huyu mwanamke mpaka hapa walipo na leo yuko mahututi kwaajili ya hawa washenzi.

Baada ya muda kidogo aliamua Zurfa aingizwe kwenye gari yake na dereva akapewa maelekezo wapi ampeleke mwanamama huyo kwakuwa dereva ni Macka Shinea basi uhakika wa safari kuwa fupi ulikuwa mkubwa maana huyu ni zaidi ya dereva.

Gari ilipigwa norinda moja matata sekunde tu ikawa inatazama walipotokea ikaondoka kwa kasi ya mwanga. Na hapo ndipo Mabaduni wengine humvulia kofia Macka Shinea gwiji la magari yaendayo kasi ya ajabu.

Macka Shinea sio tu kwamba ni mtaalamu tu wa kuendesha magari pia ni hatari sana kwa kurusha ndege za kivita na ni kinara wa kuongoza mitambo mbali mbali.

Hivyo mtu huyu ni hazina kubwa sana kwenye hili Kosi la Damu, ana maamuzi magumu sana awapo barabarani najua wale madereva wazoefu wananielewa.

Sio kwamba huwa hapati ajali la hasha bali ni vile anavyoichukulia ile hali ya kupata ajali kama sehemu tu ya maisha yake hivyo hii imemjengea ujasiri wa ajabu hata huko angani hurusha ndege na machopa katika mitindo na mazingira ya ajabu “He is just abnormal!! Yeah like that”.

Jiga Kinamba na Mwana, wao walipewa maelekezo kuwa waendelee na ratiba kama hapo awali ambapo walirudi hotelini japo Mwana alitamani sana aondoke na mama yake lakini baba yake alimzuia kuwa yeye abaki, na kuhusu afya ya mama yake asiwe na shaka kila kitu kitakaa sawa.

Fanton Mahal alibaki na walinzi wake na hawa wauaji maana alihitaji kufahamu baadhi ya mambo kutoka kwao, basi ilibidi amtume kijana mapokezi apewe funguo za gari la bi Zurfa alilokuja nalo maana mara zote Bi Zurfa hukabidhi funguo zake pale mapokezi kila akiwa hapo Hotelini.

Baada ya funguo kuletwa aliwaagiza wale wauaji waiweke ile miili kwenye gari ya Bi Zurfa ambapo baada ya hilo zoezi vijana walijua nini cha kuifanyia hiyo miili wakaondoka vijana wa Fanton Mahal wote na kumwacha akiwa peke yake na hawa wauaji.

Fanton alipanda kwenye gari yao waliyokuja nayo hawa wauaji. Wao wakiwa wamekaa mbele na yeye kakaa siti ya nyuma gari ikaondolewa eneo hilo la Crooven Hotel na kusogezwa mbali zaidi, walipofika eneo ambalo halikuonekana kuwa na makazi ya watu wala shughuli yoyote ya kijamii aliwaambia wasimamishe gari wakatii amri.

Aliwasaili vya kutosha mpaka akagundua kuwa hawakuwa raia wa Songomo bali walitoka nchi ya mbali kidogo na hapa na walikuwa wamekodiwa kuja kufanya usafi.

Usafi ambao ungeyaacha majina ya wahusika wengine waliopo uraiani wakiwa safi na salama bila tuhuma za aina yoyote ile wala kashfa za ufisadi.

Mchoro mzima wa namna kazi ilitakiwa kufanyika walikuwa nao idadi na majina ya watu waliotakiwa kuuawa na kwa namna gani vyote hivyo viliorodheshwa.

Nani alikuwa mdhamini wa kundi hilo la mauaji ?

Wauaji walisema sio mtu mmoja bali ni kikundi cha watu kama kumi na tano, lakini wauaji walidai hawana orodha kamili ya majina labda akipatikana mtu mmoja anafahamika kama Big Mouse ndie anaweza kutoa orodha kamili ya majina ya wadhamini.

Je mpaka sasa idadi ni ipi ya wauaji waliomo nchini Songomo?

Majibu ni kwamba kuna zaidi ya watu miambili walioingia nchini kwaajili ya kutekeleza majukumu tofauti kwa kila kikundi cha watu, na walikuwa wamegawanywa katika makundi hamsini ya watu wanne wanne huku makundi mengine yakiwa na watu zaidi maana hata raia wa nchini Songomo walikuwemo ili kutoa ushirikiano kwa maana ya uenyeji juu ya maeneo tofauti tofauti hivyo kulifanya zoezi kuwa rahisi.

Maeneo mengi zikiwemo pia taasisi na biashara zilizokuwa chini ya umiliki wa walengwa pia zilikuwa zimelengwa na kubwa kuliko yote ni Kwamba Jengo la SHATOTO COMPLEX

Na baadhi ya mabohari ya mafuta ambayo ni mali ya ONE OIL REFINERY kampuni tanzu chini ya GIMONCHY GROUP of COMPANIES, Makao makuu ya GIMONCHY.

Maneno haya yalimtia ubaridi Fanton Mahal ndani ya nafsi, akajaribu kuwaza itakuwaje ikiwa hawa watu watafanikiwa japo kwa asilimia kumi tu katika mipango yao?

Akaona ni muda wa kurudi kazini yeye mwenyewe maana mipango waliyo nayo hawa watu ni kuangamiza pia maisha ya watu wengi maana ikiwa maeneo hayo yatalipuliwa basi sio chini ya watu laki tano ambao wanaweza kudhurika ama kupoteza maisha maana ukubwa wa athari utategemea na aina ya mabomu watakayoyatumia.

Basi muda huo huo Fanton Mahal alivuta simu akapiga kwa mtu ambaye haikufahamika hasa ni nani akatoa maelekezo Fulani kisha akamwambia mmoja wa wale wauaji ampigie simu Big Mouse kumpa ripoti kuwa section yao tayari washaikamilisha.

Basi zoezi hilo lilifanyika muda huo huo ambapo Big mouse alitoa pongezi kwa vijana na kuwasihi jioni waonane eneo ambalo baadae angewaambia kwaajili ya kuwapa motisha kwaajili ya kazi yao.

Basi baada ya zoezi hilo Fanton Mahal aliteremka kwenye gari na kuondoka akiwaacha wauaji kwenye gari wakiwa wanajiuliza maswali lukuki kuwa, kitendo kile kilimaanisha nini. Pia ile simu waliyoambiwa wampigie mkuu wao ilikuwa na utata mwingi ambao walihitaji ufafanuzi lakini wasaa haukuwa upande wao kupata majibu.

Wakajaribu kuikagua gari yao kuona labda kuna bomu linaweza kuwa limeachwa ndani lakini hakukuwa na dalili zozote zile za hatari walizoweza kuzibaini basi walau wakapumua kwa ahueni huku wakigonga mikono kushangilia kuachwa hai na huyu mtu.

Lakini wakiwa katika hali ya kusherekea hivi, ndipo Dereva alianza kutokwa na damu puani mwenzake akamshangaa mwenzake punde na yeye hali hiyo ikamkumba ikafuatiwa na masikioni na mdomoni mara wakaanza kukohoa hovyo huku miili ikiishiwa nguvu kabisa damu ilikuwa ni nzito yenye weusi Fulani ndani yake.

Walipigwa sumu mbaya isiyokuwa na harufu wakati anashuka kwenye gari.

Mwanaume akatokomea zake.

Ndani ya Lottan Grand Villa ndimo yalikuwa makazi ya muda ya Big Mouse akiwa amestareheka upande wa mashariki wenye kila kitu maana alichukua upande mzima wa hoteli hii ili autumie na pia kwaajili ya usalama wake kuepusha mwingiliano wa watu wasiohusika na mipango hii na muda mwingi alikuwa akiwasiliana na vigogo Fulani ambao walikuwa wakiulizia maendeleo ya mipango yao.

Akiwa kaketi kwenye kakitanda kake kazuri kaliko pembezoni mwa bwawa la kuogelea akiwa amevaa kikaptura kifupi, juu akiwa kifua wazi, mkononi alikuwa na glasi kubwa ya mvinyo wa gharama, machoni aliweka miwani ya kuzuia mwanga mkali na mionzi ya jua.

Alikuwa anastareheka akijua kazi inaenda kama ilivyopangwa na aliamini ndani ya siku tatu kazi itakuwa imekamilika na siku ya tano atakuwa keshaondoka na vijana wake kurudi nchini kwao.

Akiwa anaongea na simu kwa mkono wa kulia huku wa kushoto ukiwa na glasi alishangaa kuona mtu akiibukia kwenye bwawa la kuogelea ambalo yeye ndiye alietokamo na kuja kukaa kwenye kitanda, akashangaa na kuikata ile simu akiitupia kitandani na glasi akaiweka pembeni.

Mtu huyu aliyewasili hapa sura yake ilikuwa ni ngeni kabisa na haikufahamika ni nani haswa je ni adui au ni mshirika.

Mtu huyu alikuwa amevaa gwanda nyeusi zenye material magumu sana chini alivalia kiatu cha ngozi cheusi ilikuwa ni buti ya kazi kweli kweli.

Muonekano wa huyu mtu ulitosha kumjulisha mtu yeyote kuwa hii ni Namba chafu, Mwili wa mazoezi uliofichwa ndani ya haya magwanda uliakisiwa na ujazo na wingi wa misuli iliyokuwa mikononi na shingoni. Hakuwa katuna ila mwili ulikuwa umekatika sana kimazoezi .

Mwanaume alisogea mpaka pale alipoketi Big Mouse akachuchumaa mbele yake akamtazama usoni.

Big Mouse anajikubali sana kwanza ni muuaji aliyebobea mwenye roho ya kinyama ambae hatishiki kwa namna yoyote ile. Pili hili jina la Big Mouse ikimaanisha Panya mkubwa alipewa kutokana na mbinu zake za kupotea katika mazingira tatanishi hasa pale mambo yanapoonekana kutomwendea sawia.

Mvamizi alitamka maneno yafuatayo, “Nahitaji orodha ya majina ya watu waliokukodi. Baada ya hapo unatakiwa ukusanye vijana wako wote, Uabort mission na uondoke. Mna masaa matatu ya kuwepo hapa nchini.”

Big Mouse kwanza alivua miwani yake akaiweka pembeni, asiamini anachosikia kutoka kwa mtu huyu. Maana aliona kama vichekesho kutokana na nguvu ya watu waliomkodi. hakuamini kama kuna mtu yeyote angeweza kujitokeza na kupinga maagizo ya hao vibopa.

Big Mouse alitabasamu tu kisha akamwambia mvamizi kuwa yeye na hao waliomtuma wamekwisha kuchelewa maana kazi tayari imekwisha kuanza na hakuna mtu mwenye sauti ya kutoa amri ya kuback off.

Na kuhusu waliomtuma alisema ni watu wazito hivyo asijisumbue kutaka kuwajua ni akina nani maana atapoteza tu maisha.

Mvamizi alimwambia kuwa hakuna mtu mkubwa mbele ya kitambulisho chake cha kazi ,na kama anakaidi ataua vijana wake wote mpaka ndugu zake pia waliopo,(……..) akataja mpaka mtaa waliopo ndugu zake Big Mouse huko nchini kwao.

Big Mouse alishituka sana maana hakutarajia kuwa mtu huyu anaweza kuwa na taarifa nyeti kumhusu yeye.

Akajiuliza sana mtu huyu ni nani haswa.

Mara mtu huyu akatoa tableti na kumpa Big Mouse aandike majina ya wahusika, Big Mouse akaivuta na kuiachia ijipigize chini lakini kwa nukta moja ilidakwa kwa mkono wa kushoto kisha ikarushwa juu kidogo usawa wa kichwa, maana sasa walikuwa wamesimama wote wakati tableti ikiwa inaelea hewani kwa kutumia mkono ule ule wa kushoto, Big Mouse alipigwa kofi zito la nyuma ya kiganja maarufu kama kelebu.

Kofi hili lilimtia upofu ghafla Big Mouse, kwa dakika mbili akabaki anafikicha macho yake huku damu zikimtoka puani na mdomoni.

Hajawahi kukutana na nguvu ya namna hii maana alianza kuhisi kizunguzungu. Ni kweli anakumbuka ni kama amepigwa kofi tu, lakini mvumo na mkito uliotua usoni kwake alihisi lile kofi limeambatana na kitu kingine kizito nyuma yake.

Baada ya akili yake kukaa sawa alijaribu kufumbua macho amuone mtu huyu vyema lakini alichokutana nacho alibaki ameachama mdomo wazi.

Beji ya Ancient Guards of The Nation ilikuwa mbele ya uso wake. Beji ya Dhahabu yenye muhuri wa moto ilikuwa iking’aa vyema. Alianguka chini akapiga magoti na kumshika miguu huyu mtu akaomba sana msamaha akimsisitiza na kumuomba ampe ile tableti ili aandike majina ya wahusika anaowajua.

Alikabidhiwa Tableti akaanza na jina la Wiza Marota Likaandikwa jina la Huang Feng, Levi van Bas,Ishan Arjun, Suheil Vikram, mwisho akamalizia jina la Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Songomo. Bwana Frank Kibona.

Huang Feng tulikwisha muona huko nyuma ni nani lakini pia Levi Van Bas huyu ni mmiliki wa kampuni moja kubwa inayojihusisha na uchimbaji wa madini na uagizaji wa mitambo mbali mbali nje ya nchi.

Ishan Arjun yeye anamiliki viwanda vinavyozalisha chuma na vifaa vya ujenzi. Pia anamiliki mtandao wa mawasiliano wa Mobicom cellular network.

Suheil Vikram yeye ni mmiliki wa makampuni mengi yakiwemo ya Usafirishaji na usambazaji huduma ya umeme.

Big Mouse baada ya kumaliza kuwaandika hao wahusika alichukua simu akampigia mtu mmoja akimpa maelekezo ya kukusanya vijana wote na kuachana na kazi yoyote ile na kama kuna mabomu wamekwisha kuyatega wayategue wahakikishe hawaachi hata moja.

Operation master alishangaa maana imekuwa ghafla sana hajamzoea bosi wake kuabort mission hata iweje.

Basi hakuwa na ubavu wa kumpinga japo alijawa shauku ya kujua kulikoni akaona afanye kama alivyoagizwa ndani ya masaa mawili zoezi lote lilikamilika na tayari walikuwa ndani ya meli kubwa wakiiacha pwani ya Songomo kurudi nchini mwao.

Orodha ya majina ya wahusika iliwasilishwa mikononi mwa Fanton Mahal kupitia Kau Kamale. Sasa ndipo tunabaini kuwa Kau Kamale ndiye aliyemshughulikia Big Mouse pale Lottan Grand Villa.

Jioni ya siku iliyofuata Fanton Mahal alionekana akiwa na Makamu wa Raisi wa Songomo ambae sasa madaraka yote yalikuwa chini yake, wlionekana wakiwa ikulu wakifanya mazungumzo ya kina sana yaliyofuatiwa na chakula na vinywaji kwa pamoja.

Kesho yake watu kutoka ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali walifika katika ofisi za makampuni yote yaliyo chini ya Levi van Bas, Suheil Vikram na Ishan Arjun.

Baadae ikatangazwa kuwa kampuni hizo zimefutiwa vibali vya kuendelea kufanya kazi nchini Songomo na imebainika udanganyifu mkubwa ambao umekuwa ukifanywa na wamiliki wa makampuni hayo hivyo mali na akiba zote za makampuni hayo zinataifishwa na wamiliki wake wamekamatwa kwa makosa ya Uhujumu uchumi na utakatishaji wa Fedha.

Kashfa hii ilimpitia pia Meneja wa Benki Kuu ya Songomo.

Baada ya uchunguzi kuonesha kuwa kuna kiasi cha pesa kikubwa mara kadhaa kimeidhinishwa malipo kwa makampuni haya bila kuwepo na taarifa za kimiamala zinazoridhisha, Ripoti hii ilipatikana kutoka kitengo cha kudhibiti fedha haramu na miamala batili.

Kuna kiasi cha dola billioni kumi na tano kiliidhinishwa na Serikali kwaajili ya wakulima wadogo, wafugaji na wavuvi wa ndani. lakini kiasi hicho wakakopeshwa hao wamiliki wa makampuni tajwa, kwasababu riba yake ilikuwa ndogo sana na ya muda wa miaka kumi basi hawa watu walikitumia kiasi hicho kujinufaisha wao baada ya kununua hisa za mikopo midogo midogo kwenye mabenki madogo hapo nchini kwa kutumia kiasi kile kile, hivyo wamewanyonya sana wananchi na kuwa kikwazo kwa wale waliostahili kufikiwa na huduma hiyo.

Mchambuzi mkuu wa masuala ya uchumi alipoulizwa kuwa ni hasara kiasi gani ambayo taifa limepata kutokana na uhujumu huo? akadadavua kisomi na kwa ufupi tu kuwa tusichukulie hesabu za figure maana zitawachanganya walio wengi ila kuliweka hili sawa ni hivi, ikiwa dhamira ya serikali ilikuwa kuwakopesha kila mtu dola elfu tano basi ni wazi kwamba zaidi ya watu milioni mbili wangenufaika moja kwa moja kupitia mkopo huo iwe kwa kukopeshwa ama kupata ajira ambayo ingezalishwa na mkopo huo.

Hivyo ukipiga hesabu utaona ni hasara kiasi gani taifa linaweza kuwa limeingia kwa muda wa miaka minne mpaka sasa tangu pale mkopo huo ulipoidhinishwa ukiachilia mbali malengo ya Serikali ambayo hayajatimia ya kumwinua kiuchumi mlengwa.

Kauli hii iliibua chuki na hasira kwa wakulima,wafugaji na wavuvi nchini songomo.

Wamiliki hawa walitupwa gerezani na kufilisiwa huku wakikabiliwa na adhabu ya kunyongwa.

******** ********* **********

Asubuhi na mapema Inspekta Jenerali wa polisi alitoka bafuni na kuingia chumbani kujiandaa kwaajili kwenda ofisini kuratibu mipango mbali mbali ilyolihusu jeshi hili kama ilivyo ada.

Hakuwa amelala nyumbani kwake kama siku zote bali alikuwa katika hoteli moja nzuri sana ya Sweet View. Ambapo alikuwa amezoea kufikia pindi awapo pamoja na kimada wake Vivian.

Vivian alikuwa bado amelala kitandani.

Mh Frank Kibona alitoka maliwatoni akiwa na haraka zake na pupa ambavyo vilikatishwa mara tu alipoona mazingira tofauti chumbani mwake. Ndio, mazingira tofauti!! Maana kitandani pembeni mwa alipolala Vivian alikaa mtu mmoja sura ni ngeni kabisa.

Mkononi hakuwa na silaha alikuwa akimuangalia Mh Frank anavyopiga hatua zake za haraka haraka zilizogeuka kuwa hafifu baada ya kugundua uwepo wake.

Mh Frank Kibona alisimama wima na taulo lake kiunoni asijue afanye nini, lakini kwasababu ni askari alijipa ujasiri akasonga mbele zaidi hesabu zake zilimtuma ajaribu kutumia mbinu ya kiaskari ya ghiriba.

Akaanza mazungumzo “Inakuwaje asubuhi yote hii ndugu yangu tunavamiana hivi? na inaonekana ulilala na mwanamke wangu kabisa”

“Unamaanisha kuwa hapa tulilala watatu? Na ilikuwaje ukaruhusu tukachangia mwanamke wako?”
Alijibiwa na mtu huyu.

Kichwani alianza kujiona mshindi baada ya kuona mbinu yake ya kununua muda inaanza kuzaa matunda, maana alihitaji alikaribie kabati lake la nguo ili achukue silaha, lakini laiti angejua angejitosa kupitia dirishani na taulo lake.

Pengine angekuwa na asilimia za kuokoka kutoka kwenye mikono ya huyu mtu.

Wakati akiwa na asilimia nyingi za kulifikia kabati alishtuka baada ya kupigwa mtama akapaa hewani, kabla hajatua akasindikizwa na teke la ubavuni lillilomtupa na kwenda kujibamiza ukutani sehemu ya kichwa shingo ikajikunja akauma ulimi huku mbavu kadhaa zikiwa zimevunjika.

Povu zito likamtoka mdomoni na haja ndogo, pale pale akapewa tiketi ya kuzimu. Taulo liliusaliti mwili wake akakata roho akiwa mtupu kama alivyozaliwa, Muuaji alifanya kumfunika kwa taulo pale chini ili asibaki uchi. Hii ni kwaajili ya heshima ya Mwanaume. Kwasababu Men will always be Men by morals.

Vivian yeye alikuwa akikoroma katika usingizi wa pono, hakuonekana kujitingisha wala.

Pengine huu haukuwa usingizi wake labda aliuziwa usingizi wa dukani kwa kunusishwa dawa za usingizi si unajua tena majasusi na mambo yao?

Muuaji aliondoka hapo hotelini na kushika bara bara iliyokuwa ikikatiza katika vichaka vizito ambamo ndimo alikuwa ameficha gari lake.

Baada ya kuingia kwenye gari aliitoa ile sura aliyokuwa nayo na kubaki akiwa Kau Kamale ( nyamera la kwenda).

***** ****** ********

Wiza Marota alikuwa kwenye maandalizi ndani ya hekalu lake la kutisha lililopo ndani ya mji wa Cadmon. Huku nje mbele ya Hekalu hili kukiwa na chopa moja ambalo lilikuwa likimsubiri yeye na familia yake kwaajili kuelekea Nchini Jotokali, ambako wangeishi maisha yao mpaka hapo baadae ambapo hali nchini Songomo ingetulia.

Lakini pia kwaajili ya kujipanga upya ili aendeleze mashambulizi akiwa huko huko.

Alifikia uamuzi huo baada ya washirika wake ambao walikuwa wakipanga mipango pamoja kuanza kuuawa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola.

Hii sasa ilimaanisha kuwa kuna mapinduzi makubwa yanafanyika ndani ya hili taifa hivyo yeye mwenyewe alijua kabisa mikono yake haikuwa misafi hata kwa asilimia tano tu. Kuendelea kubaki nchini Songomo kulimaanisha mwisho wake na washirika wake.

Pia nguvu ya Hawa mabaduni aliijua maana hata yeye aliwahi kuletewa ripoti mezani kwake kipindi hicho akiwa mtawala japo taarifa hazikuwa zikiweka wazi juu ya hili kosi lakini yale yaliyokuwa yakifanywa na hawa watu yalitisha mno.

Hivyo tetesi za kuwepo kwa hili kundi nyuma ya haya matukio zilizidi kumpa wasi wasi ikiwa ikatokea ikawa ni kweli basi aliona njia pekee ni kuikimbia nchi kwanza.

Ni bora apate habari juu ya hili kosi akiwa nje ya nchi mafichoni kuliko kuzishuhudia yeye mwenyewe.

Chopa hili lilitakiwa kuwapeleka mpaka kwenye bandari ndogo ya Homa bay ambako wangepanda speed boat kuelekea nchini Jotokali. Yeye na walinzi wake watatu walitakiwa kutangulia kwa chopa kisha kuingoja familia yake ya wake wawili na watoto saba na wafanyakazi wanne na walinzi watano Hivyo msafara wa gari kama nne hivi ungekuwa ukisubiriwa pale Bandarini.

Baada ya kujiandaa vyema Wiza marota alitoka huku akiwakumbatia wake zake na watoto wake akiwaasa wawahi maana hawatakiwi kuchelewa sana.

Wiza na walinzi wake waliingia kwenye chopa ambalo lilikuwa tayari kuruka maana pangaboi zilikuwa zishaanza kukata upepo.

Wakajitoma ndani na kutulia kwenye siti zao kimya wakisubiri chopa lipae.

Baada ya chopa kupaa porojo za hapa na pale zilishika hatamu Wiza akiwaambia vijana wake kuwa roho inamuuma sana kwenda mbali na nyumbani, maana amepazoea na hata familia yake pia imepazoea.

Hivyo anaona changamoto kidogo kwenda ugenini japo nako ana uraia wa kule lakini utofauti lazima uwepo hatokuwa na uhuru kama alivyokuwa huku. Alizidi kuwaonesha mazingira kwa chini yalivyoonekana hususani kijani kibichi kilichovutia na pia ni mazingira yaliyokuwa yakivutia sana kuwekeza kilimo. Hapo napo Wiza akatia neno kuwa siku moja atarudi na kuja kuwekeza katika kilimo ili awe chachu ya kuwashawishi wananchi kuwekeza katika sekta hiyo.

Haya alikuwa akiyatamani wakati huu akiwa angani kuondoka hapa nchini, na wakati amekaa kwenye utawala miaka kumi na nne akiwa kama Raisi lakini hakuwahi kukipa kilimo kipaumbele zaidi ya kutumbua pesa za UMMA kwa safari za mara kwa mara zisizo na tija kwa taifa. Akisingizia kuwa anaiunganisha Songomo kimahusiano na Dunia ya mbali.

Huyu jamaa alibarikiwa kipawa cha kuchekesha watu ukiachilia mbali roho yake ya kishenzi.

Alimtania mlinzi wake anayeitwa John, kuwa “Wewe sasa unabaki, utakuwa unavua samaki na kulima mchicha maana ulizoea kukaa pembeni yangu muda wote, angalau sasa nitakuwa navuta hewa safi sio ile iliyojaa ushuzi wako.”

Hakuna aliyemwambia mwenzake acheke, walicheka mno.

Hii ilipelekewa na mazoea yaliyojengeka na mahusiano mazuri baina ya Wiza Marota na walinzi wake, Wiza alikuwa na upendo na mcheshi pia kwa watu wake wa karibu.

Lakini kiutawala jamaa alikuwa mbovu na mwizi aliyejaa tamaa kali sana. Alizaliwa mashariki mwa Songomo miaka sabini na tano iliyopita. Lakini ukimuangalia ungedhani labda ana miaka sitini au hamsini na tano hivi, ogopa mtu anakula na kunywa kwa dhamana ya jasho la wengine atazeeka na kuchoka kwa lipi sasa?

Wakiwa wanaendelea na porojo zao ndipo mlinzi mmoja alibaini kitu chini kwenye miguu yake akashituka, ndio, viatu vyake vilikuwa vimezingirwa na damu nyingi.

Hapo ndipo walikurupuka na kuanza kuangaza chini ya siti zao, ndipo wakabaini mwili wa mtu ukiwa nyuma ya siti zao.

Ulikuwa ni mwili wa rubani, mtu ambae alitakiwa muda huu awe anaongoza hili chopa. Hapo hofu na taharuki vikawaingia wakajikuta wanamtazama vyema rubani wao ambae naye ndio alikuwa anamalizia kujifunga mikanda ya parachuti kisha akajiachia huku akiliacha chopa likiwa kwenye mwendo mkali, lakini pia ndani aliacha time bomb.

Chopa halikufika popote lilikosa mwelekeo likaenda kuchumpa kwenye kilima kidogo cha mawe na nyasi fupi kisha bomu likaripuka na kuchukua nafsi za wote waliokuwemo humo.

Taarifa ziliifikia familia kabla hata haijaondoka mjini Cadmon ikawa ni vilio na simanzi tele. Jina la Wiza Marota likabaki kwenye kumbu kumbu za maraisi wastaafu wa Songomo waliokwisha kutangulia mbele za haki. Kazi ya Macka Shinea!!.

***** ****** *******

Kila chama cha siasa Songomo kilikwishawasilisha jina la mwakilishi wake kwa mwenyekiti wa baraza la seneti, kwa ajili ya zoezi la upigaji kura kupata majina ya watu wawili ambao wangechuana vikali katika kura za wananchi wa Songomo baada ya mwezi mmoja.

Maandalizi ya kikao cha baraza la seneti yalikuwa tayari ambapo zoezi hilo lilibakiza siku moja ili kutimia na wananchi wengi wa Songomo walikuwa wakisubiri kwa hamu kubwa sana kuona ni nani na nani watachuana kwenye kura za wananchi?

Ni zoezi ambalo lilitarajiwa kuwa la haki na uwazi bila ukiritimba wa aina yoyote ile kutokana na yaliyokwisha kujiri hapo nyuma.

Chama cha Mwibale Moha cha Revolutional Movement Kilisimamisha Mwanamke katika kinyang’anyiro hicho kitendo ambacho kilitafsiriwa na wengi kama ni mbinu mbovu na ukosefu wa utashi ndani ya chama.

Na hilo lingepelekea chama kuanguka mapema tu kwenye kura za seneti kwa Imani ya wanasiasa wengi. Lakini mwenyekiti wa chama alikuwa akiyatetea maamuzi ya chama kuwa ni ukuaji na uimarikaji wa chama kisiasa kumpa nafasi ya kutawala mwanamke na wala sio dhambi kufanya hivyo na kamwe chama hakiwezi kushindwa katika duru hii ya uchaguzi.

Taarifa hii ilimfikia Mwibale Moha akiwa gerezani, kitendo cha kuona kwenye nafasi aliyotakiwa kusimama yeye kasimama mwanamke kilimuuma mno.

Aliona wazi ni nafasi ya maana sana iliyopotea kwamaana chama hakiwezi kushinda kwa kusimamisha mwanamke.

Hata kama angeshinda kwenye kura za Seneti kuna uwezekano mkubwa akaanguka kwenye kura za wananchi.

Zoezi la kupiga kura za baraza la seneti lilikamilika likiwa limehusisha wajumbe mia mbili hamsini. Na Majina mawili ya wagombea yalipitishwa baada ya zoezi la kuhesabu kura na washindi kutangazwa.

Fredinand Mbwela kutoka chama cha Liberation Front na Suzana Muguki kutoka chama cha Revolutional Movement walitangazwa washindi. Ambapo wangepigiwa kura sambamba na wagombea ubunge.Watu wengi walikuwa na shauku ya kuona kama mwanamama Suzana angeshinda na kufanikiwa kuwa mtawala wa kwanza wa kike Songomo.

Baada ya zoezi kikao cha baraza la seneti kupita hatimaye Golo Zumba aliweza kukutana na Mwibale Moha pamoja na wenzake wawili pale gerezani.

Walitengewa muda mwingi sana karibia masaa sita kwaajili ya mazungumnzo ambayo yalikuwa yamebeba taarifa nyeti.

Siha za hawa watu zilikuwa zimedorora sana na kutia huruma maana mifupa na mishipa ya shingoni ilikuwa imesimama na kuonekana wazi wazi hakika walikuwa wameisha ni kama watu waliougua sana muda mrefu.

Basi baada ya mahojiano haya ambayo yalirekodiwa video na kuhifadhiwa. Golo Zumba, aliondoka hapo gerezani na kuwaacha watatu hao.

Zikiwa zimebakia wiki mbili kuelekea uchaguzi mkuu taarifa kutoka gerezani zilidai kuwa Mwibale Moha Raisi aliepita wa Songomo amefariki dunia akiwa hospitali ya Rufaa ya Songomo baada ya vipimo kuonesha kuwa alikuwa na saratani ya ubongo iliyokuwa ikimtafuna taratibu bila yeye mwenyewe kujua mpaka pale alipozidiwa na kukimbizwa hospitali na kugundulika kuwa na ugonjwa huo.

****** ******* *********

Hali ya Mwanamama Zurfa ilizidi kuimarika na kurejea katika ukawaida wake kutokana na matibabu alyoyapata kutoka kwa madaktari bingwa pamoja na maombi ya watu wake wa karibu wakiwemo wanae wanne ambao walikuja kumtembelea baada ya kuwa ameruhusiwa kutoka chini ya uangalizi wa dakatari.

Mwana pia alifika akiwa ameambatana na Jiga Kinamba na kumwelezea mama yake na baadhi ya ndugu zake kuhusu mahusiano yake na Jiga Kinamba.

Hakukuwa na mengi zaidi ya kupewa tu Baraka juu ya maamuzi yake, maana yeye alikataa kwenda kusoma huko mbali nje ya Songomo akidai anataka kubaki karibu na wazazi wake na hakuwa na kichwa cha kusoma yeye alipendelea zaidi mitindo na urembo.

Jiga Kinamba alimuuliza wakiwa wawili ni kwanini wazazi wake wana mali lakini yeye akaamua kuishi kule uswahilini kwenye maisha ya watu wa chini?

Mwana alimjibu kuwa yeye ndiye sababu maana alimfuata yeye pale baada ya siku moja kumuona akiongea na baba yake.

Hivyo akawa amemueleza baba yake kuhusu hisia zake juu yake, ambapo baba yake alimuelekeza Jiga Kinamba anapopatikana ambapo ilimbidi na yeye afanye mpango wa kuwa karibu zaidi na Jiga Kinamba ndipo alipopanga kwenye ile nyumba akisaidiwa na Mwanamke mmoja wa pale kupata chumba pale tu kilipoachwa wazi.

Jiga Kinamba alishangaa kujua kuwa katika uchoraji wa huu mpango hata baba yake Mwana Mh Fanton Mahal alihusika pakubwa. Alishangaa ni upendo kiasi gani alionao Fanton Mahal juu ya binti yake mpaka kufikia kumsaidia ili apate hitaji la moyo wake? Lakini pia aliamini kuwa Fanton alifikia maamuzi hayo kwasababu kwanza wote wapo katika mfumo mmoja. Jiga Kinamba aliingia kwenye gari akiwa na mpenzi wake Mwana, tayari kuondoka kwenda kufurahia maisha. Lakini muda ule ule ujumbe wa maandishi uliingia kwenye simu yake ikisomeka call of duty ikitokea kwa Malone.

Hazikupita hata sekunde mbili simu ikaita kuangalia mpigaji ni Fanton Mahal.

Jiga Kinamba aliipokea na kuiweka sikioni na kusikiliza maelekezo toka kwa baba mkwe wake huyu mpya.

Simu hii ilikuwa ni wito wa ghafla wa kukutana ndani ya Arsenal yao chini ya bahari maana kuna kazi kubwa inayohitaji kufanyika haraka sana na ni jukumu la kuliokoa taifa, bila kufanya hivyo taifa linaweza kuangamia.

Jiga Kinamba alimshusha mpenzi wake na kumuaga akimwambia yeye abaki na ndugu zake yeye amepata majukumu ya dharula hivyo wangeonana baada ya hayo maju kumu.

Mwana alinuna kimtindo maana alitegemea huu uwe wakati wao mzuri wa kuwa pamoja na kufurahia maisha lakini inakuwa vingine tena si unajua tena wanawake na masuala ya kuhusu kupewa time na wapenzi wao hasa penzi likiwa bado jipya?

Jiga Kinamba aliwasili mpaka kwenye Arsenal ndani ya manuari chini ya maji ya bahari na kuwakuta wenzake wote wakiwa wameshawasili wakimsubiri yeye tu.

Huko juu vijana wa JISA wakifanya ulinzi kama kawaida chini ya maelekezo ya Malone.

Taarifa iliyowekwa mezani ilikuwa ni nzito kuwa kumbe mgombea wa kike kupitia chama cha Revolutional Movement alikuwa ni pandikizi la watu wa mashariki ambao walihitaji kuendelea kushika dola kupitia matamko ya huyu Mwanamama Suzan Muguki.

Hivyo hata zoezi zima la upigaji kura liliingiliwa na kusababisha jina la huyu mama kuwa la pili katika wingi wa kura.

Hivyo watu wa mashariki bado walikuwa na biashara ambayo haijamalizika ndani ya Songomo. Maana kama angepita mtu tofauti basi ni wazi kuwa pesa walizopokea juu ya mkataba wa LOBENG zingewatokea puani maana mkataba huo usingefanikiwa na wao tayari walikwisha kupokea nusu ya kiasi cha hongo nzima ili kulifanikisha jambo hilo.

Hivyo pia kwa upande wa Huang Feng mkurugenzi wa kampuni kubwa ya Dragon Triangle ambayo ndiyo ilikuwa inaingia mkataba na Serikali ya Songomo aliona ikiwa mkataba huu utashindwa kufanikiwa, kuna uwezekano wa kuyavuruga mahusiano yake na wanahisa wakubwa wa Kampuni hii ya Dragon Triangle kutoka huko magharibi wengi wakiwa wanatoka nchi za Ujerumani Marekani na Hispania ambapo Mdau mkubwa ndani ya kampuni hii kutoka Uhispania ilisemekana ni mtu kutoka familia ya Kifalme huko Mjini Madrid.

Hivyo kuvuruga mahusiano na Mtu kama huyu alijua fika itakuwa na madhara kiasi gani kibiashara kwa kampuni hii maana walikuwa washika dau wakubwa wakimwaga pesa za kutisha ndani ya kampuni hii kwaajili ya mradi huo wa LOBENG.

Kilichotakiwa kufanyika hapo LOBENG ilikuwa ni ajenda tofauti kabisa ambayo ilibaki kwa watu waliomo ndani ya Dragon Triangle lakini waliamini kama wangefanikiwa kuitia mikononi ardhi ya LOBENG basi ilikuwa ni hatua moja kubwa sana kiuchumi na ingewaongezea nguvu hapa ulimwenguni.

Hivyo aliamua kutumia nguvu ya kifedha na ushawishi aliokuwa nao ndani ya taifa la China akiwa anatokea Katika kijiji cha Shoshan ndani ya mji wa Hunan alikozaliwa Mao muasisi wa Jamhuri ya watu huru ya China.

Akiwa ni miongoni mwa uzao wa kizazi cha Mao na mkwasi wa kupindukia katika familia hizi tajiri tangu enzi za utawala wa mkomunisti Mao.

Akiwa na ushirika mkubwa na kundi la Peng Wang hili ni kosi lingine la damu kama walivyo Mabaduni wa Serikali Hawa wakiwa wamesambaa ukanda mkubwa wa Asia wakiwa ndani ya maccau, Shenyang,Hong Kong, Malaysia, Taiwan, Singapore na Shanghai.

Huang Feng alikutana na Andy Wong Raisi wa Peng Wang ndani ya Shanghai kumpa majukumu na mikakati juu ya kazi iliopo ndani ya Songomo. Lakini alimuonesha aina ya kosi watakalokabiliana nalo ndani ya Songomo, akamuonesha picha ya ile beji ya Dhahabu.

Andy Wong alifikiria kwanza kwa takribani dakika mbili bila kutoa jibu, huku Huang Feng akiwa anamtazama usoni kujaribu kumsoma msimamo wake juu ya hii kazi.

Andy Wong alijua fika kuwa Huang Feng hawajui vizuri hao kosi la Ancient Guards of the nation hasa juu ya uwezo wao.

Mwanzoni wakati Huang Feng anampasha habari juu ya kazi, alijua ni kazi kama kazi nyingine. Maana Huang Feng alimwambia kuwa ni kazi ngumu kidogo, lakini kwa uwezo wa kosi lake anaamini haitawachukulia muda kuitekeleza. Ambapo Andy Wong alimwambia asihofu kazi ni kazi ataipokea na kuitekeleza haijalishi itakuwa na ugumu kiasi gani.

Lakini baada ya kuoneshwa ile picha ndipo akajua kuwa sio tu kwamba ni kazi ngumu bali ni kwamba hata asilimia za kazi hiyo kukamilika ni ndogo sana na pengine haiwezekani.

Andy Wong alimtazama Huang Feng usoni kisha akamuuliza “Unawajua vyema hao Ancient Guards of the Nation?”

Huang Feng akamjibu kuwa “Nawajua vizuri tu, si ni kosi la wahuni Fulani tu hivi waliojizolea umaarufu kwa kuwatisha watu tu?”

Andy Wong alimkatisha kwa kumuuliza, “Unayakumbuka mapinduzi ya nchini Jotokali?” Huang Feng akajibu ndio, lakini akashituka sana baada ya Mapinduzi ya Jotokali kutajwa.

Andy Wong akamwambia kuwa waliosimamia mapinduzi yale ni hilo kosi la damu.

Akamuuliza tena, “Je unamkumbuka Setsen Khan?”

“Mmmhhhh.”
alibwabwaja Huang Feng.

“Humkumbuki Kublai Khan mjukuu wa Genghis Khan wewe?”

“Ahaaaa kumbe Kublai? Huyo namsikia sana habari zake.”
Alijibu Huang Feng.

“Umewahi kuzisikia habari za mageneral wake labda? The five Dogs?” Aliuliza Andy Wong.

Huang Feng akasema “Nazifahamu zinatisha sana”

“Basi hilo kosi la Ancient Guards of the Nation ni zaidi ya hao mageneral.”
Alimalizia Andy Wong.

Akamuuliza swali lingine “Je unamkumbuka Allen Dulles?”

“Ndio nani?”
Aliuliza Huang Feng akimaanisha kutokuwa na taarifa zozote juu ya mtu huyo.

Andy Wong akamuuliza “Unaingiaje kwenye vita na majasusi ilihali hauna taarifa za kutosha juu ya ulimwengu wa ujasusi?”

Andy akamwambia mambo mazito kumuhusu huyu jasusi wa marekani aliefanya kazi chini ya Maraisi wanane tofauti, akihudumu kama mkurugenzi wa Shirika la ujasusi marekani

Mtu mwenye viwango vya daraja la kwanza la ujasusi.

Akamwambia, basi uwezo wa watu ndani ya hilo kosi la damu ni sawa na uwezo wa Jasusi Allen Dulles maana wana mtu mmoja ndani yake anaitwa Jiga Kinamba.

Kitendo cha jina la jasusi mahiri ulimwenguni Jiga Kinamba kutajwa, kilitosha kumjulisha Huang Feng uzito wa hilo kosi la damu.

Akavuta kitambaa na kufuta jasho lililoanza kumteremka uso mzima na hata shati lake lilishaanza kulowa kwenye makwapa na mgongoni msitari wote kuelekea chini.

Akamuuliza Andy Wong “Sasa tunafanyaje na biashara zangu zinaingia kwenye changamoto kupitia kwa hao watu?”

Andy Wong akampa ushauri kuwa kama anataka kushinda ampe muda ajaribu kuongea na kiongozi mkuu wa kosi la damu la Red Blood hao ana Imani kubwa wanauwezo wa kupambana na hao Ancient guards of the Nation

Alimhakikishia kuwa kama ombi lake litakubaliwa na kiongozi wa Red blood Bwana Xian Xing, basi wahesabu kuwa hiyo kazi imeisha japo ilikuwa ni ngumu kumshawishi Bwana Xian Xing ama mtu aliyejisaliti kama jina lake linavyomaanisha kwa lugha ya Mandarin.

Mawasiliano yalifanyika baina ya Andy Wong, Huang Feng na Xian Xing ambapo mwanzo Xian Xing aligoma kutoa kosi lake kwa kazi ambayo ilikuwa ni mbali sana na ukanda wa asia akidai kufanya hivyo ilikuwa ni kuingia katika uhasama na ulimwengu wa nje na makundi yake.

Baada ya kumdanganya sana kuwa kazi yenyewe haingeibua mgogoro wowote ule, hatimae Xin Xiang alikubali ambapo aliwakabidhi Vijana saba wenye rangi nyeusi maana walimwambia kazi hiyo inafanyika ndani ya bara la weusi Wakiitamka (Feizhou) wakimaanisha Afrika.

Hawa watu kutoka Red Blood ni viumbe wengine wa ajabu wana uwezo mkubwa sana yaani kama vile walivyo hawa Mabaduni wa Serikali.

Kundi la Red Blood lilikwisha kutinga ndani ya Songomo na taarifa zake ziliwafikia Mabaduni wa Serikali ambao walitafuta habari kwa haraka sana kuwahusu hawa Red Blood na kubaini makao yao na uwezo wao.

Waliona kuwa huu ulikuwa ni uchokozi wa wazi kutoka kwa Bwana Huang Feng akishirikiana na Xian Xing.

Majukumu haya yaliachwa mikononi mwa Jiga Kinamba akiwa na Malone yaani wawili tu.

Walihitaji kuionesha dunia kuwa kosi lao la damu lipo na wala sio hadithi, maana kujificha kwao kwa muda mrefu kumepelekea baadhi ya watu kuanza kujenga dharau wakidhani kuwa ni hadithi.

Walipanga pia kuufanya mji wa Hunan na miji ya jirani yake pamoja na makao makuu ya kundi la Red Blood kuwa mfano. walitaka kifanyike kama kile kilichofanyika ndani ya nchi ya JotoKali miaka ile.

Raisi wa Jotokali alipotangaza kuivamia Songomo na kuifanya yote iwe miliki yake lakini kilichofuata ni kwamba robotatu yote ya jeshi la Jotokali waliuawa na baadhi ya miji pia iliharibiwa na wananchi wake kuuawa. Ilikuwa ni onyo kwa nchi yoyote inayowaza kuanzisha vita au mgogoro na Songomo.

Unaambiwa watu waliuawa mpaka damu mitaani zikafika usawa wa magoti na hilo lilifanyika na watu saba tu chini ya usimamizi wa Shetani mwenyewe Fanton Mahal akiwa na Sura ya Danstan Batona.

Mabaduni wawili tu ndio walikabidhiwa jukumu la kuwanyamazisha hawa viumbe wa Red Blood.

Kisha Mabaduni wengine watano wote waliingia kwenye chopa moja la kivita kuelekea huko Mashariki ya mbali wakilenga kuacha historia huko.

Chopa Lilikuwa na nembo ya fuvu linalovuja damu kwenye vishimo vya macho. Chopa moja la ajabu sana lisiloweza kunaswa na rada wala satelaiti yoyote likiwa linaongozwa na mtaalamu Macka Shinea.

Ndani wakiwemo mashetani watupu wakiitekeleza ile kauli ya Ukiniahidi vita kesho, jioni ya leo unanikuta mlangoni kwako nikiwa tayari kwa vita.”

Ni nini kitajiri Songomo na Huko Uchina?

Usikose sehemu ya sita na ya mwisho ya Riwaya yetu hii

Wako katika utunzi Sonko Bibo.
 
Najiuliza hii story uliwezaje kuandika kama mwandishi wew mwenyewe ni baduni wa serikali ndo maana Ipo poa sana yaani ni riwaya Kali Sana hongera

Sent from my A004SH using JamiiForums mobile app
 
Najiuliza hii story uliwezaje kuandika kama mwandishi wew mwenyewe ni baduni wa serikali ndo maana Ipo poa sana yaani ni riwaya Kali Sana hongera

Sent from my A004SH using JamiiForums mobile app
Mkuu Joseph ma, kwanza ahsante kwa pongezi lakini pia kwa upande wa mtazamo wako ni kwamba sijawahi kuwa hata mlinzi wa kampuni, ni hayo tu.
 
APPLE iPHONE 6 PLUS 220,000

BRAND NEW & CLEAN FROM CANADA

SPECIFICATIONS

Battery Health - 100%
Fingerprint Sensor - Working


RAM - 1GB
ROM/Internal - 64GB
Screen Size - 5.5 inches
Operating System - iOS
Color - Gold
Display Type - IPS LCD
Resolution - 1080 x 1920
SIM - Nano SIM
Main Camera - 8MP f/2.2
Selfie Camera - 2MP f/2.2
Battery - 3000
Bluetooth - 4.0
USB 2.0 & NFC


0783060577
Haina kasoro yoyote kwa 220,000 tu
 
APPLE iPHONE 6 PLUS 220,000

BRAND NEW & CLEAN FROM CANADA

SPECIFICATIONS

Battery Health - 100%
Fingerprint Sensor - Working


RAM - 1GB
ROM/Internal - 64GB
Screen Size - 5.5 inches
Operating System - iOS
Color - Gold
Display Type - IPS LCD
Resolution - 1080 x 1920
SIM - Nano SIM
Main Camera - 8MP f/2.2
Selfie Camera - 2MP f/2.2
Battery - 3000
Bluetooth - 4.0
USB 2.0 & NFC


0783060577
Haina kasoro yoyote kwa 220,000 tu
Mkuu Jack Obama heshimu uzi, ni bora ungepromote Hadithi but tangazo lako lafaa kule jukwaa la biashara
Ushauri huu ni kwa nia njema naomba tusihamishe attention za watu.
 
Sabakheri .... Nimefika hima hima faima. Bila shaka u kheri pasina shari. Mimi nipo mujarab kabisa. Nimekula nimeshiba nipo juu juu kama mkungu wa ndizi. Twahib sheikh sema nasi....
Maarifa mwenye uchizi wake
 
Back
Top Bottom